Mgugu
JF-Expert Member
- Jul 1, 2015
- 2,165
- 4,403
Kwa hio Kasie mpaka umri huo ulionao haujawahi kufika kileleni?Hongera mrembo, nina binamu yangu ameshapanda Kilimanjaro mara 2 kama si 3 ila anasema haina uzoefu unaweza kupanda mara nyingi na bado ukapata emergency ukadanji au ikabidi ushuke mlima na safari iishie hapo.
Huwa nawataniaga wafanyakazi wenzangu jamani tuchukue likizo ya pamoja twendeni tukapande Mlima Kilimanjaro... wanaishia kuniambia kama umechoka kula pizza tuache sie tupakatie pakacha zetu. Basi huwa nacheekaa.
Binafsi napenda sana kutembea na nilishapanda milima ya kawaida ya vijijini ikiwa ni njia ya kuelekea ninakofikia. Najiona namudu ila sijajipanga kupanda mlima wowote japo natamani.
Naishiaga kwenda Mbuga za wanyama nalala hoteli basi.
Hongera sana mamii.
Sent from my GT-P5200 using Tapatalk