KABURI LA MWANAMUZIKI ( SEASON 2)
MTUNZI: Robert Heriel
whatsApp 0693322300
Episode 01
“Utaishi hapa kama nyumbani, jisikie amani Mr. Gibson, nashindwa ni namna gani naweza kukushukuru ndugu yangu, bila ya wewe Baba yangu angekuwa ameshakufa, lakini ulimuokoa” Riadi alisema akiwa ananikaribisha nyumbani kwake. Kauli yake ya kusema Baba yake angekuwa ameshakufa ilinishtua, nikawa nawaza; kwani bado yupo hai. Nikajikuta nikijizuia kumuuliza;
“Unamaana gani kusema angekuwa ameshakufa?”
“Aaah! Namaanisha angekufa siku ileile, angekufa kifo kibaya sana” Akasema. Tukatazamana na mwishowe nikaongeza swali jingine;
“ Kwa hiyo mazishi ya Mzee ni lini?” Nikauliza.
“ Mazishi! Gibson Achana na hayo, hilo suala lipo kifamilia zaidi, kuna mambo siwezi kuyaweka wazi kwako, wewe mwenyewe unatambua tukio lililotokea la kutaka kumuua baba yangu, unafikiri wauaji wake wameisha, mazishi yake yatakuwa siri, na sisi tuu kama wanafamilia ndio tutahusika katika mazishi” Riadi alisema akiwa anajitahidi kuelezea kwa kina ili nielewe. Nilimuelewa.
Maisha mapya katika nyumba ya Riadi yalianza, Riadi alikuwa akiishi pekeake katika jumba kubwa la kisasa lenye kila aina ya samani za kuvutia, lilikuwa jumba kubwa la ghorofa mbili, nje kulikuwa na bwawa la kuogelea na bustani za kupumzikia, upande mwingine kulikuwa na sehemu iliyotengwa kwa kuegeshea magari, ndani yake yalikuwepo magari mawili ya gharama, kwakweli sikuwahi kufikiri kuna kijana mwenye umri kama wa Riadi mwenye maisha mazuri kama yale. Yalikuwa maisha ambayo ni nadra kwa vijana waliowengi kuwa nayo, umri wa Riadi haukuwa zaidi ya miaka thelasini na mbili, akiwa hajapishana na mimi sana kiumri. Lakini maisha aliyokuwa nayo ni mara elfu elfu ukilinganisha na maisha yangu.
Baada ya siku mbili kupita tangu nifike nyumbani kwa Riadi, tayari nilianza kuzoea mazingira, nikiwa nasaidia kazi za usafi na mazingira ya nje. Riadi aliniambia kuwa angeondoka kwa siku tano kwenda mkoani kwa ajili ya mazishi ya Baba yake, basi baada ya kuniachia maagizo ya namna ya kuishi katika nyumba yake, akaniaga; aliniacha pesa ambazo alisema zitanisaidie kwenye matumizi ya pale nyumbani, kiukweli tangu kuzaliwa sikuwahi kushsika milioni moja, ile ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kushika pesa nyingi kiasi kile, tena alisisitiza atanitumia tena kwani zile aliziona hazitoshi, hapo ndipo nikajua kuwa kuna watu duniani wanapesa, wakati kuna mtu anahangaika miezi na miezi apate milioni moja, kumbe kuna mwingine anatumia hiyo milioni moja kwa siku; Sasa Riadi alinambia siku tano hiyo pesa isingeweza kunitosha hivyo akifika tuu mkoani angeweza kutuma pesa nyingine. Aliniachia simu ya smartphone ambayo ilikuwa kama simu ya pale nyumbani. Kisha akaondoka na kuniacha peke yangu.
Ingawaje ilikuwa sio nyumba yangu lakini niliona fahari ya kuwa ndani yake, sasa niliona njia yangu ya mafanikio imefunguka, kuishi katika jumba kama lile kwangu nilihesabu ni bahati kubwa, “ Kuna watu maelfu kwa maelfu tangu wamezaliwa mpaka wamekufa hawajawahi hata kuingia katika majumba ya namna hii, kwa nini nisiite hii bahati” Niliwaza.
