Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA UFAHAMU WETU.



MTUNZI:SINGANOJR



SEHEMU YA 16.

Ilikuwa ni kama kila kitu kilikuwa chekundu mbele yake kama moto, mbingu na ardhi vyote vilikuwa ni rangi ya moto , lakini ilikuwa ni ghafla tu mwanga ule mwekundu ulififia na sasa alichoweza kuona ni giza totoro, ilikuwa ni kama vile anazama baharini na hakuwa tena na msaada.

Lakini akiwa katika hali ya kukata tamaa , ghafla tu ni kama vile ni kuchomoza kwa jua hatimae mwanga ulijitokeza mbele yake , kupitia mwanga ule alijihisi ni kama vile nguvu zake sasa zimemrudia kiasi na alihangaika kwa kusogea mbele ili aufikie ule mwanga.

Mara baada ya kupiga hatua aliweza kuona ule mwanga ukizidi kuwa mweupe huku giza ambalo lilikuwa nyuma yake likizidi kumezwa na mwanga ule na ndani ya sekunde kadhaa giza lote lilipotea.

“Ah…!!!”

Ghafla tu alikaa kitako na sasa alikuwa akihema kwa nguvu kama mtu alietoka ndotoni , na katika ndoto alioota alijihisi ni kama vile alikuwa akiunguzwa na moto wa jehanamu ambayo ulimfanya kutokufurukuta hata kidogo na kujihisi kuwa katika mateso makali.

Ndoto ilikuwa ni ya uhalisia mkubwa mno kiasi kwamba ilimfanya kutaharuki na mapigo yake ya moyo kwenda mbio.

Mara baada ya kuhema kwa dakika kadhaa , alijikuta akitulia na sasa aliruhusu macho yake na akili yake kufanya kazi katika uhalisia , hivyo kuanza kuangalia mazingira.

Lakini sasa mara baada ya kuangalia mazingira aliokuwepo , alizidi kutaharuki , alikuwa kwenye mazingira ambayo hakuelewa yupo wapi , kitanda alichokuwa amelalia hakikuwa cha kawaida,kwanza kilikuwa chembamba sana.

“Nipo wapi?”

Aliuliza swali hilo , katika hali kama hio alijua kabisa hakuwa katika mazingira ya kawaida , hata kama pengine alipata ajali na sasa yupo hospitalini , hilo eneo halikuwa hospitalini kabisa.

Mapigo yake ya moyo ambayo yalikuwa yametulia yalianza kwenda kasi tena , aliangaza kulia na kushoto , mbele na nyuma lakini hakukuwa na mabadiliko , alijitahidi kusimama lakini alihisi hali ya kizunguzungu ikimvaa na kidogo tu aanguke chini.

Alijitahidi kushikilia ukingo wa kitanda ili kujiegamiza asidondoke chini , alikusanya nguvu zake zote ili aweze kutoka nje , akili yake ilikuwa ikimwambia kabisa hakuwa katika mazingira ya kawaida , alitaka kujua alikuwa wapi na shauku yake ilimpa nguvu ya kujikongoja ili kutoka nje.

Mlango ndani ya chumba alichokuwemo ulikuwa umechoka sana , ulionekana ni ule wa zamani mno , pembeni ya kona hio kulikuwa na chungu kikubwa mno kilichowekwa kwenye kijisturi., haikuwa hivyo tu kulikuwa na jiko lililochakaa na kuni ambazo zilionekana kuchomwa zilikuwa zimekwisha zima na kufanya eneo hilo kuwa la baridi mno.

Kila kitu kilikuwa kigeni kwake ,hakuwa na uelewa alikuwa wapi , udhaifu na hali ya kizunguzungu aliokuwa akisikia ilimletea shida sana.

“Hii sehemu ni wapi?!, najihisi ni kama vile nimeamka kutoka kwenye ugonjwa wa ajabu…”

Mawazo mbalimbali yalipita lakini hakuwahi katika maisha yake kuwa katika hali ya ajabu kama hio, hali ya kupaniki ilimvaa pia na kitu pekee ambacho aliona pengine ni bahati hakukuwa na kitu cha kutisha wala kuhatarisha usalama wak.

Mara baada ya kuvuta pumzi nyingi hatimae alijikakamua na kisha alijongea kutoka nje kwa kusukuma mlango.

“Burn the witch !Aderon is going to burn a witch”

“Choma mchawi huyo , Aderon anaenda kuchoma mchawi”

“Kila mtu”

“Burn that damn witch to ashes!!”(Choma huyo mchawi mpuuzi mpaka awe majivu)…..

“Puuuh!!!”

Hamza alijikuta akiamka huku akihema mno , hakuamini kile alichokuwa akiona sio uhalisia bali ni ndoto.

Kilichomfanya kuamkaa ni kumwagiwa maji ya baridi kabisa na hapo ndipo aliposhituka akihema.

Alijikuta akiangaza macho yake kulia na kushoto , kama mtu ambae ana hakiki mazingira, mara baada ya kuona mwanamke aliekuwa mbele yake , alijikuta akipata ahueni na kuvuta pumzi.

Eliza ndio mwanamke ambae alimuamsha Hamza , alijitahidi sana kumuasha kwa kumtingisha , lakini alishindwa kabisa na hapo ndipo alipochukua jukumu la kumuamsha kwa maji ya baridi , na hatimae aliweza kuamka , mwanzoni alihofia mara baada ya kuona haamki, sasa kitendo cha kushituka kwa Hamza kilimfanya kupatwa na ahueni na sasa anaona alikuwa katika eneo la sebuleni ndani ya nyumba ya mrembo huyo na alianza kuvuta kumbukumbu za jana yake.

******

Hamza mara baada ya kuingia katika Bar ya muembeni mwanamke ambae alimwita alikuwa ni Eliza , mwanadada mrembo ambae alimsaidia kutoka katika mikono ya Amisi na genge lake.

“Hamza ni wewe”

“Eliza ?”

Hamza mara baada ya kugeuka ndio aliweza kumuona Eliza akiwa katika meza na kundi la wanawake wengine warembo na wote walikuwa wamevaa mavazi ya kufanana.

“Kwa muonekano wako nilidhani hufikagi kwenye mazingira kama haya”Aliongea Eliza na muda huo alionekana pia alikuwa ameanza kulewa.

Kitendo cha Hamza kumuona mwanamke huyo mrembo ambae alikuwa akimfahamu mudi yake kidogo ilirudi na alisogea katika meza yao.

“Hii ni mara yangu ya kwanza hapa”Aliongea Hamza.

“Eliza mbona hututambulishi , huyu ni boyfriend wako?”Mmoja ya mrembo aliekuwa katika meza moja na Eliza aliongea , alikuwa amevalia suti.

“Una mwanaume mtanashati kweli na mwenye kuchukua mazoezi , kumbe hii ndio aina ya wanaume unaopendelea Eliza …”Mwanamke yule hakuacha kumsifia Hamza.

“Asha , unaongea nini , huyu ni kaka yangu”Aliongea Eliza akimtambulisha Hamza kama kaka yake.

“Acha aibu Eliza , wewe tuambie huyu ni nani , nadhani wale wanaume wanaokufukuzia watakufa kwa wivu wakijua una bwana”Mwingine aliongea akitania.

Ilionekana wanawake hao wote walikuwa wakifanya kazi pamoja kutokana na mazoea yao.

“Endeleeni tu kunitania na mtaona namna nitakavyokazia tukiwa kazini..”Aliongea na muda huo huo alimwangalia Hamza.

“Hamza unaweza kuungana na sisi kama upo mwenyewe”Aliongea Eliza , hakuwa na aibu kama mara ya kwanza alivyokutana na Hamza.

Hamza mpango wake ni kutafuta mtoto wa kike yoyote yule kupitisha nae usiku lakini baada ya kukutana na wanawake warembo kama hao aliona akubali na kukaa nao.

Muda huo alikuwa tayari ashaagiza bia yake na aliendelea kunywa huku stori mbalimbali zikiendelea na aliweza kugundua wanawake wote waliokuwa hapo walikuwa chini ya idara ya Eliza kazini na ilionekana Eliza ndio aliewatoa out mara baada ya kupandishwa cheo kazini kwake.

“Eliza vipi wale watu , hawajakusumbua tena?”Aliuliza Hamza kimitego.

“Huwezi kuamini kilichotokea , hivi unajua kiongozi wao alikuja kwenye kampuni ninayofanyia kazi kwa ajili ya kuomba msamaha , mimi mwenyewe sijui nni ni kilichotokea , lakini vyovyote vile yaliopita yashapita.. sitaki hata kukumbuka namna nilivyodhalilika mtandaoni”Aliongea

“Ni vizuri kama hatokusumbua tena”

“Eliza lazima kuna mtu amekusaidia kwa siri , kwa taarifa tulizopata nasikia Amosi amekuja akiwa na nundu usoni ikionekana kama vile kuna mtu kampiga”Aliongea.

Hakuna kilichojificha ndani ya kampuni, mrembo aliekuwa pale mapokezi ndio aliesambaza umbea juu ya Amosi kuonekana kuumia usoni.

“Acha kuota , unadhani mambo ni kama kwenye filamu..”Eliza aliongea huku akikataa ile kauli.

Ukweli nin kwamba mrembo huyo alikuwa na wasiwasi pia juu ya kile kilichotokea , lakini kadri ambavyo alifikiria siku hio hakuweza kupata jibu , isitoshe kwenye maisha yake hakuwa na marafiki ambao wanaweza kumsaidia.

“Vyovyote vile , Naomba leo nilipie kila utakachonunua hapa kama asante ya kile ulichonifanyia juzi na kuniokoa kutoka kwa wale mabaradhuli”Aliongea na aliinua glasi yake akigongesehana cheers na Hamza.

Hamza alifurahi kuona mrembo huyo alivyokuwa amechangamka,ukweli hakujua kama mrembo huyo alikuwa akitumia kilevi.

“Kwahio Eliza usiniambie huyu ndio babe aliekuokoa jana”Aliongea.

“Mimi siamini kama huyu kaka yako kweli, Eliza acha kuficha bwana”Waliongea kumtania na ilimfanya Eliza kuwa mwekundu mno lakini muda uleule Eliza aliweza kuona kundi la watu wakisogelea na palepale uso wake ulibadilika.

Mabadiliko yake yalionekana kwa kila mtu aliekuwa hapo ndani na kufanya wote wageuke.

Mwanaume wa maji ya kunde ambae alikuwa mrefu na amevalia t-shrt ya Ginvenchi na saa ya Rolex alionekana , alikuwa na wajihi wa uchangamfu, akiwa ametangulizana na wanaume wanne pia ambao walikuwa wamevaa mavazi ya bei ghali.

“Aiyaa… nikadhani nilikuwa nikikufananisha , kumbe ni wewe mrembo wetu Eliza”Aliongea yule mwanaume.

Eliza alionekana kujizuia na alijifanya kama vile hajasikia na aliendelea kudili na kinywaji chake.

Asha na wale wanawake wengine walikuwa katika hali ya chuki mara baada ya kuona ni kama wanataka kuvurugiwa.

Upande wa Hamza wakati akiwa hajui kinachoendelea , tayari yule mwanaume alionekana kumwangalia kwa kejeli.

“Hey! Mzee potea na umwachie bosi nafasi yako”:Aliongea moja ya vijana waliokuwa wametangulizana nae.

Hamza hakutaka kuonewa na wale watu kizembe na alikaa vilevile bila kuonyesha wasiwasi.

“Kama una uwezo jaribu kuniondoa na akae bosi wako”

“Wewe boya , unajua mimi ni nani , uliza uambiwe , mtu yoyote ambae anajifanya kutaka kupandishiana na mimi lazima avunjike mkono au mguu”

“Kumbe ndio ulivyo, nimekuelewa?”Aliongea Hamza huku akiendelea kupiga kinywaji chake.

Mara baada ya kuona Hamza hakutaka kuondoka , bwana yule alipiga meza kwa mkono wake.

“Hili ni onyo la mwisho , ondoka kwa hiari yako”

“Zefa naomba uondoke , acha kutuharibia mudi , ondoka na genge lako tuna mambo yetu”Eliza alikosa uvumilivu.

“Haha.. Eliza naona sasa kwa hiari yako umelitaja jina langu , acha kuwa mkali hivyo , nilikuwa na wasiwasi tu na rafiki yangu wa kitambo ndio maana nimekuja kukujulia hali”

“Haina haja na hatujawahi kuwa marafiki”

“Roho mbaya hio , nilitaka nikutoe angalau hela kidogo ufanyie matumizi, nimesikia gharama za hospitali ni kubwa mnno kwa matibabu ya mama yako asiejiweza kitandani”

Mara baada ya Eliza kusikia habari za mama yake zikiingizwa hasira zilimpanda mno na hakuweza kuvumilia tena na palepale alichukua glasi iliokuwa na mvinyo na kumwagia Zefa.

“Mnyama mkubwa wewe , unatoa wapi ukijogoo wa kumuingiza mama yangu hapa”

“Wewe malaya , nadhani umekuwa kichaa”Aliongea Zefa kwa hasira na palepale alitaka kumchapa Eliza kibao lakini mkono wake uliishia hewani mara baada ya kudakwa.

Eliza alijua angepigwa na kile kibao na alifumba macho kukisikilizia lakini hakikumpata .

Hamza alitumia mkono wa kushoto kuudaka mkono wa Zefa wa kulia.

“Ni udada huu kutaka kumpiga mtoto wa kike”Aliongea Hamza akiwa katika sura ya upole.

“Niachie wewe boya , unakitafuta kifo sio”Aliongea na palepale alijaribu kutumia mkono wake mwingine wa kushoto kujaribu kumpiga Hamza usoni, lakini kabla hata ngumi ile hajamfikia Hamza kwa mkono wake wa kulia alikuwa tayari ashamsukuma Zefa na kudondoka chini.

Hata Zefa mwenyewe hakuelewa kilichotokea , kwani nguvu kubwa isiokuwa ya kawaida ilimsukuma ghafla tu na alidondoka kama vile alikuwa hajasukumwa bali amedondoka kutoka umbali wa juu , alisikia maumivu makali mno kutokana na kuteguka mkono.

“Boss, uko ssawa”

Lile genge lake la watu lilimsogelea bosi wao na kumsaidia kusimama.

Eliza na wenzake walishangaa hata baadhi ya wateja waliokuwa ndani ya bar hio waliosikia mzozo huo walishangazwa na kitendo cha Zefa kudondoka chini baada ya kusukumwa.

“Hamza , unapaswa kuondoka haraka , sidhani kama utawaweza kwa ulichomfanyia mwenzao”Aliongea Eliza akimsihi Hamza kukimbia lakini Hamza hakuwa hata na ishara ya kutaka kuondoka , alikuwa katika hali ya utulivu kabisa.

“Niondoke , halafu wewe nakuacha na nani?”Aliongea na kauli ile ilimfanya Eliza kujishangaa lakini kwa wakati mmoja alijisikia vizuri mara baada ya kuona Hamza anajaribu kumlinda.

“Umemuumiza bosi halafu unataka kuondoka , hakuna kuondoka mpaka tukushikishe adabu boya wewe”Waliongea wale vijana , wote walionekana kulewa pia akiwemo bosi wao na palepale walimsogea Hamza kutaka kumshambulia lakini kilichowatokea ilikuwa ni maumivu.

Hamza hakutaka tena kuvumilia yale makelele na alisimama na kilichoendelea ilikuwa ni vijana wale na bosi wao kuchezea kichapo cha kufa mtu.

Ki ufupi ni kwamba hali ya hewa ilibadilika kabisa na hata wale wateja waliokuwa ndani ya eneo hilo walishangazwa na uwezo wa Hamza wa kupigana , wahudumu walijitahidi kutuliza hali lakini ilishindikana.

“Wewe boya , nitakuonyesha , nitakutafuta kwa nama yoyote ile , lazima nilipe kwa leo hii”Aliongea Zefa kwa hasira na kisha alijikongoja na watu wake na kuondoka ndani ya eneo hilo mara baada ya watu kuingilia ugomvi huo.,

Wale wanawake ambao Eliza alikuwa ameambatana nao na wenyewe waliondoka na kumuacha Eliza akiwa na Hamza

Eliza alikuwa kwenye mshangao , ukweli ni kwamba licha ya siku hio ni kama mara ya pili ya Hamza kupambana na watu lakini wale wa siku ile na wa wakati huo walikuwa na utofauti , hao walikuwa na uwezo mkubwa wa kupambana , lakini Hamza kiwepesi kabisa aliwadhibiti.

Kwasababu bili haikuwa imelipwa , Eliza alilipa bili na kisha Hamza aliondoka na mrembo huyo mpaka nje.

“Hamza huna woga kabisa

“Kwanini?”

“Zefa baba yake ni mkuu wa polisi kanda ya Dar es salaam , watu wengi walipelekwa polisi kwasababu ya kugombana na Zefa , anatumia hadi magenge ya wahuni kuadhibu watu ambao ana kisasi nao na hakuna wa kumfanya lolote”

“Hata kama , kwanza simjui na nilichofanya ni kutotaka wewe kuchokozwa”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Eliza kuonyesha hali kidogo ya kuchanyikiwa na kusita na alimwangalia Hamza machoni na kushindwa kuongea neno.

“Mbona unaniangalia hivyo?”Aliuliza Hamza mara baada ya kuona mwanamke huyu kasimama.

“Tunaweza kwenda kutembea tembea kule beach, japo ni usiku lakini watu wapo”Aliongea Eliza kwa kusita sita.

Hamza japo alishangaa ombi hilo ila hakukataa, walitoka katika Bar hio ya Mwembeni na kisha walisogea upande wa Beach , kulikuwa na Bar nyingine katika beach hio na mziki ulikuwa ukisikika , baada ya kufika wote walinunua vinywaji va baridi na kisha walishikilia mkononi na kutembea katika fukwe hio , Eliza alikuwa na kibegi chake huku Hamza akiwa mikono mitupu.

“Zefa alikuwa akinifuatilia kwa muda mrefu , kwa zaidi ya miaka miwili , lakini nilimjua sio mtu mzuri hivyo nilikuwa nikimkataa kila alipokuwa akinitongoza , siku moja akiwa amelewa alifika nyumbani kwetu na alianza kunilazimisha tufanye mapenzi , wakati nikiendelea kufurukuta mama aliweza kufika na mara baada ya kuona kitendo kile alipatwa na mshituko uliompelekea kupooza kiwiliwili cha chin…”Aliongea Eliza huku machozi yakianza kujilenga lenga katika mboni za macho yake.

“Lakini kwasababu ya baba yake kuwa mkuu wa kituo cha polisi na vilevile kuwa na konekshini alikamatwa kwa siku chache tu na kisha akaachiwa huru , ilikuwa ni siku kadhaa tu mara baada ya mama kupona kutoka hospitalini lakini alipatwa na kiharusi na sasa amekuwa ni wa kulala tu hospitalini kwa zaidi ya miaka miwil, kutokana na tukio hili ndugu zangu walianza kunisema vibaya na kunifanya nisipate msaada wowote wa kumuuguza mama..”

Hamza mara baada ya kusikia mrembo huyo akiongea kwa huzuni aliweza kuona ni hali gani alikuwa akipitia kwenye maisha yake.

Juzi alimkuta kwenye matatizo na leo pia alikuwa kwenye matatizo , ilioekana kulikuwa na watu wengi sana waliokuwa wakiyafanya maisha yake kuwa magumu.

“Baada ya tukio hilo ndio nilitoka nyumbani na kuhamia kwenye Apartment na kitu kinachochukua muda wangu mwingi ni kazi na kwenda hospitalini tu”

Eliza alikuwa amejikunyata kwenye miguu yake kutokana na upepo mwingi uliokuwa ukivuma alihisi baridi na baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu aliinua macho yake na kumwangalia Hamza.

“Hamza najua hatufahamini na leo ni mara ya pili umenisaidia , kwanini umekuwa mtu mzuri kwangu ghafla tu?”Aliuliza.

“Nilifanya nilichopaswa kufanya , isitoshe mimi ni mwanaume na huwa napenda kujichukulia pointi mbele ya mrembo kama wewe”Aliongea Hamza huku akigida pombe iliokuwa mkononi mpaka ikaisha na kutupa kopo ,kauli yake ilimfanya Eliza kucheka.

“Unaonekana kuwa mtu muwazi sana , lakini napaswa kukushukuru kwa wema wako licha ya kwamba hunifahamu”

Hamza hakuongea chochote na alichukua bia nyingine ya kopo na kuifungua.

“Vipi nikupe..”

“Hapana .. nitashikwa na haja ndogo muda si mrefu , nimekunywa sana leo”Aliongea na Hamza hakutaka kumpa tena kilevi.

Baada ya kukaa kama nusu saa katika fukwe hio Hamza aliona muda umeenda.

“Eliza nitakusindikiza mpaka unapoishi , muda umeenda, sawa”Aliongea na kumfanya Eliza aliekuwa amezika kichwa chake katika mapaja kunyanyua kichwa chake na kumwangalia Hamza usoni.

“Utaweza kweli kunifikisha mpaka ninapoishi..?”Aliuliza na swali lile lilikaa kimtego.

Upande wa Hamza alijiambia kwanini ashindwe kufika , isitoshe hana pa kwenda kama ni chumba alisharudisha na mpenzi wake feki kamfukuza.

Hamza alimchukua Eliza na palepale walitoka hapo na kurudi barabarani na kisha walipanda bajajaji mpaka anapoishi Eliza.

Hamza hakuwa na mpango wa kusimama getini , aliingia kabisa hadi ndani kwenye lift na Eliza alikuwa kimya tu , baada ya kufika katika floor husika wote walitoka mpaka kwenye mlango.

Eliza alionekana kuwa na wasiwasi mno na alikuwa akijiuliza na kujiambia imekuwaje leo kuja na mwanaume mpaka anapoishi tena usiku huo, ijapokuwa alikuwa amelewa kiasu lakini fahamu zake zilifanya kazi vizuri kabisa.

Lakini hata hivyo ashamruhusu mpaka kufika hapo asingemwambia aondoke , kitendo cha kumfanya Hamza kuja mpaka hapo ni kama nia yake ilikuwa wazi kabisa

Alijiambia yeye ni mtu mzima na kama atamwambia Hamza aondoke ingeonekana kama anamchezea akili bila sababu ya msingi.

Alikumbuka tukio la juzi kusaidiwa na Hamza na leo pia kusaidiwa na Hamza mbele ya mwanaume anaemchukua, palepale alifanya maamuzi ya liwalo na liwe , hata kama simjui vizuri ngoja nimkaribishe.

“Eliza vipi , umekosea ufunguo?”Aliuliza Hamza mara baada ya kuona namna ambavyo mrembo huyo alikuwa na wasiwasi akichangua kibegi chake

Muda uleule hatimae aliweza kupata kadi ya mlango na kuweka sehemu husika na hatimae mlango kufunguka.

“Karibu ndani…”

Mara baada ya Eliza kuingia ndani alitupia mkoba wake kwenye sofa na kupunguza nguo na kubakia na shati pekee na kufanya chuchu zake zilizosimama kuonekana vizuri , ilikuwa ni jambo la kuvutia kwa Hamza kweli.

Eliza aligeuka nyuma na kupepesa macho yake mazuri huku akimwangalia Hamza aliesimama mbele yake.

“Hamza .. umeoa au una mpenzi?”Aliuliza huku akisita sita, hakuwa akimjua Hamza vizuri na kitu pekee ambacho aliona anapaswa kujua angalau ni kama mwanaume huyo ana mke au ameoa , hakutaka kujihusisha na waume za watu na kujiingiza katika matatizo, aliokuwa nayo yalimtosha.

“Nina girlfriend lakini ni feki , vipi unaweza kusema nipo kwenye mahusianno?”

“Ndio inamanisha ndio , unamaana gani kusema ni feki?”

“Ukweli ni kwamba sina mpenzi , bado nipo single”Aliongea maana hakutaka kuongea sana maswala ya Regina.

Eliza mara baada ya kusikia kauli ile alijikuta akipatwa na ahueni na alimsogelea Hamza na kisha aliinua uso wake na kumwangalia , alioekana kuwa na wasiwasi na kusitasita kwa wakati mmoja.

Hamza mara baada ya kuona mrembo huyo anajilengesha kwake hakujua acheke au aune.

“Eliza unafanya nini?”Hamza alijifanya mzembe na swali lile lilimfanya Eliza kushikwa na aibu.

“Wewe , kwani hujui ninachofanya au unanichokoza”

“Sijui”

“Kama hujui basi”Aliongea na kisha akageuka lakini dakika ambayo alitaka kuondoka Hamza alimshika mkono na kumvuta kwake na palepale alimpiga denda

“Uh..”

Eliza hata hakujua alivyofika kifuani kwaHamza lakini alishitukia tu akiwa tayari ashabusiwa, kiini cha macho yake kilicheza cheza mno na kabla hajaendelea alijitoa kwa Hamza.

“Subiri kidog”Aliongea.

“Nini shida?”Aliuliza Hamza kwa sauti nzito huku akipumua kwa nguvu maana hisia zishamvaa tayari.

“Naomba niende kwanza kujisaidia”Aliongea na hakusubiri hata jibu alikimbilia chooni.

Eliza mara baada ya kukaa chooni na kushusha mkojo hatimae alipumua kwa nguvu huku akiwa na wasiwasi , hakuwa mzoefu sana na wakati huo alijiuliza akishatoka hapo nini kinaendelea, alikuwa akivutiwa na Hamza lakini hakutaka kufika hatua ya kufanya mapenzi kwa haraka sana.

Lakini baada ya kukaa kwa muda wa dakika kumi na tano alitoka na hapo ndipo aliposhangaa mara baada ya kumkuta Hamza ashajirusha kwenye sofa na anakoHamza , akiwa usingizini, alijikuta akipatwa na ahueni na alirekebisha AC na kisha akachukua blanketi na kumfunika na kuingia chumbani kwake.

Lakini wakati huo sio kwamba Hamza alikuwa amelala , alijifanyisha alikuwa amelala tu ili kutokumfanya mrembo huyo kuwa na wasiwasi.

Baada ya nusu saa kupita ndio alipotelea usingizini na anajikuta anaota ndoto ya ajabu mno.







SEHEMU YA 17.

“Mwenzetu , unalalaje usingizi mzito hivyo?”Aliongea Eliza mara baada ya Hamza kuamka.

Hamza bado akili yake ni kama ilikuwa imetawaliwa na ndoto aliokuwa ameota na aliishia kumwangalia tu Eliza.

Akili yake ilianza kukusanya matukio na alikumbuka jana alilala kwenye sofa na sio kitandani na hio ni mara baada ya kukisi na mrembo huyo na akakimbilia chooni.

“Mbona huongei chochote Hamza , umeniogopesha ujue kwa namna nilivopata shida ya kukuamsha”

“Babe , unajua wewe ni mrembo mno”Aliongea Hamza akijitahidi kurudi katika hali ya kawaida na kupotezea kile alichoota, kauli ile ilimfanya Eliza kusahau hata namna alivyopata shida ya kumuamsha Hamza na alishikwa na viabu vya kike.

“Umeniitaje?”Aliuliza na kumfanya Hamza kutoa tabasamu.

“Tumeshakiss tayari na kugusana , sidhani kama ni kosa kukuita mpenzi”

Eliza hakujua hata namna ya kujibu kwani hakuwa akichukia pia kuitwa mpenzi , ukweli alijisikia vizuri.

“Muda umeenda , nenda kaoge na kusafisha kinywa upate kifungua , kinywa”Aliongea kupotezea ile hali.

Hamza mara baada ya kufika chooni hatimae alivuta pumzi nyingi na kuzishusha , alikuwa akijitahidi kuwa sawa mbele ya Eliza lakini bado ni kama akili yake imetawaliwa na kile alichoota.

“Bwana eh , ni ndoto tu kama ndoto nyingine”Aliongea na kisha aliangalia mazingira ya choo hicho na aliweza kuona taulo pamoja na mswaki na dawa ya meno vikiwa vimewekwa , ilionekana Eliza alishaandaa kwa ajili yake.

Alijisikia viuri kwa kuona E.liza ni mwanamke anaejua kujali mwanaume, kwa muda mrefu hajahudumiwa na mwanamke mrembo.

Mara baada ya kuoga na kujifuta alirudi na kuungana na Eliza kwenye meza kwa ajili ya kifungua kinywa , kulikuwa na mayai ya kukaanga , chapati na supu ya kuku.

“Hizi chapati umepika?”Aliuliza.

“Hapana nimenunua kwa jirani hapo anatembeza , huwa mimi sio mtu wa kukaa sana nyumbani , sio kwamba sijui kupika chapati ila mahitaji sina”Aliongea akionekana kama vile anajitetea.

“Sijamaanisha hivyo?”

“Kwanini sasa na muonekano huo?”

“Ni kwamba sijapata kifungua kinywa nje na ninapoishi kwa muda mrefu sana”

“Oh , kama ni hivyo unaweza kuja mara kwa mara nitakupikia”

“Kwahio unamaanisha unataka tuishi pamoja”Aliuliza Hamza huku akicheka.

“Wewe , sijamaanisha hivyo”Aliongea huku akiona aibu na kujiambia ni mjinga kwanini kuongea kauli ya aina hio yenye utata.

Hamza alipiga supu hio nzito na kupotezea kabisa swala la ndoto , hakutaka kujihangaisha nalo kwanza alikuwa na mambo mengi kichwani ikiwemo swala la kumtafuta Mzee.

Baada ya kumaliza kifungua kinywa Eliza alipaswa kuelekea kazini na Hamza mara baada ya kuangalia ratiba chuo aligundua alikuwa na kipindi saa nne, hivyo aliona huo ni muda wa kuondoka kwenda chuo akapoteze poteze muda.

Eliza alitumia gari la kampuni na alimpa Lift Hamza mpaka Tazara na kisha alichukua dalalada kuelekea chuo.

Licha ya kwamba hakuwa na mudi alienda kwasababu kipindi cha saa nne ni cha Profesa Singano mzee wa bonus point.

Hakukuwa na foleni kubwa sana na alitumia kama dakika ishirini hivi mpaka kufika chuo na mara baada ya kushuka alianza kutembea taratibu taratibu kusogelea geti la chuo.

Lakini kabla hata hajalifikia Toyota Corola ilifika na kusimaa pembeni yake na kioo cha mbele kikashushwa na dakika ile wanaume watatu walitoka katika gari ile.

“Hamza Mzee , ndio wewe”Aliongea mmoja ya wale watu mwenye mwili mkubwa kidogo na Hamza aliitikia kwa kutingisha kichwa.

“Sisi ni polisi kituo cha mjini kati , upo chini ya ulinzi kwa kosa la uhalifu”Aliongea mmoja ya wale polisi na kisha alimsogelea Hamza kwa nia ya kumshikilia.

Jambo lile lilimshangaza Hamza maana hakujua hata ni uhalifu upi ambao amefanya mpaka kuja kukamatwa na polisi asubuhi yote hio.

Hamza hakutaka kuvuta attention ya watu na alikubali kistaarabbu na kisha aliingizwa kwenye ile gari na ikaondoshwa kwa haraka.

Dakika chache mbele gari ile ilipita Gerezani na kusonga mbele , jambo ambalo lilimshangaza Hamza.

“Afande si mmesema mmetokea kituo cha mjini kati?”Aliuliza Hamza.

“Acha uboya dogo , kituo cha mjini kati umekisikia wapi, tunakupeleka chimbo kukushikisha adabu”Aliongea moja ya bwana mwenye sura ngumu na kumfanya Hamza sasa kuelewa kinachoendelea.

Hakutaka hata hivyo kuleta vurugu kwenye gari hio na aliacha kuona mwisho wake.

Foleni ilikuwa hakuna kabisa hivyo gari hio ilitembea kwa spidi kubwa na ndani ya dakika kadhaa waliipita Mbagala na kufuata njia ya kwenda Kongowe na kisha gari ile ikakunja kushoto na kuingia katika barabara ya Vumbi na kusonga mbele na ilikuja kupita Bar moja ambayo Hamza hata hakusoma jina lake ila ilienda kusimama nje ya moja ya jengo ambalo lilikuwa limezungushiwa ukuta na kisha ikaingia ndani.

Kitendo cha gari ile kusimama tu na mlango kufunguliwa hatimae Hamza alijua nani amekuja kumkamata,ilionekana bwana aliemshikisha adabu jana yake ndio ametafuta tena ugomvi.

Zefa ndio aliekuwa mbele yake , akiwa amezungukwa na vijana wengine , haikueleweka eneo hilo lilikuwa ni kwa ajili ya nini lakini Hamza alijua tu hio ni ngome ya kihalifu.

“Wewe boya , nadhani jana maneno yangu uliyasikia vizuri , nilisema lazima nikushikishe adabu , sasa leo utapata kipigo mara mia ya kile ulichonifanyia jana”Aliongea Zefa kwa hasira.

“Unajifanya kidume sana , mwanamke niliemhangaikia kumpata kwa muda mrefu wewe hujafanya juhudi yoyote unalala nae kizembe , leo utanitambua, Vijana mpigisheni magoti”Aliongea kwa hasira mno na sasa Hamza aliona hasira yake bwana huyo ilionekana imechanganika na wivu.

Lakini kaba hata ya vijana wale hajaanza kumshugulikia Hamza honi ya gari ilisikika nje na ndani ya sekunde kadhaa tu geti lilifunguliwa na gari aina ya Mercedenz iliingia ndani.

Vijana waliokuwa wapo tayari kwa ajili ya kumshughulikia Hamza walikakamaa na nyuso zao kuwa na wasiwasi.

“Madam!!”

Moja ya bwana ambae ndio alifika na kumkamata Hamza akijifanyisha polisi aliongea na kusogelea ile gari.

Muda uleule mlango wa gari ile ulifunguliwa na viatu vyenye visigino virefu vilianza kuonekana kabla ya mwili wote.

Mrembo Dina ndio ambae alitoka kwenye gari hio na kufanya vijana wote wamwangalie kwa heshima , hakuna kijana ambae alikuwa jasiri wa kwenda kinyume na Dina , walikuwa wakimjua vizuri ukatili wake licha ya kwamba alionekana mpole na mrembo kupindukia.

“Madam kwanini umekuja mpaka huku, hakuna taarifa kwamba leo utatutembelea”Aliongea yule bwana kwa heshima huku akifosi tabasamu , lakini alionekana kuwa na wasiwasi .

Zefa hata yeye alikuwa akimjua Dina na siku zote licha ya ubabe wake na kupenda kwake wanawake kwa Dina hakuwahi hata kuwaza kumtongoza.

Dina alionekana alikuwa na haraka sana na aliangalia mazingira kwa sekunde kadhaa na kisha alipotezea swali lile na alimsogelea Hamza na kusimama mbele yake na kuinamisha kichwa.

“Samahani , sijatarajia swala kama hili litatokea”Aliongea Dina kwa heshima mbele ya Hamza.

Genge lile ikiwemo Zefa mwenyewe walishikwa na butwaa kwani hawakuelewa ni kipi kinatokea mbele ya macho yao.

Dina malkia na mmiliki wa kundi la Chatu alikuwa akionyesha heshima mbele ya Hamza?, mwanamke mrembo ambae viongozi wa kisiasa na wa jeshi walikuwa nyuma yake, lakini leo hii anaomba msamaha mbele ya mtu kama Hamza.

Wanaume hao watukutu walikuwa wakitamani hata kumwangalia mrembo Dina kwa ukaribu , walikuwa wakimhusudu mno lakini licha ya kuwa na utofauti mkubwa kati yao na Hamza lakini aliekuwa akipewa heshima ndio yeye.

Sasa tukio lililofuatia ndio liliwashangaza zaidi kwani Hamza alimshika Dina kidevu na kukiinua juu , kama vile ni mfalme mbele ya masuria wake.

“Dina kwanini unaomba msamaha , mimi ndio nilifanya fujo na kumpiga mtu na hata sasa hawajanifanya chochote”Aliongea Hamza.

“Kwahio huna hasira yoyote na mimi?”

“Haha.. kwanini niwe na hasira , kama ningekuwa na hasira nisingekutumia ujumbe wa maandishi”Alionngea na Dina alionekana kuvuta pumzi ya ahueni.

******

Regina hakuwa na kikao asubuhi hivyo hakuharakisha kwenda kazini na saa nne ndio muda alioshuka chini kwa ajili ya kupata kifungua kinywa , hakuwa na wasiwasi wowote na baada ya kifungua kinywa alikaa kwenye sofa na kuangalia habari za kimataifa huku akila tunda la shufaa kimapozi.

Shangazi alionekana kuwa bize na alionekana akitoka nje akiwa ameshikilia nguo ambazo zimekwisha kukauka , zilikuwa ni nguo za Hamza alizofua jana na kuziacha.

“Regina, jana umemfukuza Hamza na hakurudi kabisa na nguo zake pia hajachukua , ukute amelala mtaani huko”Aliongea na sasa ni kama vile Regina anamkumbuka Hamza kwani alishikwa na mshangao.

“Hivi kumbe jana aliondoka kabisa na hakurudi?”

“Ndio , chumba chake kipo wazi usiku mzima , sijui hakuna kilichomtokea , kwanini usijaribu kumpigia simu na kumuuliza yupo wapi?”Aliongea.

“Mtu mzima kabisa yule , hakuna chochote cha kumtokea , pengine ukute amelala alikokuwa akiishi”Aliongea Regina akiwa sio mwenye ishara ya kujali kabisa lakini ilikuwa tofauti kwa Shangazi.

“Nadhani hutonichukia kwa kuongea kwangu sana , lakini jana Hamza aliongea vile mpaka ukakasirika kwasababu ya maisha aliopitia”Aliongea na kumfanya Regina kumwangalia Shangazi kwa shauku kidogo.

“Unamaanisha nini Shangazi?”

“Hebu fikiria hata wewe , hana wazazi na tokea akiwa mdogo amekuwa peke yake, pengine ana hamu kubwa kutaka kuwa hata na wazazi kama ilivyokuwa kwako , pengine kwa kukosa wazazi ameshikwa na uchungu kwa namna wewe na baba yako mlivyokuwa mkijibishana jana , sidhani hata kama akitaka baba wa kubishana nae anaweza kupata”

“Shangazi kwahio unamaanisha ni Yatima?”Aliuliza Regina huku akishangaa na kumfanya kuwa mzuri zaidi lakini kauli yake ilimshangaza Shangazi.

“Inamaana wewe hukuwa ukijua?”

Regina aliishia kumumusa lipsi zake na alikumbuka namna alivyomfukuza jana Hamza, alionekana kuelewa kwanini Hamza alitaka kuzungumzia swala la baba yake.

“Ngoja nijaribu kumpigia”Aliongea na kisha akachukua simu yake.

“Shangazi wewe ndio unataka nifanye hivyo , ila sio mimi ninaetaka kumpigia”Aliongea Regina kama vile ni mtu ambae anajihami lakini kauli yake ilimfanya Shangazi kutabasamu na kutingisha kichwa.

Baada ya kuipiga namba ya Hamza hatimae iliita na kumfanya akohoe kidogo kusaficha koo na kweli muda uleule simu ilipokelewa.

“Uko wapi?”Aliuliza Regina kistaarabu.

“Nipo kitaa” Sauti ya kikauzu ilisikika.

“Najua upo kitaa , nauliza upo kitaa gani?”

“Kuna shida?”

Kauli ile ilimfanya Regina kukunja sura , alitaka kujali kuuliza amelala wapi usiku lakini sauti ya Hamza ilimfanya kupotezea wazo hilo.

“Hakuna shida.. nauliza tu”

“Kama huna cha kuongea nakata simu”

Bila hata ya kuongea simu pale ilikatwa

Mrembo huyo sura yake ilibadilika na kwa hasira aliweka simu chini kwa nguvu na kisha aling’ata pande la Apple kwa hasira kama kwamba tunda hilo limemkosea

“Shangazi , haina haja ya kumjali , muache na maisha yake”Aliongea

Shangazi Mariposa alijikuta akitingisha kichwa , aliona ni bora asingependekeza wazo la Regina kumpigia simu.



SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTUNZI: SINGANOJR

SEHEMU YA 17.
Dina alipata ahueni mara baada ya kuona Hamza hajakasirika , alifika hapo akiwa na hofu mno, baada ya kushusha pumzi hatimae aliwageukia wale watu waliomchukua Hamza kwa kujifanyisha ni polisi.
“Nimewaambia nini kuhusu kutojihusisha na maswala ya uhalifu hasa kipindi hiki cha uchaguzi?”Dina alifoka kweli
“Boss sikujua kama unafahamiana na huyu Hamza , kama ningejua ni Braza nisingeenda mbali na kupokea maagizo ya Zefa haha..”
“Nani kasema mimi ni Braza kwako …”Aliongea Hamza lakini bwana aliefahamika kwa jina la Kidula hakutaka kujali kauli yake , bado alikuwa na chembe za dharau kwa Hamza , ilikuwa ni kama anajiamini bosi wake hawezi kumfanya lolote.
“Boss ni kweli kabisa sikuwa nikifahamu kama unamjua Hamza , tunaomba ututambulishe ili swala kama hili lisije kujirudia?”Aliongea Kidula , wakati huo Zefa alikuwa kimya tu akiwa na wasiwasi.
“Hakuna hata mwenye thamani kati yenu wa kumjua hapa”Aliongea Dina kwa dharau.
Ukweli ni kwamba huyo Dina mwenyewe hakuwa akimjua Hamza ni hisia zake tu ndio zilikuwa zikimwambia sio mtu wa kawaida ambae nchi ndogo kama Tanzania inaweza kudili nae.
“Hamza , unataka tulimalize vipi hili swala ?”Aliuliza Dina.
“Hawa watu wako sina shida nao , hakikisha siku nyingine hawajitokezi mbele yangu , kuhusu huyu nataka akiondoka hapa sio mwanaume”AliongeaHamza akiwa katika hali utulivu na kauli yake ilimshitua Zefa.,
“Mr Hama naomba tulimalize hili swala , kama ningejua mapema nisingekuchokoza , nipo tayari kukupatia kiasi chochote cha pesa , naomba tusiende mbali”Aliongea Zefa.
“Sina shida na hela zako , watu wa aina yenu hamtakiwi kuwepo uraini kama sio kufa basi ni kifungo cha maisha, lakini hayo yote nimeyasamehe kwa kukupa adhabu ndogo”Aliongea aliongea na kumfanya Zefa kuzidi kuwa na wasiwasi.
“Dina.. Madam boss , hebu fikiria mara mbilimbili, kundi lenu hili ni la kihalifu na mzee ni moja ya watu ambao wanafumbia macho uhalifu uneondelea, ukinigusa mimi jua umeigusa serikali , najua jana nimekosea lakini tunaweza kulimaiza kwa pande zote kutokuathirika”Aliongea Zefa.
“Haha.. haha….unasema nikikugusa nagusa serikali ..haha”
Dina alicheka kicheko cha ajabu kweli na ilikuwa ni ghafla tu ashatoka aliposimama na kwa spidi kubwa alipiga hatua mbele na kilichofuatia ilikuwa ni Kidula kushika shingo yake huku akianza kutetemeka na ishara ya damu kumtoka eneo la shingonni zilionekana..
Ki ufupi ni kwamba alikuwa amekatwa eneo la shingoni na hata haikueleweka mrembo huyo alitoa wapi kisu lakini miondoko yake ilikuwa ni ya kuogofya mno.
“Nimerudia zaidi ya mara tatu sitaki kusikia swala la uhalifu , hasa kipindi hiki cha uchaguzi lakini hakuna anaelewa ninachomaanisha kwa maneno , nadhani hii ndio itaonyesha ni kwa namna gani nipo siriasi”Aliongea Dina na muda uleule Kidula aliondoka huku akianza kuchezesha miguu yake akipambania uhai.
Dina licha ya kuuwa hakuonyesha ishara ya hatia hata kidogo , ilikuwa ni kama mtu alieua kuku.
Vijana wote waliokuwa ndani ya hilo eneo walirudi nyuma huku hofu ikionekana katika macho yake.
“Hivi umesema baba yako ni nani vile..?”Aliuliza Dina huku akiangalia kisu kilichokuwa mkononni kwake , ilikuwa ni kama anaangalia kuona kama kuna damu yoyote imebakia lakini hakukuwa hata na doa ikionyesha spidi yake ya kuua ilikuwa ya juu mno.
Kisu hicho kilikuwa kidogo mno kama vile vya kufanyia upasuaji , pengine ndio maana hakikuonekana mkononi kwake mpaka pale alipoua mtu.
Zefa alianza kutetemeka huku akirudi nyuma kwa hofu, ule ujasiri wake wote ulimpotea mara baada ya kuona namna ambavyo Kidula alikuwa akitapatapa kupambania uhai wake.
Dina hakuwa mwanamke mrembo tena , alikuwa ni muuaji mwenye sura ya kirembo ambae huficha matendo yake kupitia biashara ya kuuza chai , sasa Zefa anajua kwanini mrembo huyo alikuwa akiogopeka na kufanya kundi la chatu liwe na nguvu.
“Rudia kauli yako , umesema nikikugusa nimegusa nini…?”Aliuliza Dina mara baada ya Zefa kushikiliwa na moja ya mwanaume aliekuwa nyuma yake asizidi kurudi nyuma.
“Naomba unisamehe ,nitafanya chochote kile , naomba usiniue…”Zefa mara baada ya kuona hakuna dalili ya huruma kwenye macho ya mwanamke Dina aliamua kupiga magoti na kupasha viganja.
“Hamza naomba unisamehe , sitomsumbua tena Eliza , mkiniachia nitaenda kujisalimisha polisi kwa nilichomsababisia mama yake…”Mwanaume alipasha viganja na muonekano wa Zefa ni kama sasa ulimridhisha Dina.
“Naweza kuonekana mwanamke mrembo na mlaini laini, lakini hiko ndio ninachowapa walimwengu kuona , huku uhalisia wangu ukibakia siri, unadhani baba yako ana nguvu ya kuizima nguvu yangu hapa nchini, kama ni hivyo tutaona hilo kuanzia leo”Aliongea Dina na kisha alisimama.
“Kama hamtaki yawakute kama yaliomkuta mwenzenu kiukeni maagizo yangu tena, hakikisheni haondoki na korodani hata moja na mtupeni barabarani kisha nisiwaone hapa wote muwe chimbo mpaka nitakapotoa maagizo mengine”
“Sawa Madam boss”
Vijana wale angalau hali ya ahueni iliwapata mara baada ya kuona wamesamehewa na hawakutana na kifo kama ilivyokuwa kwa Kidula.
“Nadhani mnajua cha kufanya juu ya huu mwili , hakikisheni mnasafisha kwa kufuata itifaki”Aliongea na kisha aligeuka na kumwangalia Hamza.
Upande wa Hamza hakuonyesha mshituko wowote , ilikuwa ni kama anaangalia kitu cha kawaida , pengine watu kwake kushuhudia kifo ni swala la kawaida ndio maana muonekano wake haukua na mabadiliko.
“Kwahio hili ni kwasababu ya yule mwanamke tena…?”Aliongea na swali hilo lilimfanya Hamza kushangaa na hakuelewa muda huo Dina alikuwa na hasira au na furaha ilikuwa ngumu kuelezea muonekano wake.
“Ni bahati mbaya tu ilionifanya kukutana nae , ndio maana…”
“Huna haja ya kujielezea naelewa”Aliongea huku awamu hio akiwa na sura ya huzuni na kisha alimpita Hamza na kuliendea gari lake.
Hamza alikosa neno lakini hata hivyo aliona anapaswa kumpeti peti mrembo huyo, hivyo alimfuata haraka haraka katika gari yake ya Mercedenz Benz S600
Gari hio ilikuwa ya thamani , japo sio sana lakini kwa mazingira ya Tanzania ni moja ya gari za bei ghali , uzuri wake zaidi ni kwamba hio gari vioo vyake havikuwa vya kawaida , ilikuwa kama gari za mercedenz zinazoingia nchini lakini ilikuwa imetengenezwa kwa mfumo wa ki usalama wa hali ya juu.
“Dina usiwe hivi , mimi na Eliza sio kama unavyofikiria”Aliongea Hamza, alishajua mrembo huyo ana taarifa zote kuhusu Eliza ndio maana hakutaka kujizuia kumtaja jina lake.
“Huna haja ya kuongea , kunikataa kwako kote kule kumbe kuna mtu ambae ushampenda tayari , haishangazi , moyo wako umejaa ndio maana nimekosa nafasi”Aliongea na kumfanya Hamza kuvuta pumzi.
“Dina sababu ya wewe kukosa nafasi ni kwasababu tayari ushaujaza moyo wangu muda mrefu tu”Kauli ile ilimshangaza sana Dina.
“Kweli!!?”Aliuliza akiwa kama hajategemea kauli hio.
“Ni kweli , kama isingekuwa hivyo unadhani kwanini asubuhi nilikutumia ujumbe wa maandishi juu ya kufuatiliwa na watu wako, ningekuwa sikujali nisingehangaika ningewaua wote , lakini nikafikiria na kuona vipi kama nitawaua wote utajielezea vipi mbele ya Umoja , ki ufupi ningekuingiza matatizoni na ungepokonywa uongozi”.Aliongea na kumfanya Dina kufikiria hilo na kuona inaleta maana na alijikuta akitabasamu.
“Mimi na yeye nani mzuri zaidi?”Ilikuwa zamu ya Hamza kushangazwa na swali hilo.
“Bila shaka wewe ndio mrembo zaidi”Aliongea Hamza huku akimkonyeza kichokozi lakini ilimfanya Dina kucheka vizuri na kwa jinsi alivyokuwa akionekana utadhani sio yeye alieua mtu dakika chache zilizopita.
“Unachojua ni kunichokoza tu muone, kama kweli unanipenda kama unavyyosema , kwanini hutaki hata kulala usiku mmoja kwangu kama ulivyofanya kwake?, Au mimi sikuvutii kama yeye?”
“Naona umefanya uchunguzi wa kutosha mpaka ukajua nimelala kwake”
“Nani kakuambia unipotezee , unadhani nitakaa chini tu bila kufanya chochote , nilitaka kujua ni mwanamke wa aina gani huyo amekuteka”
“Sijakupotezea Dina unajua nikwasababu…”Alisita.
“Sababu gani?”
“Ni kwasababu sina malengo makubwa ya kimaisha , nilichotaka ni maisha ya amani kuishi maisha ya kawaida , kuwa na wewe moja kwa moja maisha yangu yatabadilika”Aliongea lakini kauli ile palepale ilimfanya mrembo huyo kubadilika.
“Ondoka mbele yagu”Aliongea kwa kufoka
“Nimekosea nini?”
“Nimesema ondoka mbele yangu, sitaki kukuona tena”
“Dina kama nimekosea sema , acha kukasirika basi”
“Achana na mimi , kwahio kwa macho yako unaona kuwa na mimi kutakufanya ukose amani kiasi cha kuyabadilisha maisha yako,Hamza umeniangusha sana leo”Baada ya kauli hio palepale mlango ulifungwa kwa nguvu na gari iligeuzwa na ikatolewa nduki.
Hamza aliishia kuvuta pumzi na kuzishusha huku akiwa ameshika kiuno, hakujua kauli yake ingemkasirisha mno Dina , eneo hilo lilikuwa mbali na muda umeenda na aliona hata kipindi kishampita.
Aligeuka na kuangalia namna ya kuondoka hapo ndani lakini ile gari ya Corolla iliokuwepo hapo ndani ilikuwa imepakia ile maiti kwenye buti pamoja na Zefa aliekuwa amepoteza fahamu.
Hakutaka kuingia ndani ya gari hio , hivyo alitoka na kuanza kutembea wa mguu akiamini angepata usafiri wa daladala kurudi.
Kitendo cha kufika kuipita Bar iliofahamika kwa jina la Jiteketeze tu gari aina ya subaru nyeusi ilisimama pembeni yake na kioo kilishushwa na bwana mmoja mweye muonekano wa kihindi.
“Wapi Braza nikupe lift?”Aliuliza yule bwana na kumfahya Hamza kutabasamu.
“Haina haja ya kujifanyisha wakarimu , wakati ni wiki nzima sasa tokea muanze kunifuatilia, hamchoki tu?”Aliongea na kauli ile ilimfanya yule Mhindi kutoa tabasamu na aligeuza uso wake nyuma kana kwamba kuna mtu anamwangalia ndani ya gari hio.
“Uko vizuri , hatukujua kama ushatufahamu , unaonaje ukiingia ndani ya gari tukiongea kidogo?”
“Haina tatizo , nilikuwa nikitafuta lift hata hivyo?”Aliongea Hamza na bila ya kujiuliza mara mbilimbili alifungua mlango na kuingia ndani na hapo ndipo alipoweza kuona watu wengine wawili wakiwa siti za nyuma , mmoja alikuwa ni shombeshombe(Colored) mwenye nywele ndefu kama rastafarians na mwingine alikuwa ni mzungu.
“How did you discover us?”Aliongea kwa kingereza yule mweusi mwenye rasta.
“Kuna hata haja ya kuuliza , mlilipa hadi vijana waanze kunifuatilia huku wakijifanyisha kucheza pooltable karibu na ninapoishi , hii gari ndio iliokuwa ikinifuatilia juzi nilipokuwa Morogoro road, kwa rafudhi yako inaonekana umeishi sana visiwa vya Samar, kama sikosei kwa Tattoo hio kwenye mkono wako mnatokea katika kundi la wawindaji la Waray kutoka mji usionekana wa Biringan”
Kauli ile ilimfanya yule bwana aliesuka rasta kushangaa kidogo na kuonyesha kuridhishwa na Hamza..
“Ni kama tulivyosikia sifa zako za kutokuwa binadamu wa kawaida, haishangazi ndio maana una urafiki na mtu mkubwa kama Dokta Genesha”
Hamza mara baada ya kusikia neno Dokta Genesha ni kama sasa ashajua nini kilichowaleta Tanzania kutoka Ufilipino.
“Sijali mnachotafuta wala mnachopanga , lakini hamtakiwi kuwepo Tanzania”
“Umoja wetu wa wasionekana unamtafuta Dokta Genesha dunia nzima , ndani ya maabara ya Trishaza tulikuta taarifa zako zote ikiwemo sehemu unayoishi kwasasa , kitendo cha Trishaza wa Tembo kuwa na taarifa yako inaonyesha ni kwa namna gani mna ukaribu , swali letu ni wapi alipo Trishaza wa Tembo?”
“Nadhani kila mmoja anajua Dr Genesha alishafariki , hii sio siri na hata kwenye vyombo vya habari ililiripotiwa”
“Unachosema ni kweli , lakini hapa tunamzungumzia Dr Genesha ambae ni Trishaza Wa Tembo , lolote linawezekana”
“Narudia tena mnaemtafuta alishakufa tena sio kufa ameuliwa”Aliongea Hamza na wakati huo sauti yake ilionekana kuwa siriasi.
Jamaa aliefamika kwa jiina la Mendoza , huyo mwenye marasta alimeza mate na palepale ni kama mwili wake ulianza kutuna na nguvu isioonekana ambayo haikuwa ya kawaida iliongezeka.
“Kama kweli amekufa , tunataka kujua kitabu cha ufunuo wa Njiwa Juu Ya Mti Wa Uzima kipo wapi . je unajua alipokificha kabla hajafariki au kama alikuambia itakuwa vizuri ukituambia?”Aliuliza bwana mwingine ambae alikuwa mzungu , huyo aliitwa Dodo.
“Mnachotafuta ni hadithi ya kufikirika tu na hakuna ukweli wowote kuhusu uwepo wa hicho kitabu na sidhani kama kweli kuna huo ufunuo wa Njiwa juu ya mti wa Uzima”
“Acha porojo , taarifa tulizopata ni kwamba kabla ya kufariki kwa Dokta Genesha alitoa kauli kwamba ya ‘wanachokitafuta hawawezi kukipata’ , unadhani alikuwa akimaanisha nini? , moja kwa moja tunaamini kuna mtu aliemuachia urithi na urithi huo ni juu ya kitabu hiko cha Ufunuo”
“Nadhani hamuelewi na mnataka kulazimisha vitu ambavyo havipo , kwa hiari yenu niachieni hii gari, nitahesabu mpaka tatu , sitaki kuona mtu ndani ya gari”Aliongea Hamza kwa sauti ya kibabe.
“Moja…, Mbili..”
“Tunaondoka”Aliongea Mendoza Rastamani na aliwapa ishara wenzake na kushuka katika gari.
Mara baada ya wote kuondoka Hamza hakuchelewa aliushika usukani na kuondosha gari hio kwa spidi.
“Dokta Genesha sikutaka kukuamini tokea mwanzo juu ya ulichoniambia, ila kama sio shida yangu ya kutaka kumfahamu Mzee nisingeendelea kubaki na kitu ambacho kinanifanya niwe shabaha ya watu wengi.
Kazi imeanza , maisha ya utulivu nishayaishi ni muda sahihi wa kuanza kumtafuta Mzee , nitafuata ushauri wako , kama kuna ukweli wa simulizi ya Njiwa juu ya Mti wa Uzima basi malengo yangu yatafanikiwa”Aliwaza na muda huo alifanikiwa kumkwepa mtoto aliekuwa akiendesha gurudumu barabarani na kumfanya mawazo yake yarudi katika uhalisia.
Dokta Raphaeli Genesha ndio jina lake, ni raia wa Ureno ambae amechanganya rangi kwa kuzaliwa na baba wa kijapani na mama wa kireno.
Kabla ya kutambulika kwake kama mwanasayansi aliewaacha wanasayansi wenzake mdomo wazi alikuwa ni muumini mtiifu sana wa kanisa la kikatoliki.
Mara baada ya kuishi katika misingi ya kiimani kwa miaka mingi ndipo aliposhikwa na shauku na shauku yake ndio ambayo ilimtambulisha leo hii na pengine kumsababishia kifo chake.
Huyu ndio mwanasayansi ambae alitoka hadharani na kusema kwamba Spirituality is real na anao uwezo wa kuthibitisha hilo.
Kauli yake hio iliinua mijadala mingi sana kwa wanasayansi wengi duniani huku wengi wakienda mbali kwa kusema hilo ni swala ambalo haliwezekani kwani sayansi msingi wake ni majaribio na majaribio hayo sio juu ya namna kitu kinavyofanya kazi bali ni sababu ya kitu hicho kufanya kazi kwa kufuata mchoro wa tabia husika.
Ukweli ni kwamba hata huo uthibitisho hakuwahi kuuweka wazi lakini baadhi ya watu walianza kumuunga mkono bila ya kuona ukweli husika , huku wale waliokuwa wakimuunga mkono ni kulingana na hisia zao tu juu ya matukio yaliowapata yasioelezeka.
Miaka miwili mbele baada ya Dokta Genesha kutangaza msimamo wake kama mwanasayansi ambae anaamini uwepo wa nguvu za kiroho hatimae alikutwa na umauti na ushahidi wa juu ya ukweli aliokuwa akizungumzia hakuweka wazi na stori yake ikaishia hivyo.
Ni sawa leo hii atokee mtu aseme anao ushahidi wa kisayansi wa kuthibitisha uwepo wa Mungu, ndio iliyokuwa kwa Dokta Genesha.
Sasa kuhusu kuwa na ukaribu na Hamza haikueleweka ilikuwa vipi na historia yao ipoje mpaka kuja kufatiliwa na kundi la wawindaji kutoka visiwa vya Samar.
******
Dakika kadhaa mara baada ya Hamza kuondoka , wale watu wote watatu walisogea upande wa barabarani na kuingia katika gari aina ya Toyota Crown nyeupe , ndani ya gari hio kulikuwa tayari na mtu mwingine na ilionekana walikuwa wakimwambia kilichotkea.
“Umesemaje ,unamaanisha alikuwa akijua uwepo wetu tokea muda mrefu?”Aliuliza , alikuwa na sauti ya kike hivyo ikiashiria ni mwanamke na mkononi alikuwa ameshikilia picha.
“Mbona anaonekana wa kawaida sana , inawezekana amewapiga mikwara kuwaogopesha tu”
“Haiwezekani, anaonekana sio wa kawaida kabisa na ni mtaalamu, nilikuwa karibu yake lakini kila nilipo jaribu kuamsha uwezo wangu wa kichawi pumzi zilikuwa zikiniishia, anaonekana kuwa na mwili dhaifu mno lakini sio wa kawaida, hisia zangu zimeniambia kama nitamshambulia kuna uwezekano wa kutopona”
“Uwezo wako unachukuliwa kama wa juu ndani ya umoja , haiwezekani awe amekuzidi?”Aliongea yule mwanamke.
“Kwahio vipi kama akiwa na uwezo wa juu , ijapokuwa umoja wetu unachokuliwa kama daraja B lakini kazi hii sisi ndio tumepewa kwasababu ilionekana tunao uwezo wa kuikamilisha , Tanzania inaonekana kama nchi tulivu sana ila kuna mambo mengi yasioyakawaida yanaendelea , tunapaswa kuwa makini hasa nyakati za usiku”Aliongea Mendoza.
“Ila sidhani kama itakuwa rahisi kupata uelekeo juu ya kitabu hiki kilipo, mtu ambae ana urafiki na Dokta Genesha hawezi kuwa wa kawaida”
“Mbona kama tunaogopeshana , sisi ni wawindaji na sifa ya muwindaji hawezi kuacha kitoweo kupita mbele yake kirahisi , Tumekuja mpaka Tanzania kwasababu ya kazi na tunapaswa kuimaliza ili kuwa na maelezo ya kutosha mbele ya wakuu wetu”Aliongea Dodo.
“Kwahio ni hatua gani tuendelee nayo , ashatuona tayari hivyo atakuwa ni mwenye tahadhari”
“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi , kwasasa kitu pekee tunachoweza kufanya ili kupata taarifa kutoka kwake ni kupitia watu wake wa karibu”
“Unamaanisha nini Huda?”Aliuliza Mendoza akimwangalia mwanamke aliekuwa mbele yake , alifahamika kwa jina la Huda.
“Mendoza umeshanielewa ninachomaanisha”
“Sidhani kama ni wazo zuri ila kwasababu hatuna namna na tunahitaji matokeo tuendelee kumfuatilai kwa ukaribu , Udhaifu wake utaonekana na tutautumia vizuri”Aliongea yule Mhindi na kauli yake iliungwa mkono.
***
Hamza mara baada ya kutoka hapo aliona haina haja ya kwenda chuo na kwasababu alikummbuka Regina alimpigia simu alijua kabisa alikuwa akihitaji arudi nyumbani hivyo moja kwa moja aliona aelekee huko lakini kabla ya hapo aliona kwanza arudishe gari aliokuwa akiendesha.
Gari hio ilikuwa na nembo ya kampuni ya kukodisha magari ya DriveUs na Hamza aliijua fika kwani ashawahi kukodi gari katika kampuni hio ,ilikuwa na makao yake Posta lakini Hamza hakuona haja ya kupeleka gari hio Posta kwani wenyewe walikuwa na mfumo wa kufatilia magari yao pale aliekodishwa asiporudisha.
Dakika kadhaa tu alikuwa ashafika Kigamboni na alitafuta eneo na kuegesha gari hio katika megesho ya moja ya supermakert, alitembea mpaka zilipo bodaboda na kisha alitoa maelekezo ya eneo analoelekea na alichukuliwa kuelekea huko.
Alikuwa na uhakika wa kumkuta Shangazi nyumbani hivyo hakuwa na wasiwasi.
Dakika kumi na tano zilimtosha kufika kabisa , ukweli ni kwamba hakuwa hata na haja ya kupanda pikipiki kutokana na ukaribu wa mji wa Egret lakini kwasababu kulikiuwa na jua kali hakutaka kutembea.
Baada ya kushuka tu kwenye pikipiki na kubonyeza kitufe cha kengele hatimae aliweza kusikia sauti ya furaha ya shangazi kutoka ndani.
Mfumo wa nyumba wa kengele ulikuwa umeunganishwa na kamera na kifaa cha kusafirishia sauti na muda uleule mlango wa geti la kuingilia ulijifungua na akazama ndani.
“Hatimae umerudi nyumbani , nilikuwa na wasiwasi mno “Aliongea Shangazi ambae alionekana kuwa na furaha kabisa kumuona Hamza amerudi na mapokezi hayo yalimfanya kujihisi kuwa mwenye hatia , kwani Shangazi alimchukulia Hamza kama mwanafamilia ilihali alikuwa akiujua ukweli yupo hapo kwa muda tu .
Lakini sasa wakati Hamza anataka kuingia ndani sauti ya mwanamke anayoifahamu ilimwita.
“Hamza!,Unafanya nini hapa?”
Hamza alishangaa maana hakutegemea , aliinua kichwa chake na mara baada ya kuangalia eneo la sebuleni ndio sasa aliweza kumuona Eliza akiwa amekaa kwenye sofa.




SEHEMU YA 18.
Hamza alitegemea angemkuta tu Shangazi nyumbani lakini ajabu yake ni kwamba alimkuta Eliza na Regina wote wakiwa nyumbani.
Regina alikuwa ameketi upande wa kulia mwa Eliza akiwa ameshikilia glasi ya juisi na mara baada ya Eliza kumuita Hamza kwa jina lake alishangaa.
“Eliza , unafahamiana na Hamza?”
Ijapokuwa Eliza alikuwa katika mshangao na maswali kibao ya kwanini Hamza yupo nyumbani kwa bosi wake lakini aliitikia.
“Ndio nimefahamiana nae majuzi tu hapa , ndio mtu ambae alinisaidia wakati Amosi na kundi lake walipotaka kunichukua kwa nguvu..”Aliongea Eliza.
Hakutaka kuelezea kama jana Hamza alilala nyumbani kwake na aliondoka asubuhi, isitoshe uhusiano wao ni kama haukuwa wazi kama ni wapenzi au lah.
“Oh!”
Regina hakutegemea kuona kwamba Hamza ndio mtu aliemsaidia Eliza wakati akidhalilishwa , hakuweza kujizuia kushangaa.
“Ilikuwaje akakusaidia, mlifahamiana kabla?”Aliuliza mrembo huyo , alikuwa na mapozi hata wakati wa kuongea.
“Bosi , kwani sio kama yupo hapa kama fundi pia ? , ni mtengenezaji wa AC na kuna mama mmoja ndio alinikutanisha nae baada ya Ac yangu kupata hitilafu , wakati anakuja kutengeneza ndio akanikuta nipo kwenye matatizo akanisaidia , mwenyewe anasema ni fundi wa kila kitu kinachotumia umeme”Aliongea Eliza bila kuacha kuweka chembechembe za kumsifia Hamza.
Lakini kitendo cha kusikia kauli hio , mrembo Regina alijua amedanganywa tena , na kuona ndio maana jana alifika na kuanza kutengeneza TV yake lakini haikuwa hivyo tu alikuwa mwanachuo na mwalimu kwa wakati mmoja na kujiuliza Hamza ana kazi ngapi anafanya.
Hamza upande wake alikuwa ameurudia ule muonekano wake kizembe uliomfanya kupigwa cha mbavu hadharani na Anitha wa chuo,alijifanyisha kutokumjua Eliza kwa undani.
“Boss , umemuita kwa ajili ya ufundi?”Aliuliza Eliza huku akimwangalia Hamza.
Swali lile ni kama ghafla tu lilimletea Regina maumivu ya kichwa ,hakutaka kabisa siri yake ifahamike , alijua kama itakuja kufahamika alikuwa ameajiri mtu wakuigiza kama boyfriend angeonekana mwanamke wa ajabu mno.
“Unaonaje tukienda kuongea maswala ya kazi katika ofisi yangu kwanza , kuna baadhi ya vitu pia nataka ukavifanyie kazi”Aliongea Regina akiwa na muonekano wa kibosi ,Eliza alikuwa ni mwanamke ambae anajali zaidi kazi hivyo asingeendelea kuuliza.
Kitendo cha wanawake hao kupandisha juu , ilimpa Hamza ahueni na haraka haraka alikimbilia jikoni na kuchukua maji ya baridi vikombe vitatu na kushusha vyote ili kuirudisha mudi yake.
Shangazi aliishia kumwangalia tu Hamza , kuna namna flani mwanamama huyo alielewa kinachoendelea na kumfanya hata Hamza kukosa utulivu.
“Regina alikuwa akionyesha kukujali ndio maana alikupigia , kwanini ulimkatia simu bila ya kuongea neno?”Aliuliza shangazi.
“Shangazi mbona unatania , Regina anijali mimi?, si ndio yeye alienifukuza hapa usiku usiku”
“Ni kweli ,lakini baada ya kumwambia maisha yako yalivyo na kwanini uliongea vile alionekana kukuelewa”Aliongea Shangazi , kwa namna moja alionekana kama vile alikuwa akitaka wawili hao wapatane.
Hamza na yeye alionekana kuelewa , na aliona Regina pengine ni tabia yake , ana kauli zenye ukali mno na mwenye kubadilika badilika ila ni mwenye roho nzuri , kwa alichosema Shangazi kilimfanya aone haina haja ya kuondoka.
“Tutabanana hapa hapa mpaka kieleweke, haondoki mtu hapa”Aliwaza Hamza akisahau mkataba wa kuishi maisha mazuri karibu na mrembo wa matawi ya juu unaisha ndani ya miezi mitatu tu.
Baada ya lisaa kupita , hatimae Eliza alishuka sebuleni na kumuaga Shangazi kama anaondoka , Hamza muda huo alikuwa akiangalia TV huku miguu ikiwa juu ya sofa na Eliza upande wake hakuonyesha hata kujali , kuna namna flanni ilimuambia Hamza anaishi hapo kwa namna alivyokuwa amejiachia kwenye sofa.
Hamza mara baada ya kuona mrembo huyo ameondoka kabla ya kumuaga alimuwahi.
“Eliza naomba unisikilize”Aliongea kabla hata hajaingia kwenye gari lake
“Unataka kuongea nini?”Aliuliza akiwa na uso usiokuwa na masikhara kabisa.
“Sio kama unavyofikiria mimi na Regi..”Hamza alisita kuendelea mara baada ya kukumbuka kipengele cha mkataba kilimtaka uhusiano wao kubakia kuwa siri.
Eliza aliendelea kumkazia Hamza huku akimwangalia namna ambayo anajikuna kichwa kwa kukosa kujiamini lakini kitendo cha kuona mwanaume huyo anavyohangaika kujielezea alitoa kicheko.
“Eliza mbona unacheka, inamaana unajua tayari?”Aliuliza kwa wasiwasi
“Uitana ukifanyia surprise sio , kuna haja gani ya kuficha sasa , nishajua tayari umekuwa mwajiriwa wa kampuni yetu na unaanza jumatano”Aliongea Eliza na kauli ile ilimuacha Hamza mdomo wazi.
“Ajira gani tena?”Ndio wazo la kwanza lililomjia Hamza akilini.
Kabla hata hajaongea chochote sauti kutoka ndani ilimwita.
“Hamza njooo kwenye chumba changu cha kujisomea”
“Tutaongea siku nyingine, nenda haraka bosi anakuita nawahi mwendokasi kwenda Morogoro kikazi bye”Aliongea Eliza huku akimwangalia Hamza kimahaba na kisha aliingia kwenye gari yake na kuondoka.
Hamza hakuwa akielewa chochote na ni kama alikuwa amechanganyikiwa , na kimya kimya alienda mpaka chumba cha kujisomea cha Regina.
Baada ya kuingia ndani akiwa na muonekano wake wa kizembe alifunga mlango na kuanza kujikuna kichwa kama mwanaume ambae amekosa kujiamini.
“Regina umemuambia nini Eliza juu yetu?”
“Nimemuambia mimi na wewe tulikuwa marafiki wakati tukiwa wadogo katika kituo cha kulelea Yatima na tumekutana majuzi tu hapa , kwasababu ya maisha yako kuwa magumu sana na unasoma nimeamua kukufanya msaidizi wangu binafsi, kuhusu kuishi hapa nimemuambia ni kwa ajili ya kumsaidia saidia Shangazi kazi za nyumbani na kumpeleka sokoni na gari”
“Na ameamini hayo maneno?”Aliuliza Hamza huku neno ‘maisha magumu sana’ likijirudia rudia kwenye kichwa chake na kufanya midomo yake kucheza.
“Nimefahamiana na Eliza kwa muda mrefu ukiachana kuwa mkubwa kwangu ki umri na uwezo wake mkubwa kazini lakini anapenda kuishi maisha ya kawaida na sio mtu wa kufikiria fikiria watu vibaya bila sababu , ili mradi sikuongea kitu ambacho hakina maana nina uhakika ameamini”
“Huoni kwamba ni vibaya kumdanganya mtu anekuamini?”
“Kwahio vipi sasa kama nimemdanganya , au unataka kila mtu kujua mimi na wewe ni wapenzi feki , halafu inakuuma nini kama nimemdanganya , haya ni mambo yangu binafsi haina haja ya kumwambia kila mtu kinachoendelea kwenye maisha yangu”
Hamza alijikuta akishikwa na bumbuwazi , dakika chache zilizopita aliona Regina ukauzu ulikuwa wa nje tu lakini muda huo anaona kabisa ni mpaka ndani.
“Ni kheri uache kujali ya wengine na usaini hii nyaraka”Aliongea akimpatia Hamza karatasi na Hamnza aliangalia kilichokuwemo kwenye karatasi.
“Kwahio ni kweli unataka niwe msaidizi wako , unadhani ratiba zangu za chuoni zinaniruhusu kuwa kazini masaa yote hayo?”
“Mimi na wewe uhusiaon wetu ni wa kikazi zaidi na ili kuficha kazi yako ya kuigiza ni kheri tuwe na namna ya kujitambulisha pindi tutakapoonekana pamoja , isitoshe huu ndio uongo niliomwambia Eliza , hivyo lazima uongo wangu uwe kweli, kingine una vikazi vingi kibao mara fundi mara sijui mwalimu, nani anajua kesho utakuwa unafanya kazi gani nyingine , ili usije kujiingiza kwenye matatizo ni kheri kuwa na kazi ya kueleweka inayoendana na usalama wako
Nilikupigia muda ule lakini ukawa kama vile hujataka kupokea simu yangu, nikajua labda upo na tatizo , mimi kama bosi wako usalama wako pia ni kipaumbele changu”Aliongea bila ya kuwa na hisia zozote usoni.
“Regina muda ule wakati ukiwa unapiga nilikuwa sehemu mbaya … sikuona kama itakuwa vizuri tukiongea ndio maana nilikata simu”
“Sijakuambia ujielezee na sijali unachofanya , hayo ni maisha yako binafsi , ninachotaka ni usaini mkataba huu wa kazi”Aliongea kibabe kana kwamba anajaribu kumuogopesha na Hamza akiwa katika muonekano wa kizembe alichukua karatasi na kusaini haraka haraka.
“Watu na bahati zetu bwana , mshahara milioni moja , ukijumlisha na zile … nani wa kukataa kusaini mkataba mnono aina hii”Aliongea Hamza mara baada ya kusoma karatasi hio na kutia saini kwa mbwembwe zote huku akiwa na tabasamu zito usoni , alionekana mtu anaependa pesa mno kuliko kitu chochote..
Laki tano kwa mwezi kuwa boyfriend feki ukijumlisha marupurupu ,milioni moja nyingine ya kuwa msaidizi binafsi , ki ufupi ni kwamba ndani ya miezi hio mitatu aliona atakuwa na kitita cha kutosha.
“Huyu mwanaume muonekano wake ni mzuri , anaonekana kuwa na akili na pia anajua kuongea kifaransa , kinachosikitisha ni kwamba udhaifu wake hufichi hata kidogo , yupo tayari kufanya lolote kwa ajili ya hela”Aliwaza Regina.
“Bosi kwanzia sasa mimi ni msaidizi wako binafsi , lakini vilevile ni boyfriend wako wa maigizo”Aliongea Hamza kijeshi huku akipiga saluti akiwa na tabasamu pana usoni na kitendo kile kilimfanya Regina kutoa tabasamu.
“Usichokijua ni kwamba hadhi ya msaidizi wangu binafsi mshahara wake ni milioni nne na nusu kwa mwezi…”
“Nini!!.. kwahio unanifanyia dhuluma?”
“Hii ndio njjia ya kudili na mtu kama wewe mpenda hela kupindukia , ambae unaongea kama bila tuo , hii kitaalamu inatiwa jino kwa jino , hakikisha unazingatia vipengele vya mkataba, utakatwa nusu ya mshahara wako kila unapokiuka vipengele”
Kauli ile ilimnyong’onyeza kabisa Hamza na kuona alimchukulia poa huyo mwanamke lakini anazo mbinu za kimafia za kumdhibiti.
Siku iliofuata Hamza alienda chuo kama kawaida na alikuwa na test , alifanya na akamaliza na kisha aligeuza zake na safari yake haikuwa nyumbani bali alienda Kijichi kumuona Dina lakini bahati mbaya hakumkuta hivyo alichukua baiskeli yake na kuanza safari ya kurudi Kigamboni.
Saa kumi kamili ndio muda ambao alifika na Shangazi alimshangaa sana Hamza kurudi akiwa na baisikeli ambayo ilikuwa imechakaa lakini hata hivyo hakuongea sana na Hamza alienda kupaki usafiri wake pembeni na ile Maserati ya Regina tena kwa kuigamiza.
Muda wa jioni wakati Regina anarudi kazini na kukuta ile baiskeli alikasirika mno mara baada ya kugundua alieileta hapo ni Hamza na kumwambia aitoe nyumbani kwake lakini Hamza aligoma na kumwambia ana koneksheni ya kiroho na hio baiskeli hivyo haiendi popote , mgogoro ulikuwa mkubwa mpaka Shangazi akaingilia na Regina akatulia.
Siku iliofuata Hamza hakuwa na kipindi kabisa chuoni , ki ufupi wiki hio hawakuwa na vipindi mpaka wiki inaofuata maana walikuwa mwishoni mwa semista na wangefunga moja kwa moja ingekuwa ni field na Hamza aliona ni kama kupiga ndege wawili na jiwe moja maana anao uwezo wakuomba field moja kwa moja ndani ya kampuni ya Regina.
Asubuhi ya jumatano hio ndio siku ambayo Hamza anaenda kazini na Regina kama msaidizi binafsi
Nguo zote ambazo alikuwa amevaa alipatiwa na Regina , kuanzia viatu mpaka tai , haikueleweka hata leseni ametolea wapi lakini Hamza alikabidhiwa leseni ya jina lake kabisa.
Hamza alishindwa kujizuia na kuishia kutoa pumzi nyingi ya kushangaa na aliona namna ambavyo pesa ilikuwa na nguvu , mwingine kufuatilia leseni ingechukua hata mwezi lakini kwa Regina ilikuwa ni masaa tu alikuwa nayo mkononi , gepu hilo halikuwa dogo hata kidogo.
Akiwa kama dereva ndani ya gari ya Lexus 570 nyeusi, Hamza alikuwa akiboreka kwani foleni ilikuwa kubwa mno , yaani hata baiskeli yake aliona spidi yake ilikuwa kubwa.
Hamza aliangalia kupitia kioo cha nyuma na aliweza kuona Regina alikuwa bize na Mackbook yake akifanya kazi , hakuonekana kuathirika kabisa na foleni ya magari.
Kwa jinsi ambavyo alikuwa amevalia na kupendeza ni kama vile hakuwa akielekea kazini , alikuwa amevaa gauni ambalo limevuka magoti pamoja na blazer ya rangi ya ugoro hivi na alikuwa amepiga nne na kufanya miguu yake ilionona kuwa nje nje.
Hamza alijikuta akimeza mate mengi na kujiambia inakuwaje mwanamke huyu kuwa mrembo namna hio , kwanini ngozi yake inaonekana laini hata kabla ya kuigusa.
“Pipii..!!Papaaa!!”
Sauti ya honi ya gari iliokuwa nyuma ilianza kupiga honi mara baada ya gari ya Hamza kutosogea mbele licha ya foleni kuisha.
Regina ndio aliekuwa wa kwanza kushituka na alikunja sura mara baada ya kujua Hamza alikuwa akimwangalia kwa kupitia kioo cha nyuma na kushindwa hata kuona taa ya kijani ilikuwa ishawaka.
“Hamza , unaangalia nini, taa ya kijani ishawaka”Aliongea Regina kwa kukaripia na hali ile ilimfanya Hamza uso kupata moto huku akiwahi kuendesha kusogea mbele , alikuwa amejisahau akimakinika na urembo wa Regina.
“Kwanini unanikodolea mimacho yako?”Aliuliza Regina huku akionekana hana masikhara hata kidogo
“Sikuwa nikikuangalia nilishikwa na ka usingizi ,niliamka mapema”Aliongea Hamza akiwa na sura ya mikausho kabisa kama hakujatokea kitu.
“Muongo sana ,mbahiri , tamaa zimekujaa na umekaa kihuni huni tofauti na muonekano wako , wewe ni mwanaume jitahidi hata kujizuia , huoni hata aibu”
“Mbona unanibebesha tabia ambazo sina , mimi nakubali ni mbahili ndio na napenda hela , nani hapendi hele dunia hii , kama shida nikukuangalia, ndio nilikuwa nikikuangalia , unadhani ni mwanaume gani rijali asiependa kuangalia wanawake warembo”
“Bado tu unautetea ushenzi wako? Haya nimeacha kuongea kuhusu baiskeli yako , vipi kuhusu hizi..”
Aliongea na palepale alirusha mfuko wa nguo mbele ya Hamza , ilikuwa ni mfuko ambao ulikuwa na nguo chakavu za Hamza ambazo alivaa siku ile wakati anaenda kukutana na wazazi wa Regina , sasa alizisahau kwenye gari.
“Kama sio mbahili wewe ni mtu gani ,nguo ikichakaa unabadilisha lakni wewe jana uko bize mpaka kuzipiga pasi , mpaka nguo za kazini nimekuandalia mimi , chuo ulikuwa ukienda na nguo gani , inamana hizo kazi zako hazikutoshi hata kununua nguo za bei rahisi ,halafu unaongea kwa kujiamini mbele yangu”
Ukweli ni kwamba Regina alikuwa na kisirani cha asubuhi, wakati Hamza anashuka asubuhi kwa ajili ya kwenda kazini alikuwa amevaa suruali ya pundamilia ya mtumba na tisheti ya jezi yenye bonge la chata la MoExtra.
Shangazi licha ya kwamba alikuwa mtu mzima na ambae hakujali sana mavazi lakini alichovaa Hamza kwa ajili ya kwendea kazini kilimfanya kucheka.
Kama isingekuwa Regina kuandaa nguo kwa ajili ya Hamza asingekubali kuondoka nae.
Hamza aliishia kumuona Regina kama mwanamke ambae hachuji maneno kwenye kumwambia vitu na kujiona kama mtoto mdogo.
Lakini hata hivyo hakutaka kujibishana nae, kama ilivyokuwa asubuhi alivyofokewa kwa kuvaa jezi na suruali yake pendwa ya pundamilia ndio ambavyo aliona awe mtulivu asiendelee kujibishana nae.
Hamza alijiambia yeye ni mwanaume na haina haja ya kujibishana na mwanamke, kwake nguo sio kupendeza bali ni athari za faida za nguo husika katika ulimwengu wa kiroho.
Mara baada ya kufika katika eneo la maegesho , Valet alimpa ishara ya eneo maalumu ambalo CEO ndio gari yake inaegeshwa na Hamza alienda kuisimamisha hapo , ilikuwa ni ndani kabisa ya jengo.
“Kumbuka masharti mawili niliokusisitizia jana”Aliongea Regina kabla ya kutoka nje ya gari.
“Nakumbuka bosi , sipaswi kukuita Regina bali nikuite bosi na vilevile nisitoe siri juu ya mahusiano yetu feki”Aliongea
Mara baada ya Regina kuridhika alishuka kwenye gari na akafuatia Hamza na kisha walizisogea lift maalumu ambazo hutumiwa na wafanyakazi wa ngazi ya juu wa kampuni.
Pembeni ya lift hio kulikuwa na mdada ambae alikuwa amesimama,makadirio ya umri miaka ishirini na sita hivi.alievalia suti nyeusi.mfupi wa wastani hakuwa mrembo sana lakini alikuwa mtanashati.
“Goodmornining Madam”Alisalimia yule mdada kwa heshima na Regina aliishia kutingisha kichwa kupokea salamu yake.
“Huyu ni Linda , msaidizi wangu namba moja , hakikisha unajifunza kutoka kwake”Aliongea Regina akimtambulisha Hamza.
“Hello , naitwa Hamza Mzee natumaini kujifunza mengi kutoka kwako”Aliongea Hamza akimpatia mkono Linda.
Linda alionekana kusita kwa sekunde kadhaa lakini aliishia kupeana mkono na Hamza ukweli sio mkono bali aligusanisha vidole tu na mkono wa Hamza , hakuonekana kumchukulia siriasi kabisa Hamza.
Hamza aliona ndio maana ni msaidizi wa Regina , wanaonekana kufanana kabisa wote ni makauzu na maringo yamewajaa.
Linda muda uleule alishikilia kishikwambi chake vizuri na kuanza kumsomea Regina ratiba yake ya siku hio.
“Madam , leo ratiba yako ya asubuhi ni saba , tisa , kumi na tanu , kumi na nane , ishirini , ishirini na moja na ishirini na mbili..”
Aliongea Linda na ilimfanya Hamza kushindwa kuelewa anachomaanisha lakini aliishia kufuata nyuma nyuma mara baada ya Regina kuingia kwenye lift
Sekunde ambayo lift inajifunga , muonekano wa Regina ulizidi kubadilika na sasa kuwa na usiriasi mno kama vile ni mkuu wa nchi , hali ile ilimfanya hata Hamza kumeza mate mengi na kujiambia kwahio huu ndio muonekano wake akiwa kazini, kwanini ni kama vile ni mtu tofauti na yule Regina wa nyumbani.
Regina alibinya namba mfuluulizo akianzia saba , tisa , kumi na tano na kuendelea bila kukosea kulingana na maelezo aliotaja Linda , jambo lile lilimshangaza Hamza kwani Regina alisikia mara moja tu lakini alikuwa akikumbuka vizuri , muda huo ndio sasa Hamza alielewa herufi zile zilikuwa zikimaanisha floor za jengo hilo.
“Boss , floor ya ofisi yako si mwisho kabisa , kwanini unabonyeza floor za chini?”Aliuliza Hamza ,jana yake alishasoma maelezo ya mwanzo juu ya mazingira ya kazi ya Regina hivyo alikuwa akijua ni floor ipi ofisi ya CEO inapatikana.
“Kila Floor CEO anakuwa na kikao , atatatua baadhi ya shida katika idara husika , kwa njia hii ndio namna anavyookoa muda wa wafanyakazi kupanda na kushuka kwenda ofisini kwake hivyo kuongea ufanisi wa kazi”Aliongea Linda.
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU



MTUNZI:SINGANOJR.



SEHEMU YA 19.


Kitendo cha Linda kumwelezea namna utaratibu wa CEO unavyokuwa kila akifika kazini , hatimae lift iliweza kufnguka katika floor ya saba na ndio sehemu ambapo idara ya uwekezaji inapatikana na meneja wa idara hio alikuwa tayari ameshaandaa nyaraka nje ya lift na kumpatia Regina.

