STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
SONGA NAYO................
Kwenye historia yake mama huyu kuna mambo kadhaa ambayo aliwahi kuyafanya, nafasi ambazo alikuwepo zilikuwa zinamfanya kukutana na watu wengi kwa sababu za wengine kuhitaji msaada na huruma zake lakini wengine walikuwa wanadai haki zao. Dunia ni kijiji na saa ni muongozo sahihi, kila unacho kifanya unapokuwa kwenye nafasi fulani basi ujue kwamba kuna siku kitakuja kurudi kwa namna moja ama nyingine, haijalishi utakuwa tayari kwa wakati huo ama hautakuwa tayari ila lazima kirudi tu kwa wema au kwa ubaya.
Mwanamama huyo alikuwa akiishi eneo la SAI barabara ya kwenda ITUHA, alikuwa akiishi yeye na familia yake yote maeneo hayo baada ya kustaafu na ni watu wachache ambao walikuwa wanajua ni wapi anaishi mama huyo kwa sababu za kiusalama. Alikuwa na jengo lake kubwa la gharama ndani ya eneo hilo akiamini kwamba angefia huko kwa amani lakini haikuwa kweli, dunia haikuwa imesahau aliyoyafanya ule wakati wake ambao alikuwepo kwenye nafasi kubwa serikalini.
Usiku alipokea ugeni wa watu kadhaa, watu hao walifika kwake ghafla na hakuwa na kumbukumbu kama aliwahi kuwaelekeza watu hao kwamba ni wapi yeye alikuwa akipatikana hivyo hapakuwa pema sana. Baada ya kufika hiyo sehemu, mwanaume mmoja ambaye alikuwa na umri wa makamo alimtaka mama huyo akae naye nje ya nyumba hiyo alikuwa na mambo kadhaa ya kuweza kuongea naye huku ndani akiwaacha wanaume kadhaa ambao hawakuonekana kuwa wema. Mwanamama huyo alikuwa mwingi wa wasiwasi, huenda alikuwa akiwafahamu watu hao vizuri ila kwa sababu ya kuilinda familia yake alikubali kwenda kumsikiliza bwana huyo.
"Emily imekuwa kitambo sana tangu siku ya mwisho mimi na wewe tuweze kuonana, bila shaka maisha yanaenda kasi isivyokuwa kawaida. Ni zamani sana tangu mimi na wewe tukae sehemu kufanya maongezi na wakati ule bila shaka ni mimi ambaye nilikuwa nakuomba unipe msaada japo kwa kuringa sana ila ulifanya hivyo bila shaka unakumbuka miaka ile"
"Nakumbuka, unaweza kuniambia kwamba ni kipi kimekuleta kwangu bila hata kukaribishwa?"
"Emily huwa unatambua kabisa kwamba mimi sio mtu ambaye napenda kupoteza au kupotezewa muda wangu hivyo kama ukiniona sehemu basi ujue kuna jambo la mhimu limenileta, isingekuwa hivyo basi usinge niona hapa"
"Unataka nini?"
"Gavin Luca yupo hai"
"Whaaaaat?"
"Nina uhakika umenisikia vizuri"
"Utakuwa umechanganyikiwa"
"Umesikia mpaka hotuba ya raisi halafu unasema nimechanganyikiwa"
"Najua kabisa yule mpuuzi anapika taarifa zile kwa maslahi yake"
"Hii haihusiani na raisi ila nakuhakikishia kwamba Gavin Luca yupo hai"
"Yule mtoto alikufa muda mrefu"
"Hapana aliyekufa alikuwa mwingine, Gavin Luca alikuwa bado mzima wa afya ni miaka mitano ilitopita ndipo aligundulika kwamba ni mzima wa afya kabisa na baada ya hapo tulianza kumtafuta kwa nguvu. Alipatikana huko Kenya akauawa lakini jambo la ajabu ni kwamba akaonekana tena na anafanya mauaji ya kikatili mno kwa watu wetu wote wa zamani"
"Aliuawa halafu yupo hai?"
"Nadhani aliye uawa ni mtu mwingine"
"Kivipi?"
"Hilo hata mimi sina jibu lake"
"Kwa hiyo mimi nakusaidiaje sasa hiyo ni kazi yenu nyie kupambana naye"
"Hapana Emily mambo hayaendi hivyo"
"Unamaanisha nini?"
"Nahitaji ukimya wako"
"Mimi sijawahi kuongea jambo lolote sehemu yoyote ile sasa ukimya wangu unahusikaje? Hata hivyo hakuna mtu ambaye anajua kwamba mimi bado nipo Tanzania na ninaishi huku Mbeya"
"Kama ingekuwa hivyo basi hata mimi nisingekupata maana ulikimbia bila kutuaga Emily"
"Do you wanta to kill me?" mwanamama huyo aliuliza kwa mshangao baada ya kuona watu wake mwenyewe ambao aliwafanyia kazi kubwa miaka ya huko nyuma wanataka kumuua.
"Yes, Emily"
"Why?"
"Nadhani unaelewa namna kazi hizi zinavyo enda, kama ukiwa hai Gavin atakuja kukupata siku moja kwa sababu hatujui anaishi wapi mpaka sasa, kama akikupata wewe basi atajua kila kitu hata ambacho hatakiwi kukijua hivyo you need to go Emily"
"Siwezi kuruhusu huo upuuzi ufanyike kwangu, nilikubali kuharibu utu wangu kuwasaidia leo unataka kuniua mimi, Noooooooooooo"
"Utachagua wewe au familia yako, ukiamua kumalizana na mimi basi familia yako itakuwa salama lakini kama ukikaidi hilo basi nitaua familia yako yote na unawajua wale jamaa ambao tumewaacha kule ndani wanasubiri kauli yangu tu waingie kwenye kila chumba kuua kila aliye mle ndani na wanao ambao wanasoma nje ya nchi nina uhakika unajua kabisa kwamba kuwafikia ni suala la masaa tu"
"Sikutegemea mngekuwa washenzi namna hii, hili linaenda kuwa doa kubwa sana kwenu kwa sababu watu wenu watapoteza imani kwa kuamini kwamba mnaua watu wenu wenyewe"
"Sio kweli kwa sababu hakuna mtu atajua kama ni sisi tulihusika kukuua"
"Unamaanisha nini"
"Unatakiwa kujiua mwenyewe Emily kwa kujipiga risasi kichwani"
"Whaaaaaat?"
"Umenisikia vizuri" mwanaume huyo alimrushia mama huyo silaha na kumwangalia kwa umakini.
"Ilikuwa vyema kufanya kazi na wewe Emily, kama kuna maisha mengine basi tutakutana huko tukachomwe wote moto kama vitabu vya dini vilivyo andika" aliongea na kuanza kuondoka hilo eneo akimuacha mama huyo analia machozi ya uchungu mno. Watu wake ambao walimfanya afanye mabaya wakati wa utumishi wake ndio ambao walikuwa wameenda kumuua mwisho wa siku huku akiwa na chaguo la kujiua yeye ama aachwe hai ila familia yake yote ife. Majuto ni mjukuu, ulisikika mlio wa risasi nyuma wakati wanaume hao wanatoweka kwenye hilo eneo kwa ajili ya kuilinda siri isiende kwenye mikono ya Gavin Luca.
PEENUGA GOLDEN RING.
Ndani ya ule ulingo ndiko ambako Lucas aliweza kutengeneza jina, huenda unajiuliza ilikuwaje mpaka akapata jina ndani ya ile sehemu. Ushapu na ujanja wake na kutokuwa zoba ulimfanya aaminike na kuanza kutumika kuuza madawa hata akiingia mle ndani, wakati wengine wakiwa wanafurahia watu wakitoana damu na uhai yeye alikuwa akichangamkia fursa kwa kuuza sana madawa kwa watu mle ndani ambao walipenda kupata vibe jipya na kelele zinakuwa nyingi.
Kwenye mizunguko yake ya kila ambapo kulikuwa na ngumi alikuwepo mle ndani ndiko kulimkutanisha na bwana mmoja ambaye alikuwa ni mtu wa Mexico huko. Gustavo Gaviria, huyu alikuwa ni mtu kutoka Mexico ambaye kwa miaka mingi alikuwa ni msambazaji mkubwa wa dawa za kulevya ndani ya taifa la Marekani lakini baada ya muda aligundulika na serikali hiyo ikaanza kumtafuta kila kona ndipo akaamua kuhamisha njia zake za usafirishaji kwa muda mpaka pale ambapo mambo yangeenda sawa angeweza kurudi kwenye njia zake za zamani. Hapo ndipo aligundua soko jipya ndani ya Afrika kwa sababu watumiaji wa dawa za kulevya walikuwa wakiongezeka lakini alikuwa akiitumia njia ya Afrika kusafirishia dawa zake za kulevya kutokea Afrika kwenda kwenye mataifa mengine ya Afrika hususani Afrika ya kusini na nchi za bara la Asia kama China na India.
Kwa sababu ya kutafutwa kwake sana ndipo alijikuta anaishia ndani ya mitaa hiyo ya Peenuga na ndiye ambaye alikuwa anawamiliki wauzaji wengi wa dawa za kulevya ndani ya mitaa hiyo. Soko zima lilikuwa kwenye mikono yake kwa sababu Tanzania lilikuwa kama tawi lake tu ila alikuwa na masoko kila pembe ya ulimwengu. Kujituma kwa Lucas ndiko ambako kulimfanya mtu huyo amuone bwana mdogo ambaye alionekana kuwa na njaa kali ya mafanikio akiwa anazunguka ndani ya ukumbi huo wa kutisha wa mauaji na ndipo safari ya maisha ya Lucas ilipo anzia hapo.
Lucas alichukuliwa na mwanaume huyo moja kwa moja na kuanza kumtumia kwenye biashara zake taratibu, Lucas ndiye ambaye alikuja kuwa kijana wa Gustavo ambaye alianza kumuamini sana kwa sababu hakuwahi kwenda naye kinyume hata siku moja na alikuwa anamsikiliza zaidi yeye. Robert Greene kwenye kitabu chake cha 48 Laws of Power emeandikwa hizo laws zake, law ya kwanza inasema "Never outshine your master" hiyo ndiyo ilikuwa silaha kubwa ya Lucas, alimtii bosi wake na kuwa mwaminifu kwake, kadri muda ulivyokuwa unakatika ndivyo ambavyo maisha yake yalikuwa yanabadilika taratibu.
Lucas hakuwa fala, wakati wote huo alikuwa anaisoma mifumo kwa umakini sana juu ya hiyo biashara, Lucas alikuwa akiutumia muda wake mwingi kujua namna ambavyo bosi wake anafanya biashara hiyo na uaminifu wake ulifanya yeye kuanza kusimamia biashara za Gustavo ndani ya Tanzania lakini baadae mpaka Afrika nzima. Ni yeye pekee ambaye alibahatika kupata nafasi ya kusafiri na Gustavo kila pembe ya dunia mahali ambapo wangehitajika kwenda, kwanini? Haikuwa tu kwa sababu yeye ni muaminifu bali uwezo wake wa kufanya biashara na kumwingizia bwana huyo pesa nyingi.
Lucas ikawa habari nyingine, Lucas hakuwa yule maskini ambaye hakuwa na uwezo wa kulipa bili za hospitali, taratibu jina lake likaanza kupenya kwenye maskio ya watu hususani watanzania, tajiri mpya akawa ameongezeka nchini. Baada ya muda mrefu kupita Lucas akaanza kwenda mwenyewe Mexico kumuwakilisha bosi wake, biashara za Gustavo zikawa zinasimamiwa na Lucas ambaye aliaminika kuliko mtu yeyote yule. Madawa ya kulevya yalimsafirisha mpaka Kolombia ambako alikutana na magwiji wengi wa biashara hiyo, biashara hiyo ilimkutanisha na CARTELS nyingi sana za uuzaji wa dawa za kulevya huko Mexico, dawa za kulevya zilimpa watu wapya mpaka ndani ya nchi ya Pakistani ambako kulikuwa njia mpya na salama kwa biashara hiyo.
Kwa sababu Gustavo bado Marekani walikuwa wakimuandama, biashara zake nyingi zikawa zinasimamiwa na Lucas, mikataba ya pesa yote ikawa inasimamiwa na Lucas huku Gustavo akila matunda ya kukutana na kijana huyo lakini Lucas hakuwa fala. Lucas alihakikisha amesoma kila engo ya mchezo mzima jinsi unavyo chezwa, alihakikisha anaijua mifumo yote ya biashara hiyo kwa muda mrefu tangu akiwa kijana mpaka alipofikisha miaka thelathini akawa anajua kila kitu na pesa zilikuwepo za kutupa. Ndipo akaamua kuhitaji kuwa mtawala wa hizo biashara yeye mwenyewe, alihitaji kila kitu akisimamie yeye na kiwe chini ya mikono yake ndipo akapanga safari ya mauaji kwa Gustavo, bosi wake.
Mwanaume akili yake ilikuwa inawaza pesa tu, unahisi atafanikiwa kumuua kiongozi na mfanya biashara mkongwe wa madawa ya kulevya ambaye ndiye alimuonyesha njia zote? Nini hatima ya mtafutaji huyu? Ishirini na tatu niseme bye bye.
FEBIANI BABUYA.
Sent from my SM-A107F using
JamiiForums mobile app