Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Wakuu ukiachana na hii simulizi ..ni simulizi gani nyingine kali nina mwaka mzima sikua na simu
 
tuwalaumu AZAMU..najua jamaa bdo anaugulia maumivu...akipoa atarudi2...but we are waiting 4 you bro..
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTUNZI:SINGANOJR

SEHEMU YA 127.

Joto la Moyo

Inawezakawa Regina hajaanza kumpenda Hamza kwa kiasi kikubwa,lakini siku zote kwa mwanamke anapenda kuungwa mkono na mwanaume ambae anamvutia , hivyo ilikuwa sawa tu kwa Regina kukasirika kwa kitendo cha kuanza kumsifia Yulia mbele yake ilihali ndio aliemuweka katika hali hio, Regina alikuwa akimchukulia Yulia kama mshindani wake namba moja ndio maana kitendo cha kushindwa katika dili ilimpa mawazo sana mpaka kuanza kunywa kilevi na kumpelekea kulewa.

Hamza mara baada ya kuona namna ambavyo Regina amekasirika kwa kitendo cha kumsifia Yulia aliishia kucheka na kuendelea kumkoroga Regina.

“Mwanzoni sikuwa nikijua maana nilijua mwanamke Genius kama wewe huwezi kufanya makosa kizembe na utafanikiwa kwa kila uwekezajhi kwa asilimia mia moja , nilikuona kama mwanamke ambae likija swala la biashara unaweza kushinda kila aina ya vita”Aliongea Hamza.

“Ushawahi kusikia duniani kuna mtu amabe hajawahi kufeli au kwasababu nina IQ ya 180 unaona ninaweza kufanikiwa katika kila kitu?”Aliongea Regina

“Nilikuchukulia unaweza kufanya kila kitu na huwezi kukubali mtu kama Yulia kukushinda , isitoshe tokea nijiunge na kampuni kila mtu anasema wewe ni mfanyabiashara mwenye akili kubwa , hivyo ni sawa tu kwa mimi kutodhania unaweza kufanya kosa kama hili. Mwisho wa siku unaonekana binadamu tu ambae huwezi kufanya kila kitu mwenyewe”Aliongea Hamza huku akicheka.

“Nilishindwa kwasababu ya kutokuwa makini ..”Aliongea na kisha alifuta machozi ambayo yalianza kumtoka muda mrefu na kisha akamwangalia Hamza.

“Najua wapi nilikosea mpaka nikashndwa , nipe nafasi nyingine nakuhakikishia sitomruhusu Yulia kukwapua madili yangu tena , najua kila mtu anaweza kufanya makosa na sisi binadamu sio wakamilifu siku zote,kuna muda nitafeli na kuna muda nitashinda vilevile , lakini hii ni mara yangu ya kwanza na ya mwisho kushindwa na Yulia, au wewe unadhani Yulia hakuwahi kufeli kwenye biashara?. Wakati anarudi mara ya kwanza na kupewa uongozi alishindwa mara kibao na wafanyabiashara wengine, halafu unaniambia siwezi kumshinda, kama kuna waliomuweza kwanini mimi nishindwe?”Aliongea Regina , japo sauti yake ilikuwa ya chini lakini ilikuwa imebeba usiriasi wa hali ya juu pamoja na hasira kwa Hamza.

“Kama humuwezi maana yake huwezi kushinda mbele yake, hivyo acha kujaribu kujidanganya”Aliongea Hamza na kauli hio ilimfanya Regina hasira alizokuwa nazo kuzidi kuongezeka.

“Wewe..! Wewe mjinga unajua nini wewe , unaongea ujinga tu na niondokee mbele yangu , nakuchukia sana Hamza”Aliongea kwa kufoka.

“Ndio naondoka maana nishachoka kuvumilia hasira zako zisizokuwa na msingi, nimekuleta huku kwa ajili ya kukufariji lakini unadharau ninachokwambia, kama unataka niondoke naondoka , ila usije kulaumu tu maana naenda kwa Yulia”Aliongea Hamza na kisha aligeuka akitaka kuondoka.

Regina mara baada ya kusikia Hamza anapanga kwenda kwa Yulia moyo wake ulishituka , alishindwa kujizuia na kuhisi hasira na kupaniki kwa wakati mmoja , alijikuta akihisi kumchukia Hamza mpaka meno yake yanaanza kumuwasha.

“Hamza! Ole wako , ukienda kwa Yulia ndio mwisho wetu mimi na wewe”Aliongea kwa nguvu lakini Hamza alijifanyisha kutomsikia kabisa na kitendo kile kilimkasirisha Regina zaidi kiasi cha kumrushia chupa ya Wine aliokuwa ameshikilia mkononi kwa nguvu zake zote.

Ila Hamza ni kama alijua Regina angefanya hivyo kwani alisogea pembeni na ikapita.

Regina mara baada ya kuona hivyo macho yake yalimtoka na hasira kali iliimlipuka katika moyo wake na hakujali tena chochote kile kwani alitoka nduki kumkimbilia Hamza.

Hakujua hata nguvu kaitoa wapi lakini aliweza kumfikia ndani ya sekunde kadhaa tu na kuanza kumpiga vibao na ngumi za mgongoni kwa hasira.

“Wewe mshenzi , muongo muongo leo utanitambua , lazima nikuue, huwezi kunichokoza makusudi nikuache tu”Alijikuta akimpiga mpaka akaishia kuchoka na kuinama chini,kama mtoto machozi yalikuwa karibu mno.

“Wewe Hamza sio wa kuniambia vile mimi … nimehuzunika ndio amenishinda kwasababnu ya kutokuwa kwangu makini lakini kwanini..”Aliongea huku machozi yakidondokea kwenye mchanga wa fukwe huku akilia kwa kwikwi.

Hamza palepale aligeuka na kumkumbatia kwa nguvu huko mkono mmoja akishikilia mgongo wake , hakuishia pale tu aliinama na kuanza kum’kiss’ mdomoni.

Regina ambae alikuwa akilia alikuja kushituka akiwa tayari ashapigwa denda(French kiss).

Ni machozi pekee yalioishia kupeperushwa na upepo huku pua yake ikiwa imegusana na ya Hamza.

Joto alilopata kutokana na kumbatio pamoja na busu hilo nyevu ilimfanya mwili wake wote ni kama unayeyuka, alijihisi ni kama vile alikuwa ndani ya nyumba na sio nje tena.

Hisia hasi zilikuwa nyingi mno na yale yaliomtokea siku nzima pamoja na kulewa alijikuta akimkumbatia Hamza mgongoni na kufumba macho yake, hakutaka kujali chochote tena , alichohitaji ni tulizo.

Baada ya kama dakika sita kupita Hamza alimwachia na alipeleka mkono wake kwenye mashavu yake na kumfuta machozi na kushika vimashavu vyake.

“Sumu yote ishakutoka sasa?”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.

Licha ya kwamba msichana huyo alikuwa slow sana kwenye swala la mahusiano, lakini alijua Hamza aliongea maneno yale sio kwasababu alikuwa akimaanisha bali alikuwa akimchokoza makusudi ili kutoa sumu yote iliokuwa ndani ya moyo wake.

Mbinu hio ya kinyume nyume ilimfanya kujihisi ni kama ametolewa kuzimu na kuingizwa peponi , alikubali kabisa kitendo cha kukasirishwa na Hamza na kumfanya kulia na kumpiga kwa nguvu ilifanya kutoa yale mawazo hasi yaliokuwa yamezigubika hisia zake ukijumlisha na French Kiss alilopewa alijikuta akiwa mwepesi mno , hakuwa katika mudi ya kufikiria tena kuhusu kufeli kwake katika biashara.

“Katika ulimwengu huu maisha ni muhimu zaidi kuliko kazi , usiruhusu mambo ya kupita kuindoa furaha yako”Aliongea Hamza huku akimshika nywele zake kwa kubembeleza kama mdoli.

Regina alijikuta akijisikia raha za ajabu na kufanya mwili wake kutetemeka akiwa katika kumbatio la mwanaume Hamza.

“Wewe unadhani kati yangu na Yulia nani ana uwezo zaidi?”Aliuliza kwa kudeka

“Yulia hawezi kufanana hata kidole na mke wangu”Aliongea Hamza.

“Shenzi .,. jibu kunyoosha maneno, mimi sikuamini wewe..”

“Nakuambia ukweli , nilichofanya kuongea vile ilikuwa ni kukuchokoza tu, Yulia hakuwezi namaanisha kabisa”Aliongea Hamza akiwa siriasi.

Wanawake ni viumbe ambao wanapenda kusikiliza maneno matamu yakiongelewa kuwalenga wao na si vinginevyo , hata kama yawe ni ya uongo yanawafanya kujisikia vizuri na Hamza alielewa kanuni hio vyema.

Hata Regina alijua Hamza alikuwa akiongea tu hivyo ili kumpeti peti lakini licha ya hivyo alijisikia vizuri.

“Muda si mrefu nitakuja kukuthibitishia Yulia hana uwezo kunizidi”

“Haha.. huna haja ya kufanya hivyo , Yulia yule ni mwanamke anaetegemea mgongo wa familia yake , peke yake hawezi kushindana kabisa na mke wangu”

“Upo sahihi , hata mimi najua anachotegemea ni familia yake tu ndio maana akanishinda”

“Umeona eh!Tumpotezee kabisa”Aliongea Hamza.

“Halafu sitaki kuja kukuona kabisa ukiwa na Yulia , ikija kutokea mna mahusiano yasioeleweka , mimi na wewe tunaachana kila mtu ajue yake”Aliongea Regina akiwa siriasi.

Hamza alijikuta akishindwa kutoa jibu la moja kwa moja kutokana na wasiwasi , lakini kutokana na namna Regina alivyokuwa siriasi aliishia kukubali.

“Usiwe na wasiwasi , mimi na Yulia haiwezi kutokea kitu”

Hamza alijiambia kwasababu Yulia ana ugonjwa wa akili wa kutokuweza kumpenda mtu , haitokuja kutokea mapenzi baina yao zaidi ya kutumiana tu, hivyo hakuwa na wasiwasi kukubaliana na Regina na kuamini atafanikisha hilo.

Regina mara baada ya kusikia Hamza akiongea hivyo mudi yake ilirudi kawaida.

“Turudi sasa hotelini”Aliongea na kumfanya Hamza kusita kidogo na kuangalia upande wa hotelini.

“Nataka nikatafute tafune angalau nyama alizosema zinapatikana pale”

“Nyama saa hizi?Unahisi njaa?”

“Sijala chakula cha usiku ndio maana”

“Kwanini?”

“Baada ya kuja huku niliishia kukusubiri muda mrefu hotelini na ndio nikaja kukutafuta”

Mara baada ya kusikia maneno hayo aliishia kushikwa na joto la moyo na hali ya hatia kwa wakati mmoja.

“Umenisubiri kwa muda gani?”

“Kama masaa mawili hivi ..,niliishia kunywa mvinyo kidogo tu”Aliongea na Regina aliringisha kichwa kumwelewa.

“Basi twende wote pale ukale , mimi sina njaa nitakuangalia tu”Aliongea na Hamza hakukataa na waliongozana kurudi ndani ya hoteli kwa ajili ya kuagiza nyama choma.

Ukweli hakuwa na hamu ya kula , lakini mara baada ya kutua mzigo wa kumtuliza Regina hatimae njaa ndio ilianza kumsumbua.

Waliagiza na kutokana Regina kunywa mvinyo mwingi hakugusa kabisa nyama wala chips ambazo Hamza alinunua.

Baada ya kumaliza walirudi hotelini na ilr kufika nje ya mlango Hamza swali lilimjia palepale.

“Wife , vipi nichukue chumba kingine?”Aliuliza Hamza.

