Simulizi ya kipelelezi: Idaiwe maiti yangu

Simulizi ya kipelelezi: Idaiwe maiti yangu

Jaribu kuwa muungwana siku nyingine
Wabongo bana unaleta uchawa adi kwenye story? Febian umeona wap amekerekwa na hoja yangu?mbaya zaid ilo ni ombi langu kwa mtunzi ana haki ya kuongeza au kuuchuna kama alivyofanya apo kistaarabu tu sasa ww kite cha warimu sijui haki ya kuniona sio muungwana ni amekutuma au shobo mkuu ndugu angu
 
Wabongo bana unaleta uchawa adi kwenye story? Febian umeona wap amekerekwa na hoja yangu?mbaya zaid ilo ni ombi langu kwa mtunzi ana haki ya kuongeza au kuuchuna kama alivyofanya apo kistaarabu tu sasa ww kite cha warimu sijui haki ya kuniona sio muungwana ni amekutuma au shobo mkuu ndugu angu
Mimi sio mbongo....tatizo ni kwamba watoto muliosoma shule za kata akili zenu ni fupi mno mithili ya akili za kuku,,Hakika wewe ni mtu wa hovyo mno angalia namna ulivyoandika kwanza...kila siku huwa nasema ilibidi kabla mtu hajajiunga jamii forum apimwe uelewa wake kwasababu hadhi ya jamii forum inashuka siku hadi siku
 
Mimi sio mbongo....tatizo ni kwamba watoto muliosoma shule za kata akili zenu ni fupi mno mithili ya akili za kuku,,Hakika wewe ni mtu wa hovyo mno angalia namna ulivyoandika kwanza...kila siku huwa nasema ilibidi kabla mtu hajajiunga jamii forum apimwe uelewa wake kwasababu hadhi ya jamii forum inashuka siku hadi siku
Hahaha machawa bana Ivi na akili zako za maiti unategemea ueleweke, nlkupiga spana ndogo tu ili uache shobo nashanga umepanic,najua hauezi fikiria zaid ya apo na yote uliyoandika umekaririshwa kwenye topic za uchawa, ebu tafadhali tusichafue uzi wa mkali fanya yameisha mshindi we mkunduangu au sio
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA TANO
SONGA NAYO................
Saa kumi na dakika tano usiku msafara ya kiongozi mkuu wa usalama nchini ulikuwa umeingia Moshi karibu kabisa na yalipokuwa makazi ya Sarah Martin. Walishuka walinzi kuangalia mazingira na baada ya dakika chache ndipo mheshimiwa mwenyewe aliruhusiwa kuweza kushuka ili kukutana na mwanamke huyo. Sauti ya helikopita hiyo ikiwa inashuka ndani ya uzio mrefu ambamo ilikuwepo nyumba hiyo ndiyo ambayo ilimshtua Sarah pamoja na mama yake.
Wakati inatua aliiona vizuri na alikuwa anazijua aina za helikopita hizo kwamba zilikuwa zinatumiwa na watu gani, jambo hilo lilimuongezea hofu kubwa kwani aliamini kwamba kile ambacho kilitokea kwenye ule msitu huenda kingemuwinda na kumfanya asiwe salama kwenye maisha yake yote ambayo yalikuwa yamebakia. Alimtoa mama yake hofu na kumhakikishia kwamba watu hao walikuwa ni wa kazini na kuja hapo lazima kulikuwa na jambo la mhimu hivyo alihitaji kwenda kuwasikiliza. Alitoka nje kwa tahadhari ambapo aliona mwanaume huyo mtu mzima akiwa amesimama nyuma ya watu wake ambao walimtaka yeye asimame kwanza, walimkagua kwenye mwili wake ndipo walimpisha kiongozi wao ambaye moja kwa moja aliongoza sehemu ambayo ilikuwa na bembea za kukalia ili wafanye maongezi.
Sarah kwenye maisha yake yote hakuwahi hata siku moja kukutana na mtu huyo zaidi ya kuishia kumuona kwenye picha tu siku ambayo mheshimiwa raisi alimteua kuwa mkurugenzi kwenye kitengo hicho nyeti. Baada ya hapo hakuwahi kusikia lolote kuhusu mtu huyo wala historia yake ya maisha haikuwa ikifahamika sana na hilo alitambua kwamba lilifichwa kwa sababu za kiusalama hivyo alianza kuogopa kwa kutembelewa na mtu mzito namna hiyo kwenye taifa, mkurugenzi asingejisumbua kwenda sehemu kama kusingekuwa na shida kubwa au uhitaji wa taarifa za mhimu na za haraka.
"Bila shaka utakuwa haunifahamu bibie na pole kwa kukuvamia na usiku wote huu ambao unatakiwa kupumzika lakini wote tunaelewa kwamba maisha yetu sisi taifa linakuja mbele kwanza kabla ya kila kitu hivyo pia sitakiwi kukuomba msamaha kwenye hilo kwani ni jukumu lako pia kuipigania nchi yako kwa namna yoyote ile"
"Ndiyo mheshimiwa, nimefurahi kupata bahati ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na wewe na natumai kuna jambo la mhimu ambalo naweza kusaidia" mheshimiwa alikuwa amemkazia macho mwanamke huyo kupitia taa za mwanga ambazo zilifanya eneo hilo kuwa jeupe huku walinzi wake wakizunguka kila upande kuhakiki ulinzi hususani baadhi ya maeneo ambayo yalionekana kuzungukwa na migomba mingi.
"Upo sahihi, mpaka nafika hapa basi unajua ambacho kimenileta ila wakubwa zako ndio hawajui kama nipo hapa. Usiku huu nimepokea simu moja kwa moja kutoka kwa mkurugenzi wa NIS Kenya ndiyo maana nipo hapa, nadhani unajua kile ambacho kimetokea ndani ya msitu wa Mau na jambo hilo linaenda kutuchafulia jina kwa kiasi kikubwa kwa sababu limefanyika jambo bila ruhusa ya wenye mamlaka kule hivyo kuna gharama ambazo kiusalama kama taifa lazima tuingie lakini hilo linaweza kuisha endapo utanijibu maswali yangu matatu tu Sarah" hakushangaa kiongozi huyo kuwa na jina lake kwenye kinywa chake ila kilicho muogopesha ni hayo maswali matatu.
"Swali la kwanza ni nani aliua wale watu, swali la pili nipe sababu ya msingi ya kwenda kumuulia yule mtu kwenye ule msitu, na swali la tatu ni kwanini wauawe watu wote kisha wewe uachwe hai?" ni maswali yaleyale ambayo alihisi kwamba ndiyo ambayo yanaweza kuja. Sarah hakusita kumpa mheshimiwa ile stori yake ya kusadikika ambayo aliirekebisha baada ya kushauriwa na Nick lakini bwana Micho aliishia kucheka kwa sababu alijua kabisa binti huyo anamdanganya.
"Binti kitu ambacho tunakizungumzia hapa ni usalama wa taifa kwa ujumla na mamilioni ya watu wake, nipo kwenye kazi za usalama kwa miaka zaidi ya thelathini sasa hivyo usinione mimi kama hao wanajeshi wenzako ambao unaweza kuwauzia stori za kitoto hizo. Nina mamlaka ya kuondoka na wewe muda huu ukawa mshtakiwa namba moja na habari zikafika kwa wakubwa zako na unajua kabisa nikiamua kukuchunguza ni masaa matano tu yatatosha mimi kujua kila kilicho tokea kule au tunaweza kuyamaliza hapa kwa wewe kuniambia ukweli na kunijibu hayo maswali yangu" Sarah alibaki ameganda njiapanda kwani mzee hakuonyesha urafiki licha ya kucheka, alionekana hakuwa mtu wa kupenda kupotezewa muda wake kabisa.
"Kwakweli sababu za msingi za mimi kuachwa hai mpaka sasa sizijui, alikuwa na nafasi ya kuweza kuondoka na maisha yangu lakini akaamua kuniacha tena kwa kunipa onyo kubwa. Sababu ya kumuulia yule mtu kule ni kwa sababu ndiko ambako alikuwa anaishi kwa siri kwenye nyumba moja ambayo ilionekana kutelekezwa eneo lile kwa muda mrefu bila kujulikana sababu ya msingi ya nyumba ile kujengwa lile eneo. Kuhusu mtu ambaye ameua wale wenzangu wote kule simjui na kama ningekuwa namjua kiundani basi nisingekwambia mheshimiwa, nisamehe sana kwa kusema hivi kwa sababu mtu huyu anaijua vizuri mpaka familia yangu hivyo kufungua kwangu mdomo ingemaanisha ni mwisho wa familia yangu yote" alimsikiliza mwanamke huyo kwa umakini mkubwa akiwa anaongea na kuyapima maneno yake kwa kumkazia macho.
"Ni nani ambaye mlienda kumuua kule?" lilikuwa swali lingine gumu lakini hilo alipaswa kulijibu.
"Gavin Luka"
"Gavin Luka ni nani?" ilionekana kabisa kwamba ilikuwa mara ya kwanza kabisa mheshimiwa kulisikia hilo jina kwenye maisha yake yote.
"Kiukweli mimi nilitajiwa tu jina, sikuwahi kumjua huyo mtu kabla mtu ambaye alikuwa na taarifa zote za mtu huyu alikuwa ni kiongozi wa msafara wetu Michael ila kwa bahati mbaya amekufa pale pale.
"Umeiona sura ya mtu huyo" Mr Micho aliuliza tena akiwa amemkazia macho Sarah akicheza na mboni za macho yake kuona kama zinamdanganya au zinasema ukweli. Sarah alimeza mate kwa shida akiwa kwenye mstari mgumu wa kufanya maamuzi, maneno ya mwanaume yule yalikuwa yanajirudia kwenye kichwa chake, akakumbuka mpaka namna mtu huyo alivyofika hapo kwake na kuacha barua pamoja na pesa nafsi ilimwambia huenda bado mtu huyo anamfuatilia kila hatua ambayo alikuwa anaipiga hivyo alipaswa kuwa makini isivyokuwa kawaida.
"Hapana, alikuwa amevaa kitambaa usoni sikufanikiwa kumuona kwa sababu hata nilipotaka kumhoji kutaka kumfahamu alinipiga mpaka nikazimia na wakati nazinduka hapakuwa na mtu zaidi ya maiti za wenzangu zikiwa zimezagaa na ile nyumba ikiwa imechomwa tayari" mkurugenzi alitabasamu, macho ya Sarah ni wazi yalikuwa yanadanganya lakini hakutaka kulisema jambo hilo.
"Tutakutana wakati mwingine nikikuhitaji" aliongea mkurugenzi na kusimama kisha akaanza kuzitupa hatua zake kwenda kwenye helikopter mpaka pale ambapo helikopiter hiyo ikapotea maeneo hayo. Sarah bado alikuwa haamini kuachwa kirahisi tu namna hiyo, moyo wake ulikuwa unapiga mbio isivyokuwa kawaida. Baada ya mheshimiwa huyo kuondoka, alianza kupokea simu nyingi za majirani wakitaka kujua kama kuna usalama hapo kwake kwani waliona helikopiter inaingia na baada ya muda ikatoweka. Aliwatuliza kwa kuwaambia yalikuwa na mambo ya kazini tu hakukuwa na tatizo lolote lile.

