TOP KABISA HAPA KWENYE POLE YA MNARA "Bondwa peak"
MORNING SITE HAPA
Peak
MNARA ULIOPO KWENYE PEAK YA MLIMA. TULIUPANDA PIA (NOTE KAMA UNAKIZUNGUZUNGU USIPANDE)
KILELE AMBACHO HATA UWE FUNDI VIPI KUFIKA NI NGUMU KIPO MBELE YA Bondwa peak
Habari wakuu poleni na majukumu.
Mleta mada hongera kwa kuipanda milima yote hiyo. Nakupongeza sana maana kupanda mlima sio mchezo kama ujajipanga.
Kupitia uzi huu nikaona sio vibaya niungane na Class mate wangu baada ya UE SUA tukajikoki kuupanda MLIMA ULUGURU.
Mimi na washkaji tuliipanga toka mwezi ulipita, Tulikua na shahuku sana na tulikua tunataniana sana kuwa kuna wengine wataishia Morning site 😂😂😂. Kila mtu alikua akijiona komando na ataupanda adi kileleni "Bondwa peak"
Kabla ya safari yetu hii nilikua nafanya jogging kwa wanaofahamu morogoro nilikua natoka Stand ya zamani napita old Dar road naitafuta New Dar road kupitia Jordany University College na kuzunguka Mpaka Msamvu then route naimaliziaga Masika CRDB.
Hii show sio poa ila ilinisaidia sana kupanda mlima.
Jana ndo ilikua tarehe ya kuanza safari yetu. Tuliamka saa 11 asubuhi. Tukiwa na nguvu kama zote. Sikula kitu chochote asubuhi nilichukua Maji lita 3, begi langu la kawaida ndani likiwa na Sklnzi/Mkate na Mandazi.
Sikuchukua vyakula vya mafuta nikiofia Kupata kichefuchefu wakati wa kupanda mlima. Hii ni kwakua ukipiga msosi wa mafuta mengi na maji yakutosha inaleta shida sana na unaeza tapika na usifike kilele. Bora ukabeba Eat some more au biskuit za kawaida.
Kituo cha kwanza kilikua morning site hapa kuna nyumba moja ambayo kuna mtu anaishi na familia yake. Ni ndani ndani sana karibu na mwisho wa makazi ya watu na msitu unaoelekea mlimani.
Mbele yake kuna Kituo tena ( Kabla ya kuanza msitu) Hapa kuna choo cha kiaina ila bado hakikidhi mahitaji. Kuna Maji pia. Hivyo unaweza ukamaliza haja yako.
Tukaunza msitu kama mleta mada alivyosema awali kuna nguzo za umeme saba zinazoelekea on "Bondwa peak" ambapo kuna mnara wa Abood Media.
Show ya kuitafuta nguzo ya pili ilikua balaa kwanza punzi zilianza kukata kwa watu (tulikua speed sana kama unavyojua vijana wakitaka kuoneshana ubabe wa kufika peak).
Nikachukua mti wa kunipa support nikakaza nikatoboa nguzo zote hadi ya saba ambapo ndo killele.
Kileleni tulikuta makundi mengine pia. Tukajumuika kujuana na kufurahi kwa pamoja. Pia kuna Mzee ambaye alikua zamu kulinda mnara tulipiga nae story( Honestly niliutani ugali wake vibaya mno mana njaa ilikubali😯😂😂😂😂)
KUSHUKA MLIMA.
Kushuka mlima tulitumia 45min tunashuka kama wanajeshi wa Mzinga 😂😂 mpaka Kituo cha kwanza Morning site.
ASUBUHI YANGU IKOJE.
Nimeamka poa na sina maumivu ya misuli mana nikiwa JKT 842 KJ nilijifunza kitu baada ya route ndefu unafanya Physical Training kama Kujinyoosha kiuno,Mgongo,Mikono, Miguu na Joints mbalimbali. Pia push ups kama 10.
NEXT TRIP (MOROGORO)
Trip yangu ijayo itakua ni Mindu Dam. Ambayo ipo karibu na Mzinga Jeshini.
MBEYA: Hii nayo itakua trip ya kibabe sana itakua ni kupanda Mlima Mbeya Alafu nitaoanda Mlima RUNGWE (mlima wa tatu tanzania), Gods Bridge Tukuyu Mbeya, Kyela Beach (Including Matema beach and Mwamunyange beach),
LIFE TIME TRIP; Nautamani sana Mlima Meru alafu Mlima Kilimanjaro huu utafunga kazi:
NB Kama una tour Mt Uluguru usiache kunishtua nitakupa company.