atug
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,786
- 3,522
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hyo reception ya hapo mandara nimejenga mm hyo kench kuisimamisha ilitusimbua maana kulikuwa na baridi sanaaaaHOROMBO.
![]()
Katika vituo vyote sehem niliyoipenda zaidi kukaa ni horombo. Ilituchukua masaa karibu 9/10 kufika HOROMBO. Ni sehem iliyo changamka.. kama kijiji fulani hivi..katika safari yetu Kuna vituo vya kupumzika.. Na pia kuna sehem huko huko barabarani ni stop kwa ajili ya Lunch... Kuna upepo na baridi sana yaani kuliko kukaa nje mtu unaenda chooni upepo usikupige. Vyoo ni Safi na vimejengwa vizuri.
nakumbuka nikiwa nakaribia kibao cha Horombo I was excited kwamba nimefika after a long walk, nikaanza kutembea haraka huku nashangilia na kupiga mayowe, haikuchukua hata sekunde kadhaa hali yangu ikabadilika I couldn’t walk, mapigo ya moyo hayakua sawa kutembea nikashindwa, kihere here chote kikaishia hapo.. ikabidi nipumzike chini na waanze kuniangalia hali yangu. baada ya dakika kadhaa hali yangu ilivyokua sawa ndio nikafika hapo. Yaani usicheze na mambo ya altitude..
Complication..
Ilipofika usiku nikaanza kujisikia vibaya... Yaani sijielewi elewi hali yangu sio nzuri, nikaenda kupima oxygen na vitu vingine wakanambia niko safi tu laba uoga na mawazo. Na kweli I was scared. Nikaingia kulala mapema nikashtuka kama saa 7 USIKU, MAPIGO YANGU ya moyo yanapiga kwa kasi ya ajabu, siwezi kuhema vizuri, nikiangalia pembeni naona kama kila mtu kalala, nikalaani kitendo cha kushtuka mida hiyo nikihesabu muda naona hadi kukuche its like forever. Na nikawa naogopa pia kulala usingizi what if hivi ninavyoshindwa ku breathe ndio nipitilize moja kwa moja.
Sim hazitoki... hakuna mtandao..The only thing nilifanya ni kusikiza music tu mpaka kunakucha. Nimesikiza album za Maher Zain hapoo wee.. Asubuhi tunavyohadithiana kumbe kila mtu anasema I couldn’t sleep last night..
Sent from my iPhone using JamiiForums
Nikajua leo tunafika mpaka kileleni, kumbe tunaishia njiani basi ngoja nasisi tulale.Kesho best.... Nimechoka zangu.
ASANTE
Sent from my iPhone using JamiiForums
Safari ya Mandara.
![]()
Hii ndio ilikua point yangu ya kwanza baada ya kutoka getini. Nilikua na personal porter anaitwa FREDY. Mwenyewe alinipokea bag na kijitambulisha vizuri kwangu. Ukiwa na personal guide ina maana yeye atakua na wewe bega kwa bega.. atakubebea back pack.. achana na wale guide wa group.
Tulianza kwa story akanielezea safari zake milimani.. yeye keshapanda mara 6 hadi Uhuru peak.. I was excited..mwanzo story zilikolea baadae zikakata ule uchovu.
Tunavyopanda tulikua tunakutana na makundi ya watu wanarudi na wengi walikua wanatuambia “pole pole” nadhani huu ndio msemo maarufu ukifuatiwa na “Jambo”.
Nilianza kuchoka jinsi masaa yanavyokwenda.. Nikawa kama siwezi kupumua vizuri muda mwingi Fred alikua ananisitiza kunywa maji...
Kuna muda wenzangu walikua mbele.. baada ya kupumzika nikasema hebu nikae hili kundi sitaki kubaki nyuma... Enhee bana kumbe kasi yao haiendani na mimi.. ila kutembea hata dakika 5 nyingi.. nikaona kama roho inataka kutoka mapigo ya moyo yanaenda mbio hatari roho kama yataka kuchomoka.. joto likanipanda.. Fred as usual akaniambia pumzika. Nikakaa chini vua sweta nikanywa maji.. baada ya muda ndio nikarudi hali ya kawaida.. Nilishaanza kupanick kuwa nakufa sasa. maana hapo si tulishaambiwa watu wanakufa huko sana na kila mtu unamwbia unaenda Kupanda Mlima unakuwa na doubt.. Mimi nikajua mama yangu hapa na mimi ndio bye bye
Akanishauri kuwa kila mtu ana speed yake so i should keep same speed maana tunazidi kupanda juu.. hali ya hewa ni ya mgandamizo.. Tunaingia Mandara saa 2/3 usiku. i was excited kwamba after a long walk kuna sehem tumefika tupumzike. Kitu cha kwanza ni ku register majina.. kulikua na baridi hatari mikono ilikua na ganzi hata kuandika nilishindwa waliiandikia jina nikaweka sign tu.
Tukaonyeswha dormitories nikatafuta kitanda changu cha chini..
![]()
yaani kuna bariiidi hatari nikajifunika sleeping bag nikajilaza.. nina hasira kishenzi.. ukiuliza hasira za nini sijui..
Usingizi ukanipitia baada ya muda kidogo mtu akaja kuniamsha kwa ajili ya dinner yaani nilichukia nikaona sijawahi kukutana na mtu mbaya na katili duniani kama huyo alieniamsha kula.. Na hapo tunasisitizwa kwamba ni lazima ule kama unataka kufika juu.. Kufika kileleni nataka ila kama hali ndio hii NO WAY
Nikaanza kulia ndani ya sleeping bag... lia kishenzi.. Makamasi na machozi yanatiririka tu ila nalia kimya kimya watu wasinisikie. mtu unaweza kushangaa kama ni the same person niliyekuwa nashangilia muda mchache uliopita.. Nikawa najiuliza hivi nimekuja kufanya nini huku?? Baridi lote hili tena nikale huko nje.... nikaja kuamshwa tena hapo wenzangu hawawezi kula hadi watu wote watimie.. Nimefika dinning sijataka kuongea na mtu.. wakinichekesha najilazimisha kucheka. Huo muda Akili inawaza mambo kibao.
Chakula chenyewe nakutana na vegetable soup.. macaroni.. ndio siyapendi kudadadeki.. mikate.. chai... Chakula ni kizuri ila hamu ya kula sikua nayo hata kidogo.. Duh nakula then straight in bed sisemeshani na mtu. Na mtandao ni hakuna so no whatsup. Instagram wala JF.
Hii ni asubuhi.. tunajiandaa kwenda Horombo
![]()
Huko ni njiani tu...
View attachment 981761
Sent from my iPhone using JamiiForums
View attachment 982240
Route ya Machame siyo njia ya kitoto lazima uwe na afya nzuri na mkakamavu vinginevyo pitia Marangu
View attachment 982241
Wewe ni mtu wa DAR or sisi wa kanda hii ndio kama kwenda Beach tuMY JOURNEY TO THE ROOF OF AFRICA
Kabla ya mwaka kuisha napenda ku share na nyie experience yangu ya kupanda mlima Kilimanjaro nitaambatanisha baadhi ya picha na video za safari yangu yote. Kama kuna watu wamewahi kupanda Mlima Kilimanjaro wanaweza ku share pia uzoefu wao.
Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails.. Kundi letu tulikua 21, Njia niliyotumia ni MARANGU.. Cost ilikua ni 560$ hii ili include kila kituu.. kuanzia usafiri Dar-Moshi Dar, chakula, hoteli.. vifaa.. fees za getini... personal guides... etc etc.. gharama zinapungua kutokana na huduma unayohitaji..
![]()
MAANDALIZI YA SAFARI.
Baada ya ku confirm ushiriki wangu kupanda Mlima Kilimanjaro. Jambo la kwanza nilifanya Medical check up.. nikawa 100% fit kupanda mlima na hadi kufika kileleni... Nikaanza mazoezi nakimbia uwanja nazunguka mara 7-10. Mazoezi ya kupandisha ngazi wanaojua jengo la UHURU HEIGHTS.. Nimepanda na kushuka hizo ngazi saana.. Pia tulikua tunafanya SEA CLIFF WALK haya yalikua matembezi kutoka Upanga hadi Sea cliff kwenda na kurudi kila jumamosi Kwa mwezi mara mbili. Kim beach kigamboni kutembea katika michanga Etc etc.
Pia nilijisajili na kitengo cha Flying Doctors Africa wako chini ya Amref.. wanatoa huduma ya helicopter kwa ajili ya ku rescue mlimani incase of emergency. Kusema ukweli nilikua muoga saana kwa sababu ya stories unazosikia so ilikua ni tahadhari maana ilikua ndio first time kupanda mlima.. & you never know nini kitatokea huko juu milimani. Fee ni 50$ kwa mtu mzima.
Nilisoma kila habari kuhusu kilimajaro na kupanda Mlima.. vifo vinavyotokea.. risk ukiwa mlimani..
KUPANDA MLIMA ULUGURU:Uluguru height ni kama 8600ft na hii ilikua ni moja ya majaribio kabla ya kupanda Mlima... Uluguru was the easiest tulienda Ijumaa.. Jumamosi tukapanda Mlima... Jumapili tukarudi Dar.. Mandhari ya Uluguru ni bomba sana...Kuna memories nyingi ila mojawapo ni kuoga alfajiri katika water falls...... Jambo ambalo sikupenda Uluguru ni hali ya choo pale.. Nilibanwa haja kubwa ila mzigo wangu niliubana hadi nilivyorudi town maana kushusha gogo porini nilikua siwezi. I wonder kwanini SUA hawarekebishi.
Tent tulizotumia kulala
![]()
Hii ndio camp kunaitwa Morning Site..tulikofikia.. humo kuna chata za watu wengi
![]()
The View
![]()
![]()
Nitaendelea Next post.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kesho best.... Nimechoka zangu.
ASANTE
Sent from my iPhone using JamiiForums
Pole mkuuhii story imenitoa stress za forex za leo nasoma huku niko kwenye dip red
Sent using Jamii Forums mobile app
Lile ziwa nilishafika mkuu lipo chini sana ni kama unashukia kwenye kamgodi flan hivi(sehemu ambayo natamani niende ni Ziwa Chala.....
Hilo jiwe la kubusu ndo lipoje im trying to Imagine hata sielewi
Hongera Heaven, hii njia kweli nzuri hadi kuna vitanda[emoji2297][emoji2297][emoji2297].......nilipanda mlima siku sita, kitanda nilikuja kukiona siku ya saba tulivyoshuka sijui ni mweka pale sijui mwika...nimesahau jina, ajabu tulipanda siku 6 lkn kushuka ni siku moja tu....Naenda kuleeee kileleni [emoji4]
![]()
Huyu mtoto ana miaka 10 alitokea SA.. wakiwa na Trek4Mandela.. Sijui alifika summit
![]()
Hii ndio sehem ya mwisho maji kupatikana
![]()
Angalia hao porters
![]()
![]()
Huyu baba kapanda Mlima mara 18 na siku zote alifika kileleni
![]()
Hiko kitanda cha pembeni juu kabisa ndio nililala hapo.. Chini kulikua na mdada mzungu anatapika kishenzi..
![]()
Mandhari ya Horombo
![]()
Sehem ya kupumzika
![]()
Kulikua na baridi nje.. Hiko choo nilienda kuingia ndani.. Ushawahi kuona unakaa chooni na unaona ndio sehem nzuri kabisaa kuliko nje
![]()
Sent from my iPhone using JamiiForums
Huwezi ndugu coz kulala tu kwenye huwezi kujinyoosha, unajikunja ili upate joto, halafu nguo za kulalia zinabana fulani hivi mfano zetu zilikuwa zinaitwa thermos, ukivaa hizo nguo then shuka ni kama mfuko hivi, unaingia zako kwenye hilo shuka....unajikunja kuutafuta usingiziMkuu na lile baridi kweli unaweza usiwe na habari nae, nadhani utakuwa umeamua tu kutufurahisha humu
Sent using Jamii Forums mobile app
Jiwe la kubusu ni hivi, ili kutoka pale barango kwenda karanga lazima mpite mlimani, na mkiwa pale barango mlima unauona uleeeee, mkifika pale mlimani njia ni nyembamba sana, sasa kuna sehemu kuna jiwe kubwa ili kupita hapo lazima ulikumbatie hilo jiwe na unapita upande upande lakini mbaya zaidi chini kuna korongo so ukikosea step kidogo tu unaweza kujikuta uko korongoni, so mnapita mmoja mmoja na kwa uangalifu mkubwa. Nakumbuka kundi letu tulikuwa zaidi ya watu 30 tulitumia almost 2hrs kuvuka hapo....na slogan ya mlimani ni Pole Pole....no hurryHilo jiwe la kubusu ndo lipoje im trying to Imagine hata sielewi
Ruwaa[emoji134]kumbe ndo hivyo basi hiyo njia sio poaJiwe la kubusu ni hivi, ili kutoka pale barango kwenda karanga lazima mpite mlimani, na mkiwa pale barango mlima unauona uleeeee, mkifika pale mlimani njia ni nyembamba sana, sasa kuna sehemu kuna jiwe kubwa ili kupita hapo lazima ulikumbatie hilo jiwe na unapita upande upande lakini mbaya zaidi chini kuna korongo so ukikosea step kidogo tu unaweza kujikuta uko korongoni, so mnapita mmoja mmoja na kwa uangalifu mkubwa. Nakumbuka kundi letu tulikuwa zaidi ya watu 30 tulitumia almost 2hrs kuvuka hapo....na slogan ya mlimani ni Pole Pole....no hurry
Sent using Jamii Forums mobile app