Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

Simulizi ya kipelelezi: Document number 72 (Nyaraka namba 72)

STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 17.

Majira ya usiku wa mapema kabla Calvinjr hajapiga simu kwa Gulamu Leopard, ndani ya Ikulu ndogo ambayo ilikuwa inapatikana ndani ya eneo la DOGMA TULIPO, kwenye chumba kisafi chenye hewa nzuri ambacho kiliruhusu kila aina ya upepo mwanana kuingia bila tatizo, huenda ni kwa sababu ya Ikulu hiyo kujengwa kwenye tambalale ambayo ilijengwa juu ya safu za mlima hivyo kufanya mtu akiwa ndani ya majengo hayo kuweza kuuona mji kwa upande wa chini ya mlima.

Kwenye chumba hicho kisafi alikuwa ametulia mheshimiwa raisi wa nchi ya Tanzania, Theobald Mnyika akiwa anapata wine taratibu lakini hakuwa amekaa tu kihasara ndani ya hilo eneo bali alikuwa anaendelea kupitia kwenye mitandao ya kijamii ili kujua kwamba wananchi wake walikuwa na yapi ya kuzungumza na kuongea.

Alikuwa anapitia mitandao maarufu sana ya kijamii kama Instagram na Twitter, alicho kiona kilimfanya apate tumaini jipya sana kwenye moyo wake, alijawa tabasamu mno. Watu wengi walikuwa wanamsifia raisi huyo kwa kutoa hotuba safi sana ambayo iliwagusa wananchi wengi wa Tanzania. Watu walikuwa wakimzungunzia kwa mazuri na kuungana naye kwa kipindi kugumu ambacho alipaswa kuwa mvumilivu sana kwa yale ambayo yalikuwa yametokea.

Ila walikuwa wakimuomba sana ahakikishe mhusika wa hilo tukio anawekwa hadharani ili kila mtu aweze kumjua na alipie kila alilo kifanya huku akiwataja na wenzake. Akiwa kwenye furaha hiyo mheshimiwa raisi alisikia hatua za mtu akiwa anakuja ule upande ambao yeye alikuwepo, aliiachia tableti yake na kusogea dirishani akiwa anayashuhudia mandhari ya kuvutia ya eneo hilo lililokuwa na ulinzi usiokuwa wa kawaida.

"Tumebahatika kuzaliwa kwenye moja ya nchi ambayo ni nzuri sana. Nikiwa hapa najisikia amani kuliko eneo lolote lile, natamani sana kama siku zote maisha yangu yangekuwa hivi huenda mpaka siku nastaafu kwenye nafasi yangu ningekuwa moja ya maraisi wenye bahati sana lakini kwa bahati iliyokuwa mbaya, jambo baya zaidi kwenye historia limetokea nikiwa nipo madarakani. Una kipi cha kuongea kuhusu hili bwana Gulamu" aliongea kwa kumuuliza mwanaume aliyekuwa ameingia hapo. Naye hakuwa mwingine bali mkurugenzi wa shirika la kijasusi aliyefahamika kama Gulamu Leopard.

"Kiongozi yeyote yule duniani, kitu cha kwanza anacho kiombea na kinampa furaha ni kuhakikisha wale anao waongoza wanakuwa salama. Ndiyo maana huwa nguvu kubwa ya uongozi haipo kwenye pesa wala kwa watu wanao mzunguka kiongozi husika bali kwa wananchi. Ukiweza kuishinda mioyo ya wananchi basi wewe unakuwa kiongozi mwenye nguvu sana kwani wananchi wanaweza kukulinda zaidi hata ya jeshi na vyombo vingine vya usalama vinavyoweza kufanya hivyo"

"Umanaamisha nini bwana Gulamu?"
"Namaanisha kwamba wewe ni miongoni mwa viongozi ambao wamefanikiwa kuishinda mioyo ya wananchi na ndiyo maana licha ya mambo yote lakini bado wana imani na wewe huku wakiamini kwamba utawasaidia kufanikisha baadhi ya mambo yao hivyo hautakiwi kuipoteza hiyo imani yao kwako kwa maana ndipo nguvu yako kubwa ilipo"

"Mhhhh huoni kama hili jambo ambalo limetokea leo linaweza kunitolea imani kwao?"
"Mkuu, kuna muda tatizo unaweza ukalibadili na kuwa fursa kama tu ukiweza kuzichanga karata zako vizuri, hii inaweza kuwa nafasi ya wao kukuamini zaidi na kukupenda kuliko hata huko nyuma"

"Nadhani sijakuelewa kidogo, unamaanisha hili tatizo nilibadili kuwa fursa kwangu? Kivipi?"

"Wananchi wanacho hitaji ni kupata majibu ya kile ambacho kilitokea na kuona wahusika wakipata adhabu kali sana, hilo najua lipo ndani ya uwezo wako ila kuna jambo la mhimu zaidi ambalo ndilo wanalihitaji zaidi japo hakuna ambaye analizungumza"

"Nadhani sikufanya kosa kukufanya uendelee kubakia kwenye hiyo nafasi bwana Gulamu. Naomba nipe hayo maelezo ambayo bila shaka yana umuhimu mkubwa sana kwangu kwa sasa" Mzee huyo aliongea huku akiwa anamgeukia mkurugenzi huyo ili ayapate yale madini ya mhimu ambayo yangemfanya aweze kuzishika imani za watu hao ambao walikuwa wakimzunguka kwenye nchi yake.

"Unajua bosi, duniani kote, imani ya mtu ipo kwenye udhaifu wake mkubwa. Na imani ya wengi ipo kwenye faraja ya watu wachache wenye maumivu halafu wakapewa tumaini, sijui umenielewa kiongozi wangu?"

"Hapo umeniacha kidogo"

"Iko hivi navyosema kwamba imani ya mtu ipo kwenye udhaifu wake, namanisha kwamba udhaifu wa mtu ndio unaomfanya awe makini sana na kile kitu chake hivyo hupelekea imani yake yote kuhamia kwenye kile kinacho mpa udhaifu mkubwa akiamini hapo ndipo ilipo furaha yake au karaha yake. Kwa hili lililo tokea, kwa hawa viongozi wengi kupoteza maisha ndipo zilipo imani za familia zao na ndiyo udhaifu wao mkubwa ulipo" Gulamu aliye onekana kuijua falsafa vyema alielezea na kutulia kisha akaendelea tena;

"Viongozi wengi ambao wamekufa leo hii wametokea kwenye familia za maisha ya kimaskini hivyo familia zao imani zao zilikuwa kwa watu hao ili kuyaendesha maisha yao kwa asilimia miamoja. Ina maana hapo ndipo udhaifu wao mkubwa ulipo. Maana yake kitu ambacho wewe unatakiwa kukifanya ili kuzichukua imani zote za watu hao na kuhakikisha unatoa msaada wa kutosha kwa hizo familia zote ambazo zimepatwa na matatizo ya kufiwa na watu wao kwami kwa sasa wanajua kwamba hawatakuwa na watu wa kuwajali kwa vile watu wao wa mhimu hawapo, hivyo hata maisha yao hawana imani nayo tena"

"Wewe kutenda msaada kwa hao watu inamaanisha watu hao imani zote zitahamia kwako na kuamini kwamba wewe ndiye mkombozi wa maisha yao. Sasa hapo ndipo utaitumia hiyo nafasi kuweza kulipata kundi la watu wengi ambalo linategemea kundi la kwanza" Mr Gulamu aliguna kidogo na kuendelea;

"Kundi wa watu wengi wanaamini kwamba huwezi kumsaidia kila mtu kwa wakati mmoja, ila wanaamini kukujua na kupima imani yao kwako kwa wewe kuwasaidia wale wenye uhitaji wa lazima hivyo ukiweza kulirejesha tabasamu la wale wachache wenye majonzi mazito watakuamini sana mzee" alimaliza na kutulia kuangalia raisi huyo angesema nini kwa wakati huo.

Mzee huyo alicheka, akacheka tena
"Aisee sikuwahi kufikiria kwamba hii nchi ina watu wenye akili za kuwaza na kuona mbali sana namna hii. Wewe ni moja ya watu ambao mlitakiwa kuwa washauri wangu wa karibu sana. Kitu ulicho niambia ni kidogo sana kwa kukitamka ila ni kitu kigumu sana kukifikiria hususani kwa mtu ambaye ana uwezo mdogo kichwani. Kwa leo niseme ahsante sana nadhani umeniletea kitu kipya kichwani ambacho nitatakiwa kukitangaza hadharani baada ya hizo siku tatu" raisi aliongea akiwa anampiga piga mkurugenzi huyo kwenye bega lake, alimkubali kwa akili kubwa ambayo alikuwa nayo mtu huyo.

"Nashukuru sana kiongozi kama na mimi nimechangia jambo la mhimu mbele yako, lakini nilikuwa nina swali kidogo"
"Nakusikiliza"
"Wananchi umewaahidi kwamba baada ya siku tatu utawapatia majibu pamoja na kumtaja mtu ambaye amefanya hili tukio ambaye ni kiongozi wa nchi, huoni kama umecheza ni kamali mbaya sana hii? Vipi kama asipo patikana mpaka huo muda utawajibu nini? Na watakuelewa? Naona kama umejifunga sana bosi" raisi huyo aligeuka na kumwangalia mkurugenzi wake kwa umakini kisha akamuuliza.

"Unakumbuka hili wazo wewe ndiye umenipa?"
"Ndiyo kiongozi laki...."
"Basi mimi nimeamua kukuamini wewe moja kwa moja maana yake kama jambo likishindìkana wewe ndiye utakayepaswa kubeba lawama. Nina imani una watu makini sana kwenye ufanyaji wa kazi, hata hivi hizo siku tatu ni nyingi sana, halafu si umeniambia kwamba kuna watu sana unao kwenye mkono wako?"
"Ndiyo mkuu" Mr Gulamu alijibu ila kwa kinyongo, wanasiasa walikuwa watu wa ajabu sana kwa upande wake. Jambo likifanikiwa angejisifia yeye ndiye kalitenda ila likifeli basi kiongozi huyo wa usalama angeubeba msalaba pekeyake. Hakuwa na cha kufanya, huyo alikuwa ni bosi wake.

"Sasa hapo hofu yako iko wapi? Au huamini kuhusu uhusika wa hao watu kwenye hili? Hakuna ambacho huenda mmekipata labda?"
"Kuna kitu ambacho tumekipata kinaonyesha uhusika wa moja kwa moja kuhusu mlipuko wa leo" maelezo yake yalimfanya raisi amsogelee kwa umakini
"Kitu gani hicho?"
"Rimoti iliyo tumika kulipua bomu"
"Whaaaaaaat?"
"Ndiyo mkuu na mtu ambaye alikuwa na hiyo rimoti yupo kwenye mkono wetu tayari na usiku wa leo naenda kumhoji"
"Yes kazi nzuri sana na hicho ndicho ambacho nataka nikisikie kutoka kwako. Huyo mtu hakikisha mpaka kesho asubuhi awe ameeleza kila kitu ili tuweze kuupata huo mtandao wote ambao unahusika na hili jambo haraka sana"
"Sawa mkuu nitalishughulikia hili jambo haraka sana"
"Halafu nataka kujua kitu kimoja, nahitaji kumjua huyu kijana wako ambaye amefanya kazi nzito hii ya kuhakikisha watu hawa wanapatikana kirahisi sana, nahitaji kukutana naye niweze kumpatia zawadi yake ambayo anastahili. Umewafunza vyema vijana wako wanaonekana kwamba wapo makini sana na kazi" raisi alitulia kidogo akiwa anaangalia saa yake kisha akaongeza;

"Kesho natakiwa kuwahi kwenye familia ya waziri mkuu kwenda kutoa pole kwa kupotelewa na mtu mhimu sana kwao, wanaweza kuhisi ni jambo la ajabu sana kama nisipo enda kuwapa hata pole na kutia neno la faraja kwao, hivyo kesho asubuhi wakati unaniletea ripoti ya majibu uliyo yapata kwa watu hao, muandae na msafara wangu ambao nitahitaji ulinzi kutoka kwa vijana wako mpaka Dar es salaam"

"Sawa mkuu" mkurugenzi alimaliza mazungumzo na bosi wake ambaye alikuwa amemuita hapo na kuanza kutoka ndani ila alisimama baada ya kusikia mheshimiwa raisi anaongea na simu akitoa amri kwa jeshi la polisi huko kwenye jimbo la DAMU INAYO ISHI kwamba wahakikishe wanadumisha ulinzi wa kutosha nyumbani kwa mbunge Isaya Ndango na kama wakimkuta mtu yeyote ambaye hahusiki na hiyo sehemu basi wahakikishe wanamkamata.

Na huo ndio muda ambao Calvinjr alimpigia simu kiongozi wake huyo akimweleza hali ya huko na kiongozi huyo akamtaka atoweke hilo eneo haraka sana kwa sababu alisikia taarifa ya kwamba polisi wangejazana mahali pale muda sio mrefu.

Unadhani ni kipi kinaenda kutokea humu ndani?

Episode ya 17 inafika tamati.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mbona fupiii kiongoziii ongeza zagazaga na mayonnaise kwanmbaliiiiii
 
Tuko pamoja [emoji1666]
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 18.
Baada ya kumalizana na mheshimiwa raisi, Gulamu Leopard alitoka kabisa nje ya hilo eneo ili kwenda kukutana na Tina eneo la siri kama ambavyo walikuwa wamekubaliana kukutana usiku huo. Pembezoni kabisa mwa hoteli moja kubwa ya kifahari palikuwa na car wash moja ya kisasa hapo ndipo walipokuwa wamekubaliana kukutana kwa umbali wa mita kadhaa.

Tina alikuwa amefika mapema sana na kujibanza mahali huku akiwa anamsubiri kiongozi wake afike ili waweze kuongea hayo mambo ambayo yalionekana kuwa ya mhimu kwa wakati huo. Gari ya bosi huyo ilifika muda mfupi baadae na mwenda kupaki pembeni ambapo haikuchukua hata dakika mbili Tina akawa ameingia ndani.
"Nipe ripoti yako yote" mheshimiwa huyo aliongea akiwa anahitaji mwanamke huyo aweze kumpa taarifa ya kila alicho kifanikisha. Tina hakuwa na namna zaidi ya kumweleza kila kitu ambacho alihisi kipo ndani ya uwezo wake.
"Hiyo rimoti iko wapi?" Tina aliitoa na kumpatia kiongozi huyo
"Una uhakika miongoni mwa hao walio kamatwa mmoja ndiye alikuwa na hii rimoti?"
"Ndiyo, nimemshuhudia kwa macho yangu mawili akiwa anafanya hilo jambo"
"Safi sasa nadhani hapa kazi inaenda kuwa rahisi sana, tupo karibu kuweza kumjua mtu wetu tofauti kabisa na nilivyokuwa nafikiri"
"Kwanini unadhani tunaenda kumpata kirahisi bosi?"
"Kama tunao hawa watu walio husika basi inaweza kuwa rahisi sana tukiwapa mateso makali wataongea tu kwamba ni nani yupo nyuma yao"

"Sidhani kama inaweza kuwa rahisi sana namna hiyo bosi"
"Kwanini?"
"Hawa watu wapo ndani ya mfumo. Kwenye mfumo unaweza ukawa unafanya kazi kwa malipo na maelekezo tu na hata usijue anaye kutuma nani, nina uhakika hawa watatupatia mwangaza ila sidhani kama wanahusika moja kwa moja kutupatia mtu wetu"
"Kwahiyo unadhani kwamba hawatatusaidia?"
"Hapana bosi ila nadhani inatakiwa tuwe na mpango wa pili. Hawa watu kama wakisema kwamba hawamjui mhusika walipewa tu kazi waifanye tutafanyaje? Ni wa mhimu ndiyo lakini sisi wenyewe hatutakiwi kukaa na kufurahi kwa sababu hii, kumbuka jambo lililo tokea ni la hatari na kubwa sana kwa nchi. Nina imani hata walio lipanga tukio hili walijua ukubwa wake hivyo hata namna ya kujiweka mbali na matatizo wanajua ni wapi pa kuanzia na wapi wanaishia hivyo haiwezi kuwa rahisi"
"Mhhhhh unataka kumaanisha kwamba kuna kitu nitakuwa sijui?"
"Ndiyo bosi ndiyo maana nipi hapa ili kukuelekeza"
"Sawa unaweza ukaendelea"

"Kwenye ile nyumba ambayo nimewakamata wale watu, kuna vitu nimekutana navyo vimenichanganya na huenda sijavielewa mpaka sasa na nadhani kuna muunguniko mkubwa wa matukio kuhusu jambo hili hili. Yule mtu nimemkuta na simu iliyokuwa na namba moja tu pekee ambayo nilisikia akifanya mawasiliano nayo kutoa taarifa kwamba kamaliza kazi"

"Namba ambayo nimeikuta humo nimejaribu sana kuhitaji kuifahamu ila nilicho ambiwa ni kwamba namba kama hiyo haijawahi kabisa kuwepo hapa duniani wala kusajiliwa popote hivyo hakuna kitu ningepata ila yule mwanaume kwenye mfuko wake pia alikuwa na kikaratasi ambacho kilikuwa na maneno yaliyo andikwa;"

"THE BLUE OPERATION REACHING RWANDA. TEN IMAGINARY LIFETIME. ACCOMPLISHED." Nimejaribu sana kuitafuta maana yake ila nimeshindwa kabisa kuelewa kwamba ina maana gani, lakini pia baada ya kuingia ndani ya nyumba ile, nimekutana na ramani ya bunge bila kusahau hesabu ambazo zilikuwa zinafanywa ubaoni" Tina alitulia kwanza na kumuangalia mheshimiwa aliyekuwa amemkazia macho, akatoa ramani ya jengo hilo na kuendelea;

"Wakati naangalia pale ubaoni, nimeshtuka sana kwa maneno ambayo nimeona yakiwa yameandikwa, "HIM, DID IT ALONE (OFFICIAL WITH THE SUITCASE)" Hii nadhani inaeleweka kwa maana wamesema kwamba kuna mtu ambaye ameifanya hii kazi ni mmoja tena ni mtu ambaye ni kiongozi mkubwa kwa tafsiri ya hayo maneno. Hapa moja kwa moja maneno yako yanathibitika kuwa ya kweli bosi kwamba kwenye mpango huu kuna uhusika wa kiongozi au viongozi wakubwa"

"Kwa huo ujumbe wao wanamaanisha kwamba kuna kiongozi ambaye aliingia na begi lake na kutega haya mabomu mwenyewe, maana yake huyo mtu pia bila shaka amewahi kupitia jeshini" Tina alitulia baada ya kukamilisha maelezo.

"Umeacha ushahidi wowote eneo la tukio?" Kiongozi wake alimuuliza baada ya kuhema kwa nguvu.
"Hapana bosi nilifuta kila kitu hivyo haya tunayaona mimi na wewe tu"
"Hichi ni kitu cha mhimu sana umekifanya. Nadhani uhusika unaanzia ndani mwetu sisi wenyewe"
"Sijakuelewa kiongozi"
"Namaanisha kwamba huenda kuna wahusika wengine tupo nao karibu"
"Kivipi?"
"Utanielewa baadae. Hilo jambo la kwanza nadhani Calvinjr atalishughulikia akifika kesho Dar es salaam, huenda akawa na akili mpya juu ya jambo ambalo limeandikwa hapo ndani, kwa sasa funga mkanda na ufunike sura yako tunaingia ndani kukutana na hao watu"

"Calvinjr amefanikiwa kumpata mke wa huyo mbunge?"
"Hapana"
"Unamaanisha nini kusema hapana?"
"Amechelewa kwa dakika thelathini na tano"
"Kwamba amekuta wamemuua"
"Ndiyo"
"Ooooh my God, kivipi sasa?"
"Kuna watu walifika kabla yake wakidai ni watu wetu wa usalama hivyo wakamhitaji kwa mazungumzo ambapo wameenda kumuua, Calvinjr alifanikiwa kumpata mmoja wa hao watu lakini baada ya kumdhibiti mtu huyo amejiua kwa kumeza kidonge" Mzee huyo alimaliza kuongea huku akiwasha gari maana hawakuwa na jambo lingine la kuongea hapo.

"Mkuu subiri mara moja kuja jambo jingine jipya ambalo naomba ruhusa yako nilifanyie kazi haraka sana"
"Lipi hilo?"
"Nahitaji kumtafuta na kumteka mbunge James Lewanyika" hilo jina lilimfanya mzee huyo kuzima gari kwani lilikuwa ni miongoni mwa majina ya watu ambao waliingia ndani ya jengo la bunge siku hiyo hivyo kwa namna yoyote ile lazima alikuwa amekufa
"Unasema?"
"Huyo mbunge hajafa, yupo hai ndiyo maana nimeomba ruhusa yako nataka kumchukua nikamhifadhi mahali nadhani atakuwa msaada mkubwa sana"
"Tina umelewa?"
"Hapana bosi huyo mtu hajafa, yupo hai"
"No, haiwezekani. Hakuna mtu amepona ndani ya lile jengo"
"Unakumbuka nilikuomba video za marejeo ukasema upo busy na kazi hivyo hujazipitia?"
"Yes, nakumbuka" Tina hakuongea zaidi ya kutoa video iliyokuwa inamuonyesha mbunge huyo akiwa anatokea mlango wa nyuma kabisa kwenda kwenye parking ya magari.
"Oooooh shiiit! Inamaana huyu mjinga amefanikiwa kutoka salama mle ndani"
"Ndiyo, inaonekana walitoka mle ndani wakiwa wametofautiana ndiyo maana aliamua kuchukua njia yake na kwa mwonekano wake tu inaonyesha wazi kwamba kuna mambo ambayo anayafahamu kama sio kuwa na mpango wake wa siri hivyo anatakiwa kupatikana haraka sana kabla watu hawajajua uwepo wake mtaani kwa maana utaleta mtafaruko na watu wakahisi kwamba huenda serikali ndiyo ilihusika kupanga huo mpango kama mpaka kuna watu wamepona basi watakuwa walikuwa wanajua kila kitu. Jambo hili litaichafua sana serikali na litaleta picha mbaya sana" Tina alieleza mambo ambayo yalimgusa vyema sana mzee huyo

"Kesho kukikucha huyu ndiye anatakiwa kuwa mtu wa kwanza wewe kumtafuta lazima huyu mpuuzi atakuwa anajua kitu, haiwezi kuwa hivi hivi. Hii ishu ni nzito sana kama mpaka waziri mkuu amehusika nayo moja kwa moja basi kuna jambo la hatari mno nyuma yake. Watu wanao tekeleza haya matukio huwa wanaogopa sana kufanya jambo kama hili wanapokuwa wanajua kwamba kuna viongozi wazito wanahusika ila kama walijua na bado wakaendelea na tukio hili inatakiwa tujue ni kipi ambacho Isaya Ndango alitaka kukifikisha kwa wananchi"
"si umesema huyu James ni rafiki yake alikuwa eeh?"
"Ndiyo bosi"
"Basi huyu ndiye tutaanza naye baada ya kumalizana na hawa watu wetu" alifunga hicho kikao kidogo na kuwasha gari yake. Gari iliingizwa mpaka ilipo car wash, kuna geti lilijifungua baada tu ya yeye kusogeza gari yake eneo hilo mithili ya mtu ambaye alihitaji kuoshea gari yake ndani ya jengo hilo. Gari hiyo ilisimama mahali ambapo palibonyea na kushuka chini kama lifti ambapo gari hiyo ilitua kwenye barabara iliyokuwa chini ya ardhi huko kisha juu pakajifunika kama mwanzo.

