Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ipo poa ntakuja whatsapDO NOT SHOUT
Sehemu ya..........29
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Email: saulstewarty@gmail.com
ILIPOISHIA....
Sophia anaanguka na kuzimia baada ya kushambuliwa na Caren. Anakimbizwa hospitali ya chuo upesi. Sasa Caren na Yusto wanasubiri majibu ya daktari bila kujua pia wakati huo Jasusi Brandina alikuwa akiwafuatilia kwa siri hatua kwa hatua.
Upande wa pili John anamteka mama kichaa ambae ni mama mlezi wa Yusto lakini cha ajabu mama huyo anaonekana kumfahamu John ambapo John nae pia anahisi kuwahi kumuona mama huyo lakini kumbukumbu zake haziko sawa.
Je nini kutafutaa?
SASA ENDELEEA...
Caren alibaini huenda Yusto akawa ameambiwa na Sophia tukio alilolifanya usiku wa Jana kuwapoteza kimtazamo majasusi baada ya kuigiza kama mke wa mtu na mama wa mtoto mmoja ili waache kumfuatilia.
"Ooh mungu wangu nitafanyaje Mimi" Caren aliongea huku hofu yake ya kumpoteza Yusto ikionekana dhahiri.
Wakiwa katika hali hiyo mara alifika daktari akitokea ICU chumba cha wagonjwa mahututi alipolazwa Sophia.
"Daktari daktari vipi hali ya Sophia,anaendeleaje, atapona?" Yusto aliuliza maswali mfurulizo hali akiwa na hofu.
"Ooh taratibu kijana usijali Sophia yuko salama, ajali aliyopata imemsababishia hitirafu kiasi kwenye kichwa chake amepata mtikisiko wa ubongo kitaalamu tunaita brain concussion, lakini kwa sasa yupo kwenye uangalizi maalum atapona tu japo itachukua muda kidogo, tuwe na subira tafadhali" alisema daktari Kisha akaondoka.
Yusto alibaki ameduwaa akitafakari maelezo ya daktari kwa muda Kisha akageuka na kumtazama Caren,
Caren alimtazama Yusto kwa macho ya huruma akihitaji msamaha.
Akiwa na hasira Yusto alimkamata Caren mkono akawa anamvuta huku akitembea kwa kasi hadi mbele ya mlango wa chumba alicholazwa Sophia.
Alipofika hapo akamuachia.
" Haya angalia, muangalie mwenzako, umefurahi Sasa nakuliza umefurahi" Yusto aliongea kwa ukali huku akinyooshea kidole kwa Sophia aliyekuwa amelala kitandani kimya akipumulia mtungi wa gesi.
"Yusto mpenzi nisi...."
"Kimya, nani mpenzi wako, huoni hata aibu, mwanamke tapeli wewe kwanini umekuja kwenye maisha yangu Caren kwani nini, umeniumiza mimi umeona haitoshi unataka kumuuwa hadi mtu anaeniheshimu na kujali hisia zangu mtu anaenipenda kwa dhati, Caren why why Caren mbona hata hufanani" Yusto aliongea kwa uchungu.
"Sio hivyo Yusto, sikukusudia kufanya yote hayo"
"Hukukusudia? unauhakika, una mume, una mtoto hujawahi kunieleza kwangu ulitaka nini sasa Caren, ulitaka nini nakuliza, nijibu" Yusto alifoka
Caren alibaki kimya huku akilengwa na machozi swali la Yusto lililokuwa na ugumu mno kulijibu, haikuwa rahisi kumweleza ukweli kwamba alikuwa anaigiza tu yeye sio mke wa mtu wala hana mtoto
kufanya hivyo ilikuwa ni sawa na kuharibu kazi yake, japo alimwamini Yusto lakini angeanzia wapi kumweleza.
"Kimya, maana yake huna jibu, huna cha kujitetea, ulifikiri sito jua eti Caren, haya nimejua sasa mtu anaenipenda ambae umetaka muuwa ndiyo aliyeniletea hizo taarifa na hawezi nidanganya. shukuru mungu nimedanganya kuwa ameanguka la sivyo ungekuwa polisi mda huu" Yusto alisema huku akikwepesha kuelezakuwa nae pia alikuwepo eneo la tukio na aliona na kusikia kila kitu.
Caren alitaka kusema neno lakini Yusto alinyanyua mkono wake juu ikiwa ni ishara kuwa hataki kusikia maelezo yoyote.
" Huna ulichobakiza caren, ondoka na upotee kwenye maisha yangu Jumla nisikuone tena, otherwise nitakuuwa" alisema Yusto akiwa ametoa macho akimaanisha kile alichokizungumza.
"Ondokaaa....."
Taratibu Caren alianza kupiga hatua kuondoka huku akiwa na huzuni ya hali ya juu. Alitembea hatua kadhaa akageuka kumtazama Yusto.
Yusto alikuwa akimtazama huku nae machozi yakimlenga, wawili hawa walikuwa wakipenda si kidogo.
****
Nusu saa baada ya Caren kuondoka Yusto alionekana akiwa amekaa pembeni ya kitanda alicholazwa Sophia, alikuwa akimtazama mwanamke ambae amekuwa nae kwa kipindi kirefu kama rafiki wakipita kwenye vipindi vyote vya shida na raha.
"Am real sorry Sophia"
Alisema Yusto akijiona kuwa yeye ndio mwenye hatia na chanzo cha yote.
Hapo alikumbuka simu yake, akaichukua na kuitazama,alikuwa amepigiwa simu mara kadhaa na Frank rafiki yake.
Alifungua pia upande wa WhatsApp na huku anakutana na video aliyotumiwa na John adui yake mkubwa,
video ikimuonyesha mama yake mlezi yule kichaa akikamatwa kwa nguvu na watu wasiojulikana Kisha kupelekwa kwenye gari.
"TUCHEZE KIMYA KIMYA BILA KELELE ZA POLISI UKIZINGUA HUTOMUONA MAMA YAKO KICHAA, ACHANA NA CAREN"
Maandishi haya kutoka kwa John yaliyojaa dharau na kejeli yalifuata chini ya video hiyo.
Yusto hakuamini anachokiona mkono wake ulikuwa ukimtetemeka akajikuta anashindwa kustahimili kuendelea kuishika simu yake ikadondoka chini sakafuni wala hakujali.
Ni kweli John alikuwa amemshika pabaya tena pabaya mno, Yusto alikuwa ni Moto wa kuotea mbali, alimpenda sana mama huyo pengine kuliko kitu kingine chochote.
Yusto alitoka mle ICU akiwa na ghadhabu kubwa akapiga hatua kuelekea chumbani kwake.
****
Baada ya Caren kufukuzwa na Yusto pale hospitali alijikuta anakosa nguvu za kutembea umbali mrefu akaenda na kukaa kwenye bustani moja ya maua ndani ya chuo hicho.
Machozi yalikuwa yakimtoka hakuamini kama amempoteza Yusto kirahisi namna ile moyo wake uliumia sana sana.
Ili kulinda kazi yake ilimbidi kufanya hivyo aliwaza kama ataharibu kazi basi atawapoteza mama na mdogo wake.
Caren alikuwa chini ya usimamamizi wa watu wa mama tajiri anaejulikana kama madam Jane, huyu mama ndiye aliyekuwa anammiliki Caren na wenzake na yeye ndiye aliyekuwa amewatuma kwenda kushambulia biashara za tajiri mwenzake Mark moon.
Naam hii ilikuwa ni vita ya matajiri wawili ambao wanawatumia vijana wa kazi kufanikisha malengo yao.
Caren hakuwa na budi kutii kile alichoagizwa ukizingatia watu hao walimpa msaada mkubwa kwa kuwatibu mama na mdogo wake waliokuwa karibu kufa.
kwa sababu hiyo Caren aliapa kutimiza kila jukumu atakalopewa ikiwa kama fadhila kwa Madam Jane na watu wake waliomchukua nchini Burundi akiwa binti mdogo kabisa.
"Lakini Yusto wangu nimuelewa hata nikimweleza Siri hii hawezi kuitoa kokote nina uhakika"
Mara wazo hili lilimjia Caren akawaza kuliko kumpoteza Yusto ni heri akamwambia ukweli kuwa yeye ni agent wa siri katumwa na bosi madam Jane ,pasipo kujua kuwa Yusto nae ni mlinzi wa siri wa bosi Mark moon.
Caren aliinuka pale alipokuwa ameketi akaanza kutembea haraka kurudi hospitali.
***
Alifika na kuingia moja kwa moja chumba alichokuwa amelazwa Sophia akiamini angemkuta Yusto lakini haikuwa hivyo Yusto hakuwepo badala yake aliona simu ya Yusto ikiwa chini sakafuni.
Taratibu Caren aliiokota ile simu akaitazama,
Kulikuwa na video iliyotumwa na John.
Caren akabinya 'play'
akaitazama video ile akaona kila kitu pamoja na yale maandishi ya vitisho pale chini kutoka kwa John.
"TUCHEZE KIMYA KIMYA BILA KELELE ZA POLISI UKIZINGUA HUTOMUONA MAMA YAKO KICHAA, ACHANA NA CAREN"
Caren alirudiarudia kuyasoma mandishi hayo mara mbili mbili, akawa haelewi lakini baadae akaelewa.
"Oh my God, John you you're going too far" (Oh Mungu wangu, John unafika mbali)
Alisema Caren, wakati huo pembeni yake Sophia alikuwa anafumbua macho taratibu, fahamu zikimrejea.
Je nini kitafuata?
ITAENDELEA....
BADO SAFARI YETU NI NDEFU NA SIMULIZI HII, NJOO WHATSAPP BEI PUNGUZO, TSH 1200 KUMALIZIA SIMULIZI HII HADI MWISHO ep80
KaribuIpo poa ntakuja whatsap
PamojaaHii simulizi kali sana.
0756862047 karibuIpo poa ntakuja whatsap
tupo mkuuuuWadau mpo tuendelee...!?
Tuendelee mzee arostoWadau mpo tuendelee...!?
Sawa tukutane jioniiPira limewakamkuu, ongeza petroli
jioni imepita mkuuSawa tukutane jionii