Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Aseee Mr Singanojr you are the best of the best. A content creator kias kwamba tangu nimekutana na hii simulizi nimejitahidi kupitia kila siku mpaka leo nmefikia kipande cha kwenda sambamba na wewe. Big up sana bro! Kongole nyingi kwako. Though kuna vijana wasiojua kazi ya utunzi wanaleta lawama za ovyo ila bro umefikia kiwango cha lami hauna mbambamba.
Je n'ai pas plus à dire mais j'apprecie votre travaille et je vous félicite premièrement votre capacite d'utilise beaucoup de langue. It's very rare to use such kind of artistic ✨️
Ukiniruhusu tuitengenezee series maana itauza sana zaid ya Harry Potter na Merlin.
 
Singanojr venez prendre vos fleurs ici...
 
Aseee Mr Singanojr you are the best of the best. A content creator kias kwamba tangu nimekutana na hii simulizi nimejitahidi kupitia kila siku mpaka leo nmefikia kipande cha kwenda sambamba na wewe. Big up sana bro! Kongole nyingi kwako. Though kuna vijana wasiojua kazi ya utunzi wanaleta lawama za ovyo ila bro umefikia kiwango cha lami hauna mbambamba.
Je n'ai pas plus à dire mais j'apprecie votre travaille et je vous félicite premièrement votre capacite d'utilise beaucoup de langue. It's very rare to use such kind of artistic [emoji92]️
Ukiniruhusu tuitengenezee series maana itauza sana zaid ya Harry Potter na Merlin.
Asante mkuu kwa feedback nzuri.Hapo kwenye kutengeneza filamu tunafanyaje sasa?.
 
Asante mkuu kwa feedback nzuri.Hapo kwenye kutengeneza filamu tunafanyaje sasa?.
Mkuu wewe kama story writer unawez kuchagua maana ikichezwa na wabongo tu haitanoga sana itafutiwe kidogo na Wataalamu nje ya ulingo wa bongo na msaada kdg niifikishe kwa kijana ndg yangu mwigizaji kisha afikishe wazo letu kwenye idara ya filam
 
Asante mkuu kwa feedback nzuri.Hapo kwenye kutengeneza filamu tunafanyaje sasa?.
Mimi nadhani hapa ishu ni mtaji. Unajua hii stori kuja hadi uitoe hivi ilivyo haitaki Camera ya kubabaisha, la sivyo itakosa huu mvuto. Ila hii ikitolea na Company yenye ina jiweza kama Netflix mbona ita paa sana
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZI:SINGANOJR

SEHEMU YA 141

Don’t die

Yulia hakuwa na uhakika jinsi ya kuhisi katika moyo wake, maana alihisi kama hakuna kitu alichojisikia. Hakuhisi shukrani wala chochote, alilaumu Hamza kwa kutoa Earth Axis. Alijua fika kwamba suala hilo likifika kwa viongozi, lisingekuwa na tofauti na kuisaliti nchi kwa sababu ya mwanamke.

Hata hivyo, katika akili ya Hamza, Yulia ni muhimu zaidi kuliko Earth Axis.

"Hamza, wewe ni mjinga! Ngoja viongozi wa juu wa nchi wasikie ulichokifanya, uone kama wanawake wako uliowaacha Dar watakuwa salama," aliongea Yulia huku aking'ata meno kwa hasira na kumfanya Hamza kuishia kujikuna kichwa.

"Hili lishakuwa tatizo sasa, unaonaje nikimfukuzia? Pengine ninaweza kumkamata na kumpokonya?"

"Kumfukuzia! Kama hatukuweza kumfukuzia wakati akiwa kwenye macho yetu, unadhani kila mtu anaweza kuwa mjinga kama wewe na kukuamini?" alilalama Yulia.

"Hey! Yulia, hebu acha kuzidisha. Ijapokuwa mimi ni mvumilivu sana kwa wanawake wangu, lakini kuna mpaka hupaswi kuvuka," aliongea Hamza mara baada ya kuona Yulia ni kama anataka kumkosea heshima.

Yulia alikuwa na hasira kiasi kwamba aliishia kumpiga ngumi Hamza kifuani.

"Nazidisha kivipi! Sio tu kwamba natamani kukufokea, natamani kukuua pia. Kuna haja gani ya kuishi bila ya kuwa na Earth Axis? Unadhani wakuu watatuacha salama?"

"Kwa hiyo tufanyaje? Mimi niliwazia usalama wako kwanza," aliongea Hamza na alikuwa akimaanisha; alihofia kama asingewapatia hicho kitu basi Yulia angedhurika kweli.

Mara baada ya kufikiria kuhusu alichokifanya kwa mara ya pili, aliona pengine maamuzi yake hayakuwa sahihi.

Yulia, mara baada ya kusikia maneno ya Hamza, alimwangalia kwa sekunde kadhaa na kisha hakujali tena kukasirika.

"Njia ya kutatua hili tatizo ninayo, lakini kuanzia sasa hivi unapaswa kunisikiliza kila nitakachokuambia," aliongea Yulia na Hamza kutingisha kichwa.

Hamza, tokea mwanzo, alijua Yulia kwa namna alivyokuwa na akili, lazima kuna njia anayo ya kuweza kuitumia kuirudisha Earth Axis. Ndiyo maana aliitoa bila shida.

"Hakuna tatizo, nitakusikiliza kuanzia sasa," aliongea Hamza.

Yulia hakuwa na haraka kabisa, na palepale aligeuka na kusogelea sehemu ambayo Bertha alikuwa amedondokea. Alichuchumaa na kugeuza uso wa Bertha ambao ulikuwa umetapakaa damu.

"Madaktari wetu wapo wapi?" aliuliza Yulia.

"Kanali Yulia! Madaktari wetu mmoja amefariki na mwingine ameumia," aliongea mwanajeshi aliyekuwa pembeni.

Yulia pia alikuwa ni mwanajeshi mwenye cheo maalumu cha Ukanali, na hiyo yote ni kutokana na mchango wake jeshini katika upande wa sayansi na teknolojia.

Hamza, mara baada ya kusikia kauli hiyo, aliishia kukunja sura na kisha palepale alisogea na kuchuchumaa pia kuangalia hali aliyokuwa nayo Bertha kwa kushika mkono wake.

"Ameumia ndani kwa ndani na kutoa damu, lakini sio tatizo kubwa sana. Mbinu yake ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ina nguvu sana ya kumsaidia kuimarisha afya yake na kuponya majeraha kwa haraka. Pia ashafikia levo ya nafsi huyu ambayo ni ya ukaidi wa asili. Ndani ya siku tano au kumi, atakuwa amepona kabisa," aliongea Hamza.

"Wewe unajuaje?" aliuliza Yulia.

"Ninaweza kuua na kuponya pia," alijibu Hamza.

"Una uhakika?" aliuliza Yulia akiwa na wasiwasi na kumfanya Hamza kucheka.

"Yulia, tangu lini ukawa na wasiwasi juu ya watu wengine?" aliuliza Hamza.

Yulia alijua ni kweli alikuwa tofauti na mwanzo; aina hiyo ya hisia asizozielewa ilisababisha moyo wake kuwa katika machafuko.

"Acha kuongea ujinga. Sitaki kuingia katika matatizo na viongozi wake kwa sababu yangu," aliongea.

"Kama ni hivyo basi sawa," alijibu Hamza bila kuongezea neno na akaishia kumwangalia mwanamke huyo kwa tabasamu.

Yulia hakuthubutu kumwangalia Hamza usoni. Aliishia kusimama na kisha akaanza kutembea.

"Nifuate, ni muda wa kurudisha mashambulizi," aliongea.

Hamza alimwangalia mwanamke huyo kwa nyuma na namna nywele zake zilivyokuwa zikisambazwa na upepo. Macho yake yalichanua pale pale, kisha akaifuata nyuma yake.

Wawili hao walirudi ndani ya maabara ile ya kijeshi. Watu waliokuwa ndani ya maabara hiyo walishaokolewa nje na kambi yote ilikuwa tupu.

Yulia aliwasha mfumo wa dharura wa umeme, na mara moja tarakilishi zote pamoja na skrini ziliwaka upya ndani ya sekunde chache, na kufanya eneo lote kupambwa na mwanga unaobip na kuzima kwa namna ya kupendeza macho.

"Sababu ya kuchagua kujenga maabara hii katika kisiwa cha Chole ni kwa sababu eneo hili kuna mkondo mkubwa wa bahari ambao tumeutumia kutengeneza chanzo cha umeme wa dharura. Hivyo, hata kama laini kubwa ya umeme ikiharibika, umeme unaopatikana unatosha kabisa," aliongea Yulia huku akipangusa kioo kikubwa kilichokuwa upande wa kushoto akimuonyesha Hamza mitambo ya kuzalisha umeme iliyofungwa chini ya maji.

Hamza, baada ya kuchunguza mfumo ule wa kutengeneza umeme, macho yake yalichanua baada ya kuona sio wa kawaida kabisa. Walitembea upande mwingine wa juu kabisa na Hamza alishangazwa na aina ya keyboard ndogo sana ambayo ilikuwa kama kishikwambi, aliyoanza kuitumia kuendesha kila aina ya skrini bila shida yoyote.

"Hii aina yako ya keyboard, inafanya vipi kazi kudhibiti maabara nzima?" aliuliza Hamza, akimfanya Yulia kuinua kidole chake na kuelekezea kichwani.

"Hii keyboard nimeunganisha na mawazo yangu, ninachoamua kitokee, kinatokea," aliongea.

"Mh! Kwa staili hiyo, hata kama mtu akijaribu kuvamia na kutaka kuiba tafiti zako, itakuwa ngumu sana," aliongea Hamza huku akitingisha kichwa chake.

"Ulidhani mke wako mwenye IQ ya 180 anaweza kunizidi. Ni kwamba tu sijawahi kujali sana maswala ya kupima uwezo wangu wa akili au kujiunga na hizo taasisi za kijinga jinga."

"Kwahiyo unasema unamzidi mke wangu?"

"Bila shaka namzidi kila kitu likija suala la kutumia akili, au unataka kunishindanisha naye?" aliongea Yulia.

Hamza alitingisha mabega na kisha alitembea na kumkumbatia Yulia kwa nyuma.

"Darling, vipi kwanza kuhusu mpango wako wa kurudisha mashambulizi?"

"Hebu niachie kwanza wewe mshenzi," aliongea Yulia huku aking'ata lipsi zake. Alikuwa amekosa neno juu ya matendo ya Hamza.

"Nimeshakuambia uache kuniita mshenzi, la sivyo haitakuwa habari nzuri kwako," aliongea Hamza akiwa siriasi, lakini Yulia hakuongea neno na aliendelea kuweka umakini kwa kile alichokuwa akifanya.

Baada ya kama dakika kumi ya kuandika kwa haraka, kitufe cha rangi nyekundu kilitokeza katika skrini, na alibonyeza. Palepale, ramani ya baharini ilionekana huku kukiwa na mzunguko wa radar ukifanya kazi.

"Unajaribu kufanya nini? Usiniambie unajaribu kutafuta manowari yao kupitia radar. Wametumia EMP kuingilia mawasiliano."

"Wewe unachozungumzia ni radar zile za zamani, lakini mimi radar ninayotumia hapa ni teknolojia mpya kabisa na inatumia teknolojia ya Gravity detector, na natumia kuskani juu ya uso wa maji kuona ni upande gani ilipo," aliongea Yulia.

"Kwahiyo unachomaanisha ni kwamba kama manowari yao itakuwa juu ya maji, uzito wa maji katika eneo husika utakuwa tofauti na utofauti huo unamaanisha ndiyo eneo walipo?"

"Ni kama hivyo, lakini ulichoongea wewe ni nadharia tu. Hii teknolojia bado utafiti wake sijaukamilisha na sina uwezo wa kuskani umbali mrefu na kutoa majawabu sahihi. Kama wako mbali sana na hapa, sina uhakika kama itafanya kazi," aliongea.

Hamza aliweza kuelewa kiasi nadharia juu ya teknolojia hiyo, hata hivyo, asingeweza kujua kila kitu. Kama alichoelezea ni sahihi kwa asilimia mia moja, basi Yulia hakuwa genius.

“Manowari tatu!” Yulia aliongea huku akikunja sura.

“Kama kuna manowari tatu, kazi ishakuwa ngumu tayari hii. Tutajuaje ni ipi imebeba Earth Axis?” aliendelea kuongea, akimfanya Hamza kuangalia manowari hizo kwa umakini.

“Ninaamini ambayo ipo karibu zaidi na kisiwa ndiyo imeibeba,” Hamza aliongea.

“Unajuaje? Au unadhani colonel Bird hawezi kwenda mbali na ile suti yake? Isitoshe pia wana drone maalumu ambazo zinaweza kuwapeleka kwenye manowari ya mbali,” Yulia aliongea, na kumfanya Hamza kutingisha kichwa kuonyesha kukubaliana, lakini pia kujutia.

“Nilifanya makosa kumkabidhi,” Hamza aliongea.

Yulia, baada ya kusikia kauli hiyo ya masikitiko kutoka kwa Hamza, kidogo tu atapike. Yeye kama mwanasayansi, kitu ambacho alikuwa akichukia ni kuotea jambo bila kuwa na sababu za kimantiki.

“Hebu kuwa siriasi basi! Uwezo ambao ninao ni kukupeleka katika manowari yao moja, na kama si sahihi basi tutakuwa tumefeli,” Yulia aliongea.

“Unadhani ni kipi tutafanya sasa? Katika dunia hii kila kitu tunaotea tu, na kinachofanyika ni kuelemea upande ambao tunaona kuna asilimia kubwa za ushindi. Halafu pia najua saikolojia ya wanajeshi, hivyo sidhani kama nimekosea,” Hamza aliongea.

“Ni tofauti na unavyowaza. Nisipofanikiwa kuirudisha Earth Axis sitoweza kukulinda dhidi ya kitakachokutokea,” Yulia aliongea.

Hamza alikubaliana naye na kuona kama atajijengea uadui na nchi, hawezi kuwa salama na labda kitu atakachofanya ni kuichukua familia yake na kukimbia nchi.

“Yulia, si umesema unao uwezo wa kunipeleka kwenye submarine? Nafikaje?” aliuliza Hamza.

Submarine yao inatembea kwa spidi ya kilomita tano kwa saa, ni ngumu kuwapata kwa njia ya maji. Hata kwa ndege itakuwa ngumu kuwazuia maana submarine yao ina mfumo wa kujilinda na makombora,” Yulia aliongea, kisha akamgeukia Hamza akiwa na uso uliojaa usiriasi.

“Kwahiyo unapaswa kufika eneo walipo moja kwa moja, na baada ya hapo itakuwa juu yako,” Yulia aliongea.

“Kama ni hivyo, nitafikaje moja kwa moja walipo kutoka hapa? Ni kifaa gani natumia?” Hamza aliuliza.

“Mpango wangu ulikuwa ni kukuonyesha tu majaribio yangu, na sikuwahi kudhania utahusika moja kwa moja,” Yulia aliongea na palepale alitembea na kuingia kwenye chumba kingine kilichokuwa kimefungwa kwa mfumo maalumu.

Hamza alishangazwa na kile kilichokuwa mbele yake. Kulikuwa na kifaa kikubwa kilichojengwa kwa chuma kigumu chenye mwonekano wa silver. Kifaa hicho kilikuwa na nguzo mbili pembeni za chuma, na katikati kulikuwa na duara kubwa lililokaa kama yai.

Ilikuwa ni kifaa kilichotengenezwa kufanana kabisa na ngao ya Taifa, yaani kulia na kushoto ilikuwa ni kama watu wamesimama na kushikilia ngao iliyo na tundu kubwa katikati. Nyuma ya kifaa kile kulikuwa na chupa kubwa lililounganishwa, lilikuwa kubwa mno kama yale matanki ya kuhifadhia mafuta ya petroli.

“Unakwenda kuwa binadamu wa kwanza kwenda kutumia hii teknolojia. Ukweli ni kwamba unaweza kuwa chaguo sahihi zaidi kuanza kutumia wewe kama sehemu ya majaribio yake,” Yulia aliongea huku macho yake yakiwa yamechanua kwa ari kubwa.

“Hii teknolojia nimeipa jina la Space Jumper au unaweza kusema Space warping Device,” Yulia aliongea.

“Nini!?” Hamza alihisi ni kama hakusikia vizuri kile alichoongea mwanamke huyo. Ijapokuwa alikuwa amezoea kuona vitu vikubwa vya kushangaza na alikuwa na uwezo wa kuishi maisha marefu katika hatari kuliko mtu yeyote, lakini alizidi kushangazwa na Yulia.

“Kwahiyo unasema hiki kifaa kazi yake ni kumfanya mtu kuweza kuteleport?” Hamza aliuliza.

“Ndio, na huna haja ya kuwa na wasiwasi. Nishaifanyia majaribio hii teknolojia kwa kutumia mawe, panya, na ngedere. Ijapokuwa nilifeli kwa angalau mara mia katika majaribio, lakini nilifanikiwa mara ya mwisho. Hiki kifaa kazi yake ni kukutoa eneo moja kwenda lingine mara moja tu, na kwa fitness ya mwili wako huwezi kupata shida yoyote,” Yulia alieleza.

Hamza alijikuta mwili wake ukisisimka huku akishikwa na jasho la ubaridi baada ya kugundua ukweli. Ni muda huo aliweza kujua mwanamke aliyekuwa mbele yake alikuwa akiogopesha kuliko alivyofikiria.

“Umewezaje kutengeneza kifaa kama hiki? Ni kanuni gani ya kifizikia imekuwezesha? Aina hii ya kiteknolojia imepita teknolojia ya kawaida ya kibinadamu tokea kustaarabika kwake,” Hamza aliuliza.

“Hata kama nikikuelezea, unaweza usielewe. Lakini kitu pekee ninachoweza kukuambia ni kwamba hii teknolojia sio mimi niliyeigundua. Nilichokifanya ni kutumia ramani iliyokuwepo na kutengeneza kwa malighafi za hapa hapa,” Yulia aliongea na kumfanya Hamza kutoa macho.

