Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Alama yako mimi eenh
Ebu ngoja kwanza nianze kufanya mazoezi ya kupanda huu mlima huku nilipo

Ili siku ya basidei yako tukipanda huko nisije kukusumbua kabisa
Hahaha hahaha
Hapo ndo umeongea la maana!
Si umeona madam alikuwa anakimbia mchangani eehh
 
2019 huna haja ya kuprove mtu asie
na umuhimu
Nitajitahidi kupata picha mbili tatu nadhani utajua siongopi, sijadandia treni kwa mbele, stori ya huyu dada inamsisimua kila mtu na kama uliwahi kufanya tukio lolote linalofanana na hilo ni lazima ulikumbuke, nadhani hapa ndio mahali pake ungetaka stori kama hizi tuzitolee wapi? kama wewe huna tukio lolote unaloweza kushea hapa usikonde acha walio nazo wamwagike huwezi kuzuia mzuka wa matukio kama hayo, subiri picha ni kwa vile zipo katika mtindo ule wa kizamani wa picha za makaratasi mpaka ziskaniwe ningeshaziweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeridhika mkuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuuu umeongea ukweli kabisa...mi nilienda hapo mwaka 2017...mazingira ya sasa yameboreshwa na eneo liko chini ya mwekezaji.
Pia tuliambiwa chanzo cha maji yake yanatokea mlima kilimanjaro via ardhini na hili lilithibitishwa baada ya kumwaga pumba kwenye kilele cha mlima kilimanjaro hatimae mabaki yake yalionekana lake chala.View attachment 984044

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu asante sana, wakati ule 1995 tulikuta kulikuwa na wazee fulani waliokuwa kama waangalizi tu na palikuwa na mashine zilizozeeka ambazo zilikuwa zimeletwa pale miaka mingi kwa ajili ya kuvuta maji ya kutumia wakazi wa maeneo karibu na hapo lakini zilikuwa hazifanyi kazi. Watalii kutoka upande wa Kenya walikuwa wakizungushwa hadi upande wa Tanzania, Wakenye ni wajanja sana katika biashara Upande wao kulikuwa kunaonekana majengo mazuri kwa ajili ya watalii waliofika hapo huku upande wa Tanzania kukiwa tu na wenyeji waliokuwa wakivua samaki kwa mitumbwi ya mbao, wavuvi hawa walikuwa wakarimu sana na ndio waliokuwa kama 'maguide' wetu hapo kuanzia kushuka ziwani mpaka kuogelea na walituzungusha kwa mtumbwi wao huku tukipiga picha.

Uliza aliyesoma mkuu day miaka hiyo enzi za second master Mwl Shine, kina mwalimu Kiwango, Mkumbwa, Mzee wa physics Mwl Kimario na wengineo. Head boy wetu wakati huo alikuwa akiitwa Aretas na tulikuwa naye Picnic pamoja na kina Mushi, Nikolaus wa keni mengeni, Yuda wa pale Keni-Mengwe ambaye ndiye aliyekuwa mwasisi wa hilo wazo na mhamasishaji namba moja na wengineo kibao. Natamani mmoja kati yetu tuliyekuwa nao ajitokeze kunisapoti. Tulipanga siku moja kuja kukutana tena na kufanya tour kama hiyohiyo lakini mpaka leo sijui wazo lile liliishia wapi.
 
Nguza bwana@stori za urongo zinajulikana pole km umeteseka

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona hatujaona stori yako yeyote ili nayo tuijaji kama ni ya ukweli au ya uwongo zaidi ya comments kwa stori za wengine tu tena nyingi zikiwa ni za kubezabeza tu? Unajua sometimes comments za mtu moja kwa moja huonyesha ni dizaini gani ya mtu au ana tabia zipi, hapa watu tunashea maexperience wewe unaanza kuleta kejeli zisizokuwa na tija yeyote, subiri picha nikomeshe ujuaji wako uchwara
 
Sawa mkuu ujumbe umefika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitajitahidi kupata picha mbili tatu nadhani utajua siongopi, sijadandia treni kwa mbele, stori ya huyu dada inamsisimua kila mtu na kama uliwahi kufanya tukio lolote linalofanana na hilo ni lazima ulikumbuke, nadhani hapa ndio mahali pake ungetaka stori kama hizi tuzitolee wapi? kama wewe huna tukio lolote unaloweza kushea hapa usikonde acha walio nazo wamwagike huwezi kuzuia mzuka wa matukio kama hayo, subiri picha ni kwa vile zipo katika mtindo ule wa kizamani wa picha za makaratasi mpaka ziskaniwe ningeshaziweka.
Sijawahi kufika ila kwa kusimuliwa naona kbs kuna ukweli ndani yake kwenye hii story yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepanda mlima mara ya kwanza nna miaka 15. Nikaja panda tena nna miaka 20. Mwakani mwezi wa 7 napanda tena kumpa kampani dogo, anataka birthday yake asheherekee akiwa uhuru peak.
Nitampa kampani.

