Simulizi ya Moyo na Koti Jeusi- Jamani analia sana

Simulizi ya Moyo na Koti Jeusi- Jamani analia sana

“Simulizi ya Moyo na Koti Jeusi”

Kuna wakati, nchi yenye mwanga wa jua mchana kutwa iliongozwa na mtu aliyekuwa na mtetemeko usiojulikana, mtetemeko wa kifua, lakini pia wa dhamira. Alikuwa na nguvu za ajabu; alilazimika kupiga teke mfumo hadi ukasahau jina lake. Kwa watu wengine, ilionekana kama juhudi ya kuokoa; lakini kwa walioumizwa, ilikuwa ni radi inayowasha moto wa kimya.

Kabla ya kila hatua, alihakikisha kinga iko mkononi, si kinga ya mwili, bali kinga ya utii. Alisafisha uwanja wa wachunguzi na kuweka wasikia sauti tu. Alifikiri ameweka makamu wa amani, kumbe alizima taa na kuacha wengine kuona gizani. Kilichomponyoka ni kwamba walioonekana kusukumwa nje ya ubao, walikuwa wameshachora mchezo mwingine kwenye sakafu ya chini ya meza.

Katikati ya mkanganyiko huo, alikuwepo mtu aliyevaa koti jeupe lakini lililoshonwa kwa sindano za heshima, si taaluma. Mtu huyu alikalia kitanda cha dhamira ya nchi akawa mshika mpini wa pumzi ya yule aliyekuwa juu ya viti vyote. Kila anayegusa kidonda, alikutana na jina la huyo mwenye koti jeupe.

Siku moja, mlio wa mwisho wa moyo ukasikika. Mlango ulipofunguliwa, aliyekuwa nao chumbani ni huyo huyo mwenye koti jeupe. Hapo ndipo vichwa vilipoanza kuinama, lakini si kwa maombolezo, kwa tafakuri.

Miaka ikapita. Jina la mtu huyu likasikika tena, safari hii si kwa tiba bali kwa taji – taji la bara. Aliomba kuvalishwa ushindi wa kiafya wa bara zima. Lakini kaburi la ukweli lilianza kufukua mifupa ya maswali.

Wasomi wakachambua, wakachoma, wakafunua: Koti lake jeupe halikuwa la ushonaji wa darasani, bali la shukrani za mdomo. Vyeti vya taaluma vikaonekana kuwa vya nguo za kukodi – havikupitia mvua ya mtihani. Na kama radi, CV yake ikatoweka kama moshi kwenye tovuti. Ilipoibuka tena, palikuwa hakuna tena alama ya moyo

Britanicca
Nakiri kuzeeka,macho yangu yameingia giza, siwezi tena kuona ndani,hivyo hapa niko gizani, kama kuna mwenye tochi naomba animulikie!

Sii wengi wanaofahamu kuwa japo simba ni mnyama mla nyama,simba akizeeka,hawezi tena kula nyama,hula majani!。
P
 
Bila shaka anamzungumzia yule Dr. Bingwa wa moyo, aliyehusika kumtibu mzee naniliu mpaka mauti. Inasemekana hana sifa za kitaaluma za mambo ya moyo, alifanya vi short course vya kuunga unga hapa na pale. 'Ubingwa wake' ni wa kisiasa zaidi.

Lakini pia baadi ya wambeya na waongo wanamyooshea kidole kuwa alimpotosha sana marehemu, alikuwa anamwambia ni uchovu tu asijali, kumbe anajua kuwa yaliyomo yamo na ni suala la muda tu lazima mtu atwaliwe.

In short, ukiwa kiongozi Afrika ukaugua afadhali uende ulaya, hata kama wanakuchukia lakini wana integrity. Kagame na Museveni walikuwa huko na wamerudi salama. Mambo ya kukimbilia ile 'hospitali jijini Dar es Salaam' pale makumbusho sio kabisa, kwa mujibu wa wambeya na waongo tena watu wa hovyo kabisa huko vijiweni.
 
Tatizo hapa ni MCT
Imejaa vilaza
Yaani Japan na US ikubali asome kama Cardiologist halafu MCT sijui ya bongonyoso ihoji?
Sasa WHO na X nani anaekuwa na uhalali wa kuhoji?
US hakuwahi kusoma hiyo kitu. Walimpa ceremonial tu, ndiyo maana katika CV yake mpya akiwa anagombea WHO hizo taaluma nyingine alizinyofoa au zilifafanuliwa.
 
hii inaconnect vp na current situation ?? au kuna mtu hili ni bomu analo anataka kusambaratishia wenzie 🤔🤔
 
“Simulizi ya Moyo na Koti Jeusi”

Kuna wakati, nchi yenye mwanga wa jua mchana kutwa iliongozwa na mtu aliyekuwa na mtetemeko usiojulikana, mtetemeko wa kifua, lakini pia wa dhamira. Alikuwa na nguvu za ajabu; alilazimika kupiga teke mfumo hadi ukasahau jina lake. Kwa watu wengine, ilionekana kama juhudi ya kuokoa; lakini kwa walioumizwa, ilikuwa ni radi inayowasha moto wa kimya.

Kabla ya kila hatua, alihakikisha kinga iko mkononi, si kinga ya mwili, bali kinga ya utii. Alisafisha uwanja wa wachunguzi na kuweka wasikia sauti tu. Alifikiri ameweka makamu wa amani, kumbe alizima taa na kuacha wengine kuona gizani. Kilichomponyoka ni kwamba walioonekana kusukumwa nje ya ubao, walikuwa wameshachora mchezo mwingine kwenye sakafu ya chini ya meza.

Katikati ya mkanganyiko huo, alikuwepo mtu aliyevaa koti jeupe lakini lililoshonwa kwa sindano za heshima, si taaluma. Mtu huyu alikalia kitanda cha dhamira ya nchi akawa mshika mpini wa pumzi ya yule aliyekuwa juu ya viti vyote. Kila anayegusa kidonda, alikutana na jina la huyo mwenye koti jeupe.

Siku moja, mlio wa mwisho wa moyo ukasikika. Mlango ulipofunguliwa, aliyekuwa nao chumbani ni huyo huyo mwenye koti jeupe. Hapo ndipo vichwa vilipoanza kuinama, lakini si kwa maombolezo, kwa tafakuri.

Miaka ikapita. Jina la mtu huyu likasikika tena, safari hii si kwa tiba bali kwa taji – taji la bara. Aliomba kuvalishwa ushindi wa kiafya wa bara zima. Lakini kaburi la ukweli lilianza kufukua mifupa ya maswali.

Wasomi wakachambua, wakachoma, wakafunua: Koti lake jeupe halikuwa la ushonaji wa darasani, bali la shukrani za mdomo. Vyeti vya taaluma vikaonekana kuwa vya nguo za kukodi – havikupitia mvua ya mtihani. Na kama radi, CV yake ikatoweka kama moshi kwenye tovuti. Ilipoibuka tena, palikuwa hakuna tena alama ya moyo

Britanicca
Kwahiyo we britanicca "jamani analia sana" ni kivumishi baada ya kimbau mbau kufanya yake kabla hajawa Rais wa WHO Bara la Africa!!?
 
hii inaconnect vp na current situation ?? au kuna mtu hili ni bomu analo anataka kusambaratishia wenzie 🤔🤔
Ninavyo elewa "jamani analia sana"anaelia sio hayati chuma Bali bishop ntongo!Ni baada ya kujua kwamba CV ya kimbau mbau haihusiani na moyo na alikua kwenye jopo la afya la pale!!

Inawezekana kafanya yake kabla haya ukwaa urais bara la Africa!!

Hii ni connection ya Uzi wa safari ya kisiwa na jambo la July july!!
 
Maisha baada ya hapa duniani wataorudi kwa Mungu ni wachache mno sikuwahi kujua koti jeupe angefanya jambo kama hili katika hii dunia.Kwa heshima aliyojijengea mbele ya watu kumbe ana roho katili kiasi hiki Ee Mungu tusaidie na isitoshe ule ushindi ulikuwa ni asante yake kwa kazi aliyoifanya
 
mdomo. Vyeti vya taaluma vikaonekana kuwa vya nguo za kukodi – havikupitia mvua ya mtihani. Na kama radi, CV yake ikatoweka kama moshi kwenye tovuti. Ilipoibuka tena, palikuwa hakuna tena alama ya moyo

Britanicca
Mkuu, tunao muda mchache sana, tena 'precious' kweli kweli. Tukiendelea kwa mtindo huu hadi Oktoba sioni matumaini popote.

Ni kama nawe umeungana nao kuwatoa waTanzania kwenye kuelekeza akili zao kwenye njia sahihi za kupambana na waovu hawa.

Hizi stori hizi sijui zinawasaidia kitu gani waTanzania.

Njoo na mbinu za kupambana na maadui hawa wa nchi yetu; tuache longo longo. Huu siyo wakati wake.

Kwa mfano: binafsi ningekuelewa vizuri sana wakati huu kama ungekuja na ubunifu wa kuiimarisha NO REFORM NO ELECTION.
Hata kwa kubuni tu njia za kuwasaidia waajiriwa kulazimishwa kwenda kwenye mikutano ya waovu hawa; na kupata mikakati mingine ya kuvuruga kabisa mazingaombwe ya uchafuzi hapo Oktoba.

Sasa haya ya stori, tena za kufumbafumba na kutaka kutumia akili nyingi kujuwa kinazungumziwa kitu gani; hizi zitatupeleka hadi wapi?
 
daktari wa magufuli alikuwa mchembe, kama janabi alipata access huo mchoro ulipangwa na inner circle ya magufuli
Watu wanacheza na taaluma wasizo zielewa kabisa kwa kutojuwa taratibu za taaluma hico.
Pamoja ubovu wa tulipofikia kama nchi sasa hivi; hizi stori zinazotungwa kishamba namna hii zinaonyesha kuwa na ujinga mkubwa sana katika eneo linalo tungiwa stori zenyewe.

Magufuli alikufa kwa UVIKO, kwa nini hamtaki kuelewa jambo rahisi kama hilo?
 
Jinsi janabi alivyo jipenyeza mpaka kuwa daktari wa raisi mambo ya moyo wakati phd yake ni ya research tu, sio clinical(haruhusiwi kuona wagonjwa) inafikirisha sana hii nchi
Anayo Ph.D. ya kitu gani huyo; toka chuo gani?

Jinsi huyo alivyo piganiwa huku akiwa hana kitu cha maana, ni ishara tosha ya nchi yetu ilivyo haribikiwa sasa hivi chini ya hili Genge lililo tuteka sote.

Hadi wametumia jina la nchi na heshima kubwa ilijengeka huko siku za nyuma kumpitisha mtu asiyekuwa na hadhi ya nafasi husika.
Kwa njia hizo hizo, sasa wanakitumia chama cha Mapinduzi kuwawekea waTanzania viongozi wasiofaa!

Sasa Genge limejifunua waziwazi; lakini bado tunahangaika kutafuta ni nani anayehusika na uovu huu?

Tunapoteza muda bure.
 
Back
Top Bottom