SAFARI YA MOSHI
Tunaingia Moshi usiku saa 2... Tunapokelewa na wenyeji.. wakarim kishenzi.. wale ma guide sijui walidhani tumetoka nchi gani hatuju kiswahili kumbe ni wabongo tu.. Nimesahau jina la hotel
kiwatengu anaweza kunikumbusha. Pale hotelini kulikua na wazungu kibao.. wengi wakiwa wametoka mlimani wakipongezana dinner.. wines na kupeana vyeti... Nikawa nawatizama kwamba can I do this?? unaona watu wanachechemea miguu, sura hazitamaniki wamebabuka, hapo ni bonge la mtu wengi wako hoi.ile usiku tukafanyiwa training na rescue team ya ile kampuni.. tukapewa maelekezo yote muhim.. Asubuhi Safari ya Mlimani.
SAFARI YA MARANGU.
Alfajiri tunaamka.. Mimi pamoja na kununua vifaa vya mlimani lakini still nilikua nahitaji kodi baadhi ya vifaa kama Hiking boot, balaclava, walking stick.. sleeping bag.. na hizi ni zile zenye joooto maana huko juu tushaambiwa kuna baridi la kufa mtu.
Saa 3 asubuhi tunaanza safari ya Marangu. Si umbali mrefu. usajili getini tunamaliza saa 9. miezi ni High season kuna watu kutoka nchi mbali mbali wanakua wamekuja kupanda mlima.!kulikua na nyomi la kufa mtu. Jambo nililopenda Marangu getini kuna ramani ya njia unayotimia kufika kileleni na pia kuna picha za record za watu mbali mbali walifanikiwa kupanda mlima kwa muda mchache, kuna mmoja alipanda kwa 5hrs.. huyu najiuliza hadi leo alifanyaje fanyaje .. Masaa 5 hadi kileleni its not a joke
Marangu Getini hapo.
Fuatilia next post.. huko ndio kwenye mziki
Sent from my iPhone using JamiiForums