Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

saf sana mkuu
 
SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU

MTUNZI:SINGANOJR.



SEHEMU YA 155.

Haikuwa mara ya kwanza kwa Hamza kukutana na janga kama hilo, hivyo alijifanyisha kutokumsikia na kuingia ndani kabisa.

Hamza aliweka vile alivyokuwa ameshikilia mkononi juu ya meza huku akiwa na tabasamu la kizembe.

“Wife nimekuletea vitu unavyopenda”Aliongea na kumfanya Regina kuangalia.

“Njitaongezeka uzito nikila vitu vyenye sukari saa hizi”

“Wife kwa ulivyoumbika , hata kama uongezeke uzito utazidi kupendeza, huna haja ya kuwa na waswasi, kula kidogo”

“Nimeumbika wapi , hebu acha kunisumbua nina mambo mengi ya kufanya”Aliongea akiwa mkavu kabisa.

Hamza aliishia kuwa na huzuni katika moyo wake mara baada ya kuona mbinu yake haifanyi kazi.

“Wife bado una hasira na mimi?”Aliuliza.

“Sina hasira na mtu, naomba usiniulize maswali ya ajabu , hebu toka nje”Aliongea kwa hasira

Ijapokuwa alisema hana hasira lakini kwa Hamza ilimaanisha bado alikuwa na hasira , aliishia kukuna kichwa chake tu akikosa namna ya kumlainisha Regina.

“Ulale mapema usijichoshe sana”Aliongea Hamza kwa sauti ya chini akionekana hana namna tena.

Licha ya kwamba hakuulizwa wapi ametokea lakini hali hio ilimfanya kuona ni kama kuna kitu hakipo sawa

Muda huo wakati akikaribia kutoka nje na kufunga mlango , Regina alimwita..

“Subiri kwanza”Aliongea na kumfanya Hamza kushikwa na furaha akiamini Regina amebadili mawazo.

“Vipi kuna unachotaka ?”Aliuliza kwa shauku .

Regina palepale alitoa furushi la nyaraka na kisha akamnyoooshea Hamza kupokea.

“Angalia kwa umakini ni ratiba na mipango yote ya safari wiki ijayo, hakikisha unaelewa kila kitu”Aliongea Regina akimaanisha safari ambayo walighairisha mwanzo.

Hamza alijikuta akikakamaa mwili . Alijua mrembo huyo alitaka kuongea nae mambo ya moyoni kumbe ni maswala ya kazi , hata hivyo aliishia kupokea nyaraka zile kivivu.

“Wife kuna lingine?”

“Kuhusu nini?”Aliuliza Regina huku akionyesha wasiwasi kwenye macho yake.

Hamza alijikuta akishindwa kuendelea kuongea kutokana na mwonekano wa Regina na palepale alitingisha kichwa.

“Hamna kitu .. unaonekana kuwa bize , nitakuacha uendelee”Aliongea Hamza na kisha alitoka na kuingia kwenye chumba chake , hakuwa na mpango wa kusoma kabisa zile karatasi zaidi ya kuzitupia pembeni.

Licha ya kurudi nyumbani hakujua kwanini lakini moyo wake ulikosa amani kabisa.

Siku iliofuata Hamza alitoka nje kwa ajili ya mazoezi . Regina pia alikuwa bize na mazoezi kama ilivyo kila wikiend.

Wakati wa kifungua kinywa Hamza aliona aanzishe mazungumzo ili kuendeleza mpango wake wa kumbembeleza mrembo huyo.

“Wife leo naelekea shule ya sanaa ya Kayole kuangalia mashindano ya vipaji maalumu vya kuimba na kupiga kinanda , unaonaje tukienda pamoja? Isitoshe leo ni jumapili na huendi kazini”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kushangaa kidogo.

“Unajua kupiga kinanda?”

“Najua kidogo, ni kwamba yule mwanafunzi wangu Irene niliekuambiaga namfundisha twisheni amekubaliwa kuingia katika hatua mtoano kwenye mashindano ya kuimba na kucheza kinanda na amenikaribisha kwenda kumshangalia”Aliongea Hamza.

“Ndio yule uliesema anasoma Advance?”

“Ndio”

Aliitikia na Regina alionekana kuvutiwa na jambo hilo, aliinua glasi yake ya maziwa na kunywa kidogo huku akionekana kufikiria .

“Regina tumia wikiend hii kurelax , isitoshe unapenda mashindano ya vipaji maalumu tokea ulivyo mdogo”Aliongea Shangazi aliekuwa pembeni.

Hamza mara baada ya kusikia hivyo , shangazi akimpigia chepuo , alijikuta akifurahi sana , alijiona ni mwenye bahati kupendekza kitu ambacho kipo kwenye damu ya Regina.

“Wife chukulia kama kuwaunga mkono kizazi kipya kwa kwenda na kuangalia tu”Aliongea Hamza akipigilia msumari.

“Basi sawa , nitaenda kuangalia”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa kukubali.

Ijapokuwa mashindano hayo yalikuwa yakianza saa nne kamili za asubuhi, lakini Hamza hakujua ni saa ngapi Irene ingekuwa zamu yake hivyo waliamua kutoka mapema.

Kayole Art School ilikuwa shule namba moja Tanzania kwa kuibua vipaji kwa watoto waliopo mashuleni , ni kituo ambacho kilikuwa na ufadhili mkubwa sana na haikuwa kusimamia mashindano tu , pia kilihusika katika kufundisha kuimba, uigizaji , kucheza na mambo michezo mbalimbali ya kisanaa ambayo ilihitaji mtu kuwa na kipaji.

Mazingira ya shuleni hapo yalikuwa yakivutia mno , yaliendana kwa usahihi kabisa na hadhi ya shule hio ya sanaa.

Hamza alikuwa amevalia kawaida , alikuwa amevaa shati jeupe bila tai , koti la rangi nyeusi na Dark Slacks(Suruali ya kitambaa).

Regina upande wake alikuwa amevalia koti la rangi nyeupe lenye vifungo vingi na kola ilioungwa na manyoya pamoja na surali nyeupe na Viatu vya Highheels.

Wakati wanashuka kwenye gari na kutembea kuelekea ukumbini ,ilimfanya Hamza kukumbuka siku alioenda shuleni na Dina namna wakola walivyokuwa wakimtolea macho , muda huo hali ilikuwa hivyo hivyo baada ya kutoka na Regina.

Muda ambao walifika katika eneo la kuingilia ukumbini watu kadhaa walikuwepo , kulikuwa na mabango mengi pamoja na picha za washiriki.

“Hamza!” Sauti ya Kizungu ilimwita Hamza na kumfanya ageuke palepale na alishangaa mara baada ya kumwona ni Serena akiwa ameambatana na Prisila.

Serena alikuwa amevalia gauni la rangi nyeusi , huku Prisila akiwa amevalia kigauni cha khaki mtindo wa Ivy tunic.

Regina alishangaa pia kumwona Prisila katika eneo hilo na waliishia kusalimiana kwa kukumbatiana , lakini kwa wakati mmoja akiwa na wasiwasi juu ya mwanamke wa Kizungu aliekuwa akisalimiana na Hamza.

“Wife huyu ni mjane wa marehemu rafiki yangu , Anaitwa Serena na ndio amefika Tanzania kwa mara ya kwanza”Aliongea Hamza haraka haraka ili Regina asije kufikiria vibaya.

“Hello! My name is Regina, nice to meet you”Aliongea Regina akiwa na mwonekano tulivu.

“Hamza , So this is your wife , what a beuty”Aliongea Serena kwa furaha wakati akisalimiana na Regina.

“Na nyie mmekuja kuangalia mashindano?”Aliuliza Hamza kwa kingereza.

“Ndio , nimemsindikiza Prisila amealikwa na Irene moja ya washiriki , sikuwa na chakufanya ndio maana nimeamua kuja kuangalia, Sasa sivi tumekuwa marafiki wakubwa”Aliongea Serena huku akimkonyeza Prisila.

“Prisila na wewe unamfahamu Irene?”Aliuliza Regina kwa mshangao akimwangalia Prisila kwa mshangao kwa namna alivyokuwa na ukaribu na Serena.

“Irene ni mtoto wa Madam Emilly , umemsahau?”Aliuliza Prisila na kumfanya Regina macho kuchanua.

“Kumbe ni Irene yule aliekuwa mtundu wakati wa udogo wake”Aliongea na Prisila alicheka.

“Sasa hivi kakua huyo na kawa mrembo na kipaji kikubwa cha kuimba”Aliongea na kauli hio ilimfanya Regina kumwangalia Hamza kwa maswali.

Alikuwa akimfahamu Irene wakati akiwa mdogo maana alikuwa mtundu sana na mzuri wakati huo wakiishi Msasani kama majirani.

“Hongera Prisila kwa kupata rafiki mwingine”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.

“Serena ana roho nzuri sana na pia ana akili nyingi , nimejifunza vitu vingi kutoka kwake”Aliongea huku akimwangalia Selina kwa tabasamu.

Hamza hakujua kwa nini Prisila anawaza hivyo, isitoshe mwanamke huyo alikuwa ni mwanasayansi mkubwa na IQ yake ilikuwa kubwa, vinginevyo asingeweza kuolewa na Dokta Genesha.

"Nadhani tuingie ndani kwanza, tutafute pa kukaa, ndipo tuendelee kuongea," aliongea Hamza, na wote walikubali.

Prisila alikuwa bize sana kuongea na Serena, lakini upande wa Regina alionekana kuwa kimya muda wote.

Mara baada ya kujitambulisha majina yao kwa mtu wa mapokezi, papo hapo walichukuliwa na kupelekwa katika siti za mbele kabisa za ukumbi huo.

Mara baada ya kufika mbele katika siti, waliweza kumuona mwanaume mwingine makamo akiwa amekaa, na Hamza alimfahamu papo hapo mara baada ya kumuona.

"Ni wewe, Mzee!"

Mwanaume huyo alikuwa ni baba yake Irene, alikutana naye kwa mara ya kwanza hotelini alivyokuja kumchukua Irene baada ya kulala naye.

Mzee huyo alikuwa na uso uliokuwa na tanabahi, huku akiwaangalia wanawake watatu waliokuwa nyuma ya Hamza.

"Binti yangu ndiye amekualika?" Aliuliza Baba Irene.

"Ndiyo, tumekuja hapa kwa ajili ya kumshangilia."

"Binti yangu hahitaji watu wa kumshangilia, yupo hapa kushinda na si vinginevyo," aliongea kwa kujivunia, na kumfanya Hamza awaze ikiwa ina maana Irene alikuwa na uwezo mkubwa wa kuimba kama alivyosema.

Ukweli ni kwamba hakuwahi kumuona Irene akiperfom hata mara moja, hivyo ilikuwa ngumu kwake kumtabiria kama atashinda.

Ijapokuwa Baba Irene hakuwa na furaha na ujio wa Hamza katika eneo hilo, alishindwa kutoa macho yake kwa Regina aliye kuwa pembeni ya Hamza.

"Mzee, huoni kama si vizuri kukodolea macho mke wangu hivyo?" Aliongea Hamza baada ya kukohoa.

"Nini! Huyo ni mke wako?"

"Ndiyo, si siku ile nilikuambia nimeoa au umesahau?" Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.

“Kumbe, nilikuwa nikimwangalia kwa sababu ni kama namfananisha hivi, ni kama nilimuona mahali ila si kumbuki,” aliongea.

“Haha... wanaume mara nyingi tunaanzaga hivyo hivyo,” aliongea.

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi na mimi, halafu kwa sababu una mke ni vizuri ukikaa mbali na binti yangu,” aliongea.

“Ni binti yako ndiye anayependa kukaa karibu na mimi na kunitafuta, kwa nini unanilaumu mimi, isitoshe hakuna kitu kati yetu cha kunifanya nimkwepe.”

“Ni vizuri hakuna kitu kati yenu, lakini siku nikigundua unapanga njama dhidi yake, utakiona cha mtema kuni,” aliongea huku akigeuzia uso wake upande mwingine kama mtu ambaye hataki kuendelea kusikiliza pumba.

Maneno ya mzee hayo yalimfanya Hamza kushikwa na wasiwasi na aligeuka pembeni kumwangalia Regina, lakini kwa bahati nzuri au mbaya, mwanamke huyo alikuwa na ukauzi vilevile bila ya kubadilika.

Na Selina upande wake hakuwa na neno kwa sababu hakufahamu Kiswahili, ni Prisila pekee aliyekuwa na wasiwasi dhidi ya Hamza.

Hamza aliishia kujifuta uso wake na kitambaa, huku akijiambia yaani bado hayupo kwenye mahusiano mazuri na familia yake, anaanzaje kujihusisha na msichana mtukutu kama Irene.

Baada ya kusubiri kwa dakika kadhaa kwa kuboreka, hatimaye mashindano yalianza rasmi.

Ilionekana Irene alikuwa ni kati ya washindani wazito wazito, hivyo alikuwa wa mwisho, lakini hata hivyo ratiba haikuboa sana kutokana na waimbaji wengine kuwa vyema sana.

Saa saba na nusu za mchana hatimaye zamu ya Irene iliwadia na kuitwa kwenye steji na mshereheshaji.

Kilichomshangaza Hamza ni pale mshereheshaji alivyomtambulisha baba yake Irene kama msanii wa bendi iliyowahi kupata umaarufu kabla ya kuzaliwa kwa Bongo Fleva, bendi ya Tanzania Orchestra.

Mzee huyo alisimama na kupunga mkono na kufanya kupigiwa makofi na watu wengi.

Mara baada ya Hamza kuona namna mzee huyo anavyoshangiliwa na watu, alijisikia vizuri lakini kwa wakati mmoja aliona kuna kitu hakipo sawa kwa mzee huyo, maana alikuwa akimfahamu fika ni jasusi.

Irene, aliyekuwa amevalia gauni la maua maua, aliingia kwenye steji na kabla ya kuanza kuimba pamoja na kupiga kinanda, alitoa ishara ya heshima kwa majaji na hadhira.

Hatua ya kwanza, Irene alipaswa kuonyesha uwezo wake wa kupiga kinanda, na alichagua wimbo wa La Campanella, maarufu kama Little Bell kutoka kwa Muitaliano Franz Liszt, na baada ya hapo pia angepaswa kuimba wimbo wake.

Baada ya Irene kukalia benchi la kinanda, muda ule watu wote walitulia kimya na ndipo msichana huyo aliyejaa utundu alianza kuchezesha vidole vyake katika kinanda hicho kwa ustadi mkubwa.

Ikumbukwe La Campanella ni wimbo wenye melodi ngumu sana kuizalisha kwa kutumia kinanda, lakini Irene alianza kuonekana kufanya vizuri mno.

Hata Hamza, ambaye hakuwa akimjua vizuri Irene kuhusu kipaji chake hicho, alijikuta akishangazwa na uwezo wake, na alijiambia kwa umri wake na level yake akifanya juhudi huenda akawa mpiga kinanda maarufu kuliko hata uimbaji ambao bado hajasikiliza.

Upande wa baba yake Irene alionekana kuwa na wasiwasi mno, ni kama alikuwa akiogopa binti yake angefanya makosa na kushindwa kumalizia.

Muda huo, wakati kila mmoja akiamini Irene anakwenda kushinda katika upande wa kupiga kinanda, Irene aliyekuwa nyuma ya kinanda alijikuta akishindwa kuendelea kama mtu ambaye amepoteza kumbukumbu za wimbo anaopiga.

Baada ya kuvuta pumzi na kuanza kuendelea, Irene alianza kutoka nje ya tuni za wimbo, mpaka anakuja kumaliza, jasho lilikuwa likimtoka mno na alikuwa na mwonekano usio wa kawaida. Aliishia kusimama kinyonge, kutoa heshima ya kumaliza, na kisha alirudi nyuma ya steji.

Hadhira yote pamoja na majaji walijikuta wakiwa katika mshangao; hawakuelewa kwa nini mwanzoni alicheza vizuri lakini akaja kuharibu mwishoni.

Majaji walishia kutingisha vichwa vyao wakiwa wanaangaliana, kuonyesha kwamba Irene alikuwa amefeli.

Baba yake Irene hakuwa na raha kabisa, na hakukaa tena chini bali alisimama na kuelekea nyuma ya steji.

“Hamza, nini kimemtokea Irene? Mbona alianza vizuri tu?”

“Haiwezekani, mwonekano wake… naona ni kama kuna kitu hakipo sawa kwenye mwili wake. Kwa alivyoanza, ni ngumu mtu kusahau kabisa na kutoka nje ya ala,” aliongea Hamza, na palepale alisimama.

“Nitaenda nyuma ya steji kuangalia, naona kama hayupo sawa,” aliongea Hamza.

“Nitaenda pia,” aliongea Prisila.

“Kwasababu mnaenda, kwa nini na sisi tusiende, mke wa Hamza?” Aliongea Serena akimwangalia Regina.

Regina hakupendezwa na namna ambavyo Serena alikuwa akimwita na aliishia kukunja ndita tu, lakini hata hivyo aliona haitokuwa vizuri kubakia mwenyewe, hivyo alisimama pia.

Mara baada ya kuzunguka kidogo, hatimaye walifika nyuma ya ukumbi na walivyoingia waliweza kusikia kilio kutoka kwa Irene.

Hamza aliweza kumuona Irene aliyekuwa amejiinamia kwenye kioo huku akilia.

“Unalia nini sasa? Yaani umenitoa nje ya nchi kuja kuangalia mashindano yako, lakini hiki ndio unachofanya? Umeanza kujifunza kupiga kinanda tokea ukiwa mdogo, nini kimekupata?”

“Ni kweli baba, nimechukua mazoezi vizuri tu na nilianza vizuri, ila sikujua hata nini kinanitokea. Nilijihisi kizunguzungu.”

“Unamdanganya nani? Ni kwa sababu hujiamini, ndio maana. Uliweza kufanya vizuri mbele ya wazungu kule Ujerumani, tena kwenye steji kubwa, lakini leo kwenye kijisteji kidogo hiki unashikwa na uoga?” aliongea kwa kufoka Baba Irene.

“Baba, sijui kilichonitokea…”

“Bado unabishana na mimi…”

Muda huo alijikuta akiacha kumfokea baada ya Hamza kusimama mbele yake.

“Inatosha, Mzee. Unapaswa kuamini anachoongea binti yako. Si ndio wewe uliyekuwa ukiamini uwezo wake, kwa nini unashindwa kumuamini sasa hivi?” aliongea Hamza.

“Hamza!...” Aliita Irene, na palepale alimgeukia Hamza na kumkumbatia kwa nyuma huku akiendelea kulia.

“Najisikia vibaya, sikutarajia itakuwa hivi…”

Hamza aliishia kugeuka na kumshika mabega kumtuliza, kisha akajikuta bila kupenda akimwangalia Regina, akimpa ishara kwamba hakuna kinachoendelea kati yao, anajaribu tu kumtuliza.

“Nina muelekeza binti yangu, acha kuingilia biashara za watu wengine,” aliongea Baba Irene.

“Baba Irene, muda mwingine matokeo yanatokana na hali tofauti tofauti mtu anayokuwa nayo. Irene yupo vizuri kama alivyoanza mwanzo, lakini mwishoni alianza kubadilika. Pengine ni kweli hakuwa akijisikia vizuri,” aliongea Prisila.

“Wewe ni nani?” aliuliza kibabe baada ya kuona mtu mwingine anaingia.

“Mimi ni Prisila, mtoto wa Profesa Singano. Tulikuwa majirani, nadhani umenisahau tu,” aliongea Prisila, na palepale mzee yule macho yalichanua.

“Oh, ndio maana nilikuwa nikijiuliza nimekuona wapi. Kumbe wewe ni mtoto wa Profesa. Ni juzi tu nilikutana na Profesa kabla ya kuanza safari ya kurudi,” aliongea huku mwonekano wake ukiwa na hali ya kuridhika.

“Prisila, najua unaona kama namwonea Irene kwa kumfokea kwa sababu ulikuwa na ukaribu naye wakati akiwa mdogo, lakini amezidi kudeka huyu na visingizio vyake,” aliongea.

“Sidhani kama ni kweli, hili si swala jepesi kama unavyodhani,” aliongea Hamza.

“Unamaanisha nini?” Aligeuka na kuuliza kwa sauti.

“Wewe unafanya nini?” aliuliza kwa hamaki mara baada ya kuona Hamza alikuwa ameminya mashavu ya Irene na alikuwa akisogezea pua karibu na midomo ya binti yake.

Kwa jinsi alivyokuwa akifanya, mtu yoyote angedhania Hamza anataka kumkisi. Hata Irene mwenyewe alikuwa kwenye mshituko na alimwangalia Hamza kwa macho yaliyojaa hofu. Lakini Hamza aliishia kunusa midomo yake kisha akamwachia.

“Kuna kitu ulikula ama kunywa kabla ya kupanda kwenye steji?” aliuliza Hamza, na pale sasa kila mtu alielewa ipi ilikuwa nia yake na kuamini labda Hamza amejua Irene alikuwa amekula kitu cha sumu.

Irene, aliyekuwa ameiva kama yai, alijikuta akielewa Hamza alikuwa akifanya nini na akajikuta akishindwa kuongea vizuri kutokana na presha aliyokuwa nayo.

“Sikula... Nilikunywa maji,” aliongea.

“Glasi uliotumia ipo wapi?” aliuliza Hamza, na Irene palepale aligeuza uso wake kwenye ndoo iliyokuwa imehifadhi glasi.

“Nilipatiwa na mfanyakazi, nilikuwa na kiu mno ndio maana nikaomba maji,” aliongea, na Hamza alisogelea ndoo ile kisha akachukua glasi kadhaa na kuzinusa. Alipofikia ya tatu aliinua juu na kuiangalia kisha akampatia Serena.

“Serena, hebu jaribu kunusa,” aliongea kwa Kiingereza na Serena alichukua na kuinusa kwa sekunde kadhaa kabla ya kutingisha kichwa.

“Kuna harufu ya dawa aina ya psychotropic.”

“Nini! Nyie mmejuaje kuna dawa kama Irene alishindwa kuisikia harufu yake?” Aliuliza mzee huyo akiwa katika hali ya mshangao.

