Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU



MTUNZI: SINGANOJR



SEHEMU YA 108.

Ufunguo wa uhuru

Anna mara baada ya kumuona Yonesi akiwa amejiwekea kisu shingoni alikasirika na kuanza kumfokea.

“Yonesi hebu acha ukichaaa wako na weka hicho kisu chini”Aliongea

Upande mwingne Regina pia aliweza kuona tukio lile la Yonesi kujiwekea kisu shingoni na hakuafiki pia kile anachopanga kufanya.

“Yonesi usifanye ujinga kwa kukurupuka , hawawezi kunifanya chochote wanatishia tu”Aliongea Regina na kumfanya ninja aliemuwekewa kisu shingoni kuzidi kuonyesha sura ya ukatli.

“Miss Regina itakuwa hutujui vizuri , sisi kabla ya kuwa maninja tulikuwa wanajeshi na hatuogopi kufa pamoja ili mradi malengo yetu kutimia , tumeamua kuingia kwenye uwanja wa vita maana yake tumejiandaa kwa lolote”Aliongea Anna kupitia simu ile na kisha alichomoa kisu kutoka kwenye kiuno chake na kumkabidhi Hamza.

“Hamza , hata kama Yonesi ajiue kwa hiari yake haimaanishi tutaacha kutekeleza kile tulichopanga , usipokufa leo hii wenzetu hawawezi kupumzika kwa amani”Aliongea na kumfanya Hamza macho yake kucheza lakini hakuwa na wasiwasi kabisa.

“Naona kama kiongozi wa kundi lako una mzigo mzito umeubeba mabegani , wafuasi wako walikuwa kwenye misheni na wamefia kwenye misheni , hii ndio mara yangu ya kwanza kusikia kundi la kininja likitaka kulipiza kisasi kwa maninja wao waliofarki wakiwa katika misheni”Alongea Hamza.

“Sisi sio kundi la maninja kama hayo uliozoea , sisi ni ndugu tuliokula kiapo kulindana kwa kifo , sisi ni familia moja acha kutulinganisha na makundi mengine ya kininja ambayo malengo yao makuu ni kuua tu”Alongea Anna na Hamza aliishia kutingisha kichwa chake kwa ishara ya kukubali na kisha alichukua kile kisu katika mikono ya Anna,hakuchukua kwasababu ya kujiua kama alivyotakiwa badala yake alikishika pande zote na kisha alikikunja mpaka kukatika.

Kitendo kile kilimfanya Anna na Yonesi kushangaa , kisu kilikuwa kidogo mno kukatika kirahisi lakini Hamza aliweza kukivunja kwa wepesi , nguvu ya aina hio iliwashangaza.

“Kutaka nijitoe uhai wangu na kisu kama hiki utakuwa umenidharau sana, Anna ili kuweza kuniua unatakiwa kujiandaa zaidi ya hivi”Aliongea Hamza na kumfanya Anna kuanza kuonyesha hali ya kupaniki.

“Hamza usije kufanya ujinga wowote , hata kama unao uwezo wa kunishinda lakini kumbuka mke wako yupo mikononi mwetu , ukinigusa tu jua ndio muda ambao Regina atapoteza uhai”

“Sijasema hivyo kwa nia ya kutaka kukuua wewe tu , nadhani utakuwa umeniielewa vibaya”Aliongea Hamza huku akimwangalia kwa macho yaliojaa sanifu na kisha akaendelea.

“Kama ukimuua mke wangu haiwezi kuwa uhai juu ya uhai .. maana nitawaua wote na nitaufanya utu wako kuwa wa mnyama na kujisikia ni kheri ya kifo kuliko kuishi” Aliongea Hamza na kumfanya Anna mapigo yake ya moyo kudunda kwa nguvu.

Alijikuta akikunja ngumi kwa nguvu huku akijitahidi kujikaza akishindana na mkandamizo uliokuwa umemvaa , kwenye maisha yake hakuwahi kukutana na mtu ambae anaweza kumjaza hofu kama Hamza.

Lakini hata hivyo hakuwa tayari kukata tamaa kwasababu ya hofu na mikwara hio.

“Sidhani pia kama unao moyo wa kuona mke wako akifa kwa kuchinjwa, hata kama utuue wote sidhanii utaweza kuishi pia, isitoshe hatia itakushika kwa kupelekea kifo chake”Aliongea na kumfanya Hamza kugeuza macho yake na kumwangalia Regina kupitia simu na kisha alimgeukia Yonesi pembeni na akainamisha kichwa chini na kutabasamu.

“Unacheka nini?” Aliuliza Anna huku akimshangaa .

“Anna hivi unajua ni namna gani ulivyokuwa na hali ngumu?”Aliuliza Hamza na kumfanya Anna asielewe anachomaanisha ni nini.

“Unaongelea nini?”

“Ulikuwa mwanajeshi kabla ya kujiingiza katika uninja , wakati mnajiingiza hamjawahi kujua kufa kwa ninja kazini ni jambo la kawaida sana, lakini hebu angalieni mnachokifanya sasa mmekuja kwa ajili ya kulipiza kisasi jambo ambalo sijawahi kuona kulingana na sheria za kininja, tuchukulie watu wako kila mara wanapoenda kufanya misheni na kupoteza maisha, ina maana utaendelea kulipiza kisasi kwa wale ambao wamemewaua kila siku, kama ni hivyo utatoa wapi muda wa kutafuta hela na kuyafuraha maisha?”Aliuliza Hamza.

Macho ya Anna yalilegea kidogo , alichoongea kilikuwa kama kitu kikali kilichopita katika moyo wake.

Alikuwa akijua vyema mwanzo wa kundi lake haukuwa wa kawaida kama ilivyo kwa makundi meingine ya kimauaji , wao walikuwa ni wanajeshi ambao waliingia jeshini kwa ajili ya kutumikia tafa lao , lakini taifa ndio ambalo liliwaangusha na kujikuta wakiwa katika mazingira kama hayo.

Hivyo wao kuwa maniinja ni kitu ambacho wamelazimishwa tu na hali zao na sio jambo ambalo wamelipenda , walikuwa wanajeshi na walikuwa na kila haki kama binadamu wengine kutamani maisha mazuri yenye amani na furaha.

Hamza aliweza kuona namna ambavyo Anna alibadilika kutokana na maneno yake na aliishia kupumua kama mtu ambae anamuonea huruma na aliendelea kupigilia msumari.

“Kwa ninavyokuona.., unaonekana kuchoka sana na aina ya maisha unayoishi?”Alongea Hamza na kumfanya Anna mikono yake kutetemeka kidogo.

Kitendo hicho hakukiona yeye tu hata kwa Yonesi pia na upande wa Mima waliweza kukiona.

Upande wa Yonesi alijikuta akishikwa na hatia kubwa , Mima ambae alikuwa amemshikilia Regina aliishia kukunja ndita , kulikuwa na hali isioelezeka katika macho yake.

Anna hata yeye pia alijua fika hakuwa katika mudi nzuti na alichofanya ni kuvuta pumzi nyingi na kisha akaanza kucheka lakini hakikuwa kicheko cha furaha.

“Hamza hakika upo vizuri kwenye vita ya maneno , unataka kutumia maneno kwa ajili ya kunihadaa? , samahani sana lakini huwezi kunibadilisha mawazo yangu kutokana na maneno yako , fanya kama nilivyokuambia na haraka jiue vinginevyo mke wako atakufa ukimwangalia”Aliongea Anna na kumfanya Hamza kukunja sura.

“Kama ni hivyo haraka za nini sasa , hata kama unataka nife angalau unapaswa kuniacha niyafurahie maisha angalau kwa mara ya mwisho, au unasemaje?”

“Ufurahie maisha!, unataka kufanya nini?”Aliuliza Anna akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa

Hamza macho yake yalianza kumwangalia Anna kutoka usoni mpaka chini miguuni na kisha alivuta pumzi na kuzishusha.

“Ni rahisi sana , unachotakiwa kufanya ni kunifuata floor ya juu tu”

Mara baada ya kuongea hivyo alipotezea muonekano wake na kisha alimpokonya simu iliokuwa ikionyesha tukio hilo upande wa pili na akamshika kiuno palepale kwa nguvu na kumuweka begani na kuanza kutembea nae.

Anna alijikuta akianza kufurukuta huku akitumia mikono yake kumpiga Hamza upande wa mabega lakini ni kama alikuwa akipiga jiwe maana Hamza hakuonekana kuhisi maumivu kabisa.

“Dada Anna!!”

Sauti ya Mima ndio ilioweza kusikika maana simu haikuwa imekatwa , ijapokuwa hawakuwa wakiona kinachoendelea lakini walisikia sauti.

“Hamza unafanya nini?”Aluliza Yonesi akiwa katika mshangao , hata upande wa Rergina hakujua ni nini Hamza anataka kufanya.

Upande wa Hamza alikuwa akijua floor ya pili ya jengo hilo haikuwa ikitumika kwani ilikuwa kwenye ukarabati , mara baada ya kumbeba mpaka juu alienda kumtupia kwenye sofa na kisha akaishikilia mikono yake kwa kuibana chini ili asilete vurugu.

“Hamza niachie , acha ukichaa wako wewe mwanaume”Aliongea mwanamke huyo huku akirufukuta.

“Tulia basi mrembo , unaonaje ukinifurahisha kabla ya kifo changu, nadhani takuwa vizuri zaidi , tena unaonekana kunipenda kabisa kwenye macho yako”

“Hamza ukiendelea na hiki unachokifanya nakuapia mke wako atakufa”

“Haiwezi kutokea , najua unahitaji sana dudu, ukweli ni kwamba umechoka mno na kitu pekee unachokitaka ni uhuru wako, roho ya kuishi na visasi imekuchosha na mimi nakwenda kukupa ufunguo wa uhuru”Aliongea.

Sauti yake ilikuwa ni kama ya Shetani na kumfanya mrembo Anna macho yake kuanza kupoteza usiriasi wake kadri sekunde zilivyokuwa sikisogea.

Anna aliishia kumwangalia Hamza namna alivyoubana mwili wake na hali ya joto ilimfanya kuanza kusisimka , alikuwa ni mwanamke ambae amepevuka hivyo alikuwa akitamani vitu kama hivyo mara kwa mara.

Katika shambulizi la kishenzi kama hilo alilofanyiwa na Hamza hakuwa na nguvu kabisa ya kuleta ukinzani na alijishangaa viungo vyake vya mwili vikilegea bila ya kupenda.

Alichoshangaa ni Hamza kutokata Vidio call ile, ijapokuwa ilikuwa pembeni na haikuonyesha kilichokuwa kikiendelea lakini sauti zao zilisikika vyema upande wa pili.

Mima mwanamke ninja aliemshikilia Regina asifurukute mara baada ya kuanza kusikia sauti za kimahaba kutoka kwa kiongozi wake mawazo kibao yalianza kupita katika akili yake na yale macho yaliojaa sumu na ukatiri yalianza kulainika.

Da’Anna kwanini unafanya hivyo , inamaana alichoongea huyo mwanaume ni ukweli…”Alijikuta akianza kuongea kwa kumwemwesa maneno hata yasiweze kusikika , hata mkono ambao ulikuwa umemshikilia Regina ulilegea.

Upande wa Regina uso wake ulikuwa mwekundu , ijapokuwa hajawahi kufanya mapenzi kwenye maisha yake lakini alikuwa akijua fika ni kitu gani Hamza anafanya na huyo mwanamke wa kininja.

“Huyu mshenzi inamaana katika mbinu zote alizoona zinafaaa kuwashawishi hawa wauaji ni hio?

Regina alijikuta akiwaza huku akisaga meno , ila licha ya kwamba alianza kuhisi hasira lakini pia alijisikia vibaya kwa wakati oja , alikuwa ni mwanamke wenye akili sana na alijua ni kitu gani ambacho Hamza anajaribu kufanya.

Ilikuwa ngumu pia kwa Hamza kukimbia mpaka makao makuu kwa ajili ya kumuokoa, lakini vilevile ilikuwa ngumu kwake kujiua yeye mwenyewe.

Kwahio kwa haraka haraka alijua kitu ambacho Hamza anataka kufanya ni kuharibu mfumo mzima wa kihisia wa maninja hao ili washindwe kabisa kuendelea na mpango wao.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba maninja hao wa kundi la Red sisters walikuwa ni wanajeshi kabla ya kuwa maninja na kitendo cha kujiiita maninja pengine ilikuwa ni sababu ya kuweza kuishi kutokana na yae waliokuwa wakipitia lakini ki uhalisia walikuwa ni wanajeshi wa kawaida tu ambao wasingependa kuua watu wasiokuwa na haita.

Kwahio Hamza alikuwa akijua ni rahisi kudili nao kutokana na udhaifu wao wa kutotaka kuendelea kuwa maninja kwa kumlegeza Anna na kwasababu alikuwa ni kiongozi na kitendo ambacho amefanya wamekiona moja kwa moja kwao itakuwa ni kama wamepoteza kiongozi.

Wakati huo mrembo Anna alikuwa akihisi kila aina ya hisia , alikuwa akijitahidi kadri awezavyo asahau kila kilichomtokea kwenye maisha yake na kutaka kufurahia kile ambacho Hamza anamfanyia , ki ufupi ni kwamba alikuwa akishindana na hisia zake, hisia za kuwa binadamu wa kawaida au kuendelea kuwa ninja.

Upande wa Hamza alijua nini kilichokuwa kikiendelea kwa mwanamke huyo hivyo alizidisha moto na kuzidi kuamsha hisia za mwanamke huyo.

Yonesi mara baada ya kufika katika floor hio na kuona kile kinachoendelea kwenye sofa alijikuta akigeua kichwa chake haraka akiwa hataki kuangalia.

Moyo wake ulianza kudunda kwa kasi sana na hakuwahi kufikiria kama Kamanda wake ambae alimfahamu jeshini kama mwanamke jasiri na asiependa mchezo mchezo ndio wakufanya kitu hicho na Hamza tena waziwazi bila aibu.

Ndani ya nusu saa tu Hamza alikuwa amemaliza kutoa bakora za kimkakatai na alisimama kutoka kwenye Sofa , hakuwa hata na haraka ya kuvaa nguo zake na aliishia kuokota simu iliokuwa chini na kaungalia lakini aligundua simu ile ilikikwisha kukatwa muda mrefu.

“Inaonekana yule muuaji wako Mima kashaondoka”Aliongea Hamza.

Yonesi mara baada ya kusikia kauli hio haraka haraka alimpigia Regina simu na haikuchukua hata dakika kadhaa simu iliweza kupokelewa na Regina alikuwa salama.

“Mkurugenzi yupo salama , amesema Mima ameondoka akiwa analia”Aliongea Yonesi kwa sauti hafifu huku akimwangalia Komredi wake aliekuwa amejilaza kwenye sofa kwa uchomvu.

Anna mara baada ya kusikia kauli hio palepale alijikuta akijikunyata kwenye sofa lile na kuficha kichwa chake huku akianza kulia kwa kwikwi.

“Nimefanya nini mimi.. nitawaangaliaje wadogo zangu”Alikuwa akijilaumu.

Hamza aliishia kumwangalia mrembo huyo kwa madakika kadhaa bila ya kutokuwa na hali ya mabadiliko katika sura yake na kisha alimsogelea na kumsbhika bega.

“Achana na hizo hisia unazojisikia , sio kila mtu anaeweza mapigano anaweza kuwa ninja, tokea nikuone hapa mara ya kwanza niliweza kugundua hukuwa ukinichukia mimi bali ulikuwa ukijichukia mwenyewe,pengine kwa kuwaingiza dada zako kwenye hatari mpaka kupoteza maisha”Aliongea na kauli ile ilimfanya Anna kunyanyua sura yake na kumwangalia Hamza huku akisaga meno yake kwa hasira.

“Hamza wewe ni shetani .. huwezi kuchukua moyo wangu kirahisi namna hii”

“Sijachukua moyo wako mmi , ninachokuambia ni uhalisia wa mambo , kama kweli unataka ndugu zako kuwa na furaha basi unapaswa kufuta kundi lenu la kininja na kurudi kuwa watu wa kawaida na kuishi kama watu wa kawaida tu”

“Unadhani ni rahisi kwa kuongea tu hivyo ilihali waliotusaliti hawataki kutuona tukipumua , hatuna sehemu ya kwenda na kuishi maisha ya kawaida , uninja ndio chaguo rahisi kwetu”Aliongea Anna kwa uchungu mkubwa.

“Kwani ni kitu gani kilichowatokea , inakuwaje wanajeshi kama nyie ambao mlifika hatua ya ukomandoo kuwa wahalifu wa nchi na kujiiingiza katika ulimwengu wa giza?”Aliuliza Hamza akiwa katika hali ya mshangao.

“Sina haja ya kukuelezea chochote , umenishinda na nimeshindwa naomba tu uondoke nifikirie namna ya kwenda kuwaomba radhi dada zangu”

“Dada zako , kwani sio kwamba wapo hapa tayari?”

Kauli ile ilimfanya Anna kubadilika mara moja na palepale haraka sana alivaa mavazi yake na kuweka nywele zake vizuri.

Ilikuwa ni dakika hio hio Mima aliweza kufika hapo akiwa ametangulizana na wanawake waliokakamaa miili jumla yao ikiwa sita.

Wanawake wale mara baada ya kumuona Yonesi walionekana kumtambua na muonekano wao ulikuwa na hsia ambazo ilikuwa ni ngumu kuelezeka na mara baada ya kugeuza macho yao kwa Anna kiongozi machozi yalianza kuwatoka.

“Mima naombeni mnisamehe , mimi dada yenu nimewaangusha mno”Anna alikuwa ameshikwa na aibu kubwa na hali ya hatia.

“Dada Anna sisi ndio tuliokuangusha”Waliongea wote kwa pamoja na dakika ileile walipiga magoti chini.

Kitendo kile kilimshitua Anna na aliishia kuwangaalia dada zake hao akiwa amekosa hata neno la kuongea.

“Nyie… mna matatizo gani , kwanini mimi ndio niliofanya kosa na kuwatia aibu..”Anna alishindwa hata kuongea vizuri huku machozi na yeye yakianza kumtoka.

“Hatukuwahi kuwaza tulikuwa mzigo mkubwa kwako . licha ya uwezo wako kutokuwa mkubwa sana lakini ukaamua kutuongoza kwenye kila aina ya misheni na kuhakikisha tunakuwa salama , leo ndio tumejua ni kwa namna gani ulikuwa na machungu kwenye moyo wako kuishi maisha ambayo sio yako , tunaomba msamaha kwa mzigo tuliokubebesha “

Mara baada ya kusikia hivyo Anna alijikuta akishikwa na bumubwazi , alijua yeye ndio amewasaliti wenzake lakini ilikuwa tofauti ,wao ndio walikuwa wakiona wamemsaliti kwa kuelewa hisia zake.

Yonesi mara baada ya kuona tukio hilo alikuwa akilia ndani kwa ndani, aliwaonea huruma wenzake hao alioenda nao nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo na yakutokea yakatokea mpaka kuwa katika hali hio.

Upande wa Hamza alikuwa na hisia hasi juu ya kile knachoendelea,alikuwa akiamini kuna kitu kikubwa ambacho kimewatokea wanawake hao ndio maana wakaamua kuwa maninja na alitaka kujua.

“Anna unaweza kuniambia ni kitu gani kimewatokea , pengine naweza kuwasaidia”Aliongea Hamza.

Anna macho yake yalikuwa katika hali isioelezeka na katika uso wake alikuwa na kila ishara ya kumshukuru kwa kumpa ufunguo wa uhuru.

“Mr Hamza unaonaje ukivaa nguo zako kwanza ndio tuongee”Aliongea.

“Ah,,!!”Hamza alijikuta akishikwa na aibu maana alikuwa amesahau kama alikuwa yupo uchi na haraka haraka alivaa mavazi yake.

Ukiachana na Yonesi ambae hakuwa akimwangalia Hamza muda wote , lakini kwa maninja hao hawakuwa na hali ya haya usoni hata kidogo kwa Hamza kuwa uchi.

Anna mara baada ya kutulia kwa dakika kadhaa aliwasimamisha ndugu zake na kisha alianza kumwelezea Hamza kile kilichotokea.

*****

Miaka kadhaa iliopita Serikali kupitia Jeshi waliunda kikosi maalumu kwa ajili ya mafunzo ya kikomandoo , ambapo wanajeshi kama wangefuzu mafunzo hayo moja kwa moja wangejiunga na kitengo cha Malibu.

Kikosi hicho kilipewa jina la Jani la Sumu(Poison leaf special force), kikosi hiko kilikuwa ni maalumu kwa wanawake tu ambao kwanza walipaswa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi ya miaka minne mpaka watakapofuzu.

Baada ya mpango huu kupitia serikali kupitishwa hatimae udahili wa wanajeshi ambao wangejiunga na kikosi hichi ulianza mara moja na kwasababu mpango ulikuwa ni kufanya kikosi hicho kuwa cha wanawake tu , hivyo waliodahiliwa walikuwa ni wanawake pekee.

Kati ya wanajeshi ambao walikuwa mafunzoni waliopata nafasi ni wale walionyesha uwezo wa juu sana katika kuelewa mafunzo ya kijeshi na kati ya watu hao moja wapo alikuwa ni Yonesi , Anna na Mima pamoja na wenzake wengine ambao walitolewa katika kambi tofauti tofauti.

Ni Yonesi , Anna na Mima pekee ambao walitolewa katika kambi moja na kuungana na wasichana wenzao wa kambi nyingine kwa ajili ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo maalumu ili baadae wakihitimu waje kuongeza nguvu jeshini katika idara ya imtellijensia ya ulinzi kwenye kupambana na nguvu za ziada.

Kwa Lugha nyepesi wanawake hao wa kikosi cha Jani la Sumu walikuwa wakienda nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza mafunzo ya kikomandoo lakini kwa wakati mmoja wakijifunza na mbinu nyingine ambazo zingewawezesha kudili na nguvu ambazo sio za kawaida kulingana na namna ambavyo wavuna nishati za mbingu na ardhi kwa minajili ya kihalifu duniani kuongezeka.

Mara baada ya kikosi hichi kuteuliwa hatimae walipelekwa nchini Chile katika mji wa San Pedro De Atacama mkoa wa Antofagasta katika bonde ambalo maarufu hufahamika kama Valley of the Moon au El valle de la Luna pembeni mwa jangwa la Atacama ambapo ilipatikana kambi maarufu ya mafunzo ya kijeshi hapo.

Sasa wakati ambao kikosi hicho kinaanza mafunzo rasmi upande wa Tanzania kulikuwa na vuguvugu iliokuwa ikiendelea na ilimhusisha Raisi wa nchi wa wakati huo ambae alikuwa ni mheshimiwa Eliasi alieingia madarakani kwa kushirikiana na Mgweno pamoja na baadhi ya wakuu wa majeshi.

Mgongano huu ulitokana na kwamba kikosi cha Poison Leaf kilichopo huko Atacama Chile hakikuidhinishwa na Amiri Jeshi mkuu.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba maamuzi yalifanyika bila ya mheshimiwa Raisi kutaarifiwa na jambo hili lilitokana na uhusikaji wa familia ya Wanyika ambao ndio walishawishi jeshi kuunda kikosi hiki na kukituma nchini Chile bila ya mheshimiwa Raisi kutaarifiwa , swala hili liliwezekana kwa urahisi kwasababu Familia ya Wanyika walikuwa na nguvu kubwa mno mpaka kwenye ngazi za usalama wa taifa hivyo ikawa rahisi kwa Raisi kutofahamu hilo.

Sasa mara baada ya Mgweno kujua swala hilo hakutaka kukubali na aliweka ngumu kwa kumpa presha Raisi Eliasi kutaka wanajeshi hao kurudishwa nyumbani na kuacha mafunzo haraka , lakini wawili hao yaani mstaafu Mgweno na Eliasi licha ya kujaribu kutumia nguvu sauti zao hazikuwa na nguvu ya kusikika.

Hata yeye Mgweno alijua maagizo yake hayawezi kufanyiwa kazi kutokana na nguvu iliokuwa nyuma katika mpango huo licha ya kumtumia Eliasi.

Moja ya kitu ambacho Mgweno alihofia ni kwamba , ikitokea wanajeshi hao wakifuzu maana yake ni kwamba ingekuwa ngumu sana kwa yeye kuingusha familia ya Wanyika, kwani wanajeshi hao ilimaanisha ngome imara kwa familia hio kutokana na kwamba idara hio ndio nguvu yao ilipokuwepo, kwa lugha nyepesi familia ya Wanyika walikuwa na nguvu kubwa katika kitengo cha jeshi cha Malibu kuliko vitengo vyote vya jeshi.

Sasa kwa muda mrefu mpango waMgweno ni kuifanya familia yake kuwa kubwa ndani ya Tanzania na kuwa na ushawishi sio tu katika siasa lakini mpaka jeshini na mpango wake huo ili ufanikiwe lazima apunguze nguvu ya Deepstate ya familia ya Wanyika na kuihamishia kwake.

Sasa hakutaka wanajeshi hao kufuzu kwa namna yoyote ile , kwani ingedhoofisha mpango wake , hivyo haraka sana kwa kushirikiana na Eliasi waliandaa mpango wa kuingilia mafunzo hayo ya wanajeshi.

Na mpango ambao ulifanyika ni kuwafanya wanajeshii hao waonekane wamekiuka sheria na kuasi jeshi kwa kujiingiza katika kula viapo vya damu na kundi la kininja kutokea nchi ya Haiti.

Ulikuwa ni mpango uliosukwa haswa ambao uliwafanya Yonesi na wenzake bila kujijua kuingia katika mtego wa kundi hilo la kininja lililoingia makubaliano na raisi wa Tanzania na mwisho wa siku kuonekana kama wasaliti wa taifa walioasi jeshi wakiwa mafunzoni.

Baada ya tukio hilo Mgwenno alimkabidhi Eliasi ushahidi ili kwenda kuutoa mbele ya viongozi wa jeshi juu ya kikosi hicho kilivyovunja sheria za nchi na kuasi jeshi hivyo kupaswa kurudishwa nchini na kufungwa gerezani au kunyongwa.

Ushahdi ulikuwa wazi na Mgweno ukiachana na kuwa na sapoti ya Rais Mbilu lakini pia alikuwa na watu wanaomsapoti na hakukuwa na namna ambayo ushahidi huo ungeweza kubatilishwa hivyo moja kwa moja kikosi cha Jani la Sumu baada ya kufanya mafunzo kwa miaka miwili kikaingia katika matatizo na kutakiwa kruudi Tanzania kwa ajili ya kupatiwa adhabu kulingana na sheria.

Swala hili lilimfikia kiongozi wa kikosi hicho ambae alikuwa ni Kapteni Anna lakini hakuwa cha kufanya kutokana na kwamba kilichotolewa kama ushahidi ilikuwa ni kweli , lakini tukio hilo la kuvunja shera hawakuwa wakijua walikuwa wakivunja sheria kwani nguvu za ziada zilitumika, kwa ufupi walivunja sheria bila ya wao wenyewe kujua wanavunja sheria na hatimae kuonekana wameasi jeshi.

Wakiwa hata hawajui ni nini hatima yao Yonesi mwanajeshi mwenzao alikuja kutolewa kambini kimya kimya na kurudishwa Tanzania huku wao wakisubirishwa kambini bila ya kupewa maelezo ya hatima yao.

Sababu ya kubakishwa kambini ni kutoksana na kwamba mvutano ndani ya jeshi pamoja na raisi wa nchi haukuwa umeisha kwani muafaka haukupatikana bado wengi wakitaka uchunguzi ufanyike ndio maamuzi yafanyike ya kuwarudisha ama kuendelea na mafunzo ili serikali isipate hasara.

Familia ya Yonesi, baba yake alikuwa ni mwanajeshi wa kuheshimika lakini hata hivyo hakuwa na nguvu ya kutosha ya kumuokoa binti yake katika adhabu hio , hivyo kwa haraka haraka ilibidi angie dili na moja ya familia kubwa ya kijeshi kwa ajili ya Yonesi kurudishwa nchini na kisha kuozeshwa katika familia hio na hapo sasa ndio Yonesi akaja kuchumbiwa na Afande Mdudu.

Lakini Yonesi hakukubali kufungishwa ndoa hio ilihali jeshini hakufanya kosa bali ni hila za kisiasa zilizowafanya kuonekana wameasi , hivyo Yonesi alitoroka kwao Dodoma na kuacha kujihusisha na jeshi moja kwa moja na kuhamia Dar es salaam mpaka alipokuja kukutana na Regina na kuwa mlinzi wa kampuni.

Upande wa wenzake nchini Chile mara baada ya kuona Yonesi amechukuliwa na familia yake , waliona swala lilikuwa zito mno na kwa bahati nzuri waliweza kupata taarifa ya kile kilichotokea na kujua mpango wote wa kufanywa kuwa waasi wa nchi ni hila mstaafu Mgweno.

Kutokana na kutokuwa na makosa na kuona wanakwenda kufungwa jela ama kunyongwa kabisa Anna aliamua kutoroka na wenzake kambini na kukimbilia nchini Haiti, waliamua kukimbilia huko ili kupata ushahidi wa kujitetea.

Kitu ambacho hawakuwa wakijua ni kwamba kutoroka kwao kambini mpaka kufanikiwa kuingia nchi ya Haiti yote ilikuwa ni mipango ya Mgweno.

Mgweno licha ya kuvuruga mafunzo hayo kwa kumtumia raisi hakutaka wanajeshi hao kurudishwa nchini bali alitaka wahamie katika ulimwengu wa Giza na kuwa Assasin ambao wangemsaidia kazi zake nyingi katika mpango wake wa kuiweka Tanzania kiganjani na kuongeza uimara wa ngome yake ili hatimae kuiondoa familia ya Wanyika.

Anna na Wenzake mara baada ya kufika nchini Haiti walianza kuendelea na mafunzo makali baada ya kuona hawakuwa na uwezo wa kushindana na kundi lililowaingiza matatizoni, lakini wakati huo wakiwa na kisasi moyoni kwa kile ambacho walifanyiwa na taifa lao , baada ya miaka mingi ya mafunzo ya kimauaji hatimae waliunda kundi la kininja ambalo waliliita Red Sisters na kuanza kupokea oda ya kuua watu kimya kimya na hii ni mara baada ya kujizolea umaarufu wa kuua kundi hatari la Kininja lililopatikana hapo Haiti , kundi lilelile lililoingia dili na Mgweno ili kuwafanya waonekane wameasi hivyo ni kama kazi zote za kundi hilo zilihamia kwao.

Taarifa za wanajeshi hao kwanzia kuunda kundi la kininja mpaka kusambarasha kundi hatari la Kininja ndani ya nch ya Haiti zilikuwa zikimfikia Mgweno na mara baada ya kuona mafanikio hayo haraka sana alituma vijana wake kuwapa dili kundi hilo kuua familia nzima ya Yulia wakiwa nchini Sweeden , huku malipo akiwaahidi yatakuwa ni uhuru wao wa kurudi nchini na kubatilisha kesi yao na hatimae kuwa huru lakini kuendelea kuwa maninja chini yake na kuwalipa hela nyingi sana.

Lakini wakati Mgweno akituma kazi hio kwa maninja hao upande wa familia ya Wanyika pia walituma ofa kwa kundi hilo hilo kuhakikisha usalama wa Dr Sindiga na familia yake nchini Sweeden huku wakiahidiwa uhuru wao baada ya Eliasi kumaliza muda wake serikalini na hadhi zao za jeshi kurudishwa upya na kulipwa Fidia ya miaka yao yote walioteseka.

Hivyo Anna na wenzake walijikuta wakiwa na ofa mbili mezani ya kwanza ilikuwa ni kutoka kwa Mgweno na ya pili ilitoka kwa familia ya Wanyika.

Kundi hilo lilichagua upande wa familia ya Wanyika kwa uhalisia lakini wakati huo huo walikubali ofa ya raisi Mgweno , kwa lugha nyepesi ni kwamba walikubali ofa zote mbili lakini ambayo walipanga kufanyia kazi ni iliotoka upande wa familia ya Wanyika ambao waliona ilikuwa nzuri zaidi kutokana na familia hio ilitaka tu kuwarudisha uhuru wao pekee na sio kufanya kazi chini yao kama alivyofanya Mgweno.

Sasa wakati wakiwa nchini Sweeden wakiamini mpango utaenda kama walivyopanga kutokana na wao kuwa ndio wauaji pekee, lilikuwa kosa kubwa kwao kwani mpaka wanakuja kufika eneo la tukio familia ya Dokta Sindiga ilikwisha kuuwawa kasoro Yulia peke yake ambae waliweza kumuokoa.

Wakati huo ndio ambao Hamza aliweza kufika eneo la tukio na mara baada ya kuona familia ya Yulia imekwisha kuuwawa na kuona maninja waliohusika aliwaua mara moja na kisha akamchukua Yulia.

Kitu ambacho hakujua Hamza ni kwamba aliowaua hawakuwa wahusika waliouwa familia ya Yulia bali watu ambao aliwakutaka eneo la tukio ndio waliomuokoa Yulia lakini wakachelewa.

Sasa baada ya kitendo hicho Anna na Wenzake walijikuta wakishikwa na kisasi kikubwa kutokana na Hamza kuuwa wenzake ambao hawakuwa na hatia.

Haikuwa hivyo tu wadada hao pia waishikwa na hasira maradufu mara baada ya kujua Mgweno aliwazidi akili na kutumia watu wengine kwa ajili ya kazi hio huku akiwafanya waonekane wao ndio wameimaliza familia hio.

Kwanzia hapo kundi hilo lilianza kumtafuta kwanza Hamza kwa udi na uvumba kwa ajili ya kulipa kisasi cha kuua wenzao sita ambao hawakuwa na hatia.

Upande wa Mgweno hakupoa, mara baada ya muda mrefu akiendelea kukusanya taarifa juu ya maninja hao hatmae aliweza kugundua nini kimetokea mpaka Yulia kuweza kuendelea kuwa hai na baadhi ya maninja wa kundi hilo kupoteza uhai, sasa ndio anakuja kufahamu ni Hamza aliewaua maninja wa kundi hilo na kisha kumchukua Yulia.

Mara baada ya kupata taarifa hio ndio sasa aliipenyeza kwenda kundi la Red Sisters ambao walikuwa wakimtafuta Hamza nje ya nchi na ndio walivyoweza kujua Hamza alikuwa nchini Tanzania na kuingia kwa mara ya kwanza nchini tokea wapatwe na kesi kwa ajili ya kulipiza kisasi.

Sasa bado wanawake hao hawakujua kama Mgweno alikuwa akifanya hayo yote baada ya kumshindwa Hamza na sasa alitaaka kundi hilo ndio limuondolee Hamza na mipango yake iendelee.

NB: Hiki kisa kipo kwenye simulizi nyingine , huko nimekielezea vizuri tusubirie nikitoa kitabu.

























SEHEMU YA 109.

Hamza mara baada ya kusikia kisa hicho hakika aliwaonea huruma hao wanawake , lakini kwa namna moja alishangaa na kujiuliza kama hio familia ya Wanyika ndio waliohusika katika kushawish kuundwa kwa kikosi hicho ilikuwaje wakashindwa kuwatetea kwa namna yoyote ile.

Ila hata hivyo aliona alifanya kosa siku ile na kuua watu ambao hawakuwa na hatia kumbe wahusika walikuwa ni watu wengine , kutokana na hilo pekee aliona anapaswa kuwasadia.

“Duuh , kama ni hivyo ilikuwaje familia ya Wanyika haikuwasaidia?”Aliuliza Hamza.

“Baada ya tukio la kifo cha Dokta Sindiga na familia yake Wanyika wanaamini sisi ndio tulihusika na mauaji yao na hakukuwa na namna ya kjitetea kutokana na kwamba walipaata uthibiisho tulikuwa na mawasiliano na Mgweno akitupatia dili la kuwaua , lakini pia ni Mgweno huyo huyo aliehakikisha familia hio inaamini sisi ndio wahusika”Aliongea Anna na aliona inaleta mantiki , lakini kwa namna flani aliona Mgweno alikuwa mtu ambae akili yake inafanya kazi sana , kama ameenda mbali hivyo basi ilikuwa ni dhahiiri alikuwa amedhamiria kutimiza malengo yake.

“Aisee poleni kumbe ilikuwa hivyo….”Aliongea Hamza huku akionekana kufikiria.

“Ndio hivyo.. umesema utatusaidia lakini niseme tu tunashukuru kwa kuwa na nia ya kutaka kutusaidia , lakini hii ni Tanzania ambayo watu wake ni waoga na wanaojali maslahi na sio maumivu ya wengine ,hakuna ambae anaweza kwenda kinyume na familia ya Mgweno, licha ya kwamba mara nyingi yupo katika vita na familia ya Wanyika lakini nguvu yake ni kubwa mno, anao watu kila mahali ambao wanaweza kumsapoti”Aliongea Anna.

“Kama ni hivyo kwanzia sasa mnapanga kufanya nini , kama nilivyosema hamna vigezo yva kuwa maninja kabisa , yaani kitendo cha kuonana kama ndugu na kutakaa kulindana ni sifa kuu ambayo inawapotezea sifa , Ninja ni mtu ambae anaweza kumuua mwenzake bila ya huruma pale inapotakiwa kufanya hivyo”Aliongea Hamza.

“Nadhani hakuna namna tutarudi nje ya nchi tukiendelea kujipanga upya kwa ajili ya kulipa kisasi chetu kwa Mgweno”

“Bado tu mnataka kulipa kisasi?”Aliuliza Hamza kwa mshangao.

“Sisi kujiunga jeshini tukiwa wadogo ilimaanisha tulitaka kulitumikia taifa letu, lakini kwanini tuishi kama wakimbizi ilihali hatuna kosa?, hatuwezi kuwa na amani wala kuishi maisha ya kawaida bila ya makosa yetu yaliotengenezwa kufutwa”

“Ulichoongea ni sahihi , hakuna uwezekano wa nyie kuwa na maisha ya kawaida hata mkighairi kulipa kisasi chenu , maana kama wameweza kuwafanyia hayo yote inamaanisha mkono wao nje na ndani ya nchi ni mrefu , ila kwa kuwasaidia ni kuwabakisha hapa hapa nchini na nitamwambia mke wangu awapatie nafasi katika kampuni yake mfanye kazi kama walinzi mengine niachieni mimi”Aliongea Hamza.

“Nini!?”Wote walijikuta wakaishangaa

“Mr Hamza unasema ukweli?”Aluliza Mima.

“Kwanini , au ndio hamtaki kufanya kazi ya ulinzi , mimi nimetoa pendekezo tu , kama hampendi ninao uwezo wa kuwapa nafasi nyingine,ila kwa hali yenu kwasasa hamuwezi kuwa wanajeshi tena”Aliongea Hamza

“Hapana… hatujamaanisha hivyo … ni kwamba kama utatuchukua sisi maana yake moja kwa moja utaingia katika mgogoro na familia ya Mgweno ambae anatuona kama maadui , licha ya Dosam kuwa kampuni kubwa kimataifa lakini sidhani kama inaweza kuendesha biashara yake ikiwa serikali ipo kinyume”Aliongea Anna lakini Hamza aliishia kucheka.

“Haina haja ya kuwa na wasiwasi , iwe ni familia ya Mgweno au Wanyka hawawezi kupinga hili , nitawafanya wawaombe msamaha kwa kuwafanya wanajeshi kama nyie mliojitolea kuvuja damu kwa ajili ya taifa na kuwafanya kuwa waasi , sijui watanichukuliaje lakini mimi sijali , ninachotaka ni haki yenu kupatikana”Aliongea Hamza.

“Hujali!!?”

Mara baada ya kusikia maneno ya Hamza wanawake hao walijikuta wakianza kububujikwa na machozi ya kuguswa na kauli yake.

Ilikuwa kweli kabisa ndani ya jeshi watu wengi walikuwa wakijua hawakuwa na makosa na walisingiziwa lakini hakuna ambae alijali ile nia yao ya kulipigania taifa mpaka kujitolea kuwa wanajeshi , kwa mara ya kwanza ni Hamza ambae aliona kile ambacho wanajisikia moyoni.

Hakuna maumivu yanayouma kama kusalitiwa na taifa lako mwenyewe wakati umeamua kujitolea kulipigania kwa hali na mali , aina hio ya maumivu watu wengi hawawezi kuijua lakini inauma sana na ndio maana wengi ambao wamesalitiwa na nchi zao hugeuka na kuwa magaidi, sio kama wanapenda bali ni hali ya hasira na maumivu ndio inayowafanya kuwa na msukumo huo.

“Mr Hamza asante sana kwa maneno yako ya faraja , yametugusa mno , haishangazi ndio maana mwanamke tajiri na mrembo kama Bosi Regina amekubali kuolewa na mtu kama wewe , unaonekana kuwa mwanaume unaejua nini maana ya uwajibikaji, lakini hata hivyo hatuna uhusiano wowote na wewe na kuwa karibu na kampuni ya Dosam ni kuiingiza katika matatizo.. hatuwezi kupokea ukarimu wako”Aliongea Anna.

Kauli yake iliwafanya Mima na wenzake ule msisimko wa mara ya kwanza kuishi nchini Tanzania kama raia ulishuka mara moja kutokana na kauli ya kiongozi wao, na wenyewe walitingisha kichwa kukataa , hawakutaka kuwa wabinafsi licha shida walikuwa nazo.

“Haha.. mimi sio mtu mzuri kama mnavyonifikiria , sijataka muwe walinzi ndani ya kampuni ya Dosam bure bure tu , mnakwenda kulipa pia pengine gharama mnayokwenda kulipa ni ya uhai wenu”Aliongea Hamza.

“Unataka kusema kuna watu wanaotaka kumuua bosi wa kampuni ya Dosam?”Aliuliza Anna.

“Sio lazima kuwe na mtu anaetaka kumuua , ninachotaka ni kutengeneza safu ya ulinzi ili kumlinda mke wangu , kwa wale walinzi wa kawaida waliokuwepo bado nina wasiwasii ila nyie wote hapa ni makomandoo lakini pia mmepitia mafunzo ya mbinu zote za kininja hivyo ni wataalamu wa hali ya juu na ndio mmanifaa sana”Aliongea Hamza.

Ukweli ni kwamba tokea tukio la Regina kutekwa Hamza alipatwa na wazo la kuweka walinzi ambao wana uwezo wa kumlinda Regina wakati akiwa mbali , licha ya uwepo wa Yonesi lakini aliona haiwezekani yeye peke yake akamlinda kwa ufanisi , alitamani kuita baadhi ya watu wake kutokea nje ya nchi lakini aliona lazima serikali ingeingilia pia na kuharibu mipango yake mingine , hivyo kwa Watanzania hao waliosalitiwa kama angewarudishia uhuru wao maana yake wangekuwa walinzi bora zaidi ambao pia wasingemletea shida kubwa kwasababu tayari ni Watanzania.

Kwa ufupi ni kwamba licha ya nje ilionekana hali ni shwari lakini swala la Regina kuwa katika hatari ni la muda tu , swala la watu wa Bondeni kupitia intelijensia yao ya Sky eye na kisiwa cha Binamu muda sii mrefu migogoro inayoendelea huko itamfikia Regina kama mwanafamilia pekee mwenye damu ya pete aliebakia.

Hivyo kwa haraka aliona ni vzuri kujiandaa na kila aina ya hatari ambayo itatokea mbele yake na sio baada ya hatari ndio ajiandae.

Anna uwezo wake ulikuwa ni levo ya mbingu maana yake ni kwamba alikuwa na uwezo mara mbili na wa Yonesi , Mima na wenzake wote walikuwa mwanzoni mwa levo ya mzunguko kamili.

Hivyo Hamza aliona kama atawaongezea mafunzo kidogo tu kama ambayo ameanza kumwelekeza Yonesi ndani ya miezi sita au mwaka watakuwa na uwezo wa juu mno kuzidi hata baadhi ya wanajeshi wa kitengo cha Malibu.

Upande wa Anna mara baada ya kusikia sio kwamba wanapelekwa kwenye kampuni kuwa walinzi tu bali kumlinda Regina alijikuta akishangaa.

“Kama swala ni la kumlinda bosi wa kampuni za Dosam , nadhani unaweza kupata walinzi wa kutosha tu”Aliongea Anna.

“Siwezi kuwaambia kila kitu ila kuna zaidi ya sababu ya nyie kufaa kumlinda Regina , kuhusu hilo mtakuja kujua hapo baadae , ki ufupi nawadahili kama wanafunzi wangu pia”Aliongea Hamza.

Upande wa Yonesi mara baada ya kusikia kauli hio alijawa na hisia mchanganyiko , lakini hata hivyo alimwamini Hamza sio mtu ambae anaweza kusema kitu bila ya kuwa na sababu.

“Da Anna , Mkurugenzi wetu ana maadui wengi sana na pengine sio hawa wa kawaida , anahitaji ulinzi wa hali ya juu sana na mimi mwenyewe sina nguvu za kutosha , kama utaungana na mimi itakuwa vizuri sana na nina uhakika Mkurugenzi atawachukulia kama watu wake”Aliongea Yonesi lakini bado Anna alionekana kusita, bado hakuwa na uhakika kama kesi yao inaweza kuisha kirahisi namna hio.

“Vipi kuhusu kesi yetu na kama Mgweno na watu wake wakijitokeza tena nini kitatokea?”Aliongea

Upande wa Hamza hakuwa na wasiwasi sana na familia ya Wanyika kutokana na kwamba alikuwa tayari na ukaribu na Yulia na muda si mrefu angeenda kumpatia ulinzi katika majaribio ya kisayansi na angeweza kuelezea namna tukio lilivyotokea , upande ambao alipaswa kudili nao ni familia ya Mgweno pekee.

“Licha ya Mgweno na familia yake kuwa na nguvu lakini hawana uwezo wa kuziba anga na mkono mmoja , nyie haina haja ya kuwa na wasiwasi mnachopaswa ni kuniamini mimi na hawawezi kuwafanya chochote , kama hamniamini basi mnaweza kumuuliza hata kapteni”

“Da’ Anna nadhani unaweza kuondoa wasiwasi , umeona nguvu ya Mshauri mkuu wa jeshi ilivyo , kwasasa kitengo cha Malibu wanalindwa na sheria ya kutoingiliwa kimaamuzi na wanasiasa kwa namna yoyote ile na hii inamfanya Mshauri mkuu kuwa na nguvu kubwa kuliko hata Mgweno , kwa kauli yake moja tu familia ya Mdudu iliacha kulazimisha ndoa mara moja , hii ni kuonyesha namna gani Afande Himidu ana ushawishi mkubwa serikalini”Aliongea.

Hamza alijiambia anao uwezo wa kufuta kesi yao hata bila ya kumshirikisha Himidu, ni swala la kupiga simu tu , lakini hata hivyo hakutaka kuweka wazi yeye ni nani haswa na nguvu gani anayo.

“Kama mmekubali nadhani tuongozane mpaka makao makuu ya kampuni ili nikawatambulishe na tuongelee swala la mshahara wenu”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu usoni huku akiwachunguza wanawake wote hao.

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa wanawake hao wote walikuwa warembo na maumbo yao yalikuwa ni tata sana.

Hamza hakuacha kuwazia nafasi nyingine ya kunyanduana na Anna , kwa joto ambalo aliweza kuonja kama sio misheni angeunga kingine lakini hakuwa na haraka , alijiambia ni swala la muda tu kama wataendelea kuwa ndani ya kampuni atajipakulia atakavyo , isitoshe mwanamke huyo alionekana kuwa muwazi sana.

Upande wa wanawake hao walikuwa na heshima kwa Hamza na walionekana kumuamini na kumchukulia kama mtu ambae anapenda haki , hawakujua Hamza alikuwa akiwalia mingle baadhi yao.

Ukweli ni kwamba licha ya Hamza kuua baadhi yao waliona halikuwa kosa lake , hivyo waliona haina haja ya kumlaumu , bali wa kuwalaumu ni wale ambao wamewatengenezea maisha yao kuwa magumu namna hio,waliamini hata ikitokeaa wakatumiwa watu kuwaua Hamza hawezi kuangalia tu bila ya kuingilia.

Kitu kingine pia kilichowafurahisha ni kwamba wote walikuwa wakienda kufanya kazi pamoja na kuwa na isingekuwa ngumu kurudi katika hali yao ya kiraia na hata kuwasiliana na familia zao.

Wote hatimae waliondoka katika jengo hilo la mgahawa baada ya kumuaga meneja ambae hakupokea wageni kwa ajili yao na kwenda moja kwa moja mpaka katika ofisi ya Regina makao makuu.

Wakati wanafika Regina alikuwa asharudi katika hali yake ya kawaida na alikuwa akipanga kwenda kwenye kikao na alishangaa mara baada ya kuona kundi la wanawake likiongozwa na Hamza wakiingia ofisini kwake.

“Nini kinaendelea?”Aliuliza huku akimkazia macho Anna na Mima.

“Wife usiwe na wasiwasi , nimepata wazo mujarabu na nimekuja tuliongelee”Aliongea Hamza

“Wazo gani hilo?”

“Inabdi nikuelezee vizuri.. hawa hawajaja hapa kwa nia mbaya”Aliongea Hamza na Regina aliwaangalia mmoja mmoja na kuona wana sura za kipole na alijitahidi kujituliza kwasababu alikuwa akimwamini Hamza

“Kama ni hivyo basi kaeni tuongee”

Mara baada ya kukaa chini Anna alichukua naasi hio na kumwomba Regina msamaha huku wakimhakikishia hawakuwa na nia mbaya zidi yake bali ni hali ya kisasi ndio iliowafanya kwenda mbali namna hio..

Ijapokuwa Regina alishangazwa na hilo lakini hakujali sana , isitoshe alikuwa ashazoea kutishiwa amani kutekwa na mengineyo.

Baada ya kusikiliza kwa umakini hatimae aliweza kuona mpango wa Hamza ilikuwa ni kuwachukua wanajeshi hao ili kuwa walinzi kwake na kampuni.

Regina alikuwa ashajua juu ya maswala ya watu wa bondeni na muunganko wao na watu wa Binamu hivyo ilikuwa rahisi kujua ni kitu gan ambacho Hamza anapanga , lakini bado alikuwa na wasiwasi na familia ya Mstaafu Mgweno kwani bado walikuwa na ushawshi mkubwa mno kwenye nyanja za siasa na uchumi.

“Una uhakika utaweza kulimaliza hili na familia ya Mgweno na upande wa familia ya Wanyika?”Aliuliza Regina

“Kwa namna yoyote ile siwezi kukusababishia matatizo”Aliongea na kumfanya Regina kuegamia kwenye sofa

“Kwasasa maswala yote ya ulinzi wa kampuni yapo chini ya idara ya usafirishaji na kazi kubwa ni kusimamia usalama wa usafirishaji wa hela za benki na baadhi ya bidhaa zenye thamani ya hali ya juu , kama wote mnapanga kujiunga kama walinzi basi nitaunda idara ya ulinzi na kuongeza watu wengi zaidi, kwasababu wewe na Yonesi mnafahamiana wakati mkiwa jeshini basi nitakuamini , lakini kulingana na sheria za kampuni matumaini yangu ni kuona mnazifuata .. kuna utofauti mkubwa kati ya ulinzi wa kampuni na uwanja wa vita”Aliongea Regina akimlenga Anna kama kiongozi wa wenzake.

Mara baada ya kusikia hivyo wanawake hao wote walijikuta wakishikwa na nyuso za shukrani.

“Asante sana Mkurugenzi , tunakuhakikishia tutakulipa kwa uaminifu wako kwetu”Aliongea Anna.

“Tutaongea maswala ya mishahara yenu kesho , kwasasa nina kikao na nitamwachia kazi katibu muhtasi wangu ili awapatie utaratibu wa kupatiwa maeneo ya kuishi katika apartment za kampuni”Aliongea Regina na Anna na wenzake hawakuwa na pingamizi.

Mara baada ya kuona sasa wanakwenda kukaa chini na kuachana na kazi za kuzunguka dunia nzima kwa kuua na kuiba walijihisi ni kama maisha yao yamebadilika ndani ya usiku mmoja tu.

Dakika chache Linda aliweza kuitwa na alishangaa mara baada ya kupewa maelekezo na bosi wake , lakini hata hivyo hakuwa na pingamizi na aliwachukua Anna na wenzake na kisha akafanya mawasiliano na meneja anaesimamia nyumba za wafanyakazi.

Yonesi alikuwa na furaha isiokuwa ya kawaida na aliongozana nao kwenda kwenye Apartment wanayokwenda kuanza maisha upya..

Upande wa Hamza midomo yake ilicheza mara baada ya kuona namna wanawake hao walivyokuwa na furaha na aliishia kutembea mpaka kwenye meza ya Regina.

“Wife , kwanzia sasa hivi nitahusika na kuwafundisha mbinu za mapigano na kuhakikisha wanakuwa vizuri ili niwe na hali ya kujiamini wakikupatia ulinzi”Aliongea wakati wakiwa wawili tu katika ofisi.

“Una uhakika umewachukua kwa ajili ya kunilinda mimi pekee?”Aliuliza huku akimwangalia Hamza kwa macho yenye ishara ya ukauzu ndani yake

“Ah.. sababu gani tena nyingine kama sio kukupa ulinzi , nimewachukua kwa ajili yako mke wangu”

“Hata kwa Anna Black Beuty?”Aliongea Regina.

“Black Beut..” Hamza alitaka kuongea lakini aligundua ameshaingia katika mtego wa Regina.

Ilikuwa mtego kweli maana kulingana na mwonekano wa Regina kulikuwa na hali ya kumkejeli kwenye macho yake.

“Regina mambo sio kama unavyofikiria?”

“Unadhani nafikiria nini?, Halafu unajua nini , ngoja tu nikwambie ukweli ili ukae ukielewa, ijapokuwa sijui namna ulivyokuwa ukiishi wakati ukiwa nje ya nchi na namna ambavyo ulikuwa unawachukulia wanawake lakini ukweli ni kwamba..Sijali sana na kamchezo kako ka usaliti unakopanga kufanya, ninachokusihi tu nikuwa makini na taswira ya kampuni .. kama unataka kucheza nao fanya lakini hakikisha husababishi matatizo la sivyo.. there is limit to my patience”Aliongea Regina huku akimwangalia Hamza kwa macho yaliojaa ukauzu.













SEHEMU YA 110.

Regina mara baada ya kufikiria namna ambavyo Hamza alikuwa akifanya na Anna kwenye sofa mchana kweupe alianza kupatwa na hali ya kusita na kujiuliza au sio kama ambavyo amemfikiria hapo mwanzo.

Alijiuliza pengine hisia nzuri alizokuwa nazo juu yake zilikuwa ni mtazamo wake tu na sio uhalisia wa tabia ya Hamza.

Regina alikuwa na mgogoro wa nafsi kwa wakati huo , alijua asingeweza kumzuia Hamza kutembea na mwanamke mwingine kutokana na kuweka mpaka mwanzoni wa kutokuwa nae katika mahusano ya kimwili, lakini dakika hio wakati akifikiria tukio lile alijikuta akishikwa na hasira na kuhisi amekosewa mno.

Ukweli tokea mwanzo hakutaka kujali kile ambacho Hamza anafanya na ndio maana kampa uhuru wa kufanya kile anachoona ni sawa kwake , lakini hakutegemea Hamza angeenda nje ya mipaka ya uhuru aliomuwekea na alijiuliza kama ataendelea na tabia hio ni wanawake wangapi watakuwa katika orodha.

Upande wa Hamza hakujua kile ambacho Regina anafikiria na aliishia kutingisha kichwa kukubaliana nae na kisha kutoka kwenye hio ofisi.

Upande wa Hamza mawazo yake yalikuwa tofauti , kwa alivyoweza kumsoma Regina ni kutomjali kama anatembea na wanawake wengine , lakini yeye kwa upande wake hakutaka chochote kibaya kitokee hususani kumpa mwanamke mimba na mengineyo.

Siku hio bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Dosam waliweza kupiga kura ya ndio kumteua rasmi Eliza kama Mkurugenzi msaidizi makao makuu , huku Prisila pia akipewa wadhifa wa usimamizi wa kampuni Tanzu zote ambazo zipo nje ya nchi.

Upande wa Eliza alipewa hisa ndani ya kampuni na Regina lakini kwa Prisila hakupewa kutokana na kwamba alikuwa tayari ni mmiliki wa hisa kwenye kampuni.

Wote kwa pamoja kutokana na vyeo vyao kupanda Eliza aliweza kupewa nyumba mpya mali ya kampuni kwa ajili ya kuishi na kuhama kwenye Apartment.

Licha ya maamuzi hayo kufanywa na Regina lakini katika kikao hicho ni kama Wakurugenzi walienda kukalia siti tu na kuonekana lakini hakuna hata mmoja ambae alipinga maamuzi ya Regina.

Lakini hata hivyo licha ya baadhi yao kuwa ndani ya kampuni kwa muda mrefu lakini walikuwa wameachwa mbali na utendaji wa Eliza na Prisila kwa wakati mmoja , hivyo hakuna ambae alikuwa na sababu ya kuzuia mapendekezo hayo.

Regina pia katika kikao hicho hakusahau kuwasilisha pendekezo la kuunda idara ya ulinzi ndani ya kampuni ambayo itaakuwa inahusika na maswala yote ya ulinzi katika kampuni zote ndani ya nchi na swala hilo moja kwa moja lilipitishwa pia.

Siku iliofuata Regina na wasichana hao waliokuwa ni maninja walikubaliana mshahara na nafasi zao za uongozi , Yonesi alipewa nafasi ya kuwa mkuu wa idara yote ya ulinzi huku Anna na Mima wakipewa nafasi ya usaidizi.

Kimantiki Anna ndio alipaswa kuwa na cheo kikubwa kuliko Yonesi kutokana na uwezo wake wa mapigano na daraja lake wakati wakiwa jeshini lakini Yonesi ndio aliekuwa akijua mfumo mzima wa ulinzi wa kampuni na maswala yote ya kazi siku kwa siku ndio maana akawa juu.

Elisi alikuja kuungana na wenzake mara baada ya kuachiwa huru, alikuwa amekonda mno pengine ni kukaa muda mrefu gerezani, ila yeye tofauti na wenzake alionyesha kuwa na chuki na Hamza lakini hata hivyo alielewa mambo mengi baada ya dada zake kumweleza kile kilichotokea na swala la Hamza kuua wenzao ilikuwa ni bahati mbaya na vilevile alijali zaidi maisha ya marafiki zake hao kuliko kisasi chake kwa wakati huo.

Upande wa Hamza pia alijua ni ngumu sana kuwafanya wanajeshi hao kumwamini kwa asilimia mia ndani ya muda mfupi ila hakujali sana kuhusu hilo alichokitaka kwa muda huo ni Regina kuwa salama kwanza.

Siku hio hio mchana Hamza alianza kuwafundisha mbunu mbalimbali za mapigano pamoja na mbinu yake ile ya kucheza mdundiko , ijapokuwa walishangazwa na mbinu hio lakini kutokana na uwezo wa Hamza kuwatisha ilibidi tu wafuate wakiamini matokeo yapo.

Licha ya kuidharau mwanzoni lakini mara baada ya kujaribu kwa masaa kadhaa hatimae walianza kuelewa miondoko hio ilikuwa na nguvu kubwa sana kwenye kuwianisha nishati ya ndani ya mwili na ya nje na dakika hio walijikuta wakimwangalia Hamza kwa macho ya kumkubali.

Jioni yake kwa pendekezo la Anna wote pamoja na Hamza waliona wakusanyike kwenye moja ya Mgahawa mkubwa na kuagiza nyama choma pamoja na Mvinyo na bia mbalimbali kusherehekea uhuru wao pamoja na mwanzo mpya wa kazi ndani ya kampuni ya Dosam.

Mgahawa wote uliokuwa na Bar siku ho ulijazwa na wanawake shirini walinzi wa kampuni ya Dosam na walikunywa na kula kujigalagaza mpaka kuanza kucheza mziki wakisahau shida zao zote.

Hamza aliishia kukaa kwenye sofa huku akiwa ameshikilia zake Whiskey ya JackDanniel akinywa mdogo mdogo huku akiwaangalia wanawake hao wakiwa wamecharuka.

Dakika chache mbele Anna ambae kilevi kilikuwa kimempata alimsogelea Hamza na kwenda kukaa kwenye mapaja yake huku mikono yake akiwa ameipitisha katika shingo yake na kwa namna alimvyokalia Hamza kwa mwanaume yoyote rijali angeshuhudia hio angetamani kuwa katika nafasi ya Hamza.

“Vipi leo unarudi nyumbani?”Aliuliza mwanamke huyo kwa sauti iliojaa madaha na kumfanya Hamza kumeza mate mengi mdomoni.

“Nisipoenda nyummbani ni wapi tena napaswa kwenda bibie?”Aliongea kwa kubabaika.

“Ni kwamba ndio kwanza nimehamia kwenye Apartment yangu na nahitaji mtu wa kunisaidia kuweka vitu vizuri”Aliongea huku akijilegeza zaidi na kuongea kwa sauti ya puani.

“Hebu acha um*laya .. nenda kaweke vitu vyako vizuri mwenyewe, wewe si useme tu unataka duduwasha”Aliwaza Hamza kwenye akili yake lakini viungo vyake vya mwili vilikuwa vikiongea lugha tofauti na mwisho wa siku aliona bora aheshimu msimamo wa viungo vyake na sio akili yake.

“Napenda sana kumsaidia mwanamke mrembo kama wewe kupangilia vitu vyako vya ndani , hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi nitaenda kukusaidia kwa moyo wote”Aliongea huku akiweka tabasamu lililojaa ufisi.

Mrembo huyo aliishia kung’ata lipsi zake na kisha alimwinamia Hamza na kumkisi na kisha akasimama na kwenda kuendelea kucheza disco na wenzake.

Hamza alikuwa akijihisi ameshushiwa pepo ili kufurahia maisha kama kawaida yake , lakini wakati akiwazia usiku utakavyoenda kuwa na mwanamke mwenye shepu matata kama Anna , alijikuta akitetemeka mwili mara baada ya kuangaliwa na macho makali mbele yake.

Alikuwa ni Yonesi ndio aliekuwa akimkata jicho kali kana kwamba ni mke ambae anataka kuibiwa mume.

“Kapteni ya nini kuniangalia hivyo mtoto wa mwanamke mwenzio?”Aliongea Hamza huku moyo wake ukienda mbio na kujiambia isije kuwa Yonesi anapanga kwenda kumwambia Regina.

“Nishapata majibu ya maswali yangu yote , sababu ya kutaka Da Anna na wengine kufanya kazi ndani ya kampuni ni kwasababu yako”Aliongea Yonesi.

“Kapteni huo ni uonevu wa waziwazi , ninachojaribu ni kutenda wema kwa moyo wangu wote mengine ni malipo ya Wema”

“Eti Wema , wakati ulifanikiwa kumfanya waziwazi bila hata ya aibu”

“Dada yako Anna ameshakuwa mtu mzima na alionekana kuwa na hamu, sasa mimi ningefanyaje kama ndio ufunguo wa uhuru wake”

“Yaani tena unaongea kwa kujiamini hivyo , sijui hata upoje huna aibu , usije kuniongeleshe tena”Aliongea Yonesi huku akiwa mwekundu na kuondoka karibu ya Hamza.

Hamza aliishia kumwangalia mwanamke huyo akitingisha matikiti kwa hasira na kujiambia

“Muda sii mrefu na wewe utaililia tu”

*******

Siku iliofuata saa kumi na moja na nusu Hamza alishituka akiwa juu ya kitanda kipya , huku pembeni yake akiwepo mrembo Anna akiwa amelala kwa kujiachia kihasara hasara.

Usiku wa jana mwanamke huyo hakujali hata kuvaa nguo na alijirusha kitandani na kulala , ilionekana bakora zilimchosha mno.

Hamza aliishia kutoa tabasamu tu maana alikuwa na nguvu upya na hakuwa amechoka hata kidogo.

Jana mrembo huyo alitaka kumshinda mbio lakini hakumpa hata kidirisha cha kumpita.

Hamza hakutaka hata kumwamsha, baada ya kuvaa nguo zake kimyakimya alitoka na kuianza safari ya kurudi nyumbani, alipanga akapate kifungua kinywa ndani ya muda bila kushitukiwa na kisha amchukue Regina na kwenda nae kazini.

Mara baada ya kufika alikaribshwa na Shangazi na hakuulizwa hata amelala wapi na Shangazi huyo zaidi ya kupokewa na kukaribishwa kifungua kinywa.

Regina mara baada ya kushuka chini alionekana kutoona utofauti wowote wa kulala nje na ilimpa ahueni, mara baada ya kupata kifungua kinywa aliingia kwenye gari na kisha Hamza alilitoa kuelekea kazini.

“Vipi kuhusu maandalizi ya kwenda Tour kupanua miliki yako?”Aliuliza Regina.

“Ni Safari ya kwenda Tour tu , kuna hata haja ya kujiandaa?”Aliongea Hamza huku akiangalia kioo cha nyuma.

“Ndio unapaswa kujiandaa , unaenda kwa niaba yangu , hivyo angalau unapaswa kujua majina ya wafanyakazi wote , unapaswa kwenda kuwa kiongozi na sio mfuasi”Aliongea na Hamza aliona swala la kukariri majina ya kila mmoja ingekuwa kazi kubwa mno lakini hata hivyo aliishia kutingisha kichwa na kukubali.

Regina mara baada ya kuona Hamza amejibu kikawaida macho yake yalijawa na usiriasi ghafla.

“Vipi habari za Anna , mmeridhishana vya kutosha?”Aliuliza na kufanya mapigo ya Hamza kudunda kwa nguvu.

“Wife unaongelea nini mbona sikuelewi?”Aliongea Hamza huku akiweka muonekano wa kipole.

“Sikutaka kuongea mbele ya Shangazi , unadhani sijui na unaweza kunificha unachofanya?”Kulikuwa na ishara za hasira kutoka kwa Regina na ilionekana alikuwa akijitahidi kujizuia kutokulipuka.

“Wewe umejuaje sasa?”Aliongea Hamza huku akilazimisha tabasamu.

“Wewe hujui sisi wanawake tupo sensitive na harufu ya marashi ya wanawake?”Aliongea Regina huku akiona Hamza anamuona ni mjinga kwa kuona hajui ushenzi wake anaofanya.

“Unahisi kama sijui namna ya kukuzuia unaweza kulala na kila mwanamke?”

“Regina babe sio hivyo , mimi sio mtu wa kugusa kila mwanamke , anyway nimekosea nitajitahidi kuwa makini”

“Kuwa makini!?”

Regina alijikjuta akipandisha sauti hata bila ya kujielewa huku akiwa na kila hali ya kumkatia tamaa Hamza.

“Kila siku unasema unataka uhusiano wetu upige hatua na niwe mke wako kweli lakini ni tabia gani hii unaonionyeshea , yaani juzi tu ndio umekutana na Anna nikajua umefanya vile kuniokoa lakini vipi kuhusu hii mara ya pili , mtu umejuana nae siku mbili tu lakini ushaanza kulala kwake jamani?, halafu ulivyo mshenzi mimi ninaoitwa mkeo ndio ninaepaswa kuwalipa mmoja baada ya mwingine na kisha niwapatie sehemu ya kuishi , hivi unaniona mimi ndio mwanamke mjinga juu ya wajinga si ndio , yaanii unaniona ni mwepesi mwpesi tu kudanganywa?”Aliongea Regina kwa kurudia kwa usongo mkubwa sana kiasi cha kumfanya Hamza kuchanganyikiwa kidogo na kujiuliza yote hayo yanatokea wapi.

“Eliza kwasasa ni msaidizi wangu ukiachana na hivyo kwangu ni kama dada, umekuwa na uhusano nae kabla yangu ndio maana sikutaka kuingilia mahusiano yenu , isitoshe sikutaka kumpoteza mtu muhimu kama Eliza kwa ajili yako lakini vipi kuhusu Anna , yaani kwasababu tu anaonekana kuwa mwanamke mwepesi kwako ndio unaweza kumfanya unachotaka bila kujali ninachojisikia?”

Hamza mara baada ya kusikia maneno hayo alishikwa na hatia na aliona ilikuwa kweli kabisa amekosea licha ya kwamba siku zote wanaume mbele ya mwanamke wanaongozwa na kichwa cha chini lakini haimuondolei kosa.

“Wife naomba usiwe na hasira hivyo , naomba msamaha na nakuahidi siku nyingine sitomgusa kabisa Anna , nitakaa nae mbali”Aliongea Hamza

“Inatosha sasa , siitaki hata kusikia unaomba msamaha , kama kuomba msamaha kungekuwa kuna tosha sheria zimewekwa za nini , najiona tu mjinga kutaka kuamini mwanaume kama wewe uliejaa maneno mengi unaweza kuaminika , najua tokea mwanzo ulichokuwa ukitaka ni kucheza na unaona unao uwezo wa kumtega kila mwanamke kwa maneno mazuri na kisha kwenda kulala nae , unadhani hata mimi ni aina ya hao wanawake ambao wanaweza kulainika na maneno yako pekee?”

“Sio kweli , sijawahi kuwaza kwenye maisha yangu nitakuja kufunga ndoa na mwanamke kama wewe , naheshimu sana uhusiano wetu tuliokuwa nao”Aliongea Hamza mara baada ya kutngisha kichwa.

“Sorry Mr Hamza , I didn’t notice that”Aliongea Regina kwa kejeli na kisha aligeuza kichwa chake na kuangalia nje ya gari akiwa hataki kuongea neno lingine tena.

Upande wa Hamza alijikuta akishikwa na mawazo , alitamani kusimamisha gari ili kumwelewesha Regina lakini bado hakuona kisingizio , isitoshe alikuwa amekosea sana.

Aliamua kuendesha gari hivyo hivyo akiwa amenuniwa mpaka ndani ya kampuni

Dakika ambayo alisimamisha gari waliweza kumuona Linda akisogeela gari yao kwa kasi kubwa.

“Bosi hali sio shwari”Aliongea Linda kwa wasiwasi.

“Nini kimetokea mbona haraka hivyo?”Aliongea Regina huku akikunja sura.

“Watu kutoka TRA na Wizarani wamefika na wanasema wanataka kupitia rekodi za kampuni pamoja na ulipaji wetu wa kodi .. lakini kwa namna wanavyoonekana hawajaja kukagua bali kutengeneza tatizo , wakuu wote wa Idara wanapaniki kutokana na hili”AliongeaLinda.

Mara baada ya kusikia hivyo Regina alijikuta bila ya kupenda akimwangalia Hamza

Hamza upande wake aliweza kujua nini kinaendelea , ilionyesha mara baada ya kuwachukua Anna na wenzake chini ya kampuni moja kwa moja jambo hilo halijamfurahisha Mgweno na anajaribu kuonyesha nguvu yake kutaka kuiyumbisha kampuni.

Kutokana na hilo Hamza alizidi kushikwa na haya na kuwa na wasiwasi kwenye moyo wake , alimuonea aibu hata Regina aliekuwa mbele yake

“Mkurugenzi hii ni dharula , ijapokuwa hakutakuwa na tatizo kwenye baadhi ya idara zetu lakini kwenye idara ya uwekezaji ,Ununuzi na PR lazima kuna vitu wataweza kuvipata na kama ikitokea kusambaa hisa zetu znaweza kushuka sana”Aliongea Linda kwa kupaniki.

“Una paniki nini sasa na wewe , hebu twende kwanza ofisini”Aliongea Regina kwa sauti iliojaa ukauzu.

“Ofisini bosi , sio kwamba unaenda kukutana nao kwanza?”Aliongea Linda.

“Hilo ni kundi la watu ambao wanapokea maagizo tu , kuongea nao ni kupoteza muda”Baada ya kuongea hivyo moja kwa moja aliingia kwenye lift

Hamza na Linda pia walifuatia , Hamza yeye alikuwa akifikiria ni kwa namna gani Regina anaenda kutatua hilo tatizo hivyo alikuwa na shauku.

Regina mara baada ya kuingia ofisini alitumia simu ya mezani na haraka haraka aliingiza namba na kisha kuweka mkonga sikioni na ndani ya dakika chache tu simu ile iliopokelewa.

“Hello Kamishina Mombo, ni mimi Regina…”

“Naona watu wako siku hizi majukumu yao sio mengi kabisa ni kwasababu ya uchaguzi nini , naona umeniletea mpaka watu wa kutoa ushauri namna ya kuendesha biashara…”Aliongea Regina.

Hamza mara baada ya kusikia hivyo alijua moja kwa moja Regina anaongea na Kamishina mkuu wa mapato

“Mkurugenzi huna haja ya kuwa na wasiwasi… kinachofanyika ni utaratibu wa kawaida kabisa ili kufunga mahesabu kabla ya mheshimiwa kukabidhi ofisi, Dosam ni moja ya kampuni ambayo kwa muda mrefu inaongoza kwa kuheshimu sheria na kulipa kodi zake ndani ya wakati , kampuni yenu ni ya kuigwa ndani ya Tanzania yote , nakuamini sana Bosi Regina juu ya hili..”Aliongea Kamishina huku akijifanyisha kama hakukuwa na mkono wa mtu.

“Kamishina nimepewa taarifa umepata kadi ya hadhi ya VVIP ndani ya hoteli ya Tanganyika miezi miwili iliopita , sikupata hata muda wa kukupongeza ..”Aliongea Regina na upande wa pili ulikaa kimya kwa sekunde.

“Mkurugenzi unaonekana kuwa na taarifa nyingi mno ila kwa hadhi yangu sijawahi hata kutia mguu kabisa ndani ya hio sehemu unayoongelea ni gharama sana haha..”Alijitetea.

“Nimesikia tena mtoto wako wa mwisho alikosa sifa za kujiunga chuo baada ya kufeli vibaya masomo yake ya A level , lakini sasa hivi nimeambiwa yupo chuo kimoja kikubwa tu hapa nchini , sijui na hizi pia nitakuwa nimesikia viibaya”Aliongea Regina.

“Bosi Regina naomba tuongee hili swala vizuri… nadhani sio vizuri kuhusisha maswala ya kifamilia likija swala la kazi”

“Sikutaka kuhusisha familia hata mimi pia, lakini Kamishina siku hizi sio tu hutaki hata kunipa muda wa kujiandaa lakini vilevile hata hunichukulia mimi Regina Siriasi au ni kwasababu ya Bibi..”Aliongea lakini upande wa pili ulionekana kimya.

“Kamishina nataka siku ya leo tu kujiandaa na baada ya hapo wanaweza kwenda popote katika idara zangu lakinii baada ya hapa sitaki kuwaona tena vinginevyo siwezi kujizuia zaidi juu yako”Aliongea Regina kwa ukauzu.

“Asante sana kamishina kwa kunielewa naomba nikutakie bahati katika serikali mpya ijayo na furaha kwa familia yako”Aliongea Regina mara baada ya kuonekana upande wa pili kuelewa na kisha akakata simu.

Upande wa Hamza aliekuwa pembeni akisikia mazungumzo hayo aliishia kuvuta pumzi nyingi.

Ilonekana kama mkurugenzi wa kampuni haikuwa kukaa ofisini tu na kufanya kazi zinazohusu kampuni bali alielewa kila kinachoendelea katika mfumo mzima wa siasa na watendaji wote wa serikali.

Kwa Lugha nyepesi licha ya kwamba kampuni yake hakutaka kuiingiza katika siasa haikumaanisha kwamba hakuwa na taarifa.

Kitaalamu inaitwa kujifahamu wewe mwenyewe na pia kumfahamu adui yako, sentensi hio inaweza isionekane vizuri lakini katika macho ya mfanyabishara adui yake mkubwa ni serikali , hivyo unapaswa kuielewa biashara yako na kuielewa na serikali pia.

Kuielewa serikali katika biashara haikumaanisha kuelewa sheria zake ilimaanisha kuelewa watu wanaosimamia hizo sheria na kupata udhafu wao ili kuutumia vyema pale unapopatwa na shida.

Bila kuielewa serikali nje ndani mwisho wa siku kama mfanyabiashara utaishia kuweka juhudi ili ufanikiwe lakini ukipata mafanikio unagawana nusu kwa nusu na serikali , wanasiasa ni watu ambao wana hila sana na hawapo serikarini kwa ajili ya kutumikia wananch bali wapo kwenye vitengo kwa ajili ya kujitumikia.

Hamza kwa mara nyingine alipata kumfahamu Regina kwa namna ambavyo alikuwa siriasi hasa katika neno lake la mwisho.

Kitendo cha Regina kumtamkia kamishina kwamba anamtakia bahati katika serikali mpya ijayo maana yake anampa onyo kwamba anao uwezo wa kumkosesha hio bahati na onyo hilo lazima lipokelewe kwa hofu kubwa , isitoshe hakuna mwanasiasa asiekuwa akiogopa nguvu ya kampuni ya Dosam ikitaka kuitumia kuwakosesha ulaji.

Regina mara baada ya kufungua notebook yake akitaka kupiga namba nyingine aligeuka na kukuta Hamza alikuwa akimwangalia na alijiktua akikunja sura kwa hasira.

“Wewe nae unasubiri nini hapa?”

“Kwani sitakiwi kuwa hapa?”

“Unaongea nini , nimewazuia kwa siku moja maana yake unatakiwa kumaliza hili swala ndani ya siku moja , au sio wewe uliesema utawajibika kwa chochote kitakachotokea juu ya swala hili?”Aliongea Regina na Hamza aliishia kujichekesha mwenyewe na aliona ilikuwa sahihi , lakin hata hivyo alikosa amani kutokaana na hasira alizokuwa nazo Regina.

Aliishia kuondoka kwenda kufikiria namna ya kumaliza swala hilo ili ndani ya siku iliopatikana wasije kurudi tena hapo.

ITAENDELEA IJUMAA-WATSAPP 0687151346
 
Back
Top Bottom