Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bado uko Kambi kiongoziNaweka kambi
Shukran San Mr. Singano[emoji120][emoji120]SHETANI RUDISHA AKILI ZETU
MTUNZI:SINGANOJR.
Imehaririwa na:ChatGpt
SEHEMU YA 128
Kaka Fabiani(Mkaka).
Kwa hali ilivyokuwa, ilionyesha dhahiri kabisa wahusika walikuwa wamejitega juu ya mlima na mara baada ya zoezi lao la kwanza kumalizika, walianza kushuka na magari yao.
"Wife, jifiche kwenye hili jiwe, usije ukatoka. Ngoja mimi nikaangalie kinachoendelea," aliongea Hamza.
"Usikurupuke, pengine kuna mabomu mengi zaidi," aliongea Regina kwa kuonya.
"Usiwe na wasiwasi, ukipatwa na tatizo piga kelele mara moja, ila usikimbie," aliongea Hamza na kisha, palepale, alitoka nduki kuelekea upande wa mabehewa ya nyuma ya treni.
Ukweli ni kwamba angeweza kuondoka na Regina bila ya kufanya chochote, lakini mara baada ya kuwaza, aliona kulikuwa na abiria wengi waliokuwa ndani ya treni na isingekuwa sawa kuondoka na kuwaacha.
Mara baada ya kufika upande wa kushoto wa treni hiyo, aliweza kuona watu wengi walikuwa wakitoka nje na kukimbia, lakini ni dakika ileile sauti za milio ya bunduki zilianza kusikika.
Zilikuwa zikitokea juu, zikishuka chini kwenye treni hiyo na kugonga kwenye mabehewa.
Muda huo, abiria ambao walikuwa ndani walijikuta wakishikwa na hofu huku wengi wao wakipiga makelele kutokana na milio hiyo. Hakuna ambaye alikuwa na ujasiri tena wa kutoka nje.
Dakika ile, Hamza aliweza k ugundua hayakuwa magari kama alivyokuwa amedhania, bali ni pikipiki za matairi manne zilizokuwa zimefungwa injini za jeep huku zikiwa na matairi makubwa na mbele yake zilikuwa zimeunganishwa na mtutu uliokuwa ukikohoa risasi.
Kundi la watu waliovalia kombati za jeshi ndilo lililokuwa likiziendesha huku wakisogelea treni hiyo kwa kasi kubwa.
Walikuwa wamefunga vitambaa vya rangi nyekundu kuzungusha kwenye mikono yao, na kombati zao pia hazikuwa na alama yoyote kuonyesha walikuwa jeshi gani.
"Kaeni ndani wote, mwenye kimbembe cha kutoka nje tutafumua kichwa chake," aliongea mwanaume mmoja aliyekuwa na mwili uliojaa misuli huku akiwa amejifunga bandanna usoni. Uzito wa sauti yake ulitosha kuwaogopesha watu na kuonyesha hakuwa na masihara hata kidogo.
"Namba nne, namba tano, nendeni mkamkamate," aliongea akitaja majina ya namba.
"Yes, Sir," walitikia kikakamavu, na palepale wanaume waliojivisha mavazi waliokuwa wameshikilia bunduki za AK-47 waliingia kibabe ndani ya behewa la daraja la kwanza ambapo Regina na Hamza walikuwepo mwanzo.
Hamza macho yake yalisinyaa palepale. Aligundua hawa watu walikuwa na mazoezi ya kawaida tu ya daraja la mwanzo kabisa kabla ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi, lakini bwana ambaye alionyesha kuwa ndiye kiongozi, yeye alikuwa katika daraja la nusu mzunguko katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.
Licha ya kwamba wenzake walionekana kutokuwa na levo ya juu, lakini nguvu zao hazikuwa za kawaida.
Cha kutisha zaidi ni kwamba walikuwa na silaha nzito walizoshikilia kwenye mikono yao, na aliona kama atakurupuka na kwenda kuwashambulia basi uwezekano wa abiria kuumia ni mkubwa sana. Lakini hata hivyo, alikuwa kwenye hali ya kujiuliza watu hao ni akina nani na wametokea wapi, na kwanini wamevamia treni hiyo.
Ilishangaza kwa sababu nchi kama Tanzania kiwango cha uhalifu kilikuwa chini sana na hiyo yote ni kutokana na ushirikiano mkubwa wa vyombo vya usalama kuanzia jeshi la kulinda nchi na jeshi la polisi. Sasa kitendo cha watu hao kuwa na magari ambayo wameyatengeza kuweza kutembea nje ya barabara lakini vilevile kuwa na silaha za moto ilishangaza, na kuna hisia zilimwambia pengine kuna wahusika ndani ya vyombo vya usalama waliohusika; la sivyo isingekuwa rahisi mpaka kutega mabomu.
Hamza aliishia kutokujua cha kufanya kwanza. Kwa walivyoonekana, ilionyesha kabisa kuna mtu ambaye walikuwa wakimtaka ndani ya treni hiyo, na alijiambia hapaswi kufanya chochote kwanza na anapaswa kusubiri angalau wamkamate wanaomtafuta ndio achukue hatua.
Lakini dakika ileile, kitendo cha wale wavamizi kuingia ndani ya treni hiyo, upande mwingine walitoka wanaume na wanawake waliovalia mavazi ya kawaida wakiwa wameshikilia bunduki na kuanza kushambuliana nao.
"Tututututututu, Thump, thump thump!"
Magaidiwale walionekana kutotarajia mashambulizi hayo na kujikuta wakizubaa na kuishia kupigwa risasi.
Hamza macho yake yalichanua kwa tukio hilo, na aliweza kugundua watu hao waliokuwa katika mavazi ya kiraia walikuwa ni wanajeshi wa uwezo wa juu kabisa.
"Tulitegemea tu kunaweza kuwa na shambulizi la kushitukiza. Vijana, ingieni wote na hakikisha hakuna anayepona na tunakamilisha misheni yetu," aliongea yule mwanaume kwa sauti ya amri, na palepale alishuka kutoka kwenye gari huku akiwatanguliza vijana wake mbele.
Dakika chache mbele, mirindimo ya risasi ilisikika kwa nguvu ndani ya mabehewa hayo, na kulikuwa na vilio vingi vya watu kutoka ndani. Ilionekana abiria walikuwa wakipata majeraha kutokana na patashika hiyo.