Gavin Luca huenda kweli lilikuwa jina geni kwa mkurugenzi au ni yeye tu aliamua kumdanganya mwanamke huyo. Asubuhi ya mapema kabisa wakati kumepambazuka mheshimiwa huyo alikuwa kwenye gari akielekea Bunju nyumbani kwa mkuu wa majeshi wa Tanzania Medrick Savato. Ni muda mchache alitoa taarifa ya kuweza kufika ndani ya hilo eneo ikiwa ni muda mchache tangu atoke Moshi kuonana na Sarah Martin. Alifika kwenye jumba kubwa la kiongozi huyo ambalo lilikuwa linalindwa isivyo kawaida na wanajeshi wengi, taarifa za ujio wake zilikuwa zinafahamika hivyo aliingia bila kizuizi chochote, walishuka vijana wake ambao mavazi yao meusi yaliitambulisha vyema kazi yao na kwenda kumfungulia mheshimiwa mlango huku mkuu wa majeshi akiwa amesimama na walinzi wake kumsubiri kiongozi mwenzake huyo mkubwa wa usalama nchini.
Watu hao walipeana mikono na kwenda moja kwa moja kwenye chumba maalumu ambacho kilikuwa kwa ajili ya wageni wa mhimu kufanya mazungumzo yao huku kahawa ikiletwa pale walipokuwepo.
"Haujawahi kuja kunijulia hali hapa kwangu hata siku moja Micho, leo mpaka umefika hapa basi natarajia kwamba utakuwa una jambo kubwa ambalo limekuleta"
"Upo sahihi, mimi na wewe hatujawahi kuwa na ukaribu wowote wala urafiki kwenye maisha yetu na mara nyingi ukiona tumekutana kama hivi basi ujue kabisa kwamba kuna jambo la msingi lipo nyuma ya mambo haya bila shaka unaelewa hilo"
"Ni vyema ukienda kwenye pointi ya msingi kwa sababu najua kabisa haujaja hapa ili kunijulia hali"
"Safi, nahitaji kujua ni kipi ambacho kimetokea ndani ya msitu wa Mau bila kuacha pointi hata moja kwenye maelezo yako"
"Msitu wa Kenya huo, sasa mimi nahusika nini na mambo kama hayo?"
"Tusipoteze muda kuelezea jambo ambalo limefanyika chini ya usimamizi wako, kama ulivyotaka kwenda kwenye pointi ya msingi na ndicho hicho hata wewe unatakiwa kukifanya hapa"

Sehemu ya tano inafika tamati, sehemu ya sita ndiyo inafuata, tukutane huko.

FEBIANI BABUYA
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA SITA
SONGA NAYO................
"Wewe ni nani hasa mpaka mimi nianze kukupa habari ambazo binafsi hazikuhusu?"
"Ukiona mpaka nipo hapa basi ujue zinanihusu, majigambo yako yanaweza kuhatarisha usalama wa taifa zima. Nimepigiwa simu leo na mkurugenzi wa usalaam wa taifa wa Kenya ndiyo maana unaniona kwako muda huu vinginevyo mimi na wewe tusingeonana"
"Ilikuwa ni oparesheni ya kijeshi hivyo hakuna lingine la ziada ambalo naweza kukueleza, hii ni miiko ya kazi yangu nadhani hata wewe unalijua vizuri hilo"
"Nalijua ila hiyo miiko inatolewa jambo linapokuwa la usalama wa nchi kwa ujumla"
"Wakenya wanataka nini?"
"Medrick acha kunipotezea muda wangu, Gavin Luca ni nani?" mkurugenzi aliamua kulipasua swali moja kwa moja baada ya kuona mwenzake anatafuta kichaka cha kujifichia.
"Ni mhalifu ambaye alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu hivyo kupatikana kwake alipo ikawa ni njia rahisi kuweza kumalizana naye, sioni sababu ya wewe kuhoji sana kuhusu uhalali wa ninacho kifanya, sifanyi kazi chini yako Micho"
"Hilo nalielewa vizuri ila ukienda nje na miiko ya kazi yako unatakiwa kujua kwamba mimi nahusika kwa sababu natakiwa kuwa na taarifa za raia yeyote kwenye hili taifa huoni kama taarifa zako wewe zikiwa mbaya zinaweza kupekelea ukaipoteza hata hiyo nafasi yako Medrick? Muda mwingine jaribu kuwaza kama mtu mzima, kazi za jeshi mimi hazinihusu na hata siku moja sijawahi kabisa kukuingilia ila kuhatarisha usalama wa nchi siwezi kuangalia jambo hili linatokea hivi hivi. Mimi ndiye kiongozi mkuu wa usalama, nimepigiwa simu na kuambiwa kwamba lazima Tanzania tutalipa kwa sababu Wakenya watazinyooshea mamlaka za usalaam za nchi yao kwamba ndio ambao wanahusika kuua raia wao, sasa hawawezi kukubali kubeba lawama bure bure wakati wahusika ni sisi. Kabla ya kuongea vitu kirahisi rahisi waza mara mbili matokeo ya wakati unaokuja"
"Micho upo hapa kunitisha?"
"Sijakutisha nakupa ni onyo Medrick, unajua kabisa ninaweza kukutoa kwenye kiti chako hapo kama hizi taarifa zikiwafikiwa wananchi na raisi hatataka kubeba lawama, unahisi atafanya nini zaidi ya kukurushia furushi la taka wewe kwa kukutoa kwenye hiyo nafasi ili kuwatuliza wananchi? Kama yule ni mhalifu mbona hakuna sehemu yoyote kwenye kituo cha polisi nchini ambako kuna taarifa zake? Na kama alikuwa amefanya makosa kwanini itolewe amri ya moja kwa moja kuweza kumuua badala ya kumkamata? Ambayo kiuhalisia haikuwa kazi yako, hiyo ilikuwa ni kazi ya jeshi la polisi. Kuna kitu kinanivutia kwenye hili jambo kwamba kuna mambo binafsi ndiyo yalileta huu msukumo" mkuu wa majeshi alitabasamu na kumwangalia vizuri mkurugenzi usoni kwa umakini, hao wote walikuwa vigogo lakini kwenye kete za mhimu walitofautiana kidogo.
"Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu leo natishwa kitu ambacho hata raisi wa nchi hajawahi kukifanya. Micho angalia ulimi wako kabla ya kuitoa sentensi yoyote ile mdomoni mwako kuhusu mimi, usije hapa ukahisi nakuogopa kwa sababu tu unadai unaweza kupata taarifa za mtu yeyote yule na kama unahisi hilo unaliweza basi zitafute taarifa za mtu huyo bila kuhitaji msaada kutoka kwangu. Tena usije ukarudi kwenye nyumba yangu siku nyingine kwa kuniletea upuuzi wako namna hii, kama unataka kwenda kumlilia raisi bila shaka Ikulu unapafahamu na unaruhusiwa kuingia muda wowote ule hivyo nenda muda huu kamwambie kwamba mimi nimetoa amri ya kuuawa kwa mhalifu huko Kenya natakiwa kuondolewa kwenye nafasi yangu" mkuu wa majeshi hakupendezwa na kauli za mkurugenzi, ni kama alikuwa anamdharau hivi wakati alikuwa ni miongoni mwa watu wazito mno nchini na nchi yenyewe hata kama angeamua kuichukua na kuiweka kwenye mikono yake lilikuwa ni suala la masaa ishirini na manne tu. Mafahari hao wawili walikaa na kutazamana kwa umakini mpaka pale mkurgenzi alipo simama na kumpa mkono mr Medrick ili kuweza kumuaga.
"Tutakutana wakati mwingine mr Savato" waliagana kinafiki kisha mkurugenzi akaondoka lakini kila mtu alikuwa na kinyongo na mwenzake moyoni, safari yao haikuwa njema. Baada ya mr Micho kuondoka, Jenerali Medrick Savato alipandisha mpaka chumba cha juu ya jengo lake ambacho kilikuwa kinatumika kama ofisi yake. Aliitoa simu moja kutoka kwenye droo ndogo na kuipiga mahali ambapo ilikuwa ni nje ya nchi.
"Boss" ilisikika sauti nzito iliyokuwa kavu kutoka upande wa pili.
"Kesho nahitaji uwepo Tanzania, kuna tatizo kubwa" aliongea kwa msisitizo ili mtu wa upande wa pili alichukulie jambo hilo kwa uzito zaidi.
"Nitakuwa hapo bosi" simu ilikatwa baada ya kuongea mara tatu tu. Aliizima simu yake hiyo na kuirudisha kwenye droo ndogo ambapo ilikuwepo kwa mara ya kwanza akasogea dirishani kuangalia mazingira ya nje na namna mji ulivyokuwa unaendeleza harakati zake za kila siku ili mradi tu maisha yaweze kuendelea.
"Huyu muuaji ni nani?" ndilo swali ambalo alijiuliza yeye mwenyewe kwa sauti ila huenda hata yeye hakuwa na uwezo wa kujijibu kwa wakati huo hivyo akaamua kusubiri muda uweze kumpa maelekezo sahihi zaidi juu ya jambo hilo ambalo lilikuwa linakichachafya kichwa chake.









