Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Aisee....kumbe hapo mwishoni umemaanisha "nchi gani" [emoji13] [emoji13]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna faida gani ya kupanda huo mlima?kwa wewe unayepanda
 
Mkuu Nyani Ngabu Brother nn naomba uibadirishe hii thread iwe kwa lugha ya kimalkia.
Ongezea udambwi dambwi alaf kachapishe vitabu uviuze huko ughaibuni..

Pesa itayopatikana uwape nauli ndugu zetu walio kwama huko.
 
kwa nini wanapanda usiku?
Kupanda kutoka kipo to uhuru peak inafaa upande usiku saa5,6 au7 ukichelewa ili ufike kule saa12-2au3 asubuh kabla jua a halijawa kali kidogo na itakubidi uwe na sun glass ili uzuie ile miyale ya jua inayopiga kwenye barafu inaumiza macho unaweza kuja macho yamekua kama ya mchina na yamevimba so ni swala la kuwahi jua ndo mana safari inaanza usiku ili umalize uanze kurudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina mafua ila nina allergy na baridi.
Yaani mimi na baridi ni kama mbingu na ardhi...hatupatani asilani.
Ndo najiuliza hapa
Kama una allergy na baridi kwl kbsa bila kupepesa macho sikushauri labda pitia njia ya marangu kaishie kituo cha kwanza mandara hapo uone km utaliweza baridi la uko mbele maana baridi lipo hata uvae nguo za aina gani sema wengine wanavumilia maana hawana matatizo km yako ya flu so kwako no thankyu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mpk kunguru sema nmesahau ni point gani ile na ni after mandara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na lile joto itakua sehemu za nguo zako kwny kwapa pale pameshabadilika rangi to chanikiwiti.
 
Tukumbushane Mmiliki wa Chelsea The Blues Roman Abramovich aliishia kituo gani? Maana najua hakufika kileleni ingawa ndio lilikua lengo lake

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa story nlizozikuta kwa tour guider wetu jamaa hakutoboa na hakuanzia chini alipanda kwa helicopter mpk kibo then ndo akaanza safari ya kwenda uhuru na alikua na walinzi wake si chini ya wa5 na wasaidizi wabongo so kipindi wanapanda wale wasaidizi wake wabongo ndo walimwona kua hali yake siyo nzuri ndo ikabidi wamzuie kuendelea akashushwa chapchap then akarudi UK baada ya muda hawa wasaidizi wabongo ikabidi awaite UK walikaa wiki moja akawashukuru kwa kuokoa maisha yake akawapa na mpunga then wakarudi bongo sasa cjui ilikua story tu au ni kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hostels zipo za boys na girls
Ukicheza michezo ya baba na mama ujue unajipunguzia uwezo wako wa kutoboa mpk kileleni na utampa kazi sana guider wako na bahati nzuri mkishtukiwa kua mnavunja iyo amri itabidi mfanyishwe mazoezi kidogo ili mchangamke
Ukishindwa kufika Stella na kuendelea hupati cheti na siyo kwamba utarudishwa chini kbsa hapana utasogezwa kituo mlichotoka ili uwasubirie wenzio walio endelea kuhusu pesa nahisi mtakua mmemalizana we utakua unawadai kukufikisha getini tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah!!!
Hapa sasa ndo naona live kutofikia lengo.
Maana mafua yakizidi sana hata upumuaji unakuwa mdogo kitu kinachoweza leta athari.
Asante sana mkuu kwa ushauri wako.
Nitaufanyia kazi
 
Kuna mengi ya kujifunza kutoka simulizi ya HOE ila kuna kubwa nimelitafakari kuhusu mhusika Fredy kama personal guide.

Sisi wote katika maisha yetu tuna nafasi moja au zaidi kuwa guide aidha ya kumuongoza mtu au kundi kufikia kilele cha mafanikio au kilele cha kutimiza malengo.

Tunawahitaji watu ma guide au porter ambao ni wema kama Fredy wanaoweza kututia moyo na kutuhurumia kipindi tunapambana kufika hatua fulani katika maisha yetu.

Licha ya kuwahitaji akina Fredy kama ma guide ila pia tunao wajibu wa sisi pia kuwa na moyo kama wa Fredy ili kuwawezesha na kuwasaidia wafike kileleni.( tuwafanyie wengine vile tungependa na sisi tufanyiwe)

Na watu kama Fredy/guide ni lazima tuwape heshima zao kwa kutambua thamani na umuhimu wao katika maisha yetu( jambo ambalo HOE amelifanya kwa kutambua na kumpa credit guide)

Tujiulize na kutafakari sote, je mimi na wewe tumewasaidia na kuwawezesha wangapi katika mambo tunayoyajua au tuliofanikiwa kuwafikisha wengine kilele cha mafanikio?

Tunahitaji kuwa kama Fredy katika vipindi vya maisha yetu na pia tunahitaji kujifunza kwa HOE kwa kutambua na kueleza umuhimu wa watu kama Fredy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…