Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Fredy sio Porter, ni Senior Guide...
Regardless hana certificate.
Habari boss.

Nataka kurudi tena Uhuru Peak kama mtalii sasa manake mwanzoni nilipanda kama mwanafunzi.

Ila sasahivi nataka nirudi na wadogo zangu wawili.

Nataka nijue rough estimates ya kupanda kwa mtu mmoja kama mtalii.

Na mpango wa kupanda mwezi wa 7.

Shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mods kitufe cha UNLIKE tuwakamate waongo
(5) wengi , mfano wanaojichuna ngozi n.k
umepanda miaka mitano hujaona waliochubuka ngozi ya mwili au miguu kubabuka ngozi kwa baridi
ilifikia wakati nikagombana na tour guides sijawahi kurudi tena.
Guide hamzuii mtu kutembea umeambiwa kuna mtu kapanda Mlima Kilimanjaro kkwa masaa ma5 hakuna mtu alimzuia
Mt Margarita Uganda
Hakuna Mlima bora maarufu na wa kwanza Afrika km Kilimanjaro hiyo mingine ni km Uluguru
Una akili kweli wewe? Na miongozo ya kupanda mlima Kilimanjaro unaijuwa?
.
Mt Margarita kuna mahala nimesema ni maarufu na ni bora kuliko Kilimanjaro?
.
Kwa kukusaidia tu hakuna mlima mrefu Tanzania zaidi ya Kilimanjaro unaoufikia urefu mlima Margarita.
 
Una akili kweli wewe? Na miongozo ya kupanda mlima Kilimanjaro unaijuwa?
.
Mt Margarita kuna mahala nimesema ni maarufu na ni bora kuliko Kilimanjaro?
.
Kwa kukusaidia tu hakuna mlima mrefu Tanzania zaidi ya Kilimanjaro unaoufikia urefu mlima Margarita.
Nyie ndo mnatuambia njano ni dhahabu,Tangu nasoma sijawahi sikia hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG-20190317-WA0002.jpg
TOP KABISA HAPA KWENYE POLE YA MNARA "Bondwa peak"
IMG-20190317-WA0000.jpg
MORNING SITE HAPA

IMG-20190317-WA0001.jpg
Peak

IMG_20190316_111240.jpg

MNARA ULIOPO KWENYE PEAK YA MLIMA. TULIUPANDA PIA (NOTE KAMA UNAKIZUNGUZUNGU USIPANDE)
IMG_20190316_104856.jpg
KILELE AMBACHO HATA UWE FUNDI VIPI KUFIKA NI NGUMU KIPO MBELE YA Bondwa peak
20190316_060204.jpg


Habari wakuu poleni na majukumu.

Mleta mada hongera kwa kuipanda milima yote hiyo. Nakupongeza sana maana kupanda mlima sio mchezo kama ujajipanga.

Kupitia uzi huu nikaona sio vibaya niungane na Class mate wangu baada ya UE SUA tukajikoki kuupanda MLIMA ULUGURU.

Mimi na washkaji tuliipanga toka mwezi ulipita, Tulikua na shahuku sana na tulikua tunataniana sana kuwa kuna wengine wataishia Morning site 😂😂😂. Kila mtu alikua akijiona komando na ataupanda adi kileleni "Bondwa peak"

Kabla ya safari yetu hii nilikua nafanya jogging kwa wanaofahamu morogoro nilikua natoka Stand ya zamani napita old Dar road naitafuta New Dar road kupitia Jordany University College na kuzunguka Mpaka Msamvu then route naimaliziaga Masika CRDB.

Hii show sio poa ila ilinisaidia sana kupanda mlima.

Jana ndo ilikua tarehe ya kuanza safari yetu. Tuliamka saa 11 asubuhi. Tukiwa na nguvu kama zote. Sikula kitu chochote asubuhi nilichukua Maji lita 3, begi langu la kawaida ndani likiwa na Sklnzi/Mkate na Mandazi.

Sikuchukua vyakula vya mafuta nikiofia Kupata kichefuchefu wakati wa kupanda mlima. Hii ni kwakua ukipiga msosi wa mafuta mengi na maji yakutosha inaleta shida sana na unaeza tapika na usifike kilele. Bora ukabeba Eat some more au biskuit za kawaida.

Kituo cha kwanza kilikua morning site hapa kuna nyumba moja ambayo kuna mtu anaishi na familia yake. Ni ndani ndani sana karibu na mwisho wa makazi ya watu na msitu unaoelekea mlimani.

Mbele yake kuna Kituo tena ( Kabla ya kuanza msitu) Hapa kuna choo cha kiaina ila bado hakikidhi mahitaji. Kuna Maji pia. Hivyo unaweza ukamaliza haja yako.

Tukaunza msitu kama mleta mada alivyosema awali kuna nguzo za umeme saba zinazoelekea on "Bondwa peak" ambapo kuna mnara wa Abood Media.

Show ya kuitafuta nguzo ya pili ilikua balaa kwanza punzi zilianza kukata kwa watu (tulikua speed sana kama unavyojua vijana wakitaka kuoneshana ubabe wa kufika peak).

Nikachukua mti wa kunipa support nikakaza nikatoboa nguzo zote hadi ya saba ambapo ndo killele.

Kileleni tulikuta makundi mengine pia. Tukajumuika kujuana na kufurahi kwa pamoja. Pia kuna Mzee ambaye alikua zamu kulinda mnara tulipiga nae story( Honestly niliutani ugali wake vibaya mno mana njaa ilikubali😯😂😂😂😂)

KUSHUKA MLIMA.

Kushuka mlima tulitumia 45min tunashuka kama wanajeshi wa Mzinga 😂😂 mpaka Kituo cha kwanza Morning site.

ASUBUHI YANGU IKOJE.

Nimeamka poa na sina maumivu ya misuli mana nikiwa JKT 842 KJ nilijifunza kitu baada ya route ndefu unafanya Physical Training kama Kujinyoosha kiuno,Mgongo,Mikono, Miguu na Joints mbalimbali. Pia push ups kama 10.


NEXT TRIP (MOROGORO)

Trip yangu ijayo itakua ni Mindu Dam. Ambayo ipo karibu na Mzinga Jeshini.

MBEYA: Hii nayo itakua trip ya kibabe sana itakua ni kupanda Mlima Mbeya Alafu nitaoanda Mlima RUNGWE (mlima wa tatu tanzania), Gods Bridge Tukuyu Mbeya, Kyela Beach (Including Matema beach and Mwamunyange beach),

LIFE TIME TRIP; Nautamani sana Mlima Meru alafu Mlima Kilimanjaro huu utafunga kazi:


NB Kama una tour Mt Uluguru usiache kunishtua nitakupa company.
 
nimependa vile umetembea na kutuelezea kuhusu mlima huo mkuu, japoumeelezea kifupi sana hasa kwenye hiyo safari yako, alafu kwa wengine amba hatujui hizo semehu hasa ka zile ulizokuwa wapiga mazoezi ya kukimbia ungeweza kutusaidia kwa kutupa makadirio ya kilometers mkuu ingesaidia sana maana wengine tunajifunza kupitia huku kupashana habar. huo umbali unasaidi maana namie nikija kujiandaa nijue najipangia umbali gani ili nisije shindwa kwa misuli kuuna kwa kukosa mazoezi ya kutosha.
Yote kwa yote nikupe pongezi nyingi sana pia Mungu akujalie ukamilishe dhamira yako ya safari hizo
 
nimependa vile umetembea na kutuelezea kuhusu mlima huo mkuu, japoumeelezea kifupi sana hasa kwenye hiyo safari yako, alafu kwa wengine amba hatujui hizo semehu hasa ka zile ulizokuwa wapiga mazoezi ya kukimbia ungeweza kutusaidia kwa kutupa makadirio ya kilometers mkuu ingesaidia sana maana wengine tunajifunza kupitia huku kupashana habar. huo umbali unasaidi maana namie nikija kujiandaa nijue najipangia umbali gani ili nisije shindwa kwa misuli kuuna kwa kukosa mazoezi ya kutosha.
Yote kwa yote nikupe pongezi nyingi sana pia Mungu akujalie ukamilishe dhamira yako ya safari hizo
Habari mkuu shukrani. Hiyo route ni KM 15 nafanya mbio tu bila kupumzika wala kusimama sehemu nikichoka napunguza mwendo naenda taratibu mpaka nafika point ya mwisho mkuu wangu. Lakini pia kabla ujapanda uwe unakunywa maji mara kwa mara hii itakusaidia mkuu. Kama upo morogoro napanda tena Jumamosi. Ila nitalala kuna vitu bado naitaji kujua kutoka kule mlimani.
 
Back
Top Bottom