“Haina haja , kuna hadi vitanda viwili humu ndani.. kama unahisi watu kuzusha habari zetu hata usiwe na wasiwasi maana ni swala la muda tu kujulikana tuna mahusiano”Aliongea Regina na Hamza baada ya kusikia hivyo moto uliwaka kwenye moyo wake.

“Regina kwahio unamaanisha umekubali kunitambua kama mume wako ki ukweli ukweli?”Aliuliza lakini Regina hakutaka kumfanya Hamza kuvimba.

“Usifikire mbali , kwanza bado sijasahau ulivyonidanganya bila aibu , nataka kwanza kuona mienendo yako ndio nitaamua”

“Kama ni hivyo usiwe na wasiwasi kabisa , napanga kuboresha mienendo yangu inyooke”Aliongea Hamza na palepale alikimbilia boksi la donati alizokuja nazo na kumuonyesha Regina.

“Angalia nilikununulia hizi na nimetoka nazo Dar mpaka huku Mwanza kwa ajili tu ya kuombea msamaha”Aliongea huku akizifungua ili kumtamanisha.

Regina mara baada ya kuona Donati hizo zilivyopakwa Strawberry macho yake yalichanua , lakini aliishia kugusa tumbo lake na kuona lilikuwa limevimba sana kutokana na kujaa maji.

“Tumbo langu halipo vizuri , natamani kuzila lakini siwezi..”

“Onja tu hata moja au nusu yake”Aliongea Hamza na Regina alishindwa kuizuia hamu yake na palepale alipelekea mkono na kutoa moja na kung’ata huku akiwa amekaa kitandani.

Hamza aliishia kumwangalia Regina namna alivyoshikiilia Donati hio na kuishia kutoa tabasamu kwani Regina alionekana kama mtoto kabisa mwenye mwili mkubwa , ilileta hamasa kwani pengine sio kawaida kwa mwanamke tajiri kuridhishwa na bidhaa ya jero.

“Mbona unaniangalia na unatabasamu au nachekesha?”

“Hamna tu , ila umejichafua usoni ?’

“Wapi?”Aliongea Regina na kupeleka mkono wake usoni lakini aliishia kujichafua zaidi.

“Ngoja usijiguse”Aliongea Hamza na kisha aliinama na kumfuta Regina kwenye uso kwa mkono, kitendo hicho kilimfanya Regina kuinua macho yake juu na walijikuta wakiangaliana kwa juu na chini , hisia za ajabu zilianza kusambaa katika miili yao zikianzia kichwani na kusambaa kwenye mti wa mgono na kwenda kushitua viungo vya uzazi.

Hamza aliishia kumeza mate mengi, hakujua kwanini lakini moyo wake ulidunda kwa kasi mno , macho ya Regina yalikuwa ni kama yanataka kuchomoka kutokana na ukubwa wake , alikuwa amevalia lenzi za macho na kufanya yanga’ae kama nyota kutokana na kuakisi mwanga.

Kope za macho yake , pua na lipsi zake zilimfanya Hamza utosi wa kichwa chake kumuwasha kutokana na uzuri wake.

Regina upande wake hakuwahi kuuangalia uso wa Hamza kwa namna ya kuuchunguza na aliweza kugundua muda huo Hamza alionekana kuwa handsome mno , aliona Hamza katika mazingira ya mwanga hafifu alikuwa akivutia sana, masikini asichokijua alikuwa ni mwanamke ambae moyo wake umependa.

Hali ya hewa haikuwa ya kawaida kabisa , japo chumba kilikuwa na AC ya kustahimili kiwango cha joto kinachoendana na miili yao lakini ni kama joto limeongezeka.

“Wife.!”

“Hmm!?”

“Nataka nikukiss”

“….”

Regina hakujibu na Hamza pia hakuhitaji jibu kwani tayari ashamsogelea na kuanza kudendeka.

Donati iliokuwa kwenye mikono ya Regina ilidondoka chini na kuchafua kapeti , lakini mrembo huyo hakujua kabisa , ijapokuwa ilikuwa ni mara yake ya pili kubusiwa ndani ya siku moja , Regina hakujua namna ya kurudisha , aliishia kushikilia blanketi kwa mikono yake yote huku moyo wake ukidunda haraka mno, lakini ni muda uleule tumbo lilifanya yake.

Sekunde ambayo Hamza mwili wake ulishindwwa kuvumilia kuishia kwenye Kiss pekee na kutaka kumlaza Regina kitandani , Regina alijisikia kichefu chefu cha aina yake.

“Ughh..”

Kutokana na kunywa sana mvinyo kwa kuchanganya mweupe na mwekundu machafuko yaliotokea tumboni baada ya kukaa chini ni kama mgonjwa wa Malaria, kitendo cha kuongezea ile Donati iliojaa Cream ndio iliharibu kabisa.

Hamza kutokana na namna ambavyo alimkaribia na Regina na mawazo yake kuwa upande mwingine , ilikuwa ngumu kukwepa matapishi na kitu pekee alichoweza kufanya ni kudondoka chini kabla hajatapikiwa usoni.

Hamza aliishia kummwangalia Regina akitapika mfululizo kiasi cha kusababisha hali ya hewa kubadilika.

Alitapika kwa zaidi ya nusu dakika akitoa kila kitu kilichokuwa ndani ya tumbo lake na hatimae kusimama na kufuta midomo yake , uso wake ulifubaa lakini alikuwa na hali ya ahueni.

“Duuh.. hatimae najisikia vizuri sasa”

Sekunde ambayo anaongea hivyo ndio aligundua kulikuwa na mwanaume pembeni yake aliekuwa akimkiss na alijikuta akihamaki kwa kuziba mdomo.

“Aah!”

Regina alijikuta akimaka huku akiwa na uso wa kumuonea huruma Hamza , alijikuta akishikwa na aibu na kutamani kuingia uvunguni.

“I am sorry! sikutarajia , vipi uko sawa?”

Hamza hakujua atoe kilio ama acheke , ilikuwa ni mara yake ya kwanza kwenye maisha yake ya kwanza kuonja matapishi ya mwanamke mrembo.

“Wife kusema ukweli hili busu la leo ni la aina yake”Aliongea Hamza

“Nani kakuambia usijiandae , mimi nilijisikia vibaya ghafla sana lakini wewe ukawa unaning’ang’ania tu kunikiss”Aliongea Regina huku akiangalia namna alivyochafua chumba.

“Kesho wafanyakazi wakija kusafisha nitaibika mno”

“Nini cha kukuaibisha sasa , au kama vipi wakija waambie mimi ndio nimetapika”Aliongea na kauli hio ilimfanya Regina macho yake kuchanua.

“Upo sahihi , wakija nawaambia wewe ndio umetapika , tena nawaambia sasa hivi waje, usije tu kubadilika”Aliongea kwa kuamrisha.

Hamza aliishia kukakamaa mwili na kujiambia haikuwa tu kulishwa matapishi na sasa hivi anakwenda kubeba lawama pia.

“Inaonekana ndoa muda mwingine ina faida zake kama hivi tunafichiana aibu”Aliongea Regina huku akicheka na kukimbilia bafuni kusafisha kusafisha kinywa.

Kuona tabasamu hilo adimu na tamu lililoambatana na kicheko mwili ulimsisimka na kujiambia sio yeye tu wanaume wote watachukua maamuzi magumu kama ya kwake tu na pengine na ziada.

Baada ya hoteli kuona kile kilichotokea , kilichofanyika walibadilishiwa chumba kingine hadhi hio hio , lakini awamu hio Hamza alipewa chumba chake na hakupata nafasi tena ya kuendelea kubebika na Regina.

Hamza mara baada ya kumaliza kuoga alirudi kitandani na kulaza kichwa chake huku akianza kuangalia juu ya dari kwa namna ya kufikriia , moyo wake muda ule ulijihisi ni kama umekuwa mtupu, hususani alivyoanza kufikiria tabasamu la Regina , alitamani kwenda ndani ya chumba cha mwanamke huyo na kumlazimisha kufanya mapenzi lakini asingeweza kufanya hivyo na kitu pekee alichoweza kuona ni kwamba Regina anahitaji muda wa kupenda taratibu taratibu mpaka afe na kuoza juu yake na ndio atapata wasaa wakulala nae.

Hamza alijiambia hakika ni mara yake ya kwanza kutumia muda mrefu kwa ajili tu ya kumfanya mwanamke kumpenda.

Lakini dakika ileile Hamza wakati akijiandaa kuzima taa ili alale zake , simu yake ilitoa mlio wa ujumbe wa meseji kuingia na alivyoangalia umetokea upande wa Watsapp , haraka haraka alifungua na kuangalia na kugundua alietuma alikuwa ni Regina alikuwa akimtankia usiku mwema na kumfanya Hamza kutamani kuruka ruka , ilikuwa mara ya kwanza kwa Regina kufanya hivyo ndio maana ilimletea furaha.

Hamza alichokifanya ni kurudisha ujumbe ule akimtakia usiku mwema pia na kuongezea na emoji ya Kiss.

Lakini kwa bahati mbaya ujumbe ule haikujulikana Regina alikuwa amelala au vipi , ulionekana kumfikia lakini haukujibiwa , Hamza alisubiri kwa zaidi ya nusu saa kuona ujumbe wake kama utajibiwa lakini hakukuwa na majibu na aliishia kulala zake tu.

Siku iliofuata Hamza ndio aliekuwa wa kwanza kwenda kumuamsha Regina kwa ajili ya kifungua kinywa.

Mrembo huyo alionekana kuwa katika hali yake ya kawaida na alikuwa ashavaa tayari na alitoka akiwa na ari mpya na kwenda kukaa upande unaongaliana na bahari kwa ajili ya kifungua kinywa.

Regina alikuwa kimya , hakuzungumzia kabisa kilichokuwa kimetokea jana yake , ilikuwa ni kama vile amegeuka na kurudi katika hadhi yake ya u’CEO.

Hamza aligudua Regina jana kujiachia ilikuwa ni kwasababu ya pombe na sio vinginevyo , Regina ambae alionekana kuwa na akili yake timamu alikuwa akitia hata hofu kumsogelea.

Baada ya kifungua kinywa walipanga kurudi , Regina alitaka kupanda ndege lakini Hamza alimwambia wapande Treni ya mwendokasi na Regina hakuwa na pingamizi, hakuwahi kupanda treni hio tokea izinduliwe ndio maana alikubali bila kinyongo.

Upande wa Yonesi na wenzake waliondoka na treni ya asubuhi kurejea Dar es salaam , baada ya Regina kumchukua Regina jana hawakuona sababu ya kuendelea na kazi yao ya ulinzi kwa kuamini Hamza peke yake anatosha kabisa.

Wakati wakiwa njiani kuelekea stesheni , Hamza alikosa kabisa mada ya kumuongelesha Regina na ilibakia hali ya ukimya baina yao mpaka wanafika kituoni.

Regina alikuwa maarufu na kwa wafanyakazi wa eneo h ilo ni kama wamefunzwa kutambua watu maarufu na matajiri, kwani alipokelewa kwa heshima na wahudumu na kuongozwa kwenda upande wa kusubiria treni eneo la VIP na kuketi kwenye masofa , mhudumu alimwelezea huduma zinazopatikana hapo na kumfanya Regina kutabasamu baada ya kuona wahudumu hao ni kama walikuwa wakimsuburia kumhudumia siku hio.

“Unataka kunywa nini , wanasema kuna huduma hadi ya vinywaji hapa?”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kutoa tabasamu baada ya kuona Regina ndio alienzisha maongezi.

“Kinywaji hapana”Aliongea Hamza.

“Mimi ninahisi kiu?”

“Ngoja nikuagizie basi, unatamani nini?”

“Natamani kahawa”Aliongea Regina huku akiangalia bango la Starbuck.

Katika kipindi kirefu kampuni ya Starbuck ilifanya shughuli zake katika mabara ya Asia , Ulaya , Australia na America , lakini baada ya kutofanya vizuri sokoni waliamua kuwekeza katika soko la Afrika kwa wingi katika maeneo ya vituo vya usafiri , ikiwemo kwenye viwanja vya ndege na katika Treni za mwendokasi kama hivyo.

“Ngoja nikuchukulie basi”Aliongea

“Subiri kidogo”Regina alimzuia Hamza na kisha alitoa simu yake ya Smartphone na kumpatia Hamza.

“Tiketi yangu inaonyesha hapa naweza kupata huduma za bure kwanzia vinywaji vyote vinavyopatikana eneo la kusubiria , tumia hii, pia nichukulie na Donati mbili kama zinapatikana zenye strawbery itakuwa vizuri”

“Na utajiri wote uliokuwa nao unataka huduma za bure?”

“Huna unalojua wewe, kwa mtu kama mimi huduma ya bure zina radha yake kuliko kununua kila siku”Aliongea na kumfanya Hamza kuona maisha ni kinyume nyume , mtu masikini anatamani kula kitu cha bei ghali kwa kuamini ndio chenye radha , lakini Regina kutokana na kula vitu vya ghali ashazoea na anaona vya bure vinaweza kuwa na radha nzuri zaidi.

Hamza hakutaka kujali sana aliishia kutoka na kwenda kutafuta alichoagizwa na alifanikiwa kupata kila kitu huku yeye mwenyewe akichukua kahawa pia huku akiwa ameongeza Donati mbili za ziada.

Regina mara baada ya kupokea oda yake kwa raha kama zote alikunywa na kula kwa kujiachia kutokana na eneo hilo la VIP halikuwa na watu kabisa.

“Hivi hizo donati ni tamu sana kiasi cha kufumba fumba macho?”Aliongea Hamza huku akitaka kuchukua moja atafune lakini Regina alisogeza pembeni.

“Kama unataka nenda kachukue zako sio hizi”Aliongea na kumfanya Hamza kukosa neno la kuongezea maana mtu alimwagiza mbili yeye akaleta za ziada lakini zimegeuka kuwa zake zote.

“Wife halafu kwa yaliotokea jana kwanini huongei chochote , ulivyokuwa kauzu ni kama hatujakiss jana?”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumwangalia na macho yake mazuri kwa namna ya kawaida.

“Unataka niongee nini?”

“Tatizo ni kama wewe wa jana ni tofauti na wa sasa hivi, kwa namna ulivyokauzu”

“Kwanini niwe tofauti , kwanza ukitofautisha na wakati tunakutana na sasa hivi nakujali huwezi kuniita kauzu”

“Upo sahihi , wakati tunakutana ulikuwa mkimya sana na hukuwa muongeaji, ulikuwa na ukauzu usiokuwa wa kawaida”

“Watu wote ambao hawajanizoea huwa wananiona hivyo , huwa sio kama nafanya makusudi kuwa kauzu , hata nilipokuwa nasoma wanafunzi ambao nilikuwa nao karibu walijua sikuwa kauzu ni hali yangu ya ukimya na haiba ya upole basi”

“Kuna wanafunzi uliokuwa umezoeana nao? Tofauti na Prisila sijawahi kusikia ukizungumiza watu uliosoma nao wala kukutana mara moja moja”

“Mwanzoni tulikuwa tunakutana mbona japo mara chache , lakini tokea siku nilivyopewa uongozi wa juu wa kampuni wengi wao walikuwa na wasiwasi sana kuwa karibu yangu na hawakuwa kama nilivyowazoea , baada ya hapo nilijikuta kuwa bize sana, kuna siku wanapiga na kutaka nijimuike nao lakini kutokana na utofauti wao nashindwa kwenda , baada ya hapo tukaanza kupotezeana taratibu taratibu”

“Wapo sahihi , watu kama hao unakuta ndio wengine wanahangaikia ajira wengine wanafanya kazi masaa nane kupata mshahara mdogo ,sasa kukaa meza moja na mkurugenzi wa kampuni kubwa ya kimataifa lazima wakose amani”

“Ndio maana niliamua kuwaelewa na siwalaumu kwa hilo na sikutaka kwenda , isitoshe wengi wetu mazingira tuliokulia ni tofauti na kufanya mizunguko yetu ya kijamii pia kuwa tofauti , ndio maana baada ya kuhitimu watu wengi hupotezeana pengine kusahauliana kabisa sio kwangu tu kwa watu wengi ipo hivyo”

“Kutokana na ukimya wako na namna ambavyo unaonekana kutopenda kuongea , uliwezaje kuwa na marafiki?”Aliuliza Hamza , alitamani kumjua zaidi Regina.

“Kwani kuna ugumu gani kuwa na marafiki? Wakati nikiwa mdogo walikuwa wakinifuata wenyewe , kulikuwa hadi na wanaume ambao walikuwa wakitaka kuniongelesha lakini sio kwa ajili ya urafiki ila kutaka niwe nao kimapenzi , kuhusu wasichana walitaka kuongea na mimi kutokana na wengi wao walitaka kuigilizia majibu yangu ikitokea assignment , wengine walikuwa wakiuliza kuhusu bei ya nilichovaa na mambo kibao”

“Walikuwa wakiigilizia , kwa ninavyokujuwa lazima ulikuwa bookwom mpaka kipindi hiko na kujua mambo mengi na kwa IQ yako ilivyokubwa nahisi ulikuwa unapata mia ya mia kila mtihani…”Aliongea Hamza na muda ule alikumbuka swali.

“Halafu hebu niambie wakati wako wa kusoma , ishawahi kutokea mwanaume ambae alikuwa akikughasi sana, ama je ushawahi kumpenda mwanaume yoyote?”

SEHEMU YA 128.

Upande mwingine asubuhi hio alionekana Kanali Dastani akiingia ndani ya ofisi yake kama kawaida na kitendo cha kuvua koti lake na kulining’iniza , mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na akaingia Amosi.

“Ulikuwa hapa kitengoni?”Aliuliza Kanali kwa namna ya kushangaa kidogo.

“Ndio , Mkurugenzi alinniita kwa ajili ya maswala ya kazi”

“Kazi gani?”Aliuliza.

“Kuna kazi gani tena , aliniulizia maendeleo ya uchunguzi yanavyoenda”Aliongea na kumfanya Kanali kutulia.

“Jana uliniambia unaenda kuonana na Dina , vipi amekupatia mzigo?”Aliuliza Amosi akiwa na shauku kubwa ya kusikia jibu.

“Mzigo nimeupata ndio”Aliongea na palepale alifungua mkoba wake na kumtolea Flash na kumpatia na kumfanya Amosi kutoa tabasamu.

“Nadhani unielezee kilichomo hupu ili tukajadili , nitaenda kuthibitisha baadae?”Aliongea na kumfanya Kanali kutao tabasamu hafifu kidogo na kukaa.

“Ni rekodi ambayo ina uzito wake , mwanzoni nilijua itanipa mwanga juu ya uelekeo wa kesi ya Sedekia lakini ni tofauti kabisa”

“Unamaanisha nini tofauti kabisa?”

“Inaonekana ni tofauti na ambavyo tumefikiria muda wote ,Chindezi hakufungwa kwasababu ya kumuua Sedekia, bali kaingizwa katika mfumo wa magereza ya Tanzania kwa ajili ya uchunguzi”Aliongea na kisha palepale alitoa fomu nyingine na kumpatia Amosi.

(Chindezi alikuwa ni Maddog mfungwa ambae alihusika na kifo cha Jongwe na kupigana na Hamza kwenye ulingo wa Nungungu)

Amosi alifungua fomu ile na kutoa nyaraka na kuanza kuzisoma haraka haraka na alijikuta akishangaa.

“Unataka kusema kapita katika haya magereza yote hapa ncini?”Aliuliza

“Ni kama inavyoonyesha , taarifa hio nimepata kwa shida sana”

“Kwanini iwe hivi?”

“Kuhusu hilo sijui , ila kuna mtu nimeongea nae kama ni taarifa ya kujua kwanini napaswa kuongea na Mstaafu Mgweno”Aliongea na kumfanya Amosi kukuna kichwa.

Ripoti hio ilionyesha Mad Dog alikuwa amefungwa katika magereza kumi na mbili hapa Tanzania na kulingana na siri za jeshi la polisi , magereza haya ni yale tu ambayo yalikuwa yakishikilia wafungwa wenye kesi za utata na watu maarufu.

“Nilijiuliza kwanini imetumika nguvu kubwa kutaka kuficha hii sauti , lakini kitu pekee ambacho nimegundua ni kwamba kilichokuwa kikifichwa ni huyu MadDog kulinda Cover yake , ila ni jasusi na kuna kitu ambacho alikuwa akitafuta hapa Tanzania , hakuna majibu sahihi kama amekipata au bado, ila ukifuatilia hayo maongezi kuna neno amelitamka ila sijaweza kulielewa mpaka sasa hivi kwani halipo katika lugha ya kawaida”

“Neno gani?”.

“Nashindwa kujua linavyotamkwa na kuandikwa kwasababu nimetumia akili mnemba kutafsiri mazungumzo yao , napanga baada ya hapa nikaonane na mtaalamu wa lugha labda anaweza kutupatia maana yake”Aliongea.

“Vipi kuhusu Sedekia! Amekueleza sababu ya kutupatia ile sauti?”Aliuliza Amosi.

“Dina yule mwanamke ni hatari sana , muda mrefu nilikuwa nikijiuliza kwanini kila kiongozi mkuu wa nchi hakugusa mtandao wa Chatu kabisa, ila anaonekana kumiliki siri nyingi sana ambazo pengine ni udhaifu kwa usalama wa taifa, anasema sauti ile aliikuta ni shememu ya kusanyiko la siri ambazo babu yake alimrithisha , kuhusu Sedekia kuwa hai ama kutokuwa hai anategemea majibu ya uchunguzi kutoka kwetu”Aliongea Kanali na kumfanya Amosi kufikiria.

“Unadhani inaleta mantiki?”

“Sijajua , lakini unadhani tunawezza kufanya nini zaidi ya kufanya uchunguzi zaidi na kufuata nyayo , lazima kuna sehemu tutapata uelekeo”Aliongea.

“Kama hisia zetu ni sahihi najikuta napatwa na shauku ya kutaka kujua kwanini Sedekia alipotea na kwanini akubali kudanganya kitengo na familia yake amefariki?”Aliongea na Kanali alimuunga mkono vilevile.

****

“Kwanini unaniuliza hivyo, unaona wivu?”Aliuliza Regina huku akimwangalia Hamza na mwonekano wa kejeli.

“Hamna.. ndio lazima nihisi wivu”Hamza alitaka kukataa lakini aliona kukubali sio tatizo pia na kukubali kwake kulimfanya Regina kujivunia.

“Wakati nasoma nilikuwa nikisafisha lo dawati langu kila siku la sivyo nisingeweza kuweka hata vitabu kutokana na wingi wa zawadi na vimemo”

“Mbona kama unazidisha sasa sifa wakati ulikuwa mtoto”

“Nani alikuwa mtoto! Haikuwa shule tu hata nilipokuwa chuo wanaume wengi walikuwa wakinifukuzia , wewe hujaona yale magari kule nyumbani yalivyokuwa mengi , yale yote wanaume waliniletea kama zawadi wakijaribu kunihonga na badala yake niliyapokea na kuwarudishia hela”Aliongea Regina na Hamza alikumbuka maana siku ya kwanza tu Shangazi alimuonyesha magari hayo.

“Kwahio uliwezaje kuwakataa wanaume wote , hakuna ambacho walifanya kukukasirisha?”Aliongea Hamza alitaka kumjua Regina vizuri ili asije kufanya ujinga na kumkasirisha.

“Hakuna walionisogelea, wengi walikuwa wapole sana , wakati nilipokuwa chuo kuna mkaka nilikuwa nipo nae karibu sana, alikuwa amenitangulia mwaka na alinijali sana , kuna muda aliwaambia watu mimi ni mpenzi wake ili wasinisumbue , mimi hata sikujali sana na waliona kweli labda sisi ni wapenzi lakini uhalisia hatukuwa na mahusiano , tulikuwa marafiki tu wa kawaida na nilikutana nae kwenye baraza la chuo, baadae alimaliza na nilisikia alikuwa ni mwanajeshi aliekuwa akijiendeleza kielimu na alirudishwa kambini”Aliongea Regina

“Kumbe ulikuwa na mkaka aliekuwa akikujali kabisa vyote hivyo , vipi ukimwangalia yeye na mimi nani ni handsome zaidi?”Aliongea Hamza akiwa na mwonekano wa kukunja sura kwa kumuonea wivu ‘mkaka’.

“Swali gani sasa hilo , halafu sio kwamba nilikuwa nae kwenye mahusiano kwanini nimlinganishe na wewe, hata kama nilikuwa nae kwenye mahusiano kuna haja ya kuuliza , mimi tu sijakuzuia kufanya unavyotaka na kila mwanamke anaekuvutia halafu unanizuia kutomkumbuka mkaka aliekuwa akinijali”

“Wife umenielewa vibaya , mimi nilikuwa nikiuliza tu”Aliongea Hamza huku akijiambia ni bahati huyo bwana anaeitwa ‘Mkaka’ alikuwa mwanajeshi na kuambiwa arudi jeshini mapema , la sivyo angemtembelea .

Hata kama hayakuwa mahusiano ya kimapenzi lakini skendo iliokuwepo kati ya Regina na yeye ilimfanya kukosa amani na kujiambia lazima huyo bwana alikuwa akiigiza tu kumvutia Regina.

“Vipi kuhusu wewe , nadhani ulitembea na wanawake wengi ulivyokuwa shuleni, kwa unavyoendeshwa na tamaa haiwezi kuwa tofauti”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kushika kidevu chake

“Shule gani unapozungumzia , chuo hapa Dar au nilikotoka?”Aliuliza

“Ulikotoka , ila hata Dar pia?”

“Ukweli nikwambie tu sijasoma kama ambavyo wanafunzi wa kawaida mnasoma”

“Unamaanisha nini?”

“Namaanisha sio elimu rasmi sana japo nimejifunza vingi, nilivyokuja ndio nikaona nisome elimu ya chuo ambayo ni rasmi, Wife unaonaje tukiongea kuhusu wewe kwanza , mimi nilijua ni ukauzu ndio maana watu wanashindwa kuwa marafiki zako”

“Wewe unanionaje kwani?, unadhani nakuwa kauzu tu masaa ishirini na nne, nina marafiki wengi akiwemo Prisila na wengine ambao baadhi yao wameolewa kabisa wako bize na maisha yao , wengine wapo nje ya nchi tunaishia kuwasiliana kwa njia ya mtandao , wewe unadhani sina marafiki?.Najaribu kuwa kauzu kazini kudumisha hadhi yangu pekee ndani ya kampuni , mimi ni mdogo kama nisipokuwa siriasi wengi watashindwa kunichukulia siriasi , unadhani mbele yako nakuwa kauzu ndio maana siongei , wewe ndio mwenyewe hujataka kuniongelesha unadhani mimi nitakuongelesha kitu gani , ninavyojua nyie wanaume ndio mnatakiwa kuanza kumuongelesha mwanamke na sio sisi”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kushangaa kidogo kwa kukosa neno.

Alijiuliza inamaana siku zote Regina kuonyesha ukauzu mbele y ake sio kama hakuwa akitaka kuongea nae bali alikuwa akisubiria yeye ndio aongee .

“Kwanzia sasa nitaanza mimi kukuongelesha”Aliongea Hamza huku akitabasamu kwa haya.

“Lakini Wife ni aina gani ya mada ambazo unapenda kuongelea zaidi?”Aliuliza Hamza.

Ijapokuwa walikuwa wamefahamiana kwa muda , Hamza hakuwahi kupata nafasi ya kuongea maswala binafsi na Regina .

Regina alionekana kushiba na aliishia kucheua kahawa iliomjaza tumbo na kushika tumbo lake bila wasiwasi , alikuwa huru mbele ya Hamza.

“Sijui hata ni mada gani maana mimi sio muongeaji sana, kwangu kuongea sana naona kama napoteza muda”

“Kama unaona ni kupoteza muda nitakuongelesha vipi sasa?, huku sijui hata mada unazopenda?”

“Wewe jaribu chochote tu, nikipenda utaona mwenyewe”Aliongea na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.

“Basi ngoja nikuulize swali?”

“Uliza”

“Kwanini umezaliwa na urembo kiasi hicho?”

“…”

Regina alijikuta akiganda akishindwa hata aongee nini , aliishia kugeuka pembeni huku akionyesha aibu za kike.

“Wewe mshenzi , sitaki kuongea na wewe kama hizo ndio mada”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka kwa aibu zake.

Palepale alijipa ujasiri na kisha alimshika Regina bega na kuegamiza kichwa chake kwenye bega lake , Regina mara baada ya kufanyiwa hivyo alijikuta akiwa mwekundu bila ya kupenda.

Hamza aliishia kujikubali mwenyewe kwa ujasiri wake na kwa jinsi walivyokuwa wakionekana hakukuwa na ubishi, walionekana kama ni wenza wanaopendana sana.

Lakini Regina alikaa vile kwa dakika chache tu na kisha alikaa vizuri

“Wife hutaki kuniegamia?”

“Shingo inauma?”Aliongea huku akiweka nywele zake vizuri.

Hamza aliishia kutabasamu na dakika ileile alitaka kuropoka na kusema mbona Eliza na Dina hawakuumia shingo lakini alizuia mdomo wake.

Baada ya kuongea kwa muda hatimae treni iliweza kufika na waliingia ndani.

Kwasababu walikuwa katika siti za VIP hawakupata shida kabisa kama siti ambayo Hamza alikaa wakati anakuja hapo Mwanza.

Mara baada ya Regina kukaa vizuri alitoa kitabu na kisha akaanza kusoma, vilikuwa ni vitabu vya mbinu za kibiashara zaidi kwa ajili ya kuongeza maarifa.

Hamza kwasababu hakutaka kumsumbua alitoa simu y ake na kuingia Watsapp na kisha alianza kusoma simulizi.

Regina mara baada ya kugeuza macho yake na kuona Hamza yupo bize kusoma alishikwa na shauku ya kutaka kujua anasoma nini.

“Unasoma nini?”

“Ni simulizi hii , nilianza nayo kwenye mtandao wa JamiiFroum na sasa naisomea Watsapp kwenye Group , mhusika wa hii simulizi ni kama mimi kabisa na mwanamke mhusika mkuu ni kama wewe , wakati naanza kuisoma ni kama huyu mwandishi anatuongelea sisi lakini imenivutia”Aliongea na kumfanya Regina kuinama na kuangalia.

“Inaitwa Niliemdhania kahaba mbona title ya kihuni hivyo ,Mwandishi ni nani?Oh naona hapo anaitwa SinganoJr , kama unavyosema ni kweli isije akawa ni Paparazzi anaetufuatilia na kuandika kuhusu maisha yetu , wewe huoni ni ngumu kuwa bahati mbaya”Aliongea Regina.

“Hata najali sasa , ndio mbinu yangu ya kupoteza muda hii , tatizo ni moja tu analeta mwendelezo taratibu sana , ningekuwa karibu yake ningempa kichapo akili imkae sawa awahishe mwendelezo”

“Umpige mtu kisa kachelewesha mwendelezo , unadhani kuandika ni rahisi , umekaa ki ukorofi ukorofi , sitaki kuongea na mkorofi mimi”Aliongea Regina huku akiendelea kusoma kitabnu chake.

“Hujawahi kuona watu wakorofi wewe , wakati nilipokuwa nje ya nchi , kulikuwa na wanawake ni wakorofi balaa, wanaweza kuja mbele yako na nguo zao fupi na kisha..”

Hamza aliishia kupiga mdomo wake kibao na kujiambia mdomo koma na kukaa zake vizuri akiendelea kusoma simulizi yake.

Baada ya nusu saa hivi Treni ilisimama makao makuu ya nchi na kushusha abiria na kisha iliendelea na safari.

Regina alikuwa ashaacha kusoma kitabu chake na kuishia kumwangalia Hamza aliekuwa bize na alitoa tabasamu hafifu na kujiambia licha ya Hamza kuwa na udhaifu wa kutofunga zipu yake ila alionekana mwanaume Simple sana anaejua kuwajibika.

Aliishia kuegamiza kichwa chake katika bega lake na kusinzia , Hamza aliekuwa bize mara baada ya kuhisi kitu kimemwagamia aligeuka na kuishia kupambwa na tabasamu.

Baada ya muda alimaliza kusoma maana simulizi haikuwa imefika mwisho na palepale alitumia muda huo kuangalia mazingira.

Hakuwa vizuri sana na ramani ya Tanzania lakini kwa umbali waliokuwa wametembea kutoka Dodoma alijua lazima wanakaribia Morogoro.

Sasa wakati wakiwa wametoka kwenye mji mdogo na kuingia kwenye msitu , zikiwa zimebakia dakika kadhaa kufika mjini kulingana na maelezo yalivyoonyesha ghafla tu treni hio iliokuwa kwenye spidi ilitingishika kwa nguvu na sekunde hio hio mlipuko mkubwa ulitokea kiasi cha kufanya kioo cha kulia kwao kupasuka.

Tukio lile lilimfanya Hamza kwa spidi zake zote kumkinga Regina asiumizwe na vioo vilivyosambaa na kumbeba juu juu kumtoa nje huku makelele ya watu yakiwa mengi.

“Kuna nini?”Aliuliza Regina aliekuwa katika hali ya mshituko mkubwa akiwa amedondoka chini na waliweza kuona kichwa cha treni kikiwa kimetoka kwenye reli.

“Ni mabomu haya, inaonekana sehemu hii kuna mabomu yametegwa”Aliongea na kumfanya Regina kushangaa.

“Ni kichaa gani anatega mabomu kwenye usafiri wa uma , hajui ni watu wangapi wanaweza kuathirika?Au ni mpango wa kuua watu?”Aliongea kwa kumaka.

“Hapana , hawajayatega kwa ajili ya kuua watu , kama ni hivyo wangetega mabomu mengi , walichokifanya ni kuzuia treni isiendelee kutembea ndio maana wamelipua kichwa chake”Aliongea Hamza na dakika hio hio mingurumo ya magari kusogelea eneo hilo ilisikikika kwa mbali yakitokea juu ya kimlima.

Hamza mara baada ya kusikiliza mlio wake tu hakutaka kutoka nje na kuyaangalia kwani alishajua ni magari ya aina gani na haraka sana alimbeba Regina na kwenda kumficha nyuma ya jiwe kuona nini kinaendelea.

ITAENDELEA USIKOSE
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTUNZI:SINGANOJR.

Imehaririwa na:ChatGpt

SEHEMU YA 128

Kaka Fabiani(Mkaka).

Kwa hali ilivyokuwa, ilionyesha dhahiri kabisa wahusika walikuwa wamejitega juu ya mlima na mara baada ya zoezi lao la kwanza kumalizika, walianza kushuka na magari yao.

"Wife, jifiche kwenye hili jiwe, usije ukatoka. Ngoja mimi nikaangalie kinachoendelea," aliongea Hamza.

"Usikurupuke, pengine kuna mabomu mengi zaidi," aliongea Regina kwa kuonya.

"Usiwe na wasiwasi, ukipatwa na tatizo piga kelele mara moja, ila usikimbie," aliongea Hamza na kisha, palepale, alitoka nduki kuelekea upande wa mabehewa ya nyuma ya treni.

Ukweli ni kwamba angeweza kuondoka na Regina bila ya kufanya chochote, lakini mara baada ya kuwaza, aliona kulikuwa na abiria wengi waliokuwa ndani ya treni na isingekuwa sawa kuondoka na kuwaacha.

Mara baada ya kufika upande wa kushoto wa treni hiyo, aliweza kuona watu wengi walikuwa wakitoka nje na kukimbia, lakini ni dakika ileile sauti za milio ya bunduki zilianza kusikika.

Zilikuwa zikitokea juu, zikishuka chini kwenye treni hiyo na kugonga kwenye mabehewa.

Muda huo, abiria ambao walikuwa ndani walijikuta wakishikwa na hofu huku wengi wao wakipiga makelele kutokana na milio hiyo. Hakuna ambaye alikuwa na ujasiri tena wa kutoka nje.

Dakika ile, Hamza aliweza k ugundua hayakuwa magari kama alivyokuwa amedhania, bali ni pikipiki za matairi manne zilizokuwa zimefungwa injini za jeep huku zikiwa na matairi makubwa na mbele yake zilikuwa zimeunganishwa na mtutu uliokuwa ukikohoa risasi.

Kundi la watu waliovalia kombati za jeshi ndilo lililokuwa likiziendesha huku wakisogelea treni hiyo kwa kasi kubwa.

Walikuwa wamefunga vitambaa vya rangi nyekundu kuzungusha kwenye mikono yao, na kombati zao pia hazikuwa na alama yoyote kuonyesha walikuwa jeshi gani.

"Kaeni ndani wote, mwenye kimbembe cha kutoka nje tutafumua kichwa chake," aliongea mwanaume mmoja aliyekuwa na mwili uliojaa misuli huku akiwa amejifunga bandanna usoni. Uzito wa sauti yake ulitosha kuwaogopesha watu na kuonyesha hakuwa na masihara hata kidogo.

"Namba nne, namba tano, nendeni mkamkamate," aliongea akitaja majina ya namba.

"Yes, Sir," walitikia kikakamavu, na palepale wanaume waliojivisha mavazi waliokuwa wameshikilia bunduki za AK-47 waliingia kibabe ndani ya behewa la daraja la kwanza ambapo Regina na Hamza walikuwepo mwanzo.

Hamza macho yake yalisinyaa palepale. Aligundua hawa watu walikuwa na mazoezi ya kawaida tu ya daraja la mwanzo kabisa kabla ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi, lakini bwana ambaye alionyesha kuwa ndiye kiongozi, yeye alikuwa katika daraja la nusu mzunguko katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.

Licha ya kwamba wenzake walionekana kutokuwa na levo ya juu, lakini nguvu zao hazikuwa za kawaida.

Cha kutisha zaidi ni kwamba walikuwa na silaha nzito walizoshikilia kwenye mikono yao, na aliona kama atakurupuka na kwenda kuwashambulia basi uwezekano wa abiria kuumia ni mkubwa sana. Lakini hata hivyo, alikuwa kwenye hali ya kujiuliza watu hao ni akina nani na wametokea wapi, na kwanini wamevamia treni hiyo.

Ilishangaza kwa sababu nchi kama Tanzania kiwango cha uhalifu kilikuwa chini sana na hiyo yote ni kutokana na ushirikiano mkubwa wa vyombo vya usalama kuanzia jeshi la kulinda nchi na jeshi la polisi. Sasa kitendo cha watu hao kuwa na magari ambayo wameyatengeza kuweza kutembea nje ya barabara lakini vilevile kuwa na silaha za moto ilishangaza, na kuna hisia zilimwambia pengine kuna wahusika ndani ya vyombo vya usalama waliohusika; la sivyo isingekuwa rahisi mpaka kutega mabomu.

Hamza aliishia kutokujua cha kufanya kwanza. Kwa walivyoonekana, ilionyesha kabisa kuna mtu ambaye walikuwa wakimtaka ndani ya treni hiyo, na alijiambia hapaswi kufanya chochote kwanza na anapaswa kusubiri angalau wamkamate wanaomtafuta ndio achukue hatua.

Lakini dakika ileile, kitendo cha wale wavamizi kuingia ndani ya treni hiyo, upande mwingine walitoka wanaume na wanawake waliovalia mavazi ya kawaida wakiwa wameshikilia bunduki na kuanza kushambuliana nao.

"Tututututututu, Thump, thump thump!"

Magaidiwale walionekana kutotarajia mashambulizi hayo na kujikuta wakizubaa na kuishia kupigwa risasi.

Hamza macho yake yalichanua kwa tukio hilo, na aliweza kugundua watu hao waliokuwa katika mavazi ya kiraia walikuwa ni wanajeshi wa uwezo wa juu kabisa.

"Tulitegemea tu kunaweza kuwa na shambulizi la kushitukiza. Vijana, ingieni wote na hakikisha hakuna anayepona na tunakamilisha misheni yetu," aliongea yule mwanaume kwa sauti ya amri, na palepale alishuka kutoka kwenye gari huku akiwatanguliza vijana wake mbele.

Dakika chache mbele, mirindimo ya risasi ilisikika kwa nguvu ndani ya mabehewa hayo, na kulikuwa na vilio vingi vya watu kutoka ndani. Ilionekana abiria walikuwa wakipata majeraha kutokana na patashika hiyo.

Hamza, mara baada ya kuona jambo hilo, alishikwa na hasira palepale na kujiuliza wanajeshi hao walikuwa wanafikiria nini. Aliona haikupaswa wajitokeze kwanza hadi wampate wanayemtafuta, na baada ya kumtoa nje, ndipo wachukue jukumu la kumuokoa badala ya kushambuliana katikati ya kundi la abiria. Lakini hakuna kilichoweza kufanyika kwa muda huo. Kitendo cha watu hao kuanza kushambuliana kilimaanisha kuwa hakuna tena kuangalia usalama wa raia; ilikuwa kama vita.

Ijapokuwa Hamza hakuwa na cheti cha udaktari, wazo ambalo lilimjia akilini muda huo lilikuwa kusaidia raia waliopatwa na majeraha. Hata kama alikosa leseni, aliona yeye ni daktari na anapaswa kufanya jambo.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa tete, Hamza alifyatuka na kuingia ndani ya treni hiyo ili aone namna ya kuzuia risasi zisipite kwenye behewa lililokuwa na abiria wengi. Lakini kabla hata hajachukua hatua, wanajeshi wengi waliovalia kiraia walitoka kwa wingi wakiwa wameshikilia bunduki.

Hamza, baada ya kuwaangalia tu, alijua hao walikuwa wana usalama ambao pia ni wanajeshi, kutokana na wengi wao kuwa katika mavazi ya suti. Sekunde chache mbele, alitoka mwanaume mwingine aliyekuwa amevalia koti la suti na suruali ya jeans, akiwa ameshikilia kitu kama fimbo, lakini kifaa kilichoonekana kama kisu kwa wakati mmoja.

Bwana yule hakujali risasi zilizokuwa zikirindima, bali alichomoka kwa spidi na ustadi wa hali ya juu kabisa, akawasogelea wale wavamizi na kuanza kuzungusha ile fimbo ya chuma. Sauti za kugongana kwa chuma zilianza kusikika huku wale magaidiwakidondoka chini kwa spidi kubwa wakiwa hawana uhai.

Hamza, mara baada ya kuona tukio lile, aliishia kukunja sura na kujiambia kwamba yule bwana hakuwa mwepesi. Mara baada ya kuona mtu yule alikuwa akipambana na yule bwana aliyekuwa amejifunga skafu ya rangi nyekundu, wawili wengine walijawa na ujasiri na kuanza kushambulia.

Yule bwana kiongozi wa kundi hilo la wavamizi alionekana kuwa mzuri pia kwenye mapigano, nguvu yake ya kurusha mashambulizi haikuwa ya kawaida, kwani iliambatana na nguvu za nishati za mbingu na ardhi. Lakini yule bwana aliyekuwa ameshikilia silaha ya usinga alikuwa akifanya mashambulizi yaliyo pendezesha macho kutokana na ustadi wake. Baada ya kukwepa mashambulizi mawili mfululizo, kisha akasogea kwa namna ya kuruka pembeni huku akirusha silaha yake akimlenga yule gaidishingoni.

Lakini kiongozi yule alikuwa na ustadi wa hali ya juu mno, kwani alipangua ile silaha kwa kutumia bunduki na kisha, bila kusubiri, alifanya shambulizi la mzunguko kwa kutumia nguvu bila nishati za mbingu na ardhi na kumpiga yule mwanajeshi.

“Wow!” Hamza alijikuta akivutiwa na namna mvamizi yule alivyorudisha shambulizi. Licha ya kwamba alikuwa jambazi, alifurahishwa na namna alivyotumia sanaa ya mapigano kwa ustadi mkubwa. Hamza aliangalia kidogo tu akitaka kujua wanatumia mbinu gani za kupambana, na aliweza kujua kila kitu kuhusu sanaa zao. Walionekana kuwa watu waliopitia mafunzo ya kijeshi, hususani katika mataifa ya Asia.

Hamza, mara baada ya kuona wanajeshi hao wanaweza kudili na hali hiyo bila kuingilia, aliamua kuingia kwenye behewa lingine lililokuwa na abiria waliokuwa wakitoa vilio vya maumivu kwa ajili ya kuwasaidia.

“Wasaidieni walioumia kuwatoa nje kwanza!” Aliongea Hamza kwa nguvu baada ya kufungua mlango, lakini licha ya kuongea hivyo, abiria waliishia kumwangalia tu kutokana na hofu waliokuwa nayo.

Hamza, mara baada ya kuona wapo katika hali hiyo, hakutaka kujali sana. Kwa haraka, alichukua waliokuwa na majeraha na kuwabeba, kisha kuwatoa nje nyuma ya mabehewa sehemu aliyoona kuna usalama. Alirudi na kufanya hivyo kwa kurudia rudia huku akitoa huduma ya kwanza kwa haraka.

Aliweza kupata boksi la huduma ya kwanza na alitumia bendeji na baadhi ya dawa kuwasidia watu ili damu zisizidi kuwatoka.

Regina, ambaye alikuwa amejificha katika kifusi cha jiwe, aliweza kumuona Hamza akiingia ndani ya treni akiwa amebeba watu na kurudi tena. Aligundua kwamba alikuwa akisaidia watu. Kwa kile ambacho Hamza alikuwa akifanya, Regina alionekana kuguswa. Alikumbuka jinsi alivyomdhania Hamza mwanzoni kama mtu ambaye anaweza kuua kikatili bila kujiuliza mara mbili, lakini tukio hilo la kuokoa watu lilimfanya kuona upande wake mwingine.

Muda huo, wanajeshi waliokuwa katika mavazi ya kiraia waliweza kutumia faida ya wao kuwa wengi na kuwadhibiti magaidimmoja baada ya mwingine, huku wengine wakikimbia kutaka kujiokoa, lakini waliishia kupigwa risasi za migongoni.

Yule bwana mwanajeshi aliyekuwa akitumia silaha ya usinga alikuwa mwepesi mno kwenye kushambulia na kuweka pambano. Alipambana na yule kiongozi wa magaidi, na mapambano yao yalionekana kuchukua muda mrefu, huku wakiendelea kupigana mpaka walipotoka nje kabisa. Hata hivyo, Fabi alifanikiwa kumjeruhi kiongozi yule kwa kumkata kata, hali iliyomfanya aonekane asiyetamanika.

“Wewe ni Fabiani, mwanajeshi wa kitengo cha Malibu kama sikosei, na mwenye mafunzo ya Taichi, sivyo?” alizungumza yule kiongozi wa magaidi.

“Sikutarajia gaidi kama wewe kunifahamu. Ukikubali kujisalimisha na kutueleza nani kahusika katika shambulizi hili, ninakuhakikishia hutokufa,” alisema Afande Fabi.

“Haha, unajidanganya! Nipo tayari kufa kwa silaha yako na sio kujisalimisha,” aliongea yule kiongozi, na palepale kwa spidi ya hali ya juu, alimsogelea Afande Fabi kama vile hakujali kujeruhiwa na ile silaha tena.

Fabi aliishia kutoa tabasamu la kejeli na kisha aligonganisha silaha yake kwenye reli, na kuifanya itoe mlio wa ajabu. Palepale, alifyatuka na sarakasi ya mzunguko na kumsogelea yule gaidi kiongozi akiwa ameelekeza silaha yake kumlenga.

Yule gaidi alionekana pia kutegemea mbinu yake, na kwa ustadi wa hali ya juu kabisa, alifanikiwa kuidaka ile silaha kwa nguvu. Kitendo kile kilimfanya Afande Fabi kushituka, akiwa haamini kama bwana yule alikuwa na ujasiri wa kushikilia silaha yake. Damu nyingi zilianza kutoka katika mikono ya yule gaidi kutokana na kukatwa na ile silaha, lakini hakuiachia, zaidi ya kung'ata meno yake kwa nguvu akivumilia maumivu.

Dakika ileile, alizunguka kwa ustadi wa hali ya juu, huku nguvu nyingi za nishati ya mbingu na ardhi zikiibuka katika mwili wake.

“Shi**! Unajaribu kujilipua!!” Aliongea Afande Fabi baada ya kuelewa nini ambacho gaidi yule alikuwa anajaribu kufanya. Alikuwa akitumia mbinu maalum ya kukandamiza nguvu zake za mbingu na ardhi ili kujigeuza kama bomu na kulipuka. Lakini kitendo cha kuishikilia ile silaha yake wakiwa wamesogeleana, Fabi alijua kabisa kwamba bwana yule hakutaka kufa peke yake; alitaka kulipuka karibu yake ili na yeye apate madhara.

“Afande Fabi, tunakwenda kufa pamoja,” aliongea kwa nguvu huku akicheka.

Gaidi yule alijua fika kwamba hakuwa na uwezo wa kushindana na Afande Fabi, hivyo mbinu pekee iliyobaki ilikuwa kujilipua.

“Usidhani unaweza kunidhuru,” aliongea Afande Fabi, na palepale aliachia ile silaha yake, kisha akaruka sarakasi na kurudi nyuma. Kabla hajatua chini, alikusanya nguvu zote za nishati ya mbingu na ardhi na kutengeneza wimbi kubwa la upepo lililoambatana na matone ya maji.

Sekunde hiyo hiyo, wakati akifanikisha hilo, yule jambazi alipasuka kana kwamba ndani ya mwili wake kulikuwa na bomu, na kilichoweza kuonekana ni nyama kusambaa pamoja na damu.

Ijapokuwa Afande Fabi aliweza kuzuia asipatwe na madhara kutokana na mlipuko ule, hakuweza kuhimili presha yake na alirushwa kurudishwa nyuma kwa mita kadhaa.

“Kapteni!!”

Wanajeshi wenzake waliita kwa nguvu na kumsogelea wakidhani amepata majeraha, maana haukuwa mlipuko wa kawaida.

“Kapteni Fabi, uko sawa?”

Waliuliza kwa wasiwasi. Afande Fabi aliweza kusimama kutoka kwenye kichaka cha majani na kisha alitema damu nyingi chini, na kufanya meno yake kuwa mekundu. Palepale, aliwapa ishara wenzake kwamba alikuwa sawa.

“Nimepata majeraha ya ndani kiasi, lakini huyu jambazi hana uwezo mkubwa wa kunisababishia matatizo makubwa,” alisema.

“Tulitarajia kuna uwezekano wa kutokea shambulizi, lakini sio kama hivi,” alisema mwanajeshi aliyekuwa amevalia shati la mikono mirefu.

“Ni kweli kabisa, na sikutegemea pia watakuwa na mtaalamu wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.”

“Kapteni, unadhani ni kundi gani hili la kigaidi?”

“Kwasasa ni ngumu kujua maana wote wamepoteza maisha, lakini kwa ukubwa wa tukio hili, uchunguzi lazima utatoa majibu,” alisema, kisha akageukia wanajeshi wenzake.

“Mmejitahidi sana wanajeshi kwenye kudhibiti hawa magaidi. Kipaumbele chetu kwa sasa ni usalama wa Mzee Ndiswe na kutuliza abiria ili kuwatoa hapa kuwapeleka sehemu salama,” aliongea, na kundi hilo la wanajeshi lilipokea maagizo kwa utii na kisha wakajigawa.

Dakika chache mbele, kundi la wanajeshi lilimtoa mwanaume ambaye alionekana kuwa mtu mzima, makadirio ya miaka arobaini hadi hamsini. Alikuwa amevalia koti la rangi nyeusi na miwani yenye fremu za chuma.

“Kapteni, Mzee Ndiswe ana jeraha la mkono,” aliongea mmoja ya mwanajeshi.

“Nini!” Aliongea Fabi kwa tahamaki na alimsogelea yule mzee na kuanza kumkagua.

“Si niliwaambia mtu huyu ni muhimu na mnapaswa kumlinda kwa uwezo wenu wote.”

“Haina haja ya kuwafokea kapteni, hali ilikuwa tete kweli. Wanajeshi wawili waliokuwa wakinilinda walijitoa kafara kwa ajili yangu. Kwa mchango wao, sidhani haya majeraha yanaweza kulingana na walichofanya” aliongea Mzee Ndiswe.

“Mzee Ndiswe, hili swala ni kubwa na kama chochote kitakutokea, nitakosa majibu ya kutoa kwa wakubwa wangu. Hebu fanyeni upesi tutafute daktari wa kumtibu jeraha lake,” aliongea, na wote waliitikia.

Kapteni Fabi, palepale aliweka silaha yake kwenye kiuno na kuanza kupiga hatua kusogelea mabehewa, lakini alishangaa baada ya kuona mengi hayakuwa na abiria.

Misheni yao ilikuwa ni kumlinda Mzee Ndiswe kwa uwezo wao wote, na ndio maana hawakuweka umakini kwenye usalama wa abiria.

"Kapteni, nasikia kuna mtu ambaye amewaokoa tayari, majeruhi pia wametolewa na kupelekwa upande ule," alisema mwanajeshi mmoja, na kumfanya Kapteni Fabi kushangaa.

"Oh! Kwa hali ilivyokuwa patashika, nani alipata ujasiri wa kuokoa watu?" Aliuliza huku akiongoza timu yake kuelekea upande huo.

"Labda kulikuwa na daktari ndani ya treni."

"Ngoja tukaangalie kinachoendelea," aliongea huku wakiongeza mwendo.

Baada ya kufika upande mwingine, Afande Fabi na wenzake waligundua kulikuwa na zaidi ya majeruhi ishirini, na baadhi ya abiria walikuwa wakiwasaidia. Watu wote walionekana kuona eneo hilo ni salama maana abiria zaidi ya mia mbili walikuwa wamekaa na kusimama wakisubiri. Watu hao wote waliongozwa na Hamza mpaka kufika eneo hilo, na majeruhi aliwabeba yeye peke yake. Muda huo alikuwa bize mno kutoa huduma ya kwanza kwa wale ambao damu zilikuwa zikiwatoka.

"Jaribu kwanza kuzuia hiyo damu isiendelee kutoka kwa kushika hilo jeraha kwa nguvu. Kuna risasi ndani ya paja lake na hatuwezi kuitoa hapa hapa mpaka apelekwe hospitalini ndio waitoe," aliongea Hamza akimwambia mwanamke aliyemshikilia mume wake aliyejeruhiwa mguu wake na risasi.

"Kaka mkubwa, wewe ni daktari?" Aliuliza Afande Fabi, na kumfanya Hamza kuinua macho yake na kumwangalia anayemuuliza, na aligundua ni yule bwana aliyeonekana kuwa na uwezo wa hali ya juu wa kupigana.

"Kama mmemaliza kupambana na magaidi, mbona mmesimama badala ya kuita msaada?"Aliuliza akiwa siriasi huku akiendelea kuwatibu wagonjwa.

"Wewe, hiyo ni tabia gani? Kapteni anauliza swali, wewe hutaki kujibu?" Aliongea mwanajeshi aliyekuwa pembeni yake, lakini Afande Fabi alimzuia asiendelee kuongea.

"Atakuwa hatujui, maana tumevaa mavazi ya kiraia. Mkubwa, sisi ni wanajeshi kutoka kitengo cha Malibu kikosi cha kupambana na ugaidi. Nadhani hujawahi kutusikia, ila kwa sasa tupo kwenye misheni ya kumlinda mwanasayansi muhimu sana kwa taifa, na amepatwa na majeraha madogo ya mkono. Kama wewe ni daktari, tafadhali tunakuomba ukamwangalie," aliongea.

"Kikosi cha Malibu cha kuzupambana na ugaidi?" Hamza alijiuliza kwa akili yake na palepale aliona ndio maana bwana huyo alionekana kuwa na uwezo usio wa kawaida wa kutumia sanaa ya hali ya juu ya kupigana. Kutokana na sheria, mara nyingi wanajeshi wa kitengo cha Malibu hawajulikani licha ya kuwa ndani ya jeshi. Wanajeshi kama Afande Himidu na wenzake walikuwa wanakitengo wanaoonekana, lakini haikumaanisha ndio wanajeshi wote. Ilikuwa ni kama ilivyo kwa usalama wa taifa kutotambulika, na wanajeshi hao, ukiachana na kujifunza mbinu za ziada kama mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, wote walikuwa wanajeshi ambao walishafikia levo ya ukomandoo.

Hamza alikuwa akiyajua hayo yote, lakini kwake hakujali kama walikuwa makomandoo au wana uwezo wa nishati za mwili.

"Majeraha gani kapata?" Aliuliza Hamza.

"Alikatwa na silaha ya gaidi kwenye mkono wake."

"Jeraha lake dogo sana huyo. Kamsaidieni tu kuzuia damu na atakuwa sawa. Kuna watu wanahitaji msaada wa haraka kuliko yeye hapa," aliongea Hamza, na kauli ile iliwakasirisha wanajeshi wale.

"Kwahiyo unalinganisha hadhi ya Mzee Ndiswe na hawa watu wa kawaida? Unashindwaje kujua nani ni muhimu kwanza?"

Haikueleweka sababu ni nini tokea kuanzishwa kwa kitengo cha Malibu, lakini asilimia kubwa ya wanajeshi wa kitengo hicho ni wale wanaotokea familia zinazojiweza, nyingi zikiwa za vigogo serikalini au za kijeshi. Hivyo mara nyingi wanakuwa na tabia za kubagua watu kimadaraja kulingana na hadhi zao.

Abiria waliokuwa hapo baada ya kusikia kauli yao walijikuta wakikosa kuridhika kabisa na kushikwa na hasira.

"Kwahiyo mnajiona kuwa wanajeshi ndio nini kiasi cha kudharau maisha ya watu wa kawaida?"

"Kweli kabisa huyo mnaemtaka akatibiwe ni binadamu kama sisi. Kwanini dokta amtibu yeye kwanza ilihali kuna wanaohitaji matibabu hapa? Kama alijiona ni bora sana, kwanini asafiri kwa usafiri wa umma?"

Abiria walianza kuwafokea wale wanajeshi, wakionyesha hadhi zao pia kwa kutokubali kudharauliwa.

Maneno yale yaliwafanya makomandoo wa jeshi la Malibu kushikwa na haya, na walitaka kutumia nguvu lakini Afande Fabi aliwazuia.

"Jamani ndugu abiria, naombeni mnisikilize. Wenzangu wana wasiwasi lakini wanatamani pia kuona kila mmoja wenu anapata matibabu na kuondoka ndani ya hili eneo salama salmini. Kilichowatokea leo pia ni makosa yetu kwa kutojiandaa na kuwasababishia matatizo, hivyo tunaomba radhi kwenu," aliongea Afande Fabi kwa dhati, na kufanya abiria hao kutulia.

"Dokta, naomba ukimaliza kutibu hawa majeruhi, ukamwangalie na Mzee Ndiswe," aliongea Afande.

"Mwambieni aje hapa, kwani si kaumia mkono tu na sio miguu?" aliongea Hamza, na muda ule aliwapotezea mara baada ya kuona abiria mwingine akisogezwa eneo hilo akiwa na majeraha makubwa na familia yake ilikuwa ikiomba msaada.

"Pumbavu, huyu dokta anajiamini nini mpaka kutudharau?"

"Anajiona shujaa ilihali kama sio sisi kuingilia hili sekeseke asingepata hata hiyo nafasi ya kutibu watu," walianza kuongea wao kwa wao.

Afande Fabi pia aliishia kukunja ndita akionyesha kutoridhishwa na tabia ya Hamza, lakini hakutaka kuongea kitu na badala yake alisogea upande ambao Hamza alipewa wito ili kuangalia kama kweli ni daktari maana kama hakuwa akiamini.

Muda ule, Hamza baada ya kusogea upande alioitwa, aligundua kati ya watu waliokuwa wamembeba majeruhi mmoja wao ni Regina, mke wake.

"Wife, unafanya nini hapa?" aliuliza Hamza akiwa na mshangao.

"Nimeona nisaidie kumbeba kumleta huku maana huyu mama asingeweza kumsaidia peke yake," aliongea Regina na Hamza alielewa.

"Okey, muwekeni chini nione hali yake," aliongea Hamza, na mara baada ya mwanaume yule kuwekwa chini alianza kuangalia mapigo yake ya moyo na kisha macho yake, na hakuridhika. Haraka sana alichana nguo aliyovaa na kisha akaweka mkono juu ya kifua chake na akaanza na kugonga gonga kama ngoma.

"Dokta, hali yake ipoje? Mume wangu nae amepigwa risasi?" aliuliza mwanamke wa makamo aliyekuwa pembeni.

"Hapana, hajapigwa risasi, ila inaonekana kuna shida kwenye mapafu yake," aliongea Hamza.

"Ni kweli, tunaelekea Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi, tokea juzi alikuwa akilalamika kupata shida ya kupumua."

"Ana tension hemopnrumothorax, natakiwa kumfanyia intubation haraka iwezekanavyo," aliongea Hamza, lakini hakuna aliyemwelewa ila Regina alielewa.

"Unamfanyiaje bila bomba?" aliuliza huku akiwa amekunja sura kwa wasiwasi, na Hamza palepale alisimama na kuongea kwa nguvu.

"Nani kati yenu ana karamu yenye bomba au kitu chochote chenye bomba?" aliongea, na palepale mwanaume aliyeonekana kama mwajiriwa alichomoa karamu kwenye mfuko wake wa shati na kusogea mbele.

"Hii itafaa?" aliuliza, na Hamza alitingisha kichwa na kuichukua haraka haraka na kuifungua na kutoa bomba la wino. Kisha palepale alipapasa eneo la kifua kwa sekunde kadhaa na kwa nguvu kubwa alimkita yule mgonjwa na ile karamu.

"Arhhhhhhhhh!!"

Watu walioshuhudia kitendo kile walipiga makelele kwa nguvu, hata Regina aliyekuwa karibu alipigwa na mshituko.

Muda uleule baada ya lile bomba kuzama ndani ya kifua, maji mazito yaliyochanganyika na damu yalifyatuka kwenye ile karamu.

"Damu ni chafu mno hii, anapaswa kufanyiwa upasuaji haraka iwezekanavyo," aliongea Hamza.

"Dokta, mume wangu ataweza kupona? Naomba umsaidie tafadhali, tuna watoto wawili wadogo bado," aliongea yule mwanamke huku akianza kulia.

Hamza alishindwa kufanya chochote katika hali kama hiyo ambapo alikosa kabisa vifaa vya kufanyia upasuaji. Kwa ufupi, hakuwa katika hali ya kuweza kumsaidia mgonjwa huyo.

Lakini dakika hiyo hiyo, bahati ilikuwa upande wao kwani ngurumo ya helikopta kusogelea eneo hilo ilianza kusikika na kufanya abiria wote kuangalia angani.

Hamza ari yake ilirudi upya baada ya kuona msaada umeweza kufanikishwa mapema, hivyo haraka sana alisimama na kutoa maelekezo.

"Tutatumia hii helikopta kumpeleka mgonjwa kwenye hospitali yoyote iliyokaribu kwanza, muda wa kumuokoa upo," aliongea, na kisha palepale alimbeba yule mwanaume na kutembea kuelekea uelekeo wa ile helikopta.

Lakini muda huo, wale makomandoo walimzuia Hamza mbele.

"Samahani mkuu, ila hii helikopta imeletwa kwa ajili ya kumchukua Profesa kwenda sehemu salama. Ambulance itafika hapa muda si mrefu na kumchukua mgonjwa," aliongea, na kumfanya Hamza kushikwa na hasira muda uleule.

"Hivi mnashinda kwenye akili zenu? Huyo profesa wenu anashindwa vipi kusubiri ambulance kama kuna mtu anaehitaji msaada wa haraka?" aliongea Hamza.

"Ni kweli, kama ni magaidi wameshakufa na hali imekuwa salama, kwanini msiruhusu mgonjwa akachukuliwa na helikopta kuwahishwa hospitalini?" aliongea Regina.

"Sheria ni sheria, na tunapaswa kuzitii kulingana na maagizo. Umekataa kumtibu Mzee Ndiswe na sasa hivi unataka kutumia helikopta iliyokuja kwa ajili yake. Unajikuta nani?" Wanajeshi wale waliongea kwa kejeli.

Hamza aliishia kukunja sura na alijiambia kama asingekuwa amembeba mgonjwa, angeshawashia kichapo hao wanajeshi wote mpaka wafe.

Kitendo cha kudharau maisha ya mtu wa kawaida aliona hakikubaliki kabisa, ila hata hivyo hakutaka kuwalaumu wanajeshi kwao, kwani kufanikisha misheni ilikuwa ndio kipaumbele kwa ajili ya kupandishwa vyeo.

"Hebu mpisheni apite, ngoja dokta ampeleke kwanza mgonjwa hospitalini na mimi nitawajibika," sauti ya Afande Fabi ilisikika kutoka nyuma yao, na walimpisha apite mbele.

"Lakini Kapteni..."

"Unataka kusema nini? Inamaanisha unataka kukataa maelekezo yangu?" Aliongea kwa kukoroma, na wale wanajeshi waliishia kutingisha vichwa vyao kukataa.

Lakini dakika hiyo hiyo upande wa Regina, macho yalimtoka akiwa kama haamini.

"Kaka Fabiani!!" aliongea Regina kwa mshangao, na Fabi aliweka tabasamu baada ya kumwona Regina.

SEHEMU YA 130.

Afande Fabi alikuwa na tabasamu pana usoni huku akiwa amemuangalia Regina. Hakuonekana kushangaa uwepo wa Edina katika eneo hilo, kana kwamba alikuwa amemuona muda mrefu.

“Ndio, Regina, ni siku nyingi sana hatujaonana,” aliongea.

“Ni wewe kweli au nakufananisha! Hawa ni wanajeshi wako?” aliuliza Regina, na kauli yake ilimfanya Afande Fabi kucheka.

“Hapana, mimi ni kapteni, huwezi kusema hawa ni wanajeshi wangu.”

Furaha ya Hamza ilianza kupotea pale pale, hakuhitaji kalamu na daftari kujua mwanaume huyo ni nani. Ndiyo mkaka ambaye Regina alikuwa akimuongelea asubuhi, mwanaume ambaye alihusishwa kuwa na mahusiano na Regina wakiwa chuoni.

Kilichomkera Hamza ni namna ambavyo bwana huyo alikuwa akimwita Regina. Hakuonyesha hali ya kuwa na wasiwasi, pengine kwa Regina kuwa tajiri au mkurugenzi wa kampuni, bali alionyesha hali ya kuwa na ukaribu naye.

“Wife, tunaondoka wote kwenda hospitalini,” aliongea Hamza kwa nguvu makusudi tu.

“Sidhani kama kuna haja ya mimi kwenda,” aliongea Regina.

“Hakuna haja pia ya kuendelea kukaa hapa,” alijibu Hamza.

“Regina, kumbe umeshaolewa tayari na huyu daktari ndiyo mume wako!?” aliongea Afande Fabi.

Regina aliishia kushikwa na aibu kidogo za kike. Hakujua namna ya kumtambulisha Hamza; ilikuwa kama amekosa ujasiri na kutamani kusema Hamza ni msaidizi wake, lakini kwa sababu Hamza alishamwita mke, asingeweza kukataa.

“Ndio, ni cardiothoracic surgeon,” aliongea Regina akimaanisha ni daktari wa upasuaji wa moyo. Sio kama alidanganya; Eliza ndiye alimwambia Regina Hamza ni daktari wa maswala ya moyo.

“Umeolewa na mume mzuri, ameweza kuokoa watu wengi sana hapa,” aliongea na kumfanya Regina kutingisha kichwa kwa kujivunia. Siku hiyo ndiyo kwa mara ya kwanza alimuona Hamza ana upande wake mwingine wa kujivunia nao.

Hamza upande wake alikuwa na uso uliodhihirisha chuki kwenda kwa Fabi, huku akitamani kumwambia yule bwana haina haja ya kumsifia. Lakini hata hivyo, hakutaka kuonekana mtu wa kuchukulia siriasi mambo madogo, na muda huo akili yake yote alikuwa ameiweka kwa mgonjwa.

“Regina, tutaongozana wote kwenda hospitalini. Profesa, utaongozana na sisi pia ili jeraha lako likafanyiwe matibabu,” aliongea Afande Fabi.

Regina aliishia kukubali, isitoshe helikopta hiyo ilikuwa na nafasi ya kutosha ya yeye pia kupata nafasi.

“Asante sana, Afande Fabi. Kuokoa maisha ya mtu ni sawa na kusaidia familia nzima, ni muhimu sana,” aliongea Regina akimshukuru Fabi kwa kitendo cha kukubali yule mgonjwa kupelekwa hospitalini kupitia helikopta hiyo.

“Haha... huna haja ya kunishukuru, mimi ni mwanajeshi na ni wajibu wangu kulinda usalama na afya za raia,” aliongea.

Baada ya hapo, kundi hilo la watu wachache walipanda katika ndege hiyo na kupaa kuelekea hospitalini. Ndani ya chopa hiyo, Hamza aliweza kusikiliza mazungumzo ya Regina na Fabi, na alitamani kuziba masikio yake.

“Regina, hatujakutana kwa miaka mingi sana tangu tuachane. Umezidi kuwa mrembo kuliko ulivyokuwa mwanafunzi. Najikuta nakumbuka kipindi kile watu walivyokuwa wakituhusisha kuwa wapenzi,” aliongea Fabi.

“Kaka Fabi, sitaki hata kukumbuka. Ila vipi, ulikuwa muda wote jeshini tangu utoke chuo? Nasikia jeshini kuna hatari sana,” alijibu Regina.

“Sio sana. Ukweli ni kwamba nilikuwa nje kwenye mafunzo ya kikomandoo, na sasa nimerudi nchini. Iwe ni hatari kiasi gani, nipo tayari kulitumikia taifa langu.”

“Nikijilinganisha na nyie wanajeshi, najikuta kuwa mdogo mbele yenu,” aliongea Regina, akiona kwamba wanajeshi wana mchango mkubwa sana kwa taifa kuliko yeye mfanyabiashara.

“Regina, nataka kuchukua nafasi hii kukupogeza kuwa afisa mtendaji mkuu na mwenyekiti wa kampuni ya Dosam. Hongera sana. Matunda ya juhudi zako yanaonekana. Una familia na unazidi kuwa mrembo siku hadi siku. Najikuta kujutia sikuchukua hatua kipindi kile,” aliongea Fabi.

“Haha...” Regina alijikuta akicheka kwa utamu.

“Oya, niaje wewe? Si ukae kimya! Yaani mume wake amekaa hapa halafu unaendelea kumtania mke wangu,” aliongea Hamza, na kauli yake ilimfanya Regina kumjibu.

“Hamza, una nini wewe? Kaka Fabi anatania tu, huna haja ya kupaniki,” aliongea Regina. Hamza, baada ya kuona Regina anazidi kumtetea Fabi, alizidi kuchukia.

“Hivi kuna matani ya aina hiyo? Wewe hujamsikia anasema anajutia kutokukufukuzia wakati ukiwa chuoni?”

“Wewe umemuelewa tu vibaya. Unadhani Kaka Fabi ni mtu wa kukurupuka? Wakati tukiwa chuo, hakuwahi kuhusishwa na mwanamke yoyote. Wewe unaonaje tabia yake?”

“Hakuwa na mpenzi halafu unaona sawa? Alikuwa akifanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza uzushi wa kuhusishwa naye.”

“Utakuwa mgonjwa wewe, sio bure,” aliongea Regina huku akikunja sura. Aliona Hamza anafikiria mbali sana, isitoshe yeye mwenyewe sio Ua kwamba anaweza kuchanua kwa kumwagiliwa maji na yoyote.

“Mr. Hamza, huna haja ya kuwa na wasiwasi. Mimi Fabi ni mwanajeshi niliyekomaa kimaadili. Namtania tu kwa sababu hatujaonana muda mrefu.”

“Ukirudia kuongea na mke wangu kwa staili yako hiyo, usije kunilaumu nikikurusha nje ya ndege,” aliongea Hamza kwa ukali. Ndani ya moyo wake, kama sio kumheshimu Regina, angekuwa ashafanya hivyo muda mrefu.

Ishara ya kejeli ilionekana katika macho ya Fabi, akionekana kutomzingatia kabisa Hamza.

“Usiwaze, sitomtania tena mdogo wangu. Kuwa tu makini na mgonjwa.”

Hamza aliweza kuona hali ya dharau iliyoonekana katika uso wa bwana huyo.

“Naona unadhani nashindwa kukurusha nje ya hii chopa nikiamua. Unadhani siwezi?”

Afande Fabi aliishia kutoa tabasamu lake la kejeli vilevile, kisha akageukia upande wa nje, kama vile mtu ambaye hakutaka kujibishana na Hamza.

Upande wa Regina alikuwa na hofu kwamba Hamza anaweza kumrusha nje kweli. Maana aliona suala hilo ni dogo sana kuleta mtafaruku baina yao, hivyo aliingilia haraka kupoza hali.

“Hamza, naomba usiwe hivyo. Kwanini una hasira za haraka hivyo?”

“Unaongea na huyu bwana huku hujali uwepo wa mume wako hapa. Hivi umeona namna alivyoniangalia kwa dharau kama vile hanichukulii siriasi.”

“Hamza, nyamaza bwana. Ukiendelea nitakasirika, ujue,” aliongea Regina huku akihisi aibu kutokana na namna anavyomheshimu kaka yake Fabi. Aliamini haiwezekani kabisa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Fabi, kwa ufupi alimchukulia kama rafiki yake. Hivyo, kutokana na hisia hizo, alijikuta akijisikia vibaya na aibu kwa wakati mmoja.

“Regina, haina haja ya kugombana. Mimi ninachoamini ni kwamba mwanaume aliye komaa na anayejiamini uwezo wake wa kufikiria ni mkubwa. Hamza, haina haja ya kukuza mambo.”

“Kwahiyo unasema nina uwezo mdogo wa kufikiria? Hebu acha unafiki na sema unanidharau basi. Kwa kosa lenu la kutokuwa makini nimejikuta nikifanya majukumu ambayo sio yangu, ila unajaribu kunidharau. Kama sio uwepo wa raia, nisingejali chochote mnachofanya.”

“Ni vigumu kulinda raia wote kutopata majeraha wakati wa mapambano, lakini tumefanikiwa kuwadhibiti magaidi wote. Nakubali niliapaswa kuwajibika kwa usalama wa raia na kutowasababishia matatizo, na baadhi yao kufariki. Nikirudi, nitawajibika mbele ya wakuu wangu,” aliongea Fabi.

Regina mara baada ya kumsikia Afande Fabi akiongea maneno hayo ya uwajibikaji, alitingisha kichwa kuonyesha kukubaliana naye. Lakini Hamza hakuweza kujizuia tena. Ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na mtu anayejifanya kuwa muungwana ili kupata pointi mbele ya mke wake.

“Naona huna haja ya kwenda kuwajibika mbele ya wakuu wako, nitakuwajibisha sasa hivi,” aliongea Hamza huku akisogea kwa hasira akitaka kumtoa nje.

Kitendo kile kilimfanya Regina kupaniki na alimshika Hamza mkono kabla hajachukua hatua yoyote.

"Hamza, unataka kufanya nini? Umekuwa kichaa?" aliuliza kwa hofu.

"Haha... Regina, hakika mume wako anashangaza sana," aliongea Fabiani huku akiwa hana wasiwasi kabisa. Lakini muda huo huo, helikopta ilianza kushuka na rubani kutoa taarifa.

"Hamza tushafika tayari hospitalini. Acha ugomvi, muhimu hapa ni kumuokoa mgonjwa," aliongea Regina kwa kubembeleza.

Hamza aliishia kumwangalia mgonjwa aliyeonekana kuwa katika hali mbaya na kuona kuwa hana haja ya kuendelea na msimamo wake. Isitoshe, uwezekano wa kutokutana tena na bwana huyo mwenye dharau ulikuwa mdogo. Hakutaka kugusa mwanajeshi wa kitengo cha Malibu na kujitafutia matatizo kwa dharau zake.

Baada ya kushuka, mgonjwa alichukuliwa haraka na kuingizwa ndani ya hospitali.

Hamza alimwangalia Afande Fabi kwa sekunde kadhaa, kisha akamsogelea Regina.

“Wife, tuondoke na kaa mbali na huyu mtu,” aliongea Hamza, na Regina aliona kuwa siku hiyo Hamza alikuwa paranoid sana.

"Hamza, acha kuruhusu mawazo yako kufikiria vitu visivyo sawa. Hebu nenda kamuokoe mgonjwa," aliongea Regina kwa sauti ya utulivu.

"Dokta, naomba ukamsaidie mgonjwa wangu, uhai wake unakutegemea wewe," aliongea yule mama, akiwa na imani kuwa Hamza ni daktari bingwa.

Hamza, mara baada ya kuona hali ya kuomba kutoka kwa mama huyo, alikimbilia ndani ya hospitali hiyo. Hakukuwa na uhakika kama hospitali hiyo ilikuwa na madaktari wenye uwezo wa kumsaidia mgonjwa.

Afande Fabi, baada ya kuona Hamza ameondoka, alimgeukia mwanajeshi aliyekuja naye na kumpa maagizo.

"Mchukue profesa, jeraha lake likatibiwe. Nina kazi nyingine muhimu kufanya. Kumbuka, baada ya kupatiwa huduma, mchukue na ukutane na

wenzako wengine. Wapeni maagizo kuhakikisha usalama wake mpaka anafika mahali husika."

Mara baada ya kupokea maagizo hayo, mwanajeshi huyo alimchukua Profesa na kumuingiza ndani ya hospitali kwa ajili ya kutibiwa.

Muda huo, aligeuka na kumuona Regina akiingia ndani ya hospitali, na alimsogea na kumsimamisha.

"Regina, ni ngumu sana kukutana na wewe. Unaonaje tukiongea kidogo?"

"Lakini si upo bize," aliongea Regina.

"Haha... Ndiyo, lakini sasa hivi nimepata muda. Ukweli ni kwamba mpaka sasa Profesa tayari yupo salama, maana wale magaidi tushawaua," aliongea, na kumfanya Regina kunja sura kiasi, akionekana kufikiria.

"Tunaweza kuongea hata ndani ya hospitali wakati tukiendelea kusubiri kujua hali ya mgonjwa."

"Unataka kumuona mume wako akifanya upasuaji?" aliuliza, na Regina alitingisha kichwa kukubali.

"Nimesikia ni daktari mbobevu kwenye maswala ya upasuaji, lakini sijawahi kumuona akifanya upasuaji. Nataka kumuona leo."

"Oh, kumbe! Mmekuwa pamoja kwa muda gani, maana ni kama ndio unajua ni daktari kweli?"

"Sio muda mrefu sana, kama miezi hivi," aliongea Regina, na kumfanya Afande Fabi kumwangalia kwa sekunde chache, kisha akatingisha kichwa kumwelewa.

"Kama ni hivyo, basi ngoja nikusindikize. Kwa jinsi alivyokoa watu wengi kwenye treni, naamini uwezo wake sio mdogo."

Regina alihisi kuwa kuna kitu hakipo sawa kuhusu Fabi, lakini aliishia kukubali na kuongozana naye.

Upande wa idara ya wagonjwa wa dharura, watoa huduma walikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa kutokana na hali ya mgonjwa. Hali hiyo ilisababisha kutojali vigezo vya Hamza kama daktari. Baada ya kujitambulisha tu kuwa alikuwa daktari, hakuna hata aliyeomba kuona leseni yake. Manesi na mtaalamu wa ganzi walikusanyika katika hospitali hiyo ya mkoa wa Morogoro.

Picha za CT scan zilifanywa haraka, na Hamza, mara baada ya kuziangalia, aliweza kugundua shida ya mgonjwa. Lakini kwa bahati mbaya, chumba cha upasuaji kilikuwa kikitumika muda huo, na kutokana na hali ya mgonjwa ambayo haikupaswa kucheleweshwa, ilibidi Hamza atoe maagizo kwamba atafanya upasuaji wa dharura katika eneo hilo hilo.

Muda mchache baadaye, Afande Fabi alitoka nje na kisha akarudi akiwa na kinywaji, akampatia Regina. Lakini mwanamke huyo hakuwa na hamu kabisa ya kunywa chochote.

Kutokana na ubize wa watoa huduma hao wa hospitalini walivyokuwa wakitoka kwa kukimbia na kurudi, aliona hali haikuwa ya kawaida hata kidogo. Mara baada ya kugundua Hamza anaenda kufanya upasuaji nje ya chumba maalumu, aliona ni kitu ambacho hakiwezekani.

"Hivi upasuaji unaweza kufanyika hata nje ya chumba maalumu cha upasuaji?" aliuliza kwa hofu.

"Kutokana na mazingira na hali ya mgonjwa, jibu ni ndio. Isitoshe, hii sio hospitali kubwa, kwa hiyo kwa ajili ya kumuokoa mgonjwa, Hamza hana namna. Anaweza kufanya popote," aliongea, na kumfanya Regina kuzidiwa na wasiwasi, huku bila ya kujijua akianza kuomba mgonjwa apone na asifie mikononi mwa Hamza.

Mtoto wa kike, jasho la mikono lilianza kumtoka, kana kwamba hakuwa akiamini Hamza ni daktari.

ITAENDELEA. watsapp me 0687151346
 
Shukran San Mr. Singano[emoji120][emoji120]
 
Unajua chenye hua tuna waza ila hamna ngori buddy all in all big up,hata nisemeje ila kiukwel utunzi wako ni wa kimataifa kwa kweli.
 
Mkuu mbna kama unanishawishi niisome hii simulizi.
Ni balaa hii story bro sikufichi, shida singarno anapenda kuichelewesha kweli ila ni mkali kwa maadhui,mtuririko nk. Tungo zake hakuna mahali inaboesha labda huko kuchelewesha ana chelewesha, Bora uwe umeamua kuilewa basi burudani na haki Yako....
 
Simulizi gani nyingine nzuri niisome ...nina muda sijaingia JF
 
Back
Top Bottom