Simulizi ya kipelelezi: Idaiwe maiti yangu

Simulizi ya kipelelezi: Idaiwe maiti yangu

STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA NANE
SONGA NAYO................
"Kawasalimie kuzimu mpuuzi mkubwa wewe" alipofumbua macho alichomoka pale kwa mbio kali kumuwahi mtu yule kabla hajaingia kwenye yale maduka ya jumla, ilikuwa ni ghafla na ni wakati ambao walinzi walishtuka kwamba kuna mtu anakuja ule upande wao ila kwa bahati mbaya wakati wanashtukia hilo wawili walikuwa wamepigwa risasi na yule kijana tayari hali ambayo iliwafanya wananchi wengine kuanza kukimbia hovyo huku wangine wakisahau hata maduka yao wazi, maisha yao yalikuwa mhimu zaidi. Ule muingilianao wa watu ulifanya walinzi kutopiga hovyo risasi kwani wangejikuta wanaua watu wasio na hatia.
Kijane yule aliruka mpaka juu ya gari ambapo alidunda kwa mguu wake mmoja na kutua upande wa pili kwenye shingo ya mwanaume mmoja ambaye alikufa pale pale. Walinzi wawili walikuwa wanakimbia na ile familia kuelekea kweye yale maduka, wawili ndio ambao walibakia hapo kupambana naye. Alinyanyua bastola yake kwa kasi na kuachia risasi moja ambayo ilienda kutua kwenye kichwa cha yule mwanaume wa makamo akiwa anakaribia kuzama kwenye duka mojawapo hali ambayo ilizusha kelele kwa familia yake ikabidi mwanaume mmoja aende na familia ndani mmoja ndiye akabaki pale chini akiwa anamkokota mzee yule kuelekea naye ndani pia akiwa amepigwa risasi ya kichwa anavuja damu.
Vilisikika ving'ora vya polisi vikija kwa mbali eneo hilo, kijana huyo alisonya na kuzunguka kwa kasi kiasi kwamba risasi za wa wanaume hao zilikita kwenye gari, alisubiri wapige mpaka zilipo waishia ndipo alitokezea juu ya gari kwa kujiviringisha. Alitua karibu ya mwanaume mmoja ambaye alimpokea kwa ngumi iliyotua kwenye bega lakini hakutikisika zaidi aliishika shingo ya mwanaume huyo na kuivutia kwenye kisigino chake ambapo alikutanisha mguu na kichwa, alipo muachia alitoboa shingo hiyo kwa vidole vyake na kumtupia pembeni. Yule mwenzake alikuja kwa kukimbia ila alifuatwa kule kule ambapo alikutana na ngumi nzitoa ya kifua iliyomfanya kuhema kwa nguvu na kupiga goti, akiwa pale chini alipigwa risasi tatu za kichwa kukawa kimya.
Polisi waliingia ndani ya hilo eneo ambalo lilikuwa limetapakaa damu na miili barabarani lakini muuaji hakuonekana yuko wapi. Mtaa ulikuwa kimya huku kila mwenye duka karibu akiwa amekimbia bila hata kufunga na wengine walijifungia ndani ya maduka yao. Ving'ora vya polisi ndivyo ambavyo vilimtoa mlinzi mmoja mle ndani akiwa amembeba yule mzee kwenye mkono wake na kuwataka polisi waipe ulinzi familia ipo ndani na wengine watumie gari ya polisi kumuwahisha hospitali mzee huyo kuona kama wanaweza kuyaokoa maisha yake.
Familia ilipewa ulinzi na mzee huyo akawahishwa hospitali na gari ya polisi kwa sababu ilikuwa ni ngumu kuweza kuisubiri ambulance na hali yake ilikuwa mbaya sana lakini hata kabla hawajafika huko hospitali alifia njiani hivyo walifika na maiti kule hospitali. Ni muda fupi tu tangu litokee tukio hilo afisa wa polisi kutoka Osterbay Ezra Ethan maarufu kama Double E alikuwa amefika na askari wenzake kadhaa hapo wakidai kwamba hiyo kesi wao ndio waliagizwa kuja kuisimamia kutokana na ukubwa wa mtu ambaye aliuawa hivyo wakahitaji maelezo kutoka kwa hao maaskari ambao walikuwepo eneo hilo.
Kiufupi ni kwamba mtu ambaye aliuawa hilo eneo alikuwa ni bosi wao, waziri wa mambo ya ndani ambaye idara za polisi zipo chini yake, bwana Sylivester Mboneka ndiye ambaye aliuawa hivyo hiyo kesi ilikuwa na uzito mkubwa kwa jeshi la polisi. Licha ya mtu huyo kuwa waziri lakini pia alikuwa ndiye bosi wa idara hiyo kwani ilikuwa ipo chini ya wizara yake hivyo hata msako wa mhusika ulitarajiwa kuwa mkubwa zaidi. Yalitolewa maelezo mafupi lakini mtu ambaye alikuwa na maelezo mengi zaidi ni yule bodyguard mmoja ambaye alibaki na familia ndani ya yale maduka kwa sababu mwenzake mmoja alikuwa ameenda na mheshimiwa hospitali.
Alielezea tukio zima lilivyokuwa lakini ni kama kuna sehemu walikuwa wanakosa baadhi ya matukio ya kuunganisha hivyo wakawaomba wamiliki wa yale maduka waweze kuwaonyesha video ya tukio zima kwani waliamini eneo lile lilikuwa na kamera za kutosha. Kwenye video ambayo ilionyeshwa ndani ya hizo kamera iliwasaidia kuona tukio zima namna lilivyokuwa, insipekta Ezra alishangazwa na kasi ya kijana huyo mpaka kuwa na ujasiri wa kumvamia kiongozi huyo majira ya mchana wa jua kali namna hiyo. Risasi ambayo ilipenya kwa mheshimiwa na namna ilivyopiga iliwapa tahadhari juu ya uwezo wa huyo kijana hivyo waliomba kubaki na video hiyo kwa ajili ya upelelezi zaidi maana walikuwa na kazi ya kumtafuta kijana huyo ambaye kwenye video ile alionekana kupotelea uelekeo ule ambao wao walikuwa wanatokea akiwa anakimbia kama raia ambaye alikuwa anayaponya maisha yake lakini ndiye alikuwa muuaji mwenyewe.
"Haiwezekani mtu wa kawaida tu na mwenye akili timamu aweze kufanya tukio kama hili tena mchana wa jua kali namna hii wakati anajua kabisa kwamba hili eneo la wafanya biashara kuna kamera kila sehemu" Ezra aliongea akiwa anaiangalia miili ambayo ilikuwa imefunikwa pale barabarani na barabara ilifungwa kabisa hakuna mtu aliruhusiwa kusogelea hilo eneo.
"Unahisi ni kwanini amefanya hivi labda?" aliuliza polisi mwenzake
"Bado sielewi Hassan, hainiingii akilini kabisa kwa sababu kuonyesha sura yake maana yake ni kwamba anajua kabisa atatafutwa kila kona ya nchi hii sasa kwanini afanye hivi?"
"Huenda ni moja ya makosa ambayo hata baadhi ya wahalifu huwa wanayafanya, anaweza kuwa na mipango mikali kila sehemu ila akakosea sehemu moja tu"
"Hapana, kuna watu wa kufanya makosa ya namna hiyo lakini sio mtu kama huyu, kwanza kabisa anaonekana kwamba ni mtaalamu wa mauaji, angalia ujasiri alionao kuvamia msafara wa waziri mkuu tena akiwa na walinzi saba ambao wana mafunzo ya hali ya juu, halafu muda wenyewe ni mchana? Hilo haliwezi kuniingia akilini kabisa"
"Unamaanisha kwamba amefanya hili jambo makusudi kabisa?"
"Ndiyo"
"Kwanini afanye hivyo?"
"Hiyo ndiyo kazi yetu kuweza kujua kuhusu hilo jambo, kumbuka leo asubuhi tumepokea taarifa kutoka Zanzibar kwamba kuna mauaji yametokea hotelini, siku hiyo hiyo yanatokea mauaji mengine kwa waziri wa nchi huoni kama sio jambo la kawaida hili?" Ezra wakati anaongea hilo alishtukia jambo fulani ikamlazimu kuingiza mkono wake mfukoni kuitoa simu yake ambapo moja kwa moja alienda kwenye mtandao kuangalia jambo fulani. Alishtuka kidogo na kumsogezea mwenzake simu ili aone kile ambacho kilimshtua.
"Hii picha ina uhusiano gani na hili tukio?"
"Kwenye picha hapo mmoja ni waziri ambaye amuawa hapa saivi lakini huyo mwingine ni mfanya biashara Ismail Mhammed kutoka Zanzibar. Huyo mzee ndiye ambaye mwanae amekutwa ameuawa hotelini leo, unahisi hii inaweza kuwa bahati mbaya?" mwenzake hakuwa ameligundua hilo, kidogo hata yeye alianza kupata mashaka.
"Kwamba hivi vifo vinaweza kuwa na uhusiano?"
"Ndiyo moja kwa moja kwa sababu sidhani kama kuna bahati mbaya ya namna hii, hao wazee walikuwa wanafahamiana na kama wanafahamiana maana yake muuaji alipanga haya matukio kwa ustadi mkubwa ila alicho kifanya ni kutofautisha wakati wa matukio tu"
"Sasa kwanini aue wote wawili wa kwenye hizi familia ambazo zinaonekana kuwa na uhusiano wa karibu?"
"Bado sina jibu Hassan ila huenda kuna kumuunganiko mkubwa wa matukio na hii haiwezi kuwa bahati mbaya. Muuaji anaonekana kabisa kwamba alidhamiria sisi tuweze kuona sura yake ndiyo maana akaamua kulifanya hili mchana kwa sababu kama alitaka kufanya iwe siri basi angetafuta namna nyingine ya kuweza kumfikia waziri"
"Ni mtu gani mpuuzi wa kuja kuonyesha sura yake hadharani namna hii akiwa anafanya mauaji?"
"Huenda kuna ujumbe alitaka sisi tuupate, swali la msingi ni kwamba kwanini amuue waziri na alijuaje kuhus ratiba binafsi za waziri? Maana yake huenda kuna mtu mkubwa ambaye yupo nyuma yake mwenye uwezo wa kuzipata taarifa hata za viongozi wakubwa, sema nao hawa wazee wakiambiwa wawekewe ulinzi mkubwa huwa wanakuwa wabishi sana matokeo yake ndiyo haya sasa na hapa sisi ndio ambao tunaenda kupokea lawama kwa ujinga wake mwenyewe"
"Ezra relax kwanza tuanze kazi mara moja ya kumtafuta huyu mtu kumbuka hili jambo ni kubwa ambalo linaigusa mpaka Ikulu hivyo sio muda hapa IGP ataanza kuulizia majibu ya kumpatia mheshimiwa raisi kwani wizara itatakiwa kupata mtu mwingine mapema na hilo ni jambo ambalo inabidi litekelezwe na raisi mwenyewe"
"https://jamii.app/JFUserGuide them" Ezra aliongea kwa jazba kidogo akionekana kutopendezwa na hali ambayo ilikuwa imetokea. Aliingia kwenye gari na kutuma picha za mtu huyo ofisini ili waweze kumfahamu kwamba alikuwa ni nani haswa. Ulipita muda kidogo majibu yalirudi kwamba mtu huyo hayupo kwenye mifumo rasmi ya nchi, lilikuwa jambo la kushangaza kidogo basi ikawalazimu kuomba msaada kwa shirika la kipelelezi la nchi ili liweze kuwapatia taarifa zaidi juu ya mtu huyo.

Sehemu ya nane inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA TISA
SONGA NAYO................
Majibu mengine ya kukatisha tamaa yalirudi mezani, huyo mtu haikujulikana ni wa wapi, aliishi wapi na alikuwa akifanya nini kwa sababu kitu pekee ambacho walikipata ni jina lake tu. Jina lake alikuwa anaitwa OTHMAN CHUNGA. Zaidi ya hapo hakukuwa na kitu chochote kuhusu historia yake wala sehemu ambazo aliwahi kuishi ama kuwepo, mtihani mwingine ukazaliwa mbele yao, kesi mwanzoni tu ilionyesha kiza kinene wasijue hata ni wapi walikuwa wanaelekea. Alitoka nje ya gari akiwa amenyong'onyea sana akiwa anazitupa hatua zake kumsogelea Hassan.
"Tunamtafuta ghost (mzimu), tumepata jina lake tu, hakuna historia yake yoyote, haijulikani aliwahi kuishi wapi, familia yake ni ipi wala hakuna dalili kama kuna mtu wa aina yake amewahi kuwepo kwenye haya maisha" hayo maelezo hata Hassan yalimchanganya.
"Hilo jambo haliwezekani Ezra"
"Wapo watu wa aina hiyo Hassan, na mara nyingi watu wa hivyo huwa wanatumika kwenye shughuli kama hizi kwa sababu wakiamua kupotea huwa hauwezi kuwapata mpaka labda ije itokee bahati mbaya akafanya kosa hata moja na kufanya kwao makosa ni nadra kwa sababu wapo makini kwenye kina hatua za maisha ambazo wanazipiga. Cha kushukuru Mungu tumepata hata jina na picha" Ezra alikuwa askari hodari mno lakini ni kama alikuwa amekata tamaa kabisa juu ya kesi hiyo ambayo ndo kwanza walikuwa wanaanza kuipekua lakini kuna jambo ambalo lilimpa tumaini baada ya kulikumbuka. Alikumbuka kwamba kwenye ile video kuna wakati mtu yule aligusana na wale walinzi tena wengine akiwatoboa kabisa hivyo aliona ni nafasi pekee ya kuweza kupata alama za vidole ambavyo vingewafanya wampate mhusika mara moja kama aliwahi kutumia alama zake za vidole kwenye mfumo wowote ule nchini ambao umesajiliwa kimtandao.
Madaktari walipewa maagizo na kuchukua vipimo hivyo ambapo walisubiri kwa masaa mawili, majibu ambayo yalirudi yalizidi kumkatisha tamaa Ezra na kumnyong'onyesha. Ripoti ya majibu juu ya uhalisia wa Othman Chunga yalirudi kwake, majibu hayo yalikuwa yanaonyesha kwamba alama za vidole ambazo zilikutwa kwenye miili ya wale walinzi wa waziri hazikuwa zikiendana na mtu yeyote yule ndani ya nchi ya Tanzania hivyo hakuna sehemu yoyote ile ambayo ilionyesha uhalisia wa yule mvamiaji pamoja na uwepo wa mtu wa namna hiyo nchini. Akiwa ameegamia gari akiangalia eneo la tukio ambapo miili ilikuwa imeshatolew tayari, alipokea simu kutoka kwa mkubwa wake wa ofisi ambaye alimtaka ampe majibu sehemu ambayo alikuwa amefikia kwenye kesi hiyo.
Ezra alielezea kila hatua mpaka walipofikia na hatua ambayo alikuwa ameipiga, mkuu wake alimtaka kuishia hapo hapo ambapo alikuwa amefika kwa sababu hiyo kesi ilikuwa inaenda kwenye ngazi za juu kutokana na ukubwa na unyeti wake. Alimshukuru kijana huyo kwa kufanikiwa kuyajua mambo kadhaa kuhusu hiyo kesi ila ulikuwa ni wakati wa yeye kukaa pembeni kisha wanaume kumzidi yeye waingie kazini kuipambania. Alichukia kupokea taarifa hiyo kwa sababu aliamini kazi kama hizo ndizo ambazo zingempa jina kubwa la kumfanya apande cheo kirahisi sasa kutolewa kwenye mchezo maana yake hata mchango wake mdogo usinge onekana kabisa kwenye jambo hilo. Aliapa kuifuatilia kesi hiyo mpaka ambapo angeona mwisho wake na kumpata Othman Chunga.

*******
Kuuawa kwa waziri wa mambo ya ndani Slyvester kulizua taharuki mpya ndani ya nchi, taarifa zilianza kuzagaa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii hususani kutoka kwa watu ambao walikuwa Kariakoo mchana wa siku hiyo wakati tukio hilo linatokea mbele ya macho yao.
Tukio hilo kuna watu walilifananisha na ugaidi, wengine waliamini kwamba aliyehusika lazima alikuwa ni kiongozi mwenzake na huenda walipishana kwenye maslahi upande wa siasa hivyo wakaamua kuondoka na roho yake lakini kuna watu pia walihusisha tukio hilo na wivu wakidai kwamba huenda kuna watu walikuwa wakimuonea wivu waziri huyo kutokana na tukio hilo ambalo lilikuwa limetokea. Kusambazwa wa taarifa hiyo hovyo ndiko ambako kulifanya vyombo vikubwa vya habari navyo kuanza kuizungumzia habari hiyo kwa ukubwa juu ya yale ambayo yalitokea.
Habari hiyo ndiyo ambayo ilimtoa waziri mkuu hadharani kwa ajili ya kuthibitisha taarifa hizo ikiwa ni maagizo ya raisi ambaye alikuwa nje ya nchi wakati huo kwa ajili ya mkutano wa maendeleo wa jumuiya ya nchi za Afrika za kusini mwa jangwa la sahara, waziri mkuu alieleza tu kwamba kiongozi huyo alivamiwa na kuuawa na mtu ambaye hakutambulika kwamba ni nani ila aliahidi tu kwamba jeshi la polisi linashirikiana na mamlaka zingine za usalama kuhakikisha kila ambaye amehusika na tukio hilo anaweza kupatikana mara moja na kuweza kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi ili iwe onyo kwa watu wengine ambao wanafanya mambo kama hayo.
Kesi ilikuwa ni ngumu ambayo ilizua minong'ono hivyo ikawa ni lazima kwamba ipatiwe majibu ya haraka ili kuweza kuwatuliza wananchi ambao walikuwa wameanza kuhoji kuhusu usalama wa nchi yao mpaka kiongozi mkubwa kama huyo anauawa tena mchana wa jua kali eneo la wazi kabisa, lawama zikaenda kwa upande wa jeshi la polisi na mamlaka za ulinzi kuhusu jambo hilo.

Saa kumi na moja na dakika hamsini na tano alasiri kulikuwa na kikao cha dharura yalipokuwa makao makuu ya shirika la kijasusi la taifa. Kikao hicho kilitokea kwa sababu ya taarifa ambazo walizipata juu ya tukio ambalo lilikuwa limetokea mchana wa siku hiyo, kiongozi wa shirika hilo Micho Othman bado alikuwa akiendelea kulishughulikia lile suala la wanajeshi kuweza kuuliwa huko Kenya ndipo akapata habari zingine za kuuawa kwa waziri wa mambo ya ndani wa nchi. Taarifa hiyo ilimpa hasira kali kwa sababu lilikuwa ni jukumu la polisi kuhakikisha kiongozi wao wa wizara anakuwa salama lakini kitu cha kushangaza ni kwamba mpaka wakati huo alikuwa amekufa tayari hivyo hakuona umuhimu wa lawama tena zaidi ya kushughulikia suala hilo.
Alikuwa na taarifa za awali za tukio hilo ambazo binafsi zilikuwa zikimchanganya kwa sababu sio muda mrefu alipewa taarifa ya tukio ambalo lilipatikana Zanzibar huko kuhusu kuuliwa kwa mtoto wa tajiri Ismail na utambulisho wa mtu ambaye alikutwa ndani ya eneo la tukio ni jina la mwanaume ambaye ndiye alidaiwa kuhusika kufanya mauaji ya wanajeshi huko Kenya. Kichwa chake kilianza kuuma kuhusu utambulisho wa mtu huyo, akiwa anaendelea kuwaza kuhusu jambo hilo ndipo akaongezewa mzigo mwingine wa mauaji ya waziri wa mambo ya ndani ndiyo sababu aliitisha kikao cha dharura na watu wake ambao alikuwa anawaamini ili kuweza kulishughulikia suala hilo kwa ukaribu zaidi.
Alikuwa amekunja sura yake akiwa kwenye hiyo ofisi na watu watano mbele yake, walikuwa wamefika takribani kwa dakika tano lakini hakuitikia hata salamu zao kwa sababu mawazo yalionekana kuichukua sehemu kubwa ya fikra zake. Alishtuka na kuwaangalia watu hao ambao aliwakaribisha waweze kuketi hapo ili wapate muafaka wa jambo hilo.
"Tuna kesi tatu kwa wakati mmoja ambapo kesi moja inatakiwa kupatiwa majibu haraka kwa sababu ina mkanganyiko mkubwa zaidi. Nadhani tayari wote taarifa mnazo za kuuawa kwa waziri wa mambo ya ndani na wananchi wanataka majibu haraka vinginevyo kila mtu ataendelea kuropoka anachokitaka yeye kitu ambacho kitatuletea picha mbaya kama taifa na itaonekana kwamba sisi ni dhaifu sana hatuwezi hata kuwalinda watu wetu wenyewe" alitulia kidogo kabla ya kuendelea tena.
"Tumefanikiwa kupata picha tu pekee na jina la mhusika lakini mtu mwenyewe ni kama mzimu. Hakuna taarifa zake zozote kuhusu utambulisho wake, haonyeshi kuwepo kwenye mifumo rasmi ya nchi na wala hajulikani kwamba ametokea wapi na kwa nini afanye kitu kama hiki lakini jambo moja ambalo linaleta wasiwasi ni kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya mauaji ambayo yametokea Zanzibar na haya ya waziri wa mambo ya ndani kwa sababu mzee Ismail ambaye mtoto wake ameuliwa leo alikuwa ni rafiki mkubwa wa waziri wa mambo ya ndani hivyo huenda kuna sababu ya haya yote" mkurugenzi alitulia kwa muda akiwa kama anapitia kitu kwenye kompyuta yake ambayo ilikuwa mbele ya meza alipokuwa amekaa.
"Kwa hali ilivyo mpaka sasa nataka mgawane majukumu, nimewaita hapa kwa sababu nawaamini kwenye hili na nina imani mnaweza kuniletea majibu yaliyo kamilika kwa muda mfupi. Mmoja wenu anatakiwa kwenda Zanzibar kufanya uchunguzi wa kilicho tokea kwa binti Zara, wawili mnatakiwa kwenda Kenya kupata majibu kamili ya kilicho tokea huko kwa taarifa ambayo niliwapatia mapema lakini wawili pia mnatakiwa kuishughulikia hii kesi ya waziri wa mambo ya ndani haraka kesho usiku nataka majibu yote kwa sababu nategemea kukutana na raisi akifika tu nchini. Kuna swali?" maelezo yalikuwa mafupi na yenye kueleweka. Hakuna ambaye aliuliza jambo lolote lile watu hao walitoka humo ndani kwenda kuyaanza majukumu yao, ilikuwa ni mapema kuzalisha maswali yasiyo na msingi wowote bali walitakiwa kwenda huko yaliko tokea hayo ya kutokea ili waweze kuja na majibu kamili.

Sehemu ya tisa inafika mwisho hapa.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA KUMI
SONGA NAYO................
MAKONGO JUU
Saa saba na dakika thelathini na tano majira ya usiku wa manane kwenye jengo la ghorfa tatu kulikuwa na utulivu huku nje wakiwa wanapishana walinzi kadhaa ambao walikuwa makini kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama. Walinzi walikuwa wanazunguka zunguka karibia kila kona ya jengo hilo wakiwa kwenye mavazi ya kiaskari bila shaka aliyekuwa analindwa alikuwa ni mtu mkubwa kwenye taifa.
Jumba hilo lililokuwa likionyesha ukwasi mkubwa ndani ya eneo hilo na lilikuwa likimilikwa na aliyekuwa makamu wa raisi wa zamani wa nchi ya Tanzania, Yasin Mbarouk. Ni kiongozi ambaye kwa wakati huo alikuwa amestaafu, alikuwa akila pensheni za maisha yake na makubwa ambayo alikuwa amelitendea taifa miaka ya huko nyuma. Umbali kadhaa kutoka lilipokuwepo jengo hilo kulikuwa na kivuli cha mtu karibu na ilipokuwepo taa moja kwenye majengo ambayo yalipakana na jumba hilo la kitajiri. Kivuli ambacho kilikuwa hapo kilikuwa cha mwanaume mmoja ambaye alikuwa ameifunika sura yake na kitambaa ambacho kiliishia puani kushuka mpaka karibu na shingo, kuanzia kwenye macho uso ulikuwa wazi kabisa.
Alikuwa amesimama eneo hilo akiwa analikadiria lile jengo ambalo lilikuwa hapo karibu yake, alifumba macho kwa muda baada ya kuhisi kama kulikuwa na ndoto mbaya ambazo zilikuwa zikimjia kila akilikumbuka jina la mtu ambaye alikuwa ndani ya jengo hilo lakini haikuwa sababu ya msingi ya yeye kuweza kuachana na kile ambacho kilimpeleka maeneo hayo huo usiku. Alianza kujongea taratibu kuelekea kwenye lile eneo huku akiwa makini kwa hatua zake ambazo alikuwa anazisogeza moja moja kwenda mbele. Aliufikia ule ukuta wa jengo hilo, aliangalia kila pembe na kugundua kwamba hapakuwa na mtu jirani zaidi ya minazi ambayo ilipandwa kwa ndani ya jengo hilo.
Alichomoa kifaa kidogo ambacho kilikuwa kama kisu lakini pembezoni kilitengenezewa nyota kadhaa kila pande, alikitumia kupandia kwenye ukuta huo mrefu mpaka alipofika juu. Juu kabisa kulikuwa na nyaya za umeme ambazo alizigundua baada ya kukigusisha vibaya suruali yake ikaungua karibu na kwenye paja lake. Alichungulia ndani kuwashangaa wale wanaume ambao walikuwa wanazunguka kila kona akajiachia kwenda chini na alipotua chini tu alikirusha kile kifaa chake kuelekea juu ambapo kilizigusanisha nyaya vibaya kutokana na aina ya nguvu ambayo aliitumia kuweza kukirusha. Eneo la nyumba lote lilipiga shoti kali ambayo ilisababisha umeme kuzima ndani ya jengo hilo zikawa zinasikika kelele za walinzi tu wakiambizana kwamba shoti ilikuwa imepiga hivyo walitakiwa kuliwasha genereta haraka iwezekanavyo.
Kuna mlinzi ambaye alikuwa karibu na lile eneo ambalo lilipiga shoti na aliona kama kuna kitu kinadondoka chini kikiwa cheusi na wakati huo umeme ukawa unazima. Aliwasha tochi yake kuweza kusogea lile eneo haraka ndipo chini aliona kitu cheusi kikiwa kama kisu, aligundua kwamba kilibadilika kuwa cheusi baada ya kupigwa na shoti na bila shaka ni mtu alikirusha kile kifaa kwani kisingewezekana kabisa kuwepo kule juu. Alihitaji kutoa taarifa kwa wenzake kwamba wamevamiwa lakini muda haukuwa rafiki sana kwa upande wake, aligeuka ili kuwaita wenzake ndipo alijikuta akipamiana na mtu, mara ya kwanza alihisi ni mlinzi mwenzake ila alishtuka wakati shingo yake inavunjwa. Mwanaume yule ambaye alivamia eneo hilo alisogea kwenye kile kifaa chake akakibeba na kutoweka hapo.

Alisogea mpaka mbele ya jengo hilo ambako kulikuwa na walinzi wengi, kiza kilimrahisishia kazi kuwa rahisi aliwaua walinzi wengi kikatili akiwa anatoboa toboa shingo zao kwa kutumia kile kifaa. Jenereta liliwashwa baada ya dakika mbili, miili ya walinzi walio kufa ikiwa imetepakaa kila kona ndani ya jengo lile ikawalazimu kupiga king'ora kutoa taarifa kwamba wamevamiwa na mheshimiwa alitakiwa kulindwa kwa namna yoyote ile kwa sababu mtu ambaye aliwavamia hapo alikuwa ni muuaji. Ndipo walinzi wakuu wa kiongozi huyo wa zamani kushtuka juu ya eneo hilo kuvamiwa lakini hawakujua kama mhusika alikuwa wapi mpaka wakati huo.
Mvamiaji alionekana kuijua vizuri hiyo nyumba, ramani nzima ya jumba hilo alionekana kuwa nayo kwenye kichwa chake hivyo wakati umeme umekatika baada ya mauaji alitumia huo mwanya kuingia ndani ya jumba hilo mpaka karibu ghorofa ya pili ambapo alitokea dirishani na kulitumia dirisha hilo kupandishia ghorofa ya juu kabisa ambako alijua kuna mtu wake, nako aliingilia upande wa dirishani. Alifanikiwa kuingia mpaka ndani ya chumba ambacho alikuwa analala mheshimiwa huyo wa makamo akiwa amelala ndani ya chumba hicho na mkewe. Umeme ulikatika na kurudi wa jenereta mheshimiwa akiwa bado amelala, hata wakati unarudi bado alikuwa amepitiwa na usingizi mzito mpaka pale ilipowashwa runinga ya ndani ya hicho chumba chake ndipo akakurupuka.
Alikuwa bado ana wenge la usingizi ila alicho kiona lilipotea, mtu alikuwa amekaa mbele ya sofa kubwa lililokuwa linatazamana na kitanda akiwa na bastola kwenye mkono wake pamoja na kile kifaa cha chuma chenye damu ambacho alikiweka kwenye lile sofa kubwa. Usoni sura yake ilikuwa imefunikwa, ile hofu ya mstaafu ndiyo ambayo ilimshtua hata mkewe kwenye usingizi ambaye alianza kutoa sauti ya kilio lakini aliyekuwa mbele yao alitoa ishara ya kuwataka watulie, hawakutakiwa kualika watu wengine ambao hawakuwa wakihusika.
"Nimekuja hapa kwa ajili yako mstaafu ila kama utanilazimisha sana basi sitakuwa na budi kudili na mkeo pamoja na watoto wako ambao bila shaka mpaka sasa wamelala hata hawajui ni kitu gani kinaendelea. Nina uhakika hata wewe hautaki tufike huko" ilisikika sauti nzito ya mamlaka ikimtaka mheshimiwa kuwa mpole.
"Wewe ni nani?" aliuliza kwa kitete akiwa anamkumbatia mkewe kipenzi
"Hilo sio swali la msingi kwa sasa ni vizuri zaidi ungeniuliza kwamba natafuta nini hapa, ningekuona mtu wa maana zaidi"
"Chukua kitu chochote unacho kitaka, kama ni pesa mimi nitakupa ila usifanye jambo lolote baya kwa familia yangu"
"Mimi kuigusa au kutoigusa familia yako sio maamuzi yangu, hilo ni juu yako Mr Yasin" Baada ya kuongea jambo hilo mwanaume huyo alivua kile kitambaa chake usoni, Hali ile ilimshtua mr Yasin mpakaa kajikuta anachukua kifaa chake cha kupumulia kwa ajili ya matatizo yake ya pumu ili kuivuta pumzi ambayo alianza kuishiwa.
"Wewe umekufa, nimeona picha zako na video zako. Hiawezekani haiwezekani" aliongea kwa hofu akiwa anajivuta konani mwili wote ukiwa umeloa jasho, bila shaka aliogopa mno kile ambacho alikiona mbele yake.
"Ni kweli mimi nimekufa ndiyo maana hakuna mtu anatakiwa kujua kwamba mimi ndiye nilikuwa hapa" aliyekuwa anaongea mbele yake ni yule bwana ambaye alijulikana kama Gavin Luca, mwanaume ambaye aliaminika kwamba aliuliwa ndani ya msiti wa Mau huko Kenya lakini bado alikuwa anaonekana na siku hiyo alimtembelea mstaafu huyo kwa sababu walikuwa na mengi ya kuzungumza.
"Tafadhali Gavin usiifanye lolote familia yangu hawahusiki kwa lolote wala hawajui kitu chochote kile ambacho kilitokea" alivyo ongea hayo maneno yalifanya macho ya mwanaume huyo aliyejulikana kama Gavin kuwa mekundu, watu hao walionekana kujuana kwa kipindi kirefu na kujuana kwao hakukuwa kuzuri kiasi hicho.
"Una swali moja la kulijibu mengine nitawauliza wengine, nambie ni nani alipiga ile risasi" aliuliza akiwa siriasi zaidi ya mara ya kwanza alipo ingia ndani ya eneo hilo.
"Gavin tafadhali, sio mbele ya familia yangu"
"Najua huenda mkeo hajui maisha ambayo umeyaishi na yale ambayo umeyatenda ukiwa madarakani hivyo kwake wewe ni mume na baba bora kwa familia yako, vipi kama siku akiujua ukweli juu ya ushetani wako? Bado ataendelea kukuchukulia kama ambavyo anakuchukulia hivi sasa?" aliuliza kwa ukali akiwa anaikoki ile bastola yake.
"Gavin mimi sihusiki na wala simjui ambaye alifanya hivyo, mimi nilikuwa nahakikisha nawalinda watu hao juu ya sheria tu na nilikuwa napewa maagizo bila kujua mtu wa mwisho anayenipa ni nani. Hata mimi nilikuwa kibaraka tu ambaye sina mengi niyajuayo" kujieleza kwake sana kulimnyanyua mwanaume huyo kutoka pale ambapo alikuwa amekaa na kwenda kuuchukua mto mmoja mzito ambao aliugandamizia kwa lazima kwenye mguu wa mzee yule na kuachia risasi ya kwenye goti iliyo mpa maumivu makali akapiga kelele ila alitulia baada ya kutandikwa kofi kwenye uso ambalo lilifanya machozi yaanze kutoka yenyewe.
"Douglas Shenzi, Douglas Shenzi ndiye ambaye alipiga ile risasi"
"Yuko wapi kwa sasa?"
"Mara ya mwisho alienda kuishi Afrika ya Kusini baada ya kumaliza kazi zake ndani ya Johannesburg kule anatumia jina la Master GS ikiwa ni ufupisho wa jina lak...." hakumaliza sentensi yake alipigwa risasi zote ambazo zilibaki kwenye bastola kwenye kichwa chake wakati huo mlango ulikuwa ukigongwa kwa nguvu bila shaka walikuwa ni walinzi wake wanataka kuhakikisha usalama wa bosi wao. Mumewe aliuawa mbele ya macho yake mama huyo hali iliyomfanya kuachia yowe kali na kwa nguvu kubwa kwa uoga na kuomba msaada.

Sijui huyu mheshimiwa anatokaje humo ndani ila sehemu ya kumi natupa kalamu pembeni.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
SONGA NAYO................
Gavin aliubeba mwili wa mstaafu na kuusogeza mbele yake ambapo alisogea mlangoni na kufungua mlango ghafla na kwa nguvu, kwa bahati mbaya wale walinzi waliona bastola ikiwa mbele hivyo walijua ni mvamiaji amefanya hivyo walishambulia kwa risasi nyingi ambazo ziliishia kwenye mwili wa bosi wao. Mlinzi aliyekuwa mbele wakati anawazuia wenzake kufanya hivyo alitahamaki anaangaliana na kitu chenye ncha kali ambacho kilizamishwa kwenye mdomo wake, kilipotolewa mdomo ulitoboka vibaya kwa sababu ya kukata kata nyama za pembeni mwa mdomo kwa kutumia vile vinyota ambavyo vilikuwa pembeni.
Gavin aligeuka kwa kasi na kurusha shilingi moja kwa nguvu ambayo ilikwenda kunasa kwenye paji la uso la kiongozi yule huku akigeuka kwa sarakasi ambayo ilitua kwenye kichwa cha mlinzi mmoja na kumbamiza vibaya kwenye chuma. Usoni alikuwa amejifunika kile kitambaa chake tayari, bastola haikuwa na kazi aliihifadhi kwenye kiuno chake huku vidole vyake vikiwa ndivyo vinafanya kazi kubwa ya kunyofoa makoromeo na sehemu za moyo za walinzi. Aliwachoma choma vibaya walinzi na kuziharibu shingo zao mpaka alipo wamaliza wote akatokomea kusiko julikana.
Wakati imegundulikwa kwamba wamevamiwa ndani ya eneo lile walinzi walikuwa wametoa taarifa tayari kwa polisi juu ya uvamizi ule, polisi kutoka kituo kikuu cha goba walikuwa wamefika ambapo walikuta kilio tu kwa mama na watoto wake juu ya kifo cha kiongozi wa familia lakini miili ya walinzi pia ilitapakaa vibaya kila sehemu. Taarifa hizo hazikuishia hapo tu bali zilifika mpaka ndani ya kituo kikubwa cha polisi Dar es salaam, inspekta Ezra ndiye ambaye alihitajika kwenda huko usiku huo huo na aliomba lisiendelee jambo lolote lile mpaka afike ikiwa ni amri kutoka kwa mkuu wa kituo hicho kikubwa zaidi.
Double E waweza kumuita Ezra Ethan aliingia hilo eneo kwa tahamaki, alishindwa kuamini kwamba ni binadamu ndiye ambaye alikuwa ameyafanya hayo mambo. Miili ya walinzi ilizagaa nje kiasi kwamba hata baadhi ya askari hususani ambao walikuwa waoga walikuwa wakiishia kukaa mbali wengine wakiwa wanatapika. Aliambiwa kwamba hao wa nje walikuwa na unafuu kwa sababu wa ndani ndio ambao waliuawa vibaya zaidi basi akawa hana budi zaidi ya kuingia ndani kushuhudia. Moyo wake ulianza kwenda mbilo, alitokwa na jasho kila sekunde, licha ya kujikaza lakini alihisi hali hiyo muda sio mrefu ingemshinda. Walinzi walikuwa wametobolewa vibaya huku wengine wakiwa wamenyofolewa makoromeo yao vibaya.
Aliingia mpaka ndani kabisa ya chumba cha mheshimiwa, alikuwa amekufa kwa kupigwa risasi nyingi mno kwenye mwili wake zikiwepo tano kichwani, kwenye mguu wake moja na zingine zote ziliishia kwenye kifua chake kiasi kwamba kifua kiliharibika. Alihema na kutoka nje mpaka sehemu ambayo alihifadhiwa mke wa mheshimiwa ili aweze kumpa machache ambayo yalitokea kwa sababu ni yeye ambaye alishuhudia mumewe akiuawa mbele ya macho yake.
"Mama kwanza nikupe pole kwa hili ambalo limetokea, najua kwamba upo kwenye hali ya huzuni lakini nakuomba uweze kunisaidia kujibu maswali kadhaa kwani yana umuhimu mkubwa kwa kazi ambayo ipo mbele yetu ukizingatia mtu ambaye amekufa ni mtu mkubwa kwenye taifa hili" mama huyo aliitikia kwa kichwa akiwa anajifuta machozi.
"Unamfahamu mtu ambaye amekuja kumuua mumeo?" mama huyo alitikisa kichwa kukubali
"Siwezi kusema namfahamu moja kwa moja ila nimeiona sura yake kwa sababu wakati anaongea na mume wangu alivua kitambaa chake usoni"
"Sura yake umewahi kuiona sehemu yoyote ile labda?"
"Hapana"
"Umesikia akilitaja jina lake hata mara moja?"
"Ndiyo mume wangu ndiye ambaye amelitaja jina lake kwa mshtuko akiwa anaonyesha wazi kuogopa na ni kama hakutarajia kumuona mtu huyo"
"Jina gani amelitaja?"
"Gavin" Ezra alishtuka kusikia hilo jina, ikamlazimu kuitoa simu yake na kuonyesha ile picha ambayo ilipatikana huko Zanzibar kwenye pasipoti.
"Ni huyu hapa?" Mama huyo aliiangalia kwa umakini japo mtu huyo kwenye picha alikuwa an upara lakini bado alimtambua. Aliitikia kwa kichwa kukubali, Ezra alichoka.
"Mume wako alikuwa ana ukaribu na mtu yeyote ambaye hakuwa wa kawaida au kuna mabadiliko ya kawaida ambayo mumeo alianza kuyaonyesha siku za hivi karibuni?"
"Hapana ila kwa mazungumzo yao ni kama watu ambao wanafahamiana"
"Ni kitu gani ambacho walikuwa wakiongea" mama huyo alionekana kusita kuongea jambo hilo lakini Ezra alimhakikishia usalama wake.
"Amedai kwamba kama mume wangu ningeujua ushetani wake sidhani kama ningeendelea kumchukulia kama ninavyo mchukulia"
"Ushetani gani huo?"
"Amemuuliza mume wangu kwamba ni nani alipiga ile risasi"
"Risasi?"
"Ndiyo"
"Na mumeo amejibuje?"
"Amesita sana kutaja ila baada ya kupigwa risasi ya mguuni ndipo akataja jina la Douglas Shenzi"
"Na alimpiga nani hiyo risasi?"
"Hajasema kuhusu hilo, aliuliza tu kwamba yuko wapi kwa sasa"
"Na mumeo amemjibuje?"
"Kwamba yupo Johernsburg Afrika ya Kusini"
"Kuna kitu kingine labda ambacho umekisikia na sio cha kawaida mama?"
"Hapana ila naogopopa, mume wangu amekuwa mtu mwema siku zote, amesema alifanya kwa shinikizo la mtu ambaye hata mimi simjui ila naomba jina la mume wangu lisije kuwa na dosari nataka apumzike kwa amani, yote niliyo yasikia naamini kwamba hayana ukweli wowote ule"
"Usijali mama nakuahidi haya yatabaki kwangu mimi na wewe kuhusu upande wa mumeo, naomba kwa sasa ukampumzike na watoto wako kwa sababu mnatakiwa kupelekwa sehemu ambayo ni salama" alimpa mkono mama huyo na kurudi ndani tena kwa mara nyingine ambapo miili ilikuwa inafanyiwa uchunguzi ili iweze kupelekwa mochwari.
"Who are you Gavin Luka?" aliuliza swali ambalo alitakiwa kujijibu mwenyewe kwa sababu sauti ilikuwa ndogo na hakuna mtu mwingine ambaye alitakiwa kuwepo hapo. Wakati wakiwa hapo walipokea amri kwamba walitakiwa kuacha kila kitu kama kilivyo kuna watu walikuwa wanakuja muda huo huo kufanya uchunguzi na kuichukua hiyo kesi, alisonya kwa hasira Ezra kwa sababu alijua ni yale yale ya kupokonywa kesi kama ambavyo alifanyiwa mchana wa siku hiyo japo kichwa chake hakikutulia kabisa.
Muda mfupi baadae walishuka watu wawili kwenye gari, wanaume hao walikuwa wamevaa nguo za kawaida za kiraia tu. Waliongea na askari mmoja ambaye aliwaelekeza kwa Ezra.
"Bila shaka wewe ndiye Ezra Ethan" mmoja aliongea akiwa anamwangalia
"Tunafahamiana kabla?" alijibu kwa jeuri naye
"Hakuna umuhimu wa wewe kufahamiana na sisi, tupe maelezo yote kuanzia mwanzo mpaka mwisho ulipo ishia muda huu"
"Hivi nyie mnajiona akina nani labda, kwamba kile kesi mnatoa tu amri kwa watu waondoke, mnajikuta hii nchi ni yenu sio?" Ezra aliongea kwa jazba na watu hao ambao moja kwa moja alijua kabisa wanatoka ndani ya idara ya usalama ya taifa.
"Samahani umesema?" ilisikika sauti nzito ya mwanaume ambaye hakuwa ameongea jambo lolote tangu afike hapo, alimsogelea Ezra karibu na sikio lake na kumng'ata kidogo kwa kumpa haya maneno.

Kuushi ulimwengu wa wababe unatakiwa kuwa na uhakika na kila maamuzi ambayo unayafanya vinginevyo inaweza kula kwako baadae na ukakosa msaada.

Kumi na moja sina la kukuongezea uwe na wakati mwema.
 
Kongore kwa mwandishi
 
Salute FEBIANI BABUYA
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
SONGA NAYO................
"Bwana mdogo hili nitahesabia kwamba halijawahi kutokea ila kama utakuja kurudia siku nyingine kuongea huu upuuzi, nakuhakikishia nitaondoka na ulimi wako" alimpiga piga begani kisha akapitiliza ndani kumuacha mwenzake akabidhiwe taarifa za kila ambacho kilifanyika hapo. Alipewa maelekezo yote baada ya hapo naye akaenda ndani kuungana na mwenzake, alicho kiona kilimfanya kusikitika. Hao wawili walikuwa wametoka kwenye idara ya ujasusi ya taifa, ni miongoni mwa wale watano ambao walipewa kazi na mkurenzi Micho Othman ambao waliambiwa waisimamie kesi ya kuuawa kwa waziri wa mambo ya ndani.
"The same man Gavin Luca"
"Unahisi ni yeye ndiye ambaye amehusika na matukio yote matatu?"
"Yeah ila hayupo pekeyake"
"Ana watu anafanya nao kazi?"
"Inaonekana hivyo na mmoja wao ni huyo kijana ambaye amemuua waziri mchana"
"Kama wapo wengi maana yake inahitajika gharama kubwa kuwaendesha na kuwalipa ili wafanye kazi za hatari kama zile kisha wakawa waaminifu kwake, maana yake tunamtafuta mtu ambaye hana njaa ya pesa"
"Hilo litasaidia nini kwa sasa?"
"Kuwaongoza watu wengi ni kazi ngumu kwa sababu kila mtu huwa ana tabia zake hivyo tunatakiwa kukaa chini tuwe na listi ya viongozi wote hususani ambao wamewahi kufanya jambo lolote la kihalifu huenda ikawa nafasi yetu ya bahati. Kama kweli ana watu wengi maana yake kuna wengine wanaweza kupewa kazi ya kuua wengine hivyo kuna wale ambao huenda wakafanya uzembe hata hatua moja kama nilivyo kwambia kwamba watu wanatofautiana tabia, tukimpata mmoja basi tunakuwa tumewapata wote"
"Unahisi itakuwa rahisi namna hiyo?"
"Najua sio rahisi ila inawezekana"
"Lakini kwanini mtu aue watu kikatili namna hii? Sio bure kuna jambo linaweza kuwa nyuma ya haya yote, binafsi hainiingii akilini"
"Swala la msingi hapa na kujua kwamba ni kwanini amuue makamu wa raisi mstaafu? Kuna sababu zipi hasa za mtu huyu kuingia kwenye listi ya Gavin Luka? Tukiweza kulijua hili basi tunaweza kuzipata taarifa zake nyingi zaidi za mhimu ambazo zitatuongoza ni wapi yeye alipo kwa sasa" ni wanaume wawili wa kazi walikuwa wanabadilishana akili jinsi ya kuweza kumpata mtu wao ambaye alikuwa zimwi jipya nchini, zimwi ambalo linawajua na linawala mpaka wanakwisha. Jaden Mrisho na Crepin Mkono ndio ambao walikuwa eneo hilo wakilichambua hilo tukio baada ya mauaji mengi ya kutisha kutokea.
Asubuhi kunakucha vibaya, habari zingine zinazagaa kila pembe za nchi kuhusu mauaji ya kiongozi huyo mstaafu, watu wanahamaki kuona hali kama hiyo na kutaka kujua sababu ya msingi ya viongozi wao kuanza kupotea mmoja mmoja. Kila chocho, kila mtaa, kila mji, kila chombo cha habari likawa limezagaa jina moja tu GAVIN LUCA. Watu mtaani wakaanza kuchonga mpaka vinyago wakiwa wanajiita jina hilo, watumia fursa wakatengeneza mpaka tshirt zenye jina hilo ambazo kila mtu akawa anazinunua mtaani, kutoka kuwa jina la muuaji mpaka kuwa jina la mtu ambaye mitaa ikawa inamhusudu, kwanini? Kwa sababu alikuwa anadili na viongozi tu ambao wanaanchi walikuwa wamewachoka, hakuonekana kuwa hatari kwa raisi wa kawaida mitaa ikawa inaliimba jina lake mtu ambaye hawakuwa wakimjua ni nani, GAVIN LUCA.

Zanzibar Magharibi,
Kwenye jumba kubwa la kifahari lililokuwa karibu kabisa na fukwe ya bahari ya Hindi, kulikuwa na msiba mzito. Msiba wa baba kumpoteza mwana ambaye hawakuwa sawa lakini pia familia ilimpoteza mpendwa wao wampendae, ilikuwa ni familia ya mzee Ismail Mhammed ambaye alikuwa na ukwasi wa kutosha. Ulikuwa msiba wa binti yake Zara ambaye ilipita miaka miwili tangu atoweke nyumbani na aliacha ujumbe wa kutohitaji kutafutwa kwani angeweza kurudi mwenyewe baada ya kugombana na baba yake mzazi ambaye alihitaji yeye aolewe lakini yeye akagoma kwa kudai anaipenda kazi yake ya uchunguzi.
Wakati anaoneka hakuwa yule Zara tena bali maiti yake, ulikutwa mwili wake hotelini ambako alidaiwa kuingia na mwanaume lakini hakukuwa na haja ya kumlaumu kufanya zinaa kama ilivyo miiko ya dini yake kabla ya ndoa kwani hakuwepo tena duniani. Mwanaume mmoja alisafiri kwenda huko kama maagizo ya mkurugenzi yalivyokuwa kumtaka akapate taarifa zote za huko kwani aliambiwa kwamba ndani ya tukio hilo lilipatikana jina la Gavin Luca na sura yake hivyo alihitaji kujua kama mtu huyo ni yeye kweli alikuwa anahusika kwenye jambo hilo.
Mwanaume huyo baada ya kufika huko alipokelewa na Rama Rajabu ambaye alikuwa ni afisa wa polisi wa kituo cha Kijito Upele Zanzibar Police. Rama alimpatia taarifa zote tangu aanze kuichunguza kesi hiyo mpaka pale ambapo alikuwa ameishia, mwanaume yule alimshukuru kwa taarifa zake na kumuahidi kwamba yeye angeanzia pale kulifuatilia hilo tukio mpaka ambapo wangefanikiwa kuone mwisho wake. Baada ya kumalizana na Rama sasa ulikuwa ni wakati wa kwenda kukutana na mzee Ismail mwenyewe ambaye ndilo lilikuwa moja kati ya lengo lao kuu la kuweza kwenda huko.
Licha ya msiba na kilio ambacho kilitamalaki kila eneo lakini mwanaume huyo aliomba kuweza kuongea na mzee Ismail ambaye hakuwa mzee sana huenda ni kwa sababu ya ukwasi wake mkubwa.
"Mzee wangu sitaki kukupa taharuki, najua kabisa upo kwenye msiba wa mwanao na nakupa pole za dhati kabisa juu ya hilo lakini jambo ambalo limenileta hapa ni suala la usalama wa taifa kwa ujumla" aliongea mwanaume kwa utulivu.
"Wewe ni nani?"
"Naitwa Darwin Masenya, ni afisa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam na kuna huku ni maagizo kutoka juu" Alidanganya jina lake
"Nikusaidie nini bwana Darwin?"
"Wakati mwili wa mwanao unakutwa ndani ya kile chumba, kuna kitambulisho kimekutwa mle ndani na bila shaka ni mtu ambaye ndiye kahusika na mauaji ya mwanao lakini baada ya mwanao kukutwa amekufa asubuhi, mchana wake tena waziri wa mambo ya ndani naye akauliwa na waziri huyo kwa taarifa za haraka ni kwamba alikuwa ni moja kati ya watu wako wa karibu hivyo tunahisi kwamba matukio haya yanaendana na yana uhusiano wa moja kwa moja"
"Nani amemuua mwanangu?"
"Bado hatuna jibu la moja kwa moja lakini ulishawahi kulisikia jina la mtu anaitwa Gavin Luca?" mzee Ismael alionyesha mshtuko wa haraka kana kwamba kuna kitu alikuwa anakiogopa lakini akajikaza na kuwa sawa, ile hali mwanaume yule ambaye alikuwa anamhoji aliiona vizuri ila akatulia kwanza.
"Jina ni geni kwangu, linahusiana vipi na wew kuwepo hapa na kifo cha mwanangu?"
"Tunaamini kwamba ndiye ambaye amemuua binti yako"
"Sasa kwanini msimkamate mpuuzi huyu aweze kusema kila kitu kuhusu huu uharamia ambao ameufanya kwa binti yangu?"
"Mzee bado haujanijibu swali langu"
"Simfahamu wala sijui kama ni yeye ndiye amemuua waziri, nimepata taarifa hizo juu juu tu hivyo nami sijui lolote nataka nimpumzishe mwanangu kwa amani kwa sababu mwili bado unafanyiwa uchunguzi"
"Kuna mtu ambaye uliwahi kuhisi kwamba atakuwa ni adui kwako labda au kwa waziri?"
"Sijui kuhusu maisha ya ndani ya waziri, alikuwa na maisha yake nina maisha yangu na hakuwa rafiki yangu ila ni biashara tu zilikuwa zinatukutanisha hivyo naweza kusema kwamba sina taarifa zozote za maana za mtu huyo kwa sababu hatujawahi kuzungumza kuhusu maisha binafsi kati yetu" mwanaume alitabsamu kusikiliza fiksi za mzee huyo ila hakuwa na mamlaka ya kuweza kumlazimisha.
"Mzee wangu nina zaidi ya miaka kumi kwenye hii kazi, nimedili na kesi nyingi za aina hii naweza kukuhakikishia kwamba kama kuna kitu natakiwa kujua na hutaki kuniambia basi sitakuwa na uwezo wa kukulinda. Hakuna bahati mbaya kwenye jambo kama hili kwa sababu muuaji anaonekana kabisa kwamba kuna watu ambao anawalenga na kama amemuua binti yako hashindwi kurudi na kuua mtu mwingine kwenye familia yako au wewe mwenyewe kukupoteza pia"

Anasakwa mtu asiye julikana, je watampata? Mimi sijui kazi ni kwako kuufuatilia huu wino. Kumi na mbili inafika mwisho panapo majaaliwa tukutane ndani ya sehemu inayo fuata.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
SEHEMU YA KUMI NA TATU
SONGA NAYO................
"Kama kuna jambo lolote nitalijua basi nitakujulisha ila mpaka sasa sina taarifa zozote zile ambazo nazifahamu kuhusu mtu huyo"
"Haina tatizo ila nakukumbusha kwamba ni siku chache mtu huyo inasemekana kwamba aliuawa kabisa lakini baada ya kifo chake wote ambao walikuwa huko walikutwa wamauawa na mtu asiye julikana hivyo kuwa makini mzee wangu" alimpa mkono akiwa anamuachia na kadi yake ambayo ilikuwa na namba kwa sababu alihidi kushirikiana naye pale ambapo angeujua ule ukweli. Alikuwa amedanganya jina ila jina lake la kweli alikuwa anaitwa Slyvanos Deokarius.
Mwanaume huyo hakuondoka eneo hilo kama alivyokuwa ameahidi, bado alihisi kwamba kuna kazi alikuwa anatakiwa kuifanya ndani ya hilo eneo, alijitahidi kuulizia mpaka alipo mpata dada yake na Zara aitwaye Fatima ambaye ilidaiwa kwamba kabla mwanamke huyo hajapotea walikuwa na ukaribu mkubwa. Aliamini angeyapata machache ya kumsaidia kutoka kwa dada mtu.
"Pole Fatima, najua huu sio wakati bora kukutana au kuongea ila ni mhimu kufanya hivyo, kama nilivyo jitambulisha naitwa Darwin Masenya, ni afisa upelelezi kutoka Dar es salaam"
"Karibu afisa"
"Ulikuwa unamjuaje mdogo wako?"
"Alikuwa ni binti mwenye ndoto kubwa, aliamini kufanya kile ambacho alikipenda yeye. Hakutaka kabisa kuingiliwa kwenye maamuzi yake, kuhitaji kuyajua mambo mengi na kujifunza vingi ndiko ambako kulimvuta mpaka akaenda kusomea mambo ya habari na kuamua kuwa mchunguzi binafsi na baadae akaamua kujiendeleza kwenye sayansi ya kompyuta ambayo hakufanikiwa kumaliza"
"Ukiwa naye alikuwa anapenda zaidi kuongelea vitu gani?"
"Alikuwa anapenda zaidi kujipambanua kuhusu ndoto zake, alikuwa anapenda kuelezea ubora wa kazi yake na jinsi ambavyo anatamani dunia imtambue kwenye huo ulimwengu wake"
"Akiwa anafanya kazi yake ya uchunguzi hakuna mambo ya ajabu labda ambayo amewahi kuyagundua au hukuwahi kuona utofauti wowote ule kwenye ufuatiliaji wa hilo jambo?"
"Hapana, ila ni siku moja tu ndiyo aliwahi kuniambia kwamba alipokea simu kutoka kwa mtu asiye julikana ambaye alimpongeza kwa kazi yake nzuri lakini mtu huyo pia alimsisitiza kuwa makini kwani kazi yake ya uchunguzi ingempelekea kuyajua mengi hivyo angeweza kutengeneza maadui wengi zaidi kwenye maisha yake"
"Mlichukua hatua gani baada ya kulijua jambo hilo?"
"Hatukuchukua hatua yoyote kwa sababu alijawa na furaha ya kupongezwa zile changamoto zingine hakuzipa nafasi kichwani mwake kwani alijua kabisa kwamba angekutana nazo"
"Huyo mtu ambaye alimpa tahadhari ulikuwa unamfahamu?"
"Hapana sikuwahi kumjua"
"Alikuwa na mpenzi?"
"Aliwahi kuwa naye na ndiye huyo ambaye waliachana baada ya baba kutaka aolewe naye ila yeye akagoma kwa kudai kwamba muda wa kuolewa bado anataka kutimiza ndoto zake kwanza hivyo waliachana wakati ule baada ya mpenzi wake huyo kutoonyesha uvumilivu kwani alidai anahitaji kuwa na familia na hivyo akaamua kuoa mwanamke mwingine mpaka sasa wana familia"
"Baada ya mdogo wako kumkataa bwana huyo hakuonyesha hasira au kuongea kitu ambacho hakikuwa cha kawaida kwake?"
"Hakupendezwa tu na hali ile kwa sababu alikuwa anampenda mdogo wangu sana ila aliamua kupotezea kabisa na kumuomba baba aoe mwanamke mwingine tu kama mwanae hamtaki"
"Ilikuwaje mpaka akatoroka nyumbani?"
"Hakumuaga mtu yeyote zaidi ya kuacha barua tu na tangu hapo hakuwahi kupatikana tena mpaka ilipokutwa maiti yake"
"Wewe ulikuwa mtu wake wa karibu kuliko wote, tangu aondoke hakuwahi kukutafuta labda kukwambia yuko wapi na anafanya nini?"
"Hapana hajawahi, namba zake zote hazikuwa zikipatikana kabisa na hakuwahi kunitafuta wala sikuwahi kujua yuko wapi"
"Asante kwa maelezo yako Fatima yatanipa muongozi mzuri kwenye uchunguzi wa kifo cha mdogo wako na haki yake itapatikana" Fatima aliitikia kwa kichwa tu kukubaliana na afisa huyo.
"Naomba unisaidie taarifa za huyo aliyekuwa mpenzi wake nina mazungumzo naye mafupi kisha nirudi kuendelea na majukumu ya hii kesi yangu" haikuwa tatizo, alipewa taarifa zote ambazo alikuwa anazihitaji akaondoka eneo hilo.

Ilikuwa ni tofauti kabisa na yale maelezo ambayo alikuwa ameyatoa, mzee Ismail aliingia ndani ya chumba chake akajifungia huko akiwa anahema kwa nguvu, moyo haukuwa wake, mapigo yalikuwa yanaenda kasi mno mithili ya mtu ambaye anafukuzwa. Lile jambo alilo ambiwa na jina ambalo alitajiwa lilimpa homa ya ghafla, alikuwa anajiangalia ukutani kwenye kioo akiwa haamini. Aliitoa kofia iliyokuwa kichwani kwake na kuitupia mbali, alichukua simu ndogo kwenye droo yake na kuiwasha, alipiga simu hiyo mahali ila aliambiwa kwamba namba ambayo alikuwa anapiga wakati huo ilikuwa haipatikani, alisonya na kuibamiza simu hiyo chini mpaka ikapasuka.
"Haiwezekani, haiwezekani. Gavin Luca amekufa haiwezekani aonekane kuwa hai tena ndiye ahusike na mauaji ya mwanangu! Hapanaaaaaaa" aliongea kwa jaziba akiwa anasambaratisha hovyo vitu ndani ya kile chumba. Haikujulikana sababu ya msingi ya yeye kuliogopa sana hilo jina la Gavin Luca na alipinga kwamba mtu huyo hawezi kuwa hai mpaka muda huo, alionekana kumjua vyema kama sio kwamba walikuwa wanajuana vyema. Ikabaki ni kiulizo kizito Gavin Luca ni nani?

KENYA
MAU FOREST
Kama kawaida wanaume wawili kutoka ndani ya idara ya kijasusi ya Tanzania walikuwa wametumwa huko Kenya na mkurugenzi kwa ajili ya kupata ukweli ambao ulitokea huko kwani majibu pekee ambayo aliyapata kutoka kwa Sarah Martin hayakuwa yakijitosheleza hata mkuu wa majeshi hakumpa kabisa ushirikiano hivyo alihitaji vijana wake wakakusanye hizo taarifa ambazo zingeweza kuwasaidia kutoka huko.
Walisafiri kutoka Tanzania mpaka ndani ya msitu huo, wanaume hao waliingia kama ambavyo maagizo yalikuwa yanawataka wafanye, walikuwa na ramani nzima ya eneo ambalo lilidaiwa kuwepo kwa matukio yale ambayo yalitokea hivyo hawakuahangaika kuweza kufika japo ilikuwa ni ndani mno ya msitu na walifika huko majira ya usiku mzito wa manane. Msitu ulikuwa unatisha, kulikuwa kimya hata ndege hawakuwa wakisikika kabisa, ilihitaji roho zaidi ya ngumu kufanikiwa kuingia eneo kama hilo tena usiku wa manane kama huo lakini Tigana Mdachi pamoja na Bariki Dumba waliingia huko usiku ikiwa ni kama hatua ya kutaka kukusanya taarifa juu ya mtu ambaye alikuwa anaitwa Gavin Luca.
Hawakuwa wenyeji ndani ya msitu huo hivyo iliwachukua masaa zaidi ya mawili kuweza kufika eneo ambalo ramani ilikuwa inawaelekeza kwamba ndipo ambapo walikuwa wanatakiwa kuwepo.
"Huyu alikuwa binadamu au jini? Kwamba kuna binadamu alikuwa anaishi mwenyewe ndani ya eneo kama hili?" Tigana aliuliza akiwa anamulika tochi kila kona ya hilo eneo na kumshangaa mtu ambaye alidaiwa kwamba alikuwa anaishi ndani ya eneo ambalo lilikuwa linatisha kama hilo.
"Hata mimi hii hali imenishangaza, wanadamu tuna uvumilivu na mambo ya ajabu lakini huwa tuna mipaka, sasa mtu kuvuka ile mipaka ambayo kiubinadamu ndiyo inatuongoza linakuwa jambo la ajabu. Kuna namna atakuwa hana roho ya kibinadamu tena ndiyo maana iliwezekana kwake na akachukulia kawaida huku" Bariki naye hakuwa nyuma huku macho yake akiwa ameyaangaza kwenye ramani ambayo aliitandika juu ya jiwe kubwa.
"Kuna uwezekano mkubwa hana nafsi yake ilishahama kutoka kwenye ubinadamu na kuwa kama mnyama wa kufugwa ambaye hana huruma tena na mtu"
"Nafikiri tupo eneo la tukio, ni hapa hapa hivyo tutafute ilipo nyumba ambayo inadaiwa kwamba ilikuwepo hili eneo" Tigana aliongea akiwa anaikusanya ramani na kuirudisha kwenye begi kisha akaliweka begi hilo mgongoni kwake. Wakiwa wanaanza kutembea Bariki kuna kitu alikimulika kikamuumiza macho mpaka akapatwa na mashaka, alimulika vizuri eneo lile na kugundua kwamba chini kulikuwa na shilingi ambayo ilikuwa inatumika miaka ya zamani lakini ilikuwa imetunzwa vyema kama ilitoka benki siku hiyo.

Sehemu ya kumi na tatu inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA
 
Back
Top Bottom