“Mkurugenzi malighafi mpya ambazo zinatengenezwa na Taita Chemical, zinaenda kubadilisha kabisa teknolojia ya utengenezaji wa raba na kuzima teknolojia ya zamani katika maeneo mengi , hii itapelekea kupunguza gharama za udhalishaji wa bidhaa zote zinazotumia raba kwa zaidi ya asilimia arobaini na tano, tulikubaliana katika kikao kuongeza hisa zetu ndani ya kampuni ya Taita kwa asilimia 4.3%”Meneja wa idara ya uwekezaji alisoma ripoti kwa haraka.

Regina alipitia nyaraka ambayo alikuwa amekabidhiwa haraka haraka na baada ya pale aliitupia kwenye lift na ukauzu ukamvaa.

“Uza hisa zote tunazomiliki ndanni ya kampuni ya Taita”Aliongea na kauli ile ilimfanya meneja kushangaa , kana kwamba amesikia vibaya.

“Mkurugenzi kwanini kuuza katika wakati muhimu kama huu?”

“Bidhaa zao zinaenda kupoteza thamani muda si mrefu na kudorora sokoni hivyo hisa zao kushuka”Aliongea na kauli ile ilimchanganya meneja.

“Umeshindwa kuona mabadiliko ya wafanyakazi ndani ya kampuni ya Taita , unadhani ni kwanini idara ya usafirishaji imeongeza wafanyakazi katika maghala yao?”

“Kwasababu uwezo wao wa kudhalisha umefika mwisho , hivyo presha ya bidhaa kuwa kubwa kuliko uwezo wao.., kwanini sikulifikiria hili”Aliongea yule Meneja huku akijiona mzembe .

Meneja yule kabla hata hajaanza kutaka kumsifia Regina kwa uwezo wake wa kuona mbali Linda alikuwa ashabonyeza kitufe tayari na lift ilijifunga.

Ilienda kufunguka tena katika floor nyingine na Regina hakutoa kwenye lift lakini mbele yake kulikuwa na mwanamama wa makamo na alimkabidhi Linda nyaraka ambazo alimpatia Regina.

“Mkurugenzi!, Farida Group hawapo tayari kuhamisha umiliki wa ardhi kwetu, wanasema wanataka ongezeko la milioni mia mbili , tuchukue hatua gani?”

Regina palepale alichukua karamu ya rangi nyekundu na aliandika maandishi makubwa kwa lugha ya kingereza

“Waambie tutawaongezea mpaka milioni mia tano’

Mwanamama yule mara baada ya kuona maandishi yale alishangaa na aliona pengine Boss wake amekosea.

“Mkurugenzi wanataka ongezeko la thamani la milioni mia mbili tu”

“Fanya kama nilivyokuambia , kisha subiri mpaka wafanye maamuzi na kuja kwangu kwa ajili ya kusaini”

Mwanamama yule aliishia kutoa mdomo tu lakini aliishia kutingisha kichwa asijue bosi wake anachopanga ni nini.

Lift ilijifunga tena na Hamza ambae alikuwa amesimama nyuma ya Regina alikuwa kwenye dumbuwazi na alishikwa na shauku ya kutaka kujua kauli ile ilimaanisha nini.

“Mkurugenzi au nimesikia vibaya , kama wanahitaji ongezeko la thamani ya milioni mia mbili kwanini uwaongezee mpaka milioni mia tano , inamaana unatoa milioni miatatu ya bure?”

Regina hakujibu swali lile kwani Lift ilikuwa ishafunguka tayari na kwa mara nyingine kulikuwa tayari na mtu aliekuwa akisubiri na alikabidhi nyaraka ambazo zilisainiwa na Regina.

Floor kwa floor mwanamke huyo alipita na kila floor alikuwa akifanya maamuzi na kuweka sahihi baadhi ya mambo kwa umakini mkubwa na mengi ya maamuzi yalikuwa kinyume na meneja wa idara husika lakini licha ya hivyo hakuna ambae alipinga maamuzi yake , ilikuwa ni kama vile walijua maamuzi yake yapo sahihi zaidi kuliko ya kwao waliokubaliana.

Kilichomshangaza zaidi Hamza ni namna walivyofika katika floor ya juu zaidi baada ya kukutana na mama mtu mzima alieonekana kuwa na uzoefu wa muda mrefu lakini alitii kauli ya Regina bila ya kuuliza kabisa.

Baada ya kumaliza floor zote za jengo hilo , hatimae walifika floor ya juu kabisa ambapo ndio ofisi ya mrembo huyo hupatikana , ilikuwa ni ofisi kubwa mno yenye vioo vikubwa ambavyo havipitishi risasi

Kupitia madirisha hayo ya vioo alikuwa na uwezo wa kuona hadi maeneo ambayo yapo nje ya jiji la Dar es salaam.

Hakukuwa na mapambo mengi ukiachana na vyungu vya maua na shelf kadhaa za mafaili , yaani ilikuwa ofisi kubwa lakini vitu vichache na rangi yake iliendana na wajihi wa Regina kabisa.

Regina alikaa katika kiti chake cha kibosi huku kulia akiwepo Hamza na kushoto akiwepo Linda ambae alimkabidhi Regina nyaraka nyingine kuzipitia.

Regina alitumia muda mrefu kidogo kupitia zile nyaraka na Hamza alionyesha kuchoka hivyo alijikalia zake kwenye sofa huku akicheza game la pooltable kwenye simu yake lakini muda uleule Regina aliinua macho yake na kumwangalia.

“Linda mpatie nyaraka za Farida Group”Aliongea Regina na Linda alifungua faili kupitia kishikwambi na kumpatia Hamza ambae alianza kusoma mara moja

“Hii inahusu nini?”

“Si uliuliza swali kwanini nimeongeza pesa zaidi licha ya ongezeko la thamani waliloomba katika kipande cha ardhi nilichotaka kununua?”Aliuliza Regina na Hamza alitingisha kichwa.

“Sasa nakupa nusu saa unitafutie sababu kwanini nimefanya maamuzi hayo kupitia hizo taarifa za kiuchunguzi za kampuni ya Farida Group , ukifanikiwa utapatiwa ofisi ya kwako peke yako”

“Ofisi ya kwangu , unamaanisha itakuwa na tarakishi kabisa?”Hamza alikuwa na mpango wake , alijua ofisi kubwa kama hizo zina mtandao wa internet wenye spidi hivyo atatumia muda huo kutengeneza pesa online.

“Ndio, kila kitendea kazi”Aliongea na Hamza aliona vizuri na kwa haraka sana alianza kusoma taarifa hio.

Regina hakumjali tena , alichokifanya ni kwa ajili ya kumzuia Hamza kuwa bize kwa muda , akijua fika hawezi kupata sababu ndani ya muda wa dakika ishirini ,hata Linda mwenyewe alijua kabisa Hamza hawezi kutoboa na kujua sababu , lakini baada ya dakika tano Hamza alipumua kwa nguvu huku akijinyoosha.

“Nini tatizo?”Aliuliza Regina.

“Acha kumsumbua Mkurugenzi na sauti zako za ajabu”Aliongea Linda kwa kuonya

“Sio kama namsumbua , nishaona sababu tayari”

“Mh , nakupa nafasi nyingine tafuta kwa umakini”Aliongea Regina , hata Linda mwenyewe alijua haiwezekani kwa muda mchache hivyo , ukweli ni kwamba alijua Hamza hata hakumaliza kabisa kusoma taarifa yote maana ilikuwa na kurasa za kutosha.

“Farida ni kampuni ambayo ineonekana imara kwa nje lakini kwa ndani wapo katika hatari ya mlolongo wao wa kimapato . kama hii ardhi hawatoiuza mapema ili kupata pesa , kuna uwezekano wakafirisika”Aliongea Hamza na kauli ile ilimfanya Regina kumkazia Hamza macho

Katika akili yake alikuwa akishangaa na kujiambia yaani ndani ya dakika tano tu alikuwa ashaona taarifa iliojificha ya namna hio katika nyaraka hio , spidi yake ya kusoma aliona ni ya kutisha mno.

Linda hata yeye alikuwa kwenye mshangao , hakuamini kama Hamza aliweza kumaliza kusoma tayari hio nyaraka ndani ya dakika chache.

“Murugenzi niseme tu mbinu yako ni kuntu sana , kama ungeongeza milioni mia mbili kama walivyohitaji wangekuuzia haraka , lakini kitendo cha kuongeza milioni mia tano zaidi watapatwa na mashaka na kujiuliza kwanini unataka kununua ardhi yote kwa gharama kubwa kiasi hicho , watajiuliza au kuna kitu ambacho hawakuzingatia kuhusu hio ardhi ambacho kinaweza kukupa faida kubwa , kwa mbinu hio watasita kwanza kuuza ili wajue sababu ya wewe kutaka kununua kwa gharama kubwa , lakini wakati huo hakuna kampuni ambayo itakuwa tayari kununua ardhi kwa bei kichaa kama hio , hivyo wasiwasi wao utawafanya kupitisha siku muhimu ya kuuza na siku watakayo ona wakuuzie kwa ongezeko la milioni mia tano , unachofanya ni kuwakataa tu kiana na hawatakuwa na jinsi tena , mwishowe watakuuzia kwa thamani ya mwanzo kabisa, hawatokuwa hata na ubavu wa kuomba kuongezewa milionni mia mbili nyingine kwasababu hawana muda wa kutafuta mnunuzi mwingine”

Baada ya Hamza kumaliza kuongea Regina macho yake yalionyesha ishara ya kuridhika na jibu lake , aliona hakuwa amekosea tokea mwanzo , ijapokuwa Hamza anaonekana kama mwanaume muhuni muhuni mwenye tamaa na mbahili lakini akili yake ilikuwa ikifanya kazi vizuri , anao uwezo wa kujifunza na kuelewa kitu kwa haraka na kwa tabia hio ana uwezo wa kufanya jambo kubwa baadae. Hayo ndio yalikuwa mawazo ya Regina kwenda kwa Hamza.

Linda ambae alikuwa pembeni ya Regina alijikuta akishagnaa pia , aliona alikuwa amemchukulia poa huyo msaidizi mpya wa bosi wake lakini aliona yeye ndio alikuwa na makosa , inakuwaje bosi wake mwenye akili kubwa kutafuta mtu ambae hana uwezo , hivyo hakumpa sifa Hamza kwa kuwa na akili bali sifa alizielekeza kwa bosi wake kwa kuwa na jicho la ziada katika kujua uwezo wa mtu.

“Murugenzi, kama hii mbinu ikifanikiwa , nakuambia watu wa kampuni ya Farida watakuchukia kufa , watapata athari kubwa za mzunguko wa pesa ndani ya kampuni yao”Aliongea Hamza.

“Ukiwa mfanyabiashara , soko unalichukulia kama uwanja wa vita , kwasababu wao wenyewe ndio wameonyesha tamaa na kwenda kinyume na bei ya mwanzo , sidhani wanahaki ya kunilaumu kwa kutokuwa na huruma, pili kama wana akili ni kheri wakanifuata na kuniuzia ikiwa mapema , wakichelewa watakuwa wanajiingiza wenyewe katika mtego wangu kwa tamaa zao”

“Bosi , una akili sana , mtu wa kawaida hawezi kufikiria kwa namna yako”Hamza alimsifia.

“Hata wewe upo vizuri , sio mbaya umeweza kujua sababu ndani ya dakika tano tu”

Hamza mara baada ya kusifiwa kwa mara ya kwanza aliachia cheko lakini ambalo lilikuwa la kistaarabu kidogo

“Hamna , unajua nini bosi , mimi ni wa kawaida sana, akili yangu ipo ndani ya wastani wa kila mtu”

“Don’t be too arrogant , our CEO is a member of Pars Society , don’t think that just because you’re a little smart, you’re that great”Aliongea Linda kwa kujiamini kwa kingereza akimaanisha kwamba aache majigambo kwani bosi wake ni mwanachama wa Pars , hivyo kwa viakili vyake vidogo asijione mkubwa na kuanza kupandisha mabega.

Upande wa Hamza alishangaa mara baada ya kusikia Regina ni mwanachama wa Pars.

“Kwahio Boss wetu ni moja ya wanachama wa jamii za watu wenye IQ kubwa?”

“Unaonekana kujua mengi kama umeelewa sentensi yangu , ndio bosi wetu ana IQ 180 hivyo huhesabika kama Genius , kama sio hivyo unadhani kwanini kila mtu ndani ya kampni anaamini maamuzi yake na kuyafauta?”

The Standard wisdom societies ni umoja ambao wanachama wake wana IQ kubwa, inasemekana ili kujiunga katika umoja huo mtu anapaswa kufikia angalau vipimo vya IQ kuanzia 175 na kuendelea , sio umoja ambao unaweza kujiunga kwa pesa na hadhi.

Kwa kadri ambavyo alikuwa akielewa watu ambao huhesabika kama Genius ambao IQ zao ni kuanzia 180 wana uwezo wa juu sana katika maswala ya kitafiti , ubunifu na biashara , lakini wakati huo huo wakiwa vibaya sana katika baadhi ya sehemu kiasi kwamba wanaonekana kama watu dhaifu.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba majiniasi wanaweza kuwa juu ki uwezo aidha iwe katika maswala ya kitafiti au biashara lakini likija sehemu nyingine wanafanya vibaya sana , na hili linaweza kukushangaza, ki ufupi ni kwamba wanaonekana sio wa kawaida na maamuzi yao yanaweza kuwa ajabu mno.

Hamza aliweza kuliona hilo , hasa ukizingatia na tabia ya Regina mbele ya familia yake, alikuwa na mahusiano mabaya sana na baba yake.

“Huruhusiwi kuongea kuhusu jamii hio tena siku nyingine”Aliongea Regina na kumfanya Linda kufubaa kwa kuona alifanya kosa, lakini aliitikia kwa adabu.

Hio ndio moja ya sifa nyingine ya Regina , wafanyakazi wa kampuni hio walikuwa wakijua taarifa hio nyeti juu ya kuwa mmoja ya mwanachama wa jamii ya watu wenye busara na hawakuwa wakizungumzia hilo hadharani.

Sasa hata wakurugenzi wa bodi walielewa kwanini Mkurugenzi wa Zamani yaani babu yake Regina aliweka ngumu kumfanya msichana mdogo aliekulia katika kituo cha kulelea Yatima kuwa kichwa cha kampuni , kwa taarifa walizokuwa nazo alionyesha kuwa na akili isiokuwa ya kawaida tokea akiwa mdogo, kitu pekee ambacho wakurugenzi wa bodi hawakuwa wakifahamu ni ukichaa wa Regina, kutokana na Regina kuwa na akili nyingi ndio moja ya sababu ambayo ilimpelekea kuwa na ugonjwa wa nafsi mbili.

“Mnaweza kuondoka sasa, Linda muonyeshe Hamza ofisi yake”Aliongea Regina.

Hamza alikuwa na hamu ya kuona ofisi yake hivyo hakuwa na pingamizi na mkufuata Linda kwa haraka.

“Linda ,vipi kama nisingeweza kujibu , ni ofisi gani ningepelekwa?”Aliuliza Hamza mara baada ya kufikishwa katika ofisi ndani ya floor hio hio ambayo ilikuwa haina vitu vingi zaidi ya tarakishi ya thamni ya kampuni ya Apple na printer

“Haijalishi ungejibu kwa kukosea au kupatia , hii ofisi ndio niliandaa tokea juzi kwa maelekezo ya boss”

Hamza aliona kabisa Regina alikuwa akimchora tu , aliona kabisa Regia anatumia akili yake vibaya kumchezea akili.

Hamza mara baada ya kuchunguza tarakishi hio alitoa tabasamu , ilikuwa na sifa zote za kuitwa tarakishi yenye uwezo wa juu na kwa kuliona hilo alijua kabisa mpango wake wa kuvuna Bitcoin ungeenda vizuri sana. Mara baada ya kujinyoosha kwa kuanza kazi yake ya kutengeneza pesa, Linda aliingia akiwa na rundo la nyaraka na kuzitua mezani.

“Boss amesema unajua kuongea kifaransa kwa ufasaha , anataka utafsiri nyaraka zote kuwa katika lugha ya kingereza , ndio kazi yako utakayofanya kwanzia leo mpaka Ijumaa, ukimaliza print na niletee ofisini kwangu mlango unaofuatia”Aliongea katika sauti ya kiheshima.

Hamza alipitia nyaraka hizo kwa haraka haraka na aligundua ni taarifa za moja ya kampuni ya kifaransa na ilionekana ni nyaraka ambazo hazikupatikana kirahisi ndio maana hawakutaka mtu wa nje ya kampuni kuzitafsiri kutokana na unyeti wake.

“Huyu mwanamke , inaonekana alikuwa amepanga kunipa kazi tokea muda mrefu na sio kwasababu ya kumdanganya Eliza”Aliwaza Hamza mara baada ya kuona kazi ya kwanza ni kutafsiri kifaransa.

“Naona sasa nina kazi ya kufanya”

“Hakikisha unafanya kazi na huleti uzembe , kampuni yetu inajali sana watu wachapakazi na sio watu wazembewazembe kazini”

“Sawa”

Alijibu Hamza lakini mara baada ya Linda kutoka Hamza alikimbilia mlango na kuufunga kwa ndani na kisha alirudi kwenye tarakishi yake na kuanza kazi ya kutengeneza mzingira ya kuvuna sarafu.

“Kama nilivyotarajia spidi ya hii internet ni kiboko”Alijiongelesha Hamza , lakini alishituliwa na simu yake ilioanza kuita , aliitoa mfukoni na mara baada ya kuangalia jina la anaepiga ni mama Iryn.

Hamza alishasahau kama alikuwa na mwanafunzi na ni kama simu hio ilimkumbusha alikuwa na miadi ya kumfundisha Iryn wiki hio.

“Habari za uzima mwanangu?”Sauti iliita , Mama Iryn alikuwa akipendelea kumuita Hamza mwanae.

“Salama kabisa mama , habari za nyumbani?”Hamza aliongea alikuwa na upole kabisa.

“Salama kabisa , wiki hii mwanafunzi wako alikungojea hujatokea , kanikumbusha nikupigie simu”Hamza mara baada ya kusikia kauli ile alishindwa kujua afanyaje , kama ingekuwa siku kadhaa nyuma asingekuwa na shida ya kujibu lakini muda huo ni mwajiriwa wa milioni kadhaa hakuona haja ya kwenda kufundisha.

“Naomba unisamehe sana mama , ila nipo field kwasasa , muda wa masomo unanibana sana , semister yetu hii ya mwisho mwisho”Hamza alijitetea , ndio namna pekee alivyoona ajibu.

“Oh! , ndio nilichomwambia Iryn lakini hanielewi , mimi naelewa upo mwaka wa mwisho na unahitaji muda mwingi kujiandaa”

“Ni kweli kabisa mama , nahitaji muda wa kujiandaa”Aliongea Hamza , ukweli ni kwamba hajawahi hata kufanya discussion na wenzake , maisha yake ya chuo yeye ni kama vile anafanya utani , lakini likija test hajawahi kufeli.

“Basi hakuna shida baba yangu , nikutakie masomo mema na kujiandaa kwema”

“Asante mama nikutakie na wewe afya njema na masomo mema kwa Iryn”

Baada ya kuongea hivyo mama Iryn aliaga na kukata simu na kumfanya Hamza avute pumzi na kujiambia ni bora kukiepuka kikombe hicho,alijua kwenda kwa Iryn kwa vyvoyte vile ni kujiingiza kwenye majaribu ya mwanafunzi huyo wa Advance.

Hamza hakutaka kuwaza sana na alirudi kwenye kazi aliokuwa akitaka kuendelea nayo.

Baada ya kupoteza lisaa lizima kwenye mtandao wa Blockchain alirudi katika kazi ya kutafsiri , Hamza aliangalia nyaraka alizokuwa amepewa na aliona haikuwa kifaransa kigumu, ni kile cha kibiashara hivyo alikaa vizuri kwenye tarakishi na kuanza kuchapa kwa spidi kubwa , alikuwa na spidi sio ya kawaida na ndani ya masaa matatu bila ya kupumzika alikuwa amemaliza kila kitu na alipoangalia saa ilikuwa ni saa saba kasoro mchana, hivyo alimalizia kuprint kabisa.

Baada ya kumaliza alisimama na kuanza kujivuta vuta lakini ni dakika hio hio sauti kutoka nje pamoja na kugongwa kwa mlango ilisikika , alikuwa ni Linda aliekuwa akimtaka kufungua.

“Kwanini umejifungia?”

“Ofisi ni yangu ni maamuzi yangu kufunga na kufungua”Aliongea na kumfanya Linda amwangalie kwa kejeli huku akimpita na kusogelea tarakishi.

“Ulichokuwa ukifanya umeficha wapi?”Aliuliza

“Nliichokuwa nikifanya, unamaanisha nini?”

“Ulikuwa ukicheza michezo yako ya Blockchain”

“Umejuaje nilikuwa nikifanya hivyo?”

“Unadhani idara ya IT inafanya kazi gani ,spidi ya Internet ilipungua kwa kiasi kikubwa na kufanya uanze kufuatiliwa unachofanya”

Hamza mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akianza kujikuna kichwa na kuona ni ukatili kwa kampuni kufatilia kile wanachokifanya wafanyakazi ndani ya ofisi zao.

“Nimepewa maagizo nikakuripoti kwa Mkurugenzi na kulingana na sheria mshahara wako unakatwa asilimia ishirini”Mara baada ya kuongea kauli hio Linda aligeuza kutaka kuondoka.

“Hebu subiri kwanza , kazi ulionipatia nishaimaliza , kwanini mnikate mshahara , sikuwa na chakufanya ndio maana nikaingia kwenye vitu vingine”

“Unaongea nini wewe , yaani umemaliza kazi ya siku tatu ndani ya masaa machache?”

“Ndio , kama huamini angalia , sikupata muda tu wa kukukabidhi kazi”Aliongea Hamza huku akimpatia Linda katarasi ambazo ashamaliza kuziprint.

Linda alijikuta akishangaa mara baada ya kukagua karatasi hizo , zilikuwa zimeandikwa kwa usanifu mzuri sana tena kwa kingereza rasmi cha kikazi kabisa, lakini hata hivyo hakutaka kumuamini , aliingia kwenye mtandao na kujaribu kukopi na kupaste baadhi ya maneno ya kifaransa katika programu ya kutafsiria ili kuhakiki na kweli ilikuwa sahihi kabisa na aliishia kumwangalia Hamza kwa maswali mengi.

“Umewezaje kukamilisha kazi hii kwa muda mfupi tu?”Aliuliza na Hamza alitingisha mabega.

“Halafu kuna baadhi ya maneno yalikosewa kuandikwa , nimeyawekea alama na kisha nikayabadilisha wakati wa kutafsiri unaweza hakiki pia”Aliongea Hamza huku akimkabidhi Linda zile karatasi nyingine.

Linda aliishia kumwangalia Hamza kwa sekunde kadhaa na kisha akageuka.

“Ni muda wa lunch unaweza kwenda kula , nitampatia hizi nyaraka mkurugenzi”

“Subiri kwanza ,vipi kuhusu mshahara wangu sasa?”

“Kwa leo nitaacha hili lipite , ukirudia tena kufanya mambo nje ya utaratibu wa kazi kwa tarakishi za kampuni sitolifumbia macho”Aliongea na kisha alifungua mlango kutoka nje.

“Vipi wewe huendi kula , Mkurugenzi yeye anakula wapi?”

“Nipo kwenye diet , kuhusu mkurugenzi hali chakula mchana , hivyo jali mambo yako”Aliongea na hakutaka tena kuendelea kuongea na Hamza hivyo aliondoka.

Hamza licha ya kwamba alikuwa feki mbele ya Regina lakini kusikia kwamba hakuwa akila chakula cha mchana aliona mwanamke huyo anatia huruma na pengine jambo hilo hata Shangazi hakuwa akilijua la sivyo angekuwa mkali, lakini kwasababu hakuwa na chakufanya aliamua kupotezea na kutoka ndani ya ofisi yake na kwenda chini kabisa mgahawani .

Kampuni kubwa kama hio hakukuwa na haja ya kuongelea maswala ya maisha mazuri ya wafanyakazi wakiwa kazini , mgahawa wa kampuni ulikuwa mzuri mno na kulikuwa na kila aina ya chakula kizuri

Kila mtu alikuwa bize na chakula , wafanyakazi walikuwa wengi na baadhi yao walikuwa makundi makundi , kwasababu Hamza alikuwa mgeni yeye alienda zake kuchukua chakula na kisha kutafuta pakukaa.

Kampuni hio ni kama ilikuwa na upendeleo na wanawake kwani walikuwa wengi mno kuliko wanaume , Hamza licha ya kwamba alikuwa mgeni hakutaka kujitenga hivyo aliona sehemu sahihi ni mahali ambapo kuna watu ili kujenga kidogo mazoea.

Lakini kabla hata hajapata sehemu , aliitwa na kumfanya ageuke na hapo ndio aliweza kumuona Asha pamoja na msichana mwingine aliemfahamu kwa jina la Mirium , walikuwa ni wasichana ambao aliwakuta pamoja na Eliza wakiwa mwembeni Bar.

“Hello, nakuona Asha ulivyopendeza”Aliongea Hamza.

“Kwahio umemuona Asha tu , mimi hujaniona?”Aliongea Mirium huku akijifanyisha mwanamke mwenye wivu.

“Ndio”Alijibu Hamza akiwa siriasi na kufanya warembo wale kumshangaa kidogo na kisha waliangua kicheko.

“Eliza hajarudi kutoka safarini bado , lakini alituambia umepata kazi hapa makao makuu kama msaidizi namba mbili wa bosi , Hamza usitusahau kwenye ufalme wako”Aliongea Asha kwa tabasamu.

“Ah! , msinitegemee sana , mwenyewe sijui ni kwa muda gani nitafanya kazi , pengine ninaweza kufukuzwa ndani ya miezi mitatu tu”

“Sio kirahisi hivyo , kama umemfanya bosi kukupa kazi muhimu kama hio basi ni wazi upo vizuri upstairs

“Hebu acheni soga bwana , tutafuteni pakukaa kwanza muda unaenda”Aliingilia Mirium ambae alionekana kuchoka kusimama na kuachwa kwenye mazungumzo.

Baada ya kusogea upande wa kushoto mwa mgahawa huo Hamza aliweza kuona nafasi za wazi na kulikuwa na mwanamke mmoja tu aliekuwa akila peke yake na alimfahamu , alikuwa ni Kapteni Yonesi mkuu wa idara ya usalama wa kampuni.

“Twendeni pale”Aliongea Hamza, alitokea kumkubali Yonesi , ijapokuwa alikuwa na tofauti sana na wanawake wengi waliokuwa hapo ndani lakini ukauzu wake ulimfanya kuvutia , isitoshe alikuwa mrembo

“Unamaanisha tutakae na Kapteni Yonesi, Akha hatuendi pale sie”Aliongea Asha.

“Kwanini sasa , yule si mtu kwanini kama mnamnyapaa?”

“Ana sheria ngumu sana ukikaa nae kwenye meza , hataki muongee ongee wakati wa kula, hasa umbea umbea , yaani ukikaa nae Mjeda yule hakuna amani na chakula ni kama unakula sumu”Aliongea Mirium.

“Halafu ukimchokoza kidogo tu atakasirika , lazima akushikishe adabu , ni mkali mno mbele ya wafanyakazi , na hakuna wa kumfanya lolote maana anaaminiwa sana na Mkurugenzi”

“Hamza usije kujaribu bahati yako pale , kuna wenzako waliowahi kufika hapa na wakajifanya wana swaga na kuanza kutupia maneno pale , kilichowakuta ni udhalilishaji”Asha naMirium walikuwa wakipokezana kumjadili Yonesi na washasahau walikuwa wameshikilia vyakula mkononi.

“Kama nyie hamtaki kukaa pale , tafuteni eneo lingine mimi nitakaa”Aliongea Hamza na hakusubiri hata majibu yao na alitembea mpaka katika meza aliokaa Kapteni Yonesi.

Wafanyakazi waliokuwa ndani ya mgahawa huo waliona kitendo kile na kwasababu walishamjua Hamza ni mgeni , walitaka kuona kile kitakachotokea.

Yonesi alikuwa zake bize na chakula na mara baada ya kuhisi mtu kuongezeka katika meza yake ndio aliinua uso wake na alishangaa kumuona ni Hamza.

“Ni wewe?”

“Niambie Kapteni naona tunakutana tena”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu na kukaa mkao wa kula.

“Kakae kwenye meza nyingine”Aliongea Yonesi , kibabe.











SEHEMU YA 20.

Yonesi kama bodigadi alikuwa na taarifa zote za Regina kuajili msaidizi wake mwingine na mara baada ya kufahamu ni Hamza aliishia kushangaa na kujiuliza nini kinachoendelea , hakuwa na taarifa zote, alihisi kuna kitu kinaendelea kati yao lakini aliona ni kheri ajirushe baharini aliwe na mamba kuliko kuamini Regina anaweza kutoka kimapenzi na mwanaume kama Hamza.

Kingine ambacho kilimfanya Yonesi kumdharau Hamza ni tabia yake ya kukosa aibu na uwoga woga usio na maana , yeye alipenda wanaume ngangari lakini kitendo cha siku ile kumuachia msaala kule gongo la mboto alimuondolea nyota ya heshima kama mwanaume.

“Kapteni, unapaswa kuwa na sababu ya msingi kunifukuza kwenye hii meza, hakuna sheria inayonizuia kukaa kwenye hii meza si ndio?”

“Nenda kakae meza inayofuatia haina mtu , kwani lazima ukae hapa”

“Siendi popote”Aliongea Hamza.

“Kwanini?”Aliuliza huku akiwa amekunja ndita.

“Kwasababu nataka kuona namna mwanamke mrembo kama wewe unavyokula”

Yonesi alikuwa ni mweupe kabisa , kauli ile japo haijamshangaza sana lakini kulikuwa na viashiria vyote, sura yake ilianza kubadilika rangi na kuwa nyekundu.

Ni kweli anatongozwa sana , lakini haijawahi kutokea mwanaume kuongea kuhusu muonekano wake bila wasiwasi kama Hamza, lakini ilikuwa ni dakika ile aling’ata meno yake kwa hasira

“Wewe mpuuzi , rudia kauli yako tena uone”

“Kapteni nimesema wewe ndio mrembo kuliko wote hapa , lakini ajabu umekaa mwenyewe”

“Ukiendelea kuongea ujinga wako , nitakushushia kipigo hapa hapa bila kujali watu”

“Ah!, basi yaishe Kapteni , nimeacha usije kunipig”Aliongea Hamza akijifanyisha kuwa mzembe huku akinywa juisi yake kwenye glasi.

Yonesi alikosa hata nguvu ya kumfukuza Hamza tena na aliamua kujiweka bize na chakula chake , lakini kadri alivyokuwa akila ndio alivyokosa ule uhuru aliokuwa nao na aliinua macho yae na kumwangalia Hamza , lakini ndio anaona Hamza alikuwa akimkodolea macho eneo la kifuani.

Hamza alikuwa akifurahia chakua chake , kilichomfanya kumkodolea Yonesi macho ni aneo la kifuani tu , alikuwa akiona namna manyonyo yake yalivyokuwa yakivutia.

“Mh , juzi nadhani sijamwangalia vizuri , anaita sio poa”Aliwaza Hamza ndani kwa ndani

“Unaangalia nini?”Aliuliza Yonesi kibabe.

“Unataka kujua kweli wa ninachoangalia?”

“Jibu swali?”

“Naangalia hayo mayai kwenye sahani yako”

“Kuna mayai gani kwenye sahani yangu!!?”Yonesi aliongea kwa hasira mno huku akipiga kofi meza na kufanya watu kugeuka na kuangalia kinachoendelea, lakini Hamza alijifanyisha kuwa bize kula chakula chake.

“Kapteni ni kweli nimekuona na mayai kabisa , tena mawili ..”Hamza aliendelea kumchokoza Yonesi.

“Mbwa wewe ,nani ana mayai , sema ulichokuwa ukiangalia lasivyo nitakufanya kipofu”Aliongea huku akimnyooshea Hamza na uma.

“Kama unabisha , wewe unadhani nilikuwa nikiangalia nini?”

“Kwahio unabishana na mimi , unadhani maneno yangu ni ya bure siwezi kukufanya chochote”

Yonesi kwenye maisha yake hakutaka kuonewa kizembe na kwasababu hasira zishamvaa aliona amshikishe adabu Hamza hapo hapo , hivyo alichukua uma na kumlenga nayo uelekeo wa macho.

Watu waligeuka mara baada ya kuona tukio hilo wakitaka kujua mwisho wake

Lakini Hamza hakukwepa wala kufanya chochote , alikuwa akiendelea kutafuna huku Uma ile ikimkaribia machonni .

Yonesi asingeweza kumchoma nayo kweli machoni na baada ya kufika nchi kadhaa karibu na jicho la Hamza aliishia njiani , upande wa Hamza hakupepesa macho hata kidogo.

Kitendo kile kiliwashangaza watu , maana mtu yoyote angeogopa kwa kulengwa na ncha machoni , lakini Hamza hakuonyesha hofu.

“Kapteni unajua kila mtu anatuangalia , huoni sio vizuri kunichokoza mchana yote hii”Aliongea Hamza akitabasamu , alijiambia Yonesi hata amshikilie bunduki hawezi kuogopa.

Yonesi aliishia kushusha uma chini huku akijiuliza imekuwaje huyo mpuuzi leo kujiaminni hivyo.

“Leo nitakusamehe , ukinichungulia siku nyingine hutoamini nitakachokufanyia” Aliongea na kumfanya Hamza kutabasamu tu.

“Kapteni , naomba kuuliza?”

“Nini?”

“Wewe ni D au F?”

“”…”

Yonesi alishindwa hata kuongea kutokana na namna alivyokuwa amekasirika kwa mara nyingine na Swali lile.

“Mpuuzi wewe , ulikuwa kweli ukinichungul..”

Kabla hata hajamaliza sentensi yake alijizuia mara baada ya kuona ameongea kwa sauti kubwa na kufanya watu kumwangalia , uso wake ulikuwa umebadilika mno kutokana na hasira , hakuwahi kudhalilishwa kiasi hicho ndani ya kampuni.

“Hamza nifuate”Aliongea kwa kuamrisha , hakutaka kuleta fujo ndani ya mgahawa , aliona ni bora amtoe hapo akampe kibano pembeni.

“Sijamaliza kula”Hamza alikataa.

“Wew..”

Kitendo kile kilifanya Yonesi agundue watu walikuwa wakicheka kwa siri na aliishia kusugua meno yake kwa hasira na alifyatua mkono wake wa kulia kijeshi kwa ajili ya kumshika Hamza tai , lakini Hamza alirudi nyuma na kufanya mkono wake kupita.

Yonesi aliona Hamza aliotea hivyo alizunguka upande wa pili kwa ajili ya kumshika , Hamza hakuwa na haraka mara baada ya kuona Yonesi anamkaribia alipiga kiti teke ambacho kilienda kumvaa afande Yonesi na kumfanya akose mhilimili na kuelekea chini akitanguliza uso.

“Ahh..”

Yonesi alijua alikuwa akidondoka vibaya , kitendo cha Hamza kupiga kiti teke hakukiotea kabisa ,sekunde hio akiona anakwenda kudondoka vibaya Hamza alikuwa ashamzuia kwa mkono mmoja na kumshikilia kifuani sehemu ileile ambayo ilimfanya kukasirika kwa kuchunguliwa.

Yonesi ni kama alikuwa amepigwa na shoti , alijikuta akitetemeka mara baada ya kuona namna mkono wa Hamza ulivyoyashikilia manyonyo yake

“Wewe muhuni umenigusa..”

“Kapteni , unamaanisha nini kugusa wakati nakuzuia usidondoke”Aliongea Hamza na muda uleule Yonesi alisimama vizuri, mara baada ya kuona macho ya wafanyakazi yamezidi kuongezeka , alimwangalia Hamza kwa macho makali.

“Subiri uone , inaweza isiwe sasa hivi ila nitakufanya ujutie kwa ulichonifanyia leo”Aliongea Yonesi kwa hasira na kisha aligeuka zake na kuondoka huku kichwa kikiwa chini , kwa mara ya kwanza mbabe wake ndani ya kampuni alipatikana.

Kila mtu alimwangalia Hamza kwa mshangao na kumkubali , hio ilikuwa mara yao ya kwanza kuona Yonesi akitawaliwa na mwanaume na ashindwe kufanya chochote, wanaume wengi walionekana dhaifu mbele ya Yonesi.

Hamza wala hakujali vile vitisho na baada ya kumaliza kula alichukua matunda ya apple kwenye friji na kisha akaweka kwenye mfuko na kuondoka nayo , alijua Regina hajala hivyo alijihisi sio vizuri kutopeleka chochote hata kama ataonekana anajipendekeza.

Mara baada ya kutoka kwenye lift moja kwa moja alienda mpaka kwenye mlango wa mkurugenzi na kugonga.

“Come in”

Hamza alisukuma mlango na kisha akaingia , aliweza kumuona Regina akiwa bize amekodolea tarakishi yake huku akionekana kuandika vitu kwa karamu kwenye notebook.

Mbele yake kulikuwa na nyaraka nyingi ambazo ilionekana alikuwa akizifanyia kazi pia , ki ufupi alikuwa bize.

“Weka ripoti hio juu ya meza na unaweza kuondoka”Aliongea Regina bila ya kuangalia aliengia , alijua ni Linda sekretari wake.

Mara baada ya Hamza kuweka matunda yale juu ya meza ndio sasa Regina aliinua macho na kumwangalia.

“Kwanini ni wewe?”

“Sekretari wako kasema hupendelei kula chakula cha mchana na nimeona sio vizuri , kula hata matunda nimekuletea”

“Nishakula na haikuhusu kama nimekula au sijala”Aliongea bila ya ishara ya furaha yoyote.

“Kwahio umekula?”Aliongea Hamza huku akizungusha macho yake na ndio alipoweza kuona mfuko uliojaa makopo , yalikua kama kumi na mbili hivi.

“Gum- syrup!!”Hamza alionekana kushangaa ,

“Hiki kinywaji ndio unachotumia kama chakula cha mchana ?”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumwangalia.

“Kumbe unajua hata jina lake kwa kingereza ni Gum syrup?, kweli wewe ni mwanachuo una exposure ya kujua vitu vingi”Aliongea Regina lakini Hamza hakujali.

“Hata kama unataka kuzuia njaa hutakiwi kutumia aina hii ya kinywaji cha virutubisho , unatakiwa kula chakula?”

“Chakula kinaathiri mzunguko wa damu na oxygen kwenye ubongo na muda wangu wa kufanya kazi ni muhimu sana, sitaki kusinzia, kitu kingine huna kigezo hata kimoja cha kunijali”Aliongea kikauzu.

“Kula angalau hata hayo matunda , kuliko kushinda na tumbo ambalo halina kitu”

Licha ya kwamba Hamza alikuwa akionyesha kumjali , lakini kwake alimuona kama mtu asiemfahamu tu.

“Ondoka nayo , sitokula”Aliongea lakini Hamza alitoa kicheko na kisha akashika simu yake.

“Ngoja nimpigie shangazi na kumwambia unashindia vinywaji vya virutubisho mchana na huna ratiba ya chakula cha mchana”

Regina mara baada ya kuona anachotaka kufanya Hamza alijua maana yake ni nini , kama kweli Shangazi angelifahamu hilo angekuwa na wasiwasi mno maana kwake ni kama mama.

“Weka simu chini , acha kupiga”

“Nitafanya hivyo kama utakula matunda yote nilioleta la sivyo hili swala nitalifikisha kama lilivyo kwa Shangazi”

“Mbona unapenda kunisumbua na mitunda yako mibaya mibaya”Aliongea huku akionyesha hasira za wazi.

“Nakusumbua sio,ngoja tuone kama nakusumbua , mimi nampigia”

“Wewe inakuhusu ni nini kwanza kula kwangu , unanijali kama nani?”

“Nimeshiba tayari ila kuona hujala chochote nimejikuta na shikwa na huzuni”

“”..”

Regina aliishia kuegamia kiti chake huku akimwangalia Hamza , ni kama hakuwa ametegemea angetoa jibu la aina hio.

“Huzuni utoe wapi , umekaa kiuongo uongo tu”

“Acha maswali mengi , unakula au huli”

“Nitakula , acha kuendelea kunichukiza”

“Hilo ndio jibu sasa , nitakaa hapa hapa mpaka nione umemaliza ndio naondoka”Aliongea lakini Hamza alimwangalia mara baada ya kuona Regina amekunja sura huku ameshikilia mkononi apple.

“Sipendi kula na maganda yake na mimi mvivu wa kumenya”

“Ukila na maganda yake ndio vizuri , yamebeba Asidi ya kutosha inayosaidia kuondoa uchomvu”

“Ndio hivyo sipendi sasa , unalazimisha”

“Uvivu tu ndio unasumbua “

Aliongea Hamza na kwasababu hakuwa na chaguo lingine ilibidi atafute kisu na kuanza kuyamenya moja moja na kuyaweka kwenye sahanni.

Spidi yake ya kumenya ilikuwa kubwa mno na ndani ya dakika chache tu alikuwa ashamaliza yote.

Regina alianza kuyatafuna haraka haraka , alitaka kumaliza ili aendeee na kazi yake.

“Halafu una malengo gani , kwanini unalazimisha nile haya matunda?”

“Sina malengo yoyote , ninachotaka ni ujaze hilo tumbo lako , kwanini una mawazo mabaya kila ninachofanya”

“Umekaa kimashaka mashaka ndio maana”Aliongea huku akiendelea kula kama abiria anaetaka kumaliza haraka apande basi.

Baada ya Regina kumaliza kula alionekana kukumbuka kitu na kumwangalia Hamza.

“Zile nyaraka ulizotafsiri nimeziona , umetafsiri vizuri sana kuliko hata Freelancer tuliemwajiri kututafsiria mara ya mwisho, nadhani uwezo wako wa kuongea kifaransa na kingereza ni C2?”

“C2 maana yake ndio nini?”

“Hujui?, Inamaana hujawahi kufanya DEF test?, C2 maana yake ni kiwango cha juu cha kuongea lugha ambayo sio uliozaliwa nayo”

“Sijajifunza kifaransa na kingereza kwa njia rasmi, wakati nilipokuwa nje ya nchi nilikuwa nikiongea na watu mara kwa mara ndio maana nilizidi kuzoea”

“Ushawahi kuwa nje ya nchi, masomoni au?”Aliuliza Regina kwa mshangao , alihisi ni vizuri kumjua Hamza angalau kidogo.

“Ndio nilipofikisha miaka kumi nilidhamia nje ya nchi, kutokana na maisha kuwa magumu nilijikuta nikifanya kila aina ya kazi, bahati nzuri kutokana na muonekano wangu wa kuchanganya rangi nikapata familia”

“Sasa ilikuwaje ukarudi?!!”

“Kuna mambo yalitokea ,nilishindwa kuendelea kuishi katika familia yangu mpya mara baada ya kugundulika kama mtanzania”Aliongea Hamza , Regina japo alikuwa na maswali mengi aliona aishie hapo kuuliza , alitamani kujua ilikuwaje mpaka akafika chuo.

Mara baada ya kumaliza kutafuta yale matunda alihisi ukakasi kwenye midomo na alihitaji maji ya moto kwa ajili ya kusukutua.

“Nitakusaidia kumimina maji?”Aliongea Hamza mara baada ya kumuona Regina akisogelea Dispenser ya maji ya moto.