Hamza, mara baada ya kuona jambo hilo, alishikwa na hasira palepale na kujiuliza wanajeshi hao walikuwa wanafikiria nini. Aliona haikupaswa wajitokeze kwanza hadi wampate wanayemtafuta, na baada ya kumtoa nje, ndipo wachukue jukumu la kumuokoa badala ya kushambuliana katikati ya kundi la abiria. Lakini hakuna kilichoweza kufanyika kwa muda huo. Kitendo cha watu hao kuanza kushambuliana kilimaanisha kuwa hakuna tena kuangalia usalama wa raia; ilikuwa kama vita.
Ijapokuwa Hamza hakuwa na cheti cha udaktari, wazo ambalo lilimjia akilini muda huo lilikuwa kusaidia raia waliopatwa na majeraha. Hata kama alikosa leseni, aliona yeye ni daktari na anapaswa kufanya jambo.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa tete, Hamza alifyatuka na kuingia ndani ya treni hiyo ili aone namna ya kuzuia risasi zisipite kwenye behewa lililokuwa na abiria wengi. Lakini kabla hata hajachukua hatua, wanajeshi wengi waliovalia kiraia walitoka kwa wingi wakiwa wameshikilia bunduki.
Hamza, baada ya kuwaangalia tu, alijua hao walikuwa wana usalama ambao pia ni wanajeshi, kutokana na wengi wao kuwa katika mavazi ya suti. Sekunde chache mbele, alitoka mwanaume mwingine aliyekuwa amevalia koti la suti na suruali ya jeans, akiwa ameshikilia kitu kama fimbo, lakini kifaa kilichoonekana kama kisu kwa wakati mmoja.
Bwana yule hakujali risasi zilizokuwa zikirindima, bali alichomoka kwa spidi na ustadi wa hali ya juu kabisa, akawasogelea wale wavamizi na kuanza kuzungusha ile fimbo ya chuma. Sauti za kugongana kwa chuma zilianza kusikika huku wale magaidiwakidondoka chini kwa spidi kubwa wakiwa hawana uhai.
Hamza, mara baada ya kuona tukio lile, aliishia kukunja sura na kujiambia kwamba yule bwana hakuwa mwepesi. Mara baada ya kuona mtu yule alikuwa akipambana na yule bwana aliyekuwa amejifunga skafu ya rangi nyekundu, wawili wengine walijawa na ujasiri na kuanza kushambulia.
Yule bwana kiongozi wa kundi hilo la wavamizi alionekana kuwa mzuri pia kwenye mapigano, nguvu yake ya kurusha mashambulizi haikuwa ya kawaida, kwani iliambatana na nguvu za nishati za mbingu na ardhi. Lakini yule bwana aliyekuwa ameshikilia silaha ya usinga alikuwa akifanya mashambulizi yaliyo pendezesha macho kutokana na ustadi wake. Baada ya kukwepa mashambulizi mawili mfululizo, kisha akasogea kwa namna ya kuruka pembeni huku akirusha silaha yake akimlenga yule gaidishingoni.
Lakini kiongozi yule alikuwa na ustadi wa hali ya juu mno, kwani alipangua ile silaha kwa kutumia bunduki na kisha, bila kusubiri, alifanya shambulizi la mzunguko kwa kutumia nguvu bila nishati za mbingu na ardhi na kumpiga yule mwanajeshi.
“Wow!” Hamza alijikuta akivutiwa na namna mvamizi yule alivyorudisha shambulizi. Licha ya kwamba alikuwa jambazi, alifurahishwa na namna alivyotumia sanaa ya mapigano kwa ustadi mkubwa. Hamza aliangalia kidogo tu akitaka kujua wanatumia mbinu gani za kupambana, na aliweza kujua kila kitu kuhusu sanaa zao. Walionekana kuwa watu waliopitia mafunzo ya kijeshi, hususani katika mataifa ya Asia.
Hamza, mara baada ya kuona wanajeshi hao wanaweza kudili na hali hiyo bila kuingilia, aliamua kuingia kwenye behewa lingine lililokuwa na abiria waliokuwa wakitoa vilio vya maumivu kwa ajili ya kuwasaidia.
“Wasaidieni walioumia kuwatoa nje kwanza!” Aliongea Hamza kwa nguvu baada ya kufungua mlango, lakini licha ya kuongea hivyo, abiria waliishia kumwangalia tu kutokana na hofu waliokuwa nayo.
Hamza, mara baada ya kuona wapo katika hali hiyo, hakutaka kujali sana. Kwa haraka, alichukua waliokuwa na majeraha na kuwabeba, kisha kuwatoa nje nyuma ya mabehewa sehemu aliyoona kuna usalama. Alirudi na kufanya hivyo kwa kurudia rudia huku akitoa huduma ya kwanza kwa haraka.
Aliweza kupata boksi la huduma ya kwanza na alitumia bendeji na baadhi ya dawa kuwasidia watu ili damu zisizidi kuwatoka.
Regina, ambaye alikuwa amejificha katika kifusi cha jiwe, aliweza kumuona Hamza akiingia ndani ya treni akiwa amebeba watu na kurudi tena. Aligundua kwamba alikuwa akisaidia watu. Kwa kile ambacho Hamza alikuwa akifanya, Regina alionekana kuguswa. Alikumbuka jinsi alivyomdhania Hamza mwanzoni kama mtu ambaye anaweza kuua kikatili bila kujiuliza mara mbili, lakini tukio hilo la kuokoa watu lilimfanya kuona upande wake mwingine.
Muda huo, wanajeshi waliokuwa katika mavazi ya kiraia waliweza kutumia faida ya wao kuwa wengi na kuwadhibiti magaidimmoja baada ya mwingine, huku wengine wakikimbia kutaka kujiokoa, lakini waliishia kupigwa risasi za migongoni.
Yule bwana mwanajeshi aliyekuwa akitumia silaha ya usinga alikuwa mwepesi mno kwenye kushambulia na kuweka pambano. Alipambana na yule kiongozi wa magaidi, na mapambano yao yalionekana kuchukua muda mrefu, huku wakiendelea kupigana mpaka walipotoka nje kabisa. Hata hivyo, Fabi alifanikiwa kumjeruhi kiongozi yule kwa kumkata kata, hali iliyomfanya aonekane asiyetamanika.
“Wewe ni Fabiani, mwanajeshi wa kitengo cha Malibu kama sikosei, na mwenye mafunzo ya Taichi, sivyo?” alizungumza yule kiongozi wa magaidi.
“Sikutarajia gaidi kama wewe kunifahamu. Ukikubali kujisalimisha na kutueleza nani kahusika katika shambulizi hili, ninakuhakikishia hutokufa,” alisema Afande Fabi.
“Haha, unajidanganya! Nipo tayari kufa kwa silaha yako na sio kujisalimisha,” aliongea yule kiongozi, na palepale kwa spidi ya hali ya juu, alimsogelea Afande Fabi kama vile hakujali kujeruhiwa na ile silaha tena.
Fabi aliishia kutoa tabasamu la kejeli na kisha aligonganisha silaha yake kwenye reli, na kuifanya itoe mlio wa ajabu. Palepale, alifyatuka na sarakasi ya mzunguko na kumsogelea yule gaidi kiongozi akiwa ameelekeza silaha yake kumlenga.
Yule gaidi alionekana pia kutegemea mbinu yake, na kwa ustadi wa hali ya juu kabisa, alifanikiwa kuidaka ile silaha kwa nguvu. Kitendo kile kilimfanya Afande Fabi kushituka, akiwa haamini kama bwana yule alikuwa na ujasiri wa kushikilia silaha yake. Damu nyingi zilianza kutoka katika mikono ya yule gaidi kutokana na kukatwa na ile silaha, lakini hakuiachia, zaidi ya kung'ata meno yake kwa nguvu akivumilia maumivu.
Dakika ileile, alizunguka kwa ustadi wa hali ya juu, huku nguvu nyingi za nishati ya mbingu na ardhi zikiibuka katika mwili wake.
“Shi**! Unajaribu kujilipua!!” Aliongea Afande Fabi baada ya kuelewa nini ambacho gaidi yule alikuwa anajaribu kufanya. Alikuwa akitumia mbinu maalum ya kukandamiza nguvu zake za mbingu na ardhi ili kujigeuza kama bomu na kulipuka. Lakini kitendo cha kuishikilia ile silaha yake wakiwa wamesogeleana, Fabi alijua kabisa kwamba bwana yule hakutaka kufa peke yake; alitaka kulipuka karibu yake ili na yeye apate madhara.
“Afande Fabi, tunakwenda kufa pamoja,” aliongea kwa nguvu huku akicheka.
Gaidi yule alijua fika kwamba hakuwa na uwezo wa kushindana na Afande Fabi, hivyo mbinu pekee iliyobaki ilikuwa kujilipua.
“Usidhani unaweza kunidhuru,” aliongea Afande Fabi, na palepale aliachia ile silaha yake, kisha akaruka sarakasi na kurudi nyuma. Kabla hajatua chini, alikusanya nguvu zote za nishati ya mbingu na ardhi na kutengeneza wimbi kubwa la upepo lililoambatana na matone ya maji.
Sekunde hiyo hiyo, wakati akifanikisha hilo, yule jambazi alipasuka kana kwamba ndani ya mwili wake kulikuwa na bomu, na kilichoweza kuonekana ni nyama kusambaa pamoja na damu.
Ijapokuwa Afande Fabi aliweza kuzuia asipatwe na madhara kutokana na mlipuko ule, hakuweza kuhimili presha yake na alirushwa kurudishwa nyuma kwa mita kadhaa.
“Kapteni!!”
Wanajeshi wenzake waliita kwa nguvu na kumsogelea wakidhani amepata majeraha, maana haukuwa mlipuko wa kawaida.
“Kapteni Fabi, uko sawa?”
Waliuliza kwa wasiwasi. Afande Fabi aliweza kusimama kutoka kwenye kichaka cha majani na kisha alitema damu nyingi chini, na kufanya meno yake kuwa mekundu. Palepale, aliwapa ishara wenzake kwamba alikuwa sawa.
“Nimepata majeraha ya ndani kiasi, lakini huyu jambazi hana uwezo mkubwa wa kunisababishia matatizo makubwa,” alisema.
“Tulitarajia kuna uwezekano wa kutokea shambulizi, lakini sio kama hivi,” alisema mwanajeshi aliyekuwa amevalia shati la mikono mirefu.
“Ni kweli kabisa, na sikutegemea pia watakuwa na mtaalamu wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.”
“Kapteni, unadhani ni kundi gani hili la kigaidi?”
“Kwasasa ni ngumu kujua maana wote wamepoteza maisha, lakini kwa ukubwa wa tukio hili, uchunguzi lazima utatoa majibu,” alisema, kisha akageukia wanajeshi wenzake.
“Mmejitahidi sana wanajeshi kwenye kudhibiti hawa magaidi. Kipaumbele chetu kwa sasa ni usalama wa Mzee Ndiswe na kutuliza abiria ili kuwatoa hapa kuwapeleka sehemu salama,” aliongea, na kundi hilo la wanajeshi lilipokea maagizo kwa utii na kisha wakajigawa.
Dakika chache mbele, kundi la wanajeshi lilimtoa mwanaume ambaye alionekana kuwa mtu mzima, makadirio ya miaka arobaini hadi hamsini. Alikuwa amevalia koti la rangi nyeusi na miwani yenye fremu za chuma.
“Kapteni, Mzee Ndiswe ana jeraha la mkono,” aliongea mmoja ya mwanajeshi.
“Nini!” Aliongea Fabi kwa tahamaki na alimsogelea yule mzee na kuanza kumkagua.
“Si niliwaambia mtu huyu ni muhimu na mnapaswa kumlinda kwa uwezo wenu wote.”
“Haina haja ya kuwafokea kapteni, hali ilikuwa tete kweli. Wanajeshi wawili waliokuwa wakinilinda walijitoa kafara kwa ajili yangu. Kwa mchango wao, sidhani haya majeraha yanaweza kulingana na walichofanya” aliongea Mzee Ndiswe.
