singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
- #1,041
SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU.
Mara baada ya Yonesi kusikia kauli hiyo, mwili wake ulitetemeka kwa sekunde kadhaa. Haraka aligeuza kichwa chake pembeni na kuziba uso wake kwa mikono miwili. Moyo ulikuwa ukienda mbio mno.
“Haha, Yonesi jana uliniuliza swali kwa ujasiri mno, kwanini sasa unakuwa na aibu hivyo?”
Yonesi alijikuta akivuta pumzi mara mbili. Hakuwa tayari kushindwa tena. Aligeuka na kumtazama Hamza akiwa na ujasiri.
“Unaongea ujinga, nani anaona aibu?” Aliongea, na Hamza akaona hakuna haja ya kuendelea kumchokoza.
“Okey okey, ni kweli huna aibu, basi chukua kwanza upate chochote uchangamshe tumbo, safari ndefu hii.” Aliongea Hamza, na kumfanya Yonesi kumkodolea macho, asijue mwanaume huyo anafikiria nini.
Hata chakula alipokea kimya kimya na kuendelea kula taratibu, akiendelea kuwaza.
“Hivi vidude ni vitamu mno lakini wanauza ghali…” Aliongea Hamza huku akitafuna.
Yonesi hakuona utamu wowote. Moyo wake muda huo ulikuwa umefumbwa na hisia mchanganyiko, na kumfanya kuona kama alikuwa ndotoni.
“Yonesi, unawaza nini? Mbona umekodoa macho hivyo?”
“Ni kweli unaenda nyumbani kwetu?”
“Ndio, si nishakwambia? Kama siendi kwenu kwanini nipande treni?”
“Lakini unaenda kuwaambia nini wazazi wangu? Mkurugenzi anajua unasafiri?” Aliuliza akiwa na wasiwasi mkubwa.
“Hata sijali kuhusu hilo, ninachojua nakupenda. Ijapokuwa sijui ni kwa kiasi gani, lakini siwezi kukuona ukiolewa na Mdudu.”
“Huoni kama unafanya mambo kwa kukurupuka? Ijapokuwa familia yetu si kama nyingine kubwa, lakini haimaanishi wataweza kuingilika kirahisi. Isitoshe, kama Mkurugenzi akisikia kuhusu hili atakasirika mno.”
“Hata kama familia yenu ingekuwa ya raisi, hakuna wa kunizuia. Kama familia yenu ni ya kawaida kwanini wanizuie? Kuhusu mke wangu, hilo niachie mimi. Nitajua namna ya kumbembeleza. Nikichanganywa na mwanamke mmoja kama mwanaume nitaishi vipi?”
“Wewe, aisee unajua kukurupuka kweli,” aliongea Yonesi, akikosa neno.
“Hehe… mwenzako Eliza jana kasema kanipendea kwa sababu ya kukurupuka kwangu, wewe unaonaje?”
“Kwahiyo jana ulikuwa na Da’ Eliza?”
“Ndio, nimetokea kwake asubuhi ya leo na kuja moja kwa moja stesheni.”
Yonesi alijikuta akituliza hisia na kujiambia kweli huyu playboy ameshindikana. Hata hivyo, alikuwa katika hali ya kupaniki maana alishindwa kujua ni kitu gani Hamza anapanga kufanya wakifika nyumbani.
Saa sita kasoro ndio muda walioweza kufika stesheni kuu ya treni Dodoma, na wakati wakiwa wanatoka waliweza kumuona mwanaume mzee wa makamo akiwa amesimama pamoja na wanaume wengine wawili waliovalia mavazi ya suti.
“Yonesi, hatimaye nakuona tena,” mwanaume yule aliyevalia suti ya kijivu aliongea kwa uchangamfu.
Yonesi, mara baada ya kumuona mzee huyo, na yeye pia alitabasamu na kumsogelea kumsalimia kwa furaha.
“Mjomba Sauli, unaendeleaje?” Aliuliza Yonesi, lakini swali lake lilikuwa la kijinga sana kutokana na kwamba mzee huyo alikuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi katika levo ya mzunguko kamili, maana yake umri wake wa kuishi ni mkubwa na si rahisi kuumwa kirahisi.
Hamza, mara baada ya kuona mzee huyo ndiye aliyekuja kumpokea Yonesi, aliona kweli familia ya Yonesi ilikuwa ya kijeshi na kichifu.
Kuna muda Hamza mwenyewe alikuwa akijiuliza , katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi Tanzania haikuwa na muda mrefu sana tokea ipate ufahamu wa mafunzo haya , lakini kulikuwa na wazee wengi ambao walionekana kuwa na mafunzo hayo muda mrefu sana na kujiuliza wametokea wapi.
Mzee Sauli hakuwa mwanajeshi wa moja kwa moja , alikuwa ni wazee tu waliochipukia katika familia ya Chifu Mazengo na kupewa kazi ya ulinzi na kusimamia kazi zote za familia , kama ni wazungu wangempa cheo cha Buttler.
“Unaonekana kukua kiasi chake Yonesi”Aliongea huku akichunguza mwili wa Yonesi na aliweza kuhisi amekuwa tofauti , ijapokuwa hakujua ni mafunzo gani lakini aliweza kuona utofauti hasa upande wa ukomavu wake wa kiakili.
Yote hayo yalikuwa ni mafunzo ya Hamza aliomwelekeza Yonesi kutumia.
Muda uleule yule mzee aliinua uso wake na kumwangalia Hamza . Alikuwa ameishi maisha marefu sana ndani na nje ya Tanzania na kuona watu wengi wa kawaida na wasiokuwa wa kawaida , lakini kitendo cha macho yake kutua kwa Hamza aliweza kugundua sio mtu wa kawaida palepale.
“Bwana mdogo , Yonesi ni rafiki yako?”
“Haha.. wewe endio Mzee Sauli si ndio , wakati tukiwa njiani Yonesi alikuwa akinielezea habari zako na anasema wewe ndie uliekuwa ukimpenda sana , wakati akiwa mdogo wazazi wake wakimfokea alikuja kwako kukulalamikia,. Mimi kama mpenzi wa Yonesi nichukue fursa hii kukushukuru kwa kumjali kwa wakati wote mpenzi wangu”Aliongea Hamza huku akiwa amemshika mkono yule mzee na matendo yake yalimfanya Mzee Sauli kuwa katika mshangao.