**************
Zanzibar Magharibi
The Mora Zanzibar.
Hoteli ya kifahari ya nyota tano ipatikanayo Zanzibar Magharibi, hoteli ambayo kulala usiku wake mmoja ni zaidi ya shilingi za kitanzania milioni moja na laki mbili. Ni hoteli ambayo ipo maeneo tulivu kabisa kwenye fukwe ya bahari ya hindi, sio sehemu ambayo kila mtu anaweza kwenda lazima uwe na uhakika wa milo yako mitatu kwa siku ndipo uweze kulala ama kupata chakula ndani ya hoteli hiyo ya kifahari sana.
Tarehe 17 mwezi wa 9 saa tano na nusu asubuhi unakutwa mwili wa mwanamke humo hotelini ukiwa hauna uhai ndani ya chumba kimoja. Anaye ukuta huo mwili ni mhudumu mmoja ambaye alienda kufanya usafi kwa ajili ya matumizi ya siku mpya lakini wakati anaenda kwenye ule muda wa kutoka hotelini ambao ni saa nne anagonga bila mafanikio na kuamua kuondoka kuendelea na kazi zingine ili kutomuudhi mteja akitegemea kwamba atakaporudi basi mteja huyo atakuwa ametoka lakini inakuwa tofauti hata baada ya kurudi tena baadae, hali inakuwa ni ileile.
Anagonga sana bila mafanikio ndipo anaamua kuja na ufunguo wa dharura na kufungua kwenye chumba hicho, anacho kutana nacho ni maiti ambayo ilitobolewa vibaya na kuacha alama kadhaa ndani ya mwili huo. Jambo hilo linamtisha na kumuogopesha kiasi kwamba kila ambacho kipo kwenye mkono wake kinamponyoka huku akipiga yowe na kuomba msaada akikimbia kana kwamba hatakuja kukimbia tena kwenye maisha yake. Kelele na taarifa zinamfikia meneja wa hoteli hiyo ambaye anaamua kupiga simu haraka ili isije kuwa tatizo kubwa kwao kutokana na hilo tukio.
Simu hiyo inatua mpaka kwenye kituo cha polisi cha Kijito Upele Police Station, simu hiyo inakutana na afisa wa polisi Rama Rajabu ambaye anawahi huko na vijana wake. Hali ambayo wanakutana nayo huko inawaogopesha hata wao kwa sababu ni muda mrefu tangu Zanzibar iweze kushuhudia tukio la namna hiyo ambalo kiusalama ni hatari na ndipo chumba hicho kinageuzwa kuwa CRIME SCENE, mwanamke huyo ambaye alikuwa anatakiwa kufanya usafi anaanza kuhojiwa kuhusu tukio zima lilivyokuwa mpaka yeye kuukuta mwili huo na hatua ambazo alizifuata. Maelezo ambayo afisa wa polisi huyo anayapata ndiyo ambayo yanamfungulia njia ya yeye kuweza kuufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ambalo linawashtua hata wao.
Zara Ismail, ndilo lilikuwa jina la mwanamke ambaye alikutwa amefariki ndani ya chumba cha hoteli. Mwanamke huyo baada ya kugundulika kwamba amefariki ndipo taarifa zake zilipo tafutwa kuhusu maisha yake na utambulisho wake kwa ujumla. Zara alikuwa ni mchunguzi wa kujitegeme ambapo alisomea uandishi wa habari, uchunguzi wake kwenye mambo mbalimbali ulimfanya kukutana na vitu vingi sana kwenye hiyo safari yake ya ukusanyaji wa taarifa lakini licha ya kukutana na hayo mambo bado hakuwahi hata siku moja kuweza kukata tamaa. Mwanamke huyo alikuwa ni mzaliwa wa familia ta tajiri mkubwa bwana Ismail Mhammed ambaye alikuwa anafahamika karibia kila sehemu ya huko Zanzibar kutokana na ukwasi ambao alikuwa nao.
Zara hakuwahi kuonekana kwa miaka miwili, ilipita miaka miwili bila uwepo wake ambapo alitoweka kwenye mazingira ya kutatanisha akiwa anaendelea na masomo yake ya sayansi ya komputa. Familia na ndugu walimtafuta kila sehemu na habari hiyo hata kwenye vituo vyote vya polisi ilikuwepo lakini baada ya wiki alituma barua kwa njia ya simu akidai kwamba alikuwaa ameondoka nchini na kwenda kupumzika nje ya nchi hivyo familia haikutakiwa kumtafuta ni yeye aliamua kwenda kutuliza akili yake na baada ya muda angefanikiwa kurudi mwenyewe, alidai asitafutwe kwa namna yoyote ile kwa sababu asingepatikana popote pale mpaka siku ambayo angeamua kurudi mwenyewe.
Hilo lilitokana na yeye kupishana na baba yake mzazi ambaye alikuwa anataka mwanamke huyo aolewe ili amfungulie biashara zake za kusimamia lakini mwanamke huyo aligoma kabisa na kudai kwamba yeye alikuwa akiipenda kazi yake hiyo zaidi ya kitu chochote na hakuwa tayari kuweza kuiacha. Jambo hilo lilizua mgogoro mkubwa kati yake yeye na baba yake ambaye alimwambia kama anataka kufanya mambo yake basi aondoke kwake na asije kumuona kwenye macho yake tena. Ni kweli ndicho hicho alicho kifanya Zara kuamua kuondoka na hata baada ya kutuma barua ndugu zake hawakuahangaika tena kumtafuta kwani walijua kabisa kwamba alifanya hayo yote ili tu kumkwepa baba yake na huenda siku ambayo hasira zingeshuka basi angekuja kurudi mwenyewe nyumbani lakini hawakuwa sahihi hata kidogo.

Sehemu ya sita inafika mwisho tukutane ndani ya sehemu ya saba.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA KWANZA
ANZA NAYO................

NDOTO YANGU NDANI YA MSITU WA KUTISHA

MSITU WA MAU, KENYA.

Ndani ya msitu mmoja uliokuwa na miti mirefu iliyoshonana, katikati kabisa ya msitu huo palikuwa na nyumba ndogo ambayo ilijengwa kwa mbao iliyo onekana kabisa kwamba ilikuwa imetelekezwa kwa muda mrefu kama sio mhusika kuijenga kwa ajili ya kazi yake maalumu. Msitu ulikuwa kimya, ni sauti za ndege tu ambazo zilikuwa zikipenya ndani ya eneo hilo tulivu, hakukuwa na upepo uliokuwa unasikika kwa sababu ya maeneo mengi kushonana kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu upepo kupenya mpaka chini.