“Usiniambie umeweza kutengeneza hiki kitu kwa sababu ya Earth Axis?” Hamza aliuliza na kumfanya Yulia kuvuta pumzi nyingi. Kisha palepale alitembea na kwenda kumshika Hamza shingoni kwa mbele, na kutokana na Hamza kumzidi kirefu, alijirefusha na kufikia upande wa sikio lake.

“Watu wengi wanachokijua ni kwamba Earth Axis ni kitu muhimu sana, lakini hawajui thamani yake ipoje. Ukweli ni kwamba Earth Axis ni kama kitabu kinachoelezea historia ya ustaarabu wa jamii ulioendelea zaidi kuliko wa kwetu binadamu. Kwasasa ni mimi pekee ninaweza kutafsiri na kuielewa, ndiyo maana unaona kila kitu kilichopo ndani ya hii maabara ni kigeni kwenye macho yako. Ikitokea kifaa hiki kikatua katika mikono ya watu wabaya na wakaelewa maana yake, nadhani unajua nini kitakwenda kutokea,” Yulia alieleza.

Muda huo moyo wa Hamza ulikuwa ukidunda kwa kasi mno, alijua kwanini Himidu hakutaka kumwambia chochote kuhusu majaribio haya yanahusu nini zaidi ya kumwambia kwamba atapata faida kama atahusika katika haya majaribio kwa kuja kutoa ulinzi katika eneo hilo, lakini kumbe alichokuwa akifukuzia na kufanyia kazi kwa siri ni kitu zaidi ya sayansi na teknolojia.

"Nadhani nimeelewa sasa, tuanze kazi," aliongea Hamza huku akilazimisha tabasamu.

"Hauogopi? Hii ndio mara ya kwanza naenda kufanya majaribio ya space jump na mwanadamu."

"Kuogopa! Licha ya kujua lugha nyingi na kushindwa hata kuzihesabu, kwangu neno woga ni neno ambalo sijawahi kuijua maana yake katika uhalisia."

"Hee wewe! Endelea na majigambo tu," aliongea Yulia akivuta mdomo na kisha aligeuka.

"Ngoja nikuletee vifaa vya kupigia mbizi," aliongea.

"Haina haja, hata kama huwezi kunipeleka moja kwa moja mpaka ndani ya submarine, mwili wangu una uwezo wa kutosha wa kupiga mbizi bila shida, isitoshe kutumia hivyo vifaa ni kuniongezea mzigo."

"Acha ukichaa basi, unajiona umekuwa superman?"

"Unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unanifikisha zilipo manowari zao na sitokuangusha," aliongea Hamza kwa kujiamini.

"Ni kama nilivyosema, sina uhakika asilimia mia moja kama naweza kukuingiza moja kwa moja ndani ya manowari zao, kutokana na urefu wake ni mkubwa sana na sijawahi kuufanyia majaribio, unaweza kupasuka ukiwa njiani," aliongea lakini Hamza hakuwa na wasiwasi kabisa wala kugopeshwa na maneno yake.

"Najua huwezi kuniacha nife, wakati tayari ushakufa na kuoza kwa ajili yangu," aliongea na kauli ile ilimshitua kidogo Yulia na pale pale aligeuka na kusogelea kile space jumper.

"Yulia, hata kama nisipoweza kurudi, kumbuka kuwaambia wakubwa zako nimekufa kwa ajili ya taifa, naomba usifanye mambo kuwa magumu kwa mke wangu na wengine," aliongea Hamza na kumfanya Yulia kung'ata lipsi zake bila kugeuka na kuendelea kuandika vitu kwenye keyboard.

"Hilo halitokuwa jukumu langu sasa," aliongea.

"Ninaamini utafanya kama nilivyosema," aliongea Hamza.

Yulia aliendelea kutumia mkono wake kuunganisha maumbo kwenye skrini pamoja kama maduara hivi na kisha kwa kutumia ramani alitengeneza target ya eneo ambalo Hamza anakwenda kutua na kisha alimgeukia Hamza na kumwangalia na alivyoona amekaa sehemu sahihi mbele ya mdomo wa kifaa kile alitingisha kichwa na kisha akageuka na kubonyeza kitufe.

"Utamezwa na kifaa na kutemwa ndani ya sekunde kumi tu, siwezi kusema ni hisia gani utapata wakati huo kutokana na kwamba wewe ndio binadamu wa kwanza kufanya haya majaribio. Good luck," aliongea.

Hamza alitingisha kichwa na kisha akafumba macho yake akiacha kufikiria kitu chochote.

Yulia alivuta pumzi nyingi na kisha alibonyeza kitufe cha rangi ya njano na pale pale yale maumbo aliokuwa ameyaunganisha katika skrini yalianza kujiunganisha kwa namna ya ajabu huku sauti ya kieletroniki ikisikika.

"Space Jump Device 0.17 has entered operational mode. Fusion reactor power is fully online... Initiating lock on target's 3D spatial coordinates..."

Dakika ileile ndani ya lile tanki mwanga ulionekana ukija kutoka ndani ya fusion reactor ukiwa unazunguka kwa spidi kubwa, mzunguko ule wa nishati uliokuwa ukionekana mbele yake ulitosha kutingisha dunia kutokana na ukubwa wa teknolojia yake. Kuwa na teknolojia ya kudhibiti wingi wa nishati kama hiyo ilikuwa ni kama kudhibiti nishati ya dunia, ilikuwa ni nishati safi ambayo inaweza kugeuza uchumi wa dunia.

Hamza pale pale alielewa kwanini Yulia alikuwa na ujasiri wa kusema kifaa hicho kina uwezo wa kumteleport mtu, kumbe ni kwa nguvu ya hiyo nishati.

Ni sawa na kusema teknolojia ya Yulia ilikuwa kubwa na hatari zaidi ya teknolojia ya nyuklia bila kuuma maneno.
"Ten... nine... eight..."
Sauti ya kieletroniki ilianza kuhesabu kwa kurudi nyuma, sehemu ambayo alikuwa amesimama Hamza alikuwa ashapotea tayari kwa kumezwa na mwanga, mkono ule wa chuma ulikuwa ukizunguka kwa spidi kubwa sana. Kitendo cha kuhesabu kumalizika palepale ule mwanga wa kile kifaa ulipungua kwa namna fulani ya kuzama kwenda ndani ya ile chupa kubwa na kupotea kabisa, na kila kitu kilirudi katika hali yake ya kawaida.

Yulia mara baada ya kufika juu ya Transmission Platform kumwangalia Hamza hakuonekana kabisa na aliishia kuongea maneno ya chinichini.
"Don’t die."

Katikati chini ya maji ndani ya manowari ya kijeshi isioweza kuonekana kabisa kutokana na teknolojia yake, wanajeshi wengi wa Delta Zero walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wakinywa na kula.

"To our fallen comrades! Their sacrifice was worth it! We got the Earth Axis! Long live America!" aliongea Kanali Bird akiwa amesimama juu na glasi ya mvinyo, akiwapa ishara wanajeshi wenzake ya kugongesheana cheers kama namna ya kuwaenzi wenzao walioweza kujitoa muhanga katika misheni hiyo na kufanikisha kuipata Earth Axis.

Wanajeshi hao hawakuwa na huzuni, licha ya kwamba wenzao walikufa, lakini mafanikio walioweza kufanikisha waliona sio bure na ndio maana walijazwa na vicheko wakati wakifurahia pombe.

"Kanali, naomba kuuliza swali. Hiki kitu kinachoitwa Earth Axis ni nini hasa? Tumepoteza wanajeshi wetu wengi kwa ajili ya kukipata lakini hatujui hata maana yake," mwanajeshi mmoja aliuliza na Kanali Bird alitingisha kichwa kuonyesha hajui.

"Hata mimi sijui ni nini hasa, hata Jenerali Smith hajui. Nilichoweza kusikia tu ni kwamba baadhi ya maraisi waliohudumu katika uongozi ndio wanajua kuhusu siri yake."

"Kumbe ni kitu cha siri namna hiyo, ndio maana tumetumika sisi katika kushambulia," aliongea mwingine.

"Nilimsikia General Smith akiongelea kuhusu hili na kusema Earth Axis ilionekana kwa mara ya kwanza nchini Ethiopia na ikapotea, ila baadaye ikaonekana tena nchini Cyelon lililokuwa koloni la Waingereza. Baada ya Vita ya Pili ya Dunia, Malkia Elizabeth alituma wanajeshi kwenda Cyelon kuirudisha, lakini ilipotea tena na habari yake ikaishia hapo kwa miaka mingi. Baada ya hapo, Serikali ya Marekani ilinusa uvumi wa uwepo wa hiki kitu na utafutaji ulianza mpaka ilipobainika miaka ya hivi karibuni ipo Tanzania," aliongea.

"Kanali, imewezekanaje Watanzania wakawa na kitu kama hiki kwenye mikono yao baada ya kupotea huko cyelon kama ulivyosema?" aliuliza mwenzake. Cyelon ilikuwa ni Sri Lanka.

"Hakuna anaye fahamu mpaka sasa imekuwaje Tanzania wakawa wamiliki wa Earth Axis," wanajeshi wote walionekana kusikiliza kwa umakini mkubwa.

Lakini muda huo wote waligutushwa na king’ora kilichoanza kutoa sauti kwa nguvu.
"Du... Du... Du... Du..."
"Tunakaribia kushambuliwa," wote walihamaki.

SEHEMU YA 142.

Wanajeshi hao walijikuta wakishangaa kwa kuona kitu ambacho hakiwezekani kabisa kutokana na teknolojia ya manowari yao.
“Imewezekanaje mpaka tukashambuliwa? Ina maana rada imeshindwa kufanya kazi yake?” waliuliza, maana kutokana na mfumo wao wa rada, kama adui angekuwa anaisogelea manowari yao, wangeweza kumuona akiwa umbali wa maili hata tano.
“Hapana, sio shambulizi, kuna mtu amevamia manowari yetu,” aliongea mwanajeshi mwingine aliyekuwa akiongoza mtambo huku akiangalia skrini iliyokuwa ikionyesha ramani yote ya manowari yao huku wakitoa macho kuona kuna mtu yupo ndani ya manowari yao wakijiuliza ameingiaje.
Isitoshe, walikuwa chini ya maji kwa zaidi ya mita mia nne.
“Kanali, kuna mtu kavamia ndani ya manowari yetu na sasa yupo upande wa store na anasogelea kuja uelekeo wetu,” aliongea bwana aliyekuwa akiangalia kitu cha rangi nyekundu kilichokuwa kikisogea katika ramani ya manowari hiyo.
“Kaingiaje ingiaje?”
“Haijulikani, lakini baadhi ya wanajeshi wetu wamekufa tayari,” aliongea mwingine akionyesha kamera ambazo wanajeshi walionekana wakiwa chini.

Muda huo, sauti ya upepo ilianza kusikika kupitia simu zao kutoka kwa wanajeshi waliokuwa upande mwingine.
“Requesting support, requesting support!”

Kanali, mara baada ya kusikia sauti za vijana wake kuomba msaada, alijikuta akirusha ile glasi aliyokuwa ameshikilia mkononi ukutani na ikapasuka palepale.
“Everyone, get into first-class combat readiness! Go back and support!” Aliamrisha wanajeshi wake kujipanga katika mtindo wa daraja A ili kushambulia.

Lakini sasa, wakati wanajiandaa kuondoka, ghafla eneo walilokuwepo mwanga wake ulizimika mara moja na kukawa giza.
“Hii ni hatari, huyu mtu anajaribu kuharibu manowari yetu...”
Kanali Bird sura iligeuka na kuwa ya kijani palepale na palepale alichukua kiboksi kilichokuwa na kodi maalumu.
“Naenda kuvaa suti yangu ya kijeshi, ipandishe manowari juu ya maji, ni muda wa kumuua huyu mvamizi na kisha kuondoka hapa,” -.
Aliongea na palepale wanajeshi wote walianza kukimbia kuelekea kila uelekeo huku kapteni wa manowari hiyo akifanya kazi ya kuipandisha manowari hiyo juu ya maji.

Wanajeshi wale, baada ya kukimbilia uelekeo wa eneo la mvamizi alipo, walijikuta wakikunja sura mara baada ya kuona wanajeshi wenzao zaidi ya wanne wakiwa chini tayari. Palepale waliweza kumuona mwanaume shombeshombe akitumia ngumi na mateke na chuma kuharibu manowari yao.

Hamza, mara baada ya kumezwa na ile mashine ya Yulia, alijikuta tu yupo ndani ya manowari hiyo ya kijeshi upande wa stoo. Hisia alizopata ni kama vile alikuwa ndotoni kwani ni ndani ya sekunde tu alikuwa kisiwani na wakati huo alikuwa eneo lingine kabisa.
Hamza alijua fika Yulia hakuwa amemdanganya hata kidogo. Aliamini lazima ni kweli Earth Axis ni kitu ambacho ni kutoka kwa viumbe wenye akili sana. Hata kwa akili gani angekuwa nazo, Yulia asingeweza kutengeneza kitu cha maajabu namna hiyo, hivyo ndivyo Hamza alivyofikiria.

Wanajeshi wale wa Delta Zero mara baada ya kumuona Hamza akiwa mbele yao hawakuthubutu kutumia bunduki zao wala ile mionzi kutokana na kwamba wangeharibu manowari. Hivyo, kwa spidi kubwa walimsogelea kupambana naye kwa kutumia nguvu. Na Hamza hakujali sana, isitoshe hilo ndio eneo ambalo alikuwa vizuri zaidi. Katika uchochoro mdogo wa manowari hiyo alipigana na wanajeshi hao mpaka wakaanza kuwa wekundu.

Kila Hamza alivyoshambulia, alikuwa akiharibu pia manowari hiyo mpaka pale alivyotengeneza ufa. Kutokana na presha ya bahari kuwa kubwa, maji yalitoboa na kuanza kuingia ndani kwa spidi kubwa. Kadri maji yalivyokuwa yakiingia ndani, vyuma vilishindwa kushikilia vizuri na kusababisha sehemu nyingi kuanza kuvuja.

Kwa spidi ya kuonekana kwa macho, manowari hiyo ilianza kuharibika kwa kasi kubwa.
“Huyu ni kichaa, hivi hajui hii meli ina kinu cha nyuklia?”
“Pumbavu zake, yupo wapi?”

Kutokana na maji mengi yaliyokuwa yakiingia, iliwapa ugumu wanajeshi kushindana na Hamza na aliishia kushindana na maji kujilinda wasipoteze maisha, huku Hamza akiwatoroka bila ya kuacha nyayo.

Licha ya Hamza kutowahi kuingia katika aina ya manowari hiyo yenye mfumo wa nyuklia ndani yake, lakini tayari alikuwa ameingia katika manowari nyingi sana tu. Hivyo, alikuwa akielewa namna muundo wake ulivyo na ramani yake kwa ujumla.

Mpango wake ni kutafuta wapi Earth Axis ilipohifadhiwa, na moja kwa moja aliamini lazima itakuwepo katika chumba cha Colonel Bird. Hivyo, Hamza uelekeo wake ulikuwa ni kutafuta ni wapi Colonel Bird atakuwa anahifadhi suti yake.

Hivyo, dakika ambayo maji yaliingia ndani, Hamza alitumia nafasi hiyo kwenda ndani zaidi ya vyumba vya manowari hiyo kutafuta Earth Axis. Isitoshe, aliona kama atashambuliwa pande zote na washambuliaji akiwepo Colonel Bird, basi inaweza kumpa shida sana kushinda, isitoshe teknolojia ya suti yake ilikuwa kubwa mno.

Kitu kingine pia alihofia ni Colonel Bird kutoroka na Earth Axis kutoka ndani ya manowari hiyo, ndiyo maana aliona aharakishe maana akitoweka, maana yake na mpango utakuwa umefeli.

Kanali Bird aliingia katika chumba maalumu ambacho suti yake ya kijeshi huihifadhi katika eneo maalumu ili kuendelea kujicharge. Mara baada ya kuingia ndani ya chumba hicho maalumu, alivyotoka nje alikuwa tayari amebadilika na kuwa katika umbo la roboti.

Baada ya miale ya mwanga kutoka upande wa eneo la kichwa chake, palepale aligeuka pembeni na kubeba kile kiboksi chenye Earth Axis na kujiandaa kutoka nje ya manowari hiyo ambayo ilishaanza kuonyesha dalili ya kuzama. Lakini ni dakika hiyo hiyo mtu aliingia ndani ya eneo alipo na kumgonga kwa nyuma. Kilichosikika ni sauti ya peng. Kanali Bird na suti yake alifyatuliwa na kwenda kujigonga kwenye kuta na kuharibu mpaka mlango wa kutokea nje, lakini bahati nzuri suti yake ya chuma haikuweza kuharibika, hata hivyo alishikwa na mshituko wa aina yake.

Tokea aanze kuivaa hiyo suti kama mwanajeshi maalumu wa Delta Zero, hajawahi kupigwa na shambulizi la kushitukiza kama hilo mpaka kudondoka chini.
“Wewe ni nani?” Aliongea huku akisimama na kugeuka nyuma, na alishituka mara baada ya kugundua aliekuwa mbele yake ni Hamza.
“Ni wewe tena!?” Aliuliza huku moyo wake ukianza kusukuma damu kwa spidi akiwa anamshangaa.
“Umewezaje kufika hapa?”
“Sipo hapa kucheza mchezo wa swali na jibu, Earth Axis ni kitu ambacho siwezi kukuruhusu uondoke nacho,” aliongea Hamza

“Wewe ni mwanajeshi wa Kitanzania?” Aliuliza Kanali huyo maana bado hakuamini kama Tanzania inaweza kuwa na mwanajeshi mwenye nguvu kama Hamza.

Hamza hakujibu swali lake, badala yake alipiga hatua mbele na kisha akaushika mkono wa kiroboti wa Kanali Bird. Kwa staili matata sana ya Judo, mkono ule aliweka kwenye bega lake na kuuvuta kwa nguvu. Kutokana na chumba hicho kuwa kidogo kwa saizi ya suti hiyo kugeuka, mkono ule uliharibika palepale kwa kupinda.

Shambulizi lile lilimuacha Bird katika mshituko mkubwa na kujiuliza kama mtu huyo alikuwa binadamu kweli. Haikuwa swala rahisi kuharibu mkono wa suti yake kwa staili ya Judo kama vile anashindana na binadamu wa kawaida.

Hakutaka kufikiria mara mbilimbili, kule kujiamini anaweza kumdhibiti Hamza haraka kuliisha na aliona ampe heshima inayostahili kwenye kupambana naye. Ijapokuwa alishambuliwa mara mbili na Hamza, hata hivyo suti yake haikuharibika sana zaidi ya kuachia kidogo eneo la kiungio chake cha bega. Hivyo kwa spidi kubwa alifyatuka na kumsogelea Hamza ili kumpiga ngumi.

Hamza palepale alikwepa kwenda kushoto na kisha alitumia mkono wake wa kulia kupiga suti ile eneo la kifuani kwa nguvu zake zote na kumfanya Kanali kufyatuliwa tena na kwenda kujipigisha kwenye ukuta kwa mara nyingine na kusababisha cheche.
“Mbona hutumii hayo mashambulizi yako ya mionzi kama ulivyofanya? Hata kama suti yako hiyo ya kijeshi ni silaha hatari lakini ni ngumu kunishambulia mtu kama mimi,” aliongea Hamza mara baada ya kuona ni kama Bird anajaribu kuwa makini.

Bird aliishia kubakia kimya kama mtu ambaye hakuwa na jibu. Kitendo cha Hamza kuharibu sehemu muhimu za manowari hiyo ilisababisha iwe ngumu kurudi juu na suala hilo lilimtengenezea udhaifu Afande Bird, kwani suti yake haikuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi akiwa chini ya kina kirefu cha maji na hata kama angesema atoke nje asingekuwa na uwezo wa kuogelea akiwa na suti hiyo mwilini.

Kutokana na hilo, Hamza hakuwa na wasiwasi kabisa, alijiambia ili mradi hakuna uwezekano wa mwanajeshi huyo kuingia katika manowari nyingine, hawezi kumtoroka kwa namna yoyote ile.

“You are an expert, a powerful warrior. We can negotiate whatever you want,” aliongea Kanali Bird mara baada ya kuona uwezo wake wa kushinda ni mdogo. Aliona njia pekee ni kumshawishi huyo mwanajeshi kushirikiana naye kwa kumtajia chochote anachotaka.
“Nadhani unajua nchi na jeshi letu vinathamini sana watu wenye uwezo mkubwa,” aliongea akiendelea kuongea.
“Unataka kunihonga?” Aliuliza Hamza.
“Hapana, nakualika kuwa sehemu ya kambi ya watu wa haki, kambi maalumu yenye mchango mkubwa katika uhuru na maendeleo ya binadamu kwa ujumla,” aliongea.
“Kama unataka kunihonga, unapaswa kujua gharama unayopaswa kulipa haiwezi kuwa ndogo.”

Wewe ongea tu, ni kiasi gani cha pesa unahitaji au ni nguvu kiasi gani unahitaji, tunaweza kuongea kila kitu,” aliongea Kanali akiona lazima kuna uwezo wa kumshawishi huyo bwana. Isitoshe, kwa namna alivyoonekana kuwa na asili ya uzungu ndani yake, alimuona ni kama mwenzao.
“Sitaki hela na sitaki nguvu vilevile. Ninachotaka ni Earth Axis,” aliongea Hamza huku akinyooshea mkono kiboksi alichoshikilia Kanali, na kauli yake ilimwacha Bird bila usemi.
“Inaonekana kama hutaki maongezi na mimi,” aliongea, na palepale alikunja ngumi na kufanya kwenzi za vidole vyake zifyatue mionzi kumlenga Hamza.

Aliona kama asipotumia siraha za suti yake, uwezo wa kumshinda Hamza utakuwa mdogo sana. Hivyo, aliona tofauti na kuogopa kuharibu meli hiyo zaidi kwa kutumia silaha zake, ni bora ajaribu.
Kutokana na ukaribu uliokuwepo, ilionekana kama shambulizi lile halikwepeki. Lakini Hamza, kwa spidi ya hali ya juu, alisogea nyuma ya ukuta wa chuma huku akijitahidi kadri awezavyo kuepuka mlipuko.
Boom, Boom, Boom.!!
Mionzi ile ilikuwa kama kombora kwani baada ya kugusana na chuma ilitoa mlipuko mkubwa ambao ulibaribu kebini nzima na kuzifanya sehemu hiyo kuwa na mrundikano wa vyuma.

Ijapokuwa aliweza kuepuka mionzi ile, ilifanikisha kushambulia mabomba ya mfumo wa gesi na hewa ya oksijeni na kufanya kuwe na mfululizo wa milipuko. Milipuko hiyo ilikuwa kama jehanamu inayotaka kummeza Hamza mzima mzima.
Kutokana na mlipuko ulivyotokea na eneo ambalo Hamza alipokuwa amesimama, Kanali Bird aliona kabisa ashamdhibiti mvamizi huyo na kuhusu moto, aliona kabisa hauna athari yoyote kwake kutokana na kuwa ndani ya suti.

Lakini sasa, dakika ileile Hamza alivyotoka katika lindi la moto, alikuwa na spidi ya radi na alimrukia Kanali Bird kwa kumlenga bega lake kwa nyuma.
Kanali Bird aliishia kutoa mshangao akijiuliza Hamza amewezaje kupona mlipuko ule. Licha ya kuvamimiwa kwa nyuma, aliweza kumuona Hamza vizuri kupitia kamera na kugundua hakuwa na majeraha yoyote.

Hamza hakujali mshangao wa mwanajeshi huyo. Kutokana na spidi yake aliyoruka, aliweza kutua vyema katika bega lake na kisha kwa mikono yake yote alishika lile helmeti na kulivuta kwa juu huku akinguruma kama simba.
Kanali Bird alishindwa kujua Hamza alikuwa akitaka kufanya nini, lakini dakika ileile ishara ya hatari ilianza kujionyesha katika suti yake.
“Shit!!”

Kabla hata hajachukua hatua, Hamza aliweza kunyofoa lile helmeti kwa juu na kusababisha cheche nyingi mno.

Uso uliopauka wa Kanali Bird hatimaye uliweza kuonekana wazi bila helmeti. Alikuwa katika hali ya mshituko wa matendo ya Hamza na kumfanya ashindwe hata kuongea neno zaidi ya kumwangalia kama kiumbe cha kutisha.
“Bila ulinzi wa hili helmeti lako, huwezi kufanya chochote,” aliongea Hamza.
Monster… You’re a monster, just where did you come from?” aliongea kwa sauti ya kitetemeshaji.
Selaphinii!” aliongea Hamza.
“Wewe ni…” Macho ya Kanali yalimtoka lakini Hamza hakumchelewesha kwani kabla hata hajamaliza sentensi yake, Hamza alimshambulia kwa kumlenga kichwani na palepale kichwa kiligeuka kifusi cha nyama.

Kabla Kanali hajadondoka na suti yake ya chuma, Hamza alipiga sarakasi murua kabisa na kudaka kile kiboksi kilichokuwa kwenye mikono yake. Kisha, kwa spidi ya hali ya juu, alijirusha nje ya maji kupitia mlango wa dharura wa kujiokoa na manowari ile ililipuka palepale.

Upande wa kisiwani Chole, mawasiliano yalikuwa yamerudishwa, na meli nyingi zilizokuwa mbali zilisogea kiswani hapo na kukizunguka, huku kazi kubwa ya kuzima moto na kurudisha hali katika utulivu ikifanyika kwa spidi kubwa sana.

Upande wa Yulia, yeye alikuwa ndani ya CR ya kijeshi akiendelea kurekebisha mifumo iliyoathirika. Herbert alikuwa amesimama kando ya Yulia akiwa na uso usioelezeka na alikuwa akimsumbua Yulia kwa maswali ya kutaka kujua ni wapi Hamza alipo.

“Umempeleka wapi? Au umetumia Space Warp device?” aliuliza, lakini Yulia aliendelea na shughuli zake huku akimpotezea.

“Yulia, hivi unajua unakiuka sheria? Nani karuhusu ubadili mpango mzima wa majaribio?” Herbert alibweka na kumfanya Yulia kuhisi kama ngoma zake za masikio zinataka kupasuka.

“Unatoa wapi muda wa kunipigia makelele? Kwanini usifikirie namna ya kwenda kujielezea kwa wakubwa? Si ni wewe uliefanya maamuzi ya kukabidhi Earth Axis kwa adui.”

“Acha kunisingizia, sijafanya kitu kama hicho,” alijitetea.

“Kuna ushahidi na ushahidi, ni bure tu hata ukijifanya kuwa mjanja.”

“Huo ushahidi umetoka wapi? Yulia, acha kunisingizia kitu ambacho sijafanya,” aliongea huku akiwa na wasiwasi.

“Ushasahau ndani ya hii kambi kuna umeme wa dharura, kila kitu ulichofanya katika lift ya dharura kimerekodiwa na kamera, na kwa taarifa yako, bodigadi wako Pima bado yupo hai. Ijapokuwa ulimsariti, lakini bahati ilikuwa upande wake. Hamza alimsaidia.”

“Nini!?” Herbert uso uligeuka na kuwa mkaa palepale na ishara ya chuki iliuvaa uso wake.

“Vipi, unataka kunishambulia ili kuua ushahidi?” aliuliza Yulia mara baada ya kuona mabadiliko ya Herbert na kuona nia yake.

“Kama unataka kuniua sawa tu, ila nikwambie kila kitu kilichotokea hapa kitafika makao makuu. Hata kama uamue kumuua Pima na mimi, ni bure tu.”

Jasho lilianza kumtoka Herbert mfululizo huku akionyesha tabasamu la unyonge.

“Yulia, tumefahamiana kwa muda mrefu na tumefanya kazi pamoja. Sio hivyo tu, nishawahi hata kuwa mchumba wako. Naomba ulipotezee hili swala na lisiende makao makuu. Ukinisamehe katika hili, naahidi nikija kuwa mrithi wa babu, utapata faida kubwa sana.”

“Kama hutaki kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, ondoka mbele yangu mara moja nikiwa nakuruhusu na usije kunisumbua tena,” aliongea Yulia.

Herbert alihisi kudhalilika sana lakini hakuwa na chakufanya zaidi ya kinyonge kuondoka ndani ya eneo hilo. Lakini wakati huo, mwanajeshi aliingia kwa haraka.

“Naripoti Afande…” Mwanajeshi huyo alitaka kutoa ripoti kwenda kwa Afande Herbert lakini mara baada ya kuona sura yake ilivyo, alimpotezea na kisha alimsogelea Yulia.

“Kanali Yulia, rada yetu imeweza kunasa uwepo wa manowari inayosogelea upande wa kaskazini-magharibi mwa kisiwa,” aliongea.

Herbert mara baada ya kuona mwanajeshi huyo akimpita na kutoa taarifa hiyo moja kwa moja kwa Yulia alijikuta akizidi kukunja sura. Ilionyesha dhahiri kila mwanajeshi aliye kuwa katika kisiwa hicho alikuwa akimdharau na cheo chake cha kusimamia kila kitu kuhusu majaribio hayo kimeenda moja kwa moja kwa Yulia.

“Ni manowari yetu?” aliuliza Yulia.

Tumethibitisha sio moja ya manowari yetu! Kuna haja ya kushambulia?” aliuliza. Yulia alitingisha kichwa kukataa.

“Hapana! Iache isogelee fukwe, hakuna anaeruhusiwa kushambulia bila idhini yangu,” aliongea.

Ijapokuwa mwanajeshi huyo hakuelewa kwanini, alipokea maagizo hayo na kisha akaondoka. Yulia hakuwa na muda wa kuendelea kukaa ndani ya CR (Command Room) na alitoka nje na kutoa maagizo kwa jeshi la ulinzi wa majini huku wakielekea upande wa manowari inaposogelea.

Herbert macho yake yaliishia kuchanua, huku akionyesha hali ya wasiwasi. Upande wa fukwe, magharibi mwa kisiwa hicho, wanajeshi walikuwa washajipanga tayari kwa kila aina ya siraha kushambulia. Yulia alikuwa ameshafika na alikuwa amesogea karibu akiangalia uelekeo wa maji uliojaa giza. Ilichukua kama dakika kumi na tano hivi hatimaye manowari ndogo ya kijeshi ilianza kuonekana taratibu juu ya maji na funiko la juu yake lilifunguliwa na mtu aliweza kuonekana akitoka.

“Kanali, hii inaonekana si manowari ya mashambulizi licha ya kuwa ya America,” aliongea mwanajeshi mmoja. Upande wa Yulia, uso wake ulikuwa umepambwa na tabasamu.

“Amefanikiwa,” aliongea.

“Nani?” wanajeshi wote waliosikia kauli hiyo walijikuta wakishangazwa na kauli hiyo.

“Shusheni siraha zenu chini, Hamza amefanikiwa kuirudisha Earth Axis.”

Wanajeshi hao waliishia kuangaliana na palepale walimkumbuka yule mtaalamu aliemuokoa Yulia, kumbe alikuwa akiitwa Hamza.

“Kumbe ni yeye! Basi ni muda wa kumkaribisha kisiwani.”

Kundi la wanajeshi wenye vyeo vya ukapteni waliongea wakiamini maneno ya Yulia na palepale siraha ziliweka pembeni na boti zilisogezwa karibu ili kumruhusu Hamza kupanda kurudishwa ufukweni.

Upande wa Hamza, mara baada ya kutoka katika manowari hiyo, aliishia kwanza kujivuta kunyoosha mgongo kama mtu ambaye ametoka usingizini.

“Ni muda mrefu sijaendesha submarine,” alijiwazia.

Hamza alikuwa na mafunzo ya kila aina ya udereva. Alikuwa na uwezo wa kuendesha ndege, manowari, meli za kawaida, vifaru, na hata meli kubwa za kivita.

ITAENDELEA- WhatsApp: 0687151346
Mpaka lini tena kiongozi
 
SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU

MTUNZI:SINGANOJR​

SEHEMU YA 143.

Mwanamfalme wa Omani.

“Ukiona humuwezi ungana nae”​

Hamza, mara baada ya kufika nchi kavu, alitamani kucheka kwa jinsi wanajeshi walivyokuwa wakimwangalia; ilikuwa kama vile alikuwa mgeni wa heshima. Hata hivyo, hakujali sana. Palepale, alimsogelea Yulia na kumkabidhi kile kiboksi.

“Yulia, kifaa chako hiki,” aliongea.

Yulia, mara baada ya kukipokea kiboksi hicho, alibonyeza vitufe vya nywila kwenye kiboksi hicho, na palepale kwenye kijiskrini chake kiliwaka.

“Ni Earth Axis, haijabadilishwa,” aliongea Yulia kwa furaha kubwa huku akimwangalia Hamza kwa maswali mengi.

“Umewezaje kukipata? Umeiba au umewapokonya?” aliuliza.

“Sikuwa na mtu wa kunisaidia, ningeweza vipi kukiiba? Nilishindwa kupata njia nyingine, na mpaka sasa nadhani manowari yao ya nyuklia imezama kabisa. Ni ngumu kujua ni watu wangapi wataweza kupona. Ukweli, sidhani kama kuna aliyepona maana nimeharibu hata boti za kujiokoa,” aliongea Hamza huku akicheka.

“Umeizamisha manowari yao? Umefanya nini? Umeilipua na bomu?” aliuliza Yulia kwa mshangao mkubwa.

“Bomu ningetoa wapi? Nimeiharibu kwa kuipiga ngumi tu mpaka ikatoboka. Wenyewe ndio wameilipua kwa silaha zao walipokuwa wakinishambulia,” aliongea Hamza, lakini kwa upande wa Yulia, ni kama alikosa mantiki ya kuelewa kile ambacho Hamza anaongea.

“Vipi kuhusu yule mwanajeshi mwenye suti?”

“Kuhusu yule mwanajeshi, ilikuwa ngumu sana kumshambulia akiwa ndani ya suti yake ya chuma. Nilichofanya ni kumvua kofia yake ya chuma na kumuua,” aliongea Hamza.

Ijapokuwa aliongea kwa sauti ya kawaida, Yulia alifahamu fika kuwa kumkaribia mwanajeshi yule na kisha kumuua ilikuwa ni kazi ngumu sana. Yulia aliishia kumwangalia Hamza kwa macho yasiyoelezeka.

“Uwezo wako wa mapigano upo katika daraja gani?” aliuliza, na kumfanya Hamza kutoa tabasamu.

“Unataka kujua kweli?”

“Ndiyo,” Yulia hakukataa, alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua ni daraja gani ambalo Hamza yupo mpaka kuweza kuharibu manowari ya kijeshi, jambo ambalo hata wanajeshi ishirini wa kitengo cha Malibu lingekuwa gumu kwao kukamilisha.

Hamza alimsogelea Yulia na kumnong'oneza kwenye sikio, “Nitakwambia ukiniita kidume tukiwa kitandani.”

Yulia, mara baada ya kusikia kauli hiyo, hakuongea neno. Alichukua kiboksi chake na akaondoka. Hamza hakutaka kuachwa hivyo, alifuatia nyuma huku akiendelea kumwongelesha.

“Yulia, huoni kuna jambo tunapaswa kukaa chini na kuongea?”

“Hakuna,” alijibu Yulia huku akisimama na kumkodolea Hamza macho kwa namna ya ukali, na alivyoona anakaribia kukasirika, aliona abadilishe mada.

“Herbert yupo wapi?”

“Unamtafutia wa nini? Ni kweli unapanga kumuua?”

“Anapanga kuniua mimi. Kama nisipomuwahi, nitakuwa mjinga.”

“Ni mtoto wa Mzee Alfred Kijazi, makamu wa rais mstaafu, na babu yake ni Mzee Kijazi aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi Tanzania. Shangazi yake ni mke wa pili wa Tajiri Mohamed Azim, wafadhili wakubwa wa wanajeshi wa kikosi cha Malibu waliopo chini ya shirika la Hansii. Shemeji yake ni mtoto wa Mstaafu Mgweno. Kwa mzunguko huo wa nguvu, ni bora ukaachana naye tu. Najua namna sahihi ya kudili naye, usijitafutie matatizo,” aliongea Yulia na kumfanya Hamza kufikiria kwa sekunde kadhaa.

“Kwasababu umesema hivyo, basi sawa,” aliongea.

Baada ya usiku wa kunywa mvinyo na whiskey kwenda haraka, hatimaye kulipambazuka.

Habari za Hamza kuweza kuirudisha Earth Axis zilisambaa kote kisiwani kati ya wanajeshi, hatimaye zikawafikia wakuu wa serikali. Wakati huo huo, Yulia alitoa ripoti juu ya mafanikio makubwa ya majaribio ya kifaa cha Space Warper.

Wakuu walitoa maagizo juu ya miili ya wanajeshi waliofariki kuwekwa utaratibu wa kutambuliwa na kurudishwa nyumbani kwao kwa ajili ya maziko. Walioweza kupona waliendelea kubakia kisiwani kusherehekea ushindi.

Kila mwanajeshi alikuwa na furaha, na kutokana na tukio hilo, walikuwa wamekidhi vigezo vya kupandishwa cheo, kazi ambayo ingefanywa na Mheshimiwa Rais mteule.

Ijapokuwa wanajeshi wengi wa Kitanzania walipoteza maisha, lakini kitendo cha kuharibu manowari ya jeshi la Marekani na kuua wanajeshi wao waliotengenezwa maabara ilikuwa hasara kubwa sana, zaidi ya hasara Tanzania waliopata.

Haijalishi utahesabu vipi, lakini mshindi katika vita hiyo alikuwa Mtanzania. Hata hivyo, swala hilo lisingetangazwa kwa raia kutokana na misheni zote zilizokuwa zikifanyika kisiwani Chole kuwa siri ya taifa.

Hamza akiwa juu ya jiwe katika fukwe akiendelea kuvuta sigara huku akiwa ameshikilia chupa ya whiskey, aliweza kupokea simu kutoka kwa Afande Himidu, mshauri mkuu wa jeshi.

"Bosi, haha...! Nilijua tu haiwezi kuwa tatizo wewe ukiwepo. Ila niseme ilikuwa hatari sana, mwanzoni nilidhani magaidi wanaodhaminiwa na Amerika watasababisha matatizo, lakini nani angeweza kudhania wao wenyewe ndio wameingia kazini na kufanya shambulizi la kushitukiza," aliongea Himidu na kumfanya Hamza kutoa tabasamu hafifu.

"Wewe dogo ni mtundu sana, yaani unajua fika kuna kitu cha maana kama Earth Axis halafu hujawahi kuniambia?"

"Aah! Bosi, tatizo hiki kitu ni siri sana, niliona ni risk kubwa sana kwangu nikichukua hatua ya kukuambia moja kwa moja. Njia sahihi niliyoona ni kukuambia bila kuibua wasiwasi kupitia njia hii. Kitu hiki kilipotea baada ya Vita ya Pili ya Dunia nchini Sri Lanka, miaka kumi iliyopita. Wataalamu wetu wa masuala ya kiolojia ndio waliweza kukipata. Mpaka sasa kuna makisio ni kwa namna gani na nani alikificha hapa nchini. Mara nyingi nasema, kama kitu hiki kingeishia katika mikono ya Wazungu, historia ya dunia ingekuwa tofauti sana leo hii," aliongea Himidu.

"Hiki kitu kimetokea wapi, na ni kwa kiasi gani mmekifanyia utafiti?" aliuliza Hamza.

"Bosi, unapaswa kumuuliza Yulia, amekuwa akikifasiri kwa muda mrefu na hata hatujui ni aina gani ya fizikia kimebeba. Kusema ukweli, hata kama Yulia akiongea kila kitu anachokijua kuhusu hiki kifaa, sidhani kuna atakayemwelewa. Kuhusu kilipotokea, Yulia anasema kuna uwezekano kiliachwa hapa duniani na jamii za viumbe walioendelea zaidi kuzidi sisi binadamu, lakini bado hakuna njia ya kuthibitisha kama ni kweli," aliongea Himidu.

"Kwasababu umesema kitu hiki ni muhimu sana na kina faida, basi pia nina uhakika ndani yake hakuna taarifa za fizikia pekee."

"Ni sahihi kabisa, lakini kutokana na kutaka kujilinda kwanza wenyewe na kukilinda pia kitu hiki ndio maana tuliwekeza nguvu nyingi kitusaidie katika masuala ya kijeshi," aliongea.

"Nataka uwaambie viongozi wako kwamba nahitaji kujua vitu viwili pekee, na kuhusu vingine siko na shida navyo. Nataka kujua upande wa masuala ya bailojia, hususani upande wa matibabu zaidi na upande wa lugha. Kwasababu mimi ndiye niliyefanikisha kukirudisha, nadhani wataweza kuelewa nia yangu ya dhati," aliongea Hamza.

"Usiwe na wasiwasi, bosi wangu. Ukweli ni kwamba nilishajiandaa kuhusu haya maombi yako kwa muda mrefu kulingana na misheni yako iliyokuleta hapa nchini. Kama mambo yakienda sawa, naamini utaweza kupata taarifa muhimu. Halafu bosi, uko wapi kwanza? Mbona sauti ya upepo ni kubwa mno?"

"Nipo kando ya bahari, ndio maana."

"Oh! Sawa bosi. Lakini kwasababu upo hapa nchini, kwanini usijumuike na wengine wote kupokea pongezi zako?"

"Misheni bado haijaisha, kuna mtu napaswa kumuua ndio nimalize kila kitu," aliongea Hamza.

"Kuna mtu unataka kumuua? Ni nani bosi?"

Muda huo, wakati Hamza akiulizwa swali hilo, aliweza kuona mwanaume alievalia suti akiongozwa na watu kadhaa. Alikuwa akiupanda boti na alimjua palepale, jambo lililomfanya macho yake kuchanua.

"Hebert Kijazi!!" aliongea kisha alikata simu pale pale na akaanza kutembea kwa kasi kuisogelea ile boti.

Dakika chache mbele, Hamza alipokea simu, na hiyo ni mara baada ya kuona zaidi ya missed calls tano kutoka kwa Himidu.

"Bosi, usiniambie umemuua tayari?"

"Mbona kitambo," aliongea Hamza huku akigeukia upande wa boti ile na kuangalia wanajeshi walivyokuwa wakihangaika kuutoa mwili wa Hebert majini.

"Bosi, kwanini umeamua kufanya hivi? Hili lishakuwa tatizo sasa?"

"Tatizo! Kama mtu mmoja kutoka kwa familia moja nchini anaweza kuniletea matatizo, nani ataweza kunichukulia siriasi kwenye ombi langu kuhusu Earth Axis?"

"Bosi, unapanga kuondoka Tanzania?" aliuliza Himidu.

"Mimi sio raia wa Tanzania, lakini bado kilichonifikisha hapa nchini kwenu sijakimaliza. Nataka uwaambie viongozi wako kwamba mimi sio mtu mwepesi kudanganywa kwa ahadi hewa, angalau wanapaswa kuelewa nia yangu ya dhati juu ya nilichoomba. Kuhusu familia ya Kijazi na washirika wake, wewe nisaidie kudili nao," aliongea.

"Nitafanya hivyo, isitoshe mimi ndiye mtu pekee ninaweza kufanya hivyo. Wewe ni bosi wangu," aliongea Himidu na Hamza alitoa tabasamu hafifu kisha akakata simu pale pale.

Hamza mara baada ya kurudi kwenye moja ya resort ambayo imefunguliwa kwa ajili ya dharura kwa wanajeshi wa vyeo vya juu, Yulia alikuwa amekwisha pokea taarifa ya kifo cha Kanali Mwandamizi Hebert Alfred Kijazi kilichotekelezwa na mwanajeshi wa kujitegemea Hamza Mzee.

"Hamza, wewe ni kichaa!? Si uliniambia hutomgusa Hebert wewe?" aliuliza Yulia aliyetoka haraka haraka nje.

"Yulia, hebu fikiria kwa umakini kwanza, ni wapi nilikuahidi mimi? Nilisema ‘sawa’ maana yake ni kwa muda ule na sio baadae."

"Wewe... Hao vichaa wakiungana na kutaka kulipa kisasi waambie uliamua mwenyewe. Sitaki kujiingiza kwenye matatizo mimi," aliongea Yulia kwa hasira na kisha aligeuka kutaka kuondoka, lakini Hamza alimshika mkono na kumvutia kifuani na kisha kwa sauti nzito aliongea,

"Sikiliza, unaweza kuwa mpenzi wangu lakini haimaanishi nitakusikiliza kwa kila unachoniambia. Hususani likija suala la kumuua mtu, ni matumaini yangu utakumbuka kuanzia leo hii."

Sauti ya Hamza haikuwa ya kawaida kabisa, ilikuwa ikitoka na nguvu ya ajabu ambayo ilimfanya mwanamke huyo kuhisi woga mpaka kwenye mifupa.

Yulia aliishia kutetemeka huku akiikunja mikono yake kwa nguvu, lakini hata hivyo alishindwa kuongea chochote.

Hamza mara baada ya kuona onyo lake limemwingia mwanamke huyo vizuri alimwachia kisha aliweka tabasamu lake la kizembe kwa mara nyingine.

“Babe Yuli, unaonaje tukiingia ndani? Nasikia wanajeshi wote wananiona kama shujaa wao. Hebu twende tukaungane nao kusherehekea ushindi,” aliongea Hamza.

SIKU MOJA BAADAE, KOROGWE - TANGA

Familia ya mzee Kijazi haikuwa ya kawaida hata kidogo kwa utajiri waliokuwa nao. Haikuwa tu na ushawishi mwingi nchini kwa kujishikiza katika familia zenye nguvu, lakini vilevile ilikuwa na uwekezaji mkubwa.

Katika makazi ya kifamilia ndani ya Wilaya ya Korogwe, familia hii ilikuwa na eneo ambalo lilikuwa na ukubwa wa kijiji na kulikuwa na nyumba nyingi sana. Kama ilivyo sheria ya ukoo wao, kila mwanafamilia kabla ya kujenga nyumba nje ya nyumbani, anapaswa kwanza kujenga nyumba yake ndani ya eneo hilo. Ndio maana eneo hilo lilikuwa kama kijiji kwa nyumba nyingi ambazo zote zilikuwa za hadhi.

Tofauti na siku zote, siku hiyo ndani ya eneo hilo kulikuwa tofauti sana, na hiyo yote ni kutokana na kufika kwa taarifa za msiba wa kijana Hebert Alfred Kijazi. Taarifa hizi za msiba zilifanya wanafamilia karibia wote kusafiri kuja ndani ya mji wao waliozaliwa kwa ajili ya msiba. Lakini hata hivyo, asubuhi hiyo kulikuwa na kikao cha kifamilia kilichokuwa kikiendelea ndani ya eneo hilo. Kikao hicho kilikuwa na ajenda juu ya namna kifo cha Hebert kilivyotokea. Hebert kuuliwa na Hamza haikuwa siri tena, ni habari ambayo iliwafikia wanafamilia wote na hawakutaka kuona suala hilo linapita hivi hivi, ukizingatia Hebert alikuwa tegemeo kubwa kwa familia hiyo kurithi nafasi ya uongozi.

Katika ukumbi mkubwa ambao mara nyingi hutumika kupokelea wageni, mwanaume mzee mwenye mvi nyingi kichwani alievalia koti la suti ya ugoro alikuwa amekaa mbele kabisa ya kiti kikubwa. Mwonekano wake ulikuwa wenye umakini wa kitaadhima. Mwanaume huyo mzee ndiye alifahamika kwa jina la Kijazi, Kamanda mstaafu wa jeshi la Tanzania.

Ukumbi huo ulikuwa umejaa harufu nzuri ya kuvutia pua na kulikuwa na wahudumu wawili waliosimama kulia na kushoto karibu na mzee huyo.

“Baba!!”

Muda ule sauti ya mwanaume iliita. Alikuwa ni Afredi Kijazi, Brigedia mstaafu na pia makamu rais mstaafu.

“Afredi, umekuja?”

“Ndio baba, nimekuja kwa haraka baada ya kupokea taarifa ya Hebert mwanangu kufa kifo kibaya sana kwenye mikono ya mtu asiyefahamika. Kitendo hiki ni uchokozi wa wazi kwa familia yetu lakini vilevile ni uvunjifu wa kanuni za Tanzania,” aliongea yule mwanaume na kisha alikaa chini akimwangalia baba yake ambaye alionekana kuwa na utulivu wa hali ya juu.

“Baba, makamanda wengi ndani ya jeshi wapo upande wetu. Nipe ruhusa yako na nitaenda kumkamata huyu mwanaharamu anayefahamika kwa jina la Hamza na nitamchuna ngozi mbele ya ndugu zetu wote walioguswa na kifo cha Hebert.”

“Alfredi, umeshakuwa mwanajeshi kufikia cheo cha Brigedia lakini vilevile umekuwa makamu wa Rais kwa kipindi chako. Kwanini bado unakosa utulivu wa kimaamuzi? Unamwita huyu mtu asiyefahamika, kama kweli huyu Hamza hajulikani, unadhani imekuwaje viongozi wa juu wa jeshi wakamwidhinisha kwenda kiswani kwa ajili ya kufanya kazi ambayo Nyakasura alipaswa kufanya? Kubwa zaidi, Himidu amenipigia simu na yupo njiani kuja kuongelea hili suala. Unadhani Himidu ni mtu mwenye muda wa kutoka Dodoma na kusafiri mpaka Tanga kwa ajili ya mtu asiyefahamika?”

“Nini? Baba, unasema Afande Himidu anakuja? Kama ni hivyo, ni vizuri. Nipo tayari kumsikiliza ni kitu gani ataongea. Mimi Mzee Alfredi nina watoto wa kiume wengi lakini Hebert ndiye mtoto wangu wa kwanza.”

“Upo sahihi, Alfredi. Tutahakikisha huyu mtu anaitwa Hamza analipa kwa alichomfanyia Hebert, tena kwa damu,” sauti ya mwanamke ilisikika na alienda moja kwa moja kumkumbatia Alfredi kwa nyuma.

Alikuwa ni mwanamke mrembo kweli mwenye ngozi nyeupe.

“Salome, unafanya nini hapa? Hujui hii sio sehemu yako kama mwanamke?” aliongea Alfredi.

Salome alikuwa ni mke wake Alfredi lakini vilevile alikuwa ni binamu yake. Wenyewe wanasema binamu ni nyama ya hamu, ndivyo ilivyokuwa kwa Alfredi aliyemuoa binamu yake.

“Yaani mwanangu amekufa, nianze kujali nani anapaswa kuingia hapa na nani haingii? Mtoto wako amekufa lakini huna huzuni yoyote?” aliongea mwanamke yule, ilionekana ni dhahiri alikuwa akilia siku nzima kutokana na macho yake kuvimba.

“Mshauri mkuu akifika unaweza kuja, sasa hivi kuna mambo nataka kuongea kwanza na baba,” aliongea na palepale yule mwanamke alianza kutoa kilio huku akipiga magoti.

“Baba, naomba ulipize kisasi kwa ajili ya mwanangu. Hebert ndiye mtoto wangu aliyekuwa akinijali kuliko watoto wangu wote. Ndio mtoto aliyekutembelea mara kwa mara na kukufanya ucheke muda wote,” aliongea kwa kilio na kumfanya Mzee Kijazi macho yake kushikwa na unyevunyevu wa machozi.

“Salome, nenda kwanza kapumzike, nitakuipa maelezo ya kutosha baadaye,” aliongea yule mzee.

Muda uleule wale wahudumu walimchukua yule mwanamke na kutoka naye na kufanya eneo hilo kutulia tena.

“Baba, ina maana mpaka sasa hivi Mtemi na Msafiri hawajafika tu? Yaani mwanangu amefariki halafu wao wanakuja kwa kujivuta au hawajali?” aliongea.

“Mimi ndio niliowaambia wasisogelee hili eneo, kwa sababu Mshauri mkuu anakuja, kuna baadhi ya taarifa za siri hawapaswi kusikiliza,” aliongea na bwana yule alielewa. Isitoshe, yeye na baba yake ndio ambao walikuwa wamewekeza zaidi katika kuwa na ushawishi mkubwa serikalini huku ndugu zao wengi wakiwa ni wafanyabiashara walioelemea zaidi upande wa Azim.

Kwa lugha nyepesi, Alfredi na baba yake ndio ambao walikuwa na ukaribu zaidi na familia ya Mstaafu Mgweno, huku wengine wakiwekeza mahusiano yao makubwa na familia ya kihindu ya Tajiri Azim.

Muda huo taarifa ilitolewa juu ya ujio wa Afande Himidu, na Mzee Kijazi alitoa ruhusa ya kuruhusiwa aingie.

Kijana aliyevalia kombati za kijeshi na kofia alionekana akikaribia eneo hilo huku akiwa na tabasamu usoni. Alipofika karibu, alitoa saluti kwa Mzee Kijazi.

"Mzee Kijazi, Makamu mstaafu, naomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza," aliongea kwa heshima.

"Karibu sana, Mshauri Mkuu. Tunajua wewe ni mtu bize sana, hata kwa mwaliko ni ngumu kufika hapa," Alfredi aliongea kwa heshima, akimkaribisha Kamanda Himidu.

"Tafadhali keti, Afande," Mzee Kijazi alimkaribisha.

Kamanda Himidu aliketi, na mfanyakazi aliagizwa kumletea chai. Baada ya kumiminiwa kikombe cha chai ya maziwa, aliinywa kwa utulivu mkubwa, akionekana hana wasiwasi kabisa.

"Chai nzuri sana hii, napenda sana nikija usambaani kunywa chai yenye viungo vizuri kama hii," Kamanda aliongea huku akimtabasamisha Mzee Kijazi.

"Ni maalumu kwa mgeni mzito kama wewe. Mshauri Mkuu, upo bize sana na mambo ya serikali mpya. Kama una jambo la kusema, jisikie huru, tupo hapa kukusikiliza," Mzee Kijazi alimkaribisha.

"Asante sana kwa ukaribisho, Mzee Kijazi na Makamu mstaafu. Natoa pole ya dhati kwa kuondokewa na kijana wenu," Kamanda Himidu aliongea kwa huzuni.

"Pole haiwezi kutusaidia. Tunachotaka ni maelezo ya kujitosheleza," Makamu mstaafu aliongea kwa hasira kidogo, na Kamanda Himidu alitabasamu hafifu.

"Sidhani kama itatosha kusikiliza maelezo ya upande mmoja tu kutoka kwangu. Ndio maana nimekuja na wageni wawili ambao wanamjua Hebert vizuri. Nafikiri itakuwa rahisi kuwaelewa wakielezea kilichotokea kuliko mimi," Kamanda Himidu aliongeza.

"Oh! Hakika, Mshauri Mkuu, unaonekana umejiandaa vyema. Lakini wageni hao ni akina nani?" Mzee Kijazi aliuliza kwa mshangao, na wakati huo huo, wageni walifika.

"Naripoti, Kamanda kiongozi mwakilishi wa kikosi namba 09455 na mwalimu mwakilishi wa Shirika la Hansii nchini Tanzania, Afande Adamson Ngasinda na Kamanda Pima Kichele wapo hapa kutoa salamu," Mwanajeshi mmoja alitoa taarifa hiyo.

"Afande Ngasinda na Kamanda Pima kwanini wapo hapa?" Alfredi aliuliza kwa mshangao.

Afande Adamson Ngasinda, aliyevalia kanzu ya kahawia na kibakrashia, akiambatana na Afande Pima Kichele, waliingia ndani ya ukumbi huo. Pima alikuwa amevalia mavazi ya kawaida, huku Ngasinda akiwa Kamanda kiongozi wa kambi ya mafunzo ya kijeshi ya tawi la Hansii hapa Tanzania, na Pima alikuwa mwanafunzi wake aliyesomea kwenye kambi hiyo.

"Mzee Kijazi, tuwie radhi kwa kuingilia kikao chako," Afande Ngasinda aliongea kwa heshima.

"Kamanda kiongozi, kuna kilichotokea kambini? Familia yetu na kambi yako ya mafunzo tuna ushirika mkubwa sana, na Azim Mkwe wetu ndio wafadhili wakubwa. Ijapokuwa kuna utofauti wa vipaumbele baina yetu, bado tunachukuliana kama ndugu," Mzee Kijazi aliongea kwa kujiamini.

"Ndio maana nimetangulia kuomba radhi, Mzee wangu. Sipo hapa kama kiongozi bali nimemsindikiza Afande Pima Kichele, ambaye alikuwa bodigadi wa Hebert. Yeye ndiye anayejua vizuri kuhusu kifo cha Afande Hebert. Mshauri Mkuu ameona ni jambo la busara kama tutatoa mwongozo sisi wenyewe," Kamanda Ngasinda aliongea kwa busara.

"Nimepatiwa taarifa kuwa Afande Pima ni mmoja wa wanajeshi wetu wenye uadilifu mkubwa ndani na nje ya mafunzo, na hawezi kuongea uongo. Naomba mumsikilize kile atakachokwenda kuelezea," Kamanda Himidu aliongea, na wazee hao walishangazwa.

"Pima, nakujua vizuri. Umekuwa chini ya Hebert kwa zaidi ya miaka saba sasa kama sikosei. Huna haja ya kuwa na wasiwasi wa kuelezea kile kilichotokea kisiwani," Makamu Alfredi aliongea kwa kumtuliza Pima, ambaye alianza kuelezea namna Hamza alivyotambulishwa na Yulia kama mpenzi, pamoja na jinsi Hebert alivyomshauri kushindana na Hamza kuendesha boti na matukio mengineyo.

Mpaka Pima anamaliza kuelezea, Mzee Kijazi alikuwa amefura kwa hasira. Hakuamini kuwa mtu aliyemwona kama mrithi wake alikuwa amemdhalilisha kiasi hicho. Kitendo alichokifanya Hebert, yeye kama mwanajeshi mstaafu, alikiona kama aibu kubwa.

Kwa namna moja, yeye kama mwanajeshi mstaafu aliona ilikuwa sahihi kwa Hebert kuuawa.

Baada ya Kamanda Ngasinda na Pima kuondoka, Mzee Kijazi alimwangalia Himidu kwa tabasamu lenye wasiwasi kidogo.

"Kama nilivyosema, Mshauri Mkuu, siko zote ni Mshauri Mkuu. Umetufundisha somo ndani ya dakika chache ulizofika hapa," Mzee Kijazi aliongea kwa kutambua.

"Mzee Kijazi, ilinilazimu sana. Nilitumainia swala hili linakuwa wazi kwenu wote. Ijapokuwa Hamza alikurupuka katika matendo yake, lakini kama mlivyoona, kuna sababu iliyokuwa nyuma yake. Kama marehemu asingefanya haya yote, asingepatwa na umauti," Kamanda Himidu alielezea kwa kina.

"Upo sahihi, lakini hata kama mjukuu wangu alikuwa na hatia, sheria ya jeshi ndio ilipaswa kuchukua mkondo wake. Isitoshe pia alikuwa mwanajeshi. Huyu Hamza kuchukua jukumu la kumwadhibu mwanajeshi wetu, je, ni sawa?" Mzee Kijazi aliuliza kwa mkazo.

"Inaonekana, Mzee, bado haupo radhi kumwachilia Hamza katika hili kirahisi?"

"Bila shaka, ijapokuwa Hamza alikuwa na sababu ya kumuua Hebert, lakini haimaanishi kwamba sheria inaruhusu."

"Kwa mtazamo huo, Mzee Kijazi, unadhani ni hatua gani tunapaswa kuchukua?" Kamanda Himidu aliuliza kwa uangalifu.

"Rai yangu ni yeye kukamatwa na kuhojiwa kulingana na sheria za jeshi, kisha hukumu itolewe dhidi yake," Mzee Kijazi aliongea kwa msisitizo, na Kamanda Himidu alitabasamu kidogo.

"Mzee, kama kuna mtu ambaye vitengo vyetu vya kijeshi hata vikiungana haviwezi kumkamata, ni huyu Hamza. Wasiwasi wangu ni kwamba, Mzee wangu, humjui vizuri huyu mtu yupoje na matokeo yake ni nini kama tutaamua kumkamata."

"Hata kama uwezo wa Hamza unalingana na wa Nyakasura, sidhani anao uwezo wa kupita kwenye vyuma vya magereza yetu," Makamu aliongea, lakini Kamanda alitingisha kichwa, akionyesha kutokubaliana nao.

"Je, mnajua siku kadhaa zilizopita kulitokea mzozo kati ya serikali yetu na kundi namba moja duniani la kiharamia, Sea Demons?"

"Nilisikia kuhusu habari hiyo, lakini si aliondoka mwenyewe karibu na mpaka wetu?" Makamu aliuliza kwa mshangao.

"Ukweli ni kwamba Sea Demons sio watu kabisa ambao nilitaka kujihusisha nao, na sidhani kama ingekuwa rahisi hata kama ningeenda. Badala yake, ni mimi niliemuomba Hamza kuingilia hili suala, na ndipo Leviathan alivyoondoka mwenyewe."

"Kumbe! Inaonekana huyu Hamza ana koneksheni kubwa?" Mzee Kijazi aliongea kwa mshangao, akitambua nguvu ya kundi la maharamia hao.

"Je, mshawahi kusikia ni umoja gani ambao huyu Leviathan anatokea?" Kamanda Himidu aliuliza kwa tahadhari.

"Hilo si gumu kwangu. Huyu Leviathan si anatokea umoja uliokufa wa Inferno? Umoja wa kimizimu uliokuwa kama hadithi ya kufikirika?" Makamu aliuliza, akionyesha ujuzi wake wa masuala ya kijeshi.

Mzee Kijazi alitingisha kichwa kuashiria kuwa anafahamu vizuri hilo, akionyesha kuunga mkono alichoongea mtoto wake.

"Kama ni hivyo, nadhani ni swala la kufikiria kwa kina na kujiuliza, ni nani awezae kumwamrisha mnyama ngisi kama Leviathan na kumwitikia kwa heshima?" Aliuliza, na swali hilo lilimfanya Mzee Alfred kumwangalia baba yake. Baada ya wote kutafakari, macho yao yaliwachanua.

"Unamaanisha huyu Hamza ni…?" aliuliza kwa mshangao.

"Mzee Kijazi, nakumbuka wakati ukiwa mkuu wa majeshi, hata rais aliyekuwa madarakani alikuwa akikuogopa kwa uwezo wako, na nadhani unajua ninachomaanisha," Kamanda aliongea huku akimgeukia Mzee Alfred.

"Makamu, nadhani sasa unajua kwa nini nilitoa maagizo ndani ya kitengo chetu kusitisha mara moja uchunguzi wote unaoendelea dhidi ya Hamza. Hii yote ilikuwa ni sababu ya kutotengeneza uadui. Wahenga wanasema, kama humuwezi, ungana naye. Ukweli ni kwamba, kama Hamza angekuwa jinsi ninavyomjua, isingeishia tu kwenye kifo cha Hebert bali kwa familia nzima," aliongeza kwa tahadhari.

SEHEMU YA 144.

iku tatu baada ya mapambano na sherehe kuisha, Hamza kwa mara nyingine aliweza kurudi mjini akiwa na amani kabisa, baada ya kupokea habari kutoka kwa kijana wake, Afande Himidu, kwamba familia ya Kijazi wamesitisha kisasi chao kwa muda. Hii ilimpa utulivu wa akili Hamza.

Kubwa zaidi, Himidu pia aliwasilisha pendekezo la Hamza la kuweza kushughulishwa katika masuala ya sayansi ya tiba na bailojia kupitia Earth Axis, pamoja na teknolojia ya lugha. Pendekezo hilo lilikaliwa kitako kujadiliwa, na makubaliano yangeamuliwa, lakini Hamza alipewa tahadhari kwamba haitakuwa bure.

Hamza hakujali sana gharama ya aina gani atakayoilipa. Mpango wake ulikuwa ni kukubali dili hilo na serikali, kwani kulikuwa na kila hisia kwamba pengine kuna uwezekano wa mambo yote yanayoendelea kutokea, kama vile suala la kupata zile Fuwele na kupambana na yale masanamu, vilevile suala la Earth Axis na ndoto zake, yana muunganiko na mtu anayemtafuta, yaani Mzee.

Aliamini pengine katika Earth Axis pia angeweza kupata teknolojia kubwa ya lugha na kutafsiri vitu ambavyo Dokta Genesha amemhusisha navyo.

Hamza, mara baada ya kushuka kwenye boti, wanajeshi walimsindikiza mpaka nje, lakini yeye mwenyewe alikataa wasimpeleke mpaka nyumbani kwake. Alichukua usafiri uliompeleka moja kwa moja nyumbani, ambapo Regina hakuwa amesafiri bado kwenda Ulaya kwa sababu Hamza alipata majukumu mengine, hivyo ni kama alimsubiria.

Hamza, baada ya kufika nyumbani, alijua fika hawezi kumkuta Regina maana ilikuwa ni siku ya kazi na ni mapema sana.

Mara baada ya kuingia ndani ya nyumba, alipokelewa na Shangazi ambaye alikuwa bize akiangalia marudio ya tamthilia.

"Hamza, karibu. Hatimaye umerudi," aliongea Shangazi.

"Shangazi, unaonekana kuwa na furaha sana kurudi kwangu, kwani nimekaa sana?"

"Kurudi kwako ndiyo kupunguza wasiwasi wangu. Hujui tu, lakini Regina tangu juzi amekunja sura na kununa siku nzima. Nimemuuliza nini tatizo lakini haongei. Asubuhi ya leo hata kifungua kinywa hakujihangaisha nacho na alienda kazini hivyo hivyo. Nipo najiuliza, au kuna kitu kilichotokea baina yako na mkeo?" aliongea na kumfanya Hamza kukuna kichwa.

"Hapana, tangu tuachane nje ya kampuni sijawasiliana naye kabisa."

"Au amenuna kwa sababu hujampigia simu?" Aliuliza Shangazi na kumfanya Hamza kuona pengine inawezekana. Isitoshe, wakati alipokuwa kisiwani alikuwa bize mno na Yulia pamoja na wanajeshi, kunywa na kujivinjari, na kumsahau kabisa Regina aliyemuacha nyumbani.

"Shangazi, ngoja baadaye nitamwandalia chakula kitamu ili akirudi nimbembeleze," aliongea Hamza, na Shangazi aliona ni sahihi kabisa. Hivyo, baada ya kumaliza kuangalia tamthilia, alimsaidia Hamza kumpa mapendekezo ya vyakula ambavyo Regina anapendelea.

Saa kumi na mbili na nusu hivi ilifika, lakini Regina bado hakuwa amerudi. Shangazi aliona afadhali ampigie simu amuulize anarudi saa ngapi, lakini jibu alilopata lilimshangaza.

"Hautorudi mapema na utakula huko huko? Hamza amerudi na amekuandalia chakula kitamu... oh, kumbe! Ni yule mwanaume wa jana... sawa sawa basi, kuwa makini," aliongea Shangazi na kisha akakata simu.

"Shangazi, Regina anasemaje?" aliuliza Hamza.

"Anasema hatorudi mapema, hivyo tusimhesabu kwenye chakula cha usiku. Ana marafiki wake wa chuo, anasema wanakutana," alijibu Shangazi huku akiwa na mwonekano usioelezeka.

"Unamaanisha nini? Ina maana hata jana hakurudi?" aliuliza Hamza kwa wasiwasi.

"Jana alikuwa na rafiki yake ambaye alikuwa akimchukulia kama kaka kipindi akiwa chuoni. Jana Fabi ndiye aliyemrudisha Regina nyumbani maana alikuwa kidogo amelewa," alieleza Shangazi, na Hamza alijua ni nani anayezungumziwa.

"Huyu mshenzi ananitafuta, anathubutu vipi kujenga ukaribu na mke wangu?" aliwaza Hamza huku akikunja sura. Kilichomfanya achukie zaidi ni pale aliposikia jana Regina alirudishwa na Fabiani.

"Shangazi, unajua ni sehemu gani wanaenda?" aliuliza Hamza kwa haraka.

"Unataka kufanya nini, Hamza? Regina sio mtu wa kukurupuka. Nina uhakika ameona tu aibu ya kumkatalia. Isitoshe, Fabiani pia sio mtu mbaya, ndiye aliyekuwa karibu na Regina wakati wake wa chuo."

"Hiyo ilikuwa wakati alipokuwa mwanachuo, lakini sasa hivi amekwisha kuwa mke wangu. Hawezi kukutana tu na watu, hususani wa kiume, bila mimi kujua," aliongea Hamza kwa msisitizo, na bila kujiuliza mara mbili, alitoka nje kwa hasira.

Hamza alijiambia kuwa hata kama Shangazi hajui wapi Regina anakutana na huyo Fabiani, yeye atampata tu. Shangazi aliishia kuangalia chakula kilichoandaliwa mezani huku akiona masikitiko kwa jinsi Hamza alivyokuwa akitokomea nje.

Downtown ndani ya jiji la Mzizima, unapatikana mgahawa maarufu wa Jacaranda. Ulikuwa ni mgahawa wa Kifaransa ambao wateja wake ni wale wa miadi pekee, na gharama ya chini kwa mtu mmoja kupata huduma ni laki tatu, na hapo huenda usile kabisa chakula, ukaishia kunywa juisi tu.

Wahudumu wote wa mgahawa huo walikuwa ni raia wa kigeni na ambao wamesomea kabisa kazi hiyo na kuwa na uwezo wa kuongea lugha ya Kifaransa. Eneo la maegesho nje ya mgahawa huo lilikuwa na sehemu hamsini tu za kuegesha magari, na karibu yote yaliosimama hapo yalikuwa ni ya thamani ya kiasi cha milioni mia moja za Kitanzania. Hakukuwa na gari la chini ya milioni mia moja, kulikuwa na McLaren, Lamborghini, Ferrari, na magari mengine ya kuvutia macho.

Katika eneo hilo la maegesho alionekana mwanaume mrefu aliyevalia suti ya rangi nyeupe na tai ya rangi nyekundu. Alikuwa mtanashati, mwenye mwili uliojengeka kimaozoezi, na kila dakika alikuwa akiangalia saa yake ya mkononi ya Rolex, akionekana dhahiri kabisa kwamba kuna mtu anamsubiria.

Nyuma yake walikuwa wamesimama mabodigadi wawili waliovalia suti nyeusi.

Hazikupita dakika nyingi, gari ya kifahari iliingia ndani ya eneo hilo. Ilikuwa ya rangi nyeusi metallic yenye umbo la kuvutia mno, huku tairi zake zikiwa zimenakshiwa na madini ya dhahabu. Ngurumo ya injini yake ilitosha kuijitambulisha kuwa ni gari kali zaidi ya mengi yaliyokuwa katika eneo hilo la maegesho.

Baada ya gari hiyo kuegeshwa, mwanamke mrembo sana mwenye nywele ndefu za kujiachia alishuka. Alikuwa amevalia koti la camel-colored frock coat refu lenye vifungo vipana, huku mkononi akiwa ameshikilia mkoba wenye mkanda wa platinum.

Dakika ambayo mwanaume alimwona huyu mwanamke, kivuli cha utu wake kilimfanya macho yake kuchanua, akimeza mate mengi na kupata hisia za furaha za kumpokea mwanamke mrembo kama huyo.

"Regina, hatimaye umefika," aliongea yule mwanaume kwa tabasamu.

Regina, mwanamke mrembo, alimwangalia mwanaume huyo na kisha bila kubadili mwonekano, alitingisha kichwa.

"Senior, mbona kama upo mwenyewe, wenzetu wapo wapi?" aliuliza Regina.

"Wamenitaarifu wapo bize na hawataweza kufika, lakini hakuna kilichoharibika. Nimeweka miadi ya nafasi nne, lakini sio mbaya zikiwa bure zitatusindikiza," aliongea kwa tabasamu.

Regina aliishia kukunja sura na kidogo alionekana kutokufurahi. Hakuwa mjinga; ilikuwa wazi kabisa kwamba Fabiani hakumwalika yoyote bali alitumia janja ili tu kula naye chakula cha usiku. Lakini kwa sababu alikwisha fika, aliona haitakuwa vizuri kugeuza na kuondoka. Regina ashazoea tabia za watu wengi, hivyo alikuwa vizuri kujizuia. Alijiambia kwamba wakati mwingine ni vyema kuvumilia kidogo jambo kama lilivyo na litapita.

“Sawa basi, tunaweza kuingia,” aliongea. Palepale, Fabiani alijiongeza na kumsogelea Regina karibu huku akimpa ishara ya kumpatia mkoba wake.

“Senior, unataka kufanya nini?”

“Nilitaka kukusaidia kubeba mkoba wako,” aliongea Fabiani kwa kujiamini bila kubadili sauti yake.

“Haina haja, nitabeba tu.”

“Haha… Regina hujabadilika kabisa, unapenda sana kujitegemea kwenye mambo mengi. Sidhani ndio maana kulikuwa na wanaume wengi waliokuwa wakikufukuzia lakini hakuna hata mmoja aliefanikiwa,” aliongea Fabiani kwa sauti ya utani.

Muda huo, wawili hao waliingia ndani ya mgahawa huku Fabiani akiwapa ishara wale mabodigadi kuhakikisha hakuna mtu mwingine kuingia.

“Fabiani, wewe ni mwanajeshi, kuna haja ya kuwa na mabodigadi?” aliuliza Regina.

“Huwa muda mwingine inachosha kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja. Sijawachukua kwa ajili ya kunilinda, ila kuzuia usumbufu. Halafu sio mimi niliowaleta, ni Master wangu.”

“Master wako?”

“Ndio, namaanisha mwalimu wangu wa kambi ni Kamanda kiongozi wa kambi ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi,” aliongea huku akimwangalia Regina kuona mabadiliko yake.

“Oh!” Regina hakufatilia sana kuhusu hilo zaidi ya kupepesa macho yake mazuri.

Fabiani aliona kabisa Regina hakuwa na hisia zozote juu yake, hivyo aliishia kutotoa tabasamu tu na kupadili topiki.

“Regina, ile gari uliokuja nayo ni ya kwako?”

“Ndio.”

“Niliona jana hukuiendesha?” aliongea na muda huo wote kwa pamoja walikuwa wameshafika katika siti zao na kukaa chini.

“Kwa sababu jana wewe ndio ulienirudisha nyumbani. Ile Maseratti tuliacha palepale hotelini na sikutuma mtu kuichukua, ndio maana nimekuja na lingine.”

“Haha… wewe kweli ni mmiliki wa kampuni ya Dosam. Ile gari ni nzuri sana, nimeipenda na napanga kuinunua,” aliongea, na Regina alikunjwa kidogo juisi ya Lemonade.

“Kuhusu ile gari, Senior huwezi kuinunua?”

“Kwanini? Unadhani siwezi kuwa na hela ya kuinunua? Haha, ijapokuwa ni kweli siwezi kulingana na wewe kwenye swala la hela, lakini familia yangu haipo vibaya kiuchumi,” aliongea.

“Ile gari imetengenezwa kwa oda maalumu na mpaka sasa yapo matatu tu duniani. Nilipewa kama zawadi na Prince wa Omani. Nilimkatalia kuipokea lakini akanigomea haipokei. Nilichokifanya nikamwingizia dola milioni nne kwenye akaunti yake na ikaishia hapo. Labda mtu awe tayari kukupatia kwa hiari yake vinginevyo huwezi kuinunua hata kama una hela,” aliongea Regina na kumfanya Fabiani kutoa macho.

“Dola milioni nne?”

“Ndio. Thamani yake kawaida ni milioni tatu na nusu. Mimi nilimpa nne kwa sababu sikutaka kuwa na deni la fadhila kutoka kwake, ndio maana nikaongeza hela ya ziada,” aliongea Regina na kumfanya Fabiani kuona pumzi anayovuta ina ubaridi sana. Aliishia kumwangalia Regina na mwonekano usielezeka.

Ijapokuwa alijua tokea mwanzo Regina ni tajiri, lakini kitendo cha kutokujua muundo wa gari ile kilimfanya aonekane kama mshamba. Lakini hata hivyo, swala hilo halikumfanya Fabiani kukosa kujiamini. Badala yake, ilimpa nguvu ya kimatamanio zaidi juu ya Regina. Isitoshe, mpaka mwanamfalme wa Omani kutaka kumhonga Regina hiyo gari maana yake hakuwa mwanamke wa kawaida. Palepale alijiambia lazima amfanye mrembo huyo kuwa wake kwa namna yoyote.

“Senior, mbona hutoi oda zetu?” aliuliza Regina. Alikuwa amekosa uvumilivu na alitaka kula haraka haraka na kisha aondoke.

Fabiani alijikuta akianza kubabaika na palepale aligeuka na akamwita mhudumu. Ili kujichokulia pointi kadhaa, aliamua kutumia lugha ya Kifaransa.

Kitendo cha Regina kusikia Fabiani akiizungumza Kifaransa palepale kilimfanya akumbuke sura ya Hamza. Kwa namna ambavyo Fabiani aliongea na kufananisha na Hamza, upande wa Fabiani alikuwa ni kama mwanafunzi wa Primary anaeanza kujifunza Kingereza. Alikumbuka siku ya pili aliyoonana na Hamza ilikuwa ni kwenda kumtambulisha kwa baba yake na namna alivyoongea Kifaransa ilimfanya kuona kama ni tukio la jana licha ya mgahawa kuwa tofauti. Alianza kukumbuka namna mwanaume anayeweza kuongea lugha ya Kifaransa kama mzawa, kuigiza maisha ya kimasikini kwa kupanga chumba uswazi, akiigiza kuwa mwanafunzi wa chuo na fundi. Sio hivyo tu, alikumbuka namna alivyobeza mavazi yake na kibaiskeri chake na mwisho wa siku kuumbuka.

Lakini licha ya kwamba Hamza alikuwa na mengi ya kumfanya akili yake kumfikia sana, bado hakupendezwa kabisa na matendo yake. Katika siku mbili hizo alikuwa na mawazo mengi ambayo msababishaji mkuu alikuwa ni Hamza.

Baada ya wawili hao kuagiza chakula, waliendelea kuongea stori nyingine, lakini ajabu Regina ni kama akili yake haikuwa hapo, kwani namna ambavyo stori za Fabiani zilivyomboa ndio alivyoendelea kukumbuka ucheshi na utani wa Hamza. Muda ambao chakula kilikuwa kikiandaliwa ili kuwekewa mezani, Meneja wa mgahawa huyo alisogea haraka katika meza yao. Meneja huyo pia alikuwa ni mzungu.

Sir, may I ask if the two black-clothed gentlemen outside are your bodyguards?”

“Yes, why?”
aliuliza Fabiani.

They’re having an argument with a gentleman. Would you like to take a look?” aliongea akimaanisha mabodigadi hao wapo kwenye mzozo na mwanaume mmoja kama vipi akaangalie.

“Regina, nisubiri nakuja,” aliongea Fabiani huku akisimama.

“Hapana, nitaenda na mimi kuona kinachoendelea,” aliongea Regina na kisha alichukua mkoba wake na kusimama.

Upande wa nje, mwanaume ambaye meneja alimsemea anasumbuana na mabodigadi alikuwa ni Hamza. Hamza mara baada ya kufika hapo na kuona gari ya Regina aliona aingie ndani ili akaonane naye, lakini mara baada ya kujitambulisha kwa mabodigadi hao walimzuia.

Hamza aliwaambia kwa kuwabembeleza yupo hapo kuonana na mke wake, lakini wale mabodigadi walijua bosi wao kachukua mali ya mtu, hivyo waliamua kumlinda.

“Mkeo hayupo humu,” waliongea na hapo mzozo ndio uliibuka, kwa sababu ilikuwa ni eneo la kati ya mji na watu wengi walikuwepo. Hamza hakutaka kuleta vurugu lakini ubishi wa mabodigadi hao ulimfanya kuanza kukosa uvumilivu.

“Nitaongea kwa mara ya mwisho, nipisheni nipite.”

“Unajiona nani mpaka tukupishe?” aliongea bodigadi mmoja kwa kujiamini, na Hamza palepale kwa spidi alisogea akitaka kupita kinguvu. Ila wale mabodigadi walimshika mabega na kutaka kumrushia nje.

Lakini kabla hata hawajafanya walichokusudia, Hamza alimpa shambulizi la kushitukiza bodigadi mmoja na kumfanya adondoke kama furushi.

Yule mwingine mara baada ya kuona mwenzake namna alivyoshambuliwa alishangaa na palepale alijipanga.

“Unaonekana kuwa na uwezo,” aliongea huku akiona kweli Hamza ana uwezo maana hakuwa na nguvu zozote za nishati za mbingu na ardhi.

Yule bodigadi palepale aliweka staili ya ajabu huku akitumia nishati za mbingu na ardhi kutaka kumshambulia, lakini Hamza alipangua shambulizi lake na kisha akampiga ngumi ya kifua yule bodigadi na kumfanya na yeye kudondoka chini kama kifurushi maana ni kama amegongwa na gari.

Dakika ambayo Hamza aliona ameshadhibiti mabaunsa hao na kutaka kuingia, ndio muda ambao Regina alitoka.

“Hamza! Unafanya nini?” aliuliza Regina kwa kufoka huku akiangalia mabodigadi waliokuwa chini wakigulia maumivu na alijikuta akipandwa na hasira kiasi kwamba sura yake ilianza kufubaa.
 
SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU.

MTUNZI: SINGANOJR.

SEHEMU YA 145.

Fundo la kifo.

“Shangazi kuuelewa moyo wa mtu ni ngumu kuliko kuvuna nishati za mbingu na ardhi,"

*****

Regina alikasirika baada ya kuona ni kama Hamza alikuwa ameenda mbali sana. Aliona hata kama alikuwa akimtafuta, hakupaswa kutumia nguvu kutaka kuingia ndani ya mgahawa huo.

Hamza, mara baada ya kumuona mwanamke huyo alivyokuwa amesimama kando ya Fabiani, alijikuta akishikwa na hasira moyoni.

“Umetoka out na mwanaume mwingine bila mimi, mumeo, kujua halafu unaniuliza nafanyaje?”

“Unaongea upuuzi gani?”

“Nimekosea? Kula chakula cha usiku katika mgahawa kama huu inamaanisha nini kama sio 'date'?” aliuliza Hamza kwa sauti.

“Nimekuja kwa ajili ya kula chakula na Senior, kwanini unafikiria vitu ambavyo havipo?” aliuliza Regina huku akitingishika mwili.

Hamza alikuwa na hasira ndani yake. Kadri alivyokuwa akifikiria, ndivyo hasira ilivyozidi kumpanda.

“Senior! Mara 'mkaka'! Inamaanisha wakati unasoma, yeye ndiye pekee aliyekutangulia unayemfahamu?”

“Mawazo yako ndio mabaya, na usiyasukumizie kwangu! I have a clear conscience!” aliongea Regina huku macho yake mazuri yakichanua na alimwangalia Hamza moja kwa moja bila kupepesa.

Upande wa Fabiani, mara baada ya kuona hivyo, licha ya kushangazwa na uwezo wa Hamza kuwadhibiti mabodigadi wake wawili, ugomvi wa Hamza na Regina ulimfurahisha ndani kwa ndani. Wahenga wanasema, "Hasira ya mkizi, furaha ya mvuvi." Hicho ndicho kilichomfurahisha kadri walivyoendelea kugombana, akiona nafasi ya kumpata Regina inaongezeka.

“Bwana Hamza, usitufikirie vibaya. Tulikuja hapa kwa nia ya kuonana na wenzetu wawili, lakini walipata dharura hivyo hawakufika, na ikatokea tumebakia sisi tu,” aliongea Fabiani.

“Kamwambie mtoto wa darasa la tatu anaweza kukuelewa, ila sio mimi.”

“Hamza, kama huniamini, unaonaje ukiungana nasi na kula pamoja? Mimi sijali, maana zipo nafasi mbili tayari ziko wazi,” aliongea Fabiani kwa uungwana.

Hamza hakutaka kuendelea kusikiliza maneno ya Fabiani. Palepale alimsogelea Regina na kumshika mkono.

“Twende nyumbani,” aliongea, lakini Regina alianza kuleta ukinzani, akitaka kujitoa kwa hasira.

“Niachie! Siondoki. Nimekuja kula, na nitaondoka nikimaliza. Kwanini unataka kuniondoa hapa kama mhalifu, ikiwa sina kosa?”

“Huna kosa unasema? Lakini umeamua kutoka out na mwanaume kisirisiri?” aliongea Hamza huku akimkodolea Regina macho kwa hasira.

Regina alishangazwa na kauli hiyo. Baada ya kusikia, aliishindwa kufanya chochote kwa sekunde sita, na palepale machozi yakaanza kumtoka na alimchapa Hamza kibao kwa mkono wake wa kulia.

Pah! Sauti ya kibao iliweza kusikika baada ya Hamza kupigwa kibao cha nguvu, alikuwa na uwezo wa kukwepa lakini aliacha kimfikie.

“Ndio umeanza kushikwa na hatia kwa sababu ya nilichosema? Wakati nilivyokuwa hospitalini siku ile, mlikuwa mkiongea kwa kukumbushiana mambo yenu kwa furaha kubwa mpaka mkaniita mjinga...”

“Hamza... wewe sio binadamu,” aliongea Regina huku aking’ata meno yake kwa hasira.

“Hamza, kumfanyia hivi mke wako sio jambo zuri kabisa. Umeenda mbali, ijapokuwa mimi ni rafiki tu kwa Edna, lakini matumaini yangu ni kuona anaishi maisha ya furaha. Ila kwa hiki kinachoendelea, nashindwa kukubaliana nacho,” aliongea Fabiani.

“Oh! Kwa hiyo unapanga kufanya nini? Au ndio unataka kujichukulia pointi kwa kuwa shujaa wa kumuokoa mrembo?” aliongea Hamza huku akimwangalia Fabiani kwa macho makali. Hali ile ilimfanya Regina kuanza kukosa utulivu.

“Senior, ondoa wasiwasi. Hili ni suala la mimi na yeye. Unapaswa kuondoka...”

“Hapana, Regina. Ijapokuwa sijawahi kukiri, niseme tu. Siku zote umeishi moyoni mwangu, siwezi kuvumilia kuona unafanyiwa hivi,” aliongea Fabiani huku akimsogelea Hamza bila kumwogopa.

Hamza alianza kucheka, na palepale macho yake yakaanza kubadilika taratibu.

“Senior, naomba usiongee kitu kingine,” aliongea Regina, akiogopa Fabiani anaweza kusema kitu ambacho kitamfanya Hamza kumfanyia kitu kibaya.

Ingawa alikuwa na maumivu aliyoyaficha, akili yake ilikuwa ikifanya kazi vizuri. Alihisi kuwa ikitokea vita kati ya Fabiani na Hamza, basi Fabiani angeweza kupata matatizo makubwa.

Mara baada ya kuona Regina anaingilia, Fabiani alidhani kuwa Regina anahofia kwamba yeye, akiwa mwanajeshi, anaweza kumdhuru Hamza. Lakini ukweli ulikuwa tofauti, Regina aliogopa Fabiani angepigwa vibaya na kuachwa nusu mfu.

Regina aliona asingeweza kuelezea hivyo kwani kumwambia Fabi ingekuwa kama kuchochea moto. Kingine hakujua sana kuhusu wanajeshi wenye mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, hivyo hakujua ni daraja gani la uwezo alilokuwa nalo Fabi, lakini hisia zake zilimwambia Hamza yupo juu zaidi.

"Kuongea na mke wangu unadhani nakuwa mkorofi, kabla hatujaenda mbali unataka nifanye nini labda?" aliongea Hamza.

"Ni rahisi sana, ninachotaka ni wewe kumuomba Regina msamaha na kukubali umemkosea. Kuhusu mimi, hata kama unifikirie vibaya, sijali."

"Fabi, usiongee tena, naomba uachane na hili swala kabisa," aliongea Regina.

"Regina, kwangu sijali kama nasingiziwa, lakini siwezi kuvumilia kukuona unateseka."

"Hapana Senior, huelewi ninachomaanisha..." Regina hakujua hata amwelezee vipi. Alikuwa katika hali ya wasiwasi kiasi kwamba uso ulijikunja.

"Kwahiyo kama nisipoomba msamaha, utafanya nini?" aliongea Hamza akiwa hana chembe ya utani kabisa.

"Hamza, nilikufikiria kama mwanaume ambaye unajua kuwajibika kwa matendo yako, isitoshe kama daktari, unapaswa kuwa mfano. Lakini sikutarajia utakuwa mtu ambaye hutumii akili likija swala la mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke. Usipomuomba Regina msamaha sitojizuia kutumia mbinu mbadala kukufanya usiwe msumbufu kwake baadae."

"Oh! Mbinu mbadala? Nataka kuona hizo mbinu mbadala," aliongea Hamza. Na baada ya kauli hiyo, kwa sababu hakutaka kumkosea heshima Regina kwa kuleta ugomvi, alimshika mkono Regina akimpa ishara waondoke.

"Hamza! Unafanya nini? Hebu niachie!"

Regina hakutaka kushikwa kama hivyo na alijitahidi kuondoa mkono wake, lakini Hamza hakujali na aliendelea kutembea akiwa amevimba.

Fabiani, mara baada ya kuona Regina anaondolewa mbele yake kinguvu, palepale ukali ulimwingia na alimsogelea Hamza na kutaka kumshika bega. Lakini sasa baada ya Fabiani kupeleka mkono akiamini itakuwa kazi rahisi kumshika bega Hamza, ilishindikana kwani mkono wake ulipita hewani.

Ijapokuwa aliona kuna kitu hakipo sawa, lakini bado alijitutumua na kusogea kumzuia Hamza kwa mbele.

"Mwachie Regina," aliongea na kumfanya Hamza kuinua macho yake na kumwangalia Fabiani na tabasamu lisilokuwa la kawaida lililosababisha presha ya ajabu.

Fabiani mara baada ya kukutanisha macho yake na Hamza alijikuta akihisi woga mpaka kwenye mifupa na nywele zake zilisimama kama vile amekutana na jini. Alianza kujiuliza ni msisimko wa aina gani anaohisi. Ni mwonekano gani huo Hamza anaonyesha, maana ni kama jini lililokuwa limelala kwa muda mrefu na sasa limeamka.

"Unataka kufa?" Aliuliza Hamza.

Ijapokuwa sauti ya swali hilo ni kama kitisho, lakini vilevile ilikuwa ni kama sentensi tu kwa Fabiani. Isitoshe, alikuwa ni mwanajeshi ambaye ana mafunzo ya kikomandoo lakini pia ni mwanafunzi wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kutokea Kambi ya Nyoka, na kama mwanajeshi wa kiwango chake, woga hudumu kwa sekunde kadhaa na kinachofuatia ni ujasiri. Hivyo alitunisha kifua palepale.

Sheria za hawa wanajeshi wa kikomandoo ambao wana mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, iwe umesomea mafunzo hayo China, Cuba au Brazili, au kuwa raia wa taifa gani, popote pale ulipo unapopambana unawakilisha kambi uliojifunzia kabla ya taifa lako.

"Mtu ambaye anapaswa kuuliza hili swali ni wewe Dokta Hamza. Au unataka kupigana na mimi?"

Mara baada ya kuongea vile, ili kumuonyesha Hamza yupo tayari kwa lolote, alipeleka mkono wake kiunoni na alichomoa kitu cha chuma rangi ya silver kilichokaa kama muundo wa nyoka. Na mara baada ya kutumia nguvu za mbingu na ardhi kuingiza nishati katika kile kifaa, ajabu kifaa kile kilibadilika umbo lake na kuwa upanga mrefu unaong’aa.

Kwa mbwembwe kabisa, Fabiani alianza kuuchezesha ule upanga katika vidole vyake kwa sekunde kadhaa, kisha alisimama kwa mkao wa kujivunia na kunyanyua ile siraha na kumnyooshea Hamza.

"Onyo kwa mara ya mwisho, mwachie Regina mkono! Huyo sio kifaa chako, anayohaki ya kufanya maamuzi," aliongea Fabi ki' afande kabisa.

"Senior, naomba uweke siraha yako chini, usifanye hivyo," aliongea Regina kwa kuomba.

"Regina, hili ni swala baina ya mwanaume na mwanaume, hupaswi kuingilia," aliongea Fabi na kumfanya Regina kukosa namna na kuwa na mwonekano wa ‘mwana ka utaka’ lakini bado aliomba baya lisimkute.

Hamza aliangalia siraha hiyo iliyotemwa na nyoka bila wasiwasi wowote na kimya kimya alimwachia Regina. Fabiani mara baada ya kuona alichofanya Hamza, palepale macho yake yalichanua kwa kudhania pengine Hamza anamwogopa.

Hata Regina alishangaa baada ya kuona ni kama Hamza ameamua kukubali yaishe, lakini sekunde iliyofuata ilimfanya Regina kutoa ukulele wa hamaki.

Hamza alifyatuka kwa spidi na kwa kutumia mwili wake aliuvaa ule upanga ulionyooshewa kwake kama vile anataka kutobolewa na ncha yake. Spidi yake ilikuwa kubwa mno, na hata Fabiani alikuwa hajajiandaa kabisa kwa tukio hilo. Muda ambao aliona nini Hamza anataka kufanya, siraha yake eneo la ncha ya mbele ilishauchoma mwili wa Hamza tayari.

Mwanzoni alidhania siraha yake itamchoma kirahisi sana Hamza kwa kutoboa na kupita, lakini kilichotokea kilimfanya uso wake kugeuka wa kijani kwa mshangao.

"Clang! Clang!"

Dakika ambayo upanga wake ule wa mtemo wa nyoka ulivyogusana na mwili wa Hamza, ulikatika kama vile ulikuwa umetengenezwa na barafu na kukatika vipande vipande vilivyofyatuka. Kimoja kilifyatuka na kumpitia Fabi kwenye shavu na kumchana, akapata kidonda kilichoanza kutoa damu.

Muda huo huo, wakati Fabi akiwa kwenye mshituko, Hamza alimpiga Fabiani ngumi nzito ya kifuani na kumfanya afyatuke kama punching bag na kudondoka chini.

Afande Fabi aliishia kutema damu hewani baada ya kifua chake kubobolewa ipasavyo.

Bosii!!"

Mabodigadi wale wawili walijikuta wakipiga kelele kwa mshangao mkubwa, na mara moja walimkimbilia alipodondokea Fabiani. Watu wote waliokuwa wakishuhudia tukio hilo walipigwa na butwaa. Regina macho yalimtoka, akifunika mdomo wake kwa mikono kama mtu anayezuia kulia kwa sauti.

Ingawa mwanamke huyo alijua Hamza ana uwezo, hakudhani uwezo huo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpiga ngumi moja Fabiani na kumfanya afyatuke kama mpira. Hamza alipiga hatua na kusimama mbele ya Fabiani, akimwangalia bila hisia za huruma. Alikuwa pia amekatwa ubavuni, lakini hakutokwa na damu kabisa.

Ijapokuwa Fabiani, aliyesaidiwa kusimama, alikuwa na damu zilizokauka usoni kutokana na nishati za mbingu na ardhi, mwili wake ulikuwa ukitetemeka kama vile Hamza alikuwa zimwi la kutisha.

"Wewe... wewe ni nani hasa?" aliuliza kwa woga mkubwa. Alikuwa na miaka thelathini tangu alipoanza kuiona dunia, na akiwa jeshini alikutana na wataalamu wengi wa mapigano, lakini hakuwahi kuona mtu mwenye uwezo wa ajabu kama Hamza.

"Mimi ni nani? Hustahili kabisa kujua. Si ulitaka kujionyesha mwamba mbele ya mke wangu? Uduvi mlaini kama wewe unapata wapi ujasiri wa kujigamba mbele yangu?"

Fabiani alijawa na hali ya kudhalilika isiyovumilika, akitema damu nyingine chini.

"Takataka!"

"Arghhhhhh!!!"

Hamza alimpiga teke la nguvu katikati ya mapaja, na kwa maumivu aliyoyapata, jicho lilihisi kutaka kutoka. Wazo la kwaheri uanaume halikubalika kabisa katika akili yake licha ya kukosa cha kufanya. Dakika chache zilizopita alikuwa complacent(Akijikubali) na uanaume wake, lakini sasa alikuwa amegeuzwa kuwa joka la kibisa.

Mabodigadi wa Fabiani walikosa la kufanya. Kwa kuogopa kushambuliwa na Hamza, walimwachia Fabiani, wakirahisisha kazi ya kumshambulia eneo nyeti.

Regina alitamani kulia, lakini machozi hayakutoka kwa kumwonea huruma Fabiani. Aliishia kumkimbilia Hamza na kumshika mkono asiendelee.

"Hamza, naomba usiendelee tafadhali. Ukiendelea hivi, itatusababishia matatizo."

"Unaendelea kumtetea kaka yako mzuri, eeh?"

"Ashakuwa hivi tayari, kuna utofauti gani wa kumuua na kumwacha? Hamza, ukiua mtu leo hii mimi na wewe basi," aliongea huku aking'ata meno yake kwa hasira, na kauli ile ilimwingia Hamza vyema.

"Basi sawa, nitamuacha aendelee kuishi. Isitoshe, si mbaya akiwa towashi."

"Nini!?" Regina alimaka. Alipeleka macho yake kwa Fabiani aliyekuwa amepoteza fahamu kwa maumivu. Hakutegemea Hamza angeenda mbali kiasi hicho kumvunja mwenzake mshipa.

Alifumba macho yake na kuvuta pumzi nyingi, kisha akamwangalia Hamza kwa macho ya kukaripia, akawageukia wale mabodigadi.

"Haraka mchukueni mumwahishe hospitalini."

Kauli hiyo iliwafanya wale mabodigadi kurudi kwenye akili zao, wakimbeba bosi wao na kumwingiza kwenye gari ili kumwahisha hospitalini. Regina alimtazama Hamza kwa sekunde kadhaa kabla ya kugeuka na kuelekea kwenye gari lake.

Hamza hakusema neno. Kimya kimya alimfuata na kwenda kusimama upande wa mlango wa dereva, akimzuia.

"Nipishe, sitaki kukuona tena," aliongea Regina huku macho yake yakiwa mekundu.

"Sio sahihi. Ni wajibu wangu kumrudisha mke wangu nyumbani."

"Hamza! Umezidi sasa," alifoka Regina.

"Kwamba naonekana mkatili? Ulitaka nijifanye mnafiki kupotezea kile alichojaribu kunifanyia yule mpuuzi? Umekosa mtu mwingine wa kula naye? Unafanya nini hapa mkiwa wawili tu halafu wewe mke wa mtu?"

"Nishakueleza tayari na sitaki kurudia ili uelewe. Kama unataka kunizuia, nitachukua taksi," aliongea Regina huku akielekea upande wa barabarani akiwa na mkoba wake.

Hamza hakutaka kuona akiondoka kirahisi. Alimsogelea na mara moja akambeba juu juu na kumuweka begani.

"Ahhhhhh! Hamza, umekuwa kichaa, kwa nini unanifanyia hivi?" Aliuliza huku akifurukuta, lakini Hamza hakujali. Alifungua mlango wa gari upande siti mbele kwa dereva na kumwingiza kisha akatoa ufunguo kwenye mkoba wake.

Kwasababu hakutaka Regina kushuka tena, haraka sana alitoa gari hiyo eneo hilo kwa kasi, ikikoroma kama simba dume barabarani. Ijapokuwa kulikuwa na magari kadhaa nyakati hizo za usiku katikati ya jiji, Hamza hakujali. Alitumia kila upenyo aliouona mbele yake kuchepuka.

Gari lilipoanza kupiga kasi ya kilomita mia tatu kwa saa, Regina alifumba macho na machozi yakaanza kumtiririka kama mfereji. Baada ya dakika chache, gari ilipunguza mwendo ilipokuwa ikiingia mtaa wa Egret, Kigamboni. Baada ya kusimama, Hamza aliegamia kiti cha gari, akimwangalia Regina.

Kwa jinsi sura ya Regina ilivyokuwa ya kirembo na ya kitoto kwa wakati mmoja, alionekana kutia huruma sana. Machozi yalikuwa yameacha alama kwenye mashavu yake.

"Hili suala kwanzia sasa limeisha, sitakusumbua tena. Huja kula chochote, ni vizuri uingie ndani upate chakula na upumzike," aliongea Hamza baada ya hasira zake kupungua. Regina alimwangalia kwa macho ya kejeli.

"Hivi kwanini hata mshipa wa aibu unakosa kwa yale unayoyafanya kila siku na unayonituhumu nayo?"

"Unamaanisha nini?"

"Kwamba mimi kuonekana na Fabiani inamaanisha nina mahusiano naye? Au kwa sababu nimeoelewa, sitakiwi kusalimiana na mtu wa jinsia tofauti ninaemfahamu?"

"Inategemea huyo unayesalimiana naye ana nia gani. Kwa IQ yako ya 180, hata kama EQ yako ni ndogo, inamaanisha hujui Fabiani alikuwa akipanga nini?"

"Siku zote kosa langu dogo unaligeuza kuwa kubwa, ila makosa yako ni lazima nivumilie bila kusema lolote, sivyo?"

Hamza aliposikia hayo, alifikiria kuhusu Eliza, Yonesi, Ana, na Yulia. Alijihisi na hatia, na moyo wake ulilainika.

"Sawa, tuache hili lipite. Najua na mimi nina madhaifu yangu, na kama nilivyosema mwanzo, sitayaficha kwako."

"Una uhakika huna unachonificha?" Regina aliuliza, akimwangalia Hamza kwa macho yenye kuonekana kama mtu anaejua kitu.

Hamza alijikuta akiishiwa nguvu, na ghafla suala la Yulia likamjia kichwani.

SEHEMU YA 146.

Kwenye macho ya Regina kulikuwa na hali ya kukatishwa sana tamaa . Mwanamke huyo alitoa simu yake na kisha aliingia upande wa Watsapp na kugusa faili la rekodi ya sauti.
Hamza ambae alikuwa na hali ya hatia kwa sekunde chache zilizopita alijikuta akinywea ghafla kama amegandishwa kwenye friji mara baada ya kusikia sauti hio ilikuwa ikiuhusu nini.
Voice record:

Hebert: “Bro Hamza kama sikosei utakuwa tayari na mke si ndio?”

Hamza: “Upo sahihi, naona ushafanya utafiti wako kabisa na kujua kila kitu kuhusu mimi, kwanini unauliza ilihali majibu unayo?”

Hebert: “Mkeo ni Regina, mmiliki na Afisa mtendaji mkuu wa makampuni ya Dosam, lakini pia mwanamke anaye sifika kwa kuwa na urembo wa ajabu. Kwa hiki unachofanya hawezi kupatwa na wivu?”

Hamza: “Mke wangu ni muungwana sana na anaamini mimi kama mwanaume kuwa na wanawake angalau watatu sio tatizo,”

Yulia: “Nimemjua Hamza kwa muda sasa na ni mtu alienisaidia na kutokana na hilo nipo tayari kumpa chochote. Hata kama Regina atafahamu kuhusu uhusiano wetu sidhani anaweza kufanya chochote”

Hamza: “Hehe... kwanza kabisa mke wangu ni mtu muungwana sana na kingine anajua nina michepuko mingine tofauti na Yulia, kiufupi ni mwelewa mno.”

Hamza alijikuta akibung’aa na kujiuliza hivyo sio namna walivyoongea mara ya kwanza kukutana na Hebert kisiwani Chole. Hamza alijua kabisa hiyo sauti sio feki, mazungumzo yao siku ile yalikuwa yakirekodiwa.

“Nadhani utakuwa kwenye mshangao mkubwa, kuona nina hii rekodi ya sauti zenu,” aliongea Regina huku akitoa kicheko cha kujikatia tamaa.

“Ukweli wakati napokea hii rekodi na kuisikiliza nimejutia mno, kama ningejua yaliyomo nisingeifungua kabisa..” aliongea Regina kwa sauti ya huzuni kuonyesha jinsi gani alikuwa akiumia.

Hamza alianza kuhisi kichwa kumuuma palepale. Ndio sasa anajua siku ile alikuwa ndani ya mtego wa Hebert. Hakudhania Hebert alikuwa na mpango huo kabla ya kufa kwake. Sasa anajua kwanini Shangazi alimwambia Regina alionekana kutokuwa katika hali nzuri kwa siku kadhaa; kumbe yote ya kisiwani yashamfikia. Mbaya zaidi, Hamza alishamwahidi Regina kwamba hakutokuwa na mahusiano baina yake na Yulia kabisa.

“Regina, mke wangu naomba unisikilize...”

“Huna haja ya kujielezea,” aliongea Regina na palepale alirudisha simu yake kwenye mkoba. “Isitoshe, ushaongea tayari. Wewe ni mwanaume, na sina tatizo ukiwa na wanawake angalau watatu. Wewe na Yulia mmejuana kwa muda mrefu sana, ila mimi nimekujua hata nusu mwaka haijatimia.”

Hamza kadri alivyokuwa akisikiliza ndivyo hatia ilivyomtafuna. Alioongea siku ile nusu tu ndiyo yalikuwa na ukweli, ila mengine yote yalikuwa ni utani tu kuchangamsha mazungumzo. Hata hivyo, iwe ni ukweli au uongo, kitendo cha Regina kusikiliza kilikuwa ni kumndhalilisha kwa namna ya juu sana na kumkosea heshima.

Ijapokuwa uhusiano wake na Yulia alijiambia ni kwa ajili ya kuingia katika Circle ya familia ya Wanyika ili kuazima nguvu yao kujilinda, lakini mwisho wa siku ni kisingizio tu. Ukweli alikuwa akimtanani Yulia kwa muda mrefu na kuhusu kumpenda ama kutokumpenda hilo ni swala lingine lakini mwisho wa siku ni kosa lake yeye kama mwanaume kutokujizuia.

“Nimefikiria na nimeona hatuendani,” aliongea Regina.

Hamza mara baada ya kusikia kauli hio mwili wake ni kama umemwagiwa maji ya barafu, ukisikia mwanamke anaongea kauli hio lazima imfanye mwanaume yoyote mapigo yake ya moyo kwenda spidi. Sentensi hio maana yake ni kwamba hata kama mwanamke alipanga kujitahidi imeshindikana na amejikatia tamaa.

"Regina naomba usiruhusu mawazo yako kwenda mbali, nakuahidi nitakwambia kila..." Hamza kabla hata hajamaliza, Regina alishuka kwenye gari.

Hamza haraka haraka alishuka kumuwahi na kumshika mkono ili kumbembeleza.

"Wife usiwe hivi, najua nimekosea, nakiri kukosea lakini nakuahidi sitoongea maneno ya aina hio tena," aliongea Hamza huku akijaribu kumtingisha Regina kwa kumshika mabega lakini Regina alikuwa ni kama sanam na kumfanya Hamza asijue ni kwa namna gani ya kulimaliza hilo suala.

"Wife nifanye nini ili unisamehe, nipo tayari kukupigia magoti," aliongea Hamza na palepale alishuka chini na kupiga goti na mguu mmoja huku mikono yake ikiwa imeishika miguu ya Regina.

"Regina mke wangu, sikujua itakuwa kama hivi. Hebert aliniwekea mtego na niliongea tu kama kuchangamsha mazungumzo lakini sio maneno ambayo yametoka moyoni, Halafu zaidi muda ambao naongea hivyo nilikuwa nikiigiza kuwa boyfriend tu wa Yulia baada ya kuingia dili flani na mimi."

"Sawa, inatosha usiongee tena..." Aliongea Regina akiingilia mazungumzo ya Hamza, aliongea kivivu sana kama mtu ambae amachoka.

"Sina hasira kabisa na wewe hivyo simama na acha kupiga magoti."

"Wife najua unaongea tu kutania ila bado hujanisamehe, mimi usiponisamehe nitaendelea kupiga magoti," aliongea Hamza.

"Nimefikiria kwa umakini hili swala na nikagundua hujafanya kosa lolote ndio maana nikajiuliza kuna haja gani ya mimi kukukasirikia?"

"Ah! Hapana ni kweli nimekukosea, nilikuahidi sitokuwa na uhusiano wa namna yoyote na Yulia lakini mwishowe..." Hamza alishindwa kumalizia kusema 'mwishowe kamchapa bakora za kimkakati'.

"Lakini nikaona wewe ni wewe, unachokifanya ndio utambulisho wako ndio tabia yako na pengine kama usingenioa, ungekuwa na kundi la wanawake kuliko uliokuwa nao sasa, au nakosea?" Aliongea na Hamza aliishia kubung’aa asijue kwanini Regina anaongea hivyo.

"Kila mtu ana namna yake ya kuishi na wewe hii ndio namna yako ya kuishi, unajua sana kudili na wanawake, ndio uhuru wako. Isitoshe, iwe ni Eliza, Yonesi au huyu wa Sasa Yulia, sio kwamba umewalazimisha kuwa nao. Nilifikiri mwanzoni sitojali sana kuhusu tabia yako lakini niliona nilikuwa nikijipa matumaini hewa kwani nashindwa kuvumilia, kadri siku zinavyoenda ndio nazidi kukosa uvumilivu na kujisikia vibaya. Nimekuja kujijua sipo vizuri kama nilivyojiwazia mwanzo."

Mara baada ya kuongea hivyo aliweka nywele zake vizuri na kisha akavuta pumzi nyingi na kuitoa.

"Naomba usinipigie magoti maana haitokuwa vizuri shangazi akikuona, kwasasa sitoongea chochote, Nadhani unakumbuka pia ndoa yetu ni feki. Ijapokuwa kuna kushuka na kupanda tulikopitia pamoja na kujikuta tumejisahau kwa muda, lakini nadhani ni vyema kwanzia sasa tukirudi upya na kuangalia vipengele vya mkataba."

Hamza mara baada ya kusikia hivyo alijikuta akichanganyikiwa, katika moyo wake alishikwa na hali ya kupoteza na aibu na kumfanya asijue namna ya kuongea kumshawishi tena Regina. Aliona asingeweza kusema pia ataachana na michepuko, isitoshe pia aliona uhusiano wake na Regina licha ya cheo cha mke na mume kati yao lakini hawakuwa na mahusiano makubwa sana lakini hakuwa akisahaulika pia.

Hivyo Hamza aliishia zake kusimama baada ya kuona hakuna namna na kila mmoja akaingia ndani kwa wakati wake.

Shangazi hakuwa amelala bado na pia hakuwa ameondoa chakula mezani, alikuwa mtu mzima kuona hakukuwa na maelewano mazuri baina yao na hakuthubutu kuuliza. Regina alikula kidogo na ndio aliekuwa wa kwanza kuondoka kupandisha juu kupumzika na kisha Hamza na yeye akafuatia.

Hamza mara baada ya kurudi kwenye chumba chake, hakujisumbua hata kuoga wala usingizi haukumjia kabisa, alikuwa katika hali ya msongo wa mawazo.

Upande mwingine katika hospitali ya kijeshi Lugalo, katika chumba cha ICU Fabiani alikuwa ndio kwanza ametolewa kutoka kufanyiwa upasuaji na baada ya kupewa taarifa ya kusikitisha ujasiri wote ulimpotea na alijikuta akitoa kilio kama mtoto mdogo. Mwanaume kijana kama yeye na mwanajeshi maarufu na kapteni wa kikosi cha kupambana na uvamizi kugeuzwa kuwa towashi, hisia zake zilikuwa ni zaidi ya kifo.

"Bosi timu yako ya wanajeshi wapo hapa kwa ajili ya kukutembelea," bodigadi kando yake aliongea.

"Waambie waondoke, sitaki kuonana na mtu."

"Sawa."

Bodigadi yule alielewa maagizo na kwenda kuwaambia makomandoo wa kitengo cha Malibu kuondoka.

"Gozi!" Aliita Fabiani mara baada ya bodigadi kurudi.

"Ndio bosi, kuna kitu unachotaka nikusaidie?" Aliongea na palepale Fabiani macho yake yalijawa na chuki ya kisasi kubwa mno.

"Nataka kuongea na Master," aliongea.

Hamza hakulala kabisa usiku kucha, alikuwa akiwaza swala la Regina na baada ya kuona usingizi umempotea alichokifanya ni kuanza kufanya meditation . Hamza alikumbuka andiko alilopata kutoka kwa Master Shagani na aliona inafaa kama atatumia muda huo kupoteza mawazo na ile anakuja kumaliza kulikuwa kushapambazuka tayari na alishituliwa na simu ya Afande Himidu.

"Bosi, kwanini una hasira sana siku hizi? Ndio umetoka kisiwani jana tu lakini umekwisha kumpa ukilema mwanajeshi na mwanafunzi pendwa wa Master Faruku wa kambi ya Nyoka," aliongea Himidu kwa upole mno kama mtu anaetaka kulia.

Hamza alifikiria kwa sekunde na alijua anaelengwa ni Fabiani na mara baada ya kumkumbuka alijikuta akichukia zaidi.

"Vipi kuna watu wamekulalamikia?" Aliuliza Hamza.

"Sio kulalamikiwa bosi, Fabiani ni ndugu wa rais mteule mheshimiwa Abubakari Kassim. Ijapokuwa kuwepo kwake ama kutokuwepo hakuna athari kubwa kwenye kitengo chetu, lakini kufanya hivi mheshimiwa atatafsiri ni kama anadharaulika kutolinda ndugu zake. Kama nisingemshawishi mheshimiwa, angekuwa ashatuma watu kwa ajili ya kuomba maelezo ya kilichotokea. Unapaswa kuelewa Mzee Farook ndio moja ya wanajeshi hodari zaidi ndani ya jeshi letu katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi, ijapokuwa siku zote anamtambulisha Fabiani kama mwanafunzi wake lakini ki uhalisia ni mtoto wake wa nje ya ndoa ndio maana lazima awe na wasiwasi. Farook na mheshimiwa ni ndugu wa damu ni mtu na kaka yake na tukio la mtoto wake kugeuzwa Towashi, licha ya kusema ni udhaifu wa mwanafunzi wake kushindwa kujilinda lakini ni lazima atatumia koneksheni kutaka kulipa kisasi, kama sio kuja mwenyeewe kupambana na wewe," aliongea Afande Himidu.

"Huyo Farook kama anataka kulipiza kisasi cha mtoto wake mwambie aje mwenyewe, sina wasiwasi kuwarahisishia kazi kubadili kiongozi wa kambi ya Nyoka kwa kumtanguliza mbele za haki," aliongea Hamza hakuwa katika mudi nzuri kabisa.

"Bosi kwani huyu Fabiani amekukosea nini, ni mara chache sana kukuona ukikasirika namna hii?"

"Huyo mshenzi alitaka kunishika K*nde, unadhani ningemfanya nini," aliongea Hamza na kisha alianza kumwelezea kilichotokea.

"Kwa kosa hili ana bahati hajakufa kabisa, bosi nimekuelewa ngoja nitatoa maelezo juu ya kilichotokea."

Mara baada ya kukata simu Hamza aliingia bafuni na kuoga haraka haraka na kisha akavaa mavazi yake na kushuka chini kwa ajili ya kifungua kinywa.

Regina alikuwa tayari mezani na alikuwa akipata kifungua kinywa, mwanamke huyo hakuonyesha kuwa na tofauti kabisa kutokana na kilichotokea jana. Lakini upande wa Hamza ukawaida huo ulimfanya kuzidi kukosa utulivu kwenye moyo wake, hio yote ni kutokana na kwamba ni kama gepu la kihisia kati yao lilikuwa limeongezeka mno.

Hamza alikumbuka wakati anakutana kwa mara ya kwanza na Regina alikuwa na mwonekano kama huo ambao siku zote unamfanya kujihisi ni kama yupo kwenye gereza katika kisiwa kisichokuwa na binadamu, ki ufupi Regina alirudi katika U'Regina wake.

"Wife naona mapema sana leo?" Aliongea Hamza akijitahidi kadiri ya uwezo wake kumwongelesha.

"Morning!" Aliongea Regina bila kumgeukia na kuendelea kuwa bize.

Hata shangazi ambae alikuwa jikoni mara baada ya kusikia salamu hio aliishia kukunja sura lakini hakuongea neno.

Licha ya kifungua kinywa kuwa cha kuridhisha matamanio ya mdomo lakini kwa Hamza ni kama alikuwa akila tope.

Regina mara baada ya kumaliza alisimama na kuchukua mkoba wake.

"Wife, bado sijamaliza nisubiri," aliongea Hamza.

"Haina haja, nitaendesha gari langu mwenyewe," aliongea na kisha alitoa ufunguo wa gari ya BMW M8 na kuuweka mezani.

"Kwanzia leo hii ndio itakuwa gari yako, haina haja ya kufanya kazi pamoja tena kwa vyovyote vile una mambo mengi ya kufanya hivyo unahitaji gari."

"Haina haja ya gari, nitakuendesha, nishamaliza," aliongea Hamza huku akisimama.

"Chukua, namaanisha tunapaswa kutengana kabisa, hivyo itakuwa rahisi wewe kufanya maamuzi ya kuondoka," aliongea na kisha aligeuka na kuelekea upande wa gereji akimwacha Hamza na moyo mtupu.

Katika moyo wa Regina, kuendelea kuwa na Hamza aliona ni kama mzigo na kwasababu ishafikia hatua hio aliona Hamza ndio afanye maamuzi yeye mwenyewe ya kuondoka na sio kumfukuza.

Shangazi na sikio lake la Umbeya alisikia kila kitu na baada ya kusikia mngurumo wa gari ukitokomea nje haraka alisogea karibu na Hamza.

"Hamza mara nyingi ni kawaida kwa wenza kugombana, usikate tamaa nina uhakika Regina atakaa sawa ndani ya siku chache," aliongea.

"Shangazi kuuelewa moyo wa mtu ni ngumu kuliko kuvuna nishati za mbingu na ardhi," aliongea Hamza.

Ijapokuwa hakuuliza nini kinaendelea lakini aliweza kuotea nini chanzo cha ugomvi wao. Swala la Hamza kuendelea kubakia na Regina ni fundo la kifo ambalo alifunga pamoja na bibi yake Regina kabla ya kufariki.

Hamza mara baada ya kuingia ndani ya gari simu yake iliingia ujumbe na mara baada ya kuusoma aliona umetoka kwa Irene baada ya kuusoma na kutabasamu kidogo aliona kuna ujumbe mwingine ambao hakuusoma na umetoka kwa Amiri na aliufungua na kuusoma palepale.

"Bro nasikia umeacha chuo? Kwanini usingemalizia tu kabisa bado miezi kadhaa imebaki," alisoma na kumfanya Hamza akifikirie kidogo na palepale alijiongelesha, sikusoma kwa ajili ya kumaliza bali kuongeza maarifa.

Licha ya hivyo Hamza alishangaa kidogo habari hizo kumfikia haraka Amiri, maana mara ya mwisho wakati anaenda chuoni akiambatana na Dina, ilikuwa ni taarifa iliowafikia uongozi pekee na aliomba iwe siri mpaka chuo kuisha.

Hata hivyo hakujali sana kuhusu ujumbe huo na aliweka simu chini akijiambia kwanza aelekee kazini kuona kama anaweza kupata wazo la kumuweka sawa Regina na angetumia muda huo kujibu ujumbe wa Irene na Amiri rafiki yake, tena wakati akiwaza hivyo aliona ingekuwa vizuri kama atakutana na Amiri anaweza kumpa mbinu.

Asubuhi Kanali alikuwa na ari kubwa ya kuonana na Madam, ijapokuwa alikuwa na wasiwasi namna ya kumwingia kuhusu swala aliloagizwa na mtaafu Eliasi, lakini kwa kuamini ukaribu wake na Madam kwa muda mrefu lazima angefanikiwa japo aliona haitokuwa rahisi sana.

Kwa siku karibia tatu zote alikuwa akijipanga, Madam alikuwa nje ya nchi ndio maana alitumia muda mwingi kukaa chini yeye na Tresha Noah kujipanga namna ya kufanikisha swala hilo.

Isitoshe wawili hao pia walikuwa katika kujiuliza imekuwaje Madam akaanza kushirikiana na Mstaafu Mgweno, ni jambo gani ambalo limemshawishi mpaka kukubali Mgweno akutane na Mzee wa Taifa(MT).

"Unajua MT wakati Mgweno anaingia madarakani ndio alimpa ramani yote Mgweno namna ya kujitegemea na kuongea ushawishi wake nje na ndani?" Aliongea Kanali wakati akijiandaa kutoka, alikuwa amelala hotelini na mrembo Tresha.

"Dastani unairudia hio kauli mara ya tano mpaka sasa, mbona una wasiwasi sana?" Aliongea Tresha akimwangalia Dastani aliekuwa akihaingaika kufunga tai kwenye kioo.

"Najaribu kurudia rudia ili kutengeneza makisio ninayotaka kuthibitisha, ndio namna ya kurahisisha mazungumzo na kupata ninachotaka," aliongea.

"Kwahio unataka kusema nini?" Aliuliza na Kanali aligeuka na kwenda kukaa kwenye sofa.

"Hebu fikiria huu mchezo wao wa kisiasa kwa umakini na kuna kitu hapa utakipata, baada ya mgombea Jongwe kufariki na Mheshimiwa Abubakari kusimikwa kama mgombea wa urais, maana yake Mgweno alipigwa chenga, lakini wahenga wanasema kupigwa chenga si kufungwa bao."

"Kwangu mimi Jongwe namuona kama mpira uliopasuka na kuondolewa uwanjani na Abubakari ni mpira mbadala, goli ni mlango wa Ikulu, kitendo cha Abubakari kushinda na kuingia Ikulu si inamaanisha ndio kufungwa bao huko," aliongea Tresha na kumfanya Kanali kutabasamu.

"Sheria ya mchezo ni dakika tisini, sidhani kama Mgweno aliingia uwanjani bila ya kuwa na mbinu nyingine ya kushinda, unaweza kukubali kufungwa moja ili ushinde mbili ndio maana kipindi chote cha uchaguzi Mgweno alitulia na hakukuwa na kashikashi upande wa Abubakari kuwa mgombea na hatimae kuwa rais, lakini katika kipindi hicho haikumaanisha Mgweno pia alikuwa hafanyi kitu, kwanzia swala la kumshawishi Madam wa Taifa ili akutane na Mzee wa Taifa kwa siri na kuendelea."

"Dastani haya yote tumejadili kwanini bado unayarudia, hebu acha kuzunguka na nenda moja kwa moja unachotaka kumaanisha," aliongea Tresha huku akijifanyisha kuwa na usingizi, ila upande wa Kanali alionekana kusita kuongea.

"Unaonaje kuhusu kifo cha ghafla cha Kanali Hebert Kijazi?"

"Si wametoa taarifa amefariki kutokana na ajali wakati wa Drill mission huko Chole?" Aliongea Tresha.

"Hivi unadhani inaweza kuwa rahisi kwa mwanajeshi mwenye nishati za mbingu na ardhi kupata ajali wakati wa mafunzo? Tena Hebert ni mwanajeshi cheo cha kanali yule ni ngumu kushiriki moja kwa moja zaidi ya kutoa maagizo."

"Kwa ninavyomjua Hebert alivyojaa sifa ni kweli unachoongea, ujivuni wake usingemfanya kushiriki moja kwa moja."

"Umenipata sasa, hebu angalia hizo picha kwanza," aliongea Kanali huku akiwa na hali tofauti katika macho yake lakini Tresha hakuona na aligeuka na kumrushia simu akiwa kawaida na mwanamke huyo aliangalia kwa pupa.

"Huyu si ni Hamza au namfananisha?"

"Ndio mwenyewe na picha hio imepigwa jana mchana, unaowaona hao ni FO wa kitengo cha Malibu na wanatoka kisiwani chole kwenye Drill." FO ni field officer

"Unamaanisha huyu Hamza alikuwa pia kwenye Drill pamoja na Hebert? Kama ni hivyo unataka kusema Hamza ndio kamuua Hebert?" Aliongea kwa mshangao.

"Sina uhakika lakini uwezekano huu upo, taarifa za kisiwani zimekuwa nyeti mno, ila nina uhakika kuna swala kubwa ambalo limetokea zaidi ya swala la Hebert kufariki, kulikuwa na ulinzi mkubwa mno na hata uwepo wa Hamza kisiwani naamini ni sehemu ya kuimarisha ulinzi , sina hakika kama Nyakasura alikuwepo"

"Unamaanisha nini kusema hivyo?"

"Tresha unajua ninachomaanisha? Kama tukirudi siku nne nyuma juu ya ulichofanya" Aliongea Dastani na sauti yake ilibadilika ghafla.

"Dastani mbona hivyo?"

"Swipe mara tatu uangalie picha kwenye simu yangu," aliongea na Tresha alimwangalai kwanza kanali na kisha alienda mbele akiangalia picha katika simu ya Kanali na mara bada ya kufikia picha hio macho yalimtoka lakini ni kwa sekunde tu kwani palepale alifyatuka kama mshale na kumrushia Dastani shuka.

"Wewe M*laya leo nakuua hapa hapa ulidhani sitojua," aliongea Dastani kwa hasira.

ITAENDELEA NEXT WEEK .watsap me 0687151346
 
Cool🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom