sirdelta
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 306
- 82
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Fredy sio Porter, ni Senior Guide...Hahahaa. Hata mimi mkuu kunakitu nimehisi maana Fred kamwagiwa sifa mnoo hadi kawivu kameniingia sio siri . nimetamani niwe porter 😀 😀 😀 😀
Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa uwezo wako wa kufikiri nahisi una kiwango cha SGR,heko mkuu umenena vyema sanaKuna mengi ya kujifunza kutoka simulizi ya HOE ila kuna kubwa nimelitafakari kuhusu mhusika Fredy kama personal guide.
Sisi wote katika maisha yetu tuna nafasi moja au zaidi kuwa guide aidha ya kumuongoza mtu au kundi kufikia kilele cha mafanikio au kilele cha kutimiza malengo.
Tunawahitaji watu ma guide au porter ambao ni wema kama Fredy wanaoweza kututia moyo na kutuhurumia kipindi tunapambana kufika hatua fulani katika maisha yetu.
Licha ya kuwahitaji akina Fredy kama ma guide ila pia tunao wajibu wa sisi pia kuwa na moyo kama wa Fredy ili kuwawezesha na kuwasaidia wafike kileleni.( tuwafanyie wengine vile tungependa na sisi tufanyiwe)
Na watu kama Fredy/guide ni lazima tuwape heshima zao kwa kutambua thamani na umuhimu wao katika maisha yetu( jambo ambalo HOE amelifanya kwa kutambua na kumpa credit guide)
Tujiulize na kutafakari sote, je mimi na wewe tumewasaidia na kuwawezesha wangapi katika mambo tunayoyajua au tuliofanikiwa kuwafikisha wengine kilele cha mafanikio?
Tunahitaji kuwa kama Fredy katika vipindi vya maisha yetu na pia tunahitaji kujifunza kwa HOE kwa kutambua na kueleza umuhimu wa watu kama Fredy.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio jiwe letu tunalolijua sisi, ni jiwe jabali/mwamba/rock.
Hata mimi niliposikia kubusu jiwe nilistuka.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ninauzoefu wa kupanda milima ya kawaida. Na Nahisi hata Kilimanjaro Naweza [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ila natamani sana ila naogopa kufa.. Hongera sana heaven
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kucha za vidole vya miguu ziling'ookaje? ulikuwa umevaa kandambili au? manake kabla ya kupanda mlima Kilimanjaro ni lazima ufanye preparation ya vitu vifuatavyo:
1.Viatu vigumu (Boots) lakini viwe vyepesi ili kukusaidia kutembea bila kuchoka.
2.Soksi pair 4 ndefu safi na nzito.
3.Mycotta powder.
4 Gloves safi zenye sufi ndani.
5.Jacket au pullover zito.
6.Boshori lile kofia la sweta linalofunika kichwa na kuacha sehemu ya macho tu.
7.Miwani nyeusi kupunguza mng'ao wa theluji.
7.Climbing stick
8.Kibuyu au chupa ya maji.
9.Back pack kwa ajili ya kuhifadhi vitu vidogo vidogo kama glucose,biscuits,juice n.k.
Hayo ndio mahitajio ya msingi unayotakiwa kuconsider kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni wale wasaidizi wabeba mizigo(mapota) au jina jingine ni mburuta.
Mkuu BAK jitahidi sana upande huu mlima, ni Adventure nzuri kuliko zote ndani ya Tanzania na Africa kwa Ujumla...
Ma Shaa Allah.
Kama bado, nakuombea ujaaliwe pia kwenda kuhiji au kufanya Umrah Makkah.
Mkuu, mlima Kilimanjaro unapandika kipindi chote cha Mwaka, sema bado kuna miezi mizuri.
Binafsi huwa napenda sana mtu apande kuanzia May, June, July, August na September...huwa mvua sio nyingi sana.
Mfano mwaka Jana 2018, mwezi wa 10 na 11...haikuwa mizuri kabisa.
Sitasahau siku nimepanda kupitia Machame, mvua haikukatika ndani ya siku 2 full sasa unakuta hakuna namna, mnaenda tu.
Kama kuna mvua, ni hatari kuliko upepo.
Bahati nzuri mvua huwa zinanyesha huku chini chini....
Maeneo kama ya Kibo hut au Barafu camp, hayana mvua kabisa kwa sababu ni jangwani.
Uzi unaogezeka pages unadhani Dada kaendeleza stori kumbe kuna vibibi vinapiga umbea!.
Andikeni zenu mpige umbea,au amewambia anataka replies nyingi?
Shame!