binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 11,201
- 28,642
Uooopps nimejikuta na mixed feelings, nimefurahi sana na nimeogopa mno hasa kwenye stori ya kifo hehe. Mi Tz nimeizurura hasa kwenye vivutio vingi vingi hata kwa majirani zetu, kitu sijawahi fikiria ni kupanda mlima wowote ule. Halafu kwa stori yako nimegundua i know nothing kuhusu milima kabisa, thanks Hoe umeniongezea kitu.
Swali ni je nikiamua kupanda nitaweza? Maana mimi katika maisha yakawaida situmii AC wala feni, naishi kwa kuacha windos wazi 24/7 hasa sehemu ambazo ni salama kwasababu nikitumia feni au AC hasa ikizidi nahisi kuishiwa pumzi na kichwa kuuma. Pia katika checkup mnacheck vitu haswa katika afya zenu? Big up Hoe.
Unafanyiwa checkup ya mammbo mengi sana kuona kama utahimili hali ya hewa inayobadilika badilika kadri mnavyosogea juu.
Cha kushangaza, watoto wadogo wa umri kati ya 12-14 wanapanda bila kupata dhoruba kama ilivyo kwa watu wazima,...
Dhambi nazo zinatuongezea mizigo hahahahahahhaha
Hapo kwenye dhambi hapooo! Lol
Nakupongeza tena Heaven On Earth, kupitia uzi huu:
Nimefanya mazoezi ya maandalizi na wewe,
Nimepanda na wewe,
Nimeona jamaa aliyefariki akishushwa sambamba na mkewe katika majonzi,
Nimechoka na wewe,
Nimelia na wewe,
Nimekata tamaa na wewe lakini nikajifariji na wewe na nikasonga mbele na wewe,
Nikawaona wavuta bangi wakitupita kwa kasi na badae mmoja wao akathibitisha kutangulia si kufika, akarudishwa duniani,
Kila ulipochoka, akili yangu ilikupa moyo, "twende HOE bila wewe siwezifika kileleni" ulikubali kwa machozi ya uchovu,
Nilisonga na wewe,
Simu yako iliishia chaji, nilihuzunika kwa kuwa hata kama tukisonga pamoja sitaona tena taswira nzuri ya safari yetu,
Nikawasikia ma-guide wakishauriana juu ya kuendelea ama kutoendelea na safari, nikaiona hatari ya kifo mbele yetu, nikasikitika.
Ukungu ulipozidi kule juu kiasi cha kutomuona aliyeko mbele yako, nilipatwa na hofu labda utapotea na kuporomokea upande wa Kenya,
Lakini nilikuwa na wewe,
Picha ya mwisho ambayo barafu imeziba maandishi ya kibao cha Uhuru Peak, ilinitia simanzi kubwa kwa hali ya hewa, nikajaribu kujifananisha na wewe kwa kujidumbukiza kwenye freezer ya butcher, lakini ukasema barafu niiwazayo mimi ni "cha mtoto"...
Hata hivyo, kwa jinsi ulivyotiririka kwa ustadi mkubwa, sikutamani muishie hapo na safari ya kurudi duniani ianze...
Nilitamani safari iendelee, mzuka wa simulizi yako uliniaminisha kuwa baada ya Uhuru Peak, Heaven on Earth would be taking me to the next peak... And probably it could be real Heaven like her name... Can't wait for the next episode.
Pongezi kwa guide wako Fredy kwa kukufikisha kileleni, iwe funzo kwa wanawake wengine wote kuwa, mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni haijawai kuwa kazi rahisi, yaitaji uvumilivu na kushikamana.
Hongera sana HOE.
Ngoja nielekee You tube kujazilizia elimu hii tamu.
Natamani kupanda sema mafua na joints za miguu.
Kama baridi la kwetu Magamba Lushoto linanilaza kitandani wiki na mafua juu, je nitaweza kwea Mlima Kilimanjaro?
kiwatengu naweza beba coldril kwa ajili ya kukata ukali wa mafua au siruhusiwi kunywa dawa nikiwa katikati ya safari?
Hilo nalo linawezekana kulingana na ratiba ya mtu!Hivi tokea kwenye hii thread hatuwezi kujiorganize, wale wenye nia thabiti!? Nawaza tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Will try!!Don't Give up....
[emoji23][emoji23][emoji23]madame mie naon wanaOpanda wengi ni maportable..hv wanene wanaweza kweli?yaan bado sijashawishika ..maana nikama safari ya jehanum jaman
Coldril sio dawa nzuri kwa mazingira ya kule ina mchanganyiko wa dawa ambao unaweza ukakuletea usingizi ukawa kama umelewa itakuwa ni hatari kwako na zaidi unaweza ukashindwa kupumua vizuri.Natamani kupanda sema mafua na joints za miguu.
Kama baridi la kwetu Magamba Lushoto linanilaza kitandani wiki na mafua juu, je nitaweza kwea Mlima Kilimanjaro?
kiwatengu naweza beba coldril kwa ajili ya kukata ukali wa mafua au siruhusiwi kunywa dawa nikiwa katikati ya safari?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hivi hakuna jinsi ya kupanda kwa kutumia Helicopter?
Au ni lazima kupitia the hardway!