FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #161
Unamalizia 2500 tu nakupa ilipo ishia mpaka mwisho...
WhatsApp au kawaida
0621567672
WhatsApp au kawaida
0621567672
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona tangu mwanzo nilisema itaisha hapa mdogo mdogo.Kwo mkuu ndo hailetwi tena humu.
YesHee kumbe inauzwa
AmenGod blessing you.
Sogea hapa now uwatag na wengineFabi, nakuita TENA fabi, umefia wapi? Alaa!
Watag na wengine, naweka episodes za kutosha hapaMwendelezo ln kiongoz
🪑🍜STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
SONGA NAYO................
“Sina maana hiyo”
“Ila”
“Gavina anaweza kuwa anatumia njia ambayo sio sahihi lakini binafsi nahisi anafanya kitu sahihi kwa maslahi ya wengi ambao hawawezi kufanya”
“Kwahiyo unataka tumwangalie afanye hiki anacho kifanya?”
“Dayana Comon, taifa linawahitaji watu kama hawa”
“Mbona umekuwa mlaini siku hizi Tigan nini kinaendelea kwako?”
“Nisikilize vizuri, huyu mtu inatumika nguvu kubwa kumpoteza kwa sababu anayagusa moja kwa moja maslahi ya watu fulani. Hili sio jambo la kuwa na ulaini ila ni kufanya kile ambacho ni sahihi”
“Unalijua jukumu lako ambalo lilikufanya ukala kiapo?”
“Ndiyo”
“Ni lipi?”
“Kuilinda nchi yangu pamoja na raia wake kwa gharama yoyote ile hata kuyatoa sadaka maisha yangu, amani ndiyo inapaswa kuwa kipaumbele namba moja”
“Kwa haya ambayo yanaendelea unaona yanaleta amani?”
“Hapana”
“Kwa sababu hiyo tunakubaliana kwamba Gavin anatakiwa kupatikana kwa gharama yoyote ile hivyo sitategemea kupata mawazo ya namna yako tena na kwa sasa huo mjadala unatakiwa kufa. Gavin lazima apatikane, awe amekufa au yupo hai, haiwezekani kila siku watu wakose amani kwa sababu ya kufanya mauaji ya hadharani. Japo inadaiwa kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kupigana naye ila nina uhakika hatakuwa na uwezo wa kuikimbia risasi hata kama atakuwa na uwezo wa ajabu namna gani na kama italazimu tufike huko basi nitamuua mimi mwenyewe kwa mkono wangu”
Dayana aliongea kwa msisitizo kuonyesha kwamba alikuwa anamaanisha kile alichokuwa anakizungumza, Tigana hakuongeza neno tena japo aliona kabisa bwana huyo alichokuwa anakifanya alikuwa sahihi ila ni wao ambao walikuwa wakijaribu kumfanaya aonekane ni mkosaji ama anafanya kitu kibaya.
*********
THE ERA OF GAVIN LucA
Wakati dunia inalalamika kukutana na mambo ya kutisha hususani ndani ya taifa la Tanzania, kwenye chumba kimoja alionekana mwanaume mmoja akiwa ameyafumba macho yake akiwa anafanya sala. Alikuwa amekaa chini ya zulia moja safi kwenye chumba ambacho kilikuwa kitupu zaidi ya kuzungukwa na silaha za kutosha ukutani, alitumia nusu saa nzima akiwa amefumba macho yake, alipokuja kuyafumbua yalikuwa mekundu na katikati ya mboni zake moto ulikuwa unawaka. Alikuwa anauangalia mshumaa ambao ulikuwa mbele yake mithili ya mtu ambaye alikuwa anafanya tahajudi na baada ya muda mfupi macho yalirudi kwenye hali yake.
Mwanaume yule alikuwa ni Gavin Luca mwenyewe ndiye ambaye alikuwa kwenye hicho chumba, kwenye mwili wake alikuwa amevaa suruali nyepesi tu na kujifunga kitambaa kichwani, sehemu zingine za mwili zilikuwa wazi kabisa bila kufunikwa na kitu chochote kile. Baada ya kukamilisha salamu yake alisimama, mwili ulikuwa unavutia kuuangalia lakini ulikuwa unatisha kama ni mtu ambaye ungeingia naye kwenye matatizo kwa namna ulivyokuwa umejigawa kwenye mapande mapande. Mwili haukuwa mkubwa sana ila ulijengwa vyema na mhusika, ulipangiliwa kiasi kwamba ukawa ni wa kuvutia.
Baada ya kusimama alisogea kwenye ukuta na kufungua kisanduku kidogo ambapo alitoa sarafu moja ya shilingi na kuirusha juu, aliidaka na kuirushia ukutani sehemu ambayo ilikuwa na kitufe cha kubonyeza. Shilingi iligonga sehemu ile milango ikafunguka, kwenye vile vyumba vidogo zilikuwa zinahifadhiwa roboti ambazo yeye alikuwa anazitumia kufanyia mazoezi. Zilitoka zikiwa na mapanga kwenye mikono ya chuma na kuanza kumshambulia kwa nguvu Gavin, alirudi nyuma na kuzunguka hewani na kuzifanya zipishane.
Zilikuwa zinamjia kwa kasi mno kwa sababu zenyewe zilikuwa zikitumia umeme yeye damu ila alionekana kuwa na kasi zaidi hata ya zile roboti, aliona kwa jicho lake upanga ukiwa unakuja kwenye shingo yake, aliizungushia pembeni na kujivuta, aliituma ngumi yake iliyotua kwenye moyo wa chuma wa roboti moja likapelekewa mbali huku lingine likiwa linakuja kwa kuzunguka kila sehemu ili kumshambulia, mwanaume huyo alibendi mpaka chini kisha alinyanyuka kwa nguvu za ajabu kama anataka kupaa juu, alijigeuza hewani na kuzungusha mguu wake uliokuwa peku, ulitua kwenye kichwa cha lile roboti mpaka kikameguka wakati ule alitua karibu kabisa na ukuta, aligusa kwa kidole ukutani pakafunguka, aliutoa upanga mmoja kwa nguvu kutoka kwenye ala yake.
Hakutazama nyuma bali aliutuma ule upanga bila hata kuangalia, wakati anautuma yeye mwenyewe alikuwa anaujia kwa nguvu, ulikita kwenye tumbo la roboti na kuzama kidogo wakati roboti lile linahangaika kuutoa alikuwa amelifikia ambapo alilitwisha ngumi nyingi za kifua mpaka likadondoka chini na kuzima kama limeisha chaji. Lile moja lilisogea kwa nguvu alipokuwepo Gavin, alisikika akipiga kelele ambapo aliikunja ngumi yake macho yake yakiwa kama yanawaka moto, alipoikutanisha ngumi hiyo kwenye mwili wa wa chuma wa lile roboto, lilimeguka vipande vipande yeye akibaki anahema na jasho linamtoka mwilini. Alionekana kuwa na nguvu za ziada kwenye mwili wake, hazikuwa salama sana kwa wanadamu wa kawaida.
Alitikisa kichwa chake kwa masikitiko kwa sababu alitakiwa kuzitumia nguvu hizo kwa ajili ya kuulia watu, ni jambo ambalo hakulipenda lakini kwa wakati huo hakuwa na chaguo lingine. Akiwa amesimama hapo kuyaangalia yale maroboti ambapo moja lilikuwa chini na lingine lilimeguka, ulifunguka mlango mmoja mkubwa wa kioo humo ndani akaingia mwanaume mmoja ambaye alionekana mara ya mwisho Kariakoo akifanya mambo ya kutisha, Othman chunga ndiye alipenya humo ndani.
“Boss mama anahitaji kuonana na wewe” Othman aliongea akiwa na tablet lake mkononi huku mwilini akiwa amevaa vesti tu pekee.
“Yuko wapi?”
“Kwenye chumba cha picha” hakumjibu tena Othman zaidi ya kutoka humo ndani akimuacha Othman anayaweka sawa yale maroboti.
Mwanaume alienda kuoga kisha akavaa nguo safi na kwenda moja kwa moja kwenye eneo ambalo alikuwa ameagizwa. Ndani ya eneo hilo alionekana yule mwanamama Bi Aisha waweza kumuita Aurelia, ndiye yule kanali wa zamani wa jeshi, mwanamama huyo macho yake yalikuwa ukutani. Ndani ya chumba hicho walikuwa wanaruhusiwa kuingia wao wawili tu basi kwa sababu ilikuwa ni sehemu ya kuhifadhia picha za familia ambazo zilibandikwa kila kona ya ukuta na kujengewa vizuri.
“Nakumbuka ukiwa mdogo ulikuwa msumbufu lakini tabasamu lako lilikuwa likimvutia kila mtu, kwa mwonekano tu ulionekana kabisa umeandikiwa kuja kufanya makubwa kwenye huu ulimwengu. Siku ambayo ulitakiwa kwenda mbali na mimi nilijisikia vibaya sana kwa sababu wewe na Adam mlikuwa kama mapacha kwangu, mlikuwa kila kitu ambacho niliomba kuwa nacho kwenye haya maisha na jambo ambalo lilinipa furaha zaidi ni baba yako na mama yako kuniamini mimi kuwa mama kwako, hilo ndilo jambo bora zaidi kuwahi kunitokea kwenye maisha yangu” mama huyo aliongea akiwa anazigusa picha za watoto wawili wadogo huku akimwaga machozi.
“Ukiwa mama moyo wako wote unakuwa kwa watoto wako, kama mtoto wako akipata shida yoyote hata ndogo hata chakula huwezi kula wala kufanya jambo lolote la maana, watoto wanaibeba sehemu kubwa ya moyo wako ndiyo maana huwa unaona mama yeyote hata kama mtoto wake ni mwizi au ana tabia mbaya za kuwa chukizo kwa watu wengine lakini mama yake hawezi kumchoka, atampenda mwanae kama ambavyo anawapenda wanae wengine. Nakumbuka siku moja wakati unanyonya na mwenzako, ulikuja ukatulia ghafla kiasi kwamba ukawa hauhemi vizuri, ile ndiyo siku ambayo moyo wangu uliniuma na kunifanya nilie kama mtoto, nilihisi nimekupoteza kwenye maisha yangu”
“Ukiacha mawazo ambayo nilikuwa nayo juu ya nini nitawaambia wazazi wako juu ya lile jambo ila mimi mwenyewe kwenye moyo wangu nilitamani hata kujiua kama ningekupoteza, niliwapenda na kuwazoea wote wawili ndiyo maana hata baada ya kuondoka kwenye mikono yangu bado ni mimi pekee ambaye niliruhusiwa kuja popote ulipo duniani kwa sababu ulikuwa ukihitaji upendo wa mama. Kwa bahati iliyokuwa nzuri daktari wa familia alikuwa karibu, alikushtua baada ya dakika kumi ukaanza kulia, kile kilio kilinifanya na mimi nilie kwa furaha, kuna vilio vingine vya watoto huwa ni furaha kwa mzazi kwa sababu anakuwa na uhakika kwamba mwanae yupo salama kabisa”
“Tangu wazazi wako wakukabidhi kwangu mpaka leo binafsi huwa najua nina watoto mapacha, mwenzako kwa sasa hayupo lakini namshukuru Mungu kwa uwepo wako wewe kwa sababu bado najihisi nimekamilika kwa kila kitu. Naelewa namna mama yako alivyo pitia kipindi kigumu kwenye maisha yake baada ya baba yako kumwambia ukweli kwamba wewe ulitakiwa kulelewa na mwanamke mwingine, mama yako alikuwa mtu wa kilio kila nilipokuwa namuona, kama nilivyokwambia hakuna kitu kinamuumiza mama kama kumuona mwanae yupo kwenye matatizo au anawekwa naye mbali, kila mama anahitaji kuwa na mwanae au wanae karibu wawe wanamsumbua, vile kila muda wanavyo mwita mama, mama huwa inaleta msisimko mkubwa moyoni japo machoni anaweza kuonyesha ukawaida tu”
“Kutokana na ile hali ilifanya mimi na mama yako tukawa marafiki wakubwa, tulishibana na kuna muda nilikuwa nakupeleka kwake kwa siri ili tu atumie muda wa pamoja na wewe kwa sababu nilikuwa najua jinsi ambavyo alikuwa akijisikia kuishi mbali na wewe. Mama yako alikuwa akiwapenda mno, siku zote akikubeba kwenye mikono yake ungemkuta anaimba nyimbo nzuri za zamani, muda wote ulikuwa ukicheka na kufurahi. Alikuwa anawaweka pamoja wewe na kaka yako ambaye Mungu alimbeba, mlikuwa mnafanana kwa kila kitu na kama sio kuwekwa mbali basi nina uhakika hata yeye angepata taabu kubwa kuwatofautisha. Mlikuwa mkifanana mpaka matendo yenu ambayo mlikuwa mnayafanya, ile ilikuwa ni zawadi kubwa ambayo Mungu aliipatia familia hali ambayo ilitufanya tuishi kwa furaha kubwa kwa sababu kila kitu kilikuwepo”
“Kama ambavyo ulimwengu unajieleza mwanangu, dunia kuna wakati sio sehemu salama sana kwa ajili ya kuishi, dunia imekuwa sehemu hatari zaidi kwa maisha ya binadamu. Ile furaha ndani ya muda mfupi iligeuzwa kuwa karaha ambayo imeacha vidonda vikali kweye maisha yetu. Wale watu hawakujali tena kuhusu furaha ya ile familia, hawakujali lolote juu ya majeraha ambayo wangeyaacha kwa baadhi wa wanadamu wakaamua kuyafanya yale ambayo walihisi wanaweza kuyafanya wakiwa na nguvu. Leo hawa wapendwa wetu tunaishia kuwaangalia kwenye picha badala ya kukaa nao sehemu moja kufurahi, nazikumbuka zile nyakati zangu za upendo, nayakumbuka mapenzi ya zile familia huwa naishia kutoa machozi”
Sehemu ya arobaini na saba inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.