Simulizi ya Kijasusi: Tutarudi Na Roho Zetu?

Simulizi ya Kijasusi: Tutarudi Na Roho Zetu?

SEHEMU YA 57


Umaarufu wa Von Iron dhidi ya ngozi nyeusi ulichipuka katika roho yake tangu utotoni baada ya kukua katika familia ya kitajiri ambayo iliwatenda waafrika kama wanyama. Hayati baba yake alikuwa na mgodi wa dhahabu. Watumishi wengi walifanya kazi humo huku wakilipwa ujira hafifu mno kiasi cha kuwafanya washindwe kuyamudu maisha. Jambo hilo hakuna aliyeonekana kulijali, hata katika fikra za Von ikajengeka kwamba mtu mweusi ni chombo cha mtu mweupe, ambacho hakina haki wala thamani.
Halafu ikatukia maafa katika mgodi. Baba yake alikuwa katika moja ya ziara zake adimu wakati ilipotokea hitilafu hii ambayo hadi leo chanzo chake hakifahamiki. Hitilafu hiyo ilisababisha maafa makubwa kwa wafanyakazi wengi, weusi kwa weupe. Hayati Iron mwenyewe aliponea chupuchupu. Kama asingejitokeza mtumishi wa Kiafrika, mzee mkongwe, ambaye alitumia nguvu zake zote kumtoa katika chumba kilichokuwa kimefunikwa kwa mawe, siku hiyo angeyapoteza maisha yake. Hata hivyo, jukumu hilo lilimgharimu mzee huyo maisha yake kutokana na majeraha mabaya aliyopata. Kifo hicho kilimsikitisha sana mzee Iron hata akajitolea kuishi na mtoto pekee wa mzee huyo ambaye alikuwa msichana mzuri, ingawa uzuri huo ulipotoshwa na unyonge aliokuwa nao rohoni. Uamuzi wa kuishi na Mwafrika katika nyumba moja, ukiwa jambo geni sana wakati huo, uliisababishia familia yake mgogoro mkubwa, hasa mkewe. Lakini Iron hakulikubali hilo asilani. Badala yake akazidisha mapenzi kwa msichana huyo huku akiahidi kumpeleka masomoni, nje ya nchi.
Halafu ikatokea. Mzee Iron akafumaniwa na msichana huyo. Ilikuwa habari iliyojaa aibu kubwa masikioni mwa kila mtu mweupe. Lakini Iron hakuona aibu. Alikitetea kitendo chake na kukataa matakwa ya mkewe kwamba msichana huyo yatima afukuzwe. Hata mkewe alipotishia kujiua Iron hakukubali kumtupia msichana huyo lawama ambazo hazikumstahili. Ikatokea tena. Wakafumaniwa kwa mara ya tatu. Hapo mama Iron hakustahamili zaidi. Alirudi chumbani ambako alichukua bastola na kumwua msichana yule mweusi.
Mzee Iron alizirai kwa hasira. Fahamu zilipomrudia aliipokonya bastola hiyo kutoka mikononi mwa mkewe na kumpiga risasi mbili kifuani. Kisha alijilenga kichwa na kufyatua risasi zote zilizosalia. Vifo vyao vilikuwa simulizi kubwa mitaani kwa muda mrefu. Vilimwacha Von katika msiba wa uyatima, msiba ambao ulizaa hasira dhidi ya mtu mweusi; akijua kuwa ni mtu mweusi aliyemnyima haki ya kuwa na wazazi. Jambo hilo lilimfanya siku zote awe mstari wa mbele katika kutukuza na kutekeleza taratibu zote za ubaguzi. Daima alikuwa mkatili kuliko wakatili, mnyama kuliko wanyama dhidi ya mtu mweusi. Matokeo yake yakawa kupata vyeo vilivyomwezesha kuwa na mamlaka juu ya uhai na kifo kwa kila mtu mweusi katika shirika hili la kijasusi. Wengi waliuawa kwa ajili yake, mengi yaliendelea kufanyika ili
 
kumkomoa mtu mweusi kutokana na mapendekezo yake. Lakini hakukoma kuendelea kubuni. Mtambo uliokuwa angani ukisubiri kuiharibu Afrika huru ulikuwa moja tu kati ya ubunifu wake.
Pamoja na kutenda mengi ya kikatili, pamoja na kuhakikisha watu weusi wengi wasio na hatia wakipoteza maisha yao, bado Von hakuona kama viumbe hawa walielekea kumpigia mtu mweupe magoti. Badala yake waliendelea kusimama kiume wakitetea haki yao. Alipokufa huyu, alizaliwa huyu, wimbo uleule ukiwa mdomoni. Hata Mandela, ambaye alikuwa kifungoni, alipoteswa bado aliendelea kuwa na msimamo uleule. Hilo, kiasi lilimtisha sana kaburu Von. Hakuwaelewa kabisa watu hawa. Wana nini katika damu yao?

Swali hilo lilikuwa likimletea maswali mengine ambayo yalijenga hisia fulani, maswali yaligongana kichwani mwake. Alikuwa akijiuliza: baba yake aliona nini katika nywele kavu, ngozi nyeusi na sura ya kusikitisha ya yule msichana wa Kiafrika hata akadiriki kumwua mkewe na kujiua mwenyewe! Aliwahi kusikia hadithi ya mtu mwingine ambaye alimwacha mkewe na kukimbia na msichana mweusi hadi Marekani ambako walifunga ndoa. Wana nini watu hawa? Iko siri gani ndani ya ngozi zao zinazotisha? Labda ingebidi alifumbue fumbo hili kwa kumpata mmoja ili aonje? Lakini...mweusi... Hapana. Mara kwa mara aliyafukuzia mbali maswali hayo ambayo yalimjia bila taarifa, hasa alipoukumbuka uyatima wake.
"Cheers," Von aliropoka tena.
Wenzake wakageuka na kumtazama kwa mshangao. Kisha wakatabasamu kimyakimya, wakiendelea kunywa taratibu. Baada ya vinywaji hivyo, Von aliamua waendelee na kikao chao.
Walivuta mafaili ya suala la Chonde na kuangalia wamefikia wapi juu ya kisa cha kifo chake na mali zake zilielekea wapi. Bado haikueleweka nani alimuua na maiti ya pili chumbani mle ilikuwa ya nani. Zaidi haikufahamika vitu alivyokuwa navyo, ambavyo ni vya hatari na siri kubwa, vilikwenda wapi. Kitu kimoja walikuwa na hakika nacho. Vitu hivyo havikufika mikononi mwa polisi, jambo ambalo liliwafanya waafikiane kuwa watu waliomwua Chonde na kumwibia pesa nyingi na vitu alivyokuwanavyo ni majambazi wa kawaida, ambayo yangevitupa vifaa vile muhimu kama takataka na nyaraka za siri kama uchafu. Kitu ambacho wangejua kukitumia ni pesa za Tanzania na za kigeni ambazo zingewachukua miezi mingi kabla ya kuzimaliza.
Pesa hazikuwa tatizo kwa akina Von. Walilitupa suala hilo kando bila kinyongo, hasa wakijua kuwa tayari mtu wao mwingine, Clay, alikuwa nchini Tanzania akiwa na kila kitu kilichohitajika na tayari kwa yote waliyohitaji kufanya. Alikuwa na nafasi nzuri zaidi ya Chonde kwani uongo aliokwenda nao ungemfanya aonekane kama almasi machoni mwa maafisa wa usalama wa nchi zote za mstari wa mbele za Kiafrika.
"Nadhani iliyobaki ni kuongeza ulinzi katika mtambo wetu," Von aliendelea. “Ingawa Clay yuko kwao na
 
atatuarifu kila wanachokusudia kufanya, lakini kuna mengine watakayoshindwa kumwambia. Ni wazi kuwa watatumwa wapelelezi waje, lakini sitaki warudi. Nadhani tunaelewana."
Akaungwa mkono.
Mara simu ya dharura ikaanza kulia. Ikiwa simu ambayo hulia kwa nadra sana, Von aliinua mkono na kuidaka mara moja. "Von hapa," akanguruma katika chombo cha kusemea.
"Bosi, hapa ni kikosi cha ulinzi wa anga. Ndege zetu za ulinzi zimeizunguka ndege moja ambayo ina watu wanne tu, rubani na msaidizi wake na abiria wawili ambao ni mwanamke na mwanamume. Rubani wa ndege hiyo anaomba kutua, akidai kuwa ametekwa nyara na abiria hao ambao wamejitambulisha kama Joram Kiango na mpenzi wake Nuru. Tunauliza kama tuwaruhusu kutua au tuwalipue".
"Nani, Joram?" Von aliuliza.
"Ndiyo. Joram Kiango. Yule..."
Mara Von akalikumbuka jina hilo vizuri. Halikuwa jina la kupendeza hata chembe masikioni mwake, ingawa siku mbili tatu zilizopita limesikika kwa namna ya kupendeza kiasi. Joram kuja Afrika Kusini! Baada ya kuharibu mipango yao mingi ya kuikomoa Tanzania! Bila shaka ni kujaribu kujificha baada ya kuiibia nchi yake akiba yote ya pesa za kigeni. Vizuri. Tutampa hifadhi ya kudumu. Anaweza kujificha milele katika makaburi yetu. Hatuna roho mbaya.
"Umesema Joram siyo? Sikia. Huna haja ya kutumia silaha kubwa. Anaweza kufa polepole. Mwambie atue."
Kwa Afrika Kusini ilikuwa kama nafasi ya dhahabu. Vyombo vyote vya habari vilishangilia kwa nguvu kuwasili kwa Joram na Nuru katika nchi yao. Waliipamba habari hiyo kwa kutia chumvi nyingi juu ya wizi wake. Walieleza jinsi alivyopokonya pesa hizo, alivyozitumia kwa starehe sehemu mbalimbali duniani, alivyofaulu kuwalaghai polisi wote wa dunia, na mwisho alivyoona hana hila zaidi ya kukimbilia Afrika Kusini, ili ajifiche maisha.
"Huu ni mfano hai kwa watu weusi kote ulimwenguni," mtangazaji mmoja wa televisheni alieleza. "Hakuna asiyemfahamu huyu Joram. Alijifanya mpigania haki, usawa na usalama wa watu wake. Amesababisha vifo vya watu wengi ambao walikuwa na nia njema ya kuikomboa nchi yake. Ndivyo walivyo watu weusi wote. Wanawalaghai wenzi wao na kuwafanya waote mikia misituni eti wakidai haki na uhuru. Matokeo yake ni kuwafanya, hao wenzi wao, vijakazi, wakati wao wakituna matumbo mara tu baada ya kupata madaraka. Natumaini watu weusi wote mnaodanganywa mtaitumia nafasi hii kuuona ukweli wa mambo. Ngozi nyeusi ni dalili ya laana. Nywele fupi ni dalili ya akili ndogo. Bila hekima na uongozi wa mtu mweupe Afrika ingekuwa bado gizani, na endapo ataondoka mtu mweupe giza litarudi..."
Hayo yalisemwa baada ya watu kuwatazama Joram na Nuru wakitoka katika ndege iliyowaleta, huku wakiwa wametanguliwa na rubani ambaye walikuwa wamemshikia bastola. Nje ya ndege Joram aliitupa
 
SEHEMU YA 60

chini bastola yake na kuweka mikono yake juu. Ndipo Polisi wa makaburu ambao walikuwa wameuzingira uwanja wakiwasubiri, wakajitokeza na kuwakimbilia. Wakawavamia na kuwakagua harakaharaka. Walipoona kuwa hawana silaha nyingine wakawaongoza kuliendea gari lililokuwa likisubiri. Muda wote huo kamera za televisheni na zile za wapiga picha wa magazeti ziliwaelekea Joram na Nuru kwa ukamilifu. Kama kuna chochote kilichowashangaza watazamaji ni jinsi sura za vijana hawa zilivyoonekana tulivu, nzuri, zisizo na dalili zozote za ugangwe kama walivyotegemea.
Msafara wa gari uliishia katika jumba moja kubwa lenye ghorofa kadhaa. Humo, badala ya lifti waliyoingia kuwapandisha juu iliwateremsha chini ambako walijikuta katika chumba kilichoelekea kuwa maalumu kwa kuhoji mateka. Askari waliokuwa nao waliamuru kusubiri, kisha wakatoka na kuufunga mlango nyuma yao. Baada ya muda waliletewa chakula na vinywaji. Wakala na kunywa.
Baada ya muda, kama walivyotegemea, walianza kutembelewa na maafisa wa upelelezi, ambao waliuliza maswali kemkem. Maswali yote waliyajibu kwa ukamilifu kama walivyojiandaa; kwamba walikuwa wameishiwa na hila za kuwaepuka INTERPOL wakaona hawana njia nyingine zaidi ya kukimbilia huku ambako wangehitaji hifadhi.
Baada ya maswali yalifuata mawaidha na badala ya mawaidha ikawa kashfa. "Wewe kama Joram Kiango ambaye nchi yako na Afrika nzima ilikutegemea huoni aibu kufanya ulivyofanya na kuja huku?" aliulizwa
"...Utajisikiaje utakapolazimika kufuata matakwa yote ya ubaguzi na kulazimika kushuhudia Waafrika wanavyonyanyaswa?"
"...Unaweza kukiri hadharani kuwa viongozi wote wa Afrika ni wadanganyifu na hawajui watendalo?"
"...Ukipewa bastola ili umuue mpigania uhuru yeyote atakayematwa, utafanyaje?"
"...Huyu msichana na uzuri wake wote ni malaya? Mbona anakubali kuandamana na mwizi?"
Yalisemwa mengi zaidi ya hayo. Yako ambayo Joram alijibu kwa namna ambavyo alijua walimtegemea kujibu. Mengine hakuyajibu, akijua kuwa walimtegemea kutojibu. Mengine ilimlazimu kuinama kwa haya akiwa na hakika kwamba walitarajia aone aibu. Baadhi ya maswali aliyakwepa kijanja akijua ni mitego iliyokusudiwa kumnasa.
Kutoka hapo walipelekwa katika chumba kilichokuwa na mitambo mingi ambayo eti ingeonyesha kama walikuwa wakisema ukweli au la. Waliwekwa katika mitambo hiyo na kuanza kuulizwa tena maswali. Yote hayo Joram alikwishamfafanulia Nuru kabla hawajaondoka Paris kuja Kinshasa, Zaire, ambako waliiteka nyara ndege ile ya kukodi. Alimweleza kuwa ambacho mtambo kama huo unaweza kuonyesha ni dalili za moyo kudunda na damu kuchemka mara unapoulizwa swali ambalo litakushtua au unapobuni uongo. Hivyo, endapo utazungumza kwa kujiamini haitaonekana dalili yoyote.
Ndivyo ilivyotukia. Saa chache baadaye walichukukuliwa na gari kutoka katika chumba hicho na kupelekwa katikati ya mji ambako waliingizwa katika nyumba moja kubwa na kuelekezwa katika chumba kilichokuwa na vitanda viwili. Humo walikuta mizigo yao yote. Ingawa mizigo yao ilikuwa kama
 
ilivyokuwa, lakini Joram hakusita kugundua kuwa tayari ilikuwa imekaguliwa kwa ukamilifu. Hilo alilithibitisha baada ya kufungua na kukuta kila kitu kimo isipokuwa furushi la pesa zilizokuwa zimesalia. Hilo pia alilitegemea. Hivyo, hakubabaika. Akamwendea Nuru na kumvuta mkono akimwelekeza kitandani ambako alimketisha ili ampumzike kidogo.
"Pole,” alimwambia.
"Kwa?"
"Usumbufu."
"Mbona bado sijasumbuka. Naamini huu ni mwanzo tu, kuna mengi yanayokuja na nitakuwa tayari kuyakabili yote..."
"Shii," Joram alimnyamazisha. “Usijisikie huru kiasi hicho," alinong'ona. "Bado tuko chini ya ulinzi mkali. Yawezekana wanatutazama na kutusikiliza. Kiswahili si lugha ngumu kiasi hicho. Endelea kujihadhari."

Moyoni Joram alikuwa na sherehe kubwa. Alikuwa akishangilia mafanikio ya msafara huo ambao ulienda kama alivyokusudia kuelekea kuzaa matunda. Kufika Afrika Kusini na kupata mapokezi yenye hadhi kwa kiwango hiki ilikuwa jambo pekee la pili ambalo alilihitaji sana. Jambo la awali ambalo alihakikisha limefanikiwa kabla hajabandua mguu wakekuiacha dunia huru na kujitosa jehanamu kiasi hiki ilikuwa kulisafirisha sanduku lake ambalo lilikuwa na kila kitu alichohitaji katika jukumu lililokuwa mbele yake. Kati ya vitu vilivyokuwemo ni pamoja na pesa za matumizi muhimu, silaha aina aina, madawa ya kila aina, ramani mbalimbali, ngozi na sura za bandia ambazo zingemfanya aonekane mtu mweupe, na zaidi ya yote ni vile vijigololi maalumu ambavyo alivipata kutoka kwa hayati Chonde.

Ilikuwa imemgharimu uongo mkubwa na pesa kuweza kulifikisha sanduku lile katika nchi hii. Alikuwa ametumia hila za kumwendea mfanyabiashara wa Kimarekani ambaye alikuwa akisafirisha mizigo yake moja kwa moja kutoka Ufaransa. Baada ya kujijenga kwake kwa urafiki bandia alimhadaa kuwa amepata oda ya kuuza madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini. Mmarekani huyo alikataa kabisa kujihusisha kwa hali yoyote katika biashara ya aina hiyo. Joram alikazimika kumpigia magoti kwa maneno huku akimpa pesa nyingi na kumwahidi sehemu kubwa ya faida. Ndipo sanduku hilo liliposafiri pamoja na mizigo mingine muhimu ya Joram. Na aliarifiwa kuwa sanduku hilo limefika salama. Ilimpendeza sana Joram kuona kati ya watu wengi waliokuja kiwanjani kushuhudia wateka nyara hao wakitelemka kutoka ndani ya ndege, mmoja wao alikuwa Mmarekani huyo aliyeitwa Moore. Ilimpendeza zaidi kuwa Moore hakuweza kufahamu kuwa mteka nyara huyo ndiye yule aliyekuwa rafiki yake siku tatu zilizopita nchini Ufaransa. Joram akiwa amekariri ramani ya nyumba ya Moore kama anavyovifahamu viganja vyake vya mkono, alikuwa akiisubiri kwa kiu kibwa fursa ya kuweka mikononi mwake mizigo yake.

Kabla ya kuoga kama alivyohitaji kufanya, Joram alijitia shughuli na kufanya kama anayepanga vitu chumbani kwake vizuri. Alichokuwa akifanya hasa ni kitu au vitu fulani na haukupita muda kabla ya
 
kukiona alichokuwa akitafuta. Kipande kidogo sana cha kioo kilichokuwa kimejitokeza sakafuni katika pembe moja ya chumba kama kilichosahauriwa na waashi kwa bahati mbaya. Joram alijua kuwa nyuma yake kipande hicho kulikuwa na nyaya ambazo zilisafiri hadi kwenye mtambo ambao ulikuwa na jukumu la kupeperusha kila wanachoongea au hata kuwaona. Baada ya kuona hayo Joram alilidhika, akijua kuwa alikuwa hana haraka ya kuwa msiri. Alihitaji faragha kwa usiku mmoja tu, na katika usiku huo alijua ambacho angefanya kuufanya mtambo huo ushindwe kuwajibika kwa dakika kadhaa.

Wakaoga.

Wakalala.

Jasho jembamba lilikuwa likiwatoka maofisa wanne wa Boss ambao walikuwa katika chumba fulani wakiwashuhudia Joram na Nuru walipokuwa wakifanya mapenzi katika chumba chao. Maofisa hao walikuwa wamekaa katika chumba hicho kwa muda mrefu, dhamira yao kuu ikiwa kupata hakika kama kweli Joram alikuwa hana hila nyingine iliyomleta Afrika Kusini zaidi ya ukimbizi. Taarifa za maofisa wote waliotumwa kuwahoji na ambao walikagua mizigo yao haikuonyesha hila wala ila yoyote. Hata hivyo upinzani uliokuwepo uliishia kuamuliwa kuwa wapewe chumba hiki na kuachiwa uhuru kiasi fulani ili waendelee kuchunguzwa. Chumba hiki kilikuwa maalumu na siri kubwa isipokuwa kwa maofisa wachache wa ngazi za juu. Ndipo jukumu la kuwatazama Joram na Nuru likawaangukia kaburu Von Iron na wenzake.

Ndipo walipolazimika kutokwa na jasho. Kwani walikuwa wakitazama kwa namna moja ilikuwa kama picha ya kupendeza sana, kwa maaana nyingine picha ya kuchukiza, inayotesa na kuadhibu.

Ilikuwa picha ya kupendeza wakati walipokuwa wakiwatazama Joram na mpenzi wake Nuru walipokuwa wakitazamana kwa mapenzi pindi wakati wakijiandaa kulala. Ikaanza kuchukiza walipoanza kuvua mavazi yao na kuketi kama walivyozaliwa huku wakibusiana. Na ilianza kutesa walipojibwaga kitandani na kufanya mapenzi kiroho mbaya bila kujali au kujua kama wanatazamwa, kana kwamba walikuwa wakiwaonyesha watazamani kwa makusudi.

Von Iron aliuzima mtambo huo na kulifuta jasho lililokuwa katika paji lake la uso. Hakujiamini kuwatazama wenzake machoni, akihofu wasije wakasoma kitu alichokuwa akikisoma akilini. "Tukutane kesho..." Von aliamuru akianza kutoka nje. Bila kuinua macho aliweza kuhisi kuwa wenzake walikuwa wakimhurumia zaidi ya walivyokuwa wakijihurumia wao. Alijua vilevile kuwa wenzake hao walijua kama alivyojua yeye kuwa baada ya kuagana nao angerudi katika chumba hicho.

Alirudi.

Akiwa peke yake aliwatazama kwa makini na uhuru zaidi, akisherehekea kila hatua iliyofuata katika mapenzi yaliyokuwa yakiendelea mtindo mmoja juu ya kitanda. Tangu alipokuwa amewaona Nuru na Joram katika televisheni hajua kuwa wangeweza kuwa wazuri kiasi hiki. Kadhalika hakutegemea kuwa Mwafrika aliyevua nguo angeweza kuwa kiumbe mzuri kama hawa, aliwategemea kuwa viumbe wa kutisha sana kama mizimu. Kumbe sivyo.
 
Aliendelea kuwatazama. Alijipinda na kujinyoosha kwa maumivu na tamaa kubwa huku mkono wake mmoja akiubembeleza uume wake, mkono wake wa pili ukiwa umelea kichwa kwa wivu wa masikitiko. Starehe au mateso yake yalikoma Joram alipozima taa.

Von alijifariji kwa kuizima mitambo hiyo na kubonyeza ile ambayo ilimfanya akague ulinzi na usalama wa ule mtambo wa nyuklia unaoendesha Satilaiti maalumu iliyoko angani ikisubiri kufanya kazi ambayo haitafutika katika kurasa za historia ya dunia. Aliuona ulinzi ulivyokuwa makini. Askari wanne wenye machine guns walikuwa wakipita kwa zamu kulikagua jengo hilo. Ndani mafunzi wenye silaha walikuwa machio wakikagua mwenendo wa mtambo huo kwa umakini na uangalifu mkubwa. Von aliweza kuona katika screen kubwa iliyokuwa mbele ya wanasayansi hao jinsi setileiti hiyo ilivyokuwa ikielea huku na huko katika bahari ya Hindi kando ya pwani ya Afrika Mashariki. Alitabasamu kidogo alipojikumbusha utaalamu wa hali ya juu uliotumika katika kuunda chombo hicho hata kisiweze kuonekana kwa macho ya kawaida.

Kisha alibonyeza mahali fulani kuondoa mtambo huo machoni kwake. Badala yake alibonyeza mahali ambapo palimwezesha kuona gereza la ardhini ambamo kulikuwa na mateka au wafungwa ambao walitakiwa kuteswa hadi kufa. Humo kulikuwa na kila aina ya mateso. Haikuwepo njia yoyote ya kuweza kutoka isipokuwa kwa funguo maalumu ambazo alidhihifadhi yeye mwenyewe.Von aliwatazama wafungwa au mateka hao waliokuwa wakikaribia kufa. Baadhi yao walikuwa weupe, Mmarekani mmoja ambaye alikuwa mpumbavu kiasi cha kuamua kuwasaidia wapigania haki wa Afrika Kusini, pia walikuwepo Warusi wawili ambao pia tabia zao hazikuwa tofauti na mzungu huyo pamoja na watu weusi watatu. Ni hawa watu weusi ambao walimfanya Von aangue kicheko kwa sauti. Alijiuliza walikuwa wamepatwa na nini weusi hawa hata wakathubutu kujileta wenyewe huku kama wapumbavu. Mtu atajipeleka jehanamu na kutegemea atatoka salama?

