Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
GoodSTORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA SITINI NA TANO
SONGA NAYO................
Hakuna kitu ambacho kiliundwa na intaneti au mtandao kingempiga chenga, alikuwa miongoni mwa magwiji wa IT wakati anasoma. Kama ilivyokuwa kawaida kwa taifa la Tanzania, haikujalisha mtu ana uwezo gani lakini kama hakuwa na marefa wa kumbeba basi uwezo wake ungefia ndani kwake bila kuufaidisha ulimwengu wala taifa. Kijana huyo alikuwa mmoja wao, kijana mwenye uwezo mkubwa lakini hakuwa na ajira ila hakujali kwa sababu uwezo wake ulikuwa unampa nafasi ya kufanya lolote na popote bila kuacha alama mahali popote pale. Kwa Ethan kijana huyo alionekana kama dini la dhahabu ambalo lilitupwa juu ya jalala halafu kila mtu akawa analidharau.
“Ethan mshikaji wangu, nakujua sana, hunaga muda kabisa wa kuja kunisalimia au kunijulia hali rafiki yako. Mara nyingi ukija hapa unahitaji ni msaada, kwa leo nikwambie mapema kabisa kwamba siwezi kukusaidia” kijana huyo aliongea akiwa anamwangalia mwanamke mwenye maumbile makubwa ambaye alitoka dukani kwake wakati huo. Ethan aliishia kucheka, rafiki yake alikuwa kiwembe sana linapokuja suala la kupenda ngono.
“Hili tatizo ambalo ninalo mimi haliwezi kulala Ethan ndiyo maana nipo hapa”
“Oioooooh shiit Ethan!”
“Mimi ndiye ndugu yako ambaye tutazikana hivyo najua huwezi kunitupa Brian”
“Ni kuhusu kazi yako?”
“Ndiyo”
“No, kwa leo siwezi kukusaidia kwanza nipo busy sana na kazi hapa”
“Funga duka Brian, tunaondoka muda huu kwenda kwako”
“Ethan mimi na wewe tumesha malizana”
“Kuna kiongozi mkubwa ameuawa muda mfupi uliopita?”
“Are you serious?”
“Unapoteza muda mwingi kufanya ngono, unapenda mno kukata viuno kwa wanawake vinginevyo hizi taarifa mpaka muda huu ulitakiwa kuwa nazo kwa sababu zimesambaa kila sehemu”
“Sio mbaya hawa wanasiasa nao wawe wanauawa hivi ili waone maumivu ambayo raia huwa wanayapitia wanapo wapoteza wapendwa wao kwa uzembe wa hawa wanasiasa ambao wamejaa propaganda mdomoni”
“Hii kesi nataka kuifuatilia off books Brian”
“Hilo ni jambo la hatari kama ukikutwa, sikushauri”
“Hakuna kitu unaweza kuongea kikanishawishi mimi kuachana na hili”
“Una uhakika?”
“Ndiyo Brian kwa sababu hii kesi ilikuwa kwenye mkono wangu ila mamlaka za juu wameibeba hivyo nataka kuwathibitishia kwamba naweza kuitatua kesi kwa ukubwa na kwa namna bora kuliko wao huenda kuna siku watakuja kuona umuhimu wangu ndani ya hili taifa”
“Bado unahitaji kupanda madaraja kazini kwako?”
“Ndiyo ndoto yetu Brian” kijana huyo alimsikitikia mwenzake kwa sababu alikuwa anajiingiza kwenye hatari ya waziwazi ila hakuonekana kabisa kujali juu ya jambo hilo.
“Haya mambo yatakuja kuwa na mwisho mbaya sana kwa upande wako. Huenda mambo ambayo unataka kuyagusa yanaenda kuharibu maslahi ya wengi hivyo ungeshukuru watu hawa kukutoa huenda wanakuokoa na mengi” Brian aliongea akiwa anafunga sehemu ya duka lake na kuongoza kwenye gari yake ndogo. Ethan hakujibu kitu zaidi ya kutabasamu tu maana alimjua jamaa yake huyo kwa kupenda kutoa toa ushauri ambao haukuwa na umuhimu wake kwa muda huo.
Taarifa ambazo zilikuwa zinahitajika zilikuwa ni taarifa za Othman chunga lakini pia taarifa za siri za waziri wa mambo ya ndani. Kijana huyo alihakikisha amefunga kila kitu kwenye nyumba yake, alikuwa na chumba cha siri ambacho kwenye kuta zake kulikuwa kunafunikwa kompyuta kubwa zenye uwezo mkubwa sana.
“Hivi vitu vyote huwa unavitoa wapi Brian?”
“Hahahaha Ethan ili uweze kuishi kuna muda maisha yanatufundisha mambo mengi sana. Siku ikitokea umeingia kwenye hii kazi yangu utaelewa namna ambavyo vinapatikana ila kwa sasa huwezi kuelewa kwa sababu hauna kazi navyo”
“Mhhhhhh” Ethan aliishia kuguna tu kwa sababu kwa wakati huo hakuwa na jambo la kuweza kuongezea hapo.
Sura za watu hao ziliingizwa kwenye mtambo maalumu, jambo la kushangaza ni kwamba taarifa na wasifu wa waziri ulikuja kirahisi sana lakini kwa upande wa Othman ilikuwa ni tofauti kabisa, kilikuja kivuli tu hakukuwa na taarifa ya namna yoyote ile.
“He is a ghost” kijana huyo aliongea akiwa anamgeukia Ethan
“Comon Brian, wote tunajua unaweza kuzipata taarifa zake”
“Kama ikitokea nikafanya hivyo itanilazimu kuingia kwenye taarifa za siri zaidi ambazo ili kuingia huko natakiwa kulipia na ni jambo la hatari mno kwa sababu naweza kujulikana na mhusika kwamba namtafuta na sijui ni mtu wa namna gani Ethan. Unayajua kabisa maisha yangu ni ya siri hivyo naweza kuishia kuuawa kama kuna watu watajua ninacho kifanya”
“Please Brian, hii itakuwa mara yangu ya mwisho kuuhitaji msaada wako na hiyo pesa mimi nitailipia” kijana huyo alisikitika kwa sababu alikuwa anafanya jambo la hatari mno hususani kuingia kwenye mtandao ambao kisheria haukuwa unaruhusiwa, ulikuwa unatumiwa na watu zaidi wa Dark Web nao walikuwa ni wa kuhesabika na ulikuw wa gharama kuweza kupata taarifa yoyote ile. Ni mtandao ambao ulikuwa una nguvu ya kumpata yeyote na mahali popote hata kama anaishi kwa siri vipi, kikubwa kama kungekuwa na kiunganishi chake chochote kama picha au jina.
Ilimlazimu Brian kuzima mitambo yote na kuitoa laptop yake moja ambayo ilikuwa kwenye safe, alijifikiria sana kabla ya kufanya maamuzi ya kuweza kuiwasha ili afanye kazi ambayo rafiki yake alimuomba waweze kuifanya.
“Ethan hili jambo naenda kulifanya kwa sababu wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu ila kitu unachotakiwa kukijua ni kwamba jambo kama hili mwisho wake huwa ni damu. Tunaweza kufa wote ama mmoja wetu kufa, kwamba tutaishi wote sina uhakika kabisa juu ya hili. Nimewahi kuona baadhi ya kesi za namna hii na mwisho wake haujawahi kuwa mzuri hata siku moja. Nakuuliza tena, una uhakika na hili jambo?”
“Ndiyo Brian” kijana huyo alionyesha kuwa na wasiwasi mkubwa ndani yake ila hakuwa na namna. Yalitumika masaa matano wakiwa mbele ya laptop hiyo kuweza kutafuta taarifa hata chache tu za mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Othman chunga. Baada ya muda mrefu kuweza kupita ikiwa wanaelekea kukata tamaa ndipo lilitokea jambo ambalo hata wao hawakuweza kulitegemea kama lingeweza kuja hapo.
Ilikuja picha ambayo ilionekana kuwa na mfanano na picha hiyo, haikuwa picha ambayo kwa mfanano ni kweli ilikuwa inaendana na Othman ila kwa taarifa za huo mtandao wa siri zilikuwa na mfanano kwa maana hiyo kulikuwa na nafasi kubwa kwamba watu hao walikuwa ni ndugu, sasa kama ni ndugu ni undugu upi huo? Bila shaka ulikuwa wa baba na mtoto. Jina lililokuja hapo ilionekana picha ya mwanaume mmoja ambaye alikuwa kwenye vazi la polisi mwenye nyota mbili begani.
Dato Pazu, ndilo jina ambalo lilikuja hapo na taarifa chache, mwanaume huyo alikufa kwa kukutwa ameuawa miaka kadhaa iliyokuwa imepita baada ya kujihusisha na kesi moja ambayo alikuwa anamshitaki mwanasiasa Slyvester Mboneka wakati huo akiwa mbunge. Ni jambo ambalo liliwashangaza pakubwa, kwamba ilikuwa bahati mbaya jambo hilo kutokea? Wote walikuwa na uhakika kwamba haiwezi kuwa bahati mbaya, sasa ni nini kilikuwa kinaendelea? Ikawalazimu kusoma taarifa zaidi ndipo wakagundua kwamba bwana huyo alikuwa na mtoto mmoja wa kiume. Kanaan ndilo lilikuwa jina lake.
65 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.
Mwanzo wa kujipalia makaa ya mawe...STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA SITINI NA SITA
SONGA NAYO................
Taarifa za mkewe zilikuwa fupi kwamba alikufa miaka mingi akiwa anajifungua mtoto wake wa pili ambapo mama na mtoto walikufa, sasa kama mtu huyo aliuawa huyo mtoto wake Kanaan alikuwa wapi? Taarifa zilidai ni UNKNOWN.
“Hii sio bahati mbaya, Othman ndiye Kanaan”
“Kwamba ndiye mtoto wa huyo askari ambaye tumemsoma hapa”
“Kwahiyo ni yeye amemuua waziri wa mambo ya ndani kwa sababu alimuua baba yake?”
“Kuna ukweli mkubwa kwenye hilo lakini kuna kitu bado hakiji hapa” Brian aliongea akiwa anaendelea kutafuta taarifa zaidi ya hizo ambazo walikuwa nazo.
“Kipi?”
“Kama ni mtoto wa askari kivipi taarifa zake zilipotea ghafla? Lazima taarifa zake zingekuwepo”
“Huenda baba yake hakutaka kumuweka hadharani mwanae kwa sababu alikuwa anajua kazi ambayo anaifanya” Ethan aliongea akiwa anatazama taarifa hizo mara mbili mbili.
“Hapana, Ethan kuna kitu hakipo sawa kabisa”
“Kivipi?”
“Kwanza kama ni yeye amefanya haya kwa hiyo video ilivyo ni wazi kwamba amefundishwa na mtu mwenye uwezo mkubwa sana lakini pili kuishi kama mzimu kwa muda mrefu kwenye dunia hii ya teknolojia kubwa inatakiwa uwe na rasilimali fedha nyingi sana. Ukiacha hilo huyu waziri kwa taarifa za ndani ni kwamba alikuwa anajihusisha na kuwa na ukaribu na wafanya biashara kadhaa akiwemo mmoja wa huko Zanzibar ambaye mtoto wake anadaiwa amekutwa amekufa”
“Ndiyo namfahamu, anaitwa Ismail Mhammed, kafanyaje?”
“Waza vizuri, kuna muunganiko wa haya matukio, haiwezi kuwa bahati mbaya, sasa kama huyu alimuua baba yake sawa, tuseme kwamba alikuwa na kisasi binafsi na mtu huyu. Vipi na huyo tajiri wa Zanzibar?”
“Hapo sasa Ezra alishtuka na kulikumbuka jina ambalo limekutwa huko Gavin Luca” alikuwa kama amepigwa na butwaa.
“Unamfahamu vizuri huyo mtu?”
“Hakuna anaye mjua vizuri lakini jina lake lilivuma sana kipindi cha miaka ya huko nyuma kwenye kesi moja ya muuzaji wa madawa ya kulevya. Huyu alidaiwa kuwa mtoto wa huyo bwana lakini aliuawa ila baadae akaja mtu mwingine na kuanza kutumia jina lake ambaye amekuwa akiisumbua serikali kwa muda mrefu sana wakiwa hawajui mtu husika ni nani. Mara ya kwanza walihisi kwamba ni mtu ambaye anatafuta kiki za mitandao ila kwa sasa na haya mauaji anaanza kuonekana kuwa mtu tishio zaidi kwa taifa” Ezra alielezea zaidi kwa undani kumpa mchanganuo mzuri rafiki yake.
“Kwa maana hiyo hawa wapo nyuma ya mtu mmoja”
“Wapo?”
“Kama ni hivyo maana yake huenda ni kundi la watu ambao wamejikusanya kuhitaji kulipa visasi. Huenda ni mtu mmoja aliamua kuwakusanya wote ambao wazazi au ndugu zao walionewa na watu fulani hivyo kila ambaye alihusika lazima alipe kwa dhambi zake. na inaonekana kwamba kila mhusika anamuua mtuhumiwa wake kwa mkono wake mwenyewe” Brian hakuwa na hizo taarifa kiundani zaidi ila alikuwa anajaribu kuunganisha matukio kutokana na taarifa ambazo alikuwa nazo hapo.
“Ooooh shiiit, maana yake wapo wengi hivyo ni watu wengi wataendelea kufa. Hii sio bahati mbaya maana yake ni mpango wa kulipa visasi” sasa alianza kupata muunganiko sahihi wa hayo matukio.
“Natakiwa kumjua kiundani zaidi huyu askari na maisha ya huyo mwanae kabla ya kuja kuwa muuaji namna hii”
“Kwa hili vazi ambalo amelivaa unatakiwa kukutana na The Future” Brian aliongea akiwa anaandika kitu kwenye karatasi.
“Ndiye nani?”
“Huyo ni jamaa mmoja ambaye anapatikana SKY PARK, anapenda sana wanawake ila ni mtu hatari mno, huyu atakupeleka kwa mzee mmoja ambaye alikuwa ni askari wa miaka hiyo hivyo anaweza kuwa na taarifa nyingi za huyu mtu na zitakuongoza moja kwa moja kupata kitu unakihitaji” walikaa jumla kwa masaa saba mpaka kuzipata hizo taarifa. Zilikuwa ni taarifa za ndani sana ambazo nazo zilikuwa zinaungwa ungwa ila zilimpa mwanga juu ya ile kesi yake.
Mpaka wakati huo alikuwa na uhakika kwamba Othman alikuwa analipa kisasi kwa waziri, je ungekuwa mwisho wa watu kuuawa na yeye na baada ya hapo angekuwa anafanya nini? Alikosa jibu sahihi. Alitamani kuyajua maisha ya kijana huyo yalikuwaje mpaka kuja kuwa hatari namna hiyo hivyo kwa maelezo ambayo alipewa na rafiki yake aliamini kwake angefanikiwa kupajua mahali kijana huyo alikulia hivyo ingekuwa rahisi kwake kuanza kuunganisha matukio ambayo kwa mwanzo wake tu ulivyokuwa hakuona mwisho mwema wa mambo hayo.
Alimshukuru sana rafiki yake na kuondoka hilo eneo, kuanzia ule mchana mpaka anatoka ulikuwa ni usiku tayari hivyo alihitaji kuonana na mwanaume aliye ambiwa kwamba angeweza kumsaidia kumwelekeza kwa mzee ambaye alikuwa na taarifa za maaskari wa zamani hiyo kwa kuangalia mavazi ambayo walikuwa nayo kwenye miili yao. Hakutaka kulala kabisa Ezra, alikuwa na njaa kubwa mno na hiyo kesi na alitaka kuitumia kesi hiyo kuweza kupata umaarufu, aliamini kesi hiyo ingempa jina kubwa na kumfanya wakubwa wamtambue vyema kama sio kumpa cheo kikubwa.
Lakini pia kuna maneno yalikuwa yanajirudia kwenye kichwa chake kutoka kwa Brian kwamba jambo hilo lilikuwa la hatari mno na huenda lingepita na maisha yao wote wawili ama mmoja. Walikuwa wameingia eneo baya lakini hakuwa tayari kabisa kuweza kuyapotezea maamuzi yake, aliamini kabisa kwamba hatua ambayo alikuwa anaifanya ilikuwa nzuri na mwelekeo wake ulikuwa wa ushindi. Tamaa ya umaarufu ikawa inakitafuna kichwa chake kiasi kwamba akawa hawezi kusikia kuhusu jambo lolote lingine tena.
SKY PARK LOUNGE.
Ilikuwa ni Lounge maarufu ya kisasa ambayo ilikuwa ikipatikana mjini, umaarufu wake ulizingatiwa zaidi na aina ya huduma ambazo zilikuwa zinapatikana ndani ya eneo hilo ikawa sababu kubwa ya umashuhuri wake. Walikuwa wanajazana watu wengi ambao walikuwa na ukwasi wa kutosha, kwa wanyonge haikuwa sehemu sahihi kwao kwa sababu vitu vilikuwa vinapatikana kwa bei ghali mno.
Ughali wake ukafanya sehemu hiyo kupokea wageni wengi hususani wachina ambao mara nyingi huwa wanapendelea kuwepo maeneo kama hayo kwa ajili ya kufanya starehe na kupumzisha miili yao. Hilo ndilo eneo ambalo Ezra Ethana (Double E) alielekezwa kwenda kumtafuta The Future.
Alifika ndani ya hilo eneo muda ukiwa umeenda kidogo lakini kwa sehemu kama hiyo ndiyo kwanza kulikuwa kunakucha, watu walikuwa wakimwaga radhi, pesa ilikuwa inaongea. Walijaa wanawake warembo wa kila aina, kila taifa ambalo ungelihitaji basi ni wewe tu na ukubwa wa mfuko wako ndiyo ilikuwa tiba ya kwenda kukonga mioyo na wanawake waliokuwa wanavutia kama yale maua ya uwaridi mbele ya macho ya mtu aliyezama hubani.
Ezra hakutaka kabisa kuipoteza nafasi yake ya dhahabu hiyo eneo hilo, alifika kwenye kiti kimoja safi akaketi na kuagiza champagne. Mdada ambaye alimletea alianza kumzoea zoea sana mwanaume akakubali kuwa naye kwa wakati huo, mwanamke huyo hakuwa tu anashoboka bali alikuwa anajieleza, alikuwa moja ya wanawake maridhawa ambao Ezra aliwahi kuwaona kwenye maisha yake.
“Unaitwa nani?”
“Rola”
“Nina bahati ya kuweza kuliona tunda bora kama wewe mbele yangu”
“Bila shaka usiku wa leo utakuwa mwanaume mwenye bahati kuweza kupanda juu ya kiuno changu”
66 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.
Kazi kazini.... Respect mkuuSTORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA SITINI NA SABA
SONGA NAYO................
“Natamani iwe hivyo, lakini nahitaji baadhi ya taarifa ambazo naweza kuzinunua kwako bei sawa na ambayo ningekuvua nguo”
“Huwa sifanyii mazungumzo eneo kama hili” Ezra alielewa kwamba mwanamke huyo kugoma kufanyia mazungumzo eneo hilo alikuwa anahitaji ni eneo ambalo limetulia ili waweze kufanya biashara, kama wangeondoka hapo maana yake pesa yake ingekuwa kubwa. Alilielewa hilo hivyo hakuhangaika naye kabisa, akakubali.
Bidada alimshika mkono na chupa yao akawa anamvutia bwana huyo kwenye chumba cha pembeni ambacho kilikuwa kimejitenga mbali na vyumba vingine. Ile kugusana gusana kulizalisha hali ya tofauti kwa Ezra, mwanamke yule alikuwa na joto kali mno kwenye mwili wake kiasi kwamba mnara wake ukaanza kusoma kwa kasi kubwa mpaka akashindwa kujizuia.
Alishtuka baada ya kufika juu ya kilele cha mlima ndipo akakurupuka baada ya kugundua kwamba sicho ambacho kilimpeleka ndani ya eneo hilo.
“Ni shilingi ngapi mrembo?”
“Nahitaji laki mbili”
“Mhhhhh kwa dakika tano tu hizi? Nakupatia laki moja na nusu ila naweza kukupatia laki tano kama utaniuzia taarifa”
“Zipi?”
“Namhitaji The Future”
“Ni hilo tu?”
“Ndiyo”
“Nipe pesa nikupeleke alipo” ilikuwa biashara ya muda mfupi, Ezra alifurahia baada ya kuona mambo yake yanamuendea kama anavyo hitaji yeye.
Baada ya dakika kumi alikuwa amekaa kwenye kiti kimoja sehemu ambayo mwanga ulikuwa hafifu akimwangalia mwanaume mmoja ambaye alikuwa amejisahau kwa kujirusha na mtoto wa kike kwenye kochi. Bwana huyo baada ya kama dakika thelathini alinyanyuka akaacha pesa na kuanza kutoka hilo eneo, Ezra alihisi huenda mtu huyo alikuwa anaondoka hivyo akawa naye sambamba akimfuata nyuma kujua hatima yake ilikuwa ni ipi.
Mwanaume huyo alitoka kabisa mpaka nje sehemu ambayo ilikuwa inatumika kama parking, eneo hilo lilikuwa limetulia, hapakuwa na mtu yeyote kama ilivyokuwa ndani. Aliona lilikuwa eneo zuri la kuweza kukutana naye, alimkimbilia mwanaume huyo ambaye alikuwa amepanda kwenye pikipiki lake kubwa, aliona mtu anakuja upande wake akashuka kwa sababu ilikuwa ni ghafla. Hakuuliza maswali kwa namna mtu huyo alivyo mjia, Ethan alipishana na kisu ambacho kilikita kwenye nguzo iliyokuwa pembeni kidogo na sehemu ambayo alikuwa amefika.
Alitamani kujitambulisha ila muda haukuwa unatosha kwa sababu mtu wake alikuwa amefika tayari, aliikwepa ngumi iliyokuwa inakuja usoni. Aliinama, alitaka kuuinua uso wake aligundua kwamba nyakati hazikuwa rafiki kwake, akiwa anaendelea kujitafakari zaidi ndipo alikutanishwa na ngumi ya uso ilikuwa kama imemzindua kutoka usingizini. Ezra hakuwa mgeni wa hiyo michezo na alitarajia kabisa kwamba jambo kama hilo lingeweza kumtokea hivyo haikumpa presha kubwa, alisogea kwa mahesabu makali mpaka alipokuwepo The Future akiwa anamhesabia.
Alitishia na mguu wake mwanaume yule akayumba kidogo, ilimpa nafasi kupitisha mguu wake ambao ulizama kwenye mbavu za yule bwana, akarudi nyuma kidogo. Ezra hakumpa nafasi ya kutulia, alimkimbilia na kujigeuza kwa miguu yake yote miwili ambayo iliishia kwenye mikono, aliuzamisha mmoja mpaka kifuani kabisa kwa mwanaume yule, naye hakuwa kinyonge, aliunyoosha mkono wake ambao ulitua kwenye mwili wa Ezra akayumba mpaka nyuma.
The Future alichomoa kisu kingine na kuhitaji kumrushia mwanaume huyo kwa mara nyingine tena lakini wakati huo Ezra alikuwa ameitoa bastola yake na kumnyooshea huyo bwana hivyo kisu hakikufua dafu kabisa mbele yake.
“Wewe ni nani?”
“Ni ofisa wa polisi”
“Mbona unanivamia kama jambazi ambaye ninatafutwa kwa kesi ya mauaji! Kuna nini ofisa?”
“Niligundua kwamba huwezi kunisikiliza ndiyo maana nikatumia hii njia” aliongea akiwa anaonyesha kitambulisho chake, jambo hilo lilimpa amani kidogo bwana huyo akashusha kisu chake.
“Kipi unakihitaji kwa mtu kama mimi?”
“Nimeagizwa kwako na Brian”
“Ndo wewe unaitwa Double E?”
“Bila shaka”
“Amenitumia taarifa zako na aina ya msaada wa kukupa ila naweza kukushauri kwanza?”
“Milango iko wazi”
“Kwenye hili jambo ambalo unataka kulifuatilia, ni kitu gani haswa ambacho unafaidika nacho kikubwa?”
“Haki”
“Ni haki tu basi ndiyo inakuingiza huku? Nakuona wewe bado ni kijana ambaye una nafasi ya maisha mengine zaidi ya haya”
“Unamaanisha kwamba haki kwako sio kitu cha msingi?”
“Usikimbilie kutonielewa, taarifa ambazo unaonekana unazitafuta ni hatari sana kwa upande wako kwa sababu zinaweza kwenda na maisha yako”
“Umejuaje kama ni hatari na hujui ni kitu kipi naenda kukifanya?”
“Nina uzoefu mkubwa kwenye hii dunia bwana mkubwa, zoezi lolote ambalo huwa linawahusisha wanasiasa basi damu huwa haikwepeki. Haitakuwa mara ya kwanza kwako wala haitakuwa mara ya mwisho kukutwa na matatizo pale ambapo unajivika ugwiji wa kuingilia habari za hawa wapuuzi. Naichukia sana siasa”
“Nashukuru kwa kujali kwako ila niamini mimi najua ninacho kifanya hivyo nitashukuru kama utanipa taarifa”
“Anitwa mzee Miraji, mara nyingi huwa anakuwepo kwenye jumba la sinema majira ya usiku. Anapenda kukaa pale mwenyewe baada ya kumpoteza mtoto wake wa pekee, alikuwa akipenda kwenda naye kwenye jumba hilo la sinema hivyo huwa anaenda pale ili kuweza kulinda kumbukumbu zake na mwanae”
“Natakiwa kwenda saivi?”
“Hapana, muda umekwenda sana, jitahidi uende kesho usiku”
“Asante kwa taarifa, nitaukumbuka msaada wako”
“Kama hautaingia kwenye mchanga litakuwa jambo bora zaidi kwako” mwanaume huyo aliongea akiwa anakifuata kisu kingine kisha akapanda kwenye pikipiki yake ili aweze kuondoka.
“Nina imani tutaonana kwa wakati mwingine”
“Jitahidi usimuingize Brian kwenye haya matatizo kwa sababu mpaka sasa umenunua nusu kesi na yeye yupo kwenye hii kesi”
“Usijali hakuna kitu kitamkuta Brina, nitamlinda kama italazimu kufanya hivyo”
“Wewe mwenyewe huna huo uwezo wa kujilinda halafu unaweka ahadi ya kuwalinda watu wengine? Nikutakie kazi njema” alimaliza na kuondoka The Future, jukumu lake lilikuwa dogo tu eneo hilo kumwelekeza kwa mzee ambaye alidaiwa kuwepo ndani ya jeshi la polisi miaka hiyo, mzee huyo alifanya kazi kwenye maeneo mengi hivyo alikuwa akiwajua watu wengi na mambo mengi, huyo huenda angempa muunganiko mzuri a kesi ya Othman na baba yake dhidi ya mauaji ya waziri wa mambo ya ndani na mambo ambayo yalitokea nyuma hususani ile kesi ambayo iliishia kwa waziri wa mambo ya ndani kudaiwa kumuua baba yake.
67 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.
WameyatimbaaaaSTORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA SABINI
SONGA NAYO................
Aliona kuna kitu kinakuja kwake kwa kasi na nguvu kubwa, hakuelewa kilirushwa muda gani ila jambo ambalo alilielewa ni kwamba alitakiwa kuwa makini kuweza kuendana na spidi kubwa ya kifaa hicho. Ilikuwa ni ile spana ambayo ilitua pembeni ya alipokuwa baada ya kufanikiwa kuikwepa, kama ingempata ingempatia kovu kubwa huenda la maisha.
Alifanikiwa kuikwepa lakini hakuwa salama kwa sababu alihisi kivuli kinakuja kwa kasi kubwa pale ambapo yeye alikuwepo, alihitaji kukikwepa ila yeye alionekana kuwa mzito ndani ya lile eneo, alipokea maumivu kwenye ubavu wake wa kushoto mahali ambapo buti zito la Othman lilitua. Alihema kwa maumivu makali lakini hakuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya kuweza kujishauri mara mbili, mwanaume alikutanishwa na mkono uliokomaa vyema ngumi ilitua kwenye kifua chake kiasi kwamba alihisi kuna nondo ilizama eneo hilo.
Alijihisi kutema mate lakini wakati anayatema hayakuwa mate ya kawaida bali alitema damu, hali yake ilionekana kabisa kuanza kuwa mbaya. Aliyumba na kuupanga mkono wake kwa sababu bado Othman alionekana kumjia wakati huo, alinesa kidogo Ezra na kuruka sarakasi ya mbele lakini haikuwa afadhali kwake, alitwishwa teke zito ambalo lilimbeba mpaka kwenye sakafu ya ile lami, alihisi kuna kitu kinakuja hivyo akalazimika kujigeuza kuelekea mtaroni ila alinasa kwenye kuta za mtaro.
Ule mguu ambao ulikuwa unashuka pale alipokuwepo uliishia kutua kwenye lami mpaka ulichimbua hilo eneo, watu walikuwa wanapita kwenye magari hakakuwa na muda nao kabisa, jiji lina njaa kali kila mtu alikuwa akijali biashara zake nani anafuatilia hayo mambo? Hakuna, japo ilionekana kuwa burudani kwa watazamaji na kuna watu kadhaa ambao walikuwa kwa miguu ndio ambao walionekana kuvutiwa na tukio hilo kiasi kwamba wakawa wanachukia video na kushangilia.
Ezra alijirusha mpaka barabarani, hakuelewa Othman alimfikia wakati gani, alikutana na kisigino cha uso, aliburuzwa na kuchubuka, alipigwa na mguu kwenye tumbo lake mithili ya mtu aliyekuwa anakutana na ule mpira aina ya Volley kwa ajili ya kuipatia timu yake goli ya ushindi, bwana huyo alitapika damu akiwa anaunguruma pale alipokuwepo. Othman alimsogelea kijana yule aliyekuwa na njaa ya mafanikio makubwa na kusikitika
“Una sababu ya msingi ya kunifanya nisikuue?”
“Othman nahitaji kumzuia Gavin anacho kifanya ni hatari kwa taifa letu, nakuomba unisaidie kwa hili. Anaweza kubeba kila kitu akaondoka nchini, hiki mnacho kifanya kinaenda kuwa hatari kwa watu wengi kwa sababu kinaua kabisa amani na kufanya tuingie kwenye hatua mbaya kama taifa”
“Kama ungekuwa na nafasi mbili za kuishi basi hilo jina hautakiwi kuja kulitaja tena” Othman wakati anaongea alikuwa ametoa kifaa kidogo ambacho kilikuwa kama kisu, alitaka kukizamisha kwenye shingo ya kijana huyo lakini aliona kitu kwenye hicho kisu, alikuwa ni mtu ambaye alishika bastola umbali kadhaa kutoka hapo akiwa anakuja kule ambako alikuwepo, mwanga wa jua ndio ambao ulimsaidia kuweza kuliona hilo hivyo alinyanyuka kwa sarakasi za hatari na za haraka mno wakati huo risasi zilianza kurindima na kuwafanya wale ambao walikuwa umbali kadhaa kwenye barabara kuanza kupiga mayowe kila mtu akishika njia yake.
Ezra alikuwa kwenye hali mbaya lakini aliona namna Othman alivyo ondoka eneo lile, aliogopa mno, mwanadamu kuwa vile ni jambo la hatari na hakufanikiwa kuingiza ngumi hata moja kwenye mwili wake halafu ndo yeye alikuwa anataka kukutana na Gavin? Hata yeye hakujiona kama yupo siriasi na jambo hilo. Lakini jambo ambalo lilikaa kwenye kichwa ni juu ya nani ambaye alifika na kumfanya mwanaume huyo kughaili zoezi la kuweza kumuua? Hakuwa na jibu la haraka kwa sababu bado alikuwa amegeuka kumuangalia Othman na alipokuwa ameishia. Kuna gari binafsi ya mtu ilipita ikiwa kwenye mwendo mkali, mwanaume huyo aliipigia hesabu na kudunda kwenye lami kisha akaja kunasa mpaka juu ya ile gari kama hakuna ambacho kilitokea ndani ya eneo lile akapotea nalo.
Ezra aligeuka tena kujua mtu ambaye allimpatia msaada wakati huo ndipo akapigwa na butwaa, alikuwa ni yule The Future, bwana huyo alikuwa na bastola kwenye mkono wake akiwa anakimbilia alipokuwepo Ezra. Hali yake ilikuwa mbaya akiwa hawezi kufanya jambo lolote hata kunyanyuka.
“Umejuaje kama nipo eneo hili?”
“Brian ameidukua simu yako kwa sababu alijua utafanya jambo la kipuuzi akaomba nikufuatilie. Wasiwasi wake umekulipa kwa sababu bila yeye mpaka wakati huu ungekuwa upo akhera huko kuweza kulipa dhambi zako ambazo umezifanya ukiwa hai maana kwa unavyo onekana hakuna nafasi kabisa ya wewe kuweza kuiona pepo”
“Shukrani sana ndugu yangu kwa kuweza kunisaidai kwa sababu nilikuwa najiona kabisa sina nafasi ya kuweza kuishi tena”
“Unaingiaje kwenye mikono ya watu hatari namna ile? Nimeshuhudia jinsi anavyo kupiga mpaka nikabaki nashangaa na kusikitika baada ya kuona Tanzania tuna watu hatari namna ile. Yule ni muuaji Ezra, ni nani yule?”
“Sio muda wa kuongelea haya mambo kwa sababu anaweza kurudi tena akatuua wote, kwa namna nilivyo muona watu kama mimi tunatakiwa tuwe angalau kumi ndipo tunaweza kuwa sawa naye” Ezra alikuwa kama amekata tamaa kabisa ya alichokuwa anakifanya, The Future alimbeba na kumpeleka kwenye gari yake ili kuweza kumuwahisha kupata matibabu, hali yake haikuwa ikiridhisha kabisa.
******
Nick alikuwa kwenye hali mbaya, alipigika vibaya na kitu chenye ncha kali kilizama mwilini mwake na kuutoboa toboa, afya yake kwa ujumla haikuwa ya uhakika. Licha ya kuwa kwenye hali kama hiyo lakini alijikongoja na kuhakikisha anafika kwa kiongozi wake, kiongozi wake alikuwa ni Bashir, kijana wa kutegemewa kabisa na mkuu wa majeshi.
Alifika akiwa amepoteza damu nyingi, mdomo wake ulikuwa unatema damu muda wote badala ya mate kiasi kwamba alimshtua mpaka mtaalamu huyo. Hakuelewa kijana huyo alikutwa na kitu gani huko ambako alikuwa ila bila shaka hapakuwa pema kabisa ndiyo maana alikuwa hivyo.
“Walijua kama tutakuwa pale, walijua” aliongea kwa shida akiwa anakalishwa kwenye kochi ili aweze kutoa maelezo kamili juu ya kila kilichokuwa kimetokea kule.
“Akina nani?”
“Siwajui”
“Tulia kisha uniambie ulicho kutana nacho huko ambako ulikuwa”
“Sijajua ni nani alikuwa pale ila inaonekana ni mtu ambaye alikuwa anakuja ile sehemu kwa ajili ya kumuokoa Sarah na familia yake, nikiwa nataka kumuua ndipo aliingia na kuua wenzangu wote, ni mimi pekee ambaye nimefanikiwa kutoka nikiwa mzima ndani ya ile sehemu”
“Unamaanisha kwamba Sarah hujamuua?”
“Ndiyo”
“JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala Nick, unajua kosa ambalo umelifanya hapa kuendelea kumuacha hai?”
“Sikuwa na namna, mtu ambaye amekuja lile eneo ana uwezo mkubwa kuliko sisi, hakuna hata mmoja wetu ambaye angeweza kupambana naye. Sarah alikuwa kwenye hali mbaya tayari, ilibakia mimi kumalizia kazi tu ila ikashindikana kwa sababu hiyo”
“Ni nani huyo mtu” mwanaume huyo aliuliza akiwa mwingi wa jazba na hasira ambayo ilijionyesha wazi wazi.
“Simjui”
“Humjui mtu ambaye amekuvamia na unadai kaua wenzako?”
“Ndiyo, kwa sababu alijifunika kitambaa usoni”
“Unajua maana ya kuwakimbia wenzako ukiwa vitani?”
“Naelewa lakini mimi nimekuja ili kutoa hii taarifa, na sina imani na usalama wa mheshimiwa hivyo mkuu wa majeshi anatakiwa kulindwa sana kwa sasa”
“Whaaaaat?”
70 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.
Karibu sanaBado tupate action ya kijana Othman apo then tuje kwa Gavin Luca anyway simulizi nzuri
Mpaka unamaliza hii simulizi utamsoma kwa kumuonja sana ✍️Kumbe lionela ameshaolewa na hamsemi, ni wapi hii ilitumwa sijaiona?
Sawa ngoja niingoje ☺️Mpaka unamaliza hii simulizi utamsoma kwa kumuonja sana ✍️
Japo kuna watu wamemsoma sana huyo mwanamke na wanajua ni kiumbe cha namna gani kwenye THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA
GAVIN LUCA Mwenyewe alisema huyo atakuwa binadamu hatari kuliko yeye. LIONELA.
mkuu umeniacha kidogo huyo LIONELA ni mke au mtoto wa Gavin Luka.?Mpaka unamaliza hii simulizi utamsoma kwa kumuonja sana ✍️
Japo kuna watu wamemsoma sana huyo mwanamke na wanajua ni kiumbe cha namna gani kwenye THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA
GAVIN LUCA Mwenyewe alisema huyo atakuwa binadamu hatari kuliko yeye. LIONELA.
🔥Sawa ngoja niingoje ☺️
1. IDAIWE MAITI YANGUmkuu umeniacha kidogo huyo LIONELA ni mke au mtoto wa Gavin Luka.?
Huwa sio mtu ambaye napenda sana dharau au matusi....Kaka vipi mbona unaanza upimbi kaka??
Achana nae huyo kiongoz keshavulugwa na lyfe lake [emoji1363][emoji1363]Huwa sio mtu ambaye napenda sana dharau au matusi....
So ukiona naleta upimbi upotezee Uzi huu, tafuta wale ambao wanakufurahisha mkuu.
Fanya maisha yawe rahisi.
FEBIANI BABUYA kuna watu maisha Yao yamejaa stress tupu Kila kitu kwao wanaona kero. Achana nae huyo apambane na Hali yakeHuwa sio mtu ambaye napenda sana dharau au matusi....
So ukiona naleta upimbi upotezee Uzi huu, tafuta wale ambao wanakufurahisha mkuu.
Fanya maisha yawe rahisi.
Respect kiongozi, tunakutana baadae kidogo hapa ✍️Achana nae huyo kiongoz keshavulugwa na lyfe lake [emoji1363][emoji1363]
Respect sana mkuu 👊FEBIANI BABUYA kuna watu maisha Yao yamejaa stress tupu Kila kitu kwao wanaona kero. Achana nae huyo apambane na Hali yake