“Mzee Ndiswe, hili swala ni kubwa na kama chochote kitakutokea, nitakosa majibu ya kutoa kwa wakubwa wangu. Hebu fanyeni upesi tutafute daktari wa kumtibu jeraha lake,” aliongea, na wote waliitikia.
Kapteni Fabi, palepale aliweka silaha yake kwenye kiuno na kuanza kupiga hatua kusogelea mabehewa, lakini alishangaa baada ya kuona mengi hayakuwa na abiria.
Misheni yao ilikuwa ni kumlinda Mzee Ndiswe kwa uwezo wao wote, na ndio maana hawakuweka umakini kwenye usalama wa abiria.
"Kapteni, nasikia kuna mtu ambaye amewaokoa tayari, majeruhi pia wametolewa na kupelekwa upande ule," alisema mwanajeshi mmoja, na kumfanya Kapteni Fabi kushangaa.
"Oh! Kwa hali ilivyokuwa patashika, nani alipata ujasiri wa kuokoa watu?" Aliuliza huku akiongoza timu yake kuelekea upande huo.
"Labda kulikuwa na daktari ndani ya treni."
"Ngoja tukaangalie kinachoendelea," aliongea huku wakiongeza mwendo.
Baada ya kufika upande mwingine, Afande Fabi na wenzake waligundua kulikuwa na zaidi ya majeruhi ishirini, na baadhi ya abiria walikuwa wakiwasaidia. Watu wote walionekana kuona eneo hilo ni salama maana abiria zaidi ya mia mbili walikuwa wamekaa na kusimama wakisubiri. Watu hao wote waliongozwa na Hamza mpaka kufika eneo hilo, na majeruhi aliwabeba yeye peke yake. Muda huo alikuwa bize mno kutoa huduma ya kwanza kwa wale ambao damu zilikuwa zikiwatoka.
"Jaribu kwanza kuzuia hiyo damu isiendelee kutoka kwa kushika hilo jeraha kwa nguvu. Kuna risasi ndani ya paja lake na hatuwezi kuitoa hapa hapa mpaka apelekwe hospitalini ndio waitoe," aliongea Hamza akimwambia mwanamke aliyemshikilia mume wake aliyejeruhiwa mguu wake na risasi.
"Kaka mkubwa, wewe ni daktari?" Aliuliza Afande Fabi, na kumfanya Hamza kuinua macho yake na kumwangalia anayemuuliza, na aligundua ni yule bwana aliyeonekana kuwa na uwezo wa hali ya juu wa kupigana.
"Kama mmemaliza kupambana na magaidi, mbona mmesimama badala ya kuita msaada?"Aliuliza akiwa siriasi huku akiendelea kuwatibu wagonjwa.
"Wewe, hiyo ni tabia gani? Kapteni anauliza swali, wewe hutaki kujibu?" Aliongea mwanajeshi aliyekuwa pembeni yake, lakini Afande Fabi alimzuia asiendelee kuongea.
"Atakuwa hatujui, maana tumevaa mavazi ya kiraia. Mkubwa, sisi ni wanajeshi kutoka kitengo cha Malibu kikosi cha kupambana na ugaidi. Nadhani hujawahi kutusikia, ila kwa sasa tupo kwenye misheni ya kumlinda mwanasayansi muhimu sana kwa taifa, na amepatwa na majeraha madogo ya mkono. Kama wewe ni daktari, tafadhali tunakuomba ukamwangalie," aliongea.
"Kikosi cha Malibu cha kuzupambana na ugaidi?" Hamza alijiuliza kwa akili yake na palepale aliona ndio maana bwana huyo alionekana kuwa na uwezo usio wa kawaida wa kutumia sanaa ya hali ya juu ya kupigana. Kutokana na sheria, mara nyingi wanajeshi wa kitengo cha Malibu hawajulikani licha ya kuwa ndani ya jeshi. Wanajeshi kama Afande Himidu na wenzake walikuwa wanakitengo wanaoonekana, lakini haikumaanisha ndio wanajeshi wote. Ilikuwa ni kama ilivyo kwa usalama wa taifa kutotambulika, na wanajeshi hao, ukiachana na kujifunza mbinu za ziada kama mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, wote walikuwa wanajeshi ambao walishafikia levo ya ukomandoo.
Hamza alikuwa akiyajua hayo yote, lakini kwake hakujali kama walikuwa makomandoo au wana uwezo wa nishati za mwili.
"Majeraha gani kapata?" Aliuliza Hamza.
"Alikatwa na silaha ya gaidi kwenye mkono wake."
"Jeraha lake dogo sana huyo. Kamsaidieni tu kuzuia damu na atakuwa sawa. Kuna watu wanahitaji msaada wa haraka kuliko yeye hapa," aliongea Hamza, na kauli ile iliwakasirisha wanajeshi wale.
"Kwahiyo unalinganisha hadhi ya Mzee Ndiswe na hawa watu wa kawaida? Unashindwaje kujua nani ni muhimu kwanza?"
Haikueleweka sababu ni nini tokea kuanzishwa kwa kitengo cha Malibu, lakini asilimia kubwa ya wanajeshi wa kitengo hicho ni wale wanaotokea familia zinazojiweza, nyingi zikiwa za vigogo serikalini au za kijeshi. Hivyo mara nyingi wanakuwa na tabia za kubagua watu kimadaraja kulingana na hadhi zao.
Abiria waliokuwa hapo baada ya kusikia kauli yao walijikuta wakikosa kuridhika kabisa na kushikwa na hasira.
"Kwahiyo mnajiona kuwa wanajeshi ndio nini kiasi cha kudharau maisha ya watu wa kawaida?"
"Kweli kabisa huyo mnaemtaka akatibiwe ni binadamu kama sisi. Kwanini dokta amtibu yeye kwanza ilihali kuna wanaohitaji matibabu hapa? Kama alijiona ni bora sana, kwanini asafiri kwa usafiri wa umma?"
Abiria walianza kuwafokea wale wanajeshi, wakionyesha hadhi zao pia kwa kutokubali kudharauliwa.
Maneno yale yaliwafanya makomandoo wa jeshi la Malibu kushikwa na haya, na walitaka kutumia nguvu lakini Afande Fabi aliwazuia.
