SAFARI YA ZEBRA ROCKS - ACCLIMATIZATION DAY
Hapa tunakaa one day kwa ajili ya Acclimatization. Sijui kiswahili wanasemaje. Ukipita njia ya Marangu lazima uwe na siku moja ya kukaa hapo ili kuzoea hali ya hewa ya mlimani.. hii pia wanasema inaongeza chance ya kufika summit
Asubuhi nikawa fresh sio kama yule mtu nilikua naumwa usiku. Tangu tuanze safari hii ndio siku naingia kuoga.. Kuna baridi saana yaani maji yanatoka katika bomba ila yanaganda na kuwa barafu.. ila niliona bora kuoga. Kama huogi unajisafisha na wet wipes ama wet towels na kubadili nguo tu.
NAKUMBUKA ilikua birthday wa mmoja wa crew yetu wale ma guide walifanya suprise ya cake, wakaimba nyimbo zao fresh saana, mimi mwenyewe nikawa mmoja wa waimbaji baada ya breakfast mood ikawa zero kabisaa, nikaenda kuongea na guide mkuu akanambia nisiwe na wasi wasi I will be okay. machozi yakaanza kunilenga lenga Mim nikaona kama hanitendei haki ataniambiaje niko sawa wakati mimi namwambia naumwa.
DIAMOX:Hizi ni dawa tulishauriwa kununua zinasaidia kama mtu ukipata altitude sickness na mimi kwa vile nilivyokua najisikia nikazinywa kwa mara ya kwanza.
I was so emotional and sensitive..nikapanda juu tunakolaa nikaanza kulia, ila nalia sitak mtu ajue kama nalia.. Ilivyoanza safari ya Zebra Rock nikawa wa mwisho kabisa kutoka hapo niko na FRED.. Mtu akiniongelesha ndio nahisi nipaze sauti nilieee .. Nilitembea kidogo then nikakaa katika jiwe nikaanza kulia.. Fred na porter mwingine wamesimama pembeni yangu kimya wananiacha tu nilie.. Nikaliaaa weee hapo nikawa nalia kwa sauti... hiyo point pia kuna network nikaomba simu nipige.. Nikawaza kumpigia Baby huo muda hatukua vizuri I was like what if asipokee au apokee asiniambie maneno ya kunifariji ninayotaka. Sikumpigia. I called
kiwatengu maana yeye ndio alikua kama guide wangu mkubwa katika safari hii. Alipopokea tu sim aka notice kuwa nalia.. Akaanza kunishauriii wee akanipa moyoo... Ikanisaidia kiasi chake.
Tulienda Zebra rocks na kurudi Horombo. Ni kama 4500m kufika. Kufika kule nikawa poa kabisa kama sio yule niliekua nalia huko chini.. nikajumuika na watu na pia nikapanga mawe kule. Ukitembea Zebra Rocks pembezoni watu wamepanga Mawe na hawashauri kupangua hayo mawe if you want unaweza kupanga ya kwako.
One thing nili notice watu wengi tulikua tunapata emotional break down bila sababu ya msingi.. sio mimi tu nilililia kuwa wengine pia.. na kila mtu alikua na namna alivyo i handle.
Sent from my iPhone using JamiiForums