Zimesikika habari nyingi za watu ambao waliwahi kufa na baada ya siku kadhaa kufufuka. Watu hao hudai kuwa walipokuwa wafu wamefika peponi na kuwaona malaika. Haijawa kutokea hata mtu mmoja ambaye aliwahi kwenda jehanamu na akarudi duniani. Hawa weusi aliwaona kama watu walipenda sana kufa vifo vya kikatili. Jambo la kusikitisha kwao ni kwamba BOSS iliarifiwa tangu walipoondoka Naijeria na Tanzania na kuja Botswana. Iliarifiwa pia walipoanza mbibu za kuvuka mpaka. Hivyo hila zao za mmoja kujifanya wendawazimu asiyejua analofanya na mwingine kujitia mkimbizi anayeishi kambi ya wapigania uhuru hazikuwa na mafanikio yoyote. Von hakupenda kuwaona ana kwa ana. Aliamua wafungiwe katika chumba cha mauti wasubiri kifo. Hawa walikuwa wawili tu kati ya wanane ambao
 
walikuwa wamekamatwa siku mbili zilizopita. Wawili walikuwa wameuawa kwa mateso wakati wakihojiwa. Mmoja alikuwa amejiua mwenyewe kwa sumu baada ya kumvamia askari aliyekuwa akimhoji na kumjeruhi vibaya kwa kisu kabla hajameza vidonge ambavyo vilimuua mwenyewe.

Wapelelezi hawa walikuwa ni matokeo ya juhudi za kuthibitisha uwezekano wa kuwepo kwa mtambo maalumu unaoziadhibu nchi za Kiafrika. Von alifahamu kuwa bado wangekuja wengi zaidi, weupe kwa weusi, lakini kamwe wasingefika popote pa haja. Na kamwe wasingefika popote kwani zilikuwa zimesalia siku mbili tu kabla ya Afrika huru kuipigia magoti Afrika Kusini na kusubiri vilio na maombolezo yasiyo na mfano. Von alicheka tena, safari hii kwa kujipongeza akijua kuwa sifa ndogo kuwa na wadhifa kama aliokuwa nao sasa. Roho za watu wengi kuwa mikononi mwako zikisubiri tamko lako kabla ya kuteketezwa!

Kisha Von aliufunga mtambo huo na kurudi nyumbani kwake. Akiwa kapera ambaye hakujua lini angeoa alijikuta akikosa usingizi alijikuta akimfikiria Nuru na kumwonea Joram wivu. Bila kufahamu anachokifanya Von alijikuta akiapa kwa jina la Mungu kuwa asingekufa kabla hajamuonja. "Mara moja tu..." alijiambia. "Nione wana nini wanawake weusi..."

Kesho yake aliamuru Joram na Nuru waletwe katika ofisi yake. Akiwa amezungukwa na wasaidizi wake Von alijitahidi kuwatazama Joram na Nuru kwa namna tofauti kabisa na ile iliyokuwa ikipita katika akili yake.

"Sina haja ya kuwahoji chochote", Von aliwaambia kwa sauti nzito. "Kwa kiasi mlichohojiwa naamini mmeonyesha kuwa mmechoshwa na upuuzi wa hawa viongozi wanaojiita wanamapinduzi katika nchi zenu. Sivyo?"

"Kwa maana hiyo mngependa kuishi huku daima. Msimamo wenu ni wa kishujaa. Nawapenda watu shujaa. Ni hilo ambalo limenisukuma kuwaacha hai pamoja na kuwapa heshima ya kuwaita hapa ili niwape habari njema".

Joram akiwa amesimama mbele yake, akiwa kamshika Nuru mkono, hakuwa na haja ya kuambiwa huyu ni nani katika nchi hii. Alimfahamu mara moja kuwa alikuwa mkuu wa shirika la kijasusi la utawala huu. Kwa maana nyingine alikuwa adui yake namba moja. Mtu ambaye asingeondoka bila kumpa adhabu ya risasi ya kichwa kwa hatia ya kusababisha maafa kwa Waafrika wengi wasio na hatia. Hata hivyo Joram hakuonyesha dalili yoyote katika macho yake alipouliza kwa upole, "Habari njema ipi? Tumeruhusiwa kupewa uhuru zaidi ya huu tulionao? Tunajiona kama ndio tuko kifungoni".

"Mko huru kuliko mnavyostahili", Von alimjibu Joram. "Habari njema niliyotaka kuwapeni ni juu ya uhalibifu ambao utazitokea nchi za Kiafrika kesho saa nne mchana endapo hawatawatuma viongozi wao hapa leo kuweka saini mikataba ya kuwa watiifu kwa utawala huu na kutothubutu kuwasaidia
 
SEHEMU YA 65

wendawazimu wanaodai uhuru wa Namibia na haki hapa Afrika Kusini. Kama hawatafanya hivyo hadi saa tatu na nusu za mchana. Nyie mtapewa heshima ya kushuhudia moja kwa moja Ikulu zinavyoungua, majengo yanavyoteketea na watu kupoteza maisha. Mtabahatika kushuhudia jambo la kupendeza. Jambo la kihistoria".

Macho yake yaliwatazama Joram na Nuru kwa umakini. Nao wakifahamu kuwa kuna kitu kilitakiwa kuonekana katika macho yao, Joram aliruhusu tabasamu kidogo huku Nuru akifuta machozi.

"Ni habari njema", Joram alisema polepole baadaye akauliza. "Habari njema..., tunaweza kuruhusiwa kurudi chumbani kwetu?".

Binadamu hajapata kuwa na adui mwingine, mkubwa na mkatili katika maisha yake zaidi ya kifo. Ni kifo pekee ambacho kimeishinda akili ya binadamu. Hakukosea yule mwanamuziki aliyeimba "kifo hakina huruma, kifo ni kiboko yao". Hutokea binadamu akawa na shughuli zote, siku nenda rudi bila kukipa kifo wazo lolote hadi kinapotokea bila kutegemewa. Ni hiyo sababu pekee inalomfanya mwanadamu asitokwe na jasho la hofu siku zote za maisha yake kwa kuogopa kifo. Kwa vile hutokea bila ya kutegemewa.

Hivyo hakuna kifo kibaya kama kifo cha kusubiri siku na saa. Hasa kifo cha kinyama na cha kikatili kama hiki ambacho kilikuwa kikitegemewa na watu kadha wa kadha katika nchi kadha wa kadha za Kiafrika. Leo ilikuwa imewadia siku ile. Siku ambayo Afrika ya Kusini ilikuwa imetoa kuwa ingekuwa ya mwisho kabla ya kuachia pigo la mwisho ambalo lingeiteketeza miji yote ya nchi zilizoko mstari wa mbele.

Pamoja na ukweli kwamba tukio hili lilikuwa limeamriwa kuwa siri kubwa sana miongoni mwa wahusika, kama yale mengine ambayo huishia katika masikio ya wachache na hutoweka bila ya raia wa kawaida kuyapata, lakini hili kwa njia moja ama nyingine lilikuwa limevuja na kusambaa mitaani. Jambo ambalo lilisababisha mashaka na hofu kubwa mitaani. Wananchi waumini wa dini walitoroka makazini na kukimbilia kwenye makanisa na misikiti ili kutubu dhambi zao zote na kumbembeleza Muumba awanasuwe awanasuwe katika janga hili. Wale ambao hawakumwamini Mungu walitulia katika vikundi vikundi wakizungumza kwa utulivu. Wachache sana waliamua kuyamalizia maisha yao huku wakinywa pombe katika baa ambazo hazikufunguliwa milango.

Viongozi wa Chama na Serikali walikuwa katika vikao vya dharura wakijaribu kujadiliana hili na lile. Lolote la haja halikupatikana, japokuwa yalitokea mapendekezo mengi. Jambo ambalo kila mmoja alitamani kutamka ingawa ulimi ulishindwa kutamka hadharani kwa aibu, ni ambalo lingewahakikishia wananchi uhai na usalama wao. Lakini maadamu ungekuwa uhai usio na uhuru, na usalama usio na uhakika na hakuna aliyethubutu kupendekeza hivyo. Iliyonaki ilikuwa kupeana moyo tu kuwa haiweze
 
kutokea, na endapo itatokea cha kufanya ni kujaribu kuepuka majengo ambayo yanaweza kuelekea kuyavuta macho ya muuaji. Ilielezwa pia kuwa kote nchini wananchi walikuwa wakichimba mahandaki kwa ajili ya kujificha.

Ikulu, Rais na baraza lake la mawaziri walikuwa katika kikao cha muda mrefu. Kikao ambacho kilichukua siku nzima, hata usiku ukaanza kukaribia. Inangawa kilikuwa kikao cha siri sana, lakini ilikuwa dhahiri kuwa chochote ambacho kilikuwa kikijadiliwa ndani hakikupata ufumbuzi ya tatizo. Mmoja alikuwa amependekeza kwa mara nyingine kuwa nafasi hiyo itumike kuivamia Afrika Kusini kijeshi, "Ili tukomeshe kabisa suala hili la kutishiwa na kuonewa mara kwa mara. Tutumie majeshi yetu yote ya nchi za mstari wa mbele kuingia nchini humo na kuanzisha mapambano ili kuunda utawala halali. Najua, adui ana jeshi imara na silaha kali sana. Lakini wingi witu wetu utasaidia tutashinda..."

Mapendekezo hayo yalijadiliwa lakini hayakuonekana kama yangekuwa jibu la kuziokoa nchi za Afrika na kumaliza tatizo ambalo lilikuwa mbele likisubiri saa chache ili litokee. mwingine akatoa wazo. "Si rahisi kutumia masaa manane yaliyobaki kukusanya majeshi na kuyaongoza katika nchi nyingine na kuanzisha vita. Zaidi yote, hatari au mkasa ambao uliokuwa ukisubiriwa ulikuwa ukitokea angani, hivyo uvamizi huo usingesaidia au kuzuia maafa hayo...". Baraza la mawaziri liliendelea kujadiliana kwa utulivu katika ukumbi huo wa Ikulu. Jengo hilo likiwa miongoni katika majengo kadhaa yaliyokuwa katika orodha ya kulipuliwa ilikuwa kana kwamba Rais na mawaziri wake walikuwa wameamua kikisubiri kifo hicho kwa pamoja; kufa kiofisa...

Binadamu aliyekuwa na hali mbaya kuliko wote nyumbani nchini Tanzania aliitwa Inspekta Mkwaju Kombora. Yeye alikuwa akitaabika kimwili na kiakili. Juhudi zake zote, pamoja na wenzake wa kutoka nchi mbalimbali, zilikuwa kama upuuzi. Upelelezi ulikuwa haukuzaa matunda yoyote yale. Na hasa upelelezi huo ulikuwa kama umewafanya wazidi kujipalia mkaa wa moto; kwani ilikuwa dhahiri kuwa kila jambo linaloafikiwa hapa wakati huo huo utawala wa makaburu unakuwa na taarifa nalo. Hayo yalithibitika alipoarifiwa kuwa wapelelezi wote waliotumwa kuingia Afrika Kusini walikuwa mikononi mwa makaburu. Ilikuwa kama waliopelekwa kufa makusudi kabisa. Jambo ambalo lilimfanya ashuku mara moja kwamba miongoni mwao alikuwemo chui aliyejivika ngozi ya kondoo.

Hivyo Insipekta Kombora aliugeuza upelelezi wake kutoka mstari wa mbele na kuanza kuchunguza mstari wa nyuma. Na haukupita muda kabla dalili hazijajitokeza kuwa huyu mgeni aliyedhaniwa kuwa msamaria mwema, ambaye alileta fununu nyingi kutoka Afrika Kusini angehitaji kuchunguzwa zaidi. Uchunguzi ukaanza katika vikosi vyote vya wapigania uhuru duniani, katika vyuo na hospitali ambazo alidai amepitia na hata Afrika Kusini. Taarifa zilizidi kuongeza haja ya kutazamwa kwa makini. Na
 
haukupita muda kabla kabla ya watu waliokabidhiwa jukumu la kumwangalia hawajatoa taarifa kuwa alikuwa mtu wa BOSS. Habari hiyo ilimuumiza sana Kombora. Alitoa amri kuwa mtu huyo aliyejiita Clay achunguzwe kwa makini sana, kwani kwa vyovyote leo ilikuwa siku ya mwisho iliyotolewa na utawala huo haramu na lazima angekuwa na jambo la kuarifu kwa mabwana zake.

Baada ya hayo Insipekta Kombora aliendelea na shughuli katika ofisi yake. Alipokea na kujibu simu na walkie talkie nyingi ambazo hakuona kama zilikuwa zikimsaidia chochote. Aliwasiliana na maofisa wenzake katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Angola, Msumbiji, Naijeria na kwingineko kujaribu kuona wamefikia wapi. Hakuna alichopata zaidi zaidi ya yale aliyotegemea. Kwamba wananchi walikuwa wakitaabika na kulalamika mitaani katika hali ya hofu kubwa. Kwamba hata makazini hawakuwa wamekwenda.





ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA

Baada ya hayo Kombora aliendelea na shughuli katika ofisi yake. Alipokea na kujibu simu na walkie talkie nyingi ambazo hakuona kama zilimsaidia chochote. Aliwasiliana na wenzake wa Zambia, Zimbabwe, Angola, Msumbiji, Naijeria na kwingineko kujaribu kuona wamefikia wapi. Hakuna alichokipata Zaidi ya yale aliyotegemea, kwamba wananchi walikuwa wakitaabika na kulalamika mitaani katika hali ya hofu kubwa, kwamba hawakwenda hata kazini. Ilikuwa kama waliokuwa wakisubiri kifo na maafa hayo. Watu wengi walizifungulia redio na televisheni zao kusubiri habari mbaya kokote Afrika. Na kwamba ingawa vyombo vya habari vya dunia nzima viliendelea na ratiba zao kama kawaida, lakini ilikuwa dhahiri kuwa kuna jambo, zito na la kutisha, ambalo lilikuwa likisubiriwa na kila mtangazaji. Kombora aliachana na taarifa hizo na kuulizia maendeleo ya maofisa ambao aliwakabadhi jukumu la kumtazama Clay na yote anayoyafanya. Haikumpendeza aliposikia kuwa alikuwa katika hali ya kawaida, kama ambaye hakuwa na lolote la kufanya.
“Endeleeni kumwangalia kwa makini,” aliwaamuru

SASA ENDELEA
.
Ofisi ilikuwa haikaliki. Kila Kombora alipojaribu kutulia juu ya kiti, kiti hakikuelekea kuafikiana naye. Kila alipoinuka ili atoke, hakujua angeelekea wapi. Unawezaje kutulia na huku unahesabu saa kusubiri kifo au maafa ya kusikitisha ambayo ni aibu kwako, kwa taifa lako na bara lako zima? Aliendelea kutaabika kimwili na kimawazo, akipokea na kusikiliza habari kutoka sehemu mbalimbali. Mara zilimfikia habari za Joram na Nuru kuwa walikuwa wameingia Afrika Kusini na kuomba hifadhi ya kisiasa. Kwa kombora zilikuwa habari za kushangaza sana. Habari za kusikitisha. Habari zinazotia aibu. Joram Afrika kusini! Hata hivyo, alikwishachoka kushangazwa na habari za kijana huyu anayeitwa Joram. Mambo yote aliyokuwa akiyafanya, ambayo yaliwafikia watu wa habari, Kombora aliyasikia au kuyaona katika vyombo vya habari. Angeweza kumsifu Joram kwa mbwembwe zake ambazo ziliwafanya polisi wote wa
 
miji mbalimbali na nchi zilizoendelea washindwe kumtia mikononi. Lakini kila alipokumbuka kuwa mbio hizo za Joram zilikuwa za kukimbiza akiba pekee za pesa ya kigeni alizoibia nchi yake alijisikia vibaya. Hayo yakifuatwa na tishio lililokuwa likizidi kusogea, vilimfanya ajilazimishe kuliondoa jina hilo akilini mwake.
“… Inspekta Kombora anaongea. Namba ngapi hiyo?...” alijibu sauti katika walkie talkie iliyokuwa mkononi mwake. Alipotajiwa namba alijikuta akisikiliza kwa makini zaidi. Ilitoka kwa kiongozi wa makachero ambao walikuwa wakifuatilia nyendo za Clay.
“… Inaelekea kama tutamkamata red handed, mzee. Sasa hivi anaunganisha mitambo yake ya mawasiliano…”
“Nisubiri. Nakuja mara moja.”
Dakika mbili tatu baadaye, Kombora alikuwa miongoni mwa polisi wanne waliokuwa katika chumba fulani katika hoteli ya Kilimanjaro. Chumba hiki kilikuwa cha nne kutoka chumba cha Clay. Hata hivyo, kutokana na mitambo waliyoitega kitaalamu, japo hawakuwa wakimwona, waliweza kumsikia anavyoongea katika chombo fulani cha kijasusi.
“Sikiliza mzee… sikia…” askari mmoja alimwambia Kombora huku akitweta.
“…Ndiyo. Ndiyo… nimefanikiwa kupanda katika majumba ya kutosha. Moja Ikulu.. hapa Kilimanjaro moja… jengo la IPS moja… Kitegauchumi… Muhimbili… Benki Kuu ya muda… Tipper… kiwanda cha Urafiki na sehemu mbalimbali muhimu. Tunachosubiri ni saa moja tu. Ikifika, kwa jinsi nilivyotega inaelekea jiji zima litalipuka. Mimi nitaondoka hapa wakati wowote…”
“Unasikia mzee?... Unasikia?...”
Kombora hakusubiri kumsikiliza afisa huyo. Aliwaamuru kumfuata kukiendea chumba cha Clay. Kinyume cha mategemeo yao waliukuta mlango ukiwa wazi. Naye alikuwa kaketi kwa utulivu juu ya kochi, gazeti mkononi. Yeyote ambaye angeingia bila ya kufahamu kinachotokea angemdhania kuwa alikuwa akisoma gazeti.
Aliwalaki Kombora na wenzake kwa utulivu wa kushangaza. “Karibuni. Vipi, mbona ghafla hivyo? Kuna habari mpya?” aliuliza.
“Inuka na uweke mikono yako juu,” Kombora alifoka, tayari akiwa na bastola yake mkononi akiifanya idadi ya bastola zilizomwelekea kuwa nne.
“Vipi Inspekta! Mbona sielewi?...”
“Mikono yako juu!” Kombora alinguruma.
Clay akainuka na kuiweka mikono yake angani.
“Acha gazeti.”
Aliliachia. Ndipo kilipoonekana kikasha kidogo chenye ukubwa wa kiberiti ambacho alikuwa nacho mkononi. Kombora alimsogelea na kuiweka bastola kifuani mwake huku akimwuliza kwa ukali, “Nini hicho?”
“Kwa nini Inspekta?... Hiki sikifahamu. Nimekiokota sasa hivi tu.”
Jibu hilo lilimchukiza Kombora kupita kiasi. Alijibu kwa pigo zito la ngumi ambalo lilitua barabara katika uso wake. Clay alipepesuka lakini hakuanguka, jambo ambalo lilimshangaza na kuzidi kumchukiza Kombora. Pamoja na umri wake mkubwa hakumbuki lini alipata kumpiga mtu ngumi nzuri kama hiyo na mtu huyo akaendelea kusimama. Akarudi nyuma hatua mbili na kumwamuru askari mmoja amkague. Ni hapo lilipotukia jambo ambalo halikutegemewa. Kwa wepesi usio kadirika Clay alichomoa kisu na
 
kumchoma askari huyo. Kisu cha pili kilimkwaruza Kombora mkononi. Papo hapo alichupa mlangoni akienda zake. Lakini hakuwa mwepesi zaidi ya risasi tatu za polisi ambazo zilimfanya aanguke mlangoni kifudifudi. Wakamvuta chumbani na kumlaza kitandani bila kujali damu zilizoendelea kumtiririka kutokana na majeraha makubwa ya risasi hizo. Wakamkagua na kumpokonya bastola nyingi na visu sita zaidi.
“Sema haraka, ulikuwa ukiwaarifu nini mabwana zako?” Kombora alimwuliza.
“Itakusaidia nini Inspekta?” alihoji kwa udhaifu na maumivu makali. “Huna unaloweza kufanya. Bado saa chache sana. Kama utapenda kufahamu nilikuwa nikiwaarifu mafanikio ya kazi yangu. Nimefaulu kutega katika majengo mbalimbali. Wakati utakapowadia mlipuko utakaotokea utakuwa wa kupendeza sana. Laiti ningekuwa hai nione na kusikia vilio vyenu!”.
Kombora hakujua aseme nini. Hakujua kama ilimpasa kumtisha au kumbembeleza mtu huyu ambaye kila dalili ilionyesha kuwa angekufa haraka. “Mpelekeni hospitali,” aliamuru.
“Ya nini Inspekta? Sipendi kufa kwa moto… naweza kufa kwa njia nzuri zaid…”
Kombora hakumsikiliza. Akamgeukia askari wake aliyekuwa mahututi. Yeye pia hakuwa na dalili ya kuishi sana. Kisu kilimwingia kifuani upande wa moyo. Jambo hilo lilipandisha hasira za Kombora dhidi ya Clay. Akamgeukia na kumtazama usoni.
Alimwona akitafuna kitu. Akakumbuka majasusi mengi ya utawala huo yalivyokuwa yakiishi na sumu kali mdomoni. Matumaini ya kupata habari zozote za haja yalikuwa mbali. Akamgeukia na kumwuliza taratibu, “Sema tafadhali… tunawezaje kuzuia mkasa huu ulioko mbele yetu?”
Clay alicheka kwa maumivu huku akijikongoja kusema, “Labda uchukue furushi moja katika mfuko wangu ukaangalie unachoweza kufanya.”
Moyoni alifahamu kuwa mfuko huo ulikuwa na akiba nyingine ya vile vigololi, ambavyo alikuwa hajamaliza kuvitega. Hivyo, aliamini kuwa Kombora angevifikisha Central Police na kulifanya jengo lao liwe moja ya majengo mengi yatakayopigwa na radi hii iliyoundwa na binadamu. Hilo likamfanya ajitahidi kucheka, tena kifedhuli huku akisema kwa tabu, “Usijali Inspekta… muda si mrefu tutakutana huko kuzimu… Tutakuwa wengi sana… mimi natangulia…”
Kombora hakuona kama mtu mwenye roho ya kinyama kama huyo alistahili kufa kiungwana kiasi hicho. Hivyo, akaichomoa bastola yake na kumsindikiza akhera kwa risasi ya kichwa ambayo ilimfumua kabisa fuvu lake.

***
Walitazamana kwa macho yaliyojaa hisia. Mmoja akitabasamu, mwingine akiinama kwa haya. Mmoja akainua mkono wake na kuutua juu ya paja la mwenziwe. Mwingine akaufunika mkono huo kwa kiganja chake na kuanza kuutomasatomasa kimahaba. Mkono wa pili ukainuliwa na kutua juu ya kifua cha mwenziwe, ukitafuta uwezekano wa kupenya, ndani ya mavazi yake. Vijilima viwili, laini, vilivyosimama kwa namna ya kupendeza macho katika kifua hicho havikuruhusu mkono huo kupenya kwa urahisi. Mkono ukaviacha vilima hivyo na kuanza kufungua vifungo vya vazi hilo. Mara kimojawapo cha vilima
 
SEHEMU YA 70

hivyo kikajitokeza, kikimeremeta kwa wekundu na uhai wake. Wakatazamana tena. Kisha akakisogeza kinywa chake na kukifanya kimeze chuchu za kijilima hicho. Mdomo ulipohama kifuani ulikwenda katika kinywa cha mwingine ambako ulianza kunyonya ulimi uliokuwa ukisubiri. Mara wakaachana na kuanza kuvua mavazi yao moja baada ya jingine. Tahamaki wakawa wamesimama kama walivyozaliwa, kila mmoja akishangazwa au kuridhishwa na uzuri wa mwingine. Kisha wakakumbatiana kwa nguvu. Mmoja aliguna, mwingine akanong’ona.
“Nuru…”
“Joram…”
Kitanda kikawalaki na kuwafariji. Hawakuhitaji shuka. Walikuwa kama walivyohitaji kuwa, wakifanya mapenzi kwa namna ambayo walihitaji, kwa kiwango ambacho hakikadiriki. Vitendo vyao vilifuatiwa na maneno ya mapenzi ambayo yalisikika kwa sauti ya kike, mara chache sana yakijibiwa kwa sauti nzito ya kiume.