"Jamani ndugu abiria, naombeni mnisikilize. Wenzangu wana wasiwasi lakini wanatamani pia kuona kila mmoja wenu anapata matibabu na kuondoka ndani ya hili eneo salama salmini. Kilichowatokea leo pia ni makosa yetu kwa kutojiandaa na kuwasababishia matatizo, hivyo tunaomba radhi kwenu," aliongea Afande Fabi kwa dhati, na kufanya abiria hao kutulia.
"Dokta, naomba ukimaliza kutibu hawa majeruhi, ukamwangalie na Mzee Ndiswe," aliongea Afande.
"Mwambieni aje hapa, kwani si kaumia mkono tu na sio miguu?" aliongea Hamza, na muda ule aliwapotezea mara baada ya kuona abiria mwingine akisogezwa eneo hilo akiwa na majeraha makubwa na familia yake ilikuwa ikiomba msaada.
"Pumbavu, huyu dokta anajiamini nini mpaka kutudharau?"
"Anajiona shujaa ilihali kama sio sisi kuingilia hili sekeseke asingepata hata hiyo nafasi ya kutibu watu," walianza kuongea wao kwa wao.
Afande Fabi pia aliishia kukunja ndita akionyesha kutoridhishwa na tabia ya Hamza, lakini hakutaka kuongea kitu na badala yake alisogea upande ambao Hamza alipewa wito ili kuangalia kama kweli ni daktari maana kama hakuwa akiamini.
Muda ule, Hamza baada ya kusogea upande alioitwa, aligundua kati ya watu waliokuwa wamembeba majeruhi mmoja wao ni Regina, mke wake.
"Wife, unafanya nini hapa?" aliuliza Hamza akiwa na mshangao.
"Nimeona nisaidie kumbeba kumleta huku maana huyu mama asingeweza kumsaidia peke yake," aliongea Regina na Hamza alielewa.
"Okey, muwekeni chini nione hali yake," aliongea Hamza, na mara baada ya mwanaume yule kuwekwa chini alianza kuangalia mapigo yake ya moyo na kisha macho yake, na hakuridhika. Haraka sana alichana nguo aliyovaa na kisha akaweka mkono juu ya kifua chake na akaanza na kugonga gonga kama ngoma.
"Dokta, hali yake ipoje? Mume wangu nae amepigwa risasi?" aliuliza mwanamke wa makamo aliyekuwa pembeni.
"Hapana, hajapigwa risasi, ila inaonekana kuna shida kwenye mapafu yake," aliongea Hamza.
"Ni kweli, tunaelekea Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi, tokea juzi alikuwa akilalamika kupata shida ya kupumua."
"Ana tension hemopnrumothorax, natakiwa kumfanyia intubation haraka iwezekanavyo," aliongea Hamza, lakini hakuna aliyemwelewa ila Regina alielewa.
"Unamfanyiaje bila bomba?" aliuliza huku akiwa amekunja sura kwa wasiwasi, na Hamza palepale alisimama na kuongea kwa nguvu.
"Nani kati yenu ana karamu yenye bomba au kitu chochote chenye bomba?" aliongea, na palepale mwanaume aliyeonekana kama mwajiriwa alichomoa karamu kwenye mfuko wake wa shati na kusogea mbele.
"Hii itafaa?" aliuliza, na Hamza alitingisha kichwa na kuichukua haraka haraka na kuifungua na kutoa bomba la wino. Kisha palepale alipapasa eneo la kifua kwa sekunde kadhaa na kwa nguvu kubwa alimkita yule mgonjwa na ile karamu.
"Arhhhhhhhhh!!"
Watu walioshuhudia kitendo kile walipiga makelele kwa nguvu, hata Regina aliyekuwa karibu alipigwa na mshituko.
Muda uleule baada ya lile bomba kuzama ndani ya kifua, maji mazito yaliyochanganyika na damu yalifyatuka kwenye ile karamu.
"Damu ni chafu mno hii, anapaswa kufanyiwa upasuaji haraka iwezekanavyo," aliongea Hamza.
"Dokta, mume wangu ataweza kupona? Naomba umsaidie tafadhali, tuna watoto wawili wadogo bado," aliongea yule mwanamke huku akianza kulia.
Hamza alishindwa kufanya chochote katika hali kama hiyo ambapo alikosa kabisa vifaa vya kufanyia upasuaji. Kwa ufupi, hakuwa katika hali ya kuweza kumsaidia mgonjwa huyo.
Lakini dakika hiyo hiyo, bahati ilikuwa upande wao kwani ngurumo ya helikopta kusogelea eneo hilo ilianza kusikika na kufanya abiria wote kuangalia angani.
Hamza ari yake ilirudi upya baada ya kuona msaada umeweza kufanikishwa mapema, hivyo haraka sana alisimama na kutoa maelekezo.
"Tutatumia hii helikopta kumpeleka mgonjwa kwenye hospitali yoyote iliyokaribu kwanza, muda wa kumuokoa upo," aliongea, na kisha palepale alimbeba yule mwanaume na kutembea kuelekea uelekeo wa ile helikopta.
Lakini muda huo, wale makomandoo walimzuia Hamza mbele.
"Samahani mkuu, ila hii helikopta imeletwa kwa ajili ya kumchukua Profesa kwenda sehemu salama. Ambulance itafika hapa muda si mrefu na kumchukua mgonjwa," aliongea, na kumfanya Hamza kushikwa na hasira muda uleule.
"Hivi mnashinda kwenye akili zenu? Huyo profesa wenu anashindwa vipi kusubiri ambulance kama kuna mtu anaehitaji msaada wa haraka?" aliongea Hamza.
"Ni kweli, kama ni magaidi wameshakufa na hali imekuwa salama, kwanini msiruhusu mgonjwa akachukuliwa na helikopta kuwahishwa hospitalini?" aliongea Regina.
"Sheria ni sheria, na tunapaswa kuzitii kulingana na maagizo. Umekataa kumtibu Mzee Ndiswe na sasa hivi unataka kutumia helikopta iliyokuja kwa ajili yake. Unajikuta nani?" Wanajeshi wale waliongea kwa kejeli.
Hamza aliishia kukunja sura na alijiambia kama asingekuwa amembeba mgonjwa, angeshawashia kichapo hao wanajeshi wote mpaka wafe.
