Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Napenda kutembelea vivutio mbalimbali Ila kupanda mlima big no hongera Sana kwa ujasiri huo jamani nimekutamani. [emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7]
Hicho chakula chenye jina lako kitamu Sana,mara ya mwisho kukila Zanzibar hotel moja ya kitalii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kamwili kako kalivyo simple wala hupati shida sana kufika kileleni, ila ungekua na lichura likubwa kama miss natafuta sidhani kama ungeweza kufika kwenye kilele cha kibo kwa urahisi.

Maendeleo hayana chama
Ule mlima hauna mwili wala nini cha msingi uwe umefanya mazoezi ya kutosha na uombe tu hali ya hewa isikukatate....hali ya hewa ikikugomea unarudishwa siku ya kwanza tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nilipanda 2013 nikapata na cheti kabisa njia ya marangu nlikua nafanya field kinapa..ule mlima kinachowaua watu ni change of altitude hautaki harakaharaka mwili unaweza shindwa stahimili..ila ni mlima hata mtu wa miaka 12 anapanda..nmepanga nipande tena mwezi wa nne Mungu saidia
Hongera mrembo, nina binamu yangu ameshapanda Kilimanjaro mara 2 kama si 3 ila anasema haina uzoefu unaweza kupanda mara nyingi na bado ukapata emergency ukadanji au ikabidi ushuke mlima na safari iishie hapo.

Huwa nawataniaga wafanyakazi wenzangu jamani tuchukue likizo ya pamoja twendeni tukapande Mlima Kilimanjaro... wanaishia kuniambia kama umechoka kula pizza tuache sie tupakatie pakacha zetu. Basi huwa nacheekaa.


Binafsi napenda sana kutembea na nilishapanda milima ya kawaida ya vijijini ikiwa ni njia ya kuelekea ninakofikia. Najiona namudu ila sijajipanga kupanda mlima wowote japo natamani.

Naishiaga kwenda Mbuga za wanyama nalala hoteli basi.

Hongera sana mamii.

READERS ARE LEADERS
 
Back
Top Bottom