Kisha ghafla, vitendo na sauti zao vilitoweka machoni na masikioni mwa mtu ambaye alikuwa akishuhudia kila kitendo chao, “Shit,” mtu huyo, kwa jina Von Iron, alifoka. Alikuwa akikifuatilia kila kitendo kwa tamaa kubwa, huku akiburudika. Lakini haikuwa burudani rahisi kwani kuona huko kulimfanya atetemeke mwili mzima na roho kwa uchu na tamaa, huku jasho likimtoka na damu kuchemka. Alijaribu kujifariji kwa kuubembeleza uume wake kwa mkono wake huku macho yake yakiwa yamekazwa kutazama katika mtambo wake. Mkono haukuwa na faraja yoyote. Mara mbili aliutoa na kuufuta kwa leso yake kwa jinsi ulivyochafuka kwa manii yaliyomtoka kwa wingi. Alitamani aondoke hapo na kuacha kutazama vitendo hivyo, lakini macho hayakumruhusu. Akaendelea kutazama, akiendelea kujifariji kwa mkono wake. Moyo wake ulikuwa unadunda na alishindwa kustahimili zaidi ya mkono kujifariji. Alihitaji mwananmke. Na si mwanamke yeyote isipokuwa yule mwanamke aliyekuwa akimtesa sana, mwanamke wa Kiafrika; Nuru.
Mwanamke mweusi! Von alishangaa kimoyomoyo. Ana wazimu? Hata hivyo, alijua kimoyomoyo kuwa asingestahimili hadi atakapompata. Alijifariji kwa kujiambia kuwa angemwua baaada ya kutenda naye mara moja tu, ili yasije yakampata yaliyompata hayati baba yake.
Ni tamaa hiyo ambayo ilimfanya akatae katakata madai ya wenzake waliomtaka amruhusu Joram na msichana wake wauawe mara moja.
“Ni jambo la hatari lisilo na busara kumwacha hai mtu hatari kama huyo hasa katika kipindi hiki,” mwenzake mmoja alimwambia. “Japo amekimbia kwa na hawezi kurudi, lakini ni mtu ambaye hafai kuaminika. Kumwacha hai ni sawa na kuishi na nyoka chumba kimoja.”
“Atafanya nini?” Von alikuwa amekanusha. “Hana awezalo kufanya. Bado saa chache sana tutamleta katika televisheni atazame nchi yake inavyoteketea. Baada ya hayo tutamchinja kwa urahisi kama kondoo. Usijali. Waache waishi usiku mmoja zaidi.”
***
Usiku ni kitu alichokuwa akikisubiri kwa hamu, akikumbuka yale aliyoyaona usiku wa jana. Na ulipowasili hakuwaalika wenzake kwenda kutazama. Kwa kisingizio cha “Kumchunguza kwa makini.”
 
Alikwenda peke yake. Akaburudika kwa faraja inayotesa. Hivyo, vitendo hivyo vilipotoweka machoni mwake, lilikuwa kama pigo kwake. Aliamini kuwa kulikuwa na hitilafu ya mitambo iliyowaunganisha na chumba hicho. Lakini kwa kuwa mitambo hiyo ilikuwa automatic, na ilitegeshwa kwa namna ya kuweza kujirekebisha yenyewe, alisubiri kwa utulivu..
Katika kipindi hicho cha kusubiri ndipo ilipomjia wazo la kuyafikiria mambo ambayo yangetokea mara tu baada ya usiku huu. Kesho, wakati kama huu bila shaka nchi kadhaa za Kiafrika zitakuwa katika maombolezo makubwa huku majeneza yakiwa yamejaa maiti zilizoungua na hospitali zikishindwa kuhimili idadi ya majeruhi watakaoponea chupuchupu. Mpango huo uliotokana na ubunifu wake ulipita kwa tabu sana baada ya wakubwa kulalamika kwamba ulikuwa wa kikatili mno lakini yeye Von na wenzake wachache walifaulu kuwashawishi na wakaafiki baada ya kuwakumbusha tena na tena kuwa ANC ilikuwa haifanyi mchezo bali ilikusudia kupokonya utawala, jambo ambalo lingewatia watu weupe wote mashakani, chama hicho kinapewa onyo kali, onyo ambalo kamwe lisingeweza kusahauliwa. Dawa ya moto ni moto… na sasa wakati huo wa kutumia dawa hiyo, iliyokuwa ikichemshwa kwa muda mrefu na gharama kubwa ulikuwa unawadia. Lipi lingeweza kumpendeza Von zaidi ya hilo? Nani angeweza kufurahi zaidi yake?
Mara akajisikia kucheka kwa furaha. Alijisikia kusheherekea kila chozi litakalotoka katika uso mweusi kwani machozi hayo kwake yangekuwa faraja ambayo isingemsahaulisha ukatili wa mtu mweusi ambaye alimfanya awe yatima. Maelfu ya weusi yatateketea kwaajili ya malaya mmoja mweusi, aliwaza. Watakilipia kifo cha mama yake mpendwa, pamoja nao Joram Kiango na msichana wake… aliendelea kuwaza. Lakini kabla ya kifo chao lazima ampate huyu msichana anayeitwa Nuru. Aliyoyaona kwa macho yake yalikuwa hayastahimiliki. Alihitaji kuyaona kwa vitendo. Alihitaji kuijua siri iliyomo katika ngozi hii nyeusi, siri ambayo ilimfanya amkose mama na baba milele, baada ya hapo ndipo Nuru angemfata Joram akhera.
Mawazo hayo yalimpandisha mori hata akakumbuka kuyarejesha macho yake katika screen iliyokuwa ikimwonyesha chumba cha Nuru na Joram. Hakuona chochote. Mitambo bado ilikuwa haifanyi kazi. Akaitazama saa yake. Ilikuwa ikikaribia saa kumi za alfajiri. Saa mbili zilikuwa zimepita tangu mitambo hii ilipokorofisha. Von hakuamini. Isingewezekana kuwa mitambo hiyo iwe haifanyi kazi kwa muda wote huo ilikuwa imepangwa kuwa ingeweza kujiwasha yenyewe dakika tano tu baada ya kila hitilafu. Vipi leo ikatae? Na hasa akiwemo Joram Kiango ambaye, pamoja na matatizo yote aliyokuwa nayo, iliamriwa asiachwe huru zaidi ya dakika tano?
Hima Von aliinua simu na kuzungusha namba za mmoja wa makachero waliopewa jukumu la kulala macho katika jumba hilo alimokuwemo Joram. “Sikia,” Von alimwambia kwa sauti ya amri. “Tumia kisingizio chochote uingie katika chumba chake humo ndani fanya kila hila uone kwanini mashine hii imegoma kufanya kazi.”
 
Akiwa anaijua vizuri kazi yake, mtu huyo alivaa ovaroli lake jeupe na kuchukua vifaa vya umeme hadi chumbani kwa Joram. Aligonga mlango kama kawaida. Kisha akagundua kuwa ulikuwa wazi. Akaufungua polepole na kuingia. Macho yake yalidakwa na umbo la Nuru akiwa kavaa vazi la kulalia, jepesi kiasi cha kufichua umbo lake zuri la ndani kwa kiwango cha kutosha. Kando ya Nuru alisimama kijana wa Kizungu aliyevaa nguo zake zote, suti, kama ambaye alikuwa hajalala kabisa. Fundi huyo bandia alidhani kuwa kabla ya kubisha hodi mara ya kwanza aliwasikia wakicheka. Lakini hayo yalimtoka akilini mara alipomwona msichana huyo akiangua kilio huku akisema kwa kwikwi.
“Afadhali umefika fundi, nadhani utanisaidia.”
“Kuna nini?” kachero huyo aliuliza.
“Huyu hapa,” Nuru alisema akiuelekeza mkono kwa mzungu aliyesimama kando kwa utulivu. “Huyo ameingia humu chumbani kwa nguvu na kutaka kuninajisi. Mtoe nje, tafadhali.”
“Yuko wapi bwana wako?”
“Yuko bafuni.”
“Anafanya nini muda wote huo?” fundi bandia aliuliza huku akizidi kumkodolea Nuru kwa macho yenye tamaa. Mara macho yake yaliuona mfuko uliokuwa wazi kando ya kabati. Akaona vitu vilivyokuwemo. Aligutuka kidogo na kurudi nyuma huku akiupeleka mkono wake mgongoni kuchukua bastola yake. Alikuwa amechelewa sana. Wakati huohuo kisu kilipenya katika kifua chake. Pigo la pili lilimfanya ateremke sakafuni bila ya ubishi. “Mzungu” aliyekitumia kisu hicho alikitupa uvunguni na kuifuta mikono yake kwa shuka.
“Fanya haraka Nuru,” alihimiza akiirudia maiti na kuilaza vizuri kando ya kitanda.
Dakiaka chache baadaye mlinzi aliyekuwa akililinda jengo hilo kwa mlango wa nyuma aliwaona vijana wawili wazungu, mvulana na msichana wakimjia. Mikononi walikuwa na mizigo yao ambayo haikuwa chochote zaidi ya mifuko midogomidogo.
“Tunawahi uwanja wa ndege,” kijana wa kiume alieleza.
Ingawa walizungumza kiingereza kamili lakini mlinzi huyo alishuku jambo katika sauti hiyo hasa akiwa analifahamu jengo hilo lilivyo, hakuamini kuwa walikuwa wasafiri wa kawaida.
“Naweza kuona vitambulisho vyenu?”
“Bila shaka,” mwanaume alijibu akiutia mkono wake mfukoni. Ulitoka na kisu ambacho kilididimia katika kifua cha mlinzi huyo. Maumivu makali yaliyochanganyika na mshangao vilimfanya afyatue bunduki yake bila shabaha yoyote. Mara akaanguka chini na kukata roho.
***
Mlio wa bunduki alfajiri tulivu kama hiyo, uliwashitua watu wengi. Zaidi yao wote alikuwa Von Iron, aliyekuwa bado kaketi katika chumba kilekile, akisubiri matokeo ya mtu aliyetumwa chumbani kwa Joram. Alisubiri kwa muda ambao aliuona mrefu kupindukia. Alipojaribu kuwasiliana naye kwa walkie talkie ndogo iliyokuwa imevaliwa kama saa ya mkono hakupata majibu yoyote. Akaendelea kusubiri. Na katika subira hiyo ndipo aliposikia mlio wa bunduki ambao hakuutegemea. Akafanya hima kumtuma kachero mwingine katika chumba hicho. Mara moja akapata majibu ambayo yalimfanya atokwe na jasho jembamba.
 
Dakika chache baadaye alikuwa miongoni mwa maafisa sita wa ngazi za juu katika BOSS waliosimama chumbani humo mbele ya maiti ya mwenzao, ambayo yalilala sakafuni juu ya dimbwi la damu nzito. Joram hakuwemo, wala msichana wake. Vitu vyao vichache vilikuwa vipo, ingawa baada ya kupekuliwa havikuonekana na chochote cha haja zaidi ya mavazi na vitabu. Katika vitabu hivyo kilipatikana kitabu kimoja cha Physics ambacho kilionekana kuwa kilisomwa sana kwa jinsi kilivyokuwa kimepigiwa mistari chini ya maneno fulanifulani. Baada ya uchunguzi mdogo ilidhiirika kuwa msomaji alizingatia mambo ya setilaiti na nyuklia. Hilo liliwafanya waunge mbili na mbili na kupata nne.
“Ana wazimu,” Von alifoka. “Kama amekuja hapa akiwa na ndoto ya kufahamu chochote juu ya setilaiti yetu hii maalumu wazimu unamsumbua. Amekuja kuinadi roho yake.” Akawageukia wenzake na kuwatazama kwa lile jicho lake kali la kutisha, jicho ambalo lilikuwa msingi uliowafanya waendelee kumwogopa na kutomkosoa. “Mnasikia? Mtafuteni haraka, aletwe hai, atakufa taratibu kama mbwa wenzake.”
Kabla hawajatawanyika kutoka chumbani humo, ziliwafikia habari nyingine mbaya zaidi. Maiti ya mmoja wa walinzi wa jengo hilo imeokotwa ikiwa na kisu kifuani. “Aliuawa kwa aina ya kisu ambacho kimemwua huyu.” Kachero huyo alieleza..
“Mnaona?” Von alinguruma. “Sasa namtaka akiwa hai au maiti. Haraka iwezekananvyo, tafadhali…”
Kulitangazwa msako mkali katika jiji la johanesburg mitaa yote ilifurika makachero ambao walichunguza kila uchochoro. Ilikuwa siku ngumu mno kwa watumishi weusi ambao walilazimika kuwahi kazini asubuhi hiyo. Wengi wao waliambulia kuishia katika vituo vya polisi ambako waliteswa na kusumbuliwa kwa kosa ambalo hawakulifahamu. Mtu au watu waliokuwa wakitafutwa hawakupatikana. Badala yake hadi mapambazuko kulikuwa na taarifa ya vifo vya watu wanane zaidi, watano wakiwa wameuwa kwa kisu, watatu kwa risasi za bastola. Wengi kati ya marehemu hao walikuwa watu wakubwa katika ofisi zao au walinzi wa majumba fulanifulani yenye umuhimu mkubwa. Ilikuwa dhahiri kuwa hiyo ilikuwa kazi ya Joram Kiango.
Von alizidi kupandwa na hasira. Hakuelewa kabisa dhamira na manufaa ya mauaji hayo. “Wazimu unamsumbua,” aliwaza. Kisha alihisi kuwa ameelewa. Joram alikuwa akilipiza kisasi dhidi ya maafa yatakayoipata nchi za afrika saa chache baadaye bila shaka alikuwa akijifariji kwa kumwaga damu zisizo na hatia. “Anajisumbua,” Von alisema. “Atalazimishwa kutazama katika televisheni, moto utakavyoiteketeza Dar es Salaam. baada ya hapo ndipo atakapokufa kifo cha kusikitisha…
Von akaamuru ufanyike msako mkubwa zaidi. Polisi wote na jeshi la ulinzi wakaingizwa katika msako huo. Kila mmoja aliambiwa anamtafuta nani na afanye nini baada ya kumpata. “Akileta ubishi muue, vinginevyo mlete hai.”
 
Ingawa Von alitegemea habari hiyo iwe siri, lakini hakufahamu iliyafikia vipi masikio ya watu wa habari. Ilimshangaza televisheni ilipokatiza matangazo yake ya kawaida na kueleza kutoweka kwa Joram Kiango na mauaji aliyokuwa akiyafanya. Ikatolewa picha ya Joram na msichana wake walipokuwa wakishuka kutoka ndege iliyowaleta nchini humu ikiwa imetekwa nyara. Pia zilionyeshwa baadhi ya maiti alizoziua.
“…jihadhari nae, ukimwona muue kwanza, muulize maswali badaye…”
Mtangazaji wa kipindi hicho alieleza.
Tangazo hilo liliamsha hofu ambayo haikupata kuonekana katika jiji hilo. Watu walizidi kubababika wakiogopa hata kuifungua milango yao ilipogongwa na yeyote. Wako ambao kazini hawakutaka kwenda.
Dakika chache baadaye ilibidi Von ajitokeze katika televisheni na kuwataka wananchi wasiwe na hofu yoyote, kwamba kutoroka kwa Joram lilikuwa tatizo dogo sana ambalo lingerekebishwa kwa muda mfupi. Akawafahamisha kuwa badala ya hofu leo ingekuwa siku yao ya kufanya sherehe kwani Afrika na dunia nzima itaziona nguvu za Afrika Kusini. “Wote ambao wamekuwa wakionea kijicho na kuitesa nchi yetu leo watatupigia magoti,” aliendelea. “Tulieni, msiwe na wasiwasi wowote. Ikifika saa nne fungueni redio na taelevisheni zenu muone…”

***
Watu hao ambao walikuwa wakitafutwa kwa udi na uvumba, alfajiri iliwakuta wakiwa wamesimama mbele ya hoteli moja ndogo katika mtaa uliojaa watu waliokuwa wakijadiliana. Macho yao yaliwatazama raia hao wa makaburu waliojaa wasiwasi kwa dhihaka. Kadhalika, waliwakebehi askari na poli ambao walikuwa wakipita huku na huko katika mtaa na vichochoro huku wakiwapita bila ya kuwatupia macho. Isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuwashuku kwa urahisi. Pamoja na kukesha, pamoja na kuchoka kwa kazi ya kwenda hapa na pale huku wakilazimika kuua na kuua tena, bado walijitahidi kuwa katika hali ya kawaida kama raia yeyote wa kawaida katia nchi hiyo. Hali ambao ilitokana na mavazi waliyovaa pamoja na rangi yao.
Yeyote aliyewaona aliamini kuwa alikuwa akiwaona vijana wengine wa kikaburu. Hayo yalikuwa matokeo ya moja ya shughuli nyingi ambazo Joram alifanya kwa gharama kubwa sana aliposafiri hapa na pale katika miji mbalimbali. Alimpata mtaalamu ambaye aliwatengenezea ngozi za bandia zilizovaliwa usoni, mikononi na kufunika vichwa vyao kwa nywele za kizungu. Vitu hivyo ni miongoni mwa mali zake ambazo alizisafirisha kwa hila kwa kumtumia yule Mmarekani Moole.
Kwa ujumla Joram aliona kuwa mambo yote yalikuwa yakienda kama yalivyopangwa, ingawa kiasi yalianza ghafla kuliko alivyotegemea. Alishtuka sana jana alipoambiwa na yule kiongozi wa BOSS kwamba leo saa nne wangeilipua Dar es Salaam na miji mbalimbali ya nchi za Kiafrika kwa ile silaha yao iliyoko angani. Hivyo, hakuwa na simile tena moyoni. Ndipo alipolazimika kufanya mapenzi ya hali ya juu na Nuru akiwa na hakika kuwa anatazamwa na ule mtambo wao ambao alikwisha uona. Alifanya hivyo ili
 
Back
Top Bottom