Yonesi alishindwa kuona namna uso wake umeiva , hakujua Hamza atakuwa spidi spidi kwenye kujitambulisha mapema kama mpenzi wake kama hivyo.
“Wewe.. kwahio ndio mpenzi wa Yonesi?”Aliuliza kwa shauku lakini kwa wakati mmoja akiwa katika hali ya wasiwasi.
“Mjomba tuondoke kwanza , ni stori ndefu”Aliongea Yonesi akiingilia maongezi.
Mzee Yule aliishia kuvuta pumzi na kuzishusha , alikuwa kama mtu ambae ametegemea kuna jambo kubwa litatokea wakati wa sherehe ya Mzee Chalula.
Maisha aliokuwa akiishi Yonesi Dar pamoja na kazi yake utadhania hakuwa wa kishua , familia yake ni moja ya familia tajiri sana ndani ya mji wa Dodoma na yenye historia yenye mizizi mirefu.
Baada ya kutoka nje kabisa waliingai katika Mercedenz Benz nyeusi na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwao.
Wakiwa njiani kuelekea huko Yonesi alipewa taarifa kwamba , familia ya Mdudu wapo nyumbani na wamekusanyika wengi wa ukoo wao wakiamini kabisa hatimae ile siku ya kuunganisha familia hizo mbili imewadia .
Kutokana na taarifa hio , Yonesi alizidi kushikwa na wasiwasi mkubwa mno , upande wa Hamza yeye hakuwa na wasiwasi kabisa , macho yake yote yalikuwa nje akiangalia mazingira na alikuwa akiuliza maswali yaliokuwa nje kabisa ya mada.
Mzee huyo aliishia kumwangalia Hamza na kuona hakuwa na uwezo kabisa wa kujua ni kitu gani kinamfanya Hamza kujiamini na kutokana na mwonekano huo alizidi kuona sio mtu wa kawaida.
Ukweli ni kwamba kama familia ya Mzee Chalula wangetumia koneksheni yao kutaka kumjua Hamza kupitia kitengo cha Malibu , wangeweza kujua swala la kisiwani Chole , lakini kwa bahati mbaya swala la kisiwani kule lilikuwa ni siri sana na ni watu wachache sna ndani ya vitengo cya usalama walikuwa wakilifahamu.
Baada ya nusu saa gari kutembea , hatimae gari iliingia katika mtaa maarufu wa Kwa Chifu Mazengo au Mvumi Makulu, sehemu hio ilikuwa ikiitwa kwa Chalula kutokana na kwamba Mzee Chalula ndio mtu wa kwanza kabisa kujenga hapo na baadae serikali ilifanyia eneo hilo marekebisho na kuita Mji mpya lakini hata hivyo pamezoeleka zaidi kama Kwa Chifu Chalula wa Mazengo.
Nyumbani kwa Yonesi kulikuwa kumezungukwa na miti mingi na uoto wake ulikuwa ni ule wa kupandwa na sio wa asili kutokana na maeneo mengi kutofautiana na eneo hilo.
Baada ya kushuka katika megesho maalumu , kulikuwa na magari mengi yaliokuwa ndani ya eneo hilo tayari na mengi yalikuwa ni V8 na Prado.
Mandhari ya eneo hilo yalimfurahisha Hamza, na akajiambia angalau watu wa mkoani walikuwa wakiishi vizuri, ijapokuwa nyumba zilizokuwa ndani ya eneo hilo zilikuwa na muundo wa kikale, lakini mazingira yake hayakuwa mabaya.
"Yonesi, babu yako, baba yako na mama wapo kule nyuma. Nikupeleke kwanza chumbani kwako ukabadili mavazi au unaelekea moja kwa moja kuwasalimia?" aliuliza mjomba.
"Haina haja ya kubadili. Mjomba, naomba uniitie mtu kunisaidia kubeba mabegi yangu, nitaenda kusalimiana nao kwanza," aliongea Yonesi na kisha alimgeukia Hamza.
"Mpango wako ni upi?" Aliuliza Yonesi, akimwangalia Hamza.
"Na mimi naenda kuwasalimia na pia kuwaelezea swala letu kwa familia yako," alijibu Hamza akiwa na tabasamu, lakini Yonesi alionyesha ishara ya kutaka kumzuia.
"Acha wasiwasi, tunaenda pamoja. Huwezi kunizuia hivyo, ni bora ukaanza kujiamini kuanzia hapa," alisema Hamza.
"Basi usiwe mkali sana, mama yangu afya yake si nzuri sana, akishikwa na hasira anaweza kupandwa na presha," alisema Yonesi, na Hamza alitikisa kichwa kukubaliana naye.
Staili ya ujenzi wa eneo hilo ilikuwa ya kizamani sana. Japo nyumba zilikuwa nzuri, upangiliaji wake ulifanya ionekane kama kituo cha afya.
Baada ya kuingia kwenye korido ndefu iliyojitegemea, walipita bustani kadhaa zilizotengenezwa vizuri, na hatimaye wakaingia kwenye uwanja mdogo uliokuwa umepandwa mizambarau.
Njiani, baadhi ya wafanyakazi waliomwona Yonesi na Hamza waliishia kumwangalia kwa kumshangaa na kumsalimia kwa wakati mmoja.
Baada ya kuzunguka hadi nyuma, hatimaye waliweza kufika kwenye ukumbi mmoja uliokuwa umejengwa kwa makuti, na kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakiongea na kucheka kwa sauti, hali iliyofanya eneo hilo kuwa la furaha na kuchangamka.
Kadri walivyokuwa wakisogelea eneo hilo, ndivyo Yonesi alivyozidi kujawa na wasiwasi. Aliishia kujikaza kijeshi na kufanya hatua zake zionekane kama mtu anayejiamini.
Mbele kabisa, kulikuwa na mzee mtu mzima kabisa aliyevalia koti kubwa la manyoya la kitamaduini kabila la wagogo na kofia kichwani. Huyu alikuwa babu yake Yonesi. Ijapokuwa mwonekano wake ulikuwa wa kizee, macho yake yalionekana kuona vizuri kabisa.
