Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDIHA AKII I ZETU.

MTUNZI SINGANOJR

SEHEMU YA 73.
Hamza mara baada ya kuona Regina ameshituka alirudi katika hali yake ya kawaida huku akijifanyisha hakuna kilichotokea.
“Kumbe tushafika?”Aliuliza Regina huku akijivuta.
“Ndio tumefika na nilikuwa nikijishauri hapa nikubebe au nikuamshe”
Muda ule Regina alijihisi ubaridi kwenye eneo lake la kifua na alijikuta akipeleka mkono na kugusa na palepale akikunja sura.
“Mbona nimeloa , haya maji yametokea wapi?”Swali hilo lilifanya uso wa Hamza kugeuka na kuwa wa bluu kama mtu aliekosa oksijeni kwa muda mrefu.
Lakini asingefanya chochote kwa wakati huo maana Regina alikuwa ashagusa tayari.
Kilichomchanganya zaidi Regina alikuwa na shauku ya kutaka kujua maji hayo yametokea wapi , hivyo mara baada ya kugusa alipeleka kidole puani na alijikuta akikunja sura kama vile amekula pilipili.
Licha ya kwamba Regina alionekana kuwa mwanamke ambae hajui mambo mengi lakini alikuwa na akili ya kutofautisha maji na mate., kunusa kidogo tu alijua ni mate ya mtu.
“Wewe .. wewe umenifanyia nini .. kwanini unatabia mbovu , hujawahi kuona mwanamke maisha yako yote?”
Regina alihisi ukichaa ulikuwa ukimpanda na hakujua ni kwanini anamuamini mwanaume mhenzi kama Hamza.
“Wife acha wasiwasi , mbona hakuna nilichokufanyia hebu angalia nguo zako vizuri”Aliongea Hamza na alivyosikia neno wife akili yake ilikuwa ikichemka kwa hasira na aliishia kumpiga Hamza na mkomba wake wa Hermes kwa hasira.
“Wewe ni kichaa… mtu wa kawaida hawezi nifanyia huu ujinga , nitakuonyesha leo”Aliongea huku akirusha mkoba kwa nguvu lakini kitendo kile kilimfanya kukosa balansi na kujikuta akitaka kudondoka kutoka kwenye Gari.
Hamza asingemuangalia tu mrembo huyo akidondoka na kujipigiza kwenye mlango hivyo kwa haraka alipiga hatua mbele na kumzuia asidondoke , lakini kilichotokea mkono wake uligusa sehemu ileile iliokuwa imeloa.
Dakika hio ni kama muda umegandishwa kutokana na ukimya uliotokea, ijapokuwa Hamza alitamani kuminya minya tena lakini alikuwa akiogopa Regina atakasirika zaidi na pengine mpaka kufukuzwa ndani ya hio nyumba.
“Regina sija.. sio makusudi , nimekuzuia usidondoke”Hamza alijikuta akigwaya huku akijitetea kwa kukosa kujiamini.
Regina upande wake alijihisi aibu kubwa alitamani kumpiga lakini alishindwa kuchukua hatua.
“Hebu niachilie kwanza”
“Nakuachia ila usije kunipiga”
“Hata nikupige si utakwepa tu”
“Hehe.. ni kweli”Aliongea Hamza na kumsimamisha vizuri.
Baada ya kutoka nje ya gari Regina uso wake ulikuwa umejaa aibu na hakutaka kabisa hata kumwangalia Hamza usoni kwani alitembea haraka haraka kuingia ndani.
Hamza aliishia kupumua kwa ahueni mara baada ya msala huo kumpita na kujiambia ni kheri kutafuta hela kuliko kudili na mwanamke kama Regina..
Hamza alijikuta akijitoa ufahamu na kujiambia kama atalala nae kitanda kimoja je ni raha kiasi gani atajisikia.
Kitendo cha kupata mawazo hayo alijikuta akitoa tabasamu na kujiambia leo lazima atupie swaga maana amechoka kula kwa macho , hivyo haraka haraka alipeleka gari Gereji kwa ajili ya kuligesha.
Wakati anaingia ndani alimkuta Regina akiwa jikoni akichangula changula friji akionekana anatafuta kitu cha kula.
“Mke nimeagiza chakula muda si mrefu kitaletwa huna haja ya kula hio mikate haitokushibisha””
“Halafu ni mara ngapi nakwambia usiniite na hilo jina lako”
Regina alijizuia tu kutomfanya chochote Hamza licha ya kukasirika kuitwa mke maana alijua hana uwezo wa kumpiga.
“Regina bado tu una hasira na mimi?”
“Kwanini niwe na hasira na wewe?”
“Kuna sababu nyingi za kuwa na hasira na mimi , swala la mimi kumuua mtu ,swala la Eliza na kilichotokea sasa hivi..”Aliongea Hamza akiona ni vizuri kuongea nae kuhusu hayo maswala.
“Mambo ya kuua mtu hayo ni maswala yako , wewe na Eliza kuwa wapenzi halinihusu, sio kama nina hasira ila sijisikii tu kujihusisha na wewe”
“Kivipi hutaki kujihushisha na mimi ilihali kisheria sisi ni mke na mume , hata bibi yako amenipa pete kwa ajili yako kama ishara ya mambo yangu ni mambo yako , haya ni mambo ya kifamilia”
“Hata kama bibi amekupa hio pete haimaanishi kwamba kihisia tutakuwa pamoja , karatasi ndio linasema hivyo lakini moyo wangu hapana , acha kuwa mjinga kwa kuendelea kuona unaweza kuwa mume wangu”
“Kwahio unadhani niliamua kuandikisha ndoa kwa ajili ya kucheza na wewe na kisha kila mtu kuchukua hamsini zake?”
“Labda , nikuulize swali unajua nini kuhusu mimi?”Aliongea Regina huku akionekana kuwa siriasi.
“Upande upi?”Aliuliza Hamza maana kuna baadhi ya vitu anajua na vingine hajui.
“Upande wote wa maswala ya kuzingatiwa kabla ya ndoa, unajua nini napenda na kipi sipendi , unajua napenda kula nini na kipi sipendi kula, unajua ni aina ya vitabu gani napendelea kusoma na vipi sipendelei , unajua nimesoma wapi na kumaliza wapi , unajua marafiki zangu wote, unajua mtazamo wangu wa kimaisha ukoje na ndoto zangu ni zipi ?”
“Nitajuaje hayo yote ilihali hatuna hata mwezi tokea tukutane?”
“”Ndio ninachomaanisha hapa , hatujajuana muda mrefu na unataka kulazimisha ndoa ya karatasi iwe ndoa ya kihisia , huoni kwamba ni kichekesho?, ni mchana tu hapa ulidhania nimempa Eliza gari kwasababu ya kutaka akuache ili niwe na wewe , kama kweli ungekuwa unanijua usingekuwa na mawazo kichaa ya namna hio”
Hamza alijikuta akinywea , ilionekana Regina bado alikuwa na kinyongo juu ya kumsingizia kumpa Eliza gari kwa ajili ya kumtuliza.
“Kwahio mimi kwangu hata kama uue mtu au au uwe mwizi siwezi kukasirika maana kama ni kukutana tumekutana kikazi, hivyo kama usivyonijua mimi na wewe pia sikujui, mimi ulieniona ndani ya siku hizi tulizofahamiana pengine sio mimi , kwanini nikuambie na wewe unionyeshe wewe ni nani?”
Hamza aliishia kukosa neno , hata hivyo aliona maneno ya Regina yalikuwa sahihi , ukweli ni kwamba hakuna anaemfahamu mwenzake na kwanini Regina ajali kile ambacho anafanya yeye.
Licha ya kwamba kuna mambo kadhaa yalitokea kati yao lakini yalikuwa katika msingi wa maswala ya mwajiri na mwajiriwa pekee na hakukuwa na hisia zilizohusika.
“Sikatai ni kweli umenisaidia mara kibao tokea tukutane iwe ni mimi au kampuni lakini ndoa ni swala linalojitegemea , usidhani kwasababu ya uwezo wako na koneksheni ulizokuwa nazo ndio inakufanya ujione una vigezo vya mimi kukubali, vipi kama ukanichukulia mimi kama mkeo kihisia na mwisho wa siku ukaja kugundua nilikuwa nikikutumia tu,utajisikiaje?”
Hamza alitaka kuongea neno lakini alikatishwa na simu yake ambayo ilianza kuita , alipoangalia aligundua ni mtu ambae alimwagiza kuleta chakula.
Hamza mara baada ya kwenda kuchukua delivety yake na kufungua mbele ya Hamza ilionekana aliagiza Doughnut za strawberry kwa ajili ya Regina.
Jambo ambalo lilimshangaza Regina maana hakutegemea kama Hamza angekumbuka kitu anachopenda kiasi hicho.
“Wewe umeleta nini?”Aliuliza Regina licha ya kwamba alikuwa ameona Hamza alikuwa ameagiza Dougnut.
“Licha ya kwamba tumeoana kikazi haimaanishi siruhusiwi kukujali , nimeagiza kitu unachopenda”Aliongea Hamza.
“Kumbe unaweza kuagiza hata Doughnut na kuletewa!?”
“Ulikuwa hujui kama unaweza kuagiza , hio simu yako ni ya nini sasa?”
“Ni kwasababu sijawahi kupata wazo la kuagiza ndio maana sijui”
“Basi usijali , kwanzia sasa nitakupatia namba ya mtu ambae unaweza kumuagiza muda wowote ukijisikia kula ngoja nikuonyeshe na akaunti yao ya instagram”Aliongea Hamza na alitoa simu yake na kwenda mtandaoni na kumuonyesha Regina picha za mgahawa ambao Doughnut zinapatikana.
“Nataka kula tambi”Aliongea Regina mara baada ya kuvutiwa na namna tambi zilivyokuwa zikivutia katika picha.
“Unataka tambi na sio Doughnut tena”
“ Nataka kula vyote kwa pamoja unataka nilalie Doughnut?”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka kidogo.
“Kama unataka tambi jaribu kuagiza , huu mgahawa haupo mbali na hapa tunapoishi”Aliongea Hamza huku akimpatia Regina simu yake.
Regina hajawahi kuagiza chakula kwa njia ya mtandao ndio maana hakuwa mzoefu , hio yote ni kutokana siku zote Shangazi anakuwepo.
“Nilivyokuwa kituoni, kipindi ratiba ikiwa ni ya kula tambi huwa tunakuwa na furaha kubwa, hapa nawaambia vipi wasiweke vitunguu”
“Hivi kwanini unachukia vitunguu namna hio?”
“Sipendi harufu y ake”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha kichwa
“Mtumie meseji tu mwambie asiweke asiweke vituunguu”
“Wewe hutaki tambi?”Aliuliza Regina na Hamza hakuona anaweza kula hizo Doughnut na kisha kulala hivyo alitingisha kichwa na wewe awekewe oda yake.
Hamza aliishia kumwangalia tu Regina namna ambavyo alikuwa bize kuandika meseji akiagiza chakula.
“Mimi naona kuwa mke sio kitu kibaya sana”
“Unamaanisha nini ?
“Licha ya kwamba hatujafahamina kwa muda mrefu , lakini najua unapendelea kula Doughunt kuliko kitu chochote , tena ambazo zina Strawberry, naendelea kukufahamu kwa spidi ya juu mno “
“Ni kimoja katika vitu vingi ninavyopenda sioni haja ya kujivunia”
“Mtu na mtu hawawezi kufahamina ndani ya muda mfupi , ni swala la kufahamiana kidogo kidogo , unaonaje tukijipa muda wa kufahamiana mdogo mdogo, nakiri kwasasa sikujui vizuri na pia wewe una maswali mengi kuhusu mimi , lakini sio sababu ya kutuzuia kuwa pamoja, huoni muda mwingine tulikuwa na furaha licha ya kutokufahamina”
“Unaongea nini , muda gani nilikuwa na furaha?”Aliongea huku uso wake ukiwa mwekundu.
“Sijui ila moyo wangu unaniambia kuna muda unaonekana kuwa na furaha kuwa na mimi, halafu kama unakumbuka vizuri wewe mwenyewe umesema huamini ndoa sio kwasababu hupendi kuolewa bali ni kutokana na kuipa ndoa thamani ya juu , lakini leo hii umekubali tuandikishe ndoa ya mkataba bila kunifahamu , hii inaonyesha mimi sio mtu mbaya kihiivyo,si ndio?”
“Hayo ni mawazo yako peke yako , mimi nimeamua kukutumia kwa malengo yangu kwasababu ulikuwa tayari kutumiwa”
“Ah!, kwahio muda wote ulikuwa unanitumia , kwanini huongea mapema sasa?”Aliongea Hamza huku akimshika Regina kichwa.
“Acha ujinga basi , kwanini unagusa kichwa changu?”Aliongea Regina huku akigeuka kwa hasira.
“Sio tu kukishika nataka pia kukipiga, maana kinafikiria sana hata vitu ambavyo havina maana , tunaweza kuwa hatufahamini vizuri kwasababu sisi sio wapenzi halisi lakini licha ya hivyo haimaanishi kwamba haiwezekani, kuna wenza kibao ndani ya dunia hii ambao wanapeana talaka kila uchao unadhani hawafahamiani vizuri, hisia na kufahamiana ni vitu viwili tofauti , kwasasa tunaweza kuchukulia kama tumeruka darasa kwanza kwasababu hatukuwa na muda na tulishalimaliza hivyo tunarudia darasa la nyuma , ukiona unsjisikia kunitaka nitatakika”Aliongea Hamza
“Nikiona nakutaka , acha kuota nani akutake?”Aliongea Regina huku akionyesha kukasirika
“Kwahio unamaanisha wewe unataka mimi ndio nikutak , kama unataka nikutake nitakutaka kweli”
“Achana kabisa na hayo mawazo, kama unataka kutaka watake wengine , sitaki unisumbue na kunitaka kwako”Aliongea Regina na kuchukua Doughnut na kwenda kujitenga mbali na Hamza .
“Hebu muone sasa , unaongea kwasababu unaona wivu , mimi naona moyo wako ushaanza kunipenda”
“Unaongea kila kinachokujia mdomoni kwasababu mshipa wa aibu huna, sasa wewe endelea kuongea ujinga uone hiki kisu nisipokididimiza kwenye mdomo wako”
“Basi wife yaishe , ngoja nikuwashie TV”
“Kwanini husikii , nishakwambia usiniite hivyo wewe”Aliongea Regina kwa ukauzu.
“Basi nitakuita Regina usikasirike basi ukazeeka mapema”Hamza aliamua aache kumtania zaidi maana aliona angeharibu , alijua kama Regina atatokea kupenda kweli basi itakuja kuwa ngumu sana kwa Eliza kuendelea nae.
Lakini kwa wakati mmoja aliona kitendo cha Bibi yake Regina kumlazimisha kumua Regina ilikuwa ni kama mtego kwake, licha ya kwamba hakujua alichokuwa akiwaza Bibi Mirum ni nini lakini hakuona ni jambo baya kuwa na mwanamke mrembo kama Regina kama mke wake.
Hamza alijisikia fahari kwani licha ya Regina kuonekana mgumu kuelewa lakini ilionyesha anaanza kumwelewa taratibu taratibu.
Baada ya lisaa kupita kila mtu aliweza kushiba tambi na Doughnut na kugawana vyumba kulala.
Upande wa Regina usiku alipata nafasi ya kufikiria tokea siku ambayo amekutana na Hamza na matukio yote mpaka kufikia siku hio , alijaribu kuhesabu siku na kuona zilikuwa ni siku chache mno lakini ilikuwa ni kama mwaka wamefahamiana , jambo hilo lilimshangaza maana hajawahi kumzoea mtu kwa haraka hivyo kiasi cha kugombana na kupatana ndani ya muda mfupi, mrembo huyo alijikuta akiingiwa na hisia mchanganyiko ambazo yeye mwenyewe hakuwa akizielewa vizuri , kutokana na kwamba ni kama mara yake ya kwanza kupatwa na hisia za namna hio.
*********
Aalto ni nchi inayozungukwa na safu za milima ya giza , ni mji maarufu zaidi kupitia jiji lake kubwa la kila fursa la Zaburi.
Huu ni mji wa Aderon , mji wa watu masikini ndani ya nchi ya Aalto , jina langu naitwa Luther , kazi yangu ni mbeba mizigo sokoni lakini sasa hivi sina kazi kutokana na kuugua muda mrefu.
Licha ya ufahamu wake kama Hamza ulikuwa ukifanya kazi lakini kwenye akili yake ni kama kuna fahamu mbili , fahamu moja ilikuwa ni ya Luther na ndio iliokuwa ikimwelezwa wapi alipo, zilikuwa ni hisia kana kwamba alikuwa na uwezo wa kujua kila kitu ndani ya eneo hilo asilolijua kutumia akili nyingine iliokuwa katika akili yake.
Hamza alijua yupo kwenye ulimwengu mwingine, ulimwengu ambao unaonekana katika ndoto , alikuwa akijua kabisa alikuwa akiota yupo ndani ya ulimwengu mwingine akiwa na sura tofauti,
“Huu ni ulimwengu mwingine , ulimwengu ambao miujiza na maajabu ni vitu vinavyoonekana kwa macho”Aliwaza Hamza akijua kabisa yupo ndotoni lakini nafsi yake ipo sehemu nyingine.
“Katika huu ulimwengu wanachoma watu wakiwa hai na moto wa ajabu”Aliendelea kuwaza muda huo akiwa katika kijumba ambacho alikuwa mwanzo baada ya kuachana na watu ambao aliwafahamu ni ndugu wa Luther ambae ameiba mwili wake kupitia ndoto.
Hamza alijikuta akijawa na shauku ya kujua vitu vingi kuhusu eneo hilo,baada ya kuingia kwenye chumba chake alisogelea maboksi ya mbao ambayo yalikuwa yamepangwa kwenye kona ya kijichumba hicho.
Licha ya kwamba akili yake ilimwambia yupo ndotoni , lakini alijihisi njaa kali , alikuwa akihisi njaa kali , njaa ambayo ni kama inamwambia hayupo ndotoni bali yupo katika uhalisia.
Hapana haikuwa akili yake iliokuwa ikimwambia ana njaa , ufahamu mwingine ambao ni wa Mzungu Luther ndio uliokuwa ukimwambia ananjaa na hata akili yake ilishindwa kufanya vizuri na kuendeshwa na njaa.
Mara baada ya kuchangula kwenye yale maboksi aliweza kuona kipande cha mkate uliokakamaa kama biskuti , aliangalia ndani zaidi na hakukuwa na kitu kingine zaidi ya sarafu zenye matundu katikati.
“Hizi ni sarafu kama zilizotumika Karne ya kumi na tano”Aliwaza huku akichunguza zile sarafu kwa macho ya uchunguzi , licha ya kwamba alikuwa ndotoini lakini akili yake pia ilikuwa ikimkubusha sio wa ulimwegnu huo , yupo kwenye ulimwengu huo kwa namna ya kutalii kupitia mwili wa Luther.
Baada ya kushika ule mkate mkavu aling’ata kipande ambacho kilianza kukatika mdomoni kama anakula mkaa ,akili yake ilikataana na ile radha na kujikuta akitema chini.
“Nini hiki , mbona kama nakula mkaa?”
Alijikuta akianza kuchunguza kile kipande kwa mara nyingine ili kuhakikisha ni mkate kweli .
Aliangalia kitu kingine kwenye lile Creti la mbao na aliweza kuona jiwe la kusagia(flint) na hakuchelewa alichukua na kuanza kuponda ponda ule mkate mpaka ukalainika na kisha akapeleka mdomoni na kuanza kula , lakini hakukua na radha yoyote na njaa ilikuwa kali.
“Hata kama nipo ndotoni siwezi kula kitu kibaya kama hiki , huu ni umasikini na siwezi kuishi katika huu umasikini, nataka kujifunza ile nguvu alioonyesha yule askofu na kuwa kama yeye , sijui kama nitafanikiwa .. hapana ile nguvu siitaki yule mwanamke alivyokuwa akiniangalia lazima aliona nina mafunzo ya kichawi katika uhalisia wangu licha ya kutokuwa katika mwili wangu halisi , nikijipeleka kwa ajili ya kujifunza ile nguvu ni kama kuwaambia wanichome moto”Aliwaza Hamza.
Licha ya kujihisi alikuwa kwenye ndoto , lakini moyo wake ni kama unamwambia kwamba hawezi kurudi tena , maisha yake yanaendelea kwanzia saa hio.
Wakati akijiwazia kwanini anaota ndoto ya namna hio katika uhalisia aliweza kuona kijitabu kidogo kilichokuwa pembeni ya kitanda na alisogelea na kukifungua ndani ili kujaribu kusoma.
Lakini kilichomshangaza alishindwa kabisa kusoma licha ya kwamba alikuwa akiona liugha ile ilikuwa ni ya kingereza, ni kama uelewa wake wa lugha ya kingereza ulipotea ghafla.
Hisia zilizokuwa zikimwambia hajui kusoma zilizidi kumuandama na kila alipokuwa akijaribu kufikiria ni kama anaanza kupoteza ufahamu wake na ufahamu wa Luther unamvaa.
Alijikuta akiacha kuwaza mara moja kwa hofu na kukisogelea kitanda kwa ajili ya kulala , lakini kabla hata hajapandisha miguu miguu yake iliguswa na kitu kilichomshitua..
“Panya!!”
Aliwaza mara baada ya kuhisi sauti upande wa pili, uijasiri wa Uhamza ndani yake ndio uliomfanya asihangaike na ile Panya , lakini muda huo huo sauti za panya wengi zilianza kusikika , ilikuwa ni kama vile wamebanwa sehemu na kuanza kutoa vilio , jambo ambalo lilimshangaza.
“Hapana sitaki kuota tena , ndoto isha mara moja, cut!!”Hamza alijikuta akiongea kwa nguvu kutokana na hasira , alitaka kuondoka katika ndoto ambayo anaota lakini licha ya kusema ndoto iishe haikuwezekana
Baada ya kutuliza hasira zake mara baada ya kuona ndoto imeshindikana kuisha alijikuta akisimama lakini ghafla zile sauti za panya ziliacha kulia kama panya bali sauti ya kilio cha kwikwi kutoka kwa mwanamke kilisikika.
Kuna mtu analia , kuna mtu analia tena usiku wote huu, alianza kujiwazia huku mapigo ya moyo yakienda mbio , licha ya kwamba alijihisi yeye kama Hamza sio muoga lakini ajabu mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kweli , akili yake ilishindwa kudhibiti mabadiliko ya mwili wake kutokana na woga aliokuwa akijisikia.
Hali hio ilimshangaza na aliweza kugundua licha ya kwamba alikuwa na ufahamu wa Hamza lakini alikuwa muoga , hakuwa jasiri tena , hii ndoto ni kama imemfutia baadhi ya uzoefu wake unaomfanya kuwa jasiri.
“Sio mimi ninaoogopa , ni huyu Luther mzungu, hapana ni huyu Luther , mimi sio muoga”Aliongea huku akisikiliza upande kilio kile kinapotokea , lakini licha kujifariji kwamba sio muoga mwili ulikuwa ukitetemeka kwa woga.
“Nahisi uoga maana huu sio mwili wangu , acha kuwaza huu sio mwili wako”Aliwaza lakini muda ule hakujua hata ni muda gani alikuwa ameshikilia kipande cha mbao kwa ajili ya kujilinda.
Alijaribu kutafuta sauti inatokea wapi lakini sauti ya kilio ilitokea kila upande , ni kama kila sehemu kuna hio sauti, sekunde chache mbele akizidi kuongeza umakini , ile sauti ilipotea na sasa alichoweza kusikia ni wimbo ni kama kile kilio kilikuwa kimebadilika na kuwa biti la wimbo.
“Huu ni ulimwgnu wa maajabu na uchawi , pengine hiki chumba kina mzimu au msukule”Aliwaza Hamza huku akitetemeka.
Alijaribu kutumia uwezo wake wote kujituliza kwa kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha huku akiwa amefumba macho wakati akiwa ameusogelea mlango na sasa ni kama ile sauti aliweza kusikia vizuri , sauti ilikuwa ni ya yule mwanamke alieshuhudia akichomwa moto na kilio chake ni kama kilikuwa kikimuita.
Hamza alifungua mlango na sasa ni kama masikio yake yalikuwa yakifuata upande ambao sauti ilikuwa ikitokea na alizipiga hatua bila ya kujali giza.
Kwa alichoweza kufahamu mwanamke ambae amechomwa moto alikuwa jirani yake na sauti ndio ilikokuwa ikitokea.
Ufahamu wa Luther ni kama ulikuwa ukimpigia makelele na kumwambia yule mchawi alikuwa akiishi hapa.
Hamza mara baada ya kusogelea eneo hilo alishangaa kwasababu eneo lote lilikuwa limechomwa moto na nyuma ya huyo mchawi ilikuwa imebobolewa na kilichoonekana ni kifusi cha matakataka , lakini sauti ya kilio bado ilikuwa ikisikika.
Licha ya kwamba giza lilikuwa kubwa nafsi yake ilikuwa na ujasiri kasoro mwili wake.
“Kama waliemchoma ni yule mchawi kwanini nasikia sauti yake , au hili eneo kuna vyumba vya chini ambavyo hawakuona?”Alijiuliza Hamza.
Ile sauti ghafla tu ilibadilika kutoka kuwa ya kike na kuwa kama ya mwanaume kutokana na uzito wake , lakini muda huo sauti haikuwa ikisambaa bali sauti ilikuwa ikisikika kwenye ufahamu wake tena kwa ukali mkubwa.
“Kama naota na huu mzimu ukiniua pengine ndio njia ya kutoka ndotoni na kulala kwa amani”Aliongea Hamza akiamini kwamba atatoka katika hio ndoto kwa kushambuliwa na huo mzimu unaotoa sauti.
Kitendo cha kusogelea karibu kabisa ghafla tu ile sauti ya kilio ilipotea na kukawa kimya, Hamza akijua kile kilio kilipita ghafla tu alihisi sauti ile ikitokea nyuma yake kwenye chumba alichotokea na awamu hio ilikuwa na nguvu kiasi kwamba ujasiri wa nafsi yake yeye kama Hamza ulimwambia usiogope lakini mwili mabao haukuwa wake ulikuwa kwenye mbio huku akipiga makelele.
“Jamani mzimu weee! , kuna mzimu , kuna Mzimu.!!!!!”
Hamza alikuja kugundua ambae alikuwa akiogopa sio yeye kama Hamza bali katika mazingira kama hayo ni Luther , alijitahidi kutokukimbia lakini nafsi ya Luther ni kama imeamka na mpaka anakuja kusimama alikuwa mbele ya geti la kanisa na kuzuiwa na walinzi ambao walikuwa wakimshangaa kwa makelele yake.
Kilichomuogopesha zaidi licha ya kufika mbali na nyumba yake ni bado sauti ya kilio alikuwa akiisikia huku ikiwa imeambatana na sauti za mbwa kubweka.
“Unafanya nini hapa , kwanini unapiga makelele?”Swali kutoka mlinzi , muda huo sauti yake ilikuwa imeamsha na majirani wengine.
“Mzimu , kuna mzimu kwenye ile nyumba ya mchawi”Aliongea Luther huku yeye kama Hamza akijitahidi kutoonesha woga lakini alishindwa kutawala mwili kuongea.
Muda huo mlinzi mwingine aliongezeka , ilionekana alisikia sauti za kelele za Hamza,
Wale walinzi wote mara baada ya kusikia kauli yake , walionyesha kushikwa na wasiwasi pia na kwa muonekano wa Luther wale walinzi ni kama walikuwa na wasiwasi wa kumuamini kama anaongea ukweli.
Yule mlinzi alimwangalia Luther kwa macho ya wasiwasi na kisha alimwambia mlinzi mwenzake asubiri akamwite mchungaji.
Dakika chache mbele yule mlinzi alirudi akiongozana na mwanaume mwingine mzungu ambae ana nywele nyeupe.
“Naitwa mchungaji Benjamini , niambie kilichotokea”Aliongea.
Wale walinzi waliishia kusimama nyuma ya mchunganji huku wakiwa na wasiwasi wamemsumbua tu mchungaji kutoka kwenye usingizi wake.
Hamza mara baada ya kuona anashindwa kujidhibiti kuongea aliona airuhusu akili ya Luther kuutawala mwili na palepale kwa msaada wake aliwezesha kusimulia kila ambacho alisikia.
“Umefanya vizuri , ujasiri wako unaonyesha ni kwa namna gani umejitoa kwa Mungu”Aliongea yule mchungaji na kisha aliwageukia wale walinzi.
“Thompson na Gary waiteni walinzi wengine waliopo hapa , huyu mchawi lazima atakuwa ni wa daraja la chini hivyo haina haja ya kumhusisha askofu”
“Sawa bwana wangu”
Hamza alijaribu kumfahamu huyo mchungaji kupitia akili ya Luther na aligundua alikuwa ni mchungaji wa daraja la kati na alikuwa na uwezo wa kudili na mitego ambayo imeachwa na mchawi wa daraja la chini,kulikuwa na gepu kubwa kati ya mchungaji na mchawi wa daraja la chini kinguvu.
Yule mchungaji alimuuliza Hamza jina lake , Hamza alitaka kusema anaitwa Hamza lakini mdomo ulikuwa mzito kuongea na alijikuta akisema anaitwa Luther na sio Hamza.
Muda uleule watu wengi walikuwa washatoka katika nyumba zao na kukusanyika mbele ya nyumba ya yule mchawi wakiwa na mienge ya moto kama vyanzo vya mwanga.
Hamza muda huo ndio alikumbuka kuangalia juu angani na alijikuta akishangaa mara baada ya kuona mwezi haukuwa mwezi wa kawaida , ulikuwa mwezi mwekundu kabisa kama vile umejaa damu.
Licha ya kuwepo kwa watu katika eneo hilo , ni yeye Hamza pekee ambae alkuwa akisikia sauti za kilio cha yule mwanamke na alijiuliza kwanini watu hao hawasikii chochote tofauti na yeye
“Ndio hapa kuna mzimu….”Aliongea yule mchungaji kanakwamba amejua Hamza ambacho anakifikiria.

SEHEMU YA 74
Hamza hata hakujua ndoto iliisha saa ngapi na saa ngapi alipata usingizi lakini kitu ambacho alikuwa akikumbuka usiku aliota na katika ndoto aliishia akiwa anamwita mchungaji kwa ajili ya kudili na mzimu.
Alijikuta akikaa kitandani na kufikiria juu ya uhalisia wa ndoto , ukweli ni kwamba ashawahi kusikia aina za ndoto ambazo mtu huota huku wakati akijua kabisa alikuwa akiota , ndio kilichokuwa kikimpata Hamza , alikuwa akiota yupo ulimwengu mwingine huku akijua kabisa alikuwa akiota.
Maneno ya kile kimemo ambacho kiliachwa kwake juu ya ndoto hizo kilikuwa kikijirudia rudia katika akili yake.
“The history of your past life in onother world has already begun to echo , if you fail to inherit your history ,it will be the end of your life in this world , your greatest enemy has already awakened”
Hamza alijikuta akikumbuka maneno hayo , lakini ajabu licha ya kwamba ni swala ambalo lilikuwa likimpa wasiwasi kwa kiasi flani lakini alijikuta akianza kupatwa na hamu ya kujua kinachoendelea , kwake ilikuwa ni kama anaangalia sinema ya karne za kumi na tano katika nchi za Ulaya.
Hamza kabla hajatoka kitandani aliona siku hio anapaswa kwenda kuonana na Frida , sababu ya kutaka kuonana nae ni kwamba alikuwa na uwezo wa kuota bila kutumia mshumaa wa nuru ambao alipewa , alikuwa akitaka maelezo kama kuna shida yoyote ya yeye kuota bila ya mshumaa huo , maana ukweli ni kwamba katika maisha yake ya nyuma hakuwahi kuota ndoto za maajabu namna hio , zimeanza muda mfupi tu baada ya kufahamiana na Regina.
Kwasababu alikuwa na namba ya Frida aliamua kumtafuta muda uleule na simu yake ilipokelewa na alimwambia waonane siku hio na Frida upande wake ni kama alikuwa akiisubiria simu ya Hamza kwa hamu zote.
Alikuwa na mpango wa kwenda sehemu mbili kwa wakati mmoja mpango wake wa kwanza ilikuwa ni kwenda kuonana na Frida na kisha achukue safari ya kuelekea Morogoro..
Kwasababu alijua ilikuwa ngumu kwa Regina kupika chochote alitoka na kwenda jikoni.
“Jiandae nataka twende wote kwenye kampuni”Aliongea Regina baada ya kumaliza kifungua kinywa.
“Leo ni jumamosi na kazini sina kazi hivyo sitoenda”Aliuongea Hamza maana alikuwa na mipango yake kichwani tayari.
“Sio huna kazi ni kwasababu hujatafuta kazi ya kufanya , unataka kwenda wapi kama huendi kazini?, au ni chuo si likizo inaendelea?”
“Sio chuo , kuna maswala yangu binafsi naenda kuyafuatilia”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumwangalia na muonekano usiosomeka na alionekana kuna kitu anataka kusema lakini anasita.
“Jana usiku umesema tupeane muda wa kufahamiana na kuelewana , nimefikiria kwa umakini na nimefanya maamuzi , mwanzoni sikutaka kuolewa lakini kwasababu tushafunga ndoa naamini tutakuwa na mwisho mzuri , sitaki yanayomkuta baba yangu kunikuta na mimi wala kuwa kama mama yangu ambaye ameishia kuwa mpweke…”Aliongea Regina na kauli ile ilimfanya Hamza kufurahi mno.
“Upo sahihi , kwanzia sasa hivi tunapaswa kufikiria mazuri yenye uelekeo mmoja”
“Umeongea ki usahihi hivyo naamini utaanza kufanya kazi kwa bidii na kupunguza uzembe , najua una koneksheni kubwa jambo ambalo ni zuri lakini hii ni Tanzania, nataka siku ambayo nikikubali watu wakujue kama mume wangu nijivunie kwa kile ambacho unafanya na sio kuongelewa vibaya na watu”
Hamza alielewa alichokuwa akimaanisha Regina na aliishia kukuna kichwa na hakujali kabisa msisitizo wa huyo mwanamke.
“Regina wewe mwenyewe unanijua vizuri , kwasasa nasoma lakini mpango wangu nikimaliza hata nisiwe na cha kufanya ili mradi niwe na hela ya chakula basi , sitojali watu wanachoniongelea”
“Sawa unaweza usijali lakini vipi kuhusu mimi, siwezi kuwa na mwanaume ambae hana malengo wala ndoto za kukamilisha , wanaume ambao hawana malengo wanachukiza zaidi ya wanaume wachepukaji”
Regina alikuwa siriasi , alionekana hakuwa akitania hata kidogo , alithamini sana Career yake hivyo alihitaji mtu ambae atakuwa sambamba nae.,
“Vipi kuhusu Eliza sasa , unaweza kukubali niendelee nae bila kuleta shida?”
“Inamaana hukuelewa pointi yangu au unajitoa ufahamu?”Aliongea huku hasira zikianza kumvaa.
"Hivi kwenye kichwa chako wewe malengo yako ni wanawake na sio kitu kingine , wanaume wengi wa umri wako wanafikiria namna ya kutengeneza pesa , kuanzisha biashara na kufanya kazi kwa bidii , ukiachana na wanawake ni kitu kipi kingine unataka kufanya au kukamilisha kwenye maisha yako?”Aliongea Regina akiwa siriasi.
“Kufanya kazi kwa bidii na kupata hela sio malengo yangu kwasasa naona ni kama kujishughulisha tu , kama ni hela tunazo za kutosha , kwani unataka kuwa na shilingi ngapi ili uridhike?”
“Unakwepa majukumu yako, hela zangu sio zetu , halafu wewe si ndio jana ulisema mwanaume anapaswa kujua kuwajibika , kwahjio kutofanya chochote na kupoteza muda ndio unaita uwajibikaji?”
“Regina kwanini unaweka vigezo vikubwa hivyo, mimi nipo mwaka wa mwisho chuo na sasa hivi umenipa kazi kama mfanyakazi wako wakati wewe ukiwa ndio CEO , kazi zote ninazopewa kufanyia kazi nazifanya kwa usahihi na nazidi kuwa bora siku hadi siku , nimeweza kushinda tuzo kwa ajili ya kampuni na mengineyo , kipi kingine napaswa kufanya?”
“Ninachomaanisha sitaki mwanaume anaeridhika na kitu kidogo au wewe unadhani hela ulizopata zinakutosha kabisa?”Aliuliza na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la uchungu.
“Labda ndio zinanitosha , nimepitia mengi mpaka kufika hapa na malengo yangu ni kuishi maisha ya amani na utulivu na kuwa na furaha”
“Umepitia mengi!, unamaanisha kuua watu?, mimi nataka kujua ni mafanikio gani umefanikisha , kama ni kupitia mengi kila mtu anapitia hayo mengi , wewe baada ya kupitia mengi mafanikio yako ni yapi?”
“Sijasema mafanikio yangu ni kuua watu na sio kweli kama nimeaua watu?”
“Kama sio hivyo ni mafanikio gani unayo?”Hamza alijikuta akishindwa kujibu swali lile.
Mwingine angeona Regina ana masharti makubwa lakini ukweli ni kwamba alikuwa ni bosi wa kampuni kubwa ambayo imeorodhshwa katika masoko makubwa ya hisa dunani , kama ataolewa inamaanisha na mume wake atakuwa katika rada za watu.
“Najua unashindwa kuongea , wewe ni mwanaume usie na malengo na uliepoteza tumaini , nenda kapoteze muda huko unakoenda , mimi naenda kazini”Aliongea na kisha kwa hasira alishika mkoba wake na kutokomea nje.
Hamza aliishia kuvuta pumzi tu na hakuongea chochote , sio kwamba hakuwa na mafanikio , alikuwa nayo lakini hayakuwa yakielezeka.
Yeye alijichukulia kama mtu ambae ameishuhudia Tsunami tayari na hawezi kuogopeshwa na mawimbi madogo madogo.
Lakini hata hivyo alijiambia sio muda sahihi wa kumwambia Regina chochote , isitoshe licha ya kwamba ni kweli alitamani maisha ya amani ambayo hayana usumbufu , lakini vilevile alikuja Tanzania kwa lengo moja tu , lengo la kumfahamu Mzee ni nani.
Siku zote wanawake wanajivunia kuwa na mwanaume ambae ana mafanikio kumzidi , hilo Hamza alielewa lakini aliona sio muda sahihi wa kumuonyesha chochote Regina, isitoshe sio yeye tu kama sehemu ya familia yake.
Kwasababu alikuwa na mzunguko mrefu hakuchelewa kuondoka nyumbani na hakutoka na gari bali aliona atumie usafiri wa uma , isitoshe Regina alimnanga vya kutosha hivyo hakutaka kushobokea magari yake.
Ilimchukua dakika kama arobaini hivi kufika Madale kwa ajili ya kuonana na Frida.
Na baada ya kugonga ni Frida ambae alitoka kuja kumfungulia mlango .
“Mlinzi wako leo hayupo?”Aliuliza Hamza.
“Kwasasa sina mlinzi, uliemkuta kipindi kile amerudi nyumbani kwao Singida”Aliongea na Hamza alitingisha kichwa.
Frida alikuwa mwanamke mrembo lakini Hamza aliweza kuona mabadiliko Frida alionekana kupungua mwili.
“Naona umepungua mwili , ndio kutokana na adhabu nini?”Aliuliza Hamza maana alijua mara ya mwisho wakati alipoongea na Frida alimwambia alikuwa akienda kuhojiwa.
Kitendo cha Frida kumsikia Hamza akimwambia amekonda alijisikia faraja , japo ukweli ni kwamba sababu za kukonda ni juu ya kazi yake na misheni yake kwa Hamza.
“Niliweza kutoka bila ya kupatiwa adhabu ndio maana nimewahi”Aliongea huku akimkaribisha ndani.
Eneo la sebuleni kulikuwa na makatarasi kibao pamoja na vitabu , ilionekana mwanamke huyo alikuwa bize kusoma kama sio kuandaa ripoti.
“Oh !, nilikuwa bize kidogo na ripoti ndio maana unaona makaratasi mengi”Aliongea.
“Wana taaluma hamjawahi kupumzika, kila saa mpo na mavitabu mnasoma na kufanya uchambuzi”
“Watafiti wa kisayansi hawajawahi kupata usingizi kwa muda mrefu , hata wakati wakulala tunawaza kile kilichokwama, ukiachana na kutambulika kutokana na kukamilisha kitu kikubwa lakini haya yote tunafanya kwa ajili ya faida ya dunia”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha kichwa kumwelewa.
“Nina safari ya Morogoro , hivyo sitaki kukaa hapa muda mrefu”Aliongea Hamza.
“Ukweli ni kwamba nilitaka kukutafuta pia leo tuonane kama nilivyokuambia kwenye simu , nianze mimi au uanze wewe kuongea sababu ya kutaka kuonana?” Aliongea Frida.
“Nitaanza mimi”Aliongea Hamza na Frida alitingisha kichwa akimpa ishara ya kuongea.
“Kilichonileta ni swali moja tu , wakati unanipatia ule mshumaa ulisema umetoka kwa Dokta Genesha na kazi yake ni kuamsha ndoto, je una kazi zaidi ya kuamsha ndoto?”Aliuliza Hamza na swali lile kidogo lilionekana kumshitua Frida lakini alijizuia.
“Kwanini unaongea hivyo , kuna kitu kingine ambacho kimekutokea kwasabu ya Mshumaa?”
“Hakuina kilichonitokea , ukweli ni kwamba sijawahi kuutumia tokea unipatie , ila katika kipindi chote nimekuwa nikipatwa na ndoto kama kawaida, kama mshumaa ni wa kuamsha ndoto na naota bila ya kutumia mshumaa kuna haja ya kuutumia?”Aliuliza Hamza na swali lake lilimfanya Frida kupumua kwa ahueni.
“Unachokiona kupitia ndoto sio ndoto kama ndoto bali ni uhalisia wa kumbukumbu zako, kuna kitu nilisahu kukuambia kuhusu mshumaa , licha ya kwamba ni kweli kazi yake ni kuamsha ndoto lakini pia ni kuifanya akili yake isichukulie kile ambacho unakiota kama ndoto”Aliongea na kumfanya Hamza sura kuchekza kidogo .
“”Unamaanisha nini?”
“Umesema unaonta ndoto kama kawaida, kama umeota zaidi ya mara mbili au mara tatu lazima kuna tofauti ambayo umeweza kuona?”Aliongea Frida na kumfanya Hamnza kushangaa.
“Umnejuaje kuna tofauti?”
“Umesahau mimi ni mwanafunzi wa Dokta Genesha, ukiachana na Profesa Frola rafiki yako”Aliongea na kumfanya Hamza kukunja ndita.
“Unamfahamu Dr Ronicas kama mwanafunzi wa Dokta Genesha?”
“Kila mtu anamfahamu Dr Ronicas , najua pia alikuwa hapa nchini Tanzania , wakati nikiwa kama Ajent miaka saba iliopita niliweza kumfahamu Dr Ronicas lakini ni kupitia maandishi tu”.Aliongea na Hamza hakushangaa sana maana mzunguko wa Dokta Genesha haukuwa wa kawaida.
“Licha ya kwamba ndoto zote utakazoota una husika moja kwa moja wakati wa matukio lakini utofauti unakuja pale ambapo unaota lakini hujui unaota na muda mwingine utakuwa unaota huku ukijua kabisa unaota”Aliongea Frida na kumfanya Hamza kutngisha kichwa.
“Upo sahihi mara ya kwanza niliota bila kujua naota , lakini jana nimeota huku akili yangu ikiniambia nipo ndotoni”
“Ndoto unayoota unajiona kuwa na sura ya tofauti si ndio?”Aliuliza .
“Hivi nilikusimulia , mbona ni kama unajua kila ninachoota?”Aliuliza Hamza na kumfanya Frida kutabasamu.
“Kwasababu wewe ni mteja wangu wa tano”
“Unamaanisha kuna watu wanaota kama ninavyoota mimi?”
“Ndio wapo licha ya kwamba kuna utofauti lakini wote wanaota wakiwa na sura tofauti , ni kama wamezaliwa katika miili mingine kwenye ndoto zao , utofauti ni kwamba kwa maelezo ya Dokta Genesha wewe ndoto zako zina upekee”
“Upekee! Unamaanisha nini ?”
“Sina maelezo ya kutosha, ninachojua unachoota ni kitu cha kipekee ambacho kitakufanya kutafsiri Lugha iliowashinda binadamu kutafsiri”Aliongea na Hamza alikuwa akielewa Frida alikuwa akimaanisha nini kuhusu lugha.
“Kwahio ni ipi sahihi , kuota nikiwa najua naota ama kuota nikiwa sijui naota?”.
“Swali lako nikilirudia naweza kuliweka hivi , je ni ndoto ya aina ipi unaweza kusahau haraka, kati ya ndoto ambayo unajjihisi unahusika moja kwa moja au ndoto ambayo unajua unaota?, jibu la swali hili kitaalamu ni kwamba ndoto ya kawaida ambayo hujui unaota ndio ambayo haisahauliki haraka , lakini kwa swala lako wewe ndoto yako sio kama ndoto zingine , ubongo wako sio wenye kutengeneza matukio ambayo unaona kama msingi mkuu wa ndoto bali unachoota ni koneksheni ya kimawasiliano baina ya Dimension mbili tofauti hivyo kwa swala hili unapaswa kujua unaota lakini pia uwe na uwezo wa kukatisha ndoto muda wowote”Aliongea Frida.
“Kwa kukuelewesha kwa urahisi wakati ukiwa ndotoni si unajua unaota, lakini ghafla ukakutana na tukio la kutisha na kutamani ndoto iishie palepale na ikaisha hapo utakuwa umefanikiwa , kati ya wagonja wangu ambao nishawahi kupata wengi walikuja kwasababu wanaota vitu vya ajabu ambavyo vinawafanya kushindwa kulala,hakuna dawa ya kumpa mtu kuzuia ndoto bali namtengenezea mazingira ya kuifunga ile ndoto na njia pekee ni kumfanya aote wakati akijua anaota kwa njia ya hypnosis”
“Kwahio napaswa kutumia mshumaa kama njia ya kunifanya niote wakati nikiwa naota si ndio?”
“Ndio , unapaswa kuota wakati ukijua unaota na wakati huo hisia zako zote zikiwa katika ndoto , hata baada ya ndoto isitokee ukasahau kitu chochote kile ambacho unaota , kama nilivyosema unaota ukiwa umetawala mwili mwingine, lakni nafsi ya mwili huo bado inafanya kazi, mshumaa wa nuru utakusaidia kuwa na uwezo wa kutumia akili yako na ya mtu ulietawala mwili wake kwa wakati mmoja na kila unachoota hakitasahaulika hata baada ya ndoto”Aliongea Frida.
“Kwahio unaamini kwamba kupitia hii ndoto nitaweza kutafsiri kitabu alichoniachia Dokta Genesha”
“Ndio kwasababu kupitia hio ndoto utajifunza lugha mpya ambayo hukuwahi kuijua hapo kabla na itaendana na lugha ambayo binadamu tumeshindwa kuitafsiri”
“Kuna uhakika gani kwamba nitaweza kujifunza lugha mpya na je ninachoota mnajuaje kama ni sahihi au ni ndoto tu ambazo hazina mpangilio”Aliongea Frida na kumfanya Frida kutabasamu kidogo .
“”Nadhani ni muda wa kukuambia na mimi kwanini nilitaka kuonana na wewe . ndio njia rahisi ya kujibu swali lako”Aliongea Frida na kisha alimwambia Hamza asubiri anarudi.
Dakika moja tu alitoka chumbani akiwa ameshikilia picha na kumpatia Hamza.
“Hii ni picha ambayo aliniambia nikupatie Dokta , huwezi kuita picha ni kwasababu ni mchoro tu lakini nadhani umebeba maana ambayo utaweza kuitambua”Aliongea Frida na Hamza aliingalia ile picha na macho yake yalichanua .
“Red moon!!”Aliongea Hamza akimaanisha mwezi mwekundu.
ITAENDELEA J3
Mwendekezo watsapp 0687151346
 
Big up SANA mkuu
 
Usiyoyafahamu kuhusu Vita ya Kagera

Kikosi kilichokuwa na jukumu la kuulinda mpaka wa Uganda ni Brigedi ya 202 ya Tabora chini ya Brigedia Yusuf Himid, ambaye alikuwa akisimamia Kanda ya Magharibi.

Mpakani palikuwa na batalioni ya tatu, yaani kikosi cha askari ambacho kina kombania kadhaa na ambacho ni sehemu ya brigedi au rejimenti. Hiki kilikuwa chini ya Luteni Kanali Morris Singano, ambaye miezi miwili kabla alihamishwa kutoka Mbeya kwenda Kanda ya Ziwa.

Mara baada ya zile ndege tatu za kivita za Uganda zilizoishambulia Tanzania zikiendeshwa na maluteni David Omita, Atiku na Abusala, Singano alituma taarifa hizo .
 
Nina swali mkuu
 
Back
Top Bottom