Kitendo cha kudharau maisha ya mtu wa kawaida aliona hakikubaliki kabisa, ila hata hivyo hakutaka kuwalaumu wanajeshi kwao, kwani kufanikisha misheni ilikuwa ndio kipaumbele kwa ajili ya kupandishwa vyeo.
"Hebu mpisheni apite, ngoja dokta ampeleke kwanza mgonjwa hospitalini na mimi nitawajibika," sauti ya Afande Fabi ilisikika kutoka nyuma yao, na walimpisha apite mbele.
"Lakini Kapteni..."
"Unataka kusema nini? Inamaanisha unataka kukataa maelekezo yangu?" Aliongea kwa kukoroma, na wale wanajeshi waliishia kutingisha vichwa vyao kukataa.
Lakini dakika hiyo hiyo upande wa Regina, macho yalimtoka akiwa kama haamini.
"Kaka Fabiani!!" aliongea Regina kwa mshangao, na Fabi aliweka tabasamu baada ya kumwona Regina.
SEHEMU YA 130.
Afande Fabi alikuwa na tabasamu pana usoni huku akiwa amemuangalia Regina. Hakuonekana kushangaa uwepo wa Edina katika eneo hilo, kana kwamba alikuwa amemuona muda mrefu.
“Ndio, Regina, ni siku nyingi sana hatujaonana,” aliongea.
“Ni wewe kweli au nakufananisha! Hawa ni wanajeshi wako?” aliuliza Regina, na kauli yake ilimfanya Afande Fabi kucheka.
“Hapana, mimi ni kapteni, huwezi kusema hawa ni wanajeshi wangu.”
Furaha ya Hamza ilianza kupotea pale pale, hakuhitaji kalamu na daftari kujua mwanaume huyo ni nani. Ndiyo mkaka ambaye Regina alikuwa akimuongelea asubuhi, mwanaume ambaye alihusishwa kuwa na mahusiano na Regina wakiwa chuoni.
Kilichomkera Hamza ni namna ambavyo bwana huyo alikuwa akimwita Regina. Hakuonyesha hali ya kuwa na wasiwasi, pengine kwa Regina kuwa tajiri au mkurugenzi wa kampuni, bali alionyesha hali ya kuwa na ukaribu naye.
“Wife, tunaondoka wote kwenda hospitalini,” aliongea Hamza kwa nguvu makusudi tu.
“Sidhani kama kuna haja ya mimi kwenda,” aliongea Regina.
“Hakuna haja pia ya kuendelea kukaa hapa,” alijibu Hamza.
“Regina, kumbe umeshaolewa tayari na huyu daktari ndiyo mume wako!?” aliongea Afande Fabi.
Regina aliishia kushikwa na aibu kidogo za kike. Hakujua namna ya kumtambulisha Hamza; ilikuwa kama amekosa ujasiri na kutamani kusema Hamza ni msaidizi wake, lakini kwa sababu Hamza alishamwita mke, asingeweza kukataa.
“Ndio, ni cardiothoracic surgeon,” aliongea Regina akimaanisha ni daktari wa upasuaji wa moyo. Sio kama alidanganya; Eliza ndiye alimwambia Regina Hamza ni daktari wa maswala ya moyo.
“Umeolewa na mume mzuri, ameweza kuokoa watu wengi sana hapa,” aliongea na kumfanya Regina kutingisha kichwa kwa kujivunia. Siku hiyo ndiyo kwa mara ya kwanza alimuona Hamza ana upande wake mwingine wa kujivunia nao.
Hamza upande wake alikuwa na uso uliodhihirisha chuki kwenda kwa Fabi, huku akitamani kumwambia yule bwana haina haja ya kumsifia. Lakini hata hivyo, hakutaka kuonekana mtu wa kuchukulia siriasi mambo madogo, na muda huo akili yake yote alikuwa ameiweka kwa mgonjwa.
“Regina, tutaongozana wote kwenda hospitalini. Profesa, utaongozana na sisi pia ili jeraha lako likafanyiwe matibabu,” aliongea Afande Fabi.
Regina aliishia kukubali, isitoshe helikopta hiyo ilikuwa na nafasi ya kutosha ya yeye pia kupata nafasi.
“Asante sana, Afande Fabi. Kuokoa maisha ya mtu ni sawa na kusaidia familia nzima, ni muhimu sana,” aliongea Regina akimshukuru Fabi kwa kitendo cha kukubali yule mgonjwa kupelekwa hospitalini kupitia helikopta hiyo.
“Haha... huna haja ya kunishukuru, mimi ni mwanajeshi na ni wajibu wangu kulinda usalama na afya za raia,” aliongea.
Baada ya hapo, kundi hilo la watu wachache walipanda katika ndege hiyo na kupaa kuelekea hospitalini. Ndani ya chopa hiyo, Hamza aliweza kusikiliza mazungumzo ya Regina na Fabi, na alitamani kuziba masikio yake.
“Regina, hatujakutana kwa miaka mingi sana tangu tuachane. Umezidi kuwa mrembo kuliko ulivyokuwa mwanafunzi. Najikuta nakumbuka kipindi kile watu walivyokuwa wakituhusisha kuwa wapenzi,” aliongea Fabi.
“Kaka Fabi, sitaki hata kukumbuka. Ila vipi, ulikuwa muda wote jeshini tangu utoke chuo? Nasikia jeshini kuna hatari sana,” alijibu Regina.
“Sio sana. Ukweli ni kwamba nilikuwa nje kwenye mafunzo ya kikomandoo, na sasa nimerudi nchini. Iwe ni hatari kiasi gani, nipo tayari kulitumikia taifa langu.”
“Nikijilinganisha na nyie wanajeshi, najikuta kuwa mdogo mbele yenu,” aliongea Regina, akiona kwamba wanajeshi wana mchango mkubwa sana kwa taifa kuliko yeye mfanyabiashara.
“Regina, nataka kuchukua nafasi hii kukupogeza kuwa afisa mtendaji mkuu na mwenyekiti wa kampuni ya Dosam. Hongera sana. Matunda ya juhudi zako yanaonekana. Una familia na unazidi kuwa mrembo siku hadi siku. Najikuta kujutia sikuchukua hatua kipindi kile,” aliongea Fabi.
“Haha...” Regina alijikuta akicheka kwa utamu.
“Oya, niaje wewe? Si ukae kimya! Yaani mume wake amekaa hapa halafu unaendelea kumtania mke wangu,” aliongea Hamza, na kauli yake ilimfanya Regina kumjibu.
“Hamza, una nini wewe? Kaka Fabi anatania tu, huna haja ya kupaniki,” aliongea Regina. Hamza, baada ya kuona Regina anazidi kumtetea Fabi, alizidi kuchukia.
“Hivi kuna matani ya aina hiyo? Wewe hujamsikia anasema anajutia kutokukufukuzia wakati ukiwa chuoni?”
“Wewe umemuelewa tu vibaya. Unadhani Kaka Fabi ni mtu wa kukurupuka? Wakati tukiwa chuo, hakuwahi kuhusishwa na mwanamke yoyote. Wewe unaonaje tabia yake?”
“Hakuwa na mpenzi halafu unaona sawa? Alikuwa akifanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza uzushi wa kuhusishwa naye.”
“Utakuwa mgonjwa wewe, sio bure,” aliongea Regina huku akikunja sura. Aliona Hamza anafikiria mbali sana, isitoshe yeye mwenyewe sio Ua kwamba anaweza kuchanua kwa kumwagiliwa maji na yoyote.
“Mr. Hamza, huna haja ya kuwa na wasiwasi. Mimi Fabi ni mwanajeshi niliyekomaa kimaadili. Namtania tu kwa sababu hatujaonana muda mrefu.”
“Ukirudia kuongea na mke wangu kwa staili yako hiyo, usije kunilaumu nikikurusha nje ya ndege,” aliongea Hamza kwa ukali. Ndani ya moyo wake, kama sio kumheshimu Regina, angekuwa ashafanya hivyo muda mrefu.
Ishara ya kejeli ilionekana katika macho ya Fabi, akionekana kutomzingatia kabisa Hamza.
“Usiwaze, sitomtania tena mdogo wangu. Kuwa tu makini na mgonjwa.”
Hamza aliweza kuona hali ya dharau iliyoonekana katika uso wa bwana huyo.
“Naona unadhani nashindwa kukurusha nje ya hii chopa nikiamua. Unadhani siwezi?”
Afande Fabi aliishia kutoa tabasamu lake la kejeli vilevile, kisha akageukia upande wa nje, kama vile mtu ambaye hakutaka kujibishana na Hamza.
Upande wa Regina alikuwa na hofu kwamba Hamza anaweza kumrusha nje kweli. Maana aliona suala hilo ni dogo sana kuleta mtafaruku baina yao, hivyo aliingilia haraka kupoza hali.
“Hamza, naomba usiwe hivyo. Kwanini una hasira za haraka hivyo?”
“Unaongea na huyu bwana huku hujali uwepo wa mume wako hapa. Hivi umeona namna alivyoniangalia kwa dharau kama vile hanichukulii siriasi.”
“Hamza, nyamaza bwana. Ukiendelea nitakasirika, ujue,” aliongea Regina huku akihisi aibu kutokana na namna anavyomheshimu kaka yake Fabi. Aliamini haiwezekani kabisa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Fabi, kwa ufupi alimchukulia kama rafiki yake. Hivyo, kutokana na hisia hizo, alijikuta akijisikia vibaya na aibu kwa wakati mmoja.
“Regina, haina haja ya kugombana. Mimi ninachoamini ni kwamba mwanaume aliye komaa na anayejiamini uwezo wake wa kufikiria ni mkubwa. Hamza, haina haja ya kukuza mambo.”
“Kwahiyo unasema nina uwezo mdogo wa kufikiria? Hebu acha unafiki na sema unanidharau basi. Kwa kosa lenu la kutokuwa makini nimejikuta nikifanya majukumu ambayo sio yangu, ila unajaribu kunidharau. Kama sio uwepo wa raia, nisingejali chochote mnachofanya.”
“Ni vigumu kulinda raia wote kutopata majeraha wakati wa mapambano, lakini tumefanikiwa kuwadhibiti magaidi wote. Nakubali niliapaswa kuwajibika kwa usalama wa raia na kutowasababishia matatizo, na baadhi yao kufariki. Nikirudi, nitawajibika mbele ya wakuu wangu,” aliongea Fabi.
Regina mara baada ya kumsikia Afande Fabi akiongea maneno hayo ya uwajibikaji, alitingisha kichwa kuonyesha kukubaliana naye. Lakini Hamza hakuweza kujizuia tena. Ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na mtu anayejifanya kuwa muungwana ili kupata pointi mbele ya mke wake.
“Naona huna haja ya kwenda kuwajibika mbele ya wakuu wako, nitakuwajibisha sasa hivi,” aliongea Hamza huku akisogea kwa hasira akitaka kumtoa nje.
Kitendo kile kilimfanya Regina kupaniki na alimshika Hamza mkono kabla hajachukua hatua yoyote.
"Hamza, unataka kufanya nini? Umekuwa kichaa?" aliuliza kwa hofu.
"Haha... Regina, hakika mume wako anashangaza sana," aliongea Fabiani huku akiwa hana wasiwasi kabisa. Lakini muda huo huo, helikopta ilianza kushuka na rubani kutoa taarifa.
"Hamza tushafika tayari hospitalini. Acha ugomvi, muhimu hapa ni kumuokoa mgonjwa," aliongea Regina kwa kubembeleza.
Hamza aliishia kumwangalia mgonjwa aliyeonekana kuwa katika hali mbaya na kuona kuwa hana haja ya kuendelea na msimamo wake. Isitoshe, uwezekano wa kutokutana tena na bwana huyo mwenye dharau ulikuwa mdogo. Hakutaka kugusa mwanajeshi wa kitengo cha Malibu na kujitafutia matatizo kwa dharau zake.
Baada ya kushuka, mgonjwa alichukuliwa haraka na kuingizwa ndani ya hospitali.
Hamza alimwangalia Afande Fabi kwa sekunde kadhaa, kisha akamsogelea Regina.
“Wife, tuondoke na kaa mbali na huyu mtu,” aliongea Hamza, na Regina aliona kuwa siku hiyo Hamza alikuwa paranoid sana.
"Hamza, acha kuruhusu mawazo yako kufikiria vitu visivyo sawa. Hebu nenda kamuokoe mgonjwa," aliongea Regina kwa sauti ya utulivu.