Upande wa kulia kwake kulikuwa na mwanaume mwingine wa makamo, aliyevalia kombati za kijeshi za cheo cha Meja Jenerali. Huyu alikuwa baba yake Yonesi, Afande Daudi Chalula. Pembeni yake kulikuwa na mwanamke mwenye mwonekano wa kitajiri, maarufu kama Mama Danny. Huyu ndiye mama mzazi wa Yonesi.
Kulikuwa na wanaume wengine waliokuwa katika mavazi ya kijeshi, karibu wengi wakiwa na vyeo vya nyota tatu na ngao, na ilionekana walikuwa ni ndugu wa Yonesi.
Hata hivyo, waliokuwa wakimpa wasiwasi zaidi Yonesi ni watu waliokuwa wamekaa upande wa kushoto, upande wa wageni, wakiongozwa na Afande Mdudu na wazee wachache wa ukoo wake. Macho yao yote yalikuwa kwa Yonesi kama kwamba ndiye mtu pekee waliyekuwa wakimsubiria.
"Yonesi!" Mama Danny, mara baada ya macho yake kutua kwa Yonesi, aliinuka na kumkimbilia, akamkumbatia kwa hisia kubwa.
Yonesi alikuwa amemmisi sana mama yake. Alimwangalia na kuona alikuwa amezeeka mno, na alishindwa kujizuia kushikwa na hatia, akatoa chozi.
Unaweza ukashangaa kwa nini mzazi huyo asingesafiri kuja mpaka Dar kumuona mtoto wake kama alikuwa amemmisi sana, lakini baada ya Yonesi kutoroka nyumbani akiikimbia ndoa baada ya kufeli mafunzo nchini Chile, baba yake, Meja jenerali Daudi, alipiga marufuku familia nzima kutomtafuta Yonesi, ikiwemo mke wake.
"Hamza!" Afande Mdudu aliita mara baada ya kumuona, huku uso wake ukifubaa.
"Mdudu, unamfahamu yule kijana?" wazee wa familia yake waliuliza.
"Mjomba, yule ndiye Hamza, ndiye mtu anayefahamiana na mshauri mkuu na kuniambia nisimsumbue tena Yonesi," aliongea Mdudu, huku akionyesha kuwa bado alikuwa na hasira na Hamza.
Mdudu, tokea amkose Yonesi kwa kupewa vitisho na Hamza, aliomba kuacha jeshi na kujiingiza katika siasa. Alikuwa ni mjukuu wa kwanza Chifu Mirambo. Mjomba wake Imani alikuwa ni moja ya viongozi wa juu wa serikali akiwa amehudumu kama Waziri wa ulinzi chini ya Rais Mbilu. Ijapokuwa kwa wakati huo alikuwa mbunge tu baada ya kushinda uchaguzi, lakini alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa katika nafasi za juu za kuteuliwa uwaziri katika serikali mpya.
Baada ya Imani kusikia kwamba Hamza ndiye aliyeingilia swala la ndoa ya Mdudu na Yonesi, alijikuta hakuridhishwa na hali hiyo.
"Jenerali, kwa nini huyu mtu amekuja hapa? Kuonekana kwake katika familia yako si kama kutudharau?" aliuliza Mrambo kwa hasira, huku akipiga meza.
“Yonesi sogea hapa haraka na umwambie babu yako nini kinaendelea , huyo uliekuja nae ni nani?”
Yonesi ilibidi aachiane na mama yake na kisha alienda mpaka walipo wazee na kisha kuanza kusalimia
“Anaitwa Hamza ni ra…”
“Yonesi ni mpenzi wangu”Hamza alisogea haraka na kuongea.
Mara baada ya kusikia kauli hio watu wote katika ukumbi huo walijikuta wakishikwa na mshangao . Yonesi aliishia kukunja ngumi tu huku mikono yake ikishikwa na jasho kwa wasiwasi.
“Mzee Chalula , nini kinaendelea , Hawa watoto si ndio waliosema wenyewe wanakwenda kusahau yaliopita na kukubali kuchumbiana? Mdudu mwenyewe amekubali kuacha yaliopita na yupo hiari kumuoa mjukuu wako , Au hii inamaanisha familia yenu haijawahi kuchukulia hili suala kwa uzito wake ndio maana mnaenda mbali hivi?”Aliongea Mirambo kwa hasira huku akipiga meza.
“Mzee Mrambo punguza jazba , Familia yetu imekuwa na taswira nzuri kwa muda mrefu . Kama binti yangu amekosea , nipo tayari kuomba radhi”Aliongea Afande Daudi na kisha akamgeukia binti yake.
"Yonesi, hebu tuambie kama alichoongea huyu kijana ni kweli," aliuliza, na Yonesi aliishia kukaa kimya, akiwa ameinamisha kichwa chake chini, akishindwa kukubali. Isitoshe, Hamza hakuwahi kumtongoza vizuri na kumkubali.
Mama Danny wasiwasi ulimshika kutokana na kubadilika kwa hali ya hewa na alimshika mkono binti yake.
“Yonesi ongea , Kwanini ghafla tu umekuja na mpenzi?”
“Mama ni .. nampenda Hamza”Baada ya kusita aliishia kung’ata meno kuutafuta ujasiri na hatimae akafanikiwa kuongea.
Maneno hayo baada ya kumtoka kila mtu aliekuwa katika ukumbi huo alipiga kimya .
Hamza kwa upande wake alifurahishwa na kauli hio mno na palepale kwa kujiamini alisogea mbele na kusimama kando ya Yonesi.
“Wazee wangu kwanza naomba niwape salamu wote , nadhani wachache wananijua kwa kuniona na kunisikia , kwa wale wasionijua kwa jina naitwa Hamza Mzee na kwa mpangilio wa kinachoendelea hapa nadhani litakuwa jambo la busara kama mipango ya ndoa ikibadilika kidogo . Kutoka mwanzo mpaka mwisho , hakuna mmoja wenu aliemuuliza Yonesi kama anampenda Mdudu , kwa mantiki hii naona kabisa hatua muhimu imerukwa, Karne za kumtafutia mtoto wa kumuoa ama kuolewa nae zishapitwa na wakati, Au mnasemaje wazee wangu?”
Mdudu mara baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Hamza ni kama alikuwa akisiliza matusi na alishindwa kujizuia na kusimama.l
“Hamza acha kutumia ubabe kupata kila unachotaka ! Wewe tayari umeoa na mke wako anajulikana ni Regina mmiliki wa makampuni ya Dosam , unadhani sijakufanyia uchunguzi , inamaana unataka kumgeuza Yonesi Mchepuko?”
Maneno ya Mdudu yalikuwa ni kama bomu lingine lilowaangukia wazee hao na kusababisha kila ndugu wa Yonesi sura kukunja kama wamelishwa pilipili. Yonesi aliishia kutetemeka asijue ni kipi anaweza kufanya
“Kama unadhani hiyo ni pointi sana, basi nitaanza mchakato wa kubadilisha uraia na kuchagua taifa ambalo linaruhusu mwanaume kuoa wanawake wengi, kwanza nina jina la kiislamu unasemaje hapo” aliongea Hamza.
“Wewe…” Mdudu alijikuta akishangazwa na kauli ya Hamza maana hakuitegemea. Katika maisha yake hakuwahi kuona mtu aliyekosa aibu kama Hamza.
“Kikubwa ni kwamba nampenda Yonesi, na yeye pia ananipenda, na tuna furaha kuwa pamoja iwe nimeoa ama sijaoa, na hakuna cha kufanya juu ya hili.”
“Wewe mwanaharamu usiye na heshima mbele ya wazee. Unadhani tunaweza kuendelea kuvumilia kejeli zako kwa sababu tu unajuana na Mshauri Mkuu. Mdudu anaweza kuwa mdogo na kuhofia kitengo cha Malibu, lakini mimi, Mzee Imani Mirambo, sijawahi kuogopa mtu.” Mara baada ya kuongea kauli hiyo, aligeuza macho yake na kuwaangalia ndugu wa familia ya Chalula.
“Mzee Chalula, Jenerali, naona binti yenu ni mkanuni mno. Yaani juzi amekubali, na leo anaenda kinyume na maneno yake bila hata kutupa taarifa. Tumeishia kuja tu hapa kupoteza muda wetu. Kaka akisikia hili naamini anaweza akaghairi kumsindikiza mkuu wa nchi na kuja hapa mwenyewe. Sijategemea swala kama hili kutokea hapa leo hii, ni kwa bahati nzuri kaka hajaja mwenyewe, la sivyo asingezikubali hizi dharau. Mimi, mzee Imani Mirambo, nishaongea yangu na inatosha, lakini niwahakikishie kuanzia leo na kuendelea mmejitengenezea uadui na familia yetu na hakuna rangi mtaacha kuona.”
Mara baada ya kusikia maneno hayo, ndugu wote wa familia ya Yonesi walijikuta wakianza kupaniki. Likija swala la ushawishi, familia yao ilikuwa ndogo sana kulinganisha na familia ya Mirambo.
“Mzee Mirambo, tuliza jazba na ukae chini tuongee! Unajua binti yangu ni mwenye masihala mengi, alichoongea ni maamuzi ya kukurupuka na sio sahihi, nadhani hata wewe mwenyewe unajua?”
“Jenerali, tushaongea hili na tumemaliza. Ni juu ya kuamini ama kutokuamini, lakini nikuhakikishie uwepo wangu hapa, familia ya Mirambo haiwezi kuwafanya chochote,” aliongea Hamza.
Jenerali Daudi alikuwa na hasira mno kiasi kwamba macho yalishaanza kuwa mekundu.
“Kaa kimya na ondoa mikono yako kwenye mwili wa binti yangu,” alifoka, na Hamza aliishia kushangaa kidogo. Pale pale alitoa mikono yake akiwa na haya usoni, aliona ilikuwa sio sahihi kumshika Yonesi kiuno mbele ya wazazi wake.
“Ondoka! Hatutaki kukukaribisha katika familia yetu,” aliendelea kufoka Meja Jenerali.
“Baba, usiwe hivi. Huelewi tu, lakini Hamza amenisaidia sana…”
“Kaa kimya na wewe! Tumekupigia simu na kukueleza, ukasema umekubali, na sasa hivi unaanza kumtetea huyu mshenzi mwenzako?”
“Lakini baba, sikusema kabisa kama nimekubali kuolewa na Mdudu. Nilisema nitafikiria, lakini sio kukubali. Nimekaa na kuona siwezi kuolewa na mwanaume ambaye simpendi, ni sawa na kujifunga kwenye gereza la hisia zangu mwenyewe.”
Mdudu, mara baada ya kusikia kauli hiyo, uso wake uliiva kwa hasira, na aliishia kusimama na kumwangalia Yonesi kwa macho makali.
“Yonesi, unaongea nini wewe? Kwahiyo unadhani wewe ndio mwanamke pekee ninaweza kuoa? Nimekuchagua wewe kwa sababu nimeona unafaa kuwa mke wangu, lakini unapata ujasiri wa kusema hunipendi?”
Maneno hayo mara baada ya kuwafikia ndugu wa familia ya Yonesi, waliishia kukunja sura, lakini hakuna aliyeweza kusimama na kuongea. Ni mama yake Yonesi pekee aliyepata ujasiri wa kusimama na kuongea.
“Mdudu, kwa nini unaongea hivyo wewe mtoto? Hata kama alichoongea binti yangu kinauma, lakini ana kosa gani kuchagua mtu anayempenda na kua nae?”
Mama huyo mara baada ya kuongea hivyo, Mdudu palepale alijikuta akiona haya baada ya kuona amekosea.
“Mama , naomba usikasirike kwa kunielewa vibaya. Ni kutokana na kuchanganyikiwa. Nimempenda sana Yonesi kwa muda mrefu, ndio maana nimekuja tena kumchumbia, lakini hiki kinachotokea…” Alijikuta akitingisha kichwa.
Mzee Mirambo aliishia kumwangalia mdogo wake, na palepale alimkodolea macho Hamza.
“Wewe mwanaharamu, hivi unadhani ndoa kati ya familia ya Mirambo na Mazengo ni mchezo wa kitoto eh? Unaweza kuingilia utakavyo na kuuharibu? Tayari una mke lakini bado unapata ujasiri wa kuja hapa kujitambulisha kama mpenzi wa binti wa Mzee Daudi. Kama ningekuwa wewe, ningeshikwa na aibu na nisingepata huo ujasiri. Lakini kwa ulichokifanya, umeonyesha ni kwa jinsi gani umekosa aibu,” aliongea kwa hisia kubwa sana. Maneno yale yalimwingia vizuri Afande Daudi, na palepale aliwaangalia walinzi wake.
“Njooni mumchukue, mkamtupe nje huyu mwanaharamu hatumtaqki hapa,” aliongea, na palepale walinzi wa familia hiyo wapatao nane walikimbia kuja eneo hilo. Wote walionekana kuwa na mafunzo makali na ilionyesha walikuwa ni wanajeshi wakakamavu.
SEHEMU YA 150.
Mara baada ya kuona wale walinzi wanataka kumshambulia ,Yonesi haraka sana aliingilia.
“Baba, usifanye hivyo”
“Kaa kimya na nenda kwenye chumba chako , huruhusiwi kutoka”Alifoka
Yonesi alikuwa na wasiwasi mno , hakuwa na wasiwasi juu ya Hamza bali alikuwa akiwaonea huruma hao walinzi waliotaka kumshika Hamza.
Wale walinzi hata hawakuelewa na palepale walimshika Hamza mkono wakitaka kumuweka chini ya ulinzi.
Lakini sasa kadri walivyokuwa wakijaribu kumvuta Hamza , hawakuweza kumsogeza hata inchi , licha ya kutumia nguvu zao karibia zote.Hamza alikuwa amesimama kama sanamu tu akiwa anawaangalia wanavyohangaika.
Sura za ndugu wote wa Yonesi zilifubaa. Walinzi hao walikuwa na mafunzo na mazoezi makali mno na baadhi yao walikuwa wakijifunza kuvuna nishati za mbingu na ardhi pia.Lakini kitendo cha kushindwa hata kumsogeza kidogo Hamza kiliwashangaza mno.
“Jenerali haina haja ya mimi kuondolewa hapa , nimekuja kwa ajili ya kumpongeza Babu Chalula kwa kutimiza miaka tisini , ndio maana nimeona pia kuwa muwazi juu ya uhusiano wangu na Yonesi , najua hili ni swala gumu kwako kukubali kama mzazi , lakini kulingana na historia ninavyoijua nyie kama warithi wa moja kwa moja wa Chief Mazengo familia yenu ni kubwa kuliko hata ya Mirambo , tukikaa chini na kuongea nina uhakika tunaweza kukubaliana”Aliongea Hamza.
“Kukaa chini na kuognea? Unataka kuongea na sisi nini?”
“Namaanisha unaweza kuweka masharti yako na nitaangalia namna ya kuyatimiza na kisha uniruhusu niondoke na Yonesi , nipo tayari kufanya chochote utakachoongea”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu lakini dakika hio hio mzee Mirambo aliingilia
“Haina haja ya kuendelea kuongea nae , huyu kijana anaona kujiamini kwake anaweza kudharau kila mtu aliekuwepo hapa na tukamsikiliza tu , Jenerali kama familia yako imeshindwa kumuondoa hapa familia yangu ipo tayari”
Mara baada ya kuongea hivyo aligeuka na kumwangalia mwanaume aliekuwa na sura ngumu alievalia koti la leather na miwani ya jua , alikuwa siriasi mno na alama ya kovu la upanga kwenye sura yake lilikuwa waziwazi kabisa.
“Nino hebu mfundishe huyu mpuuzi namna ya kuwa na adabu mbele ya wakubwa”
Yule bwana aliefahamika kwa jina la Nino macho yake yalionekana kuungua kwa tamaa , alionekana kama vile alitamani sana kupambana na Hamza hasa baada ya kuona wale walinzi kushindwa kumsogeza kabisa.
“Bosi wewe ndio ulietoa maagizo , mimi ni nani hata niyakatae , nayapokea kwa mikono yote miwili”Mara baada ya kusikia kauli hio ya mlinzi wa Mzee Mirambo ndugu wa Yonesi wote waliishia kukunja sura
“Mzee Mirambo hata kama unataka kumuondoa hapa huyu mtu , ila ni kheri sisi familia tukihusika katika hili na sio mtu wako maana nyie wote ni wageni”
“Unaongea nini wakati vijana wako wameshindwa hata kumsukuma , kama unahofhia uwezo wa Nino ondoa mashaka kabisa , maana ndio kinara kwenye kambi yake ya mafunzo na juzi tu hapa jeshi limemtumia barua ya kuwa mkufunzi wa Kambi ya Maji ya bluu”
Kila familia kubwa iwe zile za kichifu au za kawaida ilikuwa na kambi yao ya mafunzo ya nishati na mbingu na ardhi ambayo ilikuwa ikifadhili na kusimamia na hii ndio maana ilifanya familia baadhi kuwa na nguvu kubwa kuliko zingine , kutokana na kwamba kadri mbinu yao ya mafunzo inavyofanya kazi na kuwa na wabobezi maana yake pia wanajeshi hao wote wanakuwa chini ya familia hio kusikiliza maagizo yote.
Kambi ya familia ya Mirambo ilifahamika kwa jina la Kambi ya Maji ya Bluu , jina hilo limetokana na mbinu yao ya mafunzo ya nishati ya mbingu na ardhi.
Hamza tokea anaingia hapo alishamwona Nino muda mrefu kama mwanajeshi ambae alikuwa na uwezo mkubwa kutokea upande wa familia ya mirambo.
Upande wa familia ya Mzee Chalula au Chifu Mazengo baada ya kusikia kauli ya Mzee Mirambo , licha ya kuona sio vizuri lakini waliishia kukubali na hio yote ni kutokana na ukweli kwamba hawakuwa na mtaalamu wa kushindana na Nino upande wao.
Nino palepale alipiga hatua kusogea mbele huku akimwangalia Hamza na macho makali.
“Unatoa wapi uthubutu wa kumpokonya bosi wangu mchumba wake , nimesikia uwezo wako ni wajuu sana , nipo hapa kuona ni wa juu kiasi gani”Aliongea Nino kwa kujiamini sana na palepale alisogea ghafla tu na kumsogelea Hamza na kumrushia ngumi ya kichwa.
Hamza ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na mtaalamu wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ya ufunuo wa Maji ya bluu na alitamani kuona mbinu zao za sanaa ya mapigano zipoje , hivyo aliishia kuzuia shambulizi lile na kupiga hatua kadhaa kurudi nyuma na wawili hao walisogea mpaka eneo la uwazi mbele ya ukumbi huo.
“Anga la bluu chanzo cha maji ya bluu , hatua elfu moja za ufunuo wa miguu na mikono!”Aliongea kwa nguvu huku akianza kuchezesha mwili wake kwa namna ya upekee mno kana kwamba kuna kitu alichokuwa akitaka kimtokee.
Na kadri alivyokuwa akitengeneza mjongeo wa mikono palepale mikono yake na miguu ilianza kuongeza spidi ya hali ya juu kwa zaidi ya mara tatu, alikuwa ni kama vile ni mcheza karate lakini spidi yake ilikuwa ni tofauti na Karate na kutokana na mkono wake na mikuu ilivyokuwa ikicheza kwa spidi ghafla tu ni kama miguu yake imeongezeka na kuwa mingi, palepale alimsogelaa Hamza kwa spidi.
Hamza mara baada ya kuona nguvu yake sio haba alijikuta akilazimika kurudi nyuma zaidi ya mara tatu huku akjitahidi kumkwepa asimshambulie eneo la kifuani.
Nino alijaribu kuendeleza ile mbinu yake kwa spidi lakini kila alivyojaribu kumshambulia Hamza alikosa kabisa na alijikuta akishikwa na mshangao.
“Unashangaza , umewezaje kuzuia ufunuo wa hatua therathini za miguu na mikono yangu bila ya kuwa na nishati ya mbingu hata kidogo ?”Alishangaa.
Kikubwa ni kwamba Hamza hakuwa na mabadiliko makubwa sana , yaani wakati mwenzake akitumia juhudi kubwa kujitutumua na kukusanya nisahti za mbingu na rdhi kushambulia lakini yeye aliishia kujilinda tu na hakupata madhara.
“Unajua kwamba ufunuo wa hatua elfu moja za miguu na mikono zinaenda sawa na mbinu ya Kung Fu ya kichina maarufu kama Tyrant spear? Msingi wa mbinu hio ni kwenye nguvu ya miguu yako , bila kuwa na nguvu ya miguu huna cha maana unachoweza kufanya . Naona upo levo ya Ukaidi wa asili hatua ambayo kama unataka kushindana na mimi kwa kutumia miguu na mikono itakuwa ngumu sana , unaonaje ukijaribu kutumia siraha”
“Unaonekana kuwa mtaalamu kuweza kuona daraja ambalo nipo .. ila wewe huna siraha halafu unataka nitumie siraha , huoni kama nitakuonea?”
“Haha.. msingi wako umeanzia katika kutumia siraha , na mimi msingi wangu unategemea mikono , unannionea kivipi kama huwezi kunishinda?”Aliongea Hamza.
Palepale yule bwana alimwangalia mwenzake aliekuwa pembeni na kisha alimpa ishara na alirushiwa ‘Dhana’ maalumu ya rangi ya silver ambayo yenyewe ukali wake huamshwa na nishati ya mbingu na ardhi.
Kitendo cha Dhana ile kutua katika mikono ya Nino muonekano wake ulibadilika mara moja na kutengeneza msisimko kwa watu wote waliokuwa katika eneo hilo kama vile amegeuka na kuwa mchawi ghafla.
“Kuwa makini , hii Dhana jina lake ni Sifongo hivyo usiitolee sana macho’”Aliongea Nino huku akiwa anajiamini kuliko mwanzo na mara baada ya kuongea kauli yake hio palepale alifyatuka na hatua moja tu alikuwa mbele ya Hamza na kumshambulia na ile siraha.
Lakini Hamza ni kama kuna kiru kimemvuta kwani alisogea pembeni kwa ustadi wa juu sana na siraha ile ikapita juu ya kichwa chake , asingekuwa na wepesi kidogo tu ingemgonga kwenye paji la uso.
“Safi sana , umebobea vizuri kwenye matumizi ya hio siraha”
Ijapokuwa Hamza mwanzo alimdharau Nino , lakini aliona uwezo wake wa kutumia hio siraha ulikuwa unashangaza kiasi chake.
Nino mara baada ya kuona staili yake ya kwanza ya kushambulia haikumletea Hamza madhara yoyote alijikuta akishangaa lakini mwili ulimsisimka na kuona hatimae amepata mshindani sahihi.
“Mjongeo wa nyoka!”
Aliongea kwa nguvu huku akimsogelea Hamza na ile siraha huku akiichezesha na kuifanya kuonekana kama vile ni nyoka jamii ya Cobra.
Hamza alikuwa akikwepa kwa spidi kubwa mno na kilichomtatiza ni kwamba siraha ile ilikuwa ikiacha kivuli na kutengeneza udanganyifu wa macho.
Spidi yao ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba wale ambao hawakuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi hawakuona namna ambavyo Nino anashambulia , walichoona ni kama Nino katengeneza duara pekee.
“Mbona unakimbia tu bila kushambulia , kuna haja gani ya kuendelea kupigana sasa?”Aliongea Nino mara baada ya kuona muda wote yeye ndio aliekuwa akishambulia.
Ijapokuwa alichofanikiwa ni kumchania Hamza shati lake , lakini bado alishindwa kumgusa mwili wake kwa kushindwa kumkadiria eneo lake alipo.
Asichokijua mwenzake alikuwa akijifunza mbinu yake na Hamza mara baada ya kuona staili sita za mbinu hio aliona sasa ni wakati sahihi.
“Muda wa kumaliza mchezo”
Nino palepale alichukua fursa na kuanza kumshambulia Hamza kwa kumlenga kifuani, lakini tofauti na mwanzo Hamza alikuwa amesimama tu bila kufanya chochote na ile siraha yake ikiwa inakaribiana na mwili wake Hamza aliidaka kwa mbele na kumfanya kufadhaishwa na jambo lile.
