mtzmweusi
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 8,658
- 8,994
Kumbe we mfipa posuta mkombeBila shaka tayar [emoji120]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe we mfipa posuta mkombeBila shaka tayar [emoji120]
ThanksBila shaka tayar [emoji120]
Duh! Tupo wengi kumbe,mwalindauli mkombe?Kumbe we mfipa posuta mkombe
Eya mkwaiDuh! Tupo wengi kumbe,mwalindauli mkombe?
Hahaha kwacheleeDuh! Tupo wengi kumbe,mwalindauli mkombe?
Hichi kipande umekirudiaDO NOT SHOUT
Mtunzi: Saul David
Tel: +255756862047
Email: saulstewarty@gmail.com
ILIPOISHIA...
Yusto, Frank, majasusi pamoja na vijana wengine kwenye oparesheni hiyo walitulia kimya kusikiliza maongezi yatakayo kuwa yakiendelea kutoka meza aliyokaa Caren na wenzake.
SASA ENDELEA....
Caren alifika akavuta kiti na kukaa, pembeni yake alikuwa amekaa kijana mmoja bishoo aliyekuwa ameweka dawa(breech) nywele zake na kupigilia suti nadhifu ya bei ghali yenye rangi ya kijivu.
Mbele yao alikaa mzee mmoja wa makamo aliekuwa anakunywa kinywaji taratibu.
Simigo na watu wake wote walikuwa kimya kusikiliza maongezi yatakayo endelea huku wengi wakiamini huenda kuna watu wengine wataongezeka pale alipokuwa Caren na wenzake lakini haikuwa hivyo.
Walianza maongezi wakiwa vile vile watatu.
"Shikamoo baba" Caren alimsalimia yule mzee kwa heshima
"Marhaba mwanangu habari za siku"
"Ni nzuri"
Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa..
"Mbona humsalimii mwenzako hujamuona" aliuliza yule mzee.
"Nimemuona, mambo Revo"
"Poa za siku caren, masomo yanakwendaje"
"Safi tu mungu anasaidia"
Baada ya salamu hizo mzee alikohowa kidogo kisha akaanzisha kuzungumza.
"Sasa Kuna jambo limenifanya niwaite hapa ghafula wewe Revocatus pamoja mwezi wako Caren" alisema yule mzee huku akivua miwani yake na kuiweka mezani.
kauli ya mzee huyo ilimshtua si Yusto pekee yake ni mapoja na wenzake wote waliokuwa kimya kusikiliza maongezi hayo.
"Mwezi? mwezi gani tena?"
Hili ndilo swali lilibaki kwenye vichwa vyao.
"Caren, mwenzako kanifuata mara kadhaa ananiambia kuwa mnagombana kila wakati kila siku, yeye hataki kulea mtoto wa mtu na wewe unasema bila hivyo basi muachane, Sasa mimi nimeona niwakutanishe hapa tukae tujadili tumalize hili tatizo"
Kauli hiyo ilimfanya Caren asimame ghafula huku akionekana mwenye ghadhabu sana. Akaongea kwa hasira
"Baba hili jambo si tushazungumza tayari tukamaliza. kabla hata hajanihamisha chuo, na alikubali kuwa atamlea mwanangu kwa nini saa hizi abadilike hapana mimi siwezi baba siwezi kukaa mbali na mwanangu siwezi kabisa,
hata kama ameniowa, yeye ndio anaenilipia ada lakini hapa baba kwa hili hapanaaa"
"Kuwa mpole mwanangu hebu kaa basi tuzungumze kaa mama"
"Baba Mimi misimamo wangu ndio huo, ni kweli nampenda Revo nampenda sana lakini hii haiwezi kuwa sababu ya kuteseka kwa mwanangu hawezi kumlea basi nimemaliza" Caren aliongea huku machozi yakiwa karibu kumtoka, akachukua mkoba wake na kuanza kuondoka. Mzee alimuita bila mafanikio.
***
Maongezi hayo yalikuwa ni mwiba mchungu kwa Yusto aliyekuwa kwenye Kona moja akisikiliza mubashara kupitia kile kinasa sauti alichovaa sikioni.
"No, no, Caren, haiwezekani" alisema Yusto hali akionekana kuanza kuchanganyikiwa.
Vijana wa Simigo walitua kimya wakati Caren anatoka, pamoja na kwamba walikuwa wakisubiri amri kutoka kwa Simigo lakini pia wao hawakuona sababu ya kumkamata Caren kutokana na maongezi yale, badala yake walijikuta wakimuonea huruma.
"Misheni imehairishwa, kila mtu arudi sehemu yake" sauti ya Simigo ilisikika kutoka kwenye vile vifaa vya mawasiliano akiwataka vijana wake waachane na kazi ile.
***
Hali ya Yusto ilikuwa ni mbaya mno, hakuwa na uwezo wa kupiga hata hatua moja mbele wala nyuma alichokisikia kilimuumiza kuliko kawaida.
"Caren ana mume, ana mtoto, halafu...aah haiwezekani" Aliwaza Yusto. Maumivu aliyokuwa akiyapata hayakuwa na mfano.
Mapenzi yanauma yanauma sana hasa ukipenda na ukamuamini mtu wako kwa asilimia zote, hali hii ingemtokea yeyote, hata wewe msomaji wa simulizi hii si Yusto peke yake [emoji12].
****
Nusu saa baadae baada ya tukio hilo, Caren alionekana akiwa sehemu nyingine tofauti akiwa na yule mtu aliyemuita baba, yule kijana aliyedai kuwa mume wake na wasichana lika lake wengine wakiwa wanne.
Cha ajabu walikuwa ni wale wasichana waliopewa mafunzo kwa pamoja kambini, wakatolewa kwa misheni maalum ya kuangusha biashara za bosi mark Moon.
"Aisee poleni na kazi" alisema yule mzee
"Mmefanya kazi nzuri sana, Caren kumbe wewe ni muigizaji mzuri tu eeh, eti staki mwanangu ateseke hahahah, kwa mtoto gani Caren" alisema yule mzee, wote wakaangua kicheko na kugonganisha glasi zao za vinywaji.
"Tusifurahi sana jamani muhimu tumeweza kuwapoteza watu waliokuwa wakimuhisi Caren vibaya, Sasa Caren fanya kazi yako kwa uhuru lakini ongeza umakini"
***
Ukweli ulikuwa hivi
Siku ile ambapo Simigo alichomeka kifaa cha kudukua mawasiliano kwenye simu ya Caren ilikuwa ni siku ambayo Caren aligundua kuwa anafuatilia.
Caren hakuwa mzembe hata kidogo alishtuka mpango wa Simigo mapema sana baada ya kukiona kile kifaa,
haraka alitoa taarifa kwa wakubwa zake kutumia simu yake ndogo na hapo ndipo wakapanga mchezo wa kuwapoteza maboya majasusi hao.
Kwa kuwa walijua kuwa mawasiliano ya Caren yanafuatiliwa kwa makusudi walituma sms yenye utata yakawafanya Simigo na wenzake kumfuatilia Caren hadi ARENA HOTEL lakini huko wanakutana na mada nyingine tofauti ya mahusiano ya Caren na Revo yakiwa matatani kutokana na Revo kukataa kumlea mtoto wa Caren.
Wakati Caren na wenzake wanafanya maongezi hayo walijua kila kitu kuwa wametegeshewa vinasa sauti hivi wakacheza mchezo ndani ya mchezo.
Caren hakuwa na mume wala mtoto.
****
ITAENDELEA,......
Njoo inbox kupata SIMULIZI hii yote 1-80 kwa bei PUNGUZO... nakukumbusha bado hata hatujafika nusu ya story yetu [emoji56]
0756862047
Hapo patamu
Sawa naliona, kesho mapema sana napost...Lini tena mkuu? Kumbuka kipande cha mwisho ulikipost twice
Duh! Nitafanya hivyo soon mkuuSawa naliona, kesho mapema sana napost...
Alafu kwa nini hujalipia mpaka saa hizi wenzio wamemaliza mpaka ep 80.
0756862047
Ipo gud sanaDO NOT SHOUT
(Usipige kelele)
Sehemu ya..............27 - 28
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
ILIPOISHIA....
Wakati huo Sophia alikuwa anarudi akiwa na kopo la maji mkononi,
Alifungua mlango hata bila kubisha hodi akaingia ndani.
Moyo wake ukamfyatuka paaa!!
Hakuamini kuona kile alichokuwa anakiona mbele yake.
Naam Caren alikuwa amemkumbatia Yusto.
Sophia akahisi kuregea mwili na roho, hakuwa na nguvu tena la kuendelea kulishika lile kopo la maji likadondoka chini....
Je, nini kitafuata?
SASA ENDELEEA...
Sophia alianza kujihisi kupumua kwa shida kifua kikiwa kikamjaa, hasira aliyokuwa nayo mda huo dhidi ya Caren haikuwa na mfano.
Alikimbia kuwafuata nia na madhumuni ikiwa ni kwenda kumvaa Caren mwanamke aliyekuwa ndiyo chanzo matatizo yote.
Caren alikuwa bado amemkumbatia Yusto,
Yusto hakuweza kujitikisa wala kufanya chochote hakuwa ametegemea ujio wa Caren kabisa,
Hakujua ataanzaje kumuweka mbali mwanamke huyo ambae alikuwa ameujeruhi moyo wake kwa kiwango kikubwa mno, mwanamke aliyemwamini na kumpenda.
Hakujua kuwa kile kilichotokea Arena hoteli ilikuwa ni mchezo wa kuigiza tu Caren hakuwa na mume wala mtoto.
Yusto hakuelewa hilo
Caren akiwa bado amemkumbatia Yusto, alihisi nyuma yake kuna mtu anakuja kwa kasi.
Kwa kuwa Caren alikuwa mzoefu na mwenye mazoezi ya kutosha akili yake ilifanya kazi haraka akahisi kuna mtu anataka kuwadhuru yeye na Yusto.
kama umeme Caren alimsukuma Yusto pembeni Kisha yeye akageuka kwa staili ya ajabu akiwa ameinama chini.
Alimdaka Sophia aliyekuwa anakuja kwa kasi akiongozwa na hasira zake, akamzunguusha juu juu na kumrusha ukutani.
Kishindo kikubwa kilisikika wakati Sophia anapigiza kichwa chake ukutani akaanguka chini na kutulia kimya huku matone ya damu yakimtoka puani.
Hili tukio lilikuwa la ghafula mno yaani kufumba na kufumbua tayari Sophia alikuwa chini.
"Sophiaaaaa...."
Yusto aliita huku akikimbia na kumuwahi Sophia pale chini wakati huo akiwa katika hali ya mshangao mkubwa baada ya mfuatano wa matukio ambayo hakuyategemea.
Caren nae alibaki amesimama hali akiwa ameshika mdomo wake kwa mshangao baada ya kufanya tukio ambalo hakutegemea kulifanya,
hakujua kama mtu huyo ni Sophia akili yake haikuwaza hivyo kabisa hii ni Kutokana na mazoea aliyojengewa akiwa kambini na wenzake, wakati wote aliwaza kushambuliwa na adui.
Yusto aliweka vidole vyake juu ya pua ya Sophia, akainua uso wake uliokuwa umejawa na wasiwasi akamtazama Caren ambae nae alikuwa na wasiwasi vile vile.
Bila kuzungumza chochote Yusto alimnyanyua Sophia akambeba haraka na kutoka nae nje, Caren akiwa anafuata nyuma.
****
Ilikuwa ni maeneo ya mjini, kila mtu alionekana kuwa bize na shughuli zake, mama mmoja kichaa alionekana akiwa ameketi jirani na jalala moja kubwa lililokuwa pembezoni mwa barabara kuu ya rami.
Alikuwa anajisemesha mwenyewe kisha anacheka sana. Naam huyu alikuwa ni mama mlezi wa Yusto.
Dakika chache baadae gari mbili nyeusi zilifika eneo hilo zikasimama pembeni ya barabara, wakashuka wanaume kadhaa waliokuwa wamevalia suti nyeusi, wakaanza kutembea taratibu kumuelekea yule mama kichaa.
Mama huyo mlezi wa Yusto, alipatwa na hali hiyo baada ya kupata ajali kubwa ya kugongwa na gari tangu kipindi hicho akapata wendawazimu.
John alipanga kumtumia mama huyo kama njia ya kumuadhibu adui yake Yusto. Alifika eneo hilo akiwa na watu kadhaa aliopanga nao kufanya tukio la ajabu kwa mama huyo akiamini angemuumiza Yusto kwa kiasi kikubwa baada ya kubaini namna Yusto alivyokuwa akimpenda na kumthamini mama huyo kichaa.
John akiwa na mpambe wake wa karibu Abdullah walibaki ndani ya gari wakiwa wanatazama namna vijana wao walivyokuwa wakihangaika kumkamata mama yule kichaa.
Abdullah alichukua simu yake akampigia mmoja wa vijana wake.
"Hey hebu acheni kutumia nguvu, nimewambia huyo mama ukimwambia tu tunakupeleka kwa Yusto atakubali mwenyewe kufuata acheni Mambo ya ajabu mnataka tujaze watu hapa" alifoka Abdullah.
***
"Sitaki mbona mnanishika shika mnataka kunibaka mnataka kunibaka hahahaha" alisema yule mama Kisha akamalizia kwa kicheko.
Wakati huo Yusto alitoka ndani ya gari akawa anarekodi tukio hilo kwa simu yake, kisha bila kusita akamtumia Yusto kwa njia ya WhatsApp.
"Mama hutaki kwenda kwa Yusto"
"Eeh Yusto, mwanangu, yuko wapi"
"Yupo huko ametutuma tuje tukuchukee"
"Aah Sasa mbona hamjasemaaaaa"
Alisema yule mama kisha akaanza kuongoza njia kuelekea kwenye gari.
Wale vijana walijikuta wakitabasamu baada ya kugundua kumbe kazi ilikuwa ni nyepesi tu.
Baada ya kupiga hatua kadhaa yule mama alisimama ghafula akageuka na kuanza kurudi.
"Wapi tena mama si tunaenda kwa Yusto au hutaki"
"Zawadi, nimesahau kumbebea zawadi"
Alisema yule kichaa kisha akanyanyua kifurushi chake kimoja alichokuwa amepakia makolokolo mengi akageuza na kuanza kuelekea tena kwenye gari.
"Hicho nini Sasa"
"Zawadi ya Yusto"
"Aah hebu let's basi tukusaidie"
"Sitaki nitabeba mwenyewe, Nipande gari lipi hili au hili au nipande yote"
Aliuliza mama kichaa kauli iliyozidi kuwafurahisha vijana wa Yusto.
"Njoo upande huku mama Yusto" alisema John, na hapo yule mama alitimua mbio kumfuata.
Akiwa amekaribia kumfikia John yule mama alisimama ghafula akawa anamtazama John usoni.
John nae alimtazama ni kama vile akili yake ilimwambia kuwa aliwahi kumuona sehemu lakini hakukumbuka ni wapi, akapotezea.
"Panda twende mbona umesimama tena unanishangaa"
Alisema John huku akimuonyesha ishara yule mama aingie kwenye gari.
Yule mama aliendelea kumshangaa John huku akipiga hatua kumsogelea zaidi Kisha akamnyoshea kidole.
"John, wewe ni John umekuja tena ee umekujaa"
Alisema yule mama kichaa kauli iliyomshangaza kila mmoja, si John peke yake.
Inakuwaje kichaa kama yule alitambue jina lake na wala hakuwa akimjua.
"Mi..Mimi?" John alihoji kwa wasiwasi kidogo huku akijinyooshea kidole.
"Ee wewe kwani wewe sio John mtoto wa nanlii nani huyuuu aaa nanlii kwani wewe ni mtoto wa nani kwanza" aliuliza yule kichaa
"Bosi hebu tuondoke huyu mama ni kichaa tu pengine kasikia tunavyokuita" alisema Abdullah.
"Lakini hakuna aliyeniita jina langu Abdullah"
"Ni sawa bosi lakini tuondoke kwanza angalia watu wameanza kututazama"
"Sawa" alisema John akiingia ndani ya gari huku alimtazama yule mama kicha akijitahidi kukumbuka ni wapi aliwahi kumuona lakini kumbukumbu zake zikawa zinagoma.
"Mama ingia twende kwa Yusto basi" alisema Abdullah
"Aah hapana John ataenda kuniuwa huyu ni kama mama yake tu siendi tena Yusto atakuja mwenyewe kunichukua" alisema yule mama.
Abdullah akatoa ishara fulani kwa vijana wake haraka walimvaa yule mama na kumuingiza ndani ya gari.
"Niacheni niacheni, John atanipeleka kwa mama yake" yule mama alipiga kelele lakini hazikusaidia kitu,
Gari likaondoshwa kwa kasi huku baadhi ya watu wakishuhudia tukio hilo wasielewe kinachoendelea.
****
Ndani ya hospitali moja kubwa ya kisasa iliyokuwa ndani ya chuo cha mark moon hapo ndipo alipokuwa amelazwa Sophia akiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ICU.
Yusto na Caren walikuwa nje wakisubiri. Kila mmoja alikuwa kimya akisubiri maelezo kutoka kwa daktari.
Si Caren wala si Yusto kila mmoja alikuwa akionyesha kuwa na wasiwasi mkubwa.
Kitu ambacho Caren hakuwa akikifahamu hadi sekunde hiyo ni kuwa Yusto alikuwa amejeruhiwa vibaya na mchezo alioufanya Jana kuigiza kama mke na mama wa mtoto mmoja.
Lakini kwa kiasi alibaini kuna namna Yusto amebadilika sio yule Yusto anaemfahamu. Hapo ndipo Caren akakumbuka kuwa usiku wa Jana Sophia alikuwa akimfuatilia.
"Inamaana Sophia aliniona wakati ule? alinisikia? kwamba alijua kila kitu akaja kumwambia Yusto mungu wangu uzembe gani huu nimefanya" Caren aliwaza huku akimuangalia Yusto, mwili ukimtetemeka kwa kiasi.
Yusto nae aliinua macho yake wakatazama na Caren.
Caren aliona namna macho ya Yusto yalivyoonyesha kujawa na hasira.
"Nimefanya nini Mimi, Yusto wangu jamani, nimeharibu kila kitu" aliwaza Caren wasiwasi wake ukiwa ni mkubwa zaidi, hakuwa tayari kabisa kumpoteza Yusto, alimpenda mno.
Wakati haya yakindelea kwa mbali Jasusi mrembo Brandina alikuwa amesimama dirishani nje ya hospitali akiwatazama. Kumbe alikuwa akimfuatilia Caren kwa kila hatua.
Bado aliona kuna sababu ya kuendelea kumfuatilia.
Mara simu yake iliita haraka akaipokea, alikuwa ni Jasusi mwenzake bwana Simigo.
"Ndiyo Simigo"
"Uko wapi mbona sikuoni mda sasa"
"Niko hospitalini hapa nakuja"
"Unafanya nini huko hebu rudi kazini, usinambiee bado unamfuatilia Caren"
"Ndi...hapana nakuja" alisema Brandina Kisha akakata simu hali akionekana kukelwa na maongezi ya Simigo.
Akageuka tena na kuwatazama Caren na Yusto.
"Kwa nini bado wako pamoja, hisia zangu zinagoma kabisa kukubali hili, nahisi bado kunakitu kimejificha nitajua tu, Mimi ndiyo Brandina hakuna kazi nimewahi kushindwa.
Hebu muangalie ule mwili maziwa yake kifuani huyo mtoto alinyonya wapi, hapana hapa tumepigwa, huwezi kutufanya wajinga Caren. Hata kama wenzangu watakuwa kinyume na Mimi lakini sitakuacha hata hatua moja wewe na huyo Yusto wako"
Brandina alijisemea mwenyewe kisha akaondoka.
Je, nini kitafuata?
JOHN ATAFANYA NINI KWA MAMA KICHA?
NI KWELI YULE MAMA ANAMFAHAMU?
KUNA SIRI GANI HAPA?
YUSTO ATACHUKUA HATUA GANI AKIITAZAMA VIDEO YA MAMA YAKE ALIYOTUMIWA NA JOHN?
VIPI HALI YA SOPHIA ATAPONAA?
JE PENZI LA YUSTO NA CAREN NINI HATIMA YAKE?
BRANDINA ATAFANIKIWA KUMPATA CAREN KWENYE 18 ZAKE?
ENDELEA KUFUATILIA MKASA HUU HADI MWISHO....
(Kama umelipia tafadhali njoo inbox na screenshot ya muamala)
0756862047