Nikamkumbuka mama yangu kijijini, nilikumbuka makazi duni tuliyokuwa tunaishi na mama yangu kule kijijini, hapo mawazo mengi yakausonga ubongo wangu, “ Ni lazima nikukomboe mama yangu, lazima nawe siku moja uishi katika jumba zuri kama hili, Mama yangu..” Niliwaza,
“Ni muda wa miezi kadhaa karibu mwaka mzima sijawasiliana na Mama yangu, sijui anaendeleaje, bila shaka atakuwa na wasiwasi na mimi” Nilisema kwa sauti ndogo huku nikichukua ile simu na kubonyeza bonyeza namba, nikaiweka sikioni na simu ikaanza kuita.
“Hello Kaka, ndio mimi Gibson, ndio! Za siku nzuri Kaka, yaani kuna mambo yaliingiliana Kaka, eeh! Wewe acha tuu! Vipi wazima huko! Afadhali Kaka, Mama yangu anaendeleaje? Ooh! Upo karibu na nyumbani; nataka umpelekee simu nizungumze naye, sawa nasubiri” Nikakata simu baada ya kuongea na Kaka mmoja ambaye alikuwa jirani yetu, nilifurahi kusikia mama yangu hajambo, sasa nilikuwa nasubiria simu ya Kaka ambaye ameenda nyumbani kwetu kumuangalia mama yangu ili ampe simu nizungumze naye, nilikuwa na shauku kubwa ya kuongea na mama, nilimkumbuka sana. Nikiwa nipo sebuleni nikiwa natazama Muziki Luningani, punde simu ikaita, kisha ikakata, Nikaipigia; “Sawa Kaka, basi akirudi jioni unitafute nizungumze naye, sawa!” Simu ikakatika.
Mama alikuwa hayupo, alikuwa ametoka, taarifa hiyo ilinikata maini kweli. Ilipofika jioni nikampigia tena yule kaka lakini mara hii akawa hapatikani, hasira zilinipanda, nilimkasirikia lakini nikakumbuka kuwa nyumba yao pia haina umeme kama ilivyo nyumba yetu, pia hata kama ingekuwa na umeme sikuwa na uhalali wa kumkasirikia mtu ambaye hata hivyo ananisaidia tuu. “Ndio tatizo letu masikini, mtu anakusaidia lakini bado unamuona mbaya, sasa kaka anakosa gani mpaka nimkasirikie?” Nikawaza baada ya hasira kupungua.
Kesho ikafika, nikaendelea na shughuli zangu za usafi wa nyumba na mazingira ya nje, lakini wakati nafanya usafi wa bustani, kengele ya geri ikalia, hii ilimaanisha kuna mtu anabisha hodi, nikaenda getini nikapokelewa na mwanamke mmoja akiwa na mtoto wa kiume wa miaka kama minne hivi, nyuma yake kukiwa na gari zuri. Yule mwanamke alikuwa kava miwani ya yenye vioo vya rangi ya huzurungi, hereni sikioni na kilemba, mavazi yake yalifanana na mavazi ya kinaijeria ambayo yalikuwa sawa nayamtoto, yule mtoto wa kiume kichwani alivalishwa kofia inayofanana na lemba la yule mwanamke ambaye nilihisi ni mama na mwana.
“Habari yako Dada, naomba nikusaidie” Nikasema.
“ Unisaidie? Are you mad! Unaweza kunisaidia kwa lipi kijana wewe eehe! Embu fungua geti niingie” Yule mwanamke akasema kwa dharau, kwa kweli sikupendezwa kwa namna alivyokuwa akiuweka uso wake na kuupinda mdomo wake, nilitamani nimchape kibao kimoja achunge adabu yake lakini nafsi yangu ikanionya.
“Samahani Dada yangu, sikuwa na maana hiyo, nilikuwa naomba kujua wewe ni nani na unahitaji nini?” Nikasema nikiwa nimenywea, kwa kweli nilitia huruma, nilikumbuka kauli isemayo usipambane na mtu usiyemjua.
“ nimekuja kwangu, nipishe, utaingiza gari hili ndani, Mwanangu twende ndani” Yule mwanamke akasema huku akinisukuma nimpishe pale kwenye geti dogo kisha akaingia na mtoto wake, nikabaki nimeduwaa nsijue nifanye nini, nikakumbuka, nikampigia Riadi, nilishangaa Riadi akinambia yule aliyekuja ni Mke wake, alikuwa ametoka kidogo, akaniomba msamaha kwa usumbufu uliokuwa umejitokeza.
Nikaliingiza gari ndani, alafu nikaenda sebuleni ambapo nilimkuta yule mwanamke akigombezana na mtu kwenye simu ambaye baadaye nilijua alikuwa akigombana na Riadi, nikamuacha pale sebuleni kisha nikarudi zangu nje kuendelea na usafi wa bustanini. Baada ya kumaliza usafi nilirejea ndani kwa ajili ya kuandaa chai ya asubuhi, niliandaa chai ya maziwa, soseji na mayai ya kuchemsha mawili mawili. Kisha nikapanda ghorofani kumuita yule mwanamke na mtoto. Niliwakuta katika sebule ya juu ya ghorofa ya pili, alikuwa tayari keshabadili nguo na kukaa kihasara hasara akiwa ameshavua lemba kichwani, alikuwa na nywele bandia zilizomwagika mabegani.
“Vipi!” Yule mwanamke akanisemesha kwa ukali baada ya kuniona.
“Aaah! Samahani sana, nimekuja kuwaita, chai tayari”
“ Nini? Hivi wewe unaakili sawasawa! Eeeh!” Yule mwanamke akasema kisha akasimama na kunifuata akiwa amenitolea macho yake makubwa na makali.
“ Umechanganyikiwa!” Hapo akatingisha nywele zake, kisha akauweka uso wake kidada na kuung’ata mdomo wake, kisha akasema;
“ Mwenye njaa hapa ni wewe, sawa! Tena ukome kusogea eneo ambalo mimi nipo, haya futika”
Sikuwa na haja ya kusubiri arudie, nikaondoka harakaharaka huku nikimsikia mtoto wake akinicheka, nilijisikia vibaya sana, kudharaulika kusikia tuu, kila mwanadamu anataka kuheshimiwa, hakuna ambaye anapenda kudharauliwa, “hata kama mimi ni masikini isiwe sababu ya kunidharau” Niliwaza nikiwa nashuka ngazi kuelekea chini. Siku ile ikapita wala sikuonana na yule mwanamke ambaye ni mke wa Riadi.
Nilikuwa nikifanya mazoezi ya kuimba eneo la bustani kila jioni, nikiwa nina kalamu na daftari aliloninunulia Riadi, kidaftari kile nilikuwa nimeshaandika nyimbo kadhaa hivi ambazo nilitarajia siku zijazo ningezirekodi studio ili zipigwe redioni na kwenye televisheni, nikiwa nimekaa kwenye bembea pale bustanini ghafla mke wa Riadi akaja,
“ Wewe! Weewe! Hunisikii! Hivi unampigia nani kelele hapa, huoni mta mzima ulivyotulia, lisauti lako libaya kama kondoo ndio linachafua utulivu wa mtaa huu, unadhani huku ni kule uswahili kwenu! Eenhe!” Yule mwanamke akasema akiwa sasa amenikaribia, mikono yake ikiwa kiunoni, akinitazama kwa hasira zilizofichika. Mimi sikujua nimjibu jambo gani, na nisingependa kuongopa hapa, nilianza kumuogopa, ingawaje alikuwa hanipigi lakini maneno yake yalikuwa makali sana ni afadhali angenikuwa ananipiga. Silaha ya mwanamke ni mdomo wake, lakini silaha ya mwisho kubwa ya mwanamke ni mwili wake, hilo nilianza kuliona baada ya kuona kinguo alichokuwa amekuja nacho pale bustanini, alikuwa amevaa mtandio mwepesi alioufunga kidizaini, ulioshika kiuno chake chembamba na mapaja laini ambayo niliyaona Kupitia mtandio ule uliokuwa unaonyesha kwa ndani, alikuwa kava chupi aina ya bikini, juu alivalia kitopu, huku chini kabisa akiwa kava kikuku, macho yangu mara kwa mara yalikuwa yakikwepa kuziangalia shanga mbili zilizokuwa zinawakawake kwenye kiuno chake.
“ Unajifanya jeuri, lete hii” Akaninyang’anya kile kidaftari na kuanza kukipekua pekua, kisha akaanza kusoma moja ya nyimbo nilizokuwa nimeziandika kwa sauti, akijifanya anarapu;
“ Penzi lako pipi filimbi, Nitalinyonya na kulilamba,
Nitaoga kwa lako wimbi, mdomoni udenda ukinisomba,
Mzizi wa moyo wako sichimbi, mhogo wangu utausomba,
Refa keshapiga filimbi, mechi tayari nyavuni kumeshasoma,
Ooh! Mama, tingisha lako behewa, nishike zako mbili kuta,
Penzi lako my dear nalewa, nikikuchapa fimbo huwezi futa,
Unanivuta na kuning’ata kama muwa, utamu tamu kolea wauchakata….”
Anaacha kurapu alafu ananiangalia, kisha anatabasamu, nabaki namuangalia kama mtu wa maajabu hivi nisiyemuelewa,
“Hivi ndivyo washenzi mnavyodanganya watoto wa kike, sivyo, haya marapu rapu yako, haya! Haya!” Akawa anachana lile Daftari hali iliyofanya niamke na kumfuata na kunyang’anya lile daftari, lakini wakati tunanyang’anyana kwa bahati mbaya ule mtandio ukaanguka akabakiwa na bikini tuu, kiukweli nilipigwa na kitu mfano wa shoti ya umeme, kihoro kilinikaba, nikageuka upesi upande mwingine na kufumba macho yangu, Mke wa Riadi akavaa mtandio wake kisha akanipiga kichwani na vile vipande vya daftari alilokuwa amelichana, kisha akaondoka akiniacha pale nimesimama.
“Haya ni majaribu, ila yanipasa niyashinde, lazima niutawale mwili wangu, wakati mwingine kushindwa kutawala hisia za mwili ni kushindwa kujitawala, na kushindwa kujitawala ni kushindwa kuyaendesha maisha yako binafsi” Niliwaza mwenyewe nikiwa naokota zile karatasi zilizochanwa chanwa na mke wa Riadi ili kuondoa takataka pale bustanini.
Usiku uliigia, giza likachukua sehemu ya mchana, siku ya leo ilikuwa tofauti na siku zingine, Sebuleni kwenye meza ya kulia chakula, nilikuwepo mimi, Mke wa Riadi na mtoto, tukiwa tunakula chakula cha usiku. Tofauti na siku nyingine, Mke wa Riadi alikuwa kabadilika usiku huu, alikuwa mpole asiye na maneno maneno akiwa anaperuzi mtandaoni huku akila chakula, kwa kweli sikutegemea kama siku moja angethubutu kula chakula nilichokuwa nimepika, alikuwa na dharau sana yule mwanamke. Wakati Fulani alikuwa akinichungulia kwa kujiiba iba, hapo nikagundua jambo geni kabisa, Mke wa Riadi alikuwa akinionea aibu, sikujua aibu ile ilitokana na tukio la mchana au ilikuwa aibu iliyosababishwa na nini. Jambo lile hata mtoto aliliona akawa anamtazama mama yake alafu kuna muda alikuwa akinitazama mimi kwa udadisi.