“Kwasababu mimi sio mtaalamu lakini nipo sensitive sana na harufu ya dawa, lakini sikuwa na uhakika sana kwasababu maji mara nyingi yanawekwa Water Guard. Lakini Serena ni mtaalamu wa kutofautisha dawa kutokana na harufu yake. Ni Profesa mkubwa duniani na amethibitisha kuna dawa kama nilivyohisi,” aliongea Hamza, na kauli yake ilimfanya mzee yule kupandwa na ghadhabu baada ya kuona kuna mtu kamwekewa binti yake dawa.

“Nani anathubutu kumdhuru mwanangu?” Aliuliza lakini hakukuwa na wa kuweza kumjibu. Hamza palepale alimwangalia Irene.

“Irene, unahisi nani anaweza kukuwekea dawa kwenye maji?”

“Siwezi kujua, sijawahi kugombana na mtu na asilimia kubwa ya watu wanaonekana kunipenda.”

“Kama ni hivyo basi hakuna jinsi zaidi ya kumtafuta mfanyakazi aliyekupatia maji,” aliongea Hamza.

“Nitamtafuta mimi, najuana na Mkurugenzi, mkuu wa shule na hata mwandalizi,” aliongea mzee huyo huku akitoa simu yake na kuanza kutafuta namba. Na ndani ya dakika tu aliweza kutoa maagizo ya wahusika wa uongozi wa shule hiyo kufika nyuma ya steji.

Ndani ya dakika kumi na tano tu, Mkurugenzi Msaidizi, Bwana Thomasi Ombeni alifika akiwa ametangulizana na Mshereheshaji na Jaji Mkuu, Madam Recho Barnabasi, mara baada ya kusikia Irene aliwekewa dawa kwenye maji walionekana kushangaa mno.

“Mzee, huyo mfanyakazi yuko wapi?” Aliuliza Jaji.

“Sijui, na Bwana Thomasi hapa ndiye anayepaswa kujibu.”

Mzee Thomasi Ombeni alikuwa na wasiwasi mno. Baada ya kuuliza watu kadhaa waliokuwa wakihusika na maandalizi nyuma ya steji, aligundua aliyempatia maji Irene alikuwa ni msichana Nurha Mohamed, ambaye alikuwa mwaka wa tatu chuo kikuu.

Mara baada ya kusikia hivyo, Mzee Thomasi palepale alitoa maagizo ya Nurha kutafutwa na aliweza kuja haraka. Na hata baada ya Irene kumuona, aliweza kuthibitisha ndiye aliyempatia maji ya kunywa.

“Nura, ongea ukweli wako. Kulikuwa na dawa kwenye maji uliompatia Irene?” Aliuliza Thomasi.

Nurha alionekana kuwa msichana mpole sana. Alikuwa mfupi kiasi na mwembamba mwenye rangi ya Kiiraqwi, na mara baada ya kuulizwa swali hilo, alionekana kutetemeka.

“Hapana Mkurugenzi, nilichukua maji na kumpatia,” aliongea.

“Maji uliyatolea wapi?”

“Nilikinga pale kwenye water dispenser, kila mtu alikuwa akinywa yale maji. Yanawezekana vipi kuwa na dawa?” aliongea kwa kutetemeka, na Mzee Thomasi Ombeni alimgeukia baba yake Irene.

“Mzee, sidhani huyu msichana anaweza kudanganya. Labda mtakuwa mmekosea,” aliongea na kumfanya baba Irene bado uso wake kuwa katika wasiwasi. Isitoshe pia kwa namna Nurha alivyo, alionekana ni mwanafunzi ambaye anajitafutia hela kwa kufanya kazi za ziada.

“Kuthibitisha kama ni kweli ama uongo kwamba maji hayakuwa na dawa kama alivyosema huyu msichana ni rahisi. Tunachopaswa kufanya ni kupima tu. Uzuri ni kwamba Serena ni rafiki yangu na ni mtaalamu wa hali ya juu, hivyo lazima atakuwa na mbinu nyingi za kuweza kututhibitishia,” aliongea Hamza.

Wote walimwangalia mwanamke yule wa kizungu na maswali mengi. Serena aliomba kuambiwa kinachoendelea na palepale alitoa pasipoti yake na kumpatia Mkurugenzi.

“Hello, naitwa Serena. Kwasasa nafanya kazi kama Profesa maalumu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kabla ya hapo nilikuwa nikifanya kazi katika taasisi za kibaiolojia za kutengeneza madawa. Kama hamwamini mnaweza kuwasiliana na mkuu wa chuo, anazo taarifa zangu,” aliongea.

Kundi hilo la watu, mara baada ya kusikia utambulisho wake, walijikuta wakimwangalia kwa heshima. Isitoshe pia alikuwa ni mzungu na wazungu sio watu wa kujigamba hovyo bila ya ushahidi.

"That's great. Professor, how would you like to test it?" aliongea Madam Recho akimuuliza kama atafanyaje majaribio.























SEHEMU YA 155.

Serena, mara baada ya kuulizwa swali lile, alifikiria kidogo na kisha alionekana kuwa na jibu.

“Naamini hii sehemu haikosi vifaa vya kufanyia majaribio, namaanisha vile vya msingi sana, si ndio?”

“Kwa hapa hatuna, lakini kwa bahati nzuri tunapakana na kiwanda cha kemikali. Nadhani watakuwa navyo, ni swala la kuingia kwenye maabara yao na kuomba,” aliongea Thomasi. Palepale, Serena alitoa notebook na kisha alandika vifaa anavyohitaji na kumpatia.

“Fanya utaratibu wa vifaa hivi kuletwa, ninaweza kufanya majaribio hata hapa,” aliongea.

Mkurugenzi Msaidizi alichukua orodha ile ya vifaa na kisha alimpatia mtu kwenda kuleta, na haikuchukua muda mrefu vifaa vilifika.

Mara baada ya kukabidhiwa, alichanganya vimiminika kadhaa alivyotoa katika makopo mbele ya watu wote waliokuwa nyuma ya steji hiyo.

“Ijapokuwa sina uhakika ni aina gani ya dawa imetumika kutokana na harufu yake, lakini mara nyingi kutakuwa na mabadiliko ya kikemia dawa ikichanganyika na baadhi ya kemikali na kugeuka kuwa bluu,” aliongea.

Kisha yale maji aliyochanganya aliyaweka kidogo sana kwenye ile glasi na kuanza kuyazungusha kwa namna ya kusuuza.

Dakika chache tu, yale maji yaligeuka na kuwa rangi ya bluu. Ijapokuwa haikukolea sana, lakini ilikuwa ni bluu. Mara baada ya kuona hivyo, wote walijikuta wakigeuza macho yao na kumwangalia Nurha ambaye alizidi kuwa na wasiwasi.

Serena alimwaga yale maji mchanganyiko na kisha aliweka maji mengine na kumkaribia Irene.

“Irene, nakutaka upumulie haya maji kwa mdomo. Hiki kimiminika kipo sensitive sana. Kama kweli umekunywa maji ya dawa, kimiminika hiki kitageuka na kuwa cha bluu,” aliongea.

Irene alifanya kama alivyoambiwa na kweli kimiminika kile kibadilika rangi na kuwa cha bluu.

“Nadhani kila mtu sasa ameona, mwanangu aliwekewa dawa,” aliongea baba Irene.

Madam Rachel na Mkurugenzi walitingisha vichwa kukubali. Serena hakuishia pale tu; alisogelea dispenser na kumimina maji kwa kuchanganya na kile kimiminika, na hakukuwa na rangi ya bluu yoyote.

“Nadhani sasa mmeona, kwenye maji yalipo kwenye dispenser hayana shida,” aliongea na kisha akarudi kumwangalia Nurha akibadilisha kimiminika kingine.

“Girl, weka kidole chako katika hiki kimiminika. Kama kweli wewe ndiyo uliweka dawa, basi ni lazima kuna mabaki kwenye mikono yako, na yatafanya hiki kimiminika kugeuka na kuwa cha bluu. Kikibakia hivi basi utakuwa huna kosa,” aliongea.

Nurha, msichana mpole aliyekuwa na uso uliofubaa, baada ya kusikia hivyo hakuthubutu kuinua kidole chake na kuweka katika kile kimiminika cha kemikali.

“Usiwe na wasiwasi, hii kemikali haina madhara kwenye ngozi,” aliongea Serena, lakini palepale Nurha alitingisha kichwa na kuanza kutokwa na machozi.

“Haikuwa makusudi, ni Mkurugenzi ndiye aliniambia...” aliongea huku akianza kulia. Watu wote mara baada ya kusikia hivyo waligundua sasa kuna mtu aliyekuwa nyuma ya tukio hilo.

“Mkurugenzi, unamaanisha Mzee Jomanga?” Aliuliza kwa mshangao, na Nurha aliishia kutingisha kichwa.

“Ameahidi kuingiza jina langu katika watu watakaopata kipaumbele cha kwenda kusoma Masters nje ya nchi, ndio maana nilifanya.”

“Mzee Thomasi, nini kinaendelea?” Aliuliza baba yake Irene.

“Mzee mwenzangu, nadhani nishajua kilichotokea. Ukweli ni kwamba Mkurugenzi ana mtoto wake wa kike anashindania nafasi moja na Irene, ndiye aliyekuwa anaimba na kupiga kinanda kabla ya Irene, hivyo...”

Baba yake Irene palepale alijua nini kinaendelea.

“Kwahiyo tunafanyaje? Maana binti yangu hajatendewa haki katika hili. Haya ni kama matusi. Nataka shindano lirudiwe, na huyo Mzee Jomanga akamatwe na kuhojiwa na polisi,” aliongea.

“Kuhusu kurudia shindano, Mzee, nadhani halitowezekana. Ni swala ambalo pia polisi hawawezi kulitolea maamuzi, kwa sababu hatua ya kwanza imekwisha kupita, na kusema kurudia tena, sidhani kama inawezekana,” aliongea Chifu Jaji.

“Ni kweli kabisa, Mzee. Tafadhali punguza jazba kwanza. Naamini zipo njia nyingi za kumfidia binti yako katika hili,” aliongea Mkurugenzi. Hakutaka swala hilo kufahamika kwa watu.

“Mnafidia vipi ilihali mashindano yenu yenyewe sio ya haki? Msiniambie mnataka kumpitisha mtu ambaye hastahili?”

“Haitowezekana kubadilisha mshindi kutokana na kura zishapigwa tayari, lakini kwa kipaji alichokuwa nacho Irene tutampatia tuzo maalumu ambayo itamuwezesha kushiriki katika awamu ijayo, na naamini ataweza kupita,” aliongea Chifu.

“Ni kweli kabisa, pia shule yetu inasimamia ufadhili kwenda vyuo vingine, ijapokuwa haitokuwa chuo cha Yale kama ambavyo mshindi anapaswa kwenda, lakini vipo vyuo vingi ambavyo vinafadhili wanafunzi kupitia shule yetu. Tunaweza kumuweka Irene kama kipaumbele,” aliongea.

“Kipaumbele cha Scholarship? Mnadhani nashindwa kumsomesha mwanangu nje ya nchi? Sababu ya kukubali Irene kushindania hii nafasi ni kwa ajili ya kupata nafasi ya kusomea Yale kama angekuwa mshindi kwa juhudi zake na sio ufadhili wa huruma. Acheni kuhalalisha kosa.”

Pande zote zilijikuta katika hali ya kukinzana. Ukweli ni kwamba sio kama Irene baba yake hana hela za kutosha kumsaidia kwenda kusoma nje ya nchi; ukweli ni kwamba kutokana na wanafunzi wengi kuomba nafasi za kutaka kusoma chuo maarufu duniani cha Yale, vigezo vilikuwa vikubwa mno.

Chuo cha Yale chenyewe ndicho kilitoa nafasi moja kwa kila shule ya sanaa ndani ya mataifa ya Afrika kwa kushindanisha vipaji, na anayeibuka mshindi angeweza kupata nafasi ya moja kwa moja kusomea katika chuo hicho akishafaulu masomo ya kidato cha sita. Hata kama hela unazo, ni ngumu sana kwa mtoto wa Kiafrika kupata nafasi ya kusomea katika chuo hicho kikubwa kwa kutegemea maksi pekee.

Regina ambaye alikuwa kimya muda wote, mara baada ya kuona hali imefikia hatua hiyo aliamua kuingilia.

“Mkurugenzi, muache Irene arudie upya, na kuhusu nani mshindi, Majaji ndio wataamua,” aliongea.

Regina, mara baada ya kuongea maneno hayo, eneo hilo lilikumbwa na ukimya, kwani ilikuwa ghafla sana.

Mzee Thomasi alishangaa na alijikuta akichukia baada ya kuona kuna mtu anaingilia. Ukweli ni kwamba alitaka tukio liishe vilevile. Lakini sasa, mara baada ya kumwangalia Regina kwa umakini, alijikuta akionyesha hali ya mshangao.

Madam Rachel alijikuta akishikwa na mshangao wa shauku baada ya kumwona Mkurugenzi akabadilika ghafla.

“Mkurugenzi, nini tatizo?”

“Samahani, wewe ni bosi Regina? Kumbe ulikuwa hapa muda wote?” aliongea, na palepale alijikuta akionyesha ishara ya heshima mbele ya Regina.

“Samahani Mkurugenzi, sikukuona. Kwanini hukutoa taarifa unahudhuria pia? Nilikuwa bize sana mpaka kushindwa kutambua mtu mkubwa kama wewe,” aliendelea kuongea.

Kutokana na mtindo wake wa uvaaji, ilimfanya kuwa wa kawaida, lakini vilevile alikuwa amechanganyika na kundi la wafanyakazi wa tukio hilo, hivyo ikawa ngumu kumuona.

Irene na baba yake walijikuta wakishangaa, na muda huo ni kama akili zao zilianza kufanya kazi kwa usahihi. Ijapokuwa Irene alikuwa akimjua Regina, lakini kutokana na kuzungukwa na watu, hakumuona. Upande wa baba yake, sura yake ilikuwa ikija na kupotea.

Hawakutegemea Regina angekuwa katika eneo hilo; isitoshe, kwa mwanamke tajiri kama huyo, ujio wake ungeonekana tu kama ilivyokuwa kwa matajiri wengi—pengine angekuja na wasaidizi wake au mabodigadi.

“Madam Rachel, huyu ni Afisa Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa makampuni ya Dosam. Kampuni ya Dosam ndiyo wafadhili wakubwa wa haya mashindano ya kuibua vipaji katika shule yetu,” aliongea, na kumfanya Rachel kumwangalia. Aliweza kumtambua Regina mara moja na alijiambia ndiyo maana alikuwa akivutiwa na sura yake tokea dakika aliyoingia hapo.

Regina aliheshimika sana, sio tu kwa sababu ya pesa, bali pia katika kuinua elimu ya Tanzania kwa kufadhili wanafunzi wengi wa masomo ya juu kusomea nje ya nchi kupitia Dosam Foundation.

Mara nyingi, kampuni ya Dosam imekuwa sehemu ya wafadhili wakubwa wa shule hiyo; hivyo alikuwa kama bosi.

Ukweli ni kwamba hata Yale kuchagua Kayole kwa kugawa nafasi moja ya mwanafunzi kujiunga katika chuo chao ni kutokana na ufadhili imara. Ikitokea mtu kama Regina akilalamika ubalozini kwa kutoridhishwa na shindano hilo, moja kwa moja Kayole wanaweza kupokonywa nafasi hiyo na kupewa shule nyingine, na umaarufu wao ungeshuka mno.

“Mkurugenzi, sababu ya kampuni yangu kutoa kiasi kikubwa cha pesa kuingia katika mfuko wa shule yenu ni kwa ajili ya kuboresha elimu inayotolewa hapa. Lakini kama mmekosa ujasiri wa kuwa wa wazi katika mashindano, unadhani itakuwa rahisi kwetu kutoa hela zetu kwa ajili ya manufaa ya watu wachache?” aliongea Regina.

“Mwenyekiti, maneno yako ni ya kweli kabisa. Unaona tufanye nini kuhusu hili?” aliuliza Thomasi.

“Wewe sema, Irene hali yake ya kiafya ilibadilika ghafla, hivyo atarudia kuperform. Kama kuna mshindani ambaye hajaridhika anaweza kuomba kurudia pia,” aliongea Regina.

Mkurugenzi Msaidizi, Thomasi, na Jaji Mkuu, Madam Rachel, waliona ni jambo la kushangaza kwenda mbali namna hiyo kwa sababu tu ya Irene. Walijiuliza Irene ni nani kwa Regina mpaka ashindane mara mbili. Lakini ingekuwa ngumu sana kwa shule hiyo kukataa agizo la mfadhili mkuu, kwani ndiye aliyekuwa akiwalipa mshahara na posho.

Baada ya hapo, kwa sababu mashindano hayakuwa yamemalizika na ilikuwa zamu ya waigizaji, Chifu Jaji aliondoka kuweka maandalizi ya Irene kupewa nafasi nyingine ya kutumbuiza.

“Asante sana bosi Regina, ina maana kubwa sana hii kwa binti yangu. Isitoshe, ilikuwa ni ndoto yake kubwa kwenda kusoma Yale kupitia shindano hili,” aliongea baba yake Irene akitoa shukrani za dhati kabisa.

Irene alimwangalia Regina na kisha akamwangalia Hamza, na kisha alisogea mbele na kumshukuru.

“Asante sana Madam Regina,” aliongea.

Regina alitingisha kichwa huku akiwa na mwonekano usioelezeka, na alimwangalia Hamza kabla ya kuongea.

“Nimesikia kutoka kwake, una kipaji kikubwa. Naamini utaitumia fursa hii vizuri kutimiza ndoto zako,” aliongea, na Irene alitingisha kichwa.

Baada ya Irene kuanza kujiandaa kwa kurudia kuimba na kupiga kinanda, Serena alimsogelea Hamza na tabasamu la uchokozi.

“Hamza, kumbe mke wako ana ushawishi mkubwa namna hii?”

“Hilo lisikutishe. Mke wangu ni mwanamke wa kawaida tu nje ya kazi yake,” aliongea Hamza.

“Lazima niongee, ndio mara yangu ya kwanza kufika Tanzania na ndio kwanza nimesikia kuhusu kampuni ya Dosam, ila ningeshangaa kama ungeoa mwanamke wa kawaida,” aliongea huku akicheka.

“Miss Serena, I am just a businesswoman, nothing special,” aliongea Regina.

“No, no, you must be special. My old friend, he has seen many beauties. For him to marry you, there must be something special about you,” aliongea Serena akisema kwamba rafiki yake Hamza ameona wanawake warembo wengi, na kumchagua yeye kumuoa lazima atakuwa ni wa kipekee.

“Ukweli, naona mwanasayansi mkubwa kama wewe ni wa kipekee kuliko mimi. Kama usingekuwepo hapa na kufanya majaribio, haki isingetendeka,” aliongea Regina.

“Majaribio! Regina, na wewe unaamini nimefanya majaribio kweli?”

Mara baada ya maneno hayo kusikika, haikuwa kwa Regina tu alieshangaa, bali hata Baba Irene na wengine walishangaa, wakionyesha kuchanganyikiwa.

“Unataka kusema, majaribio yalikuwa feki?”

“Ndio, yalikuwa feki. Unadhani ni rahisi kutengeneza msingi wa majaribio ya dawa aina ya Psychotropic? Tulicheza kamchezo tu. Kawaida, Starch ikichanganyika na maji yenye iodine, inageuka rangi na kuwa bluu. Hakuna uhusiano wowote na dawa iliyokuwa kwenye maji.”

Mara baada ya kuongea hivyo, alitoa maji kwenye kijichupa flani na kudondosha tone katika ile kemikali aliotengeneza mwanzo, na yale maji yalibadilika rangi na kuwa ya bluu. Kila mtu alijikuta katika mshangao; hawakuamini tokea mwanzo mpaka mwisho. Serena alikuwa akiigiza.

“Msiniambie wote hapa mliamini nilikuwa nikifanya majaribio kweli. Kama ni hivyo, basi mimi na Hamza tumejua kuwaigizia.”

“Kama tusingewaaminisha tunafanya majaribio kweli, tusingeweza kumkamata muhusika. Naomba mtuwie radhi. Ni kweli nilinusa harufu ya dawa, lakini ni ngumu kuthibitisha haraka haraka kupitia majaribio. Ni kwamba tu Serena alielewa lugha yangu na kuendelea,” aliongea Hamza, na kufanya watu wote kushangazwa na jambo lile. Kumbe mwanzo mwisho, Hamza na Serena walikuwa wakijua ukweli.

“Serena, una akili sana. Hamza, pia wewe unaonekana kuwa vizuri kichwani mpaka uweze kufikiri kwa haraka haraka na kufanya hivi,” aliongea Prisila.

“Sio akili, ni hila tu. Ukiwa na uzoefu, hata wewe ungeweza kupata wazo kama langu,” aliongea Hamza akizikataa sifa.

Ijapokuwa matokeo yalikuwa mazuri katika maigizo hayo, karibu wote waliona wamechezewa akili, hususani Mkurugenzi na Chifu Jaji, ambao walikuwa wakijua kinachoendelea tokea mwanzo ili kumpitisha mtoto wa Mkurugenzi.

Baada ya Irene kurudia kushindana, alifanya vizuri sana; haikuwa kwenye kupiga kinanda tu, bali pia aliweza kuimba kwa sauti nzuri yenye hisia, na iliwagusa watu wengi sana.

Dakika ambayo alimaliza, kila mmoja aliyekuwepo alisimama na kumpigia makofi huku wakimtabiria makubwa.

Washindani wenzake, akiwemo mtoto wa Mkurugenzi, hawakupata ujasiri wa kuomba kurudia licha ya nafasi hiyo kutolewa. Ukweli ni kwamba, tokea mwanzo ni kama walikuwa wakimsindikiza tu Irene.

Irene hakujali macho ya chuki kutoka kwa wenzake na alipokea tuzo yake pamoja na cheti maalumu cha Special Invitation kwenda kusomea chuo kikubwa duniani kwenye maswala ya sanaa cha Yale.

Mara baada ya kutoka kwenye steji, alimsogelea Hamza na wengine na kuwaomba kuwatoa out chakula cha usiku kama ishara ya kuwashukuru.

“Baba yako atakubali?” aliuliza Hamza.

“Kwanini akatae? Nina uhakika atanipa hela ya kulipia hoteli kubwa kulingana na hadhi ya Madam Regina,” aliongea.

Hamza aliwauliza kuhusu ombi la Irene kutaka kuwatoa out, na Prisila na Serena walikubali. Ajabu, Regina alikubali maana Hamza aliona pengine angekataa.

Baada ya nusu saa, hatimaye walitoka na kisha waliingia katika magari kuelekea hotelini, na Irene ndiye aliyekuwa akiongoza njia akiwa kwenye gari lake mpya alilonunuliwa.

Lakini sasa, dakika kadhaa wakati wakikaribia kwenye mataa, ghafla tu mwanaume mzee alijaribu kuvuka barabara bila ya kujali taa ilikuwa ni ya kijani, na Irene alikuwa ameshaanza kuendesha tayari. Kilichosikika ni kilio cha maumivu kutoka kwa mzee huyo ikiashiria amegongwa.
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZIlSINGANOJR​





SEHEMU YA 156.

Tajiri mwenye moyo wa kimasikini.

Irene bado alikuwa hajaiva kwenye udereva , alichokuwa akizingatia ni taa kumuwashia kijani tu na nyekundu na ndio huendesha gari , hivyo hakuweka umakini kuona kama kuna mtu ambae alikuwa akikatiza licha ya taa kuwa kijani.

Haraka sana alisimamisha gari na kushuka akiamini amegonga mtu .

“Babu nini tatizo?’Aliuliza Irene ambae furaha yake ya ushindi imeingia doa na kuwa na wasiwasi mkubwa.

Hamza na Regina pia walishuka kutoka kwenye gari lakini Hamza kuna kitu alikiona mara baada ya kuchunguza gari ya Irene.

“ Arghhhh.. mguu wangu .. unauma sana”Alikuwa ni mzee wa umri mkubwa aliekaa chini akilalamika kuumia mguu.

Muda huo huo alisogea mwanaume wa makamo alievalia tisheti ya jezi ya Simba na aliinua macho yake na kumwangalia Irene kwa ukali.

“Unaendeshaje gari wewe , umeona sasa umemgonga baba yangu na kumvunja mguu , utafidia vipi?”Aliongea

Irene alikuwa katika hali ya hofu mno, kiasi kwamba machozi yalikuwa yashaanza kujitengeneza katika macho yake.

“Sikumuona , ngoja nimpeleke hospitalini”Aliongea

“Haina haja , nitampeleka mwenyewe , unachopaswa ni kutoa hela ya matibabu na fidia , huyu anaenda kulazwa , pamoja na dawa na kumuona daktari ni milioni moja, utanipa na namba kama haitoshi nitakupigia simu”Aliongea yule bwana.

“Milioni moja!!”Aliongea Irene kwa mshangao mkubwa akiwa haamini , lakini kutokana na hofu alijikuta akikosa namna , palepale alikumbuka alikuwa na kiasi cha milioni moja alichotumiwa na Hamza kwenye akaunti yake , ijapokuwa ndio hakiba yake ya pekee lakini aliona haina jinsi, lakini dakika ileile Hamza alimshika mkono kumzuia.

“Acha kuwa na haraka ya kumpa alichokuambia”Aliongea Hamza na kumfanya Irene kumwangalia kwa maswali.

“Hey! Unaombaje milioni moja bila hata ya kufikiria?”Aliuliza Hamza na kumfanya yule bwana kumwangalia Hamza akiwa na usiriasi mkubwa.

“Wewe ni nani kwake? Yaani amemvunja Baba mguu halafu milioni moja ya matibabu imshinde au mnatudharau kwasababu tunaonekana masikini?”

Watu waliokuwa katika eneo hilo , baadhi walionekana kusikitika na wengine walionekana kuamini kile ambacho kimetokea, lakini hakuna aliengilia zaidi ya kuangalia tu kinachokwenda kutokea.

“Umenielewa vibaya , mimi naona milioni moja haitoshi, kuvunjwa mguu gharama yake ni zaidi ya milioni moja ,angalau ungeomba hata milioni tatu”Aliongea Hamza.

Irene, Regina na Prisila mara baada ya kusikia kauli hio walijikuta wakihisi ni kama hawajasikia vizuri , yaani mtu ameomba milioni moja lakini Hamza anaongeza?.

Yule bwana alionekana kushangaa pia, yule mzee aliegongwa mara baada ya kusikia kauli hio alisahau kwanza kupiga makelele ya maumivu , alishindwa kujizuia na kuona leo wameokota dodo kwenye mwembe kwa kukutana na mjinga.

“Wife unatembea na Cheque?”Aliuliza Hamza akimwangalia Regina na tabasamu.

Ijapokuwa Regina hakuwa akielewa Hamza alikuwa akipanga kufanya nini lakini aliitikia ndio alikuwa akitumia pia kulipa kupitia cheki , hivyo aliingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa kitabu kidogo.

“Unataka cheki ya shilingi ngapi?”

“Milioni tano inatosha”Aliongea Hamza.

Regina hakuongea chochote na palepale aliandika Cheki ya milioni tano na kumpatia Hamza.

“Nadhani unajua kutumia Cheki , ukienda benki ukionyesha tu utapewa milioni tano”Aliongea Hamza na kisha aliweka cheki ile kwenye mkono wa yule bwana wa makamo.

Mwanaume yule wa makamo alionekana alikuwa akijua cheki ni nini na wakati wa kuipokea mikono ilikuwa ikimtetemeka , ukweli mpango wake ilikuwa ni kupata milioni moja tu lakini ghafla tu huyo muungwana anampatia milioni tano bure bure tu, alijiuliza huyu malaika ametokea wapi mbona ghafla sana.

“Unaonekana kuwa muungwana sana mkubwa, Asanteni”Aliongea yule bwana baada ya kupokea ile cheki na kumsogelea yule mzee na kumnyanyua lakini Hamza alimzuia.

“Usiwe na haraka , milioni moja ulioomba ilikuwa ni ya mguu mmoja wa baba yako uliovunjika , ila nimeongeza milioni nne jumla maana nataka kumvunja na huo mwngine , jumla itakuwa milioni mbili , milioni tatu ni bonasi”Aliongea Hamza

“Ahhhh!!”

Yule Mzee aliekuwa amejilaza chini baada ya kusikia kauli hio alishituka kwa mshangao mkubwa.

“Unasema unapanga kufanya nini?”Aliuliza yule mwingine wa makamo.

“Bro huelewi kiswahili , hakuna hela inayopatikana kirahisi hivyo, baba yako umekadiria mguu wake thamani yake ni milioni moja , nimeongeza hela hivyo nitamvunja na mwingine”

“Mkuu acha ukichaa”

“Usiwaze , hata unikataze nitamvunja tu mguu , hakuna namna , isitoshe hela yangu umepokea tayari”Aliongea Hamza na haraka sana aliingia katika gari ya Irene na kukanyaga pendeli ya kuongeza mwendo.

Yule bwana mara baada ya kuona tukio hilo hakutaka kumjali tena yule mzee pale chini na alitimua nduki.

Hamza na yeye alishuka haraka haraka na kuanza kumfukuza na ndani ya sekunde kumi tu alikuwa ashamfikia na kumpiga mtama na kudondoka chini na kisha alimshika mkono na kuupindisha kidogo tu na kuuvunja na kumfanya atoe yowe la maumivu.

Muda ule yule Mzee mara baada ya kuona tukio hilo alisimama na kutaka kutimua nduki lakini alizuiwa kwa mbele na jamaa mmoja na kukaslishwa chini.

Kitendo kile cha kusimama bila maumivu kiliwafanya waliokuwa wakiangalia tukio hilo kushangaa , na kuona kumbe yote yalikuwa na maigizo.

Hamza alimsogelea yule mzee na kumwangalia na alionekana akitetemeka mno.

“Yule sio mtoto wangu , naomba msinifanye chochote , aliniambia niigize tu”Aliongea akijitetea.

Hamza hakumjali tena na alimpa ishara yule bwana aliemshikilia kuachana nae na kisha aliwarudia Regina na Irene.

“Walikuwa wakidanganya?”Aliuliza Irene.

“Ni matapeli , kesi kama hizi zipo sana , muda mwingine ili kuwa salama barabarani unapaswa kuweka Kamera itakuokoa kwenye matukio mengi”Aliongea Hamza.

“Bora tumekuwa pamoja , la sivyo ningetapeliwa”Aliongea Irene.

“Hey ! Ongea maneno ambayo mke wangu hatayaelewa vibaya”Aliongea Hamza.

“Maneno gani , si naongea ukweli?”

Prisila pia ambae alikuwa kimya muda wote pembeni ya Regina alikuwa na mwonekano usio wa kawaida.

“Irene muda unaenda tuondoke sasa”Aliongea huku akilazimisha tabasamu na Irene palepale alikumbuka kuna magari aliozuia kutosogea nyuma na haraka aliingia kwenye gari.

Dakika chache tu waliingia katika mgahawa wa Mama Rahabu na mara baada ya kukaa chini kila mmoja aliagiza kile alichokuwa akihitaji. Mgahawa huo licha ya kuwa mdogo lakini chakula chake ni kitamu ndio maana Irene aliuchagua.

“Dada Regina mtu tajiri kama wewe kuingia katika mgahawa mdogo kama huu , hujisikii vibaya?”Aliuliza Irene.

“Kawaida tu , sijali ukubwa wala udogo wa mgahawa , ili mradi usafi na chakula kizuri”Aliongea Regina.

“Ndio maswali gani hayo ? Mke wangu ni mtu humble sana , hana maringo licha ya kujaliwa utajiri na urembo”Aliongea Hamza hakutaka kusahau kujichukulia pointi ndogo ndogo.

“Hehe … ukweli ni kwamba kadri mtu anavyokuwa tajiri ndio anavyoona mambo mengi hayana maana , ukiona tajiri anajali sana kujionyesha jua ni tajiri mwenye moyo wa kimasikini”Aliongea Selina kwa kingereza na Prisila mara baada ya kuona Profesa alikuwa akielewa lugha ya kiswhaili licha ya kushindwa kuongea alitabasamu.

“Profesa unamaanisha nini kuongea hivyo?”Aliuliza Irene.

“Nilishakuambia soma kwa bidii , unaona sasa unashindwa kuelewa maana rahisi katika maneno yake”Aliongea Hamza huku akisimama na kumfanya Irene kumwangalia.

“Unaenda wapi?”

“Naenda msalani , punguza maswali”Aliongea Hamza.

“Na mimi naenda”Aliongea Irene akisimama huku akishika mkoba wake.

Mara baada ya kusikia msichana huyo anataka na yeye kwenda chooni alishangaa kidogo na kuona ni ghafla sana , lakini hata hivyo hakujali na kuondoka.

Lakini sasa wakati wanaingia upande wa chooni , kutokana na mgahawa huo kuwa na eneo dogo , choo chake kilikuwa hakina mgawanyiko wa upande wa wanawake na wanaume.

Hamza kabla ya kuingia chooni alimpa ishara Irene kutangulia kwanza ndio kisha yeye aingie.

Lakini sasa muda ule , Irene ghafla tu alimrukia Hamza na kuanza kumkisi na kutokana na Hamza kuwa mrefu alijikuta akiishia kumkisi shingoni.

Hamza alikuwa ni kama amepigwa na radi maana shambulizi hilo hakulitegemea , kitendo cha harufu ya marashi ya kike kuingia kwenye pia zake alijikuta akizidi kuzubaa.

Kilichomchanganya Hamza ni kwamba Irene alikuwa mtundu mno , ni kama alikuwa akipanga tukio la namna hio muda mrefu.

“Wewe hebu ni.. Damn it..”Muda ambao Hamza alitaka kumsukuma Irene kumtoa kwenye mwili wake , ghafla tu aliweza kumuona Regina akisogea upande wa vyooni.

Hamza palepale aliamini Regina akiona kinachoendelea , hata kama Irene ndio msababishaji moja kwa moja Regina atamfikiria vibaya , hivyo bila ya kuchelewa alimshika Irene kiuno na kuzamia chooni kujificha.

Regina yeye pia alikuwa na wasiwasi muda mrefu na alitaka kuja kujisaidia , lakini mara baada ya kusogea alishangaa baada ya kuona kuna bafu moja tu.

Mwanamke huyo aliishia kusimama nje ya mlango na alishindwa kujizuia na kushangaa , akijiuliza kama choo ni kimoja Hamza na Irene wameingiaje?

Muda huo Irene nyege zilikuwa zimempanda mno baada ya kukumbatiwa na Hamza , aliinua kichwa chake juu na kumkisi Hamza mdomoni.

Hakuna aliejua msichana huyo mbinu hizo kajifunzia wapi , lakini hata hivyo ilieleweka , wasichana wa umri wa Irene walikuwa wakijua mambo mengi na vitendo vyake viliamsha moto kwa upande wa Hamza

Hamza alikuwa na wasiwasi mno , alijua fika Regina alikuwa nje ya mlango akisubiri na ukweli hakutaka kukamatika kabisa akiwa katika hali ya kutilia shaka na Irene.

Lakini kadri alivyokuwa akikaa hivyo ndio ambavyo Irene alikuwa akimletea utundu na kumfanya kushindwa kuongea chochote kwa kuogopa kusikika kwa nje.

Hamza alijiambia kama akikamatwa ni sawa na kuvuka mto akiwa na matope maana hatojua namna ya kuyasafisha tena mpaka atakapofikia mto mwingine na pengine ingechukua muda.

Wakati akiwa anawaza , upande wa Irene alianza kuonekana kulegea kutokana na joto la mapenzi kumvaa na alianza kutoa sauti wakati wa kupumua.

Sauti hio pamoja na marashi yake ilimfanya Hamza moyo wake kwenda mbio mno na bila ya kujijiua mkono ulijikuta ukianza kutalii katika mwili wake .

Irene mwanzoni alihofia Hamza angemkasirikia na kumsukuma mbali lakini mara baada ya kuona Hamza anatoa ushirikiano alijikuta akizidi kuloa na kuanza kuongeza mashambulizi.

Upande wa Hamza mawazo yake yalimpeleka siku ile Irene alivyokaa uchi mbele yake na alivyojaribu kuvuta picha ile uvumilivu ulianza kumpotea.

Lakini hata hivyo hata kama angekuwa na hisia vipi , kama mwanaume asingefanya kitu chochote ilihali Regina alikuwa nje akisubiri maana ingekuwa ni kitendo cha kumdharau mno Regina.

Ukweli kila kitu kilitokea haraka sana na aliona kwa umri wa Irene pengine alichojua ni hisia zake tu lakini hakujua kuna mambo hakuelewa.

Muda huo wakati akikosa cha kufanya hatimae walisikia sauti ya mhudumu ikimwelekeza upande mwingine wenye vyoo na Regina aliondoka na kumfanya Hamza kupumua sasa.

“Irene hebu acha kuwa hivi”Aliongea Hamza akimtoa Irene ambae moto ulikuwa umekolea na mara baada ya kusikia kauli hio alishangaa na kumwangalia Hamza.

“Inamaana hupendi au utundu wangu hautoshelezi”Aliongea na sauti ya pua.

“Hapana , simaanishi hivyo”Aliongea Hamza huku akijisi maumivu ya kichwa yakimnyelemela.

“Nimeona kwenye muvi na inaonekana kufanya kimasikhara kuna noga”Aliongea na kumfanya Hamza kukosa neno , kumbe yote yanayomtokea Irene alionekana kujipanga muda mrefu.

“Irene sisi ni marafiki , hatuwezi kufanya unachotaka”Aliongea Hamza

“Sitaki kuwa na urafiki na wewe mimi , nakupenda na unajua”Aliongea Irene akimwangalia Hamza kwa macho ya hasira.

Hamza alijikuta akishangaa maana hakutegemea mwanamke huyo angekuwa muwazi mno na hisia zake na kumfanya kukosa namna ya kujitetea , hata hivyo Hamza hakuwa mjinga , alikuwa akijua hisia za Irene muda m refu tu.

Lakini siku zote alimuona Irene kama mdogo sana , ijapokuwa ki umbo Irene alikuwa mkubwa bado alihisi ni mdogo.

Hamza alishindwa kujua namna ya kumjibu kuhusu kujielezea hisia zake , aliona akimwambia hampendi anaweza akatibua hewa na akisema anampenda atakuwa anazidi kumkosea Regina.

“Irene wewe bado umri wako ni mdogo , subiri kwanza uingie chuo kikuu na tutaongea kuhusu hili , pengine unaweza kukutana na kijana Handsome na ukanisahau”

“Hebu acha kunifanya mtoto , nazijua hisia zangu vizuri tu”

“Wewe huoni kwamba nimeoa na pia mimi sio mwanaume mzuti kama unavyodhani”Aliongea.

“Mimi sijali , kwanza najua una mwanamke mwingine tofauti ya mkeo ? mimi bado mdogo hata mkeo akijua hawezi kunichukia”Aliongea

“Sijui unawaza nini , kwa umri wako na uzuri sio ngumu kupata mwanaume anaefaa zaidi yangu ambae yupo single , kuna haja ya kuning’ang’ania mimi mume wa mtu?”

“Sitaki wanaume wengine, nishakuona wewe , kama hunipendi sema , kwani mimi nina kasoro gani , mbona najiona ni mrembo tu”Aliongea kwa kulalamika huku akionyesha kutaka kulia.

Licha ya mrembo huyo kuonyesha kuwa siriasi lakini Hamza alipata uzito mno wa kumkubalia , alijiambia kama angekuwa ni kipindi cha nyuma pengine angemkubalia bila kuwaza sana , lakini wakati huo Regina alikuwa akiumiza kichwa chake.

“Sikia Irene tuachane na hili kwanza na punguza munkari , huoni kama unajikosea mwenyewe”Aliongea Hamza.

Irene hakumjibu na haraka alipeleka mkono na kwenda kushika mkuyenge wa Hamza.

“Hey.. wee…”Hamza alijikuta akipagawa , hakujua Irene angekuwa na ujasiri wa kumshika huko.

“Muone sasa ulivyotunisha , unaonekana kabisa una hisia na mimi na unajifanyisha tu kuwa mtakatifu! Tufanye hapa hapa bafuni , ukikataa natoka na kumwambia Regina unataka kunibaka”

Mara baada ya Hamza kusikia hivyo alijikuta akikamaa mwili , ukweli asingeweza kumfanya chochote Irene kwa muda huo na kama kweli akiongea vilevile asingejua kujielezea , wazo pekee lililomjia muda huo ni kumtuliza kwa muda

“Basi sawa , ngoja nikuahidi kitu”

“Uni ahidi nini , mimi nataka ukubali tuwe wapenzi sitaki ahadi”

“Hey , hakuna haja ya kunishurutisha hivyo”

“Ndio ukubali sasa”

“Sawa nimekubali”Aliongea Hamza huku akilazimisha tabasamu.

Irene mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akitabasamu na palepale alimkumbatia Hamza kwa nguvu.

“Nimefurahi sana , sitaogopa chochote kwanzia sasa , Sikujua namna nilivyokupenda mwanzo lakini leo nilijua ni kwa jinsi gani nakupenda baada ya kunisadia kupata haki yangu na kutotapeliwa , Hata kama umeoa nashindwa kujizuia na kutaka tu kuwa na wewe”

I(japokuwa maneno hayo yalikuwa mepesi sana , lakini yalitoka moyoni kabisa kwa Irene

Irene hakuwa mtundu tu pia alikuwa muwazi kwa kile alichojisikia , akihisi kulia analia , akihisi kucheka anafanya hivyo , ndio tabia yake , pengine ni kutona na aina ya makuzi yake.

Hamza mara baada ya kusikia maneno hayo ya kimapenzi , jasho lilimtoka , aliona haijalishi ni kwa namna gani msichana huyo anampenda lakini hakuwa akitosha katika maisha yake.

“Basi sawa , nimekuelewa , osha uso wako vizuri na uniache nijisaidie la sivyo tutafikiriwa vibaya’Aliongea Hamza , hakutaka kujisahaulisha juu ya Regina aliekuwa nje.

“Kwahio naweza kukuita Babe tukiwa wenyewe tu?”

“Kuna haja ya kuitana Babe”

“Ndio , rafiki yangu anamwita mpenzi wake Babe”

“Hapana niite tu Hamza , inatosha”Aliongea na kumfanya kuguna ila alitingisha kichwa kukubali.

Hamza alikuwa na wasiwasi mno , aliogopa Irene kuja kufa na kuoza juu yake na yeye kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Lakini wakati mmoja Hamza alijihisi kama ikitokea Irene akatokea kumpenda mwanaume mwingine , angejisikia vibaya.

Hamza ilibidi kuharakisha kujisaidia ili watoke kurudi walipowaacha wenzao , lakini cha ajabu Irene hakuangalia pembeni baadala yake alisogea mbele akitaka kuona dudu ya Hamza.

“Unafanya nini?”

“Nataka kuangalia mali yangu kama ni kubwa sana au ni ndogo”Aliongea lakini Hamza hakuwa tayari kumruhusu kuona kiungo chake.

“Sikia Irene , kama unataka tuendelee kama unavyotaka basi sikiliza ninachokuambia”Aliongea Hamza akiwa siriasi.

“Mimi nimekuonyesha kila kitu kwanini unakataa mimi kuona”Aliongea huku akivuta mdomo wakati huo akisogea mbali.

Mara baada ya kumaliza haja zao , wote kwa pamoja walitoka nje , Hamza muda huo alikuwa makini mno kama ametoka kuiba hazina ya kanisa, alijifanyisha alikuwa ametokea nje.

“Mbona mmechukua muda mrefu sana?”Aliuliza Serena.

“Kulikuwa na choo kimoja , nilimuacha Irene akitumie mimi nikaenda nje”Aliongea Hamza kwa utulivu kabisa.

Regina alimwangalia Hamza na kisha akayageuza macho yake kwa Irene na hakuongea kitu.

Mara baada ya chakula kuandaliwa Hamza alijituliza na kuweka umakini wake kwenye kula , lakini alijikuta akianza kukosa amani baada ya kuona Regina alikuwa akimwangalia na macho yasiokuwa ya kawaida.

Hata Prisila alionekana kumwangalia Hamza na ni kama kuna kitu alichoona na alijikuta akimwanngalia Regina na kisha akamwangalia Irene na alionyesha hali ya kusikitika kama mtu ambae hajaridhishwa na jambo.

Katika kundi hilo la wanawake ni Irene tu pekee ambae alikula kwa furaha zote huku kila mara alikuwa akimwangalia Hamza na kutabasamu.

Mara baada ya chakula , Hamza aliendesha gari pamoja na Regina kurudi nyumbani , wakati akiwa njiani ujumbe uliingia kupitia Watsapop.

“Kwanzia sasa tutakuwa tunachati kila siku na kuambiana maneno mazuri ya kimapenzi , tuonane angalau mara mbili kwa wiki la sivyo nitakuja nyumbani kwako”

Hamza mara baada ya kusoma ujumbe huo , alijiambia kwa staili hio atajikuta akishindwa kufanya mambo mengine na kazi yake itakuwa ni kutuma meseji tu, maana Eliza alikuwa akidai , Yonesi , Dina na vilevile Yulia , ilikuwa afadhali kwa Yulia alikuwa bize mno na anapenda kulala sana.

“Wife kesho ni sikukuu ya Iddi nataka nikununulie zawadi , unaonaje tukienda shopping kesho?”

“Sina shida”Alijibu Regina.

“Upo sahihi , isitoshe una miliki maduka ya nguo mengi tu , kukununulia zawadi ya kukuridhiisha ni kazi kweli kweli , hivi kuna kitu unakosa kweli?”Aliongea Hamza.

“Sina ninachokosa , hivyo huna haja ya kuwaza sana”

“Kwanini nisiwaze , unajua mke wangu nina jina la Kiislamu na kesho ni sikukuu yangu ya kwanza tukiwa pamoja , naona ni vizuri kukupatia zawadi itakayokufanya kuwa na furaha”Aliongea Hamza.

“Kuwa na furaha?”

Regina mara baada ya kusikia kauli hio ya furaha , sura ilijikunja kama amelamba ndimu na ukauzu ulizidi kumvaa.

Mara baada ya kupita Daraja la Kigamboni na kufikia sehemu ambayo haikuwa na watu Regina alimwambia Hamza asimamishe gari.

“Simamisha gani”Aliongea na kauli yake ilimfanya Hamza kushangaa na kujiuiliza kwanini anataka asimamishe gari.

“Wife , unataka kufanya nini?”

“Nimekuambia simamisha gai”Aliongea Regina kibabe bila ya kuelezea ni kipi anataka kufanya na Hamza alijikuta akikosa jinsi na kusimamisha gari.

“Toka nje na nitaendesha mwenyewe”Mara baada ya kuonge alishuka na kisha kuzunguka upande wa dereva.

Hamza mara baada ya kuona namna Regina alivyobadilika na kuwa siriasi ghafla alichanganyikiwa maana hakujua kwanini amekuwa hivyo ghafla.

“Wife kwanini?”

“Shuka chini”Aliongea Regina akiwa siriasi mno na ukali juu.

Hamza alijikuta akishikwa na ubaridi , hakuwa ni kwa jinsi gani amemkasirisha Regina mpaka kuwa katika hali hio ghafla , alikosa jinsi na kuishia kushuka chini.





















SEHEMU YA 157.

Regina mara baada ya kuona Hamza ameshuka , palepale alipanda na kuwasha gari.

“Huna haja ya kurudi nyumbani , nenda popote unapotaka , sitaki kukuona nyumbani leo”Aliongea Regina.

“Regina nimekosea wapi mpaka umebadilika , hata kama unataka nife ni haki yangu kujua kwanza sababu ya kuniua. Ijapokuwa najua kweli nimekukosea mara nyingi lakini nafanya kila jitihada kukuomba msamaha, natamani kweli kukuona ukiwa na furaha”Aliongea Hamza aliamini kwenda na Regina kwenye mashindano na kisha kula pamoja chakula cha usiku ukaribu wao ungeimarika

“Kwahio unahisi nakunyanyasa au vipi?”Aliuliza Regina na kisha palepale alifumba macho kwa sekunde kadhaa kana kwamba anajilazimisha kuongea.

“Hamza una wanawake nje na sijali kuhusu hilo na unaweza kuwa nao unavyotaka kwasababu ni uhuru wako , lakini kama unaniigizia na unataka kucheza tu na hisia zangu nikuambie tu huwezi kufanikiwa , usinione mimi ni mjinga na naweza kusikiliza kila unachoongea”

“Ni lini nimekugizia? Nimejitahidi sana kukufanya kuwa na furaha lakini imekuwa tofauti”

“Kwahio unaona ili kunifanya kuwa na furaha ni kwenda dukani na kuninulia donati? Hivi unaniona mimi ni mtoto wa miaka mitatu kwenye macho yako , unadhani naweza kusahau kwa kula donati ulizoniletea na maisha yakaendelea?. Nimekupa nafasi na sio moja tu ili kufanya nyumba yetu iwe na amani angalau tukiwa pamoja lakini licha ya kusema unaomba msahama na unataka kunifanya niwe na furaha lakini hauniheshimu kabisa, yaani kila unachoongea wewe ni uongo”

Hamza alijhisi kichwa kumzunguka maana hakujua hayo yote yanatokea wapi.

“Regina niambie vizuri nielewe , ni kosa gani nimefanya ? Nimekuletea Donati kwasababu ni kitu unachopenda na sio kwamba ndio nimemaliza, halafu kama unachosema ni kweli sina nia ya dhati kukufanya kuwa na furaha , unadhani ningefanya juhudi yoyote?”

“Mimi najuaje kama sio kuniigizia? Mchana wewe na Serena mmeweza kuigiza na nikaamini kabisa kila mlichoongea kumbe kila kitu ni uongo , pengine una IQ kubwa kuliko mimi ndio maana unafanya uanvyotaka”

“Acha kubadilisha mada na niambie ni kitu gani nimekosea , huwezi kunitoa kwenye gari kirahisi tu halafu nikubali”Aliongea Hamza akianza kupandwa na hasira lakini Regina hakujali kabisa.

“Jiangalie kwenye kioo.. kisha ndio uanze kukasirika”Aliongea Regina na palepale alipandisha kioo na kuliondoa gari kwa spidi kubwa.

Spidi aliotoka nayo ilikuwa sio ya kawaida , ni kama hakuwa Regina na ilionekana wazi alikuwa akilitolea hasira gari.

Hamza alijikuta akiwa amesimama kama sanamu akijuliza kwanini amemuambia ajiangalie kwenye kioo , hakutaka kujiuliza mara mbilimbili na kutokana na eneo hilo hakuna kioo aliamua kujipiga picha na kuanza kuzoom sura yake na palepale alijikuta mwili ukimkamaa , eneo la shingo yake kulikuwa na alama ya busu la lipstick.

Hamza alijikuta sasa akiiamka kutoka usingizini na kukumbuka ndio maana Sio tu Reigna aliekuwa akimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida , bali hata Prisila.

Hamza alijikuta akijilamba kibao , ilionekana Irene alimuweka alama ya kiss na yeye hakujisumbua kujiangalia kwenye kioo muda ule , ijapokuwa ilikuwa tabia yake ya siku nyingi kutokujiangalia kwenye kioo , lakini aliona alikosa kuwa makini.Hamza palepale alijikuta akimpigia simu Irene.

“Wewe mtoto , umenifanyia makusudi sio , kwanini hukuniambia ulikuwa na lipstiki kwenye midomo yako?”

“Hehehe.. kabla ya kurudia mashindano nilipaka lipstick , wewe ndio ulikuwa mjinga kwa kutokujiangalia kwenye kioo , kwanini unanilaumu mimi?”

“Wewe…”Hamza alitaka kufoka lakini alijikuta akipaliwa na mate na alishia kukata simu palepale.

Muda uleule Irene alituma meseji.

“Babe jamani umetolewa kwenye gari nini , mbona nahisi kama upo njiani , niambie ulipo nije kukuchukua my babe”

“Acha kuniita Babe na nenda nyumbani”Alituma ujumbe Hamza na kisha palepale aliita Uber na kuanza safari ya kuelekea Kijichi kwa Dina.

Kama nusu saa tu hivi aliweza kufika na mtu wa kwanza kuonana nae alikuwa ni Lawrence ambae alimchangamkia sana huku akimkaribisha lakini akimwambia Madam Dina yupo na wageni.

Hamza alionyesha kushikwa na shauku na kauli hio na kutaka kujua ni wageni gani ambao Dina anakutana nao usiku hivyo alitembea na kuelekea upande wa ofisi yake.

Muda ambao anaingia aliweza kumuona Dina akiagana kwa kuepeana mkono wanaume wawili na mmoja ya wanaume hao mara baada ya Hamza kumwangalia alimtambua palepale.

Alikuwa ni Amosi mwanaume ambae alimfahamu wakati alivyokuwa akimdhalilisha Eliza na alishangaa kumuona eneo hilo.

Amosi pia macho yake yalichanua mara baada ya kumuona Hamza akiingia hapo ndani , lakini dakika ileile alikwepesha macho.

Upande wa mwanaume mwingine ambaye Hamza hakumtambua alikuwa ni Kanali Dastani.

“Miss Dina nadhani tutapata ushirikiano mzuri , wakati ujao tutakapofika hapa?”Aliongea Kanali.

“Falsafa yangu nikitaka kushirikiana na watu ambao siwaamini ni ile ya Give and take , mkizingatia kanuni hio ushirikiano wangu utakuwa mkubwa”aliongea Dina na palepale aliwapotezea na kumsogelea Hamza na kumkumbatia.

Tukio lile wote waliliona lakini hawakuwa na maneno zaidi ya kutoka nje.

“Darling nimekumisi”Aliongea Diua huku akimwangalia Hamza na macho ya kulegea.

“Leo mimi ni wako mpaka unikinai”Aliongea Hamza huku akitabasamu na kwenda kukaa kivivu kwenye sofa.

“Huyu bwana niliemuona hapa ni kama amebadilika hivi?”Aliongea Hamza.

“Unamaanisha yupi?”

“Huyo mwembaba kidogo! Unakumbuka kipindi kile nilichompa kazi Lawrence kwenda kumuogopesha ili aache kumdhalilisha Eliza”Aliongea Hamza na kumfanya Dina sasa kujua Hamza alikuwa akimlenga Amosi lakini bado kauli yake ilimfanya kushangaa.

“Kwanini unasema anaonekana kubadilika?”Aliuliza na kumfanya Hamza kuonyesha vidole vitatu katika kama ishara.

“Nimefunguliwa jicho la tatu , naona kabisa kuna kitu kimebadilika katika mwili wake , ila sijui ni kitu gani”Aliongea.

“Amosi nilikuwa nikimjua muda mrefu , alikuwa mwanajeshi kabla ya kuitwa usalama wa Taifa , alifanya kazi kwa muda mrefu na kustaafishwa ila kustaafu kwake ilikuwa Cover tu”Aliongea Dina huku akianza kuandaa chai kwa kuchanganya na majani anayoyajua na kumfanya kuonekana kupendeza mno katika macho ya Hamza.

“Kava! Unamaanisha ni jasusi kivuli ama?”

“Ndio , Amosi ni Agency Liason officer cheo ndani ya idara maalumu inayounganisha vitengo vitatu katika usalama wa Taifa yaani TISA , TIMISA na Malibu, anaweza kufanya misheni yoyote bila ya kujalisha ni idara gani yupo, Mwenzake yule ni mwanajeshi cheo cha Kanali ni Senior Overt Agent idara ya upelelezi ndani ya Malibu”Aliongea Dina na muda ule alichukua kikombe na kumpatia Hamza.

“Kuna upelelezi gani unaendelea , naona ni kama kuna kitu wanataka kutoka kwako?”.

“Kuna Mwandishi wa habari mmoja ambae alikuwa ni Covert Agent ,alipotea katika mazingira ya kutatanisha wakati akiwa katika majukumu yake ya kazi , katika moja ya nyaraka ambazo babu ameniachia , niliweza kugundua kuna utata katika kupotea kwake , kitengoni wanaamini amekufa lakini katika rekodi ilioachwa na babu inaonekana hajafariki. Huyu mwandishi ni mtoto wa Madam”

“Madam! Unamaanisha nani?”

“Ndio! Nadhani hujawahi kusikia , Madam ni cheo cha heshima kitaifa kwa mwanamke ambae amekuwa na mchangao mkubwa kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla, ni cheo kikatiba lakini ni mtu mmoja tu amekishikilia na ni rais mstaafu wa kike wa kwanza nchini kuongoza Tanzania”Aliongea Dina na palepale Hamza alimjua.

“Tuachane na hayo kwanza, unaondoka saa ngapi hapa?”Aliongea Hamza na kumfanya Dina kutabasamu huku akimkonyeza.

Tunaweza kuondoka hata sasa hivi”Aliongea.

*****

Upande mwingine , wakati Mkuu wa Majeshi akiwa nyumbani kwake alipokea simu ya usiku usiku kutoka kwa Afande Himidu.

“Niambie Afande , ni mara chache kupiga simu muda huu”Aliongea Afande Simba.

“Simba nimekupigia simu kukutaarifu Nyakasura ameondoka kuelekea Dar es salaam”Aliongea Afande Himidu na kumfanya mkuu wa majeshi mwonekno wake kubadilika kidogo.

“Amekuambia anaenda kufanya nini?”

“Kasema anaenda tu kutembea tembea . Nimekupigia kuuliza kama kuna ulazima wa kumwekea mtu wa kumfuatilia nadhani na wewe unajua huyu msichana sio mwepesi”Aliongea

“Mtu wa kumfuatiuilia? Nani anaweza labda niende mwenyewe ndio anaweza asijue anafuatiliwa . Wewe achana nae ili mradi hakuna kitakachotokea hakuna haja ya kuwa na wasiwasi”Aliongea na Himidu alitingisha kichwa kukubali.

******

Upande mwingine muda huo huo Kanali Dastani alionekana ndani ya gari aina ya Toyota Discovery nyeusi akiwa ameegesha gari hio ndani ya maegesho ya Club ya Wavuvi eneo la fukwe ya coco.

Ndani ya gari hio hakuwa peke yake , alikuwa na mwanamke na hakuwa mwingine bali ni Tresha Noah mchepuko wake.

“Dastani tokea uongee na Madam unazunguka zunguka , hutaki kunipa mrejesho”

“Nazunguka zunguka vipi Tresha?”

“Leo ni siku ya ngapi tuokea uonane na Madam?”Aliongea huku akionekana kuwa siriasi.

“Kwahio unahisi kuchelewa kwa sisi kuonekana ni kama nakukukwepa , au sikuamini . Tresha unapaswa kuelewa kabla ya sisi kuwa na uhusiano wa karibu na kushirikiana , lakini mimi pia ni Ajent wa kitengo cha Malibu , unaweza usitambue hili ila kila ninachofanya kinafuatiliwa”Aliongea lakini hata hivyo haikumfanya mwanamke huyo kuridhika.

“Usiongee sana , nipe habari namna maongezi yalivyoenda na kwanini mkaonana na Dina leo?”

“Ni kama nilivyotarajia?”

“Unamaanisha nini?”

“Madam pia anaonekana kujua Sedekia hajafariki?”Aliongea na kauli ile ilimshangaza kidogo Tresha.

“Unataka kusema kwamba , Mgweno alikuwa akijua hili na ndio gia aliotumia kumtaka Madam afanye vile ambavyo anataka , kama vile kuonana na Mzee wa Taifa?”Aliuliza Tresha.

“Upo sahihi Mgweno anaonekana anajua mengi sana kuhusu kesi ya Radi mkoani Rukwa , si hivyo tu anajua sababu ya kupotea kwa Sedekia”Aliongea na kauli ile ilimfanya Tresha kukunja sura.

“Ni sababu gani ambayo imemfanya kupotea?”Aliuliza kwa shauku.

“Mpaka sasa Madam anachojua ni kwamba Sedekia yupo hai , Kuhusu Sedekia alipo haijulikani na Mheshimiwa hajaongea chochote na inaonekana Mstaafu anatumia taarifa hii ili kusukuma mipango yake , hivyo hataki kutoa taarifa yote , Madam ameweza kupata taarifa hii kwa kumsaidia Mgweno kuonana na Mzee wa taifa pekee”

“Kwahio anachojua tu ni Sedekia yupo hai , lakini kuhusu alipo au sababu ya kupotea kwake hafahamu na Mgweno anataka kumpatia taarifa kidogo kidogo kadri atakavyokuwa anamsaidia”Aliuliza na Kanali Dastani aliishia kutingisha kichwa.

“Kwani Eliasi alitaka nini kuhusu swala hili la kuongea na Mzee?”

“Kuhusu hilo ni ngumu kufahamu , maongezi kati ya Mgweno na Mzee Wa taifa yalikuwa ya siri sana na hata Madam hakushiriki hivyo hafahamu chochote , nimeongea na Mstaafu Eliasi kanipa maagizo mengine na ndio yalionipeleka kwa Dina”Aliongea .

“Kuhusu nini?”

“Bado sijajua , ila kaniambia nipate faili ambalo Mgweno alimuuzia Babu yake Dina , faili lenye Codename ya Mshua , Eliasi anasema nikipata hili faili nitajua nini cha kufanya baada ya hapo”Aliongea.

“Mshua! Unamaanisha huyu Dina analo hili faili?”Aliuliza Tresha kwa msahngao kidogo.

“Chatu sio mtandao wa kihalifu tu wa usafirishaji , lakini vilevile ni mtandao u lioojengwa katika msingi wa kuhifadhi nyaraka za siri, Babu yake Dina alikuwa akifanya biashara ya kununua Siri katika ushahidi wa nyaraka ndio maana mpaka leo hii kitengo cha TISA kinashirikiana kwa ukaribu sana na Chatu , lengo sio kuufadhili huu mtandao ila ni kwasababu kuna kitu wanakitafuta , sijui ni kitu gani ila kuna kitu cha namna hio kinachoendelea”

“Kama ni hivyo mlivyoongea na Dina anasemaje kuhusu hili faili la Mshua”

“Sio kazi rahisi kulipata , linaonekana ni faili nyeti sana na Dina anataka faili lingine kubwa zaidi ya alilokuwa nalo ili kulitoa”

“Shenzi sana yule M*laya! Anachotaka ni kitu cha thamani ya juu zaidi , mpaka hapo kazi ishaingia ugumu. Kwahio unafanyaje kuhusu hilo?”.

“Kuna namna Mstaafu Mgweno anajua kuhusu kilichomo ndani ya hli faili , Madam kanisisitiza nifanye kazi kwa umakini , hataki kutii maagizo yoyote kutoka kwa Mgweno kama mtumwa hivyo anataka nipate ufumbuzi wa alipo Sedekia kwanza”

“Sidhani kama itakuwa rahisi , kumbuka ni baada ya miaka mingi ndio tunajua leo Sedekia yupo hai , kuna kubwa linaloendelea na ni ngumu kufungua code zote”

“Najua sio rahisi sisi wenyewe tukitafuta , lakini siku zote kadri swala linavyokuwa zito anaelibeba itafikitia wakati wa kuelemewa , ni muda mrefu Sedekia amepotea mpaka tukaamini amefariki lakini tunajua sasa kama yupo hai , hizi ni dalili za kulemewa . Ninachokwenda kufanya kwanzia sasa ni kuliongezea uzito zaidi hili swala , ili yoyote ambae amelibeba alitue”Aliongea na kumfanya Tresha kumwangalia Dastani kwa macho ya shauku.

“Kivipi!?”

“Secret amplification strategy! Kwasasa huwezi kuelewa ila utaona kitakachotokea. By the way kwa muda mrefu uchunguzi zidi ya kanisa la Wabrazili ulikuwa umesitishwa , nimesikia tetesi umeanzishwa upya”Aliongea.

“Nilijua tu lazima iwe hivyo’Aliongea Tresha.

“Kwanini?”

“Rejea kilchotokea Mjini Kilwa, lakini tokea juzi nafikiria na nahisi kuna mchezo unafanyika”

“Unamaanisha kitengo cha kutuma waumini wengi kwenda Kilwa kufungua Kanisa inaweza kuwa ni chambo tu?”

“Kuna maeneo mengi ndani ya Tanzania ambayo pengine yana watu wengi na pili wapokeaji wengepatikana kurahisi , kwanini wakafungue Kanisa Kilwa , nahisi kuna walakini”Alionea na kumfanya Dastani kutingisha kichwa.

“Hio ndio moja ya sababu ambayo serikali imeamua kufanya uchunguzi upya . vipi kuna kitu chochote ulichopata kupitia yule mtu wetu?”Aliuliza.

“Bado ila napanga kumteka Alex bila Binam kutushitukia”Aliongea na kumfanya Kanali kushangaa.

“Tresha! Itakuwa hatari sana na teknolojia yao ya Jicho la Anga?”

“Najua”

“Sasa! Bado unataka kuendelea na mpango huo ili hali unajua utakuingiza kwenye matatizo?”

“Ni kwasabu nimechoka kuwa Cutout Agent. Katika kipindi changu nilichotumikia umoja wa watu wa BINAMU sijawahi kufanya kosa , nina maksi nyingi za kuniweka huru , Mpango wangu ni kuingia katika chumba cha Kurefusha Uhai”Aliongea na kumfanya Kanali macho kumtoka.

“Tresha unapenda sana njia za mkato , Chumba cha Kurefusha uhai ni teknolojia mbadala kwa ajili ya wale ambao hawawezi kuvuna nishati za mbingu na ardhi, kwanini unataka kuichukulia hatari mikononi ilihali kuna njia salma zaidi”

“Huna unachokijua Dastani?”

“Unamaanisha nini?”Aliongea lakini palepale hakumjibu na kushuka ndani ya gari kuelekea upande ya Wavuvi.

Nyakasura ndani ya jiji? Hamza anazidi kuyatibua kwa Regina.

ITAENDELEA AFTER CHRISTMASS. WATSAPP ME KWA MWENDELEZO ,NAMBA 0687151346
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…