Kwenye nyumba ambayo ilitelekezwa hilo eneo kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa wamevaa nguo za jeshi. Ndani kabisa ya hiyo nyumba kulikuwa na mateka mmoja ambaye alikuwa amefungwa vyema kwa minyororo kwenye mwili wake. Mwili wake ulikuwa umechoka, alikuwa anavuja damu kwenye maeneo mengi ya mwili huku watu kadhaa ambao walikuwa kwenye yale mavazi ya jeshi wakiwa wamelazwa kwenye vitanda nje kidogo ya chumba hicho wakiendelea kuvuja damu.

Ni wachache ambao walikuwa ni wazima wa afya kabisa na wengine ndio ambao walikuwa naye ndani ya hicho chumba bwana huyo aliyekuwa amechakaa kwa kipigo ambacho alikipata. Pembezoni mwa hicho chumba alikuwepo mwanamke mmoja ambaye alikuwa mrembo kwa mwonekano wake japo haukuwa ukiridhisha kutokana na mazingira ambayo alikuwepo na kukosa mahitaji ya mhimu kuuweka mwili wake kwenye hali ya usafi zaidi. Mwanamke yule hakuonekana kupendezeshwa na kilichokuwa kinaendelea ndani ya lile eneo ila hakuwa na namna angeweza kufanya hivyo alitoka kwa hasira na ghadhabu kwenye nje kupunga upepo huku akiwaacha watu wale wafanye kile ambacho walikuwa wamedhamiria kukifanya humo ndani.

Ndani ya hicho chumba walibakia wanaume watatu, wawili walikuwa wamesimama pembezoni wakiwa wameegamia ukuta na mmoja ndiye ambaye alikuwa amesimama mbele ya bwana huyo aliyekuwa amefungwa kwenye kiti. Mwanaume ambaye alikuwa amesimama mbele yake, alivaa mavazi ya jeshi kasoro upande wa juu, kifuani kwake alikuwa amevaa vesti ya rangi nyeusi na kwenye mkono wake alikuwa ameishika sigara ambayo alikuwa anaivuta kwa mbwembwe iliyo changanyikana na gadhabu huku moshi akiwa anampulizia huyo mtu wake usoni.

Alitoa ishara kwa mwanajeshi mmoja, hakusita zaidi ya kulibeba dumu kubwa ambalo lilikuwa pembeni yake, dumu lilijaa mafuta ya petroli ambayo aliyamiminia kwenye mwili wa mwanaume ambaye alikuwa amefungwa kwenye kile kiti kwa umakini bila kumwaga mwaga hovyo chini. Alipo ona inatosha alisogea pembeni na kulipeleka lile dumu mbali ili isije kuwa hatari hata kwa upande wao pia, mwanaume yule ambaye alikuwa anaendelea kuivuta sigara yake aliinama kidogo mpaka alipokuwa ameketi bwana yule kwenye kiti.

"Wakati napewa kazi ya kukutafuta kwa namna na gharama yoyote, binafsi nilijua kwamba ingenichukua zaidi ya mwaka mzima au zaidi kukupata ukizingatia umetafutwa kwa miaka zaidi ya mitano na hukuwahi kujulikana kwamba ni wapi uliwahi kuwepo. Maajabu nimekupata ndani ya muda mfupi tu kiasi kwamba kazi imekuwa rahisi lakini kwa upande wako mambo hayawezi kuwa rahisi kwa sababu unatakiwa kufa leo kwa maumivu" mwanajeshi yule alivuta tena sigara na kuutoa moshi kwa mara nyingine kwa kejeli na majivuno.

"Hii usiichukulie personal ndugu yangu, hii ni kazi na walio nituma ndio wanahitaji iwe hivi kwahiyo kama nisipo kuua mimi ndiye nitakufa. It's over" aliongeza sentensi fupi kisha akasimama, alivuta sigara yake kwa mara nyingine na kuiachia kwenda kwenye mwili wa yule mwanaume ambaye alianza kupiga kelele baada ya moto kuwaka na kuanza kuuunguza mwili wake. Mwanajeshi yule aliitoa simu yake akapiga picha za kutosha na kuchukua video fupi kabla uso wa mwanaume yule haujaharibika kisha aliichomoa bastola kwenye kiuno chake, aliikoki kwa kuigongesha kwenye buti lake na kumimina risasi zote kwenye kichwa cha mwanaume ambaye alikuwa anawaka moto baada ya kuzidisha makelele.
Utulivu ulichukua nafasi, mwanajeshi mmoja alisogea na kuanza kuuzima ule moto ili usije ukaleta madhara kwenye hiyo nyumba kwa ujumla lakini kipindi anaendelea na zoezi hilo, walisikia mlio wa risasi eneo la mbali na hiyo nyumba. Hiyo hali haikuwa ya kawaida kwenye eneo kama lile, ni eneo ambalo hakuna mtu mwingine angeweza kufika kwa wakati huo, ni eneo ambalo hakuna binadamu alikuwa na ujasiri wa kwenda kufanya hata utalii kwa sababu lilikuwa linatisha na liliaminika kwamba lilikuwa na viumbe hatari ndani yake, sasa wakati huo hiyo risasi ilipigwa na nani? Kiongozi wao ambaye ndiye alitoka kumuua yule mateka wao alitoka humo ndani kwenda nje kujua ni kipi kilikuwa kinaendelea.

Kutokana na baridi kali ambalo lilikuwa huko, watu wengine ambao walikuwa pale nje ambao nao walikuwa kwenye mavazi ya jeshi walikuwa wakiota moto huku yule mwanamke ambaye alionekana wazi kwamba hakupendezwa na kile ambacho kilikuwa kinafanyika pale akiwa amejitenga mwenyewe na kuegamia kwenye mti mmoja ambao ulikuwa karibu na pale ambapo wenzake walikuwa wakiota moto na kuchoma nyama. Wote ambao walikuwa nje waliusikia ule mlio wa risasi hivyo kila mtu alitahayari kutaka kujua kwamba ni kipi kilikuwa kinaendelea.
Hawakukaa tena bali kila mtu alisimama wakiwa wanaangaza huku na huko lakini hawakuona kitu ndipo mmoja wao alishtuka baada ya kuona kuna mwenzao amekosekana hilo eneo.
"Jordan yuko wapi?" yule aliyeshtuka aliuliza kwa wasiwasi akiwa anamwangalia kila mmoja wao usoni ili kuhakiki kuhusu huyo ambaye alikuwa anamuulizia.

