Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
- Thread starter
- #81
SEHEMU YA 39
Mama hakuamini akaenda nje kuangalia, mara sauti
ikaniambia tena
"Au nizikaushe kabisa na kuzikunja?"
Nikaanza kutetemeka sasa bila ya kujua cha kusema,
ile sauti ikajirudia tena nikajikuta nikisema kwa nguvu
"Hapana"
Kwani najua yale maajabu ya zaidi sasa
yatamuogopesha hata mama.
Mara mama nae akarudi ndani na kuniuliza vizuri,
"Hivi zile nguo Sabrina umefua au umezianika tu? Na
hata kama kuanika tu ndio ndani ya dakika mbili
kweli?"
Nilikaa kimya nikimtazama mama aliyeendelea
kuongea
"Hata kama maajaabu hii ni too much jamani,
kwakweli kwa mtindo huu basi hata watu hawana
haja ya kununua mashine za kufulia, kwakweli
Sabrina leo umenipa kali ya mwaka yani umenitoa
jasho kabisa. Hivi nilizaa mtu au kitu gani jamani!"
Nikatulia kimya kamavile sio mimi ninayeambiwa
kuwa mtoto wa ajabu kwani hata cha kumuelezea
mama sikuwa nacho, mama nae hakuacha kuongea
najua sababu ya kutojielewa hata yeye pia.
"Kwakweli leo Sabrina umefanya nibaki mdomo wazi
maana hata cha kusema nakosa, hebu nikuulize kitu"
"Niulize mama"
"Wewe una majini au umekuwa mchawi mwanangu?"
"Kwanini mama?"
Mama akawa mkali kweli leo,
"Usiniulize kwanini wakati unafanya mambo ya ajabu,
usiku unaogopa unaogopa kumbe unawaogopa
wenzio wanaoruka angani huko. Haya niambie
uchawi umeutoa wapi?"
"Ila mimi sio mchawi mama"
"Kama sio mchawi umewezaje kufua zile nguo zote
kwa dakika mbili? Umewezaje Sabrina?"
"Sio mimi mama"
"Kwahiyo ni nani?"
"Sijui mama"
"Si unaona ushetani wako, eti hujui! Kwakweli leo
umenimaliza Sabrina"
Mama akakaa chini kama mtu aliyechoka sana,
sikuwa na la kufanya kwani hata mie ile hali ilinitesa
sana na machozi kunitoka tu, mama hakutaka kabisa
kuamini chochote nilichomueleza na kufanya nizidi
kupatwa na mawazo.
Mchana ulipofika dada alikuwa amesha wasili
nyumbani na kufanya tushangae kilichomuwahisha na
leo. Mama akaanza kumuuliza,
"Vipi mbona umewahi sana leo?"
"Fatuma alikuwa na matatizo kwahiyo tukaomba
ruhusa na kuondoka"
"Matatizo gani tena? Yale yale ya jini mahaba au?"
"Mmh matatizo mengine tu, inabidi kesho
nimsindikize tena kwa mtaalamu wake"
"Ukienda uende na huyo"
Akininyooshea mimi kidole,
"Kwanini mama?"
"Hebu angalia nyuma huko nikupe sababu"
Dada akachungulia dirishani,
"Khee mmefua nguo zote zile? Poleni sana"
"Pole mpe huyo mashine ya kufua kwa dakika mbili"
Huku akimuonyeshea kwangu,
"Kivipi mama?"
"Mdogo wako ana mashine ya kufulia kwenye mikono
hata nguo ziwe zingi vipi zitafuliwa kwa dakika mbili
tu"
Dada akawa anashangaa tu kwamaana hakuelewa
chochope, hapo ndipo mama akaamua kumueleza
jinsi ilivyokuwa.
"Mmh mama ya kweli haya? Yani ndani ya dakika
mbili?"
"Yani kufumba na kufumbua mwanangu nguo zote
zimefuliwa na kuanikwa, kwakweli leo Sabrina kanipa
kali ya mwaka yani sikufikiria kabisa"
"Sasa mama huko kwa mganga ataenda kutibiwa
nini?"
"Chochote tu ilimradi nimpate Sabrina wangu wa
ukweli maana mimi naona kama vile nimebadilishiwa
mtoto jamani"
"Usijali mama nitaenda nae"
Dada aliniangalia tu ila hakuniuliza kitu chochote kile
kuhusu nguo wala nini.
Nami nikatulia tu bila ya kujua cha kufanya.
Jioni yake nilienda chumbani kwangu kupumzika
maana mawazo nayo yalikuwa ni mengi sana tena
bila ya uelekeo wa maana, nilihisi kamavile naanza
kutengwa na dunia.
Simu yangu ikaingia ujumbe mfupi, ulikuwa umetoka
kwa wifi yangu Joy.
"Napenda kukusaidia Sabrina ila nasindwa sababu ya
siri yangu, ikitoka nitaumbuka sana mdogo wangu"
Nikatamani kupata huo msaada wa wifi Joy ila je
atanisaidiaje wakati kasema kuwa ameshindwa,
nikatunga sheria zangu na kuamua tena kutoka pale
nyumbani nia yangu ni kukutana na Sam labda
nimueleze yeye atanisikia.
Nikampigia simu Sam,
"Nataka kuonana na wewe Sam"
"Basi acha nije kwenu"
"Hapana, sitaki kwenu wala kwetu. Nataka tukutane
mahali"
Nikapanga mahali pa kuonana na Sam kisha
nikaondoka nyumbani bila kuaga kwani hata nikiaga
haina maana kwasasa.
Nikiwa njiani kuelekea ambapo nimepanga kukutana
na Sam, nikashtuliwa na mtu kwa kushikwa bega.
Nikageuka kumwangalia ni nani, kumbe alikuwa ni
dada Salome. Kisha akaniambia,
"Yani hapa nilikuwa nabahatisha tu kukushika ili nijue
kama ni wewe"
"Kwanini dada?"
"Sijui siku hizi mpo wawili au ni wewe mwenyewe"
"Mmh dada kwanini?"
"Nimekutana na Sabrina mwengine muda sio mrefu,
kavaa gauni la pinki na viatu virefu"
Nikamwambia anielekeze hivyo viatu, aliponielekeza
nikagundua kuwa ndio vile viatu nilivyopewa na
Carlos na aliponivua nilijikuta nikiwa nyumbani, iweje
sasa nionekane na hivyo viatu? Nikamuuliza,
"Je uliongea na huyo Sabrina?"
"Ndio, inamaana sio wewe niliyekutana nae? Basi
mpo wawili maana nilitaka kukuuliza hapa kuwa
umerudi muda gani kwenu na kubadilisha nguo hadi
sasa uko hapa!"
Nikabaki kimya maana hata cha kuongezea nilikosa
yani nimeanza kuonekana mara mbili mbili basi ni
maajabu kwakweli.
Nikaagana na dada Salome na kuendelea na safari
yangu.
Nilipofika nikamkuta Sam ameshafika tayari,
"Khee, umewahi sana Sam"
"Ndio lazima niwahi kwaajili yako"
"Ila mbona kama una mashaka sana?"
"Hapana Sabrina nipo kawaida tu"
"Ila kutoka kule kwenu hadi hapa ni mbali sana,
sikujua kama ningekukuta"
"Leo nimepata usafiri wa haraka sana Sabrina,
nimekuja kukusikiliza mpenzi"
Nikaanza kumueleza matatizo niliyo nayo na mambo
yote ninayokumbana nayo kila siku haswa hili la leo
kuhusu nguo, kisha akaniuliza
"Kilichokushtua zaidi ni nini?"
"Kilichonishtua zaidi ni kuhusu nguo mpenzi wangu"
"Sasa wewe Sabrina huoni raha hiyo? Yani unaweka
tu nguo ndani ya dakika mbili zote zimefuliwa na
kuanikwa, hiyo itatusaidia kwenye maisha yetu
tunaweza hata kufungua kampuni na kula pesa za
ufuaji tu"
"Acha masikhara Sam, yani unaona ni kitu cha
kawaida hiki mpenzi?"