“Mama mbona uko hivyo?” Mtoto akauliza akiwa anamtazama mama yake.
“ Nilikuambiaje!” Mke wa Riadi akafoka.
“Samahani Mama, uliniambia wakati wa kula sio wakati wa kuongea”
“Haya kula” Mke wa Riadi akasema bila utani. Pakawa kimya tena huku sauti ya vijiko na sahani zikiendelea kusemeshana. Tulimaliza kula, wakaondoka na kupanda ghorofani wakiniacha mimi chini,, nikatoa vyombo mezani kisha nikaenda kuoga, alafu nikarudi sebuleni kuangalia Luninga, nilijilaza kwenye sofa nikitazama muziki uliokuwa unaonyeshwa kwenye chaneli Fulani kwenye TV. Kama baada ya lisaa limoja hivi Mke wa Riadi akaja tena, muda huu alikuwa amevaa Night Dreess ya rangi ya kijibu inayong’ara ndani akiwa hajavaa nguo yoyote. Kiukweli niliona kama ananifanyia makusudi, sasa maana yake nini kuja na vinguo vya kulalia sebuleni, anataka nini sasa, nikawa nawaza, nikimuangalia kwa kijicho upembe, naye kwa makusudi akawa amesimama mahali ambapo alijua fika kabisa nitakuwa namuona, akaenda kwenye sofa na kujibwa pwaa! Kizembe zembe, alafu akakaa kiholela akiacha eneo kubwa la mapaja yake wazi, hili lilikuwa shambulio la makusudi la kunitesa kihisia, Ni kweli namheshimu sana Riadi, ni kweli kabisa amenisaidia na nipo nyumbani kwake, lakini kwa kile kilichokuwa kinaendelea kilikuwa ni kubwa zaidi ya heshima aliyonipa Riadi, wakati mwingine mtego huweza kuwa mkubwa kuliko heshima unayompa mtu.
Sio kwamba sikuyaona mapaja yake yaliyonona, rangi ya kichokozi, ma uso wake wa jinni mahaba lililodhamiria kuniteka kwa hila zake. “Gibson jizuie, huo ni mtego, jitahidi Gibson” Nilikuwa nikijiambia kimoyomoyo, sijui ni muda gani nilisahau kuwa nilikuwa naangalia muziki luningani, akili yangu ilishatekwa na Jini mbaya wa mapenzi, sasa nilikuwa kwenye miliki yake, moyo wangu ulikuwa kama askari asubiriye amri ya mkuu wake. Ghafla simu yangu ikaita ikiwa pale chini kwenye zulia, nikaichukua, zilikuwa namba za kaka jirani kule kijijini. Nilifurahia kuona akinipigia, nikakata alafu nikapiga, ikaita mara moja kisha ikapokelewa, nikaweka loud,
“Hallo Mwanangu” Ilikuwa sauti ya Mama yangu, nilifurahi sana,
“Hallo mama, shikamoo mama yangu” Nikasema.
“Marhaba Gibson, umepotelea wapi mwanangu, nilikuwa na wasiwasi mwanangu” Mama alisema kwa sauti iliyolegea sana kama mtu anayetaka kulia, nilimuelewa sana mama yangu, sauti yake ya namna hiyo ilimaanisha muda mchache ujao atalia.
“ Nisamehe Mama, nilipatwa na matatizo makubwa mama yangu, lakini kwa sasa naendelea vizuri” Nikamjibu.
“ Pole sana mwanangu, hayo ndio maisha, lazima upambane kama Mwanaume, Usikubali kushindwa kirahisi Mwanangu, lakini pia usiibe cha mtu, pia jichunge na wake za watu huko mjini” Hapo nikamtazama Mke wa Riadi ambaye naye alikuwa ananikodolea macho yake huku akiwa anakula Komamanga.
“Usijali Mama, mimi nitafuata kila ulichoniagiza mama yangu”
“Ulipatwa na nini Mwanangu?” Mama akaniuliza.
“Mamaa! Ni stori ndefu sana, siwezi kuimaliza leo, nitatafuta siku nyingine tuzungumze, kwa sasa ninachotaka kusema nimefurahi sana kujua unaendelea vizuri, kesho uende kwenye duka la simu ukachague simu nzuri nitakutumia pesa kidogo ili tuwasiliane mama yangu”
“ Gibson, unazungumzia kuninunulia simu wakati nyumba yetu ilidondoka upande wa chumba change, hapa nilipo nalala kwenye chumba chako. Kama ingefaa hiyo pesa ya kununulia simu ni bora tufanye ukarabati kwenye huu ukuta mwanangu” Mama akasema kisha akakohoa,
“Pole Mama yangu”
“Ahsante mwanangu, yaani baridi hapa inanipiga mwanangu, haya mapazia yamechakaa, tangu ulipoyaacha mpaka leo ni yaleyale, natumia vipande vya vitenge kufunika dirisha ile upepo wa baridi usiingie mwanangu” Nilimsikia mama akilia kwa sauti, nikajikuta name nikishindwa kuzuia machozi yangu.
“Mama! Mama! Usilie mama, kila kitu kitakuwa sawa Mama yangu” Nikasema,
“Sawa mwanangu nakuombea”
“Kesho ufanye nilichokuambia, simu itatusaidia kuwasiliana mimi na wewe, pia kukurushia pesa, sawa mama” Nikasema, mwishowe nikazungumza na kaka jirani na kumshukuru kwa msaada alionipa. Baada ya simu kukatika moyo wangu ulijazwa na furaha isiyokifani, nilifurahia kuongea na mama yangu.
“ Nisamehe sana Gibson” Mke wa Riadi akasema, nilishtuka kusikia akilitaja jina langu, nikakumbuka amelisikia wakati nikiongea na Mama.
“ Nikusamehe kivipi Shemeji?” Nikamuuliza.
“ Kwa yote niliyokufanyia, tangu siku ya kwanza mpaka leo jioni nilivyochana kidaftari chako. Kwa kweli sikuwa muungwana, nilifanya mambo yasiyo mazuri”
“Usijali shemeji kila jambo linasababu zake, maisha ni kujifunza” Nikasema
“ Hakika maisha ni kujifunza, name nimejifunza kwako uvumilivu na staha hata kama mtu atakukera vipi” Akasema.
“ Hata mimi umenifundisha kuomba msamaha pale ninapokuwa ninakosea, kama ulivyofanya wewe sasa hivi” Nikasema, wote tukacheka, lakini nilitamani nimuambie jambo moja, nikasita. Nilitaka kumuambia akae vizuri au akabadilishe ile nguo lakini sijui ni kwa nini nilishindwa.
Tulipiga stori nikiwa najizuia nisiangalie mapaja yake ambayo mara kwa mara alikuwa akihakikisha ninayaona na kunirembulia. Muda ulienda akaaga na kuondoka kwenda kulala, akiwa anaondoka alitembea kwa madoido huku akiyatikisa makalio yake laini, alipofika kwenye ngazi za kupanda juu ghorofani akawa anapanda kama mlimbwende huku kila akipanda ngazi tatu alizitikia nywele zake kwa madaha na kunogesha mvuto wake, akafika ngazi ya juu kabisa ili atokomee, hapo akasimama, alafu akageuka kwa upesi kunitazama, tukakutanisha macho yetu, alafu akaachia tabasamu jepesi la ulaghai kisha akainua mkono wake na kuniaga kwa ishara za kizungu, alafu akapotea kama jinni la kwenye vitabu vya Kigiriki.
Kulipambazuka, siku ya leo Shemeji alikuwa akifanya usafi wa ndani ya nyumba, nilipotaka kumzuia akanikataza, akasema yeye ni mwanamke hivyo usafi wa ndani ni jukumu lake, nikatoka kwenda nje kumwagilia maua na shughuli za nje, tulipomaliza usafi tulienda kunywa chai. Asubuhi ya leo Shemeji alikuwa na furaha zaidi kuliko siku zote.
“Kesho utaanza shule, nimekutafutia shule mwanangu” Shemeji akasema akimtamza mtoto wake.
“Shule nyingine tena mummy, Neyla naye atakuwepo” Mtoto akasema.
“ Hapana My son, Neyla atakuja siku zijazo, ukisoma vizuri naye atakuja msome wote, lakini ukiwa hautaki kwenda shule asubuhi unalialia, hatakuja kusoma na wewe”
“Sitakuwa nalia Mummy, nataka kusoma na Neyla” Mtoto alisema.
“Usijali mwanangu, maliza kula alafu leo tutatoka kwenda kuogelea” Shemeji akasema.
“ Gibson, utajiandaa tutatoka muda mfupi ujao, sawa?” Shemeji akanigeukia akinitazama kwa macho yaliyoficha hila za mapenzi.
“ Sawa! Lakini tunaenda wapi Shemeji”
“ Mmh! Gibson hujachoka tuu kukaa ndani kama mwali kwa kiluguru?”
“ Haha! Hamna shemeji, sawa nimekuelewa!” Nikajibu
“ Sawa, sisi ngoja tukajiandae, tukija uwe tayari” shemeji akasema hukua akiamka kwenye kiti na kipenzi chake kifupi kilichoacha kwa shemu kubwa mapaja yake wazi. Alikuwa akiishi maisha ya kizungu kwa kiasi kikubwa, kuna wakati nilifikiri tupo kwenye maigizo ya filamu za kisasa, lakini wala hatukuwa kwenye maigizo isipokuwa ilikuwa ni maisha halisi.
Sikuwa na mambo mengi ya kujiandaa, hivyo nilivyooga nikapaka tuu mafuta na kurudi sebuleni kuwasubiri. Shemeji alitoka akiwa amependeza mno, sikufikiria kama shemeji angefikia kiwango kile cha uzuri, alikuwa amevaa gauni la lastiki lililoushika mwili wake vizuri, likiwa limening’inia juu ya mapaja yake na kuachia mpasuo mdogo kwa mbele, lilikuwa la rangi ya kijani kibichi, shingoni alikuwa na mkufu wa silva ing’aayo, akiwa na herein zake ndogo masikioni, alivaa viatu vyenye kisigino kirefu cha wastani, mkononi akiwa na bangili ya rangi kama ya kijani mpauko, alikuwa kapendeza sana.
Nilikuwa nimeduwaa nikiwa namtazama akiwa anashuka kwenye ngazi polepole kwa madoido huku akitabasamu na kupiga hatua zake kwa tahadhari kwa mwendo wa catwalk, mara kwa mara alinyanyua mkono wake akizitoa nywele usoni kwa mbwembwe utadhani muigizaji mahiri wa filamu; akili haikunirejea mpaka aliponikaribia na kusimama mbele yangu kama malaika mwema na kujigeuza shaaa, nikasikia harufu ya manukato yake mazuri ajabu, kiukweli shemeji alikuwa mzuri wala sitaki kumsifia tena isijeonekana nilikuwa namtamani.
“OOH! My dear! Umevaa nini hii! Subiri nakuja” Shemeji akasema, kisha akapanda tena juu ghorofani. Hazikupita dakika nyingi akarudi akiwa na fuko lenye nguo ndani yake.
“Hizi nguo hazijavaliwa, Riadi aliletewa na Mwanamke mmoja wa kizungu ambaye kwa kweli ananiudhi sana, nahisi wanatoka naye” Shemeji akasema,
“Unamaana gani kusema hivyo?”
“Gibson, wewe sio mtoto mdogo, embu vaa tuondoke muda umekwenda” Akasema,
ITAENDELEA Kesho saa 7mchana