"Alisema anataka kupunga upepo nje kidogo ya hapa hivyo aliingia huko msituni" sauti ya mmoja wao ndiyo ambayo iliamsha hisia ambazo hazikuwa sawa, kiongozi wao huyo aliinyanyua simu yake kupiga kwa kutumia radio call ambayo kila mmoja wao alikuwa anatembea nayo. Simu hiyo iliita mara tatu mfululizo bila kupokelewa, jambo hilo lilitoa ishara mbaya, hapakuwa pema hivyo alimtaka mwanamke yule ambaye hakuwa kwenye mood nzuri kuangalia kwa kutumia kumpyuta yake kujua huyo mwenzao yuko wapi kwa wakati huo.
Alikimbilia ndani na kuhaki mfumo wa mawasiliano kupitia kifaa cha mwenzao, alionekana kuwa mita miambili kutoka walipokuwa wao na kifaa hicho kilionekana kusimama sehemu moja bila kujongea, hawakuwa na muda wa kusubiri, kiongozi wao aliwataka wajiandae kwenye kuangalia hali ya mwenzao kwa sababu ukimya kama huo haukuwa utaratibu kwenye kazi yao, maana yake hakukuwa na usalama kwa mwenzao na walitakiwa kumsaidia kwa haraka kama kuna shida yoyote ingekuwa imempata.

Walitembea kwa umakini kwa dakika mbili ndipo walifika ile sehemu ambayo ilionyesha kwamba kulikuwa na kifaa cha mawasiliano cha mwenzao, kifaa kilikutwa kikiwa kwenye nyasi pembeni yake kukiwa na damu ambayo ilionyesha kuendelea kuelekea mbele ikabidi waifuate. Hatua kumi kutoka hapo ndiyo sehemu ambayo waliukuta mwili wa Jordan shingo yake ikiwa na alama za kutoboka na kichwa kikiwa kimepasuka kwa nyuma. Jordan alikuwa amekufa na kichwa chake kilionekana kujibamiza kwenye mti sehemu ambayo ilikuwa na damu na nywele kiasi. Bastola yake ilikuwa pembeni ya mwili wake, aliyekufa alikuwa ni miongoni mwa watu wa kuaminika vilivyo, kifo chake tena cha ghafla namna hiyo ni ishara kwamba walikuwa wameupokea ugeni ambao hawakuutarajia kwa sababu mtu ambaye aliwaleta ndani ya hilo eneo walitoka kumuua muda sio mrefu. Sasa huyo mtu mwingine ambaye aliingilia hiyo shughuli alikuwa ni nani? Ilizaliwa hofu na maswali ambayo hata wao hawakuelewa namna ya kuweza kuyapatia majibu yake.


"Kuna mtu mwingine ndani ya huu msitu na huenda mpaka muda huu anatuona kwa kila tunacho kifanya hapa" aliongea kiongozi wao huku akiwa anainama kuufanyia uchunguzi mwili wa mwenzake. Mwili ulikuwa bado wa moto, ni ishara kwamba ni muda mfupi; ulipita tangu mtu huyo aweze kuuawa, alitoa ishara ya vijana wake kuweza kutawanyika kwa ajili ya kumsaka mgeni ambaye alikuwa ameingia ndani ya msitu bila wao kuwa na taarifa na kuanza kuwapunguza.
Yalikuwa ni majira ya jioni jua likiwa linazama hivyo chini ya msitu kulikuwa na mwanga kwa mbali ambao kadri dakika zilivyokuwa zinasonga ulikuwa unafifia taratibu. Mwanajeshi mmoja akiwa anatembea, alishangaa kuna shilingi ya zamani ambayo ilikuwa inang'aa ikitua mbele ya macho yake.

Hakuelewa ilirushwa na nani na ilitokea wapi hivyo alisogea ili kuweza kuyashuhudia hayo maajabu, akiwa ameikaribia na kuinama ili aipate mwili wake ulihisi uzito ambao haukuwa wake, akajua kabisa kwamba kulikuwa na ongezeko la mtu mwingine karibu yake. Aligeuka haraka akiwa ameinyoosha bastola yake ila hakuona kitu ikamlazimu kuyarudisha macho yake haraka kwenye ile shilingi ambayo ilikuwa nyuma yake.
Wakati anageuka alikutana na kitu cha ajabu, alifanikiwa kuyafungua macho yake mara moja tu pekee, kwa sababu ile shilingi hakuiona tena na alipo jaribu kuweza kuangalia alihisi kama kuna kivuli ndipo akayafumbua macho yake baada ya kuhisi kulikuwa na kivuli kutokea juu kwenye mti. Ni kweli kuna mwanaume alikuwa amenasa kwenye mti kwa kutumia miguu yake huku mikono ikiwa imeleelekezwa chini. Wakati anapata mshtuko, alihitaji kuielekezea bastola yake kuelekea kwa yule mtu, kwa bahati mbaya kidole kilizama kwenye koromeo lake na kulivunja, alirudi nyuma akiwa ameishika shingo yale ila hakumaliza hata sekunde tano, alikufa baada ya ile shilingi kuzamishwa kwenye paji yake la uso na kifua kilivunjwa kwa ngumi ambayo ilimgandamiza kwenye ule mti kiasi kwamba hata mifupa ya uti wake wa mgongo ikavunjika vibaya.

Ukimya wake uliokithiri ndio ambao ulimsogeza yule mwanamke ambaye alikuwa mtaalamu wa kompyuta karibu na eneo hilo, aliitoa sauti ya mshtuko huku moyo wake ukianza kwenda na kupiga kwa nguvu. Hakutarajia kukutana na kitu kama hicho kwa mara nyingine tena, ni muda mfupi walitoka kushuhudia mwili wa Jordan lakini haikuchukua muda mwingine tena mwenzao alikuwa ameuliwa kikatili kama mwanzo lakini huyo wa pili kwenye paji lake la uso iliachwa shilingi ambayo ilibaki imeshikilia hapo ikiwa inang'aa isivyokuwa kawaida.

Ile hofu yake ilimfanya aanze kurudi nyuma huku akiwa anaitoa simu yake mfukoni baada ya kugundua kwamba hata kile kifaa cha mawasiliano kwenye sikio lake hakikuwepo huenda ni kwa sababu alikisahau kule kwenye kumpyuta. Alisimama na kujibanza kwenye mti baada ya kuhisi kama kuna kitu kilikuwa kimempita kwa kasi nyuma ya alipokuwepo yeye, jambo hilo alihisi ni ndoto ila aliamini kwamba ni kweli baada ya kuiona ile simu yake ambayo alikuwa ameishika mkononi ikiwa imepasuka baada ya kubamizwa kwenye mti. Lilikuwa ni jambo la haraka kufanyika kiasi kwamba yeye mwenyewe alibaki anashangaa asijue tukio hilo lilitokeaje na kwanini aliyelifanya hakumdhuru yeye? Hakuwa na muda wa kusubiri zaidi ya kuanza kukimbia kuelekea upande ambao walikuwepo wenzao wakiwa wanaendelea kumsaka mtu ambaye bila shaka naye alikuwa anawasaka ndani ya msitu huo mzito.