Aliendesha gari kwa dakika tatu tu wakashuka humo ndani na kuelekea kwenye jengo moja ambalo lilikuwa na vifaa vya kisasa huku vijana wakiwa busy kwenye komputa. Mzee huyo hakumsemesha mtu zaidi ya kufungua lango moja zito na kuingia ndani ambapo nje ya chumba kimoja aliwakuta wanaume wawili wamesimama ambao walimpa heshima na kumfungulia mlango huo ili aingie.

Aliingia akiwa ameongoza na Tina, huko ndiko ambako walihifadhiwa wale wanaume saba. Kuna hali ya utofauti walihisi, kwani wanaume wote hao saba ambao walikuwa wamefungwa vichwa chini miguu juu walikuwa kimya sana. Ikabidi Tina awasogelee akiwa amejifunika usoni.

Jambo la kushangaza hao wanaume wote saba walikuwa wamekufa kitambo mpaka ubaridi kwa mbali umeanza kuingia kwenye miili yao, wote walishtuka.

Unahisi nini kinaendelea? Vipi wamekufaje hawa?

Episode ya 18 inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: DOCUMENT NUMBER 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 19.

Kiongozi huyo wa shirika hilo la kijasusi, alitabasamu kwenye uso wake. Ilikuwa ni kawaida sana kwake pale anapokuwa na hasira sana basi ungeuona uso wake ukiwa na bashasha tele na huo ndio wakati ambao alikuwa anakuwa hatari mno. Alitoka humo ndani akiwa ameongozana na Tina ambapo safari yao iliishia kwenye lango moja la shaba.

Aliweka mkono wake hapo na lango hilo likafunguka, hiyo ilikuwa ofisi ya kiongozi wa eneo hilo. Ndani ya ofisi alikuwepo mzee nmoja ambaye umri ulienda kidogo ila mwili wake ulinawiri kwa pesa ambazo hazikuonekana kuwa shida sana kwa upande wake. Humo ofisini alikuwa amekaa huku ameilalia meza iliyokuwa mbele yake akionekana kuwa na mawazo sana.

Alishtuka baada ya kuhisi watu wameingia humo ndani
"Heshima yako kiongozi" aliongea kwa wasiwasi, haikuwa rahisi kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kiongozi huyo mkubwa wa shirika hilo.
"Hivi ndivyo jinsi unavyo ifanya kazi ambayo imekupatia maisha mazuri kwa miaka ishirini na mitano?" Kiongozi huyo aliuliza, akionekana wazi kuwa na hasira zisizo na mfano.

"Bosi naomba unisamehe sana, najua huenda kuna mahali nimekosea ila sio kwa kupenda. Nina mawazo sana, mawazo ambayo sidhani kama yataisha kirahisi sana. Mke wangu ana kansa ya ubongo na nimeambiwa kwamba anakufa ndani ya siku sio nyingi na kwa bahati mbaya sina hata uwezo wa kuwa karibu na mke wangu angalau hata kumfariji siku zake za mwisho, imefikia hatua hata wanangu wananiona mimi baba wa hovyo sana kwa kuwa wanajua simzingatii mama yao kwani hawajui lolote kuhusu kazi yangu" Mzee huyo aliongea kwa huzuni huku chozi likimtoka.

Mtu mzima akitokwa na chozi basi ujue kuna mazito sana nyuma yake. Tina licha ya uso wake kufunikwa vyema na kitambaa ila bado chozi lilishuka kwenye macho yake. Ilimuuma sana, kwenye maisha yake yote, yeye na kaka yake hawakuwahi hàta siku moja kutamka neno baba halafu kuna watu wana baba na wanamuona ni baba wa hovyo, alitamani yeye ndiye angepata hiyo nafasi ya kuweza kuita baba.

Wakati mzee huyo anahakikisha usalama wa nchi, kuwalinda wananchi ambao huwa hawayaoni mazuri zaidi ya kutukana kupitia makosa, wakati mzee huyo akiwa anachukiwa na wanae kwa kutomjali mama yao wasijue kwamba yupo kwenye majukumu ya nchi, huku mtaani wale wananchi washinda kwenye vijiwe walikuwa wanaitukana idara hiyo nyeti ya serikali, hayo ndiyo maisha ambayo ni lazima uyaishi pale unapokuwa umezungukwa na kundi la watu.

Gulamu Leopard maneno ya mzee huyo yalimgusa sana ila hata hivyo alimezea kwanza na kumuuliza
"Ni nani ambaye umemruhusu aingie kule ndani sehemu ambayo nilikuonya haruhusiwi mwenda mtu yeyote?"

