haukupita muda kabla kabla ya watu waliokabidhiwa jukumu la kumwangalia hawajatoa taarifa kuwa alikuwa mtu wa BOSS. Habari hiyo ilimuumiza sana Kombora. Alitoa amri kuwa mtu huyo aliyejiita Clay achunguzwe kwa makini sana, kwani kwa vyovyote leo ilikuwa siku ya mwisho iliyotolewa na utawala huo haramu na lazima angekuwa na jambo la kuarifu kwa mabwana zake.
Baada ya hayo Insipekta Kombora aliendelea na shughuli katika ofisi yake. Alipokea na kujibu simu na walkie talkie nyingi ambazo hakuona kama zilikuwa zikimsaidia chochote. Aliwasiliana na maofisa wenzake katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Angola, Msumbiji, Naijeria na kwingineko kujaribu kuona wamefikia wapi. Hakuna alichopata zaidi zaidi ya yale aliyotegemea. Kwamba wananchi walikuwa wakitaabika na kulalamika mitaani katika hali ya hofu kubwa. Kwamba hata makazini hawakuwa wamekwenda.
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA
Baada ya hayo Kombora aliendelea na shughuli katika ofisi yake. Alipokea na kujibu simu na walkie talkie nyingi ambazo hakuona kama zilimsaidia chochote. Aliwasiliana na wenzake wa Zambia, Zimbabwe, Angola, Msumbiji, Naijeria na kwingineko kujaribu kuona wamefikia wapi. Hakuna alichokipata Zaidi ya yale aliyotegemea, kwamba wananchi walikuwa wakitaabika na kulalamika mitaani katika hali ya hofu kubwa, kwamba hawakwenda hata kazini. Ilikuwa kama waliokuwa wakisubiri kifo na maafa hayo. Watu wengi walizifungulia redio na televisheni zao kusubiri habari mbaya kokote Afrika. Na kwamba ingawa vyombo vya habari vya dunia nzima viliendelea na ratiba zao kama kawaida, lakini ilikuwa dhahiri kuwa kuna jambo, zito na la kutisha, ambalo lilikuwa likisubiriwa na kila mtangazaji. Kombora aliachana na taarifa hizo na kuulizia maendeleo ya maofisa ambao aliwakabadhi jukumu la kumtazama Clay na yote anayoyafanya. Haikumpendeza aliposikia kuwa alikuwa katika hali ya kawaida, kama ambaye hakuwa na lolote la kufanya.
“Endeleeni kumwangalia kwa makini,” aliwaamuru
SASA ENDELEA
.
Ofisi ilikuwa haikaliki. Kila Kombora alipojaribu kutulia juu ya kiti, kiti hakikuelekea kuafikiana naye. Kila alipoinuka ili atoke, hakujua angeelekea wapi. Unawezaje kutulia na huku unahesabu saa kusubiri kifo au maafa ya kusikitisha ambayo ni aibu kwako, kwa taifa lako na bara lako zima? Aliendelea kutaabika kimwili na kimawazo, akipokea na kusikiliza habari kutoka sehemu mbalimbali. Mara zilimfikia habari za Joram na Nuru kuwa walikuwa wameingia Afrika Kusini na kuomba hifadhi ya kisiasa. Kwa kombora zilikuwa habari za kushangaza sana. Habari za kusikitisha. Habari zinazotia aibu. Joram Afrika kusini! Hata hivyo, alikwishachoka kushangazwa na habari za kijana huyu anayeitwa Joram. Mambo yote aliyokuwa akiyafanya, ambayo yaliwafikia watu wa habari, Kombora aliyasikia au kuyaona katika vyombo vya habari. Angeweza kumsifu Joram kwa mbwembwe zake ambazo ziliwafanya polisi wote wa