FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #101
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA THELATHINI
SONGA NAYO................
JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI.
JOZI ndilo jiji kubwa zaidi ndani ya nchi ya Afrika ya kusini, ni jiji la kale sana ambalo linadaiwa kugunduliwa mnao mwaka wa 1886. Kinacho lipa zaidi umaarufu jiji hilo ni biashara ya dhahabu pamoja na mzunguko mkubwa wa fedha kiasi kwamba likapewa jina la JIJI LA DHAHABU (GOLDEN CITY).
Jozi ni ndilo jiji kubwa zaidi ndani ya nchi hiyo lakini pia ndilo jiji tajiri zaidi, utajiri wake unapambwa zaidi na biashara kubwa ya madini ambao ndio msingi mkuu wa kuendelea na kufanikiwa kwake. Taifa hilo limefikia hatua linaanza kupoteza ile ladha ya kuitwa Afrika kwa sababu ya mchanganyiko wa rangi zilizopo ndani ya taifa hilo. Ni taifa kubwa kibiashara duniani hivyo huvutia watu wengi ndani yake kiasi kwamba hata wale wazawa wanaanza kupoteza nguvu kubwa ambayo inachukuliwa na wazungu, waasia, na wamarekani kwa kiwango kikubwa.
Kuvutia kwake watu wengi kumefanya pia ndani ya nchi hiyo hususani kwenye hilo jiji kuwepo kwa matukio mengi ya kutisha hususani mauaji, watoto wa mama hawahitajiki kwenda kuishi huko kwa sababu wanahitajika wanaume zaidi. Hali hiyo imefanya sehemu hiyo kuwa kivutio kwa watu wengi ambao wanajishughulisha na shughuli haramu pia kujiingiza huko kwani wanaamini kuna fursa nyingi za maisha. Kuna watu huko huwa wanabahatika kufanikiwa lakini wengine huishia kufanyiwa unyanyasaji na hata kuuawa.
O.R. Tambo International Airport ambao ndio uwanja mkubwa zaidi wa ndege ndani ya hilo jiji, usiku ulipokea ugeni wa msafiri kutoka Tanzania. Bwana huyo uso wake ulipo onekana kutoka nje ya uwanja wa ndege, alikuwa ni bwana Mike Tores ambaye alimuaga mkewe Singida kwamba anaenda kibiashara Botswana. Uso wake ulikuwa umejaa ndevu, mwili wake ulifunikwa na kanzu safi ya kumtoa mashakani kutoka kwa mtu yeyote ambaye angemtazama. Kichwani alikuwa na barakashea ya kukamilisha mtazamo wa imani yake, mtu wa maana kabisa.
Bwana huyo aliingia kwenye nchi hiyo kama mfanya biashara wa madini na alikuwa na vibali vyote halali kabisa ndiyo maana hakupata pingamizi yoyote wakati anafanyiwa ukaguzi ndani ya uwanja wa ndege. Alifikia kwenye hoteli ambayo ilikuwa umbali mfupi tu kutoka ulipo uwanja wa ndege huo, Airport Inn and Suits Isando. Hakuwa anabahatisha kila kitu chake kilikuwa kinaenda kwa mahesabu makali.
Hakwenda Afrika ya kusini kuuza sura au kupoteza muda, hakwenda Afrika ya kusini kushangaa namna jiji la Jozi lilivyo bali alikwenda huko kumtafuta mtu wake, kuna mtu alikuwa ana shida naye kwa muda mrefu kwenye maisha yake, mtu huyo alikuwa ana historia naye mbaya isivyokuwa kawaida. Ilipita miaka mingi akiwa anamtafuta bila mafanikio, kwa mara ya kwanza alipata kuzijua habari za anapo patikana bwana huyo, asingemuacha aende kirahisi, alikuwa na mengi ya kuongea naye mezani kama wanaume lakini alijua kabisa sio rahisi kumpata mtu kwenye jiji kubwa kama hilo ambalo unakuwa hujui uanzie wapi ila kwake alijua ni sehemu zipi anatakiwa kupita. Ilikuwa ni lazima ampate bwana mkubwa Master G.S.
Mitaa ya Jozi imechangamka kwa masaa ishirini na manne ya siku, hilo likawa faida kwake Mike. Alijua muda wowote angeenda popote kufanya kile ambacho anakihitaji lakini haikuwa rahisi kama ambavyo alikuwa anahisi yeye, mwanaume ambaye alikuwa anaenda kudili naye wakati huo hakuwa wa kawaida. Ulikuwa msimu wa baridi, majira ya usiku huwa kunakuwa na baridi maeneo hayo hivyo mwanaume huyo alijua kabisa muda kama huo magenge mengi mtaani huutumia kwa ajili ya kutumia vitu vizito kama madawa ili kuipa miili joto, kazi yake ingeanzia hapo.
Alibeba mabunda kadhaa ya pesa na kutoka ndani ya hoteli ambayo alifikia, walimsihi kwamba wamsaidie na usafiri wa hoteli kwa sababu kwa mgeni kama yeye usiku angepata changamoto mtaani lakini aliishia kutabasamu tu na kuhitaji kuelekezwa tu ilipo club ndani ya hilo eneo, kazi yake ilikuwa inaenda kuanzia huko.
CHEEKY TIGER
Ni moja kati ya night clubs maarufu sana jijini hapo ambazo zipo wazi kwa masaa ishirini na manne, ni club ambayo ilikuwa maarufu hususani kwa upatikanaji wake wa wanawake ambao wanafanya biashara ya kuuza miili yao na kutoa burudani, wao wanawaita striper kwa kiswahili unaweza kusema tu malaya au wanawake ambao huwa wananengua kwenye steji wakiwa nusu uchi kwa ajili ya kuwavutia wanaume ambao wanawaangalia kwa lengo la kujipatia pesa.
Umaarufu wa club hiyo na yale ambayo yalikuwa yanaendelea ndani yake kilitumika kama kivutio kikubwa kwa vijana wengi na watu wengi hivyo kufanya eneo hilo kujaa watu wa kila namna, baada ya kupata taarifa za Club hiyo Mike aliamua kutembelea eneo hilo ambalo aliamini kwamba angeweza kupata Abc za kile ambacho kilimpeleka ndani ya hilo jiji. Mitaa ilikuwa tulivu, ulikuwa usiku wa manane, ni jiji tu lilikuwa linavutia kwa namna lilivyokuwa linawaka na kuonyesha umaridadi wake kila kona.
Alijongea mpaka ndani ya eneo hilo ambapo mara ya kwanza aligomewa kwa sababu alikuwa mgeni lakini haikuwa shida, pesa alikuwa nayo. Alimpatia mlinzi randi 1000 akaruhusiwa kuingia tena kwa heshima kubwa, pesa inaongea watu hawataki maneno mengi. Ndani kulikuwa kumechangamka isivyokuwa kawaida, watu walikuwa wakila maisha na kuzisahau shida zao wote kwa muda, humo ndani hakuna mtu alikuwa anazikumbuka shida zake tena bali ni raha tu zilitawala huku wakiamini matatizo huwa yanajileta yenyewe.
Kulikuwa na jukwaa upande wa mbele, lilikuwa kubwa ambalo lilinakishiwa vyema likawa linavutia kwa mbadilishano wa taa mbalimbali ambazo zilikuwa zinawaka eneo hilo, kuvutia kwake hakukuchagizwa tu na zile taa, lahasha! Bali maua mazuri ambayo yalikuwa yakionekana kwenye zile taa, wanawake walikuwa wamevaa vibikini tu, wengine matiti yakiwa nje kuupa ulimwengu maraha, watu walikuwa wanaweuka kila wanawake wale warembo walipokuwa wanayakata mauno.
"Sawubona mngani!" Mike alishtuka baada ya kusikia hayo maneno, ni baada ya kupamiana na mtu, alimaanisha hello rafiki huku akiwa anacheka.
"Sawubona mngani, ngiyisihambi lapha (safi rafiki mimi mgeni hapa)"
"Hahaha ngiyakubona nje (Hahaha nimekuona tu). Uphuma kuphi? (unatokea wapi?)"
"Ngivela eKenya (natokea Kenya)
"Wenzani lapha"
"Ngidla ubumnandi"
"Ake ngihambe ngiyokukhombisa lapho kukhona ubumnandi"
Mike hakuonekana kuwa mgeni ndani ya ardhi ya Mandela, alipamiana na mtu ambaye alikuwa anamuongelesha Kizulu naye alikuwa anajibu bila papara lakini hakuonekana kuwa mzulu kwa sababu hao watu lafudhi yao inaendana na hata asili yao inaendana ndiyo maana alidanganya kwamba anatokea Kenya. Bwana huyo alimuuliza kama ameenda kufanya nini ndani ya nchi hiyo akadai kwamba ameenda kura maraha ndipo akamtaka amfuate ili amuonyeshe raha zilipo.
Licha ya sauti kubwa ya mziki na kelele ambazo zilikuwepo humo ndani lakini bado walielewana vizuri, bwana huyo alitangulia akimtaka Mkenya amfuate sehemu ambayo aliahidi kwamba angepata maraha ya kutosha. Walipita eneo lile mpaka walipofika kwenye korido moja kubwa, huko kulikuwa na bar nyingine kubwa, walikaa watu na warembo wakila raha wengine wakiendelea kutumia madawa ilimradi kila mtu kile ambacho kilikuwa burudani kwake.
Upande wa mbele kulikuwa na mlango mkubwa, waliingia humo, eneo hilo lilikuwa limepambwa kuliko nje, kulikuwa na sofa kubwa mbili na kitanda ambacho kilizungukwa na maua. Kitandani alikuwepo mwanamke mmoja mrembo sana akiwa uchi kabisa. Bwana yule alimuahidi Mike kwamba angerudi muda mfupi ambao ungefuata akimuacha ale raha ambazo alikuwa anazitaka. Baada ya kutoka mrembo yule alimsogelea Mike na kuanza kukatika akiwa hana nguo hata moja lakini mwanaume huyo alimzuia, alimtolea bunda la pesa na kumtaka akae chini kwani alizihitaji taarifa na kama mwanamke huyo angezitoa basi bunda zima la pesa ambazo angezipata kwa mwaka mzima alikuwa anazipata ndani ya dakika kadhaa tu.
"Sipo hapa kwa ajili ya kufanya mapenzi na wewe bibie, nipa hapa kuna mtu namtafuta" aliamua kutumia kiingereza ambacho alijua wote wataelewana vizuri. Mwanamke yule alionekana kusita sita ikabidi atembee mpaka mlangoni akaurudishia, hakuwa tayari kuliacha bunda la pesa kama lile liende ambalo alikuwa anatakiwa kukusanya pesa za mwaka mzima ndipo alipate. Alimwangalia Mike kwa umakini akachukua shuka na kujifunika.
Sehemu ya thelathini inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app