"Dokta, naomba ukamsaidie mgonjwa wangu, uhai wake unakutegemea wewe," aliongea yule mama, akiwa na imani kuwa Hamza ni daktari bingwa.
Hamza, mara baada ya kuona hali ya kuomba kutoka kwa mama huyo, alikimbilia ndani ya hospitali hiyo. Hakukuwa na uhakika kama hospitali hiyo ilikuwa na madaktari wenye uwezo wa kumsaidia mgonjwa.
Afande Fabi, baada ya kuona Hamza ameondoka, alimgeukia mwanajeshi aliyekuja naye na kumpa maagizo.
"Mchukue profesa, jeraha lake likatibiwe. Nina kazi nyingine muhimu kufanya. Kumbuka, baada ya kupatiwa huduma, mchukue na ukutane na
wenzako wengine. Wapeni maagizo kuhakikisha usalama wake mpaka anafika mahali husika."
Mara baada ya kupokea maagizo hayo, mwanajeshi huyo alimchukua Profesa na kumuingiza ndani ya hospitali kwa ajili ya kutibiwa.
Muda huo, aligeuka na kumuona Regina akiingia ndani ya hospitali, na alimsogea na kumsimamisha.
"Regina, ni ngumu sana kukutana na wewe. Unaonaje tukiongea kidogo?"
"Lakini si upo bize," aliongea Regina.
"Haha... Ndiyo, lakini sasa hivi nimepata muda. Ukweli ni kwamba mpaka sasa Profesa tayari yupo salama, maana wale magaidi tushawaua," aliongea, na kumfanya Regina kunja sura kiasi, akionekana kufikiria.
"Tunaweza kuongea hata ndani ya hospitali wakati tukiendelea kusubiri kujua hali ya mgonjwa."
"Unataka kumuona mume wako akifanya upasuaji?" aliuliza, na Regina alitingisha kichwa kukubali.
"Nimesikia ni daktari mbobevu kwenye maswala ya upasuaji, lakini sijawahi kumuona akifanya upasuaji. Nataka kumuona leo."
"Oh, kumbe! Mmekuwa pamoja kwa muda gani, maana ni kama ndio unajua ni daktari kweli?"
"Sio muda mrefu sana, kama miezi hivi," aliongea Regina, na kumfanya Afande Fabi kumwangalia kwa sekunde chache, kisha akatingisha kichwa kumwelewa.
"Kama ni hivyo, basi ngoja nikusindikize. Kwa jinsi alivyokoa watu wengi kwenye treni, naamini uwezo wake sio mdogo."
Regina alihisi kuwa kuna kitu hakipo sawa kuhusu Fabi, lakini aliishia kukubali na kuongozana naye.
Upande wa idara ya wagonjwa wa dharura, watoa huduma walikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa kutokana na hali ya mgonjwa. Hali hiyo ilisababisha kutojali vigezo vya Hamza kama daktari. Baada ya kujitambulisha tu kuwa alikuwa daktari, hakuna hata aliyeomba kuona leseni yake. Manesi na mtaalamu wa ganzi walikusanyika katika hospitali hiyo ya mkoa wa Morogoro.
Picha za CT scan zilifanywa haraka, na Hamza, mara baada ya kuziangalia, aliweza kugundua shida ya mgonjwa. Lakini kwa bahati mbaya, chumba cha upasuaji kilikuwa kikitumika muda huo, na kutokana na hali ya mgonjwa ambayo haikupaswa kucheleweshwa, ilibidi Hamza atoe maagizo kwamba atafanya upasuaji wa dharura katika eneo hilo hilo.
Muda mchache baadaye, Afande Fabi alitoka nje na kisha akarudi akiwa na kinywaji, akampatia Regina. Lakini mwanamke huyo hakuwa na hamu kabisa ya kunywa chochote.
Kutokana na ubize wa watoa huduma hao wa hospitalini walivyokuwa wakitoka kwa kukimbia na kurudi, aliona hali haikuwa ya kawaida hata kidogo. Mara baada ya kugundua Hamza anaenda kufanya upasuaji nje ya chumba maalumu, aliona ni kitu ambacho hakiwezekani.
"Hivi upasuaji unaweza kufanyika hata nje ya chumba maalumu cha upasuaji?" aliuliza kwa hofu.
"Kutokana na mazingira na hali ya mgonjwa, jibu ni ndio. Isitoshe, hii sio hospitali kubwa, kwa hiyo kwa ajili ya kumuokoa mgonjwa, Hamza hana namna. Anaweza kufanya popote," aliongea, na kumfanya Regina kuzidiwa na wasiwasi, huku bila ya kujijua akianza kuomba mgonjwa apone na asifie mikononi mwa Hamza.
Mtoto wa kike, jasho la mikono lilianza kumtoka, kana kwamba hakuwa akiamini Hamza ni daktari.
ITAENDELEA. watsapp me 0687151346
Unajua chenye hua tuna waza ila hamna ngori buddy all in all big up,hata nisemeje ila kiukwel utunzi wako ni wa kimataifa kwa kweli.SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

Mkuu mbna kama unanishawishi niisome hii simulizi.Unajua chenye hua tuna waza ila hamna ngori buddy all in all big up,hata nisemeje ila kiukwel utunzi wako ni wa kimataifa kwa kweli.
Ni balaa hii story bro sikufichi, shida singarno anapenda kuichelewesha kweli ila ni mkali kwa maadhui,mtuririko nk. Tungo zake hakuna mahali inaboesha labda huko kuchelewesha ana chelewesha, Bora uwe umeamua kuilewa basi burudani na haki Yako....Mkuu mbna kama unanishawishi niisome hii simulizi.
Simulizi gani nyingine nzuri niisome ...nina muda sijaingia JFNi balaa hii story bro sikufichi, shida singarno anapenda kuichelewesha kweli ila ni mkali kwa maadhui,mtuririko nk. Tungo zake hakuna mahali inaboesha labda huko kuchelewesha ana chelewesha, Bora uwe umeamua kuilewa basi burudani na haki Yako....
Soma SINSimulizi gani nyingine nzuri niisome ...nina muda sijaingia JF
Ngoja niichekiSoma SIN