Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
patamu hapoSIMULIZI YA MAISHA : Mzigo wa Bosi uliharibu maisha yangu
MWANDISHI: Gilbert Evarist Mushi
PHONE: +255621249611
Sehemu ya 10
Kwa haraka akili yangu ikapata wazo ambalo sikuhitaji hata kulifikiria mara mbili, nikaushika mskani wa gari hili na kujitahidi kukunja upande wangu, cha kumshukuru Mungu gari likakubali kukunja kona na kutoka barabarani na kuanza kuporomoka kwenye mporomoko mfupi na kuingia kwenye mtaro wa maji ulipo pembezoni mwa hii barabara. Nikajikuta nikihema sana mara baada ya gari hili kutulia tuli ndani ya mtaro huu.
Hazikupita hata dakika mbili nikastukia mlango ukifunguliwa na askari walio shika bunduki zao wakijihami kwa chochote ambacho kitatokea kwa muda huu. Wakaanza kunifungua mkanda wa siti niliyokalia kisha wakanichomoa mimi na kunilaza chali huku wakinizunguka. Wakayatoa mabegi yangu ambayo yana viatu, wakamtazama Chalamala kisha na yeye wakamchomoa ndani ya gari hili. Gari maalumu la wagonjwa likafika katika eneo hili, madaktari waliovalia makoti meupe kwa haraka wakashuka katika eneo nililolazwa na askari hawa, wakaniweka juu ya machela yao.
Madaktari hawa wakaninyanyua na kunipeleka barabarani na kuniiingiza kwenye gari lao la wagojwa. Askari watatu nao wakaingia kwenye gari hili wakiwa na pingu mikononi mwao.
"Jela inanihusu mimi, ee Mola nisaidie"
Nilizungumza kimoyo moyo huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, furaha ambayo niliipata kwa muda mchache mara baada ya kuonana na Chalamala, yote imetoweka kwani kwa akili za haraka haraka tayari nimeshagundua kwamba hali imekuwa tete kwa upande wangu. Hata madaktari wanacho niuliza kwa ishara ya vitendo sikuweza kuvielewa kutokana na kujawa na hofu kubwa sana ya kukamatwa na polisi hawa.
‘Eheee mama huko ulipo nisaidie Gilbert mwanao, ninakwenda Jela mimi’
Niliendelea kuzungumza kimoyo moyo huku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu, dripu la maji niliyo tundukiwa mkononi mwangu wala sielewi hata utendaji wake wa kazi unakwenda vipi.
Nikastukia mlango wa nyuma wa hili gari ukifunguliwa, askari hawa wenye bunduki wakaanza kuruka kwenye hili gari, kisha madaktari hawa wakasaidia kunitoa katika gari hili, nikapakizwa kwenye kitanda cha wagongwa kilicho zungukwa na manesi. Nikaanza kupelekwa nisipo pajua, askari hawa hawakuhitaji kuniacha hata hatua moja kwani muda wote wapo pembeni yangu. Tukaingia ndani ya lifti, hapa nikapata nafasi ya kuhesabu namba zilizopo katika lifti hii na inaonyesha tunaelekea gorofa ya Tano. Hatukumaliza hata dakika ndani ya lift hii, ikafunguliwa na manesi wakaendelea kusukuma kitanda changu hadi tukafika katika moja ya mlango, ukafunguliwa na tukaingia. Wakanilaza kwenye kitanda kimoja tulicho kikuta humu ndani, askari mmoja akatoa pingu mfukoni mwake akauchukua mkono wangu wa kushoto na kuufunga kisha akaiiunganisha na kitanda hichi cha chuma.
Machozi yakazidi kunimwagika usoni mwangu nikiamini kwamba tayari maisha yangu yamesha haribika. Nikajikuta nikianza kulaani ni kwa nini nimeingia kwenye biashara ngumu ya kuhatarisha maisha yangu. Nikazidi kulaani ni kwa nini wazazi wangu hawakuwa na maisha mazuri yenye pesa!!!
