Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Uooopps nimejikuta na mixed feelings, nimefurahi sana na nimeogopa mno hasa kwenye stori ya kifo hehe. Mi Tz nimeizurura hasa kwenye vivutio vingi vingi hata kwa majirani zetu, kitu sijawahi fikiria ni kupanda mlima wowote ule. Halafu kwa stori yako nimegundua i know nothing kuhusu milima kabisa, thanks Hoe umeniongezea kitu.

Swali ni je nikiamua kupanda nitaweza? Maana mimi katika maisha yakawaida situmii AC wala feni, naishi kwa kuacha windos wazi 24/7 hasa sehemu ambazo ni salama kwasababu nikitumia feni au AC hasa ikizidi nahisi kuishiwa pumzi na kichwa kuuma. Pia katika checkup mnacheck vitu haswa katika afya zenu? Big up Hoe.
 
Kutokea Stella kwenda Uhuru Peak ni kipindi kwa mara ya kwanza nilipata experience ya Mama Mjamzito anakuwa anajisikiaje hadi muda wote ana kichef chef, nikitembea hatua tano tu, nakaa chini, porter amebeba kila kitu changu, lakini sijiwezi, nilijikongoja hadi kufika kileleni. Ila ile mijabali ya barafu, uwanda wa mlima na theluji zinakupa raha ambayo Heaven on Earth anasema hauwezi kuielezea kwa maneno ukaeleweka.

Nimesikitika sana kuona hicho kiwango cha barafu na dhoruba mlizopitia, mwezi wa saba kidogo hali inakua nzuri, hakuna mvua na barafu sio nyingi sana.

Baada ya kurudi, ilinichukua kama miezi miwili kichwa kukaa sawa, usiku nikilala nilikua napata maruwe ruwe kama bado nipo juu ya mlima. Nashtuka naanza kujiuliza kama nipo kwenye twent au kitandani nyumbani?
 
Uooopps nimejikuta na mixed feelings, nimefurahi sana na nimeogopa mno hasa kwenye stori ya kifo hehe. Mi Tz nimeizurura hasa kwenye vivutio vingi vingi hata kwa majirani zetu, kitu sijawahi fikiria ni kupanda mlima wowote ule. Halafu kwa stori yako nimegundua i know nothing kuhusu milima kabisa, thanks Hoe umeniongezea kitu.

Swali ni je nikiamua kupanda nitaweza? Maana mimi katika maisha yakawaida situmii AC wala feni, naishi kwa kuacha windos wazi 24/7 hasa sehemu ambazo ni salama kwasababu nikitumia feni au AC hasa ikizidi nahisi kuishiwa pumzi na kichwa kuuma. Pia katika checkup mnacheck vitu haswa katika afya zenu? Big up Hoe.

Unafanyiwa checkup ya mambo mengi sana kuona kama utahimili hali ya hewa inayobadilika badilika kadri mnavyosogea juu.
Cha kushangaza, watoto wadogo wa umri kati ya 12-14 wanapanda bila kupata dhoruba kama ilivyo kwa watu wazima,...

Dhambi nazo zinatuongezea mizigo hahahahahahhaha
 
Natamani kupanda sema mafua na joints za miguu.
Kama baridi la kwetu Magamba Lushoto linanilaza kitandani wiki na mafua juu, je nitaweza kwea Mlima Kilimanjaro?
kiwatengu naweza beba coldril kwa ajili ya kukata ukali wa mafua au siruhusiwi kunywa dawa nikiwa katikati ya safari?
 
Unafanyiwa checkup ya mammbo mengi sana kuona kama utahimili hali ya hewa inayobadilika badilika kadri mnavyosogea juu.
Cha kushangaza, watoto wadogo wa umri kati ya 12-14 wanapanda bila kupata dhoruba kama ilivyo kwa watu wazima,...

Dhambi nazo zinatuongezea mizigo hahahahahahhaha

Hapo kwenye dhambi hapooo! Lol
 
Heaven on Earth ,
..HONGERA sana.

..umezungumzia BARIDI kali kadiri mlivyokuwa mkipanda mlima.

..Je, hiyo ni mara yako ya kwanza kukutana na baridi kali.

..Umewahi kuishi ktk nchi zenye baridi kama Canada, Usa, au nchi yoyote ya bara ulaya?

..Je, kuna tofauti kubwa kati ya baridi ya majira ya winter na baridi ya wakati wa kupanda mlima Kilimanjaro?
 
Nakupongeza tena Heaven On Earth, kupitia uzi huu:
Nimefanya mazoezi ya maandalizi na wewe,
Nimepanda na wewe,
Nimeona jamaa aliyefariki akishushwa sambamba na mkewe katika majonzi,
Nimechoka na wewe,
Nimelia na wewe,
Nimekata tamaa na wewe lakini nikajifariji na wewe na nikasonga mbele na wewe,
Nikawaona wavuta bangi wakitupita kwa kasi na badae mmoja wao akathibitisha kutangulia si kufika, akarudishwa duniani,
Kila ulipochoka, akili yangu ilikupa moyo, "twende HOE bila wewe siwezifika kileleni" ulikubali kwa machozi ya uchovu,
Nilisonga na wewe,
Simu yako iliishia chaji, nilihuzunika kwa kuwa hata kama tukisonga pamoja sitaona tena taswira nzuri ya safari yetu,
Nikawasikia ma-guide wakishauriana juu ya kuendelea ama kutoendelea na safari, nikaiona hatari ya kifo mbele yetu, nikasikitika.

Ukungu ulipozidi kule juu kiasi cha kutomuona aliyeko mbele yako, nilipatwa na hofu labda utapotea na kuporomokea upande wa Kenya,
Lakini nilikuwa na wewe,
Picha ya mwisho ambayo barafu imeziba maandishi ya kibao cha Uhuru Peak, ilinitia simanzi kubwa kwa hali ya hewa, nikajaribu kujifananisha na wewe kwa kujidumbukiza kwenye freezer ya butcher, lakini ukasema barafu niiwazayo mimi ni "cha mtoto"...

Hata hivyo, kwa jinsi ulivyotiririka kwa ustadi mkubwa, sikutamani muishie hapo na safari ya kurudi duniani ianze...

Nilitamani safari iendelee, mzuka wa simulizi yako uliniaminisha kuwa baada ya Uhuru Peak, Heaven on Earth would be taking me to the next peak... And probably it could be real Heaven like her name... Can't wait for the next episode.

Pongezi kwa guide wako Fredy kwa kukufikisha kileleni, iwe funzo kwa wanawake wengine wote kuwa, mwanaume kumfikisha mwanamke kileleni haijawai kuwa kazi rahisi, yaitaji uvumilivu na kushikamana.

Hongera sana HOE.
Ngoja nielekee You tube kujazilizia elimu hii tamu.

Khaa!nikajua na ww ulikua kati ya msafara wa kupanda naye😂😂😂 jaman kuna watu mnahitaji ushauri wa Dk kbs😂😂...
 
Natamani kupanda sema mafua na joints za miguu.
Kama baridi la kwetu Magamba Lushoto linanilaza kitandani wiki na mafua juu, je nitaweza kwea Mlima Kilimanjaro?
kiwatengu naweza beba coldril kwa ajili ya kukata ukali wa mafua au siruhusiwi kunywa dawa nikiwa katikati ya safari?

😂😂😂madame mie naon wanaOpanda wengi ni maportable..hv wanene wanaweza kweli?yaan bado sijashawishika ..maana nikama safari ya jehanum jaman
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Wanaweza mbona...
Mwenyewe ni kibonge na nina mpango wa kupanda! Ila watu tuloko nao wanakata tamaa kila leo!
[emoji23][emoji23][emoji23]madame mie naon wanaOpanda wengi ni maportable..hv wanene wanaweza kweli?yaan bado sijashawishika ..maana nikama safari ya jehanum jaman
 
Natamani kupanda sema mafua na joints za miguu.
Kama baridi la kwetu Magamba Lushoto linanilaza kitandani wiki na mafua juu, je nitaweza kwea Mlima Kilimanjaro?
kiwatengu naweza beba coldril kwa ajili ya kukata ukali wa mafua au siruhusiwi kunywa dawa nikiwa katikati ya safari?
Coldril sio dawa nzuri kwa mazingira ya kule ina mchanganyiko wa dawa ambao unaweza ukakuletea usingizi ukawa kama umelewa itakuwa ni hatari kwako na zaidi unaweza ukashindwa kupumua vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom