Simulizi ya Mzee Juma Duni Haji baada ya kupewa kesi ya Uhaini inasikitisha sana .

Simulizi ya Mzee Juma Duni Haji baada ya kupewa kesi ya Uhaini inasikitisha sana .

Haya mambo yalikuwa yanafanyika awamu ambazo serikali ilikuwa haisimamii vizuri misingi ya sheria. Awamu hii ya tano chini ya JPM huyu FFU angechukuliwa hatua za kinidhamu. Leo katika vyombo vya habari nimefurahi sana kusoma habari ya askari polisi huko Zanzibar ambaye amefukuzwa kazi kwa kumpeleka mtuhumiwa akapigwe na wananchi wenye hasira kali.
Si kweli , awamu ya 5 ndio inayoongoza kwa unyama , yale ya Zanzibar ni kwa vile Zanzibar ni nchi nyingine , Mh Magufuli akihutubia kwenye Mahafali chuo cha Polisi Kurasini , alipiga marufuku polisi wanaouwa kuchunguzwa , vuta kumbukumbu vizuri
 
Si kweli , awamu ya 5 ndio inayoongoza kwa unyama , yale ya Zanzibar ni kwa vile Zanzibar ni nchi nyingine , Mh Magufuli akihutubia kwenye Mahafali chuo cha Polisi Kurasini , alipiga marufuku polisi wanaouwa kuchunguzwa , vuta kumbukumbu vizuri
Unapotosha kabisa kwanza Zanzibar sio nchi nyingine. Hapa nchini kwetu tuna nchi moja ambayo ni Tanzania. Pili jeshi la polisi ni moja tu .hakuna jeshi la polisi la Zanzibar. Tuna IGP mmoja tu. Kuhusu Rais kuruhu askari kuua na wasichunguzwe si kweli. Ndio maana wanahimizwa kufanya kazi kwa misingi ya sheria. Ila kama kuna jambazi anataka kumuua askari au raia what do you espect?
N.B soma ibara ya kwanza ya katiba ya JMT Zanzibar sio nchi nyingine. Ni sehemu ya ya Tanzania.
 
HISTORIA YA MAPINDUZI UNAPOIELEZA CHUKUA NA TAHADHARI KIDOGO

Ukiwa mwandishi watu wengi wanakujua bila wewe hata kukutananao hata siku moja.

Siku moja nilikuwa Dubai kitongoji cha Rashidiyya na ikasadifu kuwa siku hiyo ni siku ya kusoma kisa cha Isra na Miraji.

Aliyekuwa anasoma alikuwa Dr. Ahmed bin Sumeit akitokea Muscat, Omani ambae mimi nilifahamiananae kwa mara ya kwanza Kampala kwenye mkutano uliowakutanisha Waislam kutoka sehemu tofauti za dunia.

Rashidiyya hii ndiyo sehemu ambayo Wazanzibari wengi walipokelewa na wakapatiwa hifadhi baada ya kukimbia Zanzibar baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1964.

Hapa Rashidiyya kwa sababu hii kuna jamii kubwa sana ya Wazanzibari.

Nikaja kukutananae tena Johannesburgna Lamu kwenye Maulid ikawa sasa ni watu tunaofahamiana vizuri.

Ahmed bin Sumeit ni mwalimu wa ''micro biology,'' Chuo Kikuu Cha Sultan Qaboos na vile vile ni sheikh na anatoa darsa nyingi za mafunzo ya Kiislam Oman.

Sasa aliponiona pale msikitini baada ya shughuli ile akanifuata nilipokuwanimekaa kusalimiana na hapa ndipo na watu wengine wakaanza kama vile kuniangalia na kujua kuwa mingozi mwao kuna mgeni katoka Tanzania ikawa sasa, ''Wewe si Mohamed Said?'' nk. nk.

Baada ya kula chakula pale msikitini akatokea kijana mmoja akanikaribisha ofisini kwake pale msikitini akanambia angependa kunitembeza kwenye msikiti mzima anionyeshe wanayofanya pale.

Hivi ndivyo tulivyojuana ikapelekea kunieleza kisa kilichomtokea baba yake wakati wa mapinduzi.

Anasema yeye alikuwa mtoto mdogo labda wa miaka mitano.

Siku ya mapinduzi asubuhi yake nyumba yao ilivamiwa na katika hao wavamizi alikuwa jirani yao familia zao zikijuana vyema.

Baba yake alitolewa nje ya nyumba na kupigwa risasi yeye akiona kwa macho yake.

Baada ya baba yake kupigwa ile risasi alianguka chini na yule jirani yake akamfuata pale chini na kumpiga teke.

Nilimpa pole kisha sote wawili tukawa kimya mimi nimeinama nimeimisha kichwa changu na yeye pia kainamisha chake kwa huzuni bila shaka kwa kurejesha ile picha ya kumbukumbu ya marehemu baba yake.

Kwa kuuvunja ule ukimya nikamuuliza alikuja lini Dubai na kama huwa anakwenda Zanzibar.

Akaniambia kuwa anakwenda Zanzibar na katika moja ya safari zake alikutana na yule mtu aliyempiga teke marehemu baba yake.

Huyu bwana amepooza upande mmoja anatembea kwa kuburuza mguu akicha vumbi likimfuata nyuma.

Nashukuru kuwa leo nimepata nafasi ya kukieleza kisa hiki cha mtoto aliyedhulumiwa roho ya baba yake na Allah akawaweka wote wawili dhalim na yule aliyedhulumiwa na kuwakutanisha hapa hapa duniani.

Amekuja bint mtangazaji wa East African Radio kutaka tufanye mahojiano na mimi kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.

Kipindi ambacho In Shaa Allah watakirusha leo siku ya sherehe ya kumbukumbu ya mapinduzi.

Katika mengi ambayo nimeeleza nimesema kuwa historia ya mapinduzi inataka mtu unapoihadithia uchukue tahadhari sana na uchunge ulimi wako mno ili kuweka staha kwa wale ndugu zetu waliopoteza wapendwa wao kwani kuna mengi yaliyopitika ya kusikitisha.
Dah, inaumiza Sana,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili huwa uziacha nyumbani reasoning yao huwa iko chini sana,kuna kaka yangu alikuwa ana shida ya akili na ni bubu sasa ni marehemu amewahi pata dhahama kama hio aliwahipotea akasahau kurudi nyumbani akijiendea ajui aendako akanaswa na hawa jamaa walimpiga sana walimtesa sana tumesaka vituo na vituo usiku kucha asubui tumempata tazara yuko hoi kachomwa Sana na vipisi vya sigara eti aongee anajifanya bubu tulihuzunika Sana wakatuomba msamaha eti walijua sio bubu.Vitu kama hivi uleta chuki kwenye jamii,we unaona huyo ni mzee unashindwa tumia reasoning.
Mmmh, jamani Mambo yanatisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nahisi hao askari pia huwa wanaangalia na mikoa ya kufanya ukatili wa aina hyo nakumbuka mwaka fulani katika ziwa tanganyika wenyeji walikuwa na tabia ya kulima mashamba makubwa sana ya nyanya,kumbe lilikuwa kosa lakini hawakuwahi kuambiwa,basi bwana kuna mwanajeshi jina XXX akapewa ukuu wa XXX katika mkoa wa kigoma,sasa siku ya tukio.
Ametoka mwenyewe na viongozi na askari wakaenda ziwani dah walizikatakata nyanya zote hakuna hata mwananchi aliyesogea maana kama ungesogea kwenye kile kikosi ungechezea kifo cha mbwa.Basi bwana baada ya jeshi la mchana kufanya kazi yake ya mchana basi jeshi la usku likaingia pia kazini,asubuhi watu wanaamka wanaskia mkuu ana mimba mpka akaamishwa mkoa akiwa na mimba yake R.I.P
Note:kumbuka alikuwa mwanaume na mtoto alikuwa anacheza tumboni kama anamiezi mitatu au minne i hope waunganisha doti na wajuvi wa huo mkoa wanakijua hicho kisa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Aliwaweza mchana nao wakamuweza usiku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapotosha kabisa kwanza Zanzibar sio nchi nyingine. Hapa nchini kwetu tuna nchi moja ambayo ni Tanzazania. Pili jeshi la polisi ni moja tu .hakuna jeshi la polisi la Zanzibar. Tuna IGP mmoja tu. Kuhusu Rais kuruhu askari kuua na wasichunguzwe si kweli. Ndio maana wanahimizwa kufanya kazi kwa misingi ya sheria. Ila kama kuna jambazi anataka kumuua askari au raia what
do you espect?
N.B soma ibara ya kwanza ya katiba ya JMT Zanzibar sio nchi nyingine. Ni sehemu ya ya Tanzania.
Hakuna mkoa wenye Rais na wimbo wake wa Taifa , juzi kwenye sherehe za mapinduzi matukufu ulimuona aliyekagua gwaride , ni nani yule ? soma katiba ya Zanzibar achana na hilo lijitabu lenu ambalo Magufuli amelikanyaga hadi limeoza
 
Hakuna mkoa wenye Rais na wimbo wake wa Taifa , juzi kwenye sherehe za mapinduzi matukufu ulimuona aliyekagua gwaride , ni nani yule ? soma katiba ya Zanzibar achana na hilo lijitabu lenu ambalo Magufuli amelikanyaga hadi limeoza
Je ni dola huru! Inayomamlaka ya kungia mikataba na nchi zingine au jumuia za kimataifa kama OIC?
 
Hakuna mafunzo ya askari yanayolazimisha askari kuvunja sheria na kufanya ukatili. Huu ni uongo.
mzee askari ndio wanavyofunza hivo wanasomeshwa kuwa aduwi namba moja wa tz ni muislamu, muarabu na mzanzibari na akiwa muslamu anafunzwa kuwa adui namba moja ni mpizani.
 
Mabuto ndiye aliyesababisha. Wewe unapofanya mipango na wageni umwue ndugu yako, ni nani mwenye laana kati ya wewe na mgeni uliyemwalika kukusaidia kumwua ndugu yako?
Mbali na mapungufu yake, Mobutu alikuwa mateka!!
 
Back
Top Bottom