Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anazingua kwakwelihivi hiyo kesho bado haijafika tu
afunguke tu kama na yeye niwale wakuchangiwa tujueAnazingua kwakweli
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ngoja atakuja hapa sio muda ataelezaafunguke tu kama na yeye niwale wakuchangiwa tujue
Oya tupia kitu mwanaSeason 02
Vp bando limeisha ama😁😁😁Season 02
Ukipost naomba unitag[emoji3578]Simulizi: Kaburi la Mwanamuziki
Mtunzi: Robert Heriel
WhatsApp 0693322300
Sehemu ya 1
“Kazi yangu bila shaka kila mmoja wenu atakuwa ameifanya vizuri, nilifurahishwa na Richard, yeye aliimaliza tangu jana akaniletea Daftari lake, amefanya vizuri sana. Richard! Tafadhali njoo uchukue Daftari lako” Mwalimu wa Hesabu akasema. Richard akatoka, akaenda kuchukua Daftari lake wanafunzi wote tukimtazama, wengine wakimuonea donge, wengine wakimuona kama kiherehere huku wengine tukiwa hatujali lolote. Kisha mwalimu wa Hesabu akaendelea kusema;
“ Richard amekuwa akifanya vizuri tangu mkiwa kidato cha kwanza, sijui ninyi mnashindwaje na Richard, miaka ijayo Richard atakuja kuwa mtu muhimu sana ndani ya nchi hii. Sijui atakuwa Mchumi! Labda atakuwa Daktari bingwa! Huenda akawa Injinia mkubwa sana hapa nchini. Ati Richard unandoto ya kuwa nani hapo baadaye” Mwalimu wa Hesabu akasema, macho yake yakimtazama Richard huku akitabsamu. Richard naye kwa aibu akatabasamu huku akimtazama Mwalimu wa Hesabu, kisha akajibu;
“ Ningetamani niwe Daktari hilo lisingenishinda, masomao ya fizikia, kemia na Bilojia wote mnajua hayanishindi, labda ningesema niwe Injinia nako nisingeshindwa Mwalimu, Hesabu na Fizikia sijivunii lakini najitahidi kwa kiwango cha wanafunzi bora katika nchi hii. Hata ningesema niwe Mwanasheria, kote ninamudu, lakini yote hayo siyataki, nataka kile ambacho wengi hukitafuta, kile ambacho wengi wamekikosa ndicho ninataka kukisomea, nataka niwe mtaalamu wa mambo ya Fedha, nataka jambo lolote lihusulo Fedha lisinipite, ndoto yangu kubwa ni kuwa mtaalamu wa mambo ya fedha, ukiniita mchumi ni sawa, ukiniita mhasibu pia ni sawa, nataka nikiita fedha initii, nikiikagua inihofie, hiyo ndoto yangu kubwa Mwalimu” Richard alijibu, Darasa lote lilimsikiliza, majibu yake licha ya kuwa na matambo lakini yalionyesha kiburi cha ndani, majivuno ya akili alizojaliwa.
Mwalimu wa Hesabu alituamuru tumpongeze Richard kwa kupiga makofi, rafiki zake walipiga makofi kwa nguvu wakishangilia, wakati washindani wake wakipiga makofi ya kivivu, sisi Back benchers tulikuwa bora liende, tulikuwa tukisukuma tuu siku ziende, kwa kweli hatukuwahi kumuonea wivu yeyote kwa habari za masomo. Hata hivyo ilikuwa ni kero waalimu walipokuwa wakiingia kutufundisha, chanzo cha kero ilikuwa maneno ya baadhi ya waalimu kutudhalilisha sisi tuliokuwa hatufanyi vizuri kwenye masomo, walitukera kadiri ya uwezo wao, wenye mdomo walitumia maneno makali, wenye hasira walituchapa na kutupa adhabau kali. Mambo hayo yalinifanya nizidi kuichukia shule. Kama sio Mama yangu kunilazimisha kusoma basi ningekuwa nimeacha shule siku nyingi, huenda hata kidato cha nne nisingefika. Nilimuonea huruma mama, na hiyo huruma ndio iliyonifanya nivumilie kero za waalimu wa ile shule nikamaliza elimu ya upili.
” Natamani wote mngekuwa kama Richard au Alice, elimu ni ufunguo wa maisha, oneni wazazi wenu wanahangaika kwa umasikini kutokana na kuwa na elimu duni, ndio maana wamewaleta ninyi shuleni mpate elimu msipate shida kama wao wanavyopata lakini ninyi baadhi yenu hamuelewi lolote mkiambiwa, mnacheza na muda wenu, muda hauchezewi, mtoto mdogo unaharakia nini kwenye mapenzi, unaharakia nini mambo ya Starehe, juzi nilikutana na Kabali akitoka Bar akiwa kalewa. Kabali unajua ulinisikitisha sana” Mwalimu wa Hesabu alisema, macho yake yakimkabili Kabali aliyekaa nyuma kabisa.
“ Nisamehe mwalimu, Lakini mara mojamoja sio mbaya kushtua ubongo” Kabali akajibu.
“ Hahahahahahah!” Wote wanacheka kasoro Mwalimu aliyebaki anamtazama Kabali huku akitingisha kichwa kwa kumsikitikia.
“ Anyaway! Shauri yako. Kila mmoja aweke. Daftari la Mathematics juu ya dawati, alafu afungue mahali alipofanyia kazi niliyoitoa jana” Mwalimu wa hesabu akaagiza, jambo hilo likawa linafanyika, mimi ndio nilikuwa namalizia kuhamisha kazi ya Alice aliyoifanya kwenye Daftari langu, Mwalimu alikuwa anaanzia kusahisha madaftari ya wanafunzi waliokaa mbele, mara kwa mara nilimuona Alice akigeuka nyuma kunitazama, nami nilikuwa nikimpa ishara yakuwa namalizia. Alice akawa ananipa ishara nifanye hima, baada ya kujibu maswali matatu kati ya matano, nikaona isiwe kesi, nikamrudishia Alice Daftari yake kwa kulifaulisha kwa dawati lililofuata kwenda mbele mpaka lilipofika kwa Alice.
Sikuwa najua hesabu kusema ukweli, tangu naanza shule niliishi kwa kuibia ibia ilimradi nisiwe wa mwisho darasani, sasa yalibaki maswali mawili kati ya matano, nitayafanyaje, unajua hesabu za kidato cha nne sio za jumlisha wala kutoa, bora hata zingekuwa za Desimali ningejaribu lakini zilikuwa hesabu ngumu zenye alama nyingi, sikuwa naelewa chochote. Nikaandika andika namba za uongo uongo ilimradi kurasa za daftari langu lijae, nikajaza majibu na kuyapigia mstari kwa usafi wote labda nilifikiri mwalimu angenionea huruma hata kama nimekosea jibu basi angenipa vimaksi vya usafi katika kazi. Lakini kumbe jibu la uongo ni uongo tuu hata kama likirembwa na kupambwa.
Mwalimu akanifikia, akachukua Daftari langu, akasahihisha swali la kwanza mpaka la tatu, alipofika swali la nne, aka-stop, nikaanza kuhisi mwili ukilegea, nilihofia asijejua nimeibia kwa mtu. Akanipa alama ya kosa, swali la tano likamshtua,
“Iweje upate swali la kwanza na lapili alafu ukose swali la tano? Ati wanafunzi hiyo inawezakana?” Akauliza!
“ Haiwezekani!” Wakajibu wanafunzi wote mpaka yule jirani yangu niliyekaa naye wakati naye hana anachojua kwenye hisabati.
“ Wewe utakuwa umeibia tuu! Ndio maana nikashangaa tangu lini Gibson umekuwa na akili za kukokotoa milinganyo kama hii. Embu ona!” Mwalimu akawa anaanza kupekua daftari langu katika kurasa zingine zisizohusiana na kazi ya leo. Kiukweli nilikereka, nilihisi naenda kuumbuka.
“ Heeh! Hii nini! Gibson! Hiki ni kitu gani kwenye daftari langu la Hisabati?” Sauti ya mwalimu ikafanya darasa zima kugeuka na kutazama kilichokuwa kinaendelea, mwalimu akapita mbele akiwa kabeba daftari langu, kisha alipofika mbele kabisa ya darasa ulipo ubao, akaniita nami niende mbele. Nilipofika akaniambia nipige magoti chini. Kwa aibu uso wangu nikiukwepesha na nyuso za wanafunzi wenzangu nikawa naangalia chini nikiwa nimepiga magoti,
“ Kwa hiyo ukaona Daftari langu ndilo la kuandikia huu upuuzi wako, Gibson! Mara ngapi umekanywa na mama yako kujihusisha na Muziki? Mara ngapi! Muziki ni uhuni, hufanywa na watu wajinga, wapuuzi na wasio na haya, au unataka kukata kata mauno kama hivi! Eeh! Hivi na hivi! Ndio unataka?” Darasa zima linacheka baada ya mwalimu kukata mauno.
“ Lakini mwalimu hata muziki nao ni kazi tuu kama zilivyokazi zingine, napenda sana kuimba Mwalimu!”
“ KELELE!”
“ Unaongea utopolo gani hapa! Muziki! Muziki! Muziki! Upuuzi mtupu! Haya kwa hiyo kupenda kwako muziki ndio ukaona utumie daftari la hisabati kuandika mautopolo yako ya muziki! Hukuona masomo mengine mpaka uandikie kwenye daftari la hisabati? Unadharau HISABATI! Hahahaha! Unajua waalimu wa hisabati wapo wangapi kwenye hii nchi? Unaelewa? Hisabati ni somo lenye heshima, ambalo watu wenye akili za juu ndio hulimudu sio watu kama wewe” Mwalimu akasema, muda huu hasira zilikuwa zimeikaribia kabisa sura yake.
“ Nisamehe mwalimu!” Nikasema. Mikono yangu nikiwa nimeiweka kifuani kama ishara ya kuomba radhi.
“ Leo nitakuchapa bakora mpaka akili ikukae sawa! Haya shika chini mjinga wewe!” Sikuwa na namna nikashika chini, viboko sita vikatua katika makalio yangu, vilikuwa viboko vichungu sana vilivyoyatia maumivu makalio yangu. Nilimuona Alice akilengwa lengwa na machozi, moyoni nilijihisi kuumia sana kuuona uso wa Alice katika hali ile.
Mwalimu alimaliza kufundisha, hatimaye akatoka;
Kila baada ya Lunch ilikuwa mara nyingi waalimu hawaingii darasani. Hivyo muda huo niliutumia kufanya mazoezi ya kuimba, nilikuwa nikienda uwanjani kufanya mazoezi ya sauti, nilizipa mazoezi ala za sauti kama vile ulimi, mdomo, koo na hata Glota. Nilipanua mdomo kuhakikisha sauti yangu inatoka vizuri. Nilifanya mazoezi ya pumzi bila kuchoka kuhakikisha sauti yangu haikati pindi nikiimba sauti ya juu sana.
Kuna wakati nilikuwa nakaa kwenye vivuli ya miti sehemu tulivu, ili kupata tungo nzuri. Nilikuwa nikitunga tungo nzuri za mashairi na kuyarekodi katika kidaftari maalumu. Kivuli na upepo mwanana hutuliza akili, Huibua ubunifu na shauku ya fikra ya kutunga vitu vipya katika sanaa.
“ Labda ni kweli sina akili za masomo ya darasani, ufaulu wangu ni duni. Njia pekee iliyobaki ni kutumia kipaji changu cha kuimba, hakika nitakilinda kipaji change, nitailinda sauti yangu, nitalinda ala za sauti. Lakini Ala za sauti nzuri bila fikra thabiti zenye ubunifu hazitanisaidia kitu, nitalinda fikra zangu kwa kulinda vivuli vya miti ya dunia….” Nikawaza mwenyewe lakini mara Alice akatokea jambo ambalo lilikatisha mawazo yangu.
“ Gibson! Nimekutafuta sana! Nimezunguka uwanjani nikakukosa, nikaenda kwenye yale madarasa mapya pia sikukuona, hapo nikajua sehemu yako ya mwisho ni huku kwenye huu mti wa Mzambarau” Alice akasema.
“ Umekuwa mahiri wa kujua mizunguko yangu eeh! Haya je usingenikuta kwenye huu mti wa mzambarau ungedhani nimeenda wapi?”
“ Bila shaka ningedhani umeshaondoka kwenda nyumbani” Akajibu. Tukacheka wote sana. Alice alipenda kutembea akiwa na juisi ya kopo pamoja na Ubuyu wa rangi nyekundu. Tukala pale ubuyu tukipiga stori. Mara kimya kikafuata, nikamuona Alice akiangalia mbele kwa mbali kidogo, alikuwa kama anawaza mbali la kuhuzunisha. Alinishtua na kunipa hofu.
“ Kuna nini Alice! Unawaza nini?” Nilimuuliza. Alice akanigeukia akanitazama.
“ Mtihani wa mwisho umekaribia sana, sidhani kama mpenzi wangu umejiandaa vya kutosha! Nina wasiwasi sana juu yako Gibson” Alice akasema.
Nikamtazama bila kusema kitu, sikujua nimwambie jambo gani, Alice alikuwa ananijali licha ya kuwa nilikuwa natoka familia masikini, nikiwa naufaulu mdogo mno.
“ Mimi nafikiri ungeyaweka mambo mengine pembeni kwanza ujikite kwenye kusoma, kisha baad ya kumaliza mitihani yetu ya mwisho ndio uurudie muziki. Unaonaje Gibson?” Alice akasema.
“ Niache muziki! Alice umechanganyikiwa? Hivi unajua muziki unamaana gani kwenye maisha yangu? Alice! Uliwahi kujiuliza muziki kwangu ni nini? Labda hujawahi kufikiria jambo hili. Acha nikujuze; Muziki kwangu ni maisha, muziki kwangu ndiye mkombozi, wakati madaktari wakitumia taalamu zao kutibu watu, mimi Gibson nitautumia muziki kutibu hisia za watu zilizopondeka, wakati waalimu kama mwalimu wa hesabati wakielimisha watu ingawaje wanatunyanyasa siye tusiye na uwezo darasani, mimi Gibson nitatumia muziki kuelimisha jamii na taifa langu. Alice bado hujaelewa muziki kwangu nini? Bila shaka umeelewa! Haya bado utaniambia niuache muziki?” Nilizungumza nikimtazama Alice kwa macho yaliyojawa na usongo.
“ Lakini Gibson, sijamaanisha uache muziki moja kwa moja, nimemaanisha upumzike kipindi hiki ili tujiandae kwa pamoja kwenye mitihani yetu hii ya mwisho, kisha utaendelea na muziki wako, Gibson unajua mimi ndiye shabiki wako namba moja..”
“ Alice! Naomba tuachane na hayo, tuzungumze mambo mengine!” Baada ya Alice kuniona nimebaki kuwa na msimamo wangu, akaniacha. Niliona jinsi alivyoumia nikaona nijifanye nimekubaliana naye kishingo upande.
**************
“ Kesho ndio nitapiga hatua yangu ya kwanza katika muziki, lazima niwaonyeshe watu kuwa nina kipaji kikubwa, ikiwa ni hatua ya kwanza itanipasa niipige kwa kishindo ambacho kitatikisa vikwazo vyote vilivyombele yangu. Ngoja niendelee mazoezi” nikawaza, alafu nikachukua moja ya kidaftari nilichoandika nyimbo zangu. Nikaanza kuperuzi katika kidaftari kile.
“ Huu! Hapana! Nitaingia na huu! Utafuata huu! Alafu nitamalizia na huu!” Punde nikakatishwa na Alice aliyekuwa ameiingia akiwa na mfuko. Akanikumbatia kwa nguvu, kisha akanibusu!
“ Vipi maandalizi yanaendeleaje?” Akaniuliza, akiwa anachukua stuli, akakaa na kuweka chini mfuko aliokuja nao.
“ Kama unavyoona, nataka kesho mji mzima utikisike, nitaishangaza dunia Alice” Nikasema nikimtazama Alice,
“ Sijui kwa nini hawajatupa nafasi tuimbe walau nyimbo nne!” Nikasema lakini Alice akanikatisha.
“ Gibson mpenzi! Kesho watumbuizaji watakuwa wengi mno, zitakuwepo shule tatu kubwa za kanda hii. Wameona muda utakuwa mdogo, hata hizo nyimbo tatu mlizoambiwa mnaweza msiziimbe, Hivyo unapaswa ujiandae kwa lolote.” Alice akasema.
“ Hata wakisema niimbe moja, kesho nitawafunika wote, kesho ni siku yangu ya furaha. Alice kesho jiandae kufurahia kusikia sauti ya mpenzi wako, kesho utajivunia mimi” Nikasema.
“ Hata sasa najivunia wewe Gibson, mimi siku zote nitajivunia wewe, ila usijiamini sana Mpenzi, kujiamini ni kuzuri lakini isipitilize” Alice akasema, akanyanyuka kisha akatoa nguo kwenye ule mfuko aliokuja nao,
“ Embu vaa hizi tuone!” Akanipa suruali ya jeansi nyeusi hivi na T-shirt nyeupe yenye picha yenye Skull and bones kwa mbele, alafu nyuma yalikuwepo maandishi “ GIBSON ft ALICE”. Nikavaa. Kisha akatoa miwani nyeusi akanipa nivae, nikavaa. Hapo nikamuona Alice akitabasamu kama aliyefurahishwa na muonekano wangu mpya, alafu akatoa Viatu dizaini ya Supra akanipa nikavaa, kisha akaniambia nivae na kofia. Nikamwambia anisubiri niende chumbani kwa mama nikajiangalie kwenye kioo kikubwa. Nikamuacha!
Nilikuwa nimependeza sana, nilifanana kwa ukaribu na wanamuziki wa kimataifa wanaotumbuiza kwenye majukwaa ya kimataifa, baada ya kuridhishwa na muonekano wangu, nikarudi chumbani kwangu,
“ Sasa itabidi uende saluni ukazitengeneze nywele zako vizuri” Alice akasema, akatoa elfu mbili akanikabidhi za kunyolea. Kisha akaniambia nijaribu kutumbuiza mbele yake.
Nikashika kalamu kama maiki na kuisogeza mdomoni. Nikaachia sauti nyepesi na laini nikiupiga wimbo wa mwisho nitakaouimba kesho. Alice akajikuta anatoa machozi, nilifanikiwa kuzigusa hisia zake kikamilifu.
“ Waaaoh! Umeimba vizuri sana. Natamani kesho uimbe kama ulivyoimba leo?” Alice akasema.
“ Usijali mpenzi!Kesho utajionea mwanaume uliyenaye niwa namna gani. Nimekuahidi kuwa siku ya kesho ndio siku utakayojivunia tangu unijue” Nikasema,
Kisha tukaachana, mimi nikienda kunyoa na kuziweka nywele sawa, wakati Alice akirudi kwao. Hiyo ilikuwa saa moja ya jioni hivi.
Itaendelea
Ukipost naomba unitag[emoji3578]
KABURI LA MWANAMUZIKI (EPISODE 09)
Mtunzi; Robert Heriel
WhatsApp 0693322300
EPISODE 09
ILIPOISHIA
“ Baba yupo wapi ndugu yangu?” swali likaniponyoka.
Yule kijana akawa ananitazama kisha akamtazama hakimu,
“ Huyu ni nani, Gibson?” Hakimu akaniuliza.
“ Huyu ni mtoto wa Shahidi, alikuwa na Shahidi jana nilipoenda kule Hospitali kumuona, shahidi” Nikajibu. Hakimu akamtazama Yule kijana, kisha akasema;
“ Baba yako yupo wapi?’
“ Baba yangu! hayupo Amekufa usiku wa kuamkia leo” Yule kijana akasema, kwa kweli maneno yake yalinifanya nichanganyikiwe,
“ Nimekwisha! Nimekwisha mimi!” Nikawa napiga kelele pale mahakamani.
ENDELEA
Nilikata tamaa, tumaini langu la kuwa huru likapotea, niliyekuwa namtegemea kutoa ushahidi ili niwe huru ndiyo huyo ameshakufa. Tumaini linapokufa moyo hupoteza njia katika mapigo yake, hugeuka gari lililopoteza muelekeo na muda wowote litapinduka.
“ Basi ikiwa shahidi wako hayupo wa kuthibitisha maelezo yako, mahakama haiwezi kupokea maelezo yako na kuyachukulia kama maelezo ya ukweli, mahakama itatoa uamuzi kulingana na ushahidi uliotolewa kwa pande zote mbili, mlalamikaji na mlalamikiwa…” Hakimu anakohoa kidogo kisha akaendelea;
“ Labda kuna lolote Gibson unaweza kujitetea kwa makosa uliyofanya?”
“ Mhe. Hakimu, samahani kwa kuingilia mazungumzo yako” Yule kijana wa Mr. Kibadeni akasema. Hakimu akamtazama kwa macho ya udadisi, kisha akamruhusu aseme alichokuwa anataka kusema, hata mimi nilijawa na shauku ya kutaka kujua Kijana yule alikuwa anataka kusema nini, nilitamani aseme alikuwa akitania kuhusu kifo cha Baba yake, lakini mawazo yangu yalikuwa kama ndoto za Abunuasi.
“ Ndugu Mhe. Hakimu, siku ya jana; kijana huyu alikuja katika hospitali aliyolazwa Baba yangu, akanikuta nikiwa na Baba yangu wodini, Baba yangu akamtambulisha kwangu kama Gibson, jana ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona. Baba alinambia kuwa kijana huyu ndiye aliyemuokoa asiuawe na mtu mmoja aliyekuja hospitalini kumuua, na ndio sababu ya mzee wangu kubadilishwa wodi na kuongezewa ulinzi mkali”Yule kijana akameza mate lakini kabla hajaendelea Hakimu akauliza akiwa ameshika kalamu;
“ Wewe unaitwa nani?”
“ Oh! Sorry kumbe hata sikujitambulisha, naitwa Riadi Kibadeni, Mhe Hakimu”
“ Sawa Endelea Mr. Riadi”
“ Nashukuru sana Mhe. Hakimu, Baba yangu alinisimulia tukio zima jinsi lilivyokuwa siku aliponusurika kuuawa, kufupisha stori Baba yangu jana usiku aliniambia nimrekodi video, masikini Baba alijua atakufa” Riadi akaanza kulia.
“ Jikaze Mr. Riadi, tunajua inaumiza kumpoteza Baba, lakini itabidi ujikaze kama mwanaume utoe maelezo uliyonayo” Hakimu akasema.
“ Nilimrekodi kwa simu yangu hii, naomba niikabidhi mahakamani hapa huenda ikawa msaada kwa kijana aliyemsaidia Baba yangu asiuawe” Riadi anaondoka kizimbani anaenda kukabidhi simu. Hakimu akaipokea simu ya Riadi, kisha akamuamuru Riadi akakae, baada ya Riadi kukaa mimi bado nikiwa chini ya ulinzi mkali, nikamuona hakimu akimpa ishara mmoja wa wahudumu wa ile mahakama, yule mhudumu wa mahakama aliyevalia joho jeusi na skafu nyeupe hivi shingoni akanong’onezwa jambo Fulani, kisha akaondoka pale, bado pale ukumbini kulikuwa kimya sana, watu walitulia kuona nini kinaenda kutokea, kwa upande wangu kwa kweli nilijawa na hofu, nilikuwa na wasiwasi wa kupewa hukumu ya kifungo, katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kama siku moja ningefungwa jela, kwenye maisha yangu niliogopa sana maeneno mawili, hospitalini hasa ICU na Jela. Nilikuwa nikiomba kimoyomoyo Ile video iliyoletwa na Riadi iweze kumshawishi Hakimu na kuniachia huru.
Punde yule mhudumu wa mahakama akarudi akiwa amebeba laptop, kisha akaenda kwa hakimu na kuiunganisha ile simu kwa waya wa USB, akabonyeza bonyeza kwenye laptop, bila shaka alikuwa akihamisha ile video kwenye Laptop, nikamuona akiunganisha laptop na waya Fulani hivi nisiojua kazi yake, alafu akasimama akalichangua lile joho mpaka alipopata nafasi ya kupitisha mkono wake kwenye mfuko wa suruali, akatoa kifaa Fulani kama rimoti, akabonyeza kuelekea juu, jambo ambalo lilifanya karibia watu wote wainue vichwa vyao juu, hapo nikaona Projector ikiwaka kitaa chekundu. Baadaye wote tukashuhudia picha ukutani upande wa kulia.
Hapo macho ya watu wote yakavutwa kuona video ya shahidi, Marehemu Kibadeni. Haikuchukua muda Hakimu akasema;
“ Tutaenda kuona na kusikiliza ushahidi wa Mr. Kibadeni ambaye ameshindwa kuhudhuria kuja kutoa ushahidi wake kwa sababu ya kukutwa na umauti, mahakama itaangalia kisha itaamua kama ushahidi huu uzingatiwe au upuuzwe, ila kwa vile mahakama ipo kwaajili ya kutoa haki, ndio maana tumeipokea ushahidi huu kama sehemu ya kumtendea haki ndugu Gibson. Tunaweza kuanza kuona”
Sijui ni kwanini mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakienda mbio kiasi kile, nilihisi woga sana. Punde sinema ilimuonyesha Mr. Kibadeni akiwa kwenye kitanda kilekile cha hospitalini nilipomkuta jana, akiwa kavaa kichwani kofia nyepesi ya rangi ya kijani yenye matundu madogomadogo kama chujio, akiwa katundikiwa dripu, upande wa kitanda alichokuwa amekilalia ulikuwepo mtambo mmoja wenye kioo kinachoonyesha Grafu zenye mawimbi zilizokuwa zinapanda na kushuka huku pembeni kabisa kukiwa na tarakimu za namba zenye asilimia, Mr. Kibadeni alikuwa amefunikwa shuka jeupe lenye nembo ya ile hospitali; kuanzia miguuni mpaka kiunoni karibu na kitovu, juu alikuwa amevalia shati la kijani linalofanana rangi na ile kofia aliyokuwa ameivaa. Mr. Kibadeni akajiweka sawa akijilazimisha kukaa lakini akashindwa, akatokea nyuma ya kamera Mtoto wake akaenda kumnyanyua na kumsaidia kukaa kisha akamuacha na kurudi nyuma ya kamera akimuacha Mr. Kibadeni pekeake, nikajikuta nikijiuliza nani alimuachia kamera achukue tukio lile, lakini wazo hilo lilikatishwa baada ya Mr. Kibadeni kuanza kuongea;
“ Naitwa Mr. Kibadeni, sina haja ya kujitambulisha sana ila najua Hakimu utakuwa unanifahamu” Hapo nikamtazama hakimu kwa haraka, nikamuona akiwa na uso wa kukubaliana na maneno ya Mr. Kibadeni. Hali ikanifanya nishangae.
“ Nimelazwa kwa miezi mingi sana, familia na serikali vimehangaika kuyapigania maisha yangu, kwa kweli sina chakuwalipa isipokuwa shukrani zangu, katika watu walioyapigania maisha yangu ni pamoja na huyo kijana aitwaye Gibson, hakuwa akinijua; wala mimi sikuwa namfahamu, na nadhani mpaka sasa sidhani kama ananijua, hiyo ni kawaida kwa mtu wa kawaida na kijana kama yeye kufahamu watu wa aina zetu,” Mr. Kibadeni akakohoa kidogo kisha akaendelea;
“ Usiku ule sitakuja kuusahau katika maisha yangu, nikiwa nimelala nilishtuka baada ya kuamshwa na mwanaume mmoja mrefu aliyevalia koti jeupe la kidaktari, usoni akiwa kavaa barakoa iliyoficha uso wake, mikono yake alikuwa amevaa Gloves za kitambaa yenye rangi nyeusi, mkono mmoja akiwa kashika bastola, nilijua na kuamini mtu yule alikuja kwa ajili ya kuniua hata kama asingeniambia; jinsi alivyoonekana alifanana kabisa na mtoa roho. Akanitisha, kisha akachukua kichupa cha sumu kutoka kwenye mfuko wake, akatoa na sindano akaichoma ile sumu aliyoivuta kwenye sindano na kuiingiza kwenye Dripu nililokuwa nimetundikiwa” anapumua kidogo kisha anaendelea.
“ sumu ilikuwa imeshachanganyika na maji ya Dripu, sikuwa na uwezo wa kuliondoa dripu kwani nilikuwa nimezidiwa sana, sikuweza hata kujigeuza wala kunyanyua mkono, yule Mwanaume shetani baada ya kufanya ushetani wake akaondoka, hapo nikawa nakisubiri kifo changu maana muda mfupi ujao ile sumu ingekuwa imeshaanza kuingia polepole mwilini mwangu. Lakini kwa bahati kumbe yule kijana niliyekuwa nimelazwa naye wodi moja alikuwa macho, nikashangaa ameamka upesiupesi kisha akaja kunitoa lile dripu, nilikuwa siwezi hata kuongea…” Mr. Kibadeni akaanza kukohoa mfululizo, alikohoa mpaka pale mahakamani kila mmoja wetu akawa anakunja uso kwa kuhisi maumivu anayoyapata, alikohoa zaidi na zaidi mpaka akalegea kama mlenda, nikawa naomba kimoyomoyo lolote baya lisimtokee kabla hajamaliza kueleza kila kitu, lakini nilihisi kukata tamaa nilipoona akikohoa mpaka udenda unamtoka, kwa upesi tukamuona Riadi akitokea nyuma ya kamera akiwa na chupa ya maji, akaenda akamshika Baba yake na kumpiga piga mgongoni, kisha akampa ile chupa ya maji, yule mzee akanywa, lakini alikuwa amechoka wala sio utani.
Akamuegemeza kwenye kitanda, Mr. Kibadeni alikuwa kayafumba macho yake kama siku ya kwanza niliyomkuta kule wodini, kisha akayafumbua, nilikuwa nikisali sana, niliogopa, kila muda niliyafukuza mawazo mabaya yaliyokuwa yakinijia kichwani kumhusu Mr. Kibadeni.
Mr. Kibadeni akajitahidi kusema kitu lakini akaishia kukohoa maradufu zaidi mpaka macho yakawa yanamtoka, hapo nikajua basi, ule mtambo kitandani ukaanza kulia huku kukitokea mstari mwekundu na zile tarakimu za namba zikishuka kwa kasi kutoka 205 na mpaka muda ule zikawa zinasoma 162, hisia zilizotawala pale kwenye ukumbi wa mahakama zilikuwa za msisimko. Yule muuguzi aliyenishtaki nilimuona akiwa amejawa na shauku ya kuujua ukweli. Nikamuona Mr. Kibadeni akamvuta Mwanaye, Riadi mpaka kwenye uso wake na kulisogelea sikio lake, hatukusikia alisemaje, lakini tukamuona Riadi akimpekua Baba yake kwenye mifuko ya suruali yake, tukamuona Riadi akitoa kitu kama Kadilida au memorikadi ile kubwa kutoka mfukoni mwa baba yake, alafu ghafla tukasikia mlango ukifunguliwa na punde wakajitokeza madaktari wawili waliovalia makoti ya kidaktari wakiwa na stethoscope shingoni, wakampima Mr. Kibadeni na hapohapo video ikafikia tamati.
“ Ndio Mr. Riadi, huo ndio ushahidi wa Baba yako? Mbona haujakamilika, kile ulichokitoa kwenye mfuko wa suruali yake ni kitu gani?” Hakimu akauliza akiwa anamtazama Riadi.
“ Mhe. Hakimu kama ulivyoona Baba yangu alizidiwa akiwa anatoa ushahidi wake, kwa bahati mbaya kabla hajamaliza kutoa maelezo yake akazidiwa” Riadi akasema, Hakimu akawa anaandika.
“Sasa itakuwaje kama ushahidi ndio umeishia hapa, haujakamilika?” Nikawaza.
“ Lakini kuna hii device Baba aliniambia niitoe mfukoni mwake, alinambia hii ndio ushahidi wa moja kwa moja, japo sijapata nafasi ya kuiangalia” Riadi akasema akiitoa ile device inayofanana na Memorikadi kubwa. Hakimu akaipokea kisha akamuita yule mhudumu wa Mahakama, akaichomeka ile device kwenye laptop, ghafla video ikajionyesha ingawaje ilikuwa inatingishika tingishika lakini tuliweza kuona kilichokuwa kinaendelea, video ilimuonyesha yule mwanaume mrefu alivyokuwa akimuamsha Mr. Kibadeni na matukio yote aliyoyafanya, ilinionyesha na mimi nilivyoenda kumsaidia Mr. Kibadeni, nikatoka kwenda kumuita Muuguzi kisha nikarejea nikiwa na Muuguzi, ikanionyesha ugomvi wangu na Muuguzi mpaka nilipolikanyaga lile Dripu na kulipasua. Mahakama nzima ilishangazwa na ushahidi ule, muuguzi alibaki ameduwaa asiamini kilichokuwa kimetokea. Nilishukuru sana, nilijikuta nikilia kwa uchungu mwingi, sikuamini kama wokovu ungepatikana dakika za mwisho kabisa.
Baadaye hakimu alitoa hukumu ya kuniacha huru baada ya kunikuta sina hatia.
MWISHO WA SEASON 01.
Kesho tunaendelea na season 02
Nisameheni kwa kuwaweka sana, kuna mambo yaliingiliana wakuu.
Ratiba ni kila siku saa saba mchana
Sawa mkuu tunashukuru sana
Ahsante sana, Shukran Mkuu
hivi hiyo kesho bado haijafika tu
Kesho imefika