Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Ukitaka ufaidi, fuata taratibu zao tu, hata kama unajisikia bado una nguvu, usiongeze mwendo, nenda taraibu kwa kasi ile ile.
Tulipofika Lava Tower ndio tumbo lilianza kuvuruga na kukumbuka kwamba chakula kikiingia kinatakiwa kitoke kwenye mwili.

Vile vile siku ya mwisho inabidi kujitahidi kupata chakula cha kutosha, hata kama haujisikii kula na mara zote hamu ya kula inakosekana kabisa. Ile ni siku ngumu kuliko zote. Mnaanza safari saa tano usiku, mtafika kileleni kwenye saa mbili asubuhi (kutokana na ukubwa wa kundi lenu). Mkifika huko mnaanza kushuka hadi pale mlipolala, mnakula na kuanza safari ya kuja kulala kituo cha chini. Unaweza kuona siku nzima ni harakati tupu.

Lakini pamoja na shida zote, asikudanganye mtu, kileleni kuzuri sana. Ukifika unasahau shida na taabu zote. Nilichukua JIWE kule juu kama kumbu kumbu, lakini lile JIWE liko tofauti na Jiwe la Dar es Salaam.
Dar es salaam kubwa au umemaanisha jiwe la magogoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakufatilia ana kwa ana. Nimepanda sana mlima since nimemaliza six. Kiingereza kilikua kinatoka kwenye meno yangu. Nikajichanganya na maguide, mmoja rasi akanichukua. Nilikua napiga sana pesa. Wazungu wakawa wanachukua namba zangu aisee, hadi leo sijawahi kwenda nje ya inchi ila itakua haikupangwa na Mungu kwa mimi kwenda nje ya nchi manake kila kitu kilikua nje nje, nikiwa kule mlimani nikapata taarifa nimepata chuo mlimani. Nikatoroka wazungu nikarudi chini(duniani) tangu siku hiyo sijawaza tena wazungu na niliposoma nawachukia wazungu hadi leo. Namshukuru Mungu maisha yangu safi na nawaona wazungu ni sawa tu na mimi kila kitu.
Ila mlima una maajabu sana. Nimepanda mara 11 nimefika kileleni mara nne ila sikuwahi hata siku moja kuacha kushangaaa kule juu, kila siku ni siku ya kushangaa achilia mbali msitu na yale mawe kuna barafu pale juuu zimejipanga kama maua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mbongo kupanda mlima ni bei gani kulipia na gharama zingine ni zipi mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka 2003 nilipanda Mlima Kilimanjaro kwa kupitia njia ya Rongai,kwa kweli shughuli haikuwa ya kitoto.Tulifika kituo cha School Heart majira ya 1900 hrs tukiwa so exhausted na baada ya muda wa lisaa limoja tulipewa mushroom soup,hata hamu ya kunywa haikuwepo.Tulipumzika kwenye banda lililokuwa na vitanda vya double decker,baadhi walikuwa walikuwa wakilalamika fluu na maumivu ya kichwa,niliwaambia kila mtu alisoma instructions zilizokuwa zikielekeza endapo kama hali itabadilika ghafla ni vyema usiendelee wahi trolley kwa ajili ya kushuka ulikotoka upatiwe first aid,lakini kwa vile lilikuwa kundi la makamanda haikuwa issue sana,majira ya 0000hrs tuliamshwa na wakuu kila mtu akawa tayari kwa ngwe ya kwenda peak,hali kwa usiku ule ilikuwa baridi kali theluji ikiwa imetapakaa eneo lote wale mountain guides walishauri ni vyema kama mtu ana miwani tinted avae kuzuia macho yasidhurike.Safari kwenda kileleni ilianza kwa kweli zile features za kule juu zilikuwa zinatisha kiasi kwamba usipokuwa makini unaweza kuteleza na kupotea kwenye korongo.Wengi waliishia Gilmans point na baadhi tulifanikiwa kufika Uhuru peak lakini kwa mbinde!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni miongoni mwa watu wanaojifanya niendelee kuandika.. [emoji120][emoji120]


Sent from my iPhone using JamiiForums
Asante Sana ,kwa heshima hiyo hiyo nakuomba Sana uunganishe story yoote uweke mwanzo wa post maana nawasomea watoto wangu Sasa wanapata taabu kunielewa pls ma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kimoja ambacho nadhani watu wote ambao washapanda mlima kilimanjaro na kufika uhuru height lazima tukubaliane.Huu mlima unakupa sense of accomplishment kiasi kwamba unahisi hamna kitu kinachoweza kua kigumu kwako maishani.katika vitu ambavyo proud ni hiki cheti nlichopata aisee..ndo maana mwezi wa 5 nataka panda tena
 
Mrembo mimi naenda kupanda huo mlima soon asante kwa kunipa taarifa kabisa ila hujamalizia,,hivi huruhusiwi kupanda japo na wiski kwa ajili ya kukata baridi kimtindo.. au uwe na kipande cha Bang!

Sent using Jamii Forums mobile app

Nitahadithia kisa cha Bangi tulipokua tunaenda Uhuru peak. hapo wewe ndio utaona kama uwe na kipande cha bangi ama vipi...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna kitu kimoja ambacho nadhani watu wote ambao washapanda mlima kilimanjaro na kufika uhuru height lazima tukubaliane.Huu mlima unakupa sense of accomplishment kiasi kwamba unahisi hamna kitu kinachoweza kua kigumu kwako maishani.katika vitu ambavyo proud ni hiki cheti nlichopata aisee..ndo maana mwezi wa 5 nataka panda tena

Screenshot_2018-12-31-16-52-51-1.jpeg
 
Back
Top Bottom