Nesi mmoja akachukua sindano ndogo, akanichoma kwenye mkono wangu ulio fungwa pingu, taratibu nikijikuta usingizi ukianza kutawala mboni zangu za macho na mwishowe nikalala fofofo.
***
Nilikuja kufumbua macho yangu nikiwa sikumbuki yamepita masaa mangapi ama siku ngapi, Pembeni yangu nikamuona askari mwengine wa kike ambaye sijamuona tangu kuja kwangu hapa.
Askari huyu alipo gundua kwamba nimeyafumbua macho yangu, kwa kupitia simu yake ya upepo aliyo ichomeka kwenye bega lake la kushoto, akaanza kuzungumza zungumza maneno kwa Lugha ya Kingereza, hakuna hata moja ambalo ninalielewa maana kingereza sikifahamu kabisa. Mlango huu ukafunguliwa wakaingia madaktari wawili, wakazungumza kudogo na huyu askari kisha askari huyu akanisogelea hapa kwenye kitanda na kunifungua pingu yangu. Taratibu madaktari hawa wakanisaidia kunikalisha kitako, askari huyu akanishika mikono yangu vizuri na kuniomba kwa ishara niinyooshe mbele nikatii, akanifunga pingu aliyo nifungua.
Daktari mmoja akamkabidhi askari huyu kitabu ambacho sijui hata kimandikwa kitu gani, askari huyu akaandika andika kisha akamrudishia daktari huyu. Askari huyu akanishika mkono wangu na kunishusha hapa kitandani. Tukatoka ndani humu, nje nikakuta askari wengine wanne wakiwa na silaha mikononi mwao. Wakanifunga mnyororo wa miguu ambao unaniwezesha vizuri kutembea, kisha wakaniweka katikati na tukaanza kutembea kueleka kwenye lifti. Ninatamani kulia ila machozi hayatoki kabisa usoni mwangu, ninatamani sana kuiona Tanzania yangu ila sina tena nafasi ya kuweza kuiona kwa maana hapa ninakwenda kunyongwa jela na sijui kama nitatoka, Nilimlaani sana Bosi Clara maana safari ya kuja Huku Nililazimishwa nikitishiwa kuuwawa ama Kulawitiwa.
"Mungu wangu ninaomba ufanye muujiza, tazama mimi ni kijana bado mdogo sana. Ndio kwanza nina miaka 21."
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikishuhudia jinsi lifti hii inavyozidi kwenda chini, tukatoka katika lifti hii na nikaingizwa kwenye gari kubwa la polisi.
"Clara bosi wangu ninafia huku kenya, Bora ningechagua kuuwawa siku ile uliponipa machaguo mawili" ... Niliwaza
Hapakuwa na askari hata mmoja ambaye alijaribu kutabasamu mbele yangu wala kunisemesha chochote. Jinsi sura zoa zilivyo jaa ‘ukauzu’ unaweza kusema ni wanaume fulani waliotoka vitani. Baada ya dakika kama arobaini na tano hivi, tukafika katika Kambi moja, nikashushwa huku ulinzi ukiwa ni mkali sana. Moja kwa moja nikapelekwa hadi kwenye chumba kimoja kikubwa, kina meza moja na viti viwili vinayo angaliana na hapa katikati vimetenganishwa na meza hiyo. Askari akanikalisha kwenye moja ya kiti akatoka chumbani humu na kuniacha mimi peke yangu. Nikaanza kutazama kila kona ya chumba hichi, nikaona kamera za ulinzi jinsi zilivyojaa kila kona ya chumba hichi. Mara baada ya muda wakaingia wanaume wawili wakiwa wamevalia suti nzuri, mmoja ni mweusi na mrefu kwenda juu, mwengine ni mfupi kiasi ila ana asili ya Kipemba. Mkononi mwa Kaka huyu wa kipemba ameshika mabegi yangu, mapigo ya moyo yakanienda kasi sana, jasho likaanza kunimwagika japo ndani ya chumba hichi kuna hewa ya ubaridi(A/C).
“Gilbert habari yako”
Kaka huyu mweusi alizungumza huku akikaa kwenye kiti cha mbele yangu. Nikatabasamu kidogo mara baada ya kuona kwamba nimekutana na mtu anaye fahamu Kiswahili vizuri.
“Salama shikamoo”
“Marahaba, unaheshima sana Gilbert, sijategemea kama ungenisalimia shkamoo"
Nikazidisha tabasamu huku nikiwa na tumaini kubwa sana baada ya kumuona ana ukarimu ambao tangu nikamatwe na hawa Wakenya sikuweza kuupata kabisa.
“Ninaitwa Daniel, mimi ni askari mpelelezi”
Hapo nikakumbuka hata Tanzania kuna Mpelelezi mahiri anayeitwa Daniel mwaseba
Alizungumza huku akinonyesha kitambulisho chake, nikakisoma kwa sekunde kadhaa kisha akakitoa mbele yangu na kukirudisha mfukoni mwake.
“Huyu mwenzangu anaitwa Martin, naye ni askari mpelezi. Hili begi unalifahamu? ”. Aliniuliza
Ofa yetu inaendelea bado. Lipia Tshs 1000 kwenda namba
Halotel 0621249611 jina GILBERT EVARIST
Kisha nitext au njoo whatsapp kwa namba 0621249611 ujipatie vipande vyote 30.View attachment 2085053
Daaaah aseeeeeeeeeeSIMULIZI YA MAISHA : Mzigo wa bosi uliharibu maisha yangu
MWANDISHI: Gilbert Evarist Mushi
PHONE: +255621249611
Sehemu ya 11
Daniel alizungumza huku Martin akiliweka begi langu juu ya meza hii. Nikalitazama kwa woga huku nikishauri kichwani mwangu, nilikatae au kulikubali.
“Ninakuuliza unalifahamu begi hili?”
Daniel alizungumza kwa ukali sana hadi nikastuka.
“Ndio, ndio, ninalifahamu”
“Ohooo vizuri sana. Unaweza kunitajia vitu livyomo humu ndani?”
“Ndio”
“Kuna nini?”
“Kuna.... Kun....kuna Pedi za Kike...". Nilijibu kwa kujiumauma
Askari huyu mwenye asili ya Kipemba akafungua zipu ya begi hili na kuanza kutoa Pedi moja moja baada ya nyingine, akatoa Kisu kidogo cha kukunja kwenye mfukono wa koti lake la suti na kukiweka pembeni ya hizi Pedi,
“Kwa hiyo una uhakika ni Pedi hizo tu ulizozitaja?”
“Eheee”
“Unaweza kuniambia kwamba ndani ya Pedi hizi kuna nini?”
“Eheee……?”
“Mara nyingi sipendi uswahili hapa ni Kenya na sio Tanzania, ukiulizwa swali jibu swali”
Daniel akanibadilikia kabisa, hata ule ukarimu alio nionyesha alivyokuwa ameingia ndani ya chumba chihi umetoweka na amekuwa kama Mbogo aliye jeruhiwa kwa risasi. Nikameza fumba zito la mate huku mwili mzima ukiendelea kunitetemeka, nikamtazama,
“Unahitaji kwenda jela eheeee?”
“Ahaa….haaa….ahaapana”
“Sema unajua ndani ya hizo Pedi kuna vitu gani?”
“Hakuna kitu”
“Haki ya Mungu Gilbert unakwenda kunyongwa jela, sema kwenye hayo mapedi ndani kuna nini?”
Daniel alizidi kuzungumza kwa ukali, nikajikuta natetemeka huku machozi yakinibubujika kwani amezidi kuwa mkali sana kwangu.
“Dogo dogo, hapa sihitaji upuuzi wa kulia, sihitaji upuuzi wa kipumbavu sema humu ndani kuna nini?”
“Kuna dawa”
Maneno haya yalinitoka pasipo kutarajia kabisa, nikamuona Daniel akitabasamu, kisha akampa ishara askari huyu mwingine akachukua pedi moja, akaichana katikati, tukakuta pakti moja ya madawa ya kulevya iliyo fichwa kitaalamu kabisa. Wakaingia askari wengine wawili huku wakiwa wamevalia gloves mikononi mwao, wakaanza kusaidiana na askari mwenzao kuzichana hizi pedi na kukuta kila moja kuna pakti ya madawa ya kulevya. Walipo maliza zoezi hili wakatoka humu ndani na kuniacha na askari Daniel.
“Kwenye maisha kama kijana unapaswa kutafuta pesa lakini si kwa njia Haramu kama hizi"
Daniel alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti chake, akashika moja ya pakti na kuitazama vizuri kisha akairudisha juu ya meza.
“Dogo ulijua kwamba unakuja Buza eheee?”
Daniel alizungumza huku akinikazia macho usoni mwangu nikazidi kutetemaka kwa woga mwingi sana.
“Sasa ukweli wako ndio unaweza kukuweka huru, sema hizi dawa umezitoa wapi?”
Sawali lake likanirudisha kumbukumbu za makubaliano mengine ambayo nilizungumza na bosi Clara,
"Endapo ikatokea umekatwa, hakikisha kwamba hutaji ni nani amekukabidhi huu mzigo endapo utafanya hivyo basi tambua Wazazi wako waliopo mbeya nitawaua kwa mikono yangu, "
“Nimekuuliza Dogo huu mzigo umetoka wapi?”
Daniel alizidi kunifokea huku akisogela karibu, akanishika bega langu la upande wa kulia na akaanza kuliminya minya.
“Zungumza haraka”
“Ni wa kwangu”
Nikapata ujasiri wa kukubali mzigo huu kwamba ni wangu ili kuyaokoa maisha ya wazazi wangu.
“Hahaaa.. Hahahahaaaaa, Gilbert wewe bado ni kijana mdogo sana na hali yako inaonekana, unadhani unaweza kunidanganya kwamba huu ni mzigo wako”
“Ndio ni wangu kwani unahisi kwamba mimi siwezi kufanya hicho unachokiona”
Nikajikuta ujasiri ukizidi kuongezeka, woga ukanipotea kabisa tayari moyoni mwangu nimesha amua liwalo na liwe na hata kunyongwa ni bora ninyongwe kuliko kuona maisha ya wazazi wangu yanaingia kwenye hali ngumu ambayo niliwaahidi wazazi wangu kwamba nitahakikisha kwamba ninatafuta pesa kwa namna yoyote ile.
“Heee okay mimi sio mzungumzaji sana ila utawaambia hao ni wapi mzigo huu umeutoa na nini muhusika mkuu katika mzigo huu”
Wakaingia wanaume wawili wenye miili mikubwa na iliyo jijenga kwa misuli, mmoja wao akaninyanyua juu juu huku akiniweka begani mwake, kila ninavyo jaribu kukurupuka anishushe chini ninashindwa kabisa kwani amenishikilia kikamilifu.
ITAENDELEA
Ofa inaendelea. Lipia Tshs 1000 tu utumiwe whatsapp hadi mwisho vipande vyote 30. Namba ya malipo ni HALOPESA NAMBA 0621249611 au Mpesa namba 0765824715 jina Gilbert
Namba ya whatsapp ni 0621249611
nashushia na chapat ya nguvu hapaSIMULIZI YA MAISHA : Mzigo wa bosi uliharibu maisha yangu
MWANDISHI: Gilbert Evarist Mushi
PHONE: +255621249611
Sehemu ya 12
Wakaniingiza katika chumba chenye maji kwenye sakafu, wakanivua nguo zangu zote na nikabaki kama nilivyozaliwa. Mmoja akachukua mpira mrefu wa maji uliounganishwa kwenye koki iliyopo humu ndani, akafungua maji hayo na yakaanza kutoka kwa wingi.
Mwanaume huyu bila ya huruma akaanza kunimwagia maji haya yenye nguvu kubwa, ninayafananisha na maji ya kikosi cha zima moto cha nchi yetu ya Tanzania. Kusema kweli sina nguvu ya kuhimili nguvu ya maji haya, nikajikuta nikianguka chini. Mwanaume huyu akaendelea kunimwagia maji naya yalio zidi kuniumiza kila sehemu ya mwili wangu yanapo nigusa. Nikajikunja mwili wangu huku nikipiga kelele ya maumivu, sipo tayari kusema kweli kuzungumza ukweli wa nani ni muhisika wa huu mzigo.
Alipoona sizungumzi chochote na wametumia zaidi ya dakika kumi na tano kuniumiza na maji haya, wakabadilisha adhabu.
Wakasimama nje ya mlango wa chumba hichi sehemu ambayo haina maji kabisa na ipo juu kidogo, wakaingiaza nyaya mbili, mwili mzima ukaanza kutetemeshwa kitendo kilicho nifanya zidizi kulia kwa uchungu sana
“Sema mzigo ni wa nani?”
Daniel alizungumza huku akiwa amesimama mlangoni pamoja na wanaume hawa, sikumjibu chochote zaidi ya kumtazama kwa macho makali yaliyojaa hasira kali sana.
“Gilbert utakufa, huu ni umeme wewe, zungumza acha ubishi wa kijinga. Huna hamu ya kurudi Tanzania eheee?”
Wakazichomoa nyaya hizi na kujikuta nikishusha pumzi kwani umeme huwa ni rahisi sana kupita kwenye maji.
“Zungumza huo mzigo ni wa nani?”
“U…na….ataka nikuda…..nganye, nimekuambia kwamba mzigo ni wakwangu. Kama kuna cha kufanya chochote nyinyi fanyeni ila ukweli huo mzigo ni wa kwangu”... Nilizungumza kwa ujasiri sana huku nikiendelea kujikunyata mwili mzima.
“Gilbert, mdogo wangu haya ni maisha. Natambua kwamba vijana wengi wa Tanzania mnafanya hivi kwa ajili ya kutoka kimaisha, ila itakuwa ni vizuri ukanitajia ni nani muhusika wa huu mzigo kwa manaa mtoto kama wewe huwezi kuwa na mzigo kama huu, mzigo ambao kusema kweli hapa hakuna mtu anaye weza kuamini kama unaweza kuwa nao. Hembu niambie basi mdogo wangu”
Daniel alianza kunibembeleza kwa maneno malaini hali iliyonipelekea kupandisha hasira zangu. Kuniadhibu anihadhibu halafu sahivi iniite kinafiki?
"We fanya unalotaka Daniel, nishakwambia mzigo ni wangu brother, tena usiniite mimi mdogo wako kinafiki wakati unataka kuniua kwa mateso."
Maneno yangu yaliamsha hasira zake zote na akazitumbukiza zile nyanya za umeme kwenye maji yaliyomo ndani ya hichi chumba na nikaanza kupigwa na shoti mwili mzima. Nikayakaza meno yangu kwa hasira kali sana huku nikimtazama Daniel kwa Jazba. Laiti ningetoka pale hakika ningemuua,
“Gilbert utakufa mdogo wangu, Sema haya madawa ni ya nani?”
"Unataka nikudanganye sio?. Ni ya kwako basi!!"
Nilimjibu kama mbogo huku nikiendela kumtazama , akazichomoa nyaya hizi za umeme na kunifanya niheme kwa nguvu kwani mtetemesho umetoweka mwilini mwangu. Nikamuona akazungumza na Mabaunsa hawa, akaingia mmoja wao, akaninyanyua na kunitoa ndani ya chumba huku nikiwa uchi, akanisimamisha mbele ya Daniel.
"Unaonekana una sura nzuri sana Gilbert. Huku ni mombasa ujue, Sasa unakwenda gerezani, wewe si jeuri utapelekwa gereza la Wanaume watukutu walioshindikana, huko watakulawiti na sura yako hiyo kama ya kike nakwambia utajuta, Huko Tanzania si ulikuwa unasikiaga tu habari za Mombasa? Nakuhakikishia moto utakaokutana nao ni zaidi ya Kwa Mparange huko buza kwenu Tanzania."
