Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
Mimi nitakuwa naupanda kwa mara ya tatu sasaSaint Ivuga twende bas huko kupanda mlima😋
Wewe njoo nikupe mlima mwingine nitakufikisha hadi kileleni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nitakuwa naupanda kwa mara ya tatu sasaSaint Ivuga twende bas huko kupanda mlima😋
Hongera sana ila kufika kileleni mara kwa mara kunaboresha afya ya mwili na akili, kwa hio jitahidi sana usiwe mvivu ukipanda uwe unafika kileleni usiwe unaishia kati.yeah milima kama yte....
MY JOURNEY TO THE ROOF OF AFRICA
Kabla ya mwaka kuisha napenda ku share na nyie experience yangu ya kupanda mlima Kilimanjaro nitaambatanisha baadhi ya picha na video za safari yangu yote. Kama kuna watu wamewahi kupanda Mlima Kilimanjaro wanaweza ku share pia uzoefu wao.
Kampuni niliyotumia inaitwa Origin Trails.. Kundi letu tulikua 21, Njia niliyotumia ni MARANGU.. Cost ilikua ni 560$ hii ili include kila kituu.. kuanzia usafiri Dar-Moshi Dar, chakula, hoteli.. vifaa.. fees za getini... personal guides... etc etc.. gharama zinapungua kutokana na huduma unayohitaji..
![]()
MAANDALIZI YA SAFARI.
Baada ya ku confirm ushiriki wangu kupanda Mlima Kilimanjaro. Jambo la kwanza nilifanya Medical check up.. nikawa 100% fit kupanda mlima na hadi kufika kileleni... Nikaanza mazoezi nakimbia uwanja nazunguka mara 7-10. Mazoezi ya kupandisha ngazi wanaojua jengo la UHURU HEIGHTS.. Nimepanda na kushuka hizo ngazi saana.. Pia tulikua tunafanya SEA CLIFF WALK haya yalikua matembezi kutoka Upanga hadi Sea cliff kwenda na kurudi kila jumamosi Kwa mwezi mara mbili. Kim beach kigamboni kutembea katika michanga Etc etc.
Pia nilijisajili na kitengo cha Flying Doctors Africa wako chini ya Amref.. wanatoa huduma ya helicopter kwa ajili ya ku rescue mlimani incase of emergency. Kusema ukweli nilikua muoga saana kwa sababu ya stories unazosikia so ilikua ni tahadhari maana ilikua ndio first time kupanda mlima.. & you never know nini kitatokea huko juu milimani. Fee ni 50$ kwa mtu mzima.
Nilisoma kila habari kuhusu kilimajaro na kupanda Mlima.. vifo vinavyotokea.. risk ukiwa mlimani..
KUPANDA MLIMA ULUGURU:Uluguru height ni kama 8600ft na hii ilikua ni moja ya majaribio kabla ya kupanda Mlima... Uluguru was the easiest tulienda Ijumaa.. Jumamosi tukapanda Mlima... Jumapili tukarudi Dar.. Mandhari ya Uluguru ni bomba sana...Kuna memories nyingi ila mojawapo ni kuoga alfajiri katika water falls...... Jambo ambalo sikupenda Uluguru ni hali ya choo pale.. Nilibanwa haja kubwa ila mzigo wangu niliubana hadi nilivyorudi town maana kushusha gogo porini nilikua siwezi. I wonder kwanini SUA hawarekebishi.
Tent tulizotumia kulala
![]()
Hii ndio camp kunaitwa Morning Site..tulikofikia.. humo kuna chata za watu wengi
![]()
The View
![]()
![]()
Nitaendelea Next post.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hongera sana ila kufika kileleni mara kwa mara kunaboresha afya ya mwili na akili, kwa hio jitahidi sana usiwe mvivu ukipanda uwe unafika kileleni usiwe unaishia kati.
Maendeleo hayana chama
😣😣😣😣Mimi nitakuwa nupanda kwa mara ya tatu sasa
Wewe njoo nikupe mlima mwingine nitakufikisha hadi kileleni
Huyu alizisoma namba mpaka,alizania ni lele mama.ukizingatia hakuna kuoga mpaka urudi.
Mlipita njiani laini sana....marangu! Hongera kwa kukuza jiografia yako.......Wewe umewahi kupanda???
Hao Wanaweza kuwa inspired kupanda. Mimi aliyenihamasisha sana kupanda ni member wa huku anaitwa kiwatengu so you never know
Sent from my iPhone using JamiiForums
Na kamwili kako kalivyo simple wala hupati shida sana kufika kileleni, ila ungekua na lichura likubwa kama miss natafuta sidhani kama ungeweza kufika kwenye kilele cha kibo kwa urahisi.[emoji39][emoji39][emoji39]
Na kamwili kako kalivyo simple wala hupati shida sana kufika kileleni, ila ungekua na lichura likubwa kama miss natafuta sidhani kama ungeweza kufika kwenye kilele cha kibo kwa urahisi.
Maendeleo hayana chama
Hahahaha,umenichekesha unaposema nilipoona kibao cha HOROMBO ukadhani umefika .HOROMBO.
![]()
Katika vituo vyote sehem niliyoipenda zaidi kukaa ni horombo. Ilituchukua masaa karibu 9/10 kufika HOROMBO. Ni sehem iliyo changamka.. kama kijiji fulani hivi..katika safari yetu Kuna vituo vya kupumzika.. Na pia kuna sehem huko huko barabarani ni stop kwa ajili ya Lunch... Kuna upepo na baridi sana yaani kuliko kukaa nje mtu unaenda chooni upepo usikupige. Vyoo ni Safi na vimejengwa vizuri.
nakumbuka nikiwa nakaribia kibao cha Horombo I was excited kwamba nimefika after a long walk, nikaanza kutembea haraka huku nashangilia na kupiga mayowe, haikuchukua hata sekunde kadhaa hali yangu ikabadilika I couldn’t walk, mapigo ya moyo hayakua sawa kutembea nikashindwa, kihere here chote kikaishia hapo.. ikabidi nipumzike chini na waanze kuniangalia hali yangu. baada ya dakika kadhaa hali yangu ilivyokua sawa ndio nikafika hapo. Yaani usicheze na mambo ya altitude..
Complication..
Ilipofika usiku nikaanza kujisikia vibaya... Yaani sijielewi elewi hali yangu sio nzuri, nikaenda kupima oxygen na vitu vingine wakanambia niko safi tu laba uoga na mawazo. Na kweli I was scared. Nikaingia kulala mapema nikashtuka kama saa 7 USIKU, MAPIGO YANGU ya moyo yanapiga kwa kasi ya ajabu, siwezi kuhema vizuri, nikiangalia pembeni naona kama kila mtu kalala, nikalaani kitendo cha kushtuka mida hiyo nikihesabu muda naona hadi kukuche its like forever. Na nikawa naogopa pia kulala usingizi what if hivi ninavyoshindwa ku breathe ndio nipitilize moja kwa moja.
Sim hazitoki... hakuna mtandao..The only thing nilifanya ni kusikiza music tu mpaka kunakucha. Nimesikiza album za Maher Zain hapoo wee.. Asubuhi tunavyohadithiana kumbe kila mtu anasema I couldn’t sleep last night..
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kipengele cha kukumbatia jiwe kipo njia ya machame.jiwe la kubusu.
Huko ndo theory ya survival for fittest inaishi.Hongera mrembo, nina binamu yangu ameshapanda Kilimanjaro mara 2 kama si 3 ila anasema haina uzoefu unaweza kupanda mara nyingi na bado ukapata emergency ukadanji au ikabidi ushuke mlima na safari iishie hapo.
Huwa nawataniaga wafanyakazi wenzangu jamani tuchukue likizo ya pamoja twendeni tukapande Mlima Kilimanjaro... wanaishia kuniambia kama umechoka kula pizza tuache sie tupakatie pakacha zetu. Basi huwa nacheekaa.
Binafsi napenda sana kutembea na nilishapanda milima ya kawaida ya vijijini ikiwa ni njia ya kuelekea ninakofikia. Najiona namudu ila sijajipanga kupanda mlima wowote japo natamani.
Naishiaga kwenda Mbuga za wanyama nalala hoteli basi.
Hongera sana mamii.
Ulifikia kituo kipi?Sio kwa uvivu huo.. It is a great adventure Mimi nime plan kurudi 2020 nikiwa hai.. kuna jambo dogo hatukufanikisha.. So Nitarudi tena
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mlimani hakunag cha mwili,kizuri nature ikuselect.Na kamwili kako kalivyo simple wala hupati shida sana kufika kileleni, ila ungekua na lichura likubwa kama miss natafuta sidhani kama ungeweza kufika kwenye kilele cha kibo kwa urahisi.
Maendeleo hayana chama
Huyo Laini ,we kiboko.vipi ulitoboaMlipita njiani laini sana....marangu! Hongera kwa kukuza jiografia yako.......
Mie nilishapanda kwa kupitia njia machame
Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitoboa mkuu.....Huyo Laini ,we kiboko.vipi ulitoboa
Machame njia yangu.