"Amekuja mtu kutoka Ikulu na kusema kwamba yeye ni mlinzi wa raisi, ameagizwa na mheshimiwa kuja kuongea nao na kuna maelezo inabidi wayapate.
"Whaaaaat!, umesema mlinzi wa raisi?"
"Ndiyo mkuu, ndo amesema hivyo"
"Ooooooh f*******k, umemwaminije kirahisi sana namna hiyo?"
"Mkuu tumeskani vitamvulisho vyake vyote ni kweli ni halali kabisa vinatoka Ikulu"
"Hata hivyo ulipaswa kumzuia"
"Mkuu itifaki haituruhusu sisi kuwachunguza kwa chochote au kuwazuia kwa lolote watu wa Ikulu kwa sababu wale wana mamlaka makubwa na wanaweza kutushtaki moja kwa moja kwa raisi ikawa tatizo. Nilivyo thibitisha kwamba ni mtu wa Ikulu nilimruhusu moja kwa moja kwani najua hata wewe ungejua kwamba nimepingana na amri ya raisi usingenisamehe"
"Shiiiiiit!, ni muda gani tangu amefika hapa?"
"Ni kama dakika hamsini zilizo pita" jibu la mzee huyo likamfanya kiongozi wa idara hiyo ashtuke. Muda ambao ulisemwa hapo ndio muda ambao yeye alikuwa ndani ya Ikulu akiwa anafanya mazungumzo na mheshimiwa raisi na walinzi wa raisi wote walikuwepo nje ya mlango hata yule mlinzi mkuu alikuwepo, sasa huyo mlinzi wa wapi? Alishtuka

"Nionyeshe hiyo video haraka sana" haikuwa tatizo kwa sababu video za marejeo zilikuwepo, mzee huyo alibonyeza kwenye tarakishi yake kisha akairuhusu video ambayo ilikuwa inaonekana mbele yake. Video hiyo ilimuonyesha kijana mmoja akiwa kwenye suti yake huku shingoni akiwa na kitambulisho cha Ikulu. Alionekana tangu anaanza kuingia upande wa juu ya sehemu hiyo bila shaka kwa maana kile kitambulisho chake kilivyo skaniwa tu kila anapofika walikuwa wanamfungulia mlango kwa mashine maalumu mpaka alipofika kwenye ofisi ya kiongozi wa hilo eneo.

Hapo alijieleza kwamba alikuwa ameagizwa na mheshimiwa raisi kuweza kuongea na watu hao na maongezi yao yalipaswa kuwa ya faragha kwani ni maagizo ya mheshimiwa hivyo kamera za hiyo sehemu zilitakiwa kuzimwa haraka sana. Kiongozi huyo alikiskani upya kitambulisho cha mtu huyo na akathibitisha kwamba kweli ni mtu wa Ikulu hivyo akampa ruhusa ya kuelekea ndani ya chumba hicho.

"Pumbavu, kuna mtu ndani ya Ikulu anatusaliti" Mr Gulamu aliongea akiwa anauma meno yake, maana yake kama mtu ambaye hajulikani anaweza kupata kitambulisho cha Ikulu basi kuna mhusika ndani ya Ikulu ambaye anavujisha hayo mambo na kuwafanikishia watu hao kazi zao kiwepesi sana.
"Bosi unasema?" Mzee yule ni kama alitaka kuelewa kuhusu maelezo ya kiongozi wake ila alicho jibiwa ni;
"Nenda kamuuguze mkeo, kuna mtu atakaa kwenye hii nafasi yako mpaka pale utakapokuwa sawa utaniambia ili urudi kazini haraka sana" Mzee huyo baada ya kupewa ruhusa hakutaka hata kujua tena kile ambacho kilitokea bali alifurahia sana kupewa nafasi hiyo ya kwenda kumuaga mkewe kwa mara ya mwisho maana kwa namna yoyote ilikuwa ni lazima afe.

"Hisia ni kitu kibaya sana. Hii ndiyo sababu kubwa sana ambayo huwa inanifanya nasisitiza sana kwamba hii kazi inawafaa zaidi wale mayatima. Yatima anakuwa amepitia kila aina ya maumivu kwenye maisha yake, inafikia sehemu anakuwa hana cha kupoteza hivyo anakuwa hana udhaifu mkubwa, moja kwa moja anakuwa anafocus na kazi tu"

"Udhaifu wa mtu upo kwenye kitu anacho kipenda sana lakini udhaifu wa mwanaume ni familia yake, siwezi kumlaumu sana kwa sababu naelewa nini maana ya familia. Huenda nilipaswa kumpa adhabu kali sana kwa huu uzembe mkubwa ambao ameufanya ila naielewa hali yake, ni mwanaume ambaye mbele ya familia yake hawezi kizificha hisia zake na ile ni hatari sana kwa kazi"

"Hii dunia ambayo sisi tupo hautakiwi kuruhusu kwenye moyo wako kuwa na udhaifu wa aina ile, unaweza ukaiponza na kuiharibu nchi yako mwenyewe. Huu ni ulimwengu ambao maisha ya watu wengi yana thamani kuliko maisha ya mtu mmoja haijalishi ni nani kwako,hata awe ni mama yako mzazi inapofikia hatua ya hii kazi maisha yake hayana thamani unapohitajika kufanya jambo la kuokoa maisha ya watu wengi"

"Ila ukitanguliza sana hisia na ukaamua kuzipa nguvu basi badala ya kutumia akili utajikuta hisia zinakuendesha kufanya maamuzi ya hovyo. Unatakiwa kuwa na moyo mgumu ambao hauumizwi kirahisi na mtu yeyote. Unatakiwa kuwa na moyo ambao hata mpenzi wako ambaye unampenda sana akikwambia leo tuachane, jibu lako ni OK tu halafu unaendelea na mambo yako mengine" Gulamu Leopard alikuwa anatoa somo zito sana kwa Tina namna ya kuzizuia hisia zisije kumuongoza kufanya maamuzi akasahau kutumia akili.

"Bosi hivi wewe linapokuja suala la nchi na familia yako ukiambiwa uchague kitu kimoja utaanza na kipi?" Kiongozi huyo alimgeukia Tina na kumuangalia kwa umakini sana binti huyo.
"Unajua kwanini nimepewa hii nafasi kubwa kiasi hiki Tina?"
"Hapana sijui bosi"
"Unahisi kwamba kila mtu anaweza kupewa hii nafasi?"
"Hilo haliwezakani bosi kwani kuna watu hawafai kabisa kupewa madaraka makubwa kwa maana wanaweza kuiharibu nchi"
"Sasa umenielewa?"
"Hapana bosi sijaelewa unamaanisha nini"
"Nisikilize kwa umakini Tina, ikifika hatua wewe ukapewa mamlaka makubwa sehemu yoyote ile hata kwenye kampuni, ujue kwamba kampuni hiyo imejiridhisha vya kutosha kwamba maamuzi ya mwisho yatakayo toka kwako yatakuwa ya busara na yataleta mabadiliko makubwa kwenye kampuni husika hivyo akili yako hote inatakiwa kuwa kwenye kampuni na si kwingineko"

"Hii nafasi niliyopo mimi haupewi kwa bahati mbaya au kwa sababu kuna mtu anakujua kwani inaweza kukudhalilisha mchana kweupe. Unatakiwa kujua kwamba mimi ndiye mtu wa kwanza ambaye raisi akipata tatizo lolote nitapaswa kujibia na huenda hata nikauawa, mimi ndiye mtu ambaye nahakikisha nyaraka na taarifa za siri za serikali zinakuwa salama muda wote. Lakini pia mimi ndiye mtu ambaye nahakikisha wananchi wapo salama kwa ukusanyaji wa taarifa kila eneo la nchi yetu kisha eneo ambalo linagundulika kuwa na tatizo tunazipeleka taarifa hizo kwa jeshi la polisi na jeshi la nchi ambao wanamaliza kila kitu na ikishindikana huwa tunawaingiza majasusi wetu hususani maeneo ambayo ni nyeti sana"

"Kwa hayo maelezo nadhani umeelewa ni kwa kiasi gani hii nchi inahitaji akili yangu na kujitoa kwangu kwa asilimia miamoja ili isipate tatizo lolote. Je unahisi kwamba ni kitu gani kitakuja kwanza kwangu? Jibu ni rahisi sana ni nchi yangu. Mimi ninavyo amka kitu cha cha kwanza kukiwaza ni nchi yangu na raisi wangu kisha familia inafuata baadae na hivyo hata wewe ndivyo unavyotakiwa kuwa. Nchi yako ndiyo kipaumbele namba moja ukiwa kwenye hizi kazi"

"Mimi hata ingefikia hatua ya kuweza kumuua mwanangu wa damu kwa ajili ya nchi yangu basi nisingejiuliza hata mara mbili, ningemuua kwa mkono wangu haraka sana. Sio kwamba nitafanya hivyo kwa sababu mimi ni baba mbaya au siipendi familia yangu hapana. Nafanya hivyo sio kwa kupenda wala kutaka, nafanya hivyo kwa sababu inanipasa kufanya hivyo" mwanaume huyo alimaliza na kuhitaji kutoka humo ndani ila alizuiwa na Tina aliyekuwa amepata shule ya kutosha.

"Mkuu kuna jambo nataka tuongee"
"Tutaongea kesho usiku Dar es salaam, hakikisha unakuja na huyo mbunge" aliongea na kutoka humo ndani Tina akiwa anamfuata nyuma. Ila aliihifadhi ile kauli kwenye kichwa chake.
"Nitafanya hivyo sio kwa sababu napenda hapana, ila ni kwa sababu inanipasa kufanya hivyo"

Episode ya 19, inafika mwisho.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom