Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

DO NOT SHOUT
(usipige kelele)

Sehemu ya........13

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047


ILIPOISHIA....
baada ya Yusto na Caren kufanikiwa kumuokoa mtoto albino asiuwawe na majambazi,wanaludi chuoni huku kila mmoja akiwaza na kumuhisi mwenzie kuwa huenda akawa siyo mtu wa kawaida kutokana na namna walivyokabiliana na majambazi wale wakiwa wawili tu.
Asubuhi ya siku iliyofuata wakiwa chuoni wanafunzi wachuo hicho wanaandamana baada ya kuchoshwa na mfululizo wa matukio ambayo hawaelewi nini chanzo chake...


SASA ENDELEA

Hali ilionekana si shwari, wanafunzi wa chuo hicho walikuwa wamechafukwa haswaa.
Ada waliokuwa wakitoa chuoni hapo nikubwa mno ilikuwa ni aibu kwa chuo kikubwa kama icho kupitia matukio ya ajabu kiasi kile. Mara waharishe chuo kizima,mara moto uwake, mara maji yakate,mara shoti za umeme hii ilikuwa kero kubwa kwa watoto hao wa kishua
Yusto na frank wakiwa kama walinzi wa siri wa chuo hicho walijikuta kwenye sintofahamu nzito wasielewe nini cha kufanya.

⭐⭐⭐
Ndani ya chumba kimoja kikubwa cha mkutano wanaume sita wakiwa wamevalia suti nadhifu zenye rangi nyeusi walionekana wamekaa wakijadili swala nyeti mno. Naam, hao ndio walikuwa viongozi wa juu kabisa wa chuo hicho kilichokuwa kikikumbwa na mfurulizo wa matukio yaliyoibua sintofahamu.

"Kwani Frank na Yusto wanafanya kazi gani?" alihoji mmoja wa wale watu

"Mimi pia nashangaa niwazi wameshindwa kufanya hii kazi labda tufikirie njia nyingine"

"Njia gani nyingine mzee"

"Hapana tatizo siyo Yusto wala Frank tatizo ni mtu anaeshambulia biashara za bosi Mark moon anaonekana kutumia akili kubwa sana"

"Kwaiyo tufanyaje na wanafunzi wameshaandamana bosi akipata taarifa sisi sote tutaonekana niwazembe"
Majadiliano yalionekana kuwa nimazito mno kama viongozi, yaliyokuwa yakiendelea chuoni pale yaliwafanya kuchanganyikiwa

"Jamani mimi nina wazo moja " alisema mmoja wa watu hao wote wakageuka na kumtazama wakiwa na shauku ya kumsikia anataka kusema nini.
lakini kabla hajasema chochote mara mlango wa chumba icho ulitoa kishindo baada ya kufunguliwa kwa nguvu wote walishituka na kugeuka kutazama ni nani aliyekuwa akiingia.
Hakuwa mwingine bali bosi Mark moon tajiri na mmiliki wa chuo cha MARK MOON PSP INTERNATIONAL UNIVERSITY aliingia akiwa ameongozana na watu watatu nyuma yake .wote walio kuwamo ndani ya chumba kile walisimama kuonyesha heshima kwa bosi Mark moon hali nyuso zao zikionyesha wasi wasi mkubwa walio kuwa nao.

Mark moon hakuwa mtu wa masihara kabisa kazi zake alizifanya kwa umakini wa hali ya juu.
Akiwa Sudan kusini, alipata taarifa ya mambo yanayoendelea chuoni kwake alighairisha safari yake ya kwenda Canada akalazimika kurudi tanzania.
Mark Moon alipitiliza na kusimama mbele ya watu wake ambao bado walionekana kuogopa, wala hakutaka kuketi akaanza kuzungumza.

"Huyu anaitwa Simigo, huyu anaitwa Mpili,na huyu anaitwa Brandina hawa wote ni majasusi nimetoka nao kenya watatusaidia katika hili tatizo linalotokea chuoni, waiteni hapa Yusto na Frank waje mara moja na ripoti kamili walipoanzia mpaka walipofikia" alisema Mark moon na punde simu ilipigwa kuwaita Yusto na Frank walio kuwa chuoni.

Wakati wakisubiri mark moon na wale majasusi watatu walianza kujadili baadhi ya vitu ikiwa ni pamoja na kupitia ramani ya chuo,
majasusi hao walionekana kuwa makini isivyo kawaida.
Punde mlango ulifunguliwa Yusto na frank waliingia huku kila mmoja akiwa na file mkononi waliinamisha vichwa vya chini kwa heshima na kuanza kusogea mbele.
Yusto alikuwa akiwatazama watu walio kuwemo kwenye chumba kile kichwani akiwa na maswali yasiyo na majibu. Wala hakuwaza tena kuhusu Caren. Kwa sasa alijali kibalua chake kuliko kingine chochote.

Macho yake yakatua kwenye uso wa Brandina. Brandina nae akamtazama, wakawa wanatazamana kwa macho yanayozungumza.
Brandina nae alikuwa si haba bali ni mrembo haswa, kwa haraka haraka ukimuona usingefikiri anafanya kazi ile ngumu na hatari ya ujasusi. Walitazamana kwa zaidi ya sekunde 30 kiasi cha kumfanya Mark moon awatazame.


ITAENDELEA.....
Vipi kuhusu John na Sophia?
Caren kaletewa majasusi, ataweza kweli kuifanya kazi yake?
Sasa tuna Sophia, Caren na Brandina!!


SIMULIZI HII INAPATIKATA YOTE,,, WASILIANA NAMI KUPITIA NAMBA HII (call/WhatsApp)

0756862047
 
Mkuu nikihitaji mzigo wote inakuaje??
 
DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)

Sehemu ya...............14

ILIPOISHIA
...
Mark Moon tajiri na mmiliki wa chuo kikubwa na maarufu nchini Tanzania anatumia nguvu kubwa kwa kuwatafuta majasusi watatu anaowapa kazi ya kwenda kutafuta ni nini chanzo cha matatizo yaliyokuwa yanakikimba chuo chake hali akijua wazi kuwa hii ni vita ya kibiashara dhidi ya matajiri wenzanke.

SASA ENDELEA...
Brandina nae alikuwa si haba bali ni mrembo haswa, kwa haraka haraka ukimuona usingefikiri anafanya kazi ile ngumu na hatari ya ujasusi. Walitazamana kwa zaidi ya sekunde 30 kiasi cha kumfanya Mark moon awatazame.

"Simigo, tayari Yusto na Frank wamekwishafika mnaweza kuendelea na utaratibu kila kitu kipo mikononi mwenu kwa sasa fanyeni kazi" alisema Mark Moon kisha akawaruhusu watu wake kuondoka na yeye akafuata. Mle ndani walibaki Yusto, Frank pamoja na wale majasusi watatu.

Walianza kujadili namna watakavyoweza kulitatua tatizo ambalo lilikuwa likikimbua chuo cha bosi wao mark moo, tayari majasusi hao walikuwa wametengeza mpango kabambe wa kumkamata au kuwakamata ambao hasa walikuwa ni wahusika wasababishaji wa matukio hayo yaliyowanyima raha wanafunzi.

"Bosi Moon ametengeneza mfumo wa umeme mpya wa dharula pale chuoni, kwa kuwa mpango wa adui ni kuharibu sifa ya hiki chuo ninaimani atataka tena kuharibu huu mfumo wa pili wa umeme, sasa sisi tutamtega hapo na lazima tumnase" alisema Simigo akiwa kama kiongozi wa oparesheni hiyo.
Wote walitikisa kichwa kukubaliana na maelezo hayo, walijadiriana namna watavyohakikisha wahusika wananasa kwenye mtego wao na mwisho kila kitu kilikaa sawa.
"Mimi na Brandina tutaungana na Yusto pamoja na frank kuingia ndani ya hiki chuo, Mpili wewe utabaki nje ukiratibu mipango yetu yote" alisema simigo.

Mwisho walitawanyika kila mmoja akiingia rasmi kwenye jukumu lake, sasa ilikuwa ni timu ya watu watano.
⭐⭐⭐

Ikiwa ni saa kumi jioni sasa chuo kilikuwa kwenye hali ya utulivu kiasi baada ya bosi mwenyewe mark moon kufika chuoni hapo akiwa na mainjinia akaongea na wanafunzi kuwatuliza kisha mfumo mpya wa umeme ukafungwa upya na mainjinia hao.
Lilikuwa ni jambo lililo wafurahisha mno wanafunzi wa chuo hicho, hatua za dharula zilizochukuliwa ama kwa hakika ziliwaridhisha hawakuwa na sababu ya kuendeleza maandamano yao hasa baada ya bosi mwenyewe ambae ilikuwa ni ngumu kumuona lakini alifika chuoni hapo.
⭐⭐⭐

Caren alikuwa ametulia kwenye bustanimoja tulivu maeneo ya chuo cha mark Moon. Pembeni alikuwa na glass ya kinywaji akionekana mwenye mawazo kiasi.
Mara ghafula kuna mtu alifika nyuma yake na kumziba macho yake kwa mikono miwili.
Caren alitulia kwa muda huku akitaka kung'amua ni nani aliyemziba macho.

"Mmmh Yusto" alisema Caren huku akiachia tabasamu mwanana, akiwa na asilimia mia kuwa aliyekuwa nyuma yake alikuwa ni kipenzi chake Yusto.
Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa mara yule mtu alimuachia na kusogea mbele ya Caren, hakuwa ni yusto bali John. Caren alionekana kukelwa mno na ujio wa John.
John alisimama mbele ya Caren huku akimuangalia kwa macho makali.

"Hivi ni kweli una date na Yusto, umenikataa mimi Caren, nina shida gani kwanza, yule maskini Yusto atakupeleka wapi mwanamke mrembo kama wewe, mbona unajidharilisha Caren au unafikiri nataka kukuchezea" Aliuliza John wakati huo Yusto alionekana kwa mbali anakuja alipofika karibu yao akasimama nyuma ya mti mmoja akawa anawasikiliza mazungumzo yao, hakuna aliemuona.

ITAENDELEA.....


NJOO WHATSAPP JIPATIE SIMULIZI HII HADI YA MWISHO.
NAPATIKANA KWA NAMBA HII
0756862047
 
DO NOT SHOUT
(usipige kelele)
Sehemu ya................15

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...


"Hivi ni kweli una date na Yusto, umenikataa mimi Caren, nina shida gani kwanza, yule maskini Yusto atakupeleka wapi mwanamke mrembo kama wewe, mbona unajidharilisha Caren au unafikiri nataka kukuchezea" Aliuliza John wakati huo Yusto alionekana kwa mbali anakuja alipofika karibu yao akasimama nyuma ya mti mmoja akawa anawasikiliza mazungumzo yao, hakuna aliemuona.

SASA ENDELEA....

"Unaishi kizamani sana John, sasa ndio kutongoza gani huko. Achana na Yusto ongea wewe kama wewe" alisema Caren huku akimtazama John kwa macho ya dharau, kauli hiyo ilionekana kumkwaza mno John, alijiona ni kama amevuliwa nguo zake.

"Caren mimi si....." Alitaka kuzungumza lakini Caren alinyoosha mkono akimtaka anyamaze kwanza.

"Sikiliza nikwambie John huna haja ya kuhangaika na maneno meengi, mimi sina shida na pesa za mwanaume, nachotaka mimi ni upendo basi, kwanza unanionaje. Hakuna ambae hakujui taarifa zako karibu kila mtu hapa chuoni anazifahamu, umewachezea wanawake wangapi na kuwatelekeza ukiwalaghai na pesa zako, mimi ni nani hadi usinifanyie hivo, harafu siku hizi mapenzi hayalazimishwi john jibu moja tu lilitosha" Caren aliongea kwa kumaanisha.

"Kwa hiyo unamaanisha Yusto yeye ametulia, mbona sophia ana...." Kabla John hajamalizia sentesi yake mara Yusto alijitokeza mbele yake na kusimama. si caren wala john hakuna aliyetegemea ujio wa Yusto wakati huo.

"Nilisha kwambia John achana na Sophia, maisha yangu mimi na yeye hayakuhusu kwa lolote" aliongea Yusto huku akimtazama John usoni.
Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa, mwisho John alipiga hatua kuondoka alipofika usawa aliposimama Yusto akasimama na kuongea kwa sauti ya chini.
"Nilikuonya hukutaka kunisikia, ninachoenda kukufanyia nakuhakikishia utajutia maamuzi yako" alisema john kisha akaondoka kwa hasira.

Yusto hakuyajali maneno ya John japo alijua wazi wazimu alionao kijana huyo angeweza kumfanyia lolote baya lakini hakujali hata. alisogea na kukaa pembeni ya Caren kisha wakawa wanatazamana huku kila mmoja akitabasamu.

"Miss you" alisema Yusto

"Miss you more Yusto, ulikuwa wapi nimekutafuta sana, simu zangu pia hupokei" aliuliza caren hali akimtazama Yusto kwa macho ya udadisi.

"Aah nilitoka mara moja nikaacha simu chumbani, am sorry" Yusto alidanganya.

"Its okay, usijali"

"Umenisamehe?"

"Yah, why not?"

Alisema caren kisha wote wakatabasamu tena.
Mara ujumbe mfupi wamaandishi uliingia kwenye simu ya caren haraka akaufungua na kuusoma

"WAMETENGENEZA MFUMO MWINGINE WA UMEME, MPANGO WETU NI ULE ULE HAKIKISHA HICHO CHUO KINAKUWA GIZA KWA WIKI NZIMA"

Caren alimaliza kuusoma ujumbe aliotumiwa.
Wakati huo Yusto nae alikuwa bize akisoma ujumbe aliotumiwa na jasusi Brandina ambae kwa sasa tayari alikuwa ndani ya chuo hicho.

"We mwanaume mbona umenitoroka, hebu njoo tuongee ninamaswali kuhusu huyo mwanamke Caren mnaemuhisi, Frank kaniambia wewe ndio mwenye maelezo zaidi kumuhusu, njoo basi mara moja baba angu 😘"

Yusto alimaliza kusoma ujumbe huo kutoka kwa Brandina wenye utani ndani yake, akainua macho yake akamtazama Caren akakuta nae anamtazama.

"vipi"
"mmh poa tu vipi"
Waliongea baada ya kutazama kwa muda kila mmoja akaonyesha kama hamna kilichotokea, lakini haikuwa hivo.

ITAENDELEA....


NJOO WHATSAPP/NIPIGIE KWA NAMBA 0756862047 KUPATA SIMULIZI HII YOTE KWA PAMOJA HADI 80.

BADO MAMBO NI MENGI NA MAZURI, USIACHE KUFUATILIA SIMULIZI HII YENYE MKASA WA KUSISIMUA.

0756862047
 
DO NOT SHOUT

Sehemu ya................16

Mtunzi: Saul David

Phone: +255756862047

Email: Saulstewarty@gmail.com

ILIPOISHIA...

Yusto alimaliza kusoma ujumbe huo kutoka kwa Brandina wenye utani ndani yake, akainua macho yake akamtazama Caren akakuta nae anamtazama.

"vipi"
"mmh poa tu vipi"
Waliongea baada ya kutazama kwa muda kila mmoja akaonyesha kama hamna kilichotokea, lakini haikuwa hivo.


SASA ENDELEA...
Kwa mtazamo hali ilionekana kuwa shwari baina ya wawili hao wanaopendana, lakini uhalisia haukuwa hivyo kuna bomu kubwa lilikuwa kati yao. Yusto hakuwa akifahamu kuwa mwanamke anaempenda Caren, ndiye sababu ya matukio yote yanayowaumiza kichwa chuoni hapo. Ni kweli kuna wakati alihisi huenda Caren anahusika lakini baada ya penzi kuibuka katikati yao ikamfanya ajisahau na kutojishughulisha tena na hisia zake.
Caren nae akiongozwa na hisia za mapenzi kwa Yusto anajikuta kuanza kupoteza umakini katika kazi aliyoagizwa asijue kama Yusto ndiye adui yake mkubwa na wanafanya kazi mbili zinazokinzana.

Yusto anapokea ujumbe kutoka kwa jasusi Brandina akimtaka wakaongee kumuhusu Caren, wakati huo huo Caren nae anapokea ujumbe kutoka kwa wakubwa zake wakimtaka ahakikishe anakata umeme wa dharula uliofungwa chuoni hapo.
Meseji hizo zinawatoa kwenye mudi wote wawili.

"Samahani nina dharula naweza kwenda" alisema Yusto
"Jamani si umekuja sasa hivi lakini" alisimama Caren akionekana kutofurahishwa na kauli ya Yusto lakini ukweli nae alikuwa anataka kuondoka kwa ajili ya mwenda kujiandaa na kazi aliyopewa.

"Noo, nitakutafuta tena baadae Caren usijali" alisema Yusto.

Mwisho walikubaliana na Yusto akaondoka.
********


Majasusi wawili Brandina na Simigo walikuwa ndani ya chuo cha Mark Moon, waliingia kama wapishi wapya ambao huandaa vyakula vya wanafunzi chuoni hapo.

Walionekana wakiwa wamesimama kwenye dirisha kubwa la kioo wakiwa ndani ya jengo moja la kisasa ambalo ndilo lilikuwa jiko la chuo hicho.

Walikuwa wamesimama wakitazama nje huku wakizungumza baadhi ya mambo kuhusu jukumu zito walilokuwa nalo ndani ya chuo hicho.

Kwa mbali Yusto alionekana anaelekea bwenini, wakawa wanamuangalia huku wakiendelea na mazungumzo.


"Unahisi kweli Yusto yupo karibu na Caren kwa ajili tu ya kumpeleleza" aliuliza Simigo

"Sina hakika ndio maana nataka niongee nae kwanza nitajua tu, kwani unahisi wanamahusiano" alijibu Brandina nakuuliza swali huku wakiwa bado wanamuangalia Yusto.

"Sijasema hivo lakini kuna mazingira fulani hivi yananifanya nihisi hivyo"

"Mmh sina hakika Yusto yuko smart sana hawezi" alisema Brandina

Punde meseji ya Yusto iliingia kwenye simu ya Brandina

Uko wapi ,,

Niko huku jikon nakuja nikukute chumbani kwako

Alijibu Brandina kisha akamuaga Simigo na kuanza kuondoka.

"Brandina" Simigo aliita
Brandina akasimama na kugeuka.

"Hakikisha unafanya kazi yako, usilete habari nyingine"

"Unamaana gani Simigo"

"Nimeona macho yako namna unavyomuangalia Yusto"

"Unamaana gani"
"Sipendi uzembe kazini, nina wasiwasi Yusto amechanganya mapenzi na kazi ndio maana hajafanikiwa mpaka sasa ,naona na wewe unataka kudondokea huko, tangu mda nimekuwa nakufuatilia"

" Simigo haujatumwa kunifuatilia Mimi, hebu na wewe focus kwenye kazi najua nini nafanya"
Brandina aliongea kwa ukali kidogo kisha akaondoka, maneno aliyoambiwa na Simigo yalimuudhi ingawa yalikuwa na ukweli ndani yake. Japo hakuwa ameweka wazi jambo hilo lakini tayari jasusi Simigo alisha msoma akampa tahadhali asichanganye mapenzi na kazi.
***

Muda mfupi baada ya Yusto kuondoka, Caren nae alisimama na kuanza kuelekea bwenini chumbani kwake, akiwa bado hajafika mara alikutana uso kwa uso na Sophia.

"Nilikuwa nakutafuta sana, wewe ndio Caren si ndiyo" alisema Sophia huku akimtazama Caren juu mpaka chini.

Kwa mbali alionekana Brandina anaenda zake mabweni ya wanaume kwa ajili ya kwenda kuzungumza na Yusto lakini alisimama ghafula baada ya kumuona Caren kwa mbali, haikuwa sura ngeni kwake kwani tayari alikuwa na picha zake.
akatamani kujua anafanya nini wakati huo, akaanza kuwasogerea pale waliposimama na Sophia.

ITAENDELEA...


WhatsApp
0756862047
 
Kafupi mkuuu, ongeza ongeza kama inawezekana
 
Don't breath! The movie
images.jpg
huyu mzee!
 
Back
Top Bottom