"Sijaona tatizo bado, naona kawaida tu kwani
itatusaidia badae"
"Na haya mauzauza ninayokumbana nayo je?"
"Mbona sioni tatizo Sabrina! Usikuze mambo bhana,
hivyo ni vitu vya kawaida tu ila punguza uoga"
Majibu ya Sam leo yalinichanganya sana na kunipa
maswali kuwa mbona kabadilika sana au kwasababu
ya kukaa rumande! Sam wa leo alinichanganya sana
maana kila nilichoongea alinipanga hadi kufanya nijute
kuja kuonana na Sam na kumuelezea matatizo yangu,
nikaamua kumuaga kuwa narudi nyumbani.
"Poa safari njema"
"Mbona umebadilika sana Sam! Yani hata
kunisindikiza kidogo?"
"Me sijisikii kutoka hapa muda huu kwakweli"
"Kwahiyo utaondoka muda gani?"
"Muda nitakaopenda mimi"
Sikutaka kuendelea kubishana nae zaidi na kuamua
kurudi tu nyumbani maana Sam alishanikera.
Kufika tu nyumbani nikakumbana na maswali toka
kwa mama,
"Eeh umetoka wapi muda huu?"
"Nimetoka hapo tu mama"
"Kwahiyo umeanza kuondoka hapa nyumbani bila ya
kuaga?"
"Hapana mama, nisamehe"
"Au ndio unataka kunionyesha uwezo wako wa kufua
nguo kwa dakika mbili? Mbona umekuwa hivyo
Sabrina? Hukuwa hivyo mwanangu, umebadilika
sana"
"Nisamehe mama"
"Nisamehe ya kila mara haina nguvu, mtu gani wewe
muda wote unafanya mauza uza halafu unaona
kuomba msamaha ndio dili, kwakweli sipendezewi na
tabia yako ya sasa Sabrina mwanangu"
Nikaingia ndani tu huku mawazo yakinitawala kwani
hadi familia yangu imeanza kunichukia kwa haya
mauzauza ambayo nakumbana nayo.
Muda wa kula ukafika, nikala na kwenda kulala
chumbani kwangu maana najua hata mama hawezi
kukubali kulala na mimi tena.
Nikiwa chumbani kwangu, nikajaribu kupiga simu kwa
Sam ili nione kama amesharudi kwao ila simu yake
haikupokelewa nikaona Sam ananifanyia makusudi
ukizingatia na majibu ya leo aliyonipa nikadhani Sam
atakuwa amenichoka tu ila sikuwa na la kufanya
kwavile bado nampenda sana tena sana.
Usingizi ukanipitia wakati nipo kwenye mawazo.
Nikiwa kwenye ndoto, nikamuona yule kijana wa
ndotoni akija mbele yangu kwa tabasamu kali sana
huku akisema,
"Nimekukomesha leo Sabrina"
Halafu nikawa kama naangalia video vile, nikamuona
yule kijana wa ndotoni akitembea halafu mbele kidogo
akajigeuza na kuwa Sam kisha akaja kukutana na
mimi, akanipa mkono kumsalimia kisha akaanza
kucheka na sura yake ikabadilika tena na kuwa kijana
wa ndotoni akacheka na kusema,
"Umeona Sabrina! Naweza fanya chochote nitakacho"
Nikashtuka toka usingizini huku nikihema kwa nguvu
sana kwa uoga wa ile ndoto.
Nikajiuliza, inamaana niliyekutana nae leo sio Sam?
Moyo wangu ukaniambia kuwa inawezekana ni kweli
kwamba niliyekutana nae si Sam.
Nikachukua tena simu yangu na kumpigia Sam ili
kupata uhakika, iliita bila kupokelewa ila nilipopiga
tena Sam alipokea na kuongea kiusingizi;
"Mbona usiku sana Sabrina?"
"Eti leo tumekutana wapi?"
"Maeneo ya kwetu huku umesahau?"
"Hebu nikumbushe nilivaeje?"
"Mmh nawe Sabrina mbona una vituko, maswali gani
hayo ya kuulizana usiku huu? Mi nina usingizi bhana,
usiku mwema. Nakupenda"
Akakata simu ila mimi bado nilihitaji kujua ukweli
kwani hata mahali pa kukutana aliposema Sam sio
penyewe, nikaamua kumpigia simu tena ili kumuuliza
vizuri.
"Samahani mpenzi wangu Sam, naomba unijibu"
"Ulivaa gauni la pinki na viatu virefu"
Hapo nikashtuka sana, nikakumbuka nilivyoambiwa
na dada Lucy kuwa ameniona nimevaa hivyo
kwakweli nilishangaa sana kuwa kweli kuna Sabrina
wawili. Sam akanistua,
"Vipi Sabrina, una tatizo gani kwani maana hata
ulipokuja kuonana na mimi haukuwa sawa kabisa"
"Kwani mimi nilikwambia tuonane wapi mwanzoni?"
"Mwanzoni ulisema pale tulipokuwa tunakutana
zamani ila badae ukanipigia simu na kusema unakuja
mitaa ya kwetu huku, umesahau Sabrina! Tena
uliwahi kweli kabla yangu hadi nikakuuliza kuwa
umepaa nini. Umesahau?"
"Basi Sam, tutaongea kesho"
Nikakata simu na kubaki na mawazo kichwani na
sikuelewa pa kuanzia wala kuishia.
Gafla nikaitwa,
"Sabrina"
Nikashtuka sana nusu ya kuzimia kabisa jinsi
nilivyoshtuka kumbe alikuwa mama ananiita, nikatoka
chumbani kwangu na kumfata sebleni.
"Mbona usiku mama?"
"Usiku wa kikwenu huu? Ni alfajiri sasa, amka
ujiandae maana unapoenda na dada yako ni mbali,
Mwende mkayawahi yale mabasi ya asubuhi ya
mikoani ili muwahi kurudi"
Sikubisha, nikajiandaa kila kitu kwaajili ya hiyo safari.
Dada nae alipomaliza kujiandaa, tukawa tayari kwa
kuondoka.
Mama akaniita tena kabla ya kuondoka,
"Hebu nikuangalie kwanza isije kuwa na leo umevaa
yale maviatu yako ya kichawi"
Akaniangalia sana, aliporidhika akaniruhusu kuondoka
na dada.
Tukaenda moja kwa moja hadi anapoishi dada
Fatuma, tukamkuta nae ameshajiandaa na kuendelea
na safari.
Kufika njiani tulikutana na Carlos aliyetupa lifti hadi
karibu na eneo tunalokwenda huku akidai kuwa na
yeye anasafari za maeneo hayo. Dada Penina na
Fatuma walifurahi sana kuokoa nauli kwa lifti hiyo ya
masafa marefu.
Tulipofika, Carlos akatushusha na kuondoka zake
kisha na sisi kuendelea na safari yetu hadi kwa huyo
mtaalamu, kwakweli kulikuwa na umbali sana ila hadi
tukafika eneo la tukio.
Kuingia kwa mganga sasa, dada Penina na Fatuma
wakaingia ila wakati naingia mimi tukashangaa yule
mganga akipiga kelele na kuniambia,
"Vua viatu hivyo"
Nikashangaa maana leo nilivaa viatu vya kawaida na
pale mlangoni pa mganga nilishavivua, ila yule
mganga akaendelea kupiga kelele kuwa nivue viatu.
Mara gafla yule mganga akaanguka chini na kuanza
kutapatapa huku povu likimtoka mdomoni, kila mmoja
alishtuka na kushangaa mambo yale ya ajabu.
wakati nashangaa yale mambo nikainama na
kujitazama miguuni. Nikashtuka sana kwani nilijikuta
nimevaa vile viatu vya majanga.
Itaendelea