Ndiyo kwanza tunaifungua sehemu ya kwanza kabisa ya simulizi hii, ungana nami mpaka mwisho ili tuweze kwenda sawa pamoja.

FEBIANI BABUYA.View attachment 3168470
Unyama saana! Tuwekee pdf
 
Wabongo bana unaleta uchawa adi kwenye story? Febian umeona wap amekerekwa na hoja yangu?mbaya zaid ilo ni ombi langu kwa mtunzi ana haki ya kuongeza au kuuchuna kama alivyofanya apo kistaarabu tu sasa ww kite cha warimu sijui haki ya kuniona sio muungwana ni amekutuma au shobo mkuu ndugu angu
Kite kya warimu😂😂😂warimu wambue😂
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA SABA
SONGA NAYO................
Ni miaka miwili ilikuwa imepita tangu tukio hilo litokee na wakati huo ndio kwa mara ya kwanza alionekana tena ikiwa ni maiti. Jambo hilo lilizua utata na maswali mengi juu ya safari ya mwanamke huyo na familia yake mpaka kufikia hatima ya kupokelewa na mchanga kwenye futi sita. Rama Rajabu ambaye alikuwa afisa wa polisi na msimamizi wa kesi hiyo baada ya kufuatilia mambo yote hayo alimtaka meneja wa hoteli hiyo aweze kumuonyesha kamera ya matukio yote kuanzia ya jana yake wakiwa wawili tu pekee ndani ya chumba hicho cha kuweza kuongozea kamera. Meneja asingeweza kukataa kwenye jambo la msingi kama hilo hivyo akakubali kufanya hivyo.
Kwenye kamera ni kweli mwanamke huyo alionekana akiwa anaingia kwenye hiyo hoteli akiwa amejifunika hijabu na kuyaacha macho yake na uso wake tu ila sehemu yote ya mwili wake ilikuwa imefunikwa vizuri kabisa. Wakati anaingia hapo hakuwa pekeyake, alikuwa na mwanaume ambaye alivaa hood ambayo iliifunika sura yake kwa sehemu kubwa hivyo hakutoa nafasi hata moja ya uso wake kuweza kuonekana kwa watu hao. Alionekana kuwa mzoefu na kamera ndiyo maana hakutoa nafasi hata ndogo ya kuipa mwanya kamera yoyote ile kuweza kuinasa sura yake.
Walilipia kila kitu na kuelekea kwenye chumba cha hoteli hiyo mpaka wanafika ndani ambako hakukuwa na kamera. Mpaka wakati huo hawakuwa wamefanikiwa kabisa kuona kabisa sura ya mtu yule ambaye alikuwa mwanaume na kwa namna walivyokuwa wameshikana ni wazi walikuwa wapenzi waliopendana kwa kiwango kikubwa. Jambo la kushangaza lilitokea kwenye video hizo, ni kwamba kwenye kile chumba waliingia watu wawili lakini video zote ambazo zilifuatia baada ya tukio hilo mpaka unakutwa mwili wa yule mwanamke Zara hakukuwa na ishara ya yule mwanaume kutoka ndani ya chumba.
Hilo jambo likaleta mshangao kwa Rama lakini pia hata kwa meneja ambaye naye pia alionekana kutoliamini jambo hilo, ilikuwa kama mazingaombwe yanafanyika. Wakairudisha tena video hiyo nyuma lakini hali ilikuwa ni ile ile hakuna mtu yeyote ambaye alionekana kutoka ndani ya kile chumba mpaka yule mhudumu anafika mle. Rama alihitaji video ya baada ya yule mhudumu kutoka ndani ya kile chumba akiwa anapiga kelele, alihisi huenda mhusika alijificha na aliitumia ile nafasi kutoweka wakati mhudumu anapiga kelele na kuomba msaada.
Iliwekwa video hiyo lakini hakuna kitu kilitokea mpaka wakati meneja anaenda kwenye kile chumba na yeye mwenyewe kupigiwa simu. Nafsi yake iligoma kabisa kukubaliana na hiyo hali ambayo ilikuwa inaonekana kwenye hizo video, hakuwa mtu wa kuuamini uchawi duniani kana kwamba ajumlishe kuwa mhusika alipotea kichawi hivyo akaanza kuzirudia rudia zile video kwa umakini zaidi ya mwanzo. Ndipo kuna kitu kimoja aligundua kwamba hakikuwa sawa kabisa, kuna mhudumu wa kiume ambaye alipelekea chakula ambacho bila shaka kilikuwa ni supu alfajiri ya mapema kabisa ila baada ya kuingia mle ndani ilichukua dakika kumi mpaka akatoka tena jambo ambalo halikuwa la kawaida kabisa kuingia kwenye chumba cha wapendanao kupeleka chakula halafu umalize dakika kumi ndani, kuna kitu hakikuwa sawa ndipo akaamua kuipeleka hiyo video taratibu.
Mhudumu aliye ingia na aliyetoka walikuwa ni watu wawili tofauti, aliye ingia alikuwa na mwili wa kawaida tena uso ukiwa wazi ila aliyetoka humo ndani alikuwa na mwili uliojengeka kwa mazoezi tena ikionyesha kabisa kwamba zile nguo zilikuwa zinambana bila shaka hazikuwa zake. Jambo lingine ambalo liliongezeka ni kwamba yule ambaye alitoka alikuwa ameufunika uso wake kwa kitambaa na kofia kichwani bila shaka hakuhitaji kabisa kujulikana. Mpaka hapo aligundua kwamba yule mhudumu alikuwa mle mle ndani ya chumba hivyo alitoka haraka kukimbilia kwenye kile chumba, alienda kufungua moja kwa moja kabati la nguo ambapo alikutana na mtu akiwa amefichwa mle na ndiyo yule ambaye alikuwa mhudumu halisi.
Mhusika alikuwa amemvalisha mhudumu nguo zake naye alibeba nguo za mhudumu akatoweka. Alimgusa mhudumu huyo shingoni na kugundua kwamba bado alikuwa hai ila alizimishwa tu hivyo akamtoa haraka ili apewe huduma ya kwanza huenda kuna kitu angewasaidia lakini wakati anafanya hayo yote kuna kitu alikigusa kwenye nguo ambazo zilikuwa za muuaji alizo valishwa mhudumu huyo. Alikitoa kitu hicho huku akiwa anawapa madaktari nafasi kumzindua kijana huyo mhudumu.
Alikutana na business card ambayo ilikuwa na jina na picha ndogo ya paspoti, jina lilisomeka Gavin Luca na picha ambayo ilikuwepo hapo ni ya mwanaume mmoja ambaye kichwani alikuwa na upara. Alitambua kabisa kwamba muuaji huyo aliisahau kwa bahati mbaya kadi hiyo na ndiyo ambayo yeye alikuwa anaenda kuitumia kuzichanga nyekundu na nyeupe ili zijitenge kwa ajili ya kumpatata mtu huyo. Mhudumu alizinduka na kuulizwa kama alifanikiwa kumuona yule mwanaume ambaye alikuwa mle ndani, jibu ambalo alitoa liliwakatisha tamaa baada ya kudai kwamba hakumuona zaidi ya kukaribishwa ndani humo na alipogeuka ili kuufunga mlango alihisi kupigwa na kitu kizito kwenye shingo yake hivyo hakuona wala kuelewa lolote. Rama aliamua kutoa taarifa rasmi juu ya tukio hilo ambalo lilitokea kwenye hoteli hiyo.

KARIAKOO, DAR ES SALAAM.
Mji ulikuwa umetapika kama ilivyo kawaida yake siku zote, mijongeo ilikuwa ni mingi kama iivyo kawaida. Kariakoo siku zote ni sehemu au kitovu kikuu cha biashara ndani ya nchi, ni eneo ambalo linategemewa si tu na wafanya biashara bali hata uchumi wa nchi umeegamia eneo hilo kwa kiwango kikubwa kwa kuaminika kubeba matajiri na wafanya biashara wa kila aina na kila pande ya Tanzania.
Mchana wa saa nane na dakika thelathini kwa masaa ya Afrika ya mashariki pilika pilika za siku zote zilikuwa zinaendelea ndani ya eneo hilo, vijana wapigaji walikuwa wakilizungukia eneo hilo la jiji macho yakiwa juu juu lakini watafutaji walikuwa wanajaribu kukimbizana na muda kwani kila sekunde ambayo ilikuwa inaenda ilikuwa ina mahesabu makali kwao. Mtaa wa Agrey na Ndanda kuna kijana mmoja mtanashati alikuwa ameishika sigara yake kubwa mkononi akiwa anaivuta kwa sifa kana kwamba alikuwa anataka kuuaga ulimwengu.
Alikuwa amesimama pembezoni mwa duka moja kubwa ambalo ndani yake kulikuwa na vifaa vingi vya umeme na kielektroniki vikiwa vinauzwa, kama ni mara ya kwanza unafika sehemu hiyo basi moja kwa moja huenda ungehisi kwamba kijana huyo alikuwa pale kama mmiliki ila kadri wateja walivyokuwa wanaingia kwenye duka lile kubwa na kutoka bila shaka ilionyesha wazi kwamba naye alikuwa ni mteja tu kama sio mpita njia ambaye alikuwa na mambo yake ama moja kati ya matapeli wa jiji ambao walikuwa wanaendelea na kazi yao ya kutapeli watu huku wakiwa wanajiweka smart ili kumvuta kila mtu kirahisi.
Alikuwa amevaa suruali safi nyeusi ya kitambaa, juu shati nyeupe ambayo ilikuwa imenyooshwa kwa ustadi mkubwa lakini chini alivaa kiatu safi cheusi ambacho kilimfanya awe na mvuto. Nguo zilikaa kwenye mwili ambao ulikuwa umejengwa vizuri, haikuhitaji kumuangalia mara mbili ili kujua namna mtu huyo alivyokuwa akiyahusudu mazoezi na yakamkubalia. Mkononi alikuwa amevaa saa aina ya rolex, moja kati ya saa za gharama zaidi duniani lakini bila kusahau kichwani alikuwa amefuga zile rasta za asili ambazo ni muda zilionekana kutokatwa kabisa akiwa amezifungia kwa nyuma. Bila shaka alitosha kabisa kuwavutia wale mashangazi ambao huwa wanavutiwa na vijana wa namna hiyo na kuwa tayari hata kuwapatia pesa za aina yoyote ile ambazo wangezihitaji kikubwa tu ili waweze kulala nao.
Akiwa amesimama hapo hakuwa na habari na mtu yeyote zaidi ya watu kadhaa wakiwemo wanawake warembo ambao walikuwa wamempa umakini huku warembo hao wengine wakimtamani kijana huyo ambaye hakuonekana kuwa na muda na mtu yeyote yule ndani ya hilo eneo. Aliiangalia saa yake na kusonya, aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa kitambaa ambacho alikitumia kujifutia jasho huku akiwa anaitupa ile sigara yake kubwa chini. Aligeuka kuangalia kila upande kwa usahihi lakini ni kama kile ambacho alikuwa anakitafuta hakukiona kwa haraka ila baada ya dakika moja ya kuangaza alitabasamu na kurudi nyuma sehemu ambapo yalihifadhiwa mafriji ikiwa ni kama anajificha kwenye kivuli kutokana na jua kali lakini haikuwa hivyo, kuna kitu alikuwa amekiona mwanaume huyo ndicho ambacho kilimfanya akachukua maamuzi hayo na kuzipiga hizo hatua zake.
Pembezoni mwa sehemu ambayo alikuwa amesimama kulikuwa na ghorofa kubwa ambalo lilikuwa na maduka makubwa ya vitu vya jumla na ndipo hasa ambapo lengo lake lilikuwepo. Upande ule ambao alikuwa ameangaza kulikuwa na gari tatu za kifahari ambazo zilikuwa zinakuja, gari hizo zilitembea mpaka kwenye lile ghorofa kisha zikasimama pale na hapo wakatoka wanaume ambao walikuwa ndani ya suti zao nyeusi kuangaza huku na huko kisha mmoja akafungua mlango wa gari ya katikati ndipo akatoka mwanaume mmoja mtu wa makamo kidogo akiwa ndani ya kanzu yake nyeupe.
Upande mwingine alitoka mwanamke ambaye bila shaka alikuwa ni mkewe na watoto wawili wa kike na wa kiume ambao hawakupishana sana kwenye umri. Palikuwa na walinzi saba ambao walikuwa wanaangalia usalama wa ile familia ambayo haikujulikana bado ilikuwa familia ya nani na ilikuwa pale kwa ajili ya kufanya jambo gani. Yule kijana ambaye alikuwa pale kwenye yale mafriji, alitabasamu kwa mara nyingine kisha akafumba macho yake na kutamka

Sehemu ya saba nafika mwisho hapa, tukutane ndani ya sehemu ya nane.

FEBIANI BABUYA.
 
Back
Top Bottom