Maneno yake yalinishtua kiasi flani maana niliwahi kusikia Mombasa kuna Wanaume mashoga wengi sana, Lakini nilijipa matumaini nitapambana kama napelekwa gereza la wababe.................
“Poa haina shida nyie nipelekeni tu" nilimjibu kwa kujiamini
“Na kesi yako nitahakikisha ninaisimia unanyongwa hadi unakufa Mbwa wewe” Daniel aliniambia kwa jazba kama simba aliyekosa chakula.
“Sijali, Amekufa rafiki yangu, dada yangu sembuse mimi”. Nilijibu
“Hahahahahaha una kiburi etiii eheee?” Daniel alizungumza kwa dharau huku akinisogezea sura yake pembeni, nikayakusanya mate mdomoni mwangu kisha nikamtemea usoni mwake na kumfanya ayafumbe macho yake kwa muda kisha nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu la kulia na kuniyumbisha kwa muda kisha nikaanguka chini.
“Ninakuambia nilazima ufe” Shoga wewe, Mpelekeni Kwa mashoga wenzake haraka sanaaaaaaa!!"... Alipiga kelele kama mbogo
. Mabaunsa hawa wa kiume wakanikamata kwa nguvu. Wakanitoa katika chumba hichi na nikaingizwa kwenye chumba kingine ambacho nikamkuta Martin yule mwenye asili ya kipemba akiwa na Askari wengin watatu, wakanifungua pingu pamoja na nyororo za miguuni, kisha wakanikabidhi nguo aina ya overall lenye rangi ya chungwa. Sasa niliamini naenda jela maana ndio kwanza jezi nimekabidhiwa,.
Taratibu nikaanza kulivaa huku nikiwatazama kwa ujasiri. Kusema kweli sifahamu ni kitu gani kimenipata hadi nakuwa jasiri kiasi cha kujibizana na Askari kwa Dharau.
Wakanikabidhi raba nikazivaa, kisha nikafungwa pingu tena pamoja na nyororo miguuni mwangu. Wakanitoa ndani ya chumba hichi huku wakiniweka chini ya ulinzi mkali,
Tukaingia kwenye lifti, taratibu ikaanza kushuka chini, tukafika chini kabisa, nikakuta basi refu la magereza, ndani kuna wanaume wengi walio valia sare kama zangu. Nikaingizwa ndani ya basi hili, Wafungwa hawa wenye rika tofauti tofauti waliomo ndani ya hili basi wakanitazama nami nikawatazama ili nifahamu sura zao na vimo vyao, kusema kweli hakuna mwenye mwili kama wangu na wote hawa wana miili mikubwa sana na vimo kuliko mimi. Wamejazia misuli huku wakiwa na sura za kikatili, ni siti mbili tu ambazo hazina mtu na zote pembeni wamekaa Wafungwa wanene na wenye sura za kutisha kiasi huku miili yao wakiwa wamejichora chora tattoo huku mmoja kichwani mwake akiwa amenyoa upara. Taratibu nikaa pembeni ya baba mmoja, japo uso wake una jeraha la kuchanwa na kitu chenye ncha kali ila nikajikaza na kukaa naye kwani hatoweza kunifanya kitu chochote kutokana na askari wapo eneo hili. Askari akanifunga mnyororo wangu na siti kisha akaondoka zake. Uzuri wa wafungwa tuliomo ndani ya hili basi tumetoka mataifa tofauti tofuati hii ni kutokana na muonekano wa sura zoa pamoja na rangi za miili yao. Wengine waarabu, wazungu, wasomali na hata wapemba pia,
ITAENDELEA
nais jamaa atamaliza yteBora kuisubiri iishe kuepuka uraibu...
nais jamaa atamaliza yte
Kinoma nomaan,, big up Sana mzeeKitu kipo hot sana