“Nishafika tayari , haina haja”Aliongea na kumfanya Hamza arudi kukaa kwenye sofa.

Lakini sasa kitendo cha Regina kuinama ili achukue Glasi ilifanya gauni lake kupanda juu kutokana na kuwa na shepu kubwa , alikuwa amechukua tahadhari ya kugeukia upande wa nyuma lakini akasahau kuna kioo ambacho kina akisi mwanga.

Hamza alikaza macho , alikuwa na shauku ya kutaka kuona mwanamke kauzu kama Regina huko ndani atakuwa anavaaje.

Regina mara baada ya kugeuza uso wake na kumuona Hamza anapoangalia alishituka na kugeuka nyuma na hapo ndipo alipojua alikuwa akionekana kwenye kioo kwa nyuma.

“Wewe…!!!”

Regina alijikuta akisimama wima huku akijiweka vizuri na kisha akageuka huku akimkazia macho Hamza , wazo la kumuua Hamza lilimvaa palepale.

Hamza alikuwa ashageuza macho yake na alijifanyisha kushangaa kwa mabadiliko ya Regina.

“Mkurugenzi nini shida , kwanini unafoka?”

“Hujawahi kuona mwanamke , umekuwa chizi?”Aliongea akiwa amekasirika.

“Boss kama unataka kunifokea ni bora ukaniambia sababu , sijafanya kosa lolote”

“Sijawahi ona mwanaume mshenzi kama wewe ambae huna aibu na kuchungulia watu”

“Nini!, unamaanisha nini kukuchungulia , mimi muda wote nilikuwa nikifurahia mandhari mazuri ya jiji letu, Mkurugenzi utakuwa unanifikiria vibaya”

“Bado unabisha tu”Aliongea na wakati huo alimimina maji ya moto kwenye kikombe na kumsogelea Hamza.

“Boss unataka kufanya nini?”

“Kwanini?, unadhani nataka kukumwagia maji kama huna kosa?”

“Mkurugenzi , ni kweli umenifikiria vibaya . ila kama dhamira yako ni kunimwagia maji ya moto basi ni kheri nikimbie tu”Aliongea Hamza lakini muda ule mikono ya Regina ilicheza na kufanya maji ya moto kutoka katika kile kikombe na kuelekea katika miguu yake .

Lakini Hamza alikuwa na spidi kwani aliyakinga yale maji kwa kupitia viganja vyake ili yasimfikie na kitendo kile kilimshitua Regina na mara baada ya akili yake kufanya kazi aliwahi kuweka kile kikombe chini

“Hujaungua?”

“Mikono yangu inasugu na ngozi yake ni ngumu , maji kidogo hivi hayawezi niunguza”Aliongea na Regina mara baada ya kuangalia mikono ya Hamza haijaungua kidogo alijisikia amani.

“Sorry , sijamwaga makusudi”Aliongea Regina bila ya kumwangalia Hamza machoni, hakutegemea kama Hamza angechukua hatua ya kukinga maji na mikono yake yasimuunguze.

“Hakuna shida, ili mradi tu Mkurugenzi hutoendelea kunifikiria vibaya, nitaacha hili lipite”

Mara baada ya kuona namna Hamza alivyoongea kipole aliona pengine ni kweli alimfikiria vibaya na hakuwa akimchungulia.

“Ni kweli hujanichungulia?”Aliuliza kwa kusitasita.

“Kama huniamini basi siwezi kuendelea kujielezea , narudi ofisini kwangu”Mara baada ya kuongea hivyo Hamza alisimama na kupiga hatua kuondoka ndani ya ofisi hio akimuacha Regina kwenye mawazo.

“Mkurugenzi , kabla sijaondoka naomba nikuulize swali?”Aliongea Hamza mara baada ya kufika mlangoni.

“Uliza?”

“Huwa unapendelea rangi ya pink plain au pink yenye maua maua?”Aliuliza na kabla hata hajajibiwa alishatoka na kufnga mlango.

Upande wa ndani Regina alinyanyua kikombe kile cha glasi na kurusha mlangoni , lakini ashachelewa na kilichosikika ni sauti ya kuvunjika tu.

“Hamzaaa..!!!”

Regina alitoa ukulele wa hasira huku sura yake yote ikiwa nyekundu.

Aliona mpango wake wa mwanzo wa kumfundisha kazi kulingana na kozi yake anayosomea ulikua ni wa kijinga , dakika hio hio alishaona alikuwa amemsingizia kumbe yote hayo alikuwa akichezewa akili.

Upande mwingine mara baada ya Hamza kuingia tu katika ofisi yake simu yake ilianza kuita na alipoangalia jina la anaepiga alikuwa ni Amiri rafiki yake.

Alishangaa kidogo kwani tokea siku ambayo alimsaidia kutega kamera hawajaonana.

“Hello!!”

“Bro vipi?”Sauti ya Amiri ilisikika na ilikosa utulivu jambo ambalo Hamza alilijua haraka sana.

“Poa kabisa , mambo vipi?”

“Mambo sio shwari kaka?”

“Kwanini unasema hivyo?”

“Hata sijui nikuelezee vipi , ila nimechanganyikiwa tokea jana”Aliongea na Hamza aliamini lazima ni swala linalohusiana na Mellisa.

“Ni swala la Mellisa nini?”

“Ndio kaka, sijui ni mauza uza gani yanaendelea kwa huyu mwanamke , ila naomba tuonane leo hii , ikiwezekana hata sasa hivi , pengine unaweza kuwa na majibu ya nilichokiona”

“Kwasasa kuna mishe imenishika hapa , unaonaje baadae saa kumi na moja”

“Sina jinsi kaka nitasubiri , wewe ndio mtu wangu wa karibu ninaeweza kukushirikisha hili , pengine unaweza kuwa na majibu , mimi nimekwama”

“Sawa nitakushitua”

Hamza baada ya simu ile alikaa kwenye kiti , alikuwa na shauku pia ya kujua ni kitu gani ambacho kimetokea , maana kwa alichokuwa akiongea Amiri alijua kuna jambo kubwa ameona kupitia zile Kamera za siri.

******

Upande mwingine Amosi alionekana akiegesha gari yake katika kituo cha kujazia mafuta cha Puma kandokando ya barabara ya Haile Selasie na mara baada ya kutoka katika gari hio nyeusi aina ya Mercedenz alipiga hatua na kuingia uelekeo wa hoteli ya Peninsula.

Alikuwa makini mno katika tembea yake , ni kama vile mtu ambae anaogopa kufatiliwa, wakati huo simu ilikuwa sikioni na mara baada ya kuignia ndani kabisa ya hoteli hio eneo la mapokezi aliongea maneno machache tu na kisha alisonga mbele na kuzisogelea ngazi.

Jengo la hoteli hio halikuwa refu sana na mara baada ya kufika floor ya tatu alisimama katika mlango wa chumba na akagonga mlango na hazikuchukua hata dakika chache mlango wa chumba ulifunguliwa na ksiha akaingia ndani.

Chumba hakikuwa cha ghali sana , kilikuwa cha kawaida tu kitanda kikubwa cha sita kwa sita pamoja na Tv.

Mtu aliemfungulia mlango alikuwa ni mwanaume wa makamo hivi mrefu mweusi ambae ana nywele ndefu na masharubu.

“Mzigo vipi?”Aliongea Amosi mara baada ya kusalimiana kwa kugongesheana tano.

“Huu hapa boss”Aliongea yule kijana na kuchukua bahasha iliokuwa juu ya kitanda na kumpatia.

Amosi alifungua bahasha ile kwa kuihakiki na kisha alitingisha kichwa kuonyesha kuridhika.

“Kuna maagizo mengine?”

“Hamna , nimepatiwa hizo tu”Aliongea yule bwana na kumfanya Amosi kukagua chumba hicho kwa dakika kadhaa na kisha alitingisha kichwa na kugeuka kuondoka.

“Simama hapo hapo?”Sauti kutoka nyuma ilisikika ikimwamrisha na kumfanya ageuke huku akiinua mikono yake juu mara baada ya kuona amenyooshewa Bastora, huku yule mtu akiwa hana utani hata kidogo kwenye macho yake.

Ni dakika ileile mlango wa bafuni ulifunguliwa na akatoka mwanamke ambae ni kama alikuwa akitoka kuoga kutokana na kwamba hakuwa na nguo zaidi ya Bathrobe ya rangi nyeupe, alikuwa mrembo haswa.

“Tresha!!”Aliongea Amosi kwa mshangao.

“Amosi!!”

ITAENDELEA









SEHEMU YA 21

Mwanamke ambae alikuwa amepambwa na tabasamu mbele ya Amosi alikuwa ni Tresha , pengine Hamza angekuwepo ndani ya hilo eneo angemfahamu mara moja , ndio mrembo ambae alimpagawisha katika Apartment za Dosam Homes , mwanamke ambae kwa maelezo ya Amiri uzuri wake ni wa kutengeneza na inasemekana ni mfanyakazi wa Binamu Island.

Amosi alimwangalia Tresha kwa dakika kadhaa na kisha akayainua macho yake na kumwangalia mwanaume aliemnyooshea Bastora.

Upande wa Tresha hakuonyesha ishara yoyote ya furaha , ilionekana alikuwa akifahamiana na Amosi lakini muda huo alikuwa siriasi.

“Tresha nini hiki, kwanini upo hapa na nini kinaendelea?”Aliuliza Amosi.

“Nikuulize wewe Amosi unafanya nini hapa?”Aliongea Tresha na alimsogelea Amosi na kisha alichukua ile bahasha.

Amosi alikuwa na wasiwasi mno na kwa haraka haraka alijua kabisa yupo ndani ya mtego.

“Tresha najua unachomaanisha , lakini swala hili linahusiana vipi na wewe?”.

“Swali hilo ulitakiwa kumuuliza aliekupa kazi , nilishakuonya siku nyingi ikitokea umeingilia njia zangu tutakuwa maadui wakubwa na leo tupo hapa”Aliongea na hapo sasa hisia mbaya zilianza kumvaa Amosi na kitu kilichomjia akilini kwake mara moja ni kujiokoa.

Alimjua mwanamke huyo fika , licha ya kuonekana mwanamke mrembo lakini ni kibaraka wa watu wa Binamu Island ambae hana huruma hata kidogo.

“Usije kufikiria kufanya chochote cha kijinga , sekunde ambayo utasogea hata nchi moja ndio utakuwa mwisho wa uhai wako Amosi”

“Unataka nini kutoka kwangu Tresha , kama Binamu wameagiza kifo changu haikuwa na haja ya kuniwekea mtego kama huu”

“Haha.. hubadiliki hata kidogo , siku zote akili yako inafanya kazi kwa haraka ukiwa katika hatari , ungekuwa sawasawa kiakili ungejiuliza maswali mengi kabla ya kuwa mtumwa wa pesa, niambie Amosi umeahidiwa kiasi gani cha malipo kwa ajili ya kufanya kazi ya hatari namna hii , unaniuliza nini nataka kutoka kwako? , hakuna chochote ninachotaka kutoka kwako , Curiosity killed the cat

Mara baada ya kumalizia msemo ule wa shauku ilimuua paka alimpa ishara yule bwana kumpiga Amosi risasi.

“Wait!!”Amosi alizuia kifo chake na kumfanya Tresha kumpa ishara yule bwana asiruhusu risasi.

“Unataka kusema nini Amosi , kitakachokufanya uendelee kuishi”

“Naomba niulize swali?”

“Kwasababu ya historia yako unaweza kuuliza kabla ya kupoteza uhai”

“Kanali Dastani ndio aliekupatia taarifa juu ya ninachofuatilia?”Aliuliza Amosi akiwa na macho yaliojaa uchungu.

“Ukishajua ni Dastani utafanya nini , unadhani kuna uwezekano wa kulipiza kisasi hata baada ya kufa”

“Kwasababu jibu lako linaweza kunifanya nikupatie kitu cha thamani zaidi kuliko kifo changu”

“Amosi nipo hapa kwa maamgizo ya Binamu , unadhani ni kipi unaweza kuniambia nikaenda kinyume, una kitu gani cha thamani zaidi ya kifo chako?”Aliongea Tresha huku muonekano wake ukiwa siriasi lakini swali lile lilimfanya Amosi aone bado hawezi kufa kizembe.

“Nawajua nje ndani Night Shadows na namna ya kuwasiliana nao!!!”Aliongea Amosi na kauli ile ilimfanya yule bwana ambae alikuwa ameshikilia bastora kupepesa macho kwa kumwangalia Tresha na hio ndio nafasi adhimu ambayo Amosi alikuwa akiitafuta.

“Clang!!!”

Ilikuwa ni wepesi wa hali ya juu mno , kitendo cha yule mtu alieshikilia siraha kupepesa macho pembeni baada ya kutaja Night Shadows Amosi alikuwa ashahama aliposimama na kumtupia Bedlamp iliopasuka kwenye mikono yake na bastora kwenda pembeni.

Tresha ambae alikuwa mita kadhaa kutoka alipo Amosi hakuweza kufanya chochote kwani hakuwa na siraha.

Amosi hakuzubaa , mpango wake ilikuwa ni kukimbia na sio kushindana na Tresha , alijua mwanamke huyo likija swala la map[igano hamuwezi maana ni Ninja aliepitia mafunzo na mafunzo yakamzoea.

“Bang!!!”

Bahati mbaya spidi yake haikutosha na bastora iliofungwa kiwambo cha kuzuia sauti ilikohoa , kama sio kupinda kidogo tu pengine ingekuwa mwisho wake palepale.

Amosi licha ya kupigwa risasi hakutaka kusikilizia maumivu , bahati nzuri alikuwa hajauloki mlango , hivyo spidi yake ya kutoka ndani ya chumba hicho ilimfanya kukoswa koswa na risasi nyingine.

“Fuckk!!!”

Tresha alitoa tusi huku yule bwana alieshikilia bastora kutaka kukimbilia nje lakini alizuia.

“Carlos Stop!!!”Aliongea Tresha kwa nguvu na mwanaume mweusi ambae sasa tunafahamu jina lake ni Carlos aliishia mlangoni.

“Tresha tunapaswa kumuua kama oda yetu ilivyo”Aliongea Carlos.

“Umefeli kumuua akiwa mbele yako unadhani unaweza kumuua akiwa kwenye korido , unataka kuibua taharuki , unataka kuonekana katika Kamera”Aliongea Tresha huku akionyesha hali ya kukasirika.

“Wewe ndio umesababisha misheni imefeli , nilikuambia tokea mwanzo hili nitalimaliza mwenyewe , kulikuwa na haja gani ya kutaka kushiriki?”Aliongea Carlos na kauli ile ilimfanya Tresha kutoa tabasamu.

“Ndio tulipaswa kumuua , lakini ni mpaka atupe taarifa tuliohitaji , likija swala la kuua Carlos unatoka nje ya malengo ya misheni”Aliongea na kumfanya Carlos kuvuta pumzi na kuzishusha.

“Ninachojua mimi ni kuua, nimefundishwa hivyo?”

“Ndio maana ya uwepo wangu hapa Carlos, tunapaswa kupata taarifa tunayotaka kutoka kwake , ndio tumuue sio vinginevyo?”

“Ameshakimbia , unadhani itakuwa rahisi?”

“Hilo niachie mimi , namjua Amosi nje ndani , nimefanya nae kazi kwa muda mrefu”Aliongea na kisha mwanamke huyo aliangalia mazingira ya chumba na kisha alichukua bahasha ambayo Amosi alionekana kuifuata na kutoa makaratasi na kuyakagua kwa muda.

“Unapaswa kuondoka”Aliongea Tresha ambae alipanda juu ya kitanda na kujiachia na kumfanya Carlos kumwangalia mrembo huyo kwa macho ya kimatamanio lakini Tresha hakujali macho yake na palepale aliweka bastora yake kwenye kiuno na kutoka nje huku akidhibiti hasira zake.

Upande mwingine Amosi alikuwa amesambaza matone ya damu kila mahali ndani ya hoteli hio lakini hakujali , hata watu aliopishana nao wakati akiwa ameshikilia ubavu wake wa kushoto hakutaka kuwapa hata nafasi ya kuona sura yake , ki ufupi akili yake ilikuwa katika tahadhari ya kujiokoa na alikimbia kweli.

Hoteli hio ilisifika kwa ulinzi mkali na usalama lakini kilichotokea kiliwashangaza watu.

Dakika chache alikuwa ashatokezea barabarani na kuanza kujikongoja kusogelea gari lake.

“Amosi!!”

Sauti ilimwita, ilitokea katika gari nyeupe RAV4 iliosimama kando ya barabara , Amosi aliangalia gari hio na kuonekana kuitambua na bila ya kujiuliza mara mbilimbili aliisogelea, mlango wa gari hio ulifunguliwa na aliingia ndani na hapo hapo ikaondoshwa.

*****

Hamza mara baada ya kumaliza kuongea na simu iliotoka kwa Amiri alikaa kwenye tarakishi na kisha alianza kufanya utundu wake , alishajua tarakishi za wafanyakazi zinafuatiliwa hivyo alitaka kuifunga tarakishi yake ki ujanja aendelee na mambo yake bila kushitukiwa.

Dakika ambayo ndio anamaliza kuseti mitambo , Linda aliingia akiwa na rundo la makaratasi mkononi , zilikuwa nyingi kiasi kwamba hata kubeba alionekana kupata shida.

“Hizi nyaraka unatakiwa kuzitafsiri kutoka kingereza kwenda lugha ya kiswahili , ziishe zote leo hii”Aliongea kikauzu na kauli ile ilimshangaza Hamza.

“Linda haiwezekanni ni nyingi mno kumalizika kwa siku moja “

“Bosi ndio kasema , eti kwasababu uwezo huo unao hataki kuona ukipotea bure”Linda aliweka nyaraka zile mezani na kisha kwa maringo alitoka.

Alikuwa akijua kabisa Hamza amemchokoza bosi , kwani alisikia akipiga makelele kutoka ndani ya ofisi yake ndio maana akapewa adhabu hio.

Ki ufupi kwa Regina ilikuwa ni kisasi mwanzo mwisho ili kumkomesha.

Hamza aliishia kujisikia uchungu lakini hata hivyo alikuwa akiupenda mshara wake hivyo aliishia kukubali kufanya kazi.

“Bora ningejifanyisha tu sijaona kitu , angalia sasa msala niliojitengenezea”Aliwaza Hamza.

Mpaka inafika jioni Hamza aliweza kutafsiri nusu tu ya kazi yote aliopewa na aliona hakuna uwezekano wa kumaliza yote na aliona atafute namna yoyote ya kuongezewa siku.

Lakini kabla hata hajajua cha kufanya mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na Linda.

“Ni muda wa kuondoka kazini sasa , nenda maegeshoni na washa gari , washa AC na kisha msubiri bosi”Aliongea na Hamza alivuta pumzi ya ahueni , alikuwa amechoshwa kweli kuendelea kukaa hio sehemu.

Aliingia zake kwenye lift ambayo ilimpeleka moja kwa moja mpaka maegesho ya chini kabisa ya jengo hilo na kutoka , lakini wakati akitaka kusogelea gari ya Regina aliweza kumuona Kapteni Yonesi akiwa amesimama pembeni huku akimwangalia kwa macho yaliojaa sumu.

Ilionyesha ni dhahiri alikuwa amejitega hapo ili kumpata Hamza amshikishe adabu.

“Wewe mhuni hatimae umejitokeza”Aliongea kikauzu.

“Kapteni ndio unajiandaa kutoka kazini na wewe , hehe kwaheri tutaonana kesho”Aliongea Hamza akijifanyisha mjinga.

“Nani kakuambia naondoka?, unadhani naweza kusahau kirahisi kilichotokea mchana”

“Mchana kumetokea kitu gani?, mbona hata sina kumbukumbu”

“Wewe mpuuzi usie na aibu , kwahio unakataa kosa lako sio , umenidhalilisha mbele ya watu na sijakufanya chochote , huu ndio muda , nisipokushikisha adabu siwezi kuendelea kuitwa Kapteni”Aliongea na sekunde ileile alifyatuka kama mshale akitanguliza mguu akilenga maeneo nyeti ya Hamza.

Hamza aliishia kukwepa pigo lile na kumfanya Yonesi kupita.

“Kapteni ukiendelea hivi utanikasirisha ujue , mimi ni mwanaume na sio vizuri kupigana na mwanamke”

“Unajiita mwanaume , kwangu wewe ni mwanaume ulievaa suruali tu, kama unajiamini pigana na mimi tuone”Baada ya kuongea hivyo alijiandaa kumshambulia tena Hamza lakini aliishia njiani mara baada ya mlango wa lift kufunguka na Regina kutoka.

Regina mara baada ya kuona tukio lile alijikuta akishangaa huku akikunja sura.

“Yonesi , nini kimetokea?”

“Boss nina mashaka na tabia ya huyu mtu …”Aliongea Yonesi na kuanza kuelezea kilichotokea mchana juu ya Hamza kumchungulia manyonyo yake na kisha kumdhalilisha mbele ya wafanyakazi.

“Boss tusipomshikisha adabu mapema , hii tabia itafanya wafanyakazi kunidharau”Aiongea Yonesi akipigilia msumari.

“Mkurugenzi , usimsikilize Yonesi na porojo zake , mimi hio tabia ya kuchungulia watu sina kabisa , mimi nilikuwa nimekaa zangu kwenye meza tukiwa tunaangalia na nilimsifia kidogo tu kama ni mrembo na ndio akakasirika”Hamza alijitetea , lakini kwa bahati nzuri au mbaya Regina na Yonesi wote ni wahanga wa tabia ya Hamza na kwa muda huo alikuwa akimchukia mno Hamza kiasi kwamba mpaka meno yake yalikuwa yakimuwasha., Alidhani swala lile lilimtokea yeye tu kumbe alikuwa amemfanyia uhuni na Mlinzi wa kampuni .

Dakika hio hio Regina aliona aungane na Yonesi kumshikisha Hamza adabu l akini hakutaka kuonyesha kama alikuwa na yeye ni mhanga wa kupigwa chabo.

“Kama ni hivyo basi unaruhusa yangu ya kumshikisha adabu , angalia tu usije kumuua au akalazwa, anapaswa kuja kazini”Aliongea Regina na kumfanya Hamza amwangalie na kuona namna ambavyo Regina alikuwa amejaa sumu juu yake.

“Usijali mkurugenzi , najua ninachokifanya”Aliongea Yonesi na palepale muonekano wa kishujaa ulimjaa, alikuwa kama komandoo anaejiandaa kwa misheni ‘shikisha adabu’.

Subiri kwanza , twendeni mpaka floor ya pili katika chumba cha mazoezi”Aliongea Regina , alijua ikitokea mfanyakazi wa kampuni kushuhudia tukio la Yonesi kumpigwa Hamza inaweza kuleta shida

“Kuna haja ya hili , mkurugenzi au unakinyongo na mimi?”Aliuliza Hamza.

“Eliza alisema wewe ndio uliemsaidia kumuokoa katika udhalilishaji , naamini unao uwezo wa kushindana na Yonesi japo kidogo, chukulia kama mazoezi ya kukuweka fiti kidogo uonekane mwanaume”Aliongea Regina.

Hamza hakuwa na jinsi zaidi ya kutii maagizo ya Mkurugenzi na kwenda katika floor ya pili kwa ajili ya kushikishwa adabu.

Dosam ilikuwa ni kampuni yenye wafanyakazi wengi na biashara zao zilihusisha bidhaa za thamani , hivyo walikuwa na kitengo cha ulinzi ambacho ikitokea mzigo unasafirishwa basi ndio huhusika kuimarisha ulinzi , hivyo kwa ajili ya idara ya ulinzi ilitengwa floor nzima ya pili kwa ajili ya mazoezi , kulikuwa na kila aina ya vifaa ikiwemo Gym na hata eneo la kupimana nguvu.

Ilikuwa ni muda wa kuondoka kazini , hivyo hakukuwa na watu ndani ya eneo hilo.

Yonesi alimchukua Hamza na kumpeleka katika Arena , alifanya hivyo ili isitokee Hamza akakimbia wakati wa kumpiga.

“Ni kweli unataka kupigana na mimi?”Aliuliza Hamza.

“Usiwe na wasiwasi , ngoja nikunyooshe nyooshe viungo , lakini sitokuua”

“Basi hakuna shida , ila kumbuka miguu na mikono haina macho hivyo kuwa makini”

“Acha woga , jali usalama wako kwanza”

Mara baada ya kumaliza sentesi hio Yonesi alimsogelea Hamza kwa spidi huku akinuia kumchapa ngumi ya bega.

Lakini alichokifanya Hamza ni kuwa na spidi kidogo tu kwani mara baada ya ngumi ile kumfikia aliinama ikapita lakini muda huo huo bila ya Regina kuona Hamza alishainua mkono na kugusa msambwanda.

“Ahhhhhh…”

Yonesi alijikuta akipiga makelele mara baada ya kuhisi mkono ukimgusa upande wa kushoto.

“Mshenzi wewe” Ishara ya mauaji ilimvaa Yonesi.

“Kapteni vipi tena , mbona unafoka wakati tunapigana?”Aliongea Hamza ambae alikuwa amejificha kwenye kona ya steji.

“Umenigusa tena”,

“Unamaanisha nini nimekugusa , kwahio wewe unaweza kunipiga lakini mimi siruhusiwi kukugusa, kama ni hivyo unaweza kuniua hapa hapa”.

“Mhenzi wewe , hujui kupigana kazi yako ni kugusa tu”

“Nimegusa wapi?”Hamza alikuwa akijua fika ni wapi amegusa lakini alijifanyisha hajui , alijisikai vizuri, alitaka kumshikisha adabu mjeda huyu bila hata ya kumpiga.

Regina alikuwa akiangalia pambano na hakuwa akielewa kinachotokea , kutokana na spidi ya Hamza.

Yonesi hakujua namna ya kuongea tena hivyo alijiamulia kupambana tu , awamu hio alikuwa amedhamiiria kumpiga Hamza kwa kutumia mguu na sio ngumi tena

Hamza aliishia kuvuta pumzi na dakika ambayo shambulizi linamfikia alishafanikiwa kusogea kushoto.

Yonesi alijikuta akipandwa na hasira mara mbili mara baada ya kuona amepiga hewa , lakini hakutaka kujiuliza Hamza kaweza vipi kukwepa shambulizi lake hivyo aligeuka na kumsogelea tena na kuanza kurusha ngumi mfululizo.

Hamza alikuwa akijifanyisha kuwa muoga wa ngumi zile na kurudi nyuma kila mara Yonesi alipokuwa akishambulia , alionekana kama amezidiwa lakini ukweli ni kwamba yeye ndio aliekuwa na maamuzi ya kumaliza pambano hilo au kulirefusha

Yonesi aliishia kumkimbiza Hamza kila mahali alipohama lakini mwisho wa siku yeye ndio aliekuwa wa kwanza kuchoka.

“Kwanini unakuwa muoga na kukimbia kimbia kama panya , kama kweli wewe ni mwanaume usikimbie na tupigane ana kwa ana”

“Kapteni unachofanya ni kulazimisha nifanye kitu ambacho sitaki na kwasababu sitaki nitaendelea kukimbhia”

“Kuwa mwanaume basi”Aliongea kwa kufoka.

Hata Regina ambae alikuwa akiangalia alishindwa kuvumilia mara baada ya kuona Hamza anachofanya ni kukwepa tu na hashambulii.

“Hamza jikaze basi hata kidogo?”Aliongea.

“Nijikaze niumie , naogopa nisije kupoteza taifa la kesho hapa hapa”

“Huna lolote , pigana na mimi acha kukimbia”Aliongea Yonesi na palepale alimsogelea Hamza kwa mara nyingine , uwezo wa Yonesi kuanzisha mashambulizi haukuwa wa kawaida , alikuwa akijua kujipima wakati wa kushambulia mno alichokosa ni spidi tu basi na ndio maana kila shambulizi alilorusha Hamza alikuwa na uwezo wa kulikwepa bila shida yoyote

Mwishowe Yonesi aliona kabisa Hamza pengine kuna kitu anaficha , inawezekana vipi mtu wa kawaida kuweza kuwa na stamina ya aina hio , maana yeye alikuwa amechoka lakini Hamza ni kama bado ndio anaanza na anahema kawaida tu.

Kilichomkasirisha zaidi ni kwamba mpuuzi huyo alikuwa akimwigizia na hakuwa akionyesha uwezo wake kabisa , kitendo hicho kilimfanya Yonesi aone ni udhalilishaji.

Mara baada ya kufeli zaidi ya mara tano , hatimae alipata wazo ambalo lilimfanya adondoke chini kwa kupiga magoti na kufunika uso wake na viganja na kuanza kulia kwa kwikwi.

Kwa namna ambavyo Yonesi alikuwa akilia ilikuwa ni kama mke aliefiwa na mume wake , mtu yoyote angemuona mjeda huyo mrembo angemuonea huruma.

Hamza alijikuta akiingiwa na aibu baada ya kuona Yonesi analia hata kwa Regina hivyo hivyo alishangaa kuona Yonesi analia, maana ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona afande akilia baada ya kupigwa.

Ukweli ni kwamba Regina hakuona Hamza akimpiga Yonesi na upande mwingine alimjua Yonesi kama mwanamke jasiri na mkali.

“Hamza muombe msamaha Yonesi , kama mwanaume unatakiwa kujua wakati wa kuacha”Aliongea Regina lakini Hamza alijihisi ni kama anaonewa , maana hakumpiga hata kidogo Yonesi.

Hamza hakutaka kuona Yonesi akiendelea kulia na alimsogelea kwa ajili ya kumbembeleza

“Kapteni usiendelee kulia , nimekosa mimi nisamehe sa…”

Kabla hata Hamza hajamaliza kuongea Yonesi aliibuka na kibao na kumchapa nacho Hamza upande wa kushoto, baada ya kibao aliunganisha na ngumi kwenye tumbo na kumfanya Hamza kutoa mguno.

“Naomba unisamehe Kapteni , vinauma , vinauma”Hamza alibembeleza asemehewe huku akifanya kuugulia maumivu chini sakafuni.

“Wewe mpuuzi nitahakikisha kila siku utakayoniona unanikimbia”Aliongea Yonesi huku akisimama na kupumua kwa ahueni.

Regina aliekuwa chini ya steji alishia kushangaa mara baada ya kugundua kumbe Yonesi alikuwa akijifanyisha mdhaifu kutafuta nafasi ya kumshitukiza Hamza.

Mashambulizi yale yalionekana kumuumiza Hamza na Regina alijiuliza atakuwa katika hali gani.

Mara baada ya kilichotokea Regina aliishia kumlaani Hamza ndani kwa ndani kwa kujifanyisha kijeba na kuchungulia chungulia wanawake na kujiambia anastahili kweli kipigo.

Mara baada ya kumshinda Hamza , Kapteni Yonesi hakuhisi hata kidogo furaha wala mafanikio , alikuwa akijua kabisa yeye ndio ambae ameshindwa.

Aliishia kujiwazia huyu Hamza kila dakika anazidi kuonekana sio wa kawaida na pengine hata kufanywa kuwa msaidizi ni kutokana na Regina kufahamu hilo.

“Mkurugenzi , nitaondoka sasa , kwaheri”Aliongea Yonesi.

“Ni kweli unapaswa kwenda kupumzika , siku imekuwa kubwa kwako”Aliongea.

Hamza alikuwa bado amelala kwenye steji licha ya Yonesi kuondoka na Regina alimwangalia kikauzu.

“Uko sawa wewe? , kama bado hujafa amka tuondoke”

“Regi nimeumia kwa ndani”Aliongea Hamza.

“Acha maigizo , kama huamki naondoka zangu”

“Nataka busu ili niamke”Aliong ea na kauli ile ilimshangaza Regina na kumfanya kuona aibu za kike , lakini tofauti na kuwa na hasira alimuuliza.

“Wapi unataka upigwe busu?”

Hamza mara baada ya kusikia swali lile alijikuta akifurahi na kujiambia kumbe kupigwa nako kuna faida na kwa haraka haraka alitumia kidole chake kuonyesha eneo la mdomoni.

Regina alivuta pumzi nyingi huku ukauzu ukizidi kumvaa , aliangalia pembeni na kuona kifaa cha kuchukulia mazoezi ya mkono na mara baada ya kukiokota alimlenga nacho Hamza mdomoni.

“Kiss your ass!!”

Hamza aliweza kukwepa haraka kifaa kile kabla hakijampata na kusimama na kumwangalia mwanamke huyo alivyokuwa amefura kwa hasira.

“Hey! Nilikuwa nakutaia tu usikasirike hivyo”

“Ukiendelea kuongea ujjinga nitahakikisha unapata mshahara nusu”

“Ah , boss basi yaishe, nimekosa mimi naomba usinikate mshahara , nitaenda kuwasha gari tuondoke sasa”

Hamza hakutaka kukosa pesa kwa tukio dogo kama hilo , isitoshe kutafsiri makatarasi yote yale haikuwa kazi ndogo ambayo anaweza kukubali kukatwa mshahara kizembe.

Lisaa limoja baadae wote waliweza kufika nyumbani na Shangazi alikuwa bize kuandaa chakula cha usiku.

“Hamza vipi siku yako ya kwanza kazini?”Aliuliza na Hamza alitaka kusema amenyanyaswa siku nzima lakini Regina alimpiga jicho asije kuongea ujinga na akaacha na kuanza kucheka.

“Haha.. Shangazi siku yangu ilikuwa nzuri sana , sitaki tu kuongelea ilivyokuwa lakini ,itoshe kusema nimepata Vitamini ya macho”

Kauli yake ilikuwa na zaidi ya maana na kumfanya Regina aliekuwa pembeni yake kupandwa na hasira na kutaka kumpiga na rimoti palepale.

Hamza alikuwa na miadi yake hivyo hakutaka kukaa sana nyumbani , ijapokuwa chakula ndani ya nyumba hio kinawahishwa hakutaka kula kwanza mpaka amalizane na Amiri., hivyo alipandisha juu kujiandaa kuondoka lakini wakati anashuka aliweza kumsikia Regina akiongea na simu na moja kwa moja aliweza kujua ni baba yake aliekuwa akiongea nae lakini aliishia kukaa kimya , ilionekana kuna jambo ambalo liliwafanya kujibishana tena.

“Shangazi natoka kidogo , kuna rafiki yangu nataka kuonana nae”Aliongea Hamza.

“Lakini chakula cha usiku kinakaribia kuiva utawahi kurudi?”

“Sijajua Shangazi , kama nitachelewa naomba uniwekee tu nitakula nikirudi , anaonekana kuwa na matatizo”Aliongea Hamza na Shangazi alionekana kumuelewa , ukweli alifurahi kuona Hamza alikuwa angalau na rafiki.

“Sawa, wahi ukamuone rafiki yako”

Hamza mara baada ya kuaga alitaka amuage Regina lakini mwanamke huyo alionekana bado alikuwa akiongea na simu , huku muonekano wake ukiwa umebadilika hivyo alijua maongezi hayo ni siriasi.

Alitoka nje na kuchukua ile Lexus ya Regina na kuondoka , akiwa njiani alimpigia Amiri lakini hakupokea , lakini hata hivyo hakutaka kughairi , aliendelea kuendesha na wakati anakaribia daraja la kigamboni simu iliita.

“Uko wapi bro , nilikuwa nimetingwa kidogo”

“Okey , ndio nimetoka niambie tuonane wapi?”

“Samaki Samaki bro , ukikaribia nishitue”

“Poa”

Licha ya kwamba anakoenda ni mbali , lakini kutokana na kuwa na gari kali hakuona shida , pili hakuwa ametoka usiku muda mrefu.

Ilikuwa ni saa moja kwenda na nusu na foleni hazikuwa kubwa sana upande wa magari yanayorudi mjini , hivyo hakupata shida kubwa, dakika arobaini tu aliweza kufika Samaki Samaki na alimpigia simu Amiri.

“Bro umewahi mno , nikajua kwa foleni utachukua muda kidogo kufika”

“Nipo na usafiri binafsi , tuonanae wapi”

“Ah kumbe , nisubiri hapo mgahawani nakuja muda si mrefu”

Hamza aliangalia mazingira ya eneo hilo na palionekana kuchangamka, kulikuwa na magari mengi.

Kutokana na gari yake kuwa ya bei ghali hakupata shida ya kuegesha , watu waliomuona akitoka kwenye gari hio ya Lexus walimwangalia kwa macho ya maswali mengi.

“Bro!!!”

Hamza kabla hata hajapiga hatua kuingia ndani ya mgahawa aliweza kuitwa kwa nyuma na aligundua aliekuwa akimwita ni Amiri.

“Nilijua utachukua muda”Aliongea.

“Nilikuwa maeneo haya haya , njoo tuongee kwenye gari”Aliongea Amiri huku akizungusha macho.

Amiri alikuwa ameegesha Aud yake katika maegesho ya muda mfupi na waliingia ndani wote , jamaa huyo alionekana kuwa na haraka mno na hilo Hamza aliliona.

“Unaonekana akili haijatulia lakini kwa muonekano wako nadhani hali sio mbaya kama nilivyofikiria”Aliongea Hamza.

“Nimechanganyikiwa kutokana na kuwa na maswali mengi , lakini bado nina hofu , pengine unaweza kunipa jibu ambalo linaweza kuifanya hali yangu kuwa mbaya zaidi”Aliongea.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , wewe ndio ambae ulichukua hatua , inabidi kuyakabili matokeo”

“Nadhani tuongelee hapa hapa kwenye gari , nina miadi na Melisa , nimepata ahueni tumeonana kabla ya kukutana nae”

“Unakutana nae sasa hivi?”

“Ndio , nilimuahidi nitamtoa Out leo , japo nina wasiwasi na kinachoendelea lakini angalau nataka kuondoa huu mkanganyiko kabla hatujaonana”Aliongea na palepale alitoa simu pamoja na Earpod na kumpa Hamza.

“Sikiliza hio na unipe majibu”

“Nisikilize tena , nikajua ni Vidio”

“Bro , tuliweka kamera za vidio ndio lakini sikuweza kuona cha maana, mpaka siku moja nilipoona tukio ambalo sio la kawaida , ndio ambalo lilinipelekea kuweka kinasa sauti”

“Tukio gani?”Hamza aliuliza kwa shauku.

“Sikiliza kwanza hio sauti niliosikia kutoka ndani kwake”Aiongea na Hamza alitingisha kichwa kukubali.



















SEHEMU YA 21.

Hamza kadri alivyokuwa akisikiliza ndio uso wake ulionyesha mabadiliko , hayakuwa mabadiliko ya mshangao bali ya kuchanyikiwa pia.

“Mbona nasikia lugha ambayo sijawahi kuisikia popote ni lugha gani hii?”Aliongea Hamza na kumfanya Amiri na yeye kuonyesha ishara ya kutokujua.

“Hapo ndio pamenichanganya sana , hio sauti ni ya Mellisa wangu , siwezi kosea Bro , lakini anaongea lugha ambayo siijui”Aliongea Amiri na Hamza aliongeza umakini katika kusikiliza ili ajaribu kutafsiri nini kinaongelewa , alikuwa akisikia sauti ndio lakini lugha hajawahi kuisikia.

“Hii lugha sijawahi kuisikia popote , au ni lugha sizizo rasmi za kimakabila, wanaongea nini”Hamza alionekana kujiuliza.

“Baada ya hapo watabadili lugha , sikiliza kwa umakini bro”Aliongea Amiri na Hamza alitingisha kichwa na kusikiliza.

“Silvia kadri tunavyochelewa ndio uwezekano wa kurudi kuwa mdogo , tunatakiwa kumpata Princess Natasha mapema kabla ya Profesa”

“Rosaron hatujui mpaka sasa roho ya Natasha inaishi katika mwili wa nani , sio rahisi kumpata”

“Atatutafuta yeye mwenyewe baada ya teknolojia ya Somnus kufanikiwa , tunatakiwa kusubiri lakini kuwa tayari vilevile, kosa kidogo tu litamuamsha na Profesa , wakiungana itakuwa ngumu kwetu”

“Rosaron unadhani tupo sahihi , namaanisha Pincess Natasha kuwepo hapa Tanzania!!?”

“Tumefika hatua hii kutokana na imani tulioaminishwa , njia pekee ya sisi kuonekana ni kurudi, Silvia wewe ndio uliekuwa mpenzi wake , mapenzi yana nguvu akiamka atakutafuta wewe, ndio maana upo hapa”

Hio ndio namna ambavyo sauti zilisikika , lakini katika maongezi hayo Hamza na Amiri wote hakuna ambae alisikia neno Mellisa , kwa maana kwamba maongezi hayo hayakumhusu Mellisa.

“Sijasikia jina la Mellisa”Aliongea Hamza

“Sijasikia jina lake pia , lakini sauti ni yake”

“Una uhakika hio ni sauti ya Mellisa?”

“Ndio , siwezi kusahau sauti ya Mellisa hata niwe nimelewa pombe”Aliongea na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.

“Vipi sauti ya pili unaitambua , namaanisha hio ya mwanaume?”

“Sijawahi kuisikia , lakini kwa rafudhi yake anaonekana sio mbongo”Aliongea na Hamza pia alikubaliana na Amiri sauti ya pili ilikuwa sio mtu mwenye rafudhi ya kiswahili.

“Hebu subiri”Aliongea Hamza na kisha alichukua Earpord zote mbili na kuzitumbukiza kwenye masikio na kupelekea mbele ile rekodi ya sauti, Amiri alibakia kimya asijue nini ambayo Hamza anajaribu kufanya.

Hamza alikuwa akisikiliza ka kurudisha nyuma sauti na kwenda mbele na ndani ya dakika tano alitoa Eapord zile masikioni.

“Umegundua nini?”

“Najiuliza kwanini hawakuendelea kuongea kwa ile lugha na kubadilisha katika lugha ya kiswahili , pia sauti ya mwanaume tuliokuwa tukisikia ni ya Mzungu rafudhi yake , tena mzungu wa Ulaya kila kitu kinaonyesha alikuwa akiongea na Mellisa kutumia kifaa maalumu au simu”

“Unamaanisha hakuwa ndani kwa Mellisa?” Aliuliza Amiri na Hamza alitingisha kichwa.

“Kama hakuwepo unazungumzia nini kuhusu jina la Silvia , kwanini huyo mzungu kamtambua kama Silvia mpenzi wangu?”

“Hapa siwezi kukupa jibu la moja kwa moja , kuna mawili ambayo yote yanawezekana , kuna uwezekano ni kweli Mellisa ni Silvia au huenda ana multiple Personality, kuhusu kuwa Silvia hilo halina maelezo mengi lakini kama kweli ana ugonjwa wa nafsi mbili ni ngumu kufanya mawasiliano na mtu au mtu kupigia akitarajia Mellisa kuwa Silvia au Silvia kuwa Mellisa”

“Kaka sijakuelewa kabisa , umenichanganya?”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza amwangalie machoni , ni kweli bwana huyu alionekana kuchanganyikiwa.

“Ushawahi kuagalia filamu ya Split?”

“Bro mimi sio mpenzi wa Filamu kabisa”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.

“Okey , ipo hivi ninachomaanisha mpenzi wako Mellisa kuna uwezekano akawa mgonjwa wa akili wa kuwa na nafsi mbili , yaanni nafsi ya Mellisa na muda mwingine anakuwa Silvia kama ulivyosikia, ila kwa hapa nashindwa kuamini moja kwa moja , kwasababu kama kweli ni Silvia kwanini akaongea lugha ambayo haieleweki na baadae akahamia katika lugha ya kiswahili kama kawaida, vipi kuhusu alichokuwa akiongea ni kitu cha uhalisia?”

