MY JOURNEY TO THE ROOF OF AFRICA
Kabla ya mwaka kuisha napenda ku share na nyie experience yangu ya kupanda mlima Kilimanjaro nitaambatanisha baadhi ya picha na video za safari yangu yote. Kama kuna watu wamewahi kupanda Mlima Kilimanjaro wanaweza ku share pia uzoefu wao.
Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails.. Kundi letu tulikua 21, Njia niliyotumia ni MARANGU.. Cost ilikua ni 560$ hii ili include kila kituu.. kuanzia usafiri Dar-Moshi Dar, chakula, hoteli.. vifaa.. fees za getini... personal guides... etc etc.. gharama zinapungua kutokana na huduma unayohitaji..
MAANDALIZI YA SAFARI.
Baada ya ku confirm ushiriki wangu kupanda Mlima Kilimanjaro. Jambo la kwanza nilifanya Medical check up.. nikawa 100% fit kupanda mlima na hadi kufika kileleni... Nikaanza mazoezi nakimbia uwanja nazunguka mara 7-10. Mazoezi ya kupandisha ngazi wanaojua jengo la UHURU HEIGHTS.. Nimepanda na kushuka hizo ngazi saana.. Pia tulikua tunafanya SEA CLIFF WALK haya yalikua matembezi kutoka Upanga hadi Sea cliff kwenda na kurudi kila jumamosi Kwa mwezi mara mbili. Kim beach kigamboni kutembea katika michanga Etc etc.
Pia nilijisajili na kitengo cha Flying Doctors Africa wako chini ya Amref.. wanatoa huduma ya helicopter kwa ajili ya ku rescue mlimani incase of emergency. Kusema ukweli nilikua muoga saana kwa sababu ya stories unazosikia so ilikua ni tahadhari maana ilikua ndio first time kupanda mlima.. & you never know nini kitatokea huko juu milimani. Fee ni 50$ kwa mtu mzima.
Nilisoma kila habari kuhusu kilimajaro na kupanda Mlima.. vifo vinavyotokea.. risk ukiwa mlimani..
KUPANDA MLIMA ULUGURU:Uluguru height ni kama 8600ft na hii ilikua ni moja ya majaribio kabla ya kupanda Mlima... Uluguru was the easiest tulienda Ijumaa.. Jumamosi tukapanda Mlima... Jumapili tukarudi Dar.. Mandhari ya Uluguru ni bomba sana...Kuna memories nyingi ila mojawapo ni kuoga alfajiri katika water falls...... Jambo ambalo sikupenda Uluguru ni hali ya choo pale.. Nilibanwa haja kubwa ila mzigo wangu niliubana hadi nilivyorudi town maana kushusha gogo porini nilikua siwezi. I wonder kwanini SUA hawarekebishi.
Tent tulizotumia kulala
Hii ndio camp kunaitwa Morning Site..tulikofikia.. humo kuna chata za watu wengi
The View
Nitaendelea Next post.
Sent from my iPhone using JamiiForums