Kama vile niwajoin kwenye kwenye hii adventure. .....nipenyezee gharama inakiwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kufika ila kwa kusimuliwa naona kbs kuna ukweli ndani yake kwenye hii story yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huwezi amini hili Ziwa lipo pale Rombo lakini watu wengi wilayani humo wanazaliwa mpaka wanakufa bila kufika pale, sababu kubwa ni watu kutokuwa na mwamko wa utalii wa ndani kama aliokuwa nao dada yetu HEAVEN ON EARTH. Sisi wenyewe tulilazimisha kwenda huko, hata tungeliomba ruksa tungekataliwa asilimia 100%, nakumbuka nyumbani aliyejua ni mama peke yake, baba hata angesikia sijui ingekuwaje, alikujajua baadae sana.
 
Nafikiri pia ni kwa jinsi lilivyo jiografia yake kulifikia ni ngumu.
Japo pia naunga mkono hoja, sie watz ni wagumu sana kwenye ishu hizo. Nimekaa Musoma muda mrefu kidogo lkn cha ajabu kuna watu hawajawahi kufika hata alipokuwa anaishi Mwl Nyerere wala kwenda Serengeti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ziwa chala nakumbuka sana mwaka 1995 tuliokuwa tunahitimu form four mwaka huo katika shule ya sekondary iiliyojulikana kama MKUU DAY SECONDARY SCHOO Madume tu peke yetu tuliamua kufanya kile tulichokiita PICNIC YA WAGUMU katika ziwa hili, nakumbuka wasichana walilia sana tuende nao ila tulikataa kwani picniki hiyo haikuwa na baraka kutoka kwa walimu wala walezi. Tulijiandaa kwa vyakula vingi akiwemo mbuzi wa kuchinja na vinywaji vingi vikiwemo vileo. Hatukupima kabisa hatari zozote ambazo zingeliweza kutokea kule na kweli wengi wetu tulinusurika hatari nyingi mfano binafsi ilikuwa almanusura nizame wakati nikiogelea kwani lile ziwa ni la ajabu mno, ukiwa mita moja unajiona huwezi kuzama lakini sogea kidogo tu utashangaa! Lina slope kali na kukosa wenzangu waliokuwa wanajua kuogelea leo nisingelikuwepo hai.Ziwa lipo chini kina kirefu kutoka juu na mpaka ulifikie siyo mchezo unashuka kama upo juu ya mlima vile.

Baada ya kuogelea na kununua samaki kwa wenyeji waliokuwa wakivua ili tukachome jioni kabla hatujalala, usiku huo kuna hatari nyingine ilitokea ambayo hatukuiarajia, lilifumuka joka kubwa kusikojulikana na kutokomea bila shaka eneo tulipokuwa tumeweka kambi lilikuwa karibu na makazi yake, bahati halikumdhuru mtu. Usiku tulienjoy sana huku tukicheza miziki ya reggae hasa Bob marley na Lucky dube baada ya kula vyakula vyetu supu ya mbuzi na mazagazaga mengine kibao, Kesho yake kama saa 4 asubuhi hivi tukaanza safari ya kurudi shuleni huku tukiwa tumeacha historia kubwa Wilaya nzima ya Rombo katika Mashule mengine yote yaliyokuwepo wakati huo kama Ibukoni, Mashati, Shauritanga na Namfua tuliacha waliokuwa form 3 wakipanga na wao mwaka uliofuata wende lakini nafikiri hawakuweza kutimiza lengo hilo.

Wote tulirudi salama salimini na siwezi kuisahau siku hiyo, kama yupo mtu tuliyekuwa naye siku hiyo tafadhali ikiwezekana kama ana picha tulizopiga siku ile tuwasiliane ikiwezekana tuzilete hapa JF. Ziwa hili Wachagga wa Mkuu-Rombo wana simulizi nyingi kuhusiana na kutokea kwake wengine hudai ziwa mwanzoni lilijitokeza maeneo fulani ya msituni huko kijiji cha Maharo eneo ambalo hadi leo inasemekana pana dimbwi kubwa na ukirusha chochote pale kama shina la mgomba au mti husafiri mamia ya kilomita mpaka ziwa chala chini kwa chini. Lakini pia inasemekana kuwa maji ya ziwa hili hupita chini kwa chini kutokea Mlima Kilimanjaro na kuja kutua hapo chala, si hivyo tu kutoka tena hapo chala maji hayo hupita chini kwa chini mpaka ziwa jingine jirani liitwalo ziwa JIPE na ndio maana baadhi ya watu wanaozama katika ziwa hilo wengine huenda kuokotwa ziwa Jipe. Ziwa pia lina mamba hatari na wenyeji walitusihi sana tusiingie ndani sana wakati wa kuogelea wakatuonyesha maeneo salama. Upande wa Kenye kulikuwa kunaonekana Hoteli nzuri tofauti na Tanzania kwa wakati huo.
Mkuu lake chala nimenusurika kufa mara mbili, 2002 & 2006 like ziwa hapana aisee lina vituko vingi sana hatua moja kutoka ulipo unazama, na kwa chini kuna nguvu kubwa sana inayokuvuta baada ya mara ya mwisho niliapa sitakaa nitudi kwenye lile ziwa tena, kuna nyoka wengi mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom