Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Najiskia aibu mpaka sasa mtanzania mimi on my middle twenties sijapanda KLM. Kila mwaka huwa najiapiza kupanda lakini nakosa kampani sometimes nakatishwa tamaa. Mkuu umenipa moto sana.

SHAME ON ME.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikuwa na ndoto za kupanda mwaka huu, ila hope mwakani nikiwa hai na afya njema nitapanda tuu. Nilifanya utafiti nikaambiwa mkiwa kama kikundi gharama huwa inapungua tofauti na ukiwa peke yako, nilijitahiti kutafuta kampani nikakosa
 
Heaven on Earth kwenye baridi huwa si mzuka wa genye kupanda unakua speed 20

Vipi wewe umekaa kwenye ile mibarafu muda wote ule,hukuwa na mzuka kabisa

Hamnaga mahali umefika ukaona hapa angekuepo bebe angenikunjua mpk,maana panashawishi?

AU ukiwa kule ubongo haukumbuki upande wa pili wa shilingi kabisa,unawaza kifo tu?
 
Umenikumbusha mbali. Nilipanda mlima mwaka 1993 nilikua form four. Wakati huo kulikua na njia ya kupitia msituni, kuanzia Maua, sikuhizi imefungwa njia hiyo. Ilikua shughuli kwelikweli. Tulianza Maua saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni tunaingia Horombo. Hiyo ni siku moja. Na ndio iliyokua shughuli pevu. Ilipofika jioni saa tisa hivi, tukapita ukungu fulani, na tulipoupita nikaangalia nyuma kumbe ni mawingu, ndio usawa wa mawingu, yamelala chini nyuma yetu kama blanketi. Wengine wanaotokea mikoa ya uwanda wa chini wakaanza kutokwa damu puani kwasababu ya kubadilika pressure ya nje kwa haraka. Kwa msoto huo, kesho yake kutoka Horombo kwenda Kibo Hut ilikua kama tambarare tu na tulifika mapema Kibo. Nimesoma sehemu ya zoezi. Sisi zoezi tulikua tunafanya na viatu vya kupandia mlima, mwezi mzima, na ulikua unatakiwa uvivae wakati wote, ni vizito. Ugumu niliopata kutoka kibo hut kwenda kileleni ilikua ni Usingizi (ambao nadhani unatokana na upungufu wa hewa.)( Nakumbuka tulifika Hanmeyer cave, tuliambiwa tupumzike kidogo kwa dakika chache nikalala nikaonta ndoto tatu), Kichefuchefu, Baridi kali, inayoumiza viungo. Mimi na wenzangu wachache tuliishia Gilmans Point, wengine walifika Uhuru.
 
Asante dear! Ndio hali ya hewa ilikuwa Nzuri Sana according to our guide! Hakukuwa na ice Kali wala upepo mkali japo me kwangu ilikuwa ni near death experience hahahahaha uhuru ilikuwa -21 degree alafu sijawahi kukaa hata mahali kwenye -1 degree
Hongera sana kwa kuweza kupanda huo mlima mwenzio nikiamkaga asubuhi nikiona lile libarafu najiona nimeshaupanda halafu umepitia njia ngumu machame uko vizuri
 
Nilikuwa na ndoto za kupanda mwaka huu, ila hope mwakani nikiwa hai na afya njema nitapanda tuu. Nilifanya utafiti nikaambiwa mkiwa kama kikundi gharama huwa inapungua tofauti na ukiwa peke yako, nilijitahiti kutafuta kampani nikakosa
Mkuu namimi nina nia hiyo mpaka sasa. Sina kampani tu. Kwa nini tusiunganishe nguvu tutimize hili mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…