“Kwahio unamaanisha anaweza asiwe mgonjwa wa akili au vipi , mpaka kuweka hayo maswali?”

“Ndio anaweza asiwe na shida hio?”

“Kama sio hivyo atakuwa na shida gani?”

“Kuna kitu nakiwaza lakini sina uhakika nacho , hata kama nikikuambia nitazidi kukuchanganya , kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho Mellisa hakusaliti kama ulivyomdhannia, sauti ya mwanaume ukisikiliza kwa umakini sio katika ile nyumba”

“Bro unaonekana kujua vitu vingi na ndio sababu ya mimi kukushughulish, awali nilitaka kuona kama kweli Mellisa ananisaliti lakini hisia zako na zangu sasa hivi zimefanana , lakini hilo sina shida nalo , Mellisa ana tatizo na mimi kama mpenzi wake napaswa kumsaidia , Bro yule mwanamke nampenda na napanga kumuoa kabisa , hili swala lazima nilipatie ufumbuzi”Aiongea Amiri akiwa siriasi.

“Hili swala nitakusaidia lakini utahitaji kuwa mvumilivu , kitu ninachotaka kujua kutoka kwako je kuna chochote kitu ambacho sio cha kawaida ushawahi kuona pale anapoishi na kwanini ulidhania anakusaliti?”

“Alianza kubadilika , nilikuwa na tabia ya kwenda kwake usiku , lakini siku moja nakumbuka ilikuwa Jumaane miezi minne iliopita , nilikuwa nimelewa siku ile nilipofika kwa Mellisa alikataa kabisa nikiingia ndani na alipogundua ni mimi hakufungua kabisa, kutokana na pombe sikujua kilichotokea , lakini asubuhi nilikuwa ndani kwake , mwanzoni nilidhani baada ya kulewa nilikuja kwake akanifungulia kawaida nikaingia , lakini mara baada ya tukio la pili ndio kumbukumbu za siku hio zikajirudia na kukumbuka alikataa kunifungulia”

“Tukio la pili likoje”

“Hii siku hakunikatalia kuingia ndani , ila alinisubirisha kwenye mlango , jambo hili halikuwa la kawaida , baada ya dakika kama tano niliingia ndani lakini kuna harufu kama marashi hivi ambayo Mellisa hatumii , nilitafuta haya marashi wakati akiwa amelala lakini sikuyaona , haikuwa hivyo tu usiku alikataa kunipa kabisa, haikuwa mara ya kwanza au mbili tu Bro , imekuwa kama ratiba , kila nikienda kwa Mellisa siku ya Jumanne lazima anifanyie janja janja nisile mzigo”Aliongea na kumfanya Hamza kumwangalia Amiri.

“Umesema kila Jumanne , inamaana hata siku ulioenda kwake amelewa na mara ya pili kunusa harufu ambayo sio ya kawaida , ilikuwa Jumanne?”

“Ndio nakumbuka siku niliolewa ilikuwa jumanne , ki ufupi Mellisa kila ikifika Jumanne hataki tuonane kabisa , hii ndio sababu ya kumuwekea kinasa sauti , zile kamera zilikuwa zikileta picha tu ila sauti hakuna , nikaenda kuweka kinasa sauti na jana ndio nimesikia hiki ulichosikia”

Muda uleule simu ya Amiri ilianza kuita na mara baada ya kuangalia jina alimpa ishara Hamza kwamba ni Mellisa ndio anapiga.

“Muda mzee , nilioahidiana nae”Aliongea Amiri na Hamza alimpa ishara apokee simu kwanza.

“Babe uko wapi , mbona hutokei?”

“Nakuja dakika chache , nipo maeneo haya haya”

“Sawa , wahi njaa inaniuma”

“Sawa love , nakuja”

“Kwahio unasemaje Mzee?”Aliuliza Amiri mara baada ya kumaliza kuongea na simu.

“Kuwa nae karibu kwanza , angalia kama kuna kitu kisicho kawaida , au matumizi ya dawa yoyote, kwasasa nina shauku na hii lugha waliokuwa wakiongea mwanzo, naweza kuchukua sauti zao nikaitafutie ufumbuzi?”

“Nakuachia kila kitu mtaalamu , mwenyewe nina shauku ya kutaka kujua Mellisa anaongea lugha gani , mwanzoni nilijua labda ni roho mtakatifu , yule ni mkristo na wakristo kuna muda wanaongea lugha zisizoeleweka”

“Kunena kwa lugha wanaita , inawezekana mpenzi wako alikuwa akinena kwa Lugha wakati akiongea na Rosaroni”Aliongea Hamza na kumfanya Amiri kutabasamu.

“Unazingua kaka”

“Sijazingua , naamaanisha ni kitu ambacho hakiwezekani kunena kwa ligha huku unaongea na mtu , tena mzungu”

Amiri alichomoa flash na kuunganisha na OTG kisha akakopi faili lile la sauti na kumpa Hamza.

“Ukipata chochote nishitue nakuaminia sana mtaalamu”

“Nikifanikiwa nitakuambia , ila kuhusu hii lugha…anyway nitakushitua”Aliongea Hamza na kisha alishuka kwenye gari.

“Sema mzee hatujaonana kama wiki na nusu hivi ila muonekano wako umebadilika sana, umekuwa bomba”Aliongea Amiri akiwa ameshusha kioo , ni kama sasa anamuona Hamza akia na mavazi ya bei ghali.

“Nimeangukiwa na bahati , pengine ninaweza kubadilika zaidi ya hivi”Aliongea Hamza huku akitabasamu.

“Haha.. hapo kidogo mrembo Anitha anaweza kukusikiliza , halafu umekuja na usafiri gani , ulipokuwa ukiongea ni kama ulikuwa ukiendesha?”

“Nilikuwa nikiendesha ndio , kuna mtu niliomba niendeshe gari yake”Aliongea Hamza hakutaka kumuonyesha Amiri kama alikuja na ile Lexus , maswali yangekuwa mengi .

Hamza mara baada ya kuachana na Amiri alifikiria kidogo , aliwaza kurudi nyumbani lakini wazo hilo ni kama halikuwa kipaumbele kwenye halmashauri yake ya kichwa, lakini mara baada ya kukumbuka alimwahidi Shangazi angekula akirudi aliona arudi nyumbani tu moja kwa moja.

****

Upande wa Regina hakupata hata hamu ya kula mara baada ya kuongea na simu, baba yake alimpigia akimlaumu kwanini anataka kuunua kampuni ya Omega inayojihusha na uhandisi wa Programu endeshi za tarakishi.

Baba yake alimwambia sio vizuri lakini pia ingemgharimu hela nyingi kununua kampuni hio kwani hisa zake zimepanda.

“Regina kwanini unafanya maamuzi bila ya kushirikisha wajomba zako na wakurugenzi wa bodi?”

“Huu ni mpango ambao ulishapitishwa tayari katika kikao kilichofanyika mwezi uliopita”Aliongea Regina.

“Unadhani walichopitisha ndio wanachotaka , wamefanya yote kukusikiliza kwasababu wanakuamini sana lakini vilevile hawana uelewa na maswala ya komputa , Tanzania kwa mara ya kwanza tunaingia katika biashara ya uhandishi wa Programu endeshi , kwanini unataka kujiingiza katika vitu ambavyo huna uzoefu navyo , isitoshe ni mpaka wakurugenzi wote wa bodi wakubali”Aliongea Mzee Wilsoni.

“Kwanini hawakujitokeza kwenye kikao na kunipinga waziwazi?”

“Wewe mtoto , hawakujitokeza mbele yako kwasababu wanaheshimu mawazo ya babu yako , ndio watu waliokuwa wakifanya kazi na babu yako kwa miaka na miaka , wanachokifanya ni kutotaka kuona unafanya maamuzi ambayo yapo nje ya sera ya kampuni”

“Baba , ijapokuwa wewe ni moja ya mmiliki mkubwa wa hisa lakini huna nafasi yoyote ya uongozi , hivyo siwezi kuzungumza hili swala na wewe , kama wao ndio wanataka kuongea basi waache waongee na mimi mwenyewe , sio wewe kuwa msemaji wao”

“Hakuna shida , bodi ya wakurugenzi kesho itakaa kikao na unapaswa kutushawishi kwa fact , ukishindwa kutushawishi usije kutulaumu tukipiga kura ya kutokuwa na imani na wewe kuendelea kuwa katika nafasi ya ukurugenzi wa kampuni, na ikitokea hivyo utapoteza kila kitu”

Wajomba ambao walikuwa wakizungumziwa hapo mmoja wapo alikuwa ni Mzee Willium , huyu alikuwa makamu raisi wa kampuni na mwingine alikuwa ni Mzee Sebastian ambae pia alikuwa Mkurugenzi msaidizi., wote hao walishikiria nafasi hizo kutokana na hisa walizokuwa wakimiliki ndani ya kampuni ya Dosam.

Regina hakutaka kuendelea kujibishana na baba yake na alimwambia kesho ahudhurie kikao cha bodi kama kweli anataka kupinga mpango wa kununua kampuni mpya ambayo imeanza kustawi inayojihusiaha na uhandisi wa programu endeshi, pamoja na akili mnemba.

Ijapokuwa Regina alikuwa ashaweka mizizi yake kama kiongozi wa kampuni lakini bado kuna waliokuwa na nguvu ya ushawishi na haikuwa rahisi ya kuwaondoa.

Wafanyakazi kama Eliza , Prisila na wengineo ambao wananafasi za juu na wanamuamini Regina katika maamuzi ukweli ni kwamba ushaiwhi wao unahesabika kama mdogo mno , kwao walikuwa kama wafanyakazi tu.

Hivyo hata kama viongozi hao wakae kikao na kutaka kufanya maamuzi makubwa yasingepita moja kwa moja , lazima yangepita katika bodi ya wakurugenzi na kisha wao ndio wanapiga kura ya kupitisha maamuzi hayo , huo ndio utaratibu kwasababu kampuni ya Dosam haikuwa ya Regina peke yake.

Kilichokuwa kikimuuzi Regina zaidi ni pale ambapo baba yake alikuwa akitumiwa na watu wa nje kujaribu kumbadilisha mawazo , haikuwahi kutokea Mzee Wilsoni kukubaliana na mawazo ya binti yake , siku zote ni mwenye kumpinga.sio kwamba hakuwa akikubaliana nae bali ni kwasababu alikuwa akijaribu kumlinda kwa staili yake , alijua akimfanya Regina kupunguza kujiamini ndio anamlinda.

Sasa wakati Hamza akiwa SamakiSamaki kama angeingia katika mgahawa huo angeweza kumuona James na baba yake wakiwa pamoja na wazee wawili ambao wana miaka makadirio kama ya miaka hamsini hivi wakiwa wamezungukwa na wahudumu ambao walikuwa wamevalia kimitego.

“Mzee Willium kwahio ni kweli Regina anataka kuinunnua Omega?”Aliuliza baba yake James.

Mzee Willium alikuwa na nywele rangi nyeupe tupu, wakati huo walikuwa ameshikilia mrembo mmoja mkono huku akijaribu kuthaminisha maumbile yake.

“Ni kweli kikao cha wahisani kilishapita mbona”Aliongea huku akicheka.

“Mzee Willium nina marafiki zangu kadhaa na tumefanikiwa kumshawishi Wilsoni , tunapanga kupinga kila ambacho Regina ataongea kesho”Aliongea Mzee Sebastiani na kauli ile ilimshangaza kidogo baba James.

“Mzee Wilsoni amekubali?”Aliuliza.

“Wilsoni bado ni mtoto na hajui mambo mengi , tulichofanya ni kusema maneno machache ya hapa na pale na akatuamini , nadhani mpaka sasa amempigia simu binti yake na kumlalamikia lakini ninavyojua mimi Regina hawezi kumchukulia siriasi”

“Kesho katika kikao lazima Regina atakuja na mbinu za kutaka kuwashawishi ili kuinunua Omega , muda huo nitahitaji mnitumie taarifa hio”Aliongea Baba James.

“Usiwe na wasiwasi huna hata haja ya kuomba , tumekuwa tukifanya kazi pamoja kwa muda mrefu , hatuwezi kumruhusu Regina kufanikiwa kuinunua”Aliongea Mzee Willium.

“Ni kweli kabisa alichoongea Willium , tunachosubiri hapa ni James kufunga ndoa na Regina , pumbavu kabisa tunaruhusu vipi undugu wa kitajiri tuliojenga kwa miaka kuishia katika mikono ya msichana mdogo kama Regina”

James mara baada ya kusikia kauli ile alitoa cheko na kisha aliinua chupa ya wine akiwa amesimama.

“Asanteni sana wazee wangu , ili kuonyesha ni namna gani ninashukuru nitawamiminia kinywaji, Baadae kama nikifanikiwa katika mpango wangu Dosam tutainganisha na kampuni yetu , nawahakikishia sitowaangusha , mtapata hisa za kutosha katika kampuni yetu”Aliongea James na mabwana wale matabasamu yalikuwa njenje.

“Usiongee sana unamaliza mate , tunajua ukubwa wa familia yenu , hatuewezi kuishi kwa kujibana bana chini ya utawala wa yule msichana mkatili”Waliongea huku wakicheka na kwa pamoja waliinua glasi zao na kugongesheana.

Baba yake na James alimwangalia mrembo aliekuwa nyuma yake na kisha alimpa ishara, mwanamke yule alielewa somo na kimapozi kabisa alizungusha mkono katika shingo ya mzee Willium huku akilegeza jicho.

“Pedeshee Willium muda umeenda na naogopa , unaonaje ukinipa lift kwenda nyumbani”Aliongea huku akiwa amerembua , alikuwa mweupe na mapaja yake makubwa yalivutia mwanaume yoyote rijali.

“Hakuna tatizo mrembo , wewe niambie unaishi wapi , halafu kama ni mbali kwanini hukuongea mapema , pengine tungeanza safari mapema”Aliongea huku akimkonyeza.

“Aiyaa, Mzee Willium unajua … mimi sitaki bwana….”Aliongea yule mwanamke lakini wakati huo akihakikisha manyonyo yake kumsugua vilivyo Mzee Willium.

Upande wa Mzee Sebastian hakutaka kulembesha na alikuwa akichimba mgodi hapohapo mezani kwa mrembo mwenye umbo matata rangi ya kunde, wote walionekana vilevi vimewakolea.

James na baba yake waliangaliana na wote kwa pamoja walitoa tabasamu lenye uovu ndani yake.

****

Siku iliofuata Hamza alienda kazini kama kawaida na alihakiksiha tarakishi yake haifuatiliwi ili afanye mambo yake.

Hamza alijua alikuwa na kazi kubwa hivyo alihakikisha kwanza kiporo cha jana anakimaliza ili awe na muda wa kutosha wa kufanya ambo yake bila wasiwasi.

Mpaka inafika mchana alikuwa ashamaliza kazi yote na alijifisia kwa kuwa na uwezo mkubwa wa akili wa kufanya vitu haraka haraka.

Baada ya kuona njaa inauma moja kwa moja alitoka na kuelekea mpaka chini kwenye mgahawa.

Kitendo cha kuingia katika mgahawa huo wa kamuni macho yalikuwa yakimwangalia , ukweli ni kwamba tukio la jana ni kama limempa umaarufu na kufanya watu wengi wamfatilia na walifahaua laikuwa msaidizi wa bosi.

Ukiachana na alichokifanya jana siku hio wafanyakazi wa kike ikiwemo Asha na Mirium hamu yao ilikuwa ni kuona namna Yonesi na Hamza wataendeleza pale walipoishia jana, hawakuwa na uelewa kilichotokea jana kwa Yonesi kupigana na Hamza.

Wafanyakazi wengi walikuwa wakiamini lazima Yonesi na Hamza wataishia kuwa wapenzi na hicho ndio ambacho walikuwa wakitamani kuona.

Hamza marra baada ya kuchukua chakula chake hakuhaingika kutafuta sehemu ya kukaa kama jana , aliangalia tu kushoto na alimuona Yonesi akiwa peke yake na alipiga hatua na kwenda kukaa pembeni yake.

“Habari za mchana Kapteni?”Aliongea Hamza

ITAENDEEA-NITAFUTE WATSAPP 0687151346
 
Sehemu ya 18 wapi@singanojr
 
SHETANI RUDISHA AKILI YA MKE WANGU



MTUNZI: SINGANOJR.



“The difference between ordinary and extraordinary is that little extra.”-Jimmy Johnson






TULIPOISHIA

“Oya Mzee unawaza nini? , huna mpango wa kuondoka nini?”Sauti ilisikika nyuma ya Hamza na kumfanya ageuke na kukutana uso kwa uso na Alex muuza vyungu.

“Hamna ndio najiandaa kutoka hivyo”

“Haha,, Hamza una mawazo mengi sana , kila siku ambayo Profesa akimaliza kipindi chake wewe unaishia kushangaa”

“Mara nyingi namchukulia Profesa kama mchungaji pale anapokuhubiria juu ya jambo la Dhambi ambalo unalifanya, kwa urahisi ni kama Profesa anayagusa sana maisha yangu kwa ujumla”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Alex kuangua kicheko.

“Unajua nini braza ,Profesa Singano naona muda mwingi anapoteza muda wake tu lakini hakuna cha maana anachoongea na hilo sio kwangu tu nakuhakikishia ni wachache sana ambao wanaguswa na maneno yake , wengine wote wanapenda kumuona anavyoongea ili kucheka basi lakini sio ujumbe”Aliongea Alex na kumfanya Hamza asiweze kuongeza neno.

“Sio kawida yako kunitafuta wakati wa kumaliza kipindi kama huu kwa ninavyokujua sasa hivi ungekuwa na kundi la warembo kwenye gari yako mnaondoka”Aliongea Hamza.

“Upo vizuri mtu wangu , nimekufuata kwasababu nina mishe nataka msaada wako”

“Mishe gani?”

“Ni kazi nyepesi sana yenye malipo mazuri”

“Okey , nipe mchongo”

“Iko hivi leo nina oda za kupeleka vyungu sehemu mbalimbali na wafanyakazi niliokuwa nao ni wachache na hawawezi kumudu oda zote..”

“Nipo tayari, nishakuelewa unachomaanisha , wewe zungumzia kiasi cha pesa ambacho utanilipa “

“Elfu ishirini unaonaje kwa trip moja”Aliongea Alex na Hamza macho yalichanua , aliona ni dili zuri.

“Kama upo siriasi mimi nipo tayari kwa ajili ya kazi”

“Ndio maana nakukubali Mzee , huna tabia za kulemba lemba kwa kuchagua kazi , sasa sikia muda wa jioni jioni saa kumi ndio utaanza , kuna mfanyakazi wangu nitampa namba yako atakupigia na utafika maeneo ya uzalishaji na kisha utachukua mzigo na atakupa na Anuani wapi unapaswa kupeleka”Aliongea na Hamza hakuona tatizo , alikuwa na uhitaji wa pesa na kama kuna mtu alikuwa tayari kumlipa kiasi kidogo cha pesa kwa malipo ya kawaida aliona hana haja ya kukataa dili hilo.

Baada ya kuachana na Alex Hamza yeye hakuona haja ya kwenda nyumbani mapema hivyo , chuoni kulikuwa na Wife ya bure hivyo kutokana na mara nyingi kutokuwa na bando la kuosha aliona atumie muda huo kukaa chuoni hapo kupakua muvi na kwenda kuangalia getoni kwake.




SEHEMU YA 05.

Muda wa jioni Hamza akiwa chuoni aliweza kupokea simu kutoka kwa mtu aliejitambulisha ni mfanyakazi wa Alex na Hamza mara baada ya kusikia utambulisho wake aliweza kumjua mara moja na palepale alipewa maagizo ambayo Hamza alionekana kuyaelewa na kisha simu ilikatwa.

Dakika chache tu alikuwa tayari ashapata daladala ambayo ilimpeleka moja kwa moja mpaka Mwenge mahali ambapo ndio alielekezwa kushuka.

Kutokana na kuwa mzoefu aliweza kutoka kituoni na kuchukua upande wa kulia kwake na kueleka moja kwa moja mpaka eneo husika.

Hamza alijikuta akishangaa mara baada ya kugundua kazi ya Alex haikuwa kazi ndogo , kwani ilikuwa ni kama Kiwanda.

Jambo hilo lilimshangaza , watu walikuwa wakimchukulia Alex wa kawaida kutokana na kazi yake , lakini Hamza mara baada ya kupita getini na kuingia ndani aligundua ilikuwa ni zaidi ya alivyofikiria , kwani kulikuwepo wafanyakazi wengi.

“Wewe ndio Hamza?”Aliuliza jamaa mmoja mwenye nywele ndeefu mara baada ya kumuona Hamza ana shangaa shangaa”

“Ndio Bro”

“Umefanya la maana kuja haraka maana kidogo tu usingenikuta hapa , nina oda ya kupeleka , njoo nikuonyeshe Mzigo chapu”Aliongea yule bwana huku wakipita wamama ambao walikuwa bize kutengeneza vyungu.

Kulikuwa na utengenezaji wa aina tofauti tofauti , kulikuwa na vyungu ambavyo vilikuwa maalumu kwa ajili ya kuwekea maua na urembo mwingine , kitu kingine ambacho Hamza alikuja kugundua ni kwamba kilichokuwa kikitengenezwa hapo sio vyungu tu.

“Bosi mzigo huu hapa utaupeleka kwenye hii Anuani”Aliongea yule bwana huku akimpatia Hamza boksi ambalo juu lilikuwa na Sticker ambayo mzigo ulipaswa kupelekwa.

“Malipo yanakuwaje baada ya hapa?”Aliuliza.

“Bosi hajakuambia?”

“Hamna tumekubaliana ni 20k ila hajaniambia utaratibu wa kunilipa upoje?”

“Samahani mkuu, iko hivi huu mzigo bado haujalipiwa ukishafikisha utakaguliwa na baada ya hapo utalipiwa bei yake ni laki moja na nusu na gharama ya usafirishaji utapewa hapo hapo”

“Laki moja na nusu!!?”Hamza alijikuta jicho likitoka na kujiuliza ni chungu cha aina gani ambacho kinauzwa laki moja na nusu

Yule bwana alijua mshangao wa Hamza lakini hakutaka kumtolea maelezo yoyote na alionekana kuwa na haraka kwani aliingia kwenye gari na kisha akaondoka.

Hamza alitaka kuuliza kuhusu nauli vipi , lakini alikuwa amechelewa na kuishia kuangalia boksi ambalo lipo chini limefungwa kwa namna ya kipekee..

Alikuwa na shauku ya kujua ni chungu cha aina gani ambayo kinaweza kuwa na bei ghali namna hio lakini asingeweza kufungua.

Baada ya kusoma Anuani ya mzigo unapopaswa kueleka aligundua ni Madale .

Hamza alijaribu kuchunguza mazingira yaliokuwepo hapo ndani na aliweza kugundua hakuna ambaye alikuwa akimwangalia , kulikuwa na vijana wengi pamoja na wamama waliokuwa bize kuteneneza vyungu lakini hawakumwangalia usoni , ni kama hawakujali uwepo wake.

Hamza alinyanyanyua lile boksi na aliona halikuwa zito sana , alitamani kutafuta mfuko kulifunga lakini ilikuwa ngumu kuingia kwenye mfuko wa kawaida labda kwenye kiroba lingefiti lakini kiroba chenyewe hakuwa nacho hivyo aliamua kubeba hivyohivyo na kutoka ndani ya eneo hilo na kwenda kusimama kituoni.

Kama kawaida watu wa jiji la Dar hawakuwa na habari na mtu kila mtu alikuwa bize na mambo yake na Hamza na yeye hakujali watu na kuendelea kusubiri usafiri.

Hamza wakati akiwa kituoni hapo aliona ndio maana Alex alimtajia pesa kubwa kwa ajili ya kusafirisha kwa awamu moja kumbe gharama ya chungu kimoja ilikuwa kubwa hivyo.

Dakika kadhaa tu akiwa amesimama kituoni gari iliweza kusimama na Hamza licha ya kuona gari hio ilikuwa imejaa sana aliingia moja kwa moja na kisha akaweka mzigo wake sehemu husika na kisha akasimama na safari ikaanza.

Muda wa saa kumi foleni ilikuwa kubwa mno kutokana na watu wengi ndio kwanza wanatoka kazini , hivyo ilimchukua dakika nyingi sana kusimama mpaka kufika eneo husika.

Jiji la Dar lilikuwa limeboresheka sana katika maswala ya anuani za nyumba , ilikuwa ukiingia mtandao kwenye ramani unaweza kuona kila nyumba hivyo haikumpa Hamza shida kutafuta nyumba ya mzigo unapopaswa kufikishiwa.

Baada ya kushuka katika kituo husika alianza kutembea kwa kufuatisha Ramani na alitembea kwa dakika kama kumi tu alikuja kusimama kwenye nyumba kubwa iliokuwa na geti rangi nyeusi ambalo lilikuwa limenakshiwa na madini ya shaba.

Hamza aliangalia kulia na kushoto katika maeneo hayo na alionyesha kuridhika , ijapokuwa kulikuwa na nyumba za kawaida ndani ya hilo eneo lakini nyumba nyingi zilionekana ni zile za kifahari na zenye bustani za kuvutia nje.

“Ngoo… ngooo , ngooo!!!”

Hamza aligonga mara tatu na kisha akasubiria kwa dakika nzima lakini hakukuwa na dalili yoyote ya kufunguliwa, na alijikuta akigonga tena kwa dakika nyingine lakini bado mlango haujafunguliwa na aliamua awamu hio kugonga kwa nguvu lakini kabla hata mkono wake haujagusana na geti kijimlango kidogo cha nyumba hio kilifunguliwa.

“Una shida gani?”

Sauti iliokuwa ya kibabe iliweza kusikika na Hamza kwa ufahamu wake wa haraka haraka alijua mtu huyo atakuwa mlinzi kwani hata rafudhi yake haikuwa ile ilionyooka katika kiswahili chake.

“Nimeleta Mzigo”Aliongea Hamza.

“Mzigo gani?”

“Chungu”

“Hapo pembeni yako unaona nini?”

“Pembeni wapi tena?”

“Kushoto kwako?”

“Sioni kitu?”Aliongea Hamza.

Ukweli ni kwamba wakati alipofika hapo aliweza kuona kitufe cha kengele lakini hakutaka kukigusa na aliamua kugonga geti na mlinzi huyo alivyokuwa akimuuliza alikuwa akijua alichokuwa akimaanisha.

“Acha ushamba basi , angalia pembeni yako hapo kuna kengele na Camera , bonyeza hiyo na kisha utasema shida yako”Aliongea kwa hasira na kisha alifunga kijidilisha na kumuacha Hamza kutoa tabasamu la uchungu

Hamza alijiamulia kubonyeza ile kengele mara mbili na palepale aliweza kusikia sauti kutoa ndani”

“Delivery!!”Aliongea

“Ok”

Sauti ya kike iliweza kusikika kutoka ndani na mara baada ya kusubiria kwa dakika kama mbili hivi mlango wa geti ulifunguliwa.

“Kijana unaweza kuingia”Aliongea Mlinzi na sasa Hamza aliweza kumuona yule mlinzi.

Ijapokuwa sauti yake haikuwa imekaa vizuri lakini kimuonekano alikuwa vizuri sana kuliko hata yeye kwa upande wa mavazi.

Hamza mara baada ya kuingia ndani alijikuta akishangazwa na mandhari nzuri pamoja na ufahari wa jengo ambalo lilikuwa mbele yake.

Mlinzi alimuonyeshea ishara Hamza kutembea kueleka upande wa kushoto na Hamza mara baada ya kuangalia upande ambao anaelekezwa ni kando ya bwana la kuogelea sehemu ambayo imejengwa kwa ajili ya mapumziko.

Hamza kila hatua aliokuwa akipiga kueleka hilo eneo mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda mno mpaka mwenyewe kujishangaa , ijapokuwa kiumbe alichokuwa akikiangalia mbele yake kilikuwa kimempa mgongo lakini utashi wake ulimwambia huyo mwanamke alikuwa mzuri sio kawaida.

Hamza alijiambia pengine anachanganyikiwa sana kila anapowaona wanawake warembo kwasababu ni muda mrefu hajakutana na mwanamke kimwili.

Ilikuwa ni kama akili yake ilivyomwambia kwani mara baada ya kufika katika hilo eneo aliweza kukutana na mwanamke ambaye alikuwa nusu uchi , ilionekana kabisa alikuwa akiogelea kwenye hilo bwawa na muda huo alikuwa amepumzika kwani hata mwili wake haukuwa umekauka maji.

Hamza kwa akili yae palepale alijua huyo sio mtu ambaye alimwitikia baada ya kubonyeza kitufe.

Hamza mara baada ya kufika mbele ya mwanamke yule akiwa ameshikilia boksi lake mapigo yake ya moyo yalionekana kudunda sana.

Alikuwa ni msichana mweupe mwembamba kiasi ambaye alikuwa na ngozi laini mno na nywele zake ndefu, alikuwa na macho madogo ambayo yaliendana na namna uso wake ulivyoumbwa.

Ijapokuwa mrembo huyo hakuwa akimfikia yule msichana aliefahamika kwa jina la Tresha Noah ambaye alikutana nae kule kwenye jengo la Apartment la Dosam Homes lakini itoshe kusema huyo alikuwa mrembo na wakuvutia zaidi.

Katika maisha ya Hamza alishakutana na wanawake wa aina nyingi , kuna wanawake ambao alikutana nao licha ya kwamba walikuwa na uzuri wa aina yake lakini hawakuwa wakivutia kingono , kuna wanawake wengine ambao alikutana nao licha ya kwamba hawakuwa na muonekanno wa kirembo lakini walikuwa wakivutia mno kingono(Sexy), hizo ni aina mbili ambazo alikutana nazo Hamza , ijapokuwa mrembo huyo hakuwa mzuri sana lakini alikuwa na umbo ambalo linavutia kingono sana, yaani ni aina ya wanawake ambao ukimuona tu unawaza kufanya mapenzi.

“You are Hamza right?”Aliuliza yule mwanamke na sauti yake ilimuacha Hamza hoi.

“Yes.,.. yess”Alijibu kwa kubabaika.

“Okey nimepewa taarifa zako na Alex ,unaweza kufungua nithibitishe mzigo”Aliongea yule mwanamke , hakuwa na sura ya dharau wala ya ukarimu yaani alikuwa katikati huku akionekana kumkagua Hamza.

Hamza hicho ndio kitu pekee ambacho alikuwa akitaka kufanya , alikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini chungu hicho kilikuwa kikiuzwa pesa nyingi sana kuliko uhalisia.

Ilimchukua dakika chache sana kwa Hamza kufungua ndani , ijapokuwa kwa mtu wa kawaida angehitaji kisu kukata hizo gundi lakini Hamza hakuhitaji kisu na namna ambavyo alifungua ilimshangaza kudogo yule mwanadada lakini hakuongea chochote zaidi ya kubakia kimya.

Hamza mara baada ya kufungua lile boksi macho yake ni kama yamesaliti matarajio yake , ukiachana na namna ufungashaji wa chungu hicho ulivyo lakini hakikuwa na muonekano ule wa kimaajabu , kilikuwa chungu kama chungu ambacho muonekano wake ulikuwa wa kawaida sana , vilikuwa vyungu kama vile vya kitamaduni ambavyo wamama wengi hupikia.

Jambo hili lilimfanya Hamza kushangaa na kujiuliza nini kinaendelea , alijaribu kuangalia ndani yake kwani mwanzo alijua pengine kuna madawa ya kulevya kwenye hilo boksi lakini hakukuwa na kitu chochote cha kushangaza zaidi ya chungu.

“Kaka , inaonekana hii ni mara yako ya kwanza kufanya Delivery”

“Kwanini?”

“Unashangaa sana”Aliongea yule msichana huku akisimama na kumpokea Hamza kile chungu na kuanza kukichunguza kwa dakika kadhaa na mara baada ya kuridhika alitoa tabasamu na kumpatia Hamza kukirudisha kwenye boksi.

“Wait here”

Aliongea huku akibeba kile chungu na kutembea kuelekea upande mbele wa jengo hilo sehemu ambayo kuna mlango wa kuingilia ndani.

Hamza macho yake yalikuwa yakiangalia mpwito wa makalio ya mrembo huyo ambaye hakuwa akijali kama amevalia kijichupi tu na kuingia hadi ndani.

“Kuna watu wanafaidi aisee”Alijiwazia Hamza mara baada ya mrembo yule kutokomea kwenye jumba hilo ambalo lilikuwa na ghorofa mbili kwenda juu.

Hamza alitumia dakika hio kujaribu kukagua mazingira kwa haraka haraka na ile anagueza sura yake macho yake yalikutana na mlinzi aliekuwa akimwangalia na baada ya kukutanisha nae macho alionekana kama mtu ambaye alikuwa akimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida na Hamza alishindwa kuelewa lakini aliamua kupotezea na kugeuza macho yake sehemu nyingine.

Baada ya dakika kama sita hivi mwanamke yule alirudi huku awamu hio akiwa tofauti na alivyokuwa , alikuwa amejisitiri kwa kuvalia vazi refu la kitambaa cha hariri(Silk Duster) ambalo lilikuwa na vishikizo huku kichwani akiwa amevaa Bonnet.

Alikuwa hajalifunga vishikizo vyake na kumfanya bado nguo yake ya ndani kuonekana.

“Hesabu hizi?”Aliongea yule mwanamke huku awamu hii akiweka tabasamu na kumfanya Hamza kushangaa kidogo na kujiuliza mwanzoni hakuwa na mwonekano wa kusomeka lakini sasa hivi alikuwa akitabasamu.

Hamza alihesabu kwa haraka sana zile hela na baada ya kumaliza aligundua ni Shilingi laki moja na tisini.

“Hela iliozidi ni kama ofa Hamza , naamini utakuwa mwaminifu kuniletea mzigo wangu mwingine kila nitakapohitaji”Aliongea huku akiweka tabasamu na kuufanya uzuri wake kuzidi kuongezeka.

“Asante sana”Aliongea Hamza , ijapokua hakuelewa mwanamke huyo anamaanisha nini kumwambia anategemea kuletewa mzigo mwingine na yeye lakini hakutaka kuuliza.

Hamza mara baada ya kuaga aliweza kutoka nje ya geti huku bado akiwa na maswali mengi sana , swali lake kubwa ni kwanini chungu cha kawaida kama kile mwanamke huyo akakinunua kwa bei ghali,

Ilikuwa ni ajabu ambayo chungu cha kawaida ambacho kilikuwa kikiuzwa sokoni kwa shilingi elfu tatu kununuliwa kwa zaidi ya laki mbili.

Hamza alijiambia hata kama watu hao ni matajiri lakini bei hio ni kubwa sana kiasi kwamba haina uhalisia , akili yake palepale ilimwambia pengine kuna kitu cha ziada kwenye kile chungu lakini hakujua, kwani kila kitu hakikumwingia akilini.

Ijapokuwa alikuwa akijua madawa ya kulevya yalikuwa yakisafirishwa kwa mbinu nyingi lakini ilikuwa ngumu madawa kusafirishwa kwenye kile chungu, lakini hata hivyo hivyo hakutaka kufikiria zaidi.

Wakati akianza kutembea kukisogelea kituo cha daladala simu yake ilianza kuita na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Alex na palepale alipokea.

“Hahaha.. Bro kazi nzuri”Sauti ya Alex ilisikika bila hata ya salamu.

“Nimeleta mzigo tu sehemu husika , ni swala ambalo mtu yoyote anaweza kufanya”

“Hapana Bro , ni kweli linaweza kuonekana swala la kawaida lakini sio la kawaida kama unavyoona wewe”

“Unamaanisha nini?”

“Tutaongea usijali , ila nikuambie mwanangu sijui niseme una bahati au kuna siri kuhusu inayoendelea ,ila kwanzia sasa hivi utahusika na kumpelekea huyo demu kila atakapohitaji mzigo , amenipigia simu na kusema lazima iwe wewe”Aliongea Alex na kumfanya Hamza kusimama kwanza.

“Alex unajua mambo mengi umeniacha hewani , nina maswali mengi sana , itoshe kusema leo ni siku ambayo imenifanya kushangaa sana”

“Najua bro lazima utakuwa na maswali ila utajua , kwasasa elewa kwamba utakuwa unampelekea huyo manzi mzigo wake na malipo yatakuwa mazuri”Aliongea Alex na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.

“Tunakutana wapi nikupe hela ya mzigo”

“Haina haja mzee unaweza kwenda nayo, hio chukulia kama pesa ya kujikimu kwa mwanzo wa kazi yako”Aliongea na palepale simu ilikatwa na kumfanya Hamza kuzidi kuchanganyikiwa

Kitu kingine kilichomfanya kuchanganyikiwa ni kama Alex alikuwa akiongea kinafiki ila hakutaka kuwaza sana kuhusu Alex bali aliwazia vyungu.

“Kuna siri gani juu ya hivi vyungu..?”

Ndio swali ambalo liliibuka kwenye kichwa chake na hali ya kutaka kuanza udadisi ilimvaa palepale , Hamza alijikuta akitengeneza Scenerio mbalimbali kwenye kichwa chake kuhusu vyungu ambavyo anatengeneza Alex.

Ukweli ni kwamba hata yeye aliona kuna kitu ambacho sio cha kawaida tokea dakika ambayo aliingiza mguu katika kiwanda cha Alex cha utengenezaji vyungu.

Hamza alianza kufikiria mbali zaidi na kujiambia hili swala halikuwa la kawaida tokea siku ambayo anaisikia Alex alikuwa muuza vyungu , kulikuwa na wafanyabiashara wengi nchini ambao wanatengeneza vyungu iweje Alex biashara hio imtoe na kuwa na maisha mazuri namna hio.

Safari yake ya kupata majibu ni kama ndio imeanza rasmi , kwanza kabisa alishajua aina ya vyungu ambavyo vilikuwa vikitengenezwa lakini pia alijua uthamani wa vyungu vingine , kilichokuwa kimebakia ni kujua nini siri iliokuwemo kwenye vyungu hivyo.

Swali tu la kumshangaza Hamza ni kwamba kwanini maisha yake yamejaa mshangao tokea siku anajitambua.

******

Saa kumi na mbili kamili za jioni Hamza alikuwa eneo la Mwenge , ijapokuwa haikuwa mwisho wa safari yake lakini aliamua kushukia hapo huku akiwa na wazo moja akilini na hio yote ni kutokana na kuwa na pesa nyingi mfukoni.

Hamza mara baada ya kushuka kituoni alivuka barabara upande mwingine na kisha akaingia kwenye maduka ya nguo, alikuwa na wazo la kununua nguo kwa ajili ya kwenda kwenye usaili siku ya kesho.

Ijapokuwa kwake ilikuwa kichekesho kwenda kwenye usaili huo kutokana na aina ya kazi yenyewe lakini hakutaka kudharau hata kidogo , kitendo cha kupigiwa simu asubuhi kilimwaminisha yoyote ambaye alituma lile tangazo alikuwa siriasi , lakini shauku yake nyingine ni kwamba kama mtu huyo alikuwa siriasi na kuamua kumlipa mtu zaidi ya laki saba wa ajili ya magizo tu basi ilimaanisha kwamba ni mwanamke mwenye pesa , lakini vilevile huenda kuna sababu ya ziada.

Hamza moja kwa moja aliingia kwenye jengo la Dosam Shopping Mall . hili ni jengo ambalo alikuwa akitamani sana kuingia siku moja kwa ajili ya kununua nguo , lakini kutokana na kukosa pesa kila siku alikuwa akiliogopa kama ukoma,lakini siku hio alikuwa na zaidi ya laki na nusu mfukoni hivyo aliamua kuzitumia katika manunuzi ya nguo kadhaa na kisha baada ya hapo angeenda saluni kuweka muonekano wake vizuri.

Sifa kubwa ya maduka ya Dosam ambayo yametapakaa nchi nzima ni nguo zake kuwa bora lakini kwa bei nafuu kabisa , ilikuwa ni tofati kabisa na madumka ambayo yalikuuwa yakipantikana mlimani City na kwingineko.

Kwa mfano Mlimani unaweza kukuta nguo inauzwa bei lakini ubora wake ukafanana na nguo ambayo inauzwa katika maduka ya Dosam, na inasemekana tokea kampuni ya Dosam kufungua maduka ya nguo biashara nyingi zimefirisika sana kutokana na mauzo kupungua.

Sifa nyingine katika maduka haya ni huduma ya viwango vya juu sana , yaani hawakujali muonekano wa mteja ambaye alikuwa akifika kufanya manunuzi katika maduka yao, wao walimjali kila aina ya mteja na kuwakwa daraja sawa na muda wote walikuwa ni watu wenye tabasamu usoni na wangekusaidia katika machaguzi ya nguo mpaka pale utakaporidhika.

Jambo hili lilimfanya Hamza kukubali sana mmiliki wa kampuni ya Dosam Global,

Ukweli ni kwamba inasemekana kampuni ya Dosam mmiliki wake ni mwanamke tena pengine ni kosa kusema mwanamke bali ikawa sahihi kusema ni Msichana ndio mmiliki.

Mwanzoni kampuni hii ilimilikiwa na Mzee Lasuli Dosam mwenywe na mara baada ya kufariki inasemekana usimamizi na urithi wa makampuni yote ulienda kwa mjukuu wake kike.

Uzushi unaenda mbali zaidi na kusema kwamba msichana huyo ambaye ni mmiliki alikuwa ni mrembo haswa , pengine zaidi ya neno lenyewe la Urembo lakini pia kwa wakati mmoja alionekana kuwa ni mwenye akili nyingi , baadhi ya watu walikuwa wakimtaja kama kiumbe kutoka sayari nyingine.

Jina hilo liliibka kutokana na kwamba aliweza kufanya biashara nyingi katika mataifa mbalimbali kupata hasara kubwa kutokana na mbinu zake za kibiashara tokea kupewa uongozi wa kampuni , vyombo mbalimbali vya habari vishawahi kumwandika kuhusu mwanamke huyo.

Hamza yote hayo alikuwa akiyajua , isitoshe alikuwa ni mtu mpenda mitandao ya kijamii hivyo ilikuwa ni rahisi kwake kukutana na taarifa ambazo zinamzungumzia , ukweli ni kwamba kukutana na taarifa hizo kwenye mitandao sio jambo la bahati mbaya , ukweli ni kwamba kuna taarufa zake nyingi , kwa mfano tu katika mtandao wa kijamii wa JamiiForum umejaa mada zinazomzunguzia mmiliki wa kampuni ya Dosam Global mara mia nne tokea kupewa uongozi , sio hivyo tu majarida makubwa duniani na yenywe yamemzungumzia mara nyingi sana na kufanya mahojiano nae.

Ajabu ni kwamba katika kila mahojiano ambayo yalifanyika inasemekana mwanamke huyo alikataa kupigwa picha.

Kuna wengine wanasema mrembo huyo alikuwa mbaya wa sura ndio maana hakutaka kuonekana lakini wale ambao wameenda kumfanyia mahojiano walisema alikuwa mrembo wa sura na hata wale ambao walikuwa wakifanya kazi katika kampuni hio walikuwa wakisema ni mrembo wa sura.

Hamza alijikuta akiwaza kila aina ya mada ambazo alizisoma mtandaoni kuhusu mmiliki wa kampuni ya Dosam na kilichomfanya kukumbuka taarifa hizo ni siku hio mara baada ya kuingia kwenye duka hilo.

“Kaka hii itakufaa sana , kwanza kabisa inaendana na mwonekano wako wa mwili kwanzia rangi yako mpaka urefu na unene wako , kitu kimoja ambacho kitakufanya upendeze zaidi ni kunyoa nwele kwa mtindo huu”Aliongea mwanamke mrembo sana huku akimuonyesha Hamza vazi maalumu ambalo amechagua.

Hamza aliweza kushika kishikwambi huku akiangalia mtindo wa nywele ambao mfanyakazi wa eneo hilo amependekeza na aliishia kutoa tabasamu.

“Sijazoea kunyoa hivi dada”AliuongeaHamza.

Mtindo wa nywele ambao aliokuwa akiangalia kwake ni kama haukukaa kimaadili, pengine sio kwamba mtindo wenyewe haukukaa kimadili lakini kutokana na sheria zake au pengine aina ya maisha aliokulia ndio maana aliona ni mtindo ambao haukukaa kimaadili.

Ilikuwa ni kama vile wale wazee waliozaliwa miaka ya sitini na sabini uwaambie wanyoe kiduku ukweli ni kwamba hawatokuelewa, lakini sasa kidogo ilishangaza kwa Hamza kwani alionekana ni kijana kabisa ambaye hata miaka therathini hajafikisha.

Yule mfanyakazi wa kike mrembo aliishia kushangaa kidogo lakini aliubadilisha mshangao wake na tabasamu.

“Kaka niamini , huu ni mtindo ambao utamfanya mwanamke yoyote yule kukupenda , kwanza wewe ni handsome na kwa muonekano wako ni kama vile Justin Timberlake, hivyo staili yako ya nwele inakupasa kufanana…..”

Hamza kwa namna ambavyo mwanamke huyu alivyokuwa akiongea ungeweza kuamini na kujisikia vizuri lakini kilichomfanya kutokuamini maneno yake ni kwamba pembeni yake kulikuwa na bwana ambaye alikuwa ni mweusi sana na kichwa kama kibuyu aliekuwa pia akihudumiwa , ukweli katika maisha yake hakupenda kujifanananisha lakini alisema ijapokuwa yeye hakuwa akijiona Handsome lakini huyo bwana aliekuwa pembeni yake alikuwa na sura ngumu mno, ndio mwanaume hasifiwi kuwa na sura nzuri lakini kilichompa mshangao ni namna ambavyo mfanyakazi alivyokuwa akimpamba kwa kumwambia alikuwa na sura nzuri na kichwa kizuri, hivyo ilikuwa ni ‘redflag’ ya kuona hata yeye alikuwa akipambwa tu kinafiki nje ya uhalisia wa muonekano wake.

Iliimchukua kama nusu saa kuhudumiwa na kisha alipewa nguo zake na kutoka, alikuwa amenunua suruali mpya , Jeans pamoja na viatu na ajabu ni kwamba hakuwa amelipa pesa nyingi, kilichokuwa kimebakia ni kwenda Saluni na kuweka nywele zake sawa kwa ajili ya maandalizi ya kesho.

Hamza wakati akitoka kwenye Lift alijikuta akijichekea , yaani kwa namna ambavyo alikuwa akijiandaa ni kama vile anakwenda kukutana na mchumba au anaenda kwenye ‘Blind date’, alicheka kutokana na kwamba siku kadhaa zilizopita wakati wa kumtongoza mwanamke mrembo kama Anitha hakujali kabisa muonekano wake zaidi ya hisia zake, tena anakumbuka ile siku shati lake lilikuwa limechafuliwa na juisi ya matunda wakati akiwa kwenye daladala na kutengeneza doa..

Hamza alitamani kughairisha kwenda saluni lakini kuna roho ilikuwa ikimwambia ‘ingia saluni bro upendeze acha uchafu’, pengine mwanamke unaekwenda kukutana nae ni zaidi ya Anitha.

Hamza mwenyewe alishangaa na kujiuliza hio sauti inatoka wapi , lakini aliamua kuitii na kujiambia pengine ni roho mtakatifu , lakini mara baada ya kuingiwa na neno Roho mtakafitu alipotezea na kujiambia kwanza hakuelewa yeye ni dini gani hivyo aliamua kupotezea kile anachofikiria na kuamua kufuata utashi wake unakomwelekeza.

“Bro unanyoa staili gani?”Aliuliza kinyozi mara baada ya Hamza kukalishwa kwenye kiti na kinyozi kumaliza maandalizi yake.

Hamza alifikiria ni staili gani anyoe , au apige para..”Alijikuta akikosa majibu na palepale macho yake yalitua kwenye picha ambazo zilikuwa na vichwa ambavyo vimenyolewa kwa staili tofauti tofauti.

Baada ya kuangalia ni staili gani ingemfaaa palepale alijikuta akiishia kwenye staili ambayo alionyeshwa muda mchache uliopita na yule muuza nguo,.

“Bro hio staili ni nzuri na inaendana na nywele zako lakini kidogo itakugharimu, kwani ili upendeze utahitajika na kuosha pia na kupakwa dawa”Aliongea kinyozi akiwa na wasiwasi Hamza asingeweza kumdumu bei.

“Ni shilingi ngapi jumla?”

“Kwa kila kitu nilichokutajia jumla yake ni elfu kumi na tano tu?”Aliongea .

“Ni bei kubwa ndio ila nitalipia”Aliongea Hamza na yule bwana alimwangalia kidogo na kisha akaanza kupiga kazi,

Hamza hakuwa mwafrika orijinal bali alikuwa ni chotara , mchanganyiko wa Mwafrika na mzungu hivyo nywele zake zilikuwa zimekaa kizungu pia japo rangi yake ilikuwa imefubaa kidogo kupoteza ile hali ya uzungu yaani kwa maneno marahisi ni kwamba uzungu wake umeathiriwa na rangi ya kiafrika.

Zilipita dakika chache tu kama nusu saa hivi kinyozi alikuwa ashamaliza kumuweka Hamza sawa upande wa nwele na alitakiwa kuweka dawa pamoja na kuoshwa na kukaushwa na hakuwa na hiyana kufuata maelekezo kutokana na kwamba ndio mwenyewe aliamua kuyavulia maji nguo hivyo hakuwa na budi kuyaoga.

Baada ya lisaa lizima aliweza kusafishwa vizuri na alipewa na ofa ya kusafishewa uso na Scrub .

“Edmund naelekea nyumbani , bado hujamaliza tu?”Sauti ya kike iliweza kusikika katika Saluni ambayo Hamza anapunguza nywele.

“Leila nisuburi kuna bwana anamalizia kukaushwa nataka nione kama hana kasoro tuondoke”Aliongea kijana huyo na kumfanya Leila kuvuta pumzi na kisha kwenda kukaa kwenye sofa.

“Zamu yako ishaisha , leo mapema sana mpenzi”Aliongea Edmund.

“Bosi katoa maagizo kila mfanyakazi anaefikia malengo ya mauzo kwa siku anaweza kuondoka hata kama ni mchana”Alijibu na kumfanya Edmund kutingisha kichwa huku akichomoa simu yake chaji.

Dakika ileile mlango wa chumba cha wanaooshwa kwenye saluni hio kilifunguliwa na Hamza aliweza kutoka akiwa anawaka hatari na kumfanya yule mdada aliekuwa ameketi kwenye Sofa kupigwa na mshangao.

“Kaka nilikuambia hio staili ya nywele itakufaa , jamani hebu muone alivyopendeza”

Msichana Leila alikuwa ndio aliemhudumia Hamza katika kununua mavazi na aliweza kumtambua Hamza mara baada ya kumuona.

“Leila unamjua?”

“Yeah mimi ndio nilimuelekeza kuja hapa”Aliongea huku akimwangalia Hamza kwa macho ya kurembua na kumfanya Edmund kuona wivu.

Ukweli hata Hamza mara baada ya kujiangalia kwenye kioo alijiona kabisa amebadilika , ijapokuwa bado alikuwa na mavazi yake yaleyale lakini aliamini kama atavaa alionunua basi atakuwa ni mtu mwingine kabisa, aliishia kutoa tabasamu kwa kujikubali na kujiambia yeye kumbe ni Hamdsome aliekosea matunzo.

“Bro naona umekaa sawa sasa , unaweza kulipa sasa , nilikuwa nikikusubiria wewe tu”Aliongea Edmund huku akimkatisha Hamza ambaye alikuwa akijiangalia kwenye kioo pasipo ya kuridhika.

“Okey ngoja nilipe”Aliongea na palepale aliingiza mkono mfukoni na kutoa pesa nyekundu mbili na kisha kumpatia”

“Sister asante kwa kupendekeza hii staili ya kunyoa , chenchi inayobakia ni shukrani yangu kwako”Aliongea Hamza huku akitoa tabasamu na palepale alimkonyeza Leila na kuchukua mifuko yake na kutoka.

“Broo….!!”Edmund alitaka kuongea neno lakini palepale Leila aliekuwa akimwangalia Hamza kwa macho ya kurembua alimpa ishara ya kufunga mdomo wake.

Siku iliofuata Hamza hakuwa na ratiba za chuo kabisa mpaka jumatatu, yaani siku hio ilikuwa ni Ijumaa na kwa kozi aliokuwa akisomea ni kama wikiendi ndio imeanza rasmi.

Usiku hakuwa amelala kabisa , alikuwa na mawazo mengii, kwanza aliwaza sana kuhusu mtu anaefahamika kwa jina la Mzee mtu ambaye hakuwa akimjua licha ya kwamba amehusika katika maisha yake kwa kiasi kikubwa , aliwaza namna ya kumfahamu Mzee ni nani na kwanini alikuwa akimtafuta nyakati za usiku , aliwaza mambo mengi kuhusu mzee na kujijengea picha katika akili yake na kujiambia pengine Mzee ni mtu mzito serikalini .

Mawazo ya namna hio yalimjia kutokana na maisha ambayo amekulia kulingana na maagizo ambayo Mzee alitaka awe.

Yaani kwa maneno marahisi ni kwamba mpaka wakati huo Hamza hakuwa ameyaishi maisha yake , ni kama maisha aliokuwa akiishi ni kwa ajili ya Mzee kwani ndio aliekuwa akimwambia afanye hivi na vile na yeye kutii.

Alikumbuka siku ambayo hakutii maagizo ya Mzee na kilichomkuta mpaka siku hio na umri wake huo hajawahi kusahau , sasa kutokana na tukio hilo ambalo lilimtokea ilimfanya kuamini pengine mzee ni mtu mkubwa sana serikalini , ukweli ni kwamba alikuwa na mawazo mengi kuhusu Mzee.

“Kama mzee hataki kujitokeza kwangu mimi nitajitokeza mbele yake uwezo huo ninao”

Aliongea Hamza baada ya kuwaza , alionekana ameamua mwenyewe katika kichwa chake na kujiambia kama mtu huyo anaemtambua kwa jina moja tu la Mzee asipojitokeza kwake basi yeye atajitokeza kwake ,. Hakujua ni kwa namna gani ambavyo angemfahamu Mzee lakini alijiambia kutokana na uwezo wake basi lazima amfahamu mzee .

Hamza hakuwaza tu kuhusu Mzee pia aliwaza kazi ya Alex ya utengenezaji vyungu namna ambavyo ilionekana kumtajirisha nje ya uhalisia wa biashara wenyewe , alikuwa na shauku ya kutaka kujua kilichopo nyuma ya vyungu vile ni nini, kuna hali ilikuwa ikimwambia pengine ni njia nyingine ya usafirishaji madawa lakini alipingana na mawazo yake na akili yake ilimwambia kabisa pengine ni kitu kingine kabisa ambacho hajawahi kukifikiria kwenye maisha yake, kutokana na mawazo mengi alijiambia pia hilo ni swala ambalo atalitafutia ukweli.

Baada ya kuoga vizuri na kujiandaa kwa kuvaa mavazi yake mapya na viatu, licha ya kwamba hakuwa na kioo lakini aliamini alikuwa amependeza haswa.

Usaili kwa maelekezo ya mwanamke kwenye simu alimwambia ni saa nne asubuhi katika hoteli ya Dosam V

Hamza alikuwa akijua hoteli hio vizuri kwani ilikuwa ni hoteli maarufu na yenye jengo refu kwenda juu ndani ya jiji lote la Dar es salaam , pengine asilimia hamsini ya watanzania wote walikuwa wakiijua hoteli hio kwani matamasha mengi hufanyikia hapo, hata vikao vya waandishi wa habari hufanyikia ndani ya hoteli hio.

Siku hio pengine ndio inakuwa mara yake ya kwanza kuingia katika hio hoteli,lakini licha ya hivyo hakuonekana na wasiwasi kabisa.

Hakutaka hata kujihangaisha na maswala ya nchi asubuhi hio na alijiambia atajua mbele kwa mbele.

Mara baada ya kutoka nje ya eneo hilo la uswahilini wanawake na wanaume walikuwa wakimkodolea macho kwa mshangao mkubwa.

Ukweli ni kwamba muoenknao wa Hamza ulikuwa hauendani kabisa na maeneo hayo ya uswahilini , kitendo cha kuchanganya rangi ya mzungu na mwafrika ilikua ni kama sababu kubwa ya kumuona Hamza sio wa kawaida.

Hata asubuhi hio watu wengi sio kama walikuwa wakimwangalia kutokana na kupendeza kwake bali ni kwamba walikuwa wakimwangalia huku wakijiambia moyoni Hamza amerudi katika uhalisia wake na maisha ambayo alikuwa akiyaishi hapo na familia hizo ni ya magizo tu.

“Niliwaambia mimi , hakuna mtu mzungu akawa masikini hivi”Aliongea mmoja ya viijana walioamkia kucheza pooltable.

“Juma uko sahihi , hata mimi kwasasa nakuunga mkono , jamaa hakuwa mwenzetu kabisa, ule upole wake ulikuwa ukificha mambo mengi”Alichangia mwingine. Na stori juu ya Hamza hazikuishia kwa wacheza pooltable tu hata wanawake waliokuwa wakiuza vitafunwa nje ya vibaraza vya nyumba zao walikuwa wakimzungumzia Hamza.

Hamza kutokana na watu wengi kumshangaa kwake ilitosha kumwambia kwamba alikuwa amependeza.

Naam ni saa tatu na nusu Hamza aliweza kufika kandokando ya bahari ya Hindi nje ya geti la kuingilia katika hoteli ya Dosam.

Tofauti ya Hamza na wageni ambao walikuwa wakiingia ndani ya hoteli hio ni kwamba yeye alishuka na basi la mwendokasi lakini wageni wengine wote aidha walifika wakiwa kwenye gari binafsi au waliletwa hapo na Uber , Bolt na magari mengine yanayofanya huduma ya Taxing,

Licha ya hivyo swala hilo halikumpa unyonge sana Hamza , pengine kwa watu waliokuwa wakimwangalia wangesema labda Hamza alikuwa amejipa uzoefu mwingine wa kupanda magari ya abiria.

Mwonekano wake ulimbeba,alikuwa ni mtanashati mno, Hamza alikuwa ni mwanaume mrefu kwenda hewani , mwenye mwili ambao umejengeka kimazoezi akiwa na weupe wa kuchanganya rangi na macho yake ambayo yana kiini ambacho hakikuwa cheusi sana kama waafrika wengi , pengine uzungu wake ulionekana zaidi machoni kuliko sehemu yoyote ya mwili lakini hata hivyo ilikuwa kosa kumuita Mzungu.

Katika mavazi yake aliovaa kitu pekee alichokosa ilikuwa ni saa tu mkononi , pengine ingemfanya kuonekana Handsome zaidi lakini hata hivyo bado alionekana kupendeza.

Hamza alitembea kwa kujiamini kana kwamba alikuwa ni mzoefu kabisa wa eneo hilo.

“Ni muda mrefu sana nimejitenga na maeneo ya namna hii , nadhani ni mwanzo wa mimi kurudi kwenye maisha yangu”Alijiwazia Hamza huku akiongea kauli ambayo kidogo inachanganya.

“Hello!, nina miadi na mtu ndani ya hii hoteli?”Aliongea Hamza mara baada ya kufika katika Front desk.

“Karibu sana kaka , nitajie jina la mgeni unaetaka kukutana katika hoteli yetu tafadhari”Aliongea yule mwanadada na kumfanya Hamza kuwaza kidogo , ukweli ni kwamba hakuwa akijua jina lake kamili na aliambiwa tu kufika ndani ya hoteli hio muda wa saa nne.

Wakati akijiuliza ni jina gani anapaswa kutaja palepale simu yake ilianza kuita na aliitoa haraka haraka na kuangalia jina la mpigaji na alitoa tabasmau na kumwangalia yule mrembo wa mapokezi akimpa ishara kwamba anapiga.

Hamza aligeukia upande mwingine ili kuongea na simu lakini macho yake yalitua kwa mwanamke mrembo sana ambaye alikuwa akisogea katika dawati la eneo la mapokezi.

“Hello Mr , uko wapi unakumbuka miadi ni saa nne kamili?”Sauti ilisikika upande wa pili lakini wakati huo macho ya Hamza yalikuwa kwa mwanamke aliekuwa akitembea kimadaha kusogelea upande wake.

“Nipo eneo la mapokezi ndani ya hoteli ya Dosam”Aliongea Hamza na palepale yule mwanamke alisimama huku akitoa simu yake sikioni na kuangalia mbele yake na palepale alionekana kugundua kitu na haikuwa kwake tu hata kwa Hamza mwenyewe alionekana kugundua mtu aliekuwa akiongea nae kwa simu ni mwanamke aliekuwa mbele yake.

Sasa tofatui ni kwamba Hamza mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda mno kutokana na kushangaa urembo wa mwanamke ambaye alikuwa akimsogelea huku akiwa na uso uliopambwa tabasamu.

Hamza ni kama hakuamini kama huyo ndio mwanamke ambaye alikuwa akienda kuonana nae.

Kuhusu yule mwanamke hakuonyesha mshangao wowote wa Hamza , yaani ni kama Hamza alionekana wa kawaida sana na mara baada ya kumfikia alinyoosha mkono kwa ishara ya kusalimia.







SEHEMU YA 06.

Wasichana wawili ambao walikuwa eneo la mapokezi kidogo walionyesha kukosa utulivu mara baada ya kumuona mwanamke alievalia suti akisogea upande wao na walijua pengine alikuwa akiwasogelea lakini walijikuta wakishangaa mara baada ya kumuona mwanamke yule akisimama mbele ya Hamza na kunyoosha mkono.

“I Suppose wewe ndio Hamza right!!?”Aliuliza yule mwanamke akiwa na tabasamu usoni.

“Yes ndio mimi Hamza Mzee”Aliongea Hamza huku akionyesha kukosa utulivu kiasi na kunyoosha mkono wake kusalimiana nae.

Wakati wa kushikana mkono na yule mwanamke alihisi ni kama kuna shoti za umeme zinampiga kwani zilianzia mkononi na kwenda kichwani kutoa mawasiliano kama ameshikana na kitu kisichokuwa cha kawaida na baada ya pale taarifa zilitumwa kwenye moyo kwa ajili ya kuongeza msukumo wa damu kuelekea kiwiliwili cha chini na ghafla tu kiungo cha uzazi cha Hamza kilianza kusisimka.

Muunganiko wa mwili ulikuwa ni wa ajabu sana na pengine Mungu katika kazi aliopatia ni kuumba kiumbe binadamu.

Mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa ni mweupe wa wastani, mrefu kiasi mwenye mwili uliojipanga huku ngozi yake ikiwa ni kama vile imetengenezwa , itoshe kusema katika wanawake ambao Hamza alishawaona tokea afike jijini Dar es salaam huyo ndio mwanamke wa kwanza kwa uzuri , Melissa mpenzi wake Amiri alijiambia tupilia kule , Tresha Noah msichana alieambiwa alikuwa ametengenezwa muonekano wake tupilia kule , Anitha hakutaka hata kuongea zaidi ya kutamani kusonya.

“Mr Hamza!, naitwa Prisila Singano Afisa mkuu wa idara ya Rasilimali watu kampuni ya Dosam, mimi ndio niliekupigia simu nadhani sauti yangu hujaisahau”Aliongea kwa mapozi na kumfanya Hamza kuzidi kupagawa , hakuamini huyu ndio mwanamke ambaye alikuwa akitafuta mchumba wa maigizo.

‘Nimefurahi kukufahamu mrembo Prisila Singano , lakini naomba kuuliza una undugu na Profesa Stephano Singano?”Alongea Hamza huku akiwa anajiamini kiasi kwamba kama unamjua ungesema hio hali ya kujiamini kaitolea wapi, maana Hamza tunaemjua sisi ni yule Mzembe aliepigwa cha mbavu na mrembo Anitha.

Wale wafanyakazi wa mapokezi walikuwa na maswali kibao , walikuwa wakimfahamu Prisila sio mtu wa mchezo mchezo ijapokuwa alikuwa mdogo ki umri lakini alikuwa ni mkali mno kazini na hakupenda uzembe lakini sio hivyo cheo chake kilikuwa kikubwa mno ndio aliekuwa ni CHRO wa kampuni ya Dosam Global.

Kila mwanadada ndani ya jiji la Dar es salaam ambaye alikuwa ni mtaaluma alikuwa akimchukulia Prisila kama ‘role model’ wao kutokana na mafanikio yake ya haraka haraka na kuongoza kampuni kubwa Afrika na duniani.

Yaani kwa maneno marahisi yeye ndio alikuwa mwajiri mkuu wa kampuni ya Dosam hivyo watu wengi wanaotafuta ajira walikuwa lazima wapitie kwa huyu mwanamke, kutokana na watu wengi kutaka kufanyia kazi katika kampuni ya Dosam wale ambao walipata nafasi hawakutaka kuzembea kazini na kutolewa , kwani kudumu ndani ya kampuni ya Dosam ilihitajika zaidi utendaji mzuri na ujuzi na sio maswala ya GPA au ufaulu mkubwa unaonekana katika cheti chako.

Hivyo ilimfanya Prisila kuogopeka sana kwani alikuwa ni mwanamke aliekuwa akienda na falsafa yake ya 4E katika eneo la kazi ambayo ilisimama kama mbadala wa Effort(juhudi), Excellence(Ubora), Embodiment(Mfano halisi) na Environment(Mazingira).

Yaani kama mfanyakazi akikosa vigezo katika hio falsafa ya 4E basi kama ni mfanyakazi atafukuzwa au kama ndio anaomba hawezi kupatiwa kazi, ukikidhi vigezo hivyo hata kama cheti chako hakina maksi kubwa basi jihesabie unafanya kazi katika kampuni kubwa Afrika ya Dosam Global.

Prisila alicheka kwanza , hakuamini Hamza angekuwa ni mwanaume wa kujiamini namna hio tena na kwenda mbali na kumtania kama mrembo , asilimia kubwa ya wanaume wa rika la Hamza aliokutana nao wengi walionekana ni wenye kukosa hali ya kujiamini.

“Mzee Stephano ni baba yangu, sijui umefahamiana nae vipi lakini sina muda wa kuukuliza sasa hivi kwani unapaswa kukutana na bosi mwenyewe ambaye anataka kukuajiri , naomba nifuate Hamza”Aliongea na kauli yake ilimfanya Hamza kutoa macho.

Inamaana huyu mwanamke sio ambaye alikuwa akihitaji mtu wa kufanya nae maigizo ya boyfriend, alijiuliza Hamza na aliona ilikuwa ikileta maana , mwanamke mrembo kama huyo anahitaji vipi boyfriend wa maigizo kwa mfano , ilikuwa kichekesho.

Hamza alijiambia alikuwa akijidanganya tu , pengine matumaini yake ya kukutana na mwanamke mrembo yalikuwa yakienda kusambaratikika kabisa..

“Kwanini isingekuwa ni wewe , pumbavu kabisa yaani nimejitutumua vyote hivi kupendeza na kuwa jasiri mbele yako…”

“Mr Hamza come on,.. muda unaenda?”Aliongea Prisila mara baada ya kumuona Hamza amesimama tu na kumfanya bwana huyo kushitika kutoka kwenye mawazo na kuanza kutembea.

Wale wafanyakazi wa mapokezi waliishia kuangaliana kwa ishara kama vile wanajiuliza huyo mtu ni nani , kwanini bosi Prisila ndio kaja mpaka hapo kumchuka.

Asilimia kubwa ya watu ambao aliweza kuwaona ndani ya jengo hilo ni wazungu na wahindi na waliochanganya rangi kama yeye , watu weusi walikuwa ni wa kuhesabu sana , pengine ni kutokana na eneo lenyewe kuwa ghali sana , hii ilimfanya Hamza kujiambia kwamba hata kama mtu anaekutana nae kuwa mbaya lakin angalau anaonekana kuwa na pesa na kama angepita katika usaili huo ilimaanisha kwamba moja kwa moja angepata Exposire ya maeneo ya watu wazito wazito.

“Hata kama ni mbaya nnitaenda nae hivyo hivyo kibishi, pengine inaweza kuniweka na watu wazito wazito na ikawa safari ya kumjua Mzee”Aliwaza Hamza wakati akiwa kwenye lift.

Ijapokuwa alikuwa katika hali ya mawazo lakini bado hakuchoka kutazama umbo la mwanamke mrembo Prisila, alitamani kuuliza swali lakini alishindwa mara baada ya lift kufunguka na kuruhusu mtu mwingine kuingia.

Dakika chache tu walienda kutokezea katika floor ya juu kabisa na mara baada ya Hamza kutoka kwenye lift hiyo alijikuta akishangaa baada ya kuona uzuri wake lakini macho yake yalichanua mara baada ya kugundua eneo hilo lilikuwa likihudumia watu wa hadhi ya juu yaani VVIP.

Ijapokuwa alikuwa akijiamini kama vile amekunywa kiroba lakini bado mapigo yake ya moyo hayakuacha kudunda kwa kasi na kujiuliza ni mtu gani ambaye anaenda kufanya nae usaili tena eneo la VVIP katika hoteli kubwa ya hadhi kama hio.

Prisila alionyesha kutembea kama vile anafanya makusudi , pengine amevutiwa na sura ya Hamza maana bwana huyo alikuwa amependeza kweli ukijumlisha na muonekano wake wa ngozi ilimfanya kuwa wa kuvutia kwa kila mwanamke yoyote yule , lakini licha ya hivyo hali ya kimasikini ya Hamza haikujificha kwenye uso wake.

Kuonekana tajiri ni tofauti na uvaaji wa mavazi , unaweza kuwa tajiri lakini ukaamua kuishi maisha ya kawaida lakini siku zote huwezi kuonekana masikini , masikini siku zote ataonekana kwa umasikini wake na tajiri ataonekana kwa utajiri wake, kuna vitu vingi sana vya kumtofautisha tajiri na masikini au mtu aliefanikiwa na ambaye hajafanikiwa na hio inaenda kabisa kwanzia katika namna mtu unavyoongea ,wajihi , namna unavyotembea na ujengaji wa hoja wakati wa kuchangia mambo.

Tajiri anaweza akajificha katika kundi la watu masikini lakini siku zote hawezi kufanana na masikini.

Masikini na tajiri wote wanaweza kuwa na njaa kutokana na kutokula lakini kama utaamua kuwatofautisha na njaa zao utagundua masikini ndio anaeteseka zaidi na njaa kuliko yule tajiri, maana njaa ya tajiri ni ya kuchelewa kula wakati njaa ya masikini ni ya kukosa chakula.

Kwa upande wa Hamza ukweli ni kwamba ilikuwa ngumu kumtofautisha na masikini , kwa haraka haraka unaweza kusema kwamba Hamza ni mtoto wa tajiri ambaye ameamua kuishi maisha ya kimasikini.

Prisila alienda kusimama katika mlango namba 402 na kisha aligonga mlango kwa dakika kadhaa na palepale mlango ulifunguliwa na mwanadada mwenye sura iliokakamaa alievalia suti kama vile ni afisa usalama au bodigadi.

Mwanamke yule alimruhusu Prisila kuingia lakini alimwashiria Hamza kusimama nje kabla ya kuingia.

“Kijaji mruhusu, ndio mgeni anaepaswa kuonana na bosi”Aliongea Prisila lakini mtu alieitwa Kijaji bado alimwangalia Hamza kwa macho ya tahadhari na palepale alimsogelea na kuanza kumpapasa kama hana siraha ya aina yoyote na aliporidhika alimpiga jicho kali la tahadhari na kisha akamruhusu kuingia.

Hamza alijiambia huyu mwanamke ni mrembo sana lakini tabia yake ya ukakamavu inamfanya kuwa na sura ngumu.

Hata hivyo hakutaka kumfikiria sana , yeye hofu yake ni mtu ambaye anakwenda kuonana nae.

Hamza alikaribishwa na mandhari ya kuvutia ya chumba cha hadhi ya raisi(Presidential suite), haikuwa chumba cha kawaida kwa mtu wa kawaida kuingia na ilimfanya Hamza macho yake kuangalia vitu vilivyokuwemo pamoja na uzuri wake kwa haraka haraka.

Mbele yake kabisa upande wa dirisha kubwa ambalo linaangaliana na bahari ya Hindi kulikuwa na eneo la sebuleni na sofa kubwa ambalo lilikuwa imekaliwa na mtu alievalia kofia ya hat kichwani.,

“Huyo ndio bosi , nadhani mawazo yangu yapo sahihi nakwenda kukutana na mtu mbaya ambaye amekataliwa na wanaume mpaka kuamua kutafuta boyfriend feki , aisee hata hivyo maji nimeyavulia nguo sharti ni yaoge”Alijiongelesha katika mawazo yake akimwangalia yule mwanamke aliempa mgongo akisubiria surprise ya kuona sura ya mwanamke mbaya,

“Bosi , Mr Hamza kashafika kwa ajili ya usaili?”Aliongea Prisila huku akionyesha hali ya heshima.

“Okey mnaweza kuondoka , nitawaita baada ya usaili”

“Boss!!’Aliongea Kijaji kwa tahadhari.

“Hakuna kibaya kinachoweza kunitokea , mnaweza kuondoka”Aliongea bila ya kugeuka .

Upande wa Hamza sauti hio ilimsababishia mshituko wa aina yake , ilikuwa ni sauti nyororo lakini yenye madaraka ndani yake, ilikuwa ni kama wimbo wa kubembeleza unaozigonga ngoma za masikio yake.

Ilikuwa ni sauti nzuri mno na Hamza alijiuliza au mawazo yake ni tofauti na uhalisia , kwanini mwanamke anaemdhania kuwa ni mbaya wa sura kuwa na sauti nyororo hivyo , alijiambia pengine sio mbaya kila kitu , isitoshe kuna msemo wa kwamba Mungu hakupi vyote , anaweza akakupa sauti nzuri lakini akakupa sura mbovu, anaweza akakupa mguu ila akakupa Komwe kubwa.

Licha ya Prisila Singano kusita sita pamoja na mlinzi wa bosi huyo lakini waliishia kutii maagizo yake.

“Ukifanya chochote kibaya kitakachomdhuru bosi basi jua ndio kifo chako”Aliongea Kijaji kwa tahadhari na kumfanya Hamza kutoa tabasamu na kuzidi kumkera mlinzi wa watu,

Baada ya kila mtu kuondoka ndani ya hiko chumba yule mwanamke palepale aliinua mkono wake na kuitoa ile Hat.

Ilikuwa ni hat aina ya Beekeeping Veil, yaani hat ambazo huunganishwa na kitambaa cheusi ili kuzuia sura ya mtu kutokuoenekana

Hamza mara baada ya kuona mkono wa yule mwanamke ukiondoa ile hat taratibu mapigo yake yalianza kuongezeka spidi spidi , ilikuwa ni hisia ambazo kwenye maisha yake hakuwahi kuzisikia hata siku moja, kadri ile Veil ilivyokuwa ikiiacha sura wazi alizidi kujawa na hofu pamoja na mshituko wa aina yake,

Mwanamke yule baada ya kuivua alisimama na sasa namna ambavyo alikuwa akisimama ni kama vile yupo kwenye mwendo wa slow motion , ni kama vile malaika anaibukia kutoka ardhini.

Yalikuwa ni matarajio tofauti kabisa na kile alichokuwa akikiwazia Hamza , mwanamke aliekuwa mbele yake akili yake ilimwambia kabisa ni mwanamke ambaye anapaswa kusujudiwa kwa kupaza sauti.

******

MIEZI KADHAA ILIOPITA.

Ni miezi kadhaa iliopita ndani ya eneo la maegesho ya magari katika hospitali ya chuo ya Mayaya Clinic iliingia gari ya kifahari aina ya Porsche Gayenne G Coupe .

Baada ya gari hii kusimama palepale mlango wa dereva ulifunguliwa na mwanaume mtanashati alievalia suti na kwa haraka haraka alizunguka upande wa kushoto na kisha akafungua mlango wa abiria.

Mwanamke mrembo sana alievalia gauni lenye mkanda kiunoni na Blazer ya rangi ya ugoro alishuka kwenye gari lile huku yule mwanaume akionyesha heshima mbele yake.

Kwa haraka haraka anaeangalia tukio lile angeelewa kwamba yule mwanaume ni dereva wa yule mwanamke.

“Utanisubiria hapa mpaka nitakapomaliza”.

“Sawa madam”

Alijibu yule bwana kwa heshima kubwa tu mbele ya yule mwanamke , alikuwa ni msichana mrembo haswa pengine zaidi ya neno urembo , alikuwa ni msichana mdogo pia kimuonekano makadirio ya miaka kama ishirini na nne hivi , alikuwa ni mweupe wa wastani mrefu na aliejaaliwa umbo zuri.

Kitu kimoja tu ambacho pengine ambacho kinapunguza asilimia mbili ya uzuri wake ni muonekano wa yule mrembo , alikuwa ni kauzu mnno lakini hata hivo bado alikuwa amependeza.

Aliweza mkoba wake kwapani vizuri na kisha alizipiga hatua kuingia ndani ya hospitali hio kubwa.

Mayaya Clinic ni moja ya hospitali kubwa sana ndani ya ukanda wa Afrika mashariki na kati yote , ilikuwa ni hospitali ya binafsi ambayo ipo chini ya kampuni ya Vexto Group kampuni namba moja kwa ukubwa Afrika na namba kumi kwa Dunia nzima.

Yule mwanamke mrembo alitembea kwa mwendo wa kujiamini mpaka kwenye lift huku akionyesha sio mwenye kujali macho ya wanaume na wanawake wanaomwangalia.

Ukweli ni kwamba ilionekana ni kawaida kwake kuangaliwa hivyo kutokana na yeye mwenyewe alivyo , alikuwa mzuri hivyo ilileta maana kuangaliwa na kila mtu , wengine walimwangalia kwa matamanio na wengine walimwangalia kwa maswali kwa Mungu kwa kuweza kuumba mwanamke wa aina hio.

Wahenga wanasema Mungu hakupi vyote na kauli hii ilithibitishika kwa mrembo huyu ndio maana siku hio ya asubuhi alikuwa ndani ya hospitali hio

Dakika chache mbele mwanamke yule alikuja kutokezea katika floor namba saba ambayo ni idara ya Saikolojia(Psychiatric Department).

Idara ya saikolojia mara nyingi huhusiika na tiba ya magonjwa mbalimbali ya yanahusiana na akili.

“Miss Regina karibu sana , Dr Shukuru anakusubiria”Aliongea mwanadada wa mapokezi.

Kwa haraka haraka ilionekana mrembo huyu ambaye sasa anafamamika kwa jina la Regina alikuwa ni mgonjwa wa mara kwa mara kufika ndani ya hospitali hio kutokana na nesi wa mapokezi alivyompokea.

Mrembo Regina aliishia kutingisha kichwa na kisha alitembea kuelekea upande wa kulia akipita mapokezi na alisimama mbele ya mlango uliokuwa na kibao juu ofisi ya daktari au chumba cha daktari namba 01.

Mazingira ya hospitali katika idara hio ya magonjwa ya akili ilikuwa tulivu mno, pengine unaweza kusema wagonjwa wanaofika katika hospitali hio ni wachache lakini huo sio ukweli hospitali hio ina floor mbili ambazo zote hutumika kama idara ya magonjwa ya akili lakini floor ya sita ni yale magonjwa ya akili ambayo ni very comnon yaani yanayoeleweka na floor namba sita ni ya magonjwa ya akili ambayo ni special zaidi.

Unaweza ukashangaa mgawanyo huu lakini ukweli ni kwamba zama za miaka ilipita na zama za wakati huo zilikuwa zimebadilika sana tena sana , ni miaka ya hivi karibuni kulibuka wimbi la magonywa ya akili ya kipekee ambayo yamekuwa ni magumu sana kueleweka wa wataaluma na mpaka wakati huo chanzo cha magonjwa hayo hakijafahamika bado na wanasayansi wanapambana kujua chanzo chake.

Hii yote inasemekana ni mara baada ya tukio la mwaka 2020 , tukio la mwaka 2020 halikuwa na athari moja tu bali lilikuwa ni tukio ambalo lilibeba athari nyingi na moja ambazo ya athari ambazo zinahusishwa ni kuibuka kwa magonjwa ya akili ambayo sio ya kawaida.

Sasa ukiona mtu ambaye sio mfanyakazi wa hospitali ya Mayaya anaingia floor namba saba basi jua ni mwasilika wa tukio la mwaka 2020.

“Miss Regina karibu sana”

Mwanaume mmoja mtanashati wa makamo alievalia koti la udaktari alisimama mara baada ya mango kufunguliwa na mrembo Leilani.

Kwa muonekano wa daktari huyo ilionekana Regina ukiachana na uzuri wake ambao sio wa kawaida lakini kuna sababu nyingine ambayo inambeba kwani daktari aliefahamika kwa jina la Shukuru alionyesha unyenyekevu mkubwa.

“Thanks , I can see that you’re still a little nervous around me , please relax , I am regular patient remember”Aliongea yule mwanamke akitoa tabasamu hafifu kidogo akimwambia yule daktari kuacha wasiwasi akiwa nae na atulie kwani yeye ni mgonjwa wa mara kwa mara.

“Bila shaka .. ni kwamba tu wewe ni mgonjwa wangu muhimu”Aliongea Dr Shukuru huku akikaa kwenye kiti chake”

“Najua lakini mimi ni kama wagonjwa wengine tu na isitoshe bado natakiwa kuonana na daktari wakati kwa wakati”

“Ni kweli kabisa Ms Regina , umuhimu wako katika jamii unanifanya niwe makini na kutotaka kufanya makosa”

“Oh.. nashukuru naamini utafanya vizuri , isitoshe wewe ndio daktari bingwa ninaekuamini na tatizo langu , ni miaka mingi sana tokea nianze kupata matibabu kutoka kwako, ni mwaka wa tatu huu unaingia kama sikosei”

“Upo sahihi na imekuwa heshima kwangu muda wote kukusaidia kwa kila namna kuweza kupona ..”Aliongea na kisha palepale aliwasha tarakishi yake na kuandika jina la Regina kutafuta taarifa zake.

Kwa haraka haraka ilionekana mrembo huyo anaefahamika kwa jina la Regina sio mara yake ya kwanza kufika ndani ya hospitali hio.

“Awamu hii umechukua muda mfupi sana tokea appointment ya mwisho , nilikutegemea mwezi ujao , vipi kuna mabadiliko yoyote?”Aliuliza Dokta na kumfanya Regina uso wake kidogo kukosa utulivu.

“Siwezi kusema kuna mabadiliko makubwa na leo nilitaka kuonana na wewe kwa ajili ya ushauri zaidi”

“Ushauri , unaweza kuendelea nipo tayari kukupatia ushauri wowote kama ni swala linalogusa shida yako maana ndio taaluma yangu”

“Dr kwa miezi kadhaa mpaka sasa familia yangu wanalazimisha niolewe na mwanaume ambaye wamemchagua , nilikataa pendekezo lao lakini wameenda mbali na kuanza kufanya vikao kushawishi Shareholders wa kampuni ili kunilazimisha , wanasema nisipokidhi vigezo basi natakuwa kuachia nafasi yangu kwenye kampuni kama CEO na mwenyekiti wa bodi”Aliongea na kumfanya Dr kuwaza kidogo.

“Nadhani nimekuelewa unachotaka kumaanisha .. lakini ili niwe more specific kwenye ushauri wangu , hebu elezea unachukuliaje swala hili?”

“Dokta ninachofuata ni ushauri wako wa kitabibu kuhusiana na ugonjwa wangu wa ukichaa…”

“Miss Leilani naomba nikurekebishe, wewe huna tatizo la ukichaa bali una shida ya ugonjwa wa DID, nadhani nimekuambia ili matibabu yako kufanya kazi vizuri lazima utambue ugonjwa wako kwa jina hilo na sio ukichaa”

“Nimezoea kwa muda kuiita ugonjwa wa ukichaa, tukiachana na hilo nadhani katika ushauri wako wa kitabibu ulisema ugonjwa wangu unaweza kumalizwa na mapenzi?”

“Ndio nilimaanisha kutokana na shida yako kuwa ya kisaikolojia zaidi itakuhitaji kuwa na high self willing ya kuchagua ni namna gani unataka kuishi na kuishinda nafsi yako nyingine na hili litawezekana ukiwa na msaada wa nje wa kisaikolojia , kama vile kushare hisia zinazofanana na mtu mwingine , hii ni moja wapi ya njia ambazo nilipendekeza lakini haikuwa lazima sana lakini kwa wagonjwa wengi ambao nimekutana nao njia hio imeonyesha mafanikio , njia ya pili ni kuzipatanisha nafsi zako zote mbili tofauti na kuzikataa na njia hii ili kuweza kufanikiwa nilikuelezea kwamba unatakiwa ujue chanzo cha kila nafsi na pengine kujua kumbukumbu za maisha ya nyuma ambazo umepoteza”Alielezea Dokta Shukuru kwa kirefu.

DID ni kifupi cha neno la Kingereza yaani Dissociative identity Disorder ni ugonjwa wa akili ambao ulikuwa ukifahamika kwa jina la Multiple personality disorder , ugonjwa ambao unamfanya mtu kuwa na Utu wa aina mbili au nafsi mbili ambapo humvaa mtu kwa nyakati tofauti tofauti na kudhibiti tabia.

Yaani kwa mfano unaweza ukajitambbua kama John na watu pia wakakutambua kama John na tabia zako lakini muda mwingine unabadilika na kuwa Ayubu na tabia zako zinakuwa ni kama Ayubu bila ya kufanana kabisa na John.

Huo ndio ugonjwa ambao mrembo Regina alikuwa nao , yaani anatawaliwa na ugonjwa wa akili ambao unamfanya kuwa na nafsi mbili zenye tabia tofauti tofauti.

Ni ugonjwa ambao huwapa changamoto sana madaktari kuutibu lakini unatibika kupitia njia za kiushauri zaidi.

“Kwahio kulingana na tatizo langu na mipango ya familia yangu , unanipa ushauri gani?”

“Njia ambayo ni rahisi zaidi ambayo tokea mwanzo nilisisitiza ni kuishirkisha familia yako juu ya tatizo uliokuwa nalo ,lakini sio wewe tu ambaye ulikataa juu ya hili lakini babu yako pia alikataa swala ambalo naelewa kulingana na haki za mgonjwa wangu, nasema hivi kwasababu pengine kama mama yako wa kambo anajua una tatizo la namna hii asingefanya maamuzi ya kutaka kukutafutia mume wa kuolewa nae kwani haitokusaidia kupona tatizo lako , nikizingatia msingi wa matibabu nikiri kwamba familia yako maamuzi ambayo imeamua ni hatari kwa maendeleo ya shida yako, lakini naelewa pengine ni kutokana na kutokuwa na uelewa, pia najua kwa upande wako unachukua tahadhari”

“Asante Dokta kwa kuwa muwazi , ukweli tokea nafike hapa nishafanya maamuzi na nilitaka kusikia maoni yako juu ya hili”

“Ndio nipo tayari kusikia maamuzi yako”

“Napanga kuajiri mwanaume yoyote aigize kuwa boyfriend wangu ili kuzuia mpango wa wazazi wangu zidi ya kampuni”Aliongea na kumfanya Dokta Shukuru kushangaa kidogo lakini alipotezea mshangao wake.

“Kuna haja ya kwenda mbali hivyo , Ms Regina najua unalichukulia tatizo lako kwa ukubwa lakini ni tatizo la kawaida na kwa muonekano wako na mafanikio yako sidhani kama kuna haja ya kuwa na mwanaume wa maigizo , wapo wanaume wengi ambao wanaweza kukupenda na wewe kuwapenda ni swala la kutoa nafasi tu”

“Dokta kwa maelezo yako unahisi ni rahisi kupata mtu kunipenda , ushasema kwa muonekano wangu na mafanikio hivyo sidhani kuna mwanaume ambaye anaweza kunipenda kwa dhati tofauti na kutanguliza nilichokuwa nacho , nimeona wakati nikiendelea kumtafauta huyo mwanaume nitakaempenda na ambaye atanipenda kwa dhati nitafute mbadala maana mapenzi pia ni swala la mchakato na kama hili swala likishindikana nitaenda na plan B kupatanisha nafsi zangu”

“Unafikiri unaweza kupata mwanaume ambaye anaweza kukubali kuajiriwa kuigiza kuwa mchumba?”

“Naamini nguvu ya pesa ndio itafanya kazi, itakuwa ni kama ajira tu na ni swala ambalo nataka kulifanya ili kujipatia muda nikiendelea kufuatlia namna ya kumaliza tatizo langu , huenda pengine ni kapata mwanaume ninaempenda na ikawa rahisi tatizo langu kumalizika”Aliongea na kumfanya Dokra Shukuru kuwaza kwa muda.

“Nadhani sio wazo baya kulingana na hali yako , umesema pengine unaweza kupata mwanaume unaempenda wakati ukiwa na mchumba wa maigizo , hoja yangu ni kwamba pengine mchumba wa maigizo akawa ndio mtu uliepangiwa kuwa nae na mkapendana hivyo nipo tayari pia kubeti , nilisha fikiria kwa kina nitakuja kufanya chochote kwa ajili ya kuhakikisha hali ya mgonjwa wangu inaisha , kwasasa tujaribu na hiki ulichoamua” Aliongea Dr Shukuru na kumfanya Regina kutoa tabasamu.

Ugonjwa wa DID ulikuwa mgumu kudili nao ndio maana inashauriwa na daktari kuwa flexible wakati wa kushughulika na mgonjwa na hicho ndio ambacho alikifanya Dr Shukuru.

Dr Shukuru Omari ni daktari mbobezi ambaye amepitia mafunzo makubwa ya kudili na wagonjwa wa akili na haikuwa mara yake ya kwanza kudili na mgonjwa mwenye nafsi mbili.
ITAENDELEA
Tupe mwendelezo wa Hamza mkuuu. Tuipokee ijumaaa kibabe na kizembekizembe kama alivyo hamza mwenyewe
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU



MTUNZI:SINGANOJR



SEHEMU YA 23.

Yonesi aliishia kuinua kichwa na kumwangalia Hamza kwa sekunde kadhaa na kisha akampotezea na kuendelea na chakula chake , kitendo kile kiliwashangaza wengi na kuona au Hamza ameshamuweza Yonesi.

Muda huo Hamza aliweza kuona Yonesi alikuwa amejisevia Sausage kwenye sahani yake lakini hata yeye pia ni moja ya chakula alichochukuwa , ki ufupi ni kwamba hakubakisha.

Mgahawa huo wa kampuni chakula kilikuwa bure na kulikuwa na msururu wa mapot makubwa ambayo yanachakula , ni kazi yako kupita na kujisevia tu.

“Kapteni , kumbe na wewe unapenda kula Soseji , unaonaje nikikupatia na yangu?”

Maneno hayo yalisikika kikarimu lakini kadri alivyoyafikiria ndio aliona ni kama kuna zaidi ya maana na mwili wake ulianza kubadilika rangi na kujihisi kupatwa na joto licha ya eneo hilo kuwa na AC, aliona kabisa Hamza alikuwa akimfanyia hivyo makusudi kabisa.

“Usije ukanidhania vibaya , naamanisha soseji ya kwenye sahani yangu…”Aliongea Hamza huku akijifanyisha ni mwenye aibu.

Kadri alivyokuwa akiongea ndio ambavyo maneno yake yalivyoonekana ya kihuni , wafanyakazi waliokuwa karibu wakitega masikio yako kama antena baada ya kusikia kauli ya Hamza waliishia kucheka.

“Hakuna ambae atasema wewe ni bubu ukikaa kimya.”Aliongea Yonesi huku akijitahidi kuzuia hasira zake.

Watu mpaka hapo waliona kitendo cha Yonesi kuweza kuvumilia utani wa Hamza inamaanisha alikuwa hamuwezi na sifa zote walimpatia Hamza.

Hamza aliishia kushindwa kuongea na kumwangalia Yonesi namna ambavyo amevaa , lakini ilionekana kutokana na tukio la jana alikuwa amefunga shati lake mpaka kifungo cha mwisho.

Hamza aliona ngoja anyamaze adili na chakula chake , lakini Yonesi mara baada ya kuona ametulia yeye ndio aliongea.

“Wapi umejifunzia mapigano?”

Hamza alisikia hilo swali , lakini alijifanyisha hajasikia na aliendelea kuwa bize na chakula chake, lakini kitendo kile cha kupotezewa kilimuudhi Yonesi na kumfanya apige meza kofi.

“Wewe , nakuuliza swali , hujanisikia au?”

“Kapteni si umeniambia nikae kimya , kwanini unataka niongee tena , unajua unanitesa”

“Wewe..”Yonesi aliishia kusaga meno kwa hasira, alijua fika mwanaume huyo alikuwa akikwepa kujibu swali lake na kutokana na hasira zake aliishia kuinua sahani yake ya chakula na kisha akaondoka akimuacha Hamza mwenyewe.

Hamza aliishia kutoa tabasamu la kichokozi tu , huku akiangalia mandhari ya jiji , aliona inafurahisha sana kutania wafanyakazi wenzake.

Wakati akirudi kwenda juu kuendelea na kazi Hamza hakusahau kubeba tena matunda kwa ajili ya Regina , siku hio hakuchukua ma apple tu bali alibeba na zabibu.

Mara baada ya kufika katika mlango wa ofisi ya mkurugenzi , wakati akitaka kuingia aliweza kusikia majibishano kutoka ndani na kumfanya asimame.

“Mzee Sebastian, Mzee Willium , kama wakurugenzi wasaidizi , hebu niambieni sababu ya kwanini mpo kidedea kupinga hili , naona mnafanya makusudi kabisa kunipinga bila sababu”Aliongea Regina na sauti yake ilionekana imejaa hasira.

“Mkurugenzi wewe ni binti mdogo sana bado , maji unayotaka kujaribu kukanyaga yana kina kirefu , ununuzi wako wa awamu hii ni wa kukurupuka”Aliongea Mzee Willium.

“Kukurupuka?, mimi ninachoona hapa ni kwasababu hamtaki kuona kampuni inakuwa kutoka levo iliopo kwenda nyingine na wasiwasi wenu ni kuogopa kupoteza nafasi zenu , mnaonaje mkiniambia ni hisa kiasi gani mnahitaji ili muwe hiari na msishindane na mimi?”Aliuliza Regina.

“Mkurugenzi sisi ni wazee ambao tulikuwa nyuma ya mwenyekiti wa kampuni aliepita mpaka kuifikisha kampuni ilipo sasa hivi hatua kwa hatua , tunaipenda sana hii kampuni ndio maisha yetu , hivyo usiongee ujinga”

“Sitaki kusikia maneno yenu yasio na msingi , nitawapa siku tatu , kama hamtokubali kubadilisha mawazo yenu , kuweni makini maana kuna uwezekano mkaondolewa kwenye nafasi zenu, nishamaliza , mnaweza kuondoka”Aliongea kibabe.

“Wewe mtoto , kwanini unatufanyia hivi , sisi ndio wazee, msingi wa kampuni”

“In this company , only the subordinates of the superior have seniority”Aliongea Regina kikauzu kwa kutumia kingereza akimaanisha wafanyakazi waliopo chini ya uongozi ndio wenye uzoefu zaidi.

“Hakuna shida Mkukufu Mkurugenzi , Willium tuondoke zetu , haina haja ya kuongea tena”Aliongea Mzee Sebastian mara baada ya kupiga kofi kwenye sofa.

Dakika hio hio Mzee Sebastian na Mzee Willium waliweza kutoka na mara baada ya kumuona Hamza ambae amesimama mlangoni , wakurugenzi hao wasaidizi nyuso zao zilizidi kuwa ngumu na kumwangalia Hamza kwa ukali.

Hamza aliishia kupumua tu kwa ahueni huku akijiambia mambo hayo hayamhusu hata wamwangalie vibaya, hivyo aliingia zake kwa CEO.

“Unafanya nini hapa na wewe?”Aliuliza Regina mara baada ya Hamza kuingia , alikuwa amesimama kwenye sofa akiwa na ukauzu.

“Kula matunda kidogo , punguza presha na acha kujisababishia matatizo ya mwili kwa ajili ya kazi”Aliongea Hamza baada ya kumkabidhi boksi lile lenye matunda akiwa na tabasamu.

“Sina hamu ya kula chochote muda huu , unaweza kuondoka nayo tu”

“Nishakula share yangu na yaliobaki ndio nimekuletea”

“Nimesema siyataki ,unaweza kuondoka nayo tu”

“Mbona matunda mazuri haya , unataka yaharibike”Aliongea Hamza.

“Sikia , nina kazi nyingi za kufanya sasa hivi , kula mwenyewe”Aliongea na kisha alirudi kwenye kiti chake .

“Usiniambie unapanga kujipigia zako kile kinywaji tena , ukifanya hivyo nampigia sasa hivi Shangazi simu”

Regina mara baada ya kusikia hivyo aliishia kugeuza kichwa chake huku akiwa amefura.

“Kinachokuuma ni nini?, inakuhusu nini mimi kula au kutokula , sisi sio wapenzi bali tupo katika maigizo tu ya kimkataba , kwanini unanijali sana?”

“Halafu wewe ni mwanaume , kuna haja gani ya kumhusisha shangazi kila kitu , Jiamini”

Hamza mara baada ya kusikia maneno hayo aliishia kutoa tabasamu hafifu na kisha aliweka matunda yale kwenye meza.

“Upo sahihi mimi ni mfanyakazi wa mkataba tu hapa , sio jukumu langu la kujali unachokula wala afya yako , hata upatwe na vidonda vya tumbo ukweli ni kwamba halinihusu , lakini ni juu yangu kumpa mtu yoyote chakula kama hajala , unaweza kula nimeyaweka hapa au ukiona vipi yatupe tu”

“Wewe..”

“Kitu kingine , Shangazi yule kwako ni kama mzazi ambae amekulelea mpaka leo hii , kuhusu mimi sina hata wiki tokea tufahamiane , baada ya miezi mitatu kuisha iwe ni wewe au Shangazi sitokuwa na uhusiano wowote na nyie, hivyo sio kwamba najaribu kukutishia na yeye , sio swala langu hili , ninachokukumbusha ni kwamba ni sawa tu kujifanya mbishi na mwenye hasira za karibu lakini siku zote jaribu kujali na watu wanaokujali”

“Sitaki unifundishe ..”Aliongea Regina mara baada ya kusikia maneno hayo , ni kama yalimgusa kidogo.

Hamza hakuongea lolote zaidi na alitoka katika ofisi hio na kufunga mlango na kufanya hali kutulia.

Mara baada ya kuona ameondoka , Regina alisita kidogo mara baada ya kukaa katika meza yake na kuvuta droo , sasa ile alivyokuwa akitaka kuchukua kile kinywaji cha virutubisho aliishia kukirudisha chini.

Maneno ya Hamza ni kama yalikuwa yakijirudia rudia katika akili yake , alikuwa akimpenda mno Shangazi yake kwani ndio kama mzazi pekee ambae alikuwa akimwelewa , Regina alivuta pumzi na kisha alifunga ile droo na kuchukua lile boksi la matunda na kuangalia ndani , lakini mara baada ya kuona ni zabibu alielewa kwanini Hamza kafanya hivyo na aliishia kuona aibu za kike.

“Muhuni sana huyu..”Aliongea na palepale alichukua Zabibbu zile nyingi katika mkono na kuzisindilia zote mdomoni , zilikuwa na ukakasi , utamu wa aina yake na sukari.

Alitaka kumaliza haraka hivyo alikuwa akila kifujo fujo ili arudi kwenye kuendelea na kazi ,kulikuwa na vipande vya matikiti pia na alivichukua na kuvisindilia vyote na kumfanya hadi mchuzi kumtoka mdomoni.

Kitendo kile kilimfanya mashavu kuvimba mnno kama vile ni mtoto mdokozi anaejaribu kula haraka haraka asishutukiwe.

Muda uleule ndio Hamza alifungua mlango na kuchungulia ndani na aliishia kucheka namna ambavyo mashavu ya Regina yalituna.

Regina alijikuta akitoa mguno mara baada ya kugundulika alichokuwa akifanya huku akiziba mdomo na mikono yake miwili.

Mdomo wake ulikuwa umejaa , alitamani kufoka lakini haikuwezekana na vilevile alishindwa kumeza kwa haraka na aliishia kujionea aibu yeye mwenyewe , kwa mkurugenzi mwenye heshima zake na mwanamke ambae anajali taswira yake kuonekana akiwa ametuna mashavu namna hio wakati wa kula ilikuwa aibu.

“Haha.. nilijua tu , umependezaje , kula taratibu usije ukapaliwa, hebu tukupige na kapicha”Aliongea Hamza.

Regina aliishia kukasirika ndani kwa ndani na kujiuliza kwahio alikuwa amesimama muda wote mlangoni , inamaana aliotea nitakula matunda kivurugu vurugu.

Aliona kama kweli picha itachukuliwa taswira yake ya mwanamke aliestaarabika itaharibika kabisa na kwa haraka haraka aliinua karatasi na kuficha uso wake. Huku akijitahidi kutafuna na kumeza kwa haraka.

“Unataka kufanya nini , ondoka ofisini kwangu la sivyo mshahara wako utakuwa nusu”

“Ah , Boss usifanye hivyo , hii simu kimeo hata Kamera haifanyi kazi, nilikuwa natania tu”

Mara baada ya kusikia jibu hilo kidogo alijituliza lakini alivyowaza namna ambavyo ameonekana alivyotuna mashavu kwa ajili ya chakula masikio yalishika moto.

Ukweli hakujua nini kinaendelea lakini alijishangaa tu kupotezea msimamo wake mbele ya Hamza.

Alijiweka sawa na kisha akajifuta midomo na tishu na akaurudia ukauzu wake kama vile hakuna kilichotokea na kisha akaguna kidogo.

“Ukirudia tena ninakuhakikisha mshahara wako utapata nusu”Aliongea huku akionyesha hadhi yake ya ubosi.

“Sawa bosi , nitaenda kuendelea na kazi”Aliongea Hamza akiwa katika muonekano wa kizembe huku akitingisha kichwa na kuondoka.

Regina mara baada ya Hamza kuondoka alijikuta akijibwaga kwenye kiti chake kama mtu ambae ametua mzigo mzito kichwani.

Mara baada ya kuanza kufikiria kilichomtokea sekunde kadhaa zilizopita alijikuta akicheka mwenyewe na kujiambia hili ni tukio lake la ajabu kumtokea akiwa kazini.

Kwa namna alivyocheka alipendeza mno , kana kwamba ni mmea uliochanua wakati wa ukame mwingi, lakini kwa bahati mbaya tukio hilo hakuna ambae aliweza kuona.

Hamza hakuwa na chakufanya, kazi alikuwa amemaliza na alijikuta akiingiza gemu katika tarakishi na kuanza kucheza kupoteza muda lakini alikuja kusitishwa mara baada ya simu yake kuita , alipoangalia namba ilikuwa ngeni kwa maana hakuwa ameisevu.

Bila kujiuliza mara mbilimbili aliamua kuipokea ili kusikiliza ni nani anampigia , sauti iliosikika ilikuwa ya mwanamke.

“Hello , Mr Delivery”

Ilikuwa ni sauti tamu kweli , pengine aliekuwa akiongea hivyo alikuwa ameilegeza.

“Naongea na nani?”Hamza alikuwa akihisi aliekuwa akiongea nae lakini alitaka kuthibitisha.

“Mteja wa vvungu , Hamza nahitaji mzigo unifikie leo hii , nadhani Alex alikuambia”Hamza mara baada ya kuthibitisha mwili wake ulimsisimka.

Ukweli ni kwamba ni kama ana katabia ka kusahau baadhi ya vitu , ijapokuwa alikuwa na shauku ya kutaka kujua vyungu vile vilikuwa na siri gani mpaka kununuliwa kwa kiasi kikubwa cha pesa , lakini mara baada ya kujiunga na famiia ya Regina ni kama alisahau kwa muda.

“Nakumbuka ndio , nitakuletea mzigo, ngoja niwasiliane na Alex kabisa, saa ngapi nifike?”

“Muda ni uleule Mr Hamza”Aliongea mwanadada Frida upande wa pili na sauti yake ilionekana kuwa na ucheshi.

“Leo lazima nijue vungu hivi vina siri gani?”Aliwaza Hamza na kisha paleale alitoa jibu kwamba muda tajwa lazima awe hapo akiwa na chungu.

Hamza hakuwa akijua kwamba swala la Frida kumchagua yeye kama mleta vyungu lilimfanya Alex kumchukia kwa kudhania mrembo huyo ana hisia za kimapenzi na Hamza.

Muda husika mara baada ya kuwadia Hamza ilibidi kwanza akamuage Regina ili afahamu kwamba hawezi kwenda nae nyumbani , alitaka kuunganisha moja kwa moja.

Mara baada ya kumwambia kwamba kuna sehemu anapitia Regina hakuwa hata na haja ya kuuliza ni wapi , aliishia kuitikia tu.

Kwasababu hio Hamza hakuacha kujisikia vibaya , kwa namna ambavyo Regina alimchukulia , ni kama vile alikuwa na nafasi ndogo sana kwenye maisha yake , hakujua ni kwanini lakini aliona yeye na Regina hawawezi kuwa wapenzi na ndani ya miezi mitatu kila mtu atashika lake.

Kwasababu hakuwa na usafiri ilibidi achukue mwendokasi kwa mara nyingine , muda ulikuwa umeenda na kwa kuminyana sana aliweza kufika Mwenge ndani ya dakika ishirini pekee , kutoka Mlimani city yalipo makao maku ya kampuni mpaka Mwenge hapakuwa mbali.

Hamza mara baada ya kufika katika kiwanda hicho bado hakuacha kushangaa , kitu kingine siku hiio kulikuwa na mabadiliko kidogo , wale wanawake ambao walikuwa bize kutengeneza vyungu hawakuwepo ni kama vile kiwanda kimesitisha utengenezaji kwa muda.

Hamza hakujali sana , mara baada ya kujitambulisha hakukuwa na maswali mengi , alipewa mzigo na utaratibu ulikuwa ni uleule kama wa mwanzo.

Hamza alidhani angemuona Alex ndani ya hilo eneo , lakini hakuwepo hivyo pia hakujishughulisha kumpigia simu.

Muonekano wake ulikuwa mzuri zaidi kuliko wiki aliofika hapo kuchukua mzigo , alikuwwa amevaa suti ya bei ghali na viatu vya bei ghali , hivyo ilifanya watu kumwangalia kwa namna flani ya kumshangaa , wengi wao ikiwemo wadada.

Kilichombeba Hamza licha ya kuonekana muda mwingine kama Mzembe ni muonekano wake wa kuchanganya rangi , kitendo cha kuingia katika daladala na muonekano wake ni kama vile hakuwa na hadhi hio , watu walimpa hadhi ya kuwa na usafiri binafsi.

Mambo yalienda haraka haraka kuliko siku ile kwani alikuwa ashajua anuani ya nyumba mzigo ulipokuwa unaelekea.

Baada ya kufika Madale kwenye geti alibonyeza kitufe na aliitikiwa kwa ndani na mlango ukafunguliwa , lakini siku hio mlinzi alikuwa tofauti , hakuwa yule wa siku ile ambae aliikuwa akimwangalia kwa macho ya dharau dharau , aliekuwepo alikuwa ni kijana mdogo sana.

“Karibu Bro”Aliongea yule kijana , alikuwa humble kuliko ilivyokuwa kawaida, pengine ni kutokana na muonekano wa Hamza.

Hamza mara baada ya kupita getini alielekezwa aende moja kwa moja ndani , ilikuwa ni tofauti na siku ile alipofika mrembo yule alikuwa kwenye bwawa la kuongelea.

“Welcome!!”

Sauti tamu ya mrembo Frida ilimkaribisha, siku hio mwanadada huyo alikuwa na muonekano wa tofauti kabisa , alikuwa amevalia suti ya rangi nyeupe na miwani ya macho , alionekana kuwa katika mavazi ya kikazi zaidi tofauti na ya nyumbani.

Alimkaribisha Hamza kwa tabasamu , ilikuwa ni kama vile anamjua na jabo hilo Hamza aliliona pia , lakini hakufikiria sana.

“Nimeleta mzigo boss wangu , sijui utaratibu ni uleule naufungua kwanza?”Aliuliza Hamza.

“Haina haja , naamini hakuna makosa”Aliongea na Frida hakumpokea Hamza bali aligeuka na kurudi ndani na Hamza alielewa , alipaswa kuingia ndani ya jumba hilo la kifahari.

Nyumba hio kwa nje ilionekana nzuri , japo haikuwa kubwa sana kama ile ya Regina lakini ilikuwa nzuri ya kupendeza ambayo ilitosha kuitwa Mansion.

Hamza mara baada ya kuingia ndani aliweza kuona uzuri halisi sasa , staili ya upambaji ilikuwa ni ile ‘go all out’or maximalist yaani juhudi kubwa zilitumika kuhakikisha mapambo mengi kama hayo yanaendana na muonekano wa sebule na kufanya ipendeze , ilikuwa tofatui na nyumba ya Regina ambayo samani za ndani zilikuwa chache huku upambaji ukiwa ni ule mwepesi, Hamza alijiambia iwe upambaji ni vitu vichache au vingi kilicholeta maana eneo hilo linapendeza na linaendana na tabia ya mtu.

Regina alikuwa kauzu ndio maana hata mazingira yake yalikuwa mepesi , hakupenda kuzungukwa na mapambo mengi ya thamani ya juu , Frida alionekana kama mwanamke mcheshi na anaependa kujiachia na ndio maana alipenda kuzungukwa na mapambo ya kifahari.

Hamza alizungusha macho kwa haraka na aliweza kuona tarakishi ikiwa juu ya meza na baadhi ya makaratasi yalionekana , ilionekana alikuwa akifanya kazi na hivyo ilimpa ishara ya kwamba hakukuwa na chumba cha ofisi kama nyumbani kwa Regina.

“Siku ile nilidhani kwa urembo wako utakuwa celebrity , lakini napata hisia kazi yako itakuwa ni ya kutaaluma zaidi”Aliongea Hamza na kumfanya Frida kucheka kidogo, alikuwa mrembo na alipendeza alivyocheka.

“Nikajua mpole , ila unaonekana ni muongeaji”

“Mimi sio mpole , kuna muda nakuwa mkimya tu , ila nachangamka sana mbele ya wanawake warembo”

“Haha..weka kwanza mzigo chini”Aliongea na kumfanya Hamza kukumbuka kumbe alikuwa amebeba boksi.

Frida alimwangalia Hamza kwa umakini , ni kama kuna kitu alichokuwa akikitafuta.

“Nilijua pia wewe ni mtu wa Delivery , ila unaonekana sio wa kawaida?”Aliongea.

“Unamaanisha nini mimi kutokuwa wa kawaida?”

“Mavazi yako , ineonekana umetokea ofisini na sio ofisi ya kawaida , mtu wa kawaida hawezi kumudu kuvaa Armani , Jimmy Choo , Audamars Piguet na Monte Blanc, sio mavazi ya mtu wa hadhi ya delivery haya”Aliongea Frida huku akiwa amemsogelea Hamza kwa ukaribu na kuchunguza mavazi yake.

Hamza alikuwa ashasahau kama amevaa mavazi ya bei ghali , ukweli ni kwamba asubuhi alivyorushiwa na Regina nguo hizo hakujiuliza uliza ni Brand gani, pengine labda ile staili ya Regina alivyomrushia kama vile ni nguo za mtumba, lakini sasa ni kama anaambiwa alikuwa amevaa suti ya Armani , Viatu Brand yya Jimmy Choo , Saa Brand ya Audamars Piguet na mkanda wa Monte Blanc, aliishia kumlaani Regina ndani kwa ndani kwa kumvalisha mavazi yasioendana na hadhi yake, alijiambia yaani anapokea mshahara wa milioni moja lakini amevalishwa mavazi ya milioni kumi , tena akapanda kabisa daladala.

Kwa mtu wa kawaida pengine ingeonekana mavazi hayo kuwa kitu cha ajabu lakini kwa mwanamke kama Regina ambae hela ni kitu cha kawaida, ukweli ni kwamba alifanya kuagiza tu kwa kutoa vipimo na alieleta mavazi ndio alichagua ya gharama ya juu, lakini hata kama angeenda mwenyewe kununua basi angechagua mavazi ya bei hio hio , labda brand tofauti tu.

Hata hivyo aliona mrembo huyu alikuwa na uwezo wa kuzifahamu Brand, maana ilikuwa ni kwa kuangalia tu ashajua.

“Usipagawe na haya mavazi ya kawaida sana , mimi ni wale wa nimevalishwa na .. ki ufupi ni kwamba kutokana na muonekano wangu nafanya matangazo ya nguo , nikirudi navua nawarudishia wenye mali yao, nimebadilika muonekano ila sio hadhi”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu lakini kauli ile ilimfurahisha Frida maana imekaa ki uongo sana.

“Anyway , niite Dr Frida Franklin, nadhani nimejibu swali lako , mimi sio celebrity mpaka kuvalishwa nguo kwa ajili ya kutangaza biashara”Aliongea kwa tabasamu na kisha alibeba boksi lile na kuondoka sebuleni.

Hamza aliishia kutoa tabasamu tu na sasa ndio anajua mrembo huyo ni Dokta , ndio maana alionekana kitaaluma taaluma.

“Hehe. napenda wanawake wasiotabirika kama hawa..”Aliwaza Hamza na palepale alikaa kwenye sofa.

Dakika chache tu Frida alirudi akiwa na kibunda cha hela na kumpatia Hamza jambo ambalo lilimfanya ashangae.

“Mbona nyingi tofauti na malipo yaliopita?”Aliuliza kwa shauku.

“Leo nakulipa kulingana na muonekano wako , hio ni hela ya delivery kuhusu malipo ya mzigo nishalipa kwa Alex moja kwa moja”Aliongea na kauli ile ilimpagawisha Hamza , alikuwa akipenda hela , lakini kulipwa kitita cha pesa halikuwa jambo la kawaida.

“Hivi vyungu kwanini thamani yake ni kubwa , kuna haja ya kutoa kiasi chote hiki cha pesa?”

“Unataka majibu?”Aliongea Frida akiwa na tabasamu huku akikaa kwenye sofa.

“Ukinijibu utaiondoa shauku yangu?”

“Kilichokufanya kuwa na hiari ya kuleta delivery licha ya kuwa na muonekano huo ni dhahiri shauku ndio inakusukuma , kama ilivyokwako , mimi pia kutoa kiasi kikubwa hivyo kwa ajili ya kuleta delivery shauku yangu imenisukuma pia”Aliongea

“Shauku gani?”

“I see you’re in the initial stage of sorcery,what led you to the choice of delving into the study of magic??

“Naona upo hatua za mwanzoni za kujifunza uchawi,nini kimekufanya kuchukua maamuzi ya kujifunza ulozi”Aliuliza kwa kingereza lakini swali lile lilimfanya Hamza kubadilika ghafla tu.









SEHEMU YA 24.

Swali lile ilikuwa ni kama Trigger ya bunduki , Hamza alibadilika palepale , zile nywele zake za kizungu zilisimama na kuanza kuchemka kama singa singa huku sura yake ikitisha.

Ilikuwa ni kufumba na kufumbua Miwani ya Frida ilishadondoka chini huku yeye mwenyewe akielea hewani akiwa amezingirwa na kitu kama kizimba cha Dimension’tatu chenye kufika mwanga flani mweupe na kufifia kwa wakati mmoja.

Hamza hakuwa na huruma hata kidogo , muda huo alionekana sio Hamza tena , ni kama shetani.

“Wewe ni nani?”Sauti hio ndio iliomtoka Hamza huku Frida akiendelea kufurukuta.

“Naitwa… naitwa Frida Franklin Genesha , Agent Two F”Aliongea na mara baada ya kuongea vile usinga wa nywele za Hamza ulirudi katika hali yake ya kawaida na Frida alidondokea katika sofa.

Hamza alisogea mpaka katika Sofa la mbele na kukaa chini huku akikunja nne na tabasamu la uovu usoni .

“Haina haja ya kuendelea kuwa katika muonekano feki , unaonaje ukiondoa hio Mask ya kichawi tuone sura yako halisi”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu na kauli ile ilimfanya Frida aliekuwa akihema kama mbwa aliekimbia maili nyingi kutoa mshangao.

“Ulinifahamu tokea siku ya kwanza!!?”Aliuliza akiwa katika hali ya mshangao na Hamza aliishia kutoa tabasamu.

“Nilipokuja hapa siku ya kwanza sikukufahamu moja kwa moja , lakini kuna kitu kilinifanya nikushuku mara moja”Aliongea Hamza na kumfanya Frida kuongeza umakini.

“Inawezekana ikawa kawaida katika jamii , lakini ni mara chache sana kushuhudia mwanamke anaogelea akiwa na pete ya thamani kubwa kidoleni’Aliongea na palepale alinyooshea mkono wa Frida aliovaa pete.

Frida mara baada ya kusikia kauli ile sasa alielewa , ni kweli tokea avae hio pete hakujua ni lini aliivua na anasababu za kufanya hivyo.

In the Knows kati ya mwanachama na mwanachama wa Wiccan katika kutambuana mara nyingi huhusisha alama ya vito , japo zipo njia nyingi,mimi nilikufahamu na nilijua kuna uwezekano na wewe umenifahamu , nimekuja leo hii nikitarajia swali lako”Aliongea Hamza.

“Haiwezekani , ni kweli pete yangu ipo katika orodha ya In the Knows lakini hii pete aina ya Pentacle iliotumika ni siri ya dunia, alama yake inaingia katika orodha ya The lost symbols , mpaka kuifahamu inamaanisha na wewe ni mwanachama, tena katika digrii ya juu”

“Mimi sio mwanachama wa Wiccan”Aliongea Hamza kivivu huku akitoa tabasamu la kizembe.

“Kama wewe sio mwanachama wa Wiccan ni nani , wewe ni Muislamu , Mkristo au Mbuddha?”

“Unaniuliza swali la namna hio inanifanya nishangae , umejitambulisha kwangu kama Agent Two F , hii ni neno la kodi ambalo Dokta Genesha alinitajia , ulivyotaja jina hilo nikakuacha mara moja , nadhani unalifahamu hivyo , kama ndio haina haja ya kuniuliza mimi nipo upande upi wa kiimani katika ulimwengu huu , hayo ni maswali ambayo wewe unatakiwa kunijibu , Vinginevyo nitaamini hujatoka katika kivuli cha Dokta Genesha , ushajua siri yangu napaswa kukuua kama huna majibu”Aliongea na Frida alionekana kufikiria kidogo.

“Nimechukua tahadhari tokea unakaribia kufika hapa , lakini tahadhari haitoshi , umenifahamu kama mfuasi wa Wiccan na siwezi kukupa majibu nikiwa katika vifungo vya kiroho vya Wiccan”.

“Njia gani unaweza kujifungua katika vifungo na kujibu maswali yangu yote , nakupa heshima hii kwasababu ya Dokta Genesha hivyo unapaswa kuwa mkweli”Aliongea Hamza.

“Njia pekee ni kuuvua muonekano wangu katika chumba cha nuru , ndio jia pekee ambayo watu wa madhabahu hawatogundua , nikiwa katika uhalisia wangu nitaweza kujibu maswali yako yote”Aliongea na kumfanya Hamza kushangaa.

“Kwahio wewe ni Double Agent , unafanya kazi chini ya Sinagogi na Wiccan kwa wakati mmoja?”

“Wote tuliopo chini ya kivuli cha Genesha kiasili ni wanasinagogi , sidhani hili ni swala la kukushangaza , kabla sijaingia katika chumba cha nuru unapaswa kujibu swali langu kwa maelekezo ya Dokta Genesha?”

“Uliza swali lako?, maana ikija wakati wa maswali yangu unapaswa kujibu yote”

“Ushawahi kuota ndoto kama uhalisia , upo katika mazingira ambayo ni tofauti na ulimwengu wa kawaida?”Aliuliza Frida huku wakiwa na muonekano wa siriasi.

“Umejuaje nimeota ndoto ya namna hio?”Aliuliza Hamza akiwa ameshangaa , ilikuwa ni kweli kabisa aliota ndoto yupo katika mazingira ambayo sio ya kawaida.

Hamza ni kama sasa anaanza kuamini uwezo wa Frida , ukweli ni kwamba wakati anarudi Tanzania alikuwa akisubiria mtu ambae anaweza kumwambia yeye ni nani , sio kama hakuwa akijua yeye ni nani la hasa , alikuwa akijua yeye ni Hamza na historia yake kwa ufupi , lakini kuna swali kubwa ambalo linahusiana na nguvu iliopo ndani ya mwili wake.

Kwa maelekezo ya Dokta Genesha ambae alikuwa mwalimu wake , alimwambia amtafute Agent Two F na ndio maana mara baada yya Frida kutaja jina lake kamili alimuacha mara moja.

Frida alimwangalia Hamza , licha ya kuonekana kuridhika lakini alionekana akifikiria pia.

“Ulichoota sio ndoto , uhalisia wako ndio unakuita, ndio njia pekee ya kumfahamu mtu aliekuwa nyuma yako mpaka kufikia leo hii”

“Unamaanisha Mzee?”

“Hio si ndio misheni yako kwa sasa ya kumfahamu Mzee , huwezi kumfahamu kabla ya kuujua uhalisia wako , mimi sio mtu wa kujibu maswali yako, ni wa kukuongoza tu kisayansi kupitia taaluma yangu, kufupisha tu majibu yapo ndani ya nafsi ambayo imelala ndani yako”

“Nafsi unataka kumaanisha kuna nafsi zaidi ya niliokuwa nayo?”Aliongea Hamza akiwa katika mshangao na Frida tofauti na kujibu alishika ile tarakishi na kuchezesha vidole kwa dakika kadhaa na kumpatia Hamza.

“Hizi ni takwimu za wagonjwa wa akili kwa upande wa Afrika tu katika kipindi cha mwaka 2020 mpaka mwaka huu , ni idadi mara kumi zaidi ya miaka yote ya nyuma”Aliongea na Hamza alisoma takwimu ile , ilikuwa ni kweli kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa akili.

“Umegundua nini?”

“Wengi ya hawa wagonjwa naona wanafanana dalili na Diagnosis, Ugonjwa wa akili wa DID ndio umeshika kasi , Zamani ugonjwa huu wa akili ulikuwa adimu sana”

“Ndio ulikuwa adimu , hivyo inamaanisha kuongezeka kwa wagonjwa wa aina hii kuna sababu, hii ni takwimu za wale tu ambao wameripoti hospitalini , lakini wapo wengi hawajui wanaugua huu ugonjwa, japo wanaonekana kuwa wa kawaida kwa nje lakini kwa ndani kuna kitu kikubwa kinachoendelea”Hamza mara baada ya kusikia maelezo hayo alijikua akimfikiria Mellisa mpenzi wake na Amiri , alijiuliza au Mellisa alikuwa pia mhanga wa ugonjwa huo , alifikiria lakini aliona haiwezekani iwe hivyo.

“Umeongea sana , nataka kujua kinachofuata ni nini , umesea majibu ninayo mwenyewe lakini sina ninachoelewa, halafu kwanini hutaki kuwa katika uhalisia wako , hio mask unavua saa ngapi?”

“Kitendo cha kuvua hii Mask moja kwa moja najitoa katika mtandao wa Wiccan ,siwezi kufanya hivyo hapa na pia siwezi kukuingiza katika uhalisia wako nikiwa katika mtandao wa Wiccan , lazima niingie katika Chumba cha nuru kwanza”

“Chumba cha Nuru, ndio kwamba huwezi kushitukiwa unachofanya?”

“Ukishaingia katika chumba cha nuru ni kama unapotea katika mazingira ya kawaida , kwa maana mtandao wa kimadhabahu wa Wiccan hauwezi kujua eneo ulipo na unachofanya ni nini?”Hamza alionekana kumwelewa hata hivyo alikuwa na uzoefu wa aina hio.

“Tanzania kuna chumba cha Nuru?”

Hamza alikuwa akijua kuhusu chumba cha Nuru , Dokta Genesha alikuwa ndio mgunduzi mkuu wa Nuru ndio ilikuwa uthibitisho wa kisayansi aliokuwa nao wakati akitangazia ulimwengu kwamba ulimwengu wa kiroho ni uhalisia na anaweza kuthibitisha hilo, lakini ukweli ni kwamba alichogundua Dokta Genesha kilikuwepo na kikafanywa siri kama ililivyokuwa siri kwa dunia na kwanzia hapo Dokta Genesha hakuwahi kuweka wazi ni ushahidi gani aliokuwa nao mpaka kuaminisha watu kwamba ulimwengu wa kiroho ni uhalisia.

“Swali hilo napaswa nikuulize wewe , kwa maelezo niliokuwa nayo wewe ndio mtu pekee unaejua wapi kilipo chumba cha Nuru”Aliongea na kauli ile ilimsahngaza Hamza.

“Unamaanisha nini mimi ndio ninajua , kama ninajua ningeuliza?”Aliongea Hamza akiona kabisa ni kama Frida anamchezea akili.

“Mpaka sasa Wiccan udhaifu wao mkubwa ni elementi zilizounda nguvu ya Nuru , licha ya ukweli kwamba Nuru ndio ugunduzi uliokuwepo tokea zama za kale lakini hakuna mwanachama yoyote ambae alishawahi kushuhudia kwa macho ushahidi huo , imebakia kuwa katika makisio ndani ya Wiccan , lakini haibadilishi ukweli kwamba kitu hicho hakipo na wanaamini ni nguvu ambayo ni mali yao?”

“Wiccan ni wachawi kama wachawi wengine tu , kwanini wanahangaika na Nuru , kitu ambacho kina madhara kwao?”

“Hawahaingiki na Nuru , Wanaamini nguvu hio imetokana na alementi zote nne za dunia yaani , Roho , hewa , maji , moto na Ardhi,mfano mwepesi alitoa mwanachama wa juu kabisa wa Wiccan Ann -Marie Galagher , ili mmea ustawi unahitaji ardhi , maji au unyevunyevu , moto au jua na hewa ambayo ni oksijeni kutoka Carbondioxide sasa katika hivi vitatu vinawezekana kufanya kazi pamoja kwa kuunganishwa na roho , sasa unaona hapo hawahangaiki na Nuru kwani tayari Nuru ipo katika elementi hizo tano”

“Kwahio unachomaanisha ni kwamba Nuru inayozungumziwa hapa sio nuru kama nuru inayoonekana bali ni kitu tofauti kabisa?”

“Ndio lakini wanaamini msingi wake ni ndani ya elementi zote za dunia na hakuna sababu ya nje ya nuru , siri hii wamekuwa wakiiwinda kwa muda mrefu sana na wote wenye majibu walishakufa , ambae alikuwa na siri hii ni Dokta Genesha na ndie ambae ametengeneza chumba cha Nuru ambapo mpaka sasa haieleweki kipo sehemu gani lakini ndio udhaifu mkubwa wa nguvu ya Wiccan”

“Sasa kwanini mimi niwe ndio ambae najua chumba hiko , hapa mnanichanganya sijui chochote”

“Kitendo cha kuota tayari ndoto hio inamaana unaukaribia ukweli , kazi ambayo inatakiwa kukufanya kwasasa ni kuendelea pale ulipoishia?”

“Unamaanisha nilipoishia kuota ama , inawezekana vipi kumfanya mtu kuendelea kuota kama unaangalia filamu”

“Ni kitu ambacho hakikuwa kikiwezekana lakini teknolojia imekuwa, katika ulimwengu wa kiroho you’re more than yourself, wewe ni zaidi ya wewe mwenyewe”Aliongea na kumfanya Hamza asimame.

“Kabla sijaondoka nataka kwanza kujua vyungu hivyo kazi yake ni nini , kwanini gharama yake ni kubwa , tuanzie kwanza hapo na ndio tuendelee”

“Tunachonunua sio chungu , chnngu ni njia ya usafirishaji tu , kinachonunuliwa ni viungo vya akili iliolala, unaweza kusema ni kama dawa inayomsaidia mtu kuota nje ya uzoefu wa kumbukumbu za maisha yake”

“Unamaanisha kuna vitu vipo katika chungu hiko?”

“Hilo ndio jibu , kinachofanyika unapewa kifaa maalumu ambacho kinapasha joto chungu hicho na hapo hutoa marashi ya aina flani yanayokufanya mwili wako kuwa kama umekufa huku akili yako ikifanya kazi katika mazingira ya nje ya kumbukumbu zako, sijui ni siri gani ilopo juu ya marashi hayo lakini nilikuwa nikifanya utafiti mwaka wa tatu huu sijaweza kuona chochote tofauti kisayansi nje ya udongo wa kawaida uliotengenezea”

“Kwahio wewe unachukua hivi vyungu sio kwasababu unataka kutumia kama viungo vya akili , bali ni kwasababu ya kufanyia utafiti?”

“Upo sahihi , kuna siri kubwa ndani yake ,ambao ndio na itafuta , wenye kujua siri hii ni Binamu pekee na ndio wenye mtandao wa usambazaji dunia nzima , kwasasa imekuwa mbadala wa madawa ya kulevya, inaweza kuwa chanzo pia cha ongezeko kubwa la ugonjwa wa akili”.

Hamza alijikuta akiangalia saa na muda ulikuwa umeenda kweli , ilikuwa ni saa moja kamili tayari za usiku.

Alitamani kujua vitu vingi kutoka kwa Frida lakini simu yake ndio iliomshitua , alipoangalia aliekuwa akipiga ni Shangazi na alipokea haraka na baada ya kumsalimia swali lilofuatia ndio lilimshangaza Hamza.

“Hamza kuna sehemu mmepitia , mtakula huko huko au niwahesabu kwenye chakua cha usiku?”Swali lile lilimshangaza Hamza.

“Shangazi kwanini unauliza hivyo?”

“Nimeona hamjarudi wote ndio maana nauliza”

“Shangazi unamaanisha Regina hajarudi bado?”

“Ndio , kwani hampo pamoja , nimeshindwa kumpata hewani ndio maana nimekupigia wewe , nini kinaendelea?”Shangazi alionekana kuwa na wasiwasi na Hamza alisimama palepale.

“Basi sawa shangazi , usiwe na wasiwasi ngoja nimtafute nitakupa jibu muda si mrefu”Hamza kengele ya hatari ilishagonga katika akili yake na kwa haraka sana alipiga simu ya Regina na iliita ndani ya sekunde chache tu na kupokelewa.

“Regina upo wapi , Shangazi anasema hakupati hewani”Sauti iliomjibu Hamza ilimfanya uso wake kujikunja palepale.

