Malimi Jr
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 1,287
- 2,743
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Respect [emoji120][emoji120]STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA SABINI NA NANE
SONGA NAYO................
Mikono yake ilikuwa na nguvu za ajabu, alikuwa anatembea juu ya miti kama naangalia drama za wakorea. Mkono ulikuwa ukitua kwenye mti basi mara moja mti unabonyea. Nilitamani kupiga makelele ila nilijizuia na kukimbia eneo lile kurudi kulala, nilitamani kumjua kiundani zaidi ya alivyokuwa ametueleza kuhusu yeye, nilitaka kumjua upande wake mwingine kwamba ana kitu gani hasa kiasi kwamba ana uwezo wa ajabu namna ile ndipo nikaja kuyajua mambo magumu sana kuhusu yeye mambo ambayo sikuwahi kumshauri mtu mwingine yeyote aweze kuyajua kwa sababu ni hatari mno tena yanaweza kufanya mtu amuogope maisha yake yote”
“Mhhhhh simulizi ya maisha yako inasikitisha sana, nimejisikia vibaya kwa ambayo yamekukuta lakini hilo la bosi wako halionekani kuwa jambo la kawaida”
“Ni kweli sio jambo la kawaida ndiyo maana kuna vitu hautakiwi kujua kuhusu yeye kwa sababu inaweza kukufanya usije kukaa karibu naye tena, itakufanya umuogope maisha yako yote. Mambo mengi kuhusu yeye nilikuja kuyapata baada ya kuisoma diary yake, ameandika mpaka namna atakavyokuja kufa”
“Whaaaaat?”
“Yeah, ndilo jambo ambalo linanitisha kuhusu yeye. Kuna muda natamani asiimalize hii vita mapema kwa sababu siku akiimaliza tu ndiyo siku ameandika kwamba ni lazima afe”
“Anajua kama wewe unajua kuhusu hili?”
“Hapana, niliisoma kipindi yeye hayupo na hajui kama niliiona hiyo Diary yake”
“Kuna muda huwa anaondoka au?”
“Ana familia ambayo kwa sasa ameileta karibu huku japo ni eneo la siri sana ilipo”
“Unamaanisha nini kusema ana familia?”
“Ana mke na mtoto”
“Bila shaka ndio udhaifu wake mkubwa”
“Kila mwanaume udhaifu wake mkubwa ni familia yake Sarah”
“Naweza kujua sababu gani ambayo imemfanya mtu huyo ajitabirie kifo?”
“Watu ambao anajua anaenda kukutana nao sio wa kawaida nao, ni watu hatari sana ambapo lolote linaweza kutokea lakini kuna kitu ambacho kinamfanya hata baada ya hili kuisha apange kuyabeba maisha yake mwenyewe”
“Anataka kujiua?”
“Ndiyo”
“Kitu gani hicho?”
“Ana nguvu za ajabu kwenye mwili wake ambazo utafika wakati hatakuwa na uwezo wa kuweza kuzimudu tena hivyo zinaweza kuja kuwa hatari kwa huu ulimwengu”
“Nguvu gani hizo?”
“Hauwezi kunielewa, ni nguvu ambazo amekatazwa kuweza kuzitumia na kama ikilazimika akizitumia basi hatakuja kuwa binadamu wa kawaida tena ndiyo maana amepanga hadi namna ya kufa kwake ambapo hataki kabisa familia yake ije kuona mwili wake. Amepanga kufanya hivyo kwa sababu siku anamaliza kazi yake anajua itamlazimu kuzitumia nguvu hizo kwahiyo akizitumia kwa kiasi kikubwa uwezo wa kuzihimili utakuwa mdogo, itampelekea kupoteza kumbukumbu na kuwa muuaji, hapo anaweza kuja kuanza kuua kila mtu hata ambao alikuwa anawajua na kuwalinda, hataki kabisa kufikia hatua hiyo ndiyo maana amepanga kupotea kwenye nyuso wa walimwengu kabisa baada ya kazi kuisha” Sarah alikuwa anasisimka na kuogopa kwa wakati mmoja kipindi anapewa simulizi ya maisha ya mtu ambaye wakati huo ndiye alikuwa anaenda kukutana naye.
“Hizi nguvu anazo kabla au baada ya kuwa na mtoto?”
“Mtoto wake ni wa juzi tu hapa, hizo nguvu anazo hata kabla ya kuwa kabisa na familia”
“Kuna namna hizi nguvu zinaweza kuhamia kwa mtoto kwa njia ya asili?”
“Hilo jambo hajaliandika humo ndani japo huenda inawezekana ila sijui”
“Kama hilo linawezekana basi kuna hatari nyingine hata mtoto wake akaja kuwa nazo kwa baadae, hizi nguvu za asili huwa zinakuwa na nguvu zaidi kutokana na namna zinavyozidi kuhama kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.”
“Hilo tuliache kwa sasa, unaweza kwenda kuonana naye” maongezi yao yalikuwa yanafanyika nje ya lango moja kubwa sana, walikuwa wamefika sehemu ambayo Sarah alikuwa anatakiwa kwenda. Simulizi fupi ya maisha ya akina Othman aliyopewa pamoja na nguvu ambazo alikuwa nazo Gavin Luca alijikuta anatetemeka huku jasho likiwa linamtoka kwa wingi kwenye mwili wake licha ya kiyoyozi kuwepo kila kona ya jengo hilo.
“Kwanini umeamua kuniambia haya yote Othman?”
“Mpaka tumekuleta ndani ya hii sehemu ujue umeaminika na sidhani kama kuna lolote unaweza kulifanya juu ya nilicho kwambia”
“Mpo wangapi ambao aliwachukua kwa ajili ya kuwasaidia?”
“Jumla tupo wanne”
“Wote mpo humu ndani?”
“Hapana. Mmoja ni mlinzi wa mama, mmoja ni mlinzi wa mke wa bosi, mmoja ni mlinzi wa mtoto wa bosi na mimi hapa mara nyingi huwa nipo kwa ajili ya kumlinda bosi inapobidi lakini mara nyingi huwa ni ngumu kutuona jambo ambalo huwa linafanya mtu yeyote asijue kama tupo mahali husika”
“Na wote mmeshalipiza visasi vyenu?”
“Wote kwa sasa tumemaliza, bado mmoja wetu ambaye ana deni na mkuu wa majeshi japo hataki kumuua kwa mkono wake, bila shaka hamalizi masaa ishirini na manne atakuwa amemaliza kisasi chake hapo itabaki zamu ya bosi mwenyewe”
“Mnataka kumuua mkuu wa majeshi?”
“Ndiyo”
“Ni jambo gumu sana”
“Hilo ni gumu kwako, hauwajui watu ambao upo nao hapa wakati huu namna walivyo hatari Sarah, kakutane naye utaanza kunielewa” mwanaume huyo aliongea huku akiwa anaweka jicho lake ukutani kwa ajili ya kulifungua lango hilo. Lilifunguka, ndani kulikuwa na vitu vya thamani sana, pembezoni alionekana mwanaume mmoja akiwa amekaa kwenye sofa anaziangalia picha kadhaa ukutani. Ilikuwa kwa mara ya pili yeye kukutana na Gavin Luca mwenyewe, Sarah alikuwa anaogopa hata kuingia ndani ya eneo hilo, mwanadamu ambaye alikuwa anaenda kukutana naye hakuwa wa kawaida kama walivyo wengine, alikuwa ni mtu ambaye anatisha isivyokuwa kawaida ila hakuwa na namna.
Taratibu alianza kuzirusha hatua zake kuelekea kukutana na mtoto wa mfanya biashara wa dawa za kulevya ambaye alifanikiwa kuujenga mji wake mwenyewe na kulisaidia taifa kwa kulipa zaidi ya pesa za kimarekani zaidi ya bilioni kumi lakini kwa bahati mbaya sana akaishia kuuawa na mtu ambaye hakuwahi kujulikana alitoa amri, ndiyo kazi kubwa aliyokuwa nayo Gavin kuweza kumpata mtu huyo ambaye alitumia miaka mingi kuishi gizani mpaka siku hiyo hakuwa amemjua bado lakini kwenye mkono wake alikuwa na jina la Medrick Savato, mkuu wa majeshi.
Huyo alitakiwa kumpa majibu yote pindi akimtembelea na ni huyo ambaye aliahidi kwamba akirudi kutoka huko Singida ambako alienda kuifuata familia yake na kumwambia ukweli wa maisha yake mkewe alitakiwa kudili naye.
78 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.
Leo ni leo[emoji91][emoji91][emoji91]SIKU ZA MWISHO [emoji736] (GIZA LA MALAIKA)- THE DARKNESS OF AN ANGEL.....
Hii ni simulizi mpya ambayo inatoka tarehe 11 mwezi huu wa 3.....
Ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya mwendelezo wa IDAIWE MAITI YANGU na SAFARI YA GAVIN LUCA (THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA)....
Humu utajua hatima ya familia ya GAVIN LUCA na mwanae wa pekee LIONELA na hatima ya zile nguvu zao.
Kwenye SAFARI YA GAVIN LUCA uliona JABARI akionekana msaliti, hivyo kama unataka kujua sababu nyuma yake kwamba kwanini alimsaliti mkewe wa ndoa? Basi hii ndiyo sehemu sahihi ya kupata majibu yako.
JABARI alituacha wote mdomo wazi baada ya kumuoa LIONELA kisha akaanza kuua familia ya LIONELA Lakini mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Kenya (NIS) alikuwa na ajenda gani hatari kwa Tanzania na familia ya GAVIN LUCA? Jumuika nami ili uweze kupata majibu sahihi [emoji3578]
Hili ni andiko langu la kwanza kwa mwaka huu tangu uanze hivyo tarajia kukutana na mambo mazito ndani yake.
Kwa wale ambao huwa wanapenda kuwa wa kwanza kusoma unaweza kuweka order yako mapema au kunitafuta mapema ili inavyotoka uwe wa kwanza kuweza kuisoma [emoji3578]
Bux the storyteller
FEBIANI BABUYA [emoji736]
IMEACHIWA tayari mkuu..
Weka Link hapa mkuuIMEACHIWA tayari mkuu..
Collection imekamilika
1. IDAIWE MAITI YANGU
2. THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA - SAFARI YA GAVIN LUCA (LIONELA)
3. SIKU ZA MWISHO- THE DARKNESS OF AN ANGEL (Hii imeachiwa alasiri ya leo) 🔥🌹🌹
Hazipo huku mkuuWeka Link hapa mkuu
Respect mkuu kazi nzuriSTORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA SABINI NA MOJA
SONGA NAYO................
“Kama alifika lile eneo kwa wakati mwafaka maana yake huenda anajua kuhusu sisi ama ana taarifa za mhimu kuhusu sisi hivyo hatupo salama. Kuanzia wakati huu tunatakiwa kujiandaa kwa jambo lolote ambalo linakuja mbele yetu”
“Tunajiandaa?”
“Ndiyo”
“Nashukuru kwa taarifa yako lakini hauwezi kuishi, umeshindwa kufanya kazi uliyopewa ni ishara ya wazi kwamba hauna faida tena ndani ya jamii hii hivyo unatakiwa kufa”
“No, no no usinifanyie hivi, nimejitoa kwa kila kitu kwa ajili ya mheshimiwa, nimemsaliti mpaka Sarah ambaye alikuwa ameanza kuniamini sana kwa ajili ya hili halafu leo unataka kuniua tena? Tafadhali Bashir mimi nitalisahihisha hili nakuahidi”
“Too late Nickson” mshahara wa dhambi ni mauti, mwanaume huyo alimsaliti mwanamke ambaye alikuwa amemuamini kwa nafasi kubwa, aliamini yeye na bwana huyo wangeyaanza maisha ya pamoja lakini bwana huyo aloionekana kuwa na mipango tofauti kabisa kwenye kichwa chake ila mwisho wake haukuwa wa kuvutia. Bashir alimzamishia kisu kwenye koromeo lake, alikitoa na kukisimika moyoni tena kwa mara nyingine hakuwa na kauli, alibaki anababaika akiwa kama mtu ambaye alihitaji kufanya jambo fulani lakini hakuwa na huo uwezo, muda wake wa kuishi ulikuwa umeisha.
Bashir aliinua mkonga wa simu na kuuweka kwenye sikio lake, simu hiyo iliita kwa muda kidogo kisha ikapokelewa;
“Bosi kuna tatizo kubwa limetokea”
“Nakusikiliza Bashir”
“Sarah ametoroka”
“Bashir, are you serious?”
“Nimefuata maagizo yako kumtuma mhusika lakini amerudi hapa akiwa kwenye hali mbaya akidai kwamba kuna mtu ambaye alienda kumuokoa pale”
“Ni nani huyo mtu?”
“Anadai kwamba hamjui kwa sababu alijifunika kitambaa”
“Kwahiyo kuna taarifa zozote kuhusu huyo mtu?”
“Hapana bosi”
“Na huyo bwana mdogo yuko wapi?”
“Nimemuua”
“Huo mwili wake unatakiwa kutupwa karibu kabisa na barabara kisha usiku wa leo hii watafute waandishi wa habari nguli ambao wanaaminika, vujisha taarifa kuhusu Sarah, apewe kesi hadharani ya mauaji ya mke wa raisi lakini pia kwa kuua wanajeshi ambao walienda kumkamata akiwepo huyo mwanajeshi mwenzake wa karibu”
“Itahitajika ushahidi kwenye hilo bosi”
“Tuna silaha ambayo aliitumia kwenye kufanyia tukio lile, maana yake mpaka hapo ni kwamba tuna finger prints zake, maana yake hatakuwa na namna ya kuweza kukataa”
“Sawa mkuu” simu ilikatwa ambayo kiukweli haikuwa njema sana kwa Medrick Savato.
***
Upande wa pili alikuwepo mkuu wa majeshi akiongea na simu hiyo, simu ilimkutia kwenye jengo kubwa la kanisa, alikuwa ameketi katikati kabisa ya jengo hilo. Nje ya kanisa hilo ambalo lilikuwa katikati kabisa ya mji kulikuwa na ulinzi mkali mno wa makomando, hakuwa na imani sana na maisha yake, alisimuliwa na mzee Hasheem aina ya mtu ambaye alikuwa anadili naye, alimtaka bwana huyo kuwa makini kwa kile sekunde ambayo ilikuwa inazidi kwenda kwa sababu kadri saa ilivyokuwa inazidi kwenda ndivyo nafasi yake ilivyokuwa inazidi kuwa ndogo ya kuendelea kuwa hai.
Eneo hilo alikuwa na miadi ya kukutana na mtu usiku huo, simu ambayo aliipokea ilimharibia siku yake kwani ratiba haikupangwa kuwa hivyo lakini alishukuru kwa sababu alikuwa na karata ya ushindi mezani kwenye hilo. Aliamini kwamba mpaka kunakucha asubuhi, habari zingezagaa kila kona, jina la Sarah lingeonekana baya kila sehemu, mwanamke huyo alikuwa anaenda kupata umaarufu kwa kuwa na kesi nzito mbele yake ya kuhusika na mauaji ya mke wa raisi wa nchi, ilikuwa ni habari mbaya na jambo la hatari mno kwake.
Akiwa amezama kwenye mawazo hayo, alisikia mjongeo wa hatua za mtu ukiwa unakuja ile sehemu ambayo alikuwepo. Hali hiyo ndiyo ambayo ilimtoa kwenye yale mawazo ambayo alizama kuyatafakari na kupima ukubwa wa mzani ambao alikuwa anatakiwa kuutumia kupimia kilo zake, mzani haukuwa ukibalansi vizuri upande wake. Mwanamke huyo Sarah alikuwa akimuumiza mno kichwa chake, kwanini? Yeye ndiye ambaye alikuwa nyuma ya mpango wa mauaji ya mke wa raisi kwa kumtumia binti huyo lakini mpaka wakati huo binti alikuwa hai na mzima wa afya, hilo kwake lilikuwa tishio kubwa na kwa bahati mbaya alidaiwa kukimbilia kusiko julikana na familia.
Usiku huo alipanga kwenda kumchafua binti huyo ila hilo halikumpa amani, aliamini kwamba hakunaga siri ya watu wengi, siri inakuwa siri inapobaki kuwa ya mtu mmoja, sasa inabaki vipi kuwa ya mmoja wakati ni wengi wanaijua na mhusika ndiye huyo alikuwa katoweka? Aliamini kuwa hai kwa Sarah kuna siku ingekuja kumtokea puani, mwanamke huyo alitakiwa kupatikana kwa gharama yoyote ile. Mheshimiwa aliona kabisa kwamba wakati wa yeye kucheza fair play uliisha, alitakiwa kuwa na roho ngumu ya kijerumani, ubaya ubaya hakutakiwa kucheka na mtu yeyote yule.
Alikuwa na jeshi nyuma yake, sasa alitakiwa kumhofia nani? Alijishangaa, mtu pekee ambaye kwake alikuwa tishio ni raisi. Vipi kama raisi akija kujua kwamba yeye ndiye mhusika halisi wa kumuua mkewe ambaye alimpenda mno? Angemuacha? Jibu lilikuwa hapana, basi mpaka hapo karata ya ushindi ilitakiwa kuwa kwake hata kwa bao la mkono. Aliguna kumpa taarifa mgeni wake kwamba alikuwa tayari kumsikiliza kwa sababu mtu huyo alikuwa amekaa mstari mmoja na mkuu wa majeshi, wote walikuwa wakiangalia mbele kana kwamba kila mtu hakuw ana muda na mwenzake. Yalikuwa maongezi ya kitaalamu ambayo yalikuwa yanafanywa na wataalamu wa kazi, hawakuwa na mapepe, kila mtu alijua kile alikuwa anakifanya na ambacho alitakiwa kukifanya.
“Najua haupendi kuonana na mimi ila nimekuja hapa kwa sababu ya msingi mno kama utakuwa tayari kuweza kunisikiliza na kuufanyia kazi ushauri ambao nimekuja kukupatia hapa bwana Savato”
“Kama nina kumbukumbu sahihi hakuna jambo lolote lile la maana ambalo umewahi kujali kuhusu mimi”
“Kwanza nasikitika kukwambia kwamba mimi najua kila kitu kuhusu wewe”
“Mhhhh ndugu yangu ni kauli nzito sana hiyo, unamwambiaje mwanaume mwenzako kwamba unajua kila kitu kuhusu yeye?”
“Sipo hapa kwa ajili ya kukuletea misemo ya kihuni ya mtaani bali nipo hapa ili uweze kuujua ukweli, unatakiwa kujua mbivu na mbichi ili ufanye maamuzi yaliyo sahihi kwani kila unavyozidi kukosea ndivyo unaikaribisha hatari zaidi kwa upande wako” sauti hiyo haikuwa ya mtu mwingine bali mkurugenzi wa usalama wa taifa, Othman Micho ndiye ambaye alifika ndani ya eneo hilo kwa ajili ya kufanya maongezi na huyo kigogo mwenzake.
“Nakusikiliza”
“Taarifa ambazo ninazo kutoka kwa vijana wako ni kwamba huenda wewe ndiye mtu ambaye unafuata kwa sasa kufa. sina uhakika kama itakuwa ni kufa moja kwa moja ama mtu huyo anahitaji kukuteka ili akakuhoji, inaonekana mna historia ndefu kidogo nyie wawili”
“Hahaha hahaha hahaha, Othman unazeeka mapema sana ndugu yangu, kweli unaamini hayo maneno yako kwamba kuna binadamu ana hiyo jeuri ya kuweza kumteka mkuu wa majeshi? Kabla sijajibu hata hoja yako wewe unaona kwamba hilo jambo linakuja kwenye mzunguko wa afya ya akili yako?”
“Ni jambo linalowezekana kwa asilimia zaidi ya sabini, mimi na wewe wote tunaelewa kwamba jambo likifikisha kuanzia asilimia hamsini na kuendelea basi kufanikiwa kwake ni uhakika zaidi kwahiyo naweza kukuhakikishia kwamba linawezekana vizuri tu. Taifa lenye nguvu zaidi duniani limewapoteza maraisi wake wa nne kwa kuuawa, hilo ndilo taifa ambalo raisi wake ana ulinzi mkali kiasi kwamba hata sisimizi kumfikia pale alipo ni ngumu kuliko unavyodhani lakini waliuawa. Nalizungumzia taifa la Marekani.
71 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.
Heshima kwako mkuu 🫡Tuko pomoja mkuu. Kazi safi sana, nimeisoma usiku ma mchana toka juzi
Karibu sanaRespect mkuu kazi nzuri
Kikubwa namba zipo pale, basi nitapenda niipate yote kulingana na beiHeshima kwako mkuu 🫡
Baadae napandisha episodes
Karibu.Kikubwa namba zipo pale, basi nitapenda niipate yote kulingana na bei