SHETANI RUDISHA AKILI ZETU
MTUNZI:SINGANOJR
SEHEMU YA 158.
Aunt Msamehe Mjomba.
Mara baada ya kulala usiku mzima na mrembo Dina , Hamza aliondoka kijichi akiwa na nguvu na ari mpya kabisa.
Hakwenda kazini pia badala yake alimpigia Prisila simu na kumuuliza kama ana muda waelekee wote Morogoro kutembelea kituo cha kulelea Yatima.
Hamza aliona afanye hivyo maada kesho yake ilikuwa ni sikukuu , hivyo alitaka kwenda kutoa zawadi kwa baadhi ya watoto na kabla ya kuelekea huko , kwasababu Prisila alikuwa akiwajulia sana watoto hao aliona ingefaa zaidi kusindikizana pamoja kwenda dukani kuchagua.
Prisila licha ya likizo yake kutakiwa kumalizika ndani ya siku tisini , lakini tukio la kutekwa na Saidi pamoja na kuwa na mwili wenye joto sana ilimfanya kuomba kuongeza likizo kwa muda mrefu zaidi.
Ijapokuwa wakati anaomba likizo hio Regina alishangaa kwasabu ndio alitoka kumpandisha cheo Prisila lakini hakuweza kumkatalia, alijua lazima kuna sababu kubwa ya kufanya hivyo.
Mwanamke huyo alitaka kukaa chini na kujifikiria na kuweza kutambua nini kinamtokea katika maisha yake , ukweli tokea tukio lile litokee baba yake alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu na bado hakuwa ameliweka wazi kwake na alipanga kumwambia siku atakayorudi.
Hamza aliweza kukutana na Prisila njiani kuelekea Dosam Mall , alikuwa amevalia suti ya rangi nyeusi juu hadi chini na blazia nyeupe kwa ndani , kutokana na urefu wake na umbo lake ilimfanya kupendezesha sana macho.
Hamza mara baada ya kuingia ndani ya gari alimwangalia Hamza juu hadi chini na kuishia kutoa tabasamu.
Ukweli ni kwamba Prisila alikuwa amebadilika mno hasa anapokuwa mbele ya Hamza , alionekana zaidi kuwa mpole kuliko mwanzo wakati wanakutana.
“Umetokea nyumbani kweli?”Aliuliza Prisila.
“Hapana , nimetokea Kijichi kwa Dina”Aliongea Hamza na kufanya tabasamu la Prisila kupotea palepale.
“Kumbe…”Aliongea Prisila huku akishindwa kuongeza neno na Hamza aliona pia isingekuwa vyema kumwambia ameenda kwa Dina kwasababu ya kufukuzwa jana na Regina.
“Prisila hivi naonekanaje , nipo kama mwanaume muhuni hivi sio?”Aliuliza Hamza.
“Kwanini unauliza hivyo , sijawahi kusema wewe ni muhuni”
“Lakini kwa mtazamo wa haraka haraka naonekana kama aina ya wanaume ambao hawajatulia na naendeshwa na tamaa ?”Aliuliza Hamza
“Kuhusu hilo mimi sijui pia lakini bado naona kuna utofauti kati yako na wanaume wengine?”Aliongea na kumfanya Hamza macho kuchanua.
“Tofauti gani?”
“Wewe sio tapeli , Da’ Dina na wengine wanajua kuhusu mambo yako lakini bado wapo hiari kuendelea kuwa na wewe . Mimi naona kwenye maisha kikubwa ni kile kinachokupa furaha, si wanaonekana kuwa na furaha?”Aliongea na kumfanya Hamza kushangazwa na maneno hayo , hakuamini mtu makini kama Prisila angeongea namna hio.
“Prisila na wewe unadhani ipo hivyo?”Aliongea na kumfanya Prisila kutingisha kichwa kidogo.
“Nimekaa kwa siku chache na Serena na nimekuja kugundua ulimwengu ambao naujua mimi ni mdogo mno . Ijapokuwa Serena hakuongelea namna ulivyoishi nje ya nchi lakini nahisi kabisa wewe na Selina sio watu wa kawaida , hivyo naona itakuwa ngumu kutumia tamaduni na sheria za kawaida kukuhukumu”Aliongea
Hamza mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akipatwa na ahueni , alijiambia angalau katika watu aliokutana nao Prisila hakuwa akimdharau kutokana na matendo yake bali alikuwa akijaribu kumwelewa kwa mtazamo wake.
“Kama mke wangu angekuwa na mtazamo kama wako ningekuwa na amani sana”Aliongea Hamza na kumfanya Prisila kumwangalia.
“Namna ulivyokutana na Regina na jinsi ninavyoona usiriasi wa mahusiano yenu ni kitu ambacho kimenifundisha swala jipya. Kwahio jana mligombana?”
“Na wewe si umeona?”
“Ndio ! Mmeondoka pamoja lakini unasema umelala kwa Dina , naweza nisiwe na akili lakini mimi sio mjinga”
“Kwasasa sina cha kuweza kufanya na sijui namna ya kumbembeleza , kesho ni sikukuu nilipanga kuitumia kuweka mambo yetu sawa lakini naona sina jinsi tena”
“Japo tumekuwa majirani wakati wa makuzi yetu lakini maswala kama haya mitazamo yetu ni tofauti , Regina amelelewa kuyaangalia maisha kwa mtazamo tofauti, nadhani ni vyema ukifikiria katika mtazamo wake”
“Kwasasa ngoja nimuache kwanza , atakaa sawa baada ya muda”Aliongea Hamza na kumfanya Prisila kumwangalia Hamza kwa sekunde kadhaa na kisha hakuongeza neno.
Ukweli ni kwamba tokea siku ile alivyofahamu kuhusu Bibi yake Regina kusimamia ndoa ya Hamza na Regina aliona mahusiano ya wawili hao sio kitu chepesi , ijapokuwa alihusika kwa namna moja ama nyingine katika kukutana kwao lakini kufikia hatua hio hakutaka kuingilia kabisa, alipanga kukaa pembeni, muhimu tu aliamini Hamza sio mtu mbaya basi.
“Tuachane na haya kwanza , nataka tuwanunulie watoto zawadi , lakini sijui ni kipi kitafaa , unadhani watapendelea nini?”Aliuliza Hamza.
“Watoto hawana tofauti kubwa sana juu ya vile wanavyopenda , mara nyingi wanapenda midoli , vitu vya kuchezea na chakula kitamu basi”
“Mimi hapo hata sielewi , wewe utachagua mimi nitalipia tu”Aliongea Hamza huku akicheka na muda ule walikaribia kufika na kuingiza gari ndani ya maegesho..
Ndani ya maduka hayo kulikuwa bize sana lakini walifanikiwa kununua kila walichoona kinafaa kulingana na makadirio ya umri wa watoto.
Saa sita na nusu za mchana waliweza kufika Morogoro na kupokelewa kwa ukarimu mkubwa , wakati Dina akiungana na walezi wengine kuandaa chakula upande wa Hamza aligawa zawadi kwa yatima hao.
Siku hio mke wa Mzee Hizza mkuu wa kituo hicho alikuwepo, kwa muda mrefu alikuwepo kijijini akimuuguza dada yake na ndio alikuwa amerudi, tofauti na Hizza Madam huyo alionekana mwembamba zaidi na kuzeeka kulikuwa kukimnyemelea kwa kasi kubwa.
Baada ya kuona namna Hamza alivyokuwa akicheza na watoto hao , yeye na mume wake waliishia kuangaliana na kutoa tabasamu.
“Hamza leo si siku ya kazi? Kipindi kile umetupatia hela nyingi sana na tumetumia kuboresha miundo mbinu ya kituo , huna haja ya kununua vitu vingi ukija”Aliongea Mzee Hizza.
Hamza mara baada ya kumaliza kugawa zawadi alisimama na kisha kwenda kupeana mkono na mkuu huyo wa kituo.
“Kutoa hela ni kitu kingine ila kununulia zawadi za sikukuu watoto ni swala lingine kabisa.”Aliongea Hamza.
Ijapokuwa Hamza hakuishi muda mrefu katika kituo hicho , lakini ndio sehemu pekee ambapo kumbukumbu zake za utotoni ndio zilikuwa wazi kabisa kuliko zingine zote.
“Adam angekuwa na nusu ya moyo wako, sidhani kama angechagua kupita njia ile”Aliongea kwa masikitiko na Hamza palepale alijua Adam aliekuwa akizungumziwa ni Saidi.
Hamza mara baada ya kukumbuka jina hilo hakuacha kuwaza swala lililotokea baharini juu ya kundi la the Shark kupoteza maisha , kuna hisia mbaya ambazo zilikuwa zikimjia.
Wakati wa chakula cha mchana Mke wa Mkuu wa chuyo alitumia nafasi kumuuliza Hamza kuhusu maendelo ya ndoa yake , ukweli ni kwamba wote walikuwa na taarifa ya Hamza kuoa lakini hawakuwa wakijua amemuoa nani hivyo walikuwa na shauku kubwa.
Hamza aliishia kusema alikuwa katika migogoro na mke wake , hivyo walikuwa katika vita baridi.
“Vijana wa siku hisi hamjui kuthamini vitu . Sioni maana yoyote katika ulimwengu huu ya kufanya mgombane . Ila kwa ninavyoona wewe ndio utakuwa na makosa , unaonaje ukijishusha yaishe?”Aliongea Mzee Hizza, alionekana kuwa mzoefu mkubwa.
“Mzee wangu kama ingekuwa rahisi kulimaliza kwa kuomba msamaha nisingeumiza kichwa namna hii”Aliongea Hamza.
“Mke wako anajishughulisha na nini? Wewe niambie ni mtu wa namna gani na nitafikiria cha kufanya. Huwezi kuelewa mwanamke anafikiria nini tofauti na sisi wenyewe”Aliongea Madam Waden na Hamza japo alisita kidogo lakini aliona wazee hao ni kama familia yake tokea afike nchini hivyo hakuona haja ya kuficha , isitoshe Prisila alikuwa akijua kila kitu hivyo palepale aliwAambia.
Mzee huyo na mke wake ijapokuwa walikuwa wamepitia mvua nyingi , lakini mara baada ya kusikia Hamza amemwoa mmiliki na Mkurugenzi wa makampuni ya Dosam walijikuta wakishangaa mno.
“Kumbe! Nilikuwa nikijiuliza kwanini umekuwa tajiri sana , kumbe mke wako ni Regina?”Aliongea , walikuwa wote wakimjua Regina sana , alikuwa ni moja ya wafadhili wakubwa wa kituo hicho licha ya kwamba hakukua na ukaribu mkubwa.
“Mzee huwezi ongea hivyo , hela zangu nimezipata mwenyewe na sijapewa na mke wangu”Aliongea Hamza na kumfanya Mzee huyo kutingisha kichwa.
“Haina haja ya kuendelea kuwa na hasira kwa aina ya mwanamke wa aina hio , ana kila kitu hivyo hivyo ni ngumu kupenda chochote . Inaonekana kazi unayo”Aliongea
Hamza alijikuta akiwa na uso uliojaa uchungu , alichoongea ni sahihi , ijapokuwa watu wengi wanaona kuoa wanawake matajiri ni ufahari lakini sio rahisi sana kwenye kudili nao.
“Imekuwaje kwanza ukafamnya akukasirikie?”
“Ni stori ndefu mzee wangu, lakini ukweli mimi ndio mwenye makosa , ile usiwe na wasiwasi naamini tutakuwa sawa ndani ya muda”Aliongea Hamza.
Mzee huyo na mke wake hawakuongea sana , ukweli hata wao mwanzo walitamani pengine Hamza na Prisila kuwa wanandoa lakini muda huo baada ya kusikia Hamza amemuoa Regina bosi wake Prisila waliona kitu cha tofauti.
Upande wa Hamza muda huo hakuwa na mpango wa kwenda kumpigia Regina magoti na kuomba msamaha, ijapokuwa alikuwa akijua kujishusha lakini alikuwa na ukomo wake.
Kwasababu kesho ilikuwa sikukuu Prisila hakupanga kurudi nyumbani na badala yake alipanga kulala hapo hapo Morogoro nyumbani kwa Mjomba wake.
Wakati Hamza anaagana na mwanamke huyo aliingiza mkono kwenye mkoba wake na kumpatia Hamza tiketi.
“Kuna hizi tiketi hapa , nadhani hujafahamu ila Regina ni mpenzi mkubwa wa Classical music. Kesho usiku kuna show kubwa inayotarajiwa kufanyika Dar Grand Theatre, kuna band maarufu ya The Cast itaperfom , mchukue Regina nenda kaangalie nae”Aliongea Prisila akiwa siriasi na kauli ile ilimshangaza Hamza na aliangalia tiketi zile na aligundua zilikuwa za VIP kabisa.
“Hizi tiketi zinaonekana ni ghali mno , umezinunua?”.
“Hapana kuna rafiki yangu amenipa lakini sikuwa na mpango wa kwenda , nimeona zitaharibika tu nikikaa nazo”Aliongea na Hamza alionyesha kushukuru mno , ilionekana sio show ya kawaida na hakika kuna uwezekano Regina akaipenda.
“Asante Sana Prisila”Aliongea Hamza na kuzichukua akizihifadhi vizuri.
“Nawatakia kupatana kwema , mimi ngoja nirudi ndani nikaendelee na maandalizi”Aliongea.
“Prisila nakuona kama dada anemtakia mdogo wake mema”Aliongea Hamza kwa tabasamu na kumfanya Prisila nae kutabasamu huku akiwa na mwoinekano usioelezeka.
Hamza mara baada ya kutokomea barabarani Prisila aliishia kusimama na kuangalia uelekeo wake na kutoa tabasamu la huzuni.
“Nadhani nimefanya vizuri”Aliwaza huku wakati huo Mzee Hizza aliekuwa juu ya ghorofa akimwangalia mtoto wa mdogo wake kwa huzuni.
****
Saa kumi kamili za jioni ndio muda ambao Hamza aliweza kufika jijini Dar Es salaam na hakunyoosha moja kwa moja nyumbani na badala yake aliingiza gari katika magesho ya kampuni.
Baada ya kusimamisha gari alikaa kwa muda akichati na Irene ambae alikuwa akimsumbua njia nzima.
Ukweli licha ya Irene kuonekana kupagawa , upande wa Hamza hakuwa na uhakika kabisa kuendelea kuwa na aina hio ya uhusiano na msichana huyo.
Lakini hata hivyo mpaka kufikia hatua hio , aliona ingekuwa ngumu sana kumpotezea mara moja , hivyo aliona ni kheri kuendelea kumtuliza tu kwa muda kwanza.
Baada ya kuangalia saa , hatimae aligundua ni muda wa Regina kurudi nyumbani hivyo haraka haraka alitoka nje ya gari na kupandisha juu na kuelekea katika ofisi ya CEO.
Mara baada ya kuingia alimkuta Regina akiwa bize, siriasi akiangalia karatasi na mara baada ya kumwona Hamza akiingia alikunja sura.
“Unafanya nini hapa?”
“Hehe .. wife ni muda wa kurudi nyumbani huu”Aliongea Hamza akjichekesha.
“Leo sitorudi nyumbani , kuna mambo mengi ya kufanya kabla ya kusafiri”Aliongea
“Kwahio unataka kulala hapa hapa ofisini?”Aliongea Hamza huku akiona Regina anaitelekeza familia , huku familia yenyewe akiwa ni yeye.
“Ofisi yangu ina Master na Sebule na kila kitu , kwanini iwe ngumu kulala hapa?”Aliuliza.
Hamza aliona kuendelea kumshawishi Regina kurudi nyumbani isingewezekana , hivyo alitembea na kisha akatoa tiketi na kuweka kwenye meza.
“Kesho usiku The Cast Band watatumbuiza ndani ya ukumbi wa Dar Grande kwanzia saa mbili na nusu za usiku , tutaenda pamoja”Aliongea Hamza akiwa na mwonekno wa dhati kabisa.
Regina aliishia kuangalia zile tiketi kwa sekunde kadhaa na mwonekano wake haukubadilika kabisa.
“Chukua tiketi zako tu , sitoenda”Aliongea
“Kwanini? Si unapendelea Classical music au ni kwasababu bado una hasira na mimi . Nipe nafasi basi ya kujisahihisha”Aliongea Hamza kwa kubembeleza.
“Hakuna sababu ya mimi kukataa , sitaki tu kwenda”Aliongea Regina akionekana kuwa mvivu wa kujielezea na kumfanya Hamza kuvuta pumzi nyingi na kuzitoa.
“Najua kilichotokea kati yetu hakiwezi kuishda kwa muda mfupi lakini angalau natamani tuyamalize . Haijalishi unaniamini au huniamini . ila nikuambie sijawahi kuwa mnyenyekevu hivi mbele ya mwanamke , muda mwingine najiona sio mimi kabisa . Ila kwangu haijalishi ni kwa namna gani nimebadilika , ila kama unachotaka ni mimi kukupigia magoti hilo sahau , siwezi kufanya hivyo. Kitu pekee nitakachofanya ni kukusubiria kesho saa mbili na nusu mbele ya ukumbi . Show inaanza saa mbili na nusu na itaisha saa tano na nusu usiku”
Hamza aliongea , huku akijihisi hakuna kabisa sababu ya kuendelea kujielezea , hivyo aliweka tiketi zile kwenye meza na kisha aligeuka na kuondoka.
Regina alikuwa na mnuno uleule wakati akikodolea macho tiketi hizo , kulikuwa na mwonekno usio kuwa wa kawaida katika macho yake.
Alichokifanya ni kuzisogeza pembeni zile tiketi na kisha kuendelea na alichokuwa akifanya. Macho yake yalikuwa na upofu na moyo wake haukusumbuka kabisa.
Hamza mara baada ya kutoka nje ya kampuni alitamani kwenda nyumbani lakini alivyomkumbuka Shangazi aliona haya ya kurudi , hakutaka kumwingiza shangazi katika mawazo kutokana na matatizo yao yasio isha.
Hamza mara baada ya kufikiria kwa sekunde kadhaa ni wapi alekee palepale alikumbuka ni muda mrefu sana hajawahi kukaa mwenyewe ndani ya Bar na kunywa.
Muda huo sehemu pekee ambayo aliona itamfanyaa ni Elementi hivyo aliendesha gari uelekeo huo na ndani ya dakika chache aliweza kufika na kuegesha gari yake na kuingia ndani.
Kwasabau ilikuwa ni mapema hapakuwa na watu wengi sana , hivyo aliagiza zake Vodka na kunywa mdogo mdogo.
Haikuchukua muda mrefu , Hamza alihisi kuna mtu aliekuwa akimwangalia kwa nyuma na kumfanya ageuze kichwa na muda alishindwa kujizuia na macho yake yalichanua.
Alikuwa ni mwanamke alievalia kileo sana , juu alivalia Crop Top leather coat rangi ya zambarau iliokolea , buti za rangi ya kahawia na gauni aina ya Black Shawl. Alikuwa amekaa kwenye kona akinywa mvinyo peke yake.
Kile kikoti cha juu alikuwa amekiachia wazi na kufanya mabega yake yaonekane , alikuwa mweupe lakini sio mweupe sana na kufanya ngozi yake kuwa angavu sana , mwonekano wake wa sura ulivutia mno.
Alikuwa na sura ya iliopambwa na ulaini wa kipekee sana kama mtoto mdogo, licha ya kuwa Classic sana na urembo wa kati lakini vitu vingi vilimbeba sana na kuonekana mrembo , kope za macho yake zilikuwa zimechanwa na kufanya zichomoze.
“Hii pisi ni hatari”
Hamza alijiwazia huku akipiga pafu la vodka kutoka kwenye glasi , hata hivyo hakuweza kulingana na uzuri aliokuwa nao Regina , kwa jinsi alivyokuwa ilikuwa sahihi kumlinganisha na Yulia.
Muda ambao Hamza alikuwa akijiwazia kwanini mwanamke huyo alikuwa akimkodolea macho muda wote , palepale mwanamke mtu mzima kidogo mrembo alievalia Denim short na blazia ya kuchoresha manyonyo yake alikaa pembeni ya Hamza.
“Handsome upo peke yako? Ninunulie kinywaji basi?”Aliongea yule mwanamke mrembo wa wastani mwenye nyele za rasta nyingi zilizoficha mabega yake , alikuwa na lipsi za kuvutia na pozi lake alionekana kuwa mzoefu.
Hamza alikuja kukaa hapo kwa ajili ya kujitafakari kwa kitendo cha kuchuniwa na mke wake , lakini alijiuliza kwanini kukaa tu hapo ni kama amegeuka shabaha ya wanawake warembo.
“Niko peke yangu , lakini kuna ulazima wa kununulia kinywaji?”Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu hafifu.
Yule mwanamke hakuongea neno lingine na palepale aliomba glass kwa mhudumu na kisha alichukua ile chupa ya Hamza na kujimiminia na kisha akanywa kidogo kwa mapozi.
“Yo have wine and i have story to tell”Aliongea kwa kingereza kilichojaa mapozi na kumfanya Hamza tabasamu kifedhuli.
‘Stori gani hizo?”Aliuliza Hamza kwa shauku na yule mrembo(mshangazi) alijitilisha huruma kwa sekunde kadhaa.
“Nimetoka kumfumania mpenzi wangu. Hio nayo inahesabika kama stori?”Aliongea na kumfanya Hamza kutikisa mabega.
“Kama na hio ni stori basi hii club ni bora ibadilishe jina na iitwe kabisa Story Club na sio Element”Aliongea Hamza na kumfanya yule mwanamke kucheka akijua Hamza anachomaanisha.
“Handsome una vituko , nina uchungu moyoni lakini bado unanichekesha”
“Si naongea ukweli”Aliongea Hamza huku akiweka midomo yake katika staili ya kiswaga.
Staili ile ilimroga yule mwanamke na alipeleka mkono na kushika paja la Hamza kwa kuligonga gonga.
“Unajua nilimvumilia tokea kipindi hicho akiwa chuoni , hakuwa na kitu kabisa na nilimsapoti kwenye vitu vingi , sasa hivi ametajirika ananiona nimezeeka na kutwa kufukuzia vitoto vya chuo , nikimweleza swala la ndoa hataki kusikia kabisa . Moyo unaniuma mno , Sijui hata kama naweza kusahau nikinywa na kulewa”
“Sidhani , nina uhakika hata uelewe huwezi kusahau”Aliongea Hamza.
Mwanamke yule palepale alishika kifua chake na kukipandisha juu na kufanya manyonyo yake kutuna.
“Unaweza kujaribu , ninyeshwe pombe nielewe na kisha nisahaulishe kila kitu”Aliongea huku akimwangalia Hamza kwa sura ya kuomba.
“Dada kama umekuja kunywa unapaswa kuwa na macho ya kumchagua mtu sahihi ..kwa upande wangu sidhani , unahitaji mtu mwingine anaeweza kuunga mkono stori yako”Aliongea Hamza na kumfanya yule mwanamke mwonekano wake kukamaa.
“Unamaanisha nini?”Aliuliza.
Hamza alijimiminia kilevi kilichobakia kwenye glasi na kisha alipiga pafu huku akisikilizia uchungu.
“Tokea sekunde ulioingia hapa na kukaa na mimi kuna macho zaidi ya watu watatu wanaokuangalia , wangekuangalia kwa sekunde kadhaa na kukupotezea ningejua hawakufahamu , lakini ni zaidi ya sekunde hizo hivyo moja kwa moja inaniambia wanakujua vizuri , sio wanaume tu hata wanawake pia , Tatizo kubwa ni kwamba macho yao sio ya kukutamani badala yake ni tofauti, kinachoniambia moja kwa moja hawatamani mwili wako bali koneksheni uliokuwa nayo, au nakosea?”Aliongea Hamza na yule mwanamke alitabasamu vibaya.
“You sure are interesting. If you don't want to invite me, then forget it..”Aliongea yule mwanamke na kisha alisimama na kuondoka.
Baada ya mwanamke yule asiekuwa na jina kuondoka , Hamza aligeuza macho yake na kumwangalia yule mrembo na aliweza kuona kulikuwa na wanaume kibao waliokuwa wakifika katika meza yake kwa kupishana na kisha kuondoka.
Mrembo yule alionekana kutokuwa na matamanio na wanaume hao kabisa na hakuongea neno zaid ya kujiweka bize na kinywaji chake.
Hamza muda huo akili yake ilikuwa ikimwambia anapaswa kujua kwanini mwanamke huyu mrembo sana alikuwa akimkodolea macho, alikuwa akijishauri kwenda ama kutokwenda lakini mwisho wa dakika aliona ajizuie na hio ni mara baada ya kumkumbuka Regina.
Mpaka inatimia saa nne usiku , Hamza alikuwa amemaliza chupa nane za pombe kali ina ya Vodka jambo ambalo lilimshangaza mno mhudumu.
Yule mrembo upande wake alionekana kama vile alikuwa hapo kwa ajili ya kuonja radha ya mivinyo tofauti tofauti , kwani ilikuwa ikiletwa kila aina na mara baada ya kuridhika alisimama na kisha kutoka nje ya eneo hilo.
Hamza alijikuta akimkubali na kuona mwanamke huyo alikuwa vizuri mno kuhimili kilevi . Baada ya kulipa na yeye alitoka nje kuondoka zake.
Hamza mara baada ya kutoka nje hakuweza kumuona yule mrembo na wala hakujali kujua alielekea uelekeo upi , hivyo aliingia kwenye gari na kisha kulitoa ndani ya maegesho taratibu.
Kitendo cha kuingia barabarani ile anapita mbele ya mashine ya kubetia , ghafla tu ulitokea mlipuko wa moto na kumfanya Hamza kufunga breki na ile anageuza macho alishangaa kuona mashine ile ya kubetia ikiwaka moto.
Aliishia kukunja sura na kujiuliza inamaana imezidiwa na umeme au ni shoti ya kawaida.
Hata hivyo hakutaka kuwaza sana na badala yake aliendelea kuendesha gari na kutokomea.
Lakini kitu ambacho Hamza hakuwa ameona ama kukijua ni kwamba mwanamke yule hakuwa ameondoka bali alikuwa juu ya ghorofa akipulizwa na upepo wa baharini huku macho yake yakiangalia uelekeo wa gari yake ilikopotelea.
Jambo la kushangaza vidole vya mikono yake licha ya kuwekewa urembo wa kucha ndefu lakini vilikuwa vikiwaka moto wa rangi ya dhahabu kama vile vinaungua.
SEHEMU YA 159.
Siku iliofuata asubuhi Hamza alifuata ratiba zake za kila siku , ijapokuwa ilikuwa sikukuu ya Iddi lakini upande wa Shangazi kwanza haikueleweka alikuwa dini gani hivyo hakukuwa na shamra shamra zozote.
Wakati anashuka dining kwa ajili ya kupata kifungua kinywa alikuwa akijiuliza kama Regina ataweza kufika usiku kwenye show.
Baada ya kuwaza akiwa peke yake , muda uleule simu yake ilianza kuita na alivyoangalia anaepiga alikuwa ni Yulia.
Hamza alishangaa kidogo , kwa haraka haraka alijua lazima Yulia atakuwa amemalizana na maswala ya kisiwani Chole na sasa amerudi mjini.
“Niambie Yulia , umekwisha kurudi mjini?”Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu.
“Uko wapi?”
“Niko home , najiandaa kutoka”
“Nipo Cloud hotel , tuonane ndani ya lisaa , kuna kitu nataka tuongee”Aliongea Yulia na kisha palepale alikata simu bila ya kusubiria jibu kutoka kwa Hamza.
Hamza aliishia tu kushangaa na kujiuliza ana nini huyo mwanamke , kama ana kitu cha kuongea si aongee kwenye simu ni mpaka aende hotelini kwake. lakini sauti yake tu aliamini lazima kuna kitu siriasi kinaendelea hivyo baada ya kumuaga Shangazi aliendesha gari uelekeo huo.
Cloud international Hoteli pia ilikuwa chini ya kampuni ya Prima Hospitality. Yulia hakuwa na eneo maalumu la kuishi ndani ya jiji la Dar hivyo mara nyingi aliishi katika hoteli hio kwenye Presindential Suite.
Ijapokuwa kulikuwa na msongamano kidogo , lakini ndani ya dakika hamsini zilimtosha kumfikisha pembeni mwa fukwe katika hoteli hio.
Hamza mara baada ya kuingia ndani ya lobby ya hoteli hio na kutaja jina lake na mtu aliemfuata , Lobby Meneja alimsogelea Hamza akiwa na tabasamu pana usoni.
“Mr Hamza Mkurugenzi ndio ameamka sasa hivi , atachukua muda kuoga na kubadili mavazi hivyo naomba usubirie pale ukipata Kahawa”Aliongea kwa ukarimu mkubwa.
“Nini! Yaani ndio anaamka! Sasa kwanini aniwahishe kwa kunipa lisaa tu?”Aliuliza Hamza
“Kuhusu hilo.. kwa kweli hatuna taarifa , bosi ametoa maagizo kukuhudumia mpaka atakapotoka”Aliongea.
Hamza alijikuta akikosa neno na kwenda kukaa kwenye masofa ndani ya eneo hilo la lobby katika mgahawa , alisubiria takribani saa nzima akiwa amemaliza zaidi ya vikombe vitatu vya kahawa mpaka muda ambao Yulia atoka kwenye lift.
Kama kawaida mwanamke huyo alijua kuvaa , siku hio alikuwa taofuti kidogo , alikuwa amevalia kofia ukijumlisha na umbo lake ilimfanya azidi kuwa Sexy.
Wakati akiwa anatembea katika eneo hilo la mapokezi , wanawake wote pamoja na wanaume walimwangalia kwa macho ya husuda lakini hata hivyo hakujali na alitembea na kwenda kusimama mbele ya Hamza.
“Vipi naonekanaje?”aliuliza lakini Hamza alivyotaka kujibu alimpa ishara ya kufunga mdomo.
“Huna haja ya kujibu macho ya watu yashanipa majibu ninayotaka”Aliongea na kumfanya Hamza kujisikia vibaya.
“Una shida gani na mimi asubuhi asubuhi yote hii?”Aliuliza Hamza.
“Sina shida kubwa , nipo free na nimepanga kwenda kutembea tembea na kufanya shopping , sikutaka kutembea na Bertha mimi , hivyo leo utachukua nafasi yake kama bodigadi”Aliongea.
Hamza aliishia kusugua pua yake na kujiambia kuzunguka kote kule kumbe alichokuwa akitaka ni kutumia siku hio wawe pamoja.
Lakini Hamza hakutaka kumuumbua na visingizio vyake hivyo aliishia kukubali.
“Sawa tunaweza kwenda , unataka kuanza na wapi?”Aliongea Hamza huku akisimama na kumshikia Yulia mkono.
Yulia mwonekano wake ulibadilika ghafla na kutamani kuondoa mkono wake kwa Hamza lakini alishindwa na kuishia kumkodolea macho.
“Duka lolote lile kwangu sawa , ili mradi tu lisimilikiwe na kampuni yangu”Aliongea.
“Vipi kuhusu Happy Town Mall, nasikia kuna migahawa ya kisasa pale tunaweza kula kabla au baada ya shopping kabisa”
“Vyovyote vile”Aliongea Yulia akiwa hata hajamsikia Hamza vizuri na hio ni kutokana na namna wafanyakazi walivyokuwa wakimwangalia kwa mshangao.
Ilikuwa ndio mara yao ya kwanza kumuona bosi wao akiwa ameshikwa mkono na mwanaume mbele yao.
Nusu saa mbele Hamza aliingia na mrembo huyo ndani ya Shopping Mall ya Happy city Tegeta , baada ya kuingia walielekea upande wa migahawa inayopika vyakula vya kimagharibi na hio ni kutokana na Yulia bado hakupata Breakfast.
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuwa wawili tu muda wa chakula na Hamza aligundua Yulia alikuwa makini mno na chakula anachokula. Ijapokuwa Hamza alichagua eneo hilo kutokana na umaarufu wa nyama yake lakini Yulia aliagiza Salmoni , Vegetable Salad na Lemonade, hata vile vikorombwezo vingine alivyoletewa Yulia hakuvigusa kabisa , alikwepa kila kitu ambacho kilikuwa na Calories nyingi.
Ilionekana kabisa alikuwa makini sana na mwili wake , Hamza aliona mafanikio yake kibiashara na katika maswala ya kitafiti hayakuwa ya bahati mbaya.
“Mbona unaniangalia au Chakula changu kinashangaza?”Aliuliza Yulia mara baada ya kugundua muda wote Hamza alikuwa akimwangalia.
“Hamna”
“Kama hamna kwanini unaniangalia?”
“Kwasababu wewe ni mzuri”Aliongea.
Yulia alishangazwa na kauli hio kwa sekunde lakini haikumbadilisha na kuendelea kula, Baada ya kudonoa samaki kwa dakika kadhaa aliikita na uma kuonyesha ameshiba.
“Vipi kuhusu utafiti wa Earth Axis , unaendelea vizuri? Bado najiuliza maswali umewezaje kupata taarifa zake na kile kitu kipoje?”Aliuliza na Yulia hakumwangalia Hamza usoni.
“Hatuwezi kuongelea maswala ya kazi tukiwa wawili ,. Halafu hata kama uniulize sina mamlaka ya kukujibu”Aliongea na kumfanya Hamza midomo yake kucheza , aligundua Yulia ni mtu ambae sio mwepesi sana kuongelea kuhusu kazi yake , hivyo ni kama hakutegemea majibu pia.
“Kama unataka nikujibu naweza lakini unapaswa kuniahidi kitu kimoja”Aliongea Yulia huku akionyesha tabasamu la uchokozi.
“Nikuahidi nini?”
“Mpe talaka Regina kisha nioe mimi”Aliongea huku akimwangalia Hamza kwa kebehi lakini kauli ile ilimfanya Hamza kumwangaslia mrembo huyo kwa macho makavu.
“Ndhani ni muda wa kwenda shopping”Aliongea Hamza.
“Vipi kwani? Unahisi utaingia hasara sana ukimpotezqa Regina , kwanza ukinilinganisha nae , mimi nipo Sex zaidi”Aliongea huku akirembua.
“Hebu acha maigizo , unadhani mahusiano ni kitu rahisi namna hio?”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Yulia kurudi katika hali yake ya kutokuwa na hisia.
“Unajuaje kama naigiza , pengine nishaanza kukupenda kweli”Aliongea.
“Hata kama , ila jua tu siwezi kumuacha Regina , nilivyhokubali kufunga nae ndoa , nilimkubali moja kwa moja”
“Kwahio unasema mimi sio mzuri kama Regina? Au kuna vitu vya ziada anakupa nyuma ya pazia, ni mambo ya kitandani sio?”Aliuliza.
“Yulia unaongea upuuzi ujue , mimi kuwa na Regina hakuna uhusiano na unayoongea usipo acha nitaondoka”Aliongea.
“Ukiona mwanaume hakuelewi unachoongea basi hakupendi”Aliongea Yulia kwa kejeli akivuta midomo na kisha alijiweka bize kunywa juisi yake.
Baada ya Breakfast waliingia ndani ya Mall na kuanza kuzunguka , kimantiki Yulia alikuwa ni tajiri na asingekuwa mtu wa kuangalia Brand za kawaida , lakini siku hio alionekana kutojali kabisa , kila kilichomvutia macho alikuwa akichukua na kumtupia Hamza mkononi ashike.
Hamza aligundua hakuwa hapo kama bodigadi badala yake alikuwa kama mdogo wake Yulia, lakini hakutaka kulalamika isitoshe ashapewa utamu hivyo aliona sio mbaya kutumika.
Baada ya kuzunguka zaidi ya maduka manne , Hamza alijikuta akishangazwa na kutokuchoka kwa Yulia .
“Yulia unaonaje tukipumzika kidogo unaonaje tukipata Ice Cream au Keki”Aliongea Hamza na kumfanya Yulia amwangalie Hamza kwa kumkata jicho.
“Acha kujifanyisha una njaa , sitaki kula chochote ni kupoteza muda wangu tu”Aliongea na kumfanya Hamza kukosa neno.
“Kama hutaki kula unataka nini?”Aliongea na kumfanya Yulia kutoa ile kepu kichwani na kumkodolea Hamza macho na kufanya wanawake na wanaume waliokuwa ndani ya eneo hilo kuwaangalia.
“Au huoni vizuri , Mimi kama mwanamke mrembo unadhani napenda nini kama sio kuvaa vizuri?”
Mara baada ya kuongea hivyo aligeuka na kisha aliingia katika duka lingine na kuendeleza kazi.
Hamza alijikuta akijifuta jasho , katika wanawake warembo aliona Yulia ndio mrembo mkatili. Hata hivyo hakuona ni shida sana kuendelea kutumikishwa , kama mwanaume ni kawaida kuvumilia mambo madogo kama hayo.
Yulia mara baada ya kukamilisha kuchagua alitoa kofia na kumrushia Hamza na kisha kimaringo aliingia katika chumba cha kubadilishia.
Hamza alijiambia huu ni uzembe huu kufanyiwa maringo waziwazi , hivyo mara baada ya kuona eneo hilo la kujaribishia hakuna mtu alimsogelea Yulia na kumshhika kiuno kwa nguvu na kwenda kujibanza nae kwenye kona.
“Wewe.. unafanya nini?” Yulia aliruka na ile anataka kupiga makelele Hamza alivamia mdomo wake na kumpiga denda.
Mrembo huyo macho yalimtoka , huku mwili wake ukiwa umekandamizwa katika sofa , alikuwa akiusikiliza mkono wa Hamza uliokuwa ukisababisha machafuko katika mwili wake.
“Yuli hii zurura zurura inachosha ni bora nikufanyie kitu kitakacho kuchosha haraka”aliongea Hamza kwa kunong’oneza.
“Wewe.. Acha ukichaa ujue tupo chumba cha kubadilishia , watu wanaweza kuingia huku”
“Ili mradi hutotoa sauti , hakuna atakaeingia, kwa taarifa yako tunafanyia hapa hapa..”
“..Mhuni…. Acha .. Arghh”
Ijapokuwa Yulia alikuwa akileta ukinzani lakini hakuthubutu kupiga makelele , kingine hakuwa amefanya muda mrefu hivyo kuchokozwa kidogo tu alijikuta akiishiwa na nguvu.
Muda huo wa janga waliweza kusikia watu kutoka nje wakitaka kuingia ndani kwenye chumba cha kubadilishia na kumfanya Yulia kuzidi kushikwa na wasiwasi lakini kwa wakati mmoja hali hio ilimfanya kushikwa na msisimko wa ajabu.
Mara baada ya mkuyenge kumuingia na kupelekewa mawimbi, kidogo atoe yowe na alijikuta akiziba mdomo wake kwa nguvu.
Ndani ya nusu saa Hamza akipeleka moto , waliweza kusikia watu wakiingia kubadilisha na kutoka chumba cha pembeni bila kusikia kinachoendelea mpaka pale walipomaliza.
Yulia nywele zilikuwa zimechanguka huku uso wake ukiwa mwekundu , muda huo alijihisi ni kama alikuwa akiogelea angani na sasa ametua ardhini.
Hamza mara baada ya kufunga mkanda vizuri na kumwangalia namna mwanamke huyo alivyoshikwa na aibu alijikuta akitoa kicheko cha ushindi.
“Hapa sasa unaweza kunitumikisha vya kutosha na sitolalamika maana nishajilipa tayari”Aliongea.
Yulia alitamani kumpiga Hamza lakini alivyokumbuka hamuwezi aliishia kusaga meno , hakuwahi kuwaza atakuja kufanywa ndani ya Mall na kuachia kojo kabisa.
“Fanya haraka tuondoke”Aliongea Yulia , hakutaka kuonekana wakitoka katika chumba hicho na mtu kuingia na kusikia harufu.
Wakati Yulia akitembea akiwa hana ule ujasiri wa maringo tena , upande wa Hamza hakuwa na wasiwasi kabisa alitembea huku akiangalia saa yake, mpango wake ni kuendelea kuwa na Yulia mpaka saa moja na kisha awahi Grand theatre kumsubiria Regina , hata kama ni kwa kubeti.
Unadhani Regina ataenda? Je Yulia atamwacha Hamza awahi?.
******
Upande wa makao makuu ya kampuni ya Dosam , siku hio licha ya kwamba ilikuwa sikukuu , lakini kampuni ilikuwa imefunguliwa kwa wale ambao hawakuwa wa dini ya Kiislamu kuendelea na kazi, haikuwa lazima ilikuwa hiari na malipo yake yalikuwa ya siku hio hio na makubwa hivyo ilifanya watu kadhaa kuwepo.
Sasa katika eneo la mapokezi kulikuwa na kundi la wageni walikuwa wamesimama likiongozwa na mwanamke mzee hivi ambae alikuwa akiongea na mwanamke huyo anehusika na eneo hilo.
“Madam ni ngumu kuonana na bosi siku ya leo bila Appointment”Aliongea yule msichana kwa kubembeleza.
“Najua ninachofanya ni ukorofi , lakini hawa watoto ni wadogo bado na tulikotoka ni mbali mpaka kufika hapa , tukutanishe na bosi Regina hata kwa dakika tano tu”Aliongea.
Wasichana watatu waliokuwa katika eneo hilo la mapokezi walijikuta wakiangaliana na kisha macho yao yakatua kwa watoto zaidi ya therathini waliokuwa nyuma ya mama huyo huku wengine wakiwa na ulemavu wa ngozi, mwonekano wao tu ulifanya washindwe kukataa.
“Nini kinaendelea hapa, hawa watoto wote wametokea wapi?”Sauti ilisikika , ilikuwa ya mwanamke aliekuwa akitembea kwa hadhi ya kitaaluma akiingia ndani ya jengo hilo la kampuni.
Wale wadada wa mapokezi mara baada ya kumuona mwanamke huyo walisimama kikakamavu kuonyesha heshima yao.
“Makamu Mkurugenzi, huyu mama anasema ametokea Morogoro kituo cha kulelea watoto chini ya taasisi ya FOOT , amekuja na hawa watoto na anasema wanataka kuonana na wewe”Aliongea yule dada akibadilisha kutoka kwa Regina kwenda kwa Eliza.
Eliza alimwangalia yule mwanamama kwa sekunde kadhaa na kisha palepale alitabasamu.
“Wewe ni Madam Neema, shangazi yake Prisila si ndio?”Aliuliza na kumfanya yule mwanamke kushangaa.
“Unanifahamu?”
“Hapana , ila nimekusikia kutoka kwa Prisila na Hamza, wote ni marafiki zangu”Aliongea akiwa na tabasamu.
“Oh! Samahani kwa kuvamia kazini kwenu na sikukukuu , tupo hapa kwa ajili ya kuonana na Regina , sijui unaweza kutusaidia?”Aliongea.
“Ungewasiliana na Prisila isingekuwa shida kuonana nae”Aliongea Eliza huku akitingisha kichwa na mama yule aliona aibu kidogo , ukweli ni kwamba hakutaka kumsbumbua Prisila na hio ni kutokana na utu uzima wake aligundua kabisa Prisila alikuwa na hisia na Hamza.
“Kwasababu sijajua dhumuni lako la kuja hapa , unaonaje nikimpigia simu na kumuuliza kwanza?”Aliongea Eliza.
“Hata hivyo itakuwa vizuri , Asante sana na pole kwa kukusumbua”Aliongea na Eliza alimwambia usijali.
Eliza palepale alipiga simu kwenda kwa Regina na muda mfupi tu simu ilipokelewa.
“Senior kuna tatizo?”Sauti ya Regina ilisikika.
“Hapana Mkurugenzi ndio nimerudi na maongezi yameenda vizuri, ni kwamba nimefika hapa mapokezi na kuna mama anataka kuonana na wewe”Aliongea.
“Mama! Nani huyo?”
“Wadeni wa kituo cha kulelea Yatima kutoka Morogoro chini ya Ushirika wa FOOT”Aliongea na Regina alionekana kuwa kimya kwa sekunde kadhaa.
“Amesema anataka kuonana na mimi , kwanini?”
“Sijajua , nimekupigia kuuliza kama unaweza kuonana nae”Aliongea na baada ya kimya kifupi Regina alijibu.
“Sawa nashuka”Alijibu.
“Madam Mkurugenzi anashuka . Subirini kidogo”
“Asante sana , jina lako unaitwa nani?”
“Naitwa Eliza , Eliza Mlowe”
“Una jina zuri , inaonekana nafasi yako hapa pia ni ya juu si ndio?”Aliuliza na Eliza aliishia kutingisha kichwa na tabasamu hafifu.
“Niagize watu wawaletee chochote wakati mkisubiri?”
“Hapana mwanangu , umetosaidia inatosha”Aliongea na kisha alitoa chupa ndogo ya kuhifadhia maji katika mkoba wake na kunywa.
Eliza aliishia kumwangalia Mzee mwingine ambae alikuwa kimya muda wote mwishoni na kisha akawaangalia watoto hao , walivyovalishwa wakapendeza , wote walionekana kuwa na furaha.
Baada ya dakika kama tatu hivi , Regina alitoka kwenye lift na kusogelea upande wa mapokezi huku akisalimiwa na walinzi.
Regina mara baada ya kuona kundi hilo la watoto alijikuta akishangaa lakini haraka aligeuzia macho yake kwa mama mtu mzima.
Upande wa Wadeni mara baada ya kumuona Regina kulikuwa na hali ya mshangao katika macho yake na aliishia kutoa tabasamu huku macho yake yakiwa ni yale ya kumwangalia mtu kiundani zaidi na sio juu juu.
“Nadhani wewe ndio Regina . Jina langu naitwa Neema Hizza ni Mkuu msaidizi na Wadeni wa kituo cha Morogoro Orphange chini ya udhamini wa FOOT”Aliongea akijitambulisha.
“Oh! Shikamoo mama , nikusaidie nini?”Aliongea Regina akiwa na heshima mbele yake na kumfanya mama huyo kucheka kidogo .
“Sio swala kubwa sana kwa mtu kama wewe . usije ukajali sana ni huu uzee”Aliongea
“Madam Waden usiwe na wasiwasi , kama una kitu cha kuongea ongea”Aliongea na mama yule aligeuka na kuwaita wale watoto na wote wakasogea karibu yake.
Msichana alieitwa Salma alionekana kuwa mkubwa kuliko wenzake na kuiongozi na alisogea mbele ya Regina na kumpatia bahasha.
Salma alikuwa na sura ya mviringo na alikuwa akivutia mno kwa kumwangalia hata wafanyakazi waliokuwa nyuma ya Regina walimwangalia kwa macho ya kutabasamu hususani namna alivyopendezeshwa na hijab.
“Asantee!!”
Aliinama Regina na kupokea ile bahasha na msichana yule alishikwa na aibu na kukimbilia kwa wenzake.
Regina alitoa ile bahasha na kuangalia karatasi iliokuwa ndani yake , baada ya kufingua na kuangalia aligundua ulikuwa ni mchoro wa penseli
Mchoro huo katikati kulikuwa na picha ya bwana na bibi harusi ambao walionekana kufunga ndoa na wamezungushiwa na mchoro wa kopa na juu kando ya jua na mwezi kuna mchoro wa mfano wa malaika wanashangilia.
Regina mara baada ya kuangalia mchoro ule alijikuta akishangaa na kumwangalia yule Mama.
“Madam Wadeni hii ni ..”Aliuliza Regina maana hakuwa akijua maana yake ni nini
“Regina , ijapokuwa unaweza kuniona kama mwanamama nisie na mipaka lakini kwangu mimi sijali sana , Ijapokuwa Hamza hakuishi kituoni kwetu kwa muda mrefu lakini amekuwa ni moja ya watoto wa kipekee sana tokea aliporudi. Najua anaonekana kuwa mtu wa kukurupuka na kuchanganyikiwa kiasi cha kufanya mambo ambayo sitamani afanye lakini lakini ni mtu mwenye moyo mzuri sana , ni aina ya wanaume ambao wanaaminika kwa asilimia mia moja. Nimesikia uhusiano wenu haujawa mzuri sana hizi siku za karibuni , nimemuona amenyongea sana na kama mzazi nimejikuta nikishikwa na huzuni moyoni ndio maana katika safari ya kuwatembeza hawa watoto hapa mjini nimeona ni vizuri pia kuja kukuona”
Regiona mara baada ya kusikia kauli hio , mwonekano wake ulibadilika palepale na kuwa wa kikauzu , palepale alitoa ishara kwa wafanyakazi kuondoka ili wasisikie.
“Ndio amekuambia kufika hapa ili kuniambia kwa niaba yake?”
“Hapana , hapana , usije ukanielewa vibaya , Hamza hajui chochote kuhusu mimi kuwaleta watoto hawa kwa siri hapa . Naapia nimejua wewe na Hamza ni wanandoa jana , hajui kabisa..”Aliongea na kumfanya Regina mwonekano wake kulainika kidogo.
“Madam haya ni maswala binafsi baina yake na mimi., Nashukuru kwa ukarimu wako lakini sio swala jepesi..”
“Ni kweli kabisa najua mambo mengi sio marahisi . lakini hebu waangalie hawa watoto walivyopendeza juu mpaka chini , yote hii ni kazi ya Hamza. Tokea Hamza arudi miaka michache iliopita hela zote alizokuwa akipata alikuwa akituma kituoni kwa ajili ya kuboresha maisha ya watoto na muda mwingine alikuwa akifika na kusaidia kazi, ni hivi juzi tu alitoa zaidi ya milioni mia nane ambazo zilitusaidia kuboresha miundo mbinu ya kituo . Nashindwa kujua ni kwa namna gani ya kulipa juhudi zake . Hawa watoto ndio waliosema mjomba wao Hamza hana furaha na wanataka kumfanya kuwa na furaha na ndio maana nimepata ujasiri wa kuja nao ili wafanye kile walichotaka..”
Regina alijikuta akiangalia watoto hao waliokuwa wakimwangalia kwa macho ya huruma kana kwamba walikuwa wakielewa kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Ni kama sasa alielewa kwanini Hamza alikuwa mhahili.
“Aunt Msamehe Mjomba!”
Watoto hao ni kama walikuwa na mazoezi ya kutosha kwani waliongea wote kwa pamoja.
Mara baada ya sauti hio kusikika ndani ya eneo hilo la Mapokezi , Eliza na kila mtu walijikuta wakigeuka na kujiuliza ni mjomba gani anaombewa Msamaha.
Duuh! Huyo Mjomba sasa anaeombwa msamaha unadhani anasameheka?
ITAENDELEA.