Sina lengo la kukashifu dini, ila Walokole mna kelele sana

Sina lengo la kukashifu dini, ila Walokole mna kelele sana

Status
Not open for further replies.
Mkuu acha kabisa kweli wanakelele kuna mtaa mimi hama miaka miwil nyuma mzee wanasali saa usiku saa 6,saa 7 na saa 8 kelele hadi unashindwa kulala
Ukiona usiku wote huo unashindwa kulala kwa sababu ya maombi ya walokole utakuwa unashida ya kifamilia wewe sio bure kama sio shida ya kidunia mbona wengine tunalala hata pakiwa na vigodoro mtaani wala hatujali... kwa ushauri tu ukilala usilale na stress
 
Aisee tema mate chini ,waislamu wanapiga kelele kwa siku mara tano,vp kuhusu baa? Jamani katiba inasema kila mtu Ana haki ya kuabudu vp kuhusu hayo masabufa kwenye nyumba za kupanga zinazopiga rusha roho? Tuheshimu imani za wengine pia

Vp kuhusu wanao chuma udi,ubani nk mbona tunawavumilia? Mtuvumilie tu
Wewe kama sio mlokoke unayeongelewa hapa basi hujawahi kaa karibu na kanisa la kilokole la mabati.. ndani Kuna waumini wanne na speaker za bei rahisi zinazoumiza masikio.
Sauti kubwa mpo watu wawili kama sio uchokozi ni nini?
Bar wamepunguza
 
Wewe kama sio mlokoke unayeongelewa hapa basi hujawahi kaa karibu na kanisa la kilokole la mabati.. ndani Kuna waumini wanne na speaker za bei rahisi zinazoumiza masikio.
Sauti kubwa mpo watu wawili kama sio uchokozi ni nini?
Bar wamepunguza
Hhhhhhhh kimsingi upo sawa lkn kwa kiimani haupo sawa yaani kwa habari ya mabati au waumini wapo nne bado haitoi justification kuwa wamekosa sababu za kuomba Kama walokole kwa mfano umezikia walokole wanalia ,au wanapiga kelele wakiomba mala vyombo vinapiga kelele umeshawahi kujiuliza kwanini herode alituma watu wake wamwabie yesu wanafunzi wake waache kupiga kelele yesu aliwajibu nendeni mkamwambie yule mbweha nitaendelea kuhibili na hawa wakinyamaza mawe yatapiga kelele

Gesti kuna makelele
Bar kuna makelele

Kuna miikiti unakuta spika zipo dirishani kbsa lkn tunavumilia tu

Tuvumiliane tu kwa sababu kila my anamtafuta mungu
 
Na hata mwanamke wa kilokole siku zote anamuheshimu Mchungaji kuliko mume wake
 
Mwokozi wenu alisali dua zote kwa kicho, na kwa utulivu (mlimani, baharini, hata bustanini na msalabani).
Hadi mapepo aliyakemea kistaarabu.
Nyie Wazee mnapayuka kinomaaaaaaaa!!! Afu ubaya, mnayoyapayuka hamyajui maskini mweee
sawa vyovyote utakavyosema lakini huwezi elewa kwakua wewe sio mlengwa
 
Mkuu tatizo ni kwamba ibada yenu haina support ya makelele na kupayuka kwenu katika Biblia.
Biblia imeandikwa kabisa, "Abuduni kwa kicho na kimya"
matendo yanayotendeka kwani lazima yasemwe kwenye bibilia ndiyo yafanyike? siwezi nkaeleza zaidi kwakua moyoni mwako umeshaaamini kwamba ni kelele basi endelea kuamini tu
 
Hao wanaofunga maporomondo makubwa mengi alfajiri, mchana na jion wanapga kelele mji mzima, na hao wanaokesha wanapga ma nyimbo na ugomvi na karaha na makelele ya kila namna, mbona sisi hatujasema, kwahyo kuweka ka kitega uchumi kako hapo ndo unataka watu wote wakuone wew nan, na unataka kuzuia watu wasifanye mambo yako kisa wew au?
hajazuia watu kufanya ibada, tatizo kelele jaribu kuelewa sisi wa Islam muda mchache sana adhana tofauti na nyie wenzetu full kilio usiku kucha
 
halafu waache kujenga vibanda vya mabati
utafikiri ndio bulding code
pale stop over walijenga kibanda kama hicho wa kaenda kununua yale Maspika makubwa kabisi utafikiri kuna msanii anakuja kufanya SHOW, hovyo sana hakulaliki
 
Mti wenye matunda ndio hupigwa mawe.
Adhana huchukua dk 2 hadi 3 kwa siku tuna vipindi 5 vya swala 5 mara 3 utapata jibu mwenyewe ni dk ngapi ninyi hamna mchana wala usiku si siku za kazi wala weekend jibu unalo ila unaleta ushabiki tu jiulize kwanini malalamiko yanayohusu walokole ni mengi kuliko yanayohusu adhana?
 
Sio walokole tu hata waislamu nao wana makelele sana mjini hasa hasa alfajiri wanapiga sana makelele na ule wakati wanafunga huwa wanapiga sana makelele mida ya saa tatu tatu usiku ile wanaita talaweli noma saana yaani.
angalia kiwango cha sauti na muda, ila wenzetu hamna muda maalum, iwe mchana, usiku ni kelele tu
 
Naona mnatiana ujinga walokole jiulizeni kwanini kila siku ni nyie tu?
Kwa sababu tumememuaibisha shetani na malaika zake ukiwemo wewe. Moto wetu hauzimwi na wala hautazimwa na chochote hapa duniani mpaka Yesu anarudi kuja kuchukua kanisa lake. Nakushauri uokoke tu na kumkabidhi Yesu njia zako, vinginevyo unapoteza muda tu kupiga vita watu waliokombolewa kwa damu ya Yesu
 
Kama huyo Mungu humjui pole sana. Iko siku utamjua na utakwenda unalia ukiwatafuta watu waliookoka kwa machozi, ndipo utakapojua maana ya kuomba kwa machozi
Huyo Mungu gani anayependa kelele? Hujiulizi kwanini watu wenye maombi makali huenda mahala tulivu kama milimani? Pia tunaambiwa maombi tulivu kama usiku wa manane huwa na nguvu zaidi?
 
...ivi awo ndo waliendaga uwanja wa ndege (Airport) wakawa wanasali eti kwamba watapaaaa kwa ndege buree
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom