Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Shetani rudisha akili zetu na mke wangu inamuhusu nani?[emoji848]
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZI:SINGANOJR

SEHEMU YA 125.

Ajenda moja

Selina alijikuta akishikwa na huzuni kiasi cha machozi kuanza kumtoka na Hamza aliishia tu kuchukua tissue na kumpatia huku akimfariji.

“Dokta hajawahi kukulaumu hata kidogo , tokea mwanzo alijua njia alioichagua ni ngumu na ya hatari, hivyo ilikuwa sawa kwako kumpinga”

“Hapana nilipaswa kuwa nae bega kwa bega angalau asingekuwa mpweke mpaka nyakati zake za mwisho ..”Aliongea na kisha palepale alilazimisha tabasamu na kuendelea kuongea.

“Hamza asante sana, najua ila nitajitahidi kuwa sawa”

“Unapanga kukaa hapa nchini kwa muda gani?”Aliuliza Hamza.

“Sijajua pia , hii nchi nimependa mazingira na watu wake na naona kukaa kwa miezi kadhaa halitakuwa jambo baya , pia nimepata mwaliko kutoka kwa vyuo mbalimbali vya tafiti kwa ajili ya kutoa mafunzo , hivyo sidhani nitakuwa mpweke sana maana nina kitu cha kufanya”

“Kama umepata kitu cha kufanya basi huwezi kuwa bored , natamani kukualika kwa ajili ya chakula cha usiku nyumbani kwangu lakini kwa bahati mbaya nina jambo la kushughulikia “Aliongea Hamza.

“Hehe.. usiwe na wasiwasi , nitapata muda wa kutosha kwa ajili ya kukumbuka mapito yangu , kama ulivyochagua kuishia hapa natamani pia na mimi kupageuza makazi , ni kwa bahati mbaya tu watu wako wote wamesambaa dunia nzima la sivyo pangenoga kwa uwepo wa watu wengi”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha mabega.

“Hawa watu ukiwaleta hapa nchini , vitengo vya usalama sidhani kama watawaacha salama , kwasasa nimeona ni vyema kuishi maisha ya kawaida tu na kufurahi , kila mtu ana maisha yake hivyo naona ni vizuri zaidi”Aliongea Hamza.

“Naona kweli umeamua kustaafu kabisa, ila sawa , sitaki kukusumbua kwa muda mrefu unaweza kwenda kushughulukia maswala yako”Aliongea

Prisila aliekuwepo hapo alikuwa haelewi chochote walichokuwa wakiongea licha ya kwamba lugha waliokuwa wakitumia ni kingereza , hakuelewa kwasababu topiki ilikuwa mbali sana na yeye.

“Hamza napanga kesho kwenda Morogoro kumsalimia mjomba , kama utakuwa na muda twende wote basi”Aliongea Prisila.

“Sidhani kama nitaweza , nimemkasirisha Regina napanga kwenda kumpeti peti”Aliongea na kumfanya Prisila kushangaa.

“Imekuwaje?Regina sio mtu wa kukasirika haraka hivyo”.

“Jana nililala kwa Dina na asubuhi ya leo kagundua kuhusu hilo .. nimemkosea kweli hivyo napaswa kufanya linaoowezekana kumrudisha kuwa sawa”Aliongea Hamza na kauli ile ilimfanya Prisila kuwa na mshangao kiasi , hakuamini kama Regina anaweza kukasirika kwasababu tu Hamza kalala nje , alijua mahusiano yao ni ya kikazi lakini kilichokuwa kikionekana Regina alikuwa akimchukulia Hamza siriasi na swala hilo lilimfanya moyo wake kukosa amani.

Prisila aliishia kumwangalia Hamza akitokomea na gari upande wa barabarani baada ya kumwambia atachukua Uber kurudi baada ya kumalizana na Serena.

Baada ya Hamza kuondoka ilibidi Prisila kukaa chini na Serena kwa ajili ya kujadili kuhusu mkataba wa nyumba na swala hilo halikuchukua muda mrefu.

Baada ya kumaliza Serena alimuuliza Prisila kama alikuwa bize siku hio ili awe mwenyeji wake kumtembeza tembeza, Prisila alifikiria kidogo na kuona hakuwa bize sana na alikubali.

Lakini kitendo cha Prisila kukubali hali flani isiokuwa ya kawaida ilionekana katika macho ya Serena lakini aliizima haraka na tabasamu .

“Basi ni vizuri , naona kabisa tunaweza kuwa marafiki wakubwa”

******

Upande mwingine katika mgahawa wa Dina alionekana Kanali Dastani akikaribishwa na Lawrence kuingia katika ofisi ya bosi wake.

Dastani siku hio alionekana kujiamini na aliekuwa amevalia suti ya rangi nyeusi na miwani ya jua , ilikuwa ni kama vile hakutaka watu kumjua ni yeye.

Mara baada ya kuingia ndani ya ofisi hio alipokelewa na Dina ambae alionekana kuwa bize kuchambua majaini flani yaliokuwa mezaji kwa ajili ya kuandaa kanuni mpya ya utengenezaji chai.

“Karibu kanali”

“Asante Madam Dina”Aliongea Dastani akiwa na tabasamu na kisha alikaa na upande wa Dina hakuwa na haraka sana kwani alisogelea kifaa maalumu cha kukamua majani na kisha akakinga maji flani ya kijani kwa na kikombe kwa sekunde kadhaa, baada ya kumaliza alisogelea Water Dispenser ya maji ya moto na alichukua kikombe flani cha kupimia na kujaza na kisha akachanganya na ile supu ya majani na kukoroga , hakuishia hapo tu aliweka vijiko kadhaa vya asali na kukogoka na kisha alisogea kwenye sofa na kuweka kwenye meza ya kioo na kumkaribisha Dastani.

Taratibu zote hizo za kutengeneza chai Dastani alikuwa akiziangalia na alijikuta akivutiwa mno na usiriasi wa mwanamke huyo na hali flani isioelezeka iliujaza moyo wake.

“Unajua licha ya neno Kahawa kutokana na asili ya lugha ya kiarabu ya neno qahwa haikumaanisha kahawa kama kahawa , mfano hii chai jina lake maarufu ni Kashmiri Kahwa ambapo ukiweka katika lugha yetu unaweza kuita Kahawa kutoka India , siri ya neno kahawa ipo kwenye muunganiko wa malighafi ambazo zinatengeneza chai ambayo kazi yake si tu kuchangamsha mwili lakini pia husaidia kufanya ubongo kupokea kiasi kikubwa cha damu yenye oksijeni, sisi tulikosa bidhaa adimu za kutengeneza aina ya hii chai ndio maana tuliichukulia cofee kama kahawa ili kumaanisha kazi ya kinywaji katika mwili , Karibu uonje kahawa kutoka Kashimir”Aliongea Dina na kumfanya Kanali kutabasamu.

“Inaonekana kila chai inayotengenezwa hapa ina kazi yake mwilini , sio ajabu naona kuna watu wengi sana , lakini sioni vijana zaidi ya wazee”Aliongea Kanali.

“Kuna umri ukifika unajikuta una jali sana afya yako kuliko starehe, wazee wapo katika hatua hio , miili yao haijijengi hivyo wanahitaji angalau kila kinachoingia katika miili yao kina faida , ni tofauti na vijana”

“Weka chai ya kuongeza nguvu za kiume watamiminika”Aliongea na kumfanya Dina kutoa tabasamu.

“Nilidhani nitamuona Amosi?”Aliongea na Kanali alikunywa kidogo chai na kisha aliweka chini huku akisikilizia uchungu wake na kisha utamu wake.

“Majukumu ndio maana , lakini anajua uwepo wangu hapa”Aliongea.

“Nadhani kazi umeikamilisha , kwasasabu watu wa vitengo mnaonekana kuwa bize hususani na kipindi hiki cha mwanzo wa serikali mpya uenda moja kwa moja”Aliongea Dina na kumfanya Amosi kukohoa kidogo.

“Nimefanikiwa kwa kiasi kidogo kuweza kupata taarifa kuhusu familia ya Wanyika , nasema ni kidogo tu kutokana na ukweli kwamba familia hii taarifa za ke zina mkanganyiko mkubwa sana”Aliongea na kumfanya Dina kumwangalia kwa shauku.

“Naweza kusikia hata hicho kidogo na kuona kama kinanitosheleza”

“Ukweli ni kwamba familia ya Wanyika nguvu yake haitokani na kushikilia sehemu nyeti ndani ya taifa la Tanzania pekee”Aliongea huku akionekana kutafuna neno la kuongea.

“Kwanza kabisa asili ya jina la familia hii linat okana na jina lenyewe la nchi kwa upande wa Tanzania bara , ambapo ni sawa na Watanganyika , maana yake ni kwamba ni familia ya watu wa Tanzania bara,nimeshindwa kupata muundo wa familia hii haswa lakini kitu kikubwa kinachoifanya familia hii kuwa kubwa na yenye ushawishi ni kutokana na kuwa kama kituo cha mfumo wa World political power links(WPPL)

“Unamaanisha nini kusema WPPL?”Aliuliza Dina.

“Ni muunganiko wa kimadaraka wa kidunia , kwa kuelezea ni mtandao unaunganishwa na familia moja zenye nguvu ya ki utawala kwa ajili ya uwezeshaji wa Ajenda Moja”

“Ajenda Moja!!”

“Ndio labda kwa mfano tuseme dunia ina mpango wa kuhalalisha sheria ya haki za mashoga dunia nzima na hili ili lifanikiwe lazima viongozi wa juu ya nchi wakubaliane na viongozi wa nchi nyingine, ili isitokee viongozi hawa kutokubaliana viongozi baina ya nchi na nchi inabidi kuwe na mfumo wa kuteua viongozi ambao wakiwa madarakani moja kwa moja watakuwa tayari kutimiza sheria hizi, sasa hapa ndio zikaibuliwa familia zenye asili ya ukaazi wa nchi husika na kupewa nguvu ya ushawishi ili kuweza kuweka kiongozi ambae anao uwezo wa kupitisha Ajenda Moja, ni aina ya mfumo wa kifamilia katika kila taifa kwa ajili ya kuitawala dunia yote”Aliongea Kanali na kumfanya Dina kushangaa.

“Kwahio unamaanisha kwamba familia ya Wanyika ni familia ambayo ina asili ya chimbuko ambayo imeibuliwa na kuwezeshwa nguvu ili kuwezqa kuchagua kiongozi ambaye atakubali kuendana na mfumo wa Ki Ajenda wa dunia nzima?”

“Ndio na kuhusu familia ya Wanyika sio familia moja , unaweza kusema ni muunganiko wa Familia za Kitanganyika zenye asili ya ukazi wa kihistoria, hivyo nguvu yao ilitokana na msaada wa mashirika makubwa ya kidunia ambayo yanawezesha mpango wa utekelezaji wa Ajenda Moja”

“Naweza kupata mrtiriko wa hizi familia”Aliongea Dina.

“Kuhusu hili imekuwa ngumu sana kupata taarifa zake , hata swala la muunganiko wa familia pia kuna utata mkubwa, muunganiko wake wa kikabila haujawa wazi , ni swala ambalo natamani kulijua zaidi”Aliongea.

“Unazungumzia vipi kuhusu familia ya Mgweno na Wanyika , mtafaruku wao?”

“Familia ya mstaafu Mgweno ni familia kama familia ambayo haijifungamanishi na kabila bali ni sawa na kusema wewe Dina na mume wako mnapanga kutengeneza kizazi ambacho kitaunda familia yenye nguvu ndani ya taifa katika nyanja zote , familia yenu haitoitwa ya Kipare wala ya Kisukuma ,. Labda nikupe mfano wa familia kubwa duniani , mfano Rockfeller Familly au Rothchild , kwa maneno marahisi Mgweno anajaribu kutengeneza kizazi chake ambacho kitakuwa na nguvu ndani ya Tanzania kwa miaka mingi ijayo na anajairbu kuomba sapoti nje ya nchi kwa ajili ya kukamilisha mpango wake”

“Kwahio ameshindwa kupata hio sapoti?”

“Kwa taarifa ambazo sina uhakika nazo , Mgweno na Familia ya Wanyika hawakupata msaada kutoka nje kwa kipindi kirefu , uhasama mkubwa ambao uliibuka baina ya Mgweno na Wanyika ni pale alipojaribu ku’ Neutrilize ‘sapoti’ ambayo familia ya wanyika walikuwa wakipata,ukumbuke kwamba Mgweno aliingia madarakani kwa msaada wa familia ya Wanyika lakini yeye ndio aliejaribu kuwapindua na kutaka kutengeneza Legacy yake na hatua ya kwanza aliofanya ni kuomba kushindana na familia ya Wanyika bila ya mataifa ya nje kuingilia na kutokana na kuwa na marafiki wengi nje ya nchi aliweza kufanikisha hili na ndipo alipoanza vita yake na Wanyika kwanzia hapo”Aliongea Kanali na Dina alionekana sasa kupata picha

“Kwahio unataka kusema Mgweno alipewa pia nafasi ya kupata msaada kutoka nje ya nchi kama tu atafanikiwa kuishinda familia ya Wanyika?”Aliuliza na kuitikia kwa kichwa na kumfanya Dina kuelewa sasa na alionekana kuridhika.

“Wewe kama mtu wa kitengo unadhani nani ana nguvu zaidi hapa nchini kwasasa?”Aliuliza

“Kwasasa katika upande wa Siasa Wanyika kashika mpini , ila katika uchumi ni arobaini kwa ishirini”

“Unamaanisha nini kusema 40 kwa 20 kuna zaidi ya asimilia arobaini hazipo?”

“Familia ya Wanyika katika uchumi ni 20 na Mgweno katika uchumi ni 40 , lakini licha ya hivyo bado hana nguvu ya moja kwa moja kutokana na kwamba ameshindwa kuyamiliki makampuni makubwa mawili ya Tanzania ambayo yanabeba zaidi ya asilimia 40 za uchumi wote”

“Kama sikosei , unamaanisha Dosam na Vexto?”Aliongea na Kanali aliishia kuinua kikombe kumpa ishara ya cheers na kunywa chai.

“Kwa lugha rahisi hizi kampuni mbili ndio zinatengeneza uwiano na kufanya Mgweno kukosa nguvu kubwa ya kishawishi licha ya marafiki zake wengi kuwapatia mitaji ya nchi wakati wa uongozi wake huku yeye akipata asilimia , mikataba ambayo alisaini kipindi cha uongozi wake imemfanya kupata asilimia kubwa za gawio mpaka sasa”Aliongea na Dina alionekana kupata mwanga wa kile alichokuwa akitafuta.

“Kiasi flani nimeridhika na taarifa yako , lakini nina swali la mwisho,nimepata kusikia una uhusiano mkubwa zaidi na Mheshimiwa Eliasi Mbilu rais aliemaliza muda wake , unadhani kwanini Eliasi akaamua kumsaliti Mgweno?”Aliuliza na kumfanya Kanali kuweka kikombe chini.

“Taarifa unayotaka ni nje kabisa ya makubaliano yetu?”

“Najua lakini pia taarifa ulionipatia haijitoshelezi”Aliongea.

“Nadhani baada ya hapa nitafanikiuwa kupata mzigo alioachwa Mchuku?”Aliongea na kumfanya Dina kufikiria kidogo .

“Nitakupatia”Aliongea na kauli ile ilifanya macho ya Kanali kuwaka.

“Nisema tu Eliasi hakuwa na nia ya kumsaliti Mstaafu , ila hakuwa na jinsi”

“Unamaanisha nini”

“Nadhani jibu juu ya hilo unalo , Mgweno alishindwa kulinda udhaifu wake na ndio uliotumika kumfanya Eliasi kuchukua maamuzi, kumbuka Mgweno na Wanyika wote walikuwa katika vita ya nani wa kukalia kiti cha urais”Aliongea na kumfanya Dina kushangaa kidogo.

“Umejuaje kama naweza kujua majibu ya swala hilo?”

“Nani asiejua Mgweno alitaka kushindana na ulimwengu wa Giza ili kujisimika yeye , lakini babu yako akaingilia na kumtengenezea udhaifu, hii ni kitu ambacho licha ya watanzania wengi kukizungumzia kama uzushi lakini ni kitu ambacho kimetokea kabisa na Vitengo vya usalama haviwezi kuthibitisha hili”Aliongea na Dina alitingisha kichwa .

“Nadhani ni muda wako sasa wa kunipatia faili aliloacha mchuku , lakini kabla ya hapo nina swali kwa upande wangu?”Aliongea na Dina alitingisha kichwa kukubali.

“Kwanini ulitupatia faili lile la mwanzo?”Aliuliza.

“Kwasababu ulikuwa mtu sahihi wa kulipata”Aliongea Dina.

“Kivipi?”

“Unataka faili aliloacha Mchuku kwasababu unataka kufuatilia kesi ya Sedekia , ukweli ni kwamba moja ya sababu mtandao wetu unaishi ndani ya taifa ambalo linasheria kali sana zidi ya ulimwengu wa Giza ni kwsababu tunatunza siri nyingi sana, urithi ambao babu aliniachia ni nusu ya siri za nchi , sijui ni kwa namna gani alizipata , lakini baada ya mimi kuchukua nafasi yake niliunda mpango wa mimi pia kukusanya siri , ndio maana nikamwajiri Mchuku na wengineo , katika siri ambayo ilinitia shauku ni hii inayohusiana na Sedekia na kesi ya Radi Mkoani Rukwa”Aliongea Dina na kumfanya Kanali kufuta jasho.

“Kwahio na wewe unaamini Sedekia yupo hai?”Aliuliza na Dina alifikiria kidogo.

“Kuhusu Sedekia kuwa hai ama kutokuwa hai , inategemea na mafanikio ya uchunguzi wako”

“Kivipi?”

“Nitakupatia faili aliloacha Mchuku , nilikupatia faili kukupa mwanga ili kuwa na mtazamo tofauti katika uchunguzi wako”Aliongea na kisha alirudi na kuchomoa bahasha na kumpatia.

“Ndani ya hio nyaraka kuna vitu vitatu, viwili ni kukuhusu wewe mwenyewe na kimoja ni kuhusu faili la Mchuku, ukishasoma utajua maana yake”Aliongea na kumfanya Kanali macho kumtoka lakini Dina aliishia kutoa tabasamu.

******

Hamza hakwenda moja kwa moja nyumbani na badala yake alitumia saa moja kununua zawadi kwa ajili ya Regina , ikiwemo Doughnut alizopenda na vitu vingine.

Kutokana na makadirio ya muda na ratiba yake ilionyesha ndani ya saa sita za mchana Regina alipaswa kuwa nyumbani amekwisha kurudi tayari.

Lakini sasa Hamza baada ya kufika nyumbani hakuweza kumkuta Regina zaidi ya Shangazi ambae alikuwa anaangalia TV.

“Hamza mbona umebeba vitu vingi , umenunua nini?”Aliuliza Shangazi akiwa na tabasamu maana ni mara ya kwanza kumuona Hamza akirudi akiwa na vitu mkononi.

“Ni zawadi za Regina , bado tu hajarudi?”Aliongea na kumfanya Shangazi kutoa tabasamu la uvivu.

“Kwanini hujui ratiba ya Regina , hatorudi siku ya leo ni mpaka kesho”

“Si alitakuwa arudi leo mchana , kwanini ni mpaka kesho?”

“Kanipigia simu asubuhi ya leo na kusema kwamba ataondoka Afrika ya kusini lakini atatua Mwanza , hakuniambia sababu lakini nadhani ni maswala hayo hayo ya kazi”Aliongea na kumfanya Hamza kushika paji lake la uso kama vile alikuwa na mawazo na kujiambia pengine Regina hakutaka kurudi nyumbani kwasababu hakutaka kuonana nae.

“Shangazi mimi naondoka kwenda Mwanza”Aliongea akiwa ashaamua palepale.

Zamani mtu akikwambia anaenda Mwanza ilikuwa ni safari ndefu sana kwa njia ya basi, lakini serikali ilikuwa imepiga hatua kubwa sana katika usafirishaji kwani kulikuwa na treni ya umeme ya kilomita mia tatu kwa saa inayotoka Dar Es salaamu mpaka Mwanza bila kusimama njiani na kufupisha masaa ya kusafiri kutoka masaa zaidi ya kumi na mbili mpaka masa manne tu.

“Unataka kwenda mbali huko , tangu lini mahusiano yenu yakawa ya karibu hivyo kiasi cha kushindwa kuvumiliana kukutana zaidi ya siku mbili?”Aliuliza Shangazi kwa furaha

Hamza hakujua acheke ama alie ila aliishia kumwambia namna ambavyo amemkasirisha Regina na alielewa.

“Hata mimi nilishangaa inakuwaje Regina kubadili ratiba yake na kufikia Mwanza bila ya kumpumzika , kama ni hivyo unaweza kwenda”Aliongea Shangazi na Hamza alikubali na palepale aliita Uber na baada ya kuingia kwenye gari alitumia mtandao kupata tiketi na alibahatika maana treni hio ilikuwa ikijaza sana kutokana na kuwa na ratiba moja tu ya kutoka Dar kwenda Mwanza na kulikuwa na nyingine ya kutoka Mwanza kuja Dar katika wakati mmoja na kupishana katikati. Ilikuwa ni ya moja kwa moja kutokana na kwamba kulikuwa na ya kutoka Dar Kwenda Dodoma asubuhi na kisha kuna ya Dodoma kwenda Mwanza hivyo wasafiri ambao walitaka kwenda Mwanza mapema wanaunganisha wakifika Dodoma.

Saa mbili za jioni ndio muda ambao Hamza aliweza kufika katika jiji la Mwanza , alipaswa kufika saa moja lakini kutokana na kuchelewa kidogo kwa treni njiani walitumia masaa matano.

Baada ya kutoka kituoni na kuchukua Bolt hakuhangaika hata kumtafuta Regina kwasababu alikuwa akijua ameblokiwa , hivyo ilibidi awasiliane na Linda akiamini kama sekretari wake atakuwa na itinerary , lakini kabla ya ya kumpigia alipata wazo na kulifanyia kazi.

Victoria International hotel ilikuwa ni hoteli kubwa ndani ya jiji la Mwanza ambayo inamilikuwa na kampuni ya Dosam.

Mara zote Regina akisafiri kikazi kwenda Mwanza hufikia katika hoteli hio kwenye chumba cha hadhi ya rais(Presidential Suite) sasa Hamza alikumbuka juu ya hio taarifa kutokana na kuisoma akiwa kazini ndio maana akaghairi kumpigia Linda.

Taksi ilimchukua mpaka Victoria na kisha alitoa kitambulisho maalumu cha kazini na kumpatia Meneja wa hoteli ambacho kilimuoneysha kuwa msaidizi binafsi wa Regina, alipewa kitambulisho hicho baada tu ya kupata ofisi.

Baada ya kuthitbitishwa na Meneja palepale Hamza aliachwa kwenda juu kabisa kwenye floor ambayo chumba hicho cha kifahari kinapopatikana.

Hamza alikuwa na mzuka kweli akiamini kitendo chake cha kutoka Dar es salaam mpaka kuja Mwanza itakuwa ni moja ya kete ya Regina kumsamehe.

Lakini sekunde ambayo alibonyeza kengele alishangaa mtu ambae alifungua mlango hakuwa Regina.

SEHEMU YA 126.

Alikuwa ni mhudumu wa hoteli hio alievalia sare , ambae kazi yake ni kusafisha chumba hicho na mara baada ya kumuona Hamza mbele yake aliuliza kwa hali ya upole kabisa.

“Kaka naweza kusaidia shida yako”Aliongea

“Hiki si ndio chumba cha Mkurugenzi Regina alichochukua si ndio?”

“Oh , Mkurugenzi kaenda kwenye kikao lisaa limoja lililopita ndio maana nimekuja kufanya usafi”Aliongea yule mhudumu wa kike na kumfanya Hamza kushangaa kidogo.

“Unajua ni wapi kinapofanyikia?”

“Nitajuaje sasa kaka?”Aliongea na kumfanya Hamza kushika kiuno na kupumua kwa nguvu , alichokifanya ni kuweka boksi la doughnut alilokuja nalo na kisha alimsubiri ndani ya chumba hicho aweze kurudi.

Masaa mawili yalipita na ilikuwa ishatimia saa sita za usiku bila ya Regina kurudi , Hamza alikuwa akinywa mvinyo aliokuta lakini alianza kukosa uvumilivu baada ya kusubiri muda mrefu.

Palepale alitoa simu yake na kujaribu kumtafuta Regina lakini kama kawaida wenye mtandao wao walisema inatumika na kumfanya Hamza kupiga kibao kwenye paji la uso kwa kuona haikuwa na lazima kujiuliza maswali mengi na anapaswa kumpigia simu Linda.

Hamza palepale aliitafuta namba ya sekretari na kupiga simu na haikuwachuikua muda mrefu ilipokelewa.

“Hamza kuna tatizo?”Sauti ya Linda ilisikika, hakuwa amesafiri na Regina na muda huo alikuwa nyumbani.

“Nataka uniambie kama unajua ni wapi Regina ameenda kwenye kikao leo hii hapa Mwanza”

“Mkurugenzi kwani yupo Mwanza! Si alikuwa South Afrika na alipaswa kurudi leo?”Aliongea Linda kwa kushangaa pia

“Hata wewe hukuwa ukijua , Regina baada ya kutoka Afrika ya kusini aliunganisha kuja Mwanza , inaonekana kuna watu aliokuja kukutana nao, lakini mpaka sasa hajarudi hotelini na sijui nani yupo nae”

“Muda umeenda sana , ilipaswa mpaka sasa hivi awe amesharudi kama ilikuwa ni kikao tu”Aliongea Linda.

“Ndio maana nina wasiwasi , nimejaribu kumpigia lakini simpati hewani”Aliongea Hamza hakutaka kusema ameblokiwa.

“Basi jaribu kuwasiliana kwanza na Yonesi , nilisikia wanasafiri nadhani na wao pia watakuwa wameenda mwanza kwa ajili ya ulinzi”Aliongea na Hamza alikata simu palepale na kisha alipiga namba ya Yonesi na ndani ya dakika chache tu sauti ya kivivu iliweza kuisikika upande wa pili.

“Hamza!Kuna nini mbona unanipigia sasa hivi?”

“Yonesi naulizia kuhusu mke wangu, yupo wapi?”

“Yupo hapa Umoja club, tumemsubiri kwa muda mrefu lakini hajatoka bado, nadhani kuna kinachoendelea”Aliongea Yonesi.

“Nini kimetokea huko ndani , kwaniini kachukua muda mrefu hivyo?”

“Mazungumzo ya kibiashara Afrika ya kusini hayakuenda sawa baada ya Mkurugenzi wa kampuni ya Prima kuingilia dili hilo na kumsafirisha muwekezaji kutoka South Afrika mpaka Mwanza kabla ya kukutana na Regina , kutokana na mazungumzo mwanzo kufanyika baina ya muwekezaji na kampuni ya Dosam , Regina alikuwa tayari kufanya mazungumzo upya lakini Yulia akaingilia kati na ikawa ni kama ushindani”Aliongea Yonesi.

“Yulia!”Hamza sura ilijikunja palepale na kujiuliza Yulia si yupo bize na maswala yake ya utafiti , imekuwaje akapata hadi na muda wa kuingilia biashara za Dosam na kuja mpaka Mwanza.

Mpaka hapo Hamza aliona ni namna gani Regina alikuwa hatari mbele ya Yulia na palepale alijikuta akishikwa na wasiwasi na kukata simu na kisha aliingia mtandaoni na kuitafuta Club hio ilipo na kuiita Bolt impeleke.

Umoja Club ni moja ya Club kubwa zinazopatikana ndani ya jiji kubwa la pili kwa ukubwa ndani ya Tanzania , Club hii wamiliki walikuwa ni kampuni ya Yulia na ilikuwa ikihudumia matajiri zaidi kutokana na hadhi yake.

Hamza mara baada ya kufika nje ya jengo hilo la Club lililokuwa limependezesha eneo hilo alijikuta akishagaa baada ya kugundua kulikuwa na mlinzi aliekuwa na mafunzo ya hali ya juu ya kimapigano katika gari kwenye maegesho.

Lakini Hamza hakujali sana zaidi ya kusogelea mlango lakini palepale aliweza kuona watu kadhaa wakikaribia kutoka nje huku wakiongea kati yao alionekana Regina na Yulia.

Wote wawili walikuwa wamevalia mavazi ya kawaida ya suti, tatizo tu ni kwamba Regina hakuwa na mwoneknao wake ule wa siku zote na kumfanya aonekane mdogo sana mbele ya Yulia.

Yulia alikuwa na tabasamu pana na alipeana mkono na baadhi ya wanaume waliokuwa wamesimama.

“Mkurugenzi Motsepe Mkurugenzi Lewis, Mheshimiwa Shitimbi nimefurahishwa sana na maamuzi yenu ya kuendana na mpango wetu wa kampuni ya Prima , Jumatatu rasmi tutatuma watu kwa ajili ya vikao”

“Huna haja ya kutuhushukuru , sisi ndio ambao tunapaswa kukushukuru wewe Bosi Yulia kwa kutuchagua katika hii biashara”Aliongea Mzee Lewisi

Wanaume hao walionekana kuwa matajiri na walikuwa wapole sana mbele ya Yulia , ilikuwa ni ile hali ya kutoa ushirikiano kwenda kwa Yulia kwa moyo mkunjufu.

Upande wa Regina mwonekano wake haukuwa na furaha hata kidogo , midomo yake ilionekana kufubaa na pia alionekana kama mtu alietumia kilevi.

Hamza mara baada ya kumuona Regina na mwoneknao huo moyo wake ulikakamaa , alijua lazima Regina atakuwa amekunywa sana pombe kwasababu alikuwa na mawazo , haikuwa na haja ya kuelewa kinachoendelea , ilionekana Regina alikuwa akifukuzia dili la kibiashara na limefeli kwa kunyakuliwa na Yulia.

Yonesi na wenzake pia walikuwa na wasiwasi baada ya kumuona bosi wao alivyonyongea.

Baada ya mabosi wale kumaliza maongezi na Yulia , yule bwana aliefahamika kwa jina la Motsepe alimgeukia Regina na kumuomba radhi kwa makubaliano yao kutofikia muafaka na Regina hakujali sana zaidi ya kumpatia mkono huku akimwangalia Yulia kwa ukauzu mkubwa.

Yulia alijiona mshindi kwani alitoa tabasamu huku akiwa sio mwenye kujali sana mwonekano wa Regina.

“Bosi Regina kampuni yako inapiga hatua siku hadi siku , nina uhakika utaweza kupata dili kubwa tofauti na hili”Aliongea

“Bosi Yulia unaonekana upo well informed mpaka najiona labda ni kwasababu ya umri wangu kuwa mdogo”Aliongea Regina na kumfanya Yulia kucheka.

“Ukiwa haupo juu ya mlima huwezi kuona vilele vya milima mingine nyuma yako , nikupe hongera kwa kuhitimu rasmi shule ya awali katika biashara , hasara uliopata leo chukulia kama ada ya kile ulichojifunza”Aliongea na kisha palepale aligeuka akitaka kuondoka,lakini ni saa ileile macho yake yaliweza kumuona Hamza ambae alikuwa akiingia.

“Hamza unafanya nini hapa, au unadhani nimemuonea Regina mpaka anataka kulia maana sio kwa kununa huko kama unataka kunipiga?”Aliongea huku akicheka , muoneknao wake ulijaa uchokozi wa aina yake.

Hamza hakumjali kabisa hata kumwangalia usoni na badala yake alimpita na kwenda kumshika Regina mkono.

“Tuiondoke”Aliongea Hamza.

“Niachie”Alijibu Regina akimwangalia Hamza kwa mshangao kiasi lakini akikataa kushikwa kwa wakati mmoja.

Hamza hakuwa na mpango wa kumwachia na alimwangalia Yonesi ambae alikuwa akimwangalia Regina kwa kubembeleza.

“Yonesi mnaweza kuondoka mkapumzike , huyu niachieni mimi”

Yonesi aliishia kumwangalia Hamza kwa muonekano usioweza kusomeka na kisha bila ya kuongea neno alitingisha kichwa na kumtupia Hamza ufunguo wa gari na kuwapa wenzake ishara na wakageuka na kuondoka.

“Wewe niachie bwana”Aliongea Regina huku akivuta mkono wake kwa nguvu.

“Ukileta ukinzani sishindwi kukulazimisha kukukiss mdomoni mbele ya watu”Baada ya kusikia hivyo alijikuta akiacha kuleta ukinzani kwa kuamini Hamza hashindwi kufanya kama alivyoongea .

Hamza alimtoa Regina na kwenda kumuingiza ndani ya gari na kisha akaliwasha na kuondoka.

Kitendo kile kilimfanya Yulia aliekuwa amesimama kupiga kwa nguvu miguu yake chini kwa hasira na kisha akalisogelea gari lake.

Ndani ya gari hio alikuwepo mwanamke mrefu alievimba misuri na kipara kichwani huku akiwa amevalia suti nyeusi.

Baada ya kumuona Yulia amerudi kwenye gari aligeuza sura yake na kumwangalia akiwa na tabasamu na kisha akaongea kwa sauti iliojaa ucheshi.

“Mkurugenzi ushamaliza maongezi yako ni kurudishe hotelini?”Aliuliza na kumfanya Yulia amwanagalie mwanamke huyo alivyojipaka lipstick vibaya na kujikuta akikunja sura.

“Hebu geukia mbele utanifanya nitapike na lipstick yako”

“Lipstick yangu inatatizo gani wakati hii ni moja ya bidhaa maarufu kutoka Luis Vuiton kwasasa”

“Tatiuzo sio lipstick ila mtu alieipaka ,Mungu wangu sijui hata babu anafikiria nini mpaka kunipata mtu kama huyu kama bodigadi”

“Bodigadi unamuonyeshea dharau ni komandoo aliepitia mafunzo makali na kwa uwezo wake hapa ni upotevu wa rasilimali za nchi kumlinda mtu mmoja ,pia pengine sasa hivi angekuwa zake mitaani huko akiwa matembezini na mpenzi wake”Aliongea kwa nafsi ya wingi.

“Bertha kaa kimya kabla sijakuchoka”Aliongea Yulia.

“Kwani mkurugenzi shida ipo wapi , kama ni dili umeweza kumshinda Regina , lakini kwanini wewe ndio unaonekana kama ndio umeshindwa na umejaa hasira kama umekunywa diseli ?”

“Ni kwasababu ya yule mpuuzi Hamza kujifanyisha kauzu mbele yangu na kunipita bila hata ya kuniangalia usoni , yaani alichofanya ni kama kuniambia sina thamani yoyote ya hata yeye kuniangalia usoni , ngoja nitamkomesha siku sio nyingi akiwa bodigadi wangu”

“Kumbe ulikuwa ukishindana na Regina kwasababu ya mwanaume ndio maana ukaingilia dili lao?. Yulia unaonekana kuwa mwanamke kichaa kama mimi tu, kukutana kwenu naona sio kwa bahati mbaya, mimi Bertha nakupa sapoti yote kupigania penzi lako”

“Penzi!!”Aliongea Yulia kwa hali ya kejeli kama vile amesikia kituko na kisha akaendela kuongea.

“Sijawahi kuamini kuna kitu kinachoitwa mapenzi mimi , halafu Bertha unafanana na mwanaume kwanzia mwonekano mpaka matendo yako imekuwaje kuwaje ukawa kwenye mahusiano?”Aliongea na kumfanya Bertha kujishandua kwa kujitingisha.

“Mpenzi wangu kasema mimi ni mrembo na nimemuamini na sikuchukii kwa upofi wako wa kutoona urembo wangu , hivi unadhani ni wanaume wote watakupenda mwanamke kama wewe kwasababu ya mwili na sura yako?”Aliongea na kumfanya Yulia kukosa neno na kuishia kuegamia.

“Afande Bertha tafadhari naomba unirudishe hotelini nimechoka”

“Haha.. usiwe na wasiwasi mwenyewe nataka kwenda kubebika na mpenzi wangu usiku kucha , Yulia mdogo wangu pambana mpaka kieleweke acha unyonge wa kishenzi shenzi”Aliongea kwa kugonga gonga mskani kukazia sentensi yake.

“Eeeh , tafadhari naomba uendeshe”

*****

“Wapi unanipelekea wewe?”Aliuliza Regina aliekuwa amekaa kwenye gari, moyo wake ulikuwa ukipitia machafuko.

“Wife I am sorry , siku nyingine sitokudanganya ..”

“Kwahio umekuja kote huku kwa ajili ya kuongea hivyo?”

“Ulinibloku kwenye simu , kama nisingekuja kukutafuta ningefanyaje sasa?”

“Nimekublock ndio , unapanga kufanya nini?”

“Kwahio utaendelea kuniblock?”

“Nitafanya ninachojisikia , halafu unanipelekea wapi nataka kurudi zangu hotelini nikapumzike”

“Ukinitoa kwenye Blacklist ndio nitakurudisha”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kusaga meno kwa hasira na kutamani kumrukia Hamza na kumpiga ngumi za uso.

“Na sikuondoi hata ujizamishe ziwani na kufa kifo cha kutapatapa”

“Kwahio unadhani nikijizamisha kwenye maji ndio nitakufa, siwezi kufa kwasababu ya kuzama mimi”Aliongea Hamza na kauli ile ilimuuzi mno Regina na hakutaka kujizuia tena baada ya kuona Hamza anamchokoza makusudi.

Palepale alichomoa mkanda wa siti na kisha aliurukia mkono wa Hamza bila kujali anaendesha na kuung’ata kwa nguvu zake zote.

“Arghhhhhhhhh!!!”

Hamza alijikuta akikosa neno , ijapokuwa hakuhisi sana maumivu lakini alitamani kucheka na kulia kwa wakati mmoja kwa kuona namna mwanamke huyo alkivyokuwa na hasira na nguvu alizotumia kumng’ata.

“Regina tabia gani hii , kama unataka kunikissi wewe nikiss, kuning’ata si utaishia kunipa joto la mkono tu”Aliongea Hamza na Regina aliendelea kumng’ata kwa muda mrefu mpaka meno yake kuuma lakini hakuona Hamza akionyesha dalili za kuumia hata kidogo na kujikatia tamaa.

Aliishia kukaa zake kivivu na kuegamia dirisha akiangalia mandhari ya nje bila kuongea kitu.

Hamza aliendesha gari kimya kimya na kwenda kuliingiza Malaika Beach na kuliegesha upande wa fukwe ya ziwa.

Regina mara baada ya kuangalia mazingira alionekana kutokufurahisha nayo kabisa.

“Umenileta huku kufanya nini? Nataka kurudi hotelini mimi”Aliongea na Hamza wala hakujali, alifungua mlango na kisha akazunguka upande wa siti ya nyuma na kumfungulia mlango.

“Kwa jinsi ulivyolewa na sura yako ilivyovimba kwenda kulala hivyo hivyo ni kujizeesha tu haraka , wewe hujui kunywa pombe ukiwa na hasira inachangia uzee?”Aliongea Hamza.

“Wewe inakuhusu nini nikizeeka , nirudishe hotelini mimi”Aliongea na Hamza hakutaka kumjali sana kwani aliinama na kufungua mkanda wa siti na kumshika mkono kumtoa nje na kisha akafunga mlango.

Muda ulikuwa umeenda sana,watu waliokuwa wakila ‘bata’ kwa kulewa walikuwa wachache sana licha ya kuwa wikiendi, zamani eneo hilo lilikuwa maarufu na kufurika nyakati za wikiend lakini kutokana na uwekezaji mkubwa katika mahoteli na kumbi za starehe kufanyika ndani ya jiji hilo ilikuwa ni mwendo wa kugawana wateja.

Hamza baada ya kumtoa nje aliinama na kumshika mguu wake na kumfanya Regina kumwangalia kwa mshangao.

“Wewe unafanya nini?”

“Nataka kukuvua viatu”

“Sitaki , nitavua mwenyewe tu usije kunichungulia”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kusikitika.

“Umesikia wapi mume akimchungulia mke wake kwa kumvua viatu?”Aliongea huku akiangalia miguu ya Regina ilionona na kitendo cha kujaribu kuigusa tu msisimko aliopata haukuwa wa kawaida.

Regina aliishia kukubali tu na Hamza alitoa viatu na kisha akavitupia ndani ya gari na baada ya hapo alikunja suruali yake kidogo na kumwambia Regina watembee.

Ijapokuwa kulikuwa na hali ya ubaridi lakini kutokana na Regina kuleweshwa na mvinyo hakuhisi baridi kabisa.

Baada ya kutembea kimya kimya mpaka mwisho wa eneo la hoteli hio Hamza alimwangalia Regina ambae alionekana kuwa kimya muda wote.

“Regina unawaza kuhusu dili la kibiasara ambalo limefeli?”Aliuliza Hamza na Regina hakujibu zaidi ya kuangalia upande wa ziwani.

“Kwani lilikuwa dili kubwa kiasi gani , mimi ninavyojua kwenye biashara kuna muda wa kupata na kukosa vilevile?”Aliongea.

“Wewe huelewi , dili hili lilikuwa limebakia kusainishana tu na kujadili vipengele vya kimkataba lakini ghafla tu anatokea mtu na kukupokonya tonge mdomoni , kilichotokea ni hasara kubwa”

“Lakini hio ni kawaida pia kwenye biashara , kwanini ya kujitia mawazo tu”

“Nilikuwa nishafanya maandalizi tayari , kushindwa kusaini hili dili nimepata hasara zaidi ya bilioni kumi na moja , sijawahi kupata hasara kubwa kiasi hichi kwa kukosa uwekezaji , bado najiuliza imekuwaje mpaka nikafanya makosa?.Nilipaswa kufanya uchunguzi kabla kujua nani ni mshindani wangu lakini nikapotezea na mwisho wa siku Yulia akaingilia”Aliongea.

“Kama dili limefeli haina haja ya kubeba mzigo wote , kwanza hakuna mtu ndani ya kampuni atakaekusema wala kukuuliza?”

“Wewe unajuaje kama hakuna ambae hataongea na kuuliza , hata kama wasipoongea mbele yangu huko mafichoni itakuwa ni kazi ya kunijadili kadri wawezavyo mpaka meno ya wawashe. Huna haja ya kunifariji nishakubali tayari na hata kama wakiniongelea mabaya sitojali”

“Unasema hutojali lakini hebu jiangalie ulivyo sasa hivi , umekosa kabisa hata ile ari yako ya siku zote , kwani si umefanikisha mambo mengi tu kabla ya hili dili , kwanini kufeli kwa mara moja kukufanye kama umefeli mara mia moja na kutaka kukata tamaa?”Aliongea Hamza.

“Unaongea ujinga gani , kwahio unaniona mimi dhaifu?”Aliuliza huku akimwangalia Hamza kwa kumkazia macho na kisha alizipiga hatua kwa kutotaka kusimama nae ten , alitembea mpaka upande wa Bar wa hoteli hio na kisha aliulizia bei ya Wine.

“Karibu sana dada ,pia kuna nyama choma jikoni ya kiwango cha hali ya juu kwa ajili ya kushushia”Aliongea yule mhudumu kwa ucheshi kabla ya Regina kuagiza.

“Nataka hio Wine tu ni shilingi ngapi mnauza?”

“Efu ishirini na tano tu”Aliongea na Regina muda ule ndio alikumbuka hakutoka na mkoba wake kwenye gari na aliishia kumgeukia Hamza.

“Una hela hapo?”

“Regina haina haja ya kunywa wine tena , muda umeenda na sura imekuvimba”

“Una hela au huna?”Aliongea kibishi na kumfanya Hamza kukosa jinsi na kuishia kutoa Wallet na kuchomoa misimbazi mitatu.

Regina mara baada ya kupewa chupa yake hakujali hata glasi kwani baada ya kufunguliwa aliichukua na kisha akarudi ufukweni huku akinywa kwa pupa na aliishiwa kupaliwa na kukohoa mpaka machozi yakamtoka.

“Nini kinachokufanya kuwa na haraka hivyo , kunywa taratibu, hebu jiangalie ulivyolewa kwanza na unaendeleza”

“Nikilewa inakuuma nini , halafu sio kwamba nina kwenda kazini”

“Itakuletea shida kwenye mwili wako , kwanza unaonekana ni mtu ambae hujawahi kulewa , kama kinachokupa mawazo ni kushindwa kukamilisha dili hilo swala lishapita haina haja ya kujiumiza”

“Haikuhusu , niache kama nilivyo”Aliongea huku akitembea kama kichaa kuelekea upande wa ziwani , alionekana kama mwanamke mpweke ambae amefiwa.

Hamza alijikuta akiishia kukaa kimya na kutoongea chochote huku akimfuata nyuma nyuma na kadri alivyokuwa akinywa ndio alivyozidi kulewa na ilimfanya Hamza uvumilivu kumshinda.

“Regina acha kuendelea kunywa hio Wine inazidi kukulewesha , nishakuambia huna unachoweza kubadilisha hata ukinywa pombe zote”

“Acha kupoteza muda wako kwa kujairbu kunifariji , sihitaji hata supu ya kuku , akili yangu inafanya kazi kwa utimamu kabisa”

“Sio kwamba nakufariji najaribu kukuambia ukweli”

“Ukweli gani?”

“Huwezi kumshinda Yulia , nikikulinganisha wewe na yeye , wewe unaonekana kuwa dhaifu zaidi”Kitendo cha kusikia kauli hio ni kama pombe ilimwishia ghafla na alionyesha hali ya kutoikubali kauli ya Hamza.

“Kwahio unaniona mimi ni mjinga kuliko yeye na kampuni yao ni kubwa kuliko kampuni yetu ya Dosam?”

“Yulia familia yake ni ya Wanyika , nguvu ya familia yake tu inatosha kukumaliza kabisa , isitoshe uwezo wa Yulia ni kitu ambacho huwezi hata kufikiria , ukweli ni majuzi tu hapa nimekuja kugundua swala la kufanya biashara ni kama anajifurahisha tu , yule anakipaji anajua kutumia rasilimali watu na kujitengenezea matokeo anayotaka na vilevile anajua kujitumia yeye mwenyewe kupata anachotaka , haijalishi ni urembo wake au kichwa chake kila kitu ni muhimu kwake, sasa ukijilinganisha nae tofauti na wewe kuwa mdogo na mrembo sidhani kama una kitu kingine cha kujilinganisha nae”Aliongea Hamza.

Regina baada ya kusikia namna ambavyo Hamza anamsifia Yulia alijihisi moyo wake ni kama unatolewa na kushindwa hata kupumua , hakujua hata machozi yametoka wapi lakini yaliloanisha mashavu yake.

“Naona unamsifia sana , kama unampenda sana kwaninii usiende na ukamuoe , kwanini umenileta mpaka huku na kusimama mbele yangu na kuanza kumsifia, unaniona mjinga kisa kanishinda?”

ITAENDELA.
WhatsApp : 0687151346
 
Shukran San [emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom