mtzmweusi
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 8,658
- 8,994
BibieBoss hata kamoja basi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
BibieBoss hata kamoja basi
[emoji996]Mbona fupiii kiongoziii ongeza zagazaga na mayonnaise kwanmbaliiiiii
Tuko pamoja [emoji1666]STORY: DOCUMENT namba 72
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 17.
Majira ya usiku wa mapema kabla Calvinjr hajapiga simu kwa Gulamu Leopard, ndani ya Ikulu ndogo ambayo ilikuwa inapatikana ndani ya eneo la DOGMA TULIPO, kwenye chumba kisafi chenye hewa nzuri ambacho kiliruhusu kila aina ya upepo mwanana kuingia bila tatizo, huenda ni kwa sababu ya Ikulu hiyo kujengwa kwenye tambalale ambayo ilijengwa juu ya safu za mlima hivyo kufanya mtu akiwa ndani ya majengo hayo kuweza kuuona mji kwa upande wa chini ya mlima.
Kwenye chumba hicho kisafi alikuwa ametulia mheshimiwa raisi wa nchi ya Tanzania, Theobald Mnyika akiwa anapata wine taratibu lakini hakuwa amekaa tu kihasara ndani ya hilo eneo bali alikuwa anaendelea kupitia kwenye mitandao ya kijamii ili kujua kwamba wananchi wake walikuwa na yapi ya kuzungumza na kuongea.
Alikuwa anapitia mitandao maarufu sana ya kijamii kama Instagram na Twitter, alicho kiona kilimfanya apate tumaini jipya sana kwenye moyo wake, alijawa tabasamu mno. Watu wengi walikuwa wanamsifia raisi huyo kwa kutoa hotuba safi sana ambayo iliwagusa wananchi wengi wa Tanzania. Watu walikuwa wakimzungunzia kwa mazuri na kuungana naye kwa kipindi kugumu ambacho alipaswa kuwa mvumilivu sana kwa yale ambayo yalikuwa yametokea.
Ila walikuwa wakimuomba sana ahakikishe mhusika wa hilo tukio anawekwa hadharani ili kila mtu aweze kumjua na alipie kila alilo kifanya huku akiwataja na wenzake. Akiwa kwenye furaha hiyo mheshimiwa raisi alisikia hatua za mtu akiwa anakuja ule upande ambao yeye alikuwepo, aliiachia tableti yake na kusogea dirishani akiwa anayashuhudia mandhari ya kuvutia ya eneo hilo lililokuwa na ulinzi usiokuwa wa kawaida.
"Tumebahatika kuzaliwa kwenye moja ya nchi ambayo ni nzuri sana. Nikiwa hapa najisikia amani kuliko eneo lolote lile, natamani sana kama siku zote maisha yangu yangekuwa hivi huenda mpaka siku nastaafu kwenye nafasi yangu ningekuwa moja ya maraisi wenye bahati sana lakini kwa bahati iliyokuwa mbaya, jambo baya zaidi kwenye historia limetokea nikiwa nipo madarakani. Una kipi cha kuongea kuhusu hili bwana Gulamu" aliongea kwa kumuuliza mwanaume aliyekuwa ameingia hapo. Naye hakuwa mwingine bali mkurugenzi wa shirika la kijasusi aliyefahamika kama Gulamu Leopard.
"Kiongozi yeyote yule duniani, kitu cha kwanza anacho kiombea na kinampa furaha ni kuhakikisha wale anao waongoza wanakuwa salama. Ndiyo maana huwa nguvu kubwa ya uongozi haipo kwenye pesa wala kwa watu wanao mzunguka kiongozi husika bali kwa wananchi. Ukiweza kuishinda mioyo ya wananchi basi wewe unakuwa kiongozi mwenye nguvu sana kwani wananchi wanaweza kukulinda zaidi hata ya jeshi na vyombo vingine vya usalama vinavyoweza kufanya hivyo"
"Umanaamisha nini bwana Gulamu?"
"Namaanisha kwamba wewe ni miongoni mwa viongozi ambao wamefanikiwa kuishinda mioyo ya wananchi na ndiyo maana licha ya mambo yote lakini bado wana imani na wewe huku wakiamini kwamba utawasaidia kufanikisha baadhi ya mambo yao hivyo hautakiwi kuipoteza hiyo imani yao kwako kwa maana ndipo nguvu yako kubwa ilipo"
"Mhhhh huoni kama hili jambo ambalo limetokea leo linaweza kunitolea imani kwao?"
"Mkuu, kuna muda tatizo unaweza ukalibadili na kuwa fursa kama tu ukiweza kuzichanga karata zako vizuri, hii inaweza kuwa nafasi ya wao kukuamini zaidi na kukupenda kuliko hata huko nyuma"
"Nadhani sijakuelewa kidogo, unamaanisha hili tatizo nilibadili kuwa fursa kwangu? Kivipi?"
"Wananchi wanacho hitaji ni kupata majibu ya kile ambacho kilitokea na kuona wahusika wakipata adhabu kali sana, hilo najua lipo ndani ya uwezo wako ila kuna jambo la mhimu zaidi ambalo ndilo wanalihitaji zaidi japo hakuna ambaye analizungumza"
"Nadhani sikufanya kosa kukufanya uendelee kubakia kwenye hiyo nafasi bwana Gulamu. Naomba nipe hayo maelezo ambayo bila shaka yana umuhimu mkubwa sana kwangu kwa sasa" Mzee huyo aliongea huku akiwa anamgeukia mkurugenzi huyo ili ayapate yale madini ya mhimu ambayo yangemfanya aweze kuzishika imani za watu hao ambao walikuwa wakimzunguka kwenye nchi yake.
"Unajua bosi, duniani kote, imani ya mtu ipo kwenye udhaifu wake mkubwa. Na imani ya wengi ipo kwenye faraja ya watu wachache wenye maumivu halafu wakapewa tumaini, sijui umenielewa kiongozi wangu?"
"Hapo umeniacha kidogo"
"Iko hivi navyosema kwamba imani ya mtu ipo kwenye udhaifu wake, namanisha kwamba udhaifu wa mtu ndio unaomfanya awe makini sana na kile kitu chake hivyo hupelekea imani yake yote kuhamia kwenye kile kinacho mpa udhaifu mkubwa akiamini hapo ndipo ilipo furaha yake au karaha yake. Kwa hili lililo tokea, kwa hawa viongozi wengi kupoteza maisha ndipo zilipo imani za familia zao na ndiyo udhaifu wao mkubwa ulipo" Gulamu aliye onekana kuijua falsafa vyema alielezea na kutulia kisha akaendelea tena;
"Viongozi wengi ambao wamekufa leo hii wametokea kwenye familia za maisha ya kimaskini hivyo familia zao imani zao zilikuwa kwa watu hao ili kuyaendesha maisha yao kwa asilimia miamoja. Ina maana hapo ndipo udhaifu wao mkubwa ulipo. Maana yake kitu ambacho wewe unatakiwa kukifanya ili kuzichukua imani zote za watu hao na kuhakikisha unatoa msaada wa kutosha kwa hizo familia zote ambazo zimepatwa na matatizo ya kufiwa na watu wao kwami kwa sasa wanajua kwamba hawatakuwa na watu wa kuwajali kwa vile watu wao wa mhimu hawapo, hivyo hata maisha yao hawana imani nayo tena"
"Wewe kutenda msaada kwa hao watu inamaanisha watu hao imani zote zitahamia kwako na kuamini kwamba wewe ndiye mkombozi wa maisha yao. Sasa hapo ndipo utaitumia hiyo nafasi kuweza kulipata kundi la watu wengi ambalo linategemea kundi la kwanza" Mr Gulamu aliguna kidogo na kuendelea;
"Kundi wa watu wengi wanaamini kwamba huwezi kumsaidia kila mtu kwa wakati mmoja, ila wanaamini kukujua na kupima imani yao kwako kwa wewe kuwasaidia wale wenye uhitaji wa lazima hivyo ukiweza kulirejesha tabasamu la wale wachache wenye majonzi mazito watakuamini sana mzee" alimaliza na kutulia kuangalia raisi huyo angesema nini kwa wakati huo.
Mzee huyo alicheka, akacheka tena
"Aisee sikuwahi kufikiria kwamba hii nchi ina watu wenye akili za kuwaza na kuona mbali sana namna hii. Wewe ni moja ya watu ambao mlitakiwa kuwa washauri wangu wa karibu sana. Kitu ulicho niambia ni kidogo sana kwa kukitamka ila ni kitu kigumu sana kukifikiria hususani kwa mtu ambaye ana uwezo mdogo kichwani. Kwa leo niseme ahsante sana nadhani umeniletea kitu kipya kichwani ambacho nitatakiwa kukitangaza hadharani baada ya hizo siku tatu" raisi aliongea akiwa anampiga piga mkurugenzi huyo kwenye bega lake, alimkubali kwa akili kubwa ambayo alikuwa nayo mtu huyo.
"Nashukuru sana kiongozi kama na mimi nimechangia jambo la mhimu mbele yako, lakini nilikuwa nina swali kidogo"
"Nakusikiliza"
"Wananchi umewaahidi kwamba baada ya siku tatu utawapatia majibu pamoja na kumtaja mtu ambaye amefanya hili tukio ambaye ni kiongozi wa nchi, huoni kama umecheza ni kamali mbaya sana hii? Vipi kama asipo patikana mpaka huo muda utawajibu nini? Na watakuelewa? Naona kama umejifunga sana bosi" raisi huyo aligeuka na kumwangalia mkurugenzi wake kwa umakini kisha akamuuliza.
"Unakumbuka hili wazo wewe ndiye umenipa?"
"Ndiyo kiongozi laki...."
"Basi mimi nimeamua kukuamini wewe moja kwa moja maana yake kama jambo likishindìkana wewe ndiye utakayepaswa kubeba lawama. Nina imani una watu makini sana kwenye ufanyaji wa kazi, hata hivi hizo siku tatu ni nyingi sana, halafu si umeniambia kwamba kuna watu sana unao kwenye mkono wako?"
"Ndiyo mkuu" Mr Gulamu alijibu ila kwa kinyongo, wanasiasa walikuwa watu wa ajabu sana kwa upande wake. Jambo likifanikiwa angejisifia yeye ndiye kalitenda ila likifeli basi kiongozi huyo wa usalama angeubeba msalaba pekeyake. Hakuwa na cha kufanya, huyo alikuwa ni bosi wake.
"Sasa hapo hofu yako iko wapi? Au huamini kuhusu uhusika wa hao watu kwenye hili? Hakuna ambacho huenda mmekipata labda?"
"Kuna kitu ambacho tumekipata kinaonyesha uhusika wa moja kwa moja kuhusu mlipuko wa leo" maelezo yake yalimfanya raisi amsogelee kwa umakini
"Kitu gani hicho?"
"Rimoti iliyo tumika kulipua bomu"
"Whaaaaaaat?"
"Ndiyo mkuu na mtu ambaye alikuwa na hiyo rimoti yupo kwenye mkono wetu tayari na usiku wa leo naenda kumhoji"
"Yes kazi nzuri sana na hicho ndicho ambacho nataka nikisikie kutoka kwako. Huyo mtu hakikisha mpaka kesho asubuhi awe ameeleza kila kitu ili tuweze kuupata huo mtandao wote ambao unahusika na hili jambo haraka sana"
"Sawa mkuu nitalishughulikia hili jambo haraka sana"
"Halafu nataka kujua kitu kimoja, nahitaji kumjua huyu kijana wako ambaye amefanya kazi nzito hii ya kuhakikisha watu hawa wanapatikana kirahisi sana, nahitaji kukutana naye niweze kumpatia zawadi yake ambayo anastahili. Umewafunza vyema vijana wako wanaonekana kwamba wapo makini sana na kazi" raisi alitulia kidogo akiwa anaangalia saa yake kisha akaongeza;
"Kesho natakiwa kuwahi kwenye familia ya waziri mkuu kwenda kutoa pole kwa kupotelewa na mtu mhimu sana kwao, wanaweza kuhisi ni jambo la ajabu sana kama nisipo enda kuwapa hata pole na kutia neno la faraja kwao, hivyo kesho asubuhi wakati unaniletea ripoti ya majibu uliyo yapata kwa watu hao, muandae na msafara wangu ambao nitahitaji ulinzi kutoka kwa vijana wako mpaka Dar es salaam"
"Sawa mkuu" mkurugenzi alimaliza mazungumzo na bosi wake ambaye alikuwa amemuita hapo na kuanza kutoka ndani ila alisimama baada ya kusikia mheshimiwa raisi anaongea na simu akitoa amri kwa jeshi la polisi huko kwenye jimbo la DAMU INAYO ISHI kwamba wahakikishe wanadumisha ulinzi wa kutosha nyumbani kwa mbunge Isaya Ndango na kama wakimkuta mtu yeyote ambaye hahusiki na hiyo sehemu basi wahakikishe wanamkamata.
Na huo ndio muda ambao Calvinjr alimpigia simu kiongozi wake huyo akimweleza hali ya huko na kiongozi huyo akamtaka atoweke hilo eneo haraka sana kwa sababu alisikia taarifa ya kwamba polisi wangejazana mahali pale muda sio mrefu.
Unadhani ni kipi kinaenda kutokea humu ndani?
Episode ya 17 inafika tamati.
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
AbeeeeBibie
AsanteBaadae mzigo unawekwa.
Leo nawabariki episodes mbili.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Wabheja Sana FEBIANI BABUYABaadae mzigo unawekwa.
Leo nawabariki episodes mbili.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app