Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTUNZI: SINGANOJR.

SEHEMU YA 80.

Hamza alijikuta akishikwa na soni , ijapokuwa haikuwa makusudi aliona pia sio sawa , aliuliza ili kupata majibu na hakujua angemkasirisha Regina kiasi hicho, aliona pengine uelewa wake juu ya wanawake una kasoro na anatakiwa kuanza kujifunza upya.

“Toka kwenye ofisi yangu sitaki kukuona!”Aliongea Regina kwa kufoka.

Hamza aliishia kushusha pumzi akikubali kushindwa maana hakutaka kumwagia moto mafuta , hivyo kimya kimya alitoka ndani ya ofisi ya Regina.

Regina mara baada ya kuona ni kweli Hamza kaondoka aijikuta akipandwa na hasira mara mbili zaidi na kuanza kumlaani ndani kwa ndani huku macho yakiwa mekundu, aliangalia viboksi vya matunda alivyoleta Hamza na kwa hasira alivichukua na kwenda kutupia kwenye Dustbin kama kwamba ndio anamtupa Hamza.

Upande wa Hamza alikuwa na mawazo , baada ya kutoka ndani ya ofisi ya Regina alikuwa akiipiga namba ya simu ya Eliza mfululizo lakini ilionekana mwanamke huyo amezima simu.

Muda huo alichotamani ni kwenda nyumbani kwake kumuangalia lakini alikumbuka ahadi yake na Yonesi muda ule kwa ajili ya kumuelekeza baadhi ya mafunzo hivyo hakutaka kuivunja na kuona aanzie huko na kisha ndio akamtafute Eliza.

Muda ambao alifika ndano ya floor ya kufanyia mazoezi Yonesi alikuwa amekwisha kufika na alikuwa akipasha mwili, alikuwa amevalia mavazi ya mazoezi tayari na ilionekana alikuwa akitegemea kujifunza kitu kipya kutoka kwa Hamza kwa hamu zote.

“Kapteni wewe ni mwanamke , kwanini upo siriasi sana na swala la mapigano?Aliuliza Hamza mara baada ya kuona namna ambavyo Yonesi alionekana kuwa siriasi.

“Kwani ni vibaya, unadhani mwanamke hana haki ya kujifunza vitu ambavyo anaweza kujifunza mwanaume?”Aliuliza na Hamza alitingisha kichwa kukubaliana nae , isitoshe aliuliza kumtania tu.

“Ngoja tuanze haraka ili tumalize, kuna sehemu nataka kwenda”Aliongea Hamza. “Kama una haraka kwanini tusifanye siku nyingine , mimi sio jiniasi naweza nisikumbuke kila kitu kwa maelekezo ya muda mfupi”Aliongea Yonesi huku akiwa siriasi.

“Utakumbuka maana nakwenda kukufundisha kitu chepesi sana , ndani ya saa tu utakumbuka kila kitu”Aliongea Hamza na kisha alianza kuonyesha ufundi wake.

Yonesi mara baada ya kuona miondoko kadhaa kutoka kwa Hamza alijikuta akishangaa zaidi huku akikunja sura

“Hamza ijapokuwa uwezo wangu wa kimapigano ni mdogo lakini huwezi kunitania na ulichonionyesha , hayo sio mafunzo bali ni kama kucheza mziki”

“Kapteni acha uharaka, wewe fanya kama nilivyokuelekeza na uone kitakachotokea”Aliongea Hamza.

Yonesi aliishia kuonyesha kutoridhika lakini alisogea kati na kuanza kujikakamaza kuigilizia kile ambacho ameonyesha Hamza.

“Mguu wako wa kushoto unatakiwa kuukunja zaidi kwenda nyuma na viganja vya mikono yako vigeuzie kuelekea juu na mguu wa kushoto upindishe kwenda mbele…”

Hamza alianza kuelekeza huku Yonesi akifuatisha hayo maelekezo na kadri alivyokuwa amekaa katika mtindo huo wa maelekezo uzito wa mwili wake ulianza kuongezeka kila dakika na alianza kuvuta pumzi kwa haraka

“Bado kuna kitu hukipati , mguu wako wa kushoto haujaunyoosha na wa kulia haujaupindisha kwa angle sahihi, ndio maana unaanza kukosa balansi ya mwili”

“Naupandisha kwa angle ngapi sasa?”

“Angalau zifike sitini”

“Angle sitini!!”Aliongea Yonesi akishanga kwa uona ni nyingi.

“Ngoja nikusaidie kukuweka sawa”Aliongea Hamza na licha ya Yonesi kuonyesha wasiwasi alimshika vizuri paja na mikono na taratibu akaanza kumnyoosha.

Licha ya kupokea malalamiko kutoka kwa Yonesi asiende mbali kwenye kumgusa maeneo nyeti lakini Hamza alijifanyisha kuwa siriasi zaidi na kutomzingatia lawama zake.

Baada ya dakika kadhaa za kuchukua mazoezi ya kubalansi mwili alijikuta akishangaa, maana mwanzoni alidharau lakini aligundua ni kuna kitu cha upekee katika mafunzo hayo alianza kukipata.

“Hii ni aina gani ya mafunzo?”

“Hii ni mbinu ambayo nimeitengeneza mwenyewe ili kurahisisha mazoezi ya balansi mwili , ukirudia kujikunja mara mia moja nitakufundisha hatua inayofuata”

“Mara mia!!”

Aliongea Yonesi kwa mshangao maana alikuwa amechoka kwa mzunguko huo mmoja tu na kuona mara mia itakuwa ni nyingi mno.

Kwasababu Hamza alikuwa na haraka alimwambia awe siriasi na alichomwelekea ili amfunidshe hatua nyingne , licha ya Yonesi kujihisi kuchoka aliishia kutingisha kichwa kukubali na Hamza aliondoka haraka haraka kwenda kumtafuta Eliza.

*****

Ni muda wa saa nane kama na nusu hivi alionekana Kanali Dastani akiingia ndani ya ofisi yake akitokea kwenye kikao ambacho kiliitishwa na Mkurugenzi mkuu wa kitengo.

Alionekana kuwa na uso uliosawijika, mtu ambae ni kama amepokea taarifa ya kitu ambacho hajaridhishwa nacho lakini hana jinsi.

Akiwa ana nyonga tai yake vizuri mlango wa ofisi yake uligongwa na aliruhusu anaegonga kuingia na mara baada ya kugeza macho kumwangalia alieingia alionyesha tabasamu hafifu.

“Vipi Afande Mdudu kuna tatizo?”Aliongea Kanali Dastani huku akimkazia macho.

“Afande nilidhani utahitaji mtu wa kuongea nae , kwenye kikao hukupata mtu wa kukuunga mkono mawazo yako , kitu ambacho sio kawaida”

“Kwahio umekuja kuniunga mkono baada ya kikao kuisha?”Aliuliza Afande Dastani huku akikunja sura.

Afande Mdudu aliishia kutoa tabasamu na kisha alisogea na kwenda kukaa kwenye sofa.

“Hoja uliotoa ilikuwa ina mashiko Kanali , lakini unajua fika sisi ni wanajeshi , ijapokuwa mawazo yetu yanahitajika kwenye vikao lakini ikitokea kitu kishaamuliwa kikao kinafanyika kutufahamisha kinachoendelea na sio kusikiliza hoja zetu”Aliongea.

“Kama unachoongea unamaanisha basi ulipaswa kuuvaa ujasiri na kuunga mkono hoja yangu”

“Hoja yako ilikuwa na mantiki lakini haimaanishi ilikuwa uhalisia , swala la kesi zote zinazohusiana na Hamza kufungwa halipo ndani ya kitengo chetu tu mpaka TISA pia”Aliongea na kumfanya Kanali macho yake kuchanua.

“Mpaka TISA!!”

“Nimesikia taarifa hizi tokea juzi,Hamza alikuwa kwenye rada za usalama wa taifa kwa muda mrefu sana, ukiangalia hii kesi kwa umakini haina vigezo vya kuwa chini ya kitengo chetu ndio maana nikasema imekosa uhalisia licha kwa jicho pana la kichunguzi ilikuwa na mantiki” “Kama uhalisia wa hii kesi umekosekana katika kitengo chetu pekee kwanini Mshauri mkuu aingilie mpaka kwenye idara nyeti ya intelijensia ya taifa, hata kama ni swala la uchaguzi haliwezi kufanywa na watu wote wa kitengo”

“Swala la uchaguzi kwasasa ni nyeti sana kwa usalama wa taifa kosa kidogo kunaweza kutokea machafuko , swala la Jongwe kufariki limefanya idara zote za usalama kuwa katika tahadhari”

“Hio haikuwa hoja yangu Mdudu , najua

Uchaguzi ni swala la juu kabisa kwa nchi lakini hili lipo chini ya kitengo cha TISA na idara nyingine za usalama, Malibu ni Kitengo cha jeshi kazi yetu sio kuangalia upande mmoja tu wa nguvu zizisokuwa za kawaida”

“Hoja yako nakubaliana nayo , lakini mpaka sasa zimebakia siku kumi na tano tu zoezi la kupiga kura lianze, Mshauri mkuu ni mtu ambae hawezi kufanya maamuzi juu ya kitu kinachohatarisha usalama wa nchi”Aliongea Afande Mdudu na Kanali alionekana kufikiria kwa dakika kadhaa na kutingisha kichwa kukubaliaa nae.

“Unaonekana kumchukia sana huyu Hamza, Norbert na ujanja wake alishindwa kumkamata ilikuwaje wewe mpaka Mshauri mkuu akaingilia?”Aliongea.

“Huwa likija swala linalomuhusu Yonesi nakuwa jasiri mno”

“Haha.. Afande Yonesi!, kwanini?”

“Dastani acha kunikejeli ilihali unajua kinachoendelea”Aliongea Mdudu huku akiongeza usiriasi na kumfanya Afande Dastani kutoa tabasamu lilojaa ukejeli.

“Wewe na Amosi mmeteswa sana na penzi la Yonesi , ulienda mbali mpaka kumtumia baba yako umuoe lakini ‘kiko wapi’ kitisho kidogo umeufyata”

“Usinilinganishe na Mzee, Amosi ni mtu mzima aliejaribu bahati yake kwa Yonesi , mimi ni kijana ambae sikuwa nikibahatisha ila nilipigania kile ninachokitaka, mwanajeshi mwenye busara ni yule asiemdharau adui yake , natafuta namna ya kumrudia”Aliongea na kumfanya Kanali kutoa cheko.

“Likija swala la Yonesi unakuwa siriasi sana , anyway niambie unachohitaji , nadhani hujaja kwenye ofisi yangu kupiga soga wakati ni muda wa kazi huu”Aliongea na kumfanya Afande Mdudu kukaa vizuri.

“Nataka kujiunga na ushirika Black

Trinity
”Aliongea Mdudu kwa sauti ya chini na kumfanya Amnosi kushituka

“Unaongea nini Mdudu?”

“Acha hizo kanali najua wewe ni mwanachama na ili nijiunge lazima nipate mwaliko kutoka kwa mwanachama”Aliongea Mdudu na Ghafla tu ni kama Kanali Dastani amebadilika na kuwa kivuli kwani alipotea alipokuwa amesimama na kuja kusimama Mdudu alikuwa amekandamizwa kwa nguvu kwenye ukuta huku akiwa amekabwa shingo.

Kilikuwa ni kitendo cha maajabu mno na cha haraka sana alichokifanya Kanali Dastani lakini ajabu Mdudu licha ya kukabwa hakuonyesha hofu ya aina yoyote lakini upande wa Dastani hakuwa wa kawaida, ni kama amegeuka na kuwa kiumbe cha ajabu.

“Unajua unachokiongea!?”Alikoroma Dastani huku akimwangalia Mdudu wa macho ya kuogofya.

“Kanali huwezi kunifanya chochote , najua wewe na Tresha Noah mpo kwenye Uwili na kama nitapoteza maisha hapa picha zenu mkifanya mapenzi ya rafu zitasambaa mtandaoni , hebu fikiria kitakachotokea na kisha upunguze presha tuongee vizuri , siri yako ipo salama na mimi kama utanipatia mwaliko, ombi jepesi sana”Aliongea Mdudu huku akionyesha tabasamu la kejeli lililoambatana na macho kodo.

*****

Hamza aliweza kufika ndani ya Apartment anayoishi Eliza na baada ya kugonga kwa dakika kama moja hivi mlango ulifunguliwa na Eliza aliekuwa katika mavazi ya nyumbani.

“Hamza ni wewe , unafanya nini hapa?”

“Eliza nini kinaendelea , kwanini umezima simu na umeomba kwenda kufanya kazi nje ya nchi?”Aliongea Hamza akiruka hata salamu. Kwa jinsi ambavyo mwanamke huyo alivyoonekana , ilikuwa ni dhahiri kabisa kuna kilichokuwa kikiendelea, alionekana alikuwa na wasiwasi mno kiasi cha kumfanya uso wake kupauka.

“Eliza ni nani anagonga?”Sauti kutokea ndani ilisikika na Eliza aliishia kurudi nyuma akimpa nafasi Hamza ya kuingia ndani.

Muda huo sasa Hamza alipata kumuona mwanamke mtu mzima hivi ambae kwa haraka haraka ilionyesha umri umeenda.

“Mama shikamoo , naitwa Hamza mimi ni mpenzi wa Eliza”Aliongea Hamza bila aibu na kauli ile ilimfanya Eliza kukakamaa mwili na aibu juu kwani ilikuwa ni kama hakutegemea.

Haikuwa kwake tu hata kwa mama huyo alionyesha hali ya kushangaa maana ni kama hajawahi kukutana na tukio la mwanaume kujitambulisha kwa kujiamini na pili hakuwa akijua kama Eliza alikuwa na mpenzi.

“Mama Mkubwa hapana huyo sio ”

Hamza hakumpa hata muda wa kumaliza kuongea na alimsogelea yule mama.

“Mama Mkubwa kama nilivyojitambulisha, napaswa kujua nini kinaendelea ama mpenzi wake ili kumsaidia maana Eliza hataki kuniambia, nimemtafuta sana kwenye simu”

Kauli ile ilimfanya yule mama kumwangalia Eliza kwa sekunde kadhaa na ilionekana alikuwa na uzoefu wa kutosha kwani kuna kitu aliweza kukisoma tayari kutoka kwa Eliza.

Licha ya kwamba alikuwa na mshangao lakini kwa wakati mmoja pia alionyesha kuwa na tumaini.

“Baba!, wewe kweli ni mchumba wa Eliza?”Aliuliza yule mama.

“Ni kweli kabisa Mama Mkubwa , Eliza ni mpenzi wangu na nampenda sana, nipo tayari kwa lolote kwa ajili yake”Aliongea Hamza ilikuwa ni kama amepata hadhira ya watu kwa ajili ya kuelezea hisia zake.

“Eliza ni kweli?!”Aliuliza Mama Mkubwa kwa shauku huku akimkazia macho Eliza lakini mrembo huyo hakujibu zaidi ya kuinamisha kichwa chini , ukweli ni kwamba alikuwa na hisia ambazo haikuwa rahisi kuzielezea alikuwa akimpenda Hamza lakini tokea asikie Hamza ni mume wa bosi wake hakujua tena Hamza ni mpenzi wake au ni nani kwake.

Wahenga wanasema ukimya ni jibbu pia , hivyo kwa Mama Mkubwa yake Eliza aliweza kujua watakuwa kweli ni wapenzi ila kuna kinachoendelea kati yao.

“Baba nitakuelezea kilichotokea kama Eliza anagoma kukuambia unaweza kuwa na msaada”Aliongea yule Mama huku akimuona Hamza kama mtu ambae ni kweli anao uwezo wa kumsaidia kutokana na mwonekano wake wa kitajiri na kujiamini.

“Mama Mkubwa hapana..”Eliza alitaka kumzuia lakini Hamza alimkatisha.

“Mama Mkubwa naomba uniambie, nadhani unamjua Eliza ni mwanamke wa aina gani , asiponiambia nitashikwa na mawazo mengi na sitojua namna ya kusaidia”Aliongea Hamza na Mama Mkubwa alivuta pumzi na kisha alikaa chini huku akionyesha kuwa katika hali ya mawazo.

“Mama Mkubwa ngoja nimwambie”Aliongea Eliza na kuingilia mara moja , aliona sio vyema kama Mama Mkubwa akichukua nafasi yake.

Hamza maara baada ya kumsikia Eliza akiongea hivyo alijikuta akivuta pumzi ya ahueni sasa maana alijua kama hatoambiwa kinachoendelea ukichaa wa hasira ungemshika.

“Baba amekamatwa..”Aliongea kwa sauti hafifu. “Baba yako mzazi amekamatwa?”Aliuliza Hamza kana kwamba hajasikia vizuri na Eliza alitingisha kichwa kukubali.

“Imekuwaje baba yako akakamatwa na waliomkamata ni wakina nani?”

“Unakumbuka nilikuambia baba yangu ni mstaafu na yupo kijini?”

“Ndio nakumbuka?”

“Basi baba baada ya kurudi nyumbani sikuwa nikijua kinachoendelea , ubize niliokuwa nao juu ya kumuuguza mama umenifanya nisifuatiilie yanayoendelea kijijini , Baba alivyorudi alishawishiwa na kaka yangu kujiingiza katika biashara ya uchimbaji madini huko Mkoani

Njombe…”

Eliza aliendelea kumsimulia Hamza kilichotokea na ilionekana baba yake alitapeliwa.

Eliza anasema kuna wataalamu wa utafiti wa maswala ya madini walifika mkoani Njombe na kufanya utafiti wa uwepo wa Dhahabu ndani ya maeneo ya msituni ya mkoa huo , moja ya watu wa ndani ya mkoa walioshiriki katika utafiti huo ni kaka yake Eliza anaefahamika kwa jina la Hebert Mlowe, baada ya watalaamu wale kumaliza utafiti walitoa majibu yao kwa vijana wa mkoa huo ambao waliambatana nao ikiwemo Hebert na walisema eneo x katika shamba la Mzee Mlowe kuna kiasi kikubwa cha madini ya dhahabu ambacho kipo ardhini, majibu hayo ya kitaalamu yalimfanya kijana Hebert kupatwa na tamaa kubwa sana huku tamaa yake ikimpoza na kuamini kila kitu ambacho wataalamu walisema.

Baada ya watalamu wale kuondoka wakiahidi kurudi kwa ajili ya utaratibu wa kuanza uchimbaji , Hebert hakutaka fursa ya kuwa tajiri impite hivi hivi hivyo aliwajumuisha na wale vijana wenzake walioshiriki na wataalamu hao kisha walimpelekea taarifa mzee Mlowe juu ya uwepo wa madini ndani ya shamba lao la miti ya biashara , Hebert bila ya kuwa na uhakika alimhakikishia baba yake eneo hilo la shamba lao limebeba mali nzito itakayobadilisha maisha yao kabisa na Mzee Mlowe alijikuta akishawishika na kutumia kiinua mgongo chake chote kuwekeza katika uchimbaji wa Dhahabu, kiasi cha hela ambacho kilikuwa ni kidogo kutokana na kumaliza karibia ya robo tatu ya hela yote..

Baada ya kuchimba kwa muda wa mwezi mmoja hawakuambulia chochote na kiasi cha pesa walichowekeza kiliishia kwenye mchakato na kununua vifaa, yalikuwa matokeo mabaya kwao lakini Mzee Mlowe hakukata tamaa baada ya Hebert kumhakikishia wataalamu walisema madini yapo chini sana hivyo wasikate tamaa na kuendelea kuchimba..

“Nini kilitokea baada ya hapo?”Aliuliza Hamza huku akijua nini ambacho kinaenda kutokea.

“Walichukua mkopo kwa ajili ya kuendelea na aliewakopesha aliwapa kiasi mara kumi ya kile walichoomba”

“Na ndio kiasi gani?”Aliuliza Hamza na kauli ile ilimfanya hata Mama Mkubwa kujiinamia kichwa chini kuna namna Hamza aliona pia huyo mama alihusika.

“Milioni mia tatu, baada ya kupewa kiasi kikubwa hivyo cha pesa ukichaa wa hela uliwavaa, mwanzoni wakati baba amewekeza kaka na marafiki zake walihusika kwa kuchimba lakini mara baada ya kupewa mkopo hawakuchimba tena na waliweka vibarua , lakini hela yote hawakuitumia kama ilivyohitajika kwani walianza kufanya starehe na kucheza kamari”Alingea Eliza huku akiona hata aibu ya kumwangalia Hamza machoni.

“Kwanza inaoneana kilichotokea ulikuwa mpango wa hao watalaamu na pengine hawana utalaamu wowote na ndugu zako walikuwa wakiingizwa kwenye mtego , pia kitendo cha wakopeshaji kuwakopesha zaidi ya mara kumi ya kiasi cha hela walichotaka inaleta mushikeli ya matukio yote kuwa na muunganiko”Aliongea

Hamza na Eliza alitingisha kichwa kukubali.

“Sikujua kinachoendelea, mbaya zaidi baba ndio aliehusika katika taratibu zote za kuomba mkopo”

“Waliahidi nini kama dhamana ya mkopo?” “Asilimia hamsini ya faida itakayopatikana kwenye kuuza madini watakayopata”Aliongea Eliza na kauli ile ilimfanya Hamza kukunja ndita huku akipatwa na msisimko wa kujua kwa undani ni mpango gani unaendelea.

“Kwahio waliomkopesha baba yako baada ya kushindwa kulipa mkopo ndio hao waliokuja

kumkamata?”

“Bado sijajua , waliomkamata baba walijitambulisha kama polisi, lakini baada ya ndugu kwenda kituo cha polisi hakukuwa na taarifa zao jambo ambalo lilishangaza , baada ya kusumbua sana polisi wamesema Baba amesafirishwa kuja huku Dar es salaam , lakini mpaka sasa tumeshindwa kupata kujua baba ameshikiliwa gereza lipi na polisi hawataki kutoa ushirikiano..”Eliza alikuwa akitia huruma kweli.

Hata Hamza alimuonea huruma , isitoshe ilikuwa ni kama kila matatizo ya familia Eliza ndio aliekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa kuyabeba, kwanzia swala la mama yake mpaka swala hilo la familia yake.

“Kaka yako yeye yupo wapi?”

“Herbert ametoroka na milionni therathini zilizobakia na mpaka sasa hajulikani alipo”. “Poleni sana, hili swala nitalifanyia kazi ndani ya muda mrefu nitapata majibu , niambie ni watu gani ambao wametoa mkopo”

“Hamza unataka kufanya nini?”Aliuliza Eliza kwa wasiwasi.

“Hili swala mkiliendea kisheria hamtopata majibu kwa uharaka , hapa sio swala la mkopo kuna kitu kingine kinachotafutwa”

“Hamza sitaki kukuingiza kwenye matatizo yangu ya kifamilia, nimeenda benki kwa ajili ya kuomba mkopo kwa ajili ya kulipa mkopo huo na baada ya hapo nimeomba nafasi ya kwenda kufanyia kazi nje ya nchi, kule malipo ni maradufu zaidi ya hapa ,ndani ya miaka mitatu nitaweza kurudisha kiasi chote”Aliongea Eliza huku akionyesha hali ya usiriasi kwenye macho yake.

Licha ya kwamba Hamza alikuwa na hasira ya Eliza kutomhusisha katika matatizo yake lakini vilevie alizidi kumpenda , alikuwani mwanamke ambae hakosi njjia ya kutokea , lakini alijua kama akiruhusu swala hilo litokee basi mrembo huyo ataishia kupoteza ujana wake tu kwenye ulipaji wa madeni.

“Eliza unajua kabisa huu ni mtego umewekewa kwanini unataka kulipa kirahisi , ni kweli ndugu zako waliingizwa kwenye mtego lakini hujiulizi ni

kwanini iwe ni kwa familia yako tu?”Aliongea Hamza

“Najua lakini bado nashindwa kuelewa kwanini haya yanatokea?”

“Hatua ya kwanza ya kutatua tatizo ni kujua kiini chake ni nini , unaweza ukaenda nje ya nchi , unadhani kila kitu kitaishia hapo?”Aliongea Hamza huku akipandisha sauti na Eliza aliishia kuinamisha kichwa chini.

Ukweli Hamza alikuwa kuna kitu ambacho Eliza hamwambii na alijua kuna uwezekano wa hicho kitu ndio kilichoifikisha familia yake katika hatua hio ya kutengenezewa mtego.

“Eliza niambie kila kitu ili nipate kukusaidia , kukubali matatizo bila ya kujua chanzo sio njia sahihi ya kuyatatua”Aliongea Hamza huku akimwangalia Eliza.

Kitendo cha kuangaliana kwa sekunde kadhaa na Hamza machozi yalianza kumtoka mfululizo na haikuchukua hata sekunde alianza kulia kilio cha kwikwi jambo ambalo si tu kumshangaza Hamza lakini pia lilimshangaza na Mama Mkubwa wake.

Hamza alijikuta akihisi hisia mchanganyiko kwenye moyo wake , ilionyesha Eliza alikuwa akipitia wakati mgumu mno na kujitahidi sana kuficha kile ambacho anapitia na hali hio ilimfanya Hamza kuona licha ya kwamba walikuwa na muda mchache tokea wajuane ila hakuwajibika vya kutosha.

Aliishia kumkumbatia pekee na kumfuta machozi tukio ambalo lilionyesha kumgusa sana Mama Mkubwa.

“Eliza nyamaza na niambie nini kimekutokea”Aliongea Hamza kwa kumbembeleza lakini ilikuwa ni kama anaongezea mafuta kwenye moto.

Dakika chache baadae Eliza aliweza kutulia sasa na kuanza maongezi.

“Unakumbuka siku ambayo ulinikuta kwa mara ya kwanza nikidhalilishwa na watu ambao niliwakopa??”Aliuliza na Hamza alitingisha kichwa kukumbuka.

“Wale uliowakuta hawakuwa wahusika wakuu?”

“Unamaanisha kuna muhusika mwingine?”Aliuliza Hamza akiwa na utulivu na Eliza alitingisha kichwa kukubali.

“Kuna mwanaume nilikuja kukutana nae kipindi mama amelazwa hospitali ya taifa , hii ilikuwa ni siku kadhaa baada ya kupata mkopo kwa ajili ya kulipia matibabu ya mama , nakumbuka kwa mara ya kwanza nilikutan nae hoteli ya Serena akiwa pamoja na aliewahi kuwa Dokta wa hospitali ya taifa ambae alijaribu kunitaka kingono ndio mama afanyiwe matibabu , bahati nzuri nilikutana na Dokta mmoja ambae sasa hivi ni mkufunzi wa chuo cha Uchumi , ndio alienisaidia kufichua ushenzi ambao alikuwa akifanya yule Mkurugenzi kwani kesi zake zilikuwa nyingi kiasi cha serikali kumuwekea mtego”

“Ilikuwaje ukakutana nae Serena?”Aliuliza Hamza.

“Wakati mama anapatiwa matibabu huyu dokta aliniita ofisini kwake na kuanza porojo zake za kunitaka kimapenzi, nilikuwa nimechanganyikiwa kipindi kile na sikumpa jibu , siku kadhaa mbele aliniita hotelini na ndio nilikutana nae”

“Hili ni tukio la pili anaombwa rushwa ya ngono na daktari?”Aliongea Hamza ndani kwa ndani huku akikumbuka tukio lile la Kigamboni.

“Kwahio unaamini huyo mwanaume ambae ulikutana nae huko hotelini ndio chanzo?” “Ndio chanzo cha kile ambacho kilikuwa kikiendelea kwa Amosi na genge lake , Amosi ndio alienikopesha hela kwa ajili ya matibabu , kipindi kile nilikuwa desparate kumtibia mama na sikuwa na kazi ya kueleweka mpaka nilipokutana na Regina, baada ya kupata mkopo baadae ndio nilikuja kukutana na huyo mwanaume ambae alichokuwa akitaka kwangu ni kilekile , nilale nae kwa siku tano kisha afute mkopo wangu , nilimkatalia na matokeo yake yalikuwa ule udhalilishaji ulionikuta nao na nilishangaa hawakuja tena kunidai na kuomba msamaha kabisa”Aliongea Eliza.

“Wale niliwapa onyo mimi ndio maana hawakukusumbua tena , kama ulivyosema ni kweli basi huyu mtu bado hakuwahi kukata tamaa juu yako , lakini inafikirisha sana , kama yeye kweli ndio mhusika na ameenda mbali mpaka kumwingiza baba yako kwenye mtego basi kuna cha ziada”Aliongea Hamza.

“Wewe ndio uliewazuia kipindi kile? , kama ni hivyo kwanini unaamini kuna kitu cha ziada?”Aliongea Eliza huku akionyesha mshangao na macho ya shukrani kwa Hamza , hakuwahi kujua kama Amosi kutokumsumbua Hamza ndio alihusika lakini alipatwa na woga baada ya kuona pengine mzee yule sio ngono pekee anayotaka kutoka kwake.

Hamza kuna kitu ambacho alikuwa akifikiria lakini hakuwa na uhakika kama ni kweli na alipaswa kulitafutia hilo swala ufumbuzi, aliwaza hilo kutokana na uzoefu wake.

Hamza muda huo alikuwa ameweka umakini kwa Eliza na alisahau hata kuna mama aliekuwa pembeni na baada ya kugeuka aligundua Mama Mkubwa alikuwa ameloa machozi , ilionekana alikuwa ameguswa sana na maswaibu ambayo Eliza alikuwa akipitia.

“Bado sijajua ila naamini nitalifanyia ufumbuzi hili swala na lazima nitapata kitu”Aliongea Hamza lakini kwa Eliza licha ya kuwa na shukrani lakini bado alikuwa na wasiwasi na kile ambacho Hamza anakwenda kufanya , maana kwa alichokuwa akijua mtu huyo hakuwa mdogo , alikuwa tajiri ambae vigogo wengi wa kiserikali walikuwa wakimkingia kifua.

“Eliza pole sana mwanangu , hakuna aliekuwa akijua unapitia wakati mgumu kiasi hicho?”Aliongea Mama Mkubwa yake Eliza na kumfanya Eliza kutingisha kichwa.

Ukweli ni kwamba katika familia nzima ya Eliza Mama Mkubwa wake Merieta ndio ambae alikuwa akimjali mno na ndio yeye aliefunga safari kutoka kijijini kuja mpaka Dar kwa ajili ya Eliza , shida tu ni kwamba katika ukoo wote yeye ndio aliekuwa na hali ya chini ya kiuchumi , utajiri wake ulikuwa ni ukarimu na busara pekee lakini mbele ya ndugu zake hakuonekana wa maana.

Hata baba yake Eliza hakujali kabisa kuhusu mke wake wa kwanza kuumwa kwake , baada ya kupata kiinua mgongo alihamia mkoani kwa mke mdogo ambae ndio mama yake Hebert hivyo kumfanya Eliza kuhangaika mwenyewe kumtibia mama yake, uzuri wake tu ilikuwa ni kwamba licha ya kumtelekeza Eliza hawakujihusisha nae kwenye mambo yoyote na hata hela hawakumuomba baada ya kuajiriwa.

Licha ya yote Eliza alikuwa akiijali familia yake sana na alikuwa ndio kama kichwa cha familia na asingemuacha baba yake kuchukuliwa na watu bila kufanya chochote.

“Mama Mkubwa nadhani mpaka hapa nimepata pakuanzia , Eliza umesema ni watu gani wamemkopesha baba yako, kama ni shirika nitajie jina lake?”Aliongea Hamza na muda ule Eliza alimwangalia Mama Mkubwa akionekana ndio mwenye kujua jina hilo .

“Kwa ninavyojua sio kampuni wala benki , ni shirika la kukopesha watu kwa riba nafuu , wanajiita Utatu?”

“Utatu!!”Aliongea Hamza kwa kushangaa.

“Unawajua?”

“Sina uhakika lakini kuna umoja wa siri wa giza wenye washirika waliosambaa dunia nzima , unafahamika kwa jina la Black Trinity, huwezi kuelewa ila nadhani nishaanza kupata picha ya kile kinachoendelea”Aliongea Hamza.

“Nini kinaendelea Hamza mbona

unanitisha?”Aliuliza Eliza huku wasiwasi ukizidi kumvaa.

“Huna haja ya kuogopa kwanzia sasa , ili mradi nishaanza kupata picha ya kile kinachoendelea , hili ni swala ambalo napaswa kulishughulikia”Aliongea Hamza huku akipatwa na hisia mchanganyiko, alijua kama kweli ni Black Trinity ndio wanaojiita Utatu basi Eliza alikuwa kwenye hatari kubwa mno.

Hamza aliwahakikishia hakuna kitakachowapata na atamtafuta baba yake na kumrudisha salama na kisha aliaga na kuondoka.

Hamza mara baada ya kuingia kwenye gari alitoa simu yake haraka na kupiga simu kwenda kwa Dina na baada ya salamu alienda moja wa moja kwenye lengo la simu hio.

“Dina kuna kitu nataka unisaidie , Eliza yupo kwenye matatizo, unakumbuka ile siku uliniambia Eliza alikuwa shabaha inayolengwa kwa ajili ya kuingizwa ndani ya kampuni ya Dosam?”Aliuliza Hamza.

“Ndio, nini kimemtokea Eliza?”Aliuliza Dina na Hamza alimwelezea kwa ufupi kinachoendelea.

“Nataka uniambie nani alikuwa nyuma ya mkopo wa Eliza , sitaki kusikia ni yule Amosi najua kuna wa nyuma yake”Aliongea Hamza.

“Ni kweli kuna waliopo nyuma ya Amosi”

“Waliopo!?”

“Ndio ni swala nyeti sana ambao kwa kipindi kirefu nimejitahidi kukaa nje na kutokufukunyua , ila uzuri ni kwamba najua mmoja wapo na nadhani ndio huyo”Aliongea Dina na Hamza tabasamu lilimvaa palepale.

“Ni nani?”

“Acha haraka , ulivyoanza kuzungumzia hili swala umenifanya mwili wangu kusisimka , njia rahisi ya kumjua ni kupitia tukio la leo”Aliongea Dina.

“Tukio la leo!! , unamaanisha ninI?”

SEHEMU YA 81

Hamza aliona ni kama Dina anaonngea kimafumbo mafumbo na alitaka aende moja kwa moja.

“Unakumbuka nilimwambia Prisila leo kuna tukio la ufunguzi wa Albam ya msanii mmoja mkubwa hapa nchin na niende nae?”Aliongea Dina na Hamza hapo hapo alikumbbuka ndio.

“Nakumbuka vizuri?”

“Basi huyu msanii ni mkubwa mno na huyo mtu ambae namzungumzia lazima atakuwa mmoja wa wageni wa heshima wa tukio hili , nina uhakika hata mstaafu Mgweno atakuwepo , unaonaje tukishiriki wote watatu?”Aliongea Dina na Hamza hapo hapo aliona ni pendekezo zuri.

“Itakuwa vizuri nikishiriki, nitaenda kumpitia

Prisila nije nae”

“Vizuri , mimi nitatangulia na kukuwekea utaratibu wa kupata kadi ya mwaliko”Aliongea Baada ya Hamza kukata simu alimtumia ujumbe Prisila kwamba atampitia kwa ajili ya kwenda kwenye sherehe za ufunguzi wa Albamu na Prisila alijibu dakika hio hio kwamba atamsubiri.

Muda alikuwa nao wa kutosha na alitamani kurudi kwenye kampuni lakini aliona sio chaguo sahihi hivyo alipeleka gari mpaka fukwe ya Coco na kisha alishusha kiti na kusinzia.

Saa kumi na mbili hivi aliwasiliana na Prisila na alimtajia anapoishi na Hamza mara baada ya kuijua Anuani inaelekeza wapi alichoma mafuta kwenda huko na ilimchukua dakika kama kumi na tano mpaka kufika nje ya nyumba kubwa yenye ukuta na Geti jeusi lililonakshiwa na rangi ya shaba.

Lakini sasa muda ambao Hamza anasimamisha gari pembeni kwa ajili ya kugonga geti , gari nyingine ilisimama kando yake, ilikuwa ni moja ya gari ya kifahari na ilionekana pia uelekeo wake ni ndani ya nyumba hio.

Hamza mara baada ya kufungua mlango na kutoka na gari ile aina ya Cadillac S series toleo jipya ya rangi ya bluu ilifunguliwa mlango na palepale Hamza alimfahamu bwana huyo ambae alionekana kupendeza mnno.

Alikuwa amevalia suti ya Armani na suruali ya Zegna , mtu yoyote angemuona kwa macho ya haraka angeweza kumfahamu ni mtu muhimu kwenye jamii.

“Bosi Side naona ni bahati nyingine tunakutana”Alisalimia Hamza huku akikunja ndita “Hamza!, unafanya nini hapa?”Aliuliza Side huku akikunja sura kama amelishwa pilipili.

Kabla hata ya Hamza kujibu hilo swali mlango wa geti ulifunguliwa na alitoka Prisila ambae alionekana ameshavaa makeup lakini mavazi bado , urembo wake uliongezeka maradufu.

“Hamza umewahi mno , nilikuambia uchelewe chelewe”Aliongea Prisila huku akitoa tabasamu. , lakini alionyesha mshangao mara baada ya kumuona Side , ilionekana alifika hapo bila taarifa.

“Side unafanya nini na wewe hapa ?”Aliuliza.

Muda ule Side hakumjali tena Hamza na alitoa tabasamu lake la kimauaji huku akitoa ua la Rose kutoka kwenye gari.

“Prisila najua wewe ni shabiki kindaki ndaki wa msanii Almasi na leo ni siku ya kuzindua rasmi albamu yake , nina mwaliko nataka tutangulizane wote”Aliongea kwa swaga nyingi mno kama vile ni mwanamfalme.

Prisila alijikuta akiyaangalia maua na kisha bila hata ya kujielewa macho yake aliyaelekeza kwa Hamza huku akionyesha hali ya kusita.

Baada ya kujifikiria kwa sekunde aliishia kupokea lile ua kwa ajili ya kutoonyesha ujeuri.

“Asante sana Saidi , lakini umejuaje namshabikia Almasi na sio King?”

“Nimekufollow instagram na mara nyingi naona maoni yako ya kumkubali Almasi” “Oh kumbe “Aliongea huku akionyesha kutofikiria sana isitoshe hata yeye alikuwa akiona maoni ya Saidi mtandaoni.

“Saidi nilikuwa nikijiandaa kwa ajili ya kuelekea huko ndio maana Hamza yupo hapa kwa ajili ya kunichukua”

“Ulikuwa na mwaliko , wewe na Hamza!!?”Aliongea Saidi huu akionyesha mshangao.

Lakini side muda huo alikuwa akijiuliza inamaana Lea hakumwambia Prisila juu ya Hamza kujihusisha na magenge ya kihalifu.

Aliishia kumwangalia Prisila kwa namna anavyomwangalia Hamza na kila kitu kilijionyesha na ukauzu ulimvaa palepale lakini alijitahidi kujionyesha kuwa kawaida , alitamanni bora hata angekuwepo Chriss kidogo angeweza kuonyesha ukichaa wake waziwazi lakini aliupotezea mara moja.

“Prisila nataka leo uwe partner wangu usinikatae, sikukutaarifu moja kwa moja maana nilijua huna wa kwenda nae”Aliongea .

“Side kama nilivyosema nishakubaliana na Hamza kwenda nae na tuna mwaliko , ni kosa lako kuchelewa, Hamza naenda kuchukua mkoba wangu tutapitia Malkia Stylish nivae gauni langu”Aliongea Prisila na bila ya kusubiri alirudi ndani na hazikuchukua sekunde nyingi aliweza kutoka na kumpa ishara waondoke.

“Bosi Side naomba utuwie radhi tutatangulia wa kwanza”Aliongea Hamza na muda ule Saidi alijihisi ni kama atapasuka kwa hasira.

“Prisila fikiria mara mbilimbili , ukienda na mimi utakutana na watu wazito na itakuwa faida kwako”

“Asante Side naenda kumshuhudia msanii ninaemshabikia na sio kukutana na watu wazito” “Prisila kwanini hutaki kunielewa tokea tukiwa shuleni mpaka sasa najitahidi kukuonyeshea ninavyojisikia , lakini kwanini hujawahi kunisikiliza”

“Saidi kwanini ghafla tu unaongea yote hayo..”Aliongea Prisila huku hasira zikianza kumvaa na Saidi hakutaka kumsababishia hasira zaidi.

“Usikasirike Prisila , sijaja kwa ajili ya kukasirisha hivyo naondoka, Hamza hakikisha

Prisila anakuwa salama”

“Usiwaze bosi , Prisila ni mwanafamilia , hawezi kupatwa na tatizo lolote chini ya himaya yangu”Aliongea Hamza lakini kauli ile ilimfanya Side kumwangalia Hamza kwa macho makali bila kuongea neno.

Upande wa Hamza alijikuta akikunja ndita , sekunde hio kuna kitu ambacho alihisi na sio cha kawaida ni msisimko wa ajabu ambao ulimtoka Saidi.

Lakini sekunde kadhaa tu msisimko ule ulipotea na hakuweza kuhisi kitu chochote tena na alijikuta akijiuliza nini kimetokea au amehisi vibaya.

“Hamza hakuna kinachoendelea kati yangu na Saidi na haitokuja kutokea hivyo usije kunidhania vibaya , nimepokea zawadi yake ya ua kwasababu sikutaka kuonekana nina jeuri”

“Usiwe na wasiwasi , mwanamke kama wewe kufuatiliwa na wanaume wengi inamaanisha ni mzuri , sio jambo baya”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu huku akijiuliza kwanini rafiki yake huyo wa utotoni anajitetea mno kwake au ashampenda.

Prisila aliishia kutoa tabasamu baada ya kuona Hamza hana ishara yoyote ya kumdhania vibaya na muda huo huo walianza safari.

“Hamza vipi ile siku walikutoa saa ngapi?”Aliuliza Prisila.

“Ukweli nilienda kama kutalii tu na kurudi , sikukaa muda mrefu”Aliongea Hamza na Prisila alitingisha kichwa kukubali.

“Vipi Regina anaendeleaje , sijawasiliana nae muda mrefu?” “Kama kawaida yake , nadhani unamjua rafiki yako alivyo”

‘”Wee unaongea kama vile una ukaribu nae sana siku hizi”

“Ndio ukaribu wetu ni mkubwa”Aliongea Hamza na kumfanya Prisila kutoa tabasamu lililojaa maswali.

Dakika chache tu Hamza alisimamisha katika moja ya duka kubwa la nguo za kike na ilionekana wauzaji walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kumhudumia , licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda lakini walionekana uwa na ari kubwa.

Dakika chache tu lilitolewa gauni la rangi nyeupe na nyeundu kama main tone , ambalo limedariziwa shingoni na Velvet , Chiffon na vitambaa vingine vya rangi ya dhahabu na kutengeza shingo yenye upo la Almasi.

Baada ya Prisila kwenda kulivaa na kurudi wahudumu wa duka hilo walitoa macho kutokana na kupendeza kwake.

“Jamani hilo gauni limekupendeza , ni kama vile limetengenezwa kwa ajili yako pekee”Aliongea muhudumu huku akimuonea Prisila wivu kwa urembo wake.

“Prisila nakukumbusha hili gauni ni kwa ajili ya matangazo ya duka letu”Aliongea mdada mmoja mweupe hivi mwenye uso wa duara na mwanya.

“Hilda mbona unakumbushia sana wakati naelewa , isitoshe hata kama nataka kulinunua ni bei kubwa sana”Aliongea Prisila na Hamza mara baada ya kusikia kauli ile alitoa simu yake na aliingia kwenye internet na kupiga simu kwenda nje ya nchi na ndani ya dakika chache tu alianza kuongea Kifaransa.

Na kitendo kile kilimfanya Prisila kumshangaa Hamza kwani licha ya kwamba hakuwa akijua lugha ya kifaransa lakini kwa kusikia tu alikuwa akiijua lugha hio , sasa alishangaa kuona Hamza anaongea tena kwa ufanisi mkubwa.

“Hamza hicho ni kifaransa?”Aliuliza Prisila. “Ndio ni kifaransa”Aliongea na Prisila alionyesha ushangaa.

“Kumbe unajua kuongea kifaransa tena unaonekana unaongea kwa usahihi kabisa , ulikuwa ukiongea na nani?”

“Nitakuambia baadae”Aliongea Hamza huku akionyesha tabasamu , ndani ya dakika chache tu walitoka ndani ya eneo hilo na kurudi kwenye gari kwani kila kitu kiliuwa kimekamilika kwa upande wa Prisila.

Kutoka Malkia EmpireStylish mpaka Mlimanni City tukio linakofanyikia iliwachukua dakika kumi na mbili hivi na baada ya Hamza kuiingiza Maybach ndani ya eneo hilo Kamera za waandishi zilianza kumulika upande wao.

Hamza akiwa kwenye gari aliweza kumuona Dina akiwa ameshafika na alikuwa juu ya redcapert.

Watu walionekana kuwa wengi ndani ya eneo hilo na ulinzi pia ulikuwa sio wa kawaida na haraka haraka ilionyesha kuna kiongozi mkubwa ambae anakwenda kuhudhuria hilo tukio.

Hata Prisila licha ya kwamba alikuwa na hamu zote za kushiriki tukio hilo lakini baada ya kuona idadi hio kubwa ya watu maarufu mabimbali pamoja na Kamera za Redcarpet wasiwasi ulianza kumwingia , kwake ilikuwa ni mara ya kwanza kuhudhuria tukio kubwa la namna hio.

ITAENDELEA ijumaa watsapp 0687151346
 
Bunamu mgosi katushinda tabia, tumuache afanye anavyotaka. Jina binamu limenikumbusha marehemu binamu Warumi jamani
Binamu, mgosingwa sio mkimalifu katika ahadi zake kabisa....
 
  • Thanks
Reactions: ram
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTUNZI: SINGANOJR

SEHEMU YA 82.

IMEDHAMINIWA NA WATSAPP VIP GROUP

Waandishi wa habari walianza kujiuliza maswali wao kwa wao wakitaka kujua mwanamke alieshuka kwenye gari ya kifahari ni nani .

Prisila hakuzoea maisha ya Kamera hivyo aliishia kuinamisha kichwa chake chini kwa nana ya kutotaka sura yake kuonekana.

Hamza hata yeye hakujua ndani ya eneo hilo kungekuwa na vyombo vya habari ,lakini yeye hakuwa na wasiwasi hata kidogo , kama ni matukio makubwa alikuwa ashashiriki mara kibao hivyo alitembea kwa kujiamini.

Hamza na Prisila hawakusimama kwenye redcapert, Dina aliishia kuwakabidhi kadi zao mwaliko na kisha kuzionyesha na kuruhusiwa

Baada ya kuingia kwenye ukumbi Prisila mwili ulimsisika , kulikuwa na watu wengi ndani ya eneo hilo wengine wakiwa ni watu wazito ambao aliwajua lakini hakuwahi kuwa na ukaribu nao.

Wanaume kwa wanawake walimwangalia Prisila kwa macho ya matamanio na wivu , licha wanawake wengi wengi kupendeza waliona wivu kufunikwa na Prisila mrembo ambae sio maarufu.

Muda huo kabla hajawaelekea kwenye sehemu zao kukaa sauti ikiliita jina la Prisila ilisikika.

“Kwaho wewe ndio Prisila?”

Kauli ile ilimfanya Hamza na Prisila wote kugeuka na macho kwa macho waliweza kukutana na Salma , Hamza alikuwa akimjua ila upande wa Prisila alionekana kutomfahamu.

“Ni wewe tena?”Aliongea Hamza huku akikunja sura.

“Hamza huyu ni nani , ananijua lakini mimi simjui”Aliuliza Prisila.

“Jina lake anaitwa Salma ni mpenzi wake Saidi”

“oh , kumbe , mambo Salma”Alisalimia Prisila kwa upole lakini upande wa Salma alionekana kutompenda waziwazi Prisila.

“Sitaki salamu yako , nakupa onyo kaa mbali na Saidi”Aliongea Salma huku akiweka mwonekano wa kejeli mbele ya Prisila

“Hakuna kinachoendelea kati yangu na Saidi , utakuwa huna taarifa zote”

“Sina taarifa?, Saidi ametokea nyumbani kwako kwa ajili ya kukuchukua na ameenda mbali mpaka kukuandalia gauni . halafu unasema sina taarifa, huna aibu kuchanganya wanaume wawili kwa wakati mmoja”Aliongea Salma na kauli yake ilimfanya Prisila kupaniki.

“Sina mahusiano yoyote na Saidi, ni ukorofi kuwaza kitu ambacho huna uhakika nacho”Aliongea Prisila huku akianza kutokufurahishwa na tabia ya Salma , lakini alijiuzuia maana eneo hilo lilikuwa na watu wengi ambao walionekasna ni kamma wanasikiliza mazungumzo yao.

“Salma unafanya nini?”Aliongea Saidi ambae alionekana kusogea eneo hilo kwa spidi na alimwangalia Salma kwa macho makali mno na kumfanya kuwa na wasiwasi kidogo

“Saidi naomba unisamehe , najua nilikukosea usinifanyie hivi , huyu mwanamke haijui kipi ni kizuri kwake na hana thamani ya kupoteza muda wako”

“Sikia Salma usinikasirishe , nishawambia mimi na wewe basi , ondoka”Aliongea kwa hasira.

Salma uso wake ulikuwa na hasira mno , ijapokuwa Salma hakuwa maarufu sana lakini alikuwa akitokea familia ya matajiri kuliko hata Saidi ambae ni Mkurugenzi tu ndani ya shirika la mitandao ya simu.

Lakini licha ya mwanamke huyo kufokewa na Saidi hakukasirika zaidi alimwangalia Prisila kwa macho ya hasira mno.

Hamza mara baada ya kuona tukio hilo alijiambia siku zote matajiri hawakosi cha kuchukia kwa watu waliowazidi kipato.

“Saidi mimi na wewe hayajaisha bado”Aliongea Salma kwa hasira na kisha aliondoka na kuwaacha.

“Prisila umependeza sana”

“Asante sana Saidi”

Hamza hakutaka kuendelea kusimama na Saidi maana ashaanza kumchoka hivyo mara baada ya kuangalia upande ambao Dina yupo alipa ishara ya kusogea.

Saidi licha ya kuonyesha kutoridhishwa na Prisila kuwa karibu na Hamza lakini hakuwa na chakufanya kwa usiku huo.

Dina ndio ambae alionekana kufahamiana na watu wengi mno na ndio ppekee aliekuwa bize huku Hamza na Prisila wakiwa wametulia wakisubiria ratiba nzima kuanza.

Saa tatu kamili karibia wageni wote walioalikwa walikuwa wamekisha kufika mpaka wale wa muhimu zaidi ambao walikaa viti vya mbele , upande wa Hamza wao walikaa mstari wa tatu kutoka vilipo viti va VIP.

Hamza hakuwa hapo kwa ajili ya uzidundu huo wa albamu kabisa , alichokuwa akitaka ni kumuona huyo mwanaume ambae inasemekana anajihusisha na umoja wa Black Trinity.

Dina upande wake alitaka kumsaidia kwa namna yoyote Hamza lakini mpaka uzinduzi unaanza Dina hakuonyesha ishara yoyote ya kuuona mtu ambae alimtarajia na aliishia kumtingishia kichwa kumuashiria hayupo jambo ambalo lilimfanya kidogo kutoyafurahia matokeo maana alitaka kumaliza swala hilo usiku huo huo.

Prisila upande wake hakuwa akijua hata kinachoendelea kutokana na umakini wake kuueekezea jukwaani.

Wakati Hamza akijishawishi kuangalia uzinduzi huo muda uleule simu yake ilianza kunguruma ikiashiria ilikuwa ikiita , Hamza aliitoa haraka haraka na kuangalia nani anapiga na namba ilionekana ngeni na kumfanya akunje ndita.

“Prisila naenda msalani mara moja”Aliongea Hamza na Prisila aliekuwa amenogowa aliishia kutingisha kichwa.

Hamza mara baada ya kuingia msalani hakuchelewa kupokea simu ile .

“Hello”

“You are Hamza?”Sauti ya kingereza iliojaa lafudhi ya kizungu ilisikika/

“It’s me”Alijibu Hamza akimaanisha ni yeye.

“Not bad , its took me so long to find out what the hell you are

*******

Asubuhi siku iliofuata Eliza na Hamza walianza safari ya kurudi Dar Es salaam, itistshe wote walikuwa na kazi za kufanya kwa siku hio na isingekuwa vizuri kuchelewa.

Muda ambao Hamza alikuwa akitoka kwenye treni ya mwendokasi akifikiria kuchukua taksi kumpeleka kwenye kampuni , simu yake iliita na alivyoangalia aliekwua akipiga ni Shangazi.

“Hamza upo wapi?”Ndio kitu cha kwanza alichoweza kusikia Hamza huku sauti ya Shangazi ikionyesha kuwa na utofauti.

“Ndipo nje ya stendi ya treni ya mwendokasi nataka nielekee kazini , nini kimetokea shangazi?”

“Madam.. ametutoka” Sauti ya Shangazi ilionyesha alikuwa akishindaa na majjonzi.

Hamza alishikwa na mshituko kwa sekunde kadhaa licha ya kwamba ni kitu ambacho alitarajia.

“Regina anafahamu?”

“Ndio maana nimekupigia , nnimeshindwa kumpata kwa simu na nyumbani hayupo, nilijua upo nae”Aliongea Shangazi na kauli ile ilimpa mshituko Hamza na kujua lazima kuna kitu kilichomtokea Regina.

SEHEMU YA 83.

Hamza alijifikiria kwa sekunde na palepale alipata wazo juu ya kitu cha kufanya.

“Shangazi usiwe na wasiwasi , ngoja nimtafute Regina”Aliongea Hamza na kauli yake ilimfanya Shangazi kujua kuna kitu kimetokea.

“Hamza huu ni muda wa dharula kwa familia na Kampuni ya Dosam , kwasababu ya kukaa hospitalini nnimeshindwa kuwa karibu na Regina , lakini wewe mume wake kisheria hivyo unapaswa kuminda na kuhakikisha hakuna kibaya kitakachomkuta..”Aliongea Shangazi huku akionyesha usiriasi wa hali ya juu.

“Shangazi usiwe na wasiwasi , nitampata Regina muda si mrefu”

Hamza mara baada ya kukata simu alijaribu kupiga namba ya ofisini kwa Regina na aliepokea alikuwa ni Linda.

“Linda Mkurugenzi yupo ofisini?”

“Nilitaka nikuulize na wewe pia kama Mkurugenzi upo nae?”Aliongea Linda kwa sauti ya kuroridhika.

“Hapana sikuwa nae , wewe mara ya mwisho ulimuona saa ngapi?”

“Tuliachana jana baada ya Overtime, kwanini unauliza , nini kimempata mkurugenzi?”Aliuliza Linda lakini Hamza hakuwa na muda wa kujibu swali lake na alikata simu palepale na kumgeukia Eliza.

“Eliza unaweza kutangulia kwenda kazini kwanza”

“Kuna kilichompata Bosi?”Aliuliza Eliza akiwa na wasiwasi.

“Sijui nini kinaendelea kwasasa , wewe tangulia ngoja mimi nikamtafute”

Eliza aliishia kutingisha kichwa kukubaliana na Hamza maana aliona hakuna muda wa kupoteza.

Hamza alichukua taksi na kuelekea uelekeo wa kituo cha polisi na akiwa njiani aitoa simu yake na kumpigia Afande Himidu ili kumuungaisha na tu yoyote wa polisi na kazi hio ilifanywa haraka sana na Hamza aliambiwa aelekee kituo cha polisi Posta atakutana na kamishina Maningi.

Dakika kama kumi tu aliweza kufika eneo ambalo alielekezwa na mara baaada ya kushuka tu aliweza kuuona Afande huyo akiwa anamsubiri nje.

Alikuwa ni Afande yule yule ambae alimhoji siku kadhaa ziliozopita juu ya Ankh.

Hamza hakutaka kutumia njia za kawaida kripoti kupotea kwa Regina , alichotaka ni mtu wa kumsaidia ili aweze kujua ueleko wake , baada ya kukutana na Afande huyo alimwelkeza shida yake ni kutaka kuangalia uelekeo wa Regina kupitia satilaiti.

Lilikuwa ni ombi kubwa kutoka kwaHamza maana Tanzania kama Tanzania haikuwa bado na satilaiti bali jeshi la polisi lilikuwa likishirikiana na Satilaiti ya Ethiopia.

Hamza alikuwa ashafahaika ni mtu mzito tayari kutokaa na kufahaiana kwake na Mshauri mkuu , hivyo ombi lake lilishughuikiwa mara moja , yeye pia aliingizwa kwenye chumba cha Surveillance.

Dakika chache tu wataalamu wa kitengo cha picha za satilaini waliweza kupata Vidio za gari ya Regina ikiingia mtaa wa Egret jana usiku na kutoka tena asubuhi ya saa moja na nusu.

“Hii ndio gari yake asubuhi ya leo alivyotoka , lakini kitu cha kushangaza badala ya kufika hapa Ovis alitakiwa kuelekea upande wa daraja la Kigamboni na sio Kisiwani, lakini baada ya hapo gari yake haijaonekana tena , kuna uwezekano ilisimama njiani”

Hamza aliishia kuongea umakini wake kwenye rekodi hizo za matukio na alijikuta akitingisha kichwa kana kwamba kuna kitu ambacho alikuwa amepata kuona.

“Dereva wa hili gari sio Regina’Aliongea Hamza.

“Hamza unamaanisha hii sio gari ya Regina?”

‘Gari ni ya Regina lakini dereva sio yeye , hizi rekodi za matukio hazionyeshi nani ni dereva kutokana na vioo vyake kuwa giza ,hivyo kitu pekee ambacho tunaweza kutumia kumjua dereva ni ufundi katika kuendesha gari, kutoka mwanzo mpaka mwisho”

“Kwanini umefikiria hivyo?”Aliuliza Kamishina na Hamza alinyoosha kidole katika kamera tofauti tofauti zilizokamata matukio.

“Angalia picha za jana kwanza namna ambavyo alikuwa akiendesha wakati wa kurudi nyumbani na kisha fanannisha na namna anavyoendesha leo, ukiangaia za jana unaona anachukua muda mrefu sana kwenye kukata kona na spidi ya gari inapungua mno , huu ndio staili ya Regina kuendesha gari kwasababu bado sio dereva mzuri ukiangalia za leo unaona kabisa utofauti wa namna anavyokunja kona akiingia barabara kuu, angalia tena alivyofika Ovis kuingia barabara ya Mwalimu nyerer spidi yake aliotumia ni tofauti kabisa, uendeshaji huu sio staili ya Regina na inaonekana kabisa ni mtaalamu ambae ana uwezo wa juu kwenye kuendesha gari , kama hisia zangu zipo sahihi huyu dereva ndio atakuwa mtekaji”Aliongea Hamza kwa kirefu na maneno yake yaliwafanya polisi kushangaa kwani ilikuwa ni sahihi kabisa

“Hamza kwahio unachomaanisha Mkurugenzi Regina ametekwa leo asubuhi wakati akielekea kazini?”Aliuliza Kamishia na Hamza alitingisha kichwa kukubalki.

“Na waliohusika ni wataalamu wa hali ya juu sana , wameamua kutumia gari yake ili kutuchanganya katika uchunguzi ili tusijue ni muda gani ametekwa na mlolongo wa uchunguzi uchukue muda mrefu mpaka kuwafikia , lakini kitu ambacho hawajaweza kujua ni kwamba kila binadamu anafikiria tofuati na kusahau kwamba kuendesha gari ni kama kutembea kwa mguu , kila mtu anazoeleka kwa staili yake”

Polisi waliokuwa wakimsikiliza waliishia kutingisha cichwa vyao tu kuyakubali maelezo ya Hamza , alionekana fundi kwenye kutoa uchanganuzi wa tukio zima.

“Upo vizuri sana kwenye kuchanganua matukio ya ki uhalifu , lakini hapa swali bado linabakia ni wapi wamempeleka?”

“Angalia kwa kurudisha muda nyuma kidogo ili tujue magari yote yaliopita nje ya nyumba”Aliongea Hamza na mtaalamu wa Camera haraka haraka alichezesha na ndani ya sekunde kadhaa alianza kuhesabu magari , uzuri ni kwamba mtaa huo ulikuwa ukijitegemea hivyo hakuwa na magari mengi.

“Angalia Plete number ya hilo gari la mikate?”Aliongea Hamza na kazi hio ilifanywa kwa sekunde tu lakini plate naumber ile ilikuwa ni ya kufoji.

“Jaribu kuiscan tuone ni wapi na wapi ilipita”Aliongea Hamza na ndani ya sekunde chache tu ilionekana ikisimaa eneo la Tungi.

“Hio sehemu kuna Gereji maarufu kama Tungi Bay Garage na pia kuna kampuni ambayo inanunua makari chakavu ndani ya eneo hili, ni eneo ambalo pembeni yake kuna magodown mengi , kuna uwezekano atakuwa amefungiwa hapo”Aliongea Afande mmoja na Hamza alitingisha kichwa kuna uwezekano huo.

“Afande Asante kwa msaada wako , kwanzia hapa nitalishughulikia hili mwenyewe , kama kuna mabadiliko nitaomba msaada”

“Mr Hamza nadhanni ni vizuri ukiacha polisi tuifanye kazi yetu”Aliongea Kamishina Maningi kwa heshima.

“Hakuna haja , wanachokitaka hawa ni hela, kama shida ilikuwa ni kumuua haikuwa na haja ya kwenda mbali na kuanza kumteka , wametuchanganya kwa kutumia hila kwa ajili ya kuvuta muda ili wapate muda mwingi wa kufanya maongezi na kwa tabia ya Regina lazima watakuwa wamejua anaweza akawasumbbua kwa muda mrefu , nina uhakika nitampata akiwa salama, pia inaweza ikawa hatari kama Polisi wakivamia hili eneo”Aliongea Hamza kwa msisitizo na Kamishina kwasababu alihushuhudia uweo wa Hamza hakuweza kupinga na alimpa ruhusa afanye inavyowezekana lakini aliomba baada ya Regina kupatikana wao watachukua jukumu lao la kuwakamata watekaji.

Hamza hakubisha , alijua kutekwa kwa Regina lazima kuakuwa kuna husiana na hisa alizopewa na bibi yake na isitoshe bibi yake amekwisha kufariki tayari .

Hamza alijua licha ya Regina atateseka kwa muda lakini hatokuwa katika hatari kwani kama wakimjeruhi hawatopata kile wanachokita.

Hamza baada ya kuchukua taksi ndani ya dakika chache tu aliweza kufika eneo la Kibada

Muda ambao alitoka kwenye gari , hisia za kufuatiliwa zilimpata palepale, utashi wake wa kuzuia kufuatiliwa ulikuwa umebadilika mno kutoka iaka kadhaa iliopita.

Hamza alijiambia enzi zake za nyuma alikuwa mtaalamu mo na hakuna mtu wa kuweza kumnasa kwenye rada akitaka kufika ndani ya eneo kwa siri , lakini hata hivyo hakujali.

*****s

Katika chumba ambacho kina mwanga hafifu , Regina alikuwa amekalishwa kwenye kiti huku akiwa amefungwa mikono na miguu isiwe rahisi kutoroka.

Muda huo mwanamke mwenye macho makavu alionekana kumkodolea macho kwa ukauzu mkubwa

“Usiku mmja umepita lakini hutaki kula , una kiburi sana wewe mtoto , ngoja nikuabie huna muda wa kunisubirisha zaidi , masaa niliokupatia yamekwisha isha”

“Lamla najua tokea mwanzo hujawahi kunipenda lakini sijawahi kudhania unaweza kufanya kitendo cha kishenzi namna hii”Aliongea Regina huku sauti yake ikioneysha alikuwa kwenye aumivu,

Jana usiku wakati akirudi kutoka kazini alipokea simu kutoka kwa Lamla akimtaka afungue mlango na ndio muda aliotekwa , vinginevyo kwa mfumo wa ving’ora vya ulinzi wa jumba lake wasingefanikiwa kumteka kirahisi.

Alijua licha ya Lamla kutaka kupigania urithi wa mtoto wake Frank lakini hakuamini Lamla alikuwa akishirikiana na Familia ya James

“Eti ushenzi , mwisho wa siku t utajua nani ni mshezi kati yangu au wewe , mama yako alikuwa kijakazi wa familia yangu lakini akajilengesha kwa mume wangu na kupata ujauzito , wewe ni mtoto wa kishenzi ulietokana na tabia za kishenzi za mama yako halafu unataka kurithi kampuni ya Dosam ,Hao vikongwe unaowaita bibi na babu wote ni vichaa , hivyo nakwambia mtoto kama wewe wa nje ya ndoa huwezi kuchukua urithi wa mwanangu”

“Unaongea ujinga , mama alikuwa akifahamiana na baba kabla yako , kama sio kuyumba kwa biashara za familia yenu usingekuja kuwa na ukaribu na baba yangu , unadhani sijui kwa kipindi chote una mahusiano na Mzee Benjamini na baba yake hakukupenda kutokana na tabia zako ndio maana ukaangukia kwenye mikono ya baba?”Aliongea Regina kwa hasira.

Kauli ile ilimfanya uso wa kujichumbua wa Lamla kuanza kuota mapunye.

“Wewe mtoto ni mpumbavu sana , unatoa wapi ujasiri wa kuongea pumba mbele yangu ,ngoja uone kama sito..”Kabla hajamalizia sentesi yake mlango wa chumba hicho uifunguliwa kwa nnje na alionekana Mzee Benjamini na James wakiingia kwa haraka.

“Lamla tunapaswa kuhamia eneo lingine”Aliongea mzee Benjamini huku akionyesha wasiwasi.

“Nini kimetokea?”

“Hamza ashajua tupo hapa na amefika tayari”Aliongea

“Nini , inamaana Tui ametudangana kulizingira hili eneo na uchawi?, kama sio hivyo imekuwaje Hamza ameweza kutupara haraka?”Aliongea Lama huku akionyesha hasira ya wazi.

Regina mara baada ya kusikia habari hizo uso wake ulianza kushikwa na ishara ya furaha na aliishia kungata lipsi zake akiwa na muonekano usioelezeka

Jana tokea aachane na Hamza kwenye kampuni alikuwa na hasira nae mno kwa kumsingizia kitu ambacho hajafanya na kumfikiria zaidi Eliza kuliko yeye , lakini kwa muda huo mara baada ya kujua Hamza amekuja kumuokoa , ile hasira yake iliyeyuka mara moja.

Lakini hata hivyo Regina alijua adui aliemteka awamu hio sio wa kawaida maana alikuwa akitumia nguvu za kichawi na kuna uwezekano Hamza kujiingiza kwenye mtego.

Roho zilizotelekezwa ama kwa kingereza wanajiita Wandering Soul ndio watu waliohusika kumteka Regina na Mzee Benjamini na hawala wake Lamla walitumia nguvu kubwa kuwafanya mawasiliano maana shirika hili lilikuwa la siri mno lililojichimbia maeneo ya Mtwara

Waliamini kwa kutumia watu ambao wanatumia nguvu za giza kuficha uelekeo wa eneo lao ingekuwa rahisi kutimiza azma yao kupata kile wanahcokihitaji kutoka kwa Regina

Tokea binadamu aanze kujua siri iliokuwa juu ya nishati za mbingu na ardhi maeneo mengi ya mipaka ya nchi yalikubwa na aina nyingi ya nguvu za giza , hii ndio maana nchi nyingi zilifungua fitengo vya usalama vya jeshi kwa ajili ya kupambana na nguvu hizi.

Kutokana na ugumu wa kuvuna nishati za mbingu na ardhi kwa njjia ya kawaida na kufikia mafanikio , wengi walitumia kanuni hizo hizo ili kuufanya uchawi wa kawaida kuwa na nguvu maradufu na watu wengi walichukulia hilo kama fursa na kutengeneza mbinu hizo na moja ya shirika ambalo lilikuwa linafundisha mbinu ya muunganiko wa nguvu za giza na nishati za kuamsha pepo la ndani ni huu umoja wa Nafsi zilizotelekezwa.

Kundi hili kitengo cha Malibu kimetumia nguvu kubwa ya rasilimali kwa ajili ya kukiangamiza lakini walishindwa kutokana na hila nyingi ambazo zilitumika , ikiwemo matumizi makubwa ya mbinu yao ya Magiv of illusion , mbinu ambayo unaweza kufika eneo na kuhisi halina watu lakini watu wapo na wanakuangalia tu wewe huwaoni.

Kiongozi wa kundi hilo alifahamika kwa jina la Tui kwa jina la kawaida lakini akiwa ndani ya umoja huo anajiita Mpweke au The Loner.

Inaaminika kwamba The Loner alikuwa ni mwanajeshi wa kitengo cha Wachawi kabla ya kitengo hicho hakijapwa jina lingine la sasa ambalo ni la Malibu , Baada ya kusingiziwa kuwa msaliti jeshini na kufukuzwa ndio alinzisha kundi hili ambalo lilijiita Nafsi zilizotelekezwa na madhumuni yake ilikuwa ni kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa watu ambao walimsingizia ilihali hakuwahi kuwa na kosa bali alifanywa kuonekana msaliti na moja ya marafiki zake.

Serikali ilikuwa ikipambana sana na hili kundi kutokana na matukio ya wanajeshi wengi kukubwa na ukichaa na wengine kufa vifo ambavyo havikuelezeka kwa lugha ya kibinadamu na hapo ndio umaarufu wa kundila Nafsi zilizotelekezwa uliibuka.

“Madam ijapokuwa tumelizindika hili eneo kwa mbinu yetu ya Mazingara haimaanishi kwamba tupo na kinga zidi ya mtaalamu mwenye mafunzo ya aina yetu , kama ulikuwa ukiumuona Hamza kama mtu mdhaifu kwanini umetumia kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kutukodi na kuachana na kundi la Nyoka Mwenye masikio?”

“Tunajaribu kuwa makini hapa , tumebetia kiasi chetu chote cha hela kwa ajili ya kukamilisha hii kazi , hatuwezi kufanya makosa , kama huu mpango ukifeli bilioni ishirini ambazo unatudai hutoweza kuzipata”

Kilikuwa kiasi kikubwa mno cha pesa ambacho familia ya Mzee Benjamini wlaikuwa wameahidi kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kumteka Regina ili aachie umiliki wa kampuni.

Kampuni ya Zena kwa kipindi kirefu ilikuwa ikipitia changamoto ya mzunguko wa hea na mtaji wao kuwa mdogo , kitendo cha Regina kuwaingiza kwenye mtego na kununua kampuni ya Omega kwa kiasi kikubwa cha pesa ilihali kampuni hio haikuwa na Product za kueleweka ilifanya kampuni yao kuzidi kuyumba ki uchumi, namna pekee ya kuokoa kampiuni hio ni kuuinganisha na kamuni ya Dosam.

Hivyo kutoana na uzito wa matamanio yao walimuahidi The Loner watampatia kiasi cha bilioni ishirini kama tu atafanikiwa kumteka Regina na kuhakikisha Hamza hana madhara.

“Bilioni ishirini ni hela ambazo sijawahi kudhani naweza kuahidia na siwezi kuona zinapotea mbele ya macho yangu , ndoto yangu kubwa ni kupandisha hadhi kundi langu na kuingia katika nafasi ya daraja A kama kundi linaloongoza kwa matunizi ya ngubu za giza na kulipita hata kundi kubwa kama la Takahamagara, ninachomaanisha hapa hatupambanii kiasi cha hela , ina tunaipamania na heshima yetu kwenye ulimwengu wa Mamluki, hivyo hatuwezi kufeli kwenye hili”

“Sijali mnachopanga ni nini , ninachotaka kujua ni kwa namna gani mtadili na Hamza?”Aliongea Lamla.

“ Mr Tui Nazi unaonaje tukibadilisha kwanza eneo wakati huu ambao Hamza hajatuona na kisha tujipange upya , nadhani itakuwa vizuri kuliko kubahatisha”Alishauri Mzee Benjamini.

“Haina haja tokea mwanzo , mpango wangu ni kugeza hili eneo kama Kaburi la Hamza , kujileta kwake ni kujirahisishia kifo na kutupunguzia usumbufu”

“Hapo vizuri , kwahio Mzee Tui wewe mwenyewe ndio utamuua Hamza?”Aliuliza James.

“Sababu ya sisi kuitwa Wandering Souls ni kwasababu tunakuja na kupotea bila kuacha ushahidi , hatujawahi kukumbatana na tukio la kuua mtu na tukashindwa , kulingana na makisio yangu Hamza lazima atakuwa ni Mvuna nishati aliefikia levo ya nusu mzunguko kamili na mtu wa namna hii kumuua kuna gharama kubwa , hivyo kama unataka kufanikiwa tumia akili na sio nguvu”

“Kwahio kama I hivyo mpango wako unataka kumua kwa namna gani au umekodi Sniper?”

“Mdunguaji anaweza kuwa na faida kudili na mtu ambae yupo levo ya nusu \Mzunguko lakini sio ambae ameingia kwenye Mzunguko kamili ambae anaweza kuinusa hatari hata kilomita kumi., msiwaze sana kuhusu namna ya kumua watu wangu wamejipanga vizuri kumaliza kazi”Aliongea kwa kujiamini.

******

Upande wa Hamza muda huo alikuwa akiingia ndani ya mtaa huo , kwasabqabu hakuwa tayari amejua eneo husika ilibidi aanze kutafuta katika mzingo duara mdogo , huku akitumia hisia kunasa miondoko ambayo sio ya kawaida.

Baada ya kutembea kwa dakika kadhaa , hatimae nywele zake zilisimama mara baada ya kupata harufu ya damu.

Hamza aliishia kukunja sura huku akipita kwenye Viabaza vya nyumba kadhaa ilizokuwa zikipatikana ndani ya eneo hilo akielekea mwisho kwenye jengo kubwa la ghorofa ambalo lilionekana ujenzi wake haukumalizika.

Hamza mara baada ya kusogelea eneo hilo na kujaribu kutumianguzu zake za ziada kutafuta uwepo wa watu lakini ajabu hakuweza kuhisi chochote , lakini licha ya hivyo hakutaka kukata tamaa hivyo aliendelea kulisogelea hilo jumba.

Hamza mara baada ya kusogelea eneo la nje ambalo limezungushiwa na mabati aliweza kuona nyayo nyingi za watu , haikueleweka ni nyayo za mwanamke ama za mwanaume , lakini pia kulikuwa na viashiria vya matone ya damu ambayo ni kama yaaaanza kufifia.

Hamza alisukuma mlango na kuingia ndani kabisa katika floor ya kwanza , ilikuwa ni kama hisia zake zilivvomwambia eneo hilo licha ya kuwa na makolokolo mengi ya vigaa vya ujenzi na kokoto lakini kulikuwa na harufu nzito ya damu.

Kitendo cha kutaka kupoiga hatua kuziendelea ngazi la jengo hilo ili aende ghorofa ya pili alijikuta akishangaa mara baadaya macho yake kukutana na Kamera

Lakini kilichotokea ndani ya sekunde hio , Hamza alikuwa amechelewa tayari kwani ilitokea milipuko minne kutoka pande zote na kuangusha upande wa jengo hilo.

SEHEMU YA 84.

Ulikuwa mlipuko mkubwa mno kiasi kwamba mpaka watu waliokuwa kilomita nne walilala chini kwa hofu na baada ya kurejewa na akili zao walijikuta wakishuhudia moto mkubwa ukitokea kwenye jengo ambalo ujenzi wake ulitelekezwa kwa muda mrefu.

Dakika chache mbele James na genge lake walikuwa wakichekelea kwa furaha

Mzee Tui Nazi na genge lake la watu wanne walionekana wakiwa wamemshikilia Regina upande mwingine wa shamba.

Regina uso wake ulikuwa umepauka kama karatasi , macho yake yalikuwa kodo kutokana na kutokuamini kile kilichotokea , aliamini kabisa Hamza alikuwa amezikwa palepale na kifusi cha jengo lile .

“Haha.. wewe mtoto wa kahaba unaona sasa kiichotokea , nilishamwambia kumchukua mwanamke ninae mpenda kutaishia kumsababishia matatizo”Aliongea James huku akiwa ni kama haamini Hamza alikuwa ameuliwa na mlipuko ule.

Tokea mpango wao uanze alikuwa amefikiria kwa Kina , baada ya Regina kutoa umiliki wa kampuni atamchukua na kwenda kumtumia kwa ajili ya kupunguza hasira za kumhangaikia kwa muda mrefu.

Regina alijikuta akilia kama mtoto bila ya kuongea neno lolote , macho yake yalidhihirisha kile kinachoendelea kwenye moyo wake na alitingisha kichwa huku akitetemeka.

“Sijawahi kuwaza Mzee Tui utamlipua huyu Hamza kikatili namna hii , hivi kwanini hatujawahi kufikiria hi mbinu”Aliongea Mzee Benjamini.

“Yamekwisha , Shauku haikumuua tu paka , lakini pia imemuua mtaalamu”

“Mzee Tui kwanzia sasa usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu pesa , cha kwanza tubadilishe eneo kabla ya Polisi na jeshi halijafika hapa na tukajulikana”

“Niwape tahadhari tu mtimize makubaiano yetu na msije mkaenda kwenye kina cha nafsi zetu”Aliognea huku akiwa na tabasamu la kejeli na kitendo kile kiliwaogopesha.

“Usiwe na wasiwasi kabisa , tunachopaswa ni kummaliza huyu Regina na baada ya hapo tutakamilisha nusu ya malipo yaliobaki”Aliongea Mzee Benjamini.

Dakika moja mbele gari aina ya toyota Corola rangi nyeupe iliwapigia honi, kama kawaida Mzee Tui alifanya mazingara ili watu wasiwaone na kisha walimwingiza Regina na wao wenyewe kuingia.

Kitendo cha dereva kukanyaga pedeli kwa ajili ya kuondoka gari palepale mlango wa boneti uifyatuka huku moshi mwingi ukitokea , haikuwa hivyo tu na tairi zote pia zilisinyaa na kufanya waliondani kutingishika.

“Nini kinaendelea?”James ndio aliekuwa wa kwanza kumaka , lakini Mzee Tui kwa haraka haraka alitoka nje na kuangalia mataili ya nyuma ya gari pamoja na mbele na palepale alianza kuhisi kuna kitu ambacho hakipo sawa.

“Mliangalia hii gari kabla ya kuichukua?”

“Bosi hii gari tumeitoa karakana moja kwa moja na haina usajili wowote kuonyesha imetumika”Aliongea dereva.l

ALUTA CONTINUARA
WATSAPP 0687151346
 
Much respect mr Hades
 
Back
Top Bottom