MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Hakuna kosa lolote kisheria mtu kuwa na Yard ya magari kama kafuata utaratibu. Hizi akili za Chalamila ni za kurudisha nyuma maendeleo.
Kusema litafutwe eneo la kujengea yards ni kauli ya kisiasa inayopaswa kupuuzwa. Watu washawekeza na wanalipa kodi halafu uwatoe tena sehemu walipo huoni kuwa ni kuhujumu maisha yao na ya taifa kwa ujumla? Tafadhali ndugu RC fanya majukumu yako mengine.
Jiji la Dar halina hata smoking zones halafu unapoteza muda na watu wanaofanya biashara zao kihalali. Jiji la Dar hata vyoo na mabafu ya public ni changamoto kubwa ila RC yuko bize na mambo yasiyo na tija.
===============
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila, ameeleza kukerwa na uwepo wa maeneo mengi ya kuuza magari (Showrooms) katika kila kona na vichochoro vya Dar es salaam.
Chalamila amesema hayo leo jijini Dar es salaam na kuongeza kwa kuwaagiza Wakuu wa Wilaya kudhibiti showrooms hizo, kwamba kuna haja ya kuwa na eneo maalum litakalokuwa na showrooms tu (mji wa showrooms).
“Moja ya mambo nilipanga kushauri ni uwepo wa Bandari kavu maeneo mbalimbali ya Dar es salaam, na uwingi wa showrooms, sasa showrooms hivi kila mahali zinaota mpaka nina ziara, nakwenda TRA nataka nikaulize kuna jambo gani kubwa?” amesema RC Chalamila.
RC ameongeza pia kuwa “Tunataka kama showrooms za magari ziwe mahali fulani, haiwezekani kila uchochoro kuna showroom ya magari, halafu usiku unakutana na magari hayana plate number yanatembea huko mtaani hayaeleweki, unakutana na watu wanakimbiza magari hii barabara ya kuelekea Masaki mpaka unajiuliza mle ndani ni kioski cha bangi au wanauza kitu gani?”.
Chanzo: Millard Ayo