“Mr Hamza it seems like this beautiful lady real does have a special relationship with you…”

Hamza mara moja alishaijua sauti hio kutokana na lafudhi yake , alikuwa ni Mendoza jamaa mwenye Marasta aliekutana nae siku kadhaa nyuma.

“Hivi unajua unachokifanya kwanza?”Aliuliza Hamza huku akihisi miguu yake kuwa na ubaridi

Upande mwingine licha ya kwamba walikuwa mbali na Hamza lakini walikuwa na hofu kubwa mno , kama sio kwa matamanio yao juu ya kitabu walichokuwa wakifatilia wasingeenda mbali kumshika simba masharubu

“Mr Hamza tunajua kabisa tunachokifanya kitakukasirisha , lakini kuna ule msemo wa ni kheri kufa ukiwa unajaribu kuliko kutojaribu kabisa.

“Ongea unachotaka kutoka kwangu ni nini?”Aliongea Hamza.
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.



MTUNZI:SINGANO JR



SEHEMU YA 25.

“Ni rahisi sana kitabu au tuambie wapi alipo Tembo wa Trishaza na ndio tutamuachia huyu mwanamke haraka iwezekanavyo”Aliongea Mendoza

“Mabadilishano yatafanyikia wapi?”Aliuliza Hamza , hakutaka kupoteza muda.

“Kama tulivyotarajia , kumbe kitabu unacho?”Aliongea na muda ulule alimtajia eneo ambalo anapaswa kwenda.

“Mr Hamza tunakupatia masaa matatu kamili , ukipitisha hayo masaa usije kutulaumu huyu mwanamke akipotea na sisi”Aliongea na Hamza hakutaka kuendelea kusikiliza porojo zao kwani alikata simu.

“Kuna nini?”Aliuliza Frida.

“Nadhani nitakutafuta siku nyingine”Aliongea Hamza na mara moja alimuacha Frida akimwagalia kwa wasiwasi.

Hamza mara baada ya kutoka nje kabisa alimpigia Shangazi simu na kumwambia ashampata Regina na watarudi muda si mrefu ila asiwahesabu kwenye chakula cha usiku , alifanya hivyo kwa ajili ya kumtoa wasiwasi.

Sehemu ambayo Mendoza aliokuwa amemtajia ilikuwa ni Zinga ya Bagamoyo kijiji cha wavuvi.

Eneo hilo lilikuwa tulivu mno, pengine ni kwasababu wavuvi walikuwa washaondoka kuelekea baharini kuvua.

Nje kabisa ya moja ya Ghala la kampuni ya uvuvi Gari ya Regina ile Lexus ilikuwa imeegeshwa karibu kabisa na sehemu nyavu za kuvulia zinapohifadhiwa.

Ndani ya Ghala hilo kulikuwa na harufu nzito mno ya samaki , Regina alikuwa amefungwa kwenye kiti na hakuwa na uwezo wa kusogea hata kidogo, nywele zake zilikuwa zimechanguka pia kutokana na kibanio kumtoka na vile alivyokuwa akitingisha kichwa ndio alivyozidi kuchanguka.

Hakuwa akipiga kelele hata kidogo zaidi ya kuangalia wanaume wawili waliokuwa mbele yake na muonekano uliojaa sumu.

Regina alikuwa akikumbuka wakati alipokuwa akikaribia nyumbani ni mwanamke wa kizungu ambae alionekana kama mgeni ndio aliesimamisha gari yake akionekana kutaka kuuliza swali.

Matokeo yake kitendo cha kushusha kioo tu alijikuta akinusa marashi ambayo yalimpelekea kupoteza fahamu na mara baada ya kushituka alikuwa tayari ndani ya eneo lenye harufu kali katika ghala hilo akiwa amefungwa , mwanzoni alidhani yupo feri lakini mara baada ya kuangalia taa hafifu ndani ya ghala hilo na maboksi ya kutunza baridi alijikuta akiaini hakuwa karibu na jiji la Dar.

Akili yake ilimwambia kabisa watu wale hawakuwa watanzania hata kidogo na hio ni kutokana na namna walivyokuwa wakiongea.

“What is your goal , if you want money , then you should ask me to call home”Aliongea Regina kwa kingereza akimaanisha nini lengo lao, kama ni hela basi wamuache apige simu nyumbani.

“Madam , My Companion Huda is only joking , she has no ill intentions , we just want to know what kind of relationship you have with that Mr Hamza , who is he and where he’s from”Aliongea akimaanisha yeye na mwenzake Huda wanatania tu , na hawana nia mbaya , wanachotaka kujua ni uhusiano wake na Hamza , ni nani na anatokea wapi.

“Mr Hamza.. Mnamaanisha Hamza!!”Aliongea Regina akionekana kushangaa na palepale alijiuliza au hili kundi la watu lililomteka hawakuwa wakimlenga yeye bali ni Hamza.

Kitu kingine ni kwamba walikuwa wakiuliza kuhusu uhusiano wake na Hamza , sasa alijiuliza kwanini waulize swali hilo.

Regina alishindwa kujizuia kimawazo na kuamini pengine ni James ndio ametuma watekaji kwa ajili ya kuupata ukweli juu ya uhusiano wake na Hamza , lakini alijiuliza kwanini raia wa kigeni.?.

“Ni Boyfriend wangu , pia ni mwanachuo na fundi wa vifaa vya kieletroniksi”Aliongea Regina kwa kingereza.

“Boyfriend!!, Ndio maana anakujali mno mpaka kuwa tayari kutupatia Ankh, inaonekana anakupenda sana”

“Anka!! Unamaanisha nini?”Aliuliza Regina mara baada ya kusikia sauti hio lakini hakuelewa maneno hayo yalikuwa yakimaanisha nini.

Upande mwingine kati ya wanawake wawili waliokuwa katika kundi hilo , yule aliefahamika kwa jina la Corrella uso wake ulionyesha kutoridhika.

“Umesema ni fundi na mwanafunzi , mtu ambae ameweza kujua uwepo wetu hawezi kuwa mwanafunzi na fundi , acha kututania wewe mwanamke”Aliongea na dakika ileile alitoa kisu cha kung’aa sana na kumsogelea Regina na kukiweka karibu na uso wake , ilikuwa ni kama vile anataka kukata pua ya Regina.

Regina macho yake yalianza kuonyesha kupaniki , ijapokuwa siku zote hakujali sana kuupamba uso wake lakini yeye ni mwanamke na siku zote alikuwa akijivunia kuwa mzuri , ni mwanamke hata hivyo , aliona kama akipotezewa urembo wake itakuwa ni kheri ya kifo.

“Nilichosema ni kweli , kama huamini muulizeni mwenyewe”Aliongea na Mendoza alimsogelea Huda na kumzuia kwa kumshika mkono.

“Huda muache , pengine Hamza siku hizi kaamua kuwa mwanafunzi na fundi , ni jambo la kawaida kwa ninja kama yeye kuwa na utambulisho feki”

Regina mara baada ya kusikia utambulisho feki ,Ninja Regina mara baada ya kusikia maneno hayo ni sasa ni kama akili yake inafanya kazi na kuona ni kweli Hamza alionekana sio wa kawaida.

“Madam , ushawahi kusikia kitabu chochote chenye alama ya Ankh kutoka kwa Mr Hamza , au Kitabu cha Riwaya ya ndege juu ya mti wa uzima?”

“Mnasema sijui anka gani , ni kitabu cha namna gani hicho?”

“Inaonekana kweli huelewi tunachozungumzia , ni kitu muhimu hivyo uwezekano ni mkubwa hawezi kukiweka holelaholela mtu yoyote kuona , Sio rahisi kumuonyesha mpenzi wake”

Yule mwanamke aliefahamika kwa jina la Huda alichora chini alama flani hivi ,haikuwa kama msalaba bali ilikaa kama rungu yenye mkato katikati.

“Hujawahi kuona kitabu chenye alama ya namna hii?”Aliuliza yule mwanamke na Regina aliishia kutingisha kichwa kwamba hajawahi kuona , ukweli ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuona alama hio.

“Hajui chochote , inaonekana Mr Hamza alikuwa makini kuficha”Aliongea Correla.

Regina aliishia kusikiliza mazungumzo yao na yalionekana sio kati yake na Hamza kabisa na alianza kuwa na wasiwasi zaidi.

“Sio James aliewatuma?”Aliuliza Regina , ijapokuwa aliona kabisa swali hilo ni la kijinga lakini aliona aulize.

“James , ni nani huyo na anakaa wapi?, sisi ni wawindaji wa binadamu kutoka Samar , unaweza kutuita Tumbili Wenye mbawa za Tai”Aliongea kwa majisifu.

Regina japo hakuelewa walichokuwa wakimaanisha lakini alishaamini sio watu waliotumwa na James , maana ndio adui yake ambae alidhani anaweza kumteka.

“Nadhani tukamfunge ndani ya boti yetu moja kwa moja , tusipopata kitabu tunaondoka nae , ndio namna pekee ambayo hatutaweza kupambana nae ana kwa ana”Aliongea bwana mwingine , huyu hakuwepo katika kundi ambalo lilimsimamisha Hamza kule Kongowe.

“Noni, ulichoongea kinaleta maana , nitaliacha hili mikononi mwako”Aliongea Mendoza

Regina mara baada ya kuona kile kinachoenda kutokea alizidi kuwa na wasiwasi na alijiuliza au alikuwa akishikiliwa kwa kudhaniwa ni mpenzi kweli wa Hamza.

Aliona woga kwani mmoja wapo alikuwa kabisa na bastora kiunoni na moja kwa moja akili yake ilijua watu waliokuwa mbele yake wanazidi kuwa hatari kila alivyokuwa akiwafikiria na kuwachunguzana, hisia zake zilimwambia kama ni hivyo basi na Hamza atakuwa hatarini.

Alikumbuka namna ambavyo Hamza alivyokuwa akimkwepa Yonesi wakati wakipigana na kutofanya mashambulizi , aliona kabisa kitendo kile ilikuwa ni Hamza kuwa muoga.

“Subirini kwanza,mmekosea jambo moja , kunikamata kwenu hakutowapatia hicho kitabu”Aliongea Regina.

“Oh , kwanini unasema hivyo?”Aliuliza aliekuwa mlangoni.

“Mimi nimefahamiana na Hamza juzi tu hapa ni mtu muoga mno , nina uhakika anawaogopa mno na hawezi kuhatarisha maisha yake kuja kuniokoa , huu mpango wenu ushafeli tayari”

Mara baada ya kumsikia akiongea hivyo watekaji wote waliangua kicheko kana kwamba alichoongea ni ujinga wa karne.

“Unadhani tunaweza kukuamini?, Yaani Hamza atuogope sisi haha…hiki ni kichekesho cha mwaka”

“Kwanini asiwaogope? , nyie hamumjui yule vizuri , ni muoga kweli”Aliongea Regina huku akiona yeye mwenyewe maneno yake ni ya ajabu.

“Wewe mwanamke unadhani sisi ni wajinga , tulishampigia tayari wakati ukiwa hujitambui na ametuambia anakuja , nadhani muda si mrefu atafika hapa , anaonekana kujali kweli usalama wako”

“Nini!?Anakuja? , kwa uoga ule inawezekana vipi?”

Regina alionyesha kushangaa na kudhani alikuwa amemdhania Hamza vibaya lakini mara baada ya kufikiria anakuja kukutana na hawa wahalifu alianza kushikwa na wasiwasi na aliona kama Hamza ana akili ni bora asije kabisa , Hamza anaemjua yeye ni mtu ambae anaogopa mshahara wake kukatwa na amekaa kizembe zembe.

Hamza hakuwa hata mwanaume kwa kitendo chake cha kushindwa kujizuia na kumchungulia kupitia kioo , alijiambia hio sio tabia ambayo mwanaume jasiri anaweza kufanya, sasa mtu yule aliempiga chabo ndio aje kumuokoa , aliona haiwezekani lakini hata hivyo aliona atulie aone mwisho wake.

Alijikuta akifikiria na upande wa pili wa Hamza na aliona kuna muda mwingine anaonekana kuwa siriasi hivi na kuwa na akili nyingi lakini pia ni mkarimu mpaka kumletea matunda kwa ajili ya kupoza njaa , Regina hakukataa na kuona inawezekana roho yake nzuri ikamtuma kuja kumuokoa.

Wakati Regina akijiuliza maswali mengi Hamza ni nani mpaka kuwa na ujaisri wa kuja kumuokoa dio muda mlango wa ghala hilo uligongwa.

“Noni mlete huyo mwanamke kuelekea kwenye boti , nitadili nae mimi”Aliongea Mendoza mara baada ya kuona Hamza amefika.

“Hey , usiniguse”Aliongea Regina mara baada ya kuona yule mwanaume bonge wa kifilipino aliefahamika kwa jina la Noni akitaka kumgusa.

“Stupid Woman , try this”

Aliongea Corrella aliekuwa amesimama mbele ya Regina na alitoa kichupa kama cha spray na kumpulizia usoni na palepale mara baada ya kuvuta yale marashi alipoteza fahamu palepale.

Dakika hio hio kabla hata hawajamfungua kutoka kwenye kiti mlango wa mbele wa ghala ulipigwa teke na kufunguka mara moja licha ya loki zake kuwa za chuma, pengine ni kutokana na kutu ndio maana imekuwa rahisi.

Baada ya mlango kufunguka , mtu alieonekana mlangoni alikuwa ni Hamza akitafuna bublish huku mguu mmoja ukiwa hewani , akionyesha kwamba mlango huo aliupiga na teke moja tu mpaka kufunguka.

Mendoza , Huda na Noni wote walikuwa kwenye mshituko kutokana na nguvu za Hamza, kwani teke moja tu mlango ulikuwa umefunguka.

Hamza hakuwa na wasiwasi kabisa ni kama amekuja kutalii , alikuwa akitafuna bablish huku akipiga hatua za taratibu kuingia ndani kama bosi wa watekaji hao.

Lakini kadri ambavyo alikuwa akipiga hatua walijihisi miili yao kuwasisimka , ilikuwa ni kama vile ghala lote limefunikwa na nguvu isio kuwa ya kawaida, dakika ileile Vivuli vitano viliweza kuonekana katika kila upande wa ghala hilo na ilikuwa ni kama vile vivuli viilikuwa vikiwaangalia wale watekaji jambo ambalo liliwashangaza.

Walianza kushikwa na hofu na waliweza kuona ni namna gani Hamza alikuwa akitisha kama vile ni jini.

“Nadhani niliiwaambia hampaswi kuwepo Tanzania na kunifuatilia , ila naona hamkunielewa”Aliongea na palepale alimsogelea Correla ambae alikuwa karibu na Regina akiwa ameshikilia kisu.

“Usisogee kama hutaki huyu mwanamke kufa mbele yako”Aliongea kwa kuamrisha.

Hamza alionekana ni kama vile hajamsikia na aliendelea kusogea mbele,muonekano wake haukubadilika hata kidogo, alikuwa akitembea kana kwamba anapita kwenye kiambaza cha nyumba.

Lakini sasa kadri dakika zilivyokuwa zikiongezeka hali ilizidi kuwa ya baridi ndani ya eneo hilo huku Hamza akizidi kutisha na nywele zake zilianza kucheza cheza

Nori kuona vile palepale alichomoa bastora kutoka kiunoni na kumnyooshea.

“Simama hapo hapo, ukisogea tu nitakulipua”Aliongea

“Lipua tu, ila unatakiwa kwanza kuitoa katika safety deposit”Aliongea na palepale ndio aligundua hakuwa amepandisha risasi kwenye chemba kutokana na kuwa na woga., kosa la namna hilo kwa uzeofu wake halijawahi kumtokea.

Ijapokuwa kwa haraka sana aliitoa katika hali ya usalama lakini mikono yake ilianza kutetemeka.

“Mr Hamza tunachotaka ni kitabu cha Ankh, ukitupatia tunakuhakikisha huyu mwanamke atakuwa salama”Aliongea Marasta.

“Si nilishawaambia sina kitabu cha Ankh tokea muda mrefu tu”

“Nini?”

Wote waliangaliana kwa mshangao kana kwamba walikuwa hawajamsikia vizuri.

“Kama ni hivyo , tuambie alipo Dokta Genesha”

Hamza wala hakujali , ki ufupi hakuongea lolotte tena na sasa alikuwa mita kama kumi kutoka kwa watekaji watatu , mara baada ya kusikia lile swali aliishia kutingisha kichwa chake.

“Mr Hamza usitukuchukulie wepesi , au unadhani hatuwezi kumdhuru huyu mwanamke?”Mara baada ya kuongea Huda kisu chake kilikuwa kishafikia shingo ya Regina huku Nori akiwa amemlenga Hamza na bunduki.

Hamza alisimama akiwa katika umbali wa mita kama sita hivi na kuwaangalia wote wanne bila ya kupepesa macho

“Kwasababu mmeweza kuteka basi naamini mnaweza kuua pia”

“Kama unalijua hivyo unapaswa kutoa ushirikiano”Aliongea Huda na kufanya midomo ya Hamza kucheza.

“Mmethuburu kufanya utekaji lakini haimaanishi mnaweza kuua mbele yangu”

Mara baada ya kusikia kauli hio walijikuta wakiwa katika hali ya kuchanganyikiwa lakini ndani ya sekunde iliofuata nguvu kubwa ya ajabu ilitokea na kuwababishia wahisi kama vile pumzi zinawaishia huku wakati mmoja ni kama vile wameshikwa na jinamizi na washindwe hataakupiga hatua , Hamza muda huo alikuwa ashawasogelea tayari.

Wakati sasa wakijua Hamza hakuja kutii maagizo yao bali kupigana , waliishia kujitahidi kurudi nyuma , na ghafla tu Nori alivuta Triga na kumlenga Hamza na bunduki.

“Bang , Bang, Bang!!”

Risasi zilifyatuka huku zikibeba joto kali lakini ajabu risasi zile ni kama vile zimetoboa karatasi na kupita, Hamza alikuwa ni kama vile amefifia katika ile sehemu aiokuwa amesimama na ni mwanga flani wa sura yake tu ndio uliokuwa ukicheza cheza, ilikuwa ajabu kweli.

Huda mara baada ya kuona hakukuwa na madhara juu ya risasi zile kwenda kwa Hamza aliamua kudili na Regina lakini alikuwa amechelewa kwani mkono wake ulioshikilia kisu ulikuwa umeshikwa na kivuli na ushindwe kuusogeza kabisa, hakujua hata ni kitu gani kimemshika na wakati akijaribu kufurukuta Hamza alikuwa ashamsogelea tayari.

Wawindaji wale wote walijikuta wakishangazwa na tukio hilo na walimwangalia Hamza kwa woga mno.

Walijiuliza nini kimetokea , mbona alikuwa mbali mno na alipo Huda lakini ameshindwa hata kumchinja yule mwanamke , ni nguvu gani iliokuwa ikimsaidia.

“Crack , Crack!!!”

Huda hakuwa hata na muda wa kujibu shambulizi , mikono yake yote ilikuwa imevunjwa vunjwa.

“Arghhhhhh…”

Hamza hakujali hata ukulele wake alimuondoa Huda mbele ya Regina kwa teke na kwenda kudondokea kwenye kingo ya kimbweta cha kuhifadhia maboksi ya kuhifadhia samaki,kutokana na nguvu iliotumika kumrusha kuwa kubwa alijikuta akivunjika uti wa mgongo na maisha yake yalikoma palepale huku damu nyingi zikimtoka.

“Huda!!”

Walijikuta wakiita wakiwa hawaamini mwenzao alikuwa ameshapoteza maisha , kila mmoja alishikilia siraha yake , wengie wakiwa na visu na wengine wakiwa na vifaa kama misumari mirefu na kutaka kumlenga Hamza lakini Hamza alikuwa mwepesi mno kwani sarakasi alizoruka hazikuwa za kawaida na kisha kuwapiga na Roundhouse kick.

“Arghhh!!”

Mara baada ya kuwapiga na mateke kifuani watekaji wale walijikuta wakipiga ukulele mkali na kwenda kudondokea kwenye ukuta huku wakitema damu nyingi chini, ilionekana eneo walilopigwa kifuani nguvu yake ilibomoa mpaka mapafu kwani walionekana wakishidwa kuvuta hewa na waliishia kutapatapa na kupoteza uhai kwa teke moja tu la kifua.

Ndani ya sekunde kumi tu Huda , Nori na Dodo walikuwa wameshapoteza maisha

Aliebakia alikuwa ni Mendoza na Mhindi na ilionekana ndio waliokuwa na nguvu kuliko wenzao wote.Walikuwa ni maninja daraja B,ni kosa kuwafananisha na wanajeshi au makomandoo, walikuwa zaidi ya makomandoo.

Katika mapigano ogopa yule mwanafunzi ambae anafundishwa kuua na si vinginevyo , uwezo wake unakuwa sio wa kawaida kabisa na ndio kilichokuwa kwa Mendoza.

Lakini mbele ya Hamza ni kama walikuwa watoto wa darasa la tatu ambao hawakuwa na mahali pakukimbilia.

Ijapokuwa alikuwa na hofu lakini utashi wa kutaka kuishi ulimfanya kutoa kisu kutoka katika kiuno chake na kutaka kumkata nacho shingoni Hamza, alikuwa ametumia uwezo wake wote wa kininja ili kuhakikisha shambulizi lake linafanikiwa.

Hamza mara baada ya kuona kisu kinakaribia kuikata shingo yake,alikuwa ashanyoosha mkono wake kwa chini na kuwekza kukikamata kwa vidole viwili tu tena kule kwenye makali.

Mtekaji alijaribu kusukuma mbele lakini alishindwa kabisa , ilikuwa ni vidole viwili tu vilivyoshikilia kile kisu lakini ni kama vile ni chuma ndio kimeshikilia.

Hamza aligeuza macho yake na kumwangalia , alikuwa na macho sio ya kawaida , ijapokuwa hayakutoka katika ubinadamu wake lakini ilidhihirisha hakuwa mtu mwenye huruma hata kidogo kwa namna ambavyo kiini cheusi kilivyokuwa kikipotea , Mhindi mara baada ya ya kuona namna ambavyo Hamza amebadilika kwa woga aliichia kile kisu na kukaa chini.

Hamza alikuwa na macho ya kichawi , macho yake ni kama yamepoteza kiini na hicho ndio kilimuogopesha Mhindi mtekaji na kuishia kukaa chini kwa hofu huku akijuliza ni macho ya namna gani.

“Wewe ni nani?”

Mendoza aliishia kuuliza kwa hofu akimwangalia Hamza kwa mshangao lakini Hamza hakujibu zaidi ya kutoa tabasamu la kikatili.

“Haiwezekani .. au wewe ni..?”

Mendoza aliekuwa na ujasiri wote alikuwa akimwemwesa midomo kwa woga kana kwamba ukichaa umemvaa , kutokana na msukumo wa nguvu kubwa isiokuwa ya kawaida alihisi mkojo ukimtoka palepale , wazo baya lilimwingia na kujiuliza inamaana kundi lao litakwenda kufutwa kama anachohisi ni cha kweli.

Mara baada ya kuona Hamza anaweza kuwa yule anaemdhania palepale alishuka chini na kupiga magoti.

“Sikujua wala kutegemea anuani ilioachwa katika maabara ya Dokta Genesha ni kuja kukutana na wewe , kama ningejua wewe ndio rafiki yake aliemzungumzia , sisi pamoja na kundi letu tusingekubali kuibeba kazi hii , naomba kwa gharama ambayo tumekwisha kulipa kwa vifo vyetu usije kuadhibu na umoja wetu wote”Aliongea Mendoza.

Hakujali tena kama atapoteza maisha hapo hapo , alichojali ni kuokoa umoja wao tu kwa muda huo maana kitendo cha kuja kumchokoza mtu aliekuwa mbele yake inamaanisha moja kwa moja umoja wao umeingia katika vita nae.

Muda uleule Hamza alikuwa ashatoka kwenye ule muonekano wake wa kishetani na kurudi kawaida

“Mimi sijali , mnaweza kuja kunitafuta lakini nitaendelea kuwapoteza mmoja baada ya mwingine, sina mudi ya kwenda kupambana na genge lenu lote la wachawi mimi”Aliongea Hamza.

“Ni kweli kabisa , sisi kwako ni kama kunguni tu , naomba kifo changu kiondoe kinyongo baina yako na kundi letu”Aliongea na palepale aliinnua kisu kilichokuwa chini na kujichoma eneo la moyo mwenyewe na kudondoka chini.

Kilikuwa ni kitendo cha kushangaza , alijichoma yeye mwenyewe kwa ajili ya kumzuia Hamza asiweke kinyongo na kundi lao.

Mhindi mara baada ya kuona mkuu wake kashajiua hakutaka kujiua kama ilivyokuwa kwake na mara baada ya kuona Hamza ameangalia pembeni palepale alisimama na kutimua mbio lakini jambo lile lilimfanya Hamza kutoa tabasamu na kurusha kile kisu kilichokuwa mkononi mwake na ile Mhindi anaukaribia mlango kisu kiliingia kutoka kwenye kisogo na kutokezea kwa mbele kwenye koromeo na akadondoka chini akitapatapa.

Hamza hakujali kabisa hata kitendo kile na aligeuza macho yake na kumwangalia Regina aliekuwa kwenye usingizi mzito na kuishia kutabasamu.



































SEHEMU YA 25.

Wakati Regina anaamka alijikuta akiwa kwenye gari akiwa ameegamia kwenye siti.

Alijikuta akivuta kumbukumbu ya kile kilichotokea na alikaa kitako kwa haraka na ndipo aliweza kuona gari ipo kwenye mwendo na Hamza ndio dereva.

“Regina umeamka , vipi unahisi kizunguzungu?”Aliuliza Hamza akiwa amegeuka na kumwangalia na tabasamu.

Regina alijikagua na kukagua mazingiara na kuthibitisha alikuwa salama.

“Wewe ndio umeniokoa?”Aliuliza

“Unaweza kusema hivyo , lakini haina haja ya kunishukuru , isitoshe hili limekutokea kwa sababu yangu “Aliongea Hamza

Regina aliishia kubakia kimya , alikuwa na hisia zisizoelezeka katika moyo wake na kujiambia inamaana huyu mwanaume ni kweli ameamua kuhatarisha maisha yake kweli na kuja kumsaidia.

“Umewezaje kuniokoa kwa wale watu?”Aliuliza maana alikuwa hana fahamu wakati Hamza akikinukisha.

“Nilifika pale na kisha nikawashushia kipigo , walivyoona hawaniwezi wakakimbia”Aliongea Hamza.

“Acha kunidanganya , mimi sio mtoto , wale watu walikuwa na visu na bunduki , halafu wewe ambae ulikuwa mikono mitupu ndio umewaweza mpaka wakakimbia?”Aliongea huku akionyesha kukasirika maana Hamza anamchezea akili yake kwa kumwambia uongo.

“Regina wewe hujui tu , lile lilikuwa kundi la watu wazembe , walikuwa wakikukuogopesha tu uwaone sio wa kawaida . halafu ile bunduki ulioona ni feki , ni kama zile wanazochezea watoto”

“Kama unachosema ni kweli , basi niambie kitabu cha Anka ndio nini , walisema sijui cha mti wa uzima?”Aliuliza huku akimwangalia Hamza kwa macho makali.

Hamza alijikuta akiingiwa na ubaridi mara baada ya kuulizwa swali lakini alirudi katika hali ya tabasamu kuficha wasiwasi wake.

“Anka ndio nini?”Aliuliza lakini kauli ile ilimfanya Regina asage meno yake kwa hasira.

“Wewe ni nani haswa , unajulikana kama mwanafunzi wa chuo na fundi,au wewe sio mwanafunzi kweli kama ulivyosema , kuna kitu unajaribu kuficha sio?”Aliuliza.

Hamza alijua hakuna uwezekano wa kumdanganya mwanamke huyo ambae vipimo vya IQ yake ni 180, hata kama anaweza asiwe vizuri kwenye maswala ya kimaisha lakini katika kitu muhimu kama hicho ambacho kilihusisha uhai wake ingekuwa ngumu kuepuka bila ya kujibu swali lake.

Lakini Hamza alijua kama Regina atajua vitu vingi kuhusu yeye basi moja kwa moja angekuwa katika hatari.

Alitaka kujali usalama wake sana kuliko kitu chochote ili isije ikatokea ajali huko mbele ya safari.

Hamza alienda kusimamisha gari ndani ya mgahawa wa Golden fork Mbezi beach.

“Hebu tutoke tukale kwanza , baada ya kumaliza kula nakuahidi nitakujibu maswali yako yote , sawa?”Aliongea Hamza.

Ni muda huo huo ndio Regina alijua kumbe walikuwa mbali sana na nyumbani , nje kulikuwa na giza hivyo hakuweza kuangalia hata walikuwa wapi.

“Kwanini tule hapa?”Aliuliza

“Saa tatu usiku sasa hivi , huoni kwamba mpaka tufike na kuanza kutafuta chakula itatuchosha sana, chukulia hii kama nafasi ya mimi kuomba msamaha kwa kilichokutokea, au unataka kula chakula kilichopikwa na shangazi?”

Regina mara baada ya kumsikia Hamza akimtaja Shangazi ndio wasiwasi ulimwingia.

“Vipi shangazi anajua kilichonitokea?”

“Usiwe na wasiwasi , nilimpigia simu na kumwambia tupo date”

“Mimi!? , Date na wewe?”Aliuliza huku akimwangalia kwa ukali usoni lakini hata hivyo aliridhika kuona Hamza alikuwa makini kutompa presha shangazi yake.

Alikuwa na njaa pia hivyo aliamua kutoka bila ya kuleta ubishi.

Mgahawa ulikuwa bize, jiji la Dar ilikuwa ni tofauti na maeneo mengine , saa tatu ndio watu walikuwa wakitafuta chakula cha usiku , mgahawa huo ulipendwa pia na wapenzi wanaowatoa out wenza wao, hivyo meza zilikuwa zimejaa watu wawili wawili.

Waliweza kupata meza ya wazi upande wa kulia karibu na mlango wa kuingilia , watu waliokuwa ndani ya eneo hilo walikwa wakiwapiga macho mno..

Ukweli ni kwamba walikuwa wakiendana sana , kwa urembo wa Regina na muonekano wa Hamza hakukuwa na tofauti kubwa kati yao na hakuna ambae anaweza kubisha kama wawili hao sio wapenzi.

Lakini macho ya wanaume yalikuwa yakimwangalia sana Regina ambae alikuw ana urembo usiokuwa wa kawaida , ijapokuwa nywele zake hazikuwa zimemkaa vizuri lakini alikuwa akivutia mno.

Pia kwa Regina alionekana kuzoea kuagalia hivyo haikumpa shida , lakini pia alipenda mgahawa huo.

Hamza aliagiza chakula kwa wote lakini aliomba maji ya kunywa yaletwe kwanza.

“Umesema utanielezea kilichotokea na wewe ni nani , niambie sasa”Aliongea Regina , hakuweza kuificha shauku yake.

“Usiwe na haraka , hebu tunywe kwanza maji tupoze koo maana siku imekuwa ndefu sana kwetu”Aliongea huku akimpatia glasi yenye maji.

Regina alikuwa na kiu pia hivyo alipokea na kunywa glasi ya kwanza akaongeza na ya pili na akawa ametosheka , aliishia kuangalia upande wa nje kana kwamba kuna kitu anafikiria.

“Shangazi alisema wewe ni Yatima, kabla ya kuzamia nje ya nchi ulikulia katika kituo gani cha kulelea watoto?”Aliuliza.

“Sikulelewa katika kituo chochote,niliishi mtaani”Aliongea Hamza, ndio njia jibu rahisi ambalo aliona linaweza kumridhisha Regina kwa muda huo.

“Ndio maana unaonekana mjanja janja, naamini haikuwa rahisi kuendesha maisha mtaani ukiwa katika umri mdogo”.

“Ni ngumu kwa mtoto yoyote asie na wazazi , iwe ni mtaani au katika kituo cha kulelea Yatima , ni swala la unafuu tu , kulikuwa na watoto wa mtaani ambao wametoroka vituo vya kulelea Yatima pia”Aliongea Hamza.

“Nimekulia kituo cha kulelea Yatima pia , mazingira yanaweza kuwa mazuri na kupata mahitaji yote lakini kisaikolojia kuna kitu unakosa hasa ukifikia ule umri wa kujitambua , nadhani ndio maana baadhi ya watoto wanatoroka , lakini ni kheri kituoni kuliko mtaani , ni asilimia ndogo sana ya watoto wanaokulia mtaani kuwa na maisha ya kawaida”

“Nakubaliana na wewe , Vituo vya kulelea Yatima ni njia nzuri kimalezi kwa Yatima kuliko mtaani ambako watoto hujenga tabia za ajabu , lakini vipi kama wale wamiliki wa vituo wakiwa na ajenda nyingine juu ya watoto hao?”

“Unamaanisha ajenda gani kwa mfano?”Aliuliza Regina lakini muda huo waliletewa chakula chao na kumfanya Regina kukikagua.

“Sipendi vitunguu vya hivi mimi?”Aliongea Regina mara baada ya kuangalia namna samaki alivyopikwa kwa kuungwa na Scallion(Vitunguu vya kijani).

“Hio ndio Recipe sasa inafanya samaki walioungwa na Scallion kuwa watamu, inakuwaje hupendi vitunguu vya kijani wakati ni vizuri zaidi kuliko vitunguu aina ya Bombay, kama vipi niongee na watu wa jikoni wakubadilishie”

“Acha tu , hata Shangazi anavipenda kweli .. halafu mbona unaongea kwa kukunja sura hivyo kama unanifokea”

“Nimekufokea saa ngapi wakati nilikuwa nikikuelezea faida yake , au ndio umechukia kukuchagulia chakula chenye viungo usivyopenda”

‘Sijamaanisha hivyo , ila tu sipendi harufu ya hivi vitunguu”

“Mh, inaonekana Shangazi anafanya juhudi kubwa kukuridhisha na chakula anachopika”Aliongea Hamza huku akichezesha vidole.

“Haikuhusu , nitakula hizi chipsi tu , hao samaki kula wote mwenyewe”Aliongea kibishi na kumfanya Hamza aishie kutabasamu kutokana na ujeuri wa Regina.

“Angalau leo kwa mara ya kwanza na ya mwisho tunakula nje pamoja japo hatujakuwa pamoja kwa muda mrefu”

“Unataka kusema nini?”Aliongea Regina huku akimwangalia Hamza maana ni kama amekuwa siriasi ghafla tu.

“Namaanisha baada ya kutoka hapa kila mtu ataelekea uelekeo wake”Aliongea Hamza na kumfanya Regina aliekuwa akichoma chipsi na uma kusita na kumwangalia Hamza usoni na ukimya ulimvaa ghafla.

“Umesema unakuja hapa ili kuniambia kilichotokea na wewe ni nani lakini mwishowe naona unataka tuachane”.

“Hatuachani kwasababu uhusiano wetu ni feki , tunachokwenda kufanya ni kusitisha tu mkataba wa kazi na kila mtu kuendelea na maisha yake kama ilivyokuwa”Aliongea.

******

Upande mwingine katika makao makuu ya kitengo cha usalama wa taifa kinachodili na nguvu sizizoonekana kifahamikacho kwa jina la MALIBU kulikuwa na kikao kilichohusisha watu watatu , mmoja akiwa ni Kanali Msuya ambae ni mkuu msaidii wa kitengo hicho, Kapteni Kwavava na Afande Mdudu.

Wote macho yao yalikuwa kwenye skrini wakiangalia wanajeshi ambao walikuwa eneo la tukio.

“Afande wote wamepoteza maisha , hakuna hata mmoja ambae yupo hai, vifo vyao ni vya kikatili mno”sauti kupitia simu ya upepo ilisikika , simu ambayo ilikuwa imeshikwa na Afande Mdudu

Afande Msuya na Afande Kwavava waliangalia kwa mshangao na macho yao yalijaa maswali.

“Inawezekana vipi , au taarifa tulizopokea zilikuwa hazina ukweli wowote?”Aliuliza Afande Msuya.

“Sidhani kama hazikuwa na ukweli , intellijensia ile ilikuwa ni sahihi kabisa Afande”

“Kwahio inamaanisha aliehusika na vifo vyao anaweza kuwa na uwezo wa juu kuliko wao?”Aliuliza na Afande Kwavava aliishia kutingisha kichwa.

“Afande Kiduma hakikisha mnapiga picha ya tukio zima na majeraha yao ili kufanyiwa uchunguzi wa kina”Aliongea Afande Mdudu.

“Sawa Afande”

“Hakikisha hili swala linabakia siri mpaka tupate ufumbuzi wa kila kitu kilichotokea”Aliongea Kanali Msuya na Afande Mdudu alipiga saluti na kisha akakaa chini.

“Mnadhani kuna kitu gani tunamisi?”Aliuliza Afande Msuya.

“Kwanini Afande?”

“Hawa wahalifu wameingia nchini kwa zaidi ya wiki mbili zote , lakini kitengo chetu kimejua taarrifa ya uwepo wao leo hii na ndio siku wamepoteza maisha wote, mnadhani hakuna kilichokosekana katika mfumo wetu wa intellijensia?”

“Mkurugenzi , unachoongea ni sahihi kuna kitu tunamisi , lakini nadhani hii haimaanishi kitengo chetu uwezo wake ni mdogo , ni swala la kuzidiwa kitaalamu tu na kama ilivyokuwa siku zote ndio namna tunavyochukulia kama changamoto ya kujioboresha zaidi”Aliongea Kwavava.

“Hiki ni kipindi ambacho vitengo vyetu vya usalama lazima viwe katika ubora wake hasa likija swala la kukusanya intellijensia , Uchaguzi mkuu unakaribia , kosa kidogo tu usalama wa taifa unaweza kuwa hatarini , Wahalifu hatari namna hii wanaingia nchini , lakini tumeshindwa kuwadaka katika lada zetu za usalama , mtu wa nje anatupenyezea taarifa na vikosi vyetu vinakuta wamepoteza maisha wote , Nani mhusika wa tukio hili la kutisha hata pa kuanzia hatuna”

“Kwa uchunguzi wa awali wa Afande Kiduma anasema Gonzo Fisheries ndio wamiliki wa Ghala, nimeongea na Mzee Sinzwe hana taarifa ya kukodishwa kwa ghala lake”

“Inamaanisha vijana wake ndio wamekodisha ghala hilo , kama ni hivyo basi lilikodishwa kwa muda mfupi tu”

“Ndio na kwasasa wote wapo baharini wanavua hivyo imekuwa ngumu kupata taarifa ya kilichotokea”Aliongea Afande Mdudu.

“Afande kwa taarifa niliozokuwa nazo juu ya hili kundi , wanajiita Waray Bounty hunters , jina lao la utani ni Tumbili wenye mbawa za Tai , ukiachana na sifa zao za kimafia na umahili wa kutafuta watu lakini pia wanahusishwa kutokea Biringan”Aliongea Afande Mdudu.

“Unataka kumaanisha nini Mdudu?”

“Kama inavyosemwa ni kweli wanatokea Biringan basi sio watu wa kawaida , sijui kama mnajua hili ila Biringan ni eneo ambalo halipo kwenye ramani ya dunia zaidi ya hadithi za kiimani tu , pointi yangu kama watu wa aina hii wamefika Tanzania kwa ajili ya kutafuta kitu , basi moja kwa moja mpango wao umefeli na kuna uwezekano watarudi wengine”

“Mdudu unapendekeza nini?”Aliongea Afande Kwavava.

“Lazima tujue kwanza ni kipi ambacho wamekijia hapa Tanzania”

“Nadhanni tunarudi palepale tu , katika uchunguzi wetu tunachotaka kujua ni nani ambae amehusika kuwaua na ikitokea tumemfahamu basi ni dhahiri huyo ndio wanaemtaka hivyo tutaweza kupata majibu”

“Kwavava mkuu wako Dastani ana shida gani siku hizi , kwanini amekuwa bize sana , mpaka kwenye vikao muhimu kama hivi anakosekana?”

“Amekuwa akiwafatilia wale Wabrazili kwa muda mrefu , nadhani ndio kinachomfanya kuwa bize”Aliongea na Afande Msuya alionekana kutoridhika.

“Dastani ndio mtu ambae ana utashi mkubwa wa mambo kama haya , wasiliana nae na umshirikishe huu uchunguzi nahitaji majibu ya haraka”

“Sawa Afande”

“Kwavava kaa na timu yako ya intellijensia , nahitaji ripoti kamili kwanini idara yetu inazidi kuwa butu siku hadi siku na kushindwa kunusa hatari kwa haraka”

“Sawa Afande”

“Hakikisheni pia tunajua nani kapenyeza taarifa ya uwepo wa hawa wahalifu nchini kwetu , tunaweza kupata pa kuanzia”Aliongea na kisha alisimama.

“Afande kuna taarifa pia nahitaji kuripoti”

“Jnahusu nini?”

“Amosi ameshambuliwa na risasi , yupo mahututi hospitali ya jeshi?”Aliongea Mdudu na ilimfanya Afande Msuya kushangaa kidogo.

“Amosi si alikuwa chini ya Kanali Dastani , kwanini unaripoti wewe hii taarifa”

“Msemakweli katika kampeni zake ameendelea kuituhumu kushirikiana na Binamu , nadhani inafahamika ndani ya kitengo Amosi ameshawahi kufanya kazi kama undercover Agent kwa ajili ya kuwachunguza Binamu”Afande Msuya alijikuta akirudi kwenye Sofa na kuketi huku akionekana kuwaza kidogo.

“Kuna uwezekano Binamu ndio walimshambulia , lakini kwasasa hakuna uhakika kwani Amosi bado fahamu hazijamrudia, nina uhakika hili ndio sababu ya Kanali kutokuonekana katika vikao vyote leo, ila kama kweli ni Binamu basi watahakikisha wanaona kifo chake”

“Mtafute Kanali popote alipo , kesho afike katika ofisi yangu na ulinzi uimarishwe katika wodi ya Amosi , tutahitaji maelezo kutoka kwake”Aliongea na maagizo yale alipewa Mdudu na alitoa saluti na kisha akatoka nje.

“Anachosema Msemakweli sio uongo , lakini hili swala linachukua sura mpya , kumekuwa na mijadala mingi mtandaoni , inayozusha kile kinachoendelea mtandaoni , wengine wanadai Night Shadows wapo chini ya Binamu”Aliongea Afande Kwavava.

“Kwavava hivi unaamini hawa Night Shadows wapo kama watu wanavyozusha?”

“Kitengo chetu kimekuwa kikifanya uchunguzi kwa muda mrefu , lakini hatujafanikiwa kupata ushahidi wa moja kwa moja wa kuamini, maoni yangu ni aidha wapo kweli kama watu wanavyosema au kuna kundi la watu wanajaribu kujaza watu hofu”

“Sio sisi tu ambao tunawafuatilia hawa Nightshadows, serikali zote kubwa wanafatilia hili lakini hakuna ushahidi unaotolewa, inanifanya mwisho wa siku kuamini ni uzushi pia”.

“Lakini Afande una uhakika gani kama serikali kubwa duniani hawana ushahidi , vipi kama jambo hili wanalifanya kuwa siri kama ilivyotokea kwa tukio lililopita?”

“Kwasasa ni ngumu kwangu kuweka neno lolote kuhusu hili , isitoshe tunatarajia serikali mpya hivi karibuni , nadhani tulipe muda kwanza, Kwavava nadhani unajua ninachomaanisha”

“Ndio Afande”.

ITAENDELEA
jiunge nasi kwenye grupu kuendelea kupata mwendelezo kwa spidi ya 5G NAMBA 0687151346
 
Back
Top Bottom