Simulizi ya Moyo na Koti Jeusi- Jamani analia sana

Simulizi ya Moyo na Koti Jeusi- Jamani analia sana

“Simulizi ya Moyo na Koti Jeusi”

Kuna wakati, nchi yenye mwanga wa jua mchana kutwa iliongozwa na mtu aliyekuwa na mtetemeko usiojulikana, mtetemeko wa kifua, lakini pia wa dhamira. Alikuwa na nguvu za ajabu; alilazimika kupiga teke mfumo hadi ukasahau jina lake. Kwa watu wengine, ilionekana kama juhudi ya kuokoa; lakini kwa walioumizwa, ilikuwa ni radi inayowasha moto wa kimya.

Kabla ya kila hatua, alihakikisha kinga iko mkononi, si kinga ya mwili, bali kinga ya utii. Alisafisha uwanja wa wachunguzi na kuweka wasikia sauti tu. Alifikiri ameweka makamu wa amani, kumbe alizima taa na kuacha wengine kuona gizani. Kilichomponyoka ni kwamba walioonekana kusukumwa nje ya ubao, walikuwa wameshachora mchezo mwingine kwenye sakafu ya chini ya meza.

Katikati ya mkanganyiko huo, alikuwepo mtu aliyevaa koti jeupe lakini lililoshonwa kwa sindano za heshima, si taaluma. Mtu huyu alikalia kitanda cha dhamira ya nchi akawa mshika mpini wa pumzi ya yule aliyekuwa juu ya viti vyote. Kila anayegusa kidonda, alikutana na jina la huyo mwenye koti jeupe.

Siku moja, mlio wa mwisho wa moyo ukasikika. Mlango ulipofunguliwa, aliyekuwa nao chumbani ni huyo huyo mwenye koti jeupe. Hapo ndipo vichwa vilipoanza kuinama, lakini si kwa maombolezo, kwa tafakuri.

Miaka ikapita. Jina la mtu huyu likasikika tena, safari hii si kwa tiba bali kwa taji – taji la bara. Aliomba kuvalishwa ushindi wa kiafya wa bara zima. Lakini kaburi la ukweli lilianza kufukua mifupa ya maswali.

Wasomi wakachambua, wakachoma, wakafunua: Koti lake jeupe halikuwa la ushonaji wa darasani, bali la shukrani za mdomo. Vyeti vya taaluma vikaonekana kuwa vya nguo za kukodi – havikupitia mvua ya mtihani. Na kama radi, CV yake ikatoweka kama moshi kwenye tovuti. Ilipoibuka tena, palikuwa hakuna tena alama ya moyo


Britanicca
Unajifanyaga una unajimu wa kisiasa kweli, lakini nimekufuatilia kwa muda sasa. Wewe ni kalunguyeye tu!
 
Magufuli alikufa na Corona wazee tusidanganyane na vile alikua anatumia na mbaazi za Manyara ndo alienda fasta maana corona ilimpiga baada ya kugusana na Maalim Seif watu wake wa karibu wakaanza kukuputikana pia....Kijazi, akaenda na maji aliyekuwa Katibu wa Rais Ofisi ya Rais akaenda na maji ...Ukichanganya na ule Moshi wa wazee kule Ruangwa ndo basi kbs.

Hakuna cha Koti wala nini
 
Mayor Quimby huyu koti jeupe mpaka ana jipenyeza kuwa daktari wa moyo, secret service ya mwendazake walikuwa wame lala tu?
Kiongozi we mwenzetu kama umeweza ng’amua hii allegory ya britanicca labda unirahisishie na mimi.

Binafsi kwa unga-unga naweza sema labda nimeelewa kwa asilimi 20% hiyo haitoshi kusema nimeilewa post yake.

All I know huko serikalini kwa sasa inaonekana kama vile kuna vurugu machi, itaishia vipi sijui. Lakini mleta mada hapa na pale anatabia ya kutabiri mazito ya nchii hii na kutokea.
 
Jinsi janabi alivyo jipenyeza mpaka kuwa daktari wa raisi mambo ya moyo wakati phd yake ni ya research tu, sio clinical(haruhusiwi kuona wagonjwa) inafikirisha sana hii nchi
Janabi alikuwa daktari wa moyo huko Japan kabla ya kikwete kuwa Rais,

Wewe unamfahamu walipo ombwa na kikwete kuanzisha JKHI pale muhimbili?

Mkuu usiongee mambo usiyoyafahamu?
 
Kiongozi we mwenzetu kama umeweza ng’amua hii allegory ya britanicca labda unirahisishie na mimi.

Binafsi kwa unga-unga naweza sema labda nimeelewa kwa asilimi 20% hiyo haitoshi kusema nimeilewa post yake.

All I know huko serikalini kwa sasa inaonekana kama vile kuna vurugu machi, itaishia vipi sijui. Lakini mleta mada hapa na pale anatabia ya kutabiri mazito ya nchii hii na kutokea.
story ina muhusu jemedari wa awamu ya 5 ambae ali sifika kwa ubabe na dhamira yake ya mabadiliko..

jemedari huyu kwa kujua au kuto kujua ali chagua makamu kiwembe, aki amini hata msumbua kumbe hakujua kesho yake.

ina semekana jemedari huyu alikuwa na ugonjwa upande wa kushoto wa kifua, ambapo ghafla kuli ibuka daktari mmoja wa lishe aliye jifanya anao uwezo wa kumsaidia.

usaidizi wa daktari huyu wa lishe uli peleka msiba kwa familia na wapenzi wa jemedari, huku kicheko kiki tawala kwa msaidizi na ndugu zake.

Daktari wa lishe a.k.a the so called cardiac doctor ali zawadiwa uangalizi wa afya wa bara la afrika Kama shukrani, wachunguzi walipo chunguza elimu yake ili gundulika hamna kitu zaidi ya shukrani kutoka kwa msaidizi na wajomba zake Mayor Quimby
 
Back
Top Bottom