Alijikuta akijitahidi kuisukuma kutaka kumchoma nayo Hamza , lakini kadri alivyokuwa akijitahidi alishindwa kuisogeza mbele hata nchi moja , mbaya Zaidi Hamza alikuwa ameshikilia eneo la mbele la siraha ile kwenye makali lakini hakuwa na ishara yoyote ya damu kumtoka, ilikuwa ni kama vile mikono yake imetengenezwa na chuma.
“Wewe .. unawezaje ..”Nino alijikuta akibabaika huku akimwangalia Hamza kwa mshangao , wakati akiwa kwenye m shangao Hamza aliipiga ile siraha teke na kufanya mikono ya Nino kuuma na kuiachia bila kupenda na ilifyatuka na kuelekea angani.
Na Dakika hio Hamza ni kama amegeuka mpira kwani palepale alienda kumgonga kwa nguvu Nino.
Bam!!
Nino alijikuta akifyatuliwa na kwenda kutua mita kadhaa nyuma na kudondoka chini.
Tukio hilo liliwafanya watu wote waliokuwa katika bustani hio kupigwa na butwaa wakiwa wanamwangalia Hamza.
Hamza aliishia kunyoosha mkono wake juu na kuidaka ile siraha na kisha kwa nguvu aliikita ardhini.
“Imeisha , imemalizika”Aliongea Hamza akitumia msemo ambao aliusikia mahali..
Tukio hilo lilifanya hali ya watu wote kuwa kimya na zilikuwa ni sauti za vishindo vya Hamza akirudi kwenye ule ukumbi na mara baada ya kuona kundi hilo la watu walikuwa wakimwangalia kama mzimu aliishia kutoa tabasamu.
“Mbona mnaniangalia kwa mwonekno huo , sijamuua mtu , Mtu wenu Nino hajafa kaumia tu pale”Aliongea
Mdudu na Mjomba wake Mirambo nyuso zao zilikuwa zishaanza kuumuka kama unga wa ngano , hawakuwahi kuwaza Hamza anaweza kuwa na nguvu mpaka Nino kutokuwa saizi yake.
Mpaka hapo waliona kweli wapo katika hatari ,walianza kujihisi wapo hatarini .
Yonesi alitamani kuruka ruka kwa furaha kwa namna ambavyo Hamza alionyesha ujasiri, alihisi kujivunia.
Msichana kama yeye ambae amekuzwa na familia ya kijeshi , angependelea kuwa na mwanaume mwenye nguvu na sio mwanaume wa kawaida legelege , hivyo alianza kupata ujasiri mbele ya familia yake.
Pah! Pah !
Chifu Mazengo au Mzee Chalula alijiktua akishindwa kujizuia na kuanza kupiga makofi . Meja Jenerali Daudi Chalula Mazengo ambae alikuwa kimya muda wote macho yake yalichanua.
“Kijana mdogo hasira kubwa, safii, ndio maana mjukuu wangu amepata ujasiri wakuongea mbele ya wazee kwa ajili yako”Aliongea Chifu Mazengo.
“Baba tunafanya nini?”Meja jenerali Daudi alikuwa na wasiwasi.Ijapokuwa alitokea kumchukia Hamza lakini kutokana na uwezo wake hata kama hampendi hakujua namna ya kunzuia.
“Nitafanya maamuzi kama ilivyo ada kwa mkuu wa familia na Chifu wa kizazi cha pili cha Mzee Mazengo, Kijana! Yonesi yupo chini yako kwanzia sasa, mke au mpenzi sijali . Nimetokea kukukubali sana”Aliongea Mzee huyo kwa sauti hafifu lakini yenye msisitizo na kumfanya Hamza kucheka.
“Babu macho yako yanaona mbali kweli , hakika wewe ndio Chifu wa Machifu mrithi wa busara , bila kuzingatia mambo mengi lazima umeshaona urithi wa vina saba vya damu yangu utaleta familia yenye nguvu kwenye ukoo wako, si ndio?”Aliongea Hamza alikuwa akiijua vyema historia ya Chief Mazengo moja ya marafiki wakubwa wa Mwalimu Nyerere , moja ya machifu ambao ndio waliofanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.
Yonesi mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akiona aibu na kutamani kwenda kumpiga ngumi Hamza , aliona matani ya Hamza hayachagui kabisa mazingira.
Meja Daudi Chalula aliishia kukunja sura akionekana kufubaa , pembeni yake akiwepo Mzee Imani Mirambo rafiki yake ambae anakwenda kumpoteza.
“Mzee Mirambo unaonanaje ukitulia kwanza kuhusu hili swala . naahidi nitakupa maelezo wewe na familia yako”Aliongea , ukweli ni kwamba walikuwa marafiki wakubwa na siku zote Afande Daudi alitaka msaada mkubwa kutoka kwa familia hizo kubwa ili kutimiza malengo yake ya kuwa Mkuu wa majeshi.
Lakini muda huo alijikuta akishindwa kufanya chochote , Hamza alikuwa akijiamini sana na mtu asie na aibu na kumfanya ashindwe kupata udhaifu wake , ki ufupi alifikia hatua ya kushindwa kumfokea tena na kumfukuza nyumbani kwake.
“Kutupa maelezo? Unapanga kutupa maelezo gani? Binti yako ashaongea tayari anataka kuwa mchepuko na hayupo tayari kuolewa na Mdudu . Kwanzia sasa hatuna mpango wa kuendelea kukaribisha sura zetu hapa kwa ajili ya kumuwinda msichana ambae hata hajui kuja kwetu hapa ni favour tu!
“Mdudu ataenda kupata mwanamke mwingine , kuna wanawake warembo sana kutoka familia nzuri tu ndani ya Tanzania nzima , sio nyinyi tu mwenye mtoto wa kike” Mara baada ya kuongea hivyo alisimama na kisha akaamrisha watu wake kuondoka.
“Chifu Mazengo , sisi tunaondoka uniwie radhi sipo tayari kukutakia maisha marefu”Aliongea na Chifu Mazengo alitingisha tu kichwa.
Upande wa Mdudu aliishia kumwangalia Hamza kwa macho makali na kisha akamgeukia na yonesi na bila kuongea neno aliondoka.
Nino mwanajeshi wa kambi ya Maji ya Bluu alifuatia na yeye huku akionekana kuugulia maumivu.
Kitendo cha kumtoa Nino kupambana na Hamza ilikuwa ni kuwakilisha familia yake ya Kichifu , lakini baada ya kuchapika ilikuwa dharau kubwa kwa familia yake na kwa mantiki hio ni kwamba hata wanajeshi ambao wapo chini yao hawakuwa na uwezo wa kushindana na Hamza kutokana na kwamba Nino ndio aliekuwa juu zaidi na kusifika katika ukanda wao.
Baada ya familia hio ya watangulizi wa Chifu Mirambo kuondoka, Yonesi alipatwa na ujasiri wa kuongea.
“Baba , Mom , Babu najua hili linaweza lisiwe zuri kulingana na maadili , lakini nipo siriasi”
“Wewe mtoto usie na shukrani , bado tu unapata uthubutu wa kuongea , Unajua ni mume wa mtu lakini bado unataka kuwa nae ? Unadhani swala hili likitoka nje familia yetu itaonekanaje huko nje?”Aliongea Afande Chalula.
“Jenerali , si nishasema nipo tayari kufidia taswira yenu yote itakayoharibika ? Kama una ombi lolote kutoka kwangu tukae chini na tuongee”
“Kufidia ! Unaenda kufidia vipi? Sijawahi kuona mtu kichaa na mwanaharamu kama wewe”Aliongea kwa hasira.
“Vipi kama nikiifanya familia yako kuwa familia namba moja ya kichifu hapa nchini , vipi inatosha kuniachia Yonesi?”Aliongea Hamza
“…”
Afande Daudi Chalula alijikuta akishangazwa na kauli ile hata ndugu zake wengine wote walikuwa katika mshangao .
Mzee Chalula Mazengo macho yake ya kizee yalichanua huku midomo yake ikicheza na palepale alitoa tabasamu kama vile anadhihaki kile alichoongea Hamza huku akiamini kwa wakati mmoja.
“Angalia Afande sidhani kama itakuwa swala kubwa hata kama lipo nje ya maadili mimi kuendelea kuwa na Yonesi , ili mradi kile mnachopata katika makubaliano yetu ni kikubwa zaidi , ukiangalia hata mpango wenu wa kumuozesha Yoinesi kwa familia ya Mirambo si ilikuwa kwa ajili ya hadhi ya familia yenu? Tuache kuongea mambo ambayo hayana msingi nipeni masharti na nitaangalia kama naweza kuyatimiza na tumalize hili swala kiwepesi sana”Aliongea Hamza akijinadi.
Yonesi mara baada ya kuona hali ya kusita ya baba yake alijikuta moyo wake ukiuma , ukweli ashaelewa tokea mwanzo swala la kutaka kuozeshwa kwa familia ya Mdudu ni kama dili la kibiashara na kutokana na hilo aliona ni kheri kuwa mchepuko kwa mwanaume anaempenda kuliko kuuzwa kwa Mdudu.
“Mna matatizo gani nyie , mbona kila mtu ni kama anaendeshwa na nguvu za giza, Mume wangu mbona umekuwa kimya ghafla na huongei?”Aliongea mama yake Yonesi huku akiwa na sura iliopauka mno kutokana na yale yote yaliokuwa yakiendelea , mama huyo wa kichaga licha ya kwamba alitokea katika asili ya familia ya watafutaji lakini swala la mtoto wake alikuwa siriasi sana.
Afande Chalula alishindwa kuongea lolote , isitoshe bado alikuwa akifikiria kuhusu ukweli wa maneno ya Hamza , hakuwa akimjua Hamza ni nani na nyuma yake ana nguvu gani ya kuongea maneno hayo , alichojua pekee ni kwamba alikuwa na uhusiano wa karibu sana na Mshauri Mkuu.
“Yonesi mwanangu ni kweli unataka kuwa na huyu mwanaume , hata kama thamani yako inaenda kushuka unahisi upo tayari?”Aliongea
“Mama..”Yonesi aliishia kuangalia chini akishindwa kujua cha kuongea mbele ya mama yake , ukweli ni kwamba hata yeye hakujielewa alijua Hamza ameoa na yupo katika mahusiano na Eliza , lakini mara zote alipokuwa akimuona Hamza na Eliza wakiwa pamoja alijihisi kuwa na wivu mkali mno.
Mama Danny mara baada ya kuona Yonesi haongei alimsogelea na kuanza kumpiga vibao vya mgongoni.
“Wewe mtoto mjinga sana , kwanini unanipandisha presha , hivi ndio nilivyokulea?”Alijikuta akishindwa kujizuia na machozi kuanza kumtoka , hakupata picha kwa namna alivyokuwa akjitoa kwa wanawake wenzake kuhudhuria harusi zao na kutoa michango lakini binti yake ambae alimtegemea anakwenda kufidia juhudi zake ndio huyu kakubali kuwa mchepuko , ukiachana na hilo kulingana na tamaduni aliona sio sawa.
“Mama usiwe hivi .. hali yako sio nzuri bado ..” Muda ambao Yonesi anaongea hivyo palepale Mama Danny alionekana kama mtu ambae ameshikwa na pumu ghafla kwani alishindwa kuhema vizuri na alijikuta akishika kifua chake na kukaa chini taratibu.
“Mama!!”
Palepale alidondoka chini na kupoteza fahamu na kumfanya Afande Daudi na wengine kushikwa na mshituko mkubwa.
“Dokta , mwiteni daktari haraka!!”Afande Daudi aliongea kwa nguvu.
Hamza mara baada ya tukio lile haraka sana alimsogelea mama yake Yonesi na kushika mkono wake na kuanza kupima msukumo wa damu na kisha palepale aliegamiza sikio kifuani kusikiliza mapigo ya moyo.
END OF SEASON 05.. 0687151346 .
MTUNZI:SINGANOJR
SEHEMU